125 Nimeamua Kumfuata Mungu

1

Nimepotoshwa sana na Shetani, nina mfano mdogo sana wa binadamu.

Kupitia yale ambayo maneno ya Mungu yanafichua kwa ukali sana, nimeona ubaya wa upotovu wangu.

Mwenye kiburi na aliyejawa tabia ya Kishetani, sistahili kweli kuishi mbele za Mungu.

Bila huruma na wokovu wa Mungu, ningewezaje kuwa hapa leo?

Ni hukumu ya Mungu ambayo imeniokoa, nimeamua kumfuata Mungu.

2

Asili yangu ya kishetani ni ya kina sana, ikinifanya nimwasi Mungu mara kwa mara.

Nimekuwa karagosi wa mwili wangu mwenyewe, linahuzunisha na kusikitisha.

Ninaweka azimio langu kuutenda ukweli, ili niweze kuwa huru kweli.

Kama kiumbe anayeishi, nafaa kuushinda mwili na kufufua nafsi yangu ya kweli.

Ni hukumu ya Mungu ambayo imeniokoa, nimeamua kumfuata Mungu.

3

Maneno ya Mungu yanaonyesha njia ya uzima, sasa najua jinsi ya kuwa binadamu.

Kwa kumwacha Shetani na kuunyima mwili, kutenda ukweli tu, ndipo nitakuwa na ubinadamu kiasi.

Kujitumia kwa ajili ya Mungu na kumtii, ndipo nimeona baraka Zake.

Moyo wa Mungu pekee ndio unaowapenda binadamu zaidi, Mungu anastahili sifa za binadamu.

Ni hukumu ya Mungu ambayo imeniokoa, nimeamua kumfuata Mungu.

4

Nimeona wazi vita vya dunia ya kiroho, kupata mwili kwa Mungu kunawafunua watu kweli.

Mwana wa Adamu anaonyesha ukweli ili kuwaokoa binadamu, akivumilia aibu kubwa.

Nimeona jinsi upendo wa Mungu ulivyo wa kweli, nitakosaje kumpenda?

Ninapata ukweli na kumshuhudia Mungu ili nilipe upendo Wake.

Ni hukumu ya Mungu ambayo imeniokoa, nimeamua kumfuata Mungu.

5

Mbinu zote za kazi ya Mungu ni ili kumtakasa na kumkamilisha mwanadamu.

Mustakabili na majaliwa yangu vipo mikononi mwa Mungu, naamini kuwa Yeye ni mwenye haki.

Nimetambua kuwa Kristo ni ukweli, nitamfuata Mungu hadi mwisho kabisa.

Naahidi maisha yangu kumshuhudia Mungu, sitamsaliti Yeye kamwe.

Ni hukumu ya Mungu ambayo imeniokoa, nimeamua kumfuata Mungu.

Iliyotangulia: 124 Mfuate Mungu Daima

Inayofuata: 126 Fuata Mfano wa Petro na Utafute Kumpenda Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

269 Nitampenda Mungu Milele

1 Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki