279 Niliumbwa na Wewe, Mimi ni Wako

1

Kupitia milima na mabonde mengi, mabadiliko yasiyohesabika.

Nikipeperushwa na upepo na kuloweshwa na mvua, nafuata nyayo Zako.

Hatari na taabu ni upendo wa kweli na kuendelea kwa shauku.

Moyo wangu uliopenda sana unakupenda kwa upendo wa milele.

Ni mara ngapi majira ya baridi yamegeuka kuwa majira ya kuchipua?

Machungu kisha matamu, kila likifurahiwa moja moja.

Upepo wa vuli ukiwa umeisha, nakaribisha maua ya majira ya kuchipua.

Ee, mabadiliko ghafla ya maisha ya askari, najua moyo Wako.

Uliteseka Ulipoingia humu duniani kwa unyenyekevu.

Ukiwa umepigwa na upepo na mvua, hakuna aliyekuhurumia.

Kuteswa na halaiki, ni uchungu usioelezeka kwa maneno.

Na bado tamaa ya moyo Wako ingeweza kuonekana katika maneno Yako.

Maneno Yako ya maisha yanaunyunyizia moyo wangu,

hadi katika kina chake, hadi katika kina chake.

Moyo wangu, ukigeuka kuwa mwema, unakupenda.

Moyo wangu utakuwa mmoja na Wako lini?

Nimeumbwa na Wewe, na Mimi ni Wako.

Kuvunja imani itakuwa dhambi ya milele.

Nitafuta machozi yaliyomwagwa na moyo Wako uliojeruhiwa.

Ili kukupa matamanio Yako, nakupa moyo wangu.

2

Unapoenda, ni vigumu kujua Utakaporudi.

Kuachana kukali kama kifo, nalia machozi machungu kweli.

Naelea, nachukia kuondoka, moyo wangu unaonekana wote uko vipande.

Macho yangu yanajitahidi sana, natamani kurudi Kwako.

Roho ya ukiwa nisiyoweza kuficha.

Kwa goti lililopigwa, nahisi sikitiko likiudunga moyo wangu.

Rafiki karibu kama jirani, ingawa tumetengwa na bahari.

Sadaka ndogo naweka mbele Yako.

Tunapokutana, Unatabasamu kwangu.

Maneno Yako ya maisha yanaunyunyizia moyo wangu,

hadi katika kina chake, hadi katika kina chake.

Moyo wangu, ukigeuka kuwa mwema, unakupenda.

Moyo wangu utakuwa mmoja na Wako lini?

Nimeumbwa na Wewe, na Mimi ni Wako.

Kuvunja imani itakuwa dhambi ya milele.

Nitafuta machozi yaliyomwagwa na moyo Wako uliojeruhiwa.

Ili kukupa matamanio Yako, nakupa moyo wangu.

Iliyotangulia: 278 Lazima Tuchague Njia Yetu Wenyewe

Inayofuata: 280 Wewe ni Maisha Yangu ya Kweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp