67 Hatua ya Mwisho ya Ushindi Inakusudiwa Kuwaokoa Watu
1 Hatua ya mwisho ya kushinda ni ya kukomboa watu na vilevile kufichua mwisho wa kila mtu. Inaweka wazi upotevu wa watu kupitia hukumu na kwa njia hiyo kuwafanya watubu, waamke, na kufuatilia uzima na njia ya haki ya maisha ya mwanadamu. Ni ya kuamsha mioyo ya waliolala na wapumbavu na kuonyesha, kwa njia ya hukumu, uasi wao wa ndani. Hata hivyo, ikiwa watu bado hawawezi kutubu, bado hawawezi kufuata njia ya haki ya maisha ya mwanadamu na hawawezi kuutupa upotovu huu, basi watakuwa vyombo visivyoweza kukombolewa vya kumezwa na Shetani. Hii ndiyo maana ya kushinda—kuwakomboa watu na vilevile kuwaonyesha mwisho wao. Mwisho mzuri, mwisho mbaya—yote yanafichuliwa na kazi ya kushinda. Kama watu watakombolewa au kulaaniwa yote yanafichuliwa wakati wa kazi ya kushinda.
2 Siku za mwisho ni wakati ambao vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina zake kupitia kushinda. Kushinda ni kazi ya siku za mwisho; kwa maneno mengine, kuhukumu dhambi za kila mtu ni kazi ya siku za mwisho. La sivyo, watu wangeainishwa vipi? Kazi ya kuainisha inayofanywa miongoni mwenu ni mwanzo wa kazi ya aina hiyo ulimwenguni kote. Baada ya hii, wale wa kila nchi na watu wote watapitia kazi ya ushindi. Hii inamaanisha kuwa watu wote wataainishwa kimakundi na kufika mbele ya kiti cha hukumu kuhukumiwa. Hakuna mtu na hakuna kitu kitakachoepuka kupitia huku kuadibu na hukumu, na hakuna mtu au kitu kinaweza kukwepa uainishaji huu; kila mtu atawekwa katika jamii. Hii ni kwa sababu mwisho u karibu kwa vitu vyote na mbingu zote na dunia zimefikia hatima yake. Mwanadamu anawezaje kukwepa hatima ya maisha yake?
Umetoholewa kutoka katika “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili