221 Unaifuata Kazi ya Sasa ya Mungu?

1 Kama huwezi kuifuata nuru ya leo, basi umbali umefunguka katika uhusiano wako na Mungu—huenda hata ukawa umevunjwa—na huna maisha ya kiroho ya kawaida. Uhusiano wa kawaida na Mungu hujengwa juu ya msingi wa kukubali maneno ya Mungu leo. Je, una maisha ya kiroho ya kawaida? Je, una uhusiano wa kawaida na Mungu? Wewe ni mtu anayeifuata kazi ya Roho Mtakatifu?

2 Kama unaweza kufuata nuru ya Roho Mtakatifu leo, na unaweza kufahamu mapenzi ya Mungu ndani ya maneno Yake, na kuingia katika maneno haya, basi wewe ni mtu ambaye hufuata mkondo wa Roho Mtakatifu. Kama hufuati mkondo wa Roho Mtakatifu, basi wewe bila shaka ni mtu asiyefuatilia ukweli. Roho Mtakatifu hana nafasi ya kufanya kazi ndani ya wale ambao hawana hamu ya kujiendeleza wenyewe, na kutokana na hayo, watu hao hawawezi kamwe kukusanya nguvu zao, na kila mara wao huwa baridi.

3 Leo, wewe hufuata mkondo wa Roho Mtakatifu? Wewe uko ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu? Je, umeibuka kutoka kwa hali baridi? Wale wote ambao huamini katika maneno ya Mungu, ambao huchukulia kazi ya Mungu kama msingi, na hufuata nuru ya Roho Mtakatifu leo—wao wote wako ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu. Kama wewe huamini kwamba maneno ya Mungu ni kweli na sahihi kwa dhahiri, na kama wewe huamini maneno ya Mungu bila kujali kile Yeye husema, basi wewe ni mtu ambaye hufuatilia kuingia katika kazi ya Mungu, na kwa njia hii utatimiza mapenzi ya Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 220 Waumini Lazima Wafuate Nyayo za Mungu kwa Karibu

Inayofuata: 222 Kuwa Mtu Anayekubali Ukweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp