130 Enzi Tofauti, Kazi Tofauti ya Mungu

1 Leo, inapaswa kueleweka kwenu wote kwamba, katika siku za mwisho, ni kwa kiasi kikubwa ukweli wa “Neno linakuwa mwili” ambao unakamilishwa na Mungu. Kupitia kazi yake halisi duniani, Anafanya mwanadamu kumfahamu, na kushirikiana Naye, na kuona matendo Yake halisi. Anamsababisha mwanadamu kuona kwa wazi kwamba Yeye Anaweza kuonyesha ishara na maajabu na pia kuna nyakati ambapo Hawezi kufanya hivyo, na hii inategemea enzi. Kutokana na hili unaweza kuona kwamba Mungu sio kwamba Hawezi kuonyesha ishara na maajabu, lakini badala yake Anabadilisha kufanya kazi Kwake kulingana na kazi Yake, na kulingana na enzi. Katika hatua ya sasa ya kazi, Haonyeshi ishara na maajabu; kuonyesha kwake baadhi ya ishara na maajabu katika enzi ya Yesu, ilikuwa ni kwa sababu kazi Yake katika enzi hiyo ilikuwa tofauti.

2 Mungu Hafanyi kazi hiyo leo, na baadhi ya watu wanaamini Hana uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, au wanafikiri kwamba kama Haonyeshi ishara na maajabu, basi Yeye si Mungu. Hii sio hoja ya uwongo? Mungu Anaweza kuonyesha ishara na maajabu, lakini Anafanya kazi katika enzi tofauti, na hivyo Hafanyi kazi hiyo. Kwa kuwa hii ni enzi tofauti, na kwa kuwa hii ni hatua tofauti ya kazi ya Mungu, matendo yaliyowekwa wazi na Mungu pia ni tofauti. Imani ya mwanadamu kwa Mungu sio imani katika ishara na maajabu, wala imani katika miujiza, bali ni imani katika kazi Yake halisi wakati wa enzi mpya. Mwanadamu anamjua Mungu kupitia namna ambavyo Mungu Anafanya kazi, na maarifa haya yanamfanya mwanadamu amwamini Mungu, ambavyo ni kusema, imani katika kazi na matendo ya Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Kuijua Kazi ya Mungu Leo” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 129 Kazi ya Mungu Haijirudii

Inayofuata: 131 Mungu Aleta Kazi Mpya Katika Enzi Mpya

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp