500 Kuunyima Mwili ni Kutenda Ukweli

1 Tangu watu waanze kumwamini Mungu, wamekuwa na nia ambazo si sahihi. Wakati ambapo huweki ukweli katika vitendo, unahisi kuwa motisha zako ni sahihi, lakini jambo likikutokea, utaona kuwa kuna motisha nyingi ndani zisizo sahihi. Hivyo, Mungu akiwafanya watu kuwa wakamilifu, Anawafanya kugundua kuwa kuna dhana nyingi ndani yao ambazo zinawazuia kumfahamu Mungu. Ukitambua kuwa motisha zako zina makosa, kama unaweza kuacha kutenda kulingana na motisha na dhana zako, na unaweza kuwa na ushuhuda wa Mungu na kusimama imara katika msimamo wako kwa kila lifanyikalo kwako, hili linathibitisha kuwa umeuasi mwili wako. Ukiasi dhidi ya mwili wako, bila shaka kutakuwa na vita ndani yako. Shetani atajaribu kufanya watu kuifuata, atajaribu kuwafanya wafuate dhana za kimwili na kutekeleza maslahi ya kimwili—ila maneno ya Mungu yatawapa nuru watu na kuwaangazia kwa ndani, na wakati huu itakuwa juu yako ikiwa utamfuata Mungu au utamfuata Shetani.

2 Mungu anawataka watu kuweka ukweli katika matendo kimsingi kushughulikia mambo yaliyo ndani yao, kushughulikiwa fikira zao, na dhana zao ambazo haziufuati moyo wa Mungu. Roho Mtakatifu huwagusa watu ndani ya mioyo yao, na kuwapa nuru na mwangaza. Kwa hivyo katika tukio lolote katika vita: Kila wakati watu wanapoweka ukweli katika vitendo, au kuweka mapenzi ya Mungu katika vitendo, huwa kuna vita vikali, na japokuwa mambo yanaweza kuonekana shwari katika miili yao, ila ndani ya mioyo yao kutakuwa na vita vya kufa na kupona—na ni baada tu ya hivi vita vikali, baada ya kutafakari kwa kina, ndipo ushindi au kushindwa kunaweza kuamuliwa. Ni kwa sababu ya vita hivi watu huvumilia shida na usafishaji; huku ni kuteseka kwa kweli. Vita vikikukabili, kama unaweza kusimama kweli upande wa Mungu, utaweza kumridhisha Mungu. Katika harakati ya kutenda ukweli, hakuepukiki kwamba mtu atateseka kwa ndani.

Umetoholewa kutoka katika “Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 499 Tenda Ukweli na Tabia Yako Itabadilika

Inayofuata: 501 Utendaji wa Kuacha Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp