294 Thamini Fursa ya Kumpenda Mungu

1

Wakati unapita haraka sana, unafifia ndani ya mto mrefu wa wakati.

Ghafla naangalia nyuma na kukumbuka zamani, lakini tanafusi tu ndizo zilizobaki.

Nimefurahia sana upendo wa Mungu, sijawahi kumlipa na nahisi hatia sana ndani.

Upendo wangu kwa Mungu ni maneno tu midomoni mwangu, lakini moyo wangu umejaa tamaa za ubinafsi.

Nadhiri yangu ya kulipa upendo wa Mungu inashindwa jaribio la majaribu.

Mara nyingi, nimekuwa mgumu na mwasi; mara nyingi, nimekataa kurekebisha njia zangu.

Nasimama mbele za Mungu lakini moyo wangu uko mbali na Yeye.

Sijawahi kumpa moyo wangu wa kweli, Sijawahi kumbebea mzigo wowote.

Ni mbinafsi na nazungumza maneno matupu, nataka tu kumpokonya Mungu baraka Zake.

Wakati upitao umejaa kumbukumbu zisizoweza kustahimilika.

2

Nimehukumiwa na kuadibiwa mara nyingi, nimepitia majaribio mengi na usafishaji mwingi.

Upendo wa Mungu huwa nami kila wakati, Maneno Yake yanipa nuru, kuniongoza na kunielekeza.

Moyo wangu mgumu, usiohisi hatimaye waanza kuamka na kurudi nyuma.

Wakati wote njiani, ninapomfuata Mungu hadi leo, haya yote ni kwa sababu ya upendo na utunzaji wa Mungu.

Bila huruma na wokovu wa Mungu, ningewezaje kufika leo?

Nachukia kwamba nimeamka nimechelewa sana na nimepoteza wakati mwingi wa thamani sana.

Mungu amelipa gharama ya kujitahidi sana kuniokoa.

Nikikabiliwa na upendo na wokovu wa Mungu, ningewezaje kuasi tena?

Ni kwa kufuatilia ukweli, kumpenda Mungu na kumridhisha Mungu tu ndipo mwanadamu anaweza kuishi bila majuto.

Hata ninapopitia majaribu na dhiki kubwa, bado nitakamilisha wajibu wangu kumlipa Mungu.

Nitathamini siku zangu za mwisho na kujitolea upendo wangu safi kwa Mungu.

Iliyotangulia: 293 Kilio kwa Dunia ya Mikasa

Inayofuata: 295 Mungu Amenipa Upendo Mwingi Sana

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

273 Upendo Safi Bila Dosari

1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au...

84 Umuhumi wa Maombi

1 Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo...

132 Mradi tu Usimwache Mungu

Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki