486 Kujiandaa na Maneno ya Mungu ni Kipaumbele Chako cha Juu

1 Kuwa na ujuzi wa utendaji na kuwa na uwezo wa kuona wazi kazi ya Mungu—yote haya yanaonekana katika maneno Yake. Ni katika maneno ya Mungu tu ndio unaweza kupata nuru, hivyo unapaswa kujitayarisha na maneno Yake zaidi. Gawa ufahamu wako kutoka kwa maneno ya Mungu katika ushirika, na kupitia katika ushirika wako wengine wanaweza kupata nuru na unaweza kuwaongoza watu kwenye njia—njia hii ni ya utendaji. Kabla ya Mungu kuanzisha mazingira kwa ajili yenu, kila mmoja wenu lazima kwanza ajitayarishe na maneno Yake. Hiki ni kitu ambacho kila mtu anapaswa kufanya—ni kipaumbele cha haraka.

2 Kabla ya Mungu kuanzisha mazingira kwa ajili yenu, kila mmoja wenu lazima kwanza ajitayarishe na maneno Yake. Hiki ni kitu ambacho kila mtu anapaswa kufanya—ni kipaumbele cha haraka. Kitu cha kwanza cha kufanya ni kuwa na uwezo wa kula na kunywa maneno Yake. Kwa mambo ambayo huwezi kufanya, tafuta njia ya kutenda kutoka kwa maneno Yake, na angalia katika maneno Yake masuala yoyote ambayo hujui au matatizo yoyote uliyo nayo. Yafanye maneno ya Mungu yawe ruzuku yako, na uyaruhusu yaweze kukusaidia katika kutatua shida na matatizo yako ya vitendo; pia yaruhusu maneno Yake yawe msaada wako katika maisha. Mambo haya yanahitaji jitihada kwa upande wako.

3 Katika kula na kunywa neno la Mungu, lazima ufanikishe matokeo; lazima uweze kuutuliza moyo wako mbele Yake, na kutenda kulingana na maneno Yake unapokabili masuala. Wakati hujakutana na masuala yoyote, kula na kunywa tu. Wakati mwingine unaweza kuomba na kutafakari juu ya upendo wa Mungu, kuwa na ushirika juu ya ufahamu wako wa maneno Yake, na kuwasiliana juu ya kupata nuru na kupata mwanga unaoupitia ndani yako mwenyewe na majibu ambayo umekuwa nayo unapoyasoma matamko haya. Aidha, unaweza kuwapa watu suluhisho. Hili pekee ndilo la utendaji. Lengo la kufanya hili ni kuyaruhusu maneno ya Mungu kuwa utoaji wako wa vitendo.

Umetoholewa kutoka katika “Wale Wanaompenda Mungu Kwa Kweli Ni Wale Wanaoweza Kutii Utendaji Wake Kabisa” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 485 Kupitia Maneno ya Mungu Hakutenganishwi na Maneno Yake

Inayofuata: 487 Mtu Hawezi Kufuatilia Uzima Bila Neno la Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp