483 Fuata Njia Ya Mungu katika Vitu Vyote Vikubwa na Vidogo

1 Kwa sababu ili kutembea katika njia ya Mungu, hatuwezi kuwachilia chochote kinachotuhusu sisi wenyewe, au kinachofanyika karibu nasi, hata yale mambo madogo madogo. Haijalishi kama tunafikiria tunafaa kumakinika au la, mradi tu suala lolote linatukabili hatufai kuliacha. Lote linafaa kuonekana kama jaribio la Mungu kwetu. Kama unao mwelekeo aina hii, basi unathibitisha hoja moja: Moyo wako unamcha Mungu, na moyo wako uko radhi kujiepusha na maovu. Kama unalo tamanio hili la kumtosheleza Mungu, basi kile unachotia katika matendo hakiko mbali na kiwango cha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.

2 Suala kubwa ni lipi? Swala dogo ni lipi? Masuala yote yanayohusu kutembea katika njia ya Mungu hayagawanywi kwa masuala makubwa au madogo. Kunao mara nyingi wale wanaosadiki kwamba masuala ambayo hayatiliwi maanani na watu, masuala ambayo kwa kawaida hayatajwi—haya ni mambo madogo tu, na hayana chochote kuhusiana na kutia ukweli katika matendo. Wakati watu hawa wanakabiliwa na suala kama hilo, hawalifikirii sana na wanaliachilia tu. Lakini ukweli wa mambo ni kwamba, suala hili ni funzo ambalo unafaa kulidadisi, funzo kuhusu namna ya kumcha Mungu, namna ya kujiepusha na maovu. Zaidi, kile unachofaa kujali hata zaidi ni kujua kile Mungu anachofanya wakati suala hili linapoibuka kukabiliana na wewe. Mungu yuko kando yako, anaangalia kila mojawapo ya maneno na vitendo vyako, anaangalia hatua zako, mabadiliko ya akili zako—hii ni kazi ya Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 482 Wale Wanaoyathamini Maneno ya Mungu Wamebarikiwa

Inayofuata: 484 Imani ya Kweli Katika Mungu ni Kutenda na Kupitia Maneno Yake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp