332 Kanuni Nne

1 Mwanadamu “ananipenda”, si kwa sababu upendo wake Kwangu Mimi ni wa asili, lakini kwa sababu anaogopa kuadibu. Nani kati ya wanadamu alizaliwa akinipenda? Kuna yeyote hunitendea Mimi jinsi wanavyotendea mioyo yao? Na kwa hiyo Najumlisha hili na neno la hekima kwa ulimwengu wa binadamu: Miongoni mwa wanadamu, hakuna yeyote anayenipenda. Naweza kumpenda mwanadamu milele, na pia Naweza kumchukia milele, na hili kamwe halitabadilika, kwani Nina ustahamilivu. Lakini mwanadamu hana ustahamilivu huu, yeye kila mara hughairighairi Kwangu, yeye kila mara hunisikiliza kidogo tu Nifunguapo kinywa Changu, na Nifungapo kinywa Changu na kutosema chochote, yeye punde hupotea kati ya mawimbi ya ulimwengu mkubwa. Hivyo, Mimi hufupisha hili katika methali nyingine: Watu hukosa ustahimilivu, na hivyo hawawezi kuutimiza moyo Wangu.

2 Leo, bado Sijui ni kwa nini mwanadamu hazingatii wajibu wake, kwa nini hajui jinsi kimo chake kilivyo kikubwa. Watu hata hawajui kama kimo chao kina uzani gramu kadhaa au liang kadhaa. Na hivyo, bado wao wananirairai. Ni kana kwamba kazi Yangu yote imekuwa bure, kana kwamba maneno Yangu ni mwangwi ndani ya milima mpana, na hakuna ambaye amewahi kutambua asili ya maneno na matamko Yangu. Na kwa hiyo Natumia hili kama msingi wa kufanya muhtasari wa methali ya tatu: Watu hawanijui, kwa kuwa hawanioni.

3 Watu hulia kwa sababu ya maneno Yangu, na maombi yao kila mara huwa na manung’uniko kuhusu ukatili Wangu. Ni kana kwamba wote wanatafuta “upendo” Wangu wa kweli kwa mwanadamu—lakini wangewezaje kupata upendo Wangu katika maneno Yangu makali? Kutokana na hilo, wao kila mara hukata tamaa kwa sababu ya maneno Yangu. Mbona, katika kile wasemacho, watu daima hulalamika kunihusu? Hivyo, Nafanya muhtasari wa methali ya nne ya maisha ya mwanadamu: Watu hunitii kiasi kidogo tu, na hivyo wao kila mara hunichukia.

4 Ninapowahitaji kufanya mambo fulani, wao hushangaa: Hawakuwa wamewahi kufikiri kwamba Mungu, ambaye Amekuwa mwenye ukarimu na mwenye huruma kwa miaka mingi sana, Angeweza kusema maneno kama hayo, maneno ambayo ni ya kikatili na yasiyothibitika, na kwa hiyo wao huduwaa. Nyakati kama hizo, Naona kwamba chuki iliyo ndani ya mioyo ya watu Kwangu imekua mara nyingine, kwa sababu wameanza tena kazi ya kulalamika. Wao kila mara huilaumu dunia na kulaani Mbinguni. Lakini katika maneno yao, Sioni chochote kinachowalaani wao wenyewe kwa sababu wanajipenda sana. Hivyo Nafanya muhtasari wa maana ya maisha ya mwanadamu: Kwa kuwa watu wanajipenda kupita kiasi, maisha yao yote ni ya uchungu na matupu, na wao hujiletea uharibifu wa kujitakia maishani mwao kwa sababu ya chuki yao Kwangu.

Umetoholewa kutoka katika Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 331 Ni Mapenzi ya Mungu kwa Wewe Kuishi Katika Mwili?

Inayofuata: 333 Mungu Atumai Kwamba Mwanadamu Anaweza Kuwa Mwaminifu kwa Maneno Yake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp