535 Wale Wasiofuatilia Ukweli Watajuta

1 Leo, huamini maneno ninayosema, na huyatilii maanani; wakati utakapofika kwa hii kazi kuenezwa, na unaona ukamilifu wake, utajuta, na wakati huo utakuwa bubu. Kuna baraka, ilhali hujui kuzifurahia, na kuna ukweli, ilhali hujui kuufuata. Je, hujiletei dharau? Kuna kazi nyingi, na ukweli mwingi; Je, hazina maana kujulikana na wewe? Je, adabu na hukumu ya Mungu haitoshi kuamsha roho yako? Je, adabu na hukumu ya Mungu haitoshi kukufanya ujichukie? Umetosheka kuishi katika ushawishi wa Shetani, kwa amani na furaha, na raha kidogo ya kimwili? Je, wewe si mtu wa chini zaidi kati ya watu wote?

2 Hakuna aliye mpumbavu kuliko wale ambao wameona wokovu lakini hawaufuati ili kuupata; hawa ni watu ambao wanalafua mwili na kufurahia Shetani. Unatumai kwamba imani yako kwa Mungu haitakuwa na changamoto ama dhiki, ama mateso yoyote. Unafuata vile vitu ambavyo havina maana, na huambatanishi faida yoyote kwa maisha, badala yake kuweka mawazo ya fujo kabla ya ukweli. Huna maana! Unaishi kama nguruwe—kuna tofauti gani kati yako, nguruwe na mbwa? Je, hao wasiofuata ukweli na badala yake wanafuata mapenzi ya kimwili, si wote ni wanyama? Hao waliokufa na bila roho si wafu wanaotembea?

3 Maneno mangapi yamenenwa kati yenu? Je, kazi kidogo imefanywa kati yenu? Ni kiasi gani nimetoa kati yenu? Na mbona hujapata chochote? Una nini cha kulalamikia? Je, si ni kweli kuwa hujapata chochote kwa sababu unapenda mwili sana? Na ni kwa sababu mawazo yako ni ya fujo sana? Je, si kwa sababu wewe ni mpumbavu sana? Kama huna uwezo wa kupata baraka hizi, unaweza kumlaumu Mungu kwa kutokukuokoa? Nimekupa njia ya ukweli, ila hujaipata: Wewe u mkono mtupu. Je, unakubali kuendelea na maisha haya, maisha ya nguruwe? Umuhimu wa watu hao kuwa hai ni nini?

Umetoholewa kutoka katika “Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 534 Kutofuatilia Ukweli Huishia Katika Kulia na Kusaga Meno Daima

Inayofuata: 536 Wasiofuatilia Ukweli Hawawezi Kufuata Hadi Mwisho

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp