142 Unathubutu Kudai Jina la Mungu Haliwezi Kubadilika Kamwe?

1 Wengine wanasema kwamba jina la Mungu halibadiliki, hivyo, mbona basi jina la Yehova likawa Yesu? Ilitabiriwa kuja kwa Masihi, hivyo mbona basi mwanadamu kwa jina Yesu alikuja? Mbona jina la Mungu lilibadilika? Kazi kama hiyo haikufanyika muda mrefu uliopita? Hawezi Mungu leo kufanya kazi mpya? Kazi ya jana inaweza kubadilishwa, na kazi ya Yesu inaweza kufuata baada ya hiyo ya Yehova. Haiwezi kazi ya Yesu kurithiwa na kazi nyingine? Ikiwa jina la Yehova linaweza kubadilishwa kuwa Yesu, basi jina la Yesu haliwezi kubadilishwa pia? Hakuna jambo lolote hapa lisilo la kawaida; ni kwamba tu watu ni punguani sana.

2 Mungu daima atakuwa Mungu. Bila kujali mabadiliko ya kazi Yake na jina Lake, tabia na maarifa Yake hayabadiliki milele. Ikiwa unaamini kwamba Mungu anaweza tu kuitwa na jina Yesu, basi unajua machache sana. Unathubutu kudai kwamba Yesu milele ni jina la Mungu, kwamba Mungu milele na daima atajulikana kwa jina Yesu, na kwamba haya hayatabadilika? Unathubutu kudai kwa uhakika ni jina la Yesu lililohitimisha Enzi ya Sheria na pia kuhitimisha enzi ya mwisho? Nani anaweza kusema kwamba neema ya Yesu inaweza kuhitimisha enzi? Mungu daima atakuwa Mungu. Bila kujali mabadiliko ya kazi Yake na jina Lake, tabia na maarifa Yake hayabadiliki milele.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 141 Tabia ya Mungu Inaonekana Katika Kila Hatua ya Kazi Yake

Inayofuata: 143 Jina la Mungu Laweza Kuamuliwa na Viumbe?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp