766 Wito wa Wale Wampendao Mungu

1 Leo hii, watu wengi bado hawajui kazi ambayo Mungu anatimiza katika siku za mwisho, au kwa nini Mungu Anastahimili fedheha kubwa kupita kiasi kuja katika mwili na kusimama na mwanadamu katika makovu na majonzi. Mwanadamu hajui chochote kuhusu lengo la kazi ya Mungu, wala kusudi la mpango wa Mungu kwa ajili ya siku za mwisho. Kwa sababu mbalimbali, watu daima wanakuwa vuguvugu katika kuingia ambako Mungu anataka na wanabakia wenye shaka, kitu ambacho kimeleta shida kubwa katika kazi ya Mungu katika mwili. Watu wanaonekana kuwa vizuizi na, leo hii, bado wanakuwa hawana uelewa sahihi. Kwa hiyo Nitazungumza juu ya kazi ambayo Mungu anafanya kwa mwanadamu, na makusudi ya Mungu ya haraka, ili kwamba nyinyi nyote muwe watumishi waaminifu wa Mungu ambao, kama Ayubu, ni bora ufe kuliko kumkataa Mungu na utastahimili kila fedheha, na ambao, kama Petro, mtatoa utu wenu wote kwa Mungu na kuwa wandani ambao Mungu Aliwapata katika siku za mwisho.

2 Ninawasihi kaka na dada kufanya kila kitu kilichopo ndani ya uwezo wao kutoa utu wao wote kwa mapenzi ya mbingu ya Mungu, kuwa watumishi watakatifu katika nyumba ya Mungu, na kufurahia ahadi za kutokuwa na kikomo zilizotolewa na Mungu, ili kwamba moyo wa Mungu Baba ufurahie pumziko la amani. “Kukamilisha mapenzi ya Mungu Baba” kunapaswa kuwe wito wa wote wanaompenda Mungu. Maneno haya yanapaswa kutumika kama mwongozo wa mwanadamu kwa ajili ya kuingia na dira inayoongoza matendo yake. Hili ndilo suluhisho ambalo mwanadamu anapaswa kuwa nalo. Kukamilisha kabisa kazi ya Mungu duniani na kushirikiana na kazi ya Mungu katika mwili—huu ni wajibu wa mwanadamu. Siku moja, kazi ya Mungu itakapokuwa imekamilika, mwanadamu atamuaga Anaporudi mapema kwa Baba yake mbinguni. Je, huu sio wajibu ambao mwanadamu anapaswa kuutimiza?

Umetoholewa kutoka katika “Kazi na Kuingia (6)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 765 Pitia Kazi ya Mungu ili Kugundua Uzuri Wake

Inayofuata: 767 Kumwamini Mungu Lakini Kutompenda ni Maisha Matupu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp