252 Jinasue Kutoka Fikira za Uraia na Ukabila Kutafuta Kuonekana kwa Mungu

Na ndiyo maana Ninasema kuwa unafaa kujiondoa katika dhana za uraia wako au kabila lako unapokutafuta kuonekana kwa Mungu.

1 Bila kujali kama wewe ni Mmarekani, Mwingereza, au mtu wa taifa jingine, ni lazima utoke nje ya mipaka yako, ni lazima ujipite, na ni sharti uione kazi ya Mungu kama kiumbe wa Mungu. Kwa njia hii, hutaweka vikwazo katika nyayo za Mungu. Kwa sababu, leo, watu hufikiri kuwa haiwezekani Mungu kudhihirika katika nchi au taifa fulani. Umuhimu wa kazi ya Mungu una undani kiasi gani, na kuonekana kwa Mungu kuna maana ilioje! Vinawezaje kupimwa kwa dhana na fikira za mwanadamu?

2 Mungu ni Mungu wa wanadamu wote. Hawi mali binafsi ya nchi au taifa lolote na hufanya kazi ya mpango Wake bila kuzuiwa na mfumo wowote, nchi au taifa. Labda hujawahi kuwazia mfumo huu, au labda wewe hukana kuwepo kwake, au labda nchi au taifa ambapo Mungu huonekana limebaguliwa na lina maendeleo duni sana duniani. Na bado Mungu ana busara Yake. Na uwezo Wake kupitia ukweli na tabia Zake kwa hakika Amepata kundi la watu wenye mawazo sawa na Yeye. Na Amepata kundi la watu ambao alitaka kutengeneza: kundi lililoshindwa Naye, watu ambao wameyavumilia majaribu machungu na aina zote za mateso na wanaweza kumfuata mpaka mwisho.

Na ndiyo maana Ninasema kuwa unafaa kujiondoa katika dhana za uraia wako au kabila lako unapokutafuta kuonekana kwa Mungu. Kwa njia hii, hutafungwa na dhana zako mwenyewe; kwa njia hii, utahitimu kukaribisha kuonekana kwa Mungu. Vinginevyo, daima utakuwa gizani na hutapata kibali cha Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 251 Usitegemee Fikira Kuwekea Kuonekana kwa Mungu Mipaka

Inayofuata: 253 Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp