Kumjua Mungu (IV)
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 120)
Kuelewa Mamlaka ya Mungu Kutoka kwa Mitazamo Mikubwa na Midogo
Mamlaka ya Mungu ni ya kipekee. Ndiyo maonyesho ya tabia ya, na dutu maalum ya, utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Hakuna kiumbe ambacho kiliumbwa wala kile ambacho hakikuumbwa kinachomiliki maonyesho ya tabia kama hii, na dutu maalum kama hii; ni Muumba tu ndiye anayemiliki aina hii ya mamlaka. Hivyo ni kusema kwamba, ni Muumba tu—Mungu Yule wa Kipekee—ambaye anaonyeshwa kwa njia hii na ndiye aliye na dutu kama hii. Kwa nini tuzungumzie mamlaka ya Mungu? Mamlaka ya Mungu Mwenyewe yanatofautiana vipi na mamlaka yaliyomo kwenye akili ya binadamu? Ni nini maalum sana kuyahusu? Na kunao umuhimu gani haswa kuyazungumzia hapa? Kila mmoja wenu lazima aweze kutilia maanani kwa umakinifu suala hili. Kwa watu wengi zaidi, “Mamlaka ya Mungu” ni fikira isiyoeleweka, ile ambayo ni ngumu sana kupata kuielewa, na mazungumzo yoyote kuihusu huenda yasizae matunda mazuri. Kwa hivyo lazima kutakuwepo na pengo kati ya maarifa ya mamlaka ya Mungu ambayo binadamu anaweza kuwa nayo, na kiini cha mamlaka ya Mungu. Ili kuliziba pengo hili, ni lazima mtu aweze kuelewa mamlaka ya Mungu hatua kwa hatua kupitia kwa maisha halisi ya watu, matukio, vitu, au mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wa wanadamu, ambayo wanadamu wanaweza kuyaelewa. Ingawaje kauli hii “Mamlaka ya Mungu” inaweza kuonekana kama isiyoeleweka, mamlaka ya Mungu kwa kweli si ya dhahania kamwe. Yeye yupo na binadamu kila dakika ya maisha yake, akimwongoza kila siku. Kwa hivyo, katika maisha ya kila siku ya kila mtu ataweza haswa kuona na kupitia dhana halisi ya mamlaka ya Mungu. Uhalisi huu ni uthibitisho wa kutosha kwamba mamlaka ya Mungu kwa kweli yapo, na inamuruhusu mtu kutambua na kuelewa kimamilifu ukweli huu kwamba Mungu anamiliki mamlaka haya.
Mungu aliumba kila kitu, na baada ya kuviumba, Anao utawala juu ya kila kitu. Pamoja na kuwa na utawala juu ya kila kitu, pia anadhibiti kila kitu. Wazo hili linamaanisha nini “Mungu anadhibiti kila kitu”? Hali hii inaweza kuelezewa vipi? Hali hii inatumika vipi katika maisha halisi? Mnawezaje kuyajua mamlaka ya Mungu kwa kuelewa hoja hii kwamba “Mungu Anadhibiti kila kitu”? Kutoka kwenye kauli ile ile “Mungu anadhibiti kila kitu” tunafaa kuona kwamba kile ambacho Mungu anadhibiti si sehemu ya sayari, sehemu ya uumbaji, wala sehemu ya mwanadamu, lakini kila kitu: kuanzia kwa viumbe vile vikubwa hadi vile vidogovidogo, kuanzia kwa vile vinavyoonekana hadi visivyoonekana, kuanzia kwenye nyota za angani hadi kwenye vitu vilivyo na uhai ulimwenguni, pamoja na viumbe vidogovidogo visivyoweza kuonekana kwa macho ya kawaida au viumbe vilivyo katika maumbo mengine. Huu ndio ufafanuzi hakika wa “kila kitu” ambacho Mungu “anadhibiti,” na ndio upana ambao Mungu anaonyesha mamlaka Yake, kiwango cha ukuu na utawala Wake.
Kabla ya binadamu hawa kuwepo, viumbe vyote—sayari zote, nyota zote kule mbinguni—tayari vilikuwepo. Kwenye kiwango cha vitu vikubwa, vyombo hivi vya mbinguni vimekuwa vikizunguka mara kwa mara chini ya udhibiti wa Mungu, kwa kuwepo kwao kote, hata hivyo miaka mingi imepita. Ni sayari gani inaenda wapi na wakati gani haswa; ni sayari gani inafanya kazi gani, na lini; ni sayari gani inazunguka katika mzingo gani, na ni lini inatoweka au inabadilishwa—vitu hivi vyote vinasonga mbele bila ya kosa lolote dogo. Nafasi za sayari na umbali kati yazo ni masuala yanayofuata mifumo maalum, ni masuala ambayo yanaweza kufafanuliwa kwa data sahihi; njia ambazo zinasafiria, kasi na mifumo ya mizunguko yao, nyakati ambapo zinapatikana kwenye nafasi mbalimbali zinaweza kufafanuliwa kwa usahihi na kufafanuliwa kwa sheria maalum. Kwa miaka na mikaka sayari zimefuata sheria hizi na hazijawahi kukosea hata kidogo. Hakuna nguvu inayoweza kubadilisha au kuharibu njia zao au mifumo ambayo zinafuata. Kwa sababu sheria maalum ambazo zinaongoza mizunguko yao na data maalum inayozifafanua ziliamuliwa kabla na mamlaka ya Muumba, zinatii sheria hizi zenyewe, kulingana na ukuu na udhibiti wa Muumba. Kwenye kiwango cha mambo makubwamakubwa, si vigumu kwa binadamu kujua zaidi kuhusu mifumo fulani, data fulani, pamoja na sheria au matukio fulani yasiyoeleweka au yasiyoelezeka. Ingawaje binadamu hawakubali kwamba Mungu yupo, haukubali hoja kwamba Muumba aliumba na anatawala kila kitu na zaidi ya yote hautambui uwepo wa mamlaka ya Muumba, wanasayansi wa kibinadamu, wanafalaki, nao wanafizikia wanachunguza na kugundua zaidi na zaidi kwamba uwepo wa kila kitu kwenye ulimwengu, na kanuni na mifumo inayoamuru mizunguko yao, vyote vinatawaliwa na kudhibitiwa na nishati nyeusi kubwa na isiyoonekana. Ukweli huu unamlazimisha mwanadamu kukabiliana na kukiri kwamba kuna Mwenye Nguvu katikati ya mifumo hii ya mizunguko, Anayepangilia kila kitu. Nguvu zake si za kawaida, na ingawaje hakuna anayeweza kuona uso Wake wa kweli, Yeye hutawala na kudhibiti kila kitu kila dakika. Hakuna binadamu au nguvu zozote zile zinazoweza kuuzidi ukuu Wake. Huku binadamu akiwa amekabiliwa na hoja hii, lazima atambue kwamba sheria zinazotawala uwepo wa kila kitu haziwezi kudhibitiwa na binadamu, haziwezi kubadilishwa na yeyote; na wakati uo huo binadamu lazima akubali kwamba, binadamu hawezi kuelewa kikamilifu sheria hizi. Na hizi sheria hazitokei kiasili lakini zinaamrishwa na Mtawala. Haya yote ni maonyesho na mamlaka ya Mungu yanayoonyesha kwamba mwanadamu anaweza kuelewa katika kiwango cha mambo makubwa.
Kwenye kiwango cha mambo madogomadogo, milima, mito, maziwa, bahari, na maeneo ya ardhi yote ambayo binadamu anatazama nchini, misimu yote ambayo yeye anapitia, mambo yote yanayopatikana kwenye ulimwengu, kukiwemo mimea, wanyama, vijiumbe na binadamu, vyote viko chini ya ukuu wa Mungu na vinadhibitiwa na Mungu Mwenyewe. Katika ukuu na udhibiti wa Mungu, vitu vyote vinakuwepo au vinatoweka kulingana na fikira Zake, maisha ya vitu hivi yanatawaliwa na sheria fulani, na vinakua na kuzaana kulingana nazo. Hakuna binadamu au kiumbe chochote kilicho juu ya sheria hizi. Kwa nini hali iko hivi? Jibu la pekee tu ni, kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Au, nikijibu kwa njia nyingine, kwa sababu ya fikira za Mungu na matamshi ya Mungu; kwa sababu Mungu Mwenyewe hufanya haya yote. Hivi ni kusema, ni mamlaka ya Mungu na ni akili ya Mungu ambayo iliunda sheria hizi; zitasonga na kubadilika kulingana na fikira Zake, na kusonga huku na mabadiliko haya yote yanafanyika au kutoweka kwa minajili ya mpango Wake. Hebu tuchukulie magonjwa ya mlipuko, kwa mfano. Yanazuka tu bila onyo, hakuna anayejua asili yake, au sababu maalum zinazoelezea ni kwa nini huwa yanatokea, na kila wakati magonjwa ya mlipuko yanapofika mahali fulani, wale walio na bahati mbaya hawawezi kukwepa maafa. Sayansi ya binadamu inafafanua na kutuelewesha kwamba magonjwa ya mlipuko yanasababishwa na kuenea kwa vijidudu hatari au vyenye madhara, na kasi yao, eneo lao, na njia ya maambukizi haiwezi kutabiriwa au kudhibitiwa na sayansi ya wanadamu. Ingawaje watu hupingana na magonjwa ya mlipuko kwa kila njia iwezekanayo, hawawezi kudhibiti ni watu gani au wanyama gani watakaoathirika wakati magonjwa ya mlipuko yanapozuka. Kitu cha pekee ambacho binadamu wanaweza kufanya ni kujaribu kuyazuia, kuyapinga, na kuyafanyia utafiti. Lakini hakuna anayejua sababu za msingi zinazoelezea mwanzo au mwisho wa magonjwa ya mlipuko ya aina yoyote ile, na hakuna anayeweza kuyadhibiti. Wakiwa wamekabiliwa na ongezeko na kuenea kwa magonjwa ya mlipuko, suala la kwanza ambalo binadamu hufanya ni kuunda chanjo, lakini mara nyingi magonjwa hayo ya mlipuko hayo hutoweka kabisa kabla ya hata chanjo kuwa tayari. Kwa nini magonjwa ya mlipuko hutoweka kabisa? Wengine husema kwamba vijidudu vimeweza kudhibitiwa, wengine husema kwamba vimetoweka kabisa kwa sababu ya mabadiliko katika misimu…. Kuhusiana na ikiwa makisio haya ya kuchanganyikiwa ni kweli au la, sayansi haiwezi kutupa ufafanuzi wowote, na wala haitoi jibu lolote lenye uhakika. Kile ambacho binadamu wanakabiliwa nacho si makisio haya tu lakini pia ukosefu wa mwanadamu katika kuelewa na woga wa magonjwa haya ya mlipuko. Hakuna anayejua, baada ya kila kitu kuchambuliwa, ni kwa nini magonjwa haya ya mlipuko huanza au ni kwa nini huisha. Kwa sababu wanadamu wanayo imani tu katika sayansi, wanaitegemea sayansi kabisa, lakini hawatambui mamlaka ya Muumba au kuukubali ukuu Wake, hawatawahi kupata jibu kamwe.
Katika ukuu wa Mungu, vitu vyote vinazaana, vinakuwepo, na kupotea kwa sababu ya mamlaka Yake na usimamizi Wake. Baadhi ya mambo huja na kwenda polepole, na binadamu hawezi kutambua ni wapi yalitokea au kung’amua sheria ambazo mambo haya hufuata, sisemi hata kuelewa sababu za mambo haya kuja na kwenda. Ingawaje binadamu anaweza kushuhudia, kusikia, au kupitia yote yanayotokea ulimwenguni; ingawa yote yanamhusu mwanadamu, na ingawa mwanadamu bila kujua anapitia hali isiyo ya kawaida, ukawaida, au hata ugeni wa matukio mbalimbali, bado hajui chochote kuhusu nia za Muumba na mawazo Yake yaliko nyuma ya mambo hayo yanayotokea katika ulimwengu. Kunazo hadithi nyingi zinazotokana na haya mambo yote, ukweli mwingi uliofichwa. Kwa sababu binadamu amepotoka na kwenda mbali na Muumba, kwa sababu hakubali hoja hii kwamba Mamlaka ya Muumba ndiyo hutawala mambo yote, hatawahi kujua kila kitu kinachofanyika katika ukuu Wake. Kwa sehemu nyingi zaidi, udhibiti na ukuu wa Mungu huzidi mipaka ya fikra ya binadamu, maarifa ya binadamu, kuelewa kwa binadamu, na kile ambacho sayansi ya binadamu inaweza kufikia; uwezo wa binadamu walioumbwa hauwezi kushindana nayo. Baadhi ya watu husema “Kwa sababu hujashuhudia ukuu wa Mungu wewe mwenyewe, unawezaje kusadiki kwamba kila kitu kinatokana na mamlaka Yake?” Kuona si kuamini kila mara; kuona si kutambua na kuelewa kila mara. Kwa hivyo imani inatoka wapi? Ninaweza kusema kwa uhakika, “Imani huja kutokana na kiwango na kina cha uelewa wa watu wa, na uzoefu wa, uhalisia na sababu za msingi za mambo.” Kama unasadiki kwamba Mungu yupo, lakini huwezi kutambua, na wala huwezi kuelewa, hoja ya udhibiti wa Mungu na ukuu wa Mungu katika mambo yote, basi katika moyo wako hutawahi kukubali kwamba Mungu anayo mamlaka kama haya na kwamba mamlaka ya Mungu ni ya kipekee. Hutawahi kukubali kwa kweli Muumba kuwa Bwana wako, Mungu wako.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 121)
Hatima ya Binadamu na Hatima ya Ulimwengu Haviwezi Kutenganishwa na Ukuu wa Muumba
Nyinyi nyote ni watu wazima. Baadhi yenu ni wa umri wa kati; baadhi mmefikisha umri wa uzee. Kutoka kwa yule asiyeamini hadi kwa yule anayeamini, na kuanzia mwanzo wa kumwamini Mungu hadi kukubali neno la Mungu na kuweza kupitia kazi ya Mungu, je, una kiwango gani cha maarifa kuhusu ukuu wa Mungu? Je, ni uelewa gani mlioupata kuhusu hatima ya mwanadamu? Je, mtu anaweza kutimiza kila kitu anachotamani katika maisha? Je, ni mambo mangapi kwenye miongo michache iliyopita katika kuwepo kwenu mliyoweza kutimiza kama mlivyopenda? Ni mambo mangapi hayafanyiki kama yalivyotarajiwa? Ni mambo mangapi hutupata kwa mshangao mzuri? Ni mambo mangapi ambayo ungali unasubiri yatimie—unasubiri bila kufahamu muda sahihi, unasubiria mapenzi ya Mbinguni? Mambo mangapi yanakufanya uhisi kana kwamba huna wa kukusaidia na umezuiliwa? Watu wote wanayo matumaini kuhusu hatima zao, na hutarajia kwamba kila kitu katika maisha yao kitaenda sawa na wanavyopenda, kwamba hawatakosa chakula wala mavazi, kwamba utajiri wao utaongezeka pakubwa. Hakuna anayetaka maisha ya kimaskini na ya taabu, yaliyojaa ugumu, na kuandamwa na majanga. Lakini watu hawawezi kuona mbele au kudhibiti mambo haya. Pengine kwa baadhi ya watu, yaliyopita ni mchanganyiko tu wa yale mambo waliyoyapitia; hawajifunzi katu ni nini mapenzi ya Mbinguni, wala hawajali mapenzi hayo ni yapi. Wanaishi kwa kudhihirisha maisha yao bila kufikiria, kama wanyama, wakiishi siku baada ya siku, bila kujali kuhusu hatima ya binadamu ni nini, kuhusu ni kwa nini binadamu wako hai au vile wanavyostahili kuishi. Watu hawa hufikia umri wa uzee bila ya kufaidi ufahamu wowote wa hatima ya binadamu, na mpaka wakati ule wanapokufa hawana habari yoyote kuhusu maana ya maisha. Watu kama hao wamekufa; ni viumbe bila roho; wao ni wanyama. Ingawaje katika kuishi miongoni mwa mambo haya yote, watu hupata furaha kutoka kwa njia nyingi ambazo ulimwengu hutosheleza mahitaji yao ya anasa, ingawaje wanauona ulimwengu huu wa anasa ukiwa unapiga hatua bila kusita, hali yao binafsi waliyoipitia—kile ambacho mioyo yao na roho zao zinahisi na kupitia—hakina uhusiano wowote na mambo ya anasa, na hakuna kitu chochote cha anasa ambacho kinaweza kuchukua nafasi yake. Ni utambuzi ulio ndani ya moyo wa mtu, kitu ambacho hakiwezi kuonekana kwa macho. Utambuzi huu upo katika ufahamu wa mtu wa, na hisia za mtu za, maisha ya mwanadamu na hatima ya mwanadamu. Na mara nyingi humwongoza mtu katika kuelewa kwamba Bwana yule asiyeonekana anapanga vitu vyote, Anaunda kila kitu kwa ajili ya binadamu. Katikati ya haya yote, mtu hawezi kuepuka ila kukubali mipangilio na mipango ya hatima ya mambo; wakati uo huo, mtu hawezi kuepuka ila kukubali njia iliyo mbele ambayo Muumba amempangia, ukuu wa Muumba dhidi ya hatima ya mtu. Hii ndiyo hoja isiyopingika. Haijalishi ni maono na mtazamo gani ambao mtu anao kuhusu hatima yake, hakuna anayeweza kubadilisha ukweli huu.
Pale utakapoenda kila siku, kile utakachofanya, yule au kile utakachokumbana nacho, kile utakachosema, kile kitakachokufanyikia—je, kati ya vyote hivi kipo kinachoweza kutabirika? Watu hawawezi kutabiri matukio haya yote, sikutajii kudhibiti namna ambavyo yanaendelea. Katika maisha, matukio haya yasiyotabirika hufanyika kila wakati, na ni tukio la kila siku. Mabadiliko haya ya kila siku na njia ambazo yanajitokeza, au mifumo inayofuata, ni vikumbusho vya kila wakati kwa binadamu kwamba hakuna kinachofanyika bila mpango, kwamba mchakato wa kutokea kwa kila tukio, na kutoepukika kwa mambo haya, haviwezi kubadilishwa na mapenzi ya binadamu. Kila tukio linaonyesha onyo kutoka kwa Muumba kwa mwanadamu, na pia linatuma ujumbe kwamba, binadamu hawawezi kudhibiti hatima zao wenyewe; na wakati uo huo kila tukio ni upingaji wa malengo yasiyo na mwelekeo, yasiyo na maana ya binadamu na tamanio la kuchukua hatima yake na kutaka kuidhibiti yeye mwenyewe kwa mikono yake. Ni sawa na makofi yenye nguvu juu ya masikio ya binadamu moja baada ya jingine, yanayomlazimisha binadamu kufikiria upya ni nani, hatimaye, anatawala na kudhibiti hatima zao. Na kama vile malengo na matamanio yao yanavyokiukwa mara kwa mara na kusambaratika, binadamu kwa kawaida huishia kukubali bila kujua kile ambacho hatima yao imehifadhi, kukubali uhalisia, kukubali mapenzi ya mbinguni, na kukubali ukuu wa Muumba. Kutokana na mabadiliko haya ya kila siku katika hatima za maisha yote ya binadamu, hakuna kitu ambacho hakifichui mipango ya Muumba na ukuu Wake; hakuna kile ambacho hakiutumi ujumbe huu kwamba “yale mamlaka ya Muumba hayawezi kupitwa,” ambacho hakionyeshi ukweli wa milele kwamba “mamlaka ya Muumba ni ya juu zaidi.”
Hatima za binadamu na zile za ulimwengu zimeingiliana kwa undani na ukuu wa Muumba, zimefungamanishwa na haziwezi kutenganishwa na mipango ya Muumba; na hatimaye, haziwezi kutenganishwa na mamlaka ya Muumba. Kupitia kwenye sheria za mambo yote binadamu huja kuelewa mipango ya Muumba na ukuu Wake; kupitia kwenye sheria za namna ya kuishi ambazo anaona katika utawala wa Muumba; kutoka kwenye hatima za mambo yote anapata hitimisho kuhusu njia ambazo Muumba huonyesha ukuu Wake na kuvidhibiti; na katika mizunguko ya maisha ya wanadamu na vitu vyote, mwanadamu kwa kweli huja kupitia ile mipango na mipangilio ya Muumba kwa mambo yote na kwa viumbe vyote vilivyo hai na anashuhudia kwa kweli namna ambavyo mipango na mipangilio hiyo inavyozidi sheria zote za nchi, kanuni, na taasisi, mamlaka na nguvu zingine zote. Kwa mujibu wa haya, binadamu wanashawishiwa kutambua kwamba, ukuu wa Muumba hauwezi kukiukwa na kiumbe chochote kilichoumbwa, kwamba hakuna nguvu zinazoweza kuharibu au kubadilisha matukio na mambo yaliyoamuliwa kabla na Muumba. Ni kupitia kwenye sheria na kanuni hizi takatifu ambapo binadamu na viumbe vyote wanaweza kuishi na kuzaliana, kizazi baada ya kizazi. Je, huu si mfano halisi wa mamlaka ya Muumba? Ingawaje binadamu huona, kwenye sheria zile za malengo, ukuu wa Muumba na utaratibu Wake wa matukio yote na mambo yote, je, ni watu wangapi wanaweza kung’amua kanuni ya ukuu wa Muumba juu ya ulimwengu? Ni watu wangapi wanaweza kujua, kutambua, kukubali kwa kweli na kujinyenyekeza katika ukuu na mpangilio wa Muumba dhidi ya hatima zao wenyewe? Nani, ambaye baada ya kusadiki hoja ya ukuu wa Muumba juu ya viumbe vyote, ataweza kusadiki kwa kweli na kutambua kwamba Muumba pia anaamrisha hatima hii ya maisha ya binadamu? Ni nani anayeweza kuelewa kwa kweli hoja hii kwamba hatima ya binadamu imo kwenye kiganja cha mkono wa Muumba? Ni aina gani ya mtazamo ambao binadamu wanafaa kuchukua katika ukuu wa Muumba, wanapokabiliwa na ukweli kwamba Anatawala na kudhibiti hatima ya binadamu, huu ni uamuzi ambao kila binadamu ambaye kwa sasa anakabiliwa na ukweli huu ni lazima ajiamulie mwenyewe.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 122)
Awamu Sita katika Maisha ya Binadamu
Katika mkondo wa maisha ya mtu, kila mtu hufikia kwenye misururu ya awamu muhimu. Hizi ni hatua za kimsingi zaidi, na muhimu zaidi, zinazoamua hatima ya maisha ya mtu. Kile kinachofuata ni ufafanuzi mfupi kuhusu hatua hizi muhimu ambazo kila mtu lazima apitie kwenye mkondo wa maisha yake.
Awamu ya Kwanza: Kuzaliwa
Mahali ambapo mtu amezaliwa, ni familia gani alimozaliwa, jinsia ya mtu, umbo la mtu, na wakati wa kuzaliwa—haya ndiyo maelezo ya awamu ya kwanza ya maisha ya binadamu.
Hakuna yeyote aliye na chaguo kuhusu sehemu hizi za awamu hii; zote ziliamuliwa kabla, mapema kabisa na Muumba. Haziathiriwi na mazingira ya nje kwa vyovyote vile, na hakuna masuala yanayosababishwa na binadamu yanaweza kubadilisha hoja hizi ambazo Muumba aliamua kabla. Kwa mtu kuweza kuzaliwa inamaanisha kwamba Muumba tayari ametimiza hatua ya kwanza ya hatima ambayo Amempangilia mtu huyo. Kwa sababu Aliamua kabla maelezo haya yote tena mapema mno, hakuna aliye na nguvu za kubadilisha maelezo yoyote yale. Licha ya hatima ya baadaye ya mtu, hali za kuzaliwa kwa mtu ziliamuliwa kabla, na zinabakia kama zilivyo; haziathiriwi kwa njia yoyote ile na hatima ya mtu katika maisha, wala haziathiri kwa vyovyote vile ukuu wa Muumba juu yazo.
1) Maisha Mapya Yanazaliwa Kulingana na Mipango ya Muumba
Ni maelezo yapi ya awamu ya kwanza—mahali mtu anapozaliwa, familia ya mtu, jinsia ya mtu, umbo la mwili wa mtu, muda wa kuzaliwa kwa mtu—ambayo mtu anaweza kuchagua? Bila shaka, kuzaliwa kwa mtu ni tukio asiloweza kuchagua: Mtu anazaliwa bila hiari yake, katika mahali fulani, muda fulani, kwenye familia fulani, akiwa na umbo fulani la kimwili; mtu anakuwa mmojawapo wa familia fulani bila hiari, anarithi kizazi fulani cha familia. Mtu hana chaguo kwenye awamu hii ya kwanza ya maisha, lakini anazaliwa kwenye mazingira yanayochaguliwa kulingana na mipango ya Muumba, kwenye familia mahususi, na jinsia na umbo mahususi, kwenye wakati mahususi ambao unaunganishwa kwa undani na mkondo wa maisha ya mtu huyu. Mtu anaweza kufanya nini katika awamu hii muhimu? Yote yakisemwa, kwa kweli mtu hana chaguo kuhusu maelezo yoyote yale yanayohusu kuzaliwa kwake. Kama isingekuwa kuamua kabla kwa Muumba na mwongozo Wake, mtu aliyezaliwa upya kwenye ulimwengu huu asingejua ni wapi atakapoenda au ni wapi atakapoishi, asingekuwa na mahusiano yoyote, asingekuwa na popote na asingekuwa na maskani yoyote halisi. Lakini kwa sababu ya mipangilio makinifu ya Muumba, anaanza safari ya maisha yake akiwa na mahali pa kuishi, wazazi, na mahali anapoita nyumbani na watu wa ukoo. Kotekote kwenye mchakato huu, mwanzo wa maisha haya mapya unaamuliwa na mipango ya Muumba, na kila kitu ambacho mtu huyu atakuja kumiliki ataweza kukabidhiwa na Muumba. Kutoka kwenye kiumbe kinachoelea kisichokuwa na jina lolote hadi kinapoanza kuwa na nyama na damu polepole, kinachoweza kuonekana, na hatimaye kuwa binadamu anayeweza kushikika, mmojawapo wa viumbe vya Mungu, anayefikiria, anayepumua, anayehisi joto na baridi, anayeshiriki katika shughuli za kawaida za kiumbe kilichoumbwa kwenye ulimwengu yakinifu na ambaye atapitia mambo haya yote ambayo kiumbe kilichoumbwa lazima kipitie maishani. Kule Kuamuliwa kabla kwa kuzaliwa kwa mtu na Muumba kunamaanisha kwamba ataweza kumpa mtu huyu mambo yote yanayohitajika kwa kuishi kwake; na kwamba mtu anazaliwa vilevile inamaanisha kwamba yeye atapokea mambo yote yanayohitajika kutoka kwa Muumba, kwamba kuanzia wakati ule kwenda mbele yeye ataishi katika umbo jingine, linalotolewa na Muumba na linalotii ukuu wa Muumba.
2) Kwa Nini Binadamu Tofauti Wanazaliwa Katika Hali Tofauti
Mara nyingi watu wanapenda kufikiria kwamba, kama wangezaliwa tena, wangezaliwa kwenye familia maarufu; kama wangekuwa wanawake, wangefanana na Binti wa Kifalme Anayependeza na wangependwa na kila mtu, na kama wangezaliwa wanaume, wangekuwa Kaka Mwenye Mvuto na Haiba, wasikose mahitaji yoyote, huku ulimwengu mzima ukiwaitikia mara moja kila unapoitwa na wao. Mara nyingi kuna wale walio na picha nyingi kuhusu kuzaliwa kwao na huwa hawajatosheka kabisa na huko kuzaliwa kwao, wanachukia familia zao, umbo lao, jinsia yao, na hata wakati wa kuzaliwa kwao. Ilhali watu hawajawahi kuelewa ni kwa nini wamezaliwa katika familia fulani au kwa nini wanafanana jinsi fulani. Hawajui kwamba, licha ya ni wapi wamezaliwa au ni vipi wanavyoonekana, wanafaa kuendeleza wajibu mbalimbali na kutimiza kazi maalum tofautitofauti katika usimamizi wa Muumba—kusudi hili halitawahi kubadilika. Ingawa katika macho ya Muumba, mahali anapozaliwa mtu, jinsia ya mtu, umbo la mwili wa mtu hivi vyote ni vitu vya muda. Ni misururu ya mambo madogomadogo katika kila awamu ya usimamizi Wake wa mwanadamu kwa ujumla. Na hatima halisi ya mtu na mwisho wake vyote haviamuliwi kutokana na wapi ambapo yeye amezaliwa katika awamu yoyote ile, lakini vinaamuliwa na kazi maalum ambayo yeye atatekeleza katika kila maisha, na kwa hukumu ya Muumba juu yao wakati mpango Wake wa usimamizi utakapokamilika.
Inasemekana kwamba kunayo sababu katika kila athari, na kwamba hakuna athari ambayo haina sababu. Na kwa hivyo kuzaliwa kwa mtu kumefungamanishwa haswa na maisha yake ya sasa na yale ya awali. Kama kifo cha mtu kinasitisha awamu yake ya sasa ya maisha, basi kuzaliwa kwa mtu ndio mwanzo wa mzunguko mpya; kama mzunguko wa kale unawakilisha maisha ya awali ya mtu, basi mzunguko huo mpya kwa kawaida ndio maisha yao ya sasa. Kwa sababu kuzaliwa kwa mtu kunaunganishwa na maisha ya kale ya mtu huyu pamoja na maisha ya sasa ya mtu huyu, basi mambo mbalimbali yanayohusiana na mahali alipozaliwa mtu huyo, familia, jinsia, umbo, na mambo mengine kama hayo ambayo yanahusishwa na kuzaliwa kwake, yote yanahusiana na maisha yake ya zamani na ya sasa. Hii inamaanisha kwamba, mambo mbalimbali yanayohusiana na kuzaliwa kwa mtu hayaathiriwi tu na maisha ya awali ya mtu, lakini yanaamuliwa na hatima ya mtu katika maisha ya sasa. Hii inaelezea mseto wa hali tofauti ambazo watu wanazaliwa: Baadhi wanazaliwa katika familia fukara, wengine katika familia tajiri. Baadhi wanazaliwa katika kundi la watu wa kawaida, wengine wanazaliwa katika ukoo wa kipekee. Baadhi wanazaliwa kusini, wengine wanazaliwa kaskazini. Baadhi wanazaliwa jangwani na wengine wanazaliwa katika ardhi zenye rutuba. Kuzaliwa kwa baadhi ya watu kunaandamana na vifijo, vicheko, na sherehe, wengine wanaleta machozi, janga, na matatizo. Baadhi wanazaliwa ili wathaminiwe, wengine wawekwe pembeni kama magugu. Baadhi wanazaliwa wakiwa na heshima na staha na wengine wanazaliwa wakiwa na mikosi na mikasa. Baadhi wanapendeza kuwatazama, na wengine wanatisha kuwatazama. Baadhi wanazaliwa usiku wa manane, wengine wanazaliwa chini ya jua kali la utosi. … Kuzaliwa kwa watu wa kila aina kunaamuliwa na hatima ambazo Muumba ameweka kwa ajili yao; kuzaliwa kwao kunaamua hatima zao katika maisha ya sasa pamoja na wajibu ambao wataendeleza na kazi maalum watakazotimiza. Yote haya yanategemea ukuu wa Muumba, ulioamuliwa kabla na Yeye; hakuna anayeweza kuepuka hatima hii iliyoamuliwa kabla, hakuna anayeweza kubadilisha kuzaliwa kwao, na hakuna anayeweza kuchagua hatima yake binafsi.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 123)
Awamu Sita katika Maisha ya Binadamu
Awamu ya Pili: Kukua
Kulingana na aina ya familia ambayo wamezaliwa ndani, watu hukua katika mazingira tofauti ya nyumbani na wakajifunza mafunzo tofauti kutoka kwa wazazi wao. Sababu hizi zinaamua hali ambazo mtu atakulia na kukua inawakilisha awamu ya pili muhimu ya maisha ya mtu. Inajulikana kwamba, watu hawana chaguo katika awamu hii, vilevile. Hii pia imepangwa, ilipangwa kabla.
1) Hali Ambazo Mtu Hukulia Ndani Zimepangwa na Muumba
Mtu hawezi kuchagua watu, matukio au vitu anavyoadilishwa na kushawishiwa navyo anapokua. Mtu hawezi kuchagua ni maarifa au mbinu gani atapata, ni tabia gani ataishia kuwa nayo. Mtu hana kauli kuhusiana na wazazi na watu wake wa ukoo, aina ya mazingira ambayo atakulia ndani; mahusiano yake na watu, matukio, na mambo yaliyo katika mazingira yake na namna yanavyoathiri maendeleo yake, vyote viko nje ya udhibiti wake. Ni nani anayeamua mambo haya, basi? Ni nani anayeyapangilia? Kwa sababu watu hawana chaguo katika suala hili, kwa vile hawawezi kuamua mambo haya wao wenyewe, na kwa sababu bila shaka hayajipangi yenyewe kwa kawaida, ni wazi kabisa kwamba kuundwa kwa watu, matukio na vitu hivi vyote kunategemea mikono ya Muumba. Bila shaka, kama vile tu Muumba anavyopanga hali fulani za kuzaliwa kwa kila mtu, Yeye hupangilia pia hali mahususi ambazo mtu hukulia. Ikiwa kuzaliwa kwa mtu kutaleta mabadiliko kwa watu, kwa matukio, na mambo yanayomzunguka yeye, basi kukua na maendeleo ya mtu huyo vyote vitaweza kuwaathiri vilevile. Kwa mfano, baadhi ya watu wanazaliwa katika familia fukara, lakini wanalelewa wakiwa wamezungukwa na utajiri; wengine wanazaliwa katika familia tajiri lakini husababisha utajiri wa familia zao kupungua, kiasi cha kwamba wanalelewa katika mazingira ya kimaskini. Hakuna mtu anayezaliwa chini ya sheria maalum, na hakuna anayelelewa katika hali zisizozuilika, na zisizobadilika. Haya si mambo ambayo binadamu anaweza kufikiria au kudhibiti; mambo haya yote ni mazao ya hatima ya mtu, na yanaamuliwa na hatima ya mtu. Bila shaka, kimsingi ni kwamba yote haya yaliamuliwa kabla katika hatima ya mtu na Muumba, yanaamuliwa na ukuu wa Muumba juu ya, na mipango Yake ya, hatima ya mtu huyu.
2) Hali Mbalimbali Ambazo Watu Hukulia Ndani Husababisha Wajibu Tofauti
Hali za kuzaliwa kwa mtu huanzisha katika kiwango cha kimsingi mazingira na hali ambazo atakulia ndani, na hali ambazo mtu hukulia ndani vilevile ni zao la hali za kuzaliwa kwake. Kwenye wakati huu mtu anaanza kujifunza lugha, na akili za mtu zinaanza kukumbana na kuchanganua mambo mengi mapya, na katika mchakato huu mtu anakua bila kusita. Mambo ambayo mtu anasikia kwa masikio yake, anaona kwa macho yake, na anang’amua kwa akili zake huboresha na kuhuisha kwa utaratibu ulimwengu wa ndani wa mtu. Watu, matukio, na mambo ambayo mtu anakumbana nayo, akili ya kawaida, maarifa, na mbinu anazojifunza, na njia za kufikiria ambazo mtu anaathiriwa nazo, anaambiwa au kufunzwa, vyote vitamwongoza na kuathiri hatima ya maisha yake. Lugha anayojifunza mtu anapokua na njia yake ya kufikiria haviwezi kutenganishwa kutoka kwenye mazingira ambayo yeye analelewa katika ujana wake, na hayo mazingira yana wazazi, ndugu zake, na watu wengine, matukio, na mambo yanayomzunguka. Kwa hivyo mkondo wa maendeleo ya mtu unaamuliwa na mazingira ambayo yeye anakulia ndani, na pia unategemea watu, matukio, na mambo ambayo mtu anakumbana nayo kwenye kipindi hiki cha muda. Kwa sababu masharti ambayo mtu hukulia ndani yaliamuliwa kabla na tena mapema mno, mazingira anayoishi kwenye mchakato huu pia, kwa kawaida, yaliamuliwa kabla. Hayaamuliwi na chaguo na mapendeleo ya mtu, lakini yanaamuliwa kulingana na mipango ya Muumba, yanaamuliwa na mipangilio makinifu ya Muumba, na ukuu wa Muumba juu ya hatima ya mtu huyo katika maisha. Kwa hivyo watu ambao mtu yeyote hukumbana nao katika mkondo wa kukua, na mambo ambayo mtu hukutana nayo, vyote vimeunganishwa bila kuzuilika kwa mipango na mipangilio ya Muumba. Watu hawawezi kutabiri aina hizi za mahusiano yaliyo magumu kuelezeka, wala hawawezi kuyadhibiti au kuweza kuyaelewa. Mambo mengi tofauti na watu wengi tofauti wanao mwelekeo wa mazingira ambayo mtu hukulia, na hakuna binadamu anayeweza kupangilia na kupanga mtandao mpana kama huo wa muunganisho. Hakuna mtu au kitu isipokuwa Muumba anayeweza kudhibiti kujitokeza, kuwepo, na kutoweka kwa watu mbalimbali, matukio na mambo, na ni mtandao mpana ajabu wa muunganisho unaounda maendeleo ya mtu kama ilivyoamuliwa kabla na Muumba, na kuunda mazingira tofauti ambayo watu wanakulia ndani, na kuunda wajibu mbalimbali unaohitajika kwa minajili ya kazi ya Muumba ya usimamizi, kuweka misingi thabiti, yenye nguvu ili watu waweze kukamilisha kwa ufanisi kazi yao maalum.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 124)
Awamu Sita katika Maisha ya Binadamu
Awamu ya Tatu: Uhuru
Baada ya mtu kupitia utoto na wakati wake wa kubaleghe na kwa utaratibu bila kuzuilika kufikia ukomavu, hatua inayofuata ni kwake yeye kuachana kabisa na ujana wake, kuwaaga wazazi wake, na kukabiliana na barabara iliyo mbele yake akiwa mtu mzima huru. Wakati huo, lazima wakabiliane na watu, matukio na mambo yote ambayo mtu mzima lazima apitie, na kukabiliana na sehemu zote za hatima yake ambazo zitajiwasilisha hivi karibuni. Hii ndiyo awamu ya tatu ambayo lazima mtu apitie.
1) Baada ya Kuwa Huru, Mtu Huanza Kupitia Ukuu wa Muumba
Kama kuzaliwa kwa mtu na kulelewa kwake ni “kipindi cha matayarisho” katika safari ya mtu maishani, kuweka lile jiwe la msingi katika hatima ya mtu, basi uhuru wa mtu ndio ufunguzi wa pekee wa hatima ya maisha ya mtu. Kama kuzaliwa na kukua kwa mtu ni utajiri ambao wameweza kulimbikiza kwa minajili ya hatima yao maishani, basi uhuru wa mtu huyo unaanza wakati ule wanaanza kutumia au kuongeza utajiri huo. Wakati mtu anawaacha wazazi na kuwa huru, masharti ya kijamii ambayo anakabiliana nayo, na aina ya kazi na ajira inayopatikana kwa mtu, vyote vinaamriwa na hatima na havina uhusiano wowote na wazazi wa mtu. Baadhi ya watu huchagua kozi nzuri chuoni na kuishia kupata kazi ya kuridhisha baada ya kuhitimu, na hivyo basi kupiga hatua ya kwanza ya mafanikio katika safari yao ya maisha. Baadhi ya watu hujifunza na kumiliki ujuzi mwingi wa aina tofauti na kamwe hawapati kazi ambayo inawafaa au kupata vyeo vyao, sembuse kuwa na ajira yoyote; wakati wa safari ya maisha yao wanajipata wakiwa wamewekewa vipingamizi katika kila kona, wameandamwa na matatizo, matumaini yao madogo na maisha yao hayana uhakika. Baadhi ya watu wanatia bidii katika masomo yao, ilhali wanakosa kwa karibu sana fursa zao zote za kupokea elimu ya juu zaidi, na wanaonekana kuwa na hatima ya kutoweza kupata mafanikio, matamanio yao ya kwanza kabisa katika safari yao ya maisha yalitowekea tu hewani. Bila kujua kama barabara iliyo mbele ni laini au yenye miamba, wanahisi kwa mara ya kwanza namna ambavyo hatima ya binadamu imejaa vitu vya kubadilikabadilika, na wanachukulia maisha kwa tumaini na hofu. Baadhi ya watu, licha ya kutokuwa na elimu nzuri sana, huandika vitabu na kutimiza kiwango cha umaarufu; baadhi, ingawaje hawajui kusoma na kuandika sana, huunda pesa katika biashara na hivyo basi wanaweza kujikidhi…. Kazi anayochagua mtu, namna mtu anavyopata riziki: je, watu wanao udhibiti wowote kuhusu, kama wanaweza kufanya uchaguzi mzuri au uchaguzi mbaya? Je, yanapatana na matamanio na uamuzi wao? Watu wengi zaidi wanatamani wangeweza kufanya kazi kidogo na kupata mapato mengi zaidi, wasitie bidii sana katika jua na mvua, wavae vizuri, wameremete na kung’aa wakiwa kila pahali, wawe juu sana kuliko wengine kwa uwezo, na kuleta heshima kwa mababu zao. Matamanio ya watu ni kamilifu sana, lakini wakati ambao watu wanachukua hatua zao za kwanza katika safari ya maisha yao, polepole wanakuja kutambua jinsi ambavyo hatima ya mwanadamu si kamilifu, na kwa mara ya kwanza wanafahamu ukweli kwamba, ingawa mtu anaweza kufanya mipango thabiti kwa ajili ya maisha yake yajayo, ingawa mtu anaweza kuhodhi ndoto za kijasiri, hakuna yule aliye na uwezo au nguvu za kutambua ndoto zake mwenyewe, hakuna yule aliye katika hali ya kudhibiti mustakabali wake. Siku zote kutakuwepo na umbali fulani kati ya ndoto za mtu na uhalisia ambao lazima mtu akabiliane nao; mambo siku zote hayawi vile ambavyo mtu angetaka yawe, na watu wanapokumbwa na uhalisi kama huu hawawezi kutimiza hali ya kutosheka au kuridhika. Baadhi ya watu wataenda hadi kiwango chochote cha kufikirika, wataweza kutia bidii za kipekee na kujitolea pakubwa kwa minajili ya riziki na mustakabali wao, katika kujaribu kubadilisha hatima yao wenyewe. Lakini hatimaye, hata kama wataweza kutambua ndoto na matamanio yao kupitia kwa njia ya bidii yao wenyewe, hawawezi kubadilisha hatima zao, na haijalishi watajaribu vipi kwa njia ya ukaidi hawatawahi kuzidi kile ambacho hatima yao imewapangia. Licha ya tofauti katika uwezo, kiwango cha akili, na hiari ya kutenda, watu wote ni sawa mbele ya hatima, jambo ambalo halileti tofauti kati ya wakubwa na wadogo, wale wa kiwango kile cha juu na cha chini, wanaotukuzwa na wakatili. Ile kazi ambayo mtu anafuatilia, kile anachofanya mtu ili kupata riziki, na kiasi gani cha mali anachokusanya maishani hakiamuliwi na wazazi wa mtu, vipaji vya mtu, jitihada za mtu au malengo ya mtu, vyote vinaamuliwa kabla na Muumba.
2) Kuwaacha Wazazi wa Mtu na Kuanza kwa Bidii Kuendeleza Wajibu Wako Kwenye Ukumbi wa Sanaa wa Maisha
Wakati mtu anapofikia ukomavu, mtu anaweza kuacha wazazi wake na kutoka nje kwenda kuanza kujitegemea yeye mwenyewe na ni katika wakati huu ambapo mtu huanza kwa kweli kuonyesha wajibu wake binafsi, kwamba kazi maalum ya mtu maishani inaacha kuwa ya kutoeleweka na polepole kuanza kuwa wazi. Kimsingi mtu huyo bado huonyesha uhusiano wa karibu na wazazi wake, lakini kwa sababu kazi yake maalum na wajibu anaoendeleza katika maisha huwa hauna uhusiano wowote na mama na baba wa mtu huyo, kwa hakika uhusiano huu wa karibu huvunjika polepole kwa kadiri ambavyo mtu anazidi kuendelea kuwa huru. Kutoka katika mtazamo wa kibiolojia, watu bado hawana budi kutegemea wazazi katika njia za kufichika akilini, lakini kwa kusema ukweli, mara tu wanapokuwa watu wazima wanakua na maisha tofauti kabisa na yale ya wazazi wao, na wataweza kutekeleza wajibu watakaoamua kufanya kwa uhuru wao. Mbali na kuwazaa na kuwalea watoto, jukumu la kila mzazi katika maisha ya mtoto ni kuweza kuwapatia tu mazingira rasmi ya kukulia ndani, kwa maana hakuna kingine chochote isipokuwa kule kuamuliwa kabla kwa Muumba ambako kunachukua mwelekeo katika hatima ya mtu huyu husika. Hakuna anayeweza kudhibiti ni mustakabali gani ambao mtu atakuwa nao; huwa umeamuliwa kabla na mapema sana, na hata wazazi wa mtu hawawezi kubadilisha hatima yake. Kulingana na mambo ya hatima, kila mtu yuko huru na kila mtu anayo hatima yake. Kwa hivyo hakuna wazazi wa mtu yeyote wanaoweza kuiondoa hatima ya mtu katika maisha au kusisitizia ushawishi wowote ule mdogo katika wajibu ambao mtu huendeleza maishani. Inaweza kusemekana kwamba, familia ambayo mtu ameamuliwa kuzaliwa ndani, na mazingira ambayo mtu atakulia ndani, ni yale masharti ya awali ya kutimiza kazi maalum ya mtu maishani. Yote haya hayaamui kwa vyovyote vile hatima ya mtu katika maisha au aina ya hatima ambayo mtu huyo atatimiza katika kazi yake maalum. Na kwa hivyo hakuna wazazi wa mtu yeyote yule wanaweza kusaidia katika kutimiza kazi hii maalum katika maisha, hakuna watu wowote wa ukoo wanaoweza kumsaidia mtu kuchukua wajibu huu katika maisha. Vile ambavyo mtu hutimiza kazi yake maalum na katika aina gani ya mazingira ya kuishi ambayo mtu hutekeleza wajibu wake, vyote vinaamuliwa na hatima ya mtu maishani. Kwa maneno mengine, hakuna masharti mengine yoyote yanayoweza kuathiri kazi maalum ya mtu, ambayo imeamuliwa kabla na Muumba. Watu wote hukomaa katika mazingira yao binafsi ya kukulia, na kisha kwa taratibu, hatua kwa hatua, huanza safari katika barabara zao binafsi za maisha, hutimiza hatima walizopangiwa na Muumba, kwa kawaida, bila hiari wao huingia katika bahari kubwa ya binadamu na kuchukua nafasi zao binafsi katika maisha, pale ambapo wao huanza kutimiza majukumu yao kama viumbe vilivyoumbwa kwa minajili ya kuamuliwa kabla kwa Muumba, kwa minajili ya ukuu Wake.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 125)
Awamu Sita katika Maisha ya Binadamu
Awamu ya Nne: Ndoa
Kadiri mtu anavyokua na kukomaa, ndivyo anavyozidi kuwa mbali na wazazi wake na mazingira ambayo amezaliwa na kulelewa, na badala yake mtu huanza kutafuta mwelekeo wa maisha yake na kufuatilia shabaha binafsi kwa njia ya maisha iliyo tofauti na ile ya wazazi. Kwenye kipindi hiki cha muda mtu hahitaji tena wazazi wake, bali mwandani ambaye anaweza kuishi naye katika maisha yake: mwenza, ni mtu ambaye hatima ya mtu imefungamanishwa naye kwa karibu. Kwa njia hii, tukio kuu ambalo mtu hukabiliana nalo kufuatia uhuru wake ni ndoa, awamu ya nne ambayo lazima mtu apitie.
1) Mtu Hana Chaguo Kuhusu Ndoa
Ndoa ni tukio muhimu katika maisha ya mtu yeyote; ni wakati ule ambao mtu huanza kwa kweli kuendeleza aina mbalimbali za majukumu, huanza kwa utaratibu kutimiza aina mbalimbali za kazi maalum. Watu huwa na picha nyingi kuhusu ndoa kabla ya kuipitia wao wenyewe, na picha hizi zote ni nzuri. Wanawake hufikiria kwamba waume wao watakuwa Kaka Mwenye Mvuto na Haiba, nao wanaume hufikiria kwamba wataweza kuoa Binti wa Kifalme Anayependeza. Kubuni huku kwa mawazo kunaonyesha kwamba kila mtu anayo mahitaji fulani ya ndoa, orodha fulani ya kile anachohitaji na viwango anavyopenda. Ingawaje katika enzi hii ya maovu watu wanaambiwa kila mara kuhusu ujumbe uliopotoka juu ya ndoa, hali ambayo husababisha hata mahitaji mengi zaidi, pamoja na kupatia watu aina zote za mizigo na mitazamo isiyo ya kawaida, mtu yeyote aliyepitia ndoa anajua kwamba haijalishi ni kiasi kipi ambacho mtu ataielewa, haijalishi pia mtu anao mtazamo gani katika ndoa hiyo, ndoa si suala la chaguo la mtu binafsi.
Mtu hukumbana na watu wengi katika maisha yake, lakini hakuna anayejua ni nani atakayekuwa mwandani wake katika ndoa. Ingawaje kila mtu anazo fikira zake binafsi na mtazamo wake wa kibinafsi kuhusu suala la ndoa, hakuna anayeweza kuona mbele na kujua ni nani atakayekuwa mwandani wake wa kweli hatimaye, na fikira za mtu huwa zinachangia kidogo sana. Baada ya kukutana na mtu unayempenda, unaweza kumfuatilia mtu huyo; kama mtu huyo amevutiwa na wewe au la, kama mtu huyo anaweza kuwa mwandani wako au la, hilo si la kwako kuamua. Kiini cha mahaba yenu si haswa mtu ambaye utaweza kuishi naye katika maisha yako; na huku haya yakiendelea mtu ambaye hukuwahi kumtarajia anaingia katika maisha yako na kuwa mwandani wako, anakuwa msingi muhimu sana katika hatima yako, nusu yako ile nyingine, ambaye hatima yako imefungamanishwa naye ajabu. Na kwa hiyo, ingawaje kunazo ndoa milioni kwa milioni ulimwenguni, kila ndoa ni tofauti: Ni ndoa ngapi ambazo hazitoshelezi, ni ngapi zinayo furaha; ni ngapi zinazopatikana Mashariki na Magharibi, ni ngapi Kaskazini na Kusini; ni ngapi ambazo wanandoa wanafaa na wameendana, na ni ngapi ambazo wanandoa wana mwonekano bora ni ngapi zenye furaha na utulivu, ni ngapi zenye maumivu na huzuni; ni ngapi zinaonewa wivu na wengine, na ni ngapi hazieleweki na hazipendelewi kabisa; ni ngapi zimejaa furaha, na ni ngapi zimejaa machozi na zinakatisha tamaa…. Kwenye ndoa hizi zote, binadamu wanafichua utiifu na kujitolea kwa maisha katika ndoa hizo, au pendo, au mshikamano, na hali ya kutotenganishwa, au kukata tamaa na kutoeleweka, au usaliti, au hata chuki. Haijalishi kama ndoa inaleta furaha au maumivu, kazi maalum ya kila mmoja katika ndoa iliamuliwa kabla na Muumba na haitabadilika; kila mmoja lazima aitimize. Na hatima ya kila mtu iliyopo nyuma ya kila ndoa haibadiliki; iliamuliwa kitambo naye Muumba.
2) Ndoa Inazaliwa Kutokana na Hatima ya Wandani Wote Wawili
Ndoa ni awamu muhimu katika maisha ya mtu. Ni zao la hatima ya mtu, kiungo muhimu katika hatima ya mtu; haiundwi kwa misingi ya uamuzi wa mtu yeyote binafsi au mapendeleo yake, na haiathiriwi na mambo yoyote ya nje, lakini inaamuliwa kabisa na hatima za wandani wawili, kupitia kwa mipangilio ya Muumba na kuamuliwa kabla kwa Muumba kuhusiana na hatima za wanandoa hao. Ukiangalia juujuu, kusudi la ndoa ni kuendeleza kizazi cha binadamu, lakini kwa kweli ndoa si chochote ila ni utaratibu ambao mtu anapitia katika mchakato wa kutimiza kazi yake maalum. Wajibu mbalimbali ambao watu huendeleza katika ndoa si ule tu wa kuleta kizazi kinachofuata; kunao wajibu mbalimbali ambao mtu huwa anao na kazi maalum ambazo mtu lazima atimize kwenye mkondo wa kuendeleza ndoa. Kwa sababu kuzaliwa kwa mtu huathiri mabadiliko ya watu, matukio, na mambo yanayomzunguka, ndoa ya mtu itaweza pia kuathiri bila shaka watu hao, na zaidi itawabadilisha kwa njia tofauti.
Wakati mtu anapokuwa huru, mtu huanza safari yake binafsi ya maisha, inayoongoza mtu hatua kwa hatua kuelekea kwa watu, na kwa matukio, na kwa vitu vinavyohusiana na ndoa ya mtu; na wakati uo huo, yule mtu mwingine atakayeunda ile ndoa anakaribia, hatua kwa hatua, kuelekea watu hao hao, matukio na hata mambo. Kwenye ukuu wa Muumba, watu wawili wasiohusiana walio na hatima inayohusiana wanaingia kwa utaratibu kwenye ndoa na kuwa, kimiujiza, familia, “nzige wawili wanaoshikilia kamba moja.” Kwa hivyo mtu anapoingia kwenye ndoa, safari ya mtu katika maisha itaathiri na kumgusa yule mwenzake, na vilevile safari ya mwandani katika maisha itashawishi na kugusa hatima ya yule mwenzake katika maisha. Kwa maneno mengine, hatima za wanadamu zimeingiliana na hakuna yule anayeweza kutimiza kazi yake maalum maishani au kutekeleza wajibu wake kabisa akiwa huru mbali na wengine. Kuzaliwa kwa mtu kunao mwelekeo kwa msururu mkubwa wa mahusiano; kukua pia kunahusisha msururu mkubwa wa mahusiano; na vilevile, ndoa inakuwepo bila shaka na kuendelezwa katika mtandao mpana na mgumu wa miunganisho ya binadamu, ikihusisha kila mwanachama na kuathiri hatima ya kila mmoja ambaye ni sehemu yake. Ndoa si mazao ya familia za wanachama wale wawili, hali ambazo wao walilelewa, maumbo yao, umri wao, ubora wao, vipaji vyao, au mambo mengine yoyote; badala yake, inatokana na kazi maalum ya pamoja na hatima inayohusiana. Hii ndiyo asili ya ndoa, zao la hatima ya binadamu lililopangwa na lililopangiliwa na Muumba.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 126)
Awamu Sita katika Maisha ya Binadamu
Awamu ya Tano: Uzao
Baada ya kuoa, mtu anaanza kulea kizazi kijacho. Mtu hana uwezo wa kujua atakuwa na watoto wangapi na watoto hawa watakuwa wa aina gani; hili pia linaamuliwa na hatima ya mtu, iliyoamuliwa kabla na Muumba. Hii ndiyo awamu ya tano ambayo lazima mtu apitie.
Ikiwa mtu amezaliwa ili kutimiza wajibu wake akiwa mwana wa binadamu, basi kulea kizazi kijacho ni kutimiza wajibu wake akiwa kama mzazi wa mwingine. Mabadiliko haya ya majukumu yanamruhusu mtu apate uzoefu wa awamu tofauti za maisha kutoka kwa mitazamo tofauti. Pia yanampa mtu uzoefu tofauti wa mambo mbalimbali katika maisha, ambapo mtu anakuja kujua ukuu ule wa Muumba, pamoja na ukweli kwamba hakuna mtu anayeweza kuzidi au kubadilisha kile ambacho Muumba aliamua kabla.
1) Mtu Hana Udhibiti wa Hatima ya Uzao Wake
Kuzaliwa, kukua, na kuoa ni awamu ambazo zinaleta aina tofauti na viwango tofauti vya masikitiko. Baadhi ya watu hawatosheki na familia zao au maumbile yao ya kimwili; baadhi hawapendi wazazi wao; baadhi wanachukia au wanalalamikia mazingira ambayo walikulia ndani. Na kwa baadhi ya watu wengi, miongoni mwa masikitiko haya yote, ndoa ndiyo ambayo haitoshelezi zaidi. Licha ya vile ambavyo unayo masikitiko kwa kuzaliwa kwako, au kukua kwako, au ndoa yako, kila mmoja ambaye amepitia awamu hizi amejua kwamba hawezi kuchagua ni wapi au ni lini alizaliwa, ni vipi anavyofanana, wazazi wake ni nani, na mume au mke wake ni nani, lakini wanaweza kukubali tu mapenzi ya Mbinguni. Lakini wakati wa watu kulea kizazi kijacho unapowadia, wataweza kuweka matamanio yao yote ambayo hayajatimizwa katika nusu ya kwanza ya maisha yao kwenye vizazi vyao, wakitumai kwamba, uzao wao utajaliza sehemu ile ambayo wao wamepitia masikitiko, kwenye nusu ile ya kwanza ya maisha yao. Kwa hivyo watu hujihusisha katika kutunga taswira za aina zote kuhusu watoto wao: kwamba binti zao watakua na kuwa warembo ajabu, watoto wao wa kiume watakuwa wanaume wa kipekee; kwamba binti zao watakuwa na maadili na wenye vipaji nao watoto wao wa kiume watakuwa wanafunzi werevu, na wanariadha wa kusifika; na kwamba binti zao watakuwa watulivu na waadilifu, wenye busara, kwamba watoto wao wa kiume watakuwa wenye akili, wenye uwezo na wanaojali. Wanatumai kwamba wawe watoto wa kike au wa kiume wataheshimu wazee wao, watajali wazazi wao, watapendwa na kusifiwa na kila mmoja…. Kufikia hapa matumaini ya maisha yanajitokeza upya, na matamanio mapya yanapata nguvu katika mioyo ya watu. Watu wanajua kwamba hawana nguvu na tumaini katika maisha haya, kwamba hawatakuwa na fursa nyingine, tumaini jingine, la kujitokeza mbele ya watu, na kwamba hawana chaguo lolote ila kukubali hatima zao. Na kwa hivyo wanaelekeza matumaini yao yote, matamanio na maadili yao ambayo hayajatimizwa, hadi kwenye kizazi kijacho, wakitumai uzao wao unaweza kuwasaidia kutimiza ndoto zao na kutambua matamanio yao; na kwamba binti zao na watoto wao wa kiume wataleta utukufu katika jina la familia, kuwa muhimu, kuwa matajiri au maarufu; kwa ufupi, wanataka kuona bahati za watoto wao zikizidi kuongezeka. Mipango na taswira za watu ni timilifu; Je, hawajui kwamba idadi ya watoto walio nao, umbo lao, uwezo wao na kadhalika, si juu yao kuamua, kwamba hatima za watoto wao hazimo kamwe katika viganja vya mikono yao? Binadamu si waendeshaji wa hatima zao binafsi, ilhali wanatumai kubadilisha hatima ya kizazi kichanga zaidi; hawana nguvu za kutoroka hatima zao wenyewe, ilhali, wanajaribu kudhibiti zile za watoto wao wa kiume ni wa kike. Je, hawazidishi ukadiriaji wao? Je, huu si ujinga na hali ya kutojua kwa upande wa binadamu? Watu huenda kwa mapana yoyote kwa minajili ya uzao wao, lakini hatimaye, idadi ya watoto aliyonayo mtu, na vile ambavyo watoto wake walivyo, si jibu la mipango na matamanio yao. Baadhi ya watu hawana hela lakini wanazaa watoto wengi; baadhi ya watu ni matajiri ilhali hawana mtoto. Baadhi wanataka binti lakini wananyimwa tamanio hilo; baadhi wanataka mtoto wa kiume lakini wanashindwa kuzaa mtoto wa kiume. Kwa baadhi, watoto ni baraka; kwa wengine, mtoto ni laana. Baadhi ya wanandoa ni werevu, ilhali wanawazaa watoto wanaoelewa polepole; baadhi ya wazazi ni wenye bidii na waaminifu, ilhali watoto wanaowalea ni wavivu. Baadhi ya wazazi ni wapole na wanyofu lakini wana watoto wanaogeuka na kuwa wajanja na wenye chuki. Baadhi ya wazazi ni wazima kiakili na kimwili lakini wanajifungua watoto walemavu. Baadhi ya wazazi ni wa kawaida na hawajafanikiwa ilhali watoto wao wanafanikiwa pakubwa. Baadhi ya wazazi ni wa hadhi ya chini ilhali watoto wanaowalea ni wenye taadhima. …
2) Baada ya Kulea Kizazi Kijacho, Watu Wanapata Ufahamu Mpya Kuhusu Hatima
Watu wengi wanaooa hufanya hivyo karibu kwenye umri wa miaka thelathini, na kwa wakati huu wa maisha, mtu hana ufahamu wowote wa hatima ya binadamu. Lakini wakati watu wanapoanza kulea watoto, kwa kadri uzao wao unapokua, wanatazama kizazi kipya kikirudia maisha na hali zote walizopitia katika kizazi kilichopita, na wanaona maisha yao ya kale yakijionyesha kwao na wanatambua kwamba barabara inayotumiwa na kizazi kile kichanga zaidi, kama tu yao, haiwezi kupangwa wala kuchaguliwa. Wakiwa wamekabiliwa na hoja hii, hawana chaguo lolote bali kukubali kwamba hatima ya kila mtu iliamuliwa kabla; na bila ya hata kutambua wanaanza kwa utaratibu kuweka pembeni matamanio yao binafsi, na hisia kali katika mioyo yao inapungua na kuwatoka…. Kwenye kipindi hiki cha muda, mtu ameweza kupita sehemu nyingi zaidi na muhimu katika mafanikio ya maisha yake na ametimiza ufahamu mpya wa maisha, na kuchukua mtazamo mpya. Je, mtu wa umri huu anaweza kutarajia kwa siku za usoni kiasi kipi cha mambo na ni matarajio yapi wanayoyatazamia? Ni mwanamke yupi mwenye umri wa miaka hamsini angali anaota kuhusu Kaka Mwenye Mvuto na Haiba? Ni mwanamume yupi wa miaka hamsini angali anatafuta Binti wa Kifalme Anayependeza? Ni mwanamke yupi wa umri wa kati atakuwa anatumai kugeuka kutoka kwa mtoto wa bata mwenye sura mbaya hadi kuwa batamaji? Je, wanaume wazee zaidi wangali wana msukumo sawa wa ajira na wanaume vijana? Kwa ujumla, haijalishi kama mtu ni mwanamume au mwanamke, yeyote anayeishi na kuufikia umri huu anao uwezekano wa kuwa na mtazamo unaofaa kwa kiasi fulani, utakaoweza kutumika kwenye ndoa, familia, na watoto. Mtu kama huyo, kimsingi hana chaguo zozote zilizobakia, hana msukumo wowote wa kukabiliana na hatima yake. Kwa mujibu wa kile ambacho binadamu amepitia, punde tu mtu anapofikia umri huu mtu huanza kwa kawaida kuwa na mtazamo kwamba “lazima mtu akubali hatima yake; watoto wa mtu wana majaliwa yao binafsi binafsi; hatima ya binadamu Imepangwa na Mbingu.” Watu wengi ambao hawaelewi ukweli, baada ya kupitia mabadiliko, mahangaiko, na ugumu wote wa ulimwengu huu, watatoa muhtasari wa utambuzi wao wa maisha ya binadamu kwa maneno matatu: “Hiyo ndiyo hatima!” Ingawaje kauli hii inatoa muhtasari wa hitimisho ya watu wa ulimwengu na utambuzi kuhusu hatima ya binadamu, ingawaje inaelezea kutoweza kusaidika kwa binadamu na inaweza kusemekana kwamba inapenyeza na ni sahihi, ni kilio cha mbali kutoka kwa ufahamu wa ukuu wa Muumba, na haichukui nafasi ya maarifa ya mamlaka ya Muumba.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 127)
Kusadiki Katika Hatima si Mbadala wa Maarifa ya Ukuu wa Muumba
Baada ya kuwa wafuasi wa Mungu kwa miaka mingi, je, kunayo tofauti kubwa katika maarifa yenu ya hatima na yale ya watu wa ulimwengu? Je, mmeelewa kwa kweli kule kuamuliwa kabla kwa Muumba, na unaweza kujua kwa kweli ukuu wa Muumba? Baadhi ya watu wanao ufahamu wa kina, na hisia za ndani za kauli hii “hii ndiyo hatima,” ilhali hawasadiki hata kidogo katika ukuu wa Mungu, hawasadiki kwamba hatima ya binadamu hupangiliwa na kuratibiwa na Mungu, na hawako radhi kunyenyekea mbele ya ukuu wa Mungu. Watu kama hao ni kana kwamba wanaelea baharini, wanatoswatoswa na mawimbi, huku wakielea na kufuata mkondo wa maji, wasiwe na chaguo ila kusubiri kimyakimya na kuachia maisha yao hatima. Hata hivyo hawatambui kwamba hatima ya binadamu inategemea ukuu wa Mungu; hawawezi kwa hiari yao wenyewe kuutambua ukuu wa Mungu, na hivyo kupata ufahamu wa mamlaka ya Mungu, kunyenyekea katika mipango na mipangilio ya Mungu, kuacha kukinzana na hatima na kuishi katika utunzwaji, ulinzi na mwongozo wa Mungu. Kwa maneno mengine, kukubali hatima si jambo sawa na kunyenyekea kwa ukuu wa Muumba; kusadiki katika hatima haimaanishi kwamba mtu anakubali, anatambua, na anajua ukuu wa Muumba; kusadiki katika hatima ni ule utambulisho wa hoja hii na suala hili la nje, ambalo ni tofauti na kujua namna Muumba Anavyotawala hatima ya binadamu, kuanzia katika kutambua kwamba Muumba ndiye chanzo cha kutawala juu ya hatima za mambo yote na hata zaidi kunyenyekea kwa mipango na mipangilio ya Muumba kwa ajili ya hatima ya binadamu. Tuseme kwamba mtu anaamini tu katika hatima, na hata anahisi kwa undani kuihusu, lakini kwa sababu hiyo hawezi kujua na kukubali mamlaka ya Muumba juu ya hatima za watu, kuyatii na kuyakubali. Katika hali hiyo, maisha yake yatakuwa ya kusikitisha; bila shaka yatakuwa yameishiwa bure, yatakuwa utupu. Bado hataweza kutii utawala wa Muumba, kuwa mwanadamu aliyeumbwa kwa maana halisi ya neno hilo, na kupata utambuzi wa Muumba. Mtu anayejua na kupitia mamlaka ya Muumba kwa kweli anapaswa kuwa katika hali chanya, si katika hali ambayo ni hasi au ya kukata tamaa. Huku akitambua kwamba haya yote yamepangwa, moyoni mwake anamiliki ufafanuzi sahihi wa maisha na hatima, ambao ni kwamba maisha yote ya mwanadamu yako chini ya mamlaka ya Muumba. Anapotazama nyuma kwenye njia aliyoitembea, anapokumbuka kila awamu ya safari yake ya maisha, anaona kwamba katika kila hatua, iwe kwamba safari yake ilikuwa ngumu au laini, Mungu alikuwa akiiongoza njia yake, Akiipanga kwa ajili yake. Anaelewa kwamba ilikuwa ni mipango ya Mungu ya uangalifu, pamoja na mipango Yake makini, iliyowaongoza, bila kujua, hadi kufikia leo. Anatambua kwamba kuweza kukubali mamlaka ya Muumba, kukubali wokovu Wake, ndiyo baraka kubwa zaidi katika maisha ya mtu! Kama mtu ana mtazamo hasi kuelekea hatima, inathibitisha kwamba anapinga kila kitu ambacho Mungu amempangia, kwamba hana mtazamo wa utiifu. Iwapo mtu ana mtazamo chanya kuelekea mamlaka ya Mungu juu ya hatima ya mwanadamu, basi anapotazama nyuma kwenye safari yake, anapopitia mamlaka ya Mungu kweli, atatamani zaidi kutii kila kitu ambacho Mungu amepanga, na atakuwa na azimio na imani zaidi ya kumwacha Mungu aipange hatima yake na kutomwasi Mungu tena. Hii ni kwa sababu anaona kwamba wakati watu hawajui hatima inahusu nini au hawaelewi mamlaka ya Mungu, anajitahidi kimakusudi na kujikwaa katika ukungu, na safari hiyo ni ngumu sana, na husababisha maumivu mengi ya moyo. Kwa hivyo watu wanapotambua kwamba Mungu ndiye mwenye mamlaka juu ya hatima ya mwanadamu, werevu huchagua kujua na kuyakubali mamlaka ya Mungu, na kuaga siku zenye uchungu za “kujaribu kuunda maisha mazuri kwa nguvu zao wenyewe,” badala ya kuendelea kupambana dhidi ya hatima na kufuatilia hayo wanayoita malengo yao ya maisha kwa njia yao wenyewe. Mtu anapokosa kuwa na Mungu, wakati hawezi kumwona, wakati hawezi kujua mamlaka ya Mungu kwa kweli na wazi, kila siku haina maana, haina thamani, na ni yenye uchungu usioelezeka. Haijalishi alipo mtu, na kazi yake ni ipi, njia yake ya kupata riziki na malengo anayofuatilia humletea tu uchungu wa moyo usio na mwisho, na maumivu ambayo ni vigumu kuyashinda, ambayo hawezi kuvumilia kuyakumbuka. Ni kwa kukubali mamlaka ya Muumba tu, kutii mipango na mipangilio Yake, na kufuatilia kufikia maisha ya kweli ya mwanadamu, ndiyo mtu anaweza kujikomboa polepole kutoka katika maumivu yote ya moyo na uchungu, na polepole kujiondolea utupu wote wa maisha ya mwanadamu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 128)
Ni Wale tu Wanaonyenyekea kwa Ukuu wa Muumba Ndio Wanaoweza Kupata Uhuru wa Kweli
Kwa sababu watu hawatambui mipango ya Mungu, na ukuu wa Mungu, siku zote wanakabiliana na hatima hiyo kwa dharau, kwa mtazamo wa kuasi, na siku zote wanataka kutupilia mbali mamlaka na ukuu wa Mungu, na mambo yale ambayo hatima imewahifadhia, wakitumai kwamba watabadilisha hali zao za sasa na kubadilisha hatima yao. Lakini hawawezi kufaulu; wanazuiliwa kwa kila sehemu ya mabadiliko katika maisha. Mvutano huu, unaoendelea ndani ya nafsi ya mtu, ni wa maumivu; maumivu haya hayasahauliki; na wakati wote huu mtu anapoteza maisha yake mwenyewe. Sababu ya maumivu haya ni nini? Je, ni kwa sababu ya ukuu wa Mungu au kwa sababu ya mtu kuzaliwa bila bahati? Bila shaka kati ya sababu hizi hakuna iliyo ya kweli. Kimsingi, ni kwa sababu ya njia ambazo watu huchukua, njia ambazo watu huchagua kuishi katika maisha yao. Baadhi ya watu huenda wasitambue mambo haya. Lakini unapojua kwa kweli, unapotambua kwa kweli kwamba Mungu anao ukuu juu ya hatima ya binadamu, unapoelewa kwa kweli kwamba kila kitu ambacho Mungu amekupangilia na kukuamulia ni chenye manufaa makubwa, na ni ulinzi mkubwa, basi utahisi maumivu yako yakipungua polepole, na mwili wako utaanza kutulia, kuwa huru na kukombolewa. Tukitazama kutokana kwenye hali za watu wengi leo, ingawa wao wenyewe hawataki kuendelea kuishi kama walivyokuwa wakiishi awali, ingawa wanataka tulizo katika maumivu yao, kimsingi hawawezi kung’amua kwa kweli thamani na maana halisi ya ukuu wa Muumba juu ya hatima ya binadamu; hawawezi kutambua kwa kweli na kunyenyekea kwa ukuu wa Muumba, sembuse kujua namna ya kutafuta na kukubali mipango na mipangilio ya Muumba. Kwa hivyo kama watu hawawezi kutambua ukweli kwamba Muumba anao ukuu juu ya hatima ya binadamu na juu ya mambo yote ya binadamu, kama hawawezi kunyenyekea kwa kweli chini ya utawala wa Muumba, basi itakuwa vigumu sana kwao kutoendeshwa na kufungwa na, fikira hii kwamba “hatima ya mtu imo kwenye mikono ya mtu,” itakuwa vigumu kwao kutupilia mbali maumivu ya kung’ang’ana kwao kwingi dhidi ya hatima na mamlaka ya Muumba, ni wazi kwamba hali hii pia itakuwa ngumu kwao katika kuweza kukombolewa kwa kweli na kuwa huru, kuwa watu wanaomwabudu Mungu. Njia rahisi zaidi ya kujikomboa kutoka katika hali hii ni kuiaga kwaheri njia yako ya awali ya kuishi, kuaga kwaheri malengo yako ya maisha ya awali; kufanya muhtasari na kuchanganua njia ya kuishi ya awali, mtazamo wa maisha, mambo uliyoyafuatilia, matamanio, na hamu ya kupata vitu; na kisha kuyalinganisha haya yote na nia za na mahitaji ya Mungu kwa wanadamu, na kuona kama kuna yoyote kati ya hayo yanayolingana na nia za Mungu, kujua kama kuna yoyote kati ya hayo yanayolingana na mahitaji ya Mungu, iwapo kuna yoyote kati ya hayo yanayoleta maadili sahihi ya maisha, kumwongoza mtu kuelewa ukweli zaidi na zaidi, na kumruhusu mtu kuishi na ubinadamu na mfano wa mwanadamu. Unapochunguza mara kwa mara na kuchanganua malengo mbalimbali ambayo watu hufuatilia maishani na njia zao mbalimbali za kuishi, utapata kwamba hakuna hata moja kati ya hizo zote ambayo inaambatana na nia ya asili ya Muumba Aliyokuwa nayo alipowaumba binadamu. Zote hizi zinawavuta watu mbali na ukuu na mamlaka ya Muumba; zote ni mitego ambayo huwasababisha watu wawe wapotovu, na ambayo inawaelekeza jehanamu. Baada ya kutambua haya, unachopaswa kufanya ni kuachilia mtazamo wako wa zamani wa maisha, kuwa mbali na mitego mbalimbali, kumwachia Mungu kuchukua usukani wa maisha yako na kuyafanyia mipangilio, utafute tu kutii mipango na mwongozo wa Mungu bila kufanya chaguzi zako mwenyewe, na kuwa mtu anayemwabudu Mungu. Haya yote yanaonekana kuwa rahisi, lakini ni jambo gumu kufanya. Baadhi ya watu wanaweza kuvumilia maumivu yake, wengine hawawezi. Baadhi wako radhi kutii, wengine hawako radhi. Wale wasiokuwa radhi wanakosa tamanio na uamuzi wa kufanya hivyo; wanayo habari kamili kuhusu ukuu wa Mungu, wanajua vyema kabisa kwamba ni Mungu anayepanga na kupangilia hatima ya binadamu, na ilhali wangali wanang’ang’ana tu, bado hawajaridhiana na nafsi zao kuhusiana na kuziacha hatima zao kwenye kiganja cha mkono wa Mungu na kunyenyekea katika ukuu wa Mungu, na zaidi, wanachukia mipango na mipangilio ya Mungu. Kwa hivyo, siku zote kutakuwa na baadhi ya watu wanaotaka kujionea wenyewe kile wanachoweza kufanya; wanataka kubadilisha hatima zao wenyewe kwa mikono yao miwili, au kutimiza furaha kwa kutumia nguvu zao wenyewe, kuona kama wanaweza kukiuka mipaka ya mamlaka ya Mungu na kuinuka juu ya ukuu wa Mungu. Huzuni ya mwanadamu, sio juu ya yeye kutafuta maisha mazuri, si kwamba anatafuta umaarufu na utajiri au sio kwamba anapingana na hatima yake mwenyewe kwenye ukungu, lakini ni kwamba baada ya yeye kuona uwepo wa Muumba, baada ya yeye kujifunza ukweli kwamba Muumba anao ukuu juu ya hatima ya binadamu, bado hawezi kurekebisha njia zake, hawezi kuvuta miguu yake kutoka kwenye mtego, lakini anaufanya moyo wake kuwa mgumu na kudumu katika makosa yake. Afadhali aendelee kutapatapa kwenye matope, akishindana kwa ukaidi dhidi ya ukuu wa Muumba, akiupinga mpaka kufikia mwisho ulio na uchungu, bila hata chembe ya majuto. Ni mpaka pale tu anapolazwa akiwa amevunjika na anavuja damu ndipo anapoamua hatimaye kusalimu amri na kugeuka na kubadilisha mwenendo. Hii ni huzuni ya kweli ya mwanadamu. Kwa hivyo Ninasema, wale wanaochagua kunyenyekea ni wenye busara na wale waliochagua kutoroka ni wapumbavu kweli.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 129)
Awamu Sita katika Maisha ya Binadamu
Awamu ya Sita: Kifo
Baada ya mahangaiko mengi na masikitiko mengi, na kuvunjwa moyo kwingi, baada ya furaha nyingi na huzuni nyingi na baada ya misukosuko ya maisha, baada ya miaka mingi sana isiyosahaulika, baada ya kutazama misimu ikipita na kujirudia, mtu hupita kwenye hatua muhimu sana ya maisha bila ya taarifa, na kwa ghafla tu mtu anajipata kwenye miaka yake ya kufifia. Alama za muda zimejichora kotekote kwenye mwili wa mtu: Mtu hawezi tena kusimama wima, kichwa cha nywele nyeusi kinageuka na kuwa cha nywele nyeupe, macho maangavu na mazuri yanabadilika na kuanza kuwa hafifu na kuwa na ukungu mbele yao, nayo ngozi laini, na inayong’aa inageuka na kuwa na makunyanzi na madoadoa. Usikivu wa mtu unaanza kudhoofika, meno yake yanaanza kulegea na kung’ooka, mwitikio wa mtu unaanza kuchelewachelewa, kutembea kunakuwa ni kwa kujikokota…. Wakati huu mtu ameaga kwaheri kabisa miaka yake ya nguvu ya ujana wake na kuingia katika maisha yake ya kwaheri: umri wa uzee. Kisha, mtu atakabiliana na kifo, awamu ya mwisho ya maisha ya binadamu.
1) Muumba Pekee Ndiye Anayeshikilia Nguvu ya Uzima na Mauti Juu ya Mwanadamu
Kama kuzaliwa kwa mtu kulipangiwa kutokana na maisha yake ya awali, basi kifo cha mtu kinaadhimisha mwisho wa hatima hiyo. Kama kuzaliwa kwa mtu ndiyo mwanzo wa kazi maalum ya mtu katika maisha haya, basi kifo cha mtu kinaashiria mwisho wa kazi hiyo maalum. Kwa sababu Muumba ameweka mpangilio maalum wa hali kwa ajili ya kuzaliwa kwa mtu, ni wazi kwamba Yeye pia Amepanga mpangilio maalum wa hali za kifo cha mtu. Kwa maneno mengine, hakuna anayezaliwa kwa bahati na hakuna kifo cha mtu kinachotokea kwa ghafla, na kuzaliwa kwa mtu na kifo chake vyote vina uhusiano na maisha ya mtu ya awali na ya sasa. Hali za kuzaliwa na kifo cha mtu, vyote viliamuliwa kabla na Muumba; hii ni kudura ya mtu, hatima ya mtu. Kwa kuwa kuna maelezo mengi ya kuzaliwa kwa mtu, ni kweli pia kwamba kifo cha kila mtu kitatokea chini ya hali maalum zinazotofautiana. Hii ndiyo sababu ya kutofautiana kwa urefu wa maisha ya watu, njia na nyakati tofauti za vifo vyao. Baadhi ya watu wana nguvu na afya na ilhali wanakufa mapema; wengine ni wanyonge na wanauguaugua ilhali wanaishi hadi umri wa uzee, na wanaaga dunia kwa amani. Baadhi ya watu hupoteza maisha kwenye matukio yasiyotarajiwa, na wengine hufariki kutokana na sababu za kawaida. Baadhi wanakata roho wakiwa mbali na nyumbani, wengine wanayafumba macho yao kwa mara ya mwisho wakiwa na wapendwa wao kando yao. Baadhi ya watu hufia angani, na wengine hufia chini ya ardhi. Wengine huzama chini ya maji, wengine nao kwenye majanga. Baadhi hufa asubuhi, wengine hufa usiku. … Kila mtu anataka kuzaliwa kwa heshima, kuwa na maisha mazuri, na kifo kitukufu, lakini hakuna mtu anayeweza kufika zaidi ya hatima yake mwenyewe, hakuna mtu anayeweza kukwepa ukuu wa Muumba. Hii ni hatima ya binadamu. Mwanadamu anaweza kupanga kila aina ya mipango kwa ajili ya maisha yake ya baadaye, lakini hakuna mtu anayeweza kupanga njia na muda wa kuzaliwa kwake na kuondoka kwake ulimwenguni. Ingawa watu wanajitahidi kadiri wawezavyo kuepuka na kuzuia ujio wa kifo chao, lakini bado, bila wao kujua, kifo huwa kinawakaribia kimyakimya. Hakuna ajuaye ni lini ataaga dunia na kwa njia ipi, sembuse kujua ni wapi ambapo hilo litatokea. Bila shaka, si binadamu wanaoshikilia nguvu za maisha na kifo, wala si kiumbe fulani kwenye ulimwengu wa asili, bali ni Muumba, ambaye mamlaka yake ni ya kipekee. Maisha na kifo cha binadamu si zao la sheria fulani ya ulimwengu wa asili, bali ni matokeo ya ukuu wa mamlaka ya Muumba.
2) Yule Asiyejua Ukuu wa Muumba Atahangaika kwa Woga wa Kifo
Wakati mtu anapoingia kwenye umri wa uzee, changamoto anazokabiliana nazo si kutosheleza mahitaji ya familia au kuanzisha maono makubwa katika maisha yake, bali ni namna ya kuyaaga maisha yake, namna ya kukutana na mwisho wa maisha yake, namna ya kuweka kikomo kwenye mwisho wa uwepo wake binafsi. Ingawa kwa juu juu inaonekana kwamba watu hawazingatii sana kifo, hakuna anayeweza kuepuka kuchunguza suala hili, kwani hakuna anayejua ikiwa kuna ulimwengu mwingine uliopo kwenye upande ule wa mbali wa kifo, ulimwengu ambao binadamu hawawezi kuuona au kuuhisi, ulimwengu wasiojua chochote kuuhusu. Hali hii huwafanya watu kuwa na wasiwasi kukabiliana na kifo moja kwa moja, wanaogopa kukikabili kama inavyostahili, na badala yake wanafanya kadri ya uwezo wao kuepuka mada hii. Na kwa hivyo mada hii humfanya kila mmoja kutishika kuhusu kifo, huongezea uzito kwenye fumbo hili kuhusiana na ukweli huu wa maisha usioepukika, ikiweka kivuli kisichoisha juu ya moyo wa kila mmoja.
Wakati mtu anapohisi mwili wake unaanza kudhoofika, wakati mtu anapohisi kwamba kifo chake kinakaribia, mtu anahisi wasiwasi na, woga usioelezeka. Woga wa kifo humfanya mtu kuhisi kuwa mpweke zaidi na asiyejiweza, na kwa wakati huu mtu hujiuliza: Nilitoka wapi? Ninakwenda wapi? Je, hivi ndivyo nitakavyokufa, huku maisha yangu yakinipita kwa haraka hivi? Je, huu ndio wakati unaodhihirisha mwisho wa maisha yangu? Ni nini, hatimaye, maana ya maisha? Maisha yana thamani gani, kwa kweli? Je, yanahusu umaarufu na utajiri? Je, yanahusu kulea familia? … Haijalishi kama mtu amewahi kufikiria maswali haya mahususi, haijalishi ni vipi mtu ana woga wa kifo, katika kina cha moyo wa kila mmoja siku zote kuna tamanio la kutaka kuchunguza zaidi mafumbo, kuna hisia fulani za sintofahamu kuhusu maisha, pamoja na hayo, kuna hisia za matukio yaliyopita yanayohusiana na ulimwengu huu, na kutotaka kuuacha. Pengine hakuna anayeweza kufafanua zaidi ni nini ambacho binadamu huogopa, ni nini ambacho binadamu hutaka kuchunguza zaidi, na nini kile ambacho ana uhusiano wa karibu nacho na kinachomfanya kutotaka kuondoka au kukiacha nyuma …
Kwa sababu wanaogopa kifo, watu huwa na wasiwasi mno; kwa vile wanaogopa kifo, vipo vitu vingi ambavyo hawawezi kuviachilia. Wakati wanakaribia kufa, baadhi ya watu huhangaika kuhusu hiki au kile; wanakuwa na wasiwasi kuhusu watoto wao, wapendwa wao, utajiri wao, ni kana kwamba kwa kuwa na wasiwasi hivyo wanaweza kuondoa mateso na hofu ambayo kifo huleta, ni kana kwamba kwa kuendeleza aina fulani ya urafiki wa karibu na wale wanaoishi wanaweza kukwepa ile hali ya kutoweza kujisaidia na upweke unaoandamana na kifo. Katika kina cha moyo wa binadamu kunao woga usio dhahiri, woga wa kutenganishwa na wapendwa wake, woga wa kutowahi kutazama tena anga la buluu, woga wa kutowahi kuutazama tena ulimwengu huu yakinifu. Nafsi pweke, iliyozoeana na wapendwa wake, inasita kuachilia maisha yake na kuondoka, ikiwa peke yake, kuelekea kwenye ulimwengu usiojulikana, usiozoeleka.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 130)
Maisha ya Kuishi Ukitafuta Umaarufu na Utajiri Yatamwacha Mtu Akiwa na Hasara Akikabiliana na Kifo
Kwa sababu ya ukuu na kuamuliwa kabla kwa Muumba, nafsi pweke iliyoanza bila chochote kwa jina lake huweza kupata wazazi na familia, fursa ya kuwa mwanachama wa kizazi cha binadamu, fursa ya kupitia maisha ya binadamu na kuona ulimwengu; na pia inafaidi fursa ya kupitia ukuu wa Muumba, kujua uzuri wa uumbaji wa Muumba, na zaidi kuliko vyote, kujua na kutii mamlaka ya Muumba. Lakini watu wengi zaidi huwa hawatumii vizuri fursa hii nadra na ya kipekee. Mtu hutumia nguvu zake zote maishani akipigana dhidi ya hatima yake, akitumia muda wake wote kushughulika akijaribu kuilisha familia yake na akisafiri huku na kule katika kutafuta utajiri na hadhi kwenye jamii. Mambo ambayo watu huthamini ni familia, pesa, na umaarufu; wanaona mambo haya kuwa mambo yenye thamani zaidi katika maisha. Watu wote wanalalamika kuhusu hatima zao, ilhali bado wanasukuma nyuma ya akili zao maswali ambayo ni ya lazima sana kuyachunguza na kuyaelewa: kwa nini binadamu yuko hai, namna ambavyo binadamu anafaa kuishi, ni nini maana na thamani ya maisha. Katika maisha yao yote, hata hivyo haijalishi ni miaka mingapi, wanaharakisha tu kutafuta umaarufu na utajiri, mpaka pale ujana wao unapowaacha, mpaka wanapokuwa na nywele za kijivu na makunyanzi kwenye nyuso zao; mpaka wanapogundua utajiri na umaarufu ni vitu visivyoweza kumzuia mtu kuelekea katika udhaifu unaotokana na uzee, kwamba pesa haiwezi kujaza utupu wa moyo: mpaka wanapoelewa kwamba hakuna mtu ambaye anaachwa nje kutoka kwenye sheria ya kuzaliwa, kuwa mzee, magonjwa, na kifo, kwamba hakuna mtu anayeweza kutoroka hatima ile inayomsubiri. Ni mpaka tu pale ambapo anapolazimishwa kukabiliana na awamu ya mwisho maishani ndipo anapoelewa kwa kweli kwamba hata kama mtu anamiliki mamilioni ya mali, hata kama mtu anayo heshima na cheo kikubwa, hakuna anayeweza kutoroka kifo, kwamba kila mtu atarudi kwenye sehemu yake asilia: nafsi pweke, bila chochote kwa jina lake. Wakati mtu anapokuwa na wazazi, mtu husadiki kwamba wazazi wa mtu ndio kila kitu; wakati mtu anapokuwa na mali, mtu hufikiri kwamba pesa ndiyo tegemeo la mtu, kwamba hiyo ndiyo njia ambayo kwayo mtu huishi; wakati watu wanapokuwa na hadhi katika jamii, wanaishikilia na hata wanaweza kuhatarisha maisha yao kwa ajili ya hadhi hiyo. Ni pale tu ambapo watu wanakaribia kuondoka ulimwenguni ndipo wanapotambua kwamba mambo yale waliyoishi katika maisha yao wakiyafuatilia si chochote bali mawingu yanayopita, hakuna chochote kati ya vitu hivi ambacho wanaweza kushikilia, hakuna hata chochote wanachoweza kwenda nacho, hakuna hata chochote kinachoweza kuwaondolea kifo, hakuna chochote kile kinachoweza kuwasindikiza au kutoa faraja kwa nafsi yao pweke inayoelekea kufa; na hata, hakuna kati ya hivyo vyote vinavyoweza kumpa mtu wokovu, na kuwaruhusu kushinda kifo. Umaarufu na utajiri ambao mtu hupata kwenye ulimwengu yakinifu humpa mtu hisia ya kuridhika kwa muda, furaha isiyodumu, hisia ya uwongo ya utulivu, na kumfanya mtu kupoteza njia. Na kwa hivyo watu, wanapong’ang’ana kila pahali kwenye bahari kubwa ya binadamu, wakitafuta amani, faraja na utulivu wa moyo, wanafunikwa zaidi na zaidi na mawimbi. Wakati ambapo watu hawajapata maswali ambayo ni muhimu zaidi kuelewa—ni wapi wametoka, ni kwa nini wako hai, ni wapi wanakoenda na kadhalika—wanashawishiwa na umaarufu na utajiri, wanapotoshwa, wanadhibitiwa na vitu hivyo, na wanaishia kupotea bila kujua njia. Muda unayoyoma; kwa kufumba na kufumbua miaka inapita; na kabla ya mtu kutambua, mtu anaaga kwaheri miaka iliyo bora zaidi ya maisha yake. Wakati mtu anakaribia kuondoka ulimwenguni, mtu anafika katika utambuzi wa taratibu kwamba kila kitu ulimwenguni kinamwacha polepole, kwamba mtu hawezi kushikilia tena vitu alivyomiliki; kisha mtu anahisi kwa kweli kwamba hamiliki kitu chochote kile, na ni kama tu mtoto mchanga anayelia ambaye ndio kwanza amezaliwa na kubisha mlango ulimwenguni. Wakati huu, mtu anashawishiwa kutafakari kile ambacho amefanya maishani, thamani ya kuwa hai, ni nini maana yake, kwa nini mtu alikuja ulimwenguni; na wakati huu, mtu anaendelea kutaka kujua kama kwelikuna maisha ya baadaye, kama kweli Mbingu ipo, kama kweli kuna adhabu…. Kadri mtu anavyokaribia kufa, ndivyo mtu anavyotaka kuelewa maisha yanahusu nini hasa; kadri mtu anavyokaribia kufa, ndivyo moyo wake unavyoonekana kuwa mtupu; kadri mtu anavyokaribia kufa, ndivyo anavyozidi kuhisi kuwa hawezi kusaidika; na kwa hivyo hofu ya mtu kuhusu kifo inazidi kuongezeka siku baada ya siku. Kunazo sababu mbili zinazoelezea kwa nini watu huwa hivi wanapokaribia kifo: Kwanza, wapo karibu kupoteza umaarufu na utajiri ambao maisha yao yalitegemea, wapo karibu kuacha nyuma kila kitu kinachoonekana ulimwenguni; na pili, wapo karibu kukabiliana, wakiwa peke yao, na ulimwengu usiojulikana, wenye mafumbo, ulimwengu usiojulikana ambao wana woga wa kukanyaga mguu wao kule, kule wasikokuwa na wapendwa na mbinu zozote za kupata msaada. Kwa hizo sababu mbili, kila mtu anayekabiliana na kifo anahisi wasiwasi, anapitia hali ya hofu kubwa na anahisi hali ya kutoweza kusaidika ambayo hajawahi kuipitia hapo awali. Ni pale tu watu wanapofikia hatua hii ndipo wanapotambua kwamba kitu cha kwanza ambacho mtu lazima aelewe, pale anapokanyaga mguu wake hapa duniani, ni wapi ambapo wanadamu wanatoka, kwa nini watu wako hai, ni nani anayeamuru hatima ya binadamu, ni nani anayekidhi mahitaji ya binadamu, na Aliye na ukuu juu ya uwepo wa binadamu. Maarifa haya ndiyo njia ya kweli ambayo kwayo mtu huishi, msingi muhimu kwa kuwepo kwa binadamu—sio kujifunza namna ya kutosheleza familia ya mtu au namna ya kutimiza umaarufu na utajiri, sio kujifunza namna ya kujitokeza katika umati wala namna ya kuishi maisha mazuri zaidi, sembuse kujifunza namna ya kuwa bora na kushindana kwa mafanikio dhidi ya wengine. Ingawa maarifa mbalimbali ya kuishi ambayo watu hutumia maisha yao kuyamiliki yanaweza kutoa starehe nyingi za kimwili, hazijawahi kuleta amani na tulizo la kweli moyoni, lakini badala yake hufanya watu kila wakati kupoteza mwelekeo wao, kuwa na wakati mgumu kujidhibiti, na kukosa kila fursa ya kujifunza maana ya maisha; mbinu hizi za kuishi huleta wasiwasi uliofichwa ndani ya watu kuhusu jinsi ya kukabiliana na kifo kwa usahihi. Maisha ya watu yanaharibiwa kwa njia hii. Muumba humtendea kila mmoja kwa haki, Akimpatia kila mmoja fursa ya maisha yote ya kupata uzoefu na kuujua ukuu Wake, ilhali ni mpaka tu kifo kinapokaribia, wakati kivuli cha kifo kinaponing’inia karibu na mtu, ndipo mtu huyu anaanza kuona nuru—na ndipo inapokuwa kuchelewa mno.
Watu huishi maisha yao wakitafuta pesa na umaarufu; wanashikilia nyuzi hizi, wakifikiri kwamba ndizo mbinu zao pekee za msaada, ni kana kwamba wakiwa nazo wangeendelea kuishi, wangejitoa kwenye hesabu ya wale watakaokufa. Lakini nipale tu wanapokaribia kufa ndipo wanapotambua namna ambavyo vitu hivi vilivyo mbali na wao, namna walivyo wanyonge mbele ya kifo, namna wanavyosambaratika kwa urahisi, namna walivyo wapweke na wasivyoweza kusaidika, na hawana popote pa kugeukia. Wanatambua kwamba uzima hauwezi kununuliwa kwa pesa au umaarufu, kwamba haijalishi mtu ni tajiri vipi, haijalishi cheo chake kilivyo cha hadhi, watu wote ni maskini kwa njia sawa na wanaofanya mambo bila mpango mbele ya kifo. Wanatambua kwamba pesa haziwezi kununua uzima, kwamba umaarufu hauwezi kufuta kifo, kwamba si pesa wala umaarufu unaoweza kurefusha maisha ya mtu kwa hata dakika moja, hata sekunde moja. Kadiri watu wanavyohisi hivi, ndivyo wanavyotamani zaidi kuendelea kuishi; kadiri watu wanavyohisi hivi, ndivyo wanavyohofia zaidi kuikaribia kifo. Ni kwa wakati huu tu ndipo wanapotambua kwa kweli kwamba maisha waliyo nayo sio ya kwao wenyewe, sio yao kuyadhibiti, na kwamba mtu hana maamuzi juu ya iwapo ataishi au atakufa, kwamba haya mambo yote yanapatikana nje ya udhibiti wa mtu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 131)
Jisalimishe Chini ya Utawala wa Muumba na Ukabiliane na Kifo kwa Utulivu
Wakati ule ambao mtu anazaliwa, nafsi ya mtu iliyo pweke inaanza kupitia maisha hapa duniani, inapitia mamlaka ya Muumba ambayo Muumba ameipangilia. Bila shaka, kwa mtu, kwa nafsi, hii ni fursa nzuri kabisa ya kupata maarifa kuhusu ukuu wa Muumba, kujua mamlaka Yake na kuyapitia kibinafsi. Watu wanaishi maisha yao kulingana na sheria za hatima zilizowekwa kwa ajili yao na Muumba, na kwa mtu yeyote mwenye akili timamu aliye na dhamiri, kuelewa ukuu wa Muumba na kutambua mamlaka yake kwenye mkondo wa miongo yao kadhaa hapa duniani si jambo gumu kufanya. Kwa hivyo, inapaswa kuwa rahisi sana kwa kila mtu kutambua, kupitia uzoefu wao wenyewe wa maisha katika miongo kadhaa, kwamba hatima zote za wanadamu zimeamuliwa kabla, na inapaswa kuwa rahisi kufahamu au kutathmini ni nini maana ya kuishi. Kwa wakati huo huo ambao mtu anayapokea mafunzo haya ya maisha, polepole atakuja kuelewa ni wapi maisha yanapotokea, kufahamu kile ambacho moyo unahitaji kwa kweli, ni nini kitamwongoza mtu kwenye njia ya kweli ya maisha, kazi maalum na lengo la maisha ya mwanadamu inapaswa kuwa ni nini; na mtu ataanza kutambua hatua kwa hatua kwamba kama mtu hatamwabudu Muumba, kama mtu hatajisalimisha chini ya utawala Wake, basi wakati utakapofika wa mtu kukabiliana na kifo—wakati nafsi ya mtu inakaribia kumkabili Muumba kwa mara nyingine—basi moyo wa mtu utajawa na hofu na kukosa utulivu kusikoisha. Kama mtu amekuwepo ulimwenguni kwa miongo kadhaa ilhali hajajua ni wapi maisha ya binadamu hutoka, angali hajatambua ni kwenye viganja vya mikono ya nani hatima ya binadamu inategemea, basi si ajabu hataweza kukabiliana na kifo kwa utulivu. Mtu aliyepata maarifa ya ukuu wa Muumba baada ya kupitia miongo kadhaa ya maisha, ni mtu aliye na ufahamu sahihi wa maana na thamani ya maisha; mtu aliye na maarifa ya kina kuhusu kusudi la maisha, aliye na uzoefu halisi na uelewa wa ukuu wa Muumba; na hata zaidi, mtu anayeweza kunyenyekea mbele ya mamlaka ya Muumba. Mtu kama huyo anaelewa maana ya uumbaji wa Mungu wa mwanadamu, anaelewa kwamba binadamu anapaswa kumwabudu Muumba, kwamba kila kitu anachomiliki binadamu kinatoka kwa Muumba na kitarejea Kwake siku fulani isiyo mbali sana kwenye siku za usoni; mtu kama huyo anaelewa kwamba Muumba hupangilia kuzaliwa kwa binadamu na ana ukuu juu ya kifo cha binadamu, na kwamba maisha na kifo vyote vimeamuliwa kabla na mamlaka ya Muumba. Kwa hivyo, wakati mtu anapofahamu mambo haya kwa kweli, kwa kawaida mtu ataweza kukabiliana na kifo kwa utulivu, kuweka kando mali zake zote za kidunia kwa utulivu, kukubali na kunyenyekea kwa furaha kwa yote yatakayofuata, na kukaribisha awamu ya mwisho ya maisha iliyopangiliwa na Muumba badala ya kuhofu na kupambana dhidi ya kifo. Ikiwa mtu anayaona maisha kama fursa ya kupitia ukuu wa Muumba na kuja kujua mamlaka yake, ikiwa mtu anayaona maisha yake kama fursa adimu ya kutekeleza wajibu wake akiwa binadamu aliyeumbwa na kutimiza kazi yake maalum, basi mtu atakuwa ana mtazamo sahihi wa maisha, ataishi maisha yaliyobarikiwa na yanayoongozwa na Muumba, atatembea kwenye nuru ya Muumba, atajua ukuu wa Muumba, atakuwa katika utawala Wake, atakuwa shahidi wa matendo Yake ya ajabu na mamlaka Yake. Bila shaka, mtu kama huyo hakika atapendwa na kukubaliwa na Muumba, na ni mtu kama huyo tu anayeweza kuwa na mtazamo wenye utulivu mbele ya kifo, na anayeweza kukaribisha awamu hii ya mwisho ya maisha kwa furaha. Bila shaka Ayubu alikuwa na mtazamo kama huu kuelekea kifo; alikuwa katika nafasi ya kukubali kwa furaha awamu ya mwisho ya maisha, na baada ya kuhitimisha safari yake ya maisha vizuri, baada ya kukamilisha kazi yake maalum, alirudi kuwa upande wa Muumba.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 132)
Harakati na Aliyofaidi Ayubu katika Maisha Yamruhusu Kukabiliana na Kifo kwa Utulivu
Katika Maandiko imeandikwa kuhusu Ayubu: “Kwa hivyo Ayubu akafariki, akiwa mzee na aliyejawa na siku” (Ayubu 42:17). Hii inamaanisha kwamba wakati Ayubu alipoaga dunia, hakuwa na majuto na hakuhisi maumivu, lakini aliondoka kwa kawaida kutoka kwa ulimwengu huu. Kama vile kila mmoja anavyojua, Ayubu alikuwa mtu aliyemcha Mungu na kuepuka maovu alipokuwa hai; Mungu alimpongeza kwa matendo yake ya haki, watu waliyakumbuka, na maisha yake, zaidi ya yeyote yule mwingine, yalikuwa na thamani na umuhimu. Ayubu alifurahia baraka za Mungu na aliitwa mwadilifu na Yeye hapa duniani, na aliweza pia kujaribiwa na Mungu na kujaribiwa na Shetani; alisimama kuwa shahidi wa Mungu na alistahili kuitwa mtu mwenye haki. Katika miongo kadhaa baada ya kujaribiwa na Mungu, aliishi maisha ambayo yalikuwa yenye thamani zaidi, yenye maana zaidi, yenye msingi, na yenye amani zaidi kuliko hata awali. Kutokana na matendo yake ya haki, Mungu alimjaribu; na pia kwa sababu ya matendo yake ya haki, Mungu alionekana kwake na kuongea naye moja kwa moja. Kwa hiyo, kwenye miaka yake baada ya kujaribiwa, Ayubu alielewa na kufahamu thamani ya maisha kwa njia thabiti zaidi, aliweza kupata ufahamu wa kina zaidi wa ukuu wa Muumba, na akapata maarifa sahihi na yenye uhakika zaidi kuhusu namna ambavyo Muumba anavyotoa na kuzichukua baraka zake. Kitabu cha Ayubu kinarekodi kwamba Yehova Mungu alimpa hata baraka nyingi zaidi Ayubu kuliko hapo awali, Akimweka Ayubu katika nafasi bora zaidi ya kujua ukuu wa Muumba na kujua kukabiliana na kifo kwa utulivu. Kwa hiyo, Ayubu alipozeeka na kukabiliana na kifo, bila shaka asingekuwa na wasiwasi kuhusu mali yake. Hakuwa na wasiwasi wowote, hakuwa na chochote cha kujutia, na bila shaka hakuogopa kifo; kwani aliishi maisha yake akitembea ile njia ya kumcha Mungu, kuepuka maovu, na hakuwa na sababu yoyote ya kuwa na wasiwasi kuhusu mwisho wake mwenyewe. Ni watu wangapi leo wanaweza kuchukua hatua kwa njia zote hizo ambazo Ayubu alitumia alipokabiliwa na kifo chake mwenyewe? Kwa nini hakuna mtu anayeweza kuendeleza mwelekeo wa mtazamo rahisi kama huu? Kunayo sababu moja tu: Ayubu aliishi maisha yake katika hali ya kufuatilia imani, utambuzi, na unyenyekevu kwa ukuu wa Mungu, na ilikuwa ni kupitia imani, utambuzi, na unyenyekevu huu ambapo aliweza kupitia zile awamu muhimu za maisha, aliishi kwa kudhihirisha miaka yake ya mwisho, na kukaribishaa awamu yake ya mwisho ya maisha. Licha ya kile ambacho Ayubu alipitia, yale aliyoyafuatilia na malengo yake katika maisha yalikuwa ni yenye furaha, na hayakuwa na maumivu. Alikuwa na furaha si tu kwa sababu ya baraka au kibali alichopewa na Muumba, lakini muhimu zaidi kwa sababu ya yale aliyoyafuatilia na malengo yake katika maisha, kwa sababu ya maarifa yaliyoongezeka kwa utaratibu na ufahamu wa kweli wa ukuu wa Muumba ambao alitimiza kupitia kwa kumcha Mungu na kwa kuepuka maovu, na zaidi, kwa sababu ya matendo Yake ya ajabu ambayo Ayubu aliyapitia kibinafsi wakati huu akiwa chini ya ukuu wa Muumba, na hisia zenye kujali na zisizosahaulika na kumbukumbu ya mwanadamu na Mungu kuwepo pamoja, kufahamiana, na kuelewana. Ayubu alikuwa na furaha kwa sababu ya faraja na furaha iliyotokana na kujua nia za Muumba, na kwa sababu ya heshima iliyotokea baada ya kuona kwamba Yeye ni mkuu, wa ajabu, wa kupendeza na mwaminifu. Sababu iliyomfanya Ayubu aweze kukabiliana na kifo bila mateso yoyote ni kwamba alijua, katika kufa, angerudi kuwa upande wa Muumba. Na ilikuwa ni yale aliyoyafuatilia na kuyapata maishani mwake ambayo yalimruhusu kukabiliana na kifo kwa utulivu, yalimruhusu kukabiliana na matarajio ya Muumba kuuchukua uhai wake tena, akiwa na moyo wenye utulivu, na zaidi ya hayo, yalimruhusu kusimama imara bila kutikisika na bila wasiwasi mbele za Muumba. Je, watu wanaweza siku hizi kutimiza aina ya furaha ambayo Ayubu alikuwa nayo? Je, nyinyi wenyewe mko katika hali ya kufanya hivyo? Kwa kuwa watu siku hizi wana hali hizi, kwa nini hawawezi kuishi kwa furaha, kama alivyofanya Ayubu? Kwa nini hawawezi kuepuka mateso yanayotokana na hofu ya kifo? Wakati wanapokabiliwa na kifo, baadhi ya watu hujiendea haja ndogo; wengine wanatetemeka, wanazimia, wanapiga kelele kwa hasira dhidi ya Mbingu na wanadamu vilevile, wengine hata wakalia kwa huzuni na kutokwa machozi. Kwa vyovyote vile, hii siyo miitikio ya ghafla inayotokea wakati kifo kinapokaribia. Watu hutenda kwa njia hizi za aibu hasa kwa sababu, ndani ya mioyo yao, wanaogopa kifo, kwa sababu hawana maarifa yaliyo wazi na utambuzi wa ukuu wa Mungu na mipangilio Yake, sembuse kujinyenyekeza mbele ya vitu hivi; kwa sababu watu hawataki chochote isipokuwa kupanga na kutawala kila kitu wao wenyewe, kudhibiti hatima zao binafsi, maisha yao binafsi na hata kifo. Kwa hivyo, si ajabu kwamba watu hawawezi kamwe kuepuka hofu ya kifo.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 133)
Ni kwa Kukubali tu Ukuu wa Muumba Ndipo Mtu Anaweza Kurejea Upande Wake
Wakati mtu hana maarifa yaliyo wazi na hajapitia ukuu wa Mungu na mipangilio Yake, maarifa ya mtu kuhusu hatima na yale ya kifo yatakuwa yale yasiyoeleweka. Watu hawawezi kuona waziwazi kwamba haya yote yamo kwenye kiganja cha mkono wa Mungu, hawatambui kwamba kila kitu kiko chini ya udhibiti na ukuu wa Mungu, hawatambui kwamba mwanadamu hawezi kutupilia mbali au kuepuka ukuu kama huo; na kwa hivyo wakati wanapokabiliwa na kifo hakuna mwisho wowote katika maneno yao ya mwisho, wasiwasi wao, na hata majuto. Wamelemewa sana na mizigo mingi, kusitasita kwingi, kuchanganyikiwa kwingi, na haya yote yanawafanya kuogopa kifo. Kwa mtu yeyote aliyezaliwa katika ulimwengu huu, kuzaliwa kwake ni muhimu na kifo chake hakiepukiki; na hakuna mtu anayeweza kuupiga chenga mkondo huu. Kama mtu atataka kuondoka katika ulimwenguni huu bila maumivu, kama mtu atataka kukabiliana na awamu ya mwisho ya maisha bila kusitasita au wasiwasi, njia pekee ni kuondoka bila majuto. Na njia pekee ya kuondoka bila majuto ni kujua ukuu wa Muumba, kujua mamlaka yake, na kunyenyekea mbele ya vitu hivi. Ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kuwa mbali na mahangaiko ya binadamu, mbali na maovu, mbali na utumwa wa Shetani; na ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kuishi maisha kama ya Ayubu, akiongozwa na akibarikiwa na Muumba, maisha yaliyo huru na yaliyokombolewa, maisha yenye thamani na maana, maisha yenye uaminifu na moyo wazi; ni kupitia kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kunyenyekea, kama Ayubu, katika kujaribiwa na kunyang’anywa na Muumba, katika kujinyenyekeza kwenye mipango na mipangilio ya Muumba; ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kumwabudu Muumba maisha yake yote na kuweza kupata sifa Zake, kama Ayubu alivyopata, na kusikia sauti Yake, kumwona Akionekana; ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kuishi na kufa kwa furaha, kama Ayubu, bila ya maumivu, bila wasiwasi, bila majuto; ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kuishi katika nuru, kama Ayubu, na kupita kila hatua ya maisha katika nuru, kukamilisha kwa urahisi safari ya mtu katika nuru, kutimiza kwa ufanisi kazi yake maalum—kupitia, kujifunza, na kujua ukuu wa Muumba kama kiumbe kilichoumbwa—na kuiaga dunia katika nuru, na kuanzia wakati huo na kuendelea anasimama upande wa Muumba kama mwanadamu aliyeumbwa, anayesifiwa na Yeye.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 134)
Usikose Fursa ya Kujua Ukuu wa Muumba
Miongo kadhaa ambayo inaunda maisha ya binadamu si mirefu sana wala mifupi sana. Miaka zaidi ya ishirini tangu kuzaliwa hadi kufikia utu uzima kwa muda mfupi kwa kufumba na kufumbua, na ingawa katika hatua hii ya maisha mtu huchukuliwa kuwa mtu mzima, watu katika umri huu wanajua machache sana kuhusu maisha ya binadamu na hatima ya binadamu.Kadri wanavyopata uzoefu zaidi, ndivyo wanavyoingia hatua kwa hatua kufikia umri wa kati. Watu katika miaka yao ya thelathini na arubaini wanaanza kupata uzoefu wa maisha na hatima, lakini mawazo yao kuhusu mambo haya bado hayana uelewa wa wazi. Ni mpaka kufikia tu umri wa miaka arubaini ndipo baadhi ya watu huanza kupata uelewa juu ya binadamu na ulimwengu, ambavyo viliumbwa na Mungu, na kuelewa kwamba maisha ya binadamu yanahusu nini, na hatima ya binadamu ni nini. Baadhi ya watu, ingawa wamekuwa wafuasi wa Mungu kwa muda mrefu na sasa wanao umri wa kati, bado hawamiliki maarifa na ufafanuzi sahihi wa ukuu wa Mungu, sembuse utiifu wa kweli. Baadhi ya watu hawajali chochote isipokuwa namna ya kupokea baraka, na ingawa wameishi kwa miaka mingi, hawajui au hawaelewi hata kidogo ukweli wa ukuu wa Muumba juu ya hatima ya binadamu, na kwa hivyo bado hawajaingia hata kidogo kwenye mafunzo ya kivitendo ya kujitiisha katika mipango na mipangilio ya Mungu. Watu kama hao ni wapumbavu kabisa; watu kama hao wanaishi maisha yao yasiyofaa.
Kama maisha ya binadamu yangegawanywa kulingana na kiwango cha mtu cha kile alichopitia maishani na maarifa yake kuhusu hatima ya binadamu, basi yangegawanywa katika awamu tatu. Awamu ya kwanza ni ujana, ambayo ni miaka kati ya kuzaliwa na umri wa kati, au kutoka kuzaliwa hadi kufikia umri wa miaka thelathini. Awamu ya pili ni ya utu uzima, kuanzia umri wa miaka ya kati hadi umri wa uzee, au kuanzia thelathini hadi kufikia sitini. Na awamu ya tatu ni kile kipindi cha ukomavu wa mtu, unaoanzia umri wa uzee, kuanzia miaka sitini, mpaka pale mtu atakapoondoka duniani. Kwa maneno mengine, kuanzia kuzaliwa hadi umri wa miaka ya kati, maarifa ya watu wengi kuhusu hatima na maisha yanabakia tu katika kuiga mawazo ya wengine, na hayana uhalisia, wa kivitendo. Katika kipindi hiki, mtazamo wa mtu kuhusu maisha, na jinsi ambavyo mtu huingiliana na watu katika ulimwengu vyote ni vya kijuujuu na vya kijinga sana. Hiki ndicho kipindi cha ujana wa mtu. Ni baada tu ya mtu kuonja furaha na huzuni zote za maisha ndipo mtu anapataufahamu halisi wa hatima, ndipo mtu—bila kujua ndani kabisa ya moyo wake—anaanza taratibu kufahamu kuwa hatima haiwezi kubadilishwa, na anaanza kutambua polepole kwamba ukuu wa Muumba juu ya hatima ya binadamu kwa kweli upo. Kwa kweli hiki ndicho kipindi cha utu uzima wa mtu. Baada ya mtu kuacha kupambana dhidi ya hatima, na pale ambapo mtu hayuko radhi tena kuvutwa kwenye mabishano, lakini anajua msimamo wake, anajinyenyekeza kwa mapenzi ya Mbinguni, anafanya muhtasari wa mafanikio na makosa yake katika maisha, na anasubiria hukumu ya Muumba juu ya maisha yake—hiki ni kipindi cha ukomavu. Kwa kuzingatia uzoefu wa aina tofauti na ufahamu ambao watu hupata katika vipindi hivi vitatu, katika hali za kawaida fursa ya mtu ya kujua ukuu wa Muumba si kubwa sana. Kama mtu ataishi kufikisha umri wa miaka sitini, mtu anayo miaka thelathini tu au zaidi ya kuujua ukuu wa Mungu; kama mtu atataka kipindi kirefu zaidi cha muda, hilo linawezekana tu kama maisha ya mtu yatakuwa marefu zaidi, tuseme kama mtu ataweza kuishi karne moja. Kwa hivyo Ninasema, kulingana na sheria za kawaida za uwepo wa binadamu, ingawa ni mchakato mrefu sana kuanzia wakati ule mtu anakumbana na mada ya kujua ukuu wa Muumba hadi pale ambapo mtu anaweza kutambua ukweli wa ukuu wa Muumba, na kutoka hapo mpaka pale ambapo mtu anaweza kujinyenyekeza kwa utawala huo, kama kwa hakika mtu atahesabu miaka hiyo, miaka hiyo haizidi thelathini au arubaini hivi ambapo mtu anayo fursa ya kufaidi haya yote. Na mara nyingi, watu hujisahau kutokana na matamanio yao na malengo yao ya kupokea baraka; hawawezi kutambua ni wapi ambapo kiini halisi cha maisha ya binadamu kipo, hawang’amui umuhimu wa kujua ukuu wa Muumba, na kwa hivyo hawafurahii fursa hii yenye thamani ya kuingia kwenye ulimwengu wa binadamu kuhusiana na maisha ya binadamu na kile alichopitia, kupitia ukuu wa Muumba, na hawatambui namna lilivyo jambo la thamani kwa kiumbe chochote kilichoumbwa kupokea mwongozo wa kibinafsi kutoka kwa Muumba. Kwa hivyo Ninasema, wale watu wanaotaka kazi ya Mungu imalizike kwa haraka, wale wanaotamani kwamba Mungu angepangilia mwisho wa binadamu haraka iwezekanavyo, ili waweze mara moja kutazama nafsi Yake halisi na kubarikiwa haraka iwezekanavyo—ni wenye hatia ya aina mbaya zaidi ya kutotii na wao ni wapumbavu kupindukia. Na kwa wale wanaotamani, katika muda wao mfupi, kushikilia fursa hii ya kipekee ili kuujua ukuu wa Muumba, hao ni watu wenye hekima, walio na akili. Matamanio haya mawili tofauti yanafichua mitazamo miwili tofauti na ufuatiliaji tofauti: Wale wanaotafuta baraka ni wabinafsi na wa kudharauliwa, hawafikirii kamwe mapenzi ya Mungu, hawataki kamwe kujua ukuu wa Mungu, na wala hawataki kutii ukuu wa Mungu, bali wanataka tu kuishi wanavyopenda. Wao ni wapotovu wasiojali; wao ndio wameku kuangamizwa. Wale wanaotafuta kumjua Mungu wanaweza kuweka pembeni matamanio yao, wako radhi kujinyenyekeza kwa ukuu wa Mungu na mipangilio ya Mungu; wanajaribu kuwa aina ya watu ambao wananyenyekea katika mamlaka ya Mungu na kukidhi nia za Mungu. Watu kama hao wanaishi katika nuru, wanaishi katikati ya baraka za Mungu; kwa hakika wataweza kusifiwa na Mungu. Haijalishi ni nini, chaguo la binadamu halina manufaa, binadamu hawana kauli yoyote kuhusiana na muda ambao kazi ya Mungu itachukua. Ni bora zaidi kwa watu kujiweka chini ya udhibiti wa Mungu, kunyenyekea katika ukuu Wake. Usipojiweka chini ya udhibiti Wake, ni nini utakachofanya? Je, Mungu atakuwa na hasara yoyote? Usipojiweka chini ya udhibiti Wake, ukijaribu kuushika usukani, unafanya chaguo la kipumbavu, na wewe tu ndiwe utakayepata hasara hatimaye. Endapo tu watu watashirikiana na Mungu haraka iwezekanavyo, endapo tu watafanya hima kukubali mipango Yake, kujua mamlaka Yake, na kutambua yote ambayo Amewafanyia, ndipo watakapokuwa na tumaini, ndipo maisha yao yatakapokuwa hawajayaishi bure, na, ndipo watakapopata wokovu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 135)
Hakuna Anayeweza Kubadilisha Ukweli Kwamba Mungu Anashikilia Ukuu juu ya Hatima ya Binadamu
Chini ya mamlaka ya Mungu kila mtu anakubali waziwazi au kimyakimya ukuu Wake na mipangilio Yake, na haijalishi ni vipi ambavyo mtu anashughulika katika mkondo wa maisha yake, haijalishi ni njia ngapi potovu ambazo mtu ametembelea, mwishowe atarudi tu kwenye njia ya hatima ambayo Muumba amempangia yeye. Hii ndiyo hali ya kutoweza kushindwa kwa mamlaka ya Muumba, namna ambavyo mamlaka Yake yanadhibiti na kutawala ulimwengu. Ni hii hali ya kutoweza kushindwa, aina hii ya udhibiti na utawala, ambao unawajibikia sheria zinazoamuru maisha ya kila kitu, ambayo inawaruhusu wanadamu kuzaliwa upya tena na tena bila kuingiliwa, ambayo inaufanya ulimwengu kuzunguka mara kwa mara na kusonga mbele, siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka. Mmezishuhudia kweli hizi zote na mmezielewa, haijalishi kama ni za juujuu ama ni za kina; kina cha ufahamu wako kinategemea kile unachopitia na maarifa ya ukweli, na maarifa yako kuhusu Mungu. Jinsi unavyojua vyema uhalisia wa ukweli, ni kiwango kipi ambacho umepitia matamshi ya Mungu, jinsi unavyojua vyema kiini cha Mungu na tabia Yake—hii inawakilisha kina cha ufahamu wako wa ukuu na mipangilio ya Mungu. Je, kuwepo kwa ukuu na mipangilio ya Mungu kunategemea ikiwa wanadamu wanaitii? Je, ukweli kwamba Mungu anamiliki mamlaka haya inaamuliwa na iwapo wanadamu wanayanyenyekea? Mamlaka ya Mungu yapo licha ya hali mbalimbali; katika hali zote, Mungu anaamuru na kupangilia hatima ya kila binadamu na mambo yote kulingana na fikira Zake, na mapenzi Yake. Hili halitabadilika kutokana na mabadiliko ya mwanadamu; haitegemei mapenzi ya mwanadamu, haiwezi kubadilishwa na mabadiliko yoyote ya wakati, anga, na jiografia, kwa kuwa mamlaka ya Mungu ni kiini Chake hasa. Iwapo mwanadamu anaweza kujua na kukubali ukuu wa Mungu, na kama mwanadamu anaweza kuunyenyekea—hakuna lolote kati ya haya linalobadilisha hata kidogo ukweli wa ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu. Hiyo ni kusema kwamba, haijalishi ni mtazamo gani ambao binadamu atachukua kwa ukuu wa Mungu, haiwezi tu kubadilisha ukweli kwamba Mungu anashikilia ukuu juu ya hatima ya mwanadamu na juu ya vitu vyote. Hata kama hutanyenyekea katika ukuu wa Mungu, bado Anaamuru hatima yako; hata kama huwezi kuujua ukuu Wake, mamlaka Yake yangali yapo. Mamlaka ya Mungu na ukweli wa ukuu wa Mungu dhidi ya hatima ya binadamu viko huru dhidi ya mapenzi ya binadamu, na hayabadiliki kulingana na mapendeleo na machaguo ya binadamu. Mamlaka ya Mungu yapo kila mahali, kila saa, kila mara. Mbingu na nchi zitapita, lakini mamlaka Yake hayatapita kamwe, kwa kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe, Anamiliki mamlaka ya kipekee, na mamlaka Yake hayazuiliwi au kuwekewa mipaka na watu, matukio, au vitu, na anga au na jiografia. Siku zote Mungu hushikilia mamlaka Yake, huonyesha uwezo Wake, huendeleza usimamizi Wake wa kazi kama kawaida; kila wakati Anatawala vitu vyote, Anatosheleza vitu vyote, Anapangilia vitu vyote—kama tu Anavyofanya daima. Hakuna anayeweza kubadilisha hili. Huu ni ukweli; umekuwa ukweli usiobadilika tangu zamani!
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 136)
Mtazamo na Vitendo Vinavyofaa kwa Mtu Anayetamani Kujinyenyekeza katika Mamlaka ya Mungu
Je, watu wanapaswa kuwa na mtazamo gani sasa katika kuelewa na kuyachukulia mamlaka ya Mungu, na ukweli wa ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu? Hili ni tatizo halisi linalomkabili kila mmoja. Wakati wa kukabiliana na matatizo halisi katika maisha, je, unafaa kujua na kuelewa vipi mamlaka ya Mungu na ukuu Wake? Wakati hujui namna ya kuelewa, kushughulikia, na kupitia matatizo haya, je, ni mtazamo gani unaofaa kutumia ili kuonyesha nia yako, tamanio lako, na uhalisia wako wa kujinyenyekeza katika ukuu na mipangilio ya Mungu? Kwanza lazima ujifunze kusubiri; kisha lazima ujifunze kutafuta; kisha lazima ujifunze kujinyenyekeza. “Kusubiri” kunamaanisha kusubiria muda wa Mungu, kusubiria watu, matukio, na mambo ambayo Amekupangilia wewe, kusubiria mapenzi Yake ili yaweze kwa utaratibu kujifichua kwako. “Kutafuta” kunamaanisha kuchunguza na kuelewa nia za Mungu katika fikira Zake kwako wewe kupitia watu, matukio, na mambo ambayo Amekuwekea wazi, kuelewa ukweli kupitia mambo hayo, kuelewa kile ambacho binadamu lazima watimize na njia ambazo lazima wafuate, kuelewa matokeo ambayo Mungu ananuia kufanikisha kwa wanadamu na mafanikio Anayonuia kufikia ndani yao. “Kujinyenyekeza,” bila shaka, kunaashiria kukubali watu, matukio, na mambo ambayo Mungu amepanga, kukubali ukuu Wake na, kupitia kwayo, kupata kujua namna ambavyo Muumba anaamuru hatima ya binadamu, namna Anavyomjaliza binadamu na maisha Yake, na namna Anavyofanya kazi ya ukweli ndani ya mwanadamu. Vitu vyote chini ya mipango na ukuu wa Mungu vinatii sheria za asili, na kama utaamua kumwachia Mungu akupangilie na kuamuru kila kitu kwa ajili yako, unafaa kujifunza kusubiri, unafaa kujifunza kutafuta, unafaa kujifunza kujinyenyekeza. Huu ndio mtazamo ambao kila mtu anayetaka kujinyenyekeza katika mamlaka ya Mungu lazima awe nao, ubora wa kimsingi ambao kila mmoja anayetaka kuukubali ukuu na mipangilio ya Mungu lazima aumiliki. Ili kushikilia mtazamo kama huu, kumiliki ubora kama huu, lazima mfanye kazi kwa bidii zaidi; na hapo ndipo mtakapoweza kuingia kwenye uhalisi wa kweli.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 137)
Kumkubali Mungu kama Bwana Wenu wa Kipekee Ndiyo Hatua ya Kwanza katika Kufikia Wokovu
Ukweli kuhusiana na mamlaka ya Mungu ni ukweli ambao kila mmoja lazima atilie maanani kwa umakinifu, lazima apitie na aelewe katika moyo wake; kwani ukweli huu unao uhusiano katika maisha ya kila mmoja, kwenye maisha ya kale, ya sasa, na ya siku za usoni za kila mmoja, kwenye awamu muhimu ambazo kila mtu lazima apitie maishani, katika maarifa ya binadamu kuhusu ukuu wa Mungu na mtazamo ambao anafaa kuwa nao katika mamlaka ya Mungu, na kwa kawaida, kwenye hatima ya mwisho ya kila mmoja. Kwa hivyo inachukua nguvu za maisha yako yote kujua na kuyaelewa. Unapochukulia mamlaka ya Mungu kwa umakinifu, unapoukubali ukuu wa Mungu, kwa utaratibu utaanza kutambua na kuelewa kwamba mamlaka ya Mungu kwa kweli yapo. Lakini kama hutawahi kutambua mamlaka ya Mungu, hutawahi kuukubali ukuu Wake, basi haijalishi ni miaka mingapi utakayoishi, hutapata maarifa hata kidogo ya ukuu wa Mungu. Kama hutajua na kuelewa kwa kweli mamlaka ya Mungu, basi utakapofika mwisho wa barabara, hata kama utakuwa umesadiki katika Mungu kwa miongo kadhaa, hutakuwa na chochote cha kuonyesha katika maisha yako, na kwa kawaida hautakuwa na maarifa hata kidogo ya ukuu wa Mungu juu ya hatima ya mwanadamu. Je, hili si jambo la kusikitisha sana? Kwa hivyo haijalishi umetembea kwa umbali gani maishani, haijalishi unao umri wa miaka mingapi sasa, haijalishi safari yako iliyosalia itakuwa ya umbali gani, kwanza lazima utambue mamlaka ya Mungu na uyachukulie kwa uzito, na ukubali ukweli kwamba Mungu ni Bwana wako wa kipekee. Kutimiza maarifa yaliyo wazi, sahihi na kuelewa ukweli huu kuhusiana na ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu ni funzo la lazima kwa kila mmoja, ndio msingi wa kuyajua maisha ya binadamu na kupata ukweli, ndiyo maisha na funzo la msingi la kumjua Mungu ambalo kila mtu anakabiliana nalo kila siku, na ambayo hakuna yeyote anayeweza kuyakwepa. Kama mmoja wenu angependa kuchukua njia za mkato ili kufikia lengo hili, basi Ninakuambia, hilo haliwezekani! Kama mmoja wenu anataka kukwepa ukuu wa Mungu, basi hilo nalo ndilo haliwezekani zaidi! Mungu ndiye Bwana wa pekee wa binadamu, Mungu ndiye Bwana wa pekee wa hatima ya binadamu, na kwa hivyo haiwezekani kwa binadamu kuamuru hatima yake mwenyewe, haiwezekani kwake kuizidi hatima yake. Haijalishi uwezo wa mtu ni mkubwa kiasi gani, mtu hawezi kuathiri, sembuse kuunda, kupangilia, kudhibiti, au kubadilisha hatima za wengine. Ni Mungu Mwenyewe wa kipekee tu ndiye Anayeweza kuamuru mambo yote kwa binadamu, kwani Yeye tu ndiye anayemiliki mamlaka ya kipekee yanayoshikilia ukuu juu ya hatima ya binadamu; na kwa hivyo Muumba pekee ndiye Bwana wa kipekee wa binadamu. Mamlaka ya Mungu yanashikilia ukuu sio tu juu ya binadamu walioumbwa, lakini hata juu ya viumbe ambavyo havikuumbwa visivyoweza kuonekana na binadamu, juu ya nyota, juu ya ulimwengu mzima. Huu ni ukweli usiopingika, ukweli ambao upo kiuhalisia, ambao hakuna mtu au kitu kinachoweza kuubadilisha. Kama mmoja wenu angali hajatosheka na mambo kama yalivyo, akiamini kwamba kwa kiasi fulani ana ujuzi au uwezo maalum, na bado anafikiria kwamba anaweza kubahatika na kubadilisha hali yake ya sasa au hata kuiepuka; kama utajaribu kubadilisha hatima yako mwenyewe kupitia kwa juhudi za kibinadamu, na hivyo basi kujitokeza kati ya wengine na kupata umaarufu na utajiri; basi Ninakwambia, unayafanya mambo kuwa magumu kwako, unajitakia taabu tu, unajichimbia kaburi lako mwenyewe! Siku moja, hivi karibuni au baadaye, utagundua kwamba ulifanya chaguo baya, kwamba jitihada zako ziliambulia patupu. Malengo yako, tamanio lako la kupambana dhidi ya hatima, na mwenendo wako mwenyewe ulio mbaya, utakuongoza kwenye barabara isiyoweza kukurudisha kule ulikotoka, na kwa hili utaweza kujutia baadaye. Ingawa sasa huoni ubaya wa athari hiyo, unapopitia na kuelewa zaidi na zaidi ukweli kwamba Mungu ndiye Mtawala wa hatima ya mwanadamu, utaanza kwa utaratibu kutambua kile Ninachozungumzia leo na athari zake za kweli. Ikiwa kweli una moyo na roho, na ikiwa wewe ni mtu anayependa ukweli, inategemea ni mtazamo wa aina gani ambao utachukua kuhusiana na ukuu wa Mungu na kuhusiana na ukweli. Na kwa kawaida, hili linaamua kama kweli unaweza kujua na kuelewa mamlaka ya Mungu. Kama hujawahi katika maisha yako kuhisi ukuu wa Mungu na mipangilio yake, na isitoshe hujawahi kutambua na kukubali mamlaka ya Mungu, basi utakuwa huna thamani kabisa, na bila shaka utakuwa ni mlengwa wa kuchukiwa na kukataliwa na Mungu, hayo yote ni kutokana na njia uliyochukua na chaguo ulilofanya. Lakini wale ambao, katika kazi ya Mungu, wanaweza kukubali jaribio Lake, kukubali ukuu Wake, kujinyenyekeza katika mamlaka Yake, na kupata kwa utaratibu uzoefu halisi wa matamshi Yake, watakuwa wametimiza maarifa halisi ya mamlaka ya Mungu, ufahamu halisi wa ukuu Wake, na watakuwa kwa kweli wamejisalimisha kwa Muumba. Watu kama hao tu ndio watakaokuwa wameokolewa kwa kweli. Kwa sababu wameujua ukuu wa Mungu, kwa sababu wameukubali, uelewa wao na kujinyenyekeza kwao katika ukweli wa ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu ni halisi na sahihi. Wakati wanakabiliwa na kifo wataweza, kama Ayubu, kuwa na akili isiyotishwa na kifo, kujinyenyekeza katika mipango na mipangilio ya Mungu katika mambo yote, bila chaguo lolote la kibinafsi, bila tamanio lolote la kibinafsi. Mtu kama huyo tu ndiye atakayeweza kurudi katika upande wa Muumba kama mwanadamu wa kweli aliyeumbwa.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 138)
Amri ya Yehova Mungu kwa Mwanadamu
Mwa 2:15-17 Naye Yehova Mungu akamchukua mtu huyo, na kumweka ndani ya bustani ya Edeni ili ailime na kuihifadhi. Yehova Mungu akamwamrisha mtu huyo, akisema, Unaweza kula kwa uhuru matunda kutoka miti yote ya bustani: Lakini kutoka mti wa maarifa ya mema na maovu, usiyale: kwa kuwa katika siku ambapo utakula matunda kutoka mti huo bila shaka utakufa.
Nyoka Anamshawishi Mwanamke
Mwa 3:1-5 Sasa nyoka alikuwa mwenye hila kuliko wanyama wote wa mwitu ambao Yehova Mungu alikuwa amewaumba. Naye akamwambia mwanamke, Naam, Mungu amesema, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Naye mwanamke akamwambia nyoka, Tunaweza kula matunda ya miti katika bustani: Mungu amesema, Lakini msile wala kuyagusa matunda ya mti ulio katikati ya bustani, msije mkafa. Naye nyoka akamwambia mwanamke, Bila shaka hamtakufa: Kwa kuwa Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, macho yenu yatafunuliwa, nanyi mtakuwa kama miungu, mkijua mema na maovu.
Hivi vifungu viwili ni dondoo kutoka kwa kitabu cha Mwanzo katika Biblia. Je, nyinyi nyote mnavijua vifungu hivi viwili? Hiki ni kitu kilichofanyika mwanzoni wakati binadamu kwanza aliumbwa; lilikuwa ni tukio halisi. Kwanza hebu tuangalie ni amri ya aina gani ambayo Yehova Mungu aliwapa Adamu na Hawa, kwani yaliyomo katika amri hii ni muhimu sana kwa mada yetu ya leo. “Yehova Mungu akamwamrisha mtu huyo, akisema, Unaweza kula kwa uhuru matunda kutoka miti yote ya bustani: Lakini kutoka mti wa maarifa ya mema na maovu, usiyale: kwa kuwa katika siku ambapo utakula matunda kutoka mti huo bila shaka utakufa.” Amri ya Mungu kwa mwanadamu katika kifungu hiki ina nini? Kwanza, Mungu anamwambia mwanadamu kile anachoweza kula, yakiwa ni matunda ya miti ya aina nyingi. Hakuna hatari na hakuna sumu, yote yanaweza kulika na kulika atakavyo mtu, bila wasiwasi wowote. Hii ni sehemu moja. Sehemu nyingine ni onyo. Onyo hili linamwambia mwanadamu mti ambao hawezi kula tunda kutoka—lazima asile tunda kutoka kwa mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Nini kitatokea ikiwa atafanya hivyo? Mungu alimwambia mwanadamu: Ukilila hakika utakufa. Maneno haya yanaeleweka kwa urahisi? Iwapo Mungu angekwambia jambo hili lakini hukuelewa kwa nini, ungelichukulia neno Lake kama kanuni ama amri ya kutiiwa? Maneno kama hayo yanapaswa kutiiwa. Lakini iwapo mwanadamu anaweza ama hawezi kulifuata, maneno ya Mungu hayaachi shaka. Mungu alimwambia mwanadamu kwa uwazi kabisa kile anachoweza kula na kile asichoweza, na kile kitakachofanyika akila kile hapaswi kula. Umeona tabia yoyote ya Mungu katika haya maneno machache ambayo Alisema? Haya maneno ya Mungu ni ya ukweli? Kuna udanganyifu wowote? Kuna uongo wowote? Kuna chochote kinachotisha? (La.) Mungu kwa uaminifu, kwa kweli, kwa dhati Alimwambia mwanadamu kile anachoweza kula na kile asichoweza kula, wazi na dhahiri. Kuna maana iliyofichwa katika maneno haya? Maneno haya yanaeleweka kwa urahisi? Je, kuna haja yoyote ya dhana? Hakuna haja ya kukisia. Maana yake ni wazi kwa mtazamo mmoja, na unaelewa punde tu unapoyaona. Ni wazi kabisa. Yaani, kile Mungu anataka kusema na Anachotaka kuonyesha kinatoka katika moyo Wake. Mambo ambayo Mungu anaonyesha ni safi, yanaeleweka kwa urahisi na ni wazi. Hakuna nia za siri ama maana zilizofichwa. Alizungumza moja kwa moja na mwanadamu, Akimwambia kile anachoweza kula na kile asichoweza kula. Hivyo ni kusema, kupitia maneno haya ya Mungu mwanadamu anaweza kuona kwamba moyo wa Mungu ni wazi, kwamba moyo wa Mungu ni wa kweli. Hakuna uwongo kabisa hapa; si kukwambia kwamba huwezi kula kile kinacholika ama kukwambia “Ifanye na uone kitakachofanyika” na vitu ambavyo huwezi kula. Hamaanishi hivi. Chochote afikiriacho Mungu katika moyo Wake ndicho Anachosema. Nikisema Mungu ni mtakatifu kwa sababu Anaonyesha na kujifichua Mwenyewe ndani ya maneno haya kwa njia hii, unaweza kuhisi kana kwamba Nimefanya jambo lisilokuwa kubwa ama Nimenyoosha ufasiri Wangu mbali kiasi. Kama ni hivyo, usijali, hatujamaliza bado.
Hebu tuzungumze kuhusu “Ushawishi wa Nyoka kwa Mwanamke.” Nyoka ni nani? Shetani. Anashikilia jukumu la foili katika mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita, na ni jukumu ambalo hatuwezi kosa kutaja wakati tunaposhiriki utakatifu wa Mungu. Mbona Nasema hivi? Iwapo hujui uovu na upotovu wa Shetani ama asili ya Shetani, basi huna njia ya kumtambua, wala huwezi kujua utakatifu kweli ni nini. Katika mkanganyiko, watu wanaamini kwamba kile anachofanya Shetani ni chema, kwa sababu wanaishi ndani ya aina hii ya tabia potovu. Bila foili, bila kitu cha kulinganisha nacho, huwezi kujua utakatifu ni nini. Hiyo ndiyo maana lazima Shetani atajwe hapa. Matamko kama hayo si maneno matupu. Kupitia katika maneno na matendo ya Shetani, tutaona jinsi Shetani anavyotenda, jinsi Shetani anavyowapotosha binadamu, na asili na uso wa Shetani ni upi. Basi mwanamke alimwambia nini nyoka? Mwanamke alimweleza nyoka kile Yehova Mungu alikuwa amemwambia. Kwa kufuata alichosema, alikuwa amethibitisha uhalali wa yote ambayo Mungu alikuwa amemwambia? Hangeweza kuthibitisha haya. Kama mtu ambaye alikuwa ameumbwa karibuni, hakuwa na uwezo wa kutambua mema kutoka kwa maovu, wala hakuwa na uwezo wa kufahamu chochote karibu naye. Kwa kutathmini maneno aliyomwambia nyoka hakuwa amethibitisha maneno ya Mungu kuwa kweli katika moyo wake; huu ulikuwa mtazamo wake. Hivyo wakati nyoka aliona kwamba mwanamke huyo hakuwa na mtazamo wa uhakika kwa maneno ya Mungu, alisema: “Bila shaka hamtakufa: Kwa kuwa Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, macho yenu yatafunuliwa, nanyi mtakuwa kama miungu, mkijua mema na maovu.” Kuna chochote kibaya na maneno haya? Mlipomaliza kusoma sentensi hii, mlipata hisia ya nia za nyoka? Nyoka ana nia gani? Anataka kumjaribu mwanamke huyu kumfanya aache kusikiliza maneno ya Mungu, lakini hakuongea moja kwa moja. Kwa hivyo tunaweza kusema kwamba ana ujanja sana. Anaonyesha maana yake kwa njia ya udanganyifu na ya kukwepa ili kufikia malengo anayonuia ambayo anaficha kutoka kwa mwanadamu ndani yake—huu ndio ujanja wa nyoka. Shetani amewahi kuzungumza na kutenda hivi. Anasema “sio kwa uhakika,” bila kuthibitisha kwa njia moja au nyingine. Lakini baada ya kusikia haya, moyo wa huyu mwanamke mjinga uliguswa. Nyoka alifurahia kwa sababu maneno yake yalikuwa na matokeo yaliyotarajiwa—hii ilikuwa nia ya ujanja ya Nyoka. Zaidi ya hayo, kwa kuahidi matokeo ambayo mwanadamu aliamini kuwa mema, alimshawishi, akisema, “siku mtakayokula matunda ya mti huo, macho yenu yatafunuliwa.” Hivyo mwanamke anafikiria: “Kufumbuliwa macho yangu ni jambo zuri!” Na kisha akasema kitu kizuri zaidi, maneno yasiyojulikana na mwanadamu, maneno yaliyo na nguvu kubwa ya majaribu juu ya wale wanaoyasikia: “nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na maovu.” Je, maneno haya hayamvutii mwanadamu sana? Ni kama mtu kukwambia: “Uso wako una umbo zuri. Isipokuwa kwamba daraja la pua yako ni fupi kidogo. Ikiwa utarekebisha hilo, basi utakuwa mrembo wa kiwango cha kimataifa!” Je, kwa mtu ambaye hajawahi kutaka kufanya upasuaji wa urembo, moyo wake utaguswa kusikia maneno haya? Je, maneno haya ni ya kushawishi? Ushawishi huu unakuvutia? Je, ni wa kujaribu? (Ndiyo.) Je, Mungu husema mambo kama haya? Kulikuwa na dokezo lolote la haya katika maneno ya Mungu tuliyoyaangalia sasa hivi? Je, Mungu husema Anachofikiria katika moyo Wake? Mwanadamu anaweza kuona moyo wa Mungu kupitia maneno Yake? (Ndiyo.) Lakini wakati nyoka alikuwa amesema maneno haya kwa mwanamke, uliweza kuona moyo wake? La. Na kwa sababu ya ujinga wa mwanadamu, mwanadamu alishawishiwa kwa urahisi na maneno ya nyoka na alidanganywa kwa urahisi. Hivyo uliweza kuona nia za Shetani? Uliweza kuona madhumuni nyuma ya kile alichosema? Uliweza kuona njama na mpango wake wa ujanja? (La.) Ni aina gani ya tabia inayowakilishwa na njia ya mazungumzo ya Shetani? Ni aina gani ya kiini ulichoona ndani ya Shetani kupitia maneno haya? Je, ni mwenye kudhuru kwa siri? Pengine kijuujuu anakupa tabasamu ama kutofichua maonyesho yoyote. Lakini katika moyo wake anahesabu jinsi ya kufikia lengo lake, na ni lengo hili ambalo huwezi kuliona. Kisha unashawishiwa na ahadi zote anazokupa, manufaa yote anayozungumzia. Unayaona kuwa mazuri, na unahisi kwamba kile anachosema ni cha kufaa zaidi, kikubwa zaidi kuliko asemacho Mungu. Wakati haya yanafanyika, je, mwanadamu basi hawi mfungwa mtiifu? Je, mbinu hizi zinazotumiwa na Shetani si za kikatili? Unajikubali kuzama chini. Bila ya Shetani kusongeza kidole, kwa sentensi hizi mbili unafurahia kumfuata na kumtii. Lengo lake limefikiwa. Je, nia hii si mbaya? Je, huu sio uso wa kimsingi kabisa wa Shetani? Kutoka kwa maneno ya Shetani, mwanadamu anaweza kuona nia zake za husuda, kuona uso wake wenye sura mbaya na kiini chake. Sivyo? Kwa kulinganisha sentensi hizi, bila uchambuzi pengine unaweza kuhisi kana kwamba maneno ya Yehova Mungu ni matupu, ya kawaida, na yasiyo dhahiri, kwamba hayastahili kuhangaikiwa kuusifu uaminifu wa Mungu. Tunapochukua maneno ya Shetani na uso wake wenye sura mbaya na kuvitumia kama foili, hata hivyo, je, haya maneno ya Mungu yanabeba uzito mwingi kwa watu wa leo? (Ndiyo.) Kupitia foili hii, mwanadamu anaweza kuhisi kutokuwa na dosari kwa Mungu. Kila neno analosema Shetani pamoja na nia zake, malengo yake na jinsi anavyoongea—yote yamepotoshwa. Ni nini sifa muhimu ya njia yake ya kuzungumza? Anatumia maneno yasiyo dhahiri kukushawishi bila kukuruhusu kumwona, wala hakuruhusu kutambua lengo lake ni nini; anakuacha uchukue chambo, akikufanya umsifu na kuimba uzuri wake. Je, hii siyo hila ya daima ya Shetani? (Ndiyo.)
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 139)
Mazungumzo kati ya Shetani na Yehova Mungu
Ayubu 1:6-11 Sasa kulikuweko na siku ambapo wana wa Mungu walikuja kujidhihirisha mbele za Yehova, naye Shetani akaja pia kati yao. Naye Yehova akasema kwa Shetani, Ni wapi umetoka? Basi Shetani akamjibu Yehova, na kunena, Natoka katika kuenda hapa na pale duniani, na katika kutembea juu chini humo. Naye Yehova akasema kwa Shetani, je, umemfikiria mtumishi Wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu? Kisha Shetani akamjibu Yehova, na kusema, je, Ayubu anamcha Mungu bure? Wewe hujamzunguka kila upande na ukingo, na kila upande wa nyumba yake, na kila upande wa yote aliyo nayo? Umebariki kazi ya mikono yake, na mali yake inaongezeka nchini. Lakini nyosha mbele mkono Wako sasa, na uguse yote aliyo nayo, na yeye atakulaani mbele ya uso Wako.
Ayubu 2:1-5 Tena kulikuweko na siku ambapo wana wa Mungu walikuja kujidhihirisha mbele za Yehova, naye Shetani akaja pia kati yao ili kujidhihirisha mbele za Yehova. Naye Yehova akasema kwa Shetani, Ni wapi umetoka? Na Shetani akamjibu Yehova, na kunena, Natoka katika kuenda hapa na pale duniani, na katika kutembea juu chini humo. Naye Yehova akasema kwa Shetani, je, umemfikiria mtumishi Wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu? Na bado anashikilia ukamilifu wake, ingawa ulinichochea dhidi yake, ili mimi nimwangamize bila sababu. Naye Shetani akamjibu Yehova, na akasema, Ngozi kwa ngozi, ndiyo, yote ambayo mtu anayo atayatoa kwa sababu ya uhai wake. Lakini nyosha mbele mkono Wako sasa, na uguse mfupa wake na nyama yake, na yeye atakulaani mbele ya uso Wako.
Vifungu hivi viwili vinajumuisha kikamilifu mazungumzo kati ya Mungu na Shetani; vinarekodi kile alichosema Mungu na kile alichosema Shetani. Mungu hakuzungumza sana, na Aliongea kwa urahisi sana. Tunaweza kuona utakatifu wa Mungu katika maneno rahisi ya Mungu? Wengine watasema “hii si rahisi.” Hivyo tunaweza kuona ubaya wa Shetani katika majibu yake? Kwanza wacha tuangalie ni aina gani ya swali ambalo Yehova Mungu alimwuliza Shetani. “Ni wapi umetoka?” Hili ni swali linaloeleweka kwa urahisi? Kuna maana iliyofichwa? La; ni swali la moja kwa moja tu. Kama Ningekuuliza: “Unatoka wapi wewe?” mngejibu vipi? Ni swali gumu kujibu? Mngesema: “Natoka katika kuzungukazunguka, na katika kutembea huku na huku”? (La.) Hamngejibu namna hii, kwa hivyo mnahisi vipi mnapomwona Shetani akijibu kwa njia hii? (Tunahisi kwamba Shetani ni mpumbavu na mjanja.) Unaweza kusema ni nini Ninachohisi? Kila wakati Ninapoona maneno haya Nahisi kuchukizwa kwa sababu anazungumza bila kusema lolote. Je, alijibu swali la Mungu? Maneno yake hayakuwa jibu, hakukuwa na matokeo yoyote. Hayakuwa jibu lililoelekezwa kwa swali la Mungu. “Natoka katika kuenda hapa na pale duniani, na katika kutembea juu chini humo.” Unaelewa nini kutoka kwa maneno haya? Shetani ametoka wapi duniani? Mmepata jibu? (La.) Hii ndiyo “akili” ya ujanja wa Shetani, kutomwacha yeyote kujua anachosema. Baada ya kuyasikia maneno haya, bado huwezi kutambua ni nini amesema, ilhali amemaliza kujibu. Anaamini kwamba amejibu vizuri sana. Basi unahisi vipi? Kuchukizwa? (Ndiyo.) Sasa unaanza kuchukizwa na maneno haya. Maneno ya Shetani yana tabia ya aina fulani: Kile anachosema Shetani hukuacha ukikuna kichwa chako, usiweze kutambua chanzo cha maneno yake. Wakati mwingine Shetani huwa na nia na huzungumza kimakusudi, na wakati mwingine akitawaliwa na asili yake, maneno ya aina hiyo hutokea ghafla, na kutoka moja kwa moja kinywani mwa Shetani. Shetani hatumii muda mrefu kuyapima maneno ya aina hiyo; badala yake, yeye huyatoa bila kufikiri. Mungu alipouliza alipokuwa anatoka, Shetani alijibu kwa maneno machache yasiyo na maana kamili. Unahisi kuchanganyikiwa, bila kujua ametoka wapi hasa. Kuna wowote kati yenu wanaozungumza hivi? Hii ni njia ya aina gani ya kuzungumza? (Si dhahiri na haina jibu la uhakika.) Tunapaswa kutumia aina gani ya maneno kuelezea namna hii ya kuzungumza? Ni ya kupotosha na kudanganya. Tuseme mtu hataki wengine wajue kile alichofanya jana. Unamwuliza: “Nilikuona jana. Ulikuwa unaelekea wapi?” Hakwambii moja kwa moja alikokwenda. Badala yake anasema: “Jana ilikuwa siku ya ajabu kweli. Nimechoka sana!” Je, walijibu swali lako? Walijibu, lakini hilo si jibu ulilokuwa unataka. Huu ni “werevu” wa ujanja wa mwanadamu. Huwezi kugundua wanachomaanisha ama kutambua chanzo ama nia nyuma ya maneno yao. Hujui ni nini wanachojaribu kuepuka kwa sababu ndani ya mioyo yao wanayo hadithi yao wenyewe—hili ni jambo lenye kudhuru kwa siri. Je, kunao wowote kati yenu wanaozungumza namna hii mara kwa mara? (Ndiyo.) Basi madhumuni yenu ni yapi? Je, huwa ni kulinda maslahi yenu wakati mwingine, wakati mwingine kudumisha fahari, nafasi na taswira zenu, ili kulinda siri za maisha yenu binafsi? Haijalishi ni madhumuni gani, hayawezi kutenganishwa na maslahi yenu, yanahusiana na maslahi yenu. Je, hii si asili ya mwanadamu? Wote walio na asili ya aina hii wana uhusiano wa karibu na Shetani, kama sio familia yake. Tunaweza kuisema namna hiyo, sivyo? Kwa ujumla, udhihirisho huu ni wa kuchukiza na wenye kuleta karaha. Mnahisi pia sasa kuchukizwa, sivyo? (Ndiyo.)
Hebu tuangalie vifungu vifuatavyo. Shetani analijibu tena swali la Yehova, akisema: “Je, Ayubu anamcha Mungu bure?” Shetani anaanzisha mashambulizi juu ya tathmini ya Yehova kwa Ayubu, na shambulio hili linapakwa rangi na uhasama. “Wewe hujamzunguka kila upande na ukingo, na kila upande wa nyumba yake, na kila upande wa yote aliyo nayo?” Huu ndio uelewa na tathmini ya Shetani ya kazi ya Yehova kwa Ayubu. Shetani anaitathmini hivi, akisema: “Umebariki kazi ya mikono yake, na mali yake inaongezeka nchini. Lakini nyosha mbele mkono Wako sasa, na uguse yote aliyo nayo, na yeye atakulaani mbele ya uso Wako.” Shetani huongea kwa utata kila mara, lakini hapa anaongea kwa uhakika. Hata hivyo, maneno haya yaliyozungumzwa kwa uhakika ni shambulio, ni kufuru na ni upinzani kwa Yehova Mungu, kwa Mungu Mwenyewe. Mnahisi vipi mnapomsikia? Je, mnahisi chuki? Je, mnaweza kuona nia zake? Kwanza kabisa, anakataa kabisa tathmini ya Yehova ya Ayubu—yule anayemwogopa Mungu na kuepuka maovu. Kisha anakataa kabisa kila kitu anachosema na kufanya Ayubu, yaani, anakataa kumcha kwake Yehova. Je, yeye anashitaki? Shetani anashitaki, anakataa na anashuku kila anachofanya na kusema Yehova. Haamini, akisema, “Ukisema mambo yako namna hii, mbona sijaiona? Umempa baraka nyingi, anawezaje kukosa kukucha?” Je, huku si kukataa kabisa kila anachofanya Mungu? Kushitaki, kukataa, kufuru—maneno yake si ya ugomvi? Si ni maonyesho ya ukweli ya kile anachofikiria Shetani ndani ya moyo wake? Haya maneno hakika si sawa na maneno tuliyoyasoma hivi sasa: “Natoka katika kuenda hapa na pale duniani, na katika kutembea juu chini humo.” Ni tofauti sana na hayo. Kupitia maneno haya, Shetani anaweka wazi mtazamo wake kwa Mungu na kuchukizwa na kumcha Mungu kwa Ayubu ambako kuko katika moyo wake. Haya yakifanyika, ubaya wake na asili yake mbovu inafichuliwa kabisa. Anawachukia wale wanaomcha Mungu, anawachukia wale wanaoepukana na maovu, na hata zaidi anamchukia Yehova kwa sababu ya kumpa mwanadamu baraka. Anataka kutumia fursa hii kumwangamiza Ayubu ambaye Mungu alimwinua na mkono Wake mwenyewe, kumwangamiza, akisema: “Unasema Ayubu anakuogopa na kuepukana na maovu. Naiona kwa namna nyingine.” Anatumia mbinu mbalimbali kumchochea na kumjaribu Yehova, na kutumia mbinu mbalimbali ili Yehova Mungu amkabidhi Ayubu kwa Shetani ili atawaliwe, adhuriwe na ashughulikiwe kwa ukatili. Anataka kutumia fursa hii ili kumwangamiza mtu huyu ambaye ni mwenye haki na mtimilifu katika macho ya Mungu. Je, yeye kuwa na moyo wa aina hii ni msukumo wa muda mfupi? La, sivyo. Imekuwa ikiundwa kwa muda mrefu. Mungu anapofanya kazi, kumjali mtu, na kumchunga mtu huyu, na Anapompendelea na kumpa kibali mtu huyu, Shetani hufuata nyuma kwa karibu, akijaribu kumdanganya mtu huyo na kumletea madhara. Mungu akitaka kumpata mtu huyu, Shetani atafanya kila awezalo kumzuia Mungu, akitumia mbinu mbalimbali za uovu ili kuijaribu, kuivuruga na kuiharibu kazi ya Mungu, ili kufikia lengo lake lililofichika. Lengo hili ni lipi? Hataki Mungu ampate mtu yeyote; anataka kuwanyakua wale ambao Mungu anataka kuwapata, anataka kuwadhibiti, kuwasimamia ili wamwabudu, na hivyo wajiunge naye katika kutenda maovu, na kumpinga Mungu. Je, hii si nia mbaya ya Shetani? Mara nyingi ninyi husema kwamba Shetani ni mwovu sana, mbaya sana, lakini je, unaona? Unaweza kuona jinsi mwanadamu alivyo mbaya; hujaona jinsi Shetani halisi alivyo mbaya. Lakini katika suala la Ayubu, umeona wazi jinsi Shetani alivyo mwovu. Jambo hili limeuweka wazi uso wa Shetani wa kutisha na kiini chake. Katika kupigana na Mungu, na kufuata nyuma Yake, lengo la Shetani ni kubomoa kazi yote ambayo Mungu anataka kufanya, kuwachukua na kuwadhibiti wale ambao Mungu anataka kuwapata, kuwazima kabisa wale ambao Mungu anataka kuwapata. Ikiwa hawataangamizwa basi watakuja kwa milki ya Shetani kutumiwa naye—hili ndilo lengo lake. Na Mungu anafanya nini? Mungu anasema tu sentensi rahisi katika kifungu hicho; hakuna rekodi ya chochote zaidi ambacho Mungu anafanya, lakini tunaona kwamba kuna rekodi nyingi zaidi za kile ambacho Shetani anafanya na kusema. Katika kifungu kifuatacho cha maandiko, Yehova anamwuliza Shetani, “Ni wapi umetoka?” Jibu la Shetani ni nini? (Bado ni “Natoka katika kuenda hapa na pale duniani, na katika kutembea juu chini humo.”) Bado ni sentensi ile ile. Hii imekuwa kauli mbiu ya Shetani, kadi ya mwitikio wa Shetani. Imekuwaje hivi? Si Shetani ni mwenye kuchukiza? Hakika inatosha kutamka sentensi hii ya kuchukiza mara moja tu. Kwa nini Shetani anazidi kuirudiarudia? Hii inadhihirisha kitu kimoja: asili ya Shetani haibadiliki. Shetani hawezi kutumia visingizio kuficha uso wake mbaya. Mungu anamwuliza swali na hivi ndivyo anavyojibu. Kwa kuwa hivi ndivyo ilivyo, tafakari basi jinsi anavyowatendea wanadamu! Shetani hamwogopi Mungu, hamchi Mungu, na hamtii Mungu. Hivyo anathubutu kuwa na kiburi kwa ukaidi mbele ya Mungu, kutumia haya maneno ili kujaribu kupuuza swali la Mungu, kutumia jibu hili moja kwa kurudia rudia kujibu swali la Mungu, kujaribu kutumia jibu hili kumshangaza Mungu—huu ndio uso usiopendeza wa Shetani. Haamini uweza wa Mungu, haamini mamlaka ya Mungu, na hakika hayuko tayari kujinyenyekeza chini ya mamlaka ya Mungu. Daima anampinga Mungu, daima anashambulia yote anayofanya Mungu, akijaribu kuharibu yote ambayo Mungu anafanya—hili ndilo lengo lake ovu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 140)
Mazungumzo kati ya Shetani na Yehova Mungu
Ayubu 1:6-11 Sasa kulikuweko na siku ambapo wana wa Mungu walikuja kujidhihirisha mbele za Yehova, naye Shetani akaja pia kati yao. Naye Yehova akasema kwa Shetani, Ni wapi umetoka? Basi Shetani akamjibu Yehova, na kunena, Natoka katika kuenda hapa na pale duniani, na katika kutembea juu chini humo. Naye Yehova akasema kwa Shetani, je, umemfikiria mtumishi Wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu? Kisha Shetani akamjibu Yehova, na kusema, je, Ayubu anamcha Mungu bure? Wewe hujamzunguka kila upande na ukingo, na kila upande wa nyumba yake, na kila upande wa yote aliyo nayo? Umebariki kazi ya mikono yake, na mali yake inaongezeka nchini. Lakini nyosha mbele mkono Wako sasa, na uguse yote aliyo nayo, na yeye atakulaani mbele ya uso Wako.
Ayubu 2:1-5 Tena kulikuweko na siku ambapo wana wa Mungu walikuja kujidhihirisha mbele za Yehova, naye Shetani akaja pia kati yao ili kujidhihirisha mbele za Yehova. Naye Yehova akasema kwa Shetani, Ni wapi umetoka? Na Shetani akamjibu Yehova, na kunena, Natoka katika kuenda hapa na pale duniani, na katika kutembea juu chini humo. Naye Yehova akasema kwa Shetani, je, umemfikiria mtumishi Wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu? Na bado anashikilia ukamilifu wake, ingawa ulinichochea dhidi yake, ili mimi nimwangamize bila sababu. Naye Shetani akamjibu Yehova, na akasema, Ngozi kwa ngozi, ndiyo, yote ambayo mtu anayo atayatoa kwa sababu ya uhai wake. Lakini nyosha mbele mkono Wako sasa, na uguse mfupa wake na nyama yake, na yeye atakulaani mbele ya uso Wako.
Katika mpango wa Mungu wa usimamizi wa miaka elfu sita, vifungu hivi viwili ambavyo Shetani anasema na mambo ambayo Shetani anafanya katika kitabu cha Ayubu yanawakilisha upinzani wake kwa Mungu, na hivi ndivyo Shetani akidhihirisha alivyo kwa kweli. Umeyaona maneno na matendo ya Shetani katika maisha halisi? Utakapoyaona, unaweza kutoyafikiria kuwa vitu vilivyoongelewa na Shetani, lakini badala yake kuyafikiria kuwa vitu vilivyoongelewa na mwanadamu. Kipi kilichowakilishwa, wakati mambo kama hayo yanazungumzwa na mwanadamu? Shetani anawakilishwa? Hata kama utamtambua, bado huwezi kuona kwamba ukweli unazungumzwa na Shetani. Lakini hapa na sasa umeona bila shaka kile ambacho Shetani mwenyewe amesema. Sasa una uelewa usio na shaka na ulio wazi kabisa wa uso wenye sura mbaya na uovu wa Shetani. Hivyo hivi vifungu viwili vilivyozungumzwa na Shetani ni vya thamani kwa watu wa leo kuweza kujua asili ya Shetani? Hivi vifungu viwili vinastahili kukusanywa ili binadamu leo aweze kutambua uso wenye sura mbaya wa Shetani, kutambua uso wa asili na wa kweli wa Shetani? Ingawa kusema jambo hili hakuonekani kufaa sana, kulieleza kwa njia hii bado kunaweza kuchukuliwa kuwa sahihi. Naweza tu kuliweka kwa njia hii na iwapo mnalielewa, basi imetosha. Tena na tena, Shetani anayashambulia mambo ambayo Yehova anafanya, akitoa mashtaka kuhusu kumcha Yehova kwa Ayubu. Anajaribu kumchochea Yehova kwa kutumia mbinu mbalimbali, kumfanya Yehova Mungu kumkubali kumjaribu Ayubu. Maneno yake basi yanachochea sana. Basi Niambieni, baada ya Shetani kuzungumza maneno haya, Mungu anaweza kuona wazi kile ambacho Shetani anataka kufanya? (Ndiyo.) Katika moyo wa Mungu, huyu mtu Ayubu ambaye Mungu anamwangalia—huyu mtumishi wa Mungu, ambaye Mungu anamchukulia kuwa mwenye haki, mtu mtimilifu—anaweza kuyahimili majaribio ya aina hii? (Ndiyo.) Kwa nini Mungu ana uhakika sana kuhusu hilo? Mungu huchunguza moyo wa binadamu daima? (Ndiyo.) Kwa hivyo Shetani anaweza kuchunguza moyo wa binadamu? Shetani hawezi. Hata kama Shetani anaweza kuona moyo wa mwanadamu, asili yake mbovu haiwezi kuamini kwamba utakatifu ni utakatifu, ama kwamba uchafu ni uchafu. Shetani mwovu hawezi kuthamini chochote kilicho takatifu, chenye haki ama chenye kung’aa. Shetani hawezi kuepuka kuumiza kwa kutenda kupitia asili yake, uovu wake, na kupitia mbinu hizi anazotumia. Hata kwa hatari ya yeye kuadhibiwa na kuangamizwa na Mungu, hasiti kumpinga Mungu kwa ukaidi—huu ni uovu, hii ni asili ya Shetani. Kwa hivyo katika kifungu hiki, Shetani anasema: “Ngozi kwa ngozi, ndiyo, yote ambayo mtu anayo atayatoa kwa sababu ya uhai wake. Lakini nyosha mbele mkono wako sasa, na uguse mfupa wake na nyama yake, na yeye atakulaani mbele ya uso Wako.” Shetani anafikiri kwamba kumcha Mungu kwa mwanadamu ni kwa sababu mwanadamu amepata manufaa mengi kutoka kwa Mungu. Mwanadamu hupata manufaa mengi kutoka kwa Mungu, kwa hivyo anasema Mungu ni mwema. Lakini si kwa sababu Mungu ni mwema, ni kwa sababu tu mwanadamu amepata manufaa mengi na hivyo anaweza kumcha Mungu kwa njia hii: Punde Mungu anapomnyima manufaa haya, basi anaachana na Mungu. Katika asili yake mbovu, Shetani haamini kwamba moyo wa mwanadamu kwa kweli unaweza kumcha Mungu. Kwa sababu ya asili yake mbovu hajui utakatifu ni nini, na hata chini zaidi hajui heshima ya kuogopa ni nini. Hajui ni nini kumtii Mungu ama ni nini kumcha Mungu. Kwa sababu yeye mwenyewe hazijui, anafikiri mwanadamu hawezi kumcha Mungu pia. Niambieni, si Shetani ni mwovu? Isipokuwa kanisa letu, hakuna kati ya makundi ya kidini na madhehebu mbalimbali, ama makundi ya kidini na ya kijamii, yanayoamini uwepo wa Mungu, sembuse wao kuamini kwamba Mungu amekuwa mwili na Anafanya kazi ya hukumu, hivyo wanafikiri kwamba kile unachoamini si Mungu. Mwanamume mzinzi huangalia huku na kule na kumwona kila mtu mwingine kama mzinzi, kama alivyo yeye. Mwanadamu anayedanganya kila wakati anaangalia na kuona hakuna mtu mwaminifu, anawaona wote wakidanganya. Mtu mwovu anawaona watu wote wakiwa waovu na anataka kupigana na kila mtu anayemwona. Wakati wale watu ambao ni waaminifu kwa kulinganisha wanawaona wote kuwa waaminifu, na hivyo daima wanalaghaiwa, wanadanganywa, na hakuna wanachoweza kufanya kuhusu hilo. Nasema mifano hii michache ili kuwafanya kuwa na uhakika zaidi: asili mbovu ya Shetani si msukumo wa muda mfupi ama kitu kinachosababishwa na mazingira yake, wala si udhihirisho wa muda ulioletwa na sababu yoyote ama usuli wowote. Sivyo kabisa! Hana namna ila kuwa hivyo! Hawezi kufanya chochote chema! Hata anaposema kitu kinachofurahisha kusikia, anakushawishi tu. Kadiri maneno yake yanavyofurahisha, yenye busara zaidi, uungwana zaidi, ndivyo nia zake za husuda zinavyokuwa mbaya zaidi nyuma ya maneno haya. Shetani anaonyesha uso na asili ya aina gani katika vifungu hivi viwili? (Ya kudhuru kwa siri, yenye kijicho, na mbovu.) Tabia yake ya msingi ni mbovu, hasa mbovu na yenye kijicho.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 141)
Mungu alimuumba mwanadamu na tangu hapo daima Ameongoza maisha ya binadamu. Iwe kwa kuwapa wanadamu baraka, kuwapa sheria na amri Zake, ama kuweka masharti kanuni mbalimbali za maisha, mnajua lengo analonuia Mungu kwa kufanya mambo haya ni nini? Kwanza, mnaweza kusema kwa uhakika kwamba yote anayofanya Mungu ni kwa wema wa binadamu? Mnaweza kufikiria kwamba sentensi hii kwa kulinganishwa ni pana na tupu, lakini kuzungumza hasa, si kila kitu anachofanya Mungu ni cha kumwongoza na kumwelekeza mwanadamu kuishi maisha ya kawaida? Iwe ili mwanadamu ashike kanuni Zake ama ashike sheria Zake, lengo la Mungu ni kwa mwanadamu kutomwabudu Shetani, kutodhuriwa na Shetani; hili ndilo la msingi zaidi, na hili ndilo lililofanywa mwanzoni kabisa. Mwanzoni kabisa, wakati mwanadamu hakuelewa mapenzi ya Mungu, Alichukua baadhi ya sheria na kanuni rahisi na kuweka masharti yaliyoshughulikia vipengele vyote vinavyoweza kufikiriwa. Masharti haya ni rahisi, lakini ndani yake kuna mapenzi ya Mungu. Mungu anamthamini, Anamtunza na kwa hakika Anampenda mwanadamu. Kwa hivyo tunaweza kusema kwamba moyo Wake ni mtakatifu? Tunaweza kusema kwamba moyo wake ni safi? (Ndiyo.) Je, Mungu anazo nia zilizofichwa? (La.) Kwa hivyo hili lengo Lake ni sahihi na halisi? Haijalishi masharti aliyoweka Mungu, katika kazi Yake yote yana athari halisi kwa mwanadamu, na yanaongoza njia. Kwa hivyo kuna fikira zozote za kibinafsi katika akili ya Mungu? Je, Mungu anayo malengo zaidi kuhusiana na mwanadamu, ama Anataka kumtumia mwanadamu kwa jinsi fulani? La hasha. Mungu anafanya Asemavyo, na pia Anafikiria namna hii moyoni Mwake. Hakuna mchanganyiko wa madhumuni, hakuna fikira za kibinafsi. Yeye hafanyi chochote kwa ajili yake mwenyewe, lakini Anamfanyia mwanadamu kila kitu kabisa, bila malengo yoyote ya kibinafsi. Ingawa Ana mipango na nia kwa mwanadamu, Hajifanyii chochote. Kila kitu Anachofanya kinafanyiwa mwanadamu tu, kumlinda mwanadamu, kumhifadhi mwanadamu dhidi ya kupotezwa. Hivyo si moyo huu Wake ni wenye thamani? Unaweza kuona hata ishara ndogo zaidi ya moyo wenye thamani kama huu ndani ya Shetani? (La.) Huwezi kuliona dokezo moja la moyo huu kwa Shetani. Kila kitu anachofanya Mungu kinafichuliwa kiasili. Sasa, hebu tutazame jinsi ambavyo Mungu anafanya kazi; Je, anafanyaje kazi Yake? Je, Mungu anazichukua sheria hizi na maneno Yake na kuyafunga pamoja kwa kukaza juu ya kichwa cha kila mtu, kama kama laana inayofungwa na ukanda[a], Akizilazimisha kwa kila mwanadamu? Je, Anafanya kazi namna hii? (La.) Kwa hivyo Mungu anafanya kazi Yake namna gani? Je, Anatishia? Je, Yeye huwazungumzia kwa njia isiyo ya moja kwa moja? (La.) Wakati huelewi ukweli, Mungu hukuongoza vipi? Anakuangazia, akikwambia wazi kwamba kufanya haya hakuambatani na ukweli, na kisha Anakuambia kile unachofaa kufanya. Kutoka kwa njia hizi ambazo Mungu anafanya kazi, unahisi kwamba una uhusiano wa aina gani na Mungu? Je, unahisi kwamba Mungu si mwenye kufikiwa? (La.) Hivyo unahisije unapoona njia hizi ambazo kwazo Mungu hufanya kazi? Maneno ya Mungu ni halisi hasa, na uhusiano Wake na mwanadamu ni wa kawaida hasa. Mungu yuko karibu nawe kwa njia ya pekee; hakuna umbali kati yako na Mungu. Wakati Mungu anakuongoza, Anapokukimu, Anapokusaidia na kukufadhili, unahisi jinsi Mungu alivyo mpole, uchaji Anaoleta; unahisi jinsi Anavyopendeza, unahisi joto Lake. Lakini Mungu anaposhutumu upotovu wako, ama Anapokuhukumu na kukufundisha nidhamu kwa sababu ya kuasi dhidi Yake, Mungu anatumia njia gani? Anakushutumu kwa kutumia maneno? Anakufundisha nidhamu kupitia mazingira yako na kupitia kwa watu, masuala na mambo? (Ndiyo.) Nidhamu hii inafika kiwango kipi? Je, inafikia mahali sawa ambapo Shetani anamdhuru mwanadamu? (La, inafika kiwango ambacho mwanadamu anaweza kuvumilia.) Mungu anafanya kazi kwa njia ya upole, laini, yenye upendo na ya kujali, kwa njia iliyopimwa kwa namna ya ajabu na sahihi. Njia Yake haikufanyi uhisi hisia kali ya mhemuko kama vile; “Mungu lazima aniache nifanye hivi” ama “Lazima Mungu aniache nifanye vile.” Mungu kamwe hakupi mawazo hisia kali zinazofanya mambo yawe yenye kutovumilika. Sivyo? Hata unapoyakubali maneno ya Mungu ya hukumu na kuadibu, unahisi vipi basi? Unapohisi mamlaka ya Mungu na nguvu ya Mungu, unahisi vipi basi? Unahisi kwamba Mungu ni mtakatifu na asiyekosewa? Je, wewe huhisi umbali kati yako na Mungu katika nyakati hizi? Je, wewe huhisi hofu ya Mungu? La—badala yake, unahisi uchaji wenye hofu kwa Mungu. Je, si kwa sababu ya kazi ya Mungu kwamba watu huhisi mambo haya yote? Je, wangekuwa na hisia hizi ikiwa Shetani ndiye aliyekuwa akifanya kazi? La hasha. Mungu hutumia maneno Yake, ukweli Wake na uhai Wake kuendelea bila kusita kumkimu mwanadamu, kumfadhili mwanadamu. Wakati mwanadamu ni mnyonge, wakati mwanadamu anahisi huzuni, Mungu kwa hakika hazungumzi kwa ukali, akisema: “Usijisikie kukata tamaa? Kwa nini wewe ni dhaifu? Kuna sababu gani ya kuwa dhaifu? Wewe huwa dhaifu sana daima, na wewe daima huwa hasi! Kuna haja gani ya wewe kuwa hai? Kufa tu!” Je, Mungu anafanya kazi hivi? (La.) Je, Mungu ana mamlaka ya kutenda kwa namna hii? Ndiyo, Anayo. Lakini Mungu hatendi kwa namna hii. Mungu hatendi hivi kwa sababu ya kiini Chake, kiini cha utakatifu wa Mungu. Upendo Wake kwa mwanadamu, kuthamini na utunzaji Wake wa mwanadamu haviwezi kuelezwa wazi kwa sentensi moja au mbili. Si kitu kinacholetwa na kujisifu kwa mwanadamu lakini ni kitu ambacho Mungu analeta kupitia kwa vitendo halisi; ni ufunuo wa kiini cha Mungu. Je, hizi njia zote ambazo Mungu anafanya kazi zinaweza kumruhusu mwanadamu kuona utakatifu wa Mungu? Kwa hizi njia zote ambazo Mungu anafanya kazi, zikiwemo nia nzuri za Mungu, zikiwemo athari ambazo Mungu anataka kutimiza kwa mwanadamu, zikiwemo njia mbalimbali ambazo Mungu anatumia kufanya kazi kwa mwanadamu, aina ya kazi Anayofanya, kile Anachotaka mwanadamu kuelewa—umeona uovu ama ujanja wowote katika nia nzuri za Mungu? (La.) Hivyo, katika kila kitu ambacho Mungu anafanya, kila kitu ambacho Mungu anasema, kila kitu anachofikiria katika moyo Wake, na pia kiini chote cha Mungu anachofichua—tunaweza kumwita Mungu mtakatifu? (Ndiyo.) Je, kuna mtu yeyote amewahi kuona utakatifu huu duniani, ama kwake mwenyewe? Mbali na Mungu, je, umewahi kuuona ndani ya mtu yeyote ama ndani Shetani? (La.) Kutoka kwa yale tuliyoyazungumzia hadi sasa, je, tunaweza kumwita Mungu wa kipekee, Mungu mtakatifu Mwenyewe? (Ndiyo.) Yote ambayo Mungu anampa mwanadamu, yakiwemo maneno ya Mungu, njia tofauti ambazo kwazo Mungu anafanya kazi kwa mwanadamu, kile ambacho Mungu anamwambia mwanadamu, kile ambacho Mungu anamkumbusha mwanadamu kuhusu, kile ambacho Anashauri na kutia moyo, vyote vimetoka kwa kiini kimoja: Vyote vimetoka kwa utakatifu wa Mungu. Iwapo hakungekuwa na Mungu mtakatifu kama huyu, hakuna mwanadamu ambaye angechukua nafasi Yake kufanya kazi Anayofanya. Iwapo Mungu angewachukua watu hawa na kuwakabidhi kabisa kwa Shetani, mmewahi kufikiria mngekuwa katika hali ya aina gani leo? Je, nyinyi nyote mngekuwa mmeketi hapa, kamili na wasioharibika? Pia mngesema: “Natoka katika kuenda hapa na pale duniani, na katika kutembea juu chini humo”? Je, ungekuwa mshupavu sana, mwenye uhakika sana na mjeuri kupindukia kiasi cha kusema maneno kama hayo na kujigamba bila haya mbele za Mungu? Kwa hakika ungefanya, bila shaka yoyote! Mtazamo wa Shetani kwa mwanadamu unawaruhusu kuona kwamba asili na kiini cha Shetani ni tofauti kabisa na cha Mungu. Ni kiini kipi cha Shetani ambacho ni kinyume na utakatifu wa Mungu? (Uovu wake.) Asili ya uovu ya Shetani ni kinyume na utakatifu wa Mungu. Watu wengi zaidi hawatambui maonyesho haya ya Mungu na kiini hiki cha utakatifu wa Mungu ni kwa sababu wanaishi chini ya umiliki wa Shetani, ndani ya upotovu wa Shetani na ndani ya boma anamoishi Shetani. Hawajui utakatifu ni nini ama jinsi ya kufafanua utakatifu. Hata unapoona utakatifu wa Mungu, bado huwezi kuufafanua kuwa utakatifu wa Mungu kwa uhakika wowote. Hii ni tofauti katika maarifa ya mwanadamu ya utakatifu wa Mungu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV
Tanbihi:
a. “laana inayofungwa na ukanda” ni laana inayotumiwa na mtawa Tang Sanzang katika riwaya ya Kichina Safari ya Magharibi. Anatumia laana hii kumdhibiti Sun Wukong kwa kufunga ukanda wa chuma kwenye kichwa cha Sun Wukong, ukimfanya aumwe na kichwa sana, na hivyo kumfanya aweze kudhibitiwa. Imekuwa istiara ya kueleza kitu kinachomfunga mtu.
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 142)
Ni nini kinachoiwakilisha kazi ya Shetani kwa mwanadamu? Mnapaswa kuweza kujifunza hii kupitia uzoefu wenu wenyewe—ndiyo sifa halisi ya Shetani, kitu anachofanya kwa kurudiarudia, kitu ambacho anajaribu kufanya na kila mtu. Pengine hamwezi kuona sifa hii, kwa hivyo hamhisi kwamba Shetani ni wa kutisha na mwenye chuki sana. Kuna mtu anayejua sifa hii ni nini? (Anamshawishi, anamlaghai na kumjaribu mwanadamu.) Hiyo ni sahihi; hizi ni njia kadhaa ambazo kipengele hiki hujidhihirisha. Shetani pia humdanganya, humshambulia na kumshtaki mwanadamu—haya yote ni udhihirisho. Je, kuna zaidi? (Anasema uwongo.) Kudanganya na kusema uwongo ni jambo la kawaida kabisa kwa Shetani. Mara nyingi yeye hufanya mambo haya. Pia kuna kuwatawala watu, kuwachochea, kuwalazimisha wafanye mambo, kuwaamuru, na kuwamiliki kwa nguvu. Sasa nitawaelezea jambo ambalo litawafanya mjawe na woga, lakini sifanyi hivyo ili kuwatisha. Mungu hufanya kazi katika mwanadamu na humtunza mwanadamu katika mtazamo Wake na moyoni Mwake. Shetani, kwa upande mwingine, hamthamini mwanadamu hata kidogo, na hutumia muda wake wote kufikiria jinsi ya kumdhuru mwanadamu. Je, si hivyo? Anapofikiria kumdhuru mwanadamu, je, hali yake ya akili si huwa ya dharura? (Ndiyo.) Kwa hivyo, kuhusu kazi ya Shetani kwa mwanadamu, nina kauli mbili zinazoweza kuelezea kikamilifu uovu na hila za Shetani, vinavyoweza kuwaruhusu kujua chuki ya Shetani: Katika mtazamo wa Shetani kwa mwanadamu, daima anataka kumiliki na kumtawala kwa nguvu, kila mmoja wao, ili aweze kufika mahali ambapo anaweza kumdhibiti mwanadamu kabisa, kumdhuru mwanadamu, ili aweze kutimiza lengo hili na tamaa isiyowezekana. “Umiliki wa nguvu” unamaanisha nini? Unafanyika na kibali chako, ama bila kibali chako? Unafanyika na kujua kwako, ama bila kujua kwako? Ni bila kujua kwako kabisa! Katika hali ambazo huna ufahamu, pengine wakati hajasema chochote ama pengine wakati hajafanya chochote, wakati hakuna kauli kigezo, hakuna muktadha, yuko hapo karibu nawe, akikuzunguka. Anatafuta fursa ya kukunyonya, kisha anakumiliki kwa nguvu, anakutawala, akitimiza lengo lake la kukudhibiti kikamilifu na kukudhuru. Hii ni nia na tabia ya kawaida zaidi katika mapambano ya Shetani dhidi ya Mungu kwa ajili ya mwanadamu. Mnahisi vipi mnaposikia haya? (Tuna hofu na woga katika mioyo yetu.) Mnahisi kuchukizwa? (Ndiyo.) Mnapohisi kuchukizwa, mnafikiria Shetani hana haya? Mnapofikiria Shetani hana haya, mnahisi kuchukizwa na wale watu walio karibu nanyi ambao daima wanataka kuwatawala, wale walio na matarajio yasiyowezekana ya hadhi na maslahi yao? (Ndiyo.) Hivyo ni mbinu gani anazotumia Shetani kumtawala kwa nguvu na kummiliki mwanadamu? Mnaelewa hili vizuri? Mnaposikia maneno haya mawili “umiliki wa nguvu” na “utawala,” mnahisi chukizo na mnaweza kuhisi uovu uliopo katika maneno haya. Bila kibali ama maarifa yako, Shetani anakutawala, anakumiliki kwa nguvu, na kukupotosha. Unaweza kuonja nini kwa moyo wako? Je, unahisi chuki na maudhi? (Ndiyo.) Wakati unahisi hii chuki na maudhi kwa njia hii ya Shetani, una hisia gani kwa Mungu? (Shukrani.) Shukrani kwa Mungu kwa kukuokoa. Kwa hivyo sasa, wakati huu, unayo hamu ama matakwa ya kumwacha Mungu aongoze kila kitu chako na kutawala kila kitu chako? (Ndiyo.) Kwa muktadha upi? Unasema ndiyo kwa sababu unaogopa kumilikiwa kwa nguvu na kutawaliwa na Shetani? (Ndiyo.) Huwezi kuwa na mawazo kama haya, siyo sahihi. Usiwe na hofu, Mungu yuko hapa. Hakuna chochote cha kuhofia. Ukishaelewa asili mbovu ya Shetani, unapaswa kuwa na uelewa sahihi zaidi ama upendo wa kina wa mapenzi ya Mungu, nia nzuri za Mungu, huruma ya Mungu na stahamala kwa mwanadamu na tabia Yake ya haki. Shetani ni wa kuchukia sana, lakini ikiwa hili bado haliutii moyo upendo wako kwa Mungu na utegemezi na uaminifu wako kwa Mungu, basi wewe ni mtu wa aina gani? Je, uko tayari kumwacha Shetani akudhuru hivyo? Baada ya kuona uovu na ubaya wa Shetani, tunageuka na kisha kumwangalia Mungu. Maarifa yako ya Mungu sasa yamepitia mabadiliko yoyote? Tunaweza kusema Mungu ni mtakatifu? Tunaweza kusema Mungu hana dosari? “Mungu ni Mtakatifu wa kipekee.” Je, Mungu anaweza kustahili cheo hiki? (Ndiyo.) Hivyo ulimwenguni mwote na kati ya vitu vyote, je, ni Mungu Mwenyewe pekee anayeweza kustahili ufahamu huo wa wanadamu? Hivyo, ni nini hasa ambacho Mungu anampa mwanadamu? Je, Anakupa tu utunzaji mdogo, wasiwasi na kukutia maanani kidogo wakati huko makini? Mungu amempa nini mwanadamu? Mungu amempa mwanadamu uhai, Amempa mwanadamu kila kitu, na amempa mwanadamu bila masharti bila kudai chochote, bila nia zozote za siri. Anatumia ukweli, Anatumia maneno Yake, Anatumia uhai Wake kumwongoza na kumwelekeza mwanadamu, kumtoa mwanadamu mbali na madhara ya Shetani, mbali na majaribio ya Shetani, mbali na ushawishi wa Shetani na kumruhusu mwanadamu aone wazi asili mbovu ya Shetani na uso wake unaotisha. Je, upendo na wasiwasi wa Mungu kwa binadamu ni wa kweli? Ni kitu ambacho kila mmoja wenu anaweza kupitia? (Ndiyo.)
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 143)
Kumbuka maisha yenu hadi sasa kwa yote ambayo Mungu amekufanyia katika miaka yote ya imani yako. Iwapo unaihisi kwa kina au la, haikuwa ya umuhimu sana? Haikuwa kile ulichohitaji zaidi kupata? (Ndiyo.) Huu si ukweli? Huu si uhai? (Ndiyo.) Je, Mungu amewahi kukupa nuru, na kisha akuulize umpe Yeye chochote kama malipo ya yale yote Aliyokupa wewe? (La.) Kwa hivyo madhumuni ya Mungu ni yapi? Mbona Mungu anafanya hivi? Mungu pia ana lengo la kukumiliki? (La.) Je, Mungu anataka kuwa mfalme katika moyo wa mwanadamu? (Ndiyo.) Kwa hivyo ni nini tofauti kati ya Mungu kuwa mfalme na umiliki wa nguvu wa Shetani? Mungu anataka kupata moyo wa wanadamu, Anataka kumiliki moyo wa mwanadamu—hii inamaanisha nini? Je, inamaanisha kwamba Mungu anataka wanadamu wawe vibraka Wake? Mashine Yake? (La.) Kwa hivyo madhumuni ya Mungu ni nini? Kuna tofauti kati ya Mungu kutaka kumiliki moyo wa mwanadamu na umiliki wa nguvu wa Shetani na utawala wa mwanadamu? (Ndiyo.) Tofauti ni nini? Mnaweza kuniambia waziwazi? (Shetani anafanya hivyo kwa nguvu ilhali Mungu anamwacha mwanadamu ajitolee.) Je, hii ndiyo tofauti? Mungu anautaka moyo wako Afanyie nini? Na zaidi ya hayo, kwa nini Mungu anataka kukumiliki? Mnaelewa vipi ndani ya mioyo yenu “Mungu anamiliki moyo wa mwanadamu”? Ni lazima tuwe na haki kwa Mungu hapa, vinginevyo watu daima hawataelewa, na kufikiri: “Mungu daima anataka kunimiliki. Anataka kunimiliki kwa nini? Sitaki kumilikiwa, nataka tu kuwa mimi mwenyewe. Mnasema Shetani anawamiliki watu, lakini Mungu pia anawamiliki watu: Haya si sawa? Sitaki kumwacha yeyote kunimiliki. Mimi ni mimi mwenyewe!” Tofauti hapa ni nini? Chukua dakika kuifikiria. Nawauliza, je “Mungu hummiliki mwanadamu” ni kirai tupu? Umiliki wa Mungu wa mwanadamu unamaanisha kwamba Anaishi katika moyo wako na anatawala kila neno na kusonga kwako? Akikwambia uketi, huthubutu kusimama? Akikwambia uende Mashariki, huthubutu kwenda Magharibi? Je, ni umiliki unaomaanisha kiti kama hiki? (La, siyo. Mungu anamtaka mwanadamu kuishi kwa kudhihirisha kile Mungu anacho na alicho.) Kwa miaka hii yote Mungu amemsimamia mwanadamu, kwa kazi Yake kwa mwanadamu hadi sasa kwa hatua hii ya mwisho, ni athari ipi imekusudiwa kwa mwanadamu kuhusu maneno yote ambayo Amesema? Je, ni kwamba mwanadamu anaishi kulingana na kile anacho Mungu na alicho? Kwa kuangalia maana halisi ya “Mungu humiliki moyo wa mwanadamu,” inaonekana kama Mungu anachukua moyo wa mwanadamu na kuumiliki, Anaishi ndani yake na Hatoki nje tena; Anakuwa bwana wa moyo wa mwanadamu na anaweza kutawala na kupanga moyo wa mwanadamu atakavyo, ili kwamba mwanadamu lazima afanye chochote ambacho Mungu anamwambia afanye. Hali ikiwa hivi, ingeonekana kana kwamba kila mtu anaweza kuwa Mungu na awe na kiini na tabia Yake. Kwa hivyo hapa, mwanadamu pia angeweza kufanya matendo ya Mungu? Je, “umiliki” unaweza kuelezewa kwa njia hii? (La.) Kwa hivyo ni nini? Nawauliza hili: Je, maneno na ukweli wote Mungu anampa mwanadamu ni ufunuo wa kiini cha Mungu na kile Anacho na alicho? (Ndiyo.) Hii ni ya uhakika. Lakini je, maneno yote Mungu anampa mwanadamu ni ya Mungu Mwenyewe kuweka katika vitendo, ya Mungu Mwenyewe kumiliki? Chukua dakika moja kuifikiria? Wakati Mungu anamhukumu mwanadamu, Anafanya hivi kwa sababu ya nini? Maneno haya yalitoka wapi? Ni nini yaliyomo katika maneno haya ambayo Mungu anazungumza Anapomhukumu mwanadamu? Ni nini msingi wake? Msingi wake ni tabia potovu ya mwanadamu? (Ndiyo.) Kwa hivyo athari iliyofikiwa na hukumu ya Mungu ya mwanadamu imetokana na kiini cha Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo umiliki wa Mungu wa mwanadamu ni kirai tupu? Kwa hakika sicho. Kwa hivyo mbona Mungu anasema maneno haya kwa mwanadamu? Ni nini madhumuni Yake ya kusema maneno haya? Anataka kutumia maneno haya kutumika kama maisha ya mwanadamu? (Ndiyo.) Mungu anataka kutumia ukweli wote huu ambao amezungumza katika maneno haya kutumika kama maisha ya mwanadamu. Wakati mwanadamu anauchukua ukweli huu wote na neno la Mungu na kuyabadilisha katika maisha yake, mwanadamu basi anaweza kumtii Mungu? Mwanadamu basi anaweza kumcha Mungu? Mwanadamu basi anaweza kuepuka maovu? Wakati mwanadamu amefika hapa, anaweza basi kutii ukuu na mipango ya Mungu? Mwanadamu sasa yuko katika nafasi ya kutii mamlaka ya Mungu? Wakati watu kama Ayubu, ama kama Petro wanafika mwisho wa barabara yao, wakati maisha yao yanaweza kufikiriwa kuwa yamekomaa, wakati wako na uelewa halisi wa Mungu—Shetani bado anaweza kuwapoteza? Shetani bado anaweza kuwamiliki? Shetani bado anaweza kuwatawala kwa nguvu? (La.) Kwa hivyo huyu ni mtu wa aina gani? Huyu ni mtu ambaye amepatwa kabisa na Mungu? (Ndiyo.) Katika kiwango hiki cha maana, unamwonaje mtu huyu ambaye amepatwa kabisa na Mungu? Kwa Mungu, katika hali hii tayari Amemiliki moyo wa mtu huyu. Lakini mtu huyu anahisi nini? Je, ni kwamba neno la Mungu, mamlaka ya Mungu, na njia ya Mungu yamekuwa uhai ndani ya mwanadamu, basi uhai huu unamiliki utu wote wa mwanadamu, na unafanya yote anayozidi pamoja na kiini chake kutosha kumridhisha Mungu? Kwa Mungu, moyo wa binadamu wakati huu umemilikiwa na Yeye? (Ndiyo.) Mnaelewaje kiwango hiki cha maana sasa? Je, ni Roho wa Mungu anayekumiliki? (La, ni neno la Mungu ambalo linatumiliki.) Ni njia ya Mungu na neno la Mungu ambalo limekuwa maisha yako, na ni ukweli ambao umekuwa maisha yako. Wakati huu, mwanadamu basi ana maisha yanayotoka kwa Mungu, lakini hatuwezi kusema kwamba haya maisha ni maisha ya Mungu. Kwa maneno mengine, hatuwezi kusema kwamba maisha ambayo mwanadamu anapaswa kupata kutoka kwa neno la Mungu ni maisha ya Mungu. Hivyo, licha ya muda ambao mwanadamu anamfuata Mungu, licha ya idadi ya maneno ambayo mwanadamu anapata kutoka kwa Mungu, mwanadamu hawezi kuwa Mungu. Hata kama siku moja Mungu aseme, “Nimemiliki moyo wako, sasa unamiliki maisha Yangu,” utahisi basi kwamba wewe ni Mungu? (La.) Utakuwa nini basi? Hutakuwa na utii kabisa wa Mungu? Moyo wako hautajawa na maisha ambayo Mungu amekupa? Huu utakuwa udhihirisho wa kawaida kabisa wa kile kinachofanyika wakati Mungu anamiliki moyo wa mwanadamu. Huu ni ukweli. Kwa hivyo kuuangalia kutoka kipengele hiki, mwanadamu anaweza kuwa Mungu? Mwanadamu anapoweza kuishi kwa kudhihirisha uhalisi wa maneno ya Mungu, na kuwa mtu anayemcha Mungu na kuepuka maovu, je, mwanadamu anaweza kumiliki kiini cha uzima na utakatifu wa Mungu? Licha ya kile kitakachofanyika, mwanadamu bado ni mwanadamu wakati yote yamesemwa na kufanywa. Wewe ni kiumbe aliyeumbwa; wakati umepokea neno la Mungu kutoka kwa Mungu na kupokea njia ya Mungu, unamiliki tu maisha ambayo yanatoka katika maneno ya Mungu, unakuwa mtu anayesifiwa na Mungu, lakini kamwe hutakuwa na kiini cha uzima wa Mungu, sembuse utakatifu wa Mungu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 144)
Majaribu ya Shetani
Mat 4:1-4 Baada ya hapo Yesu akaongozwa mwituni na Roho kwa minajili ya kujaribiwa na ibilisi. Na baada ya Yeye kufunga kwa siku arobaini mchana na usiku, Alihisi njaa. Na aliyemjaribu alipokuja Kwake, alimwambia, Iwapo Wewe ni Mwana wa Mungu, yaamrishe mawe haya yabadilike kuwa mikate. Lakini Akamjibu na kusema, imeandikwa, Mwanadamu hatadumu kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu.
Haya ndiyo maneno ambayo ibilisi kwanza alijaribu kumjaribu Bwana Yesu. Ni nini maudhui ya aliyoyasema ibilisi? (“Iwapo Wewe ni Mwana wa Mungu, yaamrishe mawe haya yabadilike kuwa mikate.”) Maneno haya ambayo ibilisi alizungumza ni rahisi kiasi, lakini kuna tatizo na kiini chake? Ibilisi alisema, “Iwapo Wewe ni Mwana wa Mungu,” lakini katika moyo wake, alijua au hakujua kwamba Yesu alikuwa Mwana wa Mungu? Alijua au hakujua kwamba Alikuwa Kristo? (Alijua.) Basi kwa nini alisema “Iwapo Wewe ni”? (Alikuwa akijaribu kumjaribu Mungu.) Lakini ni nini madhumuni ya kufanya hivyo? Alisema, “Iwapo Wewe ni Mwana wa Mungu.” Katika moyo wake alijua kwamba Yesu Kristo alikuwa Mwana wa Mungu, alijua haya vizuri sana moyoni mwake, lakini licha ya kujua haya, je, alinyenyekea Kwake na kumwabudu Yeye? (La.) Alitaka kufanya nini? Alitaka kutumia mbinu hii na maneno haya kumghadhabisha Bwana Yesu, na kisha kumhadaa Atende kulingana na makusudi yake. Je, si hii ndiyo iliyokuwa maana ya maneno ya ibilisi? Katika moyo wa Shetani, alijua wazi kwamba huyu alikuwa Bwana Yesu Kristo, lakini alisema maneno haya hata hivyo. Je, si hii ni asili ya Shetani? Asili ya Shetani ni nini? (Kuwa mjanja, mwovu na kutokuwa na Heshima kwa Mungu.) Ni matokeo gani yangetokana na kutomcha Mungu? Je, si kwamba alitaka kumshambulia Mungu? Alitaka kutumia mbinu hii kumshambulia Mungu, na hivyo alisema: “Iwapo Wewe ni Mwana wa Mungu, yaamrishe mawe haya yabadilike kuwa mikate”; je, si hii ni nia ovu ya Shetani? Alikuwa anajaribu kufanya nini kweli? Lengo lake ni wazi sana: Alikuwa anajaribu kutumia mbinu hii kukanusha nafasi na utambulisho wa Bwana Yesu Kristo. Alichomaanisha na maneno hayo ni, “Iwapo wewe ni Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate. Usipofanya hivyo, basi wewe siwe Mwana wa Mungu na Hufanyi kazi hii.” Hii ni sahihi? Alitaka kutumia mbinu hii kumshambulia Mungu, alitaka kuvunja na kuharibu kazi ya Mungu; huu ndio uovu wa Shetani. Uovu wake ni maonyesho ya kiasili ya asili yake. Ingawaje alijua Bwana Yesu Kristo alikuwa Mwana wa Mungu, kupata mwili kwenyewe kwa Mungu Mwenyewe, hangeweza kuacha kufanya kitu kama hiki, kumfuata Mungu nyuma na kuendelea kumshambulia na kujaribu sana kuvuruga na kuharibu kazi ya Mungu.
Sasa, hebu tuchambue kirai hiki alichonena Shetani: “Yaamrishe mawe haya yabadilike kuwa mikate” Kubadili mawe yawe mikate—hili linamaanisha chochote? Iwapo kuna chakula, kwa nini usile? Kwa nini ni muhimu kubadili mawe yawe mikate? Kuna maana hapa? Ingawa alikuwa amefunga wakati huo, kwa hakika Bwana Yesu alikuwa na chakula cha kula? (Alikuwa nacho.) Kwa hivyo, hapa, tunaona upumbavu wa matumizi ya Shetani ya kirai hiki. Kwa ujanja na uovu wake wote, tunaona upumbavu na upuuzi wake. Shetani anafanya idadi fulani ya mambo. Unaona asili yake yenye kudhuru na unaona akiharibu kazi ya Mungu, na wa kuchukiza na kuudhi sana. Lakini kwa upande mwingine, unapata asili ya kitoto na ujinga nyuma ya maneno na vitendo vyake? Huu ni ufunuo kuhusu asili ya Shetani; ana asili ya aina hii na atafanya kitu kama hiki. Kwa wanadamu, kirai hiki ni cha upuuzi na cha kuchekesha. Lakini maneno kama hayo kwa hakika yanaweza kutamkwa na Shetani. Tunaweza kusema kwamba ni asiyejua? Mjinga? Uovu wa Shetani uko kila mahali na daima unafichuliwa. Na Bwana Yesu anamjibuje? (“Mwanadamu hatadumu kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu.”) Maneno haya yana nguvu yoyote? (Yanayo.) Mbona tunasema kwamba yana nguvu? Hii ni kwa sababu maneno haya ni ukweli. Sasa, mtu anaishi kwa mkate tu? Bwana Yesu alifunga kwa siku arubanini usiku na mchana. Alikufa kwa njaa? Hakufa kwa njaa, kwa hivyo Shetani alimkaribia, akimwambia abadili mawe yawe chakula kwa kusema kitu kama hiki: “Ukiyabadili mawe yawe chakula, Hutakuwa basi na vitu vya kula? Si basi Hutalazimika kufunga, Hutalazimika kuwa na njaa?” Lakini Bwana Yesu alisema, “Mwanadamu hatadumu kwa mkate pekee,” inayomaanisha kwamba, ingawa mwanadamu anaishi katika mwili, kile kinachouruhusu mwili wake kuishi na kupumua si chakula, ila maneno yote yaliyotamkwa na kinywa cha Mungu. Katika upande mmoja, maneno haya ni ukweli; yanawapa watu imani, yakiwafanya wahisi kwamba wanaweza kumtegemea Mungu na kwamba Yeye ni ukweli. Kwa upande mwingine, kuna kipengele cha vitendo katika maneno haya? Si Bwana Yesu bado amesimama pale na bado Yu hai baada ya kufunga kwa siku arubaini mchana na usiku? Je, huu si mfano? Hajala chakula chochote kwa siku arubaini mchana na usiku. Bado yuko hai. Huu ni ushahidi wa nguvu unaothibitisha ukweli wa maneno Yake. Maneno haya ni rahisi, lakini kwa Bwana Yesu, je, Aliyazungumza tu wakati ambapo Shetani alimjaribu, au yalikuwa tayari pamoja na Yeye? Kuliweka kwa njia nyingine, Mungu ni ukweli, Mungu ni uhai, lakini je, ukweli na uhai wa Mungu uliongezwa kwa kuchelewa? Je, ulitokana na uzoefu? La, ni ya asili ndani ya Mungu, Ambayo inamaanisha ukweli na uhai vipo ndani ya kiini cha Mungu. Licha ya kile kinachomfanyikia, Anachofichua ni ukweli. Ukweli huu, kirai hiki—iwapo maudhui yake ni mapana ama finyu—kinaweza kumwacha mwanadamu aishi, kimpe uhai; kinaweza kumwezesha mwanadamu kupata, ndani yake, ukweli, uwazi kuhusu njia ya maisha ya binadamu, na kumwezesha kuwa na imani kwa Mungu. Kwa maneno mengine, chanzo cha matumizi ya Mungu ya kifungu hiki ni chanya. Kwa hivyo tunaweza kusema jambo hili chanya ni takatifu? (Ndiyo.) Maneno ya Shetani yanatokana na asili ya Shetani. Shetani anafichua asili yake ovu, asili yake yenye kijicho, kila mahali, daima. Sasa, ufunuo huu, Shetani anaufanya kiasili? Kuna yeyote anayemchochea? Kuna yeyote anayemsaidia? Kuna yeyote anayemshurutisha? La. Ufunuo huu wote, yeye anautoa kwa hiari yake mwenyewe. Hii ni asili ovu ya Shetani. Licha ya kile Mungu anafanya na jinsi Anavyokifanya, Shetani yuko nyuma Yake. Kiini na sura ya ukweli ya vitu hivi ambavyo Shetani anasema na kufanya ni kiini cha Shetani—kiini ovu, kiini chenye nia mbaya.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 145)
Majaribu ya Shetani
Mat 4:5-7 Kisha Ibilisi akamchukua hadi katika mji mtakatifu, na kumweka juu ya kinara cha hekalu, Naye akamwambia, Ikiwa Wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jirushe chini: kwa kuwa imeandikwa, Atawaamuru malaika Wake wakuchunge: na watakubeba mikononi mwao, usije ukaukwaa mguu wako kwenye jiwe wakati wowote. Yesu akamwambia, Imeandikwa tena, Usimjaribu Bwana Mungu wako.
Hebu kwanza tuone maneno ambayo Shetani alizungumza hapa. Shetani alisema “Ikiwa Wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jirushe chini,” na kisha akadondoa kutoka kwenye maandiko, “Atawaamuru malaika Wake wakuchunge: na watakubeba mikononi mwao, usije ukaukwaa mguu wako kwenye jiwe wakati wowote.” Unahisi vipi unaposikia maneno ya Shetani? Si ni ya kitoto sana? Ni ya kitoto, upuuzi na kuchukiza. Mbona Nasema hivi? Daima Shetani hufanya kitu kijinga, anaamini kwamba ni mwerevu sana; na mara nyingi hutaja maandiko—hata neno la Mungu—anajaribu kuyabadili maneno haya dhidi ya Mungu kumshambulia na kumjaribu. Lengo lake la kufanya hivi ni kuharibu mpango wa kazi ya Mungu. Je, unaweza kuona chochote katika maneno haya yaliyonenwa na Shetani? (Shetani huwa na nia mbaya) Katika kila ambacho Shetani hufanya, kila mara yeye hutafuta kuwajaribu binadamu. Shetani hazungumzi kwa njia inayoeleweka kirahisi, bali kwa njia isiyo wazi akitumia majaribu, ulaghai na ushawishi. Shetani anachukulia kumjaribu kwake Mungu kana kwamba Yeye alikuwa binadamu wa kawaida, akiamini kwamba Mungu pia ni asiyejua, mjinga, na asiyeweza kutofautisha kwa wazi vitu vilivyo. Shetani anafikiri kwamba Mungu na pia mwanadamu hawataona hadi kwa kiini chake na kwamba Mungu na mwanadamu wote hawataona udanganyifu wake na nia zake mbaya. Si hapa ndipo Shetani anapata ujinga wake? Zaidi, Shetani anataja maandiko wazi; anafikiria kwamba kufanya hivyo kunamfanya kuaminika, na kwamba hutaweza kuona dosari zozote kwa haya ama kuepuka kudanganywa na haya. Si hapa ndipo Shetani anakuwa mjinga na kama mtoto? Hii ni kama wakati watu wengine wanaeneza injili na kuwa na ushuhuda kwa Mungu, si wasioamini watasema kitu kama alichosema Shetani? Mmesikia watu wakisema kitu kama hiki? Ni jinsi gani unahisi kuchukizwa unaposikia vitu kama hivyo? Je, unahisi kuchukizwa? (Ndiyo.) Unapohisi kuchukizwa, pia unahisi kutiwa kinyaa na kukirihishwa? Unapokuwa na hisia hizi unaweza kutambua kwamba Shetani na tabia potovu ambayo Shetani anamfanyia mwanadamu ni ovu? Katika mioyo yenu mmewahi kuwa na utambuzi kama, “Maneno ya Shetani yanaleta mashambulizi na majaribu, maneno yake ni ya kijinga, ya kuchekesha, ya kitoto, na ya kuchukiza. Hata hivyo, katika matamshi ya Mungu na vitendo vya Mungu, Hangetumia mbinu kama hizi kuzungumza ama kufanya kazi Yake, na Hajawahi kufanya hivyo”? Bila shaka, katika hali hii watu wana tu kiasi kidogo cha kuhisi kuendelea na hawana utambuzi wa utakatifu wa Mungu, sivyo? Na kimo chenu cha sasa, mnahisi tu hivi: “Kila kitu Mungu anasema ni ukweli, ni cha manufaa kwetu, na lazima tukikubali”; bila kujali iwapo unaweza kukubali hili au la, bila ubaguzi unasema kwamba maneno ya Mungu ni ukweli na kwamba Mungu ni ukweli, lakini hujui kwamba ukweli ni utakatifu wenyewe na kwamba Mungu ni mtakatifu.
Hivyo, jibu la Yesu kwa maneno haya ya Shetani lilikuwa lipi? Yesu alimwambia: “Imeandikwa tena, Usimjaribu Bwana Mungu wako.” Kuna ukweli katika maneno haya ambayo Yesu alisema? Bila shaka, kuna ukweli ndani yake. Juujuu inaonekana maneno haya ni amri ya watu kufuata, ni kirai rahisi, lakini hata hivyo, mwanadamu na Shetani wamekiuka maneno haya mara nyingi. Hivyo, Bwana alimwambia Shetani, “Usimjaribu Bwana Mungu wako,” kwa sababu hiki ndicho kile Shetani alifanya mara nyingi na alifanya kila juhudi kufanya hivyo, unaweza hata kusema kwamba Shetani alifanya hivyo bila haya. Ni asili ya msingi ya Shetani kutomcha Mungu na kutomheshimu Mungu kwa moyo wake. Hata wakati Shetani alikuwa kando ya Mungu na angeweza kumwona, Shetani hakuweza kuacha kumjaribu Mungu. Kwa hivyo, Bwana Yesu alimwambia Shetani, “Usimjaribu Bwana Mungu wako.” Hiki ni kirai ambacho Mungu amemwambia Shetani mara nyingi. Si kutumia kirai hiki kunafaa hata leo? (Ndiyo, kwani pia sisi humjaribu Mungu mara nyingi.) Kwa nini watu hufanya hivyo mara nyingi? Je, ni kwa sababu watu wamejawa na tabia potovu ya kishetani? (Ndiyo.) Kwa hivyo kile ambacho Shetani alisema hapa juu ni kitu ambacho watu husema mara nyingi? Na katika hali gani? Mtu anaweza kusema kwamba watu wamekuwa wakisema mambo kama haya licha ya wakati na mahali. Hii inadhihirisha kwamba tabia ya watu ni sawa kabisa na tabia potovu ya Shetani. Bwana Yesu alisema maneno rahisi, ambayo yanawakilisha ukweli na ambayo watu wanahitaji. Hata hivyo, katika hali hii Bwana Yesu alikuwa akibishana na Shetani? Je, kulikuwa na jambo lolote la kupingana katika kile Alichomwambie Shetani? (La.) Bwana Yesu aliyachukulia vipi majaribu ya Shetani kwa moyo Wake? Je, Alihisi kuchukizwa na kutiwa kinyaa? Bwana Yesu alihisi kutiwa kinyaa na kuchukizwa lakini Hakugombana na Shetani, wala hata chini zaidi Hakuzungumza kuhusu kanuni zozote kubwa. Kwa nini hivyo? (Kwa sababu Shetani daima yuko hivyo, hawezi kubadilika.) Tunaweza kusema kwamba Shetani hana akili? (Ndiyo, tunaweza.) Je, Shetani anaweza kutambua kwamba Mungu ni ukweli? Shetani hatawahi kutambua kwamba Mungu ni ukweli na hatawahi kukubali kwamba Mungu ni ukweli; hii ni asili yake. Zaidi, kuna kitu kingine kuhusu asili ya Shetani kinachotia kinyaa, ni nini? Katika majaribio yake ya kumjaribu Bwana Yesu, Shetani alifikiri kwamba, hata kama alimjaribu Mungu na hangefaulu, bado angejaribu jambo hili tu. Hata kama angeadhibiwa, angeifanya tu. Hata kama hangepata chochote chema kutoka kwa kufanya hivyo, angeifanya tu, na kuendelea na kusimama dhidi ya Mungu hadi mwisho kabisa. Hii ni asili ya aina gani? Si huo ni uovu? Yule anayekasirika sana wakati Mungu anatajwa, yule anayekuwa na hasira wakati Mungu anatajwa, je, amemwona Mungu? Je, anamjua Mungu? Hajui Mungu ni nani, hamwamini, na Mungu hajaongea naye. Mungu hajawahi kumsumbua, kwa hivyo kwa nini awe na hasira? Tunaweza kusema kwamba mtu huyu ni mwovu? Mitindo ya kidunia, kula, kunywa, na kutafuta raha, na kufuata watu mashuhuri—hakuna chochote kati ya vitu hivi kitakachomsumbua mwanadamu kama huyo. Hata hivyo, “Mungu” akitajwa tu au ukweli wa maneno ya Mungu, yeye anashikwa na hasira ghafla. Je, si huku kunajumuisha kuwa na asili ya uovu? Hili linatosha kuthibitisha kwamba hii ni asili ya uovu ya mwanadamu. Sasa, mkijizungumzia, kuna wakati ambapo ukweli unatajwa, ama wakati majaribio ya Mungu kwa mwanadamu yanatajwa ama wakati maneno ya Mungu ya hukumu dhidi ya mwanadamu yanatajwa, na mnahisi kusumbuliwa, kutiwa kinyaa, na hamtaki kusikia kuyahusu? Mioyo yenu inaweza kufikiri: Si watu wote walisema kwamba Mungu ni ukweli? Baadhi ya maneno haya si ukweli, haya bila shaka ni maneno tu ya Mungu ya maonyo kwa mwanadamu! Watu wengine hata wanaweza kuhisi kuchukizwa mioyoni mwao: Haya yanatajwa kila siku, majaribio Yake kwetu daima yanatajwa kama hukumu Yake; haya yote yataisha lini? Tutapokea lini hatima njema? Haijulikani hasira hii isiyo na sababu inatoka wapi. Hii ni asili ya aina gani? (Asili ovu.) Inasababishwa na asili ovu ya Shetani. Na kwa Mungu kuhusu asili ovu ya Shetani na tabia potovu ya mwanadamu, Hagombani kamwe wala kubishana na watu, na kamwe Halalamiki wakati watu wanatenda kutokana na ujinga. Hamtamwona Mungu akiwa na mitazamo sawa kuhusu vitu ambavyo watu wanavyo, na zaidi hamtamwona Akitumia maoni ya wanadamu, maarifa yao, sayansi yao ama filosofia yao ama fikira za mwanadamu kushughulikia vitu, Badala yake, kila kitu anachofanya Mungu na kila kitu Anachofichua kinahusiana na ukweli. Yaani, kila neno Alilolisema na kila hatua Aliyoichukua inahusiana na ukweli. Ukweli huu sio tu ndoto isiyo na msingi; ukweli huu na maneno haya yanaelezwa na Mungu kwa sababu ya kiini cha Mungu na uhai Wake. Kwa sababu maneno haya na kiini cha kila kitu ambacho Mungu amefanya ni ukweli, tunaweza kusema kwamba kiini cha Mungu ni kitakatifu. Kwa maneno mengine, kila kitu ambacho Mungu anasema na kufanya kinaleta uzima na mwangaza kwa watu, kinawaruhusu watu kuona vitu vizuri na uhalisi wa vitu hivyo vizuri, na inaelekeza njia kwa ajili ya wanadamu ili waweze kutembea katika njia sahihi. Vitu hivi vinaamuliwa kwa sababu ya kiini cha Mungu na vinaamuliwa kwa sababu ya kiini cha utakatifu Wake.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 146)
Majaribu ya Shetani
Mat 4:8-11 Tena, Ibilisi akampeleka hadi kwenye mlima mrefu sana, na kumwonyesha falme zote za dunia, na fahari yao; Na akamwambia, Hivi vyote nitakupa Wewe, Ukianguka chini na kuniabudu. Kisha Yesu akamwambia, Ondoka uende zako, Shetani; kwa kuwa imeandikwa, Muabudu Bwana Mungu wako, na ni Yeye peke Yake ndiye utakayemtumikia. Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.
Shetani, ibilisi, baada ya kushindwa katika hila zake mbili za awali, alijaribu nyingine tena: Alionyesha falme zote duniani na utukufu wa falme hizi kwa Bwana Yesu na kumwambia amwabudu ibilisi. Unaona nini kuhusu sura za ukweli za ibilisi kutoka kwa hali hii? Si Shetani ibilisi hana haya kabisa? (Ndiyo.) Anaweza kukosa haya namna gani? Kila kitu kiliumbwa na Mungu, lakini Shetani anakigeuza na kumwonyesha Mungu akisema, “Angalia utajiri na utukufu wa falme hizi zote. Hivi vyote nitakupa, ukianguka chini na kuniabudu.” Je, si hili ni mabadiliko ya jukumu? Si Shetani hana haya? Mungu aliumba kila kitu, lakini, je, ilikuwa ni kwa ajili ya kufurahia Kwake? Mungu alimpa mwanadamu kila kitu, lakini Shetani alitaka kunyakua vyote na baadaye akasema, “Niabudu! Niabudu na nitakupa Wewe haya yote.” Huu ni uso usiopendeza wa Shetani; hana haya kabisa! Shetani hata hajui maana ya neno “haya,” na huu ni mfano mwingine tu wa uovu wake. Hata hajui haya ni nini. Shetani anajua vyema kwamba Mungu aliumba kila kitu na kwamba Anavisimamia na Anavitawala. Kila kitu ni cha Mungu, si cha mwanadamu, sembuse Shetani, lakini Shetani ibilisi bila haya alisema kwamba angempa Mungu kila kitu. Si tena Shetani anafanya kitu cha ujinga na kisicho na aibu? Mungu anamchukia Shetani hata zaidi sasa, sivyo? Lakini licha ya kile Shetani alijaribu kufanya, Bwana Yesu alikiamini? Bwana Yesu alisema nini? (“Muabudu Bwana Mungu wako na umtumikie Yeye pekee.”) Je, kirai hiki kina maana ya utendaji? (Ndiyo.) Maana gani ya utendaji? Tunaona uovu na kutokuwa na aibu kwa Shetani katika matamshi yake. Kwa hivyo iwapo mwanadamu angemwabudu Shetani, hitimisho lingekuwa nini? Angepokea utajiri na utukufu wa falme zote? (La.) Angepokea nini? Je, wanadamu wangekuwa wasio na haya na wa kuchekwa kama tu Shetani? (Ndiyo.) Watakuwa hawana tofauti kabisa na Shetani. Kwa hivyo, Bwana Yesu alisema maneno haya ambayo ni muhimu kwa kila mwanadamu: “Muabudu Bwana Mungu wako, na ni Yeye peke Yake ndiye utakayemtumikia,” hii ina maana kwamba isipokuwa Bwana, isipokuwa Mungu Mwenyewe, ukimhudumia mwingine, ukimwabudu Shetani ibilisi, basi utagaagaa katika uchafu sawa na Shetani. Kisha utashiriki kutokuwa na haya na uovu wa Shetani, na kama tu Shetani ungemjaribu Mungu na kumshambulia Mungu. Na basi mwisho wako ungekuwa upi? Ungechukiwa na Mungu, kuangushwa na Mungu na kuangamizwa na Mungu. Baada ya Shetani kumjaribu Bwana Mungu mara kadhaa bila mafanikio, alijaribu tena? Shetani hakujaribu tena na kisha akaondoka. Hii inathibitisha nini? Inathibitisha kwamba asili ovu ya Shetani, kuonea kijicho kwake, na ujinga na upuuzi wake vyote havistahili kutajwa mbele ya Mungu. Bwana Yesu alimshinda Shetani kwa sentensi tatu tu, na baadaye akatoroka na mkia wake katikati ya miguu yake, akiaibika sana asiweze kuonyesha uso wake tena, na hakumjaribu Bwana Yesu tena. Kwa sababu Bwana Yesu alikuwa amelishinda jaribio hili la Shetani, Angeweza kuendelea kwa urahisi kazi ambayo Alipaswa kufanya na kuanza kazi zilizokuwa mbele Yake. Je, yote aliyoyasema Bwana Yesu na kufanya katika hali hii yanabeba maana fulani ya vitendo kwa kila mtu yakitumika sasa? (Ndiyo.) Ni aina gani ya utendaji? Je, kumshinda Shetani ni kitu rahisi kufanya? Je, ni lazima watu wawe na uelewa wazi wa asili ovu ya Shetani? Je, ni lazima watu wawe na uelewa sahihi wa vishawishi vya Shetani? (Ndiyo.) Unapopitia vishawishi vya Shetani katika maisha yako, na iwapo unaweza kuona hadi kwa asili ovu ya Shetani, utaweza kumshinda? Iwapo unajua kuhusu ujinga na upuuzi wa Shetani, bado unaweza kusimama kando ya Shetani na kumshambulia Mungu? Ikiwa unaelewa jinsi kuwa na kijicho na kutokuwa na aibu kwa Shetani vinafichuliwa kupitia kwako—iwapo unatambua wazi na kujua mambo haya—bado ungemshambulia na kumjaribu Mungu kwa njia hii? (La, hatungeweza.) Utafanya nini? (Tutaasi dhidi ya Shetani na kumwacha.) Hili ni jambo rahisi kufanya? Hili si rahisi, kufanya hivi, watu wanalazimika kuomba mara nyingi, ni lazima wajiweke mbele ya Mungu na wajichunguze. Na lazima waache kufundisha nidhamu kwa Mungu na hukumu Yake na kuadibu Kwake viwajie. Ni kwa njia hii tu ndiyo watu wataweza kujinasua polepole kutoka kwa udanganyifu na udhibiti wa Shetani.
Tunaweza kuweka pamoja mambo yanayojumuisha kiini cha Shetani kutoka kwa mambo haya ambayo amesema. Kwanza, kiini cha Shetani kwa ujumla kinaweza kusemwa kuwa ni kiovu, ambacho ni kinyume na utakatifu wa Mungu. Kwa nini Nasema kiini cha Shetani ni kiovu? Mtu anapaswa kuangalia matokeo ya kile Shetani anafanyia watu ili kuona haya. Shetani anampotosha na kumdhibiti mwanadamu, na mwanadamu anatenda chini ya tabia potovu ya Shetani, na anaishi katika dunia ya watu waliopotoshwa na Shetani. Binadamu wanamilikiwa na kusimilishwa na Shetani bila kujua; mwanadamu hivyo ana tabia potovu ya Shetani, ambayo ni asili ya Shetani. Kutoka kwa yote Shetani amesema na kufanya, umeona kiburi chake? Umeona udanganyifu na ubaya wake? Kiburi cha Shetani kimsingi kinaonekana vipi? Je, Shetani daima anataka kuchukua nafasi ya Mungu? Shetani daima anataka kuharibu kazi ya Mungu na nafasi ya Mungu na kujichukulia kuwa yake ili watu wamuunge mkono na kumwabudu Shetani; hii ni asili ya kiburi ya Shetani. Wakati Shetani anawapotosha watu, je, anawaambia moja kwa moja kile wanachopaswa kufanya? Wakati Shetani anamjaribu Mungu, je, anajitokeza na kusema, “Nakujaribu, nitakushambulia”? Hakika hafanyi hivyo. Ni mbinu gani hivyo Shetani anatumia? Anashawishi, anajaribu, anashambulia, na anaweka mitego yake, na hata kwa kutaja maandiko, Shetani anazungumza na kutenda kwa njia mbalimbali ili kutimiza dhamira na nia zake mbaya. Baada ya Shetani kufanya hivi, ni nini kinachoweza kuonekana kutoka kile kilichojitokeza kwa mwanadamu? Je, si watu wana kiburi? Mwanadamu ameteseka kutoka kwa upotovu wa Shetani kwa maelfu ya miaka na hivyo mwanadamu amekuwa mwenye kiburi, mdanganyifu, mwenye kijicho, na asiyefikiri. Haya mambo yote yameletwa kutokana na asili ya Shetani. Kwa sababu asili ya Shetani ni ovu, amempa mwanadamu asili hii ovu na kumletea mwanadamu tabia hii potovu. Kwa hivyo, mwanadamu anaishi chini ya tabia potovu ya kishetani na, kama Shetani, mwanadamu anaenda kinyume na Mungu, anamshambulia Mungu, na kumjaribu Yeye hadi kwa kiwango ambacho mwanadamu hamwabudu Mungu na hamheshimu katika moyo wake.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 147)
Jinsi Ambavyo Shetani Hutumia Maarifa Kumpotosha Mwanadamu
Je, si kila mtu angechukulia maarifa kuwa kitu chema? Ama kwa kiwango cha chini kabisa, watu wanafikiri kwamba kidokezo cha neno “maarifa” ni chema badala ya hasi. Kwa hivyo mbona tunataja hapa kwamba Shetani anatumia maarifa kumpotosha mwanadamu? Je, nadharia ya mageuko ni kipengele cha maarifa? Je, sheria za kisayansi za Newton ni sehemu ya maarifa? Je, nguvu ya mvutano wa dunia ni sehemu ya maarifa, sivyo? (Ndiyo.) Hivyo mbona maarifa yametajwa miongoni mwa maudhui anayoyatumia Shetani kumpotosha mwanadamu? Maoni yenu hapa ni yapi? Je, maarifa yana hata chembe cha ukweli ndani yake? (La.) Kwa hivyo ni nini kiini cha maarifa? Je, maarifa ambayo mwanadamu anajifunza yanategemea msingi upi? Je, yanategemea nadharia ya mageuko? Je, maarifa ambayo mwanadamu ameyapata kupitia uchunguzi na majumuisho yana msingi wa kumkana Mungu? Je, kuna sehemu yoyote ya maarifa haya ambayo yana uhusiano na Mungu? Je, yanahusiana na kumwabudu Mungu? Yanahusiana na ukweli? (La.) Hivyo Shetani anatumiaje maarifa kumpotosha mwanadamu? Nimetoka tu kusema kwamba hakuna sehemu yoyote ya maarifa haya inayohusiana na kumwabudu Mungu ama na ukweli. Watu wengine wanayafikiria hivi: “Yanaweza kutokuwa na chochote kuhusiana na ukweli, lakini hayawapotoshi watu.” Mnafikiri nini kuhusu haya? Je, ulifundishwa na maarifa kwamba furaha ya watu ilitegemea kile walichokitengeneza kwa mikono yao wenyewe? Je, maarifa yaliwahi kukufunza kwamba hatima ya mwanadamu ilikuwa mikononi mwake? (Ndiyo.) Haya ni mazungumzo ya aina gani? (Ni mazungumzo ya kishetani.) Bila shaka! Ni mazungumzo ya kishetani! Maarifa ni mada tata sana kuijadili. Unaweza kuiweka kwa urahisi kwamba eneo la maarifa ni maarifa tu. Hili ni eneo la maarifa linalofunzwa kwa msingi wa kutomwabudu Mungu na kutokuwa na uelewa kwamba Mungu aliumba mambo yote. Watu wanaposoma aina hii ya maarifa, hawaoni Mungu anatawala mambo yote, hawaoni Mungu anaongoza ama anasimamia mambo yote. Badala yake, wanayofanya tu ni kutafiti na kuchunguza, bila kikomo kwa sehemu hiyo ya maarifa, na kutafuta majibu kwa msingi wa maarifa. Hata hivyo, iwapo watu hawamwamini Mungu na badala yake wanatafiti tu, kamwe hawatapata majibu ya kweli, siyo? Maarifa yanakupa tu riziki, yanakupa tu kazi, yanakupa tu mapato ili usiwe na njaa, lakini kamwe hayawezi kukufanya umwabudu Mungu, na hayatakuweka mbali na maovu. Kadiri watu wanavyosoma maarifa, ndivyo watakavyotamani zaidi kuasi dhidi ya Mungu, kumchunguza Mungu zaidi, kumjaribu Mungu, na kwenda kinyume na Mungu. Hivyo sasa, tunaona yapi ambayo maarifa yanawafunza watu? Yote ni falsafa ya Shetani. Je, falsafa na kanuni za kuishi zinazosambazwa na shetani miongoni mwa wanadamu wapotovu zina uhusiano wowote na ukweli? Hazina uhusiano wowote na ukweli na, kwa kweli, ni kinyume cha ukweli. Watu mara nyingi husema, “Maisha ni mwendo” na “Mwanadamu ni chuma, mchele ni chuma, mwanadamu huhisi anataabika kwa njaa asipokula mlo”; misemo hii ni nini? Ni uwongo, na kuisikia kunasababisha hisia ya kuchukiza. Pengine kila mtu anajua kuhusu jinsi Shetani hutumia maarifa kumpotosha mwanadamu. Kwa yanayoitwa maarifa ya mwanadamu, Shetani amejaza kidogo falsafa yake ya kuishi na kufikiria kwake. Na wakati Shetani anafanya haya, Shetani anamruhusu mwanadamu kutumia kufikiria kwake, filosofia, na mtazamo wake ili mwanadamu aweze kukana uwepo wa Mungu, kukana utawala wa Mungu juu ya mambo yote na utawala juu ya hatima ya mwanadamu. Kwa hivyo, masomo ya mwanadamu yanapoendelea, na anapata maarifa zaidi, anahisi uwepo wa Mungu kuwa usio yakini, na anaweza hata kuhisi kwamba Mungu hayupo. Kwa sababu Shetani ameingiza mawazo, mitazamo na dhana fulani ndani ya mwanadamu, mara tu Shetani anapoingiza sumu hii ndani ya mwanadamu, je, si mwanadamu amehadaiwa na kupotoshwa na Shetani? Kwa hivyo mnaweza kusema watu wa siku hizi wanaishi kwa kufuata nini? Je, hawaishi kwa kufuata maarifa na mawazo yaliyoingizwa na Shetani? Na mambo yaliyofichwa ndani ya maarifa na mawazo haya—je, si hayo falsafa na sumu ya Shetani? Mwanadamu huishi kwa kufuata falsafa na sumu ya Shetani. Na ni nini kilicho katika msingi wa wanadamu kupotoshwa na Shetani? Shetani anataka kumfanya mwanadamu amkane, kumpinga, na kwenda dhidi ya Mungu jinsi anavyofanya yeye; hili ndilo lengo la Shetani kumpotosha mwanadamu, na pia ndiyo njia ambayo kwayo Shetani humpotosha mwanadamu.
Kwanza tutazungumzia kipengele cha juujuu zaidi cha mada hii. Je, sarufi na maneno katika masomo ya lugha yaliweza kuwapotosha watu? Je, maneno yanaweza kuwapotosha watu? Maneno hayawapotoshi watu; na ni chombo kinachowaruhusu watu kuongea na chombo ambacho watu wanatumia kuwasiliana na Mungu. Zaidi ya hayo, lugha na maneno ni jinsi ambavyo Mungu anawasiliana na watu sasa, ni vyombo, ni vya umuhimu. Moja ongeza moja ni mbili, na mbili zidisha kwa mbili ni nne; haya ni maarifa, siyo? Lakini yanaweza kukupotosha? Hii ni akili ya kawaida na kanuni kwa hivyo haiwezi kupotosha watu. Kwa hivyo ni maarifa gani yanayopotosha watu? Ni maarifa ambayo yamechanganywa mitazamo na fikira za Shetani, Shetani anataka kujaza mitazamo na fikira hizi ndani ya binadamu kupitia maarifa. Kwa mfano, katika insha, hakuna chochote kibaya na maneno yaliyoandikwa, lakini shida inaweza kuwa mitazamo na nia ya mwandishi alipoandika insha hiyo na pia maudhui ya fikira zake. Haya ni mambo ya kiroho—na yanaweza kuwapotosha watu. Kwa mfano, iwapo ungekuwa ukitazama kipindi kwenye runinga, ni mambo yapi ndani yake yangeweza kubadili mtazamo wako? Je, yale yaliyosemwa na wasanii, maneno yenyewe, yangeweza kuwapotosha watu? (La.) Ni mambo yapi ambayo yangeweza kuwapotosha watu? Yangekuwa mawazo ya msingi na yaliyomo katika onyesho, ambayo yangewakilisha maoni ya mwendeshaji, na habari iliyobebwa katika maoni haya inaweza kushawishi mioyo na akili za watu. Siyo? Sasa mnajua Narejelea nini katika mjadala Wangu wa Shetani kutumia maarifa kuwapotosha watu. Hutaelewa visivyo, siyo? Hivyo unaposoma riwaya ama insha tena, unaweza kutathmini iwapo fikira zilizoelezwa katika insha hiyo zinampotosha ama hazimpotoshi mwanadamu ama kuchangia kwa binadamu? (Tunaweza kufanya hivyo kidogo.) Hiki ni kitu ambacho lazima kisomwe na kupitiwa polepole, si kitu kinachoeleweka kwa urahisi mara moja. Kwa mfano, unapotafiti ama kusoma sehemu ya maarifa, baadhi ya vipengele vyema vya maarifa hayo vinaweza kukusaidia kuelewa mambo fulani ya kawaida kuhusu eneo hilo, na kile ambacho watu wanapaswa kuepukana nacho. Chukua mfano wa “umeme,”—huu ni uwanja wa maarifa, siyo? Je, hutakuwa mjinga iwapo hujui kwamba kwamba umeme unaweza kuwatetemesha na kuwaumiza watu? Lakini utakapoelewa sehemu hii ya maarifa, hutakuwa na uzembe kuhusu kugusa kitu cha umeme na utajua jinsi ya kutumia umeme. Haya yote ni mambo mema. Je, sasa unaelewa kile ambacho tumekuwa tukijadili kuhusiana na jinsi maarifa yanavyowapotosha watu? Kuna aina nyingi za maarifa ambazo zinasomwa duniani na lazima mchukue wakati wenu kuzitofautisha wenyewe.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 148)
Jinsi ambavyo Shetani Hutumia Sayansi Kumpotosha Mwanadamu
Sayansi ni nini? Si sayansi imewekwa kwa hadhi ya juu na kuchukuliwa kuwa muhimu katika akili za karibu kila mtu? Sayansi inapotajwa, si watu wanahisi, “Hiki ni kitu ambacho watu wa kawaida hawawezi kuelewa, hii ni mada ambayo tu watafiti wa kisayansi ama wataalam wanaweza kugusia. Haina uhusiano wowote na sisi watu wa kawaida”? Je, ina uhusiano lakini? (Ndiyo.) Shetani anatumiaje sayansi kuwapotosha watu? Hatutazungumza kuhusu mambo mengine isipokuwa mambo ambayo watu mara nyingi wanapatana nayo katika maisha yao binafsi. Je, umesikia kuhusu vinasaba? Nyote mnalijua neno hili, sivyo? Je, vinasaba viligunduliwa kupitia sayansi? Vinasaba vinamaanisha nini hasa kwa watu? Je, havifanyi watu kuhisi kwamba mwili ni kitu cha ajabu? Wakati watu wanajulishwa kwa mada hii, si kutakuwa na watu—hasa wenye kutaka kujua—ambao watataka kujua zaidi ama kutaka maelezo zaidi? Hawa watu wanaotaka kujua wataweka nguvu zao zote kwenye mada hii na wakati hawana shughuli watatafuta maelezo kwenye vitabu na Intaneti kujifunza maelezo zaidi kuihusu. Sayansi ni nini? Kuongea waziwazi, sayansi ni fikira na nadharia ya vitu ambavyo mwanadamu anataka kujua, vitu visivyojulikana, na ambavyo hawajaambiwa na Mungu; sayansi ni fikira na nadharia za siri ambazo mwanadamu anataka kuchunguza. Wigo wa sayansi ni upi? Unaweza kusema kwamba ni mpana sana; mwanadamu hutafiti na kujifunza kila kitu ambacho anavutiwa nacho. Sayansi inahusiana na kutafiti maelezo na sheria za vitu hivi na kuweka mbele nadharia zenye kukubalika ambazo zinawafanya watu wafikirie: “Wanasayansi hawa ni wakubwa mno! Wanajua mengi na wana maarifa mengi kuelewa mambo haya!” Wanavutiwa sana na watu hao, sivyo? Watu wanaotafiti sayansi, wana mitazamo ya aina gani? Je, hawataki kutafiti ulimwengu, kutafiti mambo ya ajabu katika eneo lao linalowavutia? Je, matokeo ya mwisho wa haya ni nini? Katika baadhi ya sayansi, watu wanafikia mahitimisho yao kwa kubahatisha, na katika nyingine watu wanategemea uzoefu wa kibinadamu kufikia mahitimisho yao. Bado katika nyanja zingine ya sayansi, watu hufikia mahitimisho yao kutokana na uchunguzi wa kihistoria na usuli. Sivyo? Hivyo, sayansi inawafanyia nini watu? Kile sayansi inafanya ni kwamba inawaruhusu tu watu kuona vyombo katika ulimwengu wa maumbile na tu kuridhisha kutaka kujua kwa mwanadamu; haimruhusu mwanadamu kuona sheria ambazo Mungu anatumia kutawala mambo yote. Mwanadamu anaonekana kupata majibu kutoka kwa sayansi, lakini majibu hayo yanachanganya na yanaleta tu ridhaa ya muda mfupi, ridhaa ambayo inawekea moyo wa mwanadamu mipaka kwa ulimwengu yakinifu. Mwanadamu anahisi kwamba amepata majibu kutoka kwenye sayansi, kwa hivyo licha ya suala litakaloibuka, yeye anatumia mitazamo yake ya kisayansi kama msingi wa kuthibitisha na kukubali suala hilo. Moyo wa mwanadamu unashawishiwa na sayansi na unamilikiwa nayo kiasi kwamba mwanadamu hana tena hamu ya kumjua Mungu, kumwabudu Mungu, na kuamini kwamba mambo yote yanatoka kwa Mungu na mwanadamu anapaswa kumwangalia kupata majibu. Hii si ukweli? Kadiri ambavyo mtu anaamini sayansi, anakuwa mjinga zaidi, akiamini kwamba kila kitu kina suluhisho la kisayansi, kwamba utafiti unaweza kutatua chochote. Hamtafuti Mungu na haamini kwamba Yupo. Kuna hata baadhi ya waumini wa muda mrefu wa Mungu ambao punde wanapopatwa na tatizo lolote, watatumia kompyuta kuangalia mambo na kutafuta majibu; wanapekua kila aina ya nyenzo, kwa kutumia mitazamo ya kisayansi kujaribu kutatua tatizo. Hawaamini kwamba maneno ya Mungu ni ukweli, hawaamini kwamba maneno ya Mungu yanaweza kutatua matatizo yote ya binadamu, hawaoni matatizo ya binadamu yaliyo mengi kutoka katika mtazamo wa ukweli. Haijalishi ni shida gani wanayokumbana nayo, hawamwombi Mungu kamwe au kutafuta suluhu kwa kutafuta ukweli katika maneno ya Mungu. Katika mambo mengi, wanapendelea kuamini kwamba maarifa yanaweza kutatua tatizo; kwao, sayansi ndiyo jibu kamili. Mungu hayupo kabisa katika mioyo ya watu kama hao. Wao ni wasioamini, na maoni yao kuhusu imani katika Mungu si tofauti na yale ya wasomi na wanasayansi wengi mashuhuri, ambao sikuzote hujaribu kumchunguza Mungu kwa kutumia mbinu za kisayansi. Kwa mfano, kuna wataalam wengi wa kidini walioenda kwenye mlima ambako safina ilisimama, na hivyo walithibitisha kuwepo kwa safina. Lakini katika kuonekana kwa safina hawaoni uwepo wa Mungu. Wanaamini hadithi na historia tu; haya ni matokeo ya utafiti wao wa kisayansi na utafiti wa dunia yakinifu. Ukitafiti vitu yakinifu, viwe maikrobaiolojia, falaki, ama jiografia, hutawahi kupata matokeo yanayoamua kwamba Mungu yupo ama kwamba Ana mamlaka juu ya vitu vyote, Kwa hivyo sayansi humfanyia nini mwanadamu? Si inamweka mbali na Mungu? Si hii inawaruhusu watu kumtafiti Mungu? Je, haimweki mwanadamu mbali na Mungu? Je, haiwasababishi watu wamsome Mungu? Je, haiwafanyi watu kuwa na shaka zaidi kuhusu uwepo wa Mungu na ukuu wake, na hivyo kumkana na kumsaliti Mungu? Haya ndiyo matokeo. Kwa hiyo Shetani anapotumia sayansi kumpotosha mwanadamu, Shetani anajaribu kufikia lengo gani? Anataka kutumia mahitimisho ya kisayansi kuwahadaa watu na kuwafanya wakose hisia, na kutumia majibu yenye utata kushikilia mioyo ya watu ili wasimtafute au kuuamini uwepo wa Mungu. Kwa hivyo hii ndiyo maana Ninasema kwamba sayansi ni mojawapo ya njia ambazo kwazo Shetani hupotosha watu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 149)
Jinsi Ambavyo Shetani Hutumia Desturi ya Kitamaduni Kumpotosha Mwanadamu
Je, kuna mambo mengi yanayochukuliwa kuwa sehemu ya desturi ya kitamaduni? (Ndiyo.) Hii desturi ya kitamaduni inamaanisha nini? Wengine wanasema inapitishwa kutoka kwa mababu, hiki ni kipengele kimoja. Kutoka mwanzo, familia, vikundi vya makabila, na hata jamii ya binadamu imepitisha njia yao ya maisha, ama mila, misemo, na kanuni, ambazo zimeingizwa kwenye fikira za watu. Watu wanayachukulia kuwa yasiyoweza kutengwa na maisha yao. Wanayachukua mambo haya na kuyachukulia kuwa kanuni na maisha ya kuzingatiwa, na hata kamwe hawataki kuyabadilisha ama kuyaacha mambo haya kwa sababu yalipitishwa kutoka kwa mababu. Kuna vipengele vingine vya desturi ya kitamaduni, kama kile kilichopitishwa na Confucius ama Mencius, na mambo waliyofunzwa watu na Utao ama Uconfucius. Je, hili si kweli? Ni vitu gani vinavyojumuishwa katika desturi ya kitamaduni? Je, inajumuisha sikukuu ambazo watu wanasherehekea? Kwa mfano: Tamasha la Majira ya machipuko, Tamasha la Taa, Siku ya Kufagia Kaburi, Tamasha la Mashua ya Joka, pamoja na Tamasha ya Zimwi na Tamasha ya Katikati ya Majira ya Kupukutika kwa Majani. Baadhi za familia hata husherehekea siku ambazo wazee wanahitimu umri fulani, ama wakati watoto wanahitimu umri wa mwezi mmoja au siku mia moja. Na kadhalika. Hizi zote ni sikukuu za kitamaduni. Je, hakuna desturi ya kitamaduni katika sikukuu hizi? Ni nini kiini cha desturi ya kitamaduni? Je, ina uhusiano wowote na kumwabudu Mungu? Je, ina uhusiano wowote na kuwaambia watu kuweka ukweli katika vitendo? Je, kuna sikukuu zozote za watu kumtolea Mungu dhabihu, kwenda kwenye madhabahu ya Mungu na kupokea mafundisho Yake? Kuna sikukuu kama hizi? (La.) Watu hufanya nini katika sikukuu hizi zote? Katika nyakati za sasa zinaonekana kuwa hafla za kula, kunywa, na kujiburudisha. Ni nini chanzo cha desturi ya kitamaduni? Desturi ya kitamaduni imetoka kwa nani? Imetoka kwa Shetani. Katika usuli wa hizi sikukuu za kitamaduni, Shetani anaingiza mambo ndani ya mwanadamu, haya ni mambo gani? Kuhakikisha kwamba watu wanakumbuka mababu zao, je, hili ni mojawapo ya mambo haya? Kwa mfano, wakati wa Tamasha la Kufagia Kaburi watu husafisha makaburi na kutoa sadaka kwa mababu zao, hivyo watu hawatasahau mababu zao. Pia, Shetani anahakikisha kwamba watu wanakumbuka kuwa wazalendo, kama katika Tamasha la Mashua ya Joka. Je, Tamasha la Katikati ya Majira ya Kupukutika kwa Majani? (Kupatana kwa familia.) Ni nini usuli wa kupatana kwa familia? Sababu zake ni nini? Ni kuwasiliana na kuunganika kihisia. Bila shaka, iwapo ni kusherehekea Mkesha wa Mwaka Mpya wa Mwezi ama Tamasha la Taa, kuna njia nyingi za kuelezea sababu za usuli. Haijalishi jinsi mtu anaelezea sababu iliyo nyuma yazo, kila moja ni njia ya Shetani ya kuingiza filosofia yake na kufikiria kwake kwa watu, ili waweze kupotea kutoka kwa Mungu na wasijue kwamba kuna Mungu, na kwamba watoe sadaka ama kwa mababu zao au Shetani, ama kwamba ni udhuru wa kula, kunywa na kujifurahisha kwa ajili ya matamanio ya mwili. Kila moja ya sikukuu hizi inapoadhimishwa, fikira na mitazamo ya Shetani yanapandwa kwa kina ndani ya akili za watu na hata hawajui. Wakati watu wanafikia umri wa kati ama zaidi, fikira na mitazamo hii ya Shetani tayari yamekita mizizi ndani sana ya mioyo yao. Zaidi ya hayo, watu wanafanya juhudi zao kabisa kueneza fikira hizi, ziwe sahihi ama si sahihi, kwa kizazi kifuatacho bila wasiwasi pasipo kuchagua. Sivyo? (Ndiyo.) Ni jinsi gani desturi hii ya kitamaduni na sikukuu hizi zinawapotosha watu? Je, unajua? (Watu wanawekewa mipaka na kufungwa na kanuni za hizi desturi kana kwamba hawana muda ama nguvu kumtafuta Mungu.) Hiki ni kipengele kimoja. Kwa mfano, kila mtu anasherehekea wakati wa Mwaka Mpya wa Mwezi, usingesherehekea, hungehisi huzuni? Je, kuna miiko yoyote ambayo unapaswa kushikilia? Hungehisi, “Sikusherehekea Mwaka Mpya. Siku hii ya Mwaka Mpya wa Mwezi ilikuwa mbaya sana; mwaka huu wote utakuwa mbaya”? Si ungehisi kutokuwa na utulivu na kuogopa kiasi? Kuna hata watu wengine ambao hawajatoa sadaka kwa mababu zao kwa miaka mingi na ghafla wamekuwa na ndoto ambapo mtu aliyekufa anawaomba pesa, watahisi nini ndani yao? “Inahuzunisha kwamba huyu mtu aliyekufa anahitaji pesa ya kutumia! Nitawachomea baadhi ya pesa za makaratasi, na kama sitafanya hivyo hakika haitakuwa sawa. Sisi tunaoishi huenda tukaingia kwenye matatizo ikiwa sitachoma pesa za karatasi, ni nani anayeweza kusema ni lini janga litatokea?” Daima watakuwa na wingu hili dogo la hofu na wasiwasi katika mioyo yao. Ni nani anayewapa wasiwasi? Shetani huleta wasiwasi. Si hii ndiyo njia moja ambayo Shetani anampotosha mwanadamu? Anatumia mbinu na udhuru mbalimbali ili kukudhibiti, kukutishia, kukufunga, hadi kiasi kwamba unachanganyikiwa na kumkubali na kumnyenyekea; hivi ndivyo Shetani anampotosha mwanadamu. Nyakati nyingi ambapo watu ni wanyonge ama hawaelewi vyema hali ilivyo, wanaweza bila kutaka, kufanya kitu kwa njia iliyochanganyikiwa, yaani, wanaanguka chini ya mshiko wa Shetani bila kujua na wanaweza kufanya kitu bila kujua na wasijue wanafanya nini. Hii ni njia ambayo Shetani anampotosha mwanadamu. Hata kuna watu wachache sasa ambao wanasita kuachana na desturi za kitamaduni ambazo zimekita mizizi, ambao hawawezi kuziacha kabisa. Ni hasa wakati ni wanyonge na wasioweza kujizuia ndipo wanataka kusherehekea sikukuu za aina hizi na wanataka kukutana na Shetani na kumridhisha Shetani tena, ili kuifariji mioyo yao. Ni nini usuli wa desturi hizi za kitamaduni? Je, mkono mweusi wa Shetani unavuta nyuzi nyuma ya pazia? Je, asili ovu ya Shetani inatawala na kudhibiti vitu? Je, Shetani anadhibiti hivi vitu vyote? (Ndiyo.) Wakati watu wanaishi katika desturi ya kitamaduni na kusherehekea sikukuu za kitamaduni za aina hizi, tunaweza kusema kwamba haya ni mazingira ambapo wanadanganywa na kupotoshwa na Shetani, na zaidi ya hayo kwamba wana furaha kupumbazwa na kupotoshwa na Shetani? (Ndiyo.) Hiki ni kitu ambacho nyinyi nyote mnakiri, ambacho nyote mnakijua.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 150)
Jinsi Ambavyo Shetani Hutumia Ushirikina Kumpotosha Mwanadamu
Shetani anatumiaje ushirikina kumpotosha mwanadamu? Watu wote wanataka kujua majaliwa yao, hivyo Shetani anatumia udadisi wao kuwashawishi. Watu wanashiriki katika ubashiri, upigaji ramli na kusoma uso ili kujua kile kitakachowafanyikia katika siku zijazo na ni njia ya aina gani iliyoko mbele yao. Hata hivyo, mwishowe, ni mikononi mwa nani kuna hatima na matarajio ambayo watu wana wasiwasi navyo sana? (Vipo mikononi mwa Mungu.) Vitu hivi vyote vimo katika mikono ya Mungu. Kwa kutumia mbinu hizi, Shetani anataka watu wajue nini? Shetani anataka kutumia kusoma uso na uaguzi ili kuwaambia watu kwamba anajua bahati zao zilizo mbeleni, na Shetani anataka kuwaambia watu kwamba anajua vitu hivi na anavidhibiti. Shetani anataka kutumia fursa hii na kutumia mbinu hizi kudhibiti watu, ili kwamba watu waweke imani yenye upofu ndani yake na kutii kila neno lake. Kwa mfano, ukisomwa uso, mwaguzi akifunga macho yake na kukwambia kila kitu ambacho kimekufanyikia katika miongo michache iliyopita kwa uwazi kamili, ungehisi vipi ndani yako? Ghafla ungehisi, “Yuko sahihi sana! Sijawahi kumwambia yeyote maisha yangu ya nyuma, alijuaje kuyahusu? Nimependezwa sana na huyu mwaguzi!” Haitakuwa vigumu sana kwa Shetani kujua maisha yako ya nyuma, siyo? Mungu amekuongoza hadi leo, na Shetani pia amewapotosha watu wakati huo wote na amekufuata. Kupita kwa miongo kwako si chochote kwa Shetani na si vigumu kwake kujua vitu hivi. Wakati unajua kwamba alichosema Shetani ni sahihi, si unampa moyo wako? Siku zako za baadaye na bahati yako, si unategemea udhibiti wake? Papo hapo, moyo wako utahisi heshima ama ustahi kwake, na kwa watu wengine, nafsi zao pengine tayari zimenyakuliwa naye. Na utamwuliza mwaguzi mara moja: “Napaswa kufanya nini baada ya hapa? Napaswa kuepukana na nini mwaka ujao? Ni vitu gani ambavyo sipaswi kufanya?” Na kisha atasema hupaswi kwenda pale, hupaswi kufanya hili, usivae nguo za rangi fulani, hupaswi kwenda pahali kama hapo na hapo unapaswa kufanya mambo fulani zaidi…. Si utatia vyote anavyosema moyoni mara moja? Ungevikariri haraka kuliko neno la Mungu. Mbona ungevikariri haraka hivyo? Kwa sababu ungetaka kumtegemea Shetani kwa sababu ya bahati njema. Si hapa ndipo anaunyakua moyo wako? Wakati maneno yake yanakuwa ukweli kama alivyotabiri, si ungependa kurejea kwake na kujua ni bahati gani mwaka unaokuja utaleta? (Ndiyo.) Utafanya chochote Shetani anakwambia ufanye na utaepukana na vitu anakwambia uepukane navyo, si unatii vyote anavyosema? Utajipata katika kumbatio lake haraka sana, upotoshwe, na kudhibitiwa naye. Hii inafanyika kwa sababu unaamini anachosema ni ukweli na kwa sababu unaamini kwamba anajua kuhusu maisha yako ya nyuma, maisha yako ya sasa, na vitu ambavyo siku za badaye zitaleta. Hii ni mbinu Shetani anatumia kudhibiti watu. Lakini kwa kweli, ni nani aliye katika udhibiti? Ni Mungu Mwenyewe, si Shetani. Shetani anatumia tu hila zake hapa kudanganya watu wajinga, kuwadanganya watu wanaoona tu ulimwengu yakinifu ili waumini na kumtegemea. Kisha, wataanguka katika mshiko wa Shetani na kutii kila neno lake. Lakini, je, Shetani hupunguza jitihada watu wanapotaka kumwamini na kumfuata Mungu? Shetani hapunguzi jitihada. Katika hali hii, je, Shetaniwatu wanaanguka kweli katika mshiko wa Shetani? (Ndiyo.) Je, tunaweza kusema kwamba tabia ya Shetani hapa haina haya hata kidogo? (Ndiyo.) Kwa nini tuseme hivyo? Hizi ni mbinu za ulaghai na zinadanganya. Shetani hana haya na anawadanganya watu kufikiria kwamba anadhibiti kila kitu chao na kuwadanganya watu kufikiria kwamba anadhibiti hatima zao. Hii inawafanya watu wajinga kuja kumtii kabisa na anawadanganya na sentensi moja ama mbili tu na katika kuchanganyikiwa kwao, watu wanasujudu mbele yake. Hivyo, Shetani anatumia mbinu za aina gani, anasema nini kukufanya umwamini? Kwa mfano, pengine hujamwambia Shetani idadi ya watu katika familia yako, lakini anaweza kusema kuna watu wangapi katika familia yako, na umri wa wazazi wako na watoto wako. Iwapo ulikuwa na tuhuma na shaka zako mwanzoni, hutahisi kwamba anaaminika zaidi kidogo baada ya kusikia hayo? Shetani kisha anaweza kusema jinsi kazi imekuwa ngumu kwako hivi karibuni, kwamba wakubwa wako hawakupi utambuzi unaostahili na daima wanafanya kazi dhidi yako na kadhalika. Baada ya kuyasikia hayo, ungefikiri, “Hiyo ni sahihi kabisa! Mambo yamekuwa hayaendi vizuri kazini.” Hivyo ungemwamini Shetani zaidi kidogo. Kisha angesema kitu kingine kukudanganya, kukufanya umwamini hata zaidi. Kidogo kidogo, utajipata huwezi kupinga ama kuwa na tuhuma kwake tena. Shetani anatumia tu hila chache zisizo na maana, hata ndogo zisizojalisha, kukufadhaisha. Unapofadhaishwa, hutaweza kupata njia zako, hutajua kile cha kufanya, na utaanza kufuata kile Shetani anasema. Hii ni mbinu ya “ah nzuri sana” anayotumia Shetani kumpotosha mwanadamu pahali unapoingia katika mtego wake bila kujua na unashawishiwa naye. Shetani anakwambia mambo machache ambayo watu wanafikiria kuwa mambo mazuri, na kisha anakwambia kile cha kufanya na kile cha kuepuka. Hivi ndivyo unavyodanganywa bila kujua. Punde unapoingia mtegoni mwake, mambo yatakwendea mrama; daima utakuwa ukifikiria kile alichosema Shetani na kile alichokwambia ufanye, na bila kujua utamilikiwa naye. Mbona hivi? Ni kwa sababu wanadamu hawana ukweli na hivyo hawawezi kusimama dhidi ya majaribu na ushawishi wa Shetani. Wanapokabiliwa na uovu, udanganyifu, usaliti, na kijicho cha Shetani, wanadamu ni wajinga sana, ni wachanga na wanyonge, siyo? Si hii ni mojawapo ya njia ambayo Shetani anampotosha mwanadamu? (Ndiyo.) Mwanadamu anadanganywa na kulaghaiwa bila kujua, kidogo kidogo, kupitia mbinu mbalimbali za Shetani, kwa sababu hawana uwezo wa kutofautisha kati ya mema na hasi. Hawana kimo hiki, na uwezo wa kumshinda Shetani.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 151)
Jinsi Ambavyo Shetani Hutumia Mienendo ya Kijamii Kumpotosha Mwanadamu
Mienendo ya kijamii ilianza lini? Je, ni kitu kipya? Mtu anaweza kusema kwamba mienendo ya kijamii ilianza wakati Shetani alipoanza kuwapotosha watu. Mienendo ya kijamii inajumuisha nini? (Mtindo wa mavazi na vipodozi.) Hiki ni kitu ambacho watu mara nyingi wanakutana nacho. Mtindo wa mavazi, mtindo wa kisasa na mienendo, hiki ni kipengele kidogo. Kuna kingine zaidi? Je, misemo maarufu ambayo watu wanapenda kusema inahesabika pia? Je, pia mitindo ya maisha ambayo watu wanataka inahesabika? Je, nyota wa muziki, watu mashuhuri, majarida, na riwaya ambazo watu hupenda zinahesabika? (Ndiyo.) Katika akili zenu, ni kipengele kipi cha mienendo hii kinaweza kumpotosha mwanadamu? Ni mienendo ipi inawavutia sana? Watu wengine husema: “Sisi sote tumefikia umri fulani, tuko katika miaka ya, hamsini, sitini, sabini ama themanini ambapo hatuwezi kufaa katika mienendo hii na haituvutii tena.” Je, hii ni sahihi? Wengine husema: “Hatufuati watu mashuhuri, hicho ni kitu ambacho vijana walio katika umri wa ishirini wanafanya; pia hatuvai nguo za mitindo ya kisasa, hicho ni kitu ambacho watu wanaojali sura wanafanya.” Kwa hivyo ni ipi kati ya hii inaweza kuwapotosha? (Misemo maarufu.) Je, hii misemo maarufu inaweza kuwapotosha watu? Huu ni msemo mmoja, na mnaweza kuona iwapo unawapotosha watu au la, “Pesa inaifanya dunia izunguke”; huu ni mtindo? Ikilinganishwa na mitindo ya mavazi na chakula mliyotaja, sihuu ni mbaya zaidi? “Pesa inaifanya dunia izunguke” ni falsafa ya Shetani, na inaenea miongoni mwa wanadamu wote, katika kila jamii ya binadamu. Mnaweza kusema kwamba ni mwenendo kwa sababu umewekwa ndani ya moyo wa kila mtu. Tangu mwanzo kabisa, watu hawakuukubali msemo huu, lakini kisha waliukubali kimyakimyabila kusema walipokutana na maisha halisi, na wakaanza kuhisi kwamba maneno haya kweli yalikuwa ya kweli. Je, huu si mchakato wa Shetani kumpotosha mwanadamu? Pengine watu hawaelewi msemo huu kwa kiwango sawa, lakini kila mtu ana kiwango tofauti cha tafsiri na utambuzi wa msemo huu kutokana na mambo ambayo yamefanyika karibu nao na uzoefu wao binafsi, siyo? Licha ya kiwango cha uzoefu mtu alionao katika msemo huu, ni nini athari mbaya ambayo inaweza kuwa nayo katika moyo wa mtu? Kitu fulani kinafichuliwa kupitia tabia ya binadamu katika dunia hii, ikiwemo kila mmoja wenu. Kitu hiki ni kipi? Ni kuabudu pesa. Je, ni vigumu kuondoa kitu hiki kutoka kwenye moyo wa mtu? Ni vigumu sana! Inaonekana kwamba upotoshaji wa Shetani kwa mwanadamu ni wa kina sana! Shetani hutumia pesa kuwajaribu watu, na kuwapotosha ili waabudu pesa na kuabudu vitu vya kimwili. Na ibada hii ya pesa inadhihirika vipi ndani ya watu? Je, mnahisi kwamba hamwezi kuishi katika dunia hii bila pesa yoyote, kwamba hata siku moja bila pesa haiwezi kuishika kabisa? Hadhi ya watu inatokana na kiasi cha pesa walizo nazo na pia heshima yao. Migongo ya maskini imekunjwa kwa aibu, ilhali matajiri wanafurahia hadhi zao za juu. Wanatenda kwa njia ya kujigamba na wana majivuno, wakiongea kwa sauti kubwa na kuishi kwa kiburi. Msemo na mwenendo huu unaleta nini kwa watu? Si watu wengi wanaona kupata pesa kunastahili gharama yoyote? Si watu wengi hupoteza utu na uadilifu wao wakitafuta pesa zaidi? Si watu wengi hupoteza fursa ya kufanya wajibu wao na kumfuata Mungu kwa sababu ya pesa? Je, kupoteza nafasi ya kupata ukweli na kuokolewa si ndiyo hasara iliyo kubwa zaidi kwa watu? Si Shetani ni mbaya kutumia mbinu hii na msemo huu kumpotosha mwanadamu kwa kiwango kama hicho? Si hii ni hila yenye kijicho? Unaposonga kutoka kuukataa huu msemo maarufu hadi mwishowe kuukubali kama ukweli, moyo wako unaanguka kabisa chini ya mshiko wa Shetani, na hivyo unakuja kuishi naye bila kujua. Msemo huu umekuathiri kwa kiwango kipi? Unaweza kujua njia ya ukweli, na unaweza kuujua ukweli, lakini huna nguvu ya kuufuatilia. Unaweza kujua kwa hakika kwamba maneno ya Mungu ni ukweli, lakini hauko radhi kulipa gharama au kuteseka ili kupata ukweli. Badala yake, kwako, ni afadhali utoe siku zako za baadaye na kudura yako kwenda kinyume na Mungu hadi mwisho kabisa. Licha ya kile Mungu anasema, licha ya kile Mungu anafanya, licha ya kiasi unachogundua kwamba upendo wa Mungu kwako ni wa kina na mkubwa, bado ungeendelea kwa njia hiyo kwa ukaidi na kulipa gharama ya msemo huu. Yaani, msemo huu tayari umeyadanganya na kuyadhibiti mawazo yako, tayari umeitawala tabia yako, na unaona afadhali utawale majaliwa yako kuliko uweke kando ufuatiliaji wako wa mali. Kwamba watu wanaweza kutenda namna hiyo, kwamba wanaweza kudhibitiwa na kuongozwa na maneno ya Shetani—si hili linamaanisha kwamba wamedanganywa na kupotoshwa na Shetani? Je, falsafa na mawazo ya Shetani, na tabia ya Shetani, havijakita mizizi ndani ya moyo wako? Unapofuatilia mali bila kufikiri na kuacha ufuatiliaji wa ukweli, je, Shetani hajafanikiwa katika lengo lake la kukudanganya wewe? Hii ndiyo hali halisi hasa. Kwa hivyo, je, unaweza kuhisi wakati unapodanganywa na kupotoshwa na Shetani? Huwezi. Kama huwezi kumwona Shetani akiwa amesimama mbele yako, au kuhisi kwamba ni Shetani anayetenda kisirisiri, je, utaweza kuuona uovu wa Shetani? Je, utaweza kujua jinsi Shetani huwapotosha binadamu? Shetani humpotosha mwanadamu wakati wote na pahali pote. Shetani anaifanya isiwezekane kwa mwanadamu kujilinda dhidi ya upotovu huu na anamfanya mwanadamu awe mnyonge kwake. Shetani anakufanya ukubali fikira zake, mitazamo yake na mambo maovu yanayotoka kwake katika hali ambazo hujui na huna utambuzi wa kile kinachokufanyikia. Watu wanakubali kikamilifu vitu hivi na hawavibagui. Wanapenda sana vitu hivi na kuvishikilia kama hazina, wanaviacha vitu hivi viwatawale na kuwachezea; hivi ndivyo wanavyoishi watu chini ya mamlaka ya Shetani, na wanamwabudu Shetani bila kujua, na upotoshaji wa Shetani kwa mwanadamu unazidi kuwa wa kina.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 152)
Shetani hutumia mbinu hizi nyingi kumpotosha mwanadamu. Mwanadamu ana maarifa na baadhi ya nadharia za kisayansi, mwanadamu anaishi na ushawishi wa desturi ya kitamaduni, na kila mtu ni mrithi na msambazaji wa desturi ya kitamaduni. Mwanadamu ataendeleza desturi ya kitamaduni aliyopewa kutoka kwa Shetani na pia kutenda pamoja na mienendo ya kijamii ambayo Shetani anawapa wanadamu. Binadamu hawezi kutengana na Shetani, kushiriki na kile ambacho Shetani anafanya wakati wote, kukubali uovu, udanganyifu, kijicho na kiburi chake. Mwanadamu alipomiliki tabia hizi za Shetani, je, amekuwa na furaha ama huzuni kuishi miongoni mwa binadamu hawa wapotovu? (Huzuni.) Mbona unasema hivyo? (Kwa sababu binadamu amefungwa na anadhibitiwa na vitu hivi vipotovu, anaishi dhambini na amegubikwa na mapambano makali.) Watu wengine huvaa miwani, wakionekana kuwa werevu; wanaweza kuzungumza kwa heshima sana, kwa ufasaha na mantiki, na kwa sababu wamepitia vitu vingi sana, wanaweza kuwa wenye uzoefu sana na wastaarabu. Wanaweza kuzungumza kwa undani kuhusu masuala makubwa na madogo; wanaweza pia kutathmini uhalisi na mantiki ya vitu. Wengine wanaweza kuangalia tabia na kuonekana kwa watu hawa, na vile vile tabia, ubinadamu, mwenendo, na kadhalika, na wasione kosa lolote katika haya. Watu kama hao wanaweza hasa kuzoea mitindo ya sasa ya kijamii. Ingawa mtu huyu anaweza kuwa mzee, kamwe hayuko nyuma ya nyakati na kamwe si mzee sana kufunzwa. Kijuujuu, hakuna anayeweza kupata dosari kwake, lakini ndani amepotoshwa na Shetani kabisa na kikamilifu. Kijuujuu hakuna chochote kibaya, yeye ni mpole, ni muungwana, anayo maarifa na maadili fulani; ana uadilifu na vitu anavyojua vinalingana na vile wanavyojua vijana. Hata hivyo, kuhusu asili na kiini chake, mtu huyu ni mfano kamili na unaoishi wa Shetani, ana usawa kabisa na Shetani. Hili ni “tunda” la upotovu wa Shetani kwa mwanadamu. Kile Nilichosema kinaweza kuwaumiza, lakini chote ni ukweli. Maarifa ambayo mwanadamu anasoma, sayansi anayoelewa, na mbinu anazochagua kuingiliana na mienendo ya jamii, bila ubaguzi, ni vyombo vya upotovu wa Shetani. Huu ni ukweli kabisa. Kwa hivyo, mwanadamu anaishi miongoni mwa tabia ambayo imepotoshwa kabisa na Shetani na mwanadamu hana njia ya kujua utakatifu wa Mungu ni nini na kiini cha Mungu ni nini. Hii ni kwa sababu kijuujuu mtu hawezi kupata dosari kwa njia ambazo Shetani anampotosha mwanadamu; hakuna anayeweza kuamua kutoka kwa tabia ya mtu kwamba kuna chochote kibaya. Kila mtu anaendelea na kazi yake kwa kawaida na kuishi maisha ya kawaida; wanasoma vitabu na magazeti kwa kawaida, wanasoma na kuzungumza kwa kawaida. Watu wengine wamejifunza maadili machache na ni wazuri katika kuzungumza, ni wenye kuelewa na ni wazuri, ni wenye kusaidia wengine, na hawajihusishi katika ugomvi wa mambo madogo madogo au kuwadhulumu watu wengine. Hata hivyo, tabia yao iliyopotoka ya kishetani imekita mizizi ndani yao; kiini hiki hakiwezi kubadilishwa kwa kutegemea juhudi za nje. Mwanadamu hana uwezo wa kujua utakatifu wa Mungu kwa sababu ya kiini hiki, na licha ya kiini cha utakatifu wa Mungu kuwekwa wazi kwa mwanadamu, mwanadamu hakichukulii kwa umakini. Hii ni kwa sababu Shetani tayari amemiliki kabisa hisia, fikira, mitazamo, na mawazo ya mwanadamu kupitia njia mbalimbali. Huu umiliki na upotovu si wa muda mfupi ama wa hapa na pale; upo kila mahali na kila wakati. Hivyo, watu wengi mno ambao wamemwamini Mungu kwa miaka mitatu au minne au hata miaka sita na saba, bado wanachukulia mawazo, fikira na falsafa hivi za uovu ambazo Shetani aliweka ndani yao kama vitu vya thamani, na hawawezi kuviachilia. Kwa sababu mwanadamu ameukubali uovu, kiburi, na mambo kutoka kwa asili ya kijicho ya Shetani, bila kuepukika kwa mahusiano ya ana kwa ana ya mwanadamu mara nyingi kuna migogoro, mara nyingi kuna magombano na kutokuwa na uwiano, mambo ambayo yameumbwa kwa sababu ya asili ya kiburi ya Shetani. Iwapo Shetani angempa mwanadamu vitu vyema—kwa mfano, iwapo Uconfucius na Utao wa desturi ya kitamaduni ambayo mwanadamu alikubali ilichukuliwa kuwa vitu vizuri—watu wa aina sawa wanapaswa kuweza kupatana na wengine baada ya kukubali vitu hivyo. Hivyo mbona kuna mgawanyiko mkubwa kati ya watu waliokubali vitu sawa? Mbona hivyo? Ni kwa sababu viti hivi vimetoka kwa Shetani na Shetani husababisha mgawanyiko miongoni mwa watu. Vitu ambavyo Shetani hutoa, bila kujali jinsi vinavyoonekana kuwa vya heshima na vikubwa kwa juujuu, vinamletea mwanadamu na vinaleta katika maisha ya mwanadamu kiburi pekee, na si chochote ila udanganyifu wa asili ovu ya Shetani. Sivyo? Mtu ambaye anaweza kuficha uhalisia wake, ambaye anamiliki maarifa mengi ama aliye na malezi mazuri bado angekuwa na wakati mgumu kuficha tabia yake potovu ya kishetani. Hiyo ni kusema, haijalishi mtu huyu atajificha kwa njia ngapi, kama ulimfikiri kuwa mtakatifu, ama kama ulifikiri ni mkamilifu, ama kama ulifikiri ni malaika, haijalishi ulifikiri ni mtu safi vipi, maisha yake yangekuwaje nyuma ya pazia? Utaona asili ipi katika ufunuo wa tabia yake? Bila shaka ungeona asili ovu ya Shetani. Je, mtu anaweza kusema hivyo? (Ndiyo.) Kwa mfano, tuseme mnamjua mtu wa karibu nanyi ambaye mlifikiria kuwa mtu mzuri, ama ulimfikiria kuwa mtu bora, pengine mtu uliyemwabudu kama Mungu. Kwa kimo chako cha sasa, unawafikiria vipi? Kwanza, unaangalia iwapo mtu wa aina hii anao ama hana ubinadamu, iwapo ni mwaminifu, iwapo ana upendo wa kweli kwa watu, iwapo maneno na vitendo vyao vinafaidi na kusaidia wengine. (La.) Huo unaoitwa wema, upendo na uzuri unaofichuliwa hapa, ni nini kweli? Yote ni uongo, yote ni sura ya kinafiki. Hii sura ya kinafiki ya nyuma ya pazia ina madhumuni maovu ya chinichini: Ni ya kumfanya mtu huyo apendwe na kuabudiwa kama Mungu. Je, mnaona jambo hili kwa dhahiri? (Ndiyo.)
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 153)
Mbinu ambazo Shetani anazitumia ili kuwapotosha watu zinaleta nini kwa wanadamu? Je, kuna chochote kilicho chanya kuzihusu? Kwanza, mwanadamu anaweza kutofautisha kati ya mema na mabaya? Je, unaweza kusema kwamba katika dunia hii, iwe ni mtu mashuhuri au mtu mkubwa, au jarida fulani ama toleo fulani, je, wanatumia viwango sahihi kupima iwapo kitu fulani ni chema ama kiovu, na kizuri ama kibaya? Je, tathmini zao za matukio na watu ni za haki? Kuna ukweli ndani ya tathmini hizi? Je, ulimwengu huu, ubinadamu huu, unatathmini mambo chanya na hasi kulingana na kiwango cha ukweli? (La.) Mbona watu hawana uwezo huo? Watu wamesoma maarifa mengi na wanajua mengi kuhusu sayansi, uwezo wao si mkubwa vya kutosha? Mbona hawawezi kutofautisha kati ya vitu vyema na hasi? Mbona hivi? (Kwa sababu watu hawana ukweli; sayansi na maarifa si ukweli.) Kila kitu ambacho Shetani huletea kwa wanadamu ni uovu na upotovu na hakina ukweli, uhai, na njia. Na uovu na upotovu ambao Shetani anamletea mwanadamu, unaweza kusema kwamba Shetani ana upendo? Unaweza kusema kwamba mwanadamu ana upendo? Watu wengine wanaweza kusema: “Haupo sahihi, kuna watu wengi duniani kote wanaosaidia maskini na watu wasio na makazi. Si hao ni watu wazuri? Pia kuna mashirika ya hisani ambayo hufanya kazi nzuri; je, si kazi yote wanayofanya ni kazi nzuri?” Utasema nini kuhusu hayo? Shetani anatumia mbinu na nadharia mbalimbali kumpotosha mwanadamu; huu upotovu wa mwanadamu ni dhana isiyo dhahiri? La, siyo dhahiri. Shetani pia anafanya vitu vingine vya utendaji, na pia anakuza mtazamo au nadharia katika dunia hii na katika jamii. Katika kila nasaba na katika kila kipindi cha historia, anakuza nadharia na kuingiza baadhi ya fikira ndani ya wanadamu. Fikira na nadharia hizi polepole zinakita mizizi katika mioyo ya watu, na kisha watu wanaanza kuishi kwa nadharia na fikira hizi. Punde wanapoishi kulingana na mambo haya, si wanakuwa Shetani bila kujua? Je, si watu wako kitu kimoja na Shetani? Wakati watu wamekuwa kitu kimoja na Shetani, ni nini mtazamo wao kwa Mungu mwishowe? Si ni mtazamo sawa ambao Shetani anao kwa Mungu? Hakuna anayethubutu kukubali haya, siyo? Ni ya kutisha sana! Mbona Nasema kwamba asili ya Shetani ni ovu? Hii inaamuliwa na kuchambuliwa kulingana na kile Shetani amefanya na vitu ambavyo Shetani amefichua; si bila ustahili kusema kwamba Shetani ni mwovu. Iwapo Ningesema tu kwamba Shetani ni mwovu, mngefikiri nini? Mngefikiri, “Bila shaka Shetani ni mwovu.” Hivyo nitakuuliza: “Ni kipengele kipi cha Shetani ni ovu?” Ukisema: “Shetani kumpinga Mungu ni uovu,” bado hutakuwa ukizungumza kwa uwazi. Sasa tumesema mambo maalum kwa njia hii; je, mna uelewa kuhusu maudhui maalum ya kiini cha uovu wa Shetani? (Ndiyo.) Ikiwa unaweza kuona waziwazi asili ovu ya Shetani, basi utaona hali zako mwenyewe. Je, kuna uhusiano wowote kati ya vitu hivi viwili? Je, hili ni jambo lenye manufaa kwako au la? (Ni lenye manufaa.) Ninaposhiriki kuhusu kiini cha utakatifu wa Mungu, ni muhimu Niwe na ushirika kuhusu kiini kiovu cha Shetani. Maoni yako kuhusu hilo ni yapi? (Ndiyo, ni muhimu.) Kwa nini? (Uovu wa Shetani unauweka mbali utakatifu wa Mungu.) Je, hivyo ndivyo ilivyo? Hii ni sahihi kwa kiasi fulani, ikichukuliwa kwamba bila uovu wa Shetani, watu hawangejua kwamba Mungu ni mtakatifu; ni sahihi kusema hivi. Hata hivyo, ukisema kwamba utakatifu wa Mungu upo tu kwa sababu ya tofauti yake na uovu wa Shetani, hii ni sahihi? Hii namna ya kujua ukweli kwa majadiliano si sahihi. Utakatifu wa Mungu ni kiini cha asili cha Mungu; hata ingawa Mungu anaufichua kupitia matendo Yake, hili bado ni onyesho asili la kiini cha Mungu na ni kiini cha asili cha Mungu; daima kimekuwepo na ni cha kiasili na ya asili kwa Mungu Mwenyewe, ingawa mwanadamu hawezi kukiona. Hii ni kwa sababu mwanadamu anaishi katikati ya tabia potovu ya Shetani na chini ya ushawishi wa Shetani, na hawajui kuhusu utakatifu, sembuse maudhui maalum ya utakatifu wa Mungu. Hivyo, ni muhimu kweli kwamba tushiriki kwanza kuhusu kiini kiovu cha Shetani? (Ndiyo, ni muhimu.) Watu wengine wanaweza kuonyesha baadhi ya shaka kama, “Unashiriki kuhusu Mungu Mwenyewe, mbona Unazungumza daima kuhusu jinsi Shetani anawapotosha watu na jinsi asili ya Shetani ni ovu?” Sasa umeyaweka mapumzikoni mashaka haya, siyo? Wakati watu wana utambuzi wa uovu wa Shetani na wakati wana ufafanuzi sahihi wa uovu, wakati watu wanaweza kuona wazi maudhui maalum na udhihirisho wa uovu, chanzo na kiini cha uovu—wakati utakatifu wa Mungu unajadiliwa sasa—basi watu watautambua kwa uwazi, ama kuufahamu wazi kama utakatifu wa Mungu, kama utakatifu wa kweli. Nisipojadili uovu wa Shetani, watu wengine wataamini kimakosa kwamba kitu fulani ambacho watu wanafanya katika jamii ama miongoni mwa watu—ama kitu fulani katika dunia hii—kinaweza kuhusiana na utakatifu. Si mtazamo huu ni wa kimakosa? (Ndiyo.)
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 154)
Shetani Hutumia Maarifa Kumpotosha Mwanadamu, na Yeye Hutumia Umaarufu na Faida Kumdhibiti
Kati ya njia tano ambazo Shetani anatumia kumpotosha mwanadamu, ya kwanza tuliyoitaja ni maarifa, kwa hivyo wacha kwanza tuchukue maarifa kama mada ya kushiriki. Shetani hutumia maarifa kama chambo. Sikiliza kwa makini: Ni aina tu ya chambo. Watu wanavutiwa “kusoma kwa bidii na kuliboresha kila siku,” ili kujihami kwa maarifa, kama silaha, kisha kutumia maarifa kufungua njia ya sayansi; kwa maneno mengine, kadri unavyopata maarifa zaidi, ndivyo utakavyoelewa zaidi. Shetani huwaambia watu haya yote. Shetani huwaambia watu kuwa na fikira za juu pia, wakati huo huo wanapojifunza maarifa, akiwaambia kuwa na matarajio na mawazo. Bila kujua kwa watu, Shetani anasambaza ujumbe mwingi kama huu, na kuwafanya watu kuhisi bila kujua kwamba vitu hivi ni sahihi, ama ni vya manufaa. Bila kujua, watu wanaitembea njia hii, bila kujua wanaongozwa mbele na matarajio na mawazo yao. Hatua kwa hatua, kwa kutojua wanajifunza kutoka kwa maarifa waliyopewa na Shetani njia ambazo watu wakubwa ama maarufu wanafikiria. Wanajifunza pia mambo fulani kutoka kwa matendo ya wengine ambao wanafikiriwa kuwa mashujaa. Shetani anatetea nini kwa mwanadamu katika matendo ya hawa mashujaa? Ni nini anachotaka kuingiza kwa mwanadamu? Mwanadamu lazima awe mzalendo, awe na uadilifu wa kitaifa, na awe shujaa. Ni yapi ambayo mwanadamu anajifunza kutoka kwa baadhi ya hadithi za kihistoria ama kutoka kwa wasifu wa mashujaa? Kuwa na hisia ya uaminifu wa kibinafsi, ama kufanya lolote kwa ajili ya marafiki na ndugu zako. Miongoni mwa maarifa haya ya Shetani, mwanadamu bila kujua anajifunza mambo mengi hasi. Katikati ya kutojua huku, mbegu zilizotayarishwa kwa ajili yao na Shetani zinapandwa katika akili zao zisizokomaa. Mbegu hizi zinawafanya kuhisi kwamba wanapaswa kuwa watu wakubwa, wanapaswa kuwa maarufu, wanapaswa kuwa mashujaa, kuwa wazalendo, kuwa watu wanaopenda familia zao, ama kuwa watu wanaoweza kufanya chochote kwa ajili ya rafiki na kuwa na hisia za uaminifu wa kibinafsi. Baada ya kushawishiwa na Shetani, bila kujua wanatembea njia ambayo amewatayarishia. Wanapotembea njia hii, wanalazimika kukubali kanuni za Shetani za kuishi. Bila kujua na bila wao kuwa na uelewa kabisa, wanakuwa na kanuni zao za kuishi, wakati hizi si chochote ila kanuni za Shetani ambazo zimeingizwa kwao kwa nguvu. Wakati wa mchakato wa kujifunza, Shetani anawasababisha kukuza malengo yao wenyewe, kuamua malengo yao ya maisha wenyewe, kanuni za kuishi, na mwelekeo wa maisha, wakati huo wote anawaingizia mambo ya kishetani, kwa kutumia hadithi, kwa kutumia wasifu, kwa kutumia mbinu zote zinazowezekana ili kuwapata watu, wachukue chambo polepole. Kwa njia hii, katika mkondo wa kujifunza kwao, wengine wanakuja kupenda fasihi, wengine uchumi, wengine unajimu ama jiografia. Kisha kuna wengine wanaokuja kupenda siasa, wengine wanaopenda fizikia, wengine kemia, na hata wengine wanaopenda teolojia. Haya yote ni sehemu ya maarifa. Katika mioyo yenu, kila mmoja wenu anajua jinsi mambo haya yanavyokwenda, kila mmoja amewahi kukutana nayo hapo awali. Kuhusiana na maarifa ya aina hii, yeyote anaweza kuzungumza bila kikomo juu ya aina mojawapo ya maarifa hayo. Na hivyo ni wazi jinsi maarifa haya yameingia kwa kina katika akili ya mwanadamu, pia inaonyesha nafasi iliyochukuliwa na maarifa haya katika akili ya mwanadamu na jinsi yalivyo na athari ya kina kwa mwanadamu. Punde tu mtu anapoanza kupendezwa na sehemu fulani ya maarifa, wakati katika moyo wake mtu ameipenda kwa dhati, basi bila kujua anaendeleza matamanio: Watu wengine wanataka kuwa watunzi, wengine wanataka kuwa waandishi, wengine wanataka kuwa na kazi kutokana na siasa, na wengine wanataka kushiriki katika uchumi na kuwa wanabiashara. Kisha kuna kundi la watu ambao wanataka kuwa mashujaa, kuwa wakubwa ama maarufu. Bila kujali mtu anataka kuwa mtu wa aina gani, lengo lake ni kuchukua mbinu hii ya kujifunza maarifa na kuitumia kwa ajili yake, kufikia matamanio yake, mawazo yake mwenyewe. Haijalishi inasikika kuwa nzuri namna gani—anataka kufikia ndoto yake, asiishi katika maisha haya bure, ama anataka kushiriki katika kazi—anakuza haya mawazo na matarajio ya juu lakini, kimsingi, yote ni ya nini? Je, mmeyafikiria haya awali? Kwa nini Shetani anataka kufanya hivi? Madhumuni ya Shetani ni yapi katika kuyaweka mambo haya kwa mwanadamu? Mioyo yenu lazima ielewe vizuri swali hili.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 155)
Shetani Hutumia Maarifa Kumpotosha Mwanadamu, na Yeye Hutumia Umaarufu na Faida Kumdhibiti
Katika mchakato wa mwanadamu kujifunza maarifa, Shetani atatumia mbinu zozote, inaweza iwe ni kufafanua hadithi, akimpa tu kipande kimoja cha maarifa, au kumruhusu aridhishe tamaa zake au aridhishe mawazo. Shetani anataka kukuongoza katika njia gani? Watu wanafikiri kwamba hakuna chochote kibaya na kujifunza maarifa, kwamba ni mkondo wa kiasili. Kuisema bila kutia chumvi, kukuza mawazo ya juu ama kuwa na matarajio ni kuwa na hamu ya kupata, na hii inapaswa kuwa njia sahihi katika maisha. Iwapo watu wanaweza kufanikisha mawazo yao wenyewe, ama kuwa na kazi maishani mwao—je, si ni adhimu zaidi kuishi namna hii? Kwa kufanya mambo haya, mtu anaweza kuheshimu babu zake na pia ana nafasi ya sifa yake katika historia—si hili ni jambo zuri? Hili ni jambo zuri katika macho ya watu wa kidunia na kwao linapaswa kuwa la kufaa na njema. Je, Shetani, hata hivyo, na malengo yake maovu, anawapeleka tu watu kwa njia ya aina hii na kisha kuamua amemaliza? Bila shaka la. Kwa kweli, haijalishi jinsi matamanio ya mwanadamu yalivyo makuu, haijalishi matamanio ya mwanadamu ni ya uhalisi jinsi gani ama jinsi yote yanaweza kuwa ya kufaa, yote ambayo mwanadamu anataka kufikia, yote ambayo mwanadamu anatafuta yameunganishwa bila kuchangulika na maneno mawili. Haya maneno mawili ni muhimu sana kwa kila mtu katika maisha yao yote, na ni mambo ambayo Shetani ananuia kuingiza ndani ya mwanadamu. Maneno haya mawili ni yapi? Ni “umaarufu” na “faida.” Shetani hutumia namna ya upole sana, namna ambayo inalingana kabisa na dhana za watu, na isiyokuwa na fujo sana, kuwafanya watu wakubali njia na sheria zake za kuishi, wakuze malengo ya maisha na mielekeo ya maisha, na kuja kuwa na matamanio makuu ya maisha. Haijalishi maelezo ya watu kuhusu matamanio yao maishani yanaweza kuwa ya mbwembwe kiasi gani, daima matamanio haya huzunguka umaarufu na faida. Kila kitu ambacho mtu yeyote mkuu au maarufu—au, kwa kweli, mtu yeyote—hufuatilia katika maisha yake yote kinahusiana tu na maneno haya mawili: “umaarufu” na “faida.” Watu hufikiri kwamba pindi wanapokuwa na umaarufu na faida, wanakuwa na mtaji wa kufurahia hadhi ya juu na utajiri mwingi, na kufurahia maisha. Wao hufikiri kwamba pindi wanapokuwa na umaarufu na faida, wanakuwa na mtaji wa kutafuta anasa na kujihusisha na starehe za mwili zisizo na kizuizi. Kwa ajili ya huu umaarufu na faida wanaoutamani, watu huikabidhi miili yao, mioyo yao, na hata kila kitu walicho nacho kwa Shetani kwa furaha na bila kujua, ikiwa ni pamoja na mustakabali na hatima zao. Wanafanya hivyo bila kusita, bila hata chembe ya shaka, na kamwe hawajui jinsi ya kuvidai tena vitu vyao vyote walivyokuwa navyo. Je, watu wanaweza kubaki na udhibiti wowote juu yao wenyewe punde wanapojikabidhi kwa Shetani na kuwa waaminifu kwake kwa njia hii? Bila shaka, hawawezi. Wanadhibitiwa na Shetani kikamilifu na kabisa. Wamezama kabisa na kikamilifu katika bwawa hili na hawawezi kujinasua. Baada ya mtu kukwama katika umaarufu na faida, hatafuti tena kile kilichong’aa, kile chenye haki ama yale mambo ambayo ni mazuri na mema. Hii ni kwa sababu nguvu za ushawishi ambazo umaarufu na faida yanayo juu ya watu ni kubwa mno, na vinakuwa vitu vya watu kutafuta katika maisha yao yote na pia milele bila kikomo. Hili si ukweli? Watu wengine watasema kwamba kujifunza maarifa si chochote zaidi ya kusoma vitabu ama kujifunza mambo kadhaa ambayo hawajui tayari, ili wasiwe nyuma ya wakati au wasiachwe nyuma na ulimwengu. Maarifa yanafunzwa tu ili waweze kuweka chakula mezani, kwa sababu ya siku zao za baadaye ama kwa sababu ya mahitaji ya kimsingi. Kuna mtu yeyote ambaye atastahimili mwongo wa kusoma kwa bidii kwa mahitaji ya kimsingi tu, ili kutatua swala la chakula tu? Hakuna watu kama hawa. Kwa hivyo ni nini anachotesekea miaka hii yote? Ni kwa sababu ya umaarufu na faida: Umaarufu na faida yanamngoja mbele, yanamwita, na anaamini tu kwa kupitia bidii yake mwenyewe, matatizo na mapambano ndiyo anaweza kufuata ile njia na hivyo kupata umaarufu na faida. Lazima ateseke matatizo haya kwa sababu ya njia yake ya siku za baadaye, kwa sababu ya raha yake ya siku za baadaye na kwa sababu ya maisha bora. Mnaweza kuniambia—haya maarifa kwa hakika ni nini? Je, si kanuni na falsafa za kuishi ambazo Shetani hutia ndani ya mwanadamu, kama vile “Penda Chama, penda nchi, na penda dini yako” na “Mtu mwenye hekima hutii hali”? Je, haya si “maarifa ya hali ya juu” ya maisha yaliyoingizwa kwa mwanadamu na Shetani? Chukua, kwa mfano, mawazo ya watu wakubwa, uadilifu wa watu maarufu ama roho jasiri za watu mashujaa, ama chukua uungwana na wema wa nguli na wenye upanga katika riwaya za kareti—je, si hizi zote ni njia ambazo Shetani anatia mawazo haya? Mawazo haya hushawishi kizazi kimoja baada ya kingine, na watu wa kila kizazi wanaletwa kuyakubali mawazo haya. Wao huhangaika sikuzote wakifuatilia “maarifa ya hali ya juu” ambayo hata watayatoa maisha yao kafara kwa ajili yake. Hii ndiyo njia na namna ambayo Shetani hutumia maarifa kuwapotosha watu. Hivyo baada ya Shetani kuwaelekeza watu kwenye njia hii, je, wanaweza kumtii na kumwabudu Mungu? Na, je, wanaweza kuyakubali maneno ya Mungu na kufuatilia ukweli? La hasha—kwa sababu wamepotoshwa na Shetani. Hebu tuangalie tena maarifa, mawazo, na maoni yaliyotiwa polepole ndani ya watu na Shetani: Je, mambo haya yana ukweli wa utii kwa Mungu na kumwabudu Mungu? Je, kuna ukweli wa kumcha Mungu na kuepuka maovu? Je, kuna maneno yoyote ya Mungu? Je, kuna chochote ndani yao kinachohusiana na ukweli? Hakuna chochote kabisa—vitu hivi havipo kabisa. Je, mnaweza kuwa na uhakika kwamba mambo yaliyotiwa polepole ndani ya watu na Shetani hayana ukweli wowote? Hamwezi kuthubutu—lakini haijalishi. Alimradi mtambue kwamba “umaarufu” na “faida” ni maneno mawili muhimu ambayo Shetani hutumia kuwashawishi watu kuingia njia ya uovu, basi hilo limetosha.
Acha turejelee tena kwa ufupi: Shetani hutumia nini kuendelea kumfungia mwanadamu na kumdhibiti? (Umaarufu na faida.) Shetani hutumia umaarufu na faida kudhibiti mawazo ya watu, akiwafanya wasifikirie chochote isipokuwa vitu hivi viwili, na kuwafanya wapiganie umaarufu na faida, wateseke kwa ajili ya umaarufu na faida, wavumilie fedheha na wabebe mizigo mizito kwa ajili ya umaarufu na faida, watoe kila kitu walicho nacho kwa ajili ya umaarufu na faida, na wafanye kila uamuzi au maamuzi kwa ajili ya umaarufu na faida. Kwa njia hii, Shetani anawaweka watu pingu zisizoonekana, na, wakiwa na pingu hizi, hawana uwezo wala ujasiri wa kujinasua. Bila kujua, wanabeba pingu hizi wanapojikokota mbele hatua kwa hatua, kwa ugumu mkubwa. Kwa ajili ya umaarufu huu na faida, wanadamu wanapotea kutoka kwa Mungu na Kumsaliti, na wanazidi kuwa waovu. Kwa njia hii, kizazi kimoja baada ya kingine kinaangamizwa katikati ya umaarufu na faida ya Shetani. Tukiviangalia sasa vitendo vya Shetani, je, nia zake za kudhuru kwa siri si za kuchukiza sana? Pengine leo bado hamwezi kuona kupitia nia mbaya za Shetani kwa sababu mnafikiri hakuna maisha bila umaarufu na faida. Mnafikri kwamba, iwapo watu wataacha umaarufu na faida nyuma, basi hawataweza tena kuona njia mbele, hawataweza tena kuona malengo yao, siku zao za baadaye zinakuwa zanye giza, zilizofifia na zisizo na matumaini. Lakini, polepole, nyote siku moja mtatambua kwamba umaarufu na faida ni pingu za ajabu ambazo Shetani hutumia kumfunga mwanadamu. Hadi ile siku utakuja kutambua hili, utapinga kabisa udhibiti wa Shetani na utapinga kabisa pingu anazoleta Shetani kukufunga. Wakati utakapofika wa wewe kutaka kutupilia mbali vitu vyote ambavyo Shetani ameingiza ndani yako, utakuwa basi umejiondoa kwa Shetani na pia utachukia kwa kweli vyote ambavyo Shetani amekuletea. Hapo tu ndipo utakuwa na upendo na shauku ya kweli kwa Mungu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 156)
Shetani Hutumia Sayansi Kumpotosha Mwanadamu
Shetani hutumia jina la sayansi kuridhisha hamu ya mwanadamu kutafiti sayansi na kuchunguza siri. Kwa jina la sayansi, Shetani huridhisha haja ya mwili na mahitaji ya mwanadamu kuendelea kuinua ubora wao wa maisha. Shetani hivyo, katika jina hili, hutumia njia ya sayansi kumpotosha mwanadamu. Je, ni kufikiria tu kwa mwanadamu ama akili za mwanadamu ambazo Shetani anapotosha kwa kutumia njia hii ya sayansi? Miongoni mwa watu, matukio na mambo katika mazingira yetu ambayo tunaweza kuona na ambayo tunakutana nayo, ni yapi mengine ambayo Shetani anatumia sayansi kupotosha? (Mazingira ya kiasili.) Mko sahihi. Inaonekana kwamba mmedhuriwa sana na hili, na pia mmeathirika sana na yeye. Mbali na kutumia matokeo yote ya utafiti na mahitimisho mbalimbali ya sayansi kumdanganya mwanadamu, Shetani pia hutumia sayansi kama mbinu ya kutekeleza maangamizi na unyonyaji tele wa mazingira ya kuishi aliyopewa mwanadamu na Mungu. Anafanya hivi chini ya kisingizio kwamba iwapo mwanadamu anatekeleza utafiti wa kisayansi, mazingira ya kuishi ya mwanadamu yatakuwa bora na bora zaidi na viwango vya kuishi vya mwanadamu daima vitaboreka, na zaidi ya hayo kwamba maendeleo ya kisayansi yanafanywa ili kuhudumia mahitaji ya kimwili ya mwanadamu yanayozidi kila siku na haja yao ya kuendelea kupandisha ubora wao wa maisha. Huu ni msingi wa kidhahania wa maendeleo ya Shetani ya sayansi. Hata hivyo, sayansi imemletea binadamu nini? Je, mazingira yetu ya kuishi—na mazingira ya kuishi ya binadamu wote—hayajachafuliwa? Je, si hewa anayopumua mwanadamu imechafuliwa? Je, si maji tunayokunywa yamechafuliwa? Je, chakula tunachokula bado ni halisi na cha asilia? Nafaka na mboga nyingi zimebadilishwa vinasaba, zimekuzwa kwa mbolea, na nyingine ni aina zilizoundwa kwa kutumia sayansi. Mboga na matunda tunayokula sio asili tena. Hata mayai ya asili si rahisi kupata tena, na mayai hayana tena ladha yake kwa jinsi yalivyokuwa hapo awali, baada ya kuwa tayari yamechakatwa na ile inayoitwa sayansi ya Shetani. Kwa kuangalia taswira kubwa, anga nzima imeharibika na kuchafuliwa; milima, maziwa, misitu, mito, bahari, na kila kitu juu na chini ya ardhi vyote vimeharibiwa na inayoitwa mafanikio ya kisayansi. Kwa maneno mengine, mazingira yote ya kiikolojia, mazingira ya kuishi aliyopewa mwanadamu na Mungu yameangamizwa na kuharibiwa na inayodaiwa kuwa sayansi. Ingawa kuna watu wengi waliopata walichotarajia katika suala la ubora wa maisha wanaotafuta, kuridhisha tamaa na miili yao, mazingira ambayo mwanadamu anaishi kimsingi yameharibiwa na kuangamizwa na “mafanikio” mbalimbali yaliyoletwa na sayansi. Sasa, hatuna tena haki ya kupumua pumzi moja ya hewa safi. Hii ni huzuni ya mwanadamu? Je, kuna furaha yoyote iliyosalia kuzungumzia juu ya mwanadamu, wakati lazima waishi katika aina hii ya nafasi? Nafasi hii na mazingira ya kuishi ambayo mwanadamu anaishi, kutoka mwanzoni, haya mazingira ya kuishi yaliumbwa na Mungu kwa ajili ya mwanadamu. Maji ambayo watu hunywa, hewa ambayo watu hupumua, vyakula mbalimbali ambavyo watu hula, na vilevile mimea na viumbe hai, na hata milima, maziwa, na bahari—kila sehemu ya mazingira haya ya maisha alipewa mwanadamu na Mungu; ni ya asili, na hutekeleza kulingana na amri asili iliyotolewa na Mungu. Bila sayansi, watu bado wangefuata mbinu walizopewa na Mungu, wangeweza kufurahia yote yaliyo safi na ya asili, na wangekuwa wenye furaha. Sasa, hata hivyo, haya yote yameangamizwa na kuharibiwa na Shetani; nafasi ya kimsingi ya kuishi ya mwanadamu haipo tena katika hali yake ya asili zaidi. Lakini hakuna anayeweza kutambua kilichosababisha matokeo ya aina hii ama jinsi haya yalikuja kuwa, na zaidi ya hapo hata watu zaidi wanaelewa na kukaribia sayansi kwa kutumia mawazo waliyoingiziwa na Shetani. Je, hii si ya kuchukiza sana na ya kusikitisha? Kwa kuwa Shetani sasa amechukua nafasi ambamo wanadamu wapo na mazingira yao ya kuishi na kuwapotosha kuwa katika hali hii, na kwa kuwa wanadamu wanaendelea kwa njia hii, kuna haja yoyote ya mkono wa Mungu kuwaangamiza wanadamu hawa duniani? Iwapo wanadamu watazidi kuendelea kwa njia hii, watachukua mwelekeo upi? (Wataangamizwa.) Wataangamizwa kwa njia gani? Zaidi ya mwanadamu kutafuta kwa tamaa umaarufu na faida, daima anaendelea kutekeleza uchunguzi wa sayansi na utafiti wa kina, kisha bila kikomo huridhisha mahitaji yake ya mwili na tamaa; yapi tena ni matokeo ya mwanadamu? Kwanza kabisa hakuna tena usawa wa ikolojia na, pamoja na hili, miili ya wanadamu wote imetiwa doa na kuharibiwa na mazingira ya hali hii, na magonjwa mbalimbali ya kuambukiza na mapigo kusambaa kila mahali. Hii ni hali ambayo mwanadamu sasa hawezi kudhibiti, sivyo? Sasa kwa sababu mnaelewa hili, iwapo wanadamu hawamfuati Mungu, lakini daima wanamfuata Shetani kwa njia hii—kutumia maarifa daima kujitajirisha, kutumia sayansi kuchunguza bila kikomo siku za baadaye za maisha ya binadamu, kutumia mbinu ya aina hii kuendelea kuishi—unaweza kutambua jinsi hii itawaishia binadamu? Binadamu watatoweka wasikuwepo tena kiasili: Hatua kwa hatua, binadamu wanazidi kuukaribia uharibifu, wakielekea maangamizi yao wenyewe! Je, huku si kujiletea maangamizi wenyewe? Na, je, si hili ni tokeo la maendeleo ya kisayansi? Inaonekana sasa kama sayansi ni aina ya dawa ya kichawi ambayo Shetani amemwandalia mwanadamu, ili wakati mnapojaribu kupambanua mambo mnafanya hivyo katika hali ya ukungu; haijalishi mnaangalia kwa ugumu kiasi gani, hamwezi kuona mambo kwa uwazi, na haijalishi mnajaribu sana vipi, hamwezi kuyatambua. Hata hivyo, Shetani bado anatumia jina la sayansi kuzidisha hamu yako na kukuongoza kwa pua, mguu mmoja mbele ya mwingine, kuelekea shimoni na kuelekea kifo. Na hali ikiwa hivi, watu wataona wazi kwamba kwa kweli, maangamizo ya mwanadamu yanaletwa na mkono wa Shetani—Shetani ndiye kiongozi.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 157)
Shetani Hutumia Desturi ya Kitamaduni Kumpotosha Mwanadamu
Shetani hutumia desturi ya kitamaduni kumpotosha mwanadamu. Kuna usawa mwingi kati ya desturi ya kitamaduni na ushirikina, ni kwamba tu desturi ya kitamaduni ina hadithi fulani, vidokezo, na vyanzo fulani. Shetani ametunga na kuunda ngano ama hadithi nyingi katika vitabu vya historia, na kuacha watu na hisia za kina za desturi ya kitamaduni ama watu wa kishirikina. Chukua kwa mfano Watu Wanane Wasiokufa Wanaovuka Bahari, Safari ya kwenda Magharibi, Mfalme Mkuu Jade, Nezha Anamshinda Joka Mfalme, na Uchunguzi wa Miungu, zote za Uchina. Haya hayajakita mizizi katika akili za mwanadamu? Hata iwapo baadhi yenu hawajui maelezo yote, bado mnajua hadithi za jumla, na yaliyomo kwa jumla ndiyo yanayokwama katika moyo wako na yanakwama katika akili yako, na huwezi kuyasahau. Hizi ni dhana au hadithi ambazo Shetani alimwandalia mwanadamu kitambo sana, na ambazo zimesambazwa katika nyakati tofauti. Haya mambo yanadhuru moja kwa moja na kumomonyoa nafsi za watu na kuweka watu chini ya uchawi mmoja baada ya mwingine. Hiyo ni kusema kwamba baada ya wewe kukubali aina hii ya desturi ya kitamaduni, hadithi ama vitu vya ushirikina, mara tu mambo haya yanawekwa katika akili yako, na mara tu yanakwama katika moyo wako, basi ni kama umeduwazwa—unakamatwa na kushawishika na hii mitego ya kitamaduni, haya mawazo na hadithi za kitamaduni. Yanashawishi maisha yako, mtazamo wako wa maisha na pia yanashawishi maoni yako ya mambo. Hata zaidi yanashawishi ufuataji wako wa njia sahihi ya maisha: Hakika huu ni uchawi. Unajaribu lakini huwezi kuyatupilia mbali; unayakatakata lakini huwezi kuyakatia chini; unayapiga lakini huwezi kuyapiga chini. Zaidi ya hayo, baada ya mwanadamu kuwekwa chini na aina hii ya uchawi, bila kujua, anaanza kumwabudu Shetani, kukuza taswira ya Shetani katika moyo wake. Kwa maneno mengine, anamweka Shetani kama sanamu, kifaa cha yeye kuabudu na kutazamia, hata kwenda mbali kiasi cha kumchukulia kama Mungu. Bila kujua, mambo haya yako katika mioyo ya watu yakidhibiti maneno na matendo yao. Aidha, kwanza unachukulia hadithi na hekaya hizi kuwa uongo, na kisha bila kujua unakubali kuwepo kwa hadithi hizi, kuzitengenezea sanamu halisi na kuzibadili kuwa mambo halisi yaliyopo. Kwa kutokujua kwako, unapokea mawazo haya bila kufahamu na uwepo wa vitu hivi. Pia unapokea bila kufahamu mashetani, Shetani na sanamu ndani ya nyumba yako na ndani ya moyo wako—bila shaka huu ni uchawi. Je, mnahisi hivyo pia? (Ndiyo.) Je, kuna yeyote miongoni mwenu ambaye amechoma ubani na kuabudu Budha? (Ndiyo.) Kwa hivyo madhumuni ya kuchoma ubani na kumwabudu Budha yalikuwa yapi? (Kuombea amani.) Ukifikiria jambo hilo sasa, je, ni upuuzi kusali kwa Shetani kwa ajili ya amani? Je, Shetani huleta amani? (Hapana.) Je, ulikuwa mjinga wakati huo? Aina hiyo ya tabia ni ya kipuuzi, ya kijinga na ni ushamba, sivyo? Shetani anafikiria tu jinsi ya kukupotosha na hawezi kukupa amani; anaweza tu kukupa nafasi ya kupumua ya muda mfupi. Lakini lazima uchukue kiapo na ukivunja ahadi yako ama ukivunja kiapo ulichofanya, basi utaona jinsi anavyokuadhibu. Kwa kukufanya uchukue kiapo, kwa kweli anataka kukudhibiti. Wakati mlipoombea amani, mlipata amani? (La.) Hamkupata amani, lakini kinyume na hayo alileta bahati mbaya, majanga yasiyoisha—kwa kweli bahari ya uchungu isiyo na kikomo. Amani haiko miongoni mwa miliki ya Shetani, na hili ni ukweli. Haya ndiyo matokeo kwa wanadamu ya ushirikina wa kikabila na desturi ya kitamaduni.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 158)
Shetani Hutumia Mienendo ya Kijamii Kumpotosha Mwanadamu
Shetani humpotosha na kumtawala mwanadamu kupitia mitindo ya kijamii. Mitindo ya kijamii inajumuisha vipengele vingi, ikiwa ni pamoja na maeneo mbalimbali kama vile kuabudu watu mashuhuri na wenye kusifika, na vilevile waigizaji wa filamu na wanamuziki mashuhuri, kuwaabudu watu mashuhuri, michezo ya mtandaoni, n.k.—hizi zote ni sehemu ya mitindo ya kijamii, na hakuna haja ya kuingia katika maelezo mengi hapa. Tutazungumzia tu kuhusu mawazo ambayo mitindo ya kijamii inaleta kwa watu, jinsi inavyowafanya watu wajiendeshe duniani, na malengo ya maisha na mitazamo ambayo inaleta kwa watu. Hizi ni muhimu sana; zinaweza kudhibiti na kushawishi mawazo na maoni ya watu. Mitindo hii huibuka moja baada ya nyingine, na yote huwa na ushawishi mbaya unaoendelea kumdhalilisha mwanadamu na kuwafanya watu kupoteza dhamiri, ubinadamu na akili, kudhoofisha zaidi maadili yao na ubora wa tabia zao, kiasi kwamba tunaweza hata kusema kwamba watu wengi sasa hawana uadilifu, hawana ubinadamu, na wala hawana dhamiri yoyote, sembuse kuwa na akili yoyote. Kwa hivyo mitindo hii ya kijamii ni ipi? Ni mitindo ambayo huwezi kuiona kwa macho. Wakati mtindo mpya unapoenea duniani kote, pengine ni idadi ndogo tu ya watu ndio walio na ufahamu wa juu, wakitenda kama waanzishaji mitindo. Wao huanza kwa kufanya jambo jipya, kisha kukubali aina fulani ya wazo au aina fulani ya mtazamo. Hata hivyo, watu wengi, wataendelea kuambukizwa, kuvutiwa na kustaarabishwa na mtindo huu katika hali ya kutofahamu, hadi wote bila kujua na bila kupenda wanaikubali na wanazama ndani yake na kudhibitiwa nayo. Moja baada ya nyingine, mitindo ya aina hii inawafanya watu ambao si wa mwili na akili timamu, wasiojua ukweli, na hawawezi kutofautisha kati ya vitu vyema na hasi, kuzikubali kwa furaha pamoja na mtazamo wa maisha, na maadili yatokayo kwa Shetani. Wanakubali anachowaambia Shetani kuhusu jinsi ya kuyashughulikia maisha na jinsi ya kuishi ambavyo Shetani “amewapatia.” Na hawana nguvu, wala uwezo, wala ufahamu wa kupinga. Kwa hivyo, utaitambuaje mitindo kama hii? Nimechagua mfano rahisi ambao mnaweza kuja kuelewa polepole. Kwa mfano, watu wa kale waliendesha biashara zao kwa njia ambayo haikudanganya wazee wala vijana, na ambayo iliuza bidhaa kwa bei sawa bila kujali aliyekuwa akinunua. Je, dokezo la dhamiri na ubinadamu haliwasilishwi hapa? Wakati watu walitumia aina hii ya imani walipokuwa wakifanya biashara zao, inaonyesha kwamba bado walikuwa na dhamiri fulani, ubinadamu fulani wakati huo. Lakini kutokana na uhitaji wa pesa unaoongezeka daima kwa mwanadamu, watu bila kujua walikuja kupenda pesa, kupenda faida, na kupenda raha zaidi na zaidi. Kwa hivyo watu walikuja kuona pesa kuwa muhimu zaidi? Wakati watu wanaona pesa kuwa muhimu zaidi, bila kujua wanaanza kupuuzia sifa, umashuhuri wao, ufahari, na uadilifu wao, sivyo? Unapojihusisha katika biashara, unawaona wengine wakiwa matajiri kwa kuwahadaa wengine. Ingawa pesa zinazochumwa si halali, wanazaidi kuwa matajiri. Unapoona yote ambayo familia zao zinafurahia hukukasirisha: “Sote wawili tuko katika biashara lakini walikuwa matajiri. Kwa nini nisiweze kuchuma pesa nyingi? Siwezi kuvumilia hili—lazima nitafute njia ya kupata pesa zaidi.” Baada ya hayo, unachofikiria ni jinsi ya kutengeneza utajiri wako tu. Mara tu unapoacha kuamini kwamba “fedha inapaswa kupatikana kwa dhamiri, bila kumdanganya mtu yeyote,” basi, ukiongozwa na maslahi yako mwenyewe, kufikiri kwako kunabadilika polepole, na vile vile maadili ya matendo yako. Unapomhadaa mtu kwa mara ya kwanza, unahisi ukishutumiwa na dhamiri yako, na moyo wako unakuambia, “Hili linapokamilika, hii ni mara ya mwisho ambayo nitamdanganya mtu. Kuwadanganya watu siku zote kutasababisha adhabu!” Hii ndiyo kazi ya dhamiri ya mwanadamu—kukufanya uhisi aibu na kukushutumu, ili ihisi kuwa siyo asili wakati unamdanganya mtu. Lakini baada ya wewe kufanikiwa kumdanganya mtu unaona kwamba sasa una pesa zaidi kuliko awali, na unafikiria mbinu hii inaweza kuwa ya manufaa sana kwako. Licha ya maumivu madogo ndani ya moyo wako, bado unahisi kujipongeza kwa mafanikio yako, na unahisi kuridhika mwenyewe kiasi. Kwa mara ya kwanza, unakubali tabia yako mwenyewe, njia zako mwenyewe za uwongo. Punde mwanadamu amechafuliwa na kudanganywa huku, ni sawa na mtu ambaye anahusika na kamari na kisha anakuwa mchezaji kamari. Katika kutoelewa, anapenda tabia yake ya kudanganya na anaikubali. Katika hali yako ya kutoelewa, unakubali udanganyifu. Katika hali yako ya kutoelewa unachukua udanganyifu kuwa tabia halali ya kibiashara, na unachukua kudanganya kuwa mbinu ya manufaa zaidi ya kusalimika kwako na riziki yako; unafikiria kwamba kwa kufanya hivi anaweza kutengeneza mali nyingi haraka. Huu ni mchakato: Mwanzoni mwa mchakato huu watu hawawezi kukubali tabia ya aina hii, wanadharau tabia hii na njia hii ya kufanya mambo, kisha wanajaribu tabia hii wao wenyewe, na kuijaribu kwa njia yao wenyewe, na kisha mioyo yao inaanza kubadilika polepole. Kwa hivyo mabadiliko haya ni yapi? Ni kukubali na kukiri mwenendo huu, kukiri na kukubali wazo hili lililoingizwa kwako na mwenendo wa jamii. Kwa kutojua, unahisi kwamba usipodanganya watu katika kufanya biashara nao, unahisi umebaki nyuma sana; usipodanganya watu unahisi kuwa umepoteza kitu. Bila kujua, kudanganya huku kunakuwa nafsi yako, tegemeo kuu kwako, na kunakuwa aina ya tabia ya lazima ambayo ni kanuni maishani mwako. Baada ya mwanadamu kukubali tabia hii na kufikiria huku, je, moyo wa mwanadamu unapitia mabadiliko? Moyo wako umebadilika, basi uadilifu wako umebadilika? Ubinadamu wako umebadilika? Dhamiri yako imebadilika? Nafsi yako nzima, kutoka moyoni mwako hadi mawazoni mwako, kutoka ndani hadi nje, umebadilika, na haya ni mabadiliko ya ubora. Badiliko hili linakuvuta mbali zaidi na zaidi kutoka kwa Mungu, na unakuwa karibu na Shetani zaidi na zaidi; unamfanania Shetani zaidi na zaidi, na matokeo yake ni kwamba kupotoshwa na Shetani kunakufanya uwe pepo.
Unapotazama mitindo hii ya kijamii, je, unaweza kusema kuwa ina ushawishi mkubwa kwa watu? Je, ina athari inayodhuru kwa kina kwa watu? Mitindo hii ina athari ya kudhuru kwa kina kwa watu. Je, ni vipengele vipi vya mwanadamu ambavyo Shetani hutumia kwa kila mojawapo ya mitindo hii kupotosha? Kwa kiwango cha juu, Shetani hupotosha dhamiri, hisia, ubinadamu, maadili na mitazamo ya maisha ya mwanadamu. Na, je, mitindo hii ya kijamii haiwashushi na kuwapotosha watu hatua kwa hatua? Shetani hutumia hii mitindo ya kijamii kuvuta watu hatua moja baada ya nyingine hadi katika kiota cha mashetani, ili watu walionaswa katika mitindo ya kijamii bila kujua wanatetea pesa na tamaa za mwili, na pia kutetea uovu na ukatili. Punde mambo haya yameingia moyoni mwa mwanadamu, ni nini basi mwanadamu anakuwa? Mwanadamu anakuwa ibilisi Shetani! Kwa nini? Kwa sababu, ni mwelekeo gani wa kisaikolojia uliopo ndani ya moyo wa mwanadamu? Ni kipi ambacho mwanadamu anatetea? Mwanadamu huanza kupenda uovu na ukatili. Hawapendi uzuri ama wema, wala hata amani. Watu hawako radhi kuishi maisha rahisi ya ubinadamu wa kawaida, lakini badala yake wanataka kufurahia hadhi ya juu na utajiri mkubwa, kufurahia raha za mwili, na kutumia juhudi zote kuridhisha miili yao, bila vizuizi, hakuna vifungo vya kuwashikilia nyuma, kwa maneno mengine kufanya chochote wanachotaka. Hivyo wakati mwanadamu ametumbukizwa katika mitindo ya aina hii, maarifa ambayo mmefunzwa yanaweza kuwasaidia kuwa huru? Je, desturi ya kitamaduni na ushirikina mnayojua yanaweza kuwasaidia kutupilia mbali hii hatari ya kutisha? Je, maadili ya desturi na sherehe za desturi ambazo mwanadamu huelewa zinaweza kumsaidia kujizuia? Kwa mfano, chukua riwaya ya Analects na Tao Te Ching. Je, vinaweza kuwasaidia watu kujikwamua miguu yao kutoka katika tope la mitindo hii miovu? Bila shaka hapana. Hivyo, mwanadamu anakuwa mwovu zaidi na zaidi, mwenye kiburi, mwenye kujishusha hadhi, mwenye ubinafsi, na mwenye kijicho. Hakuna tena upendo kati ya watu, hakuna tena upendo wowote kati ya wanafamilia, hakuna tena uelewa wowote miongoni mwa jamaa na marafiki; mahusiano ya binadamu yamejawa ukatili. Kila mtu anataka kutumia mbinu katili kuishi miongoni mwa wanadamu wenzake; wanakamata riziki zao kwa kutumia ukatili; wanapata vyeo vyao na kupata faida zao wenyewe kwa kutumia ukatili na wanafanya chochote watakacho kwa kutumia njia mbovu na katili. Si ubinadamu huu unatisha? Unatisha sana: Sio tu kwamba walimsulubisha Mungu, bali pia wangewachinja wote wanaomfuata—kwa sababu mwanadamu ni mwovu sana. Baada ya kusikia mambo haya yote ambayo Nimezungumzia hivi punde, hamfikiri kwamba inatisha kuishi katika mazingira haya, katika ulimwengu huu, na miongoni mwa aina hii ya umati, ambao Shetani hupitia kupotosha watu? (Ndiyo.) Kwa hivyo mmewahi kujihisi kuwa wenye kusikitisha? Lazima mnaihisi kiasi sasa, siyo? (Ndiyo.) Kwa kusikiza sauti zenu, inaonekana kana kwamba mnafikiria “Shetani hutumia njia nyingi tofauti kumpotosha mwanadamu. Anakamata kila fursa na yupo kila mahali tunapogeukia. Mwanadamu bado anaweza kuokolewa?” Je, mwanadamu bado anaweza kuokolewa? Wanadamu wanaweza kujiokoa? (La.) Je, Mfalme Mkuu wa Jade anaweza kumwokoa mwanadamu? Je, Confucius anaweza kumwokoa mwanadamu? Je, Guanyin Bodhisattva anaweza kumwokoa mwanadamu? (La.) Kwa hivyo ni nani anayeweza kumwokoa mwanadamu? (Mungu.) Watu wengine, hata hivyo, wataibua katika mioyo yao maswali kama: “Shetani anatudhuru kwa kiasi kikubwa sana, kwa hasira sana kiasi kwamba hatuna matumaini ya kuishi, wala imani katika kuishi. Sote tunaishi miongoni mwa upotovu na kila mtu anampinga Mungu hata hivyo, na sasa mioyo yetu imezama chini kadri iwezavyo. Kwa hivyo wakati Shetani anatupotosha, Mungu yuko wapi? Mungu anafanya nini? Chochote Mungu anatufanyia kamwe hatukihisi!” Watu wengine bila kuepukika wanahisi kuhuzunika na bila kuepukika wanahisi kuvunjika moyo kiasi, sivyo? Kwenu, hisia hii ni ya kina sana kwa sababu yote ambayo Nimekuwa nikiyasema yamekuwa yakiwafanya watu kuja kuelewa polepole, kuhisi zaidi na zaidi kwamba hawana matumaini, kuhisi zaidi na zaidi kwamba wameachwa na Mungu. Lakini usijali. Mada yetu ya ushirika wa leo, “uovu wa Shetani,” sio mada yetu halisi. Ili kuzungumzia kuhusu kiini cha utakatifu wa Mungu, hata hivyo, ni lazima kwanza tujadili kuhusu jinsi Shetani anavyompotosha mwanadamu na uovu wa Shetani ili kuifanya iwe wazi zaidi kwa watu kwamba ni aina gani ya hali ambayo mwanadamu sasa yuko nayo. Lengo moja la kuongea juu ya hili ni kuruhusu watu kujua uovu wa Shetani, ilhali jingine ni kuwaruhusu watu kuelewa kwa kina zaidi utakatifu ni nini.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 159)
Kuelewa Utakatifu wa Mungu Kupitia Kile Anachomfanyia Mwanadamu
Wakati wowote ambao Shetani anampotosha mwanadamu ama anashughulika na madhara yasiyodhibitiwa, Mungu hasimami bila kufanya kazi, wala hawaweki kando ama kuwapuuza wale ambao Amewachagua. Yote ambayo Shetani anafanya ni wazi kabisa na yanaeleweka na Mungu. Haijalishi anachofanya Shetani, haijalishi mwenendo anaosababisha kuibuka, Mungu anajua yote ambayo Shetani anajaribu kufanya, na Mungu hawaachi wale ambao Amewachagua. Badala yake, bila bila kujulikana kokote, kwa siri, kwa ukimya, Mungu anafanya yote yanayohitajika. Mungu Anapoanza kufanya kazi kwa mtu, wakati amemchagua mtu, Hamwambii yeyote, wala Hamwambii Shetani, wala hata kufanya maonyesho makubwa. Anafanya tu kwa ukimya, kwa asili kile ambacho kinahitajika. Kwanza, Anakuchagulia familia; usuli ambao hiyo familia inayo, wazazi wako ni akina nani, mababu zako ni akina nani—haya yote tayari yaliamuliwa na Mungu. Kwa maneno mengine, haya hayakuwa maamuzi ya mvuto wa ghafla yaliyofanywa na Yeye, lakini badala yake hii ilikuwa kazi iliyoanza kitambo. Baada ya Mungu kukuchagulia familia, pia Anachagua tarehe ambayo utazaliwa. Kwa sasa, Mungu anaangalia unapozaliwa katika dunia hii ukilia, Anatazama kuzaliwa kwako, Anatazama unapotamka maneno yako ya kwanza, Anatazama unapoanguka na kutembea hatua zako za kwanza, ukijifunza kutembea. Kwanza unachukua hatua moja na kisha unachukua nyingine … sasa unaweza kukimbia, sasa unaweza kuruka, sasa unaweza kuongea, sasa unaweza kuonyesha hisia zako. Mwanadamu anapokua, macho ya Shetani yamewekwa kwa kila mmoja wao, kama simbamarara anayetazama mawindo yake. Lakini katika kufanya kazi Yake, Mungu hajawahi kuteseka na mapungufu yoyote ya watu, matukio ama mambo, ya nafasi ama wakati; Anafanya kile anachopaswa kufanya na Anafanya kile Anacholazimika kufanya. Katika mchakato wa kukua, unaweza kukutana na mambo mengi ambayo hupendi, kukutana na magonjwa na kuvunjika moyo. Lakini unapotembea njia hii, maisha yako na siku zako za baadaye ziko chini ya ulinzi wa Mungu kabisa. Mungu anakupa hakikisho halisi litakalodumu maisha yako yote, kwani Yeye yuko kando yako, anakulinda na kukutunza. Bila kujua haya, unakua. Unaanza kukutana na mambo mapya na unaanza kujua dunia hii na wanadamu hawa. Kila kitu ni kipya kwako. Unapenda kufanya kile unachopenda. Unaishi katika ubinadamu wako mwenyewe, unaishi katika nafasi yako ya kuishi na huna hata kiasi kidogo cha mtazamo kuhusu kuwepo kwa Mungu. Lakini Mungu anakulinda katika kila hatua ya njia unapokua, na Anakutazama unapoweka kila hatua mbele. Hata unapojifunza maarifa, ama kusoma sayansi, Mungu hajawahi toka upande wako kwa hatua hata moja. Wewe ni sawa na watu wengine kwa kuwa, katika harakati za kuja kujua na kukutana na dunia, umeanzisha mawazo yako mwenyewe, una mambo yako mwenyewe ya kupitisha muda, mambo unayopenda mwenyewe, na pia unayo matamanio ya juu. Wakati mwingi unafikiria siku zako za baadaye, wakati mwingi unachora muhtasari wa jinsi siku zako za baadaye zinapaswa kuwa. Lakini haijalishi kitakachofanyika njiani, Mungu anaona vyote na macho wazi. Labda wewe mwenyewe umesahau siku zako za nyuma, lakini kwa Mungu, hakuna anayeweza kukuelewa bora kuliko Yeye. Unaishi chini ya macho ya Mungu, unakua, unapevuka. Wakati huu, jukumu muhimu la Mungu ni kitu ambacho hakuna yeyote kamwe hufahamu, kitu ambacho hakuna yeyote anayejua. Mungu hakika hakuambii kukihusu. Basi kitu hiki cha muhimu zaidi ni kipi? Inaweza kusemwa kwamba ni hakikisho kuwa Mungu atamwokoa mtu. Hii inamaanisha kwamba Mungu anataka kumwokoa mtu huyu, kwa hivyo lazima Afanye hivi, na kazi hii ni muhimu sana kwa mwanadamu na Mungu. Je, mnajua ni nini? Inaonekana kwamba hamna hisia yoyote kuhusu hili, ama dhana yoyote kuhusu hili, kwa hivyo nitawaambia. Kutoka ulipozaliwa hadi sasa, Mungu amefanya kazi nyingi sana kwako, lakini Hakupi maelezo moja baada ya nyingine ya kila kitu Alichokifanya. Mungu hakukuruhusu ujue, na Hakukwambia. Hata hivyo, kwa mwanadamu, kila kitu anachofanya Mungu ni muhimu. Kwa Mungu, ni kitu ambacho lazima Afanye. Katika moyo wake kuna kitu muhimu Anapaswa kufanya ambacho kinazidi yoyote ya mambo haya. Yaani, kutoka alipozaliwa mwanadamu hadi sasa, Mungu lazima ahakikishe usalama wao. Baada ya kusikia maneno haya, mnaweza kuhisi kana kwamba hamwelewi kikamilifu, kusema “usalama huu ni muhimu sana?” Kwa hivyo ni nini maana halisi ya “usalama”? Labda mnauelewa kumaanisha amani ama pengine mnauelewa kumaanisha kutopitia maafa ama msiba wowote, kuishi vyema, kuishi maisha ya kawaida. Lakini katika mioyo yenu lazima mjue kwamba si rahisi hivyo. Kwa hivyo ni nini hasa kitu hiki ambacho Nimekuwa nikizungumzia, ambacho Mungu anapaswa kufanya? Usalama unamaanisha nini kwa Mungu? Je, kweli ni hakikisho la maana ya kawaida ya “usalama”? La. Kwa hivyo ni nini hiki ambacho Mungu anafanya? Usalama huu unamaanisha humezwi na Shetani. Je, jambo hili ni muhimu? Wewe humezwi na Shetani, kwa hivyo hili linahusisha usalama wako, au la? Hili linahusisha usalama wako binafsi, na hakuwezi kuwa na lolote muhimu zaidi. Baada ya wewe kumezwa na Shetani, nafsi yako wala mwili wako si vya Mungu tena. Mungu hatakuokoa tena. Mungu anaziacha nafsi kama hizo na kuwaacha watu kama hao. Kwa hivyo Nasema kitu muhimu sana ambacho Mungu anapaswa kufanya ni kuhakikishia usalama wako, kuhakikisha kwamba hutamezwa na Shetani. Hili ni muhimu Sana, sivyo? Kwa hivyo mbona hamwezi kujibu? Inaonekana kwamba hamwezi kuhisi wema mkubwa wa Mungu!
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 160)
Kuelewa Utakatifu wa Mungu Kupitia Kile Anachomfanyia Mwanadamu
Mungu anafanya mengi kando na kuhakikisha usalama wa watu, kuhakikisha kwamba hawatamezwa na Shetani; pia hufanya kazi nyingi sana kwa kutayarisha kumchagua mtu na kumwokoa. Kwanza, una tabia ya aina gani, utazaliwa katika familia ya aina gani, wazazi wako ni akina nani, una kaka na dada wangapi, na hali, hadhi ya kiuchumi na tabia za familia ambayo unazaliwa ndani ni gani—haya yote unapangiwa wewe kwa uangalifu na Mungu. Je, unajua ni familia ya aina gani watu waliochaguliwa na Mungu wanazaliwa ndani mara nyingi, kama inavyohusu watu wengi? Je, ni familia mashuhuri? Hatuwezi sema kwa uhakika hakuna yoyote. Kunaweza kuwa na baadhi, lakini ni chache sana. Mungu anaziacha nafsi kama hizo na kuwaacha watu kama hao? Mara nyingi huwa si aina hii ya familia. Kwa hivyo Mungu anapangia watu hawa familia za aina gani zaidi? (Familia za kawaida.) Kwa hivyo ni familia zipi ambazo zinaweza kufikiriwa za kawaida? Familia hizi ni pamoja na zile zinazofanya kazi—zinategemea mishahara yao kuishi na zinaweza kumudu mahitaji ya kimsingi na si wenye mali nyingi; pia ni pamoja na familia za wakulima. Wakulima hutegemea kupanda mazao kwa chakula chao, na wana nafaka za kula na nguo za kuvaa, hawataona njaa au kuhisi. Kisha kuna familia zingine zinazoendesha biashara ndogondogo, na zingine ambazo wazazi ni wasomi, na hizi zinaweza kuhesabika kama familia za kawaida. Kuna baadhi ya wazazi ambao ni wafanyakazi wa ofisi ama maafisa wadogo wa serikali, ambao hawawezi kuhesabika kama familia mashuhuri pia. Watu wengi zaidi wanazaliwa katika familia za kawaida, na haya yote yanapangiliwa na Mungu. Hiyo ni kusema, kwanza kabisa, mazingira haya unayoishi si ya familia yenye uwezo mkubwa ambao mtu anaweza kufikiria, lakini badala yake ni familia uliyoamuliwa na Mungu, na watu wengi wataishi katika mipaka ya aina hii ya familia. Kwa hivyo je, vipi kuhusu hadhi ya kijamii? Hali ya uchumi ya wazazi walio wengi ni wastani na hawana hadhi ya juu ya kijamii—kwao ni vizuri tu kuwa na kazi. Je, inajumuisha magavana? Au maraisi wa mataifa? La, sivyo? Kwa zaidi ni watu kama mameneja wa biashara ndogo ama wakubwa wa muda mfupi. Hadhi zao za kijamii ni za kati, na hali zao za uchumi ni wastani. Sababu nyingine ni mazingira ya kuishi ya familia. Kwanza kabisa, hakuna wazazi ambao wangeweza kuwashawishi kwa wazi watoto wao kutembea njia ya uaguzi na kupiga ramli; hawa pia ni wachache. Wazazi wengi ni wa kawaida kiasi. Katika wakati huo ambapo Mungu huwachagua watu, Yeye huwawekea mazingira ya aina hii, ambayo ni ya manufaa sana kwa wokovu Wake kwa watu. Kwa juujuu, inaonekana kana kwamba Mungu hajamfanyia mwanadamu jambo lolote kuu; Yeye hufanya tu kila tendo bila kuficha, bila kujulikana, na kimya kimya. Lakini kwa hakika, kila afanyacho Mungu ni kuweka msingi wa wokovu wako, kuandaa njia iliyo mbele na hali zote muhimu za wokovu wako. Halafu, Mungu anawarudisha mbele Yake, kila mtu kwa wakati wake: Ni wakati huo ndipo unaposikia sauti ya Mungu; ni wakati huo ndipo unapokuja mbele Yake. Kufikia wakati hilo linafanyika, watu wengine wamekuwa wazazi tayari wenyewe, huku wengine bado ni watoto wa mtu tu. Kwa maneno mengine, watu wengine wameoa na kupata watoto huku wengine bado hawajaoa, bado hawajaanzisha familia zao. Lakini licha ya jinsi mambo yanavyoweza kuwa, wakati injili ya Mungu na maneno Yake yanapokufikia, hili ni jambo ambalo limeamuliwa kwa muda mrefu sasa Mungu. Mungu ameweka mazingira na kuamua kwamba mtu fulani atakuhubiria injili katika muktadha fulani, ili wewe upate kusikia sauti ya Mungu na kumkubali katika mazingira fulani. Haya yote yameamuliwa kabla na Mungu. Mungu tayari amekutayarishia hali zote muhimu. Kwa njia hii, watu huja mbele Yake na kurudi katika nyumba ya Mungu bila kujua. Pia bila kujua, wanamfuata Mungu katika kila hatua ya kazi Yake, wakiingia katika kila hatua ya njia za kazi ya Mungu ambazo Amewaandalia. Ni njia za aina gani ambazo Mungu hutumia wakati Anapofanya mambo kwa ajili ya mwanadamu wakati huu? Kwanza, angalau kabisa ni utunzaji na ulinzi ambao mwanadamu hufurahia. Kando na hayo, Mungu huweka watu, matukio, na vitu mbalimbali ili mwanadamu aweze kuona kuwepo Kwake na matendo Yake miongoni mwao. Kwa mfano, kuna watu wengine wanaomwamini Mungu kwa sababu mtu katika familia yao ni mgonjwa. Wakati wengine wanawahubiria injili, wanaanza kumwamini Mungu, na imani hii kwa Mungu imekuja kwa sababu ya hali hii. Kwa hivyo ni nani aliyepangilia hali hii? (Mungu.) Kwa njia ya maradhi haya, kuna familia zingine ambamo wote ni waumini, vijana na wazee, ilhali kuna familia zingine ambamo imani ni ya kibinafsi. Inavyoonekana, mtu katika familia yako ana maradhi, lakini kwa hakika ni hali uliyopewa ili uje mbele ya Mungu—huu ni wema wa Mungu. Kwa sababu maisha ya kifamilia kwa baadhi ya watu ni magumu na hawawezi kupata amani yoyote, fursa ya bahati inakuja ambapo mtu anapitisha injili na kusema, “Mwamini Bwana Yesu na utakuwa na amani.” Bila kujua, basi wanakuja kumwamini Mungu katika hali asili, kwa hivyo hii si aina ya hali? Na je, familia yake kuwa na amani si neema aliyopewa na Mungu? Kisha kuna wengine wanaokuja kumwamini Mungu kwa sababu zingine. Kuna sababu tofauti na njia tofauti za imani, lakini licha ya sababu inayokuleta kumwamini Yeye, yote hakika yamepangwa na kuongozwa na Mungu. Kwanza, Mungu hutumia njia kadhaa ili kukuchagua na kukuleta katika familia Yake. Hii ndiyo neema Mungu anayompa kila mwanadamu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 161)
Kuelewa Utakatifu wa Mungu Kupitia Kile Anachomfanyia Mwanadamu
Sasa kwa kazi ya Mungu katika siku za mwisho, Hampi tena mwanadamu neema na baraka tu kama Alivyofanya awali, wala halazimishi watu kwenda mbele. Wakati wa hatua hii ya kazi, ni nini mwanadamu ameona kutoka kwa vipengele hivi vyote vya kazi ya Mungu ambavyo wamepitia? Wameona upendo wa Mungu, na hukumu na kuadibu kwa Mungu. Kwa wakati huu, Mungu zaidi ya hayo, anamtegemeza, tia nuru, na kumwongoza mwanadamu, ili aje kujua nia Zake polepole, kujua maneno Anayozungumza na ukweli Anaompa mwanadamu. Wakati mwanadamu ni mnyonge, wakati amekata tamaa, wakati hana popote pa kugeukia, Mungu atatumia maneno Yake kufariji, kushauri na kuwatia moyo, ili mwanadamu wa kimo kidogo aweze kupata nguvu polepole, kuinuka katika hali nzuri na kuwa radhi kushirikiana na Mungu. Lakini wakati wanadamu hawamtii Mungu ama wanampinga Yeye, ama wanapofichua upotovu wao, Mungu hataonyesha huruma kuwarudi na kuwafundisha nidhamu. Kwa ujinga, kutojua, unyonge, na uchanga wa mwanadamu, hata hivyo, Mungu ataonyesha uvumilivu na ustahimilivu. Kwa njia hii, kupitia kazi yote ambayo Mungu anamfanyia mwanadamu, mwanadamu anapevuka, anakua na anakuja kujua nia za Mungu polepole, kujua baadhi ya ukweli, kujua ni nini mambo mema na ni nini mambo hasi, kujua uovu ni nini na kujua giza ni nini. Mungu hamrudi na kumfundisha nidhamu mwanadamu siku zote wala Haonyeshi uvumilivu na ustahimilivu siku zote. Badala yake anampa kila mtu kwa njia tofauti, katika hatua zao tofauti na kulingana na kimo na ubora wa tabia zao tofauti. Anamfanyia mwanadamu mambo mengi na kwa gharama kubwa; mwanadamu hafahamu lolote kuhusu gharama hii ama mambo haya ambayo Mungu anafanya, ilhali yote ambayo Anayafanya kwa kweli yanatekelezwa kwa kila mtu. Upendo wa Mungu ni wa kweli: Kupitia neema ya Mungu mwanadamu anaepuka janga moja baada ya jingine, ilhali kwa unyonge wa mwanadamu, Mungu anaonyesha ustahimilivu wake muda baada ya muda. Hukumu na kuadibu kwa Mungu huruhusu watu kuja kujua polepole upotovu wa wanadamu na kiini chao cha kishetani. Kile ambacho Mungu hutoa, nuru Yake kwa mwanadamu na uongozi Wake yote yanawaruhusu wanadamu kujua zaidi na zaidi kiini cha ukweli, na kujua zaidi kile ambacho watu wanahitaji, njia wanayopaswa kuchukua, wanapaswa kuishi kwa ajili ya nini, thamani na maana ya maisha yao, na jinsi ya kutembea njia iliyo mbele. Haya mambo yote ambayo Mungu anafanya hayatengwi na lengo Lake la awali. Ni nini, basi lengo hili? Mbona Mungu anatumia njia hizi kufanya kazi Yake kwa mwanadamu? Anataka kutimiza matokeo gani? Kwa maneno mengine, ni nini ambacho anataka kuona kwa mwanadamu na kupata kutoka kwake? Kile ambacho Mungu anataka kuona ni kwamba moyo wa mwanadamu unaweza kufufuliwa. Njia hizi ambazo anatumia kufanya kazi kwa mwanadamu ni za kuamsha bila kikomo moyo wa mwanadamu, kuamsha roho ya mwanadamu, kumfahamisha mwanadamu alikotoka, ni nani anayemwongoza, kumsaidia, kumkimu, na ni nani ambaye amemruhusu mwanadamu kuishi hadi sasa; ni ili kumruhusu mwanadamu kujua ni nani Muumbaji, ni nani wanapaswa kumwabudu, ni njia gani wanapaswa kutembelea, na mwanadamu anapaswa kuja mbele ya Mungu kwa njia gani; yanatumika kufufua moyo wa mwanadamu polepole, ili mwanadamu ajue moyo wa Mungu, aelewe moyo wa Mungu, na aelewe utunzaji mkuu na mawazo nyuma ya kazi Yake ya kumwokoa mwanadamu. Wakati moyo wa mwanadamu umefufuliwa, hataki tena kuishi maisha ya uasherati, tabia potovu, lakini badala yake anatamani kufuata ukweli ili kumridhisha Mungu. Wakati moyo wa mwanadamu umeamshwa, anaweza basi kujinusuru kutoka kwa Shetani, kutoathiriwa tena na Shetani, kutodhibitiwa na kudanganywa na yeye. Badala yake, mwanadamu anaweza kushiriki kwa bidii katika kazi ya Mungu na maneno Yake ili kuridhisha moyo wa Mungu, na hivyo kupata uchaji wa Mungu na kuepuka uovu. Hili ndilo lengo la awali la kazi ya Mungu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 162)
Kuelewa Utakatifu wa Mungu Kupitia Kile Anachomfanyia Mwanadamu
Katika kuzungumza kuhusu uovu wa Shetani hivi sasa kulimfanya kila mtu kuhisi kana kwamba watu huishi kwa huzuni sana na kwamba maisha ya mwanadamu yamejaa bahati mbaya. Lakini mnahisi vipi sasa kwani Nimezungumza kuhusu utakatifu wa Mungu na kazi ambayo anafanya kwa mwanadamu? (Furaha sana.) Tunaweza kuona sasa kwamba kila kitu Mungu anafanya, kila kitu ambacho anapanga kwa uangalifu kwa mwanadamu ni sahihi kabisa. Kila kitu anachofanya Mungu ni bila kasoro, kumaanisha ni bila dosari, hakihitaji yeyote kukosoa, kutoa mawaidha ama kufanya mabadiliko yoyote. Kila kitu ambacho Mungu anafanya kwa kila mtu hakina shaka; Anaongoza kila mtu kwa mkono, Anakuchunga kwa kila wakati unaopita na Hajawahi kuondoka upande wako. Watu wanapokua katika mazingira haya na kukua na usuli wa aina hii, tunaweza kusema kwamba watu kwa kweli wanakua katika kiganja cha mkono wa Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo sasa bado mnahisi hisia za kupotea? Je, kuna yeyote anayehisi kuvunjika moyo bado? Kuna yeyote anayehisi kwamba Mungu amewaacha wanadamu? (La.) Kwa hivyo ni nini hasa Mungu amefanya? (Anawahifadhi wanadamu.) Wazo na utunzaji mkuu nyuma ya kila anachofanya Mungu hakina shaka. Hata zaidi, wakati Mungu anapofanya kazi Yake, hajawahi kuweka sharti ama mahitaji yoyote kwa yeyote kati yenu kujua gharama anayokulipia, ili kukufanya uhisi kumshukuru sana Yeye. Je, Mungu amewahi kutaka hili kutoka kwako? (La.) Katika kipindi kirefu cha maisha ya mwanadamu, kimsingi kila mtu amekutana na hali nyingi hatari na kupitia majaribu mengi. Hii ni kwa sababu Shetani yupo kando yako, macho yake yakikutazama kila wakati. Anapenda janga linapokupata, wakati maafa yanakupata, wakati hakuna chochote kinaenda sawa kwako, na anapendelea unaponaswa na wavu wa Shetani. Kuhusu Mungu, anakulinda kila wakati, kukuweka mbali na balaa moja baada ya jingine na kukuepusha na janga moja baada ya jingine. Hii ndiyo maana Nasema kwamba kila kitu ambacho mwanadamu anacho—amani na furaha, baraka na usalama wa kibinafsi—yote hakika yanadhibitiwa na Mungu, na Anaongoza na kuamua hatima ya kila mtu. Lakini, je, Mungu ana dhana ya kujiinua kwa cheo chake, kama wanavyosema watu wengine? Je, Mungu anakutangazia, “Mimi ndiye mkuu kuliko wote, ni Mimi ninayechukua jukumu juu yenu, ni lazima wote mniombe Mimi rehema, na msipotii mtaadhibiwa kwa kifo.” Je, Mungu amewahi kutishia wanadamu kwa njia hii? (La.) Je, amewahi kusema “Wanadamu wamepotoka, kwa hivyo haijalishi ninavyowatendea, na wanaweza kutendewa kwa njia yoyote ile; sihitaji kuwafanyia mipango mizuri.” Je, Mungu anafikiria kwa njia hii? Mungu ametenda kwa njia hii? (La.) Kinyume na haya, utendeaji wa Mungu kwa kila mtu ni wa dhati na wa uwajibikaji. Anakutendea kwa uwajibikaji hata zaidi kuliko unavyojichukulia. Je, si hivyo? Mungu haongei bure, wala hasimami juu akijifanya kuwa muhimu wala hadanganyi watu. Badala yake, Anafanya vitu ambavyo Yeye Mwenyewe anapaswa kufanya kwa uaminifu na kwa ukimya. Mambo haya yanaleta baraka, amani na furaha kwa mwanadamu. Yanamleta mwanadamu kwa amani na kwa furaha katika macho ya Mungu na ndani ya familia Yake; kisha wanaishi mbele ya Mungu na kukubali wokovu wa Mungu kwa fikira na mawazo ya kawaida. Kwa hivyo Mungu amewahi kuwa mdanganyifu kwa mwanadamu katika kazi Yake? Je, Amewahi kufanya onyesho la ukarimu wa uwongo, Akitumia mambo machache ya kupendeza ili kushughulika na mwanadamu kwa njia ya kipuuzi, kisha kumpuuza mwanadamu? (La.) Je, Mungu ashawahi kusema kitu kimoja na kisha kufanya kingine? Je, Mungu ameshawahi kutoa ahadi tupu na kujigamba, Akikuambia kwamba Anaweza kukufanyia hili ama kukusaidia kufanya lile, na kisha kutoweka? (La.) Hakuna udanganyifu ndani ya Mungu, hakuna uongo. Mungu ni mwaminifu na kila kitu Anachofanya ni halisi. Ni Yeye pekee ambaye watu wanaweza kumtegemea na Mungu ambaye watu wanaweza kuyakabidhi maisha yao na yote waliyo nayo Kwake. Kwa vile hakuna udanganyifu ndani ya Mungu, tunaweza kusema kwamba Mungu ndiye wa kweli zaidi? (Ndiyo.) Bila shaka tunaweza, siyo? Ingawa, tukizungumza kuhusu neno hili sasa, linapotumiwa kwa Mungu ni dhaifu sana, ni la kibinadamu sana, hakuna tunachoweza kufanya kulihusu kwani hii ndiyo mipaka ya lugha ya mwanadamu. Si sahihi sana hapa kumwita Mungu wa kweli, lakini tutatumia neno hili kwa sasa. Mungu ni mwaminifu na mkweli. Kwa hivyo tunamaanisha nini kwa kuongea kuhusu vipengele hivi? Je, tunamaanisha tofauti kati ya Mungu na mwanadamu na tofauti kati ya Mungu na Shetani? Tunaweza kusema hivi. Hii ni kwa sababu mwanadamu hawezi kuona chembe ya tabia potovu ya Shetani kwa Mungu. Je, Niko sahihi kusema hivi? Ninaweza kupata Amina kwa sababu ya hili? (Amina!) Hatuoni uovu wowote wa Shetani ukifichuliwa kwa Mungu. Yote ambayo Mungu hufanya na kufichua ni muhimu sana na ya msaada sana kwa mwanadamu, yanafanywa kumkimu mwanadamu kabisa, yamejaa uhai na yanampa mwanadamu njia ya kufuata na mwelekeo wa kuchukua. Mungu hajapotoka, na zaidi ya hayo, tukitangalia sasa kila kitu Anachofanya Mungu, tunaweza kusema kwamba Mungu ni mtakatifu? Kwa kuwa Mungu hana tabia yoyote potovu ya mwanadamu, wala chochote kifananacho sawa na kiini cha kishetani cha binadamu waliopotoka, kutoka katika mtazamo huu tunaweza kusema kikamilifu kwamba Mungu ni mtakatifu. Mungu haonyeshi upotovu wowote, na wakati huo huo Mungu anapofanya kazi, Mungu hufichua kiini Chake Mwenyewe, ambacho kinathibitisha kikamilifu kwamba Mungu Mwenyewe ni mtakatifu. Je, mnaona hili? Sasa, ili kujua kiini kitakatifu cha Mungu, kwa wakati huu wacha tuangalie vipengele hivi viwili: 1) Hakuna tabia potovu ndani ya Mungu; 2) kiini cha kazi ya Mungu kwa mwanadamu kinamruhusu mwanadamu kuona kiini cha Mungu mwenyewe na kiini hiki ni chanya kabisa. Kwa kuwa vitu ambavyo kila namna ya kazi ya Mungu inamletea mwanadamu ni vitu vizuri. Kwanza, Mungu anamhitaji mwanadamu kuwa mwaminifu—hili si zuri? Mungu anampa mwanadamu maarifa—hili si zuri? Mungu anamfanya mwanadamu aweze kutambua kati ya mema na maovu—hili si zuri? Anamruhusu mwanadamu kuelewa maana na thamani ya maisha ya binadamu—hili si zuri? Anamruhusu mwanadamu kuona ndani ya kiini cha watu, matukio na mambo kulingana na ukweli—si hili ni jambo zuri? Ndiyo ni zuri. Na matokeo ya haya yote ni kwamba mwanadamu hadanganywi tena na Shetani, haendelei kudhuriwa na Shetani ama kudhibitiwa na yeye. Kwa maneno mengine, yanawaruhusu watu kujiweka huru kabisa kutoka kwa upotovu wa Shetani, na hivyo kutembea polepole njia ya kumcha Mungu na kuepuka maovu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 163)
Kuna Njia Sita za Msingi Ambazo Shetani Hutumia Kumpotosha Mwanadamu.
Ya kwanza ni kudhibiti na kulazimisha. Yaani, Shetani atafanya vyovyote vile kudhibiti moyo wako. “Kulazimisha” kunamaanisha nini? Kunamaanisha kutumia mbinu za kutishia na kulazimisha kukufanya umtii, kukufanya ufikirie matokeo usipomtii. Unaogopa na huthubutu kumpinga, kwa hivyo basi unamtii.
Ya pili ni kudanganya na kulaghai. “Kudanganya na kulaghai” yanahusisha nini? Shetani hutunga baadhi ya hadithi na uongo, kukulaghai wewe kuziamini. Hakwambii kamwe kwamba mwanadamu aliumbwa na Mungu, wala hasemi pia moja kwa moja kwamba hukuumbwa na Mungu. Hatumii jina “Mungu” kabisa, lakini badala yake hutumia kitu kingine mbadala, akitumia kitu hiki kukudanganya ili kimsingi usiwe na wazo la kuwepo kwa Mungu. Huu ulaghai bila shaka unahusisha vipengele vingi, sio tu hiki kimoja.
Ya tatu ni kufunza kwa nguvu. Watu wanafunzwa nini kwa nguvu? Je, kufunzwa kwa nguvu kunafanywa kwa hiari ya mwanadamu mwenyewe? Je, kunafanywa na idhini ya mwanadamu? Bila shaka sivyo. Hata usipokubali, hakuna unachoweza kufanya kuhusu hilo. Katika kutokujua kwako, Shetani anakutia mafundisho, akitia fikira zake ndani mwako, kanuni zake za maisha na kiini chake.
Ya nne ni vitisho na vishawishi. Yaani, Shetani hutumia hila mbalimbali kukusababisha umkubali, umfuate na ufanye kazi katika Huduma yake. Atafanya chochote kufikia malengo yake. Wakati mwingine yeye hukupa fadhili kidogo, wakati wote akikushawishi utende dhambi. Usipomfuata, atakufanya uteseke na kukuadhibu, na hutumia njia mbalimbali kukushambulia na kukulia njama.
Ya tano ni uongo na kutia ganzi. “Uongo na kutia ganzi” ni wakati ambapo Shetani hutia ndani ya watu maneno na mawazo yanayolingana na dhana zao na yanayoonekana ya kuaminika, kufanya ionekane kwamba anajali hali za kimwili za watu, kuhusu maisha yao na siku zao za baadaye, wakati kwa kweli lengo lake la kweli ni kukudanganya tu. Kisha anakutia ganzi ili usijue kile kilicho sahihi na kile kilicho makosa, ili udanganywe bila kujua na hivyo kuja chini ya udhibiti wake.
Ya sita ni maangamizi ya mwili na akili. Ni sehemu gani ya mwanadamu ambayo Shetani huharibu? Shetani huharibu akili yako, kukufanya kutokuwa na nguvu za kupinga, kumaanisha kuwa, kidogo kidogo, moyo wako unageuka kwa Shetani licha ya wewe mwenyewe. Huingiza mambo haya ndani yako kila siku, na kutumia mawazo na utamaduni huu kukushawishi na kuwakazia mawazo kila siku, akivunja utashi wako kidogo kidogo, ili kwamba hutamani tena kuwa mtu mwema, ili kwamba hutaki tena kutetea kile unachoita “haki.” Bila kujua, huna tena utashi wa kuogelea kinyume na mkondo wa maji, lakini badala yake kuelea na mkondo. “Maangamizi” yanamaanisha Shetani kuwatesa watu sana hadi wanakuwa vivuli vya wao wenyewe, sio wanadamu tena. Hapa ndipo Shetani huchukua fursa ya kuwameza.
Kila mojawapo ya ujanja hizi ambao Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu humfanya mwanadamu akose nguvu ya kupinga; yoyote kati ya ujanja huu inaweza kuwa ya kuangamiza kwa mwanadamu. Kwa maneno mengine, chochote anachofanya Shetani na kila ujanja wowote anatumia inaweza kukufanya upotoke, inaweza kukuleta chini ya udhibiti wa Shetani na inaweza kukuzamisha katika bwawa la uovu na dhambi. Huu ndio ujanja ambao Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 164)
Sasa uelewa wenu wa utambuzi kuhusu kiini cha Mungu bado unahitaji kipindi cha muda mrefu kujifunza, kuthibitisha, kuhisi na kuipitia, hadi siku moja mtajua utakatifu wa Mungu kutoka kwenye kina cha mioyo yenu kuwa kiini cha Mungu ambacho hakina dosari, upendo wa Mungu usio na ubinafsi, kwamba haya yote Mungu humpa mwanadamu hayana ubinafsi, na mtakuja kujua ya kwamba utakatifu wa Mungu hauna dosari wala haushutumiki. Hivi viini vya Mungu si maneno tu ambayo Yeye hutumia kuonyesha utambulisho Wake, bali Mungu hutumia kiini Chake kwa kimya na kwa dhati kushughulika na kila mtu. Kwa maneno mengine, kiini cha Mungu si tupu, wala si cha nadharia au mafundisho ya dini na hakika si aina ya maarifa. Si aina ya elimu kwa mwanadamu, lakini badala yake ni ufunuo wa kweli wa matendo ya Mungu mwenyewe na ni kiini ambacho kimefichuliwa cha kile Mungu anacho na alicho. Binadamu anapaswa kujua kiini hiki na kukifahamu, kwa kuwa kila kitu Mungu hufanya na kila neno Yeye husema ni la thamani kubwa na umuhimu mkubwa kwa kila mtu. Unapokuja kuelewa utakatifu wa Mungu, basi unaweza kweli kumwamini Mungu; unapokuja kuelewa utakatifu wa Mungu, basi unaweza kweli kutambua maana halisi ya maneno haya “Mungu Mwenyewe, wa Kipekee.” Hutafikiria tena kwamba unaweza kuchagua kutembea njia zingine, na hutakuwa tena radhi kusaliti kila kitu ambacho Mungu amekupangia. Kwa sababu kiini cha Mungu ni takatifu, hiyo ina maana kwamba kupitia tu Mungu ndipo unaweza kutembea njia yenye kung’aa na sahihi katika maisha; ni kupitia tu Mungu unaweza kujua maana ya maisha, ni tu kupitia Mungu unaweza kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu halisi, kumiliki ukweli, kujua ukweli, na ni kupitia tu Mungu unaweza kupata maisha kutoka katika ukweli. Ni Mungu Mwenyewe tu anaweza kukusaidia kuepuka maovu na kukuokoa kutoka kwenye madhara na udhibiti wa Shetani. Kando na Mungu, hakuna mtu au kitu kinaweza kukuokoa kutoka kwa bahari ya mateso, ili usiteseke tena: Hili linaamuliwa na kiini cha Mungu. Ni Mungu Mwenyewe tu hukuokoa bila ubinafsi wowote, ni Mungu pekee anayehusika na maisha yako ya baadaye, na hatima yako na maisha yako, na Yeye anapanga mambo yote kwa ajili yako. Hili ni jambo ambalo hakuna kitu ambacho kimeumbwa au hakijaumbwa kinaweza kutimiza. Kwa sababu hakuna kitu ambacho kimeumbwa au hakijaumbwa kina kiini cha Mungu kama hiki, hakuna mtu au kitu chenye uwezo wa kukuokoa au kukuongoza wewe. Huu ndio umuhimu wa kiini cha Mungu kwa mwanadamu. Labda mnahisi kuwa maneno haya Niliyoyasema yanaweza kweli kusaidia kimsingi katika kanuni. Lakini kama wewe unafuatilia ukweli, kama wewe unapenda ukweli, katika uzoefu wako wa baada ya hapa maneno haya hayataleta tu mabadiliko katika hatima yako, lakini zaidi ya hayo yatakuleta katika njia sahihi ya maisha. Je, unafahamu hili, siyo?
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 165)
Ningependa kuwazungumzia kuhusu kitu mlichofanya kilichonishangaza mwanzoni mwa mkusanyiko wetu leo. Wengine wenu pengine mlikuwa na hisia za shukrani hivi karibuni, ama kuhisi shukrani, na hivyo mlitaka kuonyesha kimwili kile mlichokuwa nacho akilini mwenu. Hili si la kushutumiwa, na si sahihi wala makosa. Lakini ningependa muelewe kitu. Ni nini hiki? Kwanza Ningetaka kuwauliza kuhusu mlichokifanya hivi sasa. Je, kulikuwa ni kusujudu ama kupiga magoti kuabudu? Kuna yeyote anayeweza kuniambia? (Tunaamini ilikuwa kusujudu.) Mnaamini kulikuwa kusujudu, kwa hivyo ni nini maana ya kusujudu? (Kuabudu.) Kwa hivyo ni nini kupiga magoti kuabudu basi? Sijashiriki hili na ninyi awali, lakini leo nahisi ni muhimu kushiriki mada hii na ninyi. Je, mnasujudu katika mikusanyiko yenu ya kawaida? (La.) Je, mnasujudu mnaposema sala zenu? (Ndiyo.) Je, mnasujudu kila wakati mnaposema sala zenu, hali zinaporuhusu? (Ndiyo.) Hivyo ni vizuri sana. Lakini kile Ningependa nyinyi muelewe leo ni kwamba Mungu hukubali tu kupiga magoti kwa aina mbili za watu. Hatuhitaji kutafuta maoni katika Biblia ama tabia za watu wa kiroho, na Nitawaambia kitu kweli hapa na sasa. Kwanza, kusujudu na kupiga magoti kuabudu si kitu kimoja. Kwa nini Mungu anakubali kupiga magoti kwa wale wanaosujudu wenyewe? Ni kwa sababu Mungu humwita mtu Kwake na humwita mtu huyu kukubali agizo la Mungu, kwa hivyo anasujudu mwenyewe mbele ya Mungu. Huyu ni mtu wa aina ya kwanza. Aina ya pili ni kupiga magoti kuabudu kwa mtu anayemcha Mungu na kuepukana na maovu. Kuna watu hawa wa aina mbili tu. Kwa hivyo mko katika aina ipi? Je, mnaweza kusema? Huu ni ukweli kabisa, ingawa unaweza kuumiza hisia zenu kidogo. Hakuna kitu cha kusema kuhusu kupiga magoti kwa watu wakati wa sala—hii ni sahihi na ndivyo inavyopaswa kuwa, kwa sababu wakati watu wanasali wakati mwingi ni kuombea kitu, kufungua mioyo yao kwa Mungu na kukutana Naye uso kwa uso. Ni mawasiliano na mazungumzo, moyo kwa moyo na Mungu. Mkiifanya kama urasmi tu, basi haipaswi kufanywa hivyo. Simaanishi kuwashutumu kwa yale ambayo mmefanya leo. Mnajua kwamba nataka tu kuweka wazi kwenu ili muelewe kanuni hii, mnajua? (Tunajua.) Ili msiendelee kufanya hili. Je, watu basi wana fursa yoyote ya kusujudu na kupiga magoti mbele ya uso wa Mungu? Daima kutakuwa na fursa. Hivi karibuni au baadaye siku itakuja, lakini wakati sio sasa. Je, mnaona? Je, hili linawafanya kuhisi vibaya? (La.) Hivyo ni vizuri. Labda maneno haya yatawatia moyo ama kuwashawishi ili muweze kujua katika mioyo yenu taabu ya sasa kati ya Mungu na mwanadamu na ni aina gani ya uhusiano uliopo sasa kati yao. Ingawa tumeongea na kuzungumza sana hivi karibuni, uelewa wa mwanadamu kuhusu Mungu bado uko mbali na kutosha. Mwanadamu bado ana umbali mrefu wa kwenda katika njia hii ya kutafuta kumwelewa Mungu. Si nia yangu kuwafanya mfanye hivi kwa dharura, ama kuwaharakisha kuonyesha matamanio na hisia za aina hizi. Yale mliyofanya leo yanaweza kufichua na kuonyesha hisia zenu za kweli, na Niliyafahamu. Kwa hivyo wakati mlipokuwa mkiyafanya, nilitaka tu kusimama na kuwatakia mema, kwa sababu Nataka nyote muwe wazima. Kwa hivyo katika maneno na vitendo vyangu vyote Ninafanya yote ninayoweza kuwasaidia, kuwaongoza, ili muwe na uelewa sahihi na mtazamo sahihi wa mambo yote. Mnaweza kuelewa haya, sivyo? (Ndiyo.) Hivyo ni vizuri sana. Ingawa watu wana baadhi ya uelewa wa tabia mbalimbali za Mungu, kipengele cha kile anacho Mungu na alicho na kazi Mungu anafanya, wingi wa uelewa huu hauendi mbali na kusoma maneno kwenye ukurasa, ama kuyaelewa katika kanuni, ama tu kuyafikiria. Yale wanayoyakosa sana watu ni uelewa na mtazamo wa kweli unaotoka kwa uzoefu halisi. Ingawa Mungu hutumia njia mbalimbali kuamsha mioyo ya wanadamu, bado kuna njia ndefu ya kutembea kabla mioyo ya wanadamu iamshwe kikamilifu. Sitaki kumwona yeyote akihisi kana kwamba Mungu amemwacha nje kwa baridi, kwamba Mungu amemwacha ama amempuuza. Ningetaka tu kuona kila mtu katika njia ya kufuatilia ukweli na kutafuta kumwelewa Mungu, akiendelea mbele kwa ujasiri na utashi usiosita, bila wasiwasi, bila kubeba mizigo. Haijalishi umefanya makosa gani, haijalishi umepotoka kiasi gani ama vile ulivyotenda dhambi, usiache haya yawe mizigo ama vikorokoro ziada vya kubeba katika ufuataji wako wa kumwelewa Mungu: Endelea kutembea mbele. Nyakati zote, Mungu hushikilia wokovu wa mwanadamu moyoni Mwake; hili halibadiliki kamwe. Hii ni sehemu ya thamani sana ya kiini cha Mungu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI