203 Wote Wasiomkubali Mungu Mwenye Mwili Wataangamizwa
1 Mungu asiyeonekana na kushikika anapendwa na kukaribishwa na wote. Kama Mungu ni Roho tu ambayo haionekani kwa mwanadamu, ni rahisi sana kwa mwanadamu kumwamini Mungu. Mwanadamu anaweza kuzipa uhuru fikra zake mwenyewe, anaweza kuchagua taswira yoyote anayotaka kama taswira ya Mungu ili kujifurahisha mwenyewe na kujifanya mwenyewe awe na furaha. Kwa njia hii, watu wanaweza kufanya yoyote yanoyompendeza zaidi Mungu wao mwenyewe, na kile ambacho Mungu huyu angempenda wakifanye, bila aibu yoyote. Aidha, mwanadamu huyu anaamini kwamba hakuna ambaye ni mwaminifu zaidi anayejitolea kwa Mungu kuliko yeye.
2 Mwanadamu hasumbuliwi na imani yake ya kutojali katika Mungu, na anamwamini Mungu kwa namna anavyotaka. Hii ni moja ya “haki na uhuru wa mwanadamu,” ambao hakuna mtu anayeweza kuuingilia kwa sababu mwanadamu anamwamini Mungu wake mwenyewe na wala si Mungu wa mtu yeyote yule; ni mali yake binafsi, na takribani kila mtu anamiliki aina hii ya mali binafsi. Mwanadamu anaichukulia mali hii kama hazina ya thamani, lakini kwa Mungu hakuna kitu ambacho ni duni au hakina thamani zaidi ya hiki, maana hakuna kiashiria cha wazi cha upinzani kwa Mungu kuliko mali hii binafsi ya mwanadamu.
3 Ni kwa sababu ya kazi ya Mungu mwenye mwili ndiyo Mungu amefanyika mwili ambaye ana umbo la kugusika, na ambaye anaweza kuonekana na kuguswa na mwanadamu. Yeye si Roho asiyekuwa na umbo, bali mwili ambao unaweza kuhusiana na kuonekana kwa mwanadamu. Hata hivyo, Miungu mingi ambayo watu wanaamini kwayo ni miungu isiyo na mwili na umbo maalumu, na ambayo haifungwi na umbo maalumu. Kwa njia hii, Mungu mwenye mwili amekuwa adui wa wengi wanaomwamini Mungu, na wale ambao hawawezi kuukubali ukweli wa Mungu mwenye mwili, vilevile, wamekuwa maadui wa Mungu.
4 Mwanadamu amejawa na dhana si kwa sababu ya namna anavyofikiri, au kwa sababu ya uasi wake, bali ni kwa sababu ya mali hii binafsi ya mwanadamu. Ni kwa sababu ya mali hii watu wengi hufa, na ni Mungu huyu asiye dhahiri, ambaye hawezi kuguswa, hawezi kuonwa, na ambaye hayupo hakika ambaye huangamiza maisha ya mwanadamu. Maisha ya mwanadamu yanapotea si kwa sababu ya Mungu mwenye mwili, sembuse na Mungu wa mbinguni, bali ni Mungu wa fikra za mwanadamu mwenyewe. Sababu pekee ambayo Mungu mwenye mwili amefanyika mwili ni kwa sababu ya mahitaji ya mwanadamu aliyepotoka. Ni kwa sababu ya mahitaji ya mwanadamu na si ya Mungu, na mateso Yake na sadaka ni kwa ajili ya mwanadamu na si kwa manufaa ya Mungu Mwenyewe.
Umetoholewa kutoka katika “Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili” katika Neno Laonekana katika Mwili