777 Iga Uzoefu wa Petro

1 Baada ya Petro kupitia kazi nyingi ya Mungu, alipata ufahamu wa mambo fulani, na pia utambuzi mwingi. Alikuja kuelewa mambo mengi kuhusu kanuni ya huduma, na baadaye aliweza kujitoa kikamilifu kwa yale ambayo Yesu alimwaminia. Usafishaji mkubwa ambao alipokea kwa kiasi kikubwa ulikuwa kwa sababu, kwa mambo ambayo alikuwa amefanya mwenyewe, alihisi kwamba alikuwa na deni kubwa la Mungu, na kwamba hangeweza kumlipa kamwe. Petro alitambua pia kwamba mwanadamu ni mpotovu sana, jambo ambalo lilimfanya ahisi hatia katika dhamiri yake.

2 Yesu alikuwa amemwambia Petro mambo mengi, lakini katika wakati ambapo mambo haya yalisemwa, aliweza kuwa na ufahamu mdogo tu, na wakati mwingine bado alikuwa na upinzani na uasi kiasi. Baada ya Yesu kusulubiwa msalabani, mwishowe alipitia mwamko fulani, na ndani mwake alihisi maumivu makali ya kujilaumu mwenyewe. Mwishowe, ilifikia hatua ambapo alihisi haikukubalika kuwa na maoni yoyote ambayo hayakuwa sahihi.

3 Aliijua hali yake mwenyewe vizuri sana, na pia alijua utakatifu wa Bwana vizuri sana. Kwa sababu hiyo, moyo wa kumpenda Bwana ulikua ndani yake hata zaidi, na akazingatia zaidi maisha yake mwenyewe. Kwa sababu ya hili alipitia shida nyingi, na ingawa wakati mwingine ilikuwa kama kwamba alikuwa na ugonjwa hatari na hata ilionekana kama kwamba alikuwa amekufa, baada ya kusafishwa kwa njia hii mara nyingi, alijielewa zaidi, na akawa na upendo wa kweli kwa Bwana.

4 Inaweza kusemekana kuwa maisha yake yote yalitumika katika usafishaji, na hata zaidi ya hayo, katika kuadibu. Uzoefu wake ulikuwa tofauti na wa mtu mwingine yeyote, na upendo wake ulizidi ule wa mtu yeyote ambaye hajakamilishwa. Sababu ya kuchaguliwa kwake kama mfano ni kwa sababu alipitia uchungu mwingi kabisa katika maisha yake, na yale aliyoyapitia yalifanikiwa zaidi. Kama mnaweza kweli kuitembea sehemu ya mwisho ya njia kama vile Petro alivyofanya, basi hakuna kiumbe yeyote anayeweza kuwanyang’anya baraka zenu.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi Unavyopaswa Kuitembea Sehemu ya Mwisho ya Njia” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 776 Petro Alishikilia Imani na Upendo wa Kweli

Inayofuata: 778 Watu Wanapaswa Kutafuta Kuishi kwa Kudhihirisha Maisha ya Maana

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp