Kumjua Mungu (V)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 166)

Je, unaielewa hoja kuu kuhusu kuifahamu tabia ya haki ya Mungu? Kuna mengi yanayoweza kusemwa kutokana na uzoefu juu ya mada hii, lakini kwana kuna hoja chache ambazo lazima Niwaambie. Kuielewa tabia ya haki ya Mungu, kwanza mtu anapaswa kuelewa hisia za Mungu: kile Anachokichukia, kile Anachokichukia kabisa, kile Anachokipenda, ni mvumilivu na mwenye huruma kwa nani, na ni aina gani ya mtu anayepokea rehema hiyo. Hii ni hoja ya msingi kufahamu. Aidha, mtu anapaswa kuelewa kwamba haijalishi Mungu ni mwenye upendo kiasi gani, haijalishi ni Mwenye rehema na upendo kiasi gani kwa watu, Mungu hamvumilii mtu yeyote anayekosea hali na nafasi Yake, wala Hamvumilii mtu yeyote anayekosea heshima Yake. Ingawa Mungu anawapenda watu, Hawadekezi. Anawapatia watu upendo Wake, rehema Yake, na uvumilivu Wake, lakini hajawahi kuwakuwadia; Ana kanuni Zake na mipaka Yake. Bila kujali ni kwa kiwango gani umeuhisi upendo wa Mungu ndani yako, bila kujali upendo huo ni wa kina kiasi gani, hupaswi kamwe kumtendea Mungu kama ambavyo ungemtendea mtu mwingine. Ingawa ni kweli kwamba Mungu anawachukulia watu kama wako karibu Naye, ikiwa mtu anamwangalia Mungu kama mtu mwingine, kana kwamba ni kiumbe mwingine wa uumbaji, kama rafiki au kama kitu cha kuabudu, Mungu atawaficha uso Wake na kuwatelekeza. Hii ndiyo tabia Yake, na watu hawapaswi kulichukulia jambo hili kwa mzaha. Hivyo, mara nyingi sisi huona maneno kama haya yakinenwa na Mungu kuhusu tabia Yake: Haijalishi umesafiri njia nyingi kiasi gani, umefanya kazi kubwa kiasi gani au umevumilia kiasi gani, mara tu unapoikosea tabia ya Mungu, Atamlipa kila mmoja wenu kulingana na kile ulichokifanya. Hii ina maana kwamba Mungu huwaona watu kama wapo karibu na Yeye, lakini watu hawapaswi kumchukulia Mungu kama rafiki au ndugu. Usimchukulie Mungu kama rafiki yako. Haijalishi ni upendo kiasi gani umepokea kutoka Kwake, haijalishi Amekuvumilia kwa kiasi gani, hupaswi kabisa kumchukulia Mungu kama rafiki tu. Hii ndiyo tabia ya haki ya Mungu. Unaelewa, sio? Je, kuna haja ya Mimi kusema zaidi kuhusu hili? Je, una uelewa wowote wa awali kuhusiana na suala hili? Kwa ujumla, hili ndilo kosa rahisi sana ambalo watu wanafanya bila kujali kama wanaelewa mafundisho, au kama hawajafikiria chochote kuyahusu hapo awali. Watu wanapomkosea Mungu, inaweza isiwe kwa tukio moja, au kitu kimoja walichokisema, bali ni kwa sababu ya mtazamo walionao na hali waliyomo. Hili ni jambo la kutisha sana. Baadhi ya watu wanaamini kwamba wana uelewa juu ya Mungu, kwamba wanamjua, hata wanaweza kufanya baadhi ya mambo ambayo yanaweza kumpendeza Mungu. Wanaanza kuhisi wako sawa na Mungu na kwamba kwa werevu wamekuwa na urafiki na Mungu. Aina hizi za hisia sio sahihi kabisa. Ikiwa huna uelewa wa kina juu ya hili, ikiwa huelewi vizuri hili, basi ni rahisi sana kumkosea Mungu na kukosea tabia Yake ya haki. Unalielewa hili sasa, siyo? Je, tabia ya haki ya Mungu sio ya kipekee? Je inaweza kamwe kuwa sawa na tabia ama maadili ya mwanadamu? Haiwezi kamwe. Hivyo, hupaswi kusahau kwamba haijalishi ni kwa namna gani Mungu anawachukulia watu, haijalishi ni namna gani Anafikiri juu ya watu, nafasi, tabia na hadhi ya Mungu kamwe havibadiliki. Kwa binadamu, Mungu siku zote ni Bwana wa vitu vyote na Muumbaji.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 167)

Hadithi ya 1. Mbegu, Ardhi, Mti, Mwanga wa Jua, Chiriku, na Mwanadamu

Mbegu ndogo ilidondoka ardhini. Baada ya mvua kubwa kunyesha, mbegu ilianza kuchipuka na mizizi yake ikamea taratibu kwenda ardhini. Chipuko lilirefuka kadri muda ulivyozidi kwenda, yakivumilia upepo mkali na mvua kubwa, yakiangalia mabadiliko ya misimu kadri mwezi unavyopevuka na kufifia. Wakati wa kiangazi ardhi ilileta zawadi ya maji ili kwamba chipuko liweze kuhimili joto kali. Na kwa sababu ya ardhi, chipuko halikuhisi joto na hivyo lilihimili joto la kiangazi. Msimu wa baridi ulipokuja, ardhi ililifunika chipuko katika kumbatio la vuguvugu lake na kushikamana kwa nguvu. Na kwa sababu ya vuguvugu la ardhi, chipuko lilihimili baridi kali, likivuka bila kudhurika katika dhoruba ya msimu wa baridi na barafu za msimu. Likivikwa na ardhi, chipuko lilikua kwa ujasiri na lilikuwa na furaha. Lilirefuka na kujivunia malezi yasiyokuwa ya ubinafsi ambayo ardhi iliyatoa. Chipuko lilikua kwa furaha. Liliimba wakati mvua ilipokuwa ikinyesha na kucheza na kuyumba kadri upepo ulivyokuwa ukivuma. Na hivyo, chipuko na ardhi hutegemeana…

Miaka ilipita, na chipuko sasa lilikuwa mnara wa mti. Lilikuza matawi manene juu yake yaliyokuwa na majani yasiyohesabika na kusimama imara juu ya nchi. Mizizi ya mti ilimea aridhini kama ilivyomea hapo kabla, lakini sasa ilizama kabisa ardhini chini kabisa. Kile ambacho mwanzo kilililinda chipuko sasa kilikuwa msingi wa mti mkubwa sana.

Mwale wa mwanga wa jua ulimulika mti na shina likatikisika. Mti ulitoa nje matawi yake kwa upana na kufaidi sana kutoka kwenye mwanga. Ardhi chini ilipumua kwa wizani pamoja na mti, na ardhi ilihisi kufanywa upya. Baada ya hapo tu, upepo mwanana ulivuma ukitokea katika matawi, na mti ulifurahia sana, ukiwa na nguvu. Na hivyo, mti na mwanga wa jua vinategemeana …

Watu walikaa katika kivuli tulivu cha mti na wakafurahia hewa changamfu inayonukia vizuri. Hewa ilitakasa mioyo na mapafu yao, na ilitakasa damu ndani yao. Watu hawakuhisi tena kuchoka au kuelemewa. Na hivyo, watu na miti wanategemeana …

Kundi la chiriku waliimba kwa uchangamfu walivyokuwa wakitua kwenye matawi ya mti. Pengine walikuwa wanamwepuka adui fulani, au walikuwa wanazaliana na kuwalea watoto wao, au pengine walikuwa wanapata pumziko fupi. Na hivyo, ndege na mti wanategemeana …

Mizizi ya mti, ikiwa imesokotana na kusongamana, ilijikita chini kabisa ardhini. Shina lake liliifunika ardhi dhidi ya upepo na mvua na kuyatoa nje matawi yake makubwa na kuilinda ardhi chini yake, na mti ulifanya hivi kwa sababu ardhi ni mama yake. Yanatiana nguvu na kutegemeana, na kamwe hayataachana …

Mambo yote Niliyoyazungumzia ni mambo ambayo mmeshawahi kuyaona hapo awali, kama vile mbegu, mnajua kuhusiana na hili, sio? Mbegu kukua na kuwa mti unaweza usiwe mchakato unaouangalia katika maelezo ya kina, lakini unajua kwamba ni ukweli, sio? Unajua kuhusu ardhi na mwanga wa jua. Taswira ya chiriku wakitua mtini ni kitu ambacho watu wote wamekwishakiona, sio? Na watu kutuliza joto chini ya kivuli cha mti, wote mmekwishawahi kuona, sio? (Tumeona hilo.) Sasa, mnapata hisia gani mnapoona mifano yote hii katika taswira moja? (Upatanifu.) Je, mifano yote hii iliyopo katika taswira hii inatoka kwa Mungu? (Ndiyo.) Kwa kuwa inatoka kwa Mungu, Mungu anajua thamani na umuhimu wa mifano hii kadhaa inayokaa pamoja ardhini. Mungu alipoviumba vitu vyote, Alipofanya mpango na kuumba kila kitu, Alifanya hivyo kwa makusudi; na Alipoumba vitu hivyo, kila kimoja kilijazwa na uzima. Mazingira Aliyotengeneza kwa ajili ya kuwepo binadamu, ambayo yamejadiliwa katika hadithi tuliyoisikia. Imejadili hali ya kutegemeana baina ya mbegu na ardhi; ardhi inastawisha mbegu na mbegu inafungamana na ardhi. Uhusiano kati ya hivi vitu viwili uliamuliwa kabla na Mungu kuanzia mwanzoni kabisa. Mti, mwanga wa jua, chiriku, na mwanadamu katika taswira hii ni mifano ya mazingira hai ambayo Mungu aliyaumba kwa ajili ya mwanadamu. Kwanza, mti hauwezi kuiacha ardhi, wala hauwezi kuishi bila mwanga wa jua. Kwa hivyo, kusudi la Mungu la kuumba mti lilikuwa ni nini? Je, tunaweza kusema kuwa ilikuwa tu ni kwa ajili ya ardhi? Je, tunaweza kusema ilikuwa tu ni kwa ajili ya chiriku? Je, tunaweza kusema ilikuwa tu ni kwa ajili ya watu? (Hapana.) Kuna uhusianao gani kati yao? Uhusianao kati yao ni wa kutiana nguvu, kutegemeana ambapo haviwezi kutengana. Yaani, ardhi, mti, mwanga wa jua, chiriku, na watu wanategemeana kwa ajili ya kuishi na wanaleana. Mti unailinda ardhi wakati ardhi inaulea mti; mwanga wa jua unatoa huduma kwa mti, wakati mti unapata hewa nzuri kutoka katika mwanga wa jua unapunguza joto jingi la mwanga wa jua juu ya ardhi. Nani anayefaidika mwishoni? Mwanadamu ndiye anayefaidika, siyo? Na hii ndiyo kanuni juu ya kwa nini Mungu alifanya mazingira ya kuishi kwa ajili ya binadamu na ambaye ndiye lengo kuu kwa ajili yake. Ingawa hii ni taswira rahisi, tunaweza kuona hekima za Mungu na nia yake. Binadamu hawezi kuishi bila ardhi, au bila miti, au bila chiriku na mwanga wa jua, sio? Ingawa ilikuwa ni hadithi, kile inachoonyesha ni mfano mdogo wa uumbaji wa Mungu wa mbingu na dunia na vitu vyote na zawadi Yake ya mazingira ambamo binadamu wanaweza kuishi.

Mungu aliumba mbingu na nchi na vitu vyote kwa ajili ya mwanadamu na pia akafanya mazingira ya kuishi. Kwanza, hoja kuu tuliyoijadili katika hadithi ni mwingiliano wa mahusiano na hali ya kutegemeana ya vitu vyote. Chini ya kanuni hii, mazingira ya kuishi kwa ajili ya binadamu yamelindwa, yanaendelea kuishi na kudumu; kwa sababu ya uwepo wa mazingira haya hai, mwanadamu anaweza akastawi na kuzaliana. Tuliona mti, ardhi, mwanga wa jua, na chiriku, na watu katika tukio. Mungu alikuwepo pia? Watu wanaweza wakose kuiona, sio? Lakini mtu aliweza kuona sheria ya kuhimizana na kutegemeana kati ya vitu katika tukio; ni kupitia kanuni hizi ndipo watu wanaweza kuona kwamba Mungu yupo na kwamba ni Mtawala. Mungu anatumia kanuni hizi na sheria kulinda uhai na uwepo wa vitu vyote. Ni kwa njia hii ndipo Anavikimu vitu vyote na Anamkimu binadamu. Je, hadithi hii ina uhusiano wowote na dhamira tuliyoijadili? Kwa juujuu inaonekana kama hakuna uhusiano, lakini kwa uhalisia, kanuni ambazo Mungu anazifanya kama Muumbaji na utawala Wake juu ya vitu vyote zinahusiana kwa karibu sana na Yeye kuwa chanzo cha uhai kwa vitu vyote na zimeunganika bila kuachana. Umejifunza angalau kidogo, sio?

Mungu anaamuru sheria zinazoongoza uendeshaji wa vitu vyote; Anaamuru sheria zinazoongoza uwepo wa vitu vyote; Yeye hudhibiti vitu vyote, na huviweka kutiana nguvu na kutegemeana, ili visiangamie au kutoweka. Hivi tu ndivyo wanadamu wanaweza kuendela kuishi; ni hivyo tu ndivyo wanaweza kuishi chini ya mwongozo wa Mungu katika mazingira kama hayo. Mungu ndiye bwana wa sheria hizi za uendeshaji, na binadamu hawawezi kuingilia na hawawezi kuzibadilisha; ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anajua kanuni hizi na ni Yeye pekee ndiye anazisimamia. Ni lini miti itachipuka, ni lini mvua itanyesha, ni maji kiasi gani na virutubisho kiasi gani ardhi itaipatia mimea, ni katika msimu gani majani yatapukutika, ni katika msimu gani miti itazaa matunda,jua litaipa miti virutubisho vingapi; kile ambacho miti itatoa nje baada ya kulishwa na jua—vitu hivi vyote viliamuliwa kabla na Mungu alipoumba vitu vyote, kama sheria ambazo hakuna mtu anayeweza kuvunja. Vitu vilivyoumbwa na Mungu—ama ni hai au vinaonekana kwa watu si hai—vyote vipo mikononi mwa Mungu na chini ya utawala Wake. Hakuna mtu anayeweza kubadilisha au kuvunja kanuni hii. Hii ni kusema, Mungu alipoviumba vitu vyote Aliweka kanuni ya jinsi vinavyopaswa kuwa. Miti isingeweza kuzamisha mizizi, kuchipua na kukua bila ardhi. Ardhi isingekuwa na miti, ingekauka. Pia, mti ni makazi ya chiriku, ni sehemu ambapo wanapata kujikinga dhidi ya upepo. Je, ingekuwa sawa ikiwa miti ingekuwa bila mwanga wa jua? (Isingekuwa sawa.) Ikiwa miti ingekuwa na ardhi peke yake hiyo isingefanya kazi. Hii yote ni kwa ajili ya mwanadamu na kuendelea kuishi kwa mwanadamu. Mwanadamu anapokea hewa safi kutoka kwenye miti, na anaishi katika ardhi inayomlinda. Mwanadamu hawezi kuishi bila mwanga wa jua, mwanadamu hawezi kuishi bila viumbe hai mbalimbali. Ingawa uhusiano baina ya vitu hivi ni changamani, mnapaswa kukumbuka kwamba Mungu alitengeneza kanuni ambazo zinaongoza vitu vyote ili kwamba viweze kuimarishana, kutegemeana na kuwepo pamoja. Kwa maneno mengine, kila kitu alichokiumba kina thamani na umuhimu. Ikiwa Mungu aliumba kitu bila kuwa na umuhimu, Mungu angeacha kipotee. Hii ni njia mojawapo Aliyoitumia katika kuvikimu vitu vyote. “Kukimu” kuna maana gani katika hadithi hii? Je, Mungu kila siku anatoka na kwenda kumwagilia mti maji? Je, mti unahitaji msaada wa Mungu ili uweze kupumua? (Hapana.) “Kukimu” hapa ina maana ya usimamizi wa Mungu wa vitu vyote baada ya uumbaji; Alichokuwa akikihitaji kilikuwa ni sheria ili kufanya vitu kwenda vizuri. Mti ulikuwa wenyewe kwa kupandwa ardhini. Masharti ili uweze kukua yote yalitengenezwa na Mungu. Alitengeneza mwanga wa jua, maji, udongo, hewa, na mazingira, upepo, umande, barafu, na mvua, na misimu minne; haya ndiyo masharti ambayo mti huyahitaji ili uweze kukua, hivi ni vitu ambavyo Mungu aliviandaa. Kwa hiyo, Mungu ni chanzo cha mazingira haya hai? (Ndiyo.) Je, Mungu analazimika kwenda kila siku na kuhesabu kila jani kwa miti? Hakuna haja, sio? Mungu pia hahitaji kuusaidia mti ili uweze kupumua. Mungu pia hahitaji kuuamsha mwanga wa jua kila siku kwa kusema, “Ni muda wa kuiangazia miti sasa.” Hana haja ya kufanya hivyo. Mwanga wa jua humulika wenyewe wakati wake wa kumulika unapofika, kulingana na sheria; unaonekana na kumulika juu ya mti na mti unafyonza huo mwanga wakati unapohitaji, na wakati hauhitajiki, mti huo bado huishi ndani ya kanuni. Pengine hamwezi kuelezea jambo hili kwa uwazi, lakini ni ukweli ambao kila mtu anaweza kuona na kuukubali. Chote unachopaswa kufanya ni kutambua kwamba kanuni kwa ajili ya uwepo wa vitu vyote inatoka kwa Mungu na kujua kwamba Mungu ni mkuu juu ya ukuaji na kuishi kwa vitu vyote.

Je, istiari imetumika katika hadithi hii, kama watu wanavyoiita? Je, ni hadithi iliyopewa sifa za kibinadamu? (Hapana.) Kile Nilichokizungumza ni ukweli. Kila kitu ambacho ni hai, kila kitu ambacho kina uhai kipo chini ya utawala wa Mungu. Kilipewa uhai baada ya Mungu kukiumba; ni uhai uliotolewa kutoka kwa Mungu na unafuata sheria na njia Alizozitengeneza kwa ajili yake. Hii haihitaji kubadilishwa na mwanadamu, na haihitaji msaada kutoka kwa mwanadamu; hivi ndivyo Mungu anavyokimu vitu vyote. Unaelewa, sio? Je, unadhani ni lazima watu watambue hili? (Ndiyo.) Hivyo, hadithi hii ina uhusiano wowote na biolojia? Je, inahusiana kwa njia fulani nauwanja wa maarifa au tawi la kujifunza? Hatujadili biolojia hapa na hakika hatufanyi utafiti wa kibiolojia. Je, hoja kuu tunayoizungumzia hapa ni ipi? (Kwamba Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.) Mnaona nini miongoni mwa vitu vyote vya uumbaji? Mmeiona miti? Mmeiona ardhi? (Ndiyo.) Mmeuona mwanga wa jua, sio? Mmewaona ndege wakikaa mtini? (Ndiyo.) Je, mwanadamu anafurahia kuishi mazingira kama hayo? (Anafurahia.) Yaani, Mungu anatumia vitu vyote—vitu alivyoviumba—kudumisha makazi ya binadamu kwa ajili ya kuishi na kulinda makazi ya binadamu, na hivi ndivyo Anavyomkimu mwanadamu na anavyokimu vitu vyote.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 168)

Hadithi ya 2. Mlima Mkubwa, Kijito Kidogo, Upepo Mkali, na Wimbi Kubwa

Kulikuwa na kijito kidogo kilichotiririka kwa kuzungukazunguka, hatimaye kikawasili chini ya mlima mkubwa. Mlima ulikuwa unazuia njia ya kijito hiki, hivyo kijito kikauomba mlima kwa sauti yake dhaifu na ndogo, “Tafadhali naomba kupita, umesimama kwenye njia yangu na umenizibia njia yangu kuendelea mbele.” Basi mlima ukauliza, “Unakwenda wapi?” Swali ambalo kijito kililijibu, “Ninatafuta makazi yangu.” Mlima ukasema, “Sawa, endelea na tiririkia juu yangu!” Lakini kwa sababu kijito kilikuwa dhaifu sana na kichanga sana, hakukuwa na namna kwake kutiririka juu ya mlima mkubwa hivyo, hivyo hakikuwa na uchaguzi bali kuendelea kutiririka chini ya mlima …

Upepo mkali ukavuma, ukiwa umekusanya mchanga na unga wa kusagika kwa mchanga kuelekea ambapo mlima ulikuwa umesimama. Upepo ukaungurumia mlima, “Hebu nipite!” Mlima ukauliza, “Unakwenda wapi?” Upepo ukavuma kwa kujibu, “Ninataka kwenda upande ule wa mlima.” Mlima ukasema, “Sawa, kama unaweza kupenya katikati yangu, basi unaweza kwenda!” Upepo mkali ukavuma huku na kule, lakini haijalishi ulikuwa mkali kiasi gani, haukuweza kupenya katikati ya mlima. Upepo ukachoka na ukaacha ili upumzike. Hivyo katika upande ule wa mlima ni upepo dhaifu tu ndio ulivuma kwa vipindi, ambao uliwafurahisha watu waliopo kule. Hiyo ilikuwa ni salamu ambayo mlima ulikuwa unaitoa kwa watu …

Ufukweni mwa bahari, mawimbi tulivu ya bahari yalizunguka taratibu kwenye mwamba. Ghafula, wimbi kubwa likaja na likanguruma kuelekea kwenye mlima. “Pisha!” wimbi kubwa lilipiga kelele. Mlima ukauliza, “Unakwenda wapi?” Wimbi kubwa halikusita, na likaendelea kutapakaa huku likijibu, “Ninapanua eneo langu na ninataka kunyoosha mikono yangu kidogo.” Mlima ukasema, “Sawa, kama utaweza kupita juu ya kilele changu, nitakupisha njia.” Wimbi kubwa likarudi nyuma kidogo, na kisha likavurumiza kuelekea mlimani. Lakini haijalishi lilijaribu kwa nguvu kiasi gani, halikuweza kufika juu ya mlima. Halikuwa na jinsi bali kurudi nyuma taratibu kurudi kule lilipotoka …

Kwa karne nyingi kijito kidogo kilichururika taratibu kuzunguka chini ya mlima. Kwa kufuata njia ambayo mlima uliifanya, kijito kidogo kilifanikiwa kufika nyumbani; kilijiunga na mto, na kutiririka kwenda baharini. Chini ya uangalizi wa mlima, kijito kidogo hakikuweza kupotea. Kijito na mlima ilihimiliana na kutegemeana; ilitiana nguvu, kutenda kwa kusaidiana, na kuwepo kwa pamoja.

Kwa karne nyingi, upepo mkali haukuacha tabia yake ya kuvuma kwenye mlima. Upepo mkali ulivumisha kimbunga “ulipoutembelea” mlima kama ulivyofanya kabla. Uliutisha mlima, lakini haukuwahi kupenya katikati ya mlima. Upepo na mlima vilihimiliana na vilitegemeana; vilitiana nguvu, vilitenda kwa kusaidiana, na kuwepo kwa pamoja.

Kwa karne nyingi, wimbi kubwa wala halikupumzika, na kamwe halikuacha kupanuka. Lingenguruma na kuvurumiza tena na tena kwenda kwenye mlima, lakini mlima haukuwahi kusogea hata inchi moja. Mlima uliilinda bahari, na kwa namna hii viumbe ndani ya bahari viliongezeka na kustawi. Wimbi na mlima mkubwa vilihimiliana na vilitegemeana; vilitiana nguvu, vilitenda kwa kusaidiana, na kuwepo kwa pamoja.

Hadithi hii imeishia hapo. Kwanza, mnaweza kuniambia nini kuhusu hadithi hii, maudhui makuu yalikuwa ni nini? Kwanza kulikuwa na mlima, kijito kidogo, upepo mkali, na wimbi kubwa. Nini kilikitokea kijito kidogo na mlima mkubwa katika sehemu ya kwanza? Kwa nini tuzungumze juu ya mlima mkubwa na kijito kidogo? (Kwa sababu mlima ulikilinda kijito, kijito hakikuweza kupotea. Walitegemeana.) Unaweza kusema kuwa mlima ulikilinda au kukizuia kijito kidogo? (Ulikilinda.) Inawezekana kuwa ulikizuia? Mlima na kijito kidogo vilikuwa pamoja; ulikilinda kijito, na pia ulikuwa ni kizuizi. Mlima ulikilinda kijito ili kiweze kutiririka kwenda mtoni, lakini pia ulikizuia kutiririka kutapakaa kila sehemu ambapo kingeweza kufurika na kuwa majanga kwa watu. Hii ndiyo hoja kuu ya sehemu hii? Ulinzi wa mlima kwa kijito na kufanya kwake kazi kama kizuizi kulilinda makazi ya watu. Kisha unapata kijito kidogo kikiunganika na mto chini ya mlima na baadaye kutiririka kwenda baharini; je, huo si umuhimu wa kijito kidogo? Kijito kilipotiririka kwenda kwenye mto halafu kwenda baharini, kilikuwa kinategemea nini? Hakikuwa kinategemea mlima? Kilikuwa kinategemea ulinzi wa mlima na mlima kufanya kazi kama kizuizi; je, hii ndiyo hoja kuu? Je, mnauona umuhimu wa milima kwa maji katika tukio hili? Je, Mungu ana makusudi Yake ya kutengeneza milima mirefu na mifupi? (Ndiyo.) Hii ni sehemu ndogo ya hadithi, na kutoka tu katika kijito kidogo na mlima mkubwa tunaweza kuona thamani na umuhimu wa Mungu kuviumba vitu hivi viwili. Tunaweza pia kuona hekima Yake na makusudi katika jinsi ya kutawala vitu hivi viwili. Sivyo?

Sehemu ya pili ya hadithi inashughulika na nini? (Upepo mkali na mlima mkubwa.) Je, upepo ni kitu kizuri? (Ndiyo.) Sio lazima, kwa kuwa wakati mwingine ikiwa upepo ni mkali sana unaweza kuwa janga. Ungejisikiaje kama ungelazimika kukaa nje kwenye upepo mkali? Inategemea na ukali wake, sivyo? Kama ulikuwa upepo wa kiwango cha tatu au cha nne ungeweza kuvumilika. Kwa kiasi cha juu zaidi, mtu angeweza kupata shida kuendelea kuacha macho wazi bila kufumba. Lakini ungeweza kuvumilia kama upepo ungevuma kwa nguvu na kuwa kimbunga? Usingeweza kuvumilia. Hivyo, ni kosa watu kusema kwamba siku zote upepo ni mzuri, au kwamba siku zote ni mbaya kwa sababu inategemeana na upepo ni mkali kiasi gani. Hivyo mlima una matumizi gani hapa? Je, kwa kiasi fulani haufanyi kazi kama kichujio cha upepo? Mlima unachukua upepo mkali na kuutuliza na kuwa nini? (Upepo mwanana.) Watu wengi wanaweza kuugusa na kuuhisi katika mazingira ambamo wanaishi—je, wanachohisi ni upepo mkali au upepo mwanana? (Upepo mwanana.) Je, hili sio kusudi mojawapo la Mungu la kuumba milima?Ingekuwaje ikiwa watu wangeishi katika mazingira ambapo mchanga ulipeperuka sana katika upepo, bila kuzuiliwa na bila kuchujwa? Je, inaweza kuwa kwamba ardhi inayokabiliwa na mchanga na mawe yanayopeperuka haingeweza kukalika? Mawe yanaweza kuwapiga watu, na mchanga unaweza kuwapofusha. Upepo unaweza kuwaangusha watu au kuwabeba hewani. Je, upepo mkali una thamani? Niliposema kuwa ni mbaya, basi watu wangeweza kuhisi kwamba hauna thamani, lakini hiyo ni sahihi? Je, kubadilika kuwa upepo mwanana hakuna thamani? Watu wanahitaji nini zaidi kunapokuwa na unyevunyevu au kusongwa? Wanahitaji upepo mwanana kuwapepea, kuchangamsha na kusafisha vichwa vyao, kuamsha kufikiria kwao, kurekebisha na kuboresha hali zao za akili. Kwa mfano, nyote mmekaa chumbani kukiwa na watu wengi na hewa sio safi, ni kitu gani mtakihitaji zaidi? (Upepo mwanana.) Katika maeneo ambapo hewa imetibuliwa na imejaa uchafu inaweza kushusha uwezo wa kufikiri wa mtu, kupunguza mzunguko wao wa damu, na kuwafanya vichwa vyao visiwe vyepesi. Hata hivyo, hewa itakuwa safi ikiwa itapata nafasi ya kujongea na kuzunguka na watu watajihisi nafuu zaidi. Ingawa kijito kidogo na upepo mkali vingeweza kuwa janga, alimradi mlima upo utavibadilisha na kuwa vitu ambavyo kwa kweli vinawanufaisha watu; hiyo si kweli?

Sehemu ya tatu ya hadithi inazungumzia nini? (Mlima mkubwa na wimbi kubwa.) Mlima mkubwa na wimbi kubwa. Mandhari hapa ni mlima mkubwa uliopo kando ya bahari ambapo tunauona mlima, mawimbi tulivu ya bahari, na pia wimbi kubwa. Mlima ni nini kwa wimbi hapa? (Mlinzi na kinga.) Ni mlinzi na pia ni kinga. Lengo la kulinda ni kuilinda sehemu hii ya bahari isipotee ili kwamba viumbe vinavyoishi ndani yake viweze kuishi, kuongezeka na kustawi. Kama kinga, mlima hulinda maji ya bahari—chanzo hiki cha maji—yasifurike na kusababisha janga, ambalo linaweza kudhuru na kuharibu makazi ya watu. Hivyo tunaweza kusema kwamba mlima ni kinga na mlinzi. Hii inaonyesha hali ya kutegemeana kati ya mlima na kijito, mlima na upepo mkali, na mlima na wimbi kubwa, na jinsi vinavyozuiliana na kutegemeana, ambayo nimezungumzia.

Huu ni umuhimu wa muungano kati ya mlima mkuu na kijito kidogo, mlima mkuu na upepo mkali, na mlima mkuu na wimbi kubwa kabisa; huu ndio umuhimu wa kutiana nguvu na kuhimiliana, nay a kuwepo kwao pamoja. Vitu hivi ambavyo nimezungumzia. Kuna kanuni na sheria inayoongoza vitu hivi ambavyo Mungu aliviumba kuendelea kuishi. Mnaweza kuona kile ambacho Mungu alifanya kutokana na kile kilichotokea kwenye hadithi? Je, Mungu aliumba ulimwengu na kupuuzia kile kilichotokea baada ya hapo? Je, Alitoa kanuni na kuunda namna ambazo wao hufanya kazi na halafu kuwapuuza baada ya hapo? Je, hicho ndicho kilichotokea? (Hapana.) Ni nini hicho sasa? Mungu bado Anadhibiti maji, upepo na mawimbi. Haviachi bila kudhibitiwa, wala haviachi visababishe madhara au kuharibu nyumba ambamo watu wanaishi. Kwa sababu ya hili, watu wanaweza kuendelea kuishi na kuongezeka na kusitawi katika nchi. Kitu kinachomaanisha kwamba Mungu alikwishapanga kanuni kwa ajili ya kuishi Alipofanya mbingu. Mungu Alipotengeneza vitu hivi, Alihakikisha kwamba vingewanufaisha binadamu, na pia Alividhibiti ili kwamba visiwe shida au majanga kwa binadamu. Ikiwa havingesimamiwa na Mungu, je, maji yangetiririka kila mahali? Je, upepo usingevuma kila sehemu? Yanafuata sheria? Ikiwa Mungu hakuvisimamia visingeongozwa na kanuni yoyote, na upepo ungevuma na maji yangeinuka na kutiririka kila sehemu. Ikiwa wimbi kubwa lingekuwa refu kuliko mlima, je, sehemu hiyo ya bahari ingekuwa bado ipo? Bahari isingeweza kuwepo. Ikiwa mlima haungekuwa mrefu kama wimbi, eneo la bahari lisingekuwepo na mlima ungepoteza thamani na umuhimu wake.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 169)

Mungu aliumba ulimwengu na ni Bwana wake; Anaisimamia yote na Yeye huruzuku vyote, na ndani ya vitu vyote, Yeye huona na kuchunguza kila neno na tendo la kila kitu kilichopo. Vivyo hivyo, pia, ndivyo Mungu huona na kuchunguza kila kona ya maisha ya wanadamu. Hivyo, Mungu anajua kwa undani kila kipengele cha kila kitu kilichopo ndani ya uumbaji Wake, kutoka kwa kazi ya kila kitu, asili yake, na sheria zake za kuishi hadi kwa umuhimu wa maisha yake na thamani ya kuwepo kwake, yote haya Mungu anayajua kwa ukamilifu. Mungu Aliuumba ulimwengu; unadhani Anapaswa kufanya utafiti juu ya kanuni hizi zinazouongoza ulimwengu? Je, Mungu Anahitajika kusoma maarifa au sayansi ya kibinadamu kufanya utafiti na kuyaelewa? (Hapana.) Je, kuna yeyote miongoni mwa binadamu aliye na elimu na maarifa ya kuelewa mambo yote kama Mungu Anavyoelewa? Hakuna, sivyo? Je, kuna mamajusi au wanabiolojia ambao wanaelewa kweli sheria ambazo kwazo vitu vinaishi na kukua? Je, wanaweza kweli kuelewa thamani ya uwepo wa kila kitu? (Hawawezi.) Hii ni kwa sababu vitu vyote viliumbwa na Mungu, na haijalishi ni kwa kiasi kikubwa au kwa kina kiasi gani binadamu anajifunza maarifa haya, au ni kwa muda mrefu kiasi gani wanajitahidi kujifunza, hawataweza kuelewa siri na makusudi ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, hiyo si sahihi? Baada ya kujadili kwa kina hadi sasa, mnahisi kwamba mna ufahamu wa juujuu wa maana ya kweli ya kirai: “Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote”? (Ndiyo.) Nilijua kwamba Nilipojadili mada hii watu wengi wangefikiri kwa haraka juu ya “Mungu ni ukweli, na Mungu hutumia neno Lake kutukimu,” lakini wangeifikiria tu katika kiwango hiki. Baadhi hata wangehisi kwamba Mungu kukimu maisha ya binadamu, kutoa chakula na kinywaji cha kila siku na mahitaji yote ya kila siku haihesabiki kama Yeye kumkimu mwanadamu. Je, baadhi ya watu hawahisi namna hii? Lakini, je, si nia ya Mungu katika uumbaji Wake ni wazi kabisa—kuwaruhusu binadamu wawepo na kuishi kwa kawaida? Mungu anadumisha mazingira ambamo watu wanaishi na anatoa vitu vyote ambavyo binadamu anahitaji ili kuishi. Aidha, Anasimamia na kuwa mkuu juu ya vitu vyote. Haya yote yanamfanya binadamu kuishi na kusitawi na kuongezeka kwa kawaida; ni kwa njia hii ndipo Mungu Anavikimu vitu vyote na binadamu. Je, watu hahitaji kutambua na kuelewa mambo haya? Pengine baadhi wanaweza kusema, “Mada hii ipo mbali sana na maarifa yetu juu ya Mungu Mwenyewe wa kweli, na hatutaki kujua hili kwa sababu binadamu hawezi kuishi kwa mkate pekee, lakini badala yake anaishi kwa neno la Mungu.” Hili ni sahihi? (Hapana.) Kosa ni lipi hapa? Je, mnaweza kuwa na uelewa kamili juu ya Mungu ikiwa mnaelewa tu vitu ambavyo Mungu amesema? Ikiwa mnakubali tu kazi Yake na hukumu Yake na kuadibu, je, mtakuwa na uelewa kamili juu ya Mungu? Ikiwa mnaelewa sehemu ndogo tu ya tabia ya Mungu, sehemu ndogo ya mamlaka ya Mungu, hiyo inatosha kupata uelewa juu ya Mungu, sio? (Hapana.) Matendo ya Mungu yanaanza na uumbaji Wake wa ulimwengu na yanaendelea leo ambapo matendo yake ni dhahiri muda wote na kila wakati. Ikiwa watu wanaamini kwamba Mungu yupo kwa sababu tu Amewachagua baadhi ya watu ambao kwao Anafanya kazi Yake kuwaokoa watu hao, na kwamba hakuna kingine chochote kinachohusiana na Mungu, si mamlaka Yake, hadhi Yake, wala matendo Yake, basi, je, mtu anaweza kuchukuliwa kuwa aliye na umfahamu wa kweli kwa Mungu? Watu walio na haya yanayodaiwa kuwa “maarifa ya Mungu” wana ufahamu wa upande mmoja tu, ambao wanatumia kuzuia matendo Yake kwa kundi moja la watu. Je, haya ni maarifa ya kweli juu ya Mungu? Sio kwamba watu wenye aina hii ya maarifa juu ya Mungu wanakataa uumbaji Wake wa vitu vyote na utawala wao juu Yao? Baadhi ya watu hawatamani kujishughulisha na hili jambo, wakijiwazia badala yake: “Sioni utawala wa Mungu juu ya vitu vyote, ni kitu ambacho kipo mbali sana na mimi na sitaki kukielewa. Mungu Anafanya kile anachotaka na wala hakinihusu. Ninakubali tu uongozi wa Mungu na neno Lake ili niweze kuokolewa na kufanywa mkamilifu na Mungu.Hakuna kingine kilicho na umuhimu kwangu. Sheria ambazo Mungu Alifanya Alipoviumba vitu vyote na kile ambacho Mungu Anafanya kuvikimu vitu vyote na kumkimu mwanadamu havinihusu.” Haya ni mazungumzo ya aina gani? Je, huu si uasi? Hii sio fedheha kabisa? Je, kuna mtu yeyote miongoni mwenu aliye na ufahamu kama huu? Ninajua kwamba kuna watu wengi sana wanaofikiri namna hii hata kama hamtasema. Aina ya mtu huyu wa kuamini katika maandiko anaweza kutumia kile kinachoitwa msimamo wao wa kiroho katika namna wanavyotazama kila kitu. Wanataka kumwekea Mungu mipaka katika Biblia, kumwekea Mungu mipaka kwa maneno Aliyoyazungumza, na kumwekea Mungu mipaka katika neno lilikoandikwa. Hawatamani kufahamu zaidi kuhusu Mungu na hawataki Mungu Aweke umakini zaidi katika kufanya mambo mengine. Aina hii ya kufikiri ni ya kitoto na ni ya kidini sana. Je, watu wenye mitazamo hii wanaweza kumjua Mungu? Wanaweza kuwa na wakati mgumu kumjua Mungu. Leo nimesimulia hadithi mbili, kila moja ikigusia kipengele tofauti. Mnaweza kuhisi kwamba ni za kina au hata ni za kidhahania kidogo na ngumu kutambua na kufahamu. Inaweza kuwa ni vigumu kuzihusianisha na matendo ya Mungu na Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, matendo yote ya Mungu na yote Aliyoyafanya miongoni mwa vitu vyote na miongoni mwa binadamu wote yanapaswa kueleweka kwa wazi na kwa usahihi kwa kila mtu na kwa kila mmoja ambaye anatafuta kumjua Mungu. Maarifa haya yatakupatia uthibitisho wa imani katika uwepo wa kweli wa Mungu. Pia yatakupatia maarifa sahihi juu ya hekima ya Mungu, nguvu Zake, na jinsi ambavyo anakimu vitu vyote. Itakufanya uelewe kwa wazi kabisa uwepo wa kweli wa Mungu na kuona kwamba siyo hadithi ya kubuni, na sio kisasili. Hii inakufanya uone kwamba si ya kidhahania, na sio tu nadharia, na kwamba Mungu hakika sio tu riziki ya kiroho, lakini ni kweli yupo. Aidha, itawaruhusu watu kujua kwamba Mungu daima amekimu viumbe na binadamu wote; Anafanya hivi kwa njia Yake mwenyewe na kulingana na wizani Wake mwenyewe. Hivyo mtu anaweza kusema kwamba ni kwa sababu Mungu Aliumba vitu vyote na Akavipatia kanuni kwamba kwa amri Yake kila kimoja kinafanya kazi zake kilizopangiwa, vinatimiza majukumu yao, na kutimiza jukumu ambalo lilipewa kila kimoja. Vitu vyote vinatimiza jukumu lao kwa ajili ya binadamu, na hufanya hivi katika sehemu, mazingira ambamo watu wanaishi. Ikiwa Mungu hangefanya mambo namna hii na mazingira ya binadamu hayangekuwa jinsi yalivyo, imani ya watu kwa Mungu au wao kumfuata Yeye—hakuna ambacho kingewezekana; yangekuwa tu mazungumzo ya bure, hii sio sahihi?

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 170)

Tumejadili mada nyingi na maudhui yanayohusiana na kirai hiki “Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote,” lakini mnajua ndani ya mioyo yenu ni vitu vipi Mungu anatoa kwa wanadamu mbali na kuwapa ninyi neno Lake na kutenda kazi Yake ya kuadibu na hukumu kwenu? Watu wengine huenda wakasema, “Mungu hunipa neema na baraka; Yeye hunifundisha nidhamu na kunifariji na Hunipa utunzaji na ulinzi kwa kila njia iwezekanayo.” Wengine watasema, “Mungu hunipa chakula cha kila siku na kinywaji,” ilhali wengine hata watasema, “Mungu hunipa kila kitu.” Kuhusu vitu hivi ambavyo watu wanaweza kukutana navyo katika maisha yao ya kila siku, nyote mnaweza kuwa na majibu yanayohusiana na matukio mnayopitia katika maisha yenu ya kimwili. Mungu humpa kila mtu mmoja vitu vingi, ingawa tunachojadili leo hakijawekewa mipaka katika eneo la mahitaji ya watu ya kila siku, lakini kinanuiwa kupanua mtazamo wa kila mmoja wenu na kuwawezesha kuona vitu kutoka mbali zaidi. Kwa sababu Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote, Anadumisha vipi uhai wa vitu vyote? Kwa maneno mengine, ni nini ambacho Mungu huleta kwa vitu vyote ili kudumisha kuwepo kwa vitu hivyo na kudumisha sheria za kuwepo kwa vitu hivyo? Hilo ndilo wazo kuu la kile tunachojadili leo. … Lakini Natumai mtaweza kuunganisha mada hii pamoja na vitu Ninavyoenda kuzungumzia kwa matendo ya Mungu, na sio kuviunganisha kwa ufahamu wowote au kuvihusisha na desturi zozote za binadamu au uchunguzi. Ninazungumza tu kuhusu Mungu na kuhusu Mungu Mwenyewe. Hilo ni pendekezo Langu kwenu. Unaelewa, sivyo?

Mungu ametoa vitu vingi kwa wanadamu. Nitaanza kwa kuzungumza kuhusu kile ambacho watu wanaweza kuona, yaani, wanachoweza kuhisi. Hivi ni vitu ambavyo watu wanaweza kuvielewa na wanaweza kukubali. Hivyo basi kwanza tuanze na ulimwengu yakinifu kujadili kile ambacho Mungu amewapa wanadamu.

1. Hewa

Kwanza, Mungu aliumba hewa ili mwanadamu aweze kupumua. Hewa ni chembechembe ambayo kwayo wanadamu wanaweza kuwasiliana nila siku na ni kitu ambacho kwacho wanadamu hutegemea mara kwa mara, hata wanapolala. Hewa ambayo Mungu aliumba ina umuhimu mkubwa sana kwa wanadamu: ni kijenzi muhimu cha kila pumzi yao na cha uhai wenyewe. Kiini hiki, kinachoweza tu kuhisiwa lakini hakionekani, kilikuwa zawadi ya Mungu ya kwanza kwa vitu vyote. Baada ya kuumba hewa, je, Mungu aliacha kufanya kazi? Baada ya kuumba hewa, je, Mungu alizingatia uzito wa hewa? Je, Mungu alizingatia yaliyomo kwenye hewa? (Ndio.) Mungu alikuwa anafikiria nini alipoumba hewa? Kwa nini Mungu aliumba hewa, na fikira Yake ilikuwa gani? Wanadamu wanahitaji hewa, na wanahitaji kupumua. Kwanza kabisa, uzito wa hewa unapaswa kuwa unaofaa mapafu ya binadamu. Kuna yeyote anayejua uzito wa hewa? Hili si jambo ambalo watu wanahitaji kujua; hakuna haja ya kujua hili. Hatuhitaji idadi kamili kuhusiana na uzito wa hewa, na kuwa na wazo la jumla ni vizuri. Mungu aliumba hewa yenye uzito ambao ungefaa zaidi mapafu ya mwanadamu kupumua. Yaani, wanadamu wanafurahia na haiwezi kudhuru mwili wanapoivuta. Hili ndilo wazo kuhusu uzito wa hewa. Basi tutaongea kuhusu yaliyomo kwenye hewa. Kwanza, yaliyomo ndani ya hewa si sumu kwa wanadamu na hivyo hayatadhuru pafu na mwili. Mungu alihitaji kuzingatia haya yote. Mungu alihitaji kuzingatia kwamba hewa ambayo wanadamu wanapumua inapaswa kuingia na kutoka taratibu, na kwamba, baada ya kuvuta hewa, kadiri na kiasi cha hewa vinapaswa kuhakikisha damu pamoja na hewa chafu ndani ya mapafu na mwili vingejenga na kuvunjavunja kemikali mwilini vizuri, na pia kwamba hewa hiyo haipaswi kuwa na vijenzi vyovyote vya sumu. Kuhusu viwango hivi viwili, Sitaki kuwalisha mafungu ya maarifa, lakini badala yake nataka tu mjue kwamba Mungu alikuwa na mchakato maalum wa mawazo akilini mwake Alipoumba kila kitu—bora zaidi. Aidha, kuhusu kiasi cha vumbi katika hewa, kiasi cha vumbi, mchanga na uchafu duniani, na vilevile vumbi inayoelekea chini kutoka angani, Mungu alikuwa na mpango wa vitu hivi pia, njia za kuviondoa ama kuvisababisha vivunjike. Huku kukiwa na vumbi kiasi, Mungu aliiumba ili vumbi isidhuru mwili na upumuaji wa mwanadamu, na kwamba vipande vya vumbi viwe na ukubwa usiokuwa na madhara kwa mwili. Je, uumbaji wa Mungu wa hewa haukuwa wa ajabu? Je, ulikuwa rahisi kama kupuliza pumzi ya hewa kutoka kinywani Mwake? (La.) Hata katika uumbaji wake wa vitu rahisi sana, maajabu ya Mungu, akili Zake, mawazo Yake, na hekima Yake vyote ni dhahiri. Je, Mungu si mwenye vitendo? (Ndiyo, yeye Ndiye). Maana ya hii ni kwamba, hata katika kuumba vitu rahisi, Mungu alikuwa akifikiria kuhusu mwanadamu. Kwanza kabisa, hewa ambayo wanadamu hupumua ni safi, yaliyomo yanafaa kwa upumuaji wa mwanadamu, si sumu na hayasababishi madhara kwa wanadamu, na uzito huo umekadiriwa kwa upumuaji wa wanadamu. Hewa hii ambayo wanadamu huvuta pumzi na kutoa ni muhimu kwa mwili wao, umbo lao. Ili wanadamu waweze kupumua kwa uhuru, bila kizuizi au wasiwasi. Waweze kupumua kwa kawaida. Hewa ni kile ambacho Mungu aliumba mwanzo na ambacho ni cha lazima kwa upumuaji wa wanadamu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 171)

2. Halijoto

Kitu cha pili ni halijoto. Kila mtu anajua halijoto ni nini. Halijoto ni kitu ambacho mazingira yanayofaa kuishi kwa wanadamu ni lazima yawe nacho. Ikiwa halijoto iko juu sana, tuseme ikiwa halijoto iko juu zaidi ya nyuzi Selisiasi 40, basi haingekuwa inachosha sana kwa wanadamu? Je, haingekuwa inachosha kwao kuishi? Je, na halijoto ikiwa chini sana, na kufikia nyuzi hasi Selisiasi 40? Wanadamu hawataweza pia kuistahimili. Kwa hiyo, Mungu alikuwa mwangalifu sana katika kuviweka vipimo hivi vya halijoto. Vipimo vya halijoto ambavyo mwili wa mwanadamu unaweza kufanya mabadiliko kimsingi ni nyuzi hasi Selisiasi 30 hadi nyuzi Selisiasi 40. Hiki ndicho kipimo cha halijoto cha msingi kutoka kaskazini mpaka kusini. Katika maeneo ya baridi, halijoto inaweza kuteremka mpaka nyuzi hasi 50 hadi 60;Selisiasi. Eneo kama hilo si mahali ambapo Mungu anamruhusu mwanadamu kuishi. Mbona kuna maeneo ya baridi hivyo? Katika hayo kuna hekima na makusudi ya Mungu. Hakuruhusu kusonga karibu na sehemu hizo. Mungu hulinda sehemu zilizo na joto sana na baridi sana, kumaanisha Hayuko tayari kumruhusu mwanadamu kuishi huko. Si kwa wanadamu. Kwa nini akaruhusu sehemu kama hizo kuwepo duniani? Ikiwa Mungu hangemruhusu mwanadamu kuishi au kuwepo huko, basi kwa nini akaziumba? Hekima ya Mungu imo humo. Yaani, halijoto ya msingi ya mazingira ya kuendelea kuishi kwa mwanadamu pia imerekebishwa na Mungu vya kutosha. Kuna sheria hapa pia. Mungu aliumba vitu vingine kusaidia kudumisha halijoto kama hiyo, kudhibiti halijoto hiyo. Ni vitu gani vinatumiwa kudumisha halijoto hii? Kwanza kabisa, jua linaweza kuwaletea watu uvuguvugu, lakini watu wataweza kustahimili iwapo ni vuguvugu sana? Je, kuna yeyote anaweza thubutu kukaribia jua? Je, kuna kifaa chochote duniani kinachoweza kusonga karibu na jua? (La.) Mbona? Ni joto sana. Kitayeyuka kikaribiapo jua. Kwa hiyo, Mungu ametengeneza kipimo maalum cha umbali wa jua kutoka kwa wanadamu: Amefanya kazi maalumu. Mungu ana kiwango cha umbali huu. Vilevile kuna Ncha ya kusini na Ncha ya Kaskazini za dunia. Kote huko kuna mito ya barafu. Wanadamu wanaweza kuishi juu ya mito ya barafu? Inafaa kuishi kwa wanadamu? (La.) La, hivyo watu hawataenda huko. Kwa vile watu hawaendi katika Ncha za Kusini na Kaskazini, mito ya barafu itahifadhiwa, na itaweza kufanya wajibu wake, ambao ni kudhibiti halijoto. Unaelewa? Ikiwa hakuna Ncha za Kusini na Kaskazini na jua linawaka juu ya dunia kila wakati, basi watu wote juu ya dunia watakufa kutokana na joto. Je, Mungu hutumia tu vitu hivi viwili kudhibiti halijoto inayofaa kuishi kwa wanadamu? La, pia kuna kila aina za viumbe vyenye uhai, kama vile nyasi juu ya mbuga za malisho, aina mbalimbali za miti na kila aina ya mimea iliyo ndani ya misitu vinafyonza joto la jua na kwa kufanya hivyo, vinabatilisha nishati ya joto ya jua kwa njia inayorekebisha halijoto ya mazingira ambamo wanadamu wanaishi. Pia kuna vyanzo vya maji, kama vile mito na maziwa. Sehemu ya juu ya mito na maziwa si kitu kinachoweza kuamuliwa na yeyote. Hakuna yeyote anayeweza kudhibiti kiasi cha maji yaliyo juu ya dunia, wapi maji hayo yanatiririka, mwelekeo wa kutiririka huko, wingi wa maji hayo, au spidi ya mtiririko huo. Mungu pekee ndiye ajuaye. Vyanzo hivi mbalimbali vya maji, yakiwemo maji ya chini ya ardhi na mito na maziwa yaliyo juu ya ardhi ambayo watu wanaweza kuona, yanaweza pia kurekebisha halijoto ambayo wanadamu wanaishi ndani. Zaidi ya hayo, kuna kila aina ya uumbaji wa kijiografia, kama vile milima, tambarare, korongo kuu na ardhi ya majimaji wa uumbaji huu mbalimbali wa kijiografia na sehemu zao za juu na ukubwa vyote vina umuhimu katika kudhibiti halijoto. Kwa mfano, ikiwa mlima una mzinga wa kilomita mia moja, kilomita hizi 100 zitakuwa na athari ya kilomita 100. Lakini kuhusu safu za milima na korongo kuu ngapi kama hizo ambazo Mungu ameumba juu ya dunia, hili ni jambo ambalo Mungu amelifikiria kabisa. Kwa maneno mengine, nyuma ya kuwepo kwa kila kitu kilichoumbwa na Mungu kuna hadithi, na pia kina hekima na mipango ya Mungu. Tuseme, kwa mfano, misitu na kila aina mbalimbali za mimea—safu na ukubwa wa eneo ambamo vinapatikana na kukua haudhibitiwi na mwanadamu yeyote na hakuna anayetawala vitu hivi. Kiasi cha maji ambayo vinafyonza, kiasi cha nishati ya joto ambayo vinafyonza kutoka kwa jua pia haviwezi kudhibitiwa na mwanadamu yeyote. Vitu hivi vyote viko katika eneo la kile kilichopangwa na Mungu alipoumba vitu vyote.

Ni kwa sababu tu ya upangaji wa makini, fikira, na utaratibu wa Mungu katika vipengele vyote ndio mwanadamu anaweza kuishi katika mazingira yaliyo na halijoto ya kufaa hivyo. Kwa hiyo, kila kitu ambacho mwanadamu anakiona kwa macho yake, kama vile jua, Ncha za Kusini na Kaskazini ambazo watu mara nyingi husikia kuzihusu, vilevile viumbe mbalimbali vilivyo hai juu na chini ya ardhi na ndani ya maji, na sehemu za juu zenye misitu na aina zingine za mimea, na vyanzo vya maji, mikusanyiko mbalimbali ya maji, kuna kiasi gani cha maji chumvi na maji baridi, kuongezea mazingira mbalimbali ya kijiografia—Mungu hutumia vitu hivi kudumisha halijoto ya kawaida kwa kuishi kwa mwanadamu. Hii ni thabiti. Ni kwa sababu tu Mungu ana fikira kama hizi ndio mwanadamu anaweza kuishi katika mazingira yaliyo na halijoto ya kufaa hivyo. Haiwezi kuwa baridi zaidi wala joto zaidi: sehemu zenye joto zaidi na ambapo halijoto inazidi kile ambacho mwili wa mwanadamu unaweza kuzoea bila shaka hazijatayarishwa na Mungu kwa ajili yako. Sehemu zenye baridi zaidi na ambapo halijoto ni ya chini zaidi; sehemu ambazo, punde tu wanadamu wanapowasili, zitawafanya wagande sana baada ya dakika chache mpaka wasiweze kuzungumza, ubongo wao utaganda, wasiweze kufikiri, na hatimaye watakosa hewa—sehemu kama hizo pia hazijatayarishwa na Mungu kwa ajili ya wanadamu. Haijalishi ni aina gani ya uchunguzi wanadamu wanataka kufanya, au kama wanataka kuvumbua au wanataka kutengua mipaka hiyo—haijalishi watu wanafikiria nini, hawataweza kamwe kuzidi mipaka ya kile ambacho mwili wa mwanadamu unaweza kuzoea. Hawataweza kuondoa mipaka hiyo ambayo Mungu alimuumbia mwanadamu. Hii ni kwa sababu Mungu aliwaumba wanadamu, na Mungu anajua bora zaidi ni halijoto gani mwili wa mwanadamu unaweza kuzoea. Lakini wanadamu wenyewe hawajui. Mbona nasema wanadamu hawajui? Ni mambo gani ya upumbavu ambayo wanadamu wamefanya? Je, hakujakuwa na watu wachache ambao kila mara wanataka kushindana na Ncha za Kaskazini na Kusini? Watu kama hao daima wametaka kwenda kwenye sehemu hizo kumiliki ardhi hiyo, ili waweze kujisitawisha huko. Hiki kingekuwa kitendo cha upumbavu. Hata iwapo umechunguza kikamilifu pembe za dunia, halafu nini? Hata iwapo unaweza kuzoea joto na una uwezo wa kuishi hapo, ingeweza kumfaa mwanadamu kwa njia yoyote iwapo “ungeboresha” hali ya sasa ya maisha katika Ncha za Kusini na Kaskazini? Wanadamu hawana mazingira ambayo kwayo wanaweza kuendelea kuishi ndani, lakini wanadamu hawabaki hapo kwa ukimya na utiifu, ila badala yake wanasisitiza kuenda maeneo ambapo hawawezi kuishi. Kwa nini ni hivyo? Wamechoshwa na kuishi katika halijoto hii ya kufaa. Wamefurahia baraka nyingi sana. Mbali na hayo, haya mazingira ya kuishi ya kawaida yameharibiwa kiasi sana na wanadamu, hivyo wanaweza basi kwenda kwa Ncha ya Kusini na Ncha ya Kaskazini ili wafanye madhara mengi zaidi au kujihusisha katika “kusudi,” fulani ili waweze kuwa “watangulizi” wa aina fulani. Si huu ni upumbavu? Hivyo ni kusema, chini ya uongozi wa babu yao Shetani, wanadamu hawa wanaendelea kufanya kitu kimoja cha upuuzi baada ya kingine, wakiharibu bila hadhari na kwa utukutu makao mazuri ambayo Mungu aliwaumbia wanadamu. Hili ndilo Shetani alifanya. Zaidi ya hayo, kwa kuona kwamba kuendelea kuishi kwa wanadamu duniani kuko katika hatari kidogo, watu wengi sana wanataka kutafuta njia za kwenda kuishi juu ya mwezi, kutafuta njia ya kuondoka kwa kuona ikiwa wanaweza kuishi huko. Hatimaye, inakosekana kwenye mwezi. Je, wanadamu wanaweza kuendelea kuishi bila oksijeni? Kwa vile mwezi hauna oksijeni, si mahali ambapo mwanadamu anaweza kuishi huko, ilhali mwanadamu anaendelea kutaka kwenda huko. Hii ni nini? Ni kujiangamiza, sivyo? Ni mahali pasipo na hewa, na halijoto haifai kwa kuendelea kuishi kwa mwanadamu, hivyo hapajatayarishwa na Mungu kwa ajili ya mwanadamu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 172)

3. Sauti

Kitu cha tatu ni nini? Pia ni kitu ambacho mazingira ya kuishi ya kawaida ya wanadamu yanatakiwa kuwa nacho. Ni kitu ambacho Mungu alishughulikia alipoumba vitu vyote. Hiki ni kitu muhimu sana kwa Mungu na pia kwa kila mtu. Kama Mungu hakushughulikia suala hilo, ingekuwa kizuizi kikubwa kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu. Hiyo ni kusema kwamba ingekuwa na athari yenye maana sana kwa mwili na maisha ya mwanadamu, kiasi kwamba wanadamu hawangeweza kuendelea kuishi katika mazingira kama hayo. Pia inaweza kusemwa kwamba viumbe vyote vyenye uhai haviwezi kuendelea kuishi katika mazingira kama hayo. Hivyo hiki ni kitu gani? Ni sauti. Mungu aliumba kila kitu, na kila kitu kinaishi mikononi mwa Mungu. Machoni pa Mungu, vitu vyote vinasonga na vinaishi. Yaani kuwepo kwa kila mojawapo ya vitu vilivyoumbwa na Mungu kuna thamani na maana. Yaani, vyote vina umuhimu katika kuwepo kwao. Kila kitu kina uhai machoni pa Mungu; kwa kuwa vyote viko hai, vitatoa sauti. Kwa mfano, dunia daima inazunguka, jua daima linazunguka, na mwezi daima unazunguka pia. Sauti daima zinatolewa katika uzalishaji na kuendelea na miendo ya vitu vyote. Vitu juu ya dunia daima vinazaa, kukua na kusonga. Kwa mfano, misingi ya milima inasonga na kubadilisha nafasi, na vitu vyote vyenye uhai katika kina cha bahari vinasonga na kuogelea na kwenda hapa na pale. Hii inamaanisha kwamba vitu hivi vyenye uhai, vitu vyote anavyoviona Mungu, vyote viko mara kwa mara, kwa mwendo wa kawaida, kulingana na mifumo iliyoanzishwa. Kwa hivyo, ni nini kinaletwa na uzalishaji wa siri na maendeleo na miendo ya vitu hivyo? Sauti za nguvu. Mbali na dunia, kila aina ya sayari daima ziko katika mwendo, na viumbe vyenye uhai na viumbe hai juu ya sayari hizo pia daima vinazaa, vinakua na viko katika mwendo. Yaani, vitu vyote vilivyo na uhai na visivyo na uhai daima vinasonga mbele machoni pa Mungu, na pia vinatoa sauti wakati huo huo. Mungu pia ameshughulikia sauti hizi. Mnapaswa kujua sababu ya mbona sauti hizi zinashughulikiwa, sivyo? Unaposonga karibu na ndege, sauti ya kunguruma ya ndege itakufanyia nini? Masikio yako yatazibwa muda unavyozidi kusonga. Je, mioyo yenu itaweza kuistahimili? Wengine wenye mioyo hafifu hawataweza kuistahimili. Bila shaka, hata wale wenye mioyo yenye nguvu hawataweza kuistahimili ikiendelea kwa muda mrefu. Hiyo ni kusema, athari ya sauti kwa mwili wa mwanadamu, kama ni kwa masikio au moyo, ni yenye maana kabisa kwa kila mtu, na sauti ambazo ni za juu sana zitaleta madhara kwa watu. Kwa hiyo, Mungu alipoumba vitu vyote na baada ya hivyo kuanza kufanya kazi kwa kawaida, Mungu pia aliweka sauti hizi—sauti za vitu vyote vilivyo katika mwendo—kupitia kwa utendeaji wa kufaa. Hii pia ni mojawapo ya fikira muhimu alizokuwa nazo Mungu alipoumbia wanadamu mazingira.

Kwanza kabisa, kimo cha angahewa kutoka kwa uso wa dunia kitaathiri sauti. Pia, ukubwa wa utupu ndani ya mchanga, pia utaendesha na kuathiri sauti. Kisha kuna mahali mito miwili inapoungana pa mazingira mbalimbali ya kijiografia, ambapo pia pataathiri sauti. Hiyo ni kusema, Mungu hutumia mbinu fulani kuondoa sauti zingine, ili wanadamu waweze kuendelea kuishi katika mazingira ambayo masikio na mioyo yao vinaweza kustahimili. La sivyo sauti zitaleta kizuizi kikubwa kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu; zitaleta matatizo makubwa kwa maisha yao. Hili litakuwa tatizo kubwa kwao. Hiyo ni kusema, Mungu alikuwa mwenye kujali sana katika uumbaji Wake wa nchi, angahewa, na aina mbalimbali za mazingira ya kijiografia. Hekima ya Mungu iko ndani ya haya yote. Ufahamu wa wanadamu kuhusu haya hauhitaji kuwa kinaganaga sana. Kila wanachohitaji kujua ni kwamba kitendo cha Mungu kimo humo. Sasa Niambieni, hii kazi ambayo Mungu alifanya ilikuwa muhimu? Yaani, uendeshaji wa taratibu sana wa sauti ili kudumisha mazingira ya kuishi ya wanadamu na maisha yao ya kawaida. (Ndiyo.) Ikiwa kazi hii ilikuwa muhimu, basi kutokana na mtazamo huu, je, inaweza kusemwa kwamba Mungu alitumia mbinu kama hii kupeana vitu vyote? Mungu aliwapa wanadamu na kuumba mazingira haya tulivu, ili kwamba mwili wa mwanadamu uweze kuishi kwa kawaida kabisa katika mazingira haya bila vizuizi vyovyote, na ili kwamba mwanadamu ataweza kuwepo na kuishi kwa kawaida. Je, hii si njia mojawapo ambayo kwayo Mungu huwapa wanadamu? Je, jambo hili alilofanya Mungu lilikuwa muhimu sana? (Ndiyo.) Lilikuwa muhimu sana. Je, ni vipi ambavyo mnashukuru hili? Hata kama hamwezi kuhisi kwamba hiki kilikuwa kitendo cha Mungu, wala hamjui vile Mungu alikifanya wakati huo, je, bado mnaweza kuhisi umuhimu wa Mungu kufanya hilo? Je, mnaweza kuhisi hekima ya Mungu au umakini na wazo Aliyoweka katika jambo hili? (Ndiyo.) Kuweza tu kuhisi hili ni sawa. Yatosha. Kuna vitu vingi ambavyo Mungu amefanya miongoni mwa vitu vyote ambavyo watu hawawezi kuhisi na kuona. Lengo la Mimi kukitaja hapa ni kuwapa tu habari kiasi kuhusu matendo ya Mungu ili muweze kuanza kumjua Mungu. Vidokezo hivi vinaweza kuwafanya mjue na kumwelewa Mungu vizuri zaidi.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 173)

4. Nuru

Kitu cha nne kinahusiana na macho ya watu—nacho ni, nuru. Hiki pia ni muhimu sana. Unapoona nuru inayong’aa, na mwangaza wa nuru hiyo ukafikia kiasi fulani, macho yako yatapofushwa. Hata hivyo, macho ya wanadamu ni macho ya mwili. Hayawezi kustahimili kuwashwa. Je, kuna yeyote anayethubutu kulitazama jua moja kwa moja? Watu wengine wamejaribu. Unaweza kutazama ukiwa umevaa miwani ya jua, sivyo? Hilo linahitaji usaidizi wa vifaa. Bila vifaa, macho makavu ya mwanadamu hayathubutu kutazama jua moja kwa moja. Hata hivyo, Mungu aliumba jua ili awape wanadamu nuru, na pia aliendesha nuru hii. Mungu hakuliacha tu jua na kulipuuza baada ya kuliumba. “Nani anajali iwapo macho ya mwanadamu yanaweza kulistahimili!” Mungu hafanyi vitu hivyo. Yeye hufanya vitu kwa uangalifu sana na huzingatia vipengele vyote. Mungu aliwapa wanadamu macho ili waweze kuona, lakini Mungu ametayarisha pia umbali wa mwangaza ambao wanaweza kutazama chini yake. Haitawezekana iwapo hakuna nuru ya kutosha. Iwapo kuna giza sana mpaka watu hawawezi kuona mkono wao ulio mbele yao, kisha macho yao yatapoteza kazi yake na hayatakuwa na faida yoyote. Sehemu iliyo na mwangaza mwingi itakuwa haivumiliki kwa macho ya mwanadamu na pia hawataweza kuona chochote. Hivyo katika mazingira wanayoishi ndani wanadamu, Mungu amewapa kiasi cha nuru kinachofaa macho ya wanadamu. Nuru hii haitaumiza wala kudhuru macho ya watu. Zaidi ya hayo, haitayafanya macho ya watu yapoteze matumizi yake. Hii ndiyo sababu ambayo Mungu aliongeza mawingu yanayozunguka jua na dunia, na uzito wa hewa unaweza pia kuchuja kwa kawaida nuru inayoweza kuumiza macho ya watu au ngozi. Haya yanahusiana. Kuongezea, rangi ya dunia iliyoumbwa na Mungu huakisi pia nuru ya jua na kuondoa ile sehemu ya mwangaza katika nuru inayofanya macho ya wanadamu kutokuwa na raha. Kwa njia hiyo, watu hawahitaji kila mara kuvaa miwani myeusi sana ya jua ili waweze kutembea huko nje na kufanya shughuli za maisha yao. Katika hali za kawaida, macho ya wanadamu yanaweza kuona vitu vilivyo katika eneo la kuona kwao na hayataingiliwa kati na nuru. Yaani, nuru hii haiwezi kuwa ya kuchoma sana wala ya kufifiliza, ikiwa ya kufifiliza sana, macho ya watu yatadhuriwa na hawataweza kuyatumia kwa muda mrefu sana kabla ya macho yao kuacha kutumika; ikiwa ina mwangaza sana, macho ya watu hayataweza kuistahimili. Nuru ii hii ambayo watu wanayo inapaswa iwe ya manufaa kwa macho ya wanadamu kuona, na madhara yanayoletwa kwa macho ya wanadamu na nuru yamepunguzwa na Mungu kupitia kwa mbinu mbalimbali. Haijalishi ikiwa nuru huleta faida au kikwazo kwa macho ya wanadamu, inatosha kuyawezesha macho ya watu kuendelea kuishi mpaka mwisho wa maisha yao. Je, Mungu hajalifikiria hilo kikamilifu sana? Lakini wakati Shetani, ibilisi, anafanya mambo, hafikirii mambo haya. Nuru hiyo ama ina mwangaza sana au inafifiliza sana Hivi ndivyo Shetani hufanya vitu.

Mungu alifanya vitu hivi katika vipengele vyote vya mwili wa mwanadamu—kuona, kusikia, kuonja, kupumua, hisia … kuongeza hadi upeo uwezo wa kubadilisha wa kuendelea kuishi kwa wanadamu ili waweze kuishi kwa kawaida na kuendelea kuishi. Yaani ni kusema, mazingira ya kuishi kama hayo yaliyopo yaliyoumbwa na Mungu ni mazingira ya kuishi yanayofaa zaidi na yenye faida kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu. Wengine wanaweza kufikiri kwamba hii haitoshi na kwamba yote ni ya kawaida sana. Sauti, nuru, na hewa ni vitu ambavyo watu hufikiria kwamba walizaliwa navyo, vitu wanavyoweza kufurahia tangu wakati wa kuzaliwa. Lakini kile alichofanya Mungu kinachosababisha kufurahia kwao kwa vitu hivi ni kitu wanachohitaji kujua na kuelewa. Haijalishi ikiwa unahisi kuna haja ya kuelewa au kujua vitu hivi, kwa ufupi, Mungu alipoumba vitu hivi, alikuwa ametumia fikira, Alikuwa na mpango, Alikuwa na mawazo fulani. Hakuwaweka wanadamu katika mazingira ya kuishi kama haya kwa kawaida, kwa bahati, au bila kufikiria. Huenda mkadhani kwamba Nimezungumza kwa kwa fahari kuhusu vitu hivi vyote vidogo, lakini kwa mtazamo Wangu, kila kitu ambacho Mungu aliwapa wanadamu ni muhimu kwa kuendelea kuishi kwa binadamu. Kuna tendo la Mungu katika hili.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 174)

5. Bubujiko la Hewa

Kitu cha tano ni kipi? Kitu hiki kinahusiana sana na kila siku ya mwanadamu, na uhusiano huu thabiti. Ni kitu ambacho mwili wa mwanadamu hauwezi kuishi bila katika ulimwengu huu yakinifu. Kitu hiki ni bubujiko la hewa. “Bubujiko la hewa” ni neno ambalo watu wote labda wanaelewa. Hivyo bubujiko la hewa ni nini Mngesema kwamba kububujika kwa hewa kunaitwa “bubujiko la hewa.” Bubujiko la hewa ni upepo ambao jicho la mwanadamu haliwezi kuona. Pia ni njia ambayo gesi husonga. Lakini ni bubujiko la hewa gani tunalozungumzia hapa? Mtaelewa punde Nitakaposema. Dunia hubeba milima, bahari, na vitu vyote inapogeuka, na inapogeuka kuna spidi. Hata ikiwa huwezi kuhisi kuzunguka kokote, mzunguko wake upo kweli. Mzunguko wake huleta nini? Huwa kuna upepo kando ya masikio yako unapokimbia? Ikiwa upepo unaweza kuzalishwa unapokimbia, inawezekanaje kutokuwepo kwa nguvu za upepo dunia inapozunguka? Dunia inapozunguka, vitu vyote viko katika mwendo. Iko katika mwendo na kuzunguka katika spidi fulani, wakati vitu vyote duniani daima vinazaa na kukua. Kwa hiyo, kusonga kwa spidi fulani kwa kawaida kutaleta bubujiko la hewa. Hilo ndilo bubujiko la hewa. Bubujiko la hewa hilo litaathiri mwili wa mwanadamu kwa kiasi fulani? Unaona, tufani za kawaida hazina nguvu sana, lakini zinapotokea, watu hawawezi kusimama kwa utulivu na huona vigumu kutembea katika upepo huo. Ni vigumu hata kutembea hatua moja. Ina nguvu sana, baadhi ya watu wanasukumwa na upepo dhidi ya kitu na hawawezi kusonga. Hii ni mojawapo ya njia ambazo bubujiko la hewa linaweza kuathiri wanadamu. Ikiwa dunia nzima ingekuwa imejaa tambarare, ingekuwa vigumu mno kwa mwili wa binadamu kuhimili bubujiko la hewa ambalo lingezalishwa na mzunguko wa dunia na mwendo wa vitu vyote katika spidi fulani. Ingekuwa vigumu zaidi kustahimili. Ingekuwa hivyo, hili bubujiko la hewa halingeleta tu madhara kwa wanadamu, bali uharibifu. Hakuna ambaye angeweza kuendelea kuishi katika mazingira hayo. Ndio maana Mungu hutumia mazingira mbalimbali ya kijiografia kutatua aina hiyo ya mabubujiko ya hewa—katika mazingira tofauti, mabubujiko ya hewa hufifia, hubadili mwelekeo wake, hubadili kasi yake na hubadili nguvu yake. Ndio maana watu wanaweza kuona mazingira ya jiografia mbalimbali, kama vile milima, safu za milima, tambarare, vilima, vidimbwi, mabonde, uwanda wa juu, na mito. Mungu hutumia haya mazingira mbalimbali ya jiografia kubadilisha spidi, mwelekeo na nguvu za bubujiko la hewa, akitumia mbinu kama hiyo kupunguza au kuiendesha kuwa spidi ya upepo, mwelekeo wa upepo, na nguvu za upepo zinazofaa, ili wanadamu waweze kuwa na mazingira ya kuishi ya kawaida. Je, ni lazima kufanya hivyo? (Ndiyo.) Kufanya jambo kama hilo kunaonekana kuwa vigumu kwa wanadamu, lakini ni rahisi kwa Mungu kwa sababu Anaangalia kwa makini vitu vyote. Kwa Yeye kuumba mazingira yenye bubujiko la hewa linalofaa wanadamu ni kitu sahili sana, rahisi sana. Kwa hiyo, katika mazingira kama hayo yaliyoumbwa na Mungu, kila kitu na vitu vyote miongoni mwa vitu vyote ni vya lazima. Kuna thamani na umuhimu katika kila kuwepo kwa vitu hivyo. Hata hivyo, kanuni hii haieleweki na Shetani au kwa mwanadamu ambaye amepotoshwa. Wanaendelea kuharibu na kukuza, wakiota bure juu ya kugeuza milima kuwa ardhi tambarare, kujaza korongo kuu, na kujenga magorofa juu ya ardhi tambarare kuunda misitu ya saruji. Ni matumaini ya Mungu kwamba wanadamu wataishi kwa furaha, kukua kwa furaha, na kutumia kila siku kwa furaha katika mazingira ya kufaa zaidi Aliyowatayarishia. Ndiyo maana Mungu hajawahi kuwa mzembe inapohusu kushughulikia mazingira ya kuishi ya wanadamu. Kutoka kwa halijoto mpaka kwa hewa, kutoka kwa sauti mpaka kwa nuru, Mungu amefanya mipango na utaratibu tatanishi, ili mazingira ya kuishi ya wanadamu na miili yao visiweze kupatwa na kuharibiwa kokote kutoka kwa hali za asili, na badala yake wanadamu waweze kuishi na kuongezeka kawaida na kuishi na vitu vyote kawaida kwa kuishi pamoja kwa amani yenye kuridhisha. Hii yote inapeanwa na Mungu kwa vitu vyote na wanadamu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 175)

Je, sasa mnahisi tofauti kubwa kabisa kati ya Mungu na wanadamu? Nani hasa ndiye bwana wa vitu vyote? Ni mwanadamu? (La.) Basi ni nini tofauti kati ya vile Mungu na wanadamu hushughulikia vitu vyote? (Mungu hutawala na kupanga vitu vyote, ilhali mwanadamu hufurahia vitu hivyo vyote.) Je, mnakubaliana na maneno hayo? Tofauti kubwa kabisa kati ya Mungu na wanadamu ni kwamba Mungu hutawala vitu vyote na hupeana vitu vyote. Mungu ni chanzo cha vitu vyote, na wanadamu hufurahia vitu vyote wakati Mungu anawapa. Hiyo ni kusema, mwanadamu hufurahia vitu vyote anapokubali maisha ambayo Mungu anatoa kwa vitu vyote. Wanadamu hufurahia matokeo ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, ilhali Mungu ni Bwana. Kisha kutokana na mtazamo wa vitu vyote, ni nini tofauti kati ya Mungu na wanadamu? Mungu anaweza kuona vizuri mipangilio ya ukuaji wa vitu vyote, na kudhibiti na kutawala mipangilio ya ukuaji wa vitu vyote. Yaani, vitu vyote vipo machoni mwa Mungu na katika eneo Lake la ukaguzi. Je, wanadamu wanaweza kuona vitu vyote? Kile ambacho wanadamu huona kimewekewa mipaka—ni tu kile wanachoona mbele ya macho yao. Ukiukwea mlima huu, unachoona ni mlima huu. Huwezi kuona kilicho upande mwingine wa mlima huo. Ukienda pwani, unaweza kuona upande huu wa bahari, lakini hujui upande ule mwingine wa bahari ulivyo. Ukiwasili katika msitu huu, unaweza kuona mimea iliyo mbele ya macho yako na inayokuzunguka, lakini huwezi kuona iliyo mbele zaidi. Wanadamu hawawezi kuona sehemu zilizo juu sana, mbali sana na kina sana. Kile wanachoweza kuona ni kilicho mbele ya macho yao na katika mpaka wa uwezo wao wa kuona. Hata kama wanadamu wanajua mpangilio wa misimu minne katika mwaka na mpangilio wa ukuaji wa vitu vyote, hawawezi kusimamia au kutawala vitu vyote. Kwa upande mwingine, vile Mungu aonavyo vitu vyote ni kama vile Mungu angeona mashine Aliyotengeneza binafsi. Angejua kila kijenzi vizuri kabisa. Kanuni zake ni zipi, mipangilio yake ni ipi, na kusudi lake ni lipi—Mungu anajua vitu hivi vyote wazi na dhahiri. Kwa hiyo Mungu ni Mungu, na mwanadamu ni mwanadamu! Hata mwanadamu akiendelea kuchunguza sayansi na sheria za vitu vyote, ni katika eneo lililowekewa mipaka pekee, ilhali Mungu anadhibiti vitu vyote. Kwa mwanadamu, hiyo ni isiyo na kikomo. Wanadamu wakichunguza kitu fulani kidogo ambacho Mungu alifanya, wangetumia maisha yao yote kukichunguza bila kupata matokeo yoyote ya kweli. Ndiyo maana ukitumia ufahamu na kile ulichojifunza kumsoma Mungu, hutaweza kamwe kujua au kuelewa Mungu. Lakini ukitumia njia ya kutafuta ukweli na kumtafuta Mungu, na kumtazama Mungu kutokana na mtazamo wa kuanza kumjua Mungu, basi siku moja utakubali kwamba matendo na hekima ya Mungu viko kila mahali, na utajua pia hasa ni kwa nini Mungu huitwa Bwana wa vitu vyote na chanzo cha uhai kwa vitu vyote. Kadiri unavyokuwa na maarifa kama hayo, ndivyo utakavyoelewa ni kwa nini Mungu huitwa Bwana wa vitu vyote. Vitu vyote na kila kitu, pamoja na wewe, daima vinapokea mtiririko thabiti wa upeanaji wa Mungu. Utaweza pia kuhisi dhahiri kwamba katika ulimwengu huu, na miongoni mwa wanadamu hawa, hakuna yeyote isipokuwa Mungu anayeweza kuwa na nguvu kama hizo na kiini kama hicho kutawala, kusimamia, na kudumisha kuwepo kwa vitu vyote. Ukitimiza ufahamu kama huo, utakubali kwa kweli kwamba Mungu ni Mungu wako. Ukifikia kiwango hiki, umemkubali Mungu kwa kweli na kumruhusu awe Mungu wako na Bwana wako. Ukiwa na ufahamu kama huo na maisha yako yakifikia kiwango kama hicho, Mungu hatakujaribu na kukuhukumu tena, wala Hatakushurutisha ufanye mambo, kwa sababu unamfahamu Mungu, unajua moyo Wake, na umemkubali Mungu kwa kweli ndani ya moyo wako. Hii ni sababu muhimu ya kuwasilisha mada hizi kuhusu utawala na usimamizi wa Mungu juu ya vitu vyote. Ni kuwapa watu maarifa na ufahamu zaidi; sio tu kukufanya ukubali, lakini kukupa maarifa zaidi na ufahamu wa utendaji wa matendo ya Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 176)

Nafaka, matunda na mboga, na kila aina ya njugu vyote ni vyakula vya wala mboga. Hata kama ni vyakula vya wala mboga, vina lishe za kutosha kuridhisha mahitaji ya mwili wa mwanadamu. Kwa hali yoyote, Mungu hakusema: “Kuwapa wanadamu hiki kunatosha. Wanadamu wanaweza tu kula vitu hivi.” Mungu hakuachia hapo na badala yake aliwatayarishia wanadamu vitu vyenye ladha nzuri zaidi. Vitu hivi ni gani? Ni aina mbalimbali ya nyama na samaki wengi wenu mnaweza kuona na kula kila siku. Kuna aina nyingi sana za nyama na samaki ambazo Mungu amemtayarishia mwanadamu. Samaki wote huishi majini; umbile asili la nyama yao ni tofauti na la nyama inayokuzwa juu ya ardhi na wanaweza kuwapa wanadamu lishe mbalimbali. Sifa za samaki zinaweza kubadilisha baridi na joto ndani ya mwili wa mwanadamu, kwa hiyo ni za manufaa makubwa sana kwa wanadamu. Lakini kilicho na ladha nzuri hakitakiwi kuliwa zaidi. Bado msemo ni huo huo: Mungu huwapa wanadamu kiasi sahihi kwa wakati sahihi, ili watu waweze kufurahia kwa kawaida na vizuri vitu hivi kulingana na msimu na wakati. Ndege wa kufugwa wanahusisha nini? Kuku, kware, njiwa, n.k. Watu wengi hula pia bata na bata bukini. Ingawa Mungu alitayarisha aina hizi za nyama, Alitoa masharti fulani kwa watu Wake aliowachagua na kuweka mipaka maalum kwa chakula chao wakati wa Enzi ya Sheria. Sasa eneo hili linatojkana na kupendelea kwa mtu binafsi na ufahamu wa mtu binafsi. Aina hizi mbalimbali za nyama hupatia mwili wa mwanadamu lishe mbalimbali, zinazoweza kusheheneza protini na madini ya chuma, kusitawisha damu, kuimarisha misuli na mifupa, na kupeana nguvu zaidi. Haijalishi ni mbinu gani watu hutumia kupika na kula vitu hivyo, kwa ufupi, vitu hivi vinaweza kwa upande mmoja kuwasaidia watu kuendeleza ladha na hamu ya chakula, na kwa upande mwingine kuridhisha matumbo yao. Kitu cha muhimu zaidi ni kwamba zinaweza kupatia mwili wa mwanadamu mahitaji yao ya lishe ya kila siku. Hizi ndizo fikira ambazo Mungu alikuwa nazo Alipowatayarishia wanadamu chakula. Kuna vyakula vya wala mboga na pia nyama—je, hiyo si ya fahari na nyingi? Lakini watu wanapaswa kuelewa kusudi la asili la Mungu lilikuwa gani Mungu alipowatayarishia wanadamu vyakula vyote. Je, ilikuwa ni kuwafanya wanadamu kutumia kupita kiasi hivi vyakula? Nini hutendeka wakati mtu hunaswa kwa kujaribu kuridhisha tamaa hizi za vitu? Je, hapati lishe ya kupita kiasi? Je, lishe ya kupita kiasi haidhuru mwili wa mwanadamu kwa njia nyingi? (Ndiyo.) Hiyo ndiyo maana Mungu hutoa kiasi sahihi kwa wakati sahihi na kuwaacha watu wafurahie vyakula mbalimbali kulingana na vipindi vya wakati na misimu. Kwa mfano, baada ya kuishi katika majira ya joto sana, watu watakusanya kiasi fulani cha joto, la kusababisha ukavu wa viini na unyevunyevu katika miili yao. Majira ya kupukutika kwa majani yakija, matunda ya aina nyingi sana yataiva, na watu watakapokula baadhi ya tunda unyevunyevu wao utaondolewa. Wakati huo huo, ng’ombe na kondoo watakuwa wamekua na kupata nguvu, ili watu wale nyama kiasi kama lishe. Baada ya kula aina mbalimbali za nyama, miili ya watu itakuwa na nguvu na joto la kuisaidia kustahimili baridi ya majira ya baridi, na kutokana na hayo wataweza kupita katika majira ya baridi kwa amani. Wakati upi wa kutayarisha vitu vipi kwa ajili ya wanadamu, na wakati upi wa kuacha vitu vipi vikue, vizae matunda na kuiva—yote haya yanadhibitiwa na kupangwa na Mungu kwa kupimwa kabisa. Hii ni mada kuhusu “jinsi Mungu alitayarisha chakula kilicho muhimu kwa maisha ya mwanadamu ya kila siku.” Mbali na aina zote za chakula, Mungu pia huwapa wanadamu vyanzo vya maji. Watu huhitaji kunywa maji kiasi baada ya kula. Je, kula matunda tu kunatosha? Watu hawataweza kustahimili kula matunda pekee, licha ya hayo, huwa hakuna matunda katika misimu mingine. Hivyo tatizo la wanadamu la maji litawezaje kutatuliwa? Kwa Mungu kutayarisha vyanzo vingi vya maji juu ya ardhi na chini ya ardhi, ikiwemo maziwa, mito, na chemchemi. Vyanzo hivi vya maji vinaweza kunywewa maji katika hali ambazo hakuna kuchafuliwa kokote, au maendeleo ya wanadamu au uharibifu. Yaani, kuhusu vyanzo vya chakula kwa maisha ya miili ya wanadamu, Mungu amefanya matayarisho sahihi sana, yasiyo na hitilafu yoyote na ya kufaa sana, ili maisha ya watu yawe ya fahari na yenye wingi na yasiyokosa chochote. Hiki ni kitu ambacho watu wanaweza kuhisi na kuona.

Kuongezea, miongoni mwa vitu vyote Mungu aliumba baadhi ya mimea, wanyama, na mitishamba mbalimbali ambayo hususan hukusudiwa kuponya majeraha ama kutibu magonjwa katika mwili wa mwanadamu. Utafanya nini, kwa mfano, ukichomeka au kuungua kiajali na maji moto? Je, unaweza kufoka kwa maji? Je, unaweza kutafuta kitambaa na kufunika mahali hapo? Huenda pakajaa usaha au kuambukizwa kwa njia hiyo. Kwa mfano, ukipata homa, upate mafua, upate majeraha kutokana na kazi ya viungo, maradhi ya tumbo kutokana na kula kitu kibaya, au kupata magonjwa fulani kwa sababu ya mienendo ya maisha au masuala ya hisia, kama vile magonjwa ya mishipa ya damu, hali za kisaikolojia au magonjwa ya ogani zilizo ndani ya mwili—kuna mimea inayolingana ya kutibu haya yote. Kuna mimea inayoendeleza mzunguko wa damu kuondoa ukwamaji, kutuliza maumivu, kukomesha kutokwa na damu, kutia ganzi, kuwasaidia watu kupata tena ngozi ya kawaida, kuondoa ukwamaji wa damu mwilini, na kuondoa sumu mwilini. Kwa ufupi, yote inaweza kutumiwa katika maisha ya kila siku. Ni ya kufaa watu na imetayarishwa na Mungu kwa ajili ya mwili wa mwanadamu iwapo inahitajika. Baadhi ya hiyo iliruhusiwa na Mungu kugunduliwa bila uangalifu na mwanadamu, ilhali mingine iligunduliwa na watu ambao Mungu aliwachagua kufanya hivyo, ama kama matokeo ya matukio maalum Aliyoyapanga. Baada ya ugunduzi wao, wanadamu wangeipitisha kwa wengine, na halafu watu wengi wangejua kuihusu. Kwa njia hii, uumbaji wa Mungu wa mimea hii unakuwa na thamani na maana. Kwa ufupi, vitu hivi vyote vinatoka kwa Mungu na vilitayarishwa na kupandwa Alipowaumbia wanadamu mazingira ya kuishi. Vitu hivi vyote ni muhimu sana. Je, fikira Zake Mungu zilifikiriwa vizuri sana kuliko za wanadamu? Unapoona yote ambayo Mungu amefanya, unaweza kuhisi upande wa Mungu wa vitendo? Mungu alifanya kazi katika siri. Kabla ya mwanadamu kuingia katika ulimwengu huu, kabla ya kukutana na wanadamu hawa, Mungu alikuwa tayari ameviumba vitu hivi vyote. Kila kitu alichofanya kilikuwa kwa ajili ya wanadamu, kwa ajili ya kuendelea kuishi kwao, na kwa ajili ya kufikiria juu ya kuwepo kwa wanadamu, ili wanadamu waweze kuishi kwa furaha katika ulimwengu huu yakinifu wa ufahari na wingi ambao Mungu aliwatayarishia, bila kuwa na wasiwasi kuhusu chakula au nguo, na bila kukosa chochote. Wanadamu wanaendelea kuzaa na kuendelea kuishi katika mazingira hayo.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 177)

Hapo mwanzo, tulizungumza kuhusu mazingira ya kuishi ya wanadamu na kile Mungu alifanya, alitayarisha, na kushughulikia kwa ajili ya mazingira haya, na vilevile mahusiano kati ya vitu vyote ambavyo Mungu aliwatayarishia wanadamu na jinsi Mungu alishughulikia mahusiano haya yote kuzuia vitu vyote kuleta madhara kwa wanadamu. Mungu pia alitatua athari hasi katika mazingira ya wanadamu zilizosababishwa na vitu mbalimbali vya asili ambavyo vinaletwa na mambo yote, Akaruhusu vitu vyote kuongeza hadi upeo shughuli za vitu hivyo, na Akawaletea wanadamu mazingira ya kufaa na vitu vyote vya asili vyenye manufaa, kuwawezesha wanadamu kuwa wepesi kubadilika kwa mazingira hayo na kuendelea na mfuatano wa kuzaa na wa maisha kwa kawaida. Kilichofuata kilikuwa chakula kilichohitajika na mwili wa mwanadamu—chakula cha kila siku na kinywaji. Hii pia ni hali muhimu ya kuendelea kuishi kwa mwanadamu. Hiyo ni kusema, mwili wa mwanadamu hauwezi kuishi tu kwa kupumua, kuwa na mwangaza wa jua au upepo pekee, au halijoto za kufaa tu. Wanahitaji pia kujaza matumbo yao. Vitu hivi vya kujaza matumbo yao vyote vimetayarishwa pia na Mungu kwa ajili ya wanadamu—hiki ni chanzo cha chakula cha wanadamu. Baada ya kuona mazao haya ya fahari na mengi—vyanzo vya chakula cha wanadamu na kinywaji—unaweza kusema kwamba Mungu ni chanzo cha kupeana wanadamu na vitu vyote? Ikiwa Mungu angeumba tu miti na nyasi au hata viumbe mbalimbali vyenye uhai Alipoumba vitu vyote, ikiwa hivyo viumbe mbalimbali vyenye uhai vyote vingekuwa vya ng’ombe na kondoo kula, au vingekuwa vya pundamilia, paa na aina nyingine mbalimbali za wanyama,kwa mfano, simba walipaswa kula vitu kama pundamilia na paa, na chui wakubwa wenye milia walipaswa kula vitu kama kondoo na nguruwe—lakini kusiwe na hata kitu kimoja cha kufaa wanadamu kula, je, hilo lingefaulu? Halingefaulu. Wanadamu hawangeweza kuendelea kuishi. Na je, wanadamu wangekula tu majani ya miti? Hilo lingefaulu? Wanadamu wangeweza kula nyasi ambayo kondoo hutayarishiwa? Huenda ikawa sawa wakijaribu kidogo tu, lakini wakiendelea kula kwa muda mrefu, matumbo ya wanadamu hayataweza kustahimili tena na hawatadumu kwa muda mrefu. Na hata kuna vitu vingine ambavyo vinaweza kuliwa na wanyama, lakini wanadamu wakivila watapata sumu. Kuna vitu vingine vyenye sumu ambavyo wanyama wanaweza kuvila bila kuathiriwa, lakini wanadamu hawawezi kufanya vivyo hivyo. Kwa maneno mengine, Mungu aliwaumba wanadamu, hivyo Mungu anajua vizuri sana kanuni na muundo wa mwili wa mwanadamu na wanachohitaji wanadamu. Mungu ana hakika kamili kuhusu sehemu na vijenzi vyake, na inachohitaji, vilevile jinsi sehemu za ndani ya mwili wa mwanadamu hufanya kazi, hufyonza, huondosha, na kuvunjavunja kemikali mwilini. Watu hawana hakika kuhusu hili na wakati mwingine hula na kujaliza bila kujua. Wao hujaliza kupita kiasi na mwisho husababisha kutolingana nguvu. Ukila na kufurahia vitu hivi alivyokutayarishia Mungu kwa kawaida, hutakuwa na shida yoyote. Hata kama wakati mwingine una hali mbaya ya moyo na una ukwamaji wa damu, haidhuru. Unahitaji tu kula aina fulani ya mmea na ukwamaji utatatuliwa. Mungu ametayarisha vitu hivi vyote. Kwa hivyo, machoni mwa Mungu, wanadamu wako juu zaidi ya kiumbe chochote kingine chenye uhai. Mungu alitayarishia kila aina ya mimea mazingira ya kuishi na Akatayarishia kila aina ya wanyama chakula na mazingira ya kuishi, lakini mahitaji ya wanadamu pekee kwa mazingira yao ya kuishi ndiyo makali zaidi na yasiyostahamili kutotunzwa. La sivyo, wanadamu hawangeweza kuendelea kukua na kuzaa na kuishi kwa kawaida. Mungu anajua hili vizuri zaidi moyoni Mwake. Mungu alipofanya hili, alilipa umuhimu zaidi kuliko kitu chengine chochote. Labda huwezi kuhisi umuhimu wa kitu fulani kisicho na maana unachokiona na kufurahia au kitu unachohisi ulizaliwa nacho na unaweza kufurahia, ilhali kisiri, au pengine muda mrefu uliopita, Mungu alikuwa tayari amekutayarishia hekima Yake. Mungu ameondoa na kutatua kwa kiwango kikubwa zaidi iwezekanavyo vipengele vyote hasi visivyofaa kwa wanadamu na vinavyoweza kudhuru mwili wa mwanadamu. Nini ambacho hiki kinaweka wazi? Je, kinahakikisha mtazamo wa Mungu kwa wanadamu Alipowaumba wakati huu? Mtazamo huo ulikuwa upi? Mtazamo wa Mungu ulikuwa wa msimamo na maana kubwa, na Hakustahimili kuingilia kati kwa vipengele au hali au nguvu zozote za adui isipokuwa Mungu. Kutokana na hili, unaweza kuona mtazamo wa Mungu alipoumba wanadamu na katika usimamizi Wake wa wanadamu wakati huu. Mtazamo wa Mungu ni upi? Kupitia kwa mazingira ya kuishi na kuendelea kuishi ambayo wanadamu wanafurahia pamoja na chakula chao cha kila siku na kinywaji na mahitaji ya kila siku, tunaweza kuona mtazamo wa Mungu wa wajibu kwao wanadamu ambao Anao tangu Awaumbe, na vilevile uamuzi wa Mungu wa kuwaokoa wanadamu wakati huu. Je, tunaweza kuona uhalisi wa Mungu kupitia kwa haya yote? Tunaweza kuona ustaajabishaji wa Mungu? Tunaweza kuona kutoweza kueleweka kwa Mungu? Tunaweza kuona kudura ya Mungu? Mungu anatumia tu njia Zake za uweza na hekima kuwapa wanadamu wote, na vilevile kuvipa vitu vyote. Licha ya hayo, baada ya Mimi kusema mengi sana, mnaweza kusema kwamba Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote? (Ndiyo.) Hili ni hakika. Je, mna shaka yoyote? (La.) Upeanaji wa Mungu wa vitu vyote ni wa kutosha kuonyesha kwamba Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote, kwa sababu Yeye ni chanzo cha ruzuku ambao umewezesha vitu vyote kuwepo, kuishi, kuzaa, na kuendelea, na hakuna chanzo kingine ila Mungu Mwenyewe. Mungu huruzuku mahitaji yote ya vitu vyote na mahitaji yote ya wanadamu, bila kujali iwapo ni mazingira ya msingi kabisa ya watu kuishi, wanachohitaji watu kila siku, au upeanaji wa ukweli kwa roho za watu. Kutokana na mitazamo yote, inapofikia utambulisho wa Mungu na hadhi Yake kwa wanadamu, ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye chanzo cha uhai kwa vitu vyote. Hili ni sahihi? (Ndiyo.) Yaani, Mungu ni Mtawala, Bwana, na Mpaji wa dunia hii yakinifu ambayo watu wanaweza kuona kwa macho yao na kuhisi. Kwa wanadamu, je, huu si utambulisho wa Mungu? Hii ni kweli kabisa. Hivyo unapoona ndege wakiruka angani, unapaswa kujua kwamba Mungu aliumba vitu vinavyoweza kuruka. Lakini kuna viumbe vyenye uhai vinavyoogelea majini, navyo pia huendelea kuishi kwa njia mbalimbali. Miti na mimea inayoishi ndani ya udongo huchipuka katika majira ya kuchipuka na huzaa matunda na kupoteza majani katika majira ya kupukutika kwa majani, na ifikapo wakati wa majira ya baridi majani yote huwa yameanguka na kupitia katika majira ya baridi. Hiyo ni njia yao ya kuendelea kuishi. Mungu aliumba vitu vyote, na kila kimojawapo huishi kupitia taratibu mbalimbali na njia mbalimbali na hutumia mbinu mbalimbali kuonyesha nguvu zake na taratibu ya maisha. Haijalishi ni mbinu gani, yote iko chini ya utawala wa Mungu. Ni nini kusudi la Mungu la kutawala taratibu zote mbalimbali za maisha na viumbe vyenye uhai? Je, ni kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa wanadamu? (Ndiyo.) Anadhibiti sheria zote za maisha kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa wanadamu. Hii inaonyesha hasa vile kuendelea kuishi kwa wanadamu ni muhimu kwa Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 178)

Mungu si Mungu wa watu Wake wateule pekee. Wewe sasa unamfuata Mungu, na Yeye ni Mungu wako, lakini, je, Yeye ni Mungu wa wale wasiomfuata? Je, Mungu ni Mungu wa watu wote walio nje ya wale wanaomfuata Yeye? Mungu ni Mungu wa vitu vyote? (Ndiyo.) Basi Mungu hutenda kazi Yake na kutekeleza matendo Yake kwa wale tu wanaomfuata Yeye? (La.) Mawanda ya kazi Yake na matendo Yake ni yapi? Kwa kiwango kidogo zaidi, mawanada ya kazi Yake na matendo Yake yanajumuisha wanadamu wote na vitu vyote vya uumbaji. Kwa kiwango cha juu inajumuisha ulimwengu wote ambao watu hawawezi kuuona. Hivyo tunaweza kusema kwamba Mungu hufanya kazi Yake na kutekeleza matendo Yake miongoni mwa wanadamu wote. Hili ni la kutosha kuwafanya watu wajue yote kuhusu Mungu Mwenyewe. Ikiwa unataka kumjua Mungu na upate kweli kumjua na kumfahamu Yeye, basi usizuiwe tu katika hatua tatu za kazi ya Mungu, na usizuiwe tu katika hadithi za kazi ambayo Mungu alitekeleza wakati mmoja. Ukijaribu kumjua hivyo, basi unajaribu kumzuilia Mungu kwa mipaka fulani. Wewe unamwona Mungu kitu kidogo Ni jinsi gani kufanya hivyo kungeathiri watu? Hungeweza kujua maajabu na mamlaka ya juu kabisa ya Mungu, na hungeweza kamwe kujua nguvu za Mungu na kudura na eneo la mamlaka Yake. Ufahamu kama huo ungeathiri uwezo wako wa kukubali ukweli kwamba Mungu ni Mtawala wa vitu vyote, na vilevile maarifa yako ya utambulisho wa kweli na hadhi ya Mungu. Kwa maneno mengine, iwapo ufahamu wako wa Mungu umewekewa mipaka katika eneo, unachoweza kupokea pia kimewekewa mipaka. Ndiyo maana ni lazima upanue eneo na kufungua upeo wa macho yako. Iwe ni eneo la kazi ya Mungu, usimamizi wa Mungu, na utawala wa Mungu, au vitu vyote vinavyotawaliwa na kusimamiwa na Mungu, unapaswa kujua yote na kupata kujua matendo ya Mungu yaliyo ndani. Kupitia njia hii ya ufahamu, utahisi bila kujua kwamba Mungu anatawala, anasimamia na kupeana vitu vyote miongoni mwao. Wakati huo huo, utahisi kweli kwamba wewe ni sehemu ya vitu vyote, na kiungo cha vitu vyote. Mungu anapovipa vitu vyote, wewe pia unakubali utawala na upeanaji wa Mungu. Huu ni ukweli usioweza kupingwa na yeyote. Vitu vyote viko chini ya mamlaka ya sheria zao, ambazo ziko chini ya utawala wa Mungu, na vitu vyote vina sheria zao za kuendelea kuishi, ambazo pia ziko chini ya utawala wa Mungu, huku majaliwa ya wanadamu na wanachohitaji pia vikihusiana kwa karibu na utawala wa Mungu na upeanaji Wake. Ndiyo maana, chini ya utawala wa Mungu na uongozi, wanadamu na vitu vyote vinahusiana, vinategemeana, na vinafumana. Hili ni kusudi na thamani ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 179)

Tangu Mungu alipoviumba, kulingana na sheria ambazo Aliziamua, vitu vyote vimekuwa vikitenda kazi na vimekuwa vikiendelea kukua kwa kawaida. Chini ya uangalizi Wake, chini ya kanuni Yake, vitu vyote vimekuwa vikiendelea kwa kawaida sambamba na kuendelea kuishi kwa binadamu. Hakuna kitu hata kimoja kinaweza kubadilisha sheria hizi, na hakuna hata kitu kimoja kinachoweza kuziharibu sheria hizi. Ni kwa sababu ya kanuni ya Mungu ndipo viumbe vyote vinaweza kuongezeka, na kwa sababu ya kanuni na usimamizi Wake ndipo vitu vyote vinaweza kuendelea kuishi. Hii ni kusema kwamba chini ya kanuni ya Mungu, viumbe vyote vinakuwepo, vinastawi, vinatoweka, na kuzaliwa upya kwa namna ya mpangilio. Msimu wa machipuo unapowadia, mvua ya manyunyu huleta hisia hiyo ya machipuo na kuipatia nchi unyevunyevu. Ardhi huanza kuyeyuka, na majani huota na kujipenyeza juu ya udongo na kuanza kuchipuka, ilihali miti kwa utaratibu hubadilika kuwa ya kijani. Viumbe hai hivi vyote vinaleta uzima mpya katika dunia. Hii ndiyo picha ya viumbe vyote kuwepo na kustawi. Wanyama wa kila aina pia hutoka matunduni mwao ili kupata uvuguvugu wa msimu wa machipuo na kuanza mwaka mpya. Viumbe vyote vinaota jua kwenye joto wakati wa kiangazi na kufurahia uvuguvugu unaoletwa na msimu huu. Vinakua haraka; miti, nyasi, na aina zote za mimea inakua haraka sana, kisha inachanua na kuzaa matunda. Viumbe vyote vinakuwa vimetingwa sana wakati wa kiangazi, binadamu wakiwemo. Katika msimu wa majani kupukutika, mvua inaleta utulivu wa msimu wa majani kupukutika, na aina zote za viumbe hai vinaanza kuhisi majilio ya msimu wa kiangazi. Viumbe vyote vinazaa matunda, na binadamu wanaanza kuvuna matunda haya ya aina mbalimbali ili kuwa na chakula kwa ajili ya msimu wa baridi. Katika msimu wa baridi viumbe vyote taratibu vinaanza kupumzika katika ubaridi, kuwa kimya, na watu pia wanachukua pumziko wakati wa msimu huu. Mabadiliko haya kutoka msimu wa machipuo kwenda msimu wa kiangazi kwenda msimu wa mapukutiko na kwenda msimu wa baridi—mabadiliko haya yote yanatokea kulingana na sheria zilizoanzishwa na Mungu. Anaongoza vitu vyote na wanadamu kwa kutumia sheria hizi na amebuni maisha yenye utajiri na ya kupendeza kwa ajili ya mwanadamu, akiandaa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo yana halijoto tofautitofauti na misimu tofautitofauti. Chini ya mazingira haya yaliyopangiliwa kwa ajili ya kuendelea kuishi, binadamu wanaweza kuendelea kuishi na kuongezeka kwa namna ya mpangilio. Wanadamu hawawezi kuzibadilisha sheria hizi, na hakuna mtu hata mmoja au kiumbe ambacho kinaweza kuzivunja. Ingawa mabadiliko yasiyohesabika yametokea—bahari zimekuwa mbuga, ilhali mbuga zimekuwa bahari—sheria hizi zinaendelea kuwepo. Sheria hizi zipo kwa sababu Mungu yupo, na kwa sababu ya sheria na usimamizi Wake. Kwa aina hii ya mpangilio, mazingira makubwa, maisha ya watu yanaendelea ndani ya sheria na kanuni hizi. Sheria hizi ziliendeleza kizazi baada ya kizazi cha watu na kizazi baada ya kizazi cha watu wameendelea kuishi ndani ya sheria hizi. Watu wamefurahia mazingira haya ya mpangilio kwa ajili ya kuendelea kuishi vilevile vyote miongoni mwa vingi vilivyoumbwa na Mungu kwa ajili ya kizazi baada ya kizazi cha binadamu. Ingawa watu wanahisi kwamba aina hii ya sheria ni za kiasili, ingawa wanazipuuza kabisa sheria hizo, na ingawa hawawezi kuhisi kuwa Mungu ndiye anaweka utaratibu wa sheria hizi, kwamba Mungu anatawala sheria hizi, haijalishi, Mungu siku zote anajihusisha katika kazi hii isiyobadilika. Kusudi lake katika kazi hii isiyobadilika ni kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi, na ili binadamu waweze kuendelea.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 180)

Kwanza, Mungu alipoviumba vitu vyote, Aliweka mipaka kwa ajili ya milima, tambarare, majangwa, vilima, mito, na maziwa. Duniani kuna milima, tambarare, majangwa, vilima, vilevile vyanzo mbalimbali vya maji. Je, hayo si mandhari tofautitofauti? Mungu aliweka mipaka kati ya mandhari haya yote tofautitofauti. Tunapozungumza juu ya kuweka mipaka, ina maana kwamba milima ina mipaka yake, tambarare zina mipaka yake, majangwa yana mawanda fulani, na vilima vina eneo mahususi. Pia kuna kiwango mahususi cha vyanzo vya maji kama vile mito na maziwa. Yaani, Mungu alipoumba vitu vyote aligawanya kila kitu vizuri kabisa. Mungu ameshajua nusu kipenyo cha mlima ni kilometa ngapi, mawanda yake ni mapana kiasi gani. Mungu ameshajua nusu kipenyo cha tambarare ni kilometa ngapi, mawanda yake ni mapana kiasi gani. Alipokuwa anaumba viumbe vyote, Aliamua pia mipaka ya majangwa, vilevile masafa ya vilima na uwiano wao, na vile vilivyopakana navyo—pia Aliamua yote haya. Aliamua mawanda ya mito na maziwa Alipokuwa anaviumba—vyote vina mipaka yao. Kwa hiyo ina maana gani tunaposema “mipaka”? Tulizungumza tu kuhusu ambavyo Mungu huongoza vitu vyote kwa kuanzisha sheria kwa vitu vyote. Yaani, masafa na mipaka ya milima havitaongezeka au kupungua kwa sababu ya mzunguko wa dunia au muda kupita. Hizi ni thabiti, hazibadiliki na ni Mungu ambaye huamrisha kutobadilika kwayo. Kwa maeneo ya tambarare, masafa yao, kile kilichopakana nayo, hii imewekwa na Mungu. Yana mipaka, na tuta haliwezi kutokea tu bila mpangilio, katikati ya tambarare. Tambarare haiwezi tu kubadilika na kuwa mlima—hii haitatokea. Sheria na mipaka tuliyoizungumzia inarejelea hili. Kwa jangwa, hatutataja wajibu wa jangwa au mandhari nyingineyo au eneo la kijiografia hapa, ni mipaka yake tu. Chini ya kanuni ya Mungu mawanda ya jangwa nayo pia hayatapanuka. Hii ni kwa sababu Mungu amelipatia sheria yake, mawanda yake. Eneo lake ni kubwa kiasi gani na wajibu wake ni upi, kile kilichopakana nalo, na lipo mahali gani—hii imeshawekwa na Mungu tayari. Halitazidisha mawanda yake, kuhamisha sehemu yake, na halitaongeza eneo lake kiholela tu. Ingawa mtiririko wa maji kama vile mito na maziwa yote yapo katika mpangilio na mwendelezo, hayajawahi kwenda nje ya mawanda yao au kwenda zaidi ya mipaka yao. Yote yanafuata mwelekeo mmoja kwa namna ya mpangilio, yakitiririka kuelekea mwelekeo yanaopaswa kwenda. Kwa hiyo chini ya sheria ya kanuni ya Mungu, hakuna mto au ziwa ambalo litakauka kiholela tu, au kubadilisha mwelekeo au kiwango cha kutiririka kwake kiholela tu kwa sababu ya mzunguko wa dunia au kupita kwa muda. Hii yote ipo ndani ya maarifa ya Mungu. Hiyo ni sawa na kusema, vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu miongoni akiwemo binadamu, vina sehemu zao, maeneo yao, na mipaka yao. Yaani, Mungu alipoviumba viumbe vyote, mipaka yao ilianzishwa na hii haiwezi kugeuzwa kiholela tu, kufanywa upya au kubadilishwa. “Kiholela” inamaanisha nini? Ina maana kwamba havitahama, kupanuka, au kubadilisha umbo lao asilia bila mpangilio kwa sababu ya hali ya hewa, halijoto, au kasi ya mzunguko wa dunia. Kwa mfano, mlima una kimo fulani, kitako chake ni cha eneo fulani, una mwinuko fulani, na una kiasi fulani cha uoto. Hii yote imepangwa na kukokotolewa na Mungu na haitabadilishwa kiholela. Kwa tambarare, idadi kubwa ya binadamu wanaishi katika tambarare, na hakuna mabadiliko ya hali ya hewa yatakayoathiri maeneo yao au thamani ya uwepo wao. Sio hata kile ambacho kimejumuishwa katika mandhari haya na mazingira ya kijiografia ambayo yaliumbwa na Mungu yatabadilika kiholela. Kwa mfano, vipengele vya jangwa ni vipi, ni aina gani ya madini yaliyopo chini ya ardhi, yanajumuisha mchanga kiasi gani na rangi ya mchanga, upana wake—haya hayatabadilika kiholela. Kwa nini hayatabadilika kiholela? Ni kwa sababu ya kanuni ya Mungu na usimamizi Wake. Ndani ya mandhari haya yote tofautitofauti na mazingira ya kijiografia yaliyoumbwa na Mungu, Anasimamia kila kitu kwa njia iliyopangwa na kwa mpangilio. Kwa hiyo mazingira haya yote ya kijiografia bado yapo kwa miaka elfu kadhaa, makumi elfu ya miaka baada ya kuwa yameumbwa na Mungu. Bado yanatimiza kila wajibu wao. Ingawa wakati wa vipindi fulani volkano hulipuka, wakati wa vipindi fulani matetemeko ya ardhi hutokea, na kuna mabadiliko makubwa ya ardhi, hakika Mungu hataruhusu aina yoyote ya mandhari kupoteza kazi yake ya asili. Ni kwa sababu tu ya usimamizi huu unaofanywa na Mungu, utawala Wake na udhibiti wa sheria hizi, kwamba yote haya—yote haya yanayofurahiwa na binadamu na kuonwa na binadamu—yanaweza kuendelea kuishi duniani kwa njia ya mpangilio. Sasa kwa nini Mungu anasimamia mandhari yote haya yaliyopo duniani kwa njia hii? Kusudi ni ili viumbe hai vinavyoendelea kuishi katika mazingira mbalimbali ya kijiografia yote yatakuwa na mazingira imara, na kwamba wataweza kuendelea kuishi na kuongezeka katika mazingira hayo imara. Vitu hivi vyote—vile vinavyotembea na vile ambavyo havitembei, vile ambavyo vinapumua kupitia mapua yao na vile ambavyo havitumii mapua—vinaunda mazingira ya tofauti kabisa kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Ni aina hii tu ya mazingira ndiyo inaweza kulea kizazi baada ya kizazi cha binadamu, na ni aina hii tu ya mazingira inaweza kuruhusu binadamu kuendelea kuishi kwa amani, kizazi baada ya kizazi.

Yale nimetoka tu kuyazungumzia ni mada kubwa kiasi, kwa hivyo labda inaonekana imeondolewa maishani mwenu, lakini naamini nyote mnaweza kuyaelewa, sivyo? Yaani, sheria za Mungu katika utawala wake wa vitu vyote ni muhimu sana—muhimu sana! Je, masharti ya awali ni yapi kwa viumbe vyote kukua ndani ya sheria hizi? Ni kwa sababu ya kanuni ya Mungu. Ni kwa sababu ya kanuni Yake ndipo vitu vyote vinafanya kazi zao ndani ya kanuni Yake. Kwa mfano, milima inalea misitu, halafu misitu inalea na kuwalinda ndege mbalimbali na wanyama wanaoishi ndani yake. Tambarare ni jukwaa lililoandaliwa kwa ajili ya binadamu kupanda mazao vilevile kwa ajili ya ndege na wanyama mbalimbali. Zinaruhusu idadi kubwa ya binadamu kuishi katika ardhi tambarare na kutoa hali isiyo na taabu katika maisha ya binadamu. Na tambarare pia zinajumuisha ukanda wa mbuga—malundo ya ukanda wa mbuga. Ukanda wa mbuga ni uoto wa nchi. Unalinda ardhi na kuwalea ng’ombe, kondoo na farasi wanaoishi katika ukanda wa mbuga. Jangwa pia linafanya kazi yake. Sio sehemu kwa ajili ya binadamu kuishi; jukumu lake ni kufanya hali ya hewa ya unyevunyevu kuwa kavu. Mitiririko ya mito na maziwa kunaleta hali isiyo ya usumbufu kwa ajili ya watu kunywa maji. Mahali popote yanapotiririka, watu watakuwa na maji kwa ajili ya kunywa, na mahitaji ya maji ya vitu vyote yataridhishwa kwa urahisi. Hii ni mipaka iliyochorwa na Mungu kwa ajili ya mandhari mbalimbali.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 181)

Kwa sababu ya mipaka hii ambayo Mungu ameichora, mandhari mbalimbali yamezalisha mazingira tofautitofauti kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi, na mazingira haya kwa ajili ya kuendelea kuishi yamekuwa na hali isiyokuwa na usumbufu kwa ajili ya aina tofautitofauti ya ndege na wanyama na vilevile kuleta nafasi kwa ajili ya kuendelea kuishi. Kutokana na hili, mipaka kwa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa viumbe hai mbalimbali imeendelezwa. Hii ndiyo hoja ya pili tutakayokwenda kuzungumzia baadaye. Kwanza kabisa ni aina gani ya mazingira ambamo ndege na wanyama na wadudu wanaishi? Je, wanaishi katika misitu na vijisitu? Haya ndiyo makazi yao. Kwa hivyo, kando na kuanzisha mipaka kwa ajili ya mazingira mbalimbali ya kijiografia, Mungu pia Aliweka mipaka kwa ajili ya ndege na wanyama, samaki, wadudu mbalimbali, na mimea yote. Pia alianzisha sheria. Kwa sababu ya tofauti za mazingira mbalimbali ya kijiografia na kwa sababu ya uwepo wa mazingira tofauti ya kijiografia, aina tofautitofauti za ndege na wanyama, samaki, wadudu, na mimea vina mazingira tofauti kwa ajili ya kuendelea kuishi. Ndege na wanyama na wadudu wanaishi miongoni mwa mimea, samaki wanaishi majini, na mimea inakua kwenye nchi kavu. Nchi kavu inajumuisha maeneo mbalimbali kama vile milima, tambarare, na vilima. Punde tu ndege na wanyama wanapokuwa na makazi yao yasiyobadilika, hawataweza kuzungukazunguka wakielekea njia yeyote . Makazi yao ni misitu na milima. Ikiwa, siku moja makazi yao yataharibiwa, mpangilio utakuwa machafuko. Mara tu mpangilio huo unapokuwa machafuko, madhara yake ni yapi? Wa kwanza kuumizwa ni akina nani? (Binadamu.) Ni binadamu. Ndani ya sheria na mipaka hii ambayo Mungu ameianzisha, je, mmewahi kuona tukio lolote la ajabu? Kwa mfano, tembo wakitembea jangwani kwa kawaida. Mmewahi kuona tukio hilo? Kama ingekuwa hivyo, lingekuwa ni tukio la ajabu sana, kwa sababu tembo wanaishi msituni, na ni mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliwaandalia. Wana mazingira yao wenyewe kwa ajili ya kuendelea kuishi na wana makazi yao yasiyobadilika, sasa kwa nini watangetange? Je, kuna mtu yeyote ambaye amewahi kuona simba au duma wakitembea ufuoni? Hapana, hamjawahi. Makazi ya simba na duma ni msituni na kwenye milima. Je, kuna mtu yeyote ambaye amewahi kumwona nyangumi au papa wa bahari akiogelea kupitia jangwani? Hakuna ambaye ameona hayo, siyo? Nyangumi na papa makazi yao ni baharini. Katika mazingira ya kuishi ya binadamu, je, kuna watu ambao wanaishi pamoja na dubu wa kahawia? Je, kuna watu ambao siku zote wamezungukwa na tausi au ndege wengineo, ndani au nje ya makazi yao? Je, kuna yeyote ambaye amewahi kuwaona tai au bata bukini wa mwituni wakicheza na tumbili? (Hakuna.) Haya yatakuwa ni matukio ya pekee sana. Sababu Ninazungumza juu ya vitu hivi ambavyo vinaonekana kuwa vya kipekee masikioni mwenu ni kuwafanya muelewe kwamba vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu—haijalishi kama vimewekwa katika sehemu moja au iwapo vinapumua kupitia mapuani—vina sheria zao kwa ajili ya kuendelea kuishi. Zamani kabla Mungu hajaumba viumbe hai hivi Alikuwa ameviandalia makazi yao, mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi. Viumbe hai hivi vilikuwa na mazingira yao yasiyobadilika kwa ajili ya kuendelea kuishi, chakula chao, makazi yao yasiyobadilika, sehemu zao zisizobadilika zinazowafaa kwa ajili ya kuendelea kuishi, maeneo yenye halijoto inayowafaa kwa ajili ya kuendelea kuishi. Kwa njia hiyo wasingezungukazunguka au kuhafifisha hali ya mwanadamu kuendelea kuishi au kuathiri maisha yao. Hivi ndivyo Mungu anavyoongoza vitu vyote, akiwaandalia wanadamu mazingira mazuri kabisa kwa ajili ya kuendelea kuishi. Viumbe hai chini ya vitu vyote kila kimoja kina chakula chao kinachokimu maisha yao wenyewe ndani ya mazingira yao wenyewe kwa ajili ya kuendelea kuishi. Kwa chakula hicho, vinajifunga katika mazingira yao ya asili kwa ajili ya kuendelea kuishi. Katika aina hiyo ya mazingira bado vinaendelea kuishi, kuzaliana, na kuendelea kulingana na sheria za Mungu alizozianzisha kwa ajili yao. Kwa sababu ya aina hizi za sheria, kwa sababu ya majaaliwa ya Mungu, vitu vyote vinaishi kwa upatanifu na wanadamu, na wanadamu huishi pamoja na vitu vyote kwa kutegemeana.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 182)

Mungu aliviumba vitu vyote na akaanzisha mipaka kwa ajili yao; miongoni mwao Akalea aina zote za viumbe hai. Wakati huo, pia Aliandaa mbinu tofauti kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi, hivyo unaweza kuona kwamba binadamu hawana njia moja tu kwa ajili ya kuendelea kuishi. Pia hawana aina moja tu ya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi. Hapo kabla tulizungumza juu ya Mungu kuandaa aina mbalimbali za chakula na vyanzo vya maji kwa ajili ya binadamu, kitu ambacho ni muhimu sana kufanya uhai wa binadamu katika mwili kuendelea. Hata hivyo, miongoni mwa binadamu huyu, sio watu wote wanaishi kwa kula nafaka. Watu wana mbinu tofautitofauti za kuendelea kuishi kwa sababu ya tofauti za mazingira ya kijiografia na mandhari. Mbinu hizi za kuendelea kuishi zote zimeandaliwa na Mungu. Hivyo si binadamu wote wanajihusisha na kilimo. Yaani, si watu wote wanapata chakula chao kwa kulima mazao. Hii ni hoja ya tatu ambayo tutakwenda kuizungumzia. Mipaka imetengenezwa kutokana na mitindo mbalimbali ya maisha ya binadamu. Kwa hiyo ni aina nyingine ipi ya mtindo wa maisha ambayo binadamu wanayo? Kwa suala la vyanzo tofauti vya vyakula, ni aina gani nyingine ya vyakula ambavyo wanadamu wanavyo? Kuna aina za msingi kadhaa.

Ya kwanza ni mtindo wa maisha wa uwindaji. Kila mmoja anajua hiyo ni nini. Watu wanaoishi kwa kuwinda wanakula nini? (Windo.) Wanakula ndege na wanyama wa mwituni. “Windo” ni neno la kisasa. Wawindaji hawaoni kwamba ni mchezo, wanaona kama chakula, kama riziki yao ya kila siku. Kwa mfano, wangepata paa. Wanapopata paa huyu ni sawa tu na mkulima kupata mazao kutoka ardhini. Mkulima hupata mazao kutoka ardhini, na anapoona mazao yake anakuwa na furaha na anahisi amani. Familia haitakuwa na njaa ya mazao ya kula. Moyo wake una amani na anahisi kuridhika. Na mwindaji pia anahisi amani na kuridhika akiangalia kile ambacho amekamata kwa sababu hana haja ya kuwa na wasiwasi tena kuhusu chakula. Kuna kitu cha kula kwa ajili ya mlo unaofuata, hakuna haja ya kuwa na njaa. Huyu ni mtu ambaye anawinda kwa ajili ya kuishi. Wengi wa wale ambao hutegemea uwindaji wanaishi katika misitu ya milima. Hawalimi. Sio rahisi kupata ardhi inayolimika hapo, kwa hiyo wanaishi kwa kutegemea viumbe hai mbalimbali, aina mbalimbali za mawindo. Hii ni aina ya kwanza ya mtindo wa maisha ambao ni tofauti na ule wa watu wa kawaida.

Aina ya pili ni mtindo wa maisha wa ufugaji. Je, wale ambao wanafuga kwa ajili ya kuishi wanalima? (La.) Kwa hiyo sasa wanafanya nini? Wanaishije? (Kwa sehemu kubwa, wanafuga ng’ombe na kondoo kwa ajili ya kuishi, na msimu wa baridi wanawachinja na kuwala mifugo wao. Chakula chao cha msingi ni nyama ya ng’ombe na nyama ya kondoo, na wanakunywa chai ya maziwa. Ingawa wafugaji ni wenye shughuli misimu yote minne, wanakula vizuri. Wana kiwango kikubwa cha maziwa, bidhaa za maziwa, na nyama.) Watu wanaofuga mifugo kwa ajili ya kuishi kimsingi hula nyama ya ng’ombe na nyama ya kondoo, hunywa maziwa ya kondoo na ng’ombe, na wanaendesha madume ya ng’ombe na farasi uwandani na upepo kwenye nywele zao, jua usoni pao. Hawana msongo wa mawazo juu ya maisha ya kisasa. Siku nzima wanaona tu upana wa wingu la bluu na tambarare za majani. Wengi wa watu wanaofuga mifugo kwa ajili ya kuishi wanaishi kwenye uwanda wa mbuga na wanaweza kuendelea na mtindo wao wa maisha ya kuhamahama kwa kizazi baada ya kizazi. Ingawa maisha katika uwanda wa mbuga ni ya upweke kidogo, pia ni maisha ya furaha. Si mtindo mbaya wa maisha!

Aina ya tatu ni mtindo wa maisha ya uvuvi. Kuna sehemu ndogo ya binadamu wanaoishi pembezoni mwa bahari au kwenye visiwa vidogo. Wamezungukwa na maji, wakikabiliana na bahari. Watu hawa huvua kwa ajili ya kuishi. Ni nini chanzo cha chakula kwa wale wanaovua kwa ajili ya kuishi? Vyanzo vyao vya vyakula ni pamoja na aina zote za samaki, vyakula vya baharini, na mazao mengine ya baharini. Watu wanaovua kwa ajili ya kuishi hawalimi mashamba, lakini badala yake wao huenda kuvua kila siku. Chakula chao cha msingi kinajumuisha aina mbalimbali za samaki, na bidhaa za vyakula vya baharini. Mara chache waliweza kubadilishana bidhaa hizi na mchele, unga, na mahitaji ya kila siku. Huu ni mtindo tofauti wa maisha wa watu wanaoishi karibu na maji. Wale wanaoishi karibu na maji wanayategemea kwa ajili ya chakula chao, na uvuvi ni riziki yao. Ni chanzo cha riziki yao vilevile chanzo chao cha chakula.

Licha ya wale ambao hulima kwa ajili ya kuishi, kimsingi kuna aina tatu tofauti za mtindo wa maisha zilizotajwa hapo juu. Licha ya wale ambao wanaishi kwa kutegemea ufugaji, uvuvi, na kuwinda, idadi kubwa ya watu hulima kwa ajili ya chakula. Na watu wanaolima kwa ajili ya kuishi wanahitaji nini? Wanahitaji udongo. Wao wanategemea kupanda mazao kwa vizazi. Haijalishi wanapanda mbogamboga, matunda au nafaka, wanapata chakula chao na mahitaji yao ya kila siku kutoka ardhini.

Masharti ya msingi kwa mitindo tofauti ya maisha ya binadamu ni yapi? Je, hayahitaji utunzaji wa msingi wa mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi? Yaani, ikiwa wale wanaotegemea uwindaji wangepoteza misitu ya milima au ndege na wanyama, chanzo cha riziki yao kingepotea. Mwelekeo ambao kabila hili na watu wa aina hii wanapaswa kuchukua ungekuwa wa mashaka, na hata huenda wakatoweka. Na wale ambao wanafuga kwa ajili ya riziki yao hutegemea nini? Kile ambacho kweli wanakitegemea si mifugo yao, lakini ni mazingira ambayo mifugo wao wanaendelea kuishi—uwanda wa mbuga. Kama kusingekuwa na uwanda wa mbuga, wangelishia wapi mifugo wao? Kondoo na ng’ombe wangekula nini? Bila mifugo, watu wanaohamahama hawangekuwa na riziki. Bila chanzo cha riziki yao, watu hawa wangekwenda wapi? Kuendelea kuishi kungekuwa vigumu sana; wasingekuwa na maisha ya baadaye. Bila vyanzo vya maji, mito na maziwa yangekauka. Je, samaki hao wote wanaotegemea maji kwa ajili ya maisha yao wangeendelea kuwepo? Samaki hao wasingeendelea kuishi. Je, watu hao ambao wanategemea maji na samaki kwa ajili ya riziki yao wangeendelea kuishi? Ikiwa hawakuwa na chakula, ikiwa hawakuwa na chanzo cha riziki zao, watu hao wasingeweza kuendelea kuishi. Yaani, kama kuna tatizo na riziki zao au kuendelea kwao kuishi, jamii hizo zisingeendelea kuwepo. Zisingeweza kuendelea kuishi, na zingeweza kupotea, kufutiliwa mbali kutoka duniani. Na ikiwa wale ambao wanalima kwa ajili ya riziki yao wangepoteza ardhi yao, kama hawangeweza kupanda vitu, na kupata vyakula vyao kutoka kwa mimea mbalimbali, matokeo yake yangekuwa nini? Bila chakula, je, watu wasingekufa kwa njaa? Ikiwa watu wangekufa kwa njaa, je, aina hiyo ya watu isingefutiliwa mbali? Kwa hiyo hili ni kusudi la Mungu katika kudumisha mazingira mbalimbali. Mungu ana kusudi moja tu katika kudumisha mazingira mbalimbali na mifumo ya ikolojia, kudumisha viumbe hai tofautitofauti ndani ya kila mazingira—ni kulea aina zote za watu, kuwalea watu pamoja na maisha katika mazingira ya kijiografia tofautitofauti.

Ikiwa vitu vyote vya uumbaji vingepoteza sheria zao, visingeishi tena; ikiwa sheria za vitu vyote zingekuwa zimepotea, basi viumbe hai miongoni mwa vitu vyote visingeweza kuendelea. Wanadamu pia wangepoteza mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo wanayategemea kwa ajili ya kuendelea kuishi. Ikiwa binadamu wangepoteza hayo yote, wasingeweza kuendelea kuishi na kuongezeka kizazi baada ya kizazi. Sababu ya wanadamu kuendelea kuishi mpaka sasa ni kwa sababu Mungu amewapatia wanadamu viumbe vyote vya uumbaji kuvilea, kuwalea wanadamu kwa namna tofauti. Ni kwa sababu tu Mungu anawalea binadamu kwa namna tofauti ndio maana wameendelea kuishi mpaka sasa, kwamba wameendelea kuishi hadi siku ya leo. Kwa aina hiyo ya mazingira yasiyobadilika kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo ni ya kufaa na yapo katika mpangilio, aina zote za watu duniani, aina zote za jamii zinaweza kuishi ndani ya mawanda yao husika. Hakuna anayeweza kwenda zaidi ya mawanda haya au mipaka hii kwa sababu ni Mungu ambaye ameichora. Kwa nini Mungu aichore kwa namna hii? Hii ni muhimu sana kwa binadamu wote—ni muhimu sana!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 183)

Nne, Mungu alichora mipaka kati ya jamii za rangi tofautitofauti. Duniani kuna watu weupe, watu weusi, watu wa kahawia na watu wa njano. Hawa ni aina tofauti za watu. Mungu pia aliweka mawanda kwa ajili ya maisha ya aina hizi tofauti za watu, na bila kutambua, watu wanaishi ndani ya mazingira yao stahiki kwa kuendelea kuishi chini ya usimamizi wa Mungu. Hakuna anayeweza kwenda nje ya hapa. Kwa mfano, wazungu, ni maeneo gani ambayo wanaishi kwa kiasi kikubwa? Kwa kiasi kikubwa wanaishi Ulaya na Marekani. Watu weusi kimsingi wanaishi Afrika. Na watu wa rangi ya kahawia wanaishi ndani ya eneo gani? Hasa wanaishi Kusini-mashariki mwa Asia na Asia Kusini, kama vile Tailandi, Bara Hindi, Myanmar, Vietnam na Laos. Watu wenye rangi ya hudhurungi kimsingi wanaishi Asia, yaani, China, Japan, Korea ya Kusini na nchi nyinginezo kama hizo. Mungu amegawanya aina hizi tofautitofauti za jamii kwa usawa kiasi kwamba jamii hizi tofautitofauti zimegawanywa katika sehemu tofautitofauti za dunia. Katika sehemu tofautitofauti hizi za dunia, Mungu aliandaa zamani sana mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi yanayofaa kwa ajili ya kila jamii tofauti ya binadamu. Ndani ya aina hizi za mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi, Mungu amewaandalia rangi na vijenzi vya udongo. Kwa maneno mengine, vijenzi katika miili ya watu weupe havifanani na vile vilivyo ndani ya miili ya watu weusi, na pia ni tofauti na vijenzi vya miili ya watu wa jamii nyinginezo. Mungu alipoumba vitu vyote, tayari Alikuwa ameandaa mazingira ya namna hiyo kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa jamii hiyo. Lengo Lake katika hili lilikuwa kwamba pale ambapo aina hiyo ya watu inaanza kuongezeka, watakapoanza kuongezeka kwa idadi, wangeweza kuwekwa ndani ya mawanda hayo. Kabla Mungu hajawaumba binadamu alikuwa amekwishatafakari yote—Angeweza kutoa Ulaya na Amerika kwa watu weupe na kuwaruhusu kuliendeleza na kuendelea kuishi. Kwa hiyo Mungu alipokuwa anatengeneza dunia tayari Alikuwa na mpango, alikuwa na nia na kusudi katika kile alichokuwa anakiweka katika kipande hicho cha ardhi, na kile ambacho kingelelewa katika kipande hicho cha ardhi. Kwa mfano, Mungu zamani sana aliandaa mlima upi, tambarare ngapi, vyanzo vya maji vingapi, ni aina gani ya ndege na wanyama, samaki gani, na mimea gani ingeweza kuwepo katika ardhi hiyo. Alipokuwa anaandaa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa ajili ya aina ya binadamu, kwa ajili ya jamii, Mungu aliangalia vipengele vingi vya masuala: mazingira ya kijiografia, vijenzi vya udongo, aina ya ndege na wanyama, ukubwa wa aina tofautitofauti za samaki, vijenzi katika samaki, ubora tofauti wa maji, vilevile aina tofauti za mimea…. Mungu alikuwa ameandaa yote hayo zamani sana. Mazingira ya aina hiyo ni mazingira ya asili kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyaumba na kuyaandaa kwa ajili ya watu weupe na kwa hivyo ni yao kiasili. Mmeweza kuona kwamba Mungu alipoviumba vitu vyote Alitafakari sana na Alitenda kwa mpango? (Ndiyo, tumeona kwamba fikira za Mungu kwa aina mbalimbali za watu zilikuwa ni za uangalifu sana. Kwa mazingira aliyoyaumba kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa ajili ya aina tofautitofauti za binadamu, aliandaa aina za ndege na wanyama na aina za samaki, milima mingapi na tambarare ngapi zitakuwepo. Yote haya yalifikiriwa kwa uangalifu sana na kwa usahihi.) Kwa mfano, vyakula wanavyokula wazungu hasa ni vipi? Vyakula ambavyo watu weupe wanakula ni tofauti sana na vyakula ambavyo watu wa Asia wanakula. Vyakula vikuu ambavyo watu weupe wanakula hasa ni nyama, mayai, maziwa, na kuku. Nafaka kama vile mkate na mchele kwa ujumla sio chakula kikuu ambacho kinawekwa pembeni mwa sahani. Hata pale wanapokula kachumbari ya mboga, wanaweka kiasi cha nyama ya kukaanga au kuku ndani yake. Hata kama wanakula vyakula vinavyotokana na ngano, wanaongeza siagi, mayai, au nyama kwenye chakula hicho. Hiyo ni kusema, vyakula vyao vikuu havijumuishi hasa vyakula vinavyotokana na ngano au mchele; wanakula sana nyama na siagi. Mara nyingi wanakunywa maji ya barafu kwa sababu wanakula vyakula vyenye kalori ya juu sana. Kwa hiyo watu weupe ni wenye afya kweli. Hivi ndivyo vyanzo vya maisha yao, mazingira yao kwa ajili ya kuishi yaliandaliwa na Mungu kwa ajili yao, yanawafanya wawe na aina hiyo ya mtindo wa maisha. Mtindo huo wa maisha ni tofauti na mitindo ya maisha ya watu wa jamii nyingine. Hakuna baya au zuri katika mtindo huu wa maisha—ni wa kuzaliwa, uliamuliwa kabla na Mungu na kwa sababu ya kanuni ya Mungu na mipangilio Yake. Aina hii ya mbari ina mtindo fulani wa maisha na vyanzo fulani vya riziki zao kitu ambacho ni kwa sababu ya mbari yao, vilevile ni kwa sababu ya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi yaliyoandaliwa na Mungu kwa ajili yao. Mngeweza kusema kwamba mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyaandaa kwa ajili ya watu weupe na chakula cha kila siku wanachokipata kutoka katika mazingira hayo ni kingi na kimejaa tele.

Mungu pia aliandaa mazingira yanayofaa kwa ajili ya mbari nyingine kuendelea kuishi. Pia kuna watu weusi—watu weusi wanapatikana wapi? Hasa wanapatikana katikati na kusini mwa Afrika. Mungu aliwaandalia nini kwa ajili ya kuishi katika aina hiyo ya mazingira? Misitu ya kitropiki, aina zote za ndege na wanyama, pia majangwa, na aina zote za mimea ambayo inaambatana nao. Wana vyanzo vya maji, riziki zao, na chakula. Mungu hakuwabagua. Bila kujali kile walichowahi kukifanya, kuendelea kuishi kwao hakujawahi kuwa tatizo. Pia wanachukua mahali fulani maalumu na eneo fulani katika sehemu ya dunia.

Sasa, hebu tuzungumze kidogo kuhusu watu wa njano. Watu wa njano hasa wanapatikana nchi za Mashariki. Kuna tofauti gani kati ya mazingira na sehemu za kijiografia za nchi za Mashariki na nchi za Magharibi? Katika nchi za Mashariki, eneo kubwa la ardhi ni la rutuba, na zina hazina kubwa ya vitu na madini. Yaani, aina zote za rasilimali za juu ya ardhi na za chini ya ardhi zimejaa tele. Na kwa kundi hili la watu, kwa mbari hii, Mungu pia aliandaa udongo, hali ya hewa inayofanana nao, na mazingira mbalimbali ya kijiografia ambayo yanawafaa. Ingawa kuna tofauti kubwa kati ya mazingira hayo ya kijiografia na mazingira ya nchi za Magharibi, chakula cha lazima cha watu, riziki, na vyanzo kwa ajili ya kuendelea kuishi viliandaliwa na Mungu. Ni mazingira tofauti tu kwa ajili ya kuishi kuliko yale ambayo watu weupe wanayo katika nchi za Magharibi. Lakini ni kitu kipi kimoja ambacho Ninahitaji kuvuta usikivu wenu, ambacho Ninahitaji kuwaambia? Idadi ya mbari ya Mashariki kiasi fulani ni kubwa, hivyo Mungu aliongeza vipengele vingi katika kipande hicho cha ardhi ambavyo ni tofauti na vya Magharibi. Katika upande huo wa dunia, Aliongeza mandhari mengi mbalimbali na aina zote za vitu vingi. Huko rasilimali za asili ni tele; mandhari pia yanatofautiana na anuwai, yanatosha kwa ajili ya kulea idadi kubwa ya mbari ya Mashariki. Kitu fulani ambacho ni tofauti na Magharibi ni kwamba Mashariki—kutoka kusini kwenda kaskazini, kutoka mashariki kwenda magharibi—hali ya hewa ni nzuri kuliko ya Magharibi. Misimu minne imeoneshwa kinaganaga, hali ya joto ni nzuri, rasilimali za asili zipo tele, mazingira ya asili na aina za mandhari ni mazuri zaidi kuliko ya Magharibi. Kwa nini Mungu alifanya hivi? Mungu alitengeneza uwiano razini kabisa kati ya watu weupe na watu wa njano. Hii inamaanisha nini? Inamaanisha kuwa kila kipengele cha chakula chao, vitu ambavyo wanatumia, kile ambacho watu weupe wanacho cha kujifurahisha ni kizuri zaidi kuliko kile ambacho watu wa njano wanaweza kukifurahia. Hata hivyo, Mungu habagui mbari yoyote. Mungu aliwapatia watu wa njano mazingira mazuri na bora zaidi kwa ajili ya kuendelea kuishi. Hii ni uwiano.

Mungu amjalia kabla ni aina gani ya watu wanastahili kuishi katika sehemu ipi ya dunia; je, wanadamu wanaweza kupita hii mipaka? (La.) Kitu cha ajabu kweli! Hata kama kuna vita au uvamizi katika enzi mbalimbali au nyakati fulani, vita hivi, uvamizi huu, hakika hauwezi kuharibu mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyaamua kabla kwa ajili ya kila mbari. Yaani, Mungu amewaweka aina fulani ya watu katika eneo fulani la dunia na hawawezi kwenda nje ya mawanda hayo. Hata kama watu wana lengo la kubadilisha au kuongeza eneo lao, bila ruhusa ya Mungu, hii itakuwa vigumu sana kufanikiwa. Itakuwa vigumu sana kufanikiwa. Kwa mfano, watu weupe walitaka kuongeza maeneo yao na wakazitawala kwa mabavu baadhi ya nchi. Wajerumani walivamia baadhi ya nchi, Uingereza waliitwaa India. Matokeo yalikuwa ni nini? Mwishowe walishindwa. Tunaona nini kutokana na kushindwa huku? Kile ambacho Mungu amekiamua kabla hakiwezi kuharibiwa. Kwa hiyo, haijalishi ni nguvu kubwa kiasi gani ambayo umeweza kuiona katika upanuzi wa Uingereza, mwishowe walitakiwa bado kuondoka, na kuacha ardhi hiyo ikiwa bado ni ya India. Wale ambao wanaishi katika ardhi hiyo bado ni Wahindi, na si Waingereza. Hii ni kwa sababu ni kitu ambacho Mungu haruhusu. Baadhi ya wale ambao wanatafiti historia au siasa wametoa tasnifu juu ya hili. Wanatoa sababu kwa nini Uingereza ilishindwa, wanasema kwamba pengine ilikuwa ni kwa sababu mbari fulani isingeweza kushindwa, au pengine ni kwa sababu ya sababu nyinginezo za kibinadamu.… Hizi sio sababu za kweli. Sababu ya kweli ni kwa sababu ya Mungu—Haruhusu hilo! Mungu anaamua mbari waishi katika nchi fulani na Anawaweka hapo, na kama Mungu hawaruhusu kuhama hawataweza kuhama kamwe. Ikiwa Mungu ataamua mawanda kwa ajili yao, wataishi ndani ya mawanda hayo. Binadamu hawezi kuvunja bure au kwenda nje ya mawanda haya. Hii ni hakika. Haijalishi nguvu za wavamizi ni kubwa kiasi gani, au jinsi gani wale wanaovamiwa ni dhaifu, mafanikio yao mwishowe yanamtegemea Mungu. Ameshaliamua hili tayari na hakuna anayeweza kulibadilisha.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 184)

Tukiangalia kwa mtazamo wa sheria zilizoamriwa na Mungu kwa ukuaji wa vitu vyote, yote hii si kwa ajili ya mwanadamu, haijalishi ni wa aina gani, anaishi chini ya uangalizi wa Mungu—je, wote hawaishi chini ya malezi Yake? Ikiwa sheria hizi zingeharibiwa au Mungu hakuanzisha aina hizi za sheria kwa ajili ya binadamu, majaliwa yao yangekuwa ni nini? Baada ya binadamu kupoteza mazingira yao ya msingi kwa ajili ya kuendelea kuishi, je, wangekuwa na chanzo chochote cha chakula? Inawezekana kwamba vyanzo vya chakula vingekuwa tatizo. Ikiwa watu wangepoteza vyanzo vyao vya chakula, yaani, ikiwa hawangeweza kupata kitu chochote cha kula, ni siku ngapi wangeweza kuvumilia? Pengine wasingeweza kuvumilia hata kwa mwezi mmoja, na kuendelea kuishi kwao kungekuwa ni tatizo. Kwa hiyo kila kitu ambacho Mungu anafanya kwa ajili ya watu kuendelea kuishi, kwa ajili ya wao kuendelea kuwepo, kuongezeka, na ruzuku ni muhimu sana. Kila kitu ambacho Mungu anafanya miongoni mwa vitu vyote vinahusiana kwa karibu na haviwezi kutenganishwa na watu kuendelea kuishi. Ikiwa kuendelea kuishi kwa binadamu kulikuwa tatizo, je, usimamizi wa Mungu ungeweza kuendelea? Je, usimamizi wa Mungu bado ungekuwepo? Usimamizi wa Mungu unakwenda sambamba na kuendelea kuishi kwa binadamu wote ambao Anawalea, kwa hivyo haijalishi Mungu anaandaa kitu gani kwa ajili ya vitu vyote na kile Anachofanya kwa ajili ya binadamu, hii yote ndiyo lazima Kwake, na ni muhimu sana kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Ikiwa sheria zote hizi ambazo Mungu aliziamua kwa ajili ya vitu vyote zingekuwa zimeachwa, ikiwa sheria hizi zingekuwa zimevunjwa au zimeharibiwa, vitu vyote visingeweza kuwepo, mazingira ya binadamu ya kuendelea kuwepo yasingekuwepo, na wala riziki zao za kila siku, na wala wao wenyewe. Kwa sababu hii, Usimamizi wa Mungu wa wokovu wa binadamu wala nao usingekuwepo pia.

Kila kitu ambacho tumejadili, kila kitu, kila kipengele kimeungana kikamilifu na kuendelea kuishi kwa kila mtu. Mnaweza kusema, “Unachokizungumzia ni kikubwa sana, hatuwezi kukiona,” na pengine kuna watu ambao wangeweza kusema “Unachokizungumzia hakinihusu.” Hata hivyo, usisahau kwamba unaishi kama sehemu tu ya vitu vyote; wewe ni mshirika wa vitu vyote ndani ya kanuni ya Mungu. Vitu vyote haviwezi kutenganishwa na kanuni ya Mungu, na hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kujitenganisha kwenye kanuni Yake. Kupoteza kanuni Yake na kupoteza uangalizi wake kungekuwa na maana kwamba maisha ya watu, maisha ya watu katika mwili yangetoweka. Huu ndio umuhimu wa Mungu kuanzisha mazingira kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Haijalishi wewe ni mbari gani au unaishi katika ardhi gani, iwe ni Magharibi au Mashariki—huwezi kujitenganisha na mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu ameyaanzisha kwa ajili ya binadamu, na huwezi kujitenga na malezi na uangalizi wa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Ameyaanzisha kwa ajili ya binadamu. Haijalishi riziki yako ni nini, kile unachokitegemea kwa ajili ya kuishi, na kile unachokitegemea kudumisha uhai wako katika mwili, huwezi kujitenganisha na kanuni ya Mungu na usimamizi wake. Baadhi ya watu wanasema: “Mimi sio mkulima, sipandi mazao kwa ajili ya kuishi. Sitegemei mbingu ili nipate chakula changu, kwa hiyo siendelei kuishi katika mazingira ambayo aliyaanzisha Mungu kwa ajili ya kuendelea kuishi. Aina hiyo ya mazingira haijanipatia kitu chochote.” Hii ni kweli? Unasema kwamba hupandi mazao kwa ajili ya kuishi, lakini huli nafaka? Huli nyama na mayai? Je, huli mbogamboga na matunda. Kila kitu unachokula, vitu hivi vyote unavyovitaka havitenganishwi na mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi yaliyoanzishwa na Mungu kwa ajili ya binadamu. Na chanzo cha kila kitu ambacho binadamu anahitaji hakiwezi kutenganishwa na vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, aina hizo za mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi. Maji unayokunywa, nguo unazovaa, na vitu vyote unavyotumia—ni kitu gani kati ya hivi ambacho hakipatikani kutoka katika vitu hivi vyote? Baadhi ya watu husema: “Kuna baadhi ya vitu ambavyo havipatikani kutoka katika vitu vyote hivi. Unaona, plastiki haitokani na vitu vyote hivi. Ni kitu cha kemikali, kitu kilichotengenezwa na mwanadamu.” Hii ni sahihi? Plastiki imetengenezwa na mwanadamu, ni kitu cha kemikali, lakini vijenzi asilia vya plastiki vilitoka wapi? Vijenzi asilia vilipatikana kutoka katika vitu ambavyo kwa asili vilitengenezwa na Mungu. Vitu ambavyo unavifurahia, ambavyo unaona, kila kitu ambacho unatumia, vyote vinapatikana kutoka katika vitu vyote ambavyo vilitengenezwa na Mungu. Hiyo ni sawa na kusema, haijalishi ni mbari gani, haijalishi ni riziki gani, au ni katika aina gani ya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo watu wanaishi, hawawezi kujitenganisha na uangalizi wa Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 185)

Vyovyote vile uelewa juu ya Mungu ulivyo mkubwa katika mioyo ya watu, unaamua nafasi kubwa kiasi gani Anachukua katika mioyo yao. Vyovyote vile kiwango cha maarifa ya Mungu kilivyo katika mioyo yao ndivyo kwa kiwango kikubwa Mungu alivyo katika mioyo yao. Ikiwa Mungu unayemfahamu yupo tupu na ni yule asiye yakini, basi yule Mungu unayemwamini pia ni tupu na ni yule asiye yakini. Mungu unayemfahamu anaishia ndani ya mipaka ya upeo wa maisha yako binafsi, na hahusiani na Mungu wa kweli Mwenyewe. Kwa hiyo, kuyajua matendo ya Mungu, kuujua uhalisi wa Mungu na uweza Wake, kuujua utambulisho wa kweli wa Mungu Mwenyewe, kujua kile Anacho na alicho kujua kile Alichokuonyesha miongoni mwa vitu vyote—haya ni muhimu sana kwa kila mtu anayetafuta maarifa ya Mungu. Haya yana uhusiano wa moja kwa moja na iwapo watu wanaweza kuingia kwa uhalisi wa ukweli. Ikiwa unauwekea mipaka uelewa wako juu ya Mungu katika maneno tu, ikiwa unauwekea mipaka uelewa wako mdogo tu, Neema ya Mungu unayoihesabu, au shuhuda zako ndogo kwa Mungu, basi Ninasema kwamba yule Mungu unayemwamini si Mungu Mwenyewe wa kweli kabisa, na inaweza pia kusemwa kuwa Mungu unayemwamini ni Mungu wa fikira tu, si Mungu wa kweli. Hii ni kwa sababu Mungu wa kweli ni Yule ambaye Anatawala kila kitu, ambaye Anatembea miongoni mwa kila kitu, ambaye Anasimamia kila kitu. Yeye ndiye Anashikilia majaliwa ya binadamu wote—ambaye anashikilia majaliwa ya kila kitu. Kazi na matendo ya Mungu ambaye Ninamzungumzia hayaishii kwa sehemu ndogo tu ya watu. Yaani, haiishii tu kwa watu tu ambao sasa wanamfuata. Matendo Yake yameonyeshwa miongoni mwa vitu vyote, katika vitu vyote kuendelea kuishi, na katika sheria za mabadiliko ya vitu vyote.

Kama huwezi kuona au kutambua matendo yoyote ya Mungu kati ya vitu vyote, basi huwezi kutoa ushuhuda kwa matendo Yake yoyote. Ikiwa huwezi kuwa na ushuhuda wowote kwa Mungu, ikiwa unaendelea kuzungumza juu ya huyo anayeitwa Mungu mdogo ambaye unamfahamu, Mungu huyo ambaye anaishia kwenye mipaka ya mawazo yako tu, na yupo ndani ya akili yako finyu, ikiwa unaendelea kuzungumza juu ya aina hiyo ya Mungu, basi Mungu hataisifu imani yako. Unapokuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu, ikiwa unatumia tu jinsi unavyofurahia neema ya Mungu, kukubali adhabu na kurudi Kwake, na kufurahia baraka Zake katika ushuhuda wako Kwake, ambao kwa kiasi kikubwa hautoshi na hauwezi kumridhisha. Ikiwa unataka kuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu kwa namna ambayo inakubaliana na mapenzi Yake, kuwa na ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe wa kweli, basi unapaswa kuona kile Mungu anacho na alicho kutokana na matendo Yake. Unapaswa kuona mamlaka ya Mungu kutoka katika udhibiti Wake wa kila kitu, na kuona ukweli wa jinsi Anavyowakimu binadamu wote. Ikiwa unakiri tu kwamba chakula chako cha kila siku na kinywaji na mahitaji yako katika maisha yanatoka kwa Mungu, lakini huoni ukweli kwamba Mungu anawakimu binadamu wote kwa njia ya vitu vyote, kwamba anawaelekeza wanadamu, basi hutaweza kamwe kuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu. Lengo Langu la kusema haya yote ni lipi? Iko hivyo ili usiweze kulichukulia hili kirahisi, ili msiamini kwamba mada hizi Nilizozizungumzia hazina uhusiano na kuingia kwenu binafsi katika maisha, na ili msichukue mada hizi kama tu aina ya maarifa au mafundisho. Ikiwa unasikiliza ukiwa na mtazamo kama huo, hutapata kitu hata kimoja. Mtapoteza fursa kubwa hii ya kumjua Mungu.

Lengo Langu la kuzungumza juu ya mambo haya yote ni nini? Lengo langu ni kuwafanya watu wamjue Mungu, kuwafanya watu waelewe matendo halisi ya Mungu. Mara utakapomuelewa Mungu na ukaelewa matendo Yake, ni baada ya hapo tu ndipo utakuwa na fursa au uwezekano wa kumjua Mungu. Kwa mfano, ikiwa unataka kumwelewa mtu, ni jinsi gani unaweza kumwelewa? Je, inaweza kuwa kupitia kuangalia umbo lao la nje? Je, inaweza kuwa kupitia kile wanachokivaa, jinsi wanavyovaa? Je, inaweza kuwa ni kupitia kuangalia jinsi wanavyotembea? Je, inaweza kuwa ni kupitia kuangalia mawanda ya maarifa yao? (Hapana.) Kwa hiyo unamwelewaje mtu? Unafanya hukumu kupitia maneno na tabia ya mtu, kupitia mawazo zake, kupitia kile anachokionyesha na kile anachokifichua. Hivyo ndivyo unavyomjua mtu, unavyomwelewa mtu. Kwa njia ile ile, ikiwa mnahitaji kumjua Mungu, ikiwa mnataka kuelewa upande Wake wa vitendo, upande Wake wa kweli, mnapaswa kumjua Yeye kupitia matendo Yake na kupitika kila kitu halisi Anachofanya. Hii ndiyo njia bora zaidi na ndiyo njia pekee.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 186)

Mungu alipoumba vitu vyote, alitumia aina zote za mbinu na njia za kuziwekea uwiano, kuweka uwiano katika mazingira ya kuishi kwa ajili ya milima na maziwa, kuweka uwiano katika mazingira ya kuishi kwa ajili ya mimea na aina zote za wanyama, ndege, wadudu—lengo Lake lilikuwa ni kuruhusu aina zote za viumbe hai kuishi na kuongezeka ndani ya sheria ambazo alikuwa Amezianzisha. Hakuna hata kimoja katika viumbe wote kinachoweza kwenda nje ya sheria, na sheria haziwezi kuvunjwa. Ni ndani ya aina hii tu ya mazingira ya msingi ndipo binadamu wanaweza kuendelea kuishi kwa usalama na kuongezeka, kizazi baada ya kizazi. Ikiwa kiumbe yeyote anakwenda zaidi ya ukubwa au mawanda yaliyoanzishwa na Mungu, au ikiwa anazidi kiwango cha ukuaji, marudio, au idadi chini ya utawala Wake, mazingira ya binadamu kwa ajili ya kuendelea kuishi yangepata uharibifu wa viwango vinavyotofautiana. Na wakati uo huo, kuendelea kuishi kwa binadamu kungetishiwa. Ikiwa aina moja ya kiumbe hai ni kubwa sana kwa idadi, itawanyang’anya watu chakula chao, kuharibu vyanzo vya maji ya watu, na kuharibu makazi yao. Kwa njia hiyo, kuzaliana kwa binadamu au hali ya kuendelea kuishi ingeathiriwa mara moja. Kwa mfano, maji ni muhimu sana kwa vitu vyote. Ikiwa kuna idadi kubwa sana ya panya, siafu, nzige, na vyura, au wanyama wengine wa kila aina, watakunywa maji zaidi. Kadri kiwango cha maji wanachokunywa kinaongezeka, ndani ya mawanda haya yasiyobadilika ya vyanzo vya maji ya kunywa na maeneo ya majimaji, maji ya kunywa ya watu na vyanzo vya maji vitapungua, na watapungukiwa maji. Ikiwa maji ya kunywa ya watu yataharibiwa, kuchafuliwa au kukatwa kwa sababu aina zote za wanyama zimeongezeka kwa idadi, chini ya aina hiyo ya mazingira katili kwa ajili ya kuendelea kuishi, kuendelea kuishi kwa binadamu hakika kutakuwa kumetishiwa vikali. Ikiwa kuna aina moja au aina kadhaa za viumbe hai ambavyo vinazidi idadi yao inayofaa, hewa, halijoto, unyevunyevu, na hata vijenzi vya hewa ndani ya eneo la binadamu kwa ajili ya kuendelea kuishi litakuwa na sumu na kuharibiwa kwa viwango vinavyotofautiana. Hali kadhalika, chini ya mazingira haya, kuendelea kuishi kwa binadamu na hatma bado vitakuwa chini ya tishio la aina hiyo ya mazingira. Kwa hiyo, ikiwa watu watapoteza uwiano huu, hewa wanayovuta itaharibiwa, maji wanayokunywa yatachafuliwa, na halijoto ambayo wanahitaji pia itabadilika, itaathiriwa kwa viwango tofautitofauti. Ikiwa hiyo itatokea, mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo kiasili ni ya wanadamu yataandamwa na madhara na changamoto kubwa. Chini ya aina hii ya mazingira ambapo mazingira ya msingi ya binadamu kwa ajili ya kuendelea kuishi yameharibiwa, hatma na matarajio ya binadamu yatakuwa ni nini? Ni tatizo kubwa sana! Kwa sababu Mungu anajua vitu vyote ni nini kwa binadamu, wajibu wa kila aina ya kitu Alichokiumba, aina gani ya athari kinacho kwa watu, na faida kubwa kiasi gani kinaleta kwa binadamu—katika moyo wa Mungu kuna mpango kwa ajili ya haya yote na Anasimamia kila kipengele cha vitu vyote alivyoviumba, kwa hiyo kwa binadamu, kila kitu Anachofanya ni muhimu sana—vyote ni lazima. Kwa hiyo wakati unaona baadhi ya matukio ya kiikolojia miongoni mwa vitu vyote, au baadhi ya sheria za asili miongoni mwa vitu vyote, hutashuku tena ulazima wa kila kitu ambacho kiliumbwa na Mungu. Hutatumia tena maneno ya kijinga kufanya hukumu zisizokuwa na msingi juu ya mipangilio ya Mungu juu ya vitu vyote na njia zake mbalimbali za kuwakimu binadamu. Pia hutafanya mahitimisho yasiyokuwa na msingi juu ya sheria za Mungu kwa ajili ya vitu vyote ambavyo Aliviumba.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 187)

Kwa ulimwengu yakinifu, watu wakikosa kuelewa vitu au jambo fulani, wanaweza kutafuta taarifa mwafaka, vinginevyo wanaweza kutumia njia mbalimbali kubaini asili ya habari kuvihusu. Lakini inapokuja kwa ulimwengu huu mwingine ambao tunauzungumzia leo—ulimwengu wa kiroho ulio nje ya ulimwengu yakinifu—watu hawana hasa mbinu au njia za kujifunzia chochote kuuhusu. Mbona Ninasema hivi? Kwa sababu, katika ulimwengu wa mwanadamu, kila kitu cha ulimwengu yakinifu hakijitengi na uwepo wa kimwili wa mwanadamu, na kwa sababu watu wanahisi kwamba kila kitu katika ulimwengu yakinifu hakitenganishwi na maisha yao ya kimwili na uhai wao wa kimwili, watu wengi wanafahamu tu kuhusu, au kuona, vitu yakinifu mbele ya macho yao, vitu vinavyoonekana kwao. Bali inapokuja katika ulimwengu wa kiroho—yaani, kila kilicho cha ule ulimwengu mwingine—ni haki kusema kuwa watu wengi hawaamini. Kwa sababu watu hawawezi kuuona, wanaamini kuwa hakuna haja ya kuuelewa au kujua kitu chochote kuuhusu, sembuse jinsi ulimwengu wa kiroho ni ulimwengu tofauti kabisa na ulimwengu yakinifu na kutoka kwa mtazamo wa Mungu, uko wazi—ingawa kwa wanadamu, ni wa siri na umefungwa—kwa hivyo watu huona ikiwa vigumu sana kupata njia ya kuelewa vipengele mbalimbali vya ulimwengu huu. Vipengele tofauti ambavyo nitazungumzia kuhusu ulimwengu wa kiroho vinahusu utawala na ukuu wa Mungu tu. Sifichui miujiza, wala Siwaambii siri zozote mnazotaka kugundua, kwani hili linahusu ukuu wa Mungu, utawala wa Mungu, na riziki ya Mungu, na kwa hivyo Sitazungumzia tu sehemu ambayo ni muhimu nyinyi kuijua.

Kwanza, hebu Niwaulize swali: katika mawazo yenu, ulimwengu wa kiroho ni nini? Kuzungumza kwa ujumla, ni ulimwengu ulio nje ya ulimwengu yakinifu, ambao hauonekani na haushikiki na watu. Lakini kwa fikra zenu, ulimwengu wa kiroho unafaa uwe ulimwengu wa aina gani? Pengine, kwa sababu ya kutoweza kuuona, mnaweza kushindwa kuufikiria. Lakini mtakaposikia hadithi kuuhusu, bado mtafikiri, hamtaweza kujizuia nyinyi wenyewe. Na kwa nini Ninasema hili? Kuna kitu kinachowatokea watu wengi wanapokuwa wachanga: mtu akiwasimulia hadithi ya kuogofya—juu ya mazimwi, na roho—wanaogopeshwa kabisa. Na kwa nini wanaogopeshwa? Ni kwa kuwa wanavifikiria vitu hivyo; hata japo hawawezi kuviona, wanahisi kuwa vipo kila pembe ya chumba chao, vimejificha sehemu fulani, au sehemu fulani yenye giza, na wanaogopa sana kiasi kwamba hawawezi kuthubutu kulala. Hasa wakati wa usiku, hawathubutu kuwa chumbani peke yao, au uani peke yao. Huo ndio ulimwengu wa kiroho wa fikra zenu, na ni ulimwengu ambao watu hudhani unaogofya. Kwa kweli, kila mtu ana fikra fulani, na kila mtu anaweza kuhisi kitu.

Ulimwengu wa kiroho ni nini? Hebu Niwape maelezo mafupi na rahisi. Ulimwengu wa kiroho ni sehemu muhimu, ambayo ni tofauti na ulimwengu yakinifu. Na mbona Ninasema kwamba ni muhimu? Tutalizungumzia hili kwa kina. Uwepo wa huu ulimwengu wa kiroho umeungana na ulimwengu yakinifu wa mwanadamu kwa njia isiyoweza kufumbulika. Una jukumu katika mzunguko wa uhai na mauti wa mwanadamu katika utawala wa Mungu juu ya vitu vyote; hili ndilo jukumu lake, na sababu mojawapo inayofanya uwepo wake kuwa muhimu. Kwa sababu ni mahali ambapo hapawezi kutambuliwa kwa milango mitano ya fahamu ya mwanadamu, hakuna anayeweza kubaini kwa hakika kuwepo au kutokuwepo kwake. Shughuli za ulimwengu wa kiroho zimeunganika kikamilifu na uwepo wa mwanadamu, na kwa sababu hiyo mpango wa maisha ya wanadamu pia unaathiriwa kwa kiwango kikubwa na ulimwengu wa kiroho. Je, hili linahusiana na ukuu wa Mungu? Linahusiana. Nisemapo hili, unaelewa ni kwa nini Ninajadili mada hii; Kwa sababu inahusu ukuu wa Mungu, na utawala Wake. Katika ulimwengu kama huu—ulimwengu ambao hauonekani kwa watu—kila sheria yake ya peponi, amri na mfumo wake wa utawala ni wa juu zaidi kuliko sheria na mifumo ya nchi yoyote katika ulimwengu yakinifu, na hakuna kiumbe aishiye katika ulimwengu huu anaweza kuzivunja au kujitwalia bila haki. Je, hili linahusiana na ukuu na utawala wa Mungu? Katika ulimwengu huu kuna amri wazi za utawala, sheria wazi za mbinguni, na masharti wazi. Katika viwango tofauti na katika mawanda tofauti, wasimamizi huzingatia kikamilifu katika wajibu wao na kufuata sheria na masharti, kwa kuwa wanajua matokeo ya kukiuka sheria ya mbinguni ni yapi, wanafahamu wazi jinsi ambavyo Mungu anaadhibu maovu na kutuza mazuri, na kuhusu jinsi Anavyoviendesha vitu vyote, jinsi Anavyotawala vitu vyote, na zaidi, wanaona wazi ni jinsi gani Mungu anaendesha sheria za mbinguni na masharti Yake. Je, hizi ni tofauti na ulimwengu yakinifu unaokaliwa na wanadamu? Ni tofauti kwa kiasi kikubwa. Ni ulimwengu ambao ni tofauti kabisa na ulimwengu yakinifu. Kwa kuwa kuna sheria na masharti ya mbinguni, inahusu ukuu wa Mungu, utawala, aidha, tabia ya Mungu ya kile Anacho na alicho. Baada ya kusikia hili, hamhisi kwamba ni muhimu sana Mimi kuzungumzia hii mada? Hamtaki kujifunza siri zilizomo? (Ndiyo, tunataka.) Hiyo ndiyo dhana ya ulimwengu wa kiroho. Japo unapatikana sambamba na ulimwengu yakinifu, na wakati ule ule ukiwa chini ya utawala na ukuu wa Mungu, utawala na ukuu wa Mungu ya huu ulimwengu ni makali zaidi kuliko ulivyo ulimwengu yakinifu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 188)

Miongoni mwa wanadamu, Ninawaainisha watu katika aina tatu. Aina ya kwanza ni wasioamini, wale wasio na imani za kidini. Wanaitwa wasioamini. Wengi wa wasioamini wanaamini tu katika pesa, wanatafuta tu maslahi yao wenyewe, wana tamaa ya vitu, na wanaamini katika ulimwengu yakinifu, si katika mzunguko wa uhai na mauti au katika semi za miungu na mapepo. Ninawaainisha kama wasioamini na ni wa aina ya kwanza. Aina ya pili ni watu mbalimbali wenye imani tofauti na wasioamini. Miongoni mwa wanadamu, Ninawagawa hawa wenye imani katika aina kuu kadhaa: Ya kwanza ni Wayahudi, wa pili ni Wakatoliki, ya tatu ni Wakristo, ya nne ni Waislamu, na ya tano ni wafuasi wa Budha—kuna aina tano. Hizi ndizo aina mbalimbali za watu wenye imani. Aina ya tatu ni wale wanaomwamini Mungu, inayohusiana nanyi. Waumini kama hawa ni wale wanaomfuata Mungu leo. Hawa watu wamegawanyika katika aina mbili. Wateule wa Mungu na watendaji huduma. Hizi aina kuu zimebainishwa wazi. Basi sasa, akilini mwenu mnaweza kutofautisha wazi aina na madaraja ya binadamu, siyo? Ya kwanza ni wasioamini—nimesema wasioamini ni watu gani. Je, wale wanaomwamini Mtu Mzee aliye Angani wanahesabika kama wasioamini? Wengi wa wasioamini wanamwamini yule Mzee aliye Angani; wanaamini kuwa upepo, mvua na radi, na kadhalika vyote vinadhibitiwa na huyu mtu ambaye wanamtegemea kwa upanzi wa mimea na uvunaji wa mazao—lakini wakati imani katika Mungu inatajwa, hawataki kumwamini. Je, hii yaweza kuitwa imani katika Mungu? Watu kama hao wanahesabiwa katika wasioamini. Mnaelewa hili, siyo? —Msifahamu visivyo vikundi hivi. Aina ya pili ni watu wa imani. Aina ya tatu ni wale wanaomfuata Mungu leo. Na kwa nini Nimewagawa wanadamu wote katika aina hizi? (Kwa sababu aina kadhaa za watu wana vituo na hatima tofautitofauti.) Hicho ni kipengele kimoja. Kwa sababu, wakati haya matabaka na aina mbalimbali za watu wanarudi katika ulimwengu wa kiroho, kila mmoja atakuwa na sehemu tofauti ya kuenda, watapitia sheria ya mzunguko tofauti wa uhai na mauti na hii ndiyo sababu Nimewaainisha wanadamu katika hizi aina kuu.

Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Wasioamini

Hebu tuanze na mzunguko wa uhai na mauti wa wasioamini. Baada ya watu kufa, wanachukuliwa na msimamizi kutoka ulimwengu wa kiroho. Na ni kitu gani chao kinachukuliwa? Sio miili yao, bali ni roho zao. Roho zao zikichukuliwa, wanawasili katika sehemu ambayo ni ofisi ya ulimwengu wa kiroho, sehemu ambayo hasa hupokea roho za watu ambao wamekufa. (Kumbuka: sehemu ya kwanza wanapokwenda baada ya mtu yeyote kufa ni pageni kwa roho.) Wanapofikishwa mahali hapa, afisa anafanya ukaguzi wa kwanza, akithibitisha majina yao, anwani, umri, na uzoefu wao wote. Kila kitu walichofanya walipokuwa hai kinanakiliwa kwenye kitabu na usahihi wake unahakikishwa. Baada ya kukaguliwa, matendo na mienendo ya mtu maishani mwake vinatumika kuamua ikiwa ataadhibiwa au ataendelea kupata mwili kama mwanadamu, ambayo ni hatua ya kwanza. Je, hii hatua ya kwanza inaogofya? Haiogopeshi sana, kwani kitu cha pekee kilichofanyika ni kwamba mtu amewasili katika mahali pa giza na pageni.

Katika hatua ya pili, ikiwa mtu huyu amefanya mambo mengi mabaya maishani mwake, kama ametenda vitendo vingi viovu, basi atapelekwa mahali pa adhabu ili kuadhibiwa. Hiyo ndiyo itakuwa mahali ambapo kwa hakika ni kwa ajili ya adhabu ya watu. Maelezo kuhusu jinsi watakavyoadhibiwa yanategemea dhambi ambazo wamezitenda, pia ni vitendo vingapi viovu walitenda kabla hawajafa—hili ni tukio la kwanza ambalo linatokea katika hatua hii ya pili. Kwa sababu ya mambo mabaya waliyoyafanya, na maovu waliyoyafanya kabla hawajafa, wapatapo mwili baada ya adhabu yao—wazaliwapo upya tena katika ulimwengu yakinifu—watu wengine wataendelea kuwa wanadamu, na wengine watakuwa wanyama. Yaani, baada ya mtu kurudi katika ulimwengu wa kiroho, wanaadhibiwa kwa sababu ya maovu waliyotenda; zaidi, kwa sababu ya mambo maovu waliyofanya, watakapozaliwa tena katika mwili mpya huenda hawawi wanadamu, ila watakuwa mnyama. Baadhi ya wanyama watakaokuwa ni ng’ombe, farasi, nguruwe, na mbwa. Watu wengine wanaweza kuwa ndege kule angani, au bata au bata bukini.… Baada ya kupata mwili kama mnyama, wanapokufa wanarudi katika ulimwengu wa kiroho, na sawa na mara ya kwanza, kutegemea mienendo yao kabla hawajafa, ulimwengu wa kiroho utaamua kama wapate mwili kama mwanadamu au la. Watu wengi hutenda maovu mengi sana, dhambi zao ni nzito sana, na kwa hivyo wapatapo mwili wanakuwa wanyama mara saba hadi mara kumi na mbili. Mara saba hadi mara kumi na mbili—hilo linaogopesha? (Linaogopesha.) Ni nini kinawaogopesha? Mtu kuwa mnyama, hilo linaogopesha. Na kwa mwanadamu, ni kipi cha uchungu zaidi kuhusu kuwa mnyama? Kutokuwa na lugha, kuwa tu na mawazo sahili, kuweza tu kufanya vitu ambavyo wanyama hufanya na kula vitu ambavyo wanyama hula, na kuwa na fikira sahili na kuwa na viziada lugha vya mnyama, kutoweza kutembea wima, kutoweza kuwasiliana na wanadamu, na mienendo yoyote na vitendo vya wanadamu kutokuwa na uhusiano na wanyama. Yaani, miongoni mwa vitu vyote, kuwa mnyama kunakufanya kuwa chini zaidi ya viumbe hai wote, na ni kuchungu zaidi kuliko kuwa mwanadamu. Hiki ni kipengele kimoja cha adhabu ya ulimwengu wa kiroho kwa wale waliofanya maovu mengi na kutenda dhambi kubwa. Ukali wa adhabu utakavyokuwa, hili hubainishwa na aina ya mnyama ambaye mtu anakuwa. Kwa mfano, kuwa nguruwe ni bora kuliko kuwa mbwa? Je, nguruwe huishi vizuri au vibaya kuliko mbwa? Vibaya zaidi, siyo?. Watu wakiwa ng’ombe au farasi, je, wataishi vizuri zaidi au vibaya kuliko jinsi wangesishi kama nguruwe? (Vizuri zaidi.) Je, mtu atakuwa wa faraja zaidi kama mtu angezaliwa kama paka? Angekuwa mnyama sawa tu, na kuwa paka ingekuwa rahisi zaidi kuliko kuwa ng’ombe au farasi, kwa sababu paka huweza kuupitisha muda wao mwingi kulala. Kuwa ng’ombe au farasi ni kazi nzito. Hivyo basi, iwapo mtu atapata mwili na kuwa ng’ombe au farasi, wanapaswa kutia bidii—ambayo ni sawa na adhabu nzito. Kuwa mbwa kungekuwa ni afadhali kidogo kuliko kuja kuwa ng’ombe au farasi, kwa kuwa mbwa ana uhusiano wa karibu na bwana wake. Baadhi ya mbwa, baada ya kuwa kipenzi kwa miaka mingi, wanaweza kuelewa mengi ya yale bwana wao wanasema! Wakati mwingine na mahitaji yake na bwana anamtunza mbwa vyema, na mbwa anakula na kunywa vyema, na akiwa na maumivu anatunzwa zaidi. Je, mbwa basi hapati maisha ya furaha? Hivyo basi, kuwa mbwa ni bora kuliko kuwa ng’ombe au farasi. Katika hili, ukali wa adhabu ya mtu unaamua ni mara ngapi mtu hupata mwili kuwa mnyama, pia wa aina gani.

Kwa sababu walitenda dhambi nyingi sana walipokuwa hai, watu wengine wataadhibiwa kwa kupatiwa miili kama wanyama mara saba hadi kumi na mbili. Baada ya kuadhibiwa vya kutosha, wanaporudi katika ulimwengu wa kiroho wanapelekwa mahali pengine. Roho mbalimbali mahali hapa zimeadhibiwa tayari, na ni aina ya roho ambazo ziko tayari kupata mwili kama wanadamu. Mahali hapa panaziainisha roho katika makundi kulingana na aina ya familia watakamozaliwa, ni aina gani ya nafasi watashikilia baada ya kupata mwili, na kadhalika. Kwa mfano, watu wengine watakuwa waimbaji wakija katika ulimwengu huu, na kwa hivyo wanawekwa miongoni mwa waimbaji; wengine watakuwa wafanyabiashara wakija katika ulimwengu huu, na kwa hivyo wanawekwa miongoni mwa wafanyabiashara; na ikiwa mtu atakuwa mtafiti wa kisayansi akiwa mwanadamu, basi anawekwa miongoni mwa watafiti wa kisayansi. Baada ya kuwekwa katika makundi, kila mmoja anatumwa kulingana na wakati tofauti na tarehe iliyowekwa, sawa tu na jinsi watu hutuma barua pepe siku hizi. Katika hili kutakuwa kumekamilika mzunguko mmoja wa uhai na mauti. Tangu siku mtu anapowasili katika ulimwengu wa kiroho hadi mwisho wa adhabu yake, ama hadi anapozaliwa upya kama mnyama mara nyingi na anajitayarisha kuzaliwa upya kama mwanadamu, huu ni mchakato mzima.

Na wale waliokamilisha adhabu yao, na hawajapata mwili kuwa wanyama, je, watapelekwa kwa haraka katika ulimwengu yakinifu kuwa wanadamu? Au watachukua muda gani ndipo waje miongoni mwa wanadamu? Hili linaweza kurudiwa mara ngapi? Kwa hili kuna mipaka ya wakati. Kila kitu kinachofanyika katika ulimwengu huu wa kiroho kinapitia mipaka ifaayo kwa wakati na sheria—ambayo, Nikiieleza kutumia tarakimu, mtaelewa. Kwa wapatao mwili baada ya muda mfupi, wakati wanapokufa kuzaliwa kwao upya kama wanadamu kutatayarishwa. Wakati mfupi zaidi ni siku tatu. Kwa watu wengine, ni miezi mitatu, kwa wengine ni miaka mitatu, kwa wengine ni miaka thelathini, kwa wengine ni miaka mia tatu, kwa wengine hata ni miaka elfu tatu, na kadhalika. Hivyo basi ni nini kinaweza kusemwa kuhusu hizi sheria za wakati, na vipimo vyake ni vipi? Vinalingana na ulimwengu yakinifu, ulimwengu wa mwanadamu unahitaji kutoka kwa roho, na nafasi itakayochukuliwa na hii roho duniani. Watu wakipata mwili kama wanadamu wa kawaida, wengi wao wanapewa mwili haraka sana, kwa sababu dunia ya wanadamu ina uhitaji mkubwa wa watu wa kawaida kama hao, na kwa hiyo siku tatu baadaye wanatumwa tena katika familia ambayo ni tofauti kabisa na ile waliyokuwa kabla hawajafa. Lakini wapo ambao wana nafasi maalum katika ulimwengu huu. “Maalum” inamaanisha kuwa hakuna uhitaji mkubwa wa hawa watu katika ulimwengu wa wanadamu; si watu wengi wanaohitajika kuishikilia nafasi hiyo, kwa hiyo basi inaweza kuwa miaka mia tatu kabla hawajapata mwili. Ambako ni kusema, hii roho itakuja mara moja tu katika kila miaka mia tatu, au hata mara moja kila baada ya miaka elfu tatu. Na ni kwa nini hivi? Ni kwa sababu kwa miaka mia tatu au miaka elfu tatu, nafasi hiyo haihitajiki katika dunia ya mwanadamu, na kwa hiyo wanatunzwa mahali fulani katika ulimwengu wa kiroho. Tazama Confucius, kwa mfano. Alikuwa na athari kubwa katika utamaduni wa jadi wa Uchina. Kuwasili kwake kulikuwa na athari kubwa kwenye utamaduni, elimu, desturi, na kufikiri kwa watu wa wakati ule. Lakini mtu kama huyu hahitajiki katika kila enzi, na kwa hiyo alilazimika kubaki katika ulimwengu wa kiroho, akisubiri huko kwa miaka mia tatu au miaka elfu tatu kabla ya kupata mwili. Kwa kuwa ulimwengu wa mwanadamu haukuhitaji mtu kama huyu, alilazimika kusubiri bila kufanya chochote, kwa kuwa kulikuwa na nafasi chache sana kama yake, kulikuwa na machache ya yeye kufanya, na hivyo basi alitunzwa sehemu fulani katika ulimwengu wa kiroho kwa muda mrefu, bila kufanya chochote, na kutumwa wakati ambapo ulimwengu wa mwanadamu ulimhitaji. Hizo ndizo sheria za wakati za milki ya kiroho kuhusu haraka ambayo watu wengi wanapata miili. Iwe ni mtu wa kawaida au maalum, ulimwengu wa kiroho una sheria mwafaka na desturi sahihi kwa utayarishaji wa watu kuzaliwa katika mwili mpya, na hizi sheria na desturi zinatumwa kutoka kwa Mungu, na haziamuliwi au kudhibitiwa na msimamizi yeyote au kiumbe chochote katika ulimwengu wa kiroho.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 189)

Kwa nafsi yoyote, kuzaliwa kwake katika mwili mpya, nafasi yake ni ipi katika haya maisha, atazaliwa katika familia gani, na maisha yake yatakuwaje vinahusiana kwa karibu na maisha yake ya zamani. Watu wa kila aina huja katika dunia ya wanadamu, na nafasi zao ni tofauti, kama zilivyo kazi wazifanyazo. Na hizi ni kazi gani? Watu wengine wanakuja kulipa deni: Ikiwa walikuwa na pesa nyingi za watu katika maisha yao ya awali, wanakuja kulipa deni. Katika maisha haya Wakati uleule, watu wengine, wamekuja kuchukua madeni yao: Walitapeliwa vitu vingi sana, na pesa nyingi sana katika maisha yao yaliyopita, na kwa hiyo, baada ya kuwasili katika ulimwengu wa kiroho, ulimwengu wa kiroho utawapa haki na kuwapa fursa ya kukusanya madeni yao katika maisha haya. Watu wengine wamekuja kulipa deni la shukrani: katika maisha yao yaliyopita—kabla hawajafa—mtu alikuwa mkarimu kwao, na katika maisha haya wamepatiwa fursa nzuri kupata mwili ili kwamba waweze kuzaliwa upya ili kulipa upya deni hili la shukrani. Wakati uleule, wengine wamezaliwa upya katika haya maisha ili kudai uhai. Na wanadai uhai wa nani? Uhai wa mtu aliyewaua katika maisha yao yaliyopita. Kwa ujumla, maisha ya sasa ya kila mtu yana uhusiano mkubwa na maisha yao yaliyopita, yameungana kwa njia isiyoachana. Yaani, maisha ya sasa ya kila mtu yanaathiriwa pakubwa na maisha yao yaliyopita. Kwa mfano, kabla ya kufariki, Zhang alimtapeli Li kiwango kikubwa cha pesa. Je, Zhang ana deni la Li? Kwa kuwa analo, ni kawaida kwamba Li anapaswa kuchukua deni lake kutoka kwa Zhang? Hivyo basi baada ya wao kufa, kuna deni kati yao ambalo linatakiwa kulipwa. Wakati wanapata mwili mpya na Zhang anakuwa mwanadamu, je, Li anapataje deni hili kutoka kwake? Mbinu moja ni kwamba Li anapata deni lake kwa kuzaliwa upya kama mwana wa Zhang, Zhang anapata pesa nyingi, na zinaliwa na Li. Haijalishi Zhang anapata pesa nyingi kiasi gani, mwana wa Li anazitumia ovyo. Haijalishi Zhang anapata kiasi gani cha pesa, katu hazitoshi, wakati uleule, mwanawe, kwa namna fulani daima anazitumia pesa za babake kupitia njia na mbinu mbalimbali. Zhang anachanganyikiwa: “Kwa nini mwanangu daima amekuwa kisirani? Mbona wana wa watu wengine ni wema sana? Ni kwa nini mwanangu hana lengo, ni kwa nini hana maana na hana uwezo wa kuchuma pesa zozote, kwa nini daima ninapaswa kumsaidia? Kwa kuwa ni lazima nimsaidie, nitamsaidia, ila kwa nini hata nimpe pesa kiasi gani, daima anataka zaidi? Ni kwa nini asifanye kazi halali, lakini atafanya chochote—kuzurura, kula, kunywa, kuzini, na kucheza kamari? Nini kinaendelea?” Halafu Zhang anafikiria kidogo: “Inaweza kuwa ni kwa sababu nilikuwa na deni lake katika maisha ya zamani. Sawa basi, nitalilipa! Haya hayataisha hadi nilipe kikamilifu!” Inaweza kufika siku ambayo Li anafidia deni lake, na akiwa na umri wa miaka arobaini au hamsini, itafika siku ambayo atajitambua: “Sijafanya kitu kizuri hata kimoja katika hii nusu ya kwanza ya maisha yangu! Nimefuja pesa zote alizozipata baba—ninapaswa kuwa mtu mwema! Nitajikakamua: nitakuwa mtu ambaye ni mwaminifu, na anayeishi ipasavyo, na sitamletea babangu huzuni tena!” Kwa nini anafikiria hivi? Mbona anageuka kuwa mwema ghafla? Kuna sababu ya hili? Ni sababu gani? (Kwa sababu Li amepokea deni lake; Zhang amelipa deni lake.) Katika hili, kuna chanzo na matokeo. Kisa kilianza zamani sana, kabla hawa wawili hawajazaliwa, na hiki kisa cha maisha yao ya zamani kimeletwa katika maisha yao ya sasa, na hakuna anayeweza kumlaumu mwingine. Haijalishi Zhang alimfundisha nini mwanake, mwanake hakumsikiliza, na hakufanya kazi halali hata ya siku—lakini siku ambayo deni lilipwa, hapakuwa na haja ya kumfundisha; mwanake alielewa kiasili. Huu ni mfano rahisi. Kuna mifano mingine mingi kama huu? (Ndiyo.) Na unawafunza watu kitu gani? (Wanapaswa kuwa wema na hawapaswi kutenda maovu.) Kwamba hawapaswi kutenda maovu, na kutakuwa na adhabu kwa maovu yao! Wengi wa wasioamini, hutenda maovu mengi na utendaji maovu wao umekutwa na adhabu, sawa? Je, hii adhabu ni ya kinasibu? Kila linalokutwa na adhabu lina asili na sababu. Unadhani hakuna litakalotendeka baada ya kumlaghai mtu pesa? Unadhani baada ya kuwatapeli pesa zao hakutakuwa na matokeo kwako baada ya kuchukua pesa zao? Hilo halitawezekana, na kutakuwa na athari! Bila kujali yeye ni nani, au kama anaamini ama haamini kuwa kuna Mungu, kila mtu ni lazima atawajibikia mienendo yake na kubeba matokeo ya matendo yake. Kwa kurejelea huu mfano rahisi—Zhang kuadhibiwa, na Li kulipwa—je hii si haki? Watu wakifanya vitu kama hivyo, kuna aina hiyo ya matokeo. Haitenganishwi na utawala wa ulimwengu wa kiroho. Licha ya kuwa wasioamini, wale wasiomwamini Mungu, uwepo wao uko chini ya amri za peponi na sheria ambazo haziwezi kuepukika na yeyote na hakuna mtu anayeweza kuuepuka ukweli huu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 190)

Wale ambao hawana imani huamini kuwa kila kitu ambacho kinaweza kuonekana kipo, ilhali kila kitu kisichoonekana, au ambacho kiko mbali sana na watu, hakipo. Wanapenda kuamini kuwa hakuna “mzunguko wa uhai na mauti,” na hakuna “adhabu,” na kwa hiyo wanatenda dhambi na kufanya maovu bila majuto—ambayo baadaye wataadhibiwa kwayo, au watapata miili kama mnyama. Wengi wa watu mbalimbali miongoni mwa Wasioamini wanapatikana katika mzunguko huu. Ni kwa sababu hawajui kuwa ulimwengu wa kiroho ni mkali katika kuviendesha viumbe hai wote. Ikiwa unaamini au la, huu ukweli upo, na hakuna mtu hata mmoja au chombo chochote kinaweza kuepuka mawanda ya ambacho kinaonwa na macho ya Mungu, na hakuna mtu hata mmoja au chombo kinachoweza kuepuka sheria na mipaka ya sheria za peponi na amri za Mungu. Na hivyo basi mfano huu rahisi unamwambia kila mtu kwamba haijalishi kama unamwamini au humwamini Mungu, haikubaliwi kutenda dhambi na kufanya maovu, na kuna matokeo. Wakati mtu aliyemlaghai mwingine pesa anaadhibiwa hivyo, hiyo adhabu ni ya haki. Mienendo inayoonekana ya kawaida kama hii inaadhibiwa na ulimwengu wa kiroho, inaadhibiwa na amri na sheria za mbinguni za Mungu, na vivyo hivyo uhalifu mkubwa na matendo maovu—ubakaji na unyang’anyi, ulaghai na udanganyifu, wizi na ujambazi, mauaji na uchomaji, na kadhalika—yanapitia adhabu za aina zenye ukali wa viwango mbalimbali. Na hizi adhabu zenye ukali wa viwango mbalimbali zinajumuisha nini? Baadhi yake zinatumia muda kufikisha kiwango cha ukali, na nyingine hufikiwa kwa mbinu mbalimbali, na nyingi hufikiwa kupitia mahali mtu aendapo akipata mwili. Kwa mfano, watu wengine wana maneno machafu. Kuwa na “maneno machafu” kunamaanisha nini? Kunamaanisha kuwaapiza wengine mara kwa mara, na kutumia lugha chafu, lugha inayowalaani watu wengine. Lugha yenye nia mbaya inaashiria nini? Inaashiria kuwa mtu ana roho mbaya. Lugha yenye nia mbaya inayowalaani watu wengine mara nyingi inatoka vinywani mwa watu kama hao, na lugha yenye nia mbaya kama hiyo mara nyingi inaandamana na matokeo makali. Baada ya hawa watu kufa na kupokea adhabu stahili, wanaweza kuzaliwa kama mabubu. Watu wengine ni wajanja sana wakiwa hai, mara kwa mara wanawatumia watu wengine kwa manufaa yao, njama zao huwa zimepangwa barabara, na wanafanya mengi yanayowadhuru wengine. Wakizaliwa upya, wanaweza kuwa wazimu au punguani. Watu wengine mara nyingi huwachungulia watu wengine wakiwa faraghani; macho yao huona mengi ambayo hawakutakiwa kuona, na hujua mengi ambayo hawakupaswa kujua, hivyo basi wazaliwapo upya, wanaweza kuwa vipofu. Watu wengine ni hodari sana wakiwa hai, wanapigana mara kwa mara, na kufanya mengi ambayo ni maovu, na kwa hiyo wanapozaliwa upya, wanaweza kuwa vilema au wakakosa mkono, vinginevyo wanaweza kuwa vibyongo, au wenye shingo iliyopinda, huenda wakatembea wakichechemea, au wakawa na mguu mmoja mfupi kuliko mwingine, na kadhalika. Katika hali hii, wanapewa adhabu mbalimbali kutegemea kiwango cha maovu waliyotenda walipokuwa hai. Mwasemaje, kuhusu ni kwa nini watu huwa na makengeza? Je, kuna watu wengi wa hivyo? Kuna wengi wao siku hizi. Watu wengine wana makengeza kwa sababu waliyatumia macho yao sana katika maisha yao yaliyopita, walifanya mambo mengi mabaya, na kwa hiyo wazaliwapo katika haya maisha macho yao hupata makengeza, na katika hali mbaya, hata huwa vipofu. Haya ni malipo! Watu wengine wanaelewana vizuri na wengine kabla hawajafa, wanafanya mambo mengi mazuri kwa wapendwa wao, marafiki, wenza, au watu wanaohusiana nao. Wanatoa hisani na matunzo kwa wengine, au kuwasaidia kifedha, wengine wanawaheshimu sana, na watu kama hao warudipo katika ulimwengu wa kiroho hawaadhibiwi. Kwa asiyeamini kukosa kuadhibiwa kwa njia yoyote inamaanisha alikuwa mtu mzuri sana. Badala ya kuamini katika uwepo wa Mungu, wanaamini tu katika Mzee aliye Angani. Wanaamini tu kuwa kuna roho juu yao akitazama yote wafanyayo—hayo tu ndiyo wanaamini. Na matokeo ni kwamba wanakuwa na mwenendo mzuri zaidi. Hawa watu ni wenye huruma na wakarimu, na mwishowe wakirudi katika ulimwengu wa kiroho, ulimwengu wa kiroho utawapokea vizuri sana na watapata mwili na kuzaliwa upya mapema. Wanapozaliwa tena, watafikia katika familia za aina gani? Japo familia yake haitakuwa ya kitajiri, itakuwa tulivu, kutakuwa na maelewano miongoni mwa wanafamilia, watakuwa na siku mwanana, za kupendeza, kila mmoja atafurahia, na watakuwa na maisha mazuri. Naye atakapokuwa mtu mzima, atakuwa na familia kubwa na jamaa wengi, watoto wake watakuwa na vipawa na kufanikiwa, na familia yake watakuwa na bahati nzuri—na matokeo kama hayo yanahusiana kwa kiasi kikubwa na maisha ya zamani ya mtu. Yaani, mahali mtu huenda baada ya kufa na kupata mwili, wawe wanaume au wanawake, wito wao ni upi, watapitia nini maishani, vikwazo vyao, watapata baraka gani, watakutana na nani, ni nini kitawatokea—hakuna awezaye kulitabiri hili, kuliepuka, au kujificha kutokana nalo. Yaani, baada ya maisha yako kupangwa, kitakachokutokea, hata ujaribu namna gani kukikwepa, hata ukitumia mbinu gani kukiepuka, huna njia ya kuvuruga mkondo wa maisha uliopangiwa na Mungu katika ulimwengu wa kiroho. Kwani upatapo mwili, majaaliwa yako tayari huwa yameishapangwa, ikiwa yatakuwa mazuri au mabaya, kila mtu anapaswa kuyakubali yalivyo, na anapaswa kusonga mbele; hili ni jambo ambalo hakuna mtu aishiye katika maisha haya anaweza kuliepuka, na huu ndio uhalisia.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 191)

Mnaona kwamba Mungu ana uangalizi unaolipiza sana na mkali pamoja na utawala kwa mzunguko wa uhai na mauti wa wasioamini? Kwanza, Mungu ameweka sheria mbalimbali za mbinguni, amri, na mifumo katika milki ya kiroho, na baada ya kutangazwa kwa hizi sheria za mbinguni, amri na mifumo, ambazo zinatekelezwa kabisa, kama zilivyopangwa na Mungu, na viumbe wenye nyadhifa rasmi mbalimbali katika ulimwengu wa kiroho, na hakuna anayethubutu kuzikiuka. Na kwa hivyo, katika Mzunguko wa uhai na mauti wa wanadamu katika dunia ya mwanadamu, mtu awe amepata mwili kama mwanadamu au mnyama, kuna sheria kwa yote mawili. Kwa kuwa sheria hizi zinatoka kwa Mungu, hakuna anayethubutu kuzivunja, wala hakuna awezaye kuzivunja. Ni kwa sababu tu ya huo ukuu wa Mungu, na kwa sababu kuna sheria hizo, ndiyo ulimwengu yakinifu uonekanao kwa mwanadamu ni wa kawaida na wenye mpangilio; ni kwa sababu tu ya ukuu wa Mungu ndipo mwanadamu anaweza kuishi kwa amani pamoja na ulimwengu mwingine ambao hauonekani kabisa kwa mwanadamu, na kuweza kuishi nao kwa amani—vitu ambavyo vyote haviwezi kutenganishwa na mamlaka ya Mungu. Baada ya maisha ya mtu ya kimwili kufa, roho bado huwa na uhai, basi ni nini kingetendeka ikiwa roho ingekosa utawala wa Mungu? Roho ingezurura kila mahali, ikiingia kila sehemu, na hata kudhuru viumbe hai katika ulimwengu wa wanadamu. Madhara hayo hayangekuwa tu kwa mwanadamu bali pia kwa mimea na wanyama—ila wa kwanza kudhuriwa wangekuwa watu. Kama hili lingetukia—roho kama hiyo ingekosa uendeshaji, na kuwadhuru watu kwa hakika, na kufanya mambo maovu kwa hakika—basi pia kungekuwa na ushughulikiaji ufaao wa roho hii katika ulimwengu wa kiroho: Ikiwa mambo yangekuwa mabaya, roho haingeendelea kuwepo, ingeangamizwa; ikiwezekana, ingewekwa mahali fulani halafu ipatiwe mwili. Yaani, utawala wa ulimwengu wa kiroho kwa roho mbalimbali umepangiliwa, na kutekelezwa kulingana na hatua na sheria. Ni kwa sababu tu ya utawala huo ndiyo ulimwengu yakinifu wa mwanadamu haujatumbukia kwenye machafuko, ndiyo mwanadamu wa ulimwengu wa kuonekana ana akili ya kawaida, urazini wa kawaida, na maisha ya kimwili yenye mpangilio. Ni baada tu ya mwanadamu kuwa na maisha ya kawaida ndiyo wale wanaoishi katika mwili wanaweza kuendelea kufanikiwa na kuzaana katika vizazi vyote.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 192)

Ikija kwa wasioamini, je, kanuni iongozayo matendo ya Mungu ni ile ya kutuza mazuri na kuadhibu mabaya? Kuna upekee wowote? (La.) Je, mnaona kwamba kuna kanuni katika matendo ya Mungu? Wasioamini kwa hakika hawamwamini Mungu, hawatii mipango ya Mungu, na hawafahamu ukuu wa Mungu, na hawamtambui Mungu hata kidogo. Zito zaidi, wanamkufuru Mungu, na kumlaani, na ni mahasimu wa wale wanaomwamini Mungu. Japo watu hawa wana mwelekeo huo kwa Mungu, bado uongozi wa Mungu kwao hauachani na kanuni Zake; Anawaongoza kwa njia ya utaratibu kulingana na kanuni Zake na tabia Yake. Je, Mungu anauchukuliaje uhasama wao? Kama ujinga! Na kwa hiyo Amewasababisha hawa watu—wengi wa wasioamini—wakati mmoja kuwahi kupata mwili kama wanyama. Basi wasioamini ni nini machoni mwa Mungu? Wao ni mifugo. Mungu anaongoza mifugo na kwa watu kama hao Ana kanuni sawa. Hata kwa utawala wa Mungu kwa watu hawa, tabia Yake kwao, bado inaweza kuonekana, kama inavyowezekana sheria Zake kama chanzo cha utawala Wake juu ya vitu vyote. Hivyo basi, unaona mamlaka ya Mungu katika kanuni ambazo kwazo Anawaongoza wasioamini ambao Nimezungumzia hivi punde? Je, mnaona tabia ya haki ya Mungu? (Tunaona.) Yaani, haijalishi Anashughulikia kitu gani kati ya vitu vyote Anavyoshughulikia, Mungu anatenda kulingana na kanuni na tabia Yake. Hiki ndicho kiini cha Mungu. Hangeweza kujitenga kiholela na amri au sheria za mbinguni Alizozipanga kwa sababu Anamwona mtu wa aina hii kama mfugo. Mungu anatenda kulingana na kanuni, bila kuzivuruga hata kidogo, matendo Yake hayaathiriwi na jambo lolote, na haijalishi Anafanya nini, yote ni kulingana na kanuni Zake mwenyewe. Hili ni kwa sababu Mungu ana kiini cha Mungu Mwenyewe, ambacho ni kipengele cha kiini Chake ambacho hakimo kwenye kiumbe yeyote. Mungu ni Mwangalifu na Anawajibika katika kushughulikia Kwake, njia Zake, usimamizi, uongozi, na utawala wa kila chombo, mtu, na kiumbe hai miongoni mwa vitu vyote Alivyoumba, na Hajawahi kuwa mzembe katika hili. Yeye ni mwenye neema na mkarimu kwa wale walio wazuri; Kwa wale waovu, Anawapa adhabu bila huruma; na kwa viumbe hai mbalimbali, Anafanya mipango ifaayo kwa wakati na kwa njia ya kawaida kulingana na mahitaji mbalimbali ya ulimwengu wa wanadamu katika nyakati mbalimbali, kiasi kwamba hawa viumbe hai mbalimbali wanapata miili kulingana na nafasi wanayochukua kwa njia ya utaratibu, na kuhama kati ya ulimwengu yakinifu na ulimwengu wa kiroho kwa njia ya utaratibu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 193)

Kifo cha kiumbe hai—kuondokewa na uhai wa kimwili—kinaashiria kwamba kiumbe hai huyu ametoka katika ulimwengu yakinifu hadi ulimwengu wa kiroho, ilhali kuzaliwa kimwili kunaashiria kwamba kiumbe hai ametoka ulimwengu wa kiroho na kuja ulimwengu yakinifu kuanza kufanya kazi yake, kuchukua nafasi yake. Iwe ni kuondoka au kuwasili kwa kiumbe, vyote havitenganishwi na kazi ya ulimwengu wa kiroho. Mtu akija katika ulimwengu yakinifu, mipango kabambe na fafanuzi huwa tayari imetengenezwa na Mungu katika ulimwengu wa kiroho kuhusu atakwenda katika familia gani, atafikia enzi gani, atawasili saa ngapi, na nafasi yake. Hivyo basi, maisha yote ya mtu huyu—mambo afanyayo, na njia azichukuazo—yanasonga kulingana na mipango ya ulimwengu wa kiroho, bila hitilafu hata kidogo. Wakati ambapo maisha ya kiroho yanaisha, wakati huo, na namna na mahali ambapo yanaishia, ni wazi na yanaonekana katika ulimwengu wa kiroho. Mungu anatawala ulimwengu yakinifu, na Anatawala ulimwengu wa kiroho, na Hawezi kuchelewesha mzunguko wa kawaida wa uhai na mauti wa roho, wala Hawezi kufanya makosa katika mpangilio wa mzunguko wa uhai na mauti wa roho. Kila msimamizi katika nyadhifa rasmi katika ulimwengu wa kiroho anafanya majukumu yake na kufanya ambacho anapaswa kufanya, kulingana na maelezo na sheria za Mungu. Na kwa hiyo, katika ulimwengu wa wanadamu, kila tukio la kuonekana lishuhudiwalo na binadamu lina utaratibu, na halina vurugu yoyote. Haya yote ni kwa sababu ya utawala uliopangiliwa wa Mungu juu ya vitu vyote, hali kadhalika kwa sababu mamlaka ya Mungu yanatawala kila kitu, na kila kitu Anachokitawala kinajumuisha ulimwengu yakinifu ambamo mwanadamu anaishi, aidha, ulimwengu wa kiroho usioonekana nyuma ya mwanadamu. Na kwa hiyo, ikiwa mwanadamu anataka kuwa na maisha mazuri, na anataka kuishi katika mazingira mazuri, hali kadhalika kupewa ulimwengu yakinifu mzima, mwanadamu sharti pia apatiwe ulimwengu wa kiroho, ambao hauwezi kuonekana kwa yeyote, ambao unaongoza kila kiumbe hai kwa niaba ya mwanadamu, na ambao una utaratibu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 194)

Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Mbalimbali Wenye Imani

Tumemaliza kujadili mzunguko wa uhai na mauti wa kundi la kwanza, wasioamini. Hebu sasa tujadili ule wa kundi la pili, watu mbalimbali wenye imani. “Mzunguko wa uhai na mauti wa watu mbalimbali wenye imani” vilevile ni mada muhimu sana, na inafaa kwamba muwe na kiasi fulani cha uelewa wake. Kwanza, hebu tuseme ni imani gani “imani” kwa watu wa imani inaashiria: dini tano kuu za Uyahudi, Ukristo, Ukatoliki, Uisilamu, na Ubudha. Pamoja na wasioamini, watu ambao ni waumini katika hizi dini tano wanajumuisha idadi kubwa ya watu duniani. Miongoni mwa dini hizi tano, wale ambao wametengeneza ajira kutokana na imani yao ni wachache, lakini hizi dini zina waumini wengi. Waumini wake huenda sehemu tofauti wanapokufa. “Tofauti” na nani? Na wasioamini, watu wasiokuwa na imani, ambao tumemaliza kuzungumzia. Baada ya kufa, waumini wa hizi dini tano huenda mahali pengine, mahali tofauti na wasioamini. Lakini ni mchakato sawa. Ulimwengu wa kiroho pia utafanya uamuzi juu yao kutegemea yale yote waliyoyafanya kabla wafe, baadaye watatayarishwa ipasavyo. Lakini mbona hawa watu wanawekwa sehemu tofauti kutayarishwa? Kuna sababu muhimu ya hili. Na hii sababu ni gani? Nitawaambia kutumia mfano. Lakini kabla nifanye hivyo, mnaweza kuwa mkijiwazia: “Labda ni kwa sababu wana imani ndogo katika Mungu! Wao si wasioamini kabisa.” Hii ndiyo sababu mbona. Kuna sababu muhimu sana kwa wao kuwekwa mahali pengine.

Chukua Ubudha: Hebu Niwaambie ukweli. Mfuasi wa Budha, kwanza kabisa, ni mtu aliyebadili dini kwenda Ubudha, na ni mtu ajuaye imani yake ni nini. Mfuasi wa Budha akinyoa nywele zake na kuwa mtawa wa kiume au mtawa wa kike, hii inamaanisha kuwa amejitenga na mambo ya kidunia na kuacha nyuma ghasia ya dunia ya mwanadamu. Kila siku anakariri maandiko ya sutra na kuimba majina ya Budha, na kula chakula bila nyama, anaishi maisha ya kujinyima anasa za kimwili, na kupitisha siku zake ndani ya mwangaza baridi, na hafifu wa taa ya mafuta ya siagi. Anaishi maisha yake yote kwa njia hii. Maisha yake ya kimwili yaishapo, anatengeneza muhtasari wa maisha yake, ila mioyoni mwake hajui atakapoenda baada ya kufa, atakutana na nani, na atakuwa na hatima ya aina gani—mioyoni mwake hana uhakika na haya mambo. Hajafanya chochote zaidi ya kuishi bila mwelekeo maisha yake yote akiambatana na imani, baadaye anaondoka duniani akiambatana na matamanio na maadili asiyoyafahamu. Hiyo ndiyo tamati ya maisha yake ya kimwili anapoiaga dunia ya walio hai, na baada ya hapo, anarudi katika sehemu yake asilia katika ulimwengu wa kiroho. Kama mtu hutu atapata mwili na kurudi duniani kuendelea na kujikuza kwake kunategemea mienendo na kujikuza kwake kabla ya kifo chake. Ikiwa hakufanya kitu kibaya wakati wa uhai wake, atapata mwili haraka na kurudishwa duniani, ambapo atakuwa mtawa wa kiume au mtawa wa kike tena. Kulingana na utaratibu wa mara ya kwanza, mwili wake unajikuza wenyewe, baada ya hapo anakufa na kurudi katika ulimwengu wa kiroho, ambapo anatathminiwa, na baada ya hapo—ikiwa hakuna shida—anaweza kurudi tena katika ulimwengu wa wanadamu, na kuweza kubadili dini hadi Ubudha tena na kuendelea kujikuza. Baada ya kupata mwili mara tatu hadi mara saba, atarudi tena katika ulimwengu wa kiroho, ambapo anakwenda kila mara ambapo maisha yake ya kimwili yanamalizika. Ikiwa viwango na mienendo yake mbalimbali katika ulimwengu wa wanadamu inaambata na sheria za mbinguni za ulimwengu wa kiroho, basi atabaki huko kutoka wakati huu kuendelea; hatapata mwili tena kama mwanadamu; wala hakutakuwa na tishio la yeye kuadhibiwa kwa kutenda maovu duniani. Hatawahi kupitia tena mchakato huu. Badala yake, kulingana na hali zake, atachukua nyadhifa katika milki ya kiroho. Hili ndilo wafuasi wa Budha wanaliita kufikia hali ya Ubudha.” Kufikia hali ya Ubudha hasa kunamaanisha kufanikiwa kama afisa wa ulimwengu wa kiroho, na baada ya hapo kutozaliwa tena katika mwili mpya ama kuwa katika hatari ya kuadhibiwa. Aidha, kunamaanisha kwamba hakuna kupata taabu tena ya kuwa mwanadamu baada ya kuzaliwa upya. Hivyo basi, bado kuna uwezekano wake kupata mwili tena kama mnyama? (La.) Hili linamaanisha kwamba anabaki kushika nafasi katika ulimwengu wa kiroho, na kamwe hatazaliwa upya. Huu ni mfano mmoja wa kufanikiwa kufikia hali ya Ubudha katika dini ya Ubudha. Na kuhusu wale ambao hawafanikiwi, baada ya wao kurudi katika ulimwengu wa kiroho, wanachunguzwa na kuthibitishwa na ofisa mhusika, ambaye anagundua kuwa ingawa wako hai, hawakujikuza kwa makini au kuwa makini katika kukariri maandiko ya sutra na kuimba majina ya Budha kama inavyotakiwa na dini ya Ubudha, na badala yake, walikuwa wametenda matendo mengi maovu na kujihusisha katika mienendo mingi mibaya. Basi katika ulimwengu wa kiroho hukumu inatolewa juu ya uovu wao, na baada ya hapo wana hakika ya kuadhibiwa. Hakuna vighairi katika hili. Basi, mtu kama huyu atafanikiwa lini? Katika maisha ambamo hakutenda maovu yoyote—wakati, baada ya kurudi katika ulimwengu wa kiroho, inaonekana hakufanya chochote kibaya kabla afariki. Basi anaendelea kuzaliwa upya, akiendelea kukariri maandiko ya sutra na kuimba majina ya Budha, akipitisha siku zake ndani ya mwangaza baridi na hafifu wa taa ya mafuta ya siagi, bila kuua chochote chenye uhai, bila kula nyama, na hafurahii ulimwengu wa mwanadamu, akiachana na vurugu zake kabisa, na kuepuka migogoro na wengine. Katika mchakato huu, hafanyi maovu, na kufuatia hayo anarudi katika ulimwengu wa kiroho, na baada ya matendo na mienendo yake yote kutathminiwa, anatumwa tena katika ulimwengu wa wanadamu, kwa mzunguko unaojirudia mara tatu au saba. Ikiwa hakuna kikwazo wakati huu, basi kupata kwake Ubudhaa hakutaathiriwa, na hakutacheleweshwa. Hii ni sifa ya mzunguko wa uhai na mauti wa watu wote wenye imani: Wanaweza “kufanikiwa” na kushikilia wadhifa katika ulimwengu wa kiroho; hili ndilo linawafanya kuwa tofauti na wasioamini. Kwanza kabisa, wanapokuwa hai duniani, matendo ya wale wanaoweza kushika wadhifa katika ulimwengu wa kiroho ni yapi? Ni sharti wasifanye kabisa ovu lolote: ni lazima wasifanye mauaji, uchomaji, ubakaji, au wizi; wakifanya hila, udanganyifu, au ujambazi, basi hawawezi kufanikiwa. Yaani, wakiwa na uhusiano au ushirikishaji wowote na uovu, hawataweza kuepukana na adhabu ya ulimwengu wa kiroho. Ulimwengu wa kiroho unafanya mipango inayofaa kwa wafuasi wa Budha wanaofikia hali ya Ubudha: wanaweza kuteuliwa kusimamia wale ambao wanaonekana kuamini katika Ubudha, na yule Mzee aliye Angani, na wafuasi wa Budha watapewa mamlaka, wanaweza tu kuteuliwa kuwasimamia wasioamini, vinginevyo wanaweza kuwa wasimamizi wadogo sana. Ugavi huo unalingana na asili ya hizi roho. Huu ni mfano wa Ubudha.

Miongoni mwa dini tano tulizozungumzia, Ukristo ni maalum kiasi fulani. Ni nini maalum kuhusu Ukristo? Hawa ni watu wanaomwamini Mungu wa kweli. Je, inawezekanaje wale wanaomwamini Mungu wa kweli waorodheshwe hapa? Kwa sababu Ukristo ni aina ya imani, basi, bila shaka, unahusiana tu na imani—ni aina ya sherehe, aina ya dini, na kitu tofauti na imani ya wale wanaomfuata Mungu kweli. Kilichonifanya kuuorodhesha miongoni mwa hizi dini tano ni kwa sababu Ukristo umeshushwa hadi kiwango sawa na Uyahudi, Ubudha, Uislamu. Wakristo wengi hawaamini kuna Mungu, au kwamba Anatawala juu ya vitu vyote, seuze kuamini katika uwepo Wake. Badala yake, wanatumia tu Maandiko Matakatifu kuzungumza kuhusu elimu ya dini, wakitumia elimu ya dini kuwafundisha watu kuwa wema, kuvumilia mateso, na kufanya vitu vizuri. Ukristo ni wa aina hiyo ya dini: Unazingatia tu nadharia za mafundisho ya kidini, hauna kabisa uhusiano wowote na kazi ya Mungu ya kusimamia na kuokoa wanadamu, ni dini ya wale wanaomfuata Mungu ambayo haitambuliwi na Mungu. Lakini pia Mungu ana kanuni kuhusu mtazamo Wake kwao. Hawatendei na kuwashughulikia wapendavyo bila mpango, njia sawa na wasioamini. Mtazamo Wake kwao ni sawa na Alio nao kwa wafuasi wa Budha: Ikiwa, angali hai, Mkristo anajiheshimu, anaweza kuzifuata kabisa Amri Kumi za Mungu na kuzingatia sheria na amri katika mahitaji yao kwa tabia zao wenyewe—na ikiwa wanaweza kufanya hivi katika maisha yao yote—basi pia watalazimika kuchukua muda sawa kupitia mzunguko wa uhai na mauti kabla hawajaweza kweli kupata huko kuitwako kuchukuliwa kuenda mbinguni. Baada ya kupata huku kunyakuliwa wanabaki katika ulimwengu wa kiroho, ambapo wanashika wadhifa na kuwa miongoni mwa wasimamizi. Vivyo hivyo, wakifanya maovu duniani, ikiwa ni watenda dhambi na kufanya dhambi nyingi, basi haiepukiki kwamba wataadhibiwa kwa ukali unaotofautiana. Katika Ubudha, kufanikiwa kunamaanisha kufika kwa Nchi Safi ya Furaha Kubwa Sana, lakini hii inaitwaje katika Ukristo? Inaitwa “kuingia mbinguni” na “kunyakuliwa.” Wale ambao kwa kweli “wananyakuliwa” pia wanapitia mzunguko wa uhai na mauti mara tatu hadi saba, halafu, wakiwa wamekufa, wanaingia katika ulimwengu wa kiroho, kana kwamba walikuwa usingizini. Ikiwa walikuwa wanafaa wanaweza kusalia kushika wadhifa, na tofauti na watu walio duniani, hawatapata mwili kwa njia rahisi, au kulingana na mazoea.

Miongoni mwa dini hizi zote, mwisho zinaozungumzia na ambao zinajitahidi kufikia ni sawa na kufanikiwa katika Ubudha; ni vile tu “kufanikiwa” huku kunatimizwa kwa njia tofauti. Wote ni wa aina moja. Kwa hili kundi la watu wa dini hizi ambao wanaweza kufuata kabisa maadili ya kidini katika tabia zao, Mungu huwapa hatima nzuri, sehemu nzuri ya kwenda, na kuwatendea inavyofaa. Haya yote ni sawa, ila si jinsi ambavyo watu wanadhani, sawa? Sasa, baada ya kusikia kuhusu yanayowatokea watu katika Ukristo, mnahisi vipi? Je, mnahisi kwamba shida zao si za haki? Mnawahurumia? (Kidogo.) Hakuna kitu kinachoweza kufanywa; watajilaumu wenyewe. Kwa nini Ninasema hivi? Kazi ya Mungu ni ya kweli; Yeye yu hai na kweli, na kazi Yake inawalenga wanadamu wote na kila mmoja. Kwa nini basi wasikubali hili? Ni kwa nini wanampinga kwa nguvu na kumtesa Mungu? Wana bahati hata kuwa na mwisho kama huu, basi mbona mnawaonea huruma? Kwa wao kutendewa namna hii kunaonyesha uvumilivu mkubwa. Kulingana na kiasi ambacho wanampinga Mungu, wanapaswa kuangamizwa—bali Mungu hafanyi hili, anaushughulikia Ukristo sawa tu na dini ya kawaida. Sasa kuna haja ya kutoa maelezo ya kina kuhusu dini nyinginezo? Maadili ya dini zote hizi ni kuwa watu wapitie shida zaidi, wasifanye maovu, watende mambo mema, wasiwaapize watu wengine, wasiwahukumu wengine, wajitenge na ugomvi, na wawe watu wazuri—mafundisho ya kidini mengi ni ya aina hii. Na kwa hiyo, kama hawa watu wa imani—hawa watu wa dini na madhehebu mbalimbali—wanaweza kufuata kabisa maadili ya kidini, basi hawatafanya makosa au dhambi nyingi wakati wangali duniani, na baada ya kupata mwili mara tatu hadi saba, basi kwa jumla watu hawa, watu ambao wanaweza kufuata kabisa maadili ya kidini, watabaki kushikilia wajibu katika ulimwengu wa kiroho. Na je, kuna watu wengi wa aina hii? (La, hakuna wengi.) Jibu lako linategemea nini? Si rahisi kutenda mazuri, au kufuata amri na sheria. Ubudha hauwaruhusu watu kula nyama—unaweza kufanya hilo? Ungepaswa kuvaa kanzu za kijivu na kukariri maandiko ya sutra na kuimba majina ya Budha katika hekalu la wafuasi wa Budha siku nzima, ungeweza kufanya hivyo? Haingekuwa rahisi. Ukristo una Amri Kumi za Mungu, amri na sheria, je, ni rahisi kufuata? Si rahisi! Chukua mfano wa kutowaapia wengine: Watu hawawezi kufuata hii amri. Kwa kushindwa kujizuia wenyewe, wanaapa—na baada ya kuapa hawawezi kurudisha kiapo, basi wanafanya nini? Usiku wanakiri dhambi zao. Wakati mwingine baada ya kuwaapia wengine, bado kuna chuki mioyoni mwao, na hata wanazidi zaidi na kupanga ni lini watawadhuru. Kwa jumla, kwa wale wanaoishi katika hii imani iliyokufa, si rahisi kukosa kufanya dhambi au kutenda maovu. Na kwa hiyo, katika kila dini, ni watu wachache sana tu ndio wanaweza kufanikiwa kweli. Unadhani kwamba kwa sababu watu wengi sana wanafuata hizi dini, wengi wataweza kubaki kuchukua nafasi katika milki ya kiroho. Lakini si wengi hivyo, ni wachache tu ndio wanaweza kulifikia hili. Kwa jumla ni hayo tu kwa mzunguko wa uhai na mauti wa watu wenye imani. Kinachowatofautisha ni kwamba wanaweza kufanikiwa, na hiki ndicho kinawatofautisha na wasioamini.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 195)

Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Wafuasi wa Mungu

Baada ya hayo, hebu tuzungumzie mzunguko wa uhai na mauti wa wale wanaomfuata Mungu. Hili linawahusu, hivyo kuweni makini. Kwanza, fikiria kuhusu ni makundi gani ambamo watu wanaomfuata Mungu wanaweza kugawika. (Wateule wa Mungu na watendaji huduma.) Kuna mawili: wateule wa Mungu na watendaji huduma. Kwanza tutazungumza kuhusu wateule wa Mungu, ambao ni wachache. “Wateule wa Mungu” inarejelea nini? Baada ya Mungu kuumba vitu vyote na baada ya kuwepo wanadamu, Mungu alichagua kundi la watu ambao walimfuata, na wanaitwa tu “wateule wa Mungu.” Kuna mipaka maalum na umuhimu katika uchaguzi wa Mungu wa watu hawa. Mipaka ni maalum kwa vile ilizuiliwa kwa wachache waliochaguliwa,ambao ni lazima waje Anapofanya kazi muhimu. Na umuhimu ni upi? Kwa kuwa wao ni kikundi kilichochaguliwa na Mungu, umuhimu ni mkubwa. Yaani, Mungu anataka kuwakamilisha watu hawa, na kuwafanya wawe wakamilifu, na baada ya kazi Yake ya usimamizi kuisha, Atawachukua watu hawa. Je, umuhimu huu si mkubwa? Kwa hiyo, hawa wateule ni wa umuhimu mkubwa kwa Mungu, kwa kuwa ni wale ambao Mungu anakusudia kuwapata. Lakini watendaji huduma—vyema, hebu tuachane na uamuzi uliokwisha kufanywa na Mungu, na kwanza tuzungumzie asili yao. Maana ya kawaida ya “mtendaji huduma” ni mtu anayehudumu. Wanaohudumu ni wa kupita; hawahudumu kwa muda mrefu, au milele, ila wanaajiriwa au kuandikwa kwa muda mfupi. Wengi wao wanachaguliwa kutoka miongoni mwa wasioamini. Wajapo duniani ndipo inapoamriwa kwamba watachukua nafasi ya watendaji huduma katika kazi ya Mungu. Wanaweza kuwa walikuwa mnyama katika maisha yao yaliyopita, lakini pia wanaweza kuwa walikuwa mmoja wa wasioamini. Hiyo ndiyo asili ya watendaji huduma.

Hebu turejee kwa wateule wa Mungu. Wanapokufa, wateule wa Mungu huenda sehemu fulani tofauti kabisa na wasioamini na watu mbalimbali wenye imani. Ni sehemu ambayo wanaambatana na malaika na wajumbe wa Mungu, na ambayo inaendeshwa na Mungu binafsi. Japo katika sehemu hii, wateule wa Mungu hawawezi kumwona Mungu kwa macho yao wenyewe, si kama sehemu nyingine yoyote katika milki ya kiroho; ni sehemu ambayo hili kundi la watu huenda baada ya kufa. Wakifa, wao pia hupitia uchunguzi mkali kutoka kwa wajumbe wa Mungu. Na ni nini kinachochunguzwa? Wajumbe wa Mungu huchunguza njia zilizopitiwa na hawa watu katika maisha yao yote katika imani yao kwa Mungu, ikiwa waliwahi au hawakuwahi kumpinga Mungu wakati huo, au kumlaani, na ikiwa walitenda au hawakutenda dhambi mbaya au maovu. Uchunguzi huu unajibu swali la ikiwa mtu fulani ataondoka au atabaki. “Kuondoka” kunarejelea nini? Na “kubaki” kunarejelea nini? “Kuondoka” kunarejelea ikiwa, kulingana na mienendo yao, watabaki miongoni mwa madaraja ya wateule wa Mungu. “Kubaki” kunarejelea kuwa wanaweza kubaki miongoni mwa watu ambao wanafanywa na Mungu kuwa kamili katika siku za mwisho. Mungu ana mipango maalum kwa wale wanaobaki. Katika kila kipindi cha kazi Yake, Mungu atatuma watu kufanya kazi kama mitume au kufanya kazi ya kuyaamsha makanisa, au kuyahudumia. Lakini watu ambao wana uwezo wa kazi kama hizo hawapati miili mara kwa mara kama wasioamini, ambao wanazaliwa upya tena na tena; badala yake, wanarudishwa duniani kulingana na mahitaji na hatua ya kazi ya Mungu, na si wale wapatao mwili mara kwa mara. Je, kuna amri kuhusu ni lini wapate mwili? Je, wanakuja mara moja baada ya kila miaka michache? Je, wanakuja na hiyo haraka? Hawafanyi hivyo. Hii inategemea kazi ya Mungu, hatua ya kazi ya Mungu, na mahitaji Yake, na hakuna amri. Amri moja tu ni kwamba Mungu akifanya hatua ya mwisho ya kazi Yake katika siku za mwisho, wateule hawa wote watakuja. Wakija wote, hii itakuwa mara ya mwisho ambapo wanapata mwili. Na kwa nini hivyo? Hii inategemea matokeo yatakayopatikana katika hatua ya mwisho ya kazi ya Mungu—kwani katika hatua hii ya mwisho ya kazi, Mungu atawafanya wateule hawa kuwa kamili kabisa. Hili linamaanisha nini? Ikiwa, katika hii awamu ya mwisho, watu hawa watafanywa kuwa kamili, na kufanywa wakamilifu, basi hawatapata mwili kama awali; mchakato wa kuwa wanadamu utakamilika kabisa, sawa na mchakato wa kuzaliwa katika mwili mpya. Hili linawahusu wale watakaobaki. Je, wale ambao hawawezi kubaki huenda wapi? Wasioweza kubaki wanakuwa na sehemu mwafaka ya kwenda. Kwanza kabisa kwa sababu ya maovu yao, makosa waliyofanya, na dhambi walizofanya, wao pia wanaadhibiwa. Baada ya kuadhibiwa, Mungu atafanya mpango wawe miongoni mwa wasioamini, vinginevyo miongoni mwa watu mbalimbali wenye imani, kulingana na hali. Yaani, kuna hali mbili kwao: Moja ni, baada ya kuadhibiwa, labda kuishi miongoni mwa watu wa dini fulani wanapopata mwili tena, na nyingine ni kuwa wasioamini. Kama watakuwa wasioamini, basi watapoteza kila fursa. Lakini wakiwa watu wa imani—kwa mfano, wakiwa Wakristo—bado wangali na nafasi ya kurudi miongoni mwa madaraja ya wateule wa Mungu; kwa hili kuna uhusiano changamano sana. Kwa ufupi, ikiwa mmoja wa wateule wa Mungu atafanya kitu kitakachomkosea Mungu, wataadhibiwa sawa tu na watu wengine. Chukulia Paulo, kwa mfano, ambaye tulizungumzia awali. Paulo ni mfano wa wale wanaoadhibiwa. Je, mnapata picha ya yale ninayozungumzia? Je, mipaka ya wateule wa Mungu ni ya kudumu? (Kwa kiasi kikubwa ni ya kudumu.) Kiasi kikubwa chake ni cha kudumu, lakini sehemu ndogo si ya kudumu. Kwa nini hivyo? Nimerejelea hapa sababu moja dhahiri: kutenda maovu. Wanapotenda maovu, Mungu hawataki, na wakati Mungu hawataki, anawatupa miongoni mwa makabila na aina mbalimbali za watu, kitu ambacho kinawaacha bila tegemeo na kufanya kurudi kwao kuwe kugumu. Haya yote yanahusu mzunguko wa uhai na mauti wa wateule wa Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 196)

Kinachofuata ni mzunguko wa uhai na mauti wa watendaji huduma. Tulizungumzia tu asili za watendaji huduma, yaani, walipata mwili kutoka kwa wasioamini na wanyama katika maisha yao ya awali. Na ujio wa hatua ya mwisho ya kazi, Mungu amechagua kundi la watu hawa kutoka kwa wasioamini, na ni kundi ambalo ni maalum. Nia ya Mungu ya kuchagua watu hawa ni kuhudumia kazi Yake. “Huduma” si neno la jamala kutamka, wala si kitu ambacho mtu yeyote angependa, lakini tunapaswa kuona ambao linawalenga. Kuna umuhimu maalum katika uwepo wa watendaji huduma wa Mungu. Hamna mwingine awezaye kuchukua nafasi yao, kwa kuwa walichaguliwa na Mungu. Na ni ipi nafasi ya watendaji huduma? Kuwahudumia wateule wa Mungu. Kwa ujumla, kazi yao ni kuihudumia kazi ya Mungu, kushirikiana na kazi ya Mungu, na kushirikiana na ukamilisho wa Mungu wa wateule Wake. Haijalishi kama wanafanya kazi ngumu, wanafanya kazi fulani, au wanajiandaa kufanya kazi fulani, ni yapi mahitaji ya Mungu kwa hawa watu? Je, anawadai sana kwa masharti Yake kwao? (La, Mungu anawataka wawe waaminifu.) Watendaji huduma pia wanapaswa kuwa waaminifu. Haijalishi asili zako, au kwa nini Mungu alikuchagua, ni lazima uwe mwaminifu kwa Mungu, kwa kile anachokuagiza, na vilevile kazi unayoiwajibikia na jukumu unalolifanya. Ikiwa watendaji huduma wanaweza kuwa waaminifu, na kumridhisha Mungu, basi hatima yao itakuwaje? Wataweza kubaki. Je, ni baraka kuwa mtendaji huduma anayebaki? Kubaki kunamaanisha nini? Hii baraka inamaanisha nini? Kihadhi, hawafanani na wateule wa Mungu, wanaonekana tofauti. Kwa hakika, hata hivyo, wakipatacho katika maisha haya siyo sawa na wakipatacho wateule wa Mungu? Angalau, katika haya maisha ni sawa. Hamlipingi hili, naam? Matamko ya Mungu, neema ya Mungu, riziki ya Mungu, baraka za Mungu—ni nani hafurahii vitu hivi? Kila mtu anafurahia wingi wa haya. Kitambulisho cha mtendaji huduma ni mtendaji huduma, lakini kwa Mungu, ni miongoni mwa vitu vyote Alivyoumba—tofauti ni kwamba tu nafasi yao ni ile ya watendaji huduma. Kama mmoja wa viumbe wa Mungu, kuna tofauti kati ya watendaji huduma na wateule wa Mungu? Kwa hakika, hakuna. Kwa mazungumzo ya kawaida, kuna tofauti, katika kiini kuna tofauti, kwa kurejelea nafasi wanazoshika kuna tofauti, ila Mungu hawabagui hawa watu. Hivyo ni kwa nini hawa watu wanatambuliwa kama watendaji huduma? Unapaswa kuelewa hili. Watendaji huduma wanatokana na wasioamini. Kutaja wasioamini kunatuambia kuwa maisha yao ya awali ni mabaya: Wote ni wakana Mungu, katika maisha yao ya nyuma walikuwa wakana Mungu, hawakumwamini Mungu, na walikuwa mahasimu wa Mungu, wa ukweli, na vitu vizuri. Hawakumwamini Mungu, hawakuamini kuwa kuna Mungu, hivi wana uwezo wa kuelewa maneno ya Mungu? Ni haki kusema kwamba, kwa kiwango kikubwa, hawana. Sawa tu na wanyama wasivyo na uwezo wa kuelewa maneno ya mwanadamu, watendaji huduma hawaelewi Mungu anasema nini, Anahitaji nini, kwa nini Ana mahitaji kama hayo—hawaelewi, hivi vitu havieleweki kwao, wanabaki bila nuru. Na kwa sababu hii, watu hawa hawana uhai tuliouzungumzia. Je, bila uhai, watu wanaweza kuelewa ukweli? Je, wana ukweli? Je, wana uzoefu na ufahamu wa maneno ya Mungu? (La.) Hizo ndizo asili za watendaji huduma. Lakini kwa kuwa Mungu anawafanya hawa watu watendaji huduma, bado kuna viwango Anavyohitaji wawe navyo; Hawadharau, na Hawachukulii kwa uzembe. Japo hawaelewi maneno yake, na hawana uhai, bado Mungu ni mwema kwao, na bado kuna viwango Anavyohitaji wawe navyo. Mmevizungumzia hivi viwango hivi karibuni: Kuwa mwaminifu kwa Mungu, na kufanya Asemacho. Katika huduma yako ni lazima uhudumu unapohitajika, na ni lazima uhudumu hadi mwisho. Ikiwa unaweza kuwa mtendaji huduma mwaminifu, unaweza kuhudumu hadi mwisho, na unaweza kutimiza agizo uliloaminiwa na Mungu kikamilifu, basi utaishi maisha ya thamani, na utaweza kubaki. Ukitia bidii kidogo, ukijaribu kwa nguvu, ukiongeza maradufu jitihada zako za kumjua Mungu, ukiweza kuongea kidogo kuhusu ufahamu wa Mungu, ukiweza kumshuhudia Mungu, na zaidi, ukielewa kitu kuhusu mapenzi ya Mungu, ukiweza kushirikiana katika kazi ya Mungu, na ukiyazingatia kidogo mapenzi ya Mungu, basi wewe, mtendaji huduma, utapata bahati. Na hili litakuwa badiliko gani katika bahati? Hutaweza kubaki tu. Kutegemea tabia yako na malengo na juhudi zako binafsi, Mungu atakufanya mmoja wa wateule. Hii itakuwa bahati yako. Kwa watendaji huduma, ni nini kizuri kuhusu hili? Ni kwamba unaweza kuwa mmoja wa wateule wa Mungu. Wakiwa mmoja wa wateule wa Mungu, inamaanisha kuwa hawatapata tena mwili kama wanyama au wasioamini. Je, hiyo ni habari njema? Ndiyo, na ni habari njema. Inamaanisha, watendaji huduma wanaweza kufinyangwa. Si kwamba kwa mtendaji huduma, Mungu akimpangia awali kuhudumu, daima atahudumu; si lazima iwe hivyo. Kutegemea tabia yake binafsi, Mungu atamtendea tofauti, na kumjibu tofauti.

Lakini kuna watendaji huduma ambao hawana uwezo wa kumtumikia Mungu hadi mwisho; wakati wa huduma yao, kuna wale ambao wanajitoa nusu na kutelekeza Mungu, kuna wale ambao hufanya mambo mengi mabaya, na hata wale ambao wanasababisha madhara makubwa na kufanya uharibifu mkubwa kwa Kazi ya Mungu, kuna hata watendaji huduma ambao humlaani Mungu, na kadhalika—na ni nini maana ya matokeo haya yasiyorekebishika? Matendo maovu yoyote kama hayo humaanisha kufikia mwisho kwa huduma yao. Kwa sababu matendo yako wakati wa huduma yamekuwa maovu sana, kwa sababu umevuka mipaka yako, wakati Mungu anaona huduma yako haijafikia kiwango Atakutoa ustahiki wa kutoa huduma, Hatakubali ufanye huduma, Atakutoa mbele ya macho Yake, na kutoka katika nyumba ya Mungu. Au ni kwamba hutaki kufanya huduma? Je, siku zote hutamani kufanya maovu? Je, siku zote wewe si mwaminifu? Sawa basi, kuna suluhisho rahisi: Utanyang’anywa ustahiki wako wa kuhudumu. Kwa Mungu, kunyang’anya mtendaji huduma ustahiki wa kufanya huduma kuna maana kuwa mwisho wa mtendaji huduma huyu umetangazwa, na hatakuwa anastahili kufanya huduma kwa Mungu tena, Mungu hahitaji huduma zake tena, na haijalishi ni vitu vipi vizuri atasema, maneno haya yatabaki ya bure. Mambo yanapofikia kiwango hiki, hii hali itakuwa isiyorekebishika; watendaji huduma kama hawa hawana njia ya kurudi nyuma. Na Mungu huwafanyia nini watendaji huduma kama hawa? Anawaachisha tu kutoa huduma? La! Je, Anawazuia tu wasibaki? Au anawaweka katika upande mmoja. Na kuwangoja wabadilike? Hafanyi hivyo. Kwa kweli Mungu hana upendo sana kwa watendaji huduma. Iwapo mtu ana aina hii ya mwelekeo katika huduma yake kwa Mungu, Mungu, kutokana na matokeo ya mwelekeo huu, Atamnyang’anya ustahiki wake wa kutoa huduma, na kwa mara nyingine tena kumtupa miongoni mwa wasioamini. Na ni ipi hatima ya watendaji huduma waliorudishwa tena kati ya wasioamini? Ni sawa na ile ya wasioamini; kupata mwili kama wanyama na kupokea adhabu ya wasioamini katika ulimwengu wa kiroho. Na Mungu hatakuwa na maslahi ya kibinafsi katika adhabu yao, kwa kuwa hawana umuhimu wowote tena katika kazi ya Mungu. Huu si mwisho tu wa maisha yao ya imani kwa Mungu, ila mwisho wa hatima yao pia, kutangazwa kwa hatima yao. Kwa hiyo watendaji huduma wakihudumu vibaya, watapata matokeo wao wenyewe. Kama mtendaji huduma hana uwezo wa kufanya huduma hadi mwisho kabisa, au amenyang’anywa ustahiki wake wa kutoa huduma katikati ya njia, basi watatupwa miongoni mwa wasioamini—na kama watatupwa miongoni mwa wasioamini watashughulikiwa sawa na jinsi mifugo wanavyoshughulikiwa, sawa na watu wasio na akili au urazini. Ninapoielezea namna hiyo, unaelewa, naam?

Ilivyo hapo juu ndivyo Mungu anavyoushughulikia mzunguko wa uhai na mauti wa wateule wake na watendaji huduma. Mnajihisi vipi baada ya kusikia haya? Nimewahi kuzungumza kuhusu mada ambayo Nimeitaja sasa hivi, mada ya wateule wa Mungu na watendaji huduma? Kwa kweli Nimewahi, lakini hamkumbuki. Mungu ni mwenye haki kwa wateule wake na watendaji huduma. Kwa vyovyote vile Yeye ni mwenye haki, siyo? Kuna mahali popote unaweza kupata makosa? Wapo watu ambao watasema: “Kwa nini Mungu ni mvumilivu sana kwa wateule? Na kwa nini anawavumilia kidogo sana watendaji huduma?” Kuna yeyote angependa kuwatetea watendaji huduma? “Je, Mungu anaweza kuwapa watendaji huduma muda zaidi, na kuwa mstahimilivu na mvumilivu zaidi kwao?” Haya maneno yako sahihi? (Hapana, hayapo sahihi.) Na ni kwa nini hayapo sahihi? (Kwa kuwa tumeonyeshwa neema kweli kwa kufanywa kuwa watendaji huduma.) Watendaji huduma wameonyeshwa neema kwa kuruhusiwa kufanya huduma! Bila ya dhana “watendaji huduma,” na bila Kazi ya watendaji huduma, hawa watendaji huduma wangekuwa wapi? Miongoni mwa wasioamini, wakiishi na kufa pamoja na mifugo. Ni neema kubwa wanayoifurahia leo, kuruhusiwa kuja mbele za Mungu, na kuja katika nyumba ya Mungu! Hii ni neema kubwa! Kama Mungu hakukupa nafasi ya kutoa huduma, usingekuwa na nafasi ya kuja mbele za Mungu. Kwa kusema machache, hata kama wewe ni Mbudha na umefanikiwa, sanasana wewe ni mtumwa katika ulimwengu wa kiroho; hutaweza kamwe kumwona Mungu, au kusikia sauti Yake, au kusikia maneno Yake, au kuhisi upendo Wake na baraka Zake kwako, na hata isingewezekana kamwe kuonana na Yeye uso kwa uso. Kilicho tu mbele ya wafuasi wa Budha ni kazi rahisi. Hawawezi kamwe kumjua Mungu, na wanaitikia na kutii kiupofu tu, wakati ambapo watendaji huduma wanafaidi mengi sana katika hatua hii ya kazi. Kwanza, wanaweza kuonana na Mungu uso kwa uso, kusikia sauti Yake, kuyasikia maneno Yake, na kupitia neema na baraka Anazowapa watu. Aidha, wanaweza kufurahia maneno na ukweli unaopewa na Mungu. Watendaji huduma kwa kweli hupata mengi zaidi! Basi, kama mtendaji huduma, huwezi hata kutia juhudi inayofaa, je, Mungu bado atakuweka? Hawezi kukuweka. Hataki mengi kutoka kwako lakini hufanyi chochote Anachotaka vizuri, hujawajibika ipasavyo—na kwa hivyo, bila shaka, Mungu hawezi kukuweka. Hiyo ndiyo tabia ya haki ya Mungu. Mungu hakudekezi, lakini wala Hakubagui. Mungu anafanya kazi na kanuni hizo. Mungu hutekeleza mambo jinsi hii kwa watu na viumbe wote.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 197)

Inapokuja katika ulimwengu wa kiroho, kama viumbe mbalimbali waliomo watafanya kitu kibaya, kama hawafanyi kazi yao inavyostahili, Mungu pia ana sheria za peponi na amri zifaazo kuwashughulikia—hili halipingwi. Basi, katika maelfu kadhaa ya miaka ya kazi ya usimamizi ya Mungu, wasimamizi wengine ambao walifanya maovu wameangamizwa, wengine, leo, wangali wanazuiliwa na kuadhibiwa. Hili ndilo linafaa kukabiliwa na kila kiumbe aliye katika ulimwengu wa kiroho. Akifanya kitu kibaya au kutenda maovu, anaadhibiwa—ambayo ni sawa na jinsi Mungu anavyotenda kwa wateule Wake na watendaji huduma. Na kwa hivyo, iwe ni katika ulimwengu wa kiroho au ulimwengu yakinifu, kanuni ambazo Mungu hutekeleza matendo hazibadiliki. Bila kujali kama unaweza kuona matendo ya Mungu au la, kanuni zao hazibadiliki. Daima, Mungu amekuwa na kanuni sawa kwa jinsi Anavyotekeleza matendo kwa vitu vyote na kuvishughulikia vitu vyote. Hili halibadiliki. Mungu atakuwa mkarimu kwa wale walio miongoni mwa wasioamini ambao angalau wanaishi ipasavyo, na kuwapa nafasi wale walio katika kila dini ambao wana tabia nzuri na hawatendi maovu, kwa kuwaruhusu kutekeleza wajibu wao katika vitu vyote vinavyosimamiwa na Mungu, na kufanya kile ambacho wanafaa kufanya. Vivyo hivyo, kati ya wale wanaomfuata Mungu, kati ya wateule Wake, Mungu habagui mtu yeyote kulingana na kanuni Zake hizi. Ni mwema kwa kila mtu anayeweza kumfuata kwa dhati, na kupenda kila mtu anayemfuata kwa dhati. Ni kwamba tu kwa aina hizi mbalimbali za watu—wasioamini, aina tofauti za watu wenye imani, na wateule wa Mungu—anachowazawadia wao ni tofauti. Chukulia wasioamini: hata kama hawamwamini Mungu, na Mungu huwaona kama mifugo, miongoni mwa kila kitu kila mmoja wao ana chakula, mahali pao wenyewe, na mzunguko wa kawaida wa uhai na mauti. Wanaotenda maovu wanaadhibiwa, na wanaofanya mazuri wanabarikiwa na hupokea wema wa Mungu. Hivyo ndivyo ilivyo? Kwa watu wenye imani, kama wanaweza kutii hasa maadili ya kidini, kizazi baada ya kizazi, basi baada ya hivi vizazi vyote Mungu hatimaye atatoa uamuzi Wake kwao. Vivyohivyo, kwa wewe leo, awe mmoja wa wateule wa Mungu au mtendaji huduma, Mungu vilevile atakuwazisha na kuamua mwisho wako kulingana na kanuni na amri za utawala ambazo Ameziweka. Miongoni mwa aina hizi kadhaa za watu—aina tofauti za watu wa imani, walio katika dini tofauti—je, Mungu amewapa nafasi ya kuishi? Uko wapi Uyahudi? Mungu ameingilia katika imani yao? Hajaingilia, siyo? Na vipi kuhusu Ukristo? Hajaingilia pia? Anawaruhusu kufuata mipangilio yao wenyewe, na Hasemi nao, au kuwapa nuru yoyote, na, zaidi ya hayo, Hawafichulii kitu chochote: “Kama unafikiria ni sahihi, basi amini hivyo.” Wakatoliki wanamwamini Maria, na kwamba ni kupitia kwa Maria ambapo habari zilimfikia Yesu; hiyo ndiyo aina yao ya imani. Na Mungu amewahi kurekebisha imani yao? Mungu huwapa uhuru, Mungu hawasikizi, na huwapa sehemu fulani ambapo wataishi. Na kwa Waisilamu na wafuasi wa Budha, je, Yuko hivyo pia? Ameweka mipaka kwa ajili yao, pia, na kuwaruhusu kuwa na mahali pao wenyewe pa kuishi, bila ya kuingilia imani zao. Yote yamepangwa vizuri. Na unaona nini katika haya yote? Kwamba Mungu ana mamlaka, lakini hatumii vibaya mamlaka Yake. Mungu hupanga vitu vyote katika mpangilio taratibu, na ni mwenye utaratibu, na katika hili busara na kudura Zake vinadhihirika.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 198)

Utambulisho na Hadhi ya Mungu Mwenyewe

Mungu ndiye mtawala wa vitu vyote, na anayeendesha vitu vyote. Aliumba vitu vyote, Anaendesha vitu vyote, na pia Anatawala vitu vyote na kukimu vitu vyote. Hii ndiyo hadhi ya Mungu, na utambulisho wa Mungu. Kwa vitu vyote na vyote vilivyopo, utambulisho wa kweli wa Mungu ni Muumbaji, na Mtawala wa vitu vyote. Huo ni utambulisho unaomilikiwa na Mungu, na ni wa kipekee miongoni mwa vitu vyote. Hakuna Kati ya viumbe wa Mungu—wawe miongoni mwa wanadamu, au katika ulimwengu wa kiroho—ambao wanaweza kutumia namna yoyote au kisingizio kuiga au kuchukua nafasi ya utambulisho wa Mungu na hadhi Yake, kwa kuwa kuna mmoja tu kati ya vitu vyote anayemiliki huu utambulisho, nguvu, mamlaka, na uwezo wa kutawala vitu vyote: Mungu wetu wa kipekee Mwenyewe. Anaishi na kutembea miongoni mwa vitu vyote; Anaweza kufikia palipo mbali zaidi, juu ya vitu vyote; Anaweza kunyenyekea kwa kuwa mwanadamu, kuwa mmoja wa wenye mwili na damu, kuonana ana kwa ana na watu na kushiriki na wao dhiki na faraja; wakati huo huo, Anaamuru vitu vyote, na Huamua hatima ya vitu vyote, na njia itakayofuata, zaidi na hayo, Anaongoza hatima za wanadamu wote, na njia za wanadamu. Mungu kama huyu anastahili kuabudiwa, kuheshimiwa, na kujulikana na viumbe wote. Na hivyo, pasipo kujali uko katika kundi na aina gani ya wanadamu, kumwamini Mungu, kumfuata Mungu, kumheshimu Mungu sana, kukubali utawala wa Mungu, na kukubali mipango ya Mungu katika hatima yako ndio uamuzi wa pekee, na uamuzi unaofaa, kwa mtu yeyote, kwa kiumbe chochote kinachoishi. Katika upekee wa Mungu, watu huona kwamba mamlaka Yake, tabia Yake ya haki, kiini Chake, na namna ambazo Anakirimia vitu vyote ni za kipekee; upekee Wake unabainisha utambulisho wa kweli wa Mungu Mwenyewe, na unabaini hadhi Yake. Na kwa hivyo, miongoni mwa viumbe vyote, kama kuna kiumbe anayeishi katika ulimwengu wa kiroho au miongoni mwa wanadamu angetamani kusimama badala ya Mungu, haingewezekana, sawa na kujaribu kumuiga Mungu. Huu ni ukweli. Ni mahitaji yapi kwa mwanadamu aliyonayo Muumbaji na Mtawala kama huyu, ambaye Aliye na utambulisho, nguvu, na hadhi ya Mungu Mwenyewe? Hili linapaswa kuwa wazi kwa kila mtu, na linapaswa kukumbukwa nanyi, na ni muhimu sana kwa Mungu na mwanadamu!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 199)

Mielekeo Mbalimbali ya Wanadamu kwa Mungu

Jinsi watu wamtendeavyo Mungu huamua hatima yao, na huamua jinsi Mungu anavyowatendea na kuwashughulikia. Kufikia sasa nitawapa mifano kadhaa ya jinsi watu wanavyotenda mbele za Mungu. Hebu tusikie kitu kuhusu ama mienendo na tabia ambazo kwazo wanamtendea Mungu ni sahihi au la. Hebu tuangalie mwenendo wa aina saba za watu wafuatao:

1) Kuna aina moja ya watu ambao mwelekeo wao kwa Mungu haswa ni wa kipuuzi. Wanafikiria kuwa Mungu ni kama Bodhisattva au kiumbe takatifu wa masimulizi ya kibinadamu, na kuwataka watu kusujudu mara tatu wanapokutana na kuchoma ubani baada ya kula. Kwa hivyo, katika mioyo yao, wanapomshukuru Mungu kwa neema Yake, na kuwa wenye shukrani kwa Mungu, mara nyingi wana msukumo kama huo. Hivyo wanatamani Mungu wanaomwamini leo, kama kiumbe takatifu wanayemtamania ndani ya mioyo yao, anaweza kukubali mienendo yao Kwake ambapo wanasujudu mara tatu wanapokutana, na kuchoma ubani baada ya kula.

2) Watu wengine wanamwona Mungu kama Budha anayeishi, mwenye uwezo wa kutoa wanaoishi wote kutoka kwenye mateso, na kuwaokoa; wanaona Mungu kama Budha anayeishi mwenye uwezo wa kuwatoa kwenye mateso mengi. Imani ya watu hawa kwa Mungu ni kumwabudu Mungu kama Buddha. Ijapokuwa hawachomi ubani, kusujudu, au kutoa sadaka, katika nyoyo zao Mungu ni kama tu Buddha, na huwataka tu wawe wema na wenye huruma, kuwa wasiue chochote kilicho hai, wasiwaapie wengine, waishi maisha yanayoonekana kuwa manyoofu, na wasifanye chochote kibaya—vitu hivi tu. Huyu ndiye Mungu mioyoni mwao.

3) Watu wengine humwabudu Mungu kama mtu mkubwa au maarufu. Kwa mfano, kwa namna yoyote mtu huyu mkubwa hupenda kuongea, kwa kiimbo chochote huongea, maneno na msamiati anaotumia, kiimbo chake, ishara zake za mikono, maoni na matendo yake, ukali wake—wanaiga yote, na hivi ndivyo vitu ambavyo ni lazima watavisababisha katika mwendo wa imani yao kwa Mungu.

4) Watu wengine wanamwona Mungu kama mfalme, wanahisi kuwa Yuko juu ya vitu vyote vingine, na hakuna anayejaribu kumkosea—na wakifanya hivyo, wataadhibiwa. Wanaabudu mfalme kama huyo kwa sababu wafalme huwa wanashikilia sehemu fulani kwenye mioyo yao. Mawazo, tabia, mamlaka, na asili ya wafalme—hata na maslahi na maisha yao ya kibinafsi—yote huwa kitu ambacho watu hawa lazima waelewe, masuala na mambo ambayo wanashughulika nayo, na hivyo wanamwabudu Mungu kama mfalme. Imani ya namna hiyo inachekesha.

5) Watu wengine wana imani fulani katika uwepo wa Mungu, ambayo ni kubwa na isiyotingishika. Kwa sababu ufahamu wa Mungu kwao ni wa juujuu mno na hawana mazoea ya maneno ya Mungu, wanamwabudu kama sanamu. Sanamu hii ni Mungu aliye ndani ya mioyo yao, ni kitu ambacho wanafaa kuogopa na kusujudia, na ambayo wanalazimika kufuata na kuiga. Wanamwona Mungu kama sanamu, ambayo wanafaa kufuata maisha yao yote. Wanaiga sauti ambayo kwayo Mungu huzungumza, na kwa nje wanaiga wale ambao Mungu anapenda. Aghalabu wanafanya mambo ambayo yanaonekana kuwa manyoofu, safi, na ya kweli, na wanafuata hii sanamu kama mwenzao au mwandani wao ambaye wanaweza kushirikiana. Hiyo ndiyo aina ya imani yao.

6) Kuna watu ambao, kando na kusoma maneno mengi ya Mungu na kuwa wameyasikia mahubiri mengi, wanahisi ndani ya nyoyo zao kuwa msimamo tu wa mienendo yao kwa Mungu ni kuwa kila wakati wanafaa wawe watiifu na kujipendekeza, la sivyo wanafaa kumsifu Mungu na kumwabudu kwa njia isiyo halisi. Wanaamini kuwa Mungu ni Mungu anayewahitaji kutenda hivyo, na wanaamini kuwa wasipofanya hivyo, basi wakati wowote wanaweza kuchochea hasira Yake au kumtenda dhambi, na kwamba kwa sababu ya kutenda dhambi Mungu atawaadhibu. Huyo ndiye Mungu mioyoni mwao.

7) Kisha kuna watu wengi, wanaotafuta riziki ya kiroho katika Mungu. Kwa sababu wanaishi katika ulimwengu huu, hawana amani au furaha, na hakuna wanapopata faraja. Baada ya kumpata Mungu, wanapokuwa wameona na kusikia maneno Yake, ndani ya mioyo yao wanafurahi na kusisimka kisiri. Hii ni kwa sababu wanaamini kuwa tayari wamepata mahali ambapo patawapa furaha, kwamba hatimaye wamepata Mungu ambaye atawapa riziki ya kiroho. Baada ya kukubali Mungu na kuanza kumfuata, wanakuwa wenye furaha, maisha yao yanakamilishwa, hawako kama wengine wasioamini tena, wanaotembea usingizini maishani mwao kama wanyama, na wanahisi kuwa kuna kitu cha kutamania katika maisha. Kwa hivyo, wanafikiri kuwa huyu Mungu anaweza kuwatimizia mahitaji yao ya kiroho na kuleta furaha kubwa katika mawazo na Roho. Bila ya kujua, wanakuwa hawawezi kumwacha huyu Mungu anayewapa riziki ya kiroho, Anayeleta furaha katika Roho na familia zao. Wanaamini kuwa imani katika Mungu haihitaji zaidi ya kuwapa riziki ya kiroho.

Je, mielekeo kumwelekea Mungu ya watu hawa wa aina mbalimbali waliotajwa hapo juu ipo miongoni mwenu? (Ipo.) Kama, katika imani yao katika Mungu, moyo wa mtu una mwelekeo wowote kati ya hii, je, kweli wanaweza kuja mbele za Mungu? Kama watu wana mwelekeo wowote kati ya hii katika mioyo yao, je, wanamwamini Mungu? Je, wanamwamini Mungu Mwenyewe yule wa kipekee? (La.) Kwa kuwa humwamini Mungu wa kipekee Mwenyewe, unamwamini nani? Kama unachoamini si Mungu Mwenyewe wa kipekee, kuna uwezekano unaamini katika sanamu, mtu maarufu, au Bodhisattva, kuwa unamwabudu Budha moyoni mwako. Zaidi ya hayo, kuna uwezekano unaamini katika mtu wa kawaida. Kwa muhtasari, kwa sababu ya aina tofautitofauti za imani za watu na mielekeo kwa Mungu, watu humweka Mungu wa utambuzi wao wenyewe katika nyoyo zao, wanamlazimishia Mungu fikira zao, wanaweka fikira na mielekeo yao kuhusu Mungu sambamba na Mungu Mwenyewe wa kipekee, na baadaye wanayadhihirisha ili yafanywe kuwa takatifu. Ina maana gani watu wakiwa na mielekeo hiyo isiyofaa kwa Mungu? Ina maana kuwa wamemkataa Mungu wa kweli Mwenyewe na kuabudu Mungu bandia, na ina maana kuwa wakati uleule wanapomwamini Mungu, wanamkataa Mungu, wanampinga, na kuwa wanakana uwepo wa Mungu wa kweli. Kama watu watazidi kushikilia imani za aina hiyo, matokeo yao yatakuwa gani? Kwa aina hiyo ya imani, je, wanaweza kufikia karibu na kutimiza matakwa ya Mungu? (La, hawawezi.) Kinyume cha hayo, kwa sababu ya dhana na fikira zao, watu watazidi kuwa mbali na njia ya Mungu, kwa kuwa njia wanayoifuata ni kinyume cha njia ambayo Mungu anawahitaji waifuate. Umekwisha kusikia hadithi ya “kwenda kusini kwa kuendesha gari la farasi kuelekea kaskazini”? Hii yaweza kuwa ni mfano wa kwenda kusini kwa kuendesha gari la farasi kuelekea kaskazini. Watu wakimwamini Mungu kwa njia hii ya kipumbavu, basi kadiri unavyojaribu kwa nguvu, ndivyo utakavyokuwa mbali zaidi na Mungu. Na kwa hiyo nakuonya hivi: Kabla ya kufunga safari, ni lazima kwanza ujue kama unaenda njia iliyo sawa. Lenga katika juhudi zako, kuwa na uhakika na kujiuliza, “Je, Mungu ninayemwamini ni Mtawala wa vitu vyote? Je, huyu Mungu ninayemwamini ni mtu tu wa kunipa riziki ya kiroho? Ni sanamu yangu? Je, huyu Mungu ninayemwamini anataka nini kutoka kwangu? Mungu huwa anakubali chochote ninachokifanya? Je, kila kitu ninachokifanya na kutafuta kinalingana na kazi ya kumjua Mungu? Je, kinalingana na mahitaji ya Mungu kwangu? Je, njia ninayoifuata inajulikana na kukubaliwa na Mungu? Je, Mungu anaridhishwa na imani yangu?” Aghalabu na mara kwa mara unafaa ujiulize haya maswali. Kama ungetaka kuutafuta ufahamu wa Mungu, basi lazima uwe na dhamiri safi na malengo wazi ndipo uweze kumridhisha Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 200)

Mwelekeo Ambao Mungu Anahitaji Mwanadamu Awe Nao Kwake

Kwa kweli, Mungu hana mahitaji sana kwa wanadamu—au angalau, hana mahitaji kama watu wanavyodhani. Ikiwa Mungu hangetamka maneno yoyote, ikiwa hangeonyesha tabia Yake au matendo yoyote, basi kumjua Mungu kungekuwa kugumu sana kwenu, kwa sababu watu wangelazimika kukisia nia ya Mungu na mapenzi Yake, kitu ambacho ni kigumu sana kwao. Lakini katika hatua ya mwisho ya Kazi Yake, Mungu amenena maneno mengi, kufanya kiwango kikubwa cha kazi, na kufanya mahitaji mengi kwa wanadamu. Katika maneno Yake, na kiwango kikubwa cha kazi Yake, amejulisha watu anachokipenda, anachokichukia, na wanafaa kuwa aina gani ya watu. Baada ya kuelewa vitu hivi, ndani ya nyoyo watu wanafaa kuwa na maelezo sahihi ya mahitaji ya Mungu, kwa kuwa hawamwamini Mungu wakiwa katika hali isiyo dhahiri na ya kinadharia, nahawamwabudu tena yule Mungu asiye yakini, au kumfuata Mungu katika ukosefu uyakini na udhahania na utupu; badala yake, watu wanaweza kusikia maneno ya Mungu, wanaweza kuelewa viwango vya mahitaji ya Mungu, na kuvifikia, na Mungu hutumia lugha ya wanadamu kuwaambia watu yale yote wanafaa kujua na kulewa. Leo, kama watu bado hawamjui Mungu na kile Anachohitaji kutoka kwao; ikiwa hawajui kwa nini mtu anapaswa kumwamini Mungu, wala jinsi ya kumwamini ama kumtendea—basi kuna shida na hili. … Mahitaji sahihi ya Mungu kwa wanadamu na wale ambao wanamfuata ni kama ifuatavyo. Mungu anahitaji mambo matano kutoka kwa wale wanaomfuata; imani ya kweli, ufuasi wenye uaminifu, utiifu kamili, ufahamu wa kweli na heshima za kutoka moyoni.

Katika mambo haya matano, Mungu anahitaji kuwa watu wasimshuku tena, wala kumfuata wakitumia fikira zao au mitazamo ikosayo uyakini na iliyo dhahania; Ni lazima wamfuate Mungu bila fikira au dhana zozote. Mungu anahitaji kuwa wote wanaomfuata wafanye hivyo kwa uaminifu, sio kwa shingo upande au bila kujizatiti. Mungu anapokupa mahitaji yoyote, au kukujaribu, kukuhukumu, kukushughulikia na kukupogoa, au kukuadhibu na kukuangamiza, unapaswa kuwa mtiifu kabisa Kwake. Hufai kuuliza kilichosababisha, au kuweka masharti, au hata uongee kuhusu sababu. Utiifu wako lazima uwe usio na shaka. Maarifa ya Mungu ni kipengele ambacho watu wengi wanakosea. Mara kwa mara wanamlazimishia Mungu misemo, matamshi, na maneno ambayo hayahusiani na Yeye, wakiamini kuwa haya maneno ndiyo ya kweli kuhusu kumfahamu Mungu. Kumbe hawajui kuwa hii misemo, ambayo inatoka kwa fikira za watu, ung'amuzi wao, na busara zao, havina uhusiano wowote na kiini cha Mungu. Na kwa hiyo, Ninataka kukwambia kuwa, katika ufahamu wa watu unaotamaniwa na Mungu, Mungu haulizi tu kwamba umtambue Mungu na maneno Yake, lakini kuwa ufahamu wako juu ya Mungu ni sahihi. Hata kama unaweza kusema sentensi moja tu, au una ufahamu mdogo tu, huu ufahamu mdogo ni sahihi na wa kweli, na unalingana na kiini cha Mungu Mwenyewe. Kwa kuwa Mungu hapendi sifa na wao kumtukuza Yeye kwa hali isiyo halisi na yenye nia mbaya. Zaidi ya hayo, Anachukia watu wanapomchukulia kama hewa. Anachukia ambapo, wakati wa majadiliano juu ya mada kuhusu Mungu, watu wanazungumza kimzaha, wakiongea kwa hiari bila ya kujali, wakiongea wapendavyo; zaidi ya hayo, anawachukia wale wanaojifanya wanamjua Mungu, na wanaringa kuhusu ufahamu wa Mungu, wakijadili mada kuhusu Mungu bila mipaka au kipimo. La mwisho Kati ya yale mahitaji matano lilikuwa ni kumheshimu Mungu kutoka moyoni. Hili ndilo hitaji kuu la Mungu kwa wale wote wanaomfuata. Wakati mtu ana ufahamu wa kweli na sahihi kumhusu Mungu, anaweza kumheshimu Mungu na kuepuka maovu. Heshima hii hutoka ndani ya moyo wake, ni ya hiari, na sio kwa sababu Mungu amemshurutisha. Mungu hataki utoe zawadi ya mwelekeo wowote wa kupendeza, au tabia, au mienendo ya nje Kwake; badala yake, anataka kwamba umheshimu na umwogope kutoka ndani ya moyo wako. Heshima hii inaafikiwa kutokana na mabadiliko katika tabia ya maisha yako, kwa sababu una ufahamu juu ya Mungu, kwa sababu unaelewa matendo ya Mungu, kwa sababu ya uelewa wako wa kiini cha Mungu, na kwa sababu umetambua ukweli kuwa wewe ni mmoja wa viumbe wa Mungu. Na kwa hiyo, nia yangu ya kutumia neno “kutoka moyoni” kwa kurejelea heshima hapa ni kwamba wanadamu waelewe kuwa heshima ya watu kwa Mungu inapaswa kutoka ndani ya mioyo yao.

Sasa yafikirie hayo matakwa matano: kuna yeyote kati yenu anaweza kupata matatu ya kwanza? Ambapo Ninamaanisha uaminifu wa kweli, ufuasi wenye uaminifu, na utiifu kamili. Kuna wowote kati yenu wanaoweza mambo haya? Najua Nikisema yote matano, basi bila kuuliza hapatakuwa na hata mmoja kati yenu anayeweza—lakini nimeyapunguza hadi matatu. Tafakari kama umeyapata au la. Je, “uaminifu wa kweli” ni rahisi kuupata? (La, sio rahisi.) Sio rahisi, kwa kuwa mara nyingi watu humtilia Mungu mashaka. Na, je, “ufuasi wenye uaminifu”? Huu “uaminifu” una maana gani? (Sio kwa shingo upande ila kwa moyo wote.) Sio kwa shingo upande ila kwa moyo wote. Mmegonga ndipo! Kwa hiyo, je, mna uwezo wa kupata hili hitaji? Inabidi mjitahidi zaidi—siyo? Kwa sasa bado hamjapata hili hitaji. Kuhusu “utiifu kamili”—je, mmepata hilo? (Hapana.) Bado hamjapata hilo, pia. Mara nyingi nyinyi si watiifu na ni waasi, mara nyingi hamsikilizi, au kupenda kutii, au kutaka kusikia. Haya ndiyo mahitaji matatu ya msingi wanayopata watu baada ya kuingia katika maisha yao, na bado hamjayapata. Kwa hiyo, kwa wakati huu, mna uwezo mkubwa? Leo, baada ya kunisikia nikisema maneno haya, mna wasiwasi? (Ndiyo.) Ni sawa kuwa mna wasiwasi. Msiwe na wasiwasi Ninahisi wasiwasi kwa niaba yenu. Sitakwenda katika mahitaji hayo mengine mawili; bila shaka, hakuna anayeweza kuyafikia. Mna shauku. Kwa hivyo mmebaini malengo yenu? Malengo yapi, kuelekeza upande gani, mnapaswa kuyafuata, na kujitolea jitihada zenu? Mna lengo? Hebu niongee waziwazi: mnapofikia mahitaji haya matano, mtakuwa mmemridhisha Mungu. Kila mojawapo ni ishara, ishara ya watu wakiingia katika maisha wakiwa wamefikia ukomavu, na lengo la mwisho la hii. Hata kama Ningechukua moja kati ya mahitaji na kuongea kwa kina kulihusu na kinachohitajika, haiwezi kuwa rahisi kupata; ni lazima mpitie kiwango fulani cha matatizo na kufanya kiasi fulani cha juhudi. Na ni aina gani ya mawazo mnapaswa kuwa nayo? Yanapaswa kuwa sawa na yale ya mgonjwa wa saratani anayesubiri kwenda kwenye meza ya upasuaji. Na ni kwa nini Ninasema haya? Kama ungependa kumwamini Mungu, na kumpata Mungu na kupata ridhaa Yake, basi kama hutapitia katika kiasi fulani cha shida, au kufanya kiwango fulani cha juhudi, hutaweza kupata vitu hivi. Umesikia mahubiri mengi, lakini kuyasikia hakumaanishi kuwa haya mahubiri ni yako; ni lazima uyachukue na kuyageuza yawe kitu ambacho ni chako, ni lazima uyasimilishe maishani mwako, na kuyaleta katika uwepo wako, ukiyaruhusu maneno na mahubiri haya yakuongoze katika maisha yako, na kuleta dhamana na maana ya uhai katika maisha yako—na hivyo basi itakuwa ni thamani kuwa uliyasikia maneno haya. Kama maneno haya Ninayoyanena hayaleti mabadiliko yoyote katika maisha yenu, au thamani yoyote katika uwepo wako, basi hakuna haja ya kuyasikiliza. Mnaelewa haya, ndiyo? Baada ya kuelewa haya, basi kilichobaki ni juu yenu wenyewe. Ni lazima mfanye kazi! Ni lazima muwe na bidii katika kila jambo! Msiwe huku na kule—wakati unapita upesi! Wengi wenu wamemwamini Mungu kwa zaidi ya miaka kumi. Fikiria nyuma kwa hii miaka kumi: Umenufaika kiasi gani? Na mmesalia na miongo mingapi ya haya maisha? Sio mirefu. Sahau kuhusu iwapo kazi ya Mungu inakusubiri, iwapo Amekuachia nafasi, iwapo Atafanya kazi ile ile tena; usizungumze kuhusu hili. Unaweza kurudisha nyuma miaka yako kumi iliyopita? Kwa kila siku inayopita, na kila hatua unayochukua, siku ambazo unazo hupunguzwa kwa siku moja. Muda haumsubiri mwanadamu yeyote! Utanufaika tu kutokana na imani kwa Mungu kama utaichukulia kama kitu kikubwa zaidi maishani mwako, muhimu zaidi kuliko chakula, mavazi, au kitu kingine chochote! Kama huwa unaamini tu unapokuwa na wakati, na huwezi kutoa umakini wako wote kwa imani yako, kama siku zote umetatizwa na vurugu, basi hutafaidi chochote.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Iliyotangulia: Kumjua Mungu (IV)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp