855 Matokeo Hatari ya Kumsaliti Mungu

1 Roho zote ambazo zimepotoshwa na Shetani ziko chini ya udhibiti wa miliki ya Shetani. Ni wale tu wanaomwamini Kristo ndio waliotengwa kando, wakiokolewa kutoka katika kambi ya Shetani, na kuletwa katika ufalme wa leo. Watu hawa kamwe hawaishi chini ya ushawishi wa Shetani. Hata hivyo, asili ya mwanadamu bado imekita mizizi katika mwili wa mwanadamu. Ijapokuwa roho zenu zimeokolewa, asili yenu bado ni ya mwonekano wake wa zamani na uwezekano kuwa mtanisaliti unabakia asilimia mia moja. Ndiyo maana kazi Yangu ni ya kudumu muda mrefu sana, kwa kuwa asili yenu ni isiyotikiswa kabisa.

2 Sasa hivi nyote mnateseka jinsi mnavyoweza katika kutimiza wajibu wenu, lakini ukweli usiopingika ni huu: Kila mmoja wenu ana uwezo wa kunisaliti Mimi na kuirudia miliki ya Shetani, katika kambi yake, na kuyarudia maisha yenu ya zamani. Wakati huo haitawezekana kwenu kuwa hata na chembe ya utu au mwonekano wa binadamu kama mlionao sasa. Katika hali nzito, mtateketezwa, na zaidi mtalaaniwa milele, msipate mwili tena lakini muadhibiwe vikali. Kazi Yangu ni kazi ya kuziokoa roho za watu. Roho yako ikiingia mikononi mwa Shetani, basi mwili wako hautakuwa na siku tulivu.

3 Kama Ninaulinda mwili wako, basi roho yako kwa hakika itakuwa chini ya ulinzi Wangu. Ikiwa Ninakuchukia kwa kweli, basi mwili wako na roho yako vitaingia mara moja mikononi mwa Shetani. Unaweza kufikiri hali yako itakuwaje wakati huo? Kama siku moja maneno Yangu hatashindwa kuwashawishi, basi Nitawakabidhi nyote kwa Shetani awatese maradufu hadi wakati hasira Yangu imeyeyuka kabisa, ama Nitawaadhibu binafsi nyie binadamu msiokomboleka, kwa kuwa mioyo yenu ya kunisaliti haijawahi kubadilika.

Umetoholewa kutoka katika “Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 854 Hadithi ya Tomaso ni Onyo kwa Vizazi vya Baadaye

Inayofuata: 856 Matokeo ya Kutojua Tabia ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

263 Njia Yote Pamoja na Wewe

1 Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani. Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga....

83 Upendo wa Kweli

1 Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao, nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini. Neno Lake linanijaza na raha na furaha...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki