278 Lazima Tuchague Njia Yetu Wenyewe

1 Kristo wa siku za mwisho huonyesha ukweli na kufichua haki ya Mungu. Mungu ndiye ukweli na kwa wote ni mwenye haki. Tukimwamini Mungu bila kufuatilia ukweli tutaondolewa mishowe. Mungu huamua matokeo ya mwisho ya mwanadamu kulingana na ikiwa ana ukweli au la. Tabia nzuri kwa nje haimaanishi kuwa na uzima. Bila matendo mema na bila ukweli, Mungu atatuacha. Tabia ya Mungu ni takatifu na yenye haki, Haruhusu kosa lolote. Wale wafanyao uovu mwingi na kumpinga Mungu wataadhibiwa. Tunapaswa kuchagua njia yetu wenyewe na hakuna anayeweza kutufanyia. Watu waaminifu wanaotii ukweli tu ndio watu walio na ubinadamu. Tunaweza tu kupata sifa za Mungu kwa kutenda ukweli na kuishi kwa kudhihirisha uhalisi.

2 Kupata sifa za Mungu katika imani ya mtu, kumpenda Mungu na kumtii Mungu ni muhimu sana. Ni wale tu wanaokubali hukumu na kuadibu kwa Mungu ili kutakaswa ndio wenye busara. Hakuna thamani au maana katika kutafuta nafasi, umaarufu, utajiri, au majisifu. Ni wale tu wanaotimiza wajibu wao na kutenda ukweli ndio wafuasi wa Mungu. Ikiwa mtu anaweza tu kuhubiri lakini asitende ukweli, basi yote ni tupu. Tunaweza tu kuishi maisha ya kweli ikiwa tunampenda Mungu kweli na kuwa na ushuhuda mzuri. Hukumu na kuadibu, upogoaji na ushughulikiaji—vyote ni upendo wa Mungu. Kuwa shahidi majaribu na usafishaji vinapokuja kunamtukuza Mungu. Mateso na majaribu yanaonyesha wazi ikiwa mwanadamu ana uhalisi wa ukweli. Tunaweza tu kumshuhudia Mungu tunapopata ukweli na kumjua Mungu. Na tunafanikiwa tu tunapofuatilia ukweli na kupata mabadiliko ya tabia.

Iliyotangulia: 277 Nimeamua Kumfuata Mungu

Inayofuata: 279 Niliumbwa na Wewe, Mimi ni Wako

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp