488 Jinsi ya Kuingia Katika Uhalisi wa Maneno ya Mungu

1 Wale ambao kwa kweli hujitumia wenyewe kwa ajili ya Mungu huweka nafsi zao zote mbele Yake. Wao hutii kwa kweli matamshi Yake yote, na wana uwezo wa kuweka maneno Yake katika matendo. Wao hufanya maneno ya Mungu kuwa msingi wa kuwepo kwao, na wanaweza kutafuta kwa kweli sehemu za matendo katika neno la Mungu. Huyu ni mtu ambaye kwa kweli anaishi mbele ya Mungu. Ikiwa unachofanya ni cha manufaa kwa maisha yako, na kwa njia ya kula na kunywa maneno Yake, unaweza kukidhi mahitaji yako ya ndani na upungufu ili tabia yako ya maisha inabadilishwa, basi hii itatimiza mapenzi ya Mungu.

2 Ikiwa unatenda kulingana na mahitaji ya Mungu, ikiwa huuridhishi mwili lakini unaridhisha mapenzi Yake, huku ni kuingia katika uhalisi wa maneno Yake. Wakati unazungumza juu ya kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu kwa kweli zaidi, kunamaanisha unaweza kutekeleza wajibu wako na kukidhi mahitaji ya Mungu. Aina hizi tu za vitendo ndizo zinazoweza kuitwa kuingia katika uhalisi wa maneno Yake. Ikiwa una uwezo wa kuingia katika uhalisi huu, basi una ukweli. Huu ndio mwanzo wa kuingia katika uhalisi; lazima kwanza ufanye mazoezi haya na ni baada tu ya hayo ndio utakuwa na uwezo wa kuingia katika hali halisi za kina zaidi.

Umetoholewa kutoka katika “Wale Wanaompenda Mungu Kwa Kweli Ni Wale Wanaoweza Kutii Utendaji Wake Kabisa” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 487 Mtu Hawezi Kufuatilia Uzima Bila Neno la Mungu

Inayofuata: 489 Soma Maneno ya Mungu Kuhusiana na Hali Zako

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp