350 Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu

1 Vitendo vyote na matendo ya Shetani vinaonyeshwa kupitia kwa binadamu. Sasa vitendo vyote na matendo yote ya binadamu ni maonyesho ya Shetani na hivyo basi haviwezi kumwakilisha Mungu. Binadamu ni mfano halisi wa Shetani, na tabia ya mwanadamu haiwezi kuiwakilisha tabia ya Mungu. Baadhi ya wanadamu ni wenye tabia nzuri; Mungu anaweza kufanya baadhi ya kazi kupitia kwa tabia hiyo nayo kazi yao inatawaliwa na Roho Mtakatifu. Ilhali tabia yao haiwezi kumwakilisha Mungu. Kazi ambayo Mungu hufanya ndani yao ni kule tu kufanya kazi na pamoja na kupanua kile ambacho tayari kimo ndani yao. Wawe ni manabii au binadamu wanaotumiwa na Mungu kutoka kwa enzi zilizopita, hakuna yeyote anayeweza kumwakilisha Mungu moja kwa moja.

2 Yote ambayo hutoka kwa njia ya moja kwa moja kutoka kwa Mungu ni mema. Hata hivyo, tabia ya binadamu imetengenezwa na Shetani na haiwezi kumwakilisha Mungu. Ni Mungu mwenye mwili tu—mapenzi Yake, nia Yake ya kuteseka, haki, utiifu, unyenyekevu na kujificha Kwake—hivi vyote humwakilisha Mungu moja kwa moja. Hii ni kwa sababu Alipokuja, Hakuwa na asili ya dhambi na alikuja moja kwa moja kutoka kwa Mungu bila ya kutengenezwa na Shetani. Yesu yumo tu katika mfano wa mwili wenye dhambi na hawakilishi dhambi; kwa hivyo, vitendo Vyake, matendo na maneno, mpaka wakati ule kabla ya mafanikio Yake ya kazi kupitia kwa kusulubishwa vyote ni viwakilishi vya moja kwa moja vya Mungu.

Mfano wa Yesu unatosha kuthibitisha kwamba binadamu yeyote aliye na asili ya dhambi hawezi kumwakilisha Mungu, na kwamba dhambi ya binadamu inamwakilisha Shetani. Hiyo ni kusema kwamba dhambi haimwakilishi Mungu na Mungu hana dhambi. Hata kazi inayofanywa ndani ya binadamu na Roho Mtakatifu inaweza tu kuchukuliwa kuwa imetawaliwa na Roho Mtakatifu na haiwezi kusemwa kwamba ilifanywa na binadamu kwa niaba ya Mungu. Lakini kwa kadiri ambavyo binadamu anahusika, si dhambi yake wala tabia yake inamwakilisha Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 349 Hii ni Taswira Kamili Kabisa ya Shetani

Inayofuata: 351 Ni Watu Wachache Mno Wanaolingana na Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp