Kumjua Mungu (III)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 83)

Mungu Hutumia Maneno Kuumba Vitu Vyote

Mwa 1:3-5 Na Mungu akasema, Na kuwe na mwanga; kukawa na mwanga. Mungu akauona mwanga, na kuwa ulikuwa mzuri: na Mungu akautenga mwanga na kiza. Naye Mungu akauita mwanga Mchana, na kiza akaliita Usiku. Na jioni na asubuhi yalikuwa siku ya kwanza.

Mwa 1:6-7 Na Mungu alisema, Na kuwe na mbingu katikati ya maji, na uigawanye maji kutoka kwa maji. Na Mungu akaitengeneza mbingu, na akayagawanya yale maji yaliyokuwa chini ya mbingu kutoka kwa yale maji yaliyokuwa juu ya mbingu: na kukawa vivyo hivyo.

Mwa 1:9-11 Naye Mungu akasema, Nayo maji yaliyo chini ya mbingu yakonge pahali pamoja, na ardhi kavu ionekane; na kukawa vivyo hivyo. Naye Mungu akaiita nchi kavu Dunia: na kukonga kwa maji akakuita Bahari: naye Mungu akaona kwamba ni vyema. Naye Mungu akasema, Na dunia izae majani, mche ambao unatoa mbegu, na mti wa matunda ambao unazaa tunda kwa aina yake, ambao mbegu zake ziko ndani yake, juu ya dunia: na kukawa vivyo hivyo.

Mwa 1:14-15 Naye Mungu akasema, Kuwe na mwangaza katika anga la mbingu kwa minajili ya kutenga mchana na usiku; na uwe ndio ishara; na majira, na siku na miaka: Na tena uwe ndio mwangaza katika anga la mbingu kwa minajili ya kupa nchi nuru; na ikawa vile.

Mwa 1:20-21 Na Mungu akasema, Na maji yalete kwa wingi kiumbe asongaye aliye na uhai, na ndege wanaoweza kuruka juu ya nchi katika anga wazi la mbingu. Naye Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na viumbe wote walio na uhai wasongao, ambao maji yalileta kwa wingi, kwa aina yao, na kila ndege anayeruka kwa aina yake: na Mungu akaona kuwa ilikuwa vizuri.

Mwa 1:24-25 Naye Mungu akasema, Dunia na ilete kiumbe kilicho hai kwa namna yake, mifugo, na kitu kinachotambaa, na wanyama wa mwituni kwa namna yake: na ikafanyika. Naye Mungu akaumba wanyawa wa mwituni kwa namna yake, na mifugo kwa namna yake, na chote kinachotambaa duniani kwa namna yake: na Mungu akaona kwamba ni vizuri.

Kwenye Siku ya Kwanza, Mchana na Usiku wa Mwanadamu Vinazaliwa na Kujitokeza Waziwazi kwa Msaada wa Mamlaka ya Mungu

Hebu tuangalie kifungu cha kwanza: “Na Mungu akasema, Na kuwe na mwanga; kukawa na mwanga. Mungu akauona mwanga, na kuwa ulikuwa mzuri: na Mungu akautenga mwanga na kiza. Naye Mungu akauita mwanga Mchana, na kiza akaliita Usiku. Na jioni na asubuhi yalikuwa siku ya kwanza” (Mwa 1:3-5). Kifungu hiki kinafafanua kitendo cha kwanza cha Mungu wakati wa kuanza uumbaji, na siku ya kwanza ambayo Mungu aliipitisha ambapo kulikuwa na jioni na asubuhi. Lakini ilikuwa siku ya kipekee: Mungu alianza kutayarisha nuru kwa vitu vyote, na, zaidi ya hayo, Alitenganisha nuru na giza. Katika siku hii, Mungu alianza kunena, na matamshi na mamlaka Yake vyote vilikuwa pamoja. Mamlaka Yake yalianza kujitokeza miongoni mwa vitu vyote, na nguvu Zake zikaenea miongoni mwa vitu vyote kutokana na maneno Yake. Kuanzia siku hii na kuendelea, vitu vyote viliumbwa na vikawa thabiti kwa sababu ya maneno ya Mungu, mamlaka ya Mungu na nguvu za Mungu, na vikaanza kufanya kazi kwa msaada wa maneno ya Mungu, mamlaka ya Mungu na nguvu za Mungu. Wakati Mungu aliposema maneno haya “Na kuwe na mwanga,” kulikuwepo na nuru. Mungu hakuanza kushughulikia shughuli yoyote; nuru ilikuwa imeonekana kama matokeo ya maneno Yake. Hii ilikuwa nuru ambayo Mungu aliita mchana, na ambayo binadamu angali anaitegemea kwa minajili ya kuwepo kwake leo. Kwa amri ya Mungu, kiini na thamani yake havijawahi kubadilika na havijawahi kutoweka. Uwepo wake unaonyesha mamlaka na nguvu za Mungu, na unatangaza uwepo wa Mungu, na unathibitisha, tena na tena, utambulisho na hadhi ya Muumba. Siyo isiyoonekana, au isiyo halisi, lakini ni nuru halisi inayoweza kuonekana na binadamu. Tangu wakati huo na kuendelea, kwenye ulimwengu huu mtupu ambao “nchi ilikuwa yenye ukiwa tena tupu, na giza lilikuwajuu ya uso wa vilindi vya maji,” hapo kuliumbwa kitu cha kwanza kinachoonekana. Kitu hiki kilitokana na maneno ya kinywa cha Mungu na kikaonekana kwenye tukio la kwanza la kuumbwa kwa vitu vyote kwa sababu ya mamlaka na matamshi ya Mungu. Muda mfupi baadaye, Mungu aliamuru nuru na giza kutengana…. Kila kitu kilibadilika na kilikamilishwa kwa sababu ya maneno ya Mungu…. Mungu akaiita nuru hii “Mchana,” na giza hili Akaliita “Usiku.” Kuanzia wakati huo, jioni ya kwanza na asubuhi ya kwanza ziliweza kuumbwa katika ulimwengu ambao Mungu alinuia kuumba, na Mungu akasema hii ndiyo iliyokuwa siku ya kwanza. Siku hii ilikuwa siku ya kwanza ya uumbaji wa Muumba wa vitu vyote, na ilikuwa mwanzo wa uumbaji wa vitu vyote, na ilikuwa ndio mara ya kwanza ambapo mamlaka na uwezo wa Muumba ulikuwa umeonyeshwa katika ulimwengu huu ambao Alikuwa ameuumba.

Kupitia kwa maneno haya, binadamu anaweza kuona mamlaka ya Mungu, na mamlaka ya maneno ya Mungu, na nguvu za Mungu. Kwa sababu ni Mungu pekee ndiye anayemiliki nguvu kama hizo, na kwa hivyo ni Mungu pekee ndiye aliye na mamlaka haya, na kwa sababu Mungu ndiye anayemiliki mamlaka kama hayo, kwa hivyo Mungu pekee ndiye aliye na nguvu kama hizo. Je, kuna mtu yeyote au kitu chochote kinachoweza kumiliki mamlaka na nguvu kama hizi? Je, kunalo jibu katika moyo wako? Mbali na Mungu, je, kuna kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa kinachomiliki mamlaka kama hayo? Je, umewahi kuona mfano wa kitu kama hicho kwenye vitabu vingine vyovyote au machapisho? Je, kuna rekodi yoyote kwamba kuna mtu aliumba mbingu na nchi na vitu vyote? Jambo hili halionekani katika vitabu au rekodi nyingine zozote; haya ndiyo, bila shaka, maneno ya kipekee yenye mamlaka na nguvu kuhusu uumbaji mkuu wa Mungu wa ulimwengu, yaliyorekodiwa kwenye Biblia, na maneno haya yanazungumzia mamlaka ya kipekee ya Mungu, na utambulisho wa kipekee wa Mungu. Je, mamlaka na nguvu kama hizi zinaweza kusemwa kuwa zinaashiria utambulisho wa kipekee wa Mungu? Je, yanaweza kusemwa yanamilikiwa na Mungu, na Mungu pekee? Bila shaka, Mungu Mwenyewe pekee ndiye anayemiliki mamlaka na nguvu kama hizi! Mamlaka na nguvu hizi vyote haviwezi kumilikiwa au kubadilishwa na kiumbe chochote kingine kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa! Je, hii ni mojawapo ya sifa za Mungu Mwenyewe wa kipekee? Je, umewahi kuishuhudia? Maneno haya yanaruhusu watu kuelewa kwa haraka na kwa uwazikweli kwamba Mungu anamiliki mamlaka ya kipekee, na nguvu za kipekee, na Anamiliki utambulisho na hadhi ya juu kabisa. Kutokana na ushirika wa hapa juu, je, unaweza kusema kwamba Mungu unayemwamini ndiye Mungu Mwenyewe wa kipekee?

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 84)

Mungu Hutumia Maneno Kuumba Vitu Vyote

Kwenye Siku ya Pili, Mamlaka ya Mungu Yalipangilia Maji, na Kufanya Anga, na Nafasi za Mahitaji ya Kuishi kwa Kimsingi Zaidi kwa Binadamu Kuonekana

“Na Mungu alisema, Na kuwe na mbingu katikati ya maji, na uigawanye maji kutoka kwa maji. Na Mungu akaitengeneza mbingu, na akayagawanya yale maji yaliyokuwa chini ya mbingu kutoka kwa yale maji yaliyokuwa juu ya mbingu: na kukawa vivyo hivyo” (Mwa 1:6-7). Ni mabadiliko gani yaliyofanyika baada ya Mungu kusema “Na kuwe na mbingu katikati ya maji, na uigawanye maji kutoka kwa maji”? Maandiko yanasema: “Na Mungu akaitengeneza mbingu, na akayagawanya yale maji yaliyokuwa chini ya mbingu kutoka kwa yale maji yaliyokuwa juu ya mbingu.” Ni nini kilichokuwa matokeo baada ya Mungu kutamka hivi na kufanya hivyo? Jibu linapatikana kwenye sehemu ya mwisho ya kifungu hiki: “na kukawa vivyo hivyo.”

Sentensi hizi mbili zilizo fupi zinarekodi tukio adhimu, na zinaelezea tukio la kustaajabisha—kazi kubwa ambayo kwayo Mungu aliyatenga maji, na kuunda nafasi ambayo mwanadamu angeweza kuishi …

Katika picha hii, maji na anga vinaonekana mbele ya macho ya Mungu papo hapo, na vyote vinagawanywa kwa mamlaka ya matamshi ya Mungu, na kugawanywa kwa sehemu ya juu na ya chini kwa njia ambayo iliteuliwa na Mungu. Hivi ni kusema, anga iliyoumbwa na Mungu haikufunika tu maji yaliyo chini, lakini pia ilishikilia maji yaliyo juu…. Katika haya, binadamu hawezi kufanya chochote ila kutazama, kupigwa na butwaa, na kushusha pumzi yake kwa kuvutiwa na maajabu ya onyesho hilo ambalo Muumba aliyahamisha maji, na kuyaamuru maji, na kuumba anga, na yote haya Alifanya kupitia kwa nguvu za mamlaka Yake. Kupitia kwa matamshi ya Mungu, na nguvu za Mungu, na mamlaka ya Mungu, Mungu aliweza kutimiza tendo jingine kubwa. Je, hizi si nguvu za mamlaka ya Muumba? Hebu na tutumie maandiko haya katika kufafanua matendo ya Mungu: Mungu aliyatamka matamshi Yake na kwa sababu ya matamshi haya ya Mungu kulikuwa na anga katikati ya maji. Wakati uo huo, badiliko kubwa sana lilitokea kwenye nafasi hii kwa sababu ya matamshi haya ya Mungu, na halikuwa badiliko katika hali ya kawaida, lakini aina fulani ya mbadala ambao kitu kisichokuwepo kiligeuka na kuwa kitu kilichopo. Yote haya yalizaliwa kwenye fikira za Muumba, na yakawa kitu kilichopo kutoka kwenye kitu kisichokuwepo kwa sababu ya matamshi yaliyotamkwa na Muumba, na, vilevile, kuanzia wakati huo na kuendelea yangekuwepo na kuwa imara, kwa minajili ya Muumba, na yangesonga, kubadilika, na kufanywa upya kulingana na fikira za Muumba. Kifungu hiki kinaelezea tendo la pili la Muumba katika uumbaji Wake wa ulimwengu wote. Ilikuwa ni onyesho jingine la mamlaka na nguvu za Muumba, na pia ni uumbaji mwingine wa Muumba. Siku hii ndio iliyokuwa siku ya pili ambayo Muumba alikuwa ameipitia tangu kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu, na ilikuwa ni siku nyingine ya ajabu Kwake: Alitembea katika nuru, Alileta anga, Aliyapangilia na kuyadhibitimaji, na vitendo Vyake, mamlaka Yake, na nguvu Zake vyote viliweza kuanza kazi kwenye siku hiyo mpya …

Je, kulikuwepo na anga katikati ya maji kabla ya Mungu kutamka matamshi Yake? Bila shaka la! Na je, baada ya Mungu kusema “Na liwe anga katikati ya maji”? Vitu vilivyokusudiwa na Mungu vilionekana; palikuwa na anga katikati ya maji, na maji yakatengana kwa sababu Mungu alisema, “na likayatenge maji na maji.” Kwa njia hii, kufuatia maneno ya Mungu, vitu viwili vipya, vitu vipya viwili vilivyozaliwa vilionekana miongoni mwa vitu vyote kama matokeo ya mamlaka na nguvu za Mungu. Je, unajisikiaje kuhusu kuonekana kwa vitu hivi viwili vipya? Je, unahisi ukuu wa uwezo wa Muumba? Je, unahisiile nguvu ya kipekee na isiyo ya kawaida ya Muumba? Ukubwa wa msukumo na nguvu kama hizo zinatokana na mamlaka ya Mungu na mamlaka haya ni kiwakilishi cha Mungu Mwenyewe, na sifa ya kipekee ya Mungu Mwenyewe.

Je, kifungu hiki kimekupa hisia nyingine ya kina zaidi kuhusu upekee wa Mungu? Lakini haya ni machache tu kati ya mengi; mamlaka na nguvu za Muumba vinazidi haya yote. Upekee wake hauko hivyo tu kwa sababu Anamiliki asili tofauti na ile ya kiumbe chochote, bali pia ni kwa sababu mamlaka na nguvu Zake ni zisizo za kawaida, zisizo na mipaka, ni kuu juu ya yote, na zinasimama juu ya vitu vyote, na vilevile, kwa sababu mamlaka Yake na kile Anacho na alicho kinaweza kuumba maisha, na kufanya miujiza, na Anaweza kuumba yaliyo ya kustaajabisha na yasiyo ya kawaida kwa kila dakika na sekunde, na wakati uo huo, Anaweza kutawala maisha Anayoyaumba na kushikilia ukuu Wake juu ya miujiza na kila mojawapo ya dakika na sekunde Anazoumba.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 85)

Mungu Hutumia Maneno Kuumba Vitu Vyote

Kwenye Siku ya Tatu, Matamshi ya Mungu Yazaa Ardhi na Bahari, na Mamlaka ya Mungu Yasababisha Ulimwengu Kujaa Maisha

Hebu na tusome sentensi ya kwanza ya Mwanzo 1:9-11: “Naye Mungu akasema, Nayo maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike pahali pamoja, ili ardhi kavu ionekane.” Ni mabadiliko gani yaliyotokea baada ya Mungu kusema tu, “Nayo maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili ardhi kavu ionekane”? Ni nini kingine kilichotokea katika nafasi hii mbali na nuru na anga? Katika Maandiko, imeandikwa: “Naye Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji Akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.” Hivi ni kusema, kulikuwepo sasa na nchi kavu na bahari katika nafasi hii, nayo nchi na bahari viliweza kutenganishwa. Kujitokeza kwa vitu hivi vipya kulifuata amri kutoka kwenye kinywa cha Mungu, “na ikawa hivyo.” Je, Maandiko yanafafanua Mungu akiwa ameshughulika kila pahali wakati Akifanya haya? Je, yanafafanua Mungu akiwa anajihusisha katika kazi ngumu? Kwa hivyo, haya yote yaliwezaje kufanywa na Mungu? Mungu aliwezaje kusababisha vitu hivi vipya kuumbwa? Tunaelewa wenyewe bila kuelezewa, kwamba Mungu alikamilisha haya yote, na Aliumba haya yote kwa maneno Yake.

…………

Hebu na tuendelee hadi kwenye sentensi ya mwisho ya fungu hili: “Naye Mungu akasema, Na dunia izae majani, mche ambao unatoa mbegu, na mti wa matunda ambao unazaa tunda kwa aina yake, ambao mbegu zake ziko ndani yake, juu ya dunia: na kukawa vivyo hivyo.” Wakati Mungu alipokuwa anazungumza, kila kitu kilifanyika kulingana na mawazo ya Mungu, na papo hapo, aina mbalimbali za viumbe vidogo vidogo vilaini vyenye uhai vilikuwa vinachomoza vichwa vyao kwa kuyumba-yumba juu ya udongo, na hata kabla havijakung’uta chembechembe za uchafu kutoka kwenye miili yao vilikuwa vikipungiana kwa shauku katika kusalimiana, vitikisa vichwa vyao na kuufurahia ulimwengu. Vilimshukuru Muumba kwa uhai Aliowapa, na kuutangazia ulimwengu kwamba vilikuwa ni sehemu ya vitu vyote, na kwamba kila kimoja kingejitolea uhai wake ili kuonyesha mamlaka ya Muumba. Wakati maneno ya Mungu yaliponenwa, nchi ilisitawi na kuwa ya kijani kibichi, aina zote za miti ambayo ingeweza kufurahiwa na binadamu iliweza kuota na kuchipuka kutoka kwenye ardhi, na milima na nchi tambarare vyote vikawa na idadi kubwa ya miti na misitu…. Ulimwengu huu uliokuwa jangwa, ambao haukuwa na dalili yoyote ya uhai, ulifunikwa kwa kasi na wingi wa nyasi, mimea na miti na kuenea kwa kijani kibichi…. Harufu ya nyasi na harufu ya udongo ilienea kwa njia ya hewa, na safu za mimea zilianza kupumua kulingana na mzunguko wa hewa, na vikaanza pia mchakato wa kukua. Wakati uo huo, kutokana na maneno ya Mungu na kufuatia fikira za Mungu, mimea yote ilianza mizunguko isiyoisha ya maisha ambapo inakua, inachanua, inazaa matunda na kuzaana na kuongezeka. Ilianza kutii kwa umakinifu mikondo yao husika ya maisha na kuanza kutekeleza wajibu wao husika miongoni mwa viumbe vyote…. Yote ilichipuka na kuishi, kwa sababu ya matamshi ya Muumba. Zingepokea utoaji na utunzaji usikoma wa Muumba, na daima zingedumu kwa ushupavu katika kila pembe ya nchi ili kuonyesha mamlaka na nguvu za Muumba, na daima zingeonyesha nguvu za uhai walizopewa na Muumba …

Maisha ya Muumba ni ya ajabu, fikira Zake ni za ajabu, na mamlaka Yake ni ya ajabu, na kwa hivyo, wakati matamshi Yake yalipotamkwa, yale matokeo ya mwisho yalikuwa “na ikawa hivyo.” Ni wazi kwamba, Mungu hahitaji kufanya kazi kwa mikono Yake wakati Anapotenda; Anatumia tu fikira Zake kuamuru na maneno Yake kupangilia, na kwa njia hii mambo yanatimizwa. Kwenye siku hii, Mungu aliyakusanya maji katika mahali pamoja, na Akaiacha ardhi kavu kujitokeza, baada ya hapo Mungu aliifanya nyasi kuota kutoka kwenye ardhi, na papo hapo palimea mimea iliyozaa mbegu, na miti ya kuzaa matunda, na Mungu akaainisha kila mojawapo kulingana na aina, na kusababisha kila mmea kuwa na mbegu yake. Haya yote yalitimizwa kulingana na fikira za Mungu na amri za matamshi ya Mungu, na kila mmea ulijitokeza, mmoja baada ya mwingine, kwenye ulimwengu huu mpya.

Wakati Akiwa bado hajaanza kazi Yake, Mungu tayari alikuwa na picha ya kile Alichonuia kutimiza katika akili Zake, na wakati ambapo Mungu alianza kutimiza mambo haya, ndio wakati ambao pia Mungu alikifungua kinywa Chake kuongea kuhusu maudhui ya picha hii, mabadiliko katika vitu vyote yalianza kutokea shukrani kwa mamlaka na nguvu za Mungu. Bila ya kujali jinsi Mungu alivyofanya, au jinsi Alivyoonyesha mamlaka Yake, kila kitu kilitimizwa hatua kwa hatua kulingana na mpango wa Mungu na kwa sababu ya matamshi ya Mungu, na mabadiliko ya hatua kwa hatua yalifanyika kati ya mbingu na dunia kutokana na matamshi na mamlaka ya Mungu. Mabadiliko na matukio haya yote yalionyesha mamlaka ya Muumba, na pia yalionyesha ajabu na ukuu wa nguvu za maisha ya Muumba. Fikira Zake si mawazo mepesi, au picha tupu, bali ni mamlaka kuu na yenye nguvu isiyo ya kawaida, na ndio nguvu zinazosababisha vitu vyote kubadilishwa, kuhuishwa, kufanywa upya na kupotea. Kwa sababu ya haya, vitu vyote hufanya kazi kwa sababu ya fikira Zake, na, wakati uo huo, yote haya yanatimizwa kwa sababu ya matamshi kutoka kinywani Mwake …

Kabla ya vitu vyote kuonekana, katika mawazo ya Mungu mpango wa Mungu ulikuwa umeundwa kitambo, na ulimwengu mpya ulikuwa umetimizwa kitambo. Ingawa kwenye siku ya tatu kila aina ya mimea ilijitokeza ardhini, Mungu hakuwa na sababu yoyote ya kusitisha hatua za uumbaji Wake kwa ulimwengu huu, Alinuia kuendelea kunena matamshi Yake, kuendelea kutimiza uumbaji wa kila kitu kipya. Angenena, angetoa amri Zake, na Angetumia mamlaka Yake na kuonyesha nguvu Zake, na Alitayarisha kila kitu Alichokuwa amepanga kutayarisha kwa ajili ya vitu vyote na wanadamu Ambao Alikusudia kuwaumba. …

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 86)

Mungu Hutumia Maneno Kuumba Vitu Vyote

Kwenye Siku ya Nne, Misimu, Siku, na Miaka ya MwanadamuVilikuja Kuwepo Mungu Alipotumia Mamlaka Yake kwa Mara Nyingine Tena

Muumba alitumia matamshi Yake kutimiza mpango Wake, na kwa njia hii Alipitisha siku tatu za kwanza kwenye mpango Wake. Kwenye siku hizi tatu, Mungu hakuonekana kushughulika kila pahali, au kujichosha Yeye Mwenyewe; kinyume cha mambo ni kwamba, Alikuwa na siku tatu za kwanza nzuri katika mpango Wake na Alitimiza utekelezaji mkubwa wa mabadiliko makubwa ya ulimwengu. Ulimwengu mpya kabisa ulionekana mbele za macho Yake, na, sehemu kwa sehemu, picha nzuri na ya kupendeza ambayo ilikuwa imefichwa ndani ya fikira Zake ilikuwa tayari imefichuliwa kwa matamshi ya Mungu. Kuonekana kwa kila kitu kipya kulikuwa sawa na kuzaliwa kwa mtoto mchanga, na Muumba alifurahia sana picha hii ambayo iliwahi kuwa kwenye fikira Zake, lakini ambayo sasa ilikuwa imepewa uhai. Kwa wakati huu, moyo Wake uliweza kuridhika kidogo, lakini mpango Wake ulikuwa ndio umeanza tu. Kufumba na kufumbua, siku mpya ilikuwa imewadia—na je, ni ukurasa gani uliofuata katika mpango wa Muumba? Ni nini Alichosema? Na Aliwezaje kuonyesha mamlaka Yake? Na, wakati uo huo, ni mambo yapi mapya yaliyokuja kwenye ulimwengu huu mpya? Kufuatia mwongozo wa Muumba, matazamio yetu yanaangukia katika siku ya nne ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, siku ambayo ilikuwa ni mwanzo mwingine mpya. Bila shaka, kwa Muumba, ilikuwa ni siku nyingine ya ajabu kwa hakika, na siku nyingine yenye umuhimu mkubwa kwa wanadamu wa leo. Ilikuwa, bila shaka, siku yenye thamani isiyopimika. Je, ni kwa jinsi gani ilikuwa ya ajabu, ni kwa jinsi gani ilikuwa ya muhimu sana, na ni kwa jinsi gani ilikuwa yenye thamani isiyopimika? Hebu kwanza tusikilize maneno yaliyosemwa na Muumba….

“Naye Mungu akasema, Kuwe na mwangaza katika anga la mbingu kwa minajili ya kutenga mchana na usiku; na uwe ndio ishara; na majira, na siku na miaka: Na tena uwe ndio mwangaza katika anga la mbingu kwa minajili ya kupa nchi nuru; na ikawa vile” (Mwa 1:14-15). Haya yalikuwa maonyesho mengine ya mamlaka ya Mungu yaliyoonyeshwa kwa viumbe kufuatia uumbaji Wake wa nchi kavu na mimea iliyokuwa juu yake. Kwa Mungu, kitendo kama hicho kilikuwa tu rahisi kama kile Alichokuwa tayari Amefanya, kwa sababu Mungu ana nguvu kama hizo; Mungu ni mmwema kama vile tu neno Lake lilivyo, na neno Lake litatimizwa. Mungu aliamuru mwanga uonekane mbinguni, na mwanga huu haukuangaza tu angani na juu ya nchi, bali pia zilihudumu kama ishara za mchana na usiku, kwa minajili ya misimu, siku, na miaka. Kwa njia hii, kama vile Mungu alivyoongea kwa matamshi Yake, kila kitendo ambacho Mungu alipenda kutimiza kilitimizwa kulingana na mapenzi ya Mungu na kwa njia iliyoteuliwa na Mungu.

Mwanga kwenye mbingu ni kitu kilicho kwenye mbingu kinachoweza kuangaza nuru; vinaweza kuangazia mbingu, na vinaweza kuangazia ardhi na bahari. Vinazunguka kulingana na mifuatano maalum na kulingana na idadi maalum ya mizunguko ambayo imeamriwa na Mungu, na vinaangaza katika vipindi tofauti vya wakati juu ya ardhi, na kwa njia hii mizunguko ya mianga hii husababisha mchana na usiku kujitokeza upande wa mashariki na magharibi mwa nchi, na wala si tu ishara za usiku na mchana, lakini kupitia kwa mizunguko hii tofauti inaweza kuadhimisha pia siku kuu na siku mbalimbali maalum za mwanadamu. Ndizo ambazo zinakamilisha kikamilifu na kuambatana na misimu minne—masika, kiangazi, vuli, na kipupwe—iliyotolewa na Mungu, pamoja na vile ambavyo mianga hii hutumika kama viashiria vya mara kwa mara na sahihi kwa ajili ya majira, siku, na miaka ya mwanadamu. Ingawa ilikuwa baada tu ya mwanzo wa kilimo ndipo mwanadamu alipoanza kuelewa na kukumbana na utofautishaji wa vipimo vya muda, siku, na miaka iliyosababishwa na nuru hizi zilizoumbwa na Mungu, kwa hakika, vipindi vya muda, siku, na miaka ambavyo binadamu anaelewa leo vilianza kutolewa kitambo kwenye siku ya nne ya uumbaji wa viumbe vyote na Mungu, na vilevile ndivyo ilivyokuwa kwenye mizunguko inayobadilishana ya mchipuko, kiangazi, mapukutiko, na kipupwe ambavyo binadamu anapitia na vinaanza kitambo kwenye siku ya nne ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote. Nuru zile zilizoumbwa na Mungu zilimwezesha binadamu kuweza kutofautisha mara kwa mara, kwa hakika, na waziwazi usiku na mchana, na kuhesabu siku, na kuweza kufuatilia waziwazi vipindi vile vya muda na miaka. (Siku ya mwezi mzima ilikuwa kukamilika kwa mwezi mmoja, na kutokana na haya binadamu alijua kwamba kule kuangazia kwa nuru kulianzisha mzunguko mpya; siku ile ya nusu mwezi ilikuwa ni kukamilika kwa nusu moja ya mwezi, jambo ambalo lilimfahamisha binadamu kwamba kipindi kipya cha muda kilikuwa kimeanza, ambapo binadamu angeweza kujua ni mchana na usiku ngapi vilikuwa kwenye kipindi cha muda, na ni vipindi vingapi vya muda vilikuwa kwenye msimu, na ni misimu mingapi ilikuwa kwenye mwaka, na vyote hivi vilionyeshwa mara kwa mara.) Kwa hivyo, binadamu angeweza kufuatilia kwa urahisi vipindi vya muda, siku, na miaka iliyowekewa alama na mizunguko ya nuru hizo. Kuanzia sasa kusonga mbele, mwanadamu na viumbe vyote viliishi bila kufahamu miongoni mwa mabadiliko yenye mpangilio ya usiku na mchana na kubadilishwa kwa misimu iliyotokana na mizunguko ya nuru. Huu ndio ulikuwa muhimu wa uumbaji wa Muumba wa nuru kwenye siku ya nne. Vilevile, nia na umuhimu wa hatua hii ya Muumba vilikuwa bado haviwezi kutenganishwa na mamlaka na nguvu Zake. Na kwa hivyo, nuru zilizoumbwa na Mungu na thamani ambayo zingeleta hivi karibuni kwa binadamu ilikuwa ni mafanikio mengine katika uonyeshaji wa mamlaka ya Muumba.

Katika ulimwengu huu mpya, ambao mwanadamu bado alikuwa hajaonekana, Muumba alikuwa ametayarisha jioni na asubuhi, ile anga, ardhi na bahari, nyasi, mimea na aina mbalimbali za miti, na nuru, misimu, siku, na miaka kwa minajili ya maisha mapya ambayo Angeumba hivi karibuni. Mamlaka na nguvu za Muumba vyote vilionyeshwa katika kila kitu kipya Alichokiumba, na maneno Yake na mafanikio Yake vyote vilifanyika sawia, bila ya hitilafu hata kidogo, na bila ya kuchelewa hata kidogo. Kuonekana na kuzaliwa kwa vitu hivi vyote vipya kulikuwa uthibitisho wa mamlaka na nguvu za Muumba: Anamaanisha kile Anachosema, na kile Anachosema kitatimizwa, na kile ambacho kinatimizwa kitadumu milele. Ukweli huu haujawahi kubadilika: ndivyo ilivyokuwa zamani, ndivyo ilivyo leo, na ndivyo itakavyokuwa milele yote. Unapoyaangalia kwa mara nyingine maneno hayo ya maandiko, unahisi kwamba yangali mapya kwako? Je, umeyaona maudhui mapya, na kufanya ugunduzi mpya? Hii ni kwa sababu matendo ya Muumba yamechochea mioyo yenu na kuongoza mwelekeo wa maarifa yako ya mamlaka na nguvu Zake, na yakakufungulia mlango wa ufahamu wa Muumba, na vitendo na mamlaka Yake vimeweza kupatia maneno haya uhai. Na kwa hivyo katika maneno haya binadamu ameona maonyesho halisi, na wazi ya mamlaka ya Muumba, na kuweza kushuhudia kwa kweli mamlaka makuu ya Muumba, na kutazama mamlaka yake yasiyokuwa ya kawaida na nguvu za Muumba.

Mamlaka na nguvu za Muumba hutoa muujiza baada ya muujiza, na Anavutia umakinifu wa binadamu, naye binadamu hawezi kujizuia ila kutazama kwa butwaa matendo haya ya kustaajabisha yanayotokana na matumizi ya mamlaka Yake. Nguvu zake za ajabu huleta furaha baada ya furaha, na mwanadamu anaachwa akishangaa na kufurahi sana, naye anatweta kwa kuvutiwa, anastaajabishwa, na kushangilia; zaidi ya hayo, mwanadamu anaonekana kuguswa, na kunazalishwa ndani yake heshima, hofu, na mshikamano. Mamlaka na matendo ya Muumba yana athari kubwa katika roho ya mwanadamu, na yanatakasa roho ya mwanadamu, na, zaidi ya hayo, yanatosheleza roho ya mwanadamu. Kila moja ya mawazo Yake, kila moja ya matamshi Yake, na kila ufunuo wa mamlaka Yake ni kazi bora kati ya vitu vyote, na ni utekelezaji mkuu unaostahili zaidi ufahamu na maarifa ya kina ya mwanadamu aliyeumbwa.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 87)

Mungu Hutumia Maneno Kuumba Vitu Vyote

Kwenye Siku ya Tano, Maisha ya Maumbo Mbali na Tofauti Yalionyesha Mamlaka ya Muumba kwa Njia Tofauti

Maandiko yanasema, “Na Mungu akasema, Na maji yalete kwa wingi kiumbe asongaye aliye na uhai, na ndege wanaoweza kuruka juu ya nchi katika anga wazi la mbingu. Naye Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na viumbe wote walio na uhai wasongao, ambao maji yalileta kwa wingi, kwa aina yao, na kila ndege anayeruka kwa aina yake: na Mungu akaona kuwa ilikuwa vizuri” (Mwa 1:20-21). Maandiko yanatwambia waziwazi kwamba, kwenye siku hii, Mungu aliumba viumbe vya majini na ndege wa angani, hivi ni kusema kwamba Aliwaumba samaki na ndege mbalimbali, na akawaainisha kila mmoja wao kulingana na aina. Kwa njia hii, ardhi, mbingu, na maji vyote vilitajirishwa na uumbaji wa Mungu …

Maneno ya Mungu yalipokuwa yakitamkwa, viumbe hai vyenye maumbo mbalimbali, papo hapo, vilipata uhai katika matamshi ya Muumba. Viliingia ulimwenguni vikigombania kupata nafasi, vikirukaruka, na kucheza kwa furaha…. Samaki wenye maumbo na ukubwa tofauti wote waliweza kuogelea majini; samakigamba wa kila aina waliweza kuzaliana kwenye mchanga, viumbe vyenye magamba, vyenye maganda na vile visivyokuwa na uti wa mgongo viliweza kukua kwa haraka kwa maumbo tofauti, haijalishi kama vilikuwa vikubwa au vidogo, virefu au vifupi. Na ndivyo pia ilivyokuwa kwa aina tofauti za magugu ya baharini yalianza kukua kwa haraka, zikiyumbayumba kwenye mwendo wa viumbe mbalimbali vya majini, zikijipindua, zikiyasukuma maji yaliyotuama, kana kwamba yanataka kuyaambia: Tikisa mguu! Walete marafiki zako! Kwa maana hautawahi kuwa peke yako tena! Kuanzia wakati huo ambao viumbe hai mbalimbali vilivyoumbwa na Mungu vilionekana ndani ya maji, kila uhai mpya ulileta uhai kwa maji ambayo yalikuwa yametulia kwa muda mrefu sana, na kuanzisha enzi mpya…. Kuanzia wakati huo na kuendelea, viumbe hivi viliishi pamoja, kimoja kando ya kingine na vikaweza kukaa kwa pamoja, na havikuweka umbali kati yao. Maji yalikuwepo kwa ajili ya viumbe vilivyokuwa ndani yake, yakistawisha kila uhai uliokaa ndani ya kumbatio lake, na kila uhai ulikuwepo kwa ajili ya maji kwa sababu ya utunzaji wake. Kila kimoja kilimpa mwenzake uhai, na wakati huo huo, kila kimoja, kwa njia hiyo, kilitoa ushuhuda wa maajabu na ukuu wa uumbaji wa Muumba, na kwa nguvu zisizo na kifani za mamlaka ya Muumba …

Kwa vile bahari haikuwa tulivu tena, ndivyo pia uhai ulivyoanza kuijaza anga. Kimoja baada ya kingine, ndege, wakubwa kwa wadogo, walipaa juu angani kutoka ardhini. Tofauti na viumbe vya baharini, walikuwa na mbawa na manyoya ambayo yalifunika maumbo yao membamba na yenye kupendeza. Walipigapiga mbawa zao, kwa maringo na majivuno wakionyesha koti lao la kupendeza la manyoya na kazi zao maalum pamoja na ustadi waliopewa na Muumba. Walipaa kwa uhuru, na kwa ustadi walisafiri huku na kule kati ya mbingu na dunia, katika ukanda wa nyasi na misitu…. Walikuwa ni vipenzi vya anga, na vipenzi vya vitu vyote. Hivi karibuni wangekuwa ndio kiunganishi kati ya mbingu na dunia, na wangepitisha ujumbe kwa vitu vyote…. Waliimba, waliruka huku na kule kwa furaha, walileta shangwe, vicheko, na uchangamfu kwenye ulimwengu huu uliojaa utupu hapo mwanzoni…. Walitumia sauti zao zinazosikika vizuri, zenye kuvutia, na walitumia maneno yaliyokuwa ndani ya mioyo yao kumsifu Muumba kwa ajili ya uhai waliopewa. Walicheza kwa furaha ili kuonyesha ukamilifu na maajabu ya uumbaji wa Muumba, na wangejitolea maisha yao yote kushuhudia mamlaka ya Muumba kupitia maisha maalum ambayo Alikuwa amewapa …

Haijalishi kama vilikuwa majini, ama angani, kwa amri ya Muumba, wingi huu wa viumbe hai ulikuwepo katika mipangilio tofauti ya maisha, na kwa amri ya Muumba, vilikusanyika pamoja kulingana na aina zao mbalimbali—na sheria hii, kanuni hii, ilikuwa isiyoweza kubadilishwa na viumbe vyovyote. Kamwe hawakuthubutu kuvuka mipaka waliyowekewa na Muumba, na wala visingeweza kufanya hivyo. Kama walivyoamriwa na Muumba, waliishi na kuzaliana, na kutii kikamilifu mkondo wa maisha na sheria walizowekewa na Muumba, na kwa uangalifu wakafuata amri Zake zisizotamkwa na amri na maagizo ya mbinguni Aliyowapa, kutoka hapo hadi leo. Walizungumza na Muumba kwa njia yao maalum, na wakaja kufahamu maana ya Muumba, na wakatii amri Zake. Hakuna kati yao aliyewahi kukiuka mamlaka ya Muumba, na ukuu na amri Yake juu yao ilitekelezwa ndani ya fikira Zake; hakuna maneno yaliyotolewa, lakini mamlaka yaliyokuwa ya kipekee kwa Muumba yalidhibiti vitu vyote kwa ukimya ambavyo havikuwa na matumizi yoyote ya lugha, na ambavyo vilitofautiana na wanadamu. Maonyesho ya mamlaka Yake kwa njia hii maalum yalimlazimisha mwanadamu kupata maarifa mapya, na kufanya tafsiri mpya, ya mamlaka ya kipekee ya Muumba. Hapa, lazima niwaambie kwamba katika siku hii mpya, utekelezaji wa mamlaka ya Muumba yalionyesha kwa mara nyingine ule upekee wa Muumba.

Kinachofuata, wacha tuangalie sentensi ya mwisho ya kifungu hiki cha maandiko: “Mungu akaona ya kuwa ni vyema.” Unafikiri hii inamaanisha nini? Hapa, tunapata kuziona hisia za Mungu. Mungu alitazama vitu vyote Alivyokuwa ameviumba vikitokea na kusimama imara kwa sababu ya matamshi Yake, na polepole vilianza kubadilika. Je, kwa wakati huu, Mungu alikuwa Ameridhika na vitu mbalimbali Ambavyo alikuwa Amevifanya kwa matamshi Yake, na vitendo mbalimbali Alivyokuwa ametimiza? Jibu ni kwamba “Mungu akaona kwamba ni vizuri.” Je unaona nini hapa? Kunawakilisha nini kwamba “Mungu akaona kwamba ni vizuri”? Kusema hivi kunaashiria nini? Kunamaanisha kwamba Mungu alikuwa na nguvu na hekima ya kukamilisha kile Alichokuwa amepanga na kuamua, ili kutimiza malengo ambayo Alikuwa amekusudia kuyatimiza. Baada ya Mungu kukamilisha kila kazi, je, Alijutia chochote? Jibu lingali kwamba “Mungu akaona kwamba ni vizuri.” Kwa maneno mengine, sio tu kwamba Hakujutia chochote, bali pia Aliridhika. Inamaanisha nini kwamba Hakujutia chochote? Inamaanisha kwamba mpango wa Mungu ni sahihi, kwamba nguvu na hekima Zake ni kamili, na kwamba ni kwa mamlaka Yake tu ndipo ukamilifu huo unaweza kutimizwa. Wakati binadamu anapotekeleza kazi, je, anaweza, kama Mungu, kuona kwamba kazi hiyo ni nzuri? Je, kila kitu anachofanya binadamu kinaweza kufikia ukamilifu? Je, binadamu anaweza kukamilisha kitu mara moja na kikawa hivyo daima dawamu? Kama vile tu binadamu anavyosema, “hakuna kitu kilicho kamili, kinaweza tu kuwa bora zaidi,” hakuna kitu ambacho binadamu hufanya kinaweza kufikia ukamilifu. Wakati Mungu alipoona kwamba kile Alichokuwa amefanya na kutimiza kilikuwa chema, kila kitu kilichoumbwa na Mungu kiliwekwa kwa matamshi Yake, hivi ni kusema kwamba, wakati “Mungu alipoona ya kuwa ni vyema,” kila kitu Alichokiumba kilichukua umbo la kudumu, kikaainishwa kulingana na aina, na kikapewa nafasi maalum, kusudio, na kazi, kwa mara ya kwanza na milele yote. Zaidi ya hayo, jukumu lao miongoni mwa vitu vyote, na safari ambayo ni lazima waichukue wakati wa usimamizi wa Mungu wa vitu vyote, ilikuwa tayari imeamriwa na Mungu, na isingebadilishwa. Hii ilikuwa ni sheria ya mbinguni iliyotolewa na Muumba kwa vitu vyote.

“Mungu akaona kwamba ni vizuri,” maneno haya mepesi, yasiyothaminiwa, yanayopuuzwa mara nyingi, ni maneno ya sheria ya mbinguni na amri ya mbinguni iliyotolewa na Mungu kwa viumbe vyote. Ni udhihirisho mwingine wa mamlaka ya Muumba, ambao ni wa kivitendo zaidi, na wa kina zaidi. Kupitia kwa matamshi Yake, Muumba hakuweza tu kupata yale yote Aliyokusudia kuyapata, na kutimiza yale yote Aliyokusudia kuyatimiza, lakini pia Aliweza kudhibiti mikononi Mwake, kila kitu Alichokuwa amekiumba, na kutawala kila kitu Alichokuwa amekiumba chini ya mamlaka Yake, na, vilevile, kila kitu kilikuwa na utaratibu na cha kawaida. Viumbe vyote pia viliongezeka, vikawepo, na kupotea kwa matamshi Yake na, vilevile, kwa mamlaka Yake, vilikuwepo katikati ya sheria Aliyokuwa ameiweka wazi, na hakuna kinachoweza kukiuka! Sheria hii ilianza punde tu “Mungu alipoona ya kuwa ni vyema,” na itakuwepo, itaendelea, na kufanya kazi kwa minajili ya mpango wa Mungu wa usimamizi mpaka siku ile itakapobatilishwa na Muumba! Mamlaka ya kipekee ya Muumba hayakuonyeshwa tu katika uwezo Wake wa kuumba vitu vyote na kuamuru vitu vyote vije kuwepo, lakini pia katika uwezo Wake wa kutawala na kushikilia ukuu juu ya vitu vyote, na kuweka uhai na nguvu juu ya vitu vyote, na, zaidi ya hayo, katika uwezo Wake wa kusababisha, kwa mara ya kwanza na kwa milele yote, vitu vyote ambavyo Angeviumba katika mpango Wake vionekane na kuwepo katika ulimwengu vilivyofanywa na Yeye katika umbo kamili, na muundo kamili wa uhai, na jukumu kamili. Na ndivyo pia ilivyoonyeshwa kwa njia ambayo mawazo ya Muumba hayakuwa chini ya vizuizi vyovyote, hayakuwekewa mipaka ya muda, nafasi, au jiografia. Kama mamlaka Yake, utambulisho wa kipekee wa Muumba utabakia bila kubadilika milele hata milele. Mamlaka yake siku zote yatakuwa uwakilishi na ishara ya utambulisho Wake wa kipekee, na mamlaka Yake yatakuwepo milele sambamba na utambulisho Wake!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 88)

Mungu Hutumia Maneno Kuumba Vitu Vyote

Kwenye Siku ya Sita, Muumba Anazungumza, na Kila Aina ya Kiumbe Hai Mawazoni Mwake Chajitokeza, Kimoja Baada ya Kingine

Bila kujua, kazi ya Muumba ya kuumba vitu vyote ilikuwa imeendelea kwa siku tano, na punde tu baada ya hapo ndipo Muumba alipokaribisha siku ya sita ya uumbaji Wake wa vitu vyote. Siku hii ilikuwa ni mwanzo mwingine mpya, na siku nyingine ya ajabu. Je, basi, mpango wa Muumba ulikuwa ni upi usiku wa kuamkia siku hii mpya? Ni viumbe gani vipya ambavyo Angevizalisha, ambavyo Angeviumba? Sikiliza, hii ndiyo sauti ya Muumba …

“Naye Mungu akasema, Dunia na ilete kiumbe kilicho hai kwa namna yake, mifugo, na kitu kinachotambaa, na wanyama wa mwituni kwa namna yake: na ikafanyika. Naye Mungu akaumba wanyawa wa mwituni kwa namna yake, na mifugo kwa namna yake, na chote kinachotambaa duniani kwa namna yake: na Mungu akaona kwamba ni vizuri” (Mwa 1:24-25). Ni viumbe gani hai ndivyovinavyojumuishwa hapa? Maandiko yanasema: mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake. Hivi ni kusema kwamba, katika siku hii hakukuweko tu na aina zote za viumbe hai juu ya nchi, lakini pia vyote vilikuwa vimeainishwa kulingana na aina, na, vilevile, “Mungu akaona ya kuwa ni vyema.”

Kama tu kwenye siku zile tano za awali, kwa sauti ile ile, siku ya sita Muumba aliamuru kuzaliwa kwa viumbe hai Alivyotamani, na kwamba vilionekana juu ya nchi, kila kimoja kulingana na aina yake. Wakati Muumba anatumia mamlaka Yake, hakuna matamshi Yake yanayotamkwa bure, na kwa hivyo, kwenye siku ya sita, kila kiumbe hai ambacho Alikuwa amenuia kuumba kilionekana wakati ule Aliochagua. Kama vile Muumba alivyosema “Nchi na ilete kiumbe kilicho hai kwa jinsi yake,” nchi ilijawa mara moja na uhai, na juu ya ardhi kukaibuka pumzi za aina zote za viumbe hai…. Katika nyika za kijani kibichi, ng’ombe wanene, wakichezesha mikia yao huku na kule, walijitokeza mmoja baada ya mwingine, kondoo waliokuwa wakitoa milio walikusanyika kwa makundi, na farasi waliotoa milio wakaanza kukimbia…. Mara moja, eneo kubwa lenye nyasi tulivu lilijawa na uhai…. Kujitokeza kwa mifugo hii mbalimbali ilikuwa ni mandhari ya kupendeza kwenye mbuga tulivu, na kuleta uhai usio na kikomo…. Wangekuwa ni marafiki wa nyika, na wenyeji wakuu wa nyika, kila kimoja kikitegemea kingine; na vilevile ndivyo pia wangekuwa walezi na walinzi wa ardhi hizi, ambazo zingekuwa makao yao ya kudumu, na ambazo zingewapa kila kitu walichohitaji, chanzo cha lishe ya milele kwa minajili ya kuwepo kwao …

Kwenye siku iyo hiyo ambayo mifugo hii mbalimbali ilijitokeza, kwa tamko la Muumba, wadudu wengi pia walijitokeza, mmoja baada ya mwingine. Hata Ingawa ndio waliokuwa viumbe hai wadogo zaidi miongoni mwa viumbe vyote, nguvu zao za uhai zilikuwa bado uumbaji wa kimiujiza wa Muumba, na hawakuwasili wakiwa wamechelewa sana…. Baadhi yao walipigapiga mabawa yao madogo, huku wengine wakitambaa polepole; baadhi waliruka na kunesa, wengine waliyumba-yumba; wengine walienda mbele kwa haraka, huku wengine wakirudi nyuma kwa haraka; wengine walienda upandeupande, wengine waliruka juu na chini…. Wote walijishughulisha katika kujaribu kujitafutia makazi: Baadhi walijipenyeza kwenye nyasi, baadhi walianza kuchimba mashimo ardhini, baadhi wakapaa hadi kwenye miti, iliyojificha msituni …. Ingawa walikuwa wadogo kwa ukubwa, hawakuwa radhi kuvumilia mateso ya njaa, na baada ya kupata makao yao binafsi, walikimbia kutafuta chakula ili kuweza kujilisha. Baadhi yao walipanda juu ya nyasi ili wale ncha zake laini, baadhi yao walikamata uchafu kwenye vinywa vyao na kuanza kulisha matumbo yao, wakila kwa bidii na kwa furaha (kwao, hata uchafu ulikuwa mlo wenye ladha); wengine walikuwa wamejificha misituni, lakini hawakusubiri wapumzike, kwani majimaji ndani ya majani yale ya kijani kibichi yenye kung’aa yalitoa chakula kitamu …. Baada ya wao kushiba, bado wadudu hawakuacha kufanya shughuli zao; ingawa walikuwa wadogo kwa kimo, walikuwa na nguvu nyingi sana na uchangamfu usio na kikomo, na kwa hivyo kati ya viumbe vyote, wao ndio walikuwa hodari zaidi na wenye bidii zaidi. Hawakuwahi kuwa wazembe, na hawakuhusika katika mapumziko yoyote. Baada ya kushiba, bado walifanya bidii katika kazi zao kwa ajili ya siku zao za baadaye, wakijishughulisha wenyewe na kukimbia hapa na pale kwaajili ya kesho zao, kwa ajili ya kuendelea kuishi…. Kwa utaratibu waliweza kuimba nyimbo zenye midundo tofauti ili kuhimizana na kusihi kila mmoja wao aendelee na kazi. Waliweza pia kuongeza furaha kwenye nyasi, miti, na kila chembe ya udongo, huku wakifanya kila siku, na kila mwaka kuwa wa kipekee…. Wakiwa na lugha zao binafsi na kwa njia zao wenyewe, walipitisha taarifa kwa viumbe vyote vilivyokuwa ardhini. Na kwa kutumia njia zao maalum za kuishi, waliweka alama katika viumbe vyote, ambavyo juu yake waliacha alama…. Walikuwa na uhusiano wa karibu sana na udongo, nyasi, na misitu, na walileta nguvu na uhai kwenye udongo, nyasi, na misitu, na wakaweza kuleta ushawishi na salamu za Muumba kwa viumbe hai vyote …

Macho ya Muumba yalikagua vitu vyote Alivyoviumba, na kwa wakati huu macho Yake yalitulia juu ya misitu na milima, mawazo Yake yalikuwa yakizunguka. Maneno Yake yalipokuwa yakitamkwa, katika misitu minene, na juu ya milima, palionekana aina ya viumbe vilivyo tofauti na vilivyokuja hapo awali: Walikuwa ni wanyama wa mwituni waliotamkwa kwa kinywa cha Mungu. Kwa muda mrefu, walitikisa vichwa vyao na kupigapiga mikia yao, kila mmoja wao akiwa na sura yake ya kipekee. Baadhi yao walikuwa na manyoya mengi, baadhi yao walikuwa na kiunzi nje cha kujikinga, baadhi yao walikuwa wakionyesha meno yao makali, baadhi yao walikuwa wanakenua, baadhi yao walikuwa na shingo ndefu, baadhi yao walikuwa na mkia—mfupi, baadhi walikuwa na macho—makali, baadhi walikuwa na macho ya woga, baadhi walikuwa wamejiinamia ili wale nyasi, baadhi walikuwa na damu midomoni mwao, baadhi walikuwa wakiruka-ruka kwa miguu miwili, baadhi walikuwa wakitembea kwa kwato nne, baadhi yao walikuwa juu ya miti wakitazama kwa mbali, baadhi walikuwa wakivizia msituni, baadhi walikuwa wakitafuta mapango ya kupumzikia, baadhi walikuwa wakikimbiakimbia na kucheza kwa furaha kwenye nchi tambarare, baadhi walikuwa wakinyatianyatia kwenye misitu…; baadhi yao walikuwa wakinguruma, baadhi walikuwa wakitoa milio mikali, baadhi yao walikuwa wakibweka, wengine walikuwa wakilia…; baadhi walikuwa na sauti za juu, baadhi walikuwa na sauti za chini, baadhi walikuwa na sauti nzito, baadhi walikuwa na sauti nyororo na nzuri…; baadhi walikuwa ni wakali, na baadhi walikuwa ni wapole, baadhi walikuwa wanachukiza kutazama, baadhi walikuwa wanavutia, baadhi walikuwa wanaogopesha, baadhi walikuwa wa kirafiki na wasiodhuru…. Mmoja baada ya mwingine, kila mmoja alijitokeza. Tazama jinsi wanavyojidai na walivyo wakorofi, wenye kujiachia kwa uhuru, wasijue chochote kuhusu wenzao waliokuwa kando yao, wasitake hata kuchukua muda wa kutazamana…. Kila mmoja akiwa amebeba maisha maalum aliyopewa na Muumba, walionekana katika misitu na juu ya milima, na ukali wao wenyewe, na ukatili wao. Viumbe vyenye dharau kati ya vyote, na vyenye kujidai na kutawala—ni nani aliyewafanya kuwa mabwana wa kweli wa milimani na misituni? Kuanzia wakati ambao kuonekana kwao kuliamriwa na Muumba, waliweza “kumiliki” katika misitu na katika milima, kwani Muumba alikuwa tayari Amepangilia mipaka yao na kuamua upana wa eneo la kuwepo kwao. Walikuwa tu ni mabwana wa kweli wa milimani na misituni, na ndiyo maana walikuwa ni wakali sana, wenye dharau sana. Waliitwa “wanyama wa mwituni” kimsingi kwa sababu, kati ya viumbe vyote, ndio waliokuwa wakali sana, wakatili, na wasiofugwa. Wasingeweza kufugwa, hivyo basi wasingeweza kulelewa na wasingeweza kuishi kwa amani na mapatano na mwanadamu au kufanya kazi kwa niaba ya mwanadamu. Ni kwa Sababu hawakuweza kufugwa, hawakuweza kumfanyia kazi mwanadamu, ndiyo maana iliwalazimu kuishi kwa umbali fulani kutoka kwa mwanadamu, na wasingeweza kusongelewa na mwanadamu. Kwa upande mwingine, ilikuwa ni kwa sababu waliishi kwa umbali fulani kutoka kwa wanadamu, na wasingeweza kukaribiwa na wanadamu, ndio maana waliweza kutimiza jukumu walilopewa na Muumba: kuilinda milima na misitu. Ule ukali wao uliilinda milima na kuilinda misitu, na ndio uliokuwa ulinzi bora zaidi na wenye hakikisho la kuwepo kwao na kuongezeka kwao. Wakati huo huo, ukali wao ulidumisha na kuhakikisha usawa kati ya vitu vyote. Kuwasili kwao kulileta msaada na uhifadhi wa milima na misitu; kuwasili kwao kuliingiza nguvu na uzima wa kudumu kwenye milima ile mitupu na misitu mitupu. Kuanzia wakati huu na kuendelea, milima na misitu ikawa ni makao yao ya kudumu, na wasingewahi kupoteza maskani yao, kwa sababu milima na misitu ilionekana na ikawepo kwa ajili yao, na wanyama wa mwituni wangetimiza wajibu wao na kufanya kila kitu ambacho wangeweza ili kuilinda. Kwa hivyo, pia, wanyama wa mwituni wangeweza kutii kwa umakinifu maagizo ya Muumba ili waweze kubakia katika eneo lao, na kuendelea kutumia asili yao ya kinyama ili kudumisha usawa wa vitu vyote vilivyowekwa na Muumba, na kuonyesha waziwazi mamlaka na nguvu za Muumba!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 89)

Katika Mamlaka ya Muumba, Vitu Vyote ni Vikamilifu

Vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, vikiwemo vile ambavyo vingeweza kujongea na vile ambavyo visingeweza kujongea, kama vile ndege na samaki, kama vile miti na maua, na hata ikiwemo mifugo, wadudu, na wanyama wa mwituni walioumbwa kwenye siku ya sita—vyote vilikuwa ni vyema machoni pa Mungu, na, vilevile, machoni mwa Mungu, vitu hivi, kulingana na mpango Wake, vilikuwa vimetimiza kilele cha ukamilifu, navyo vilikuwa vimefikia viwango ambavyo Mungu alitaka kutimiza. Hatua kwa hatua, Muumba alifanya kazi Aliyonuia kufanya kulingana na mpango Wake. Kimoja baada ya kingine, vitu hivi Alivyonuia kuumba vilijitokeza, na kujitokeza kwa kila kiumbe kulikuwa onyesho la Mamlaka ya Muumba, na udhihirisho wa mamlaka Yake, na kwa sababu ya udhihirisho huu, viumbe vyote visingeweza kujizuia ila kushukuru kwa neema ya Muumba na riziki ya Muumba. Wakati matendo ya kimiujiza ya Mungu yalipokuwa yakijidhihirisha, ulimwengu huu ulijawa, kidogo kidogo, kwa vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, na ulibadilika kutoka kwenye machafuko na giza hadi kwenye ubayana na nuru, kutoka kwenye utulivu wa kutisha hadi kwenye uchangamfu na uhai usio na kikomo. Miongoni mwa vitu vyote vya uumbaji, kutoka kwa vitu vikubwa hadi vidogo, kutoka kwa vile vidogo hadi kwa vile vinavyoweza kutazamwa tu kwa hadubini, hakuna chochote ambacho hakikuumbwa kupitia kwa Mamlaka na nguvu za Muumba, na vilikuwa na umuhimu wa kipekee na asili na thamani ya kuwepo kwa kila kiumbe. Licha ya tofauti zao katika maumbo na muundo, lazima viumbe hivi vingeumbwa na Muumba ili viwepo chini ya mamlaka ya Muumba. Wakati mwingine watu wataona mdudu, yule aliye na sura mbaya kabisa na watasema, “Mdudu yule anatisha, hakuna namna ambavyo kiumbe chenye sura mbaya kama hicho kinaweza kuwa kiliumbwa na Mungu—hakuna njia ambayo Angeumba kitu chenye sura mbaya hivyo.” Mtazamo wa kipumbavu kweli! Kile wanachofaa kusema ni, “Ingawa mdudu huyu ana sura mbaya sana, lakini aliumbwa na Mungu, na kwa hivyo, lazima awe na kusudio lake la kipekee.” Katika fikira za Mungu, Alinuia kutoa kila aina ya mwonekano, na kila aina ya jukumu na matumizi, kwa viumbe hai mbalimbali Alivyoviumba, na kwa hivyo hakuna kati ya viumbe hivyo ambavyo Mungu aliumba vilivyoumbwa vikiwa vimefanana. Kuanzia mwonekano wao wa nje hadi viungo vyao vya ndani, kutoka kwenye tabia zao za kuishi hadi katika eneo ambalo wanaishi—kila kiumbe ni tofauti. Ng’ombe wana mwonekano wa ng’ombe, punda wana mwonekano wa punda, kulungu wana mwonekano wa kulungu na tembo wana mwonekano wa tembo. Je, unaweza kusema ni yupi mwenye mwonekano bora zaidi, na ni yupi mwenye mwonekano mbaya zaidi? Je, unaweza kusema ni yupi mwenye manufaa zaidi, na ni uwepo wa yupi una umuhimu mdogo zaidi? Baadhi ya watu wanapenda namna ambavyo ndovu huonekana, lakini hakuna anayetumia ndovu kutayarisha mashamba ya kupanda: baadhi ya watu wanapenda namna simba na chui-milia wanavyoonekana, kwani mwonekano wao unavutia zaidi miongoni mwa viumbe vyote, lakini je, unaweza kuwafuga nyumbani? Kwa ufupi, kuhusiana na vitu vyote vya uumbaji, mwanadamu anapaswa kunyenyekea chini ya mamlaka ya Muumba, ambavyo ni kusema kwamba, nyenyekea katika mpangilio uliochaguliwa na Muumba katika vitu vyote; huu ndio mtazamo wenye busara zaidi. Mtazamo pekee wa kutafuta, na wa kuwa mtiifu, kwa nia za asili za Muumba ndio kukubali kwa kweli na kuwa na uhakika wa mamlaka ya Muumba. Ni chema machoni pa Muumba, kwa hivyo mwanadamu ana sababu gani ya kutafuta kosa?

Hivyo basi, vitu vyote vilivyo chini ya mamlaka ya Muumba vinapaswa kucheza wimbo mpya kwa ajili ya ukuu wa Muumba, vinapaswa kuanzisha wimbo wa utukufu kwa ajili ya kazi Yake ya siku mpya, na kwa wakati huu Muumba ataufungua ukurasa mpya katika kazi ya usimamizi Wake! Kulingana na sheria iliyowekwa na Muumba ya kuchipua wakati wa masika, kustawi wakati wa kiangazi, mavuno wakati wa vuli, na kuhifadhi majira ya kipupwe, vitu vyote vitaendana na mpango wa usimamizi wa Muumba, na vitakaribisha siku yao mpya, mwanzo mpya na mkondo mpya wa maisha. Vitaendelea kuishi na kuzaliana kwa mfululizo usioisha ili waweze kukaribisha kila siku chini ya ukuu wa mamlaka ya Muumba …

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 90)

Hakuna Kiumbe Chochote Kilichoumbwa na Kisichoumbwa Kinachoweza Kubadilisha Utambulisho wa Muumba

Tangu Alipoanza uumbaji wa vitu vyote, nguvu za Mungu zilianza kuonyeshwa na zikaanza kufichuliwa, kwani Mungu alitumia maneno kuumba vitu vyote. Haijalishi ni kwa njia gani Aliviumba, haijalishi ni kwa nini Aliviumba, vitu vyote viliumbwa na kusimama imara na kuwepo kwa sababu ya matamshi ya Mungu, na haya ndiyo mamlaka ya kipekee ya Muumba. Kwa wakati ambao bado mwanadamu hajaonekana ulimwenguni, Muumba alitumia nguvu na mamlaka Yake kuumba vitu vyote kwa ajili ya mwanadamu, na Akatumia mbinu Zake za kipekee kutayarisha mazingira yanayofaa kuishi mwanadamu. Kwa yote Aliyoyafanya, ilikuwa ni kwa kumtayarishia mwanadamu ambaye hivi karibuni angepokea pumzi Yake. Hivi ni kusema kwamba, kwenye muda ule kabla ya mwanadamu kuumbwa, mamlaka ya Mungu yalionyeshwa kupitia kwa viumbe vyote tofauti na mwanadamu, na vitu vikubwa kama vile mbingu, mwanga, bahari, na ardhi, na vile vilivyo vidogo kama vile wanyama na ndege, pamoja na wadudu na vijiumbe vyote vya kila aina, vikiwemo vimelea mbalimbali visivyoonekana kwa macho ya kawaida. Kila kimoja kilipewa uhai kwa matamshi ya Muumba, na kila kila kimoja kiliongezeka kwa sababu ya matamshi ya Muumba na kila kimoja kiliishi chini ya ukuu wa Muumba kwa sababu ya matamshi ya Muumba. Ingawa hawakupokea pumzi ya Muumba, bado walionyesha uhai na nguvu walizopewa na Muumba kupitia kwa maumbo na miundo yao tofauti; Ingawa hawakupokea uwezo wa kuongea waliopewa wanadamu na Muumba, kila kimoja kilipokea namna ya kuelezea uhai wao ambao wamepewa na Muumba, na ambao ulitofautiana na ile lugha ya wanadamu. Mamlaka ya Muumba sio tu kwamba yanatoa nguvu za uhai katika vitu vinavyoonekana kuwa tulivu, ili visiwahi kutoweka, bali pia, Anatoa silika ya kuzaliana na kuongezeka kwa kila kiumbe hai, ili visiwahi kutoweka, na ili kizazi baada ya kizazi, viweze kupitisha sheria na kanuni za kuishi walizopewa na Muumba. Namna ambavyo Muumba anatumia mamlaka Yake haifuati kwa uthabiti mtazamo wa mambo makubwa makubwa au madogomadogo, na haiwekewi mipaka na taratibu zozote; Anaweza kuamuru utendakazi wa ulimwengu na kushikilia ukuu juu ya uhai na kifo kwa vitu vyote, na, vilevile, Anaweza kuendesha vituvyote ili viweze kumhudumia Yeye; Anaweza kusimamia kazi zote za milima, mito, na maziwa, na kutawala vitu vyote ndani yake, na, zaidi ya hayo, Anaweza kutoa kile ambacho kinahitajika na viumbe vyote. Haya ndiyo maonyesho ya mamlaka ya kipekee ya Muumba miongoni mwa vitu vyote mbali na mwanadamu. Maonyesho kama hayo si tu katika maisha haya tunayoishi; kamwe hayatakoma, au kupumzika, na hayawezi kubadilishwa au kuharibiwa na mtu yeyote au kitu chochote, wala hayawezi kuongezwa au kupunguzwa na mtu yeyote au kitu chochote—kwani hamna kile kinachoweza kuchukua nafasi ya utambulisho wa Muumba, na, hivyo basi, mamlaka ya Muumba hayawezi kubadilishwa na kiumbe chochote kilichoumbwa, na hayawezi kufikiwa na kiumbe chochote ambacho hakikuumbwa. Chukulia wajumbe na malaika wa Mungu kwa mfano. Hawamiliki nguvu za Mungu, isitoshe hawamiliki mamlaka ya Muumba, na sababu ambayo hawana nguvu na mamlaka ya Mungu ni kwa sababu hawamiliki kiini cha Muumba. Vile viumbe ambavyo havikuumbwa, kama vile wajumbe na malaika wa Mungu, Ingawa vinaweza kufanya baadhi ya mambo kwa niaba ya Mungu, haviwezi kumwakilisha Mungu. Ingawa wanamiliki nguvu fulani zisizomilikiwa na binadamu, hawamiliki mamlaka ya Mungu, hawamiliki mamlaka ya Mungu ya kuumba vitu vyote, kuamuru vitu vyote, na kushikilia ukuu juu ya viumbe vyote. Na kwa hivyo upekee wa Mungu hauwezi kubadilishwa na kiumbe chochote ambacho hakikuumbwa, na vilevile, mamlaka na nguvu za Mungu haziwezi kubadilishwa na kiumbe chochote ambacho hakikuumbwa. Katika Biblia, je, umewahi kusoma kuhusu mjumbe yeyote wa Mungu aliyeumba vitu vyote? Na kwa nini Mungu hakuwahi kumtuma yeyote kati ya wajumbe Wake au malaika kuumba vitu vyote? Kwa sababu hawakumiliki mamlaka ya Mungu, na kwa hivyo hawakumiliki uwezo wa kutekeleza mamlaka ya Mungu. Sawa tu na viumbe vyote vilivyoumbwa, vyote viko chini ya ukuu wa Muumba, na chini ya mamlaka ya Muumba, na kwa hivyo, kwa njia ile ile, Muumba pia ni Mungu wao na pia ndiye Mtawala wao. Miongoni mwa kila mmoja wao—haijalishi kama wao ni bora au duni, wenye nguvu nyingi au kidogo—hakuna hata mmoja anayeweza kuzidi mamlaka ya Muumba, na kwa hivyo miongoni mwao, hakuna hata mmoja wao anayeweza kuchukua nafasi ya utambulisho wa Muumba. Hawatawahi kuitwa Mungu, na hawatawahi kuweza kuwa Muumba. Huu ni ukweli na hoja zisizobadilika!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 91)

Mungu Hutumia Matamshi Yake Kuanzisha Agano na Binadamu

Mwa 9:11-13 Na nitaweka agano langu na ninyi, wala miili yote haitaondolewa tena na maji ya gharika; wala hakutakuwa na gharika tena kuiharibu dunia. Naye Mungu akasema, Hii ni alama ya agano ambayo naifanya kati ya Mimi na ninyi na viumbe vyote vyenye uhai vilivyo nanyi, kwa vizazi vya kudumu: naweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa alama ya agano kati ya Mimi na dunia.

Baada ya Kuumba Vitu Vyote, Mamlaka ya Muumba Yanathibitishwa na Kuonyeshwa kwa Mara Nyingine Tena Kwenye Agano la Upinde wa Mvua

Mamlaka ya Muumba siku zote yanaonyeshwa na kutekelezwa miongoni mwa viumbe vyote, Naye sio tu kwamba Anatawala hatima ya vitu vyote, bali pia Anawatawala wanadamu, kiumbe maalum ambacho Alikiumba kwa mikono Yake mwenyewe, na kinachomiliki muundo tofauti wa uhai na kinachopatikana kwa mfumo tofauti wa maisha. Baada ya kuumba vitu vyote, Muumba hakuacha kuonyesha mamlaka na nguvu Zake; kwake Yeye, mamlaka ambayo Alishikilia ukuu juu ya vitu vyote na hatima ya mwanadamu kwa ujumla, ilianza rasmi tu pale ambapo mwanadamu alizaliwa kwa kweli kutoka kwenye mkono Wake. Alinuia kumsimamia mwanadamu, kumtawala mwanadamu, Alinuia kumwokoa mwanadamu, Alinuia kumpata mwanadamu kwa kweli, kumpata mwanadamu ambaye angetawala vitu vyote, na Alinuia kumfanya mwanadamu kama huyo kuishi chini ya mamlaka Yake, na kujua mamlaka Yake, na kutii mamlaka Yake. Hivyo basi, Mungu akaanza kuonyesha rasmi mamlaka Yake miongoni mwa binadamu kwa kutumia matamshi Yake, na Akaanza kutumia mamlaka Yake kufanikisha matamshi Yake. Bila shaka, mamlaka ya Mungu yalionyeshwa mahali pote wakati wa mchakato huu; Nimeweza kuchukua tu baadhi ya mifano mahususi, inayojulikana ambayo unaweza kuelewa na kujua upekee wa Mungu na kuelewa na kujua upekee wa mamlaka ya Mungu.

Kunao mfanano kati ya kifungu cha kwenye Mwanzo 9:11-13 na vifungu vilivyo hapo juu vinayohusu rekodi ya uumbaji wa Mungu wa ulimwengu, lakini pia kuna tofauti. Mfanano ni upi? Mfanano umo katika matumizi ya matamshi na Mungu kuweza kufanya kile ambacho Alinuia, na tofauti ni kwamba, kifungu hiki ni mazungumzo ya Mungu na binadamu, ambapo Alianzisha agano na binadamu, na Akamwambia binadamu kuhusu kile ambacho kilikuwa ndani ya agano hilo. Utekelezaji huu wa mamlaka ya Mungu ulitimizwa wakati wa mazungumzo Yake na mwanadamu, ambavyo ni kusema kwamba, kabla ya uumbaji wa mwanadamu, maneno ya Mungu yalikuwa maagizo, na amri ambavyo vilitolewa kwa viumbe ambavyo Alinuia kuumba. Lakini sasa kulikuwa na mtu wa kusikiliza matamshi ya Mungu, na hivyo basi matamshi Yake yalikuwa ya mazungumzo na binadamu, na pia maagizo na maonyo kwa binadamu, na zaidi ya hayo, maneno ya Mungu yalikuwa ni amri zilizobeba mamlaka Yake na ambazo zilitolewa kwa vitu vyote.

Ni hatua gani ya Mungu imerekodiwa katika kifungu hiki? Kifungu kinarekodi agano ambalo Mungu alianzisha na binadamu baada ya Yeye kuangamiza ulimwengu kwa gharika, linamwambia binadamu kwamba Mungu asingesababisha tena uharibifu kama huo juu ya ulimwengu, na kwamba, kwa mwisho huu, Mungu aliumba ishara—na ishara hii ilikuwa nini? Katika maandiko inasemwa kwamba “Mimi nauweka upinde Wangu mawinguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati Yangu na nchi.” Haya ni matamshi halisi yaliyotamkwa na Muumba kwa mwanadamu. Aliposema matamshi haya, upinde wa mvua ulionekana mbele ya macho ya binadamu, ambapo ulibakia mpaka leo. Kila mmoja ameuona upinde wa mvua kama huo, na unapouona, je, unajua namna unavyojitokeza? Sayansi haiwezi kuthibitisha haya, au kutafuta chanzo chake, au kutambua mambo yanayosababisha upinde huu wa mvua. Hiyo ni kwa sababu, upinde wa mvua ni ishara ya agano lilioanzishwa kati ya Muumba na binadamu; hauhitaji msingi wowote wa kisayansi, haukuumbwa na binadamu, wala binadamu hawezi kuubadilisha. Ni maendelezo ya mamlaka ya Muumba baada ya Yeye kuongea matamshi Yake. Muumba alitumia mbinu Yake mahususi kutii agano lake na binadamu na ahadi Yake, na hivyo basi matumizi Yake ya upinde wa mvua kama ishara ya agano ambalo Alianzisha ni maelekezo na sheria ya mbinguni yatakayobakia milele bila kubadilika, haijalishi kama ni kuhusiana na Muumba au mwanadamu aliyeumbwa. Ilhali sheria hii isiyobadilika ni, inaweza kusemwa, maonyesho mengine ya kweli ya mamlaka ya Muumba kufuatia uumbaji Wake wa vitu vyote, na lazima isemwe kwamba mamlaka na nguvu za Muumba hayana mipaka; matumizi Yake ya upinde wa mvua ni ishara ya maendelezo na upanuzi wa mamlaka ya Muumba. Hiki kilikuwa kitendo kingine kilichotekelezwa na Mungu kwa kutumia matamshi Yake, na ilikuwa ni ishara ya agano ambalo Mungu alikuwa ameanzisha na mwanadamu kwa kutumia matamshi. Alimwambia binadamu kuhusu kile ambacho Aliamua kuleta, na kwa njia gani kingekamilishwa na kutimizwa, na kwa njia hii suala liliweza kutimizwa kulingana na matamshi kutoka kwenye kinywa cha Mungu. Mungu pekee ndiye anayemiliki nguvu kama hizo, na leo, miaka elfu kadhaa baada ya Yeye kuongea matamshi haya, binadamu angali bado anaweza kuangalia upinde wa mvua uliozungumziwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu. Kwa sababu ya matamshi hayo yaliyotamkwa na Mungu, kitu hiki kimebakia bila ya kusongezwa na kubadilishwa mpaka kufikia leo. Hakuna anayeweza kuuondoa upinde huu wa mvua, hakuna anayeweza kubadilisha sheria zake, na upo kimsingi kutokana na matamshi ya Mungu. Haya kwa hakika ni mamlaka ya Mungu. “Mungu humaanisha kile Anachokisema, na kile Anachokisema kinatimizwa, na kile Anachokitimiza kitadumu milele.” Matamshi kama haya kwa kweli yanaonyeshwa waziwazi hapa, na ni ishara na sifa wazi kuhusu mamlaka na nguvu za Mungu. Ishara au sifa kama hiyo haimilikiwi na au kuonekana katika viumbe vyovyote vile vilivyoumbwa, wala kuonekana kwenye viumbe vyovyote vile ambavyo havikuumbwa. Inamilikiwa tu na Mungu wa kipekee, na inatofautisha utambulisho na kiini kinachomilikiwa na Muumba pekee na kile cha viumbe vilivyoumbwa. Wakati uo huo, ni ishara na sifa pia ambayo mbali na Mungu Mwenyewe, haitawahi kuzidiwa kiwango na kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa.

Uanzishaji wa agano Lake na binadamu ilikuwa ni kitendo chenye umuhimu mkubwa, na ambao Alinuia kutumia ili kuwasilisha hoja kwa binadamu na kumwambia binadamu mapenzi Yake, na mpaka kufikia hapa, Alitumia mbinu ya kipekee, kwa kutumia ishara maalum ya kuanzisha agano na binadamu, ishara ambayo ilikuwa ahadi ya agano ambalo Alikuwa ameanzisha na binadamu. Kwa hivyo, je, uanzishaji wa agano hili ulikuwa ni tukio kubwa? Na tukio hili lilikuwa kubwa kiasi gani? Hii haswa ndiyo inayoonyesha namna ambavyo agano hili lilivyo maalum: si agano lililoanzishwa kati ya binadamu mmoja na mwingine, au kundi moja na jingine, au nchi moja na nyingine, lakini agano lililoanzishwa kati ya Muumba na wanadamu kwa ujumla, na litabakia halali mpaka siku ambayo Muumba atakomesha mambo yote. Mtekelezaji wa agano hili ni Muumba, na mwendelezaji pia ni Muumba. Kwa ufupi, ukamilifu wa agano la upinde wa mvua ulioanzishwa pamoja na mwanadamu ulikamilishwa na kutimizwa kulingana na mazungumzo kati ya Muumba na mwanadamu, na umebakia vivyo hivyo mpaka leo. Ni nini kingine ambacho viumbe vinaweza kufanya mbali na kujinyenyekeza, na kutii, na kusadiki, na kufahamu, na kutolea ushuhuda, na kusifu mamlaka ya Muumba? Kwa kuwa hakuna yeyote yule isipokuwa Mungu wa pekee anayemiliki nguvu za kuanzisha agano kama hilo. Kujitokeza kwa upinde wa mvua mara kwa mara, kunatangaza kwa mwanadamu na kumtaka azingatie agano lile kati ya Muumba na mwanadamu. Katika muendelezo wa kuonekana kwa agano kati ya Muumba na binadamu, kile kinachoonyeshwa kwa mwanadamu si upinde wa mvua au agano lenyewe, bali ni mamlaka ya Muumba yasiyobadilika. Kujitokeza kwa upinde wa mvua, mara kwa mara, kunaonyesha yale matendo ya ajabu na ya kimiujiza ya Muumba katika mahali pa siri, na, kwa wakati huo huo ni onyesho muhimu la mamlaka ya Muumba ambayo hayatawahi kupungua, na wala kubadilika. Je, hili si onyesho la kipengele kingine cha mamlaka ya kipekee ya Muumba?

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 92)

Baraka za Mungu

Mwa 17:4-6 Na kuhusu mimi, tazama, agano langu liko na wewe, na wewe utakuwa baba yao mataifa mengi. Nalo jina lako halitakuwa Abramu tena, ila jina lako litaitwa Ibrahimu; kwa kuwa nimekufanya uwe baba yao mataifa mengi. Na Mimi nitafanya uwe na uzao ulio mwingi mno, na nitayaunda mataifa kutoka kwako, nao wafalme watatoka kwako.

Mwa 18:18-19 Ibrahimu hakika atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa ndani yake. Kwani namjua, kuwa atawatawala watoto wake na nyumba yake kufuata yeye, na wataishika njia ya Yehova, kufanya haki na hukumu; ili Yehova aweze kumletea Ibrahimu yale ambayo amemwambia.

Mwa 22:16-18 Mimi nimeapa kwa nafsi yangu, akasema Yehova, kwa maana umefanya jambo hili, na hujamzuilia mwana wako, mwana wako wa pekee: Kuwa katika kubariki nitakupa baraka, na katika kuzidisha uzao wako nitazidisha mithili ya nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utakuwa na mlango wa maadui zao; Na kupitia uzao wako kila taifa la dunia litabarikiwa; kwa kuwa umeitumikia sauti yangu.

Ayu 42:12 Kwa hivyo Yehova akabariki mwisho wa Ayubu zaidi kuliko mwanzo wake: kwa sababu alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na elfu moja ya jozi za ng’ombe, na elfu moja ya punda wa kike.

Mbinu na Sifa za Kipekee za Matamshi ya Muumba Ni Ishara ya Utambulisho na Mamlaka ya Kipekee ya Muumba

Wengi wanatamani kutafuta, na kupata, baraka za Mungu, lakini si kila mtu anayeweza kupata baraka hizi, kwani Mungu anazo kanuni Zake binafsi, na Yeye hubariki binadamu kulingana na njia Zake binafsi. Ahadi ambazo Mungu hutoa kwa binadamu, na kiwango cha neema ambacho Yeye humpa binadamu, vyote vinatolewa kulingana na fikira na vitendo vya binadamu. Hivyo, ni nini huonyeshwa kupitia kwa baraka za Mungu? Watu wanaweza kuona nini ndani yake? Wakati huu, hebu tuweke kando mazungumzo kuhusu ni aina gani ya watu ambao Mungu hubariki, na kanuni anazofuata Mungu katika kubariki binadamu. Badala yake, hebu tuangalie baraka za Mungu kwa binadamu kwa lengo la kujua mamlaka ya Mungu, kutoka kwenye mtazamo wa kujua mamlaka ya Mungu.

Vifungu vinne vya maandiko hapo juu ni rekodi zote kuhusu baraka za Mungu kwa mwanadamu. Vinatupa ufafanuzi wenye maelezo kuhusu wapokeaji wa baraka za Mungu, kama vile Ibrahimu na Ayubu, vilevile vinatupa sababu zinazoelezea kwa nini Mungu alitoa baraka Zake, na ni nini kilichokuwa ndani ya baraka hizi. Ile sauti na mbinu ya matamshi ya Mungu, mtazamo na nafasi ambayo Yeye alizungumza kutoka kwayo, inawaruhusu watu kufahamu kwamba Yule ambaye hutoa baraka na mpokeaji wa baraka hizo ni wa utambulisho, hadhi na kiini tofauti kabisa. Sauti na mbinu ya matamshi haya, na nafasi ambayo yalizungumzwa, ni ya kipekee kwa Mungu, anayemiliki utambulisho wa Muumba. Anayo mamlaka na uwezo, pamoja na heshima ya Muumba, na ukuu ambao hakuna mtu yeyote anayeweza kuitilia shaka.

Kwanza hebu tuangalie Mwa 17:4-6: “Tazama, mimi agano langu nimefanya na wewe, na wewe utakuwa baba wa mataifa mengi. Nalo jina lako halitakuwa Abramu tena, ila jina lako litaitwa Ibrahimu; kwa kuwa nimekufanya uwe baba wa mataifa mengi. Na Mimi nitafanya uwe na uzao ulio mwingi mno, na nitayaunda mataifa kutoka kwako, nao wafalme watatoka kwa wewe.” Matamshi haya ndiyo yaliyokuwa agano ambalo Mungu alianzisha na Ibrahimu, pamoja na baraka za Mungu kwa Ibrahimu: Mungu angemfanya Ibrahimu kuwa baba wa mataifa, Angemfanya kuwa na uzao mwingi, na Angemfanya kuwa na mataifa mengi, nao wafalme wangetoka kwake. Je, unayaona mamlaka ya Mungu katika maneno haya? Na unayaonaje mamlaka kama hayo? Ni kipengele gani cha kiini cha mamlaka ya Mungu unachokiona? Kutokana na usomaji wa makini wa maneno haya, si vigumu kutambua kwamba mamlaka na utambulisho wa Mungu vyote vimefichuliwa waziwazi katika maneno ya matamshi ya Mungu. Kwa mfano, Mungu anaposema “agano langu nimefanya na wewe, na wewe utakuwa … kuwa nimekufanya … Mimi nitafanya uwe…,” kauli kama vile “wewe utakuwa” na “nitayaunda,” ambazo maneno yake yanasheheni thibitisho la utambulisho na mamlaka ya Mungu, kwa upande mmoja ni onyesho la uaminifu wa Muumba; kwa upande mwingine, ni maneno maalum yaliyotumiwa na Mungu, anayemiliki utambulisho wa Muumba—pamoja na kuwa sehemu ya msamiati wa kawaida. Kama mtu atasema anatumai kuwa mtu mwingine atazidisha uzao, kwamba mataifa yatafanywa kutoka kwao, na kwamba wafalme watatoka kwao, basi hiyo bila shaka ni aina ya tamanio, na si ahadi wala baraka. Na hivyo, watu wasithubutu kusema “Nitakufanya uwe hivi na hivi, utakuwa hivi na hivi,” kwa kuwa wanajua kwamba hawamiliki nguvu kama hizo; si juu yao, na hata kama watasema maneno kama hayo, maneno yao yatakuwa matupu, na ya kipuzi, yanayoendeshwa na matamanio na maono yao. Je, yupo yeyote anayethubutu kuongea kwa sauti kuu kama hiyo ilhali wanahisi kwamba hawawezi kutimiza matamanio yao? Kila mtu hutamani mema yafikie kizazi chake, na kutumai kwamba kitafanikiwa na kufurahia mafanikio makubwa. “Ingekuwa ni bahati iliyoje kama mmoja wao angekuwa ni mfalme! Kama mmoja angekuwa gavana ingekuwa vizuri, pia—mradi tu wawe ni watu muhimu!” Haya yote ni matamanio ya watu, lakini watu wanaweza kutamani tu baraka juu ya kizazi chao, na hawawezi kutimiza au kufanya ahadi zao zozote kuwa kweli. Katika mioyo yao, kila mtu anajua waziwazi kwamba wao hawamiliki nguvu za kutimiza mambo kama hayo, kwani kila kitu chao kipo nje ya udhibiti wao, na hivyo basi watawezaje kuamuru hatima za wengine? Sababu inayomfanya Mungu kusema maneno kama haya ni kwa sababu Mungu anamiliki mamlaka kama hayo, na Anaweza kutekeleza na kusababisha ahadi zote Anazotoa kwa ajili ya binadamu, na kufanya baraka zote Anazompa binadamu kuwa kweli. Binadamu aliumbwa na Mungu, na kwa Mungu kumfanya mtu awe na uzao mwingi sana ni jambo ambalo litakuwa rahisi sana; kufanya kizazi cha mtu kufanikiwa kutahitaji neno moja tu kutoka Kwake. Hangelazimika kujishughulisha Mwenyewe na kutoa jasho kwa ajili ya kitu kama hicho, au kushughulisha akili Yake, au kujiweka katika taabu juu ya hilo; hii ndiyo nguvu halisi ya Mungu, mamlaka halisi ya Mungu.

Baada ya kusoma “Ibrahimu hakika atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia yeye” kwenye Mwanzo 18:18, je, unaweza kuhisi mamlaka ya Mungu hapo? Je, unaweza kuhisi ubora wa ajabu wa Muumba? Je, unaweza kuhisi ukuu wa Muumba? Maneno ya Mungu yana uhakika. Mungu hasemi maneno kama hayo kwa sababu ya, au katika uwakilishi wa, ujasiri Wake katika ufanisi; badala yake, hayo ni, uthibitisho wa mamlaka ya matamshi, na ni amri inayotimiza maneno ya Mungu. Kuna maneno mawili ambayo unapaswa kuzingatia hapa. Wakati Mungu anaposema “Ibrahimu hakika atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia yeye,” je, kuna dalili ya kutoeleweka katika maneno haya? Je, kuna dalili yoyote ya wasiwasi? Je, kuna dalili yoyote ya hofu? Kwa sababu ya maneno “hakika utakuwa” na “watakuja” katika matamshi ya Mungu, dalili hizi, ambazo zinapatikana tu kwa binadamu na mara nyingi zinajionyesha ndani yake, hazijawahi kupata uhusiano wowote na Muumba. Hakuna mtu angethubutu kutumia maneno kama haya wakati akiwatakia wengine mema, hakuna ambaye angethubutu kumbariki mwingine apate taifa kubwa na lenye nguvu kwa uhakika kama huo, au kutoa ahadi kwamba mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia kwake. Kadiri maneno ya Mungu yanavyokuwa ya hakika zaidi, ndivyo yanavyothibitisha zaidi kitu fulani—na kitu hicho ni nini? Yanathibitisha kuwa Mungu anayo mamlaka kama hayo, kuwa mamlaka Yake yanaweza kutimiza mambo haya, na kwamba utimizaji wake hauzuiliki. Mungu alikuwa na uhakika katika moyo Wake, bila kusita kokote, kwa kila kitu Alichombariki Ibrahimu. Aidha, ukamilifu wa haya utakamilishwa kulingana na maneno Yake, na hakuna nguvu ingeweza kubadilisha, kuzuia, kuharibu, au kutatiza kukamilika kwake. Haijalishi kile ambacho kingetokea, hakuna kitu ambacho kingebatilisha au kuathiri kutimia na kukamilika kwa matamshi ya Mungu. Huu ndio uwezo mkubwa wa maneno yaliyotamkwa kutoka kinywa cha Muumba, na mamlaka ya Muumba ambayo hayavumilii kanusho la binadamu! Baada ya kuyasoma maneno haya, ungali unahisi shaka? Maneno haya yalitamkwa kutoka kinywani mwa Mungu, na kuna nguvu, ukuu na mamlaka katika maneno ya Mungu. Uwezo na mamlaka kama haya, na kutozuilika kwa kukamilika kwa hoja, haviwezi kufikiwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa na haviwezi kupitwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa. Muumba pekee ndiye anaweza kuongea na binadamu kwa sauti na mkazo kama huo, na ukweli umethibitisha kwamba ahadi Zake si maneno matupu, au majigambo yasiyo na maana, bali ni maonyesho ya mamlaka ya kipekee yasiyoweza kupitwa na mtu, kitu, au kifaa chochote.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 93)

Baraka za Mungu

Mwa 17:4-6 Na kuhusu mimi, tazama, agano langu liko na wewe, na wewe utakuwa baba yao mataifa mengi. Nalo jina lako halitakuwa Abramu tena, ila jina lako litaitwa Ibrahimu; kwa kuwa nimekufanya uwe baba yao mataifa mengi. Na Mimi nitafanya uwe na uzao ulio mwingi mno, na nitayaunda mataifa kutoka kwako, nao wafalme watatoka kwako.

Mwa 18:18-19 Ibrahimu hakika atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa ndani yake. Kwani namjua, kuwa atawatawala watoto wake na nyumba yake kufuata yeye, na wataishika njia ya Yehova, kufanya haki na hukumu; ili Yehova aweze kumletea Ibrahimu yale ambayo amemwambia.

Mwa 22:16-18 Mimi nimeapa kwa nafsi yangu, akasema Yehova, kwa maana umefanya jambo hili, na hujamzuilia mwana wako, mwana wako wa pekee: Kuwa katika kubariki nitakupa baraka, na katika kuzidisha uzao wako nitazidisha mithili ya nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utakuwa na mlango wa maadui zao; Na kupitia uzao wako kila taifa la dunia litabarikiwa; kwa kuwa umeitumikia sauti yangu.

Ayu 42:12 Kwa hivyo Yehova akabariki mwisho wa Ayubu zaidi kuliko mwanzo wake: kwa sababu alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na elfu moja ya jozi za ng’ombe, na elfu moja ya punda wa kike.

Mbinu na Sifa za Kipekee za Matamshi ya Muumba Ni Ishara ya Utambulisho na Mamlaka ya Kipekee ya Muumba

Ni nini tofauti kati ya maneno yanayotamkwa na Mungu na yale yanayotamkwa na binadamu? Unaposoma maneno haya yaliyotamkwa na Mungu, unahisi nguvu za maneno ya Mungu, na mamlaka ya Mungu. Je, unahisi vipi unaposikia watu wakitamka maneno kama hayo? Je, unafikiria kuwa wao wana kiburi kupindukia, na ni wenye kujigamba na wanajionyesha wenyewe? Kwa kuwa hawana nguvu hizi, hawamiliki mamlaka kama haya, na hivyo basi hawawezi kabisa kutimiza mambo kama hayo. Kwamba wao wana uhakika kabisa kuhusu ahadi zao, yaonyesha tu uzembe kwa matamshi yao. Kama mtu anasema maneno kama hayo, basi bila shaka watakuwa wenye kiburi, na waliozidisha ujasiri wao, huku wakijifichua kama mfano wa pekee wa tabia ya malaika mkuu. Maneno haya yalitoka kinywani mwa Mungu; je, unahisi dalili yoyote ya kiburi hapa? Je, unahisi ya kwamba matamshi ya Mungu ni mzaha tu? Matamshi ya Mungu ni mamlaka, maneno ya Mungu ni ukweli, na kabla hajatamka maneno kutoka kinywani Mwake, hivi ni kusema, wakati Anapofanya uamuzi wa kufanya kitu, tayari kitu hicho kimefanyika. Yaweza kusemwa kwamba kila kitu alichosema Mungu kwa Ibrahimu kilikuwa agano ambalo Mungu alianzisha na Ibrahimu, na ahadi Mungu alizozitoa kwa Ibrahimu. Ahadi hii ilikuwa ukweli uliothibitishwa, pamoja na ukweli uliotimizwa, na ukweli huu ulitimizwa hatua kwa hatua katika fikira za Mungu kulingana na mpango wa Mungu. Kwa hivyo, Mungu kusema maneno kama hayo haimaanishi kuwa Ana tabia ya kiburi, kwani Mungu anaweza kutimiza mambo kama hayo. Anazo nguvu na mamlaka, na Anao uwezo kamili wa kutimiza vitendo hivi, na utimizaji wake upo ndani ya upeo wa uwezo Wake. Wakati maneno kama haya yanapotamkwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu, yanakuwa ufunuo na maonyesho ya tabia ya kweli ya Mungu, ufunuo na udhihirisho kamili wa kiini na mamlaka ya Mungu, na hakuna kitu ambacho kinafaa zaidi na kizuri kama uthibitisho wa utambulisho wa Mungu. Namna, sauti, na mpangilio wa maneno ya matamshi kama hayo ndiyo alama haswa ya utambulisho wa Muumba, na vyote hivi vinalingana kikamilifu na maonyesho na utambulisho wa Mungu, na ndani yao hakuna kujifanya, au kasoro; vyote hivi, kwa ukamilifu na kwa ujumla ni, maonyesho kamili ya kiini na mamlaka ya Muumba. Lakini Kuhusu viumbe, havimiliki mamlaka haya, wala kiini hiki, sembuse kumiliki nguvu inayotolewa na Mungu. Kama mwanadamu atadhihirisha tabia kama hiyo, basi hali hiyo itakuwa bila shaka udhihirisho wa tabia yake iliyopotoka, na itaishia katika athari ya kujihusisha visivyofaa na kiburi cha binadamu na tamaa mbaya, na kufichuliwa kwa nia ovu za yule ibilisi, Shetani, anayependa kuwadanganya watu na kuwashawishi waweze kumsaliti Mungu. Na je Mungu anachukuliaje kile ambacho kimefichuliwa kwa lugha kama hii? Mungu angesema kwamba unataka kunyakua nafasi yake na kwamba unataka kumwiga Yeye na kumbadili Yeye. Wakati unaiga sauti ya matamshi ya Mungu, nia yako ni ya kubadilisha nafasi ya Mungu katika mioyo ya watu, kujitwalia mwanadamu ambaye anamilikiwa kihalali na Mungu. Huyu ni Shetani, halisi na bila kukuficha; haya ni matendo ya vizazi vya malaika mkuu visivyovumilika Mbinguni! Miongoni mwenu, je, wapo ambao wamewahi kumuiga Mungu kwa njia fulani kwa kuongea maneno machache, kwa nia ya kupotosha na kudanganya watu na kuwafanya watu kuhisi kuwa maneno na matendo ya mtu huyu yana mamlaka na nguvu za Mungu, kana kwamba kiini na utambulisho wa mtu huyu ni vya kipekee, na hata ni kana kwamba sauti ya mtu huyu ni sawa na ile ya Mungu? Je, umewahi kufanya jambo kama hili? Je, umewahi kuiga sauti ya Mungu katika usemi wako, kwa ishara zinazodaiwa kuiwakilisha tabia ya Mungu, kwa kile unachodhania kuwa ni uwezo na mamlaka? Je, wengi wenu huwa mara nyingi mnatenda, au kupanga kutenda kwa njia kama hiyo? Sasa, unapoona kwa kweli, kuelewa na kujua mamlaka ya Muumba, na kutazama kile ulichokuwa ukikifanya, na ulichokuwa ukifichua kujihusu, je, unahisi vibaya? Je, unatambua ujinga wako na kutokuwa na aibu? Baada ya kuchambua tabia na asili za watu kama hao, je, inaweza kusemwa kuwa wao ndio walaaniwa wa jahanamu? Je, inaweza kusemwa kwamba kila mtu anayefanya mambo kama haya anajiletea udhalilishaji? Je, unatambua uzito wa asili yake? Na uzito wake ni wa kiasi kipi? Nia ya watu wanaotenda mambo kwa njia hii ni kumwiga Mungu. Wanataka kuwa Mungu, na kuwafanya watu kuwaabudu kama Mungu. Wanataka kuondoa nafasi ya Mungu katika mioyo ya watu, na kutupilia mbali yule Mungu anayefanya kazi miongoni mwa binadamu, ili kutimiza nia ya kuwadhibiti watu, na kuwateketeza watu, na kuwamiliki watu hao. Kila mtu ana matamanio na matarajio kama haya yaliyofichika akilini, na kila mtu anaishi katika aina hii ya kiini kipotovu cha shetani, katika asili hiyo ya kishetani ambamo wako katika uadui na Mungu, kumsaliti Mungu, na kutamanikuwa Mungu. Kufuatia Ushirika Wangu katika mada hii ya mamlaka ya Mungu, bado ungependa au ungetamani kujifanya wewe ni Mungu, au kumwiga Mungu? Je, bado unatamani kuwa Mungu? Ungali unapenda kuwa Mungu? Mamlaka ya Mungu hayawezi kuigwa na binadamu, na utambulisho na hadhi ya Mungu haiwezi kuigizwa na binadamu. Ingawa unaweza kuiga sauti ambayo Mungu huongea nayo, huwezi kuiga kiini cha Mungu. Ingawa unaweza kusimama katika nafasi ya Mungu na kujifanya kuwa Mungu, hutawahi kuweza kufanya kile ambacho Mungu ananuia kukifanya, na hutawahi kutawala na kuamuru vitu vyote. Katika macho ya Mungu, utabakia kuwa kiumbe kidogo, na haijalishi ni vipi ambavyo mbinu na uwezo wako ulivyo mkubwa, haijalishi ni vipaji vingapi unavyo, vitu vyote kuhusu wewe vipo chini ya utawala wa Muumba. Ingawa unaweza kusema baadhi ya maneno yenye ukali, hilo haliwezi kuonyesha kwamba una kiini cha Muumba, wala kuwakilisha ya kwamba unamiliki mamlaka ya Muumba. Mamlaka na nguvu za Mungu ni kiini cha Mungu Mwenyewe. Hayakufunzwa wala kusomwa, au kuongezewa kutoka nje, lakini ni kiini cha Mungu Mwenyewe. Na kwa hivyo uhusiano kati ya Muumba na viumbe vilivyoumbwa hauwezi kamwe kubadilishwa. Kama mmoja wa wanadamu walioumbwa, lazima ushikilie nafasi yako inayofaa, na ujiendeshe kwa adabu. Shikilia kwa uwajibikaji kile ulichokabidhiwa na Muumba. Usivuke mipaka, au kufanya mambo yaliyo nje ya upeo wa uwezo wako au ambayo yanamchukiza Mungu. Usifuatilie kuwa mtu mkuu, mtu mwenye uwezo upitao wa kibinadamu, au mtu adhimu sana, na usifuatilie kuwa Mungu. Yote haya ni matamanio ambayo watu hawapaswi kuwa nayo. Kufuatilia kuwa mtu mkuu au mtu mwenye uwezo upitao wa kibinadamu ni upuuzi. Kufuatilia kuwa Mungu ni jambo la aibu zaidi; ni jambo la kuchukiza, na la kudharauliwa. Kilicho cha thamani kweli, na kile ambacho viumbe walioumbwa wanapaswa kushikilia kuliko kitu kingine chochote, ni kuwa kiumbe aliyeumbwa wa kweli; hili ndilo lengo pekee ambalo watu wote wanapaswa kufuatilia.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 94)

Mamlaka ya Muumba Hayawekewi Mipaka ya Muda, Nafasi, au Jiografia, na Mamlaka ya Muumba Hayahesabiki

Hebu tuangalie Mwanzo 22:17-18. Hiki ni kifungu kingine kilichozungumziwa na Yehova Mungu, ambapo Alimwambia Ibrahimu, “Kuwa katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha uzao wako nitazidisha mithili ya nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa maadui zao; Na kupitia uzao wako kila taifa la dunia litabarikiwa; kwa kuwa umeitumikia sauti yangu.” Yehova Mungu alimbariki Ibrahimu mara nyingi ili uzao wake uweze kuzidishwa—na kuzidishwa hadi kiwango gani? Hadi kiwango kilichozungumziwa katika Maandiko: “kama nyota za mbinguni na mchanga ulio pwani.” Hii ni kusema kwamba Mungu alipenda kumpa Ibrahimu uzao uliokuwa mwingi kama nyota za mbinguni, na tele kama mchanga wa pwani. Mungu aliongea akitumia taswira, na kutoka kwenye taswira hii si vigumu kuona kwamba Mungu asingempa tu Ibrahimu uzao mmoja, wawili, au hata maelfu, lakini idadi isiyohesabika, kiasi kwamba wangekuwa uzao wa mataifa mengi ya dunia, kwani Mungu alimwahidi Ibrahimu kuwa atakuwa baba wa mataifa mengi. Na je, idadi hiyo iliamuliwa na binadamu au iliamuliwa na Mungu? Je, binadamu anaweza kudhibiti kiasi cha uzao atakaokuwa nao? Je, hilo ni juu yake? Si hata juu ya mwanadamu kama atakua na uzao kadhaa ama la, sembuse kuwa nao wengi kama “nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani.” Ni nani asiyetamani uzao wake kuwa mwingi kama nyota? Kwa bahati mbaya mambo huwa hayaendi namna unavyotaka. Licha ya vile mwanadamu anaweza kuwa na mbinu au kuweza kufanya jambo fulani, haitegemei binadamu; hakuna anayeweza kusimama nje ya kile ambacho kimeamriwa na Mungu. Kiasi ambacho Atakuruhusu, hicho ndicho utakachokuwa nacho: Kama Mungu atakupa kidogo, basi hutawahi kuwa na kingi, na kama Mungu Atakupa kingi haina faida wewe kuchukia kingi hicho ulichonacho. Je, hayo si kweli? Haya yote ni juu ya Mungu, si binadamu! Binadamu hutawaliwa na Mungu, na hakuna yule anayeachwa!

Wakati Mungu alisema “uzao wako nitazidisha,” hili lilikuwa agano ambalo Mungu alianzisha na Ibrahimu, sawa na agano la upinde wa mvua, lingeweza kutimizwa milele hata milele, na pia ilikuwa ahadi iliyotolewa na Mungu kwa Ibrahimu. Ni Mungu pekee ndiye mwenye sifa na uwezo wa kufanya ahadi hii itimie. Bila kujali kama binadamu anaisadiki au la, bila kujali kama binadamu aikubali au la, na bila kujali namna binadamu anavyoitazama, na namna anavyoichukulia, haya yote yatatimizwa kwa uhakika, kulingana na matamshi yaliyotamkwa na Mungu. Matamshi ya Mungu hayatabadilishwa kwa sababu ya mabadiliko katika mapenzi au dhana za binadamu, na hayatabadilishwa kwa sababu ya mabadiliko ndani ya mtu yeyote, kitu au kifaa. Vitu vyote vitaweza kutoweka lakini matamshi ya Mungu yatabaki milele hata milele. Kwa hakika, siku ambayo vitu vyote vitatoweka ndiyo siku hasa ambayo matamshi ya Mungu yataweza kutimizwa kabisa, kwani Yeye ndiye Muumba, na Anamiliki mamlaka ya Muumba, na nguvu za Muumba, na Anadhibiti vitu vyote na nguvu zote za maisha; na Anaweza kusababisha kitu kutoka kule kusikokuwa na kitu, au kufanya kitu kiwe si kitu, na Anadhibiti mabadiliko ya vitu vyote vilivyo na uhai na vile vilivyokufa, na kwa hivyo kwake Mungu, hakuna kinachokuwa rahisi zaidi kama kuzidisha uzao wa mtu. Haya yote yanaonekana ya kulifikiria tu akilini mwa binadamu, sawa na hadithi za uwongo, lakini kwa Mungu, kile Anachoamua kufanya, na kuahidi kufanya, si cha kulifikiria tu akilini wala si hadithi za uwongo. Badala yake ni uhalisia ambao Mungu tayari aliuona, na ambao kwa hakika utaweza kutimizwa. Je, unaelewa hili? Je, ukweli wa mambo unathibitisha kwamba wazao wa Abrahamu walikuwa wengi? Na je, walikuwa ni wengi kiasi gani? Je, walikuwa ni wengi kama “nyota za mbinguni, na kama mchanga uliokopwani” kama ilivyosemwa na Mungu? Je, waliweza kuenea kotekote katika mataifa na maeneo, kwenye kila sehemu ya ulimwengu? Na ni nini kilichotimiza ukweli huu? Je, iliweza kutimizwa kutokana na mamlaka ya matamshi ya Mungu? Kwa mamia au maelfu kadhaa ya miaka baada ya matamshi ya Mungu kutamkwa, matamshi ya Mungu yaliendelea kutimizwa, na siku zote yaliendelea kuwa halisi; huu ndio uwezo wa matamshi ya Mungu, na uthibitisho wa mamlaka ya Mungu. Wakati Mungu alipoumba vitu vyote hapo mwanzo, Mungu alisema na hebu kuwe na nuru, na kukawa na nuru. Tokeo hili lilifanyika haraka sana, lilitimizwa kwa muda mfupi sana, na hakukuwa na kuchelewa kokote kuhusu kukamilika na kutimizwa kwake; athari za matamshi ya Mungu zilitokea papo hapo. Vyote vilikuwa onyesho la mamlaka ya Mungu, lakini wakati Mungu alipombariki Ibrahimu, Alimruhusu binadamu kuuona upande mwingine wa kiini cha mamlaka ya Mungu, na Akamruhusu binadamu kuona mamlaka ya Muumba yasiyopimika, na zaidi ya hayo, Alimruhusu binadamu kuona upande halisi, bora zaidi wa mamlaka ya Muumba.

Punde tu matamshi ya Mungu yanapotamkwa, mamlaka ya Mungu yanachukua amri ya kazi hii, na ukweli ulioahidiwa kwa kinywa cha Mungu polepole unaanza kuwa halisi. Kama matokeo, mabadiliko yanaanza kuonekana kati ya vitu vyote, kama vile, wakati wa majira ya kuchipua, nyasi hubadilika kuwa kijani kibichi, maua huchanua, chipukizi huchipuka kutoka kwenye miti, ndege wanaanza kuimba, nao batabukini wanaanza kurejea, nayo mashamba yanaanza kujaa watu…. Majira ya kuchipua yanapowadia vitu yote vinahuishwa, na hili ndilo tendo la kimiujiza la Muumba. Mungu anapotimiza ahadi zake, vitu vyote mbinguni na duniani vinafanywa upya na kubadilika kulingana na fikira za Mungu—na hakuna kiumbe ambacho kinaachwa. Wakati patano au ahadi inapotamkwa kutoka katika kinywa cha Mungu, vitu vyote vinatimiza wajibu wao, na vinaongozwa kwa minajili ya kutimizwa kwao, na viumbe vyote vinaundwa na kupangiliwa chini ya utawala wa Mungu, na vinaendeleza wajibu wao maalum, na kutumikia jukumu lao husika. Haya ndiyo maonyesho ya mamlaka ya Muumba. Unaona nini katika mambo haya? Unajuaje mamlaka ya Mungu? Je, kuna kiwango cha mamlaka ya Mungu? Je, kuna ukomo wa wakati? Je, yanaweza kusemwa kuwa na kimo fulani, au urefu fulani? Je, yanaweza kusemwa kuwa na ukubwa fulani au nguvu fulani? Je, yanaweza kupimwa kwa vipimo vya kibinadamu? Mamlaka ya Mungu sio kitu kinachopepesa, hayaonekani na kutoweka ghafla, na hakuna mtu anayeweza kupima jinsi mamlaka Yake yalivyo makubwa. Haijalishi ni muda gani utakaopita, Mungu anapombariki mtu, baraka hizi zitaendelea kuwepo, na kuendelea kwake kutadhihirisha agano la mamlaka ya Mungu yasiyokadirika, na kutamruhusu mwanadamu kutazama kule kujitokeza upya kwa nguvu za uhai zisizozimika za Muumba, mara kwa mara. Kila onyesho la mamlaka Yake ni onyesho kamili la maneno kutoka kinywani Mwake, ambayo yanaonyeshwa katika vitu vyote, na kwa wanadamu. Zaidi ya hayo, kila kitu kinachokamilishwa kwa mamlaka Yake ni chenye ubora usio na kifani, na hakina dosari kabisa. Inaweza kusemwa kwamba fikira Zake, matamshi Yake, mamlaka Yake, na kazi zote Anazozikamilisha, zote ni picha nzuri isiyo na kifani, na kwa viumbe, lugha ya binadamu haiwezi kuelezea umuhimu na thamani yake. Mungu anapotoa ahadi kwa mtu, kila kitu kinachomhusu kinafahamika kwa Mungu kama tu sehemu ya nyuma ya mkono Wake mwenyewe, haijalishi kama ni kuhusiana na pale wanapoishi, au kile wanachofanya, asili yao kabla na baada ya kupata ahadi, au jinsi ambavyo mageuzi yamekuwa makubwa katika mazingira yao ya kuishi. Haijalishi ni muda gani umepita baada ya matamshi ya Mungu kutamkwa, kwake Yeye, ni kana kwamba ndio yametoka tu kutamkwa. Hivi ni kusema kwamba Mungu anazo nguvu, na Anayo mamlaka kama hayo, kiasi cha kwamba Anaweza kufuatilia, kudhibiti, na kutimiza kila ahadi Anayotoa kwa mwanadamu, haijalishi ahadi hiyo ni nini, haijalishi ni muda gani itachukua kutimizwa kikamilifu, na, zaidi, haijalishi upana wa sehemu ambazo kukamilika huko kunagusia—kwa mfano, muda, jiografia, kabila, na kadhalika—ahadi hii itakamilishwa, na kutimizwa, na, zaidi ya hayo, kukamilishwa kwake na kutimizwa kwake hakutahitaji jitihada Zake hata kidogo. Na haya yanathibitisha nini? Kwamba ukubwa wa mamlaka na nguvu za Mungu unatosha kuudhibiti ulimwengu mzima, na wanadamu wote. Mungu aliumba nuru, lakini hiyo haimaanishi kuwa Mungu anasimamia tu nuru, kwamba Yeye anasimamia maji tu kwa sababu Aliyaumba maji, na kwamba kila kitu kingine hakina uhusiano na Mungu. Je, hii siyo suitafahamu? Ingawa baraka za Mungu kwa Ibrahimu zilikuwa zimepotea polepole kutoka kwenye kumbukumbu ya binadamu baada ya miaka mia kadhaa, kwake Mungu, ahadi hii ilibaki vilevile. Ilikuwa kwenye mchakato wa kukamilishwa, na haikuwahi kusitishwa. Binadamu hakuwahi kujua au kusikia namna ambavyo Mungu alitumia mamlaka Yake, jinsi ambavyo vitu vyote vilipangwa na kupangiliwa, na ni hadithi ngapi za ajabu zilifanyika miongoni mwa vitu vyote vya uumbaji wa Mungu kwenye kipindi hiki cha muda, lakini kila sehemu ya ajabu ya onyesho la mamlaka ya Mungu na ufunuo wa matendo Yake vilipitishwa na kuinuliwa kati ya vitu vyote, vitu vyote vilijitokeza na kuzungumza juu ya matendo ya kimiujiza ya Muumba, na kila hadithi iliyosimuliwa sana kuhusu ukuu wa Muumba juu ya vitu vyote itatangazwa na vitu vyote milele yote. Mamlaka ambayo kwayo Mungu anatawala vitu vyote, na nguvu za Mungu, zinaonyesha vitu vyote kwamba Mungu yuko kila mahali na wakati wote. Wakati utakapokua umeshuhudia kuenea kwamamlaka na nguvu za Mungu, utaona kwamba Mungu anapatikana kila mahali na nyakati zote. Mamlaka na nguvu za Mungu haviwekewi mipaka ya muda, jiografia, nafasi, au mtu yeyote, jambo au kitu. Upana wa mamlaka na nguvu za Mungu unazidi mawazo ya binadamu; haufikiriki kwa binadamu, hauwaziki kwa binadamu, na hautawahi kujulikana na binadamu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 95)

Mamlaka ya Muumba Hayawekewi Mipaka ya Muda, Nafasi, au Jiografia, na Mamlaka ya Muumba Hayahesabiki

Baadhi ya watu wanapenda kukisia na kufikiria, lakini fikira za mwanadamu zinaweza kwenda umbali gani? Je, zinaweza kwenda zaidi ya ulimwengu huu? Je, mwanadamu ana uwezo wa kukisia na kufikiria uhalisi na usahihi wa mamlaka ya Mungu? Je, makisio na mawazo ya mwanadamu yana uwezo wa kumruhusu kupata ujuzi wa mamlaka ya Mungu? Je, yanaweza kumfanya mwanadamu afahamu na kunyenyekea kwa kweli mbele ya mamlaka ya Mungu? Ukweli unathibitisha kwamba makisio na mawazo ya mwanadamu ni zao tu la akili ya mwanadamu, na haitoi msaada au manufaa hata kidogo kwa maarifa ya mwanadamu kuhusu mamlaka ya Mungu. Baada ya kusoma makala za kidhahania za kisayansi, baadhi wanaweza kufikiria mwezi, na vile nyota zilivyo. Ilhali hii haimanishi kwamba binadamu anao ufahamu wowote wa mamlaka ya Mungu. Kufikiria kwa binadamu ni hivyo tu: ni kufikiria. Kuhusiana na ukweli wa mambo haya, hivi ni kusema kwamba, kuhusiana muunganiko wao kwa mamlaka ya Mungu, hana ung’amuzi wowote. Na je, inamaanisha nini hata kiwa umeenda hadi kwenye mwezi? Je, hii inaonyesha kuwa una ufahamu wa vipengele vingi kuhusu mamlaka ya Mungu? Je, hii, inaonyesha kwamba wewe unaweza kufikiria upana wa mamlaka na nguvu za Mungu? Kwa sababu makisio na fikira za mwanadamu hazina uwezo wa kumruhusu kuyatambua mamlaka ya Mungu, je, mwanadamu anapaswa kufanya nini? Uchaguzi wenye busara zaidi ungepaswa kuwa kutokukisia au kufikiria, hivi ni kusema kwamba, ni lazima mwanadamu asitegemee kamwe fikira na asitegemee kamwe makisio inapokuja katika suala lakujua mamlaka ya Mungu. Ni nini ambacho Ningependa kukwambia hapa? Maarifa ya mamlaka ya Mungu, nguvu za Mungu, utambulisho wa Mungu mwenyewe, na kiini cha Mungu hayawezi kupatikana kwa kutegemea fikira zako. Kwa kuwa huwezi kutegemea fikira ili kutambua mamlaka ya Mungu, basi ni kwa njia gani unaweza kupata maarifa ya kweli ya mamlaka ya Mungu? Kwa kula na kunywa maneno ya Mungu, kupitia ushirika, na kupitia kwa uzoefu wa maneno ya Mungu, utaweza kuwa na uzoefu na uthibitisho wa mamlaka ya Mungu hatua kwa hatua, na hivyo basi utapata kuelewa kwa utaratibu na kuongeza maarifa kuyahusu. Hii ndiyo njia pekee ya kupata maarifa ya mamlaka ya Mungu; hakuna njia za mkato. Kukuambia kwamba usifikirie sio sawa na kukufanya ukae kimya ukisubiria uharibifu, au kukuzuia usifanye lolote. Kutotumia ubongo wako kuwaza na kufikiria kunamaanisha kutotumia mantiki kukisia, kutotumia maarifa kuchanganua, kutotumia sayansi kama msingi, lakini badala yake kufahamu, kuhakikisha, na kuthibitisha kuwa Mungu unayemsadiki anayo mamlaka, kuthibitisha kwamba Yeye anashikilia ukuu juu ya hatima yako, na kwamba nguvu Zake nyakati zote zinathibitisha kuwa Yeye ndiye Mungu Mwenyewe wa kweli, kupitia kwa matamshi ya Mungu, kupitia ukweli, kupitia kwa kila kitu unachokabiliana nacho maishani. Hii ndiyo njia pekee ambayo mtu yeyote anaweza kutimiza ufahamu wa Mungu. Baadhi ya watu husema kwamba wangependa kupata njia rahisi ya kutimiza lengo hili, lakini, je, unaweza kufikiria kuhusu njia kama hiyo? Ninakwambia, hakuna haja ya kufikiria: Hakuna njia nyingine! Njia ya pekee ni kujua na kuthibitisha kwa uangalifu na kwa uthabiti kile ambacho Mungu anacho na alicho kupitia kwa kila neno Analonena na kwa kila kitu Anachofanya. Hii ndiyo njia ya pekee ya kumjua Mungu. Kwani kile ambacho Mungu anacho na alicho, na kila kitu cha Mungu, si kitu kisicho na maana na tupu, bali ni halisi.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 96)

Ukweli wa Udhibiti na Utawala wa MuumbaJuu ya Vitu Vyote na Viumbe Vilivyo Hai Unazungumzia Uwepo wa Kweli wa Mamlaka ya Muumba

Baraka za Yehova kwa Ayubu zimerekodiwa katika Kitabu cha Ayubu. Ni nini ambacho Mungu alimpa Ayubu? “Kwa hivyo Yehova akabariki mwisho wa baadaye wa Ayubu zaidi kuliko mwanzo wake: kwa sababu alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na elfu moja ya jozi za ng’ombe, na elfu moja ya punda wa kike” (Ayubu 42:12). Kwa mtazamo wa kibinadamu, ni vitu gani ambavyo Ayubu alipewa? Je, zilikuwa ni mali za kibinadamu? Akiwa na mali hizi, je, Ayubu angeweza kuwa tajiri sana kwa kipindi hicho? Na je, aliwezaje kupata mali kama hizo? Ni nini kilichosababisha utajiri wake? Bila shaka—ilikuwa ni shukrani kwa baraka ya Mungu kwamba Ayubu alikuja kuzimiliki. Jinsi ambavyo Ayubu alizitazama mali hizi, na jinsi alivyozichukulia baraka za Mungu, si jambo ambalo tutalizungumzia hapa. Inapokuja katika baraka za Mungu watu wote hutamani, mchana na usiku, kubarikiwa na Mungu, ilhali binadamu hana udhibiti wowote kuhusiana na kiasi cha mali anachoweza kupata katika maisha yake yote, au kama anaweza kupokea baraka kutoka kwa Mungu—huu ni ukweli usiopingika! Mungu ana mamlaka, na Anazo nguvu za kumpatia mwanadamu mali zozote zile, kumruhusu binadamu kupata tamko lolote la baraka, ilhali kuna kanuni kwa baraka za Mungu. Je, ni watu wa aina gani ambao Mungu anawabariki? Ni wale watu Anaowapenda, bila shaka! Ibrahimu na Ayubu wote walibarikiwa na Mungu, ilhali baraka walizopokea hazikuwa sawa. Mungu alimbariki Ibrahimu kwa vizazi vingi kama mchanga na nyota. Mungu alipombariki Ibrahimu, Alisababisha vizazi vya mtu mmoja, taifa moja, kuwa na nguvu na ufanisi. Katika haya mamlaka ya Mungu yalimtawala mwanadamu, ambaye alipumua pumzi ya Mungu kati ya vitu vyote na viumbe vyote vyenye uhai. Chini ya ukuu wa mamlaka ya Mungu, mwanadamu huyu aliongezeka na kuwepo kwa kasi iliyoamuliwa na Mungu, na ndani ya upeo ulioamuliwa na Mungu. Kwa hakika, uwezo wa taifa hili, kasi ya upanuzi, na muda wa kuishi vyote vilikuwa sehemu ya mipangilio ya Mungu, na kanuni ya haya yote ilitegemea kabisa ahadi ambayo Mungu alimpa Ibrahimu. Hivi ni kusema kwamba, licha ya hali zozote zile, ahadi za Mungu zingeendelea bila kizuizi na zingetekelezwa chini ya usimamizi wa mamlaka ya Mungu. Katika ahadi ambayo Mungu alimpa Ibrahimu, bila kujali mageuzi ya ulimwengu, bila kujali enzi, bila kujali maafa ambayo wanadamu wamevumilia, wazao wa Ibrahamu hawangekabiliwa na hatari ya kuangamizwa, na taifa lao lisingeweza kutokomea. Baraka ya Mungu kwa Ayubu, hata hivyo, ilimfanya awe tajiri sana. Kile alichopewa na Mungu kilikuwa ni makundi ya viumbe hai, vinavyopumua, ambavyo taarifa zao kuhusu—idadi yao, kasi yao ya kuzaliana, muda wao wa kuishi, ikiwa ni wanene na wenye nguvu, na kadhalika—vyote vilikuwa chini ya udhibiti wa Mungu. Ingawa viumbe hawa hawakuwa na uwezo wa kuzungumza, wao pia walikuwa sehemu ya mipangilio ya Muumba, na kanuni za mipangilio ya Mungu zilikuwa kulingana na baraka ambayo Mungu aliahidi kwa Ayubu. Katika baraka ambazo Mungu aliwapa Ibrahimu na Ayubu, ingawa kile kilichoahidiwa kilikuwa tofauti, mamlaka ambayo Muumba alitawala vitu vyote na viumbe hai yalikuwa sawa. Kila maelezo ya mamlaka na uwezo wa Mungu unaonyeshwa katika ahadi na baraka Zake tofauti kwa Ibrahimu na Ayubu, na yanawaonyesha wanadamu, kwa mara nyingine tena kwamba, mamlaka ya Mungu ni zaidi ya mawazo ya mwanadamu. Maelezo haya yanawaambia wanadamu kwa mara nyingine tena kwamba, ikiwa wanataka kuyajua mamlaka ya Mungu, basi hili linaweza tu kufikiwa kupitia kwa maneno ya Mungu na kwa kuweza kupitia kazi ya Mungu.

Mamlaka ya Mungu ya ukuu juu ya vitu vyote yanamruhusu mwanadamu kuona ukweli kwamba: Mamlaka ya Mungu hayapo tu katika maneno “Mungu akasema, Iwe nuru, ikawa nuru, na, Kuwe na anga, na kukawa na anga, na, Kuwe na nchi, na kukawa na nchi,” lakini, zaidi ya hayo, mamlaka Yake pia yamejumuishwa katika jinsi Alivyoifanya nuru ile iendelee kuwepo, Alivyoizuia anga dhidi ya kutoweka na Akaiweka ardhi milele ikiwa kando na maji, na vilevile katika maelezo ya jinsi Alivyotawala na kuvisimamia vitu Alivyoviumba: nuru, anga, na ardhi. Je, ni nini kingine unachoona katika baraka za Mungu kwa wanadamu? Kwa uwazi, baada ya Mungu kuwabariki Ibrahimu na Ayubu, nyayo za Mungu hazikukoma, kwani Alikuwa tu ameanza kuyatumia mamlaka Yake, na Alinuia kufanya kila moja ya maneno Yake kuwa halisi, na kufanya kila moja ya maelezo Aliyozungumza kuwa kweli, na kwa hivyo kwenye miaka iliyofuata, Aliendelea kufanya kila kitu Alichonuia. Kwa sababu Mungu ana mamlaka, pengine inaonekana kwa binadamu kwamba Mungu huongea tu, na Hahitaji kuinua hata kidole chake ili mambo yote na vitu vyote viweze kutimizwa. Mawazo kama haya ni ya kipuuzi kabisa! Kama utachukua tu mtazamo wa upande mmoja wa Mungu kuanzisha agano na binadamu kwa kutumia maneno, na ukamilishaji wa kila kitu wa Mungu kwa kutumia maneno, na huwezi kuona ishara na ukweli tofautitofauti kwamba mamlaka ya Mungu yanashikilia utawala juu ya uwepo wa vitu vyote, basi ufahamu wako kuhusu mamlaka ya Mungu ni mtupu na wa kipuuzi! Ikiwa mwanadamu anamfikiria Mungu kuwa hivyo, basi, ni, lazima isemwe, maarifa ya binadamu kuhusu Mungu yameendeshwa hadi kwenye shimo la mwisho, na sasa yamefika mwisho wenyewe, kwani Yule Mungu ambaye binadamu anamfikiria kuwa ni kama mashine tu ya kutoa amri, na si Mungu anayemiliki mamlaka. Je, umeona nini kupitia kwenye mifano ya Ibrahimu na Ayubu? Je, umeuona upande wa kivitendo wa mamlaka na nguvu za Mungu? Baada ya Mungu kuwabariki Ibrahimu na Ayubu, Mungu hakubakia mahali Alipokuwa, wala Hakuwaweka wajumbe Wake kazini huku Akisubiri kuona matokeo yake yatakuwa yapi. Kinyume cha mambo ni kuwa, mara tu Mungu alipotamka maneno Yake, chini ya uongozi wa mamlaka ya Mungu, vitu vyote vilianza kuendana na kazi ambayo Mungu alinuia kufanya, na kulikuwepo na watu waliokuwa wamejitayarisha, vitu, na vifaa ambavyo Mungu alihitaji. Hivi ni kusema kwamba, punde tu maneno hayo yalipotamkwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu, mamlaka ya Mungu yalianza kutekelezwa katika nchi nzima, na Aliweka njia ya kuweza kukamilisha na kutimiza ahadi Alizotoa kwa Ibrahimu na Ayubu, huku Akifanya pia mipango na matayarisho yote kuhusiana na kila kitu kilichohitajika kwa kila awamu Aliyopanga kutekeleza. Kwa wakati huu, Mungu hakuwadhibiti tu wajumbe Wake, bali pia vitu vyote vilivyokuwa vimeumbwa na Yeye. Hivi ni kusema kwamba, upeo ambao mamlaka ya Mungu yalitekelezwa haukujumuisha wajumbe tu, bali, vitu vyote katika uumbaji, ambavyo viliongozwa ili kuendana na kazi Aliyokusudia kuikamilisha; hizi ndizo tabia mahususi ambazo mamlaka ya Mungu yalitekelezwa. Katika mawazo yenu, wengine wanaweza kuwa na ufahamu ufuatao wa mamlaka ya Mungu: Mungu ana mamlaka, na Mungu ana nguvu, na hivyo Mungu anahitaji tu kubaki katika mbingu ya tatu, au sehemu moja tu, na hahitaji kufanya kazi yoyote mahususi, na ukamilifu wa kazi ya Mungu unakamilishwa katika fikira Zake. Baadhi wanaweza kusadiki kuwa, Ingawa Mungu alimbariki Ibrahimu, Mungu hakuhitaji kufanya lolote, na ilitosha Kwake tu kutamka maneno Yake. Je, hivi ndivyo ilivyofanyika kweli? Bila shaka, sivyo! Ingawa Mungu anamiliki mamlaka na nguvu, mamlaka Yake ni ya kweli na halisi, si matupu. Uhalisi na ukweli wa mamlaka na nguvu za Mungu hufichuliwa na kuonyeshwa hatua kwa hatua katika uumbaji Wake wa vitu vyote, katika udhibiti Wake juu ya vitu vyote, na katika mchakato ambao Yeye anawaongoza na kuwasimamia wanadamu. Kila mbinu, kila mtazamo na kila maelezo ya ukuu wa Mungu juu ya wanadamu na vitu vyote, na kazi yote ambayo Amekamilisha, vilevile ufahamu Wake kuhusu vitu vyote—yote yanathibitisha kwa kweli kwamba mamlaka na nguvu za Mungu si maneno matupu. Mamlaka na nguvu Zake vyote vinaonyeshwa na kufichuliwa kila mara, na katika mambo yote. Maonyesho haya na ufunuo vyote vinazungumzia uwepo halisi wa mamlaka ya Mungu, kwani Yeye ndiye anayetumia mamlaka na nguvu Zake kuendeleza kazi Yake, na kuamuru vitu vyote, na kutawala vitu vyote kila wakati, na nguvu na mamlaka Yake, vyote haviwezi kubadilishwa na malaika, au wajumbe wa Mungu. Mungu aliamua ni baraka gani Angewapa Ibrahimu na Ayubu—ilikuwa ni uamuzi wa Mungu kuufanya. Ingawa wajumbe wa Mungu waliwatembelea Ibrahimu na Ayubu wao binafsi, matendo yao yalikuwa kulingana na amri za Mungu, na kulingana na mamlaka ya Mungu, na pia walikuwa wakifuata ukuu wa Mungu. Ingawa binadamu anawaona wajumbe wa Mungu wakimtembelea Ibrahimu, na hamshuhudii Yehova Mungu binafsi akifanya chochote katika rekodi za Biblia, kwa hakika, Yule pekee ambaye kwa kweli anatumia nguvu na mamlaka ni Mungu Mwenyewe, na hili haliwezi kutiliwa shaka na binadamu yeyote! Ingawa umewaona malaika na wajumbe wakimiliki nguvu nyingi, na wametenda miujiza, au wamefanya baadhi ya mambo yaliyoagizwa na Mungu, vitendo vyao ni kwa minajili tu ya kukamilisha agizo la Mungu, na wala si tu kuonyesha mamlaka ya Mungu—kwani hakuna binadamu au kitu kimoja kilicho, au kinachomiliki, mamlaka ya Muumba ya kuumba vitu vyote na kutawala vitu vyote. Na kwa hivyo hakuna binadamu au kitu chochote kinachoweza kutumia au kuonyesha mamlaka ya Muumba.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 97)

Mamlaka ya Muumba Hayabadiliki na Hayawezi Kukosewa

1. Mungu Hutumia Maneno Kuumba Vitu Vyote

Mwa 1:3-5 Na Mungu akasema, Na kuwe na mwanga; kukawa na mwanga. Mungu akauona mwanga, na kuwa ulikuwa mzuri: na Mungu akautenga mwanga na kiza. Naye Mungu akauita mwanga Mchana, na kiza akaliita Usiku. Na jioni na asubuhi yalikuwa siku ya kwanza.

Mwa 1:6-7 Na Mungu alisema, Na kuwe na mbingu katikati ya maji, na uigawanye maji kutoka kwa maji. Na Mungu akaitengeneza mbingu, na akayagawanya yale maji yaliyokuwa chini ya mbingu kutoka kwa yale maji yaliyokuwa juu ya mbingu: na kukawa vivyo hivyo.

Mwa 1:9-11 Naye Mungu akasema, Nayo maji yaliyo chini ya mbingu yakonge pahali pamoja, na ardhi kavu ionekane; na kukawa vivyo hivyo. Naye Mungu akaiita nchi kavu Dunia: na kukonga kwa maji akakuita Bahari: naye Mungu akaona kwamba ni vyema. Naye Mungu akasema, Na dunia izae majani, mche ambao unatoa mbegu, na mti wa matunda ambao unazaa tunda kwa aina yake, ambao mbegu zake ziko ndani yake, juu ya dunia: na kukawa vivyo hivyo.

Mwa 1:14-15 Naye Mungu akasema, Kuwe na mwangaza katika anga la mbingu kwa minajili ya kutenga mchana na usiku; na uwe ndio ishara; na majira, na siku na miaka: Na tena uwe ndio mwangaza katika anga la mbingu kwa minajili ya kupa nchi nuru; na ikawa vile.

Mwa 1:20-21 Na Mungu akasema, Na maji yalete kwa wingi kiumbe asongaye aliye na uhai, na ndege wanaoweza kuruka juu ya nchi katika anga wazi la mbingu. Naye Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na viumbe wote walio na uhai wasongao, ambao maji yalileta kwa wingi, kwa aina yao, na kila ndege anayeruka kwa aina yake: na Mungu akaona kuwa ilikuwa vizuri.

Mwa 1:24-25 Naye Mungu akasema, Dunia na ilete kiumbe kilicho hai kwa namna yake, mifugo, na kitu kinachotambaa, na wanyama wa mwituni kwa namna yake: na ikafanyika. Naye Mungu akaumba wanyawa wa mwituni kwa namna yake, na mifugo kwa namna yake, na chote kinachotambaa duniani kwa namna yake: na Mungu akaona kwamba ni vizuri.

2. Mungu Hutumia Matamshi Yake Kuanzisha Agano na Binadamu

Mwa 9:11-13 Na nitaweka agano langu na ninyi, wala miili yote haitaondolewa tena na maji ya gharika; wala hakutakuwa na gharika tena kuiharibu dunia. Naye Mungu akasema, Hii ni alama ya agano ambayo naifanya kati ya Mimi na ninyi na viumbe vyote vyenye uhai vilivyo nanyi, kwa vizazi vya kudumu: naweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa alama ya agano kati ya Mimi na dunia.

3. Baraka za Mungu

Mwa 17:4-6 Na kuhusu mimi, tazama, agano langu liko na wewe, na wewe utakuwa baba yao mataifa mengi. Nalo jina lako halitakuwa Abramu tena, ila jina lako litaitwa Ibrahimu; kwa kuwa nimekufanya uwe baba yao mataifa mengi. Na Mimi nitafanya uwe na uzao ulio mwingi mno, na nitayaunda mataifa kutoka kwako, nao wafalme watatoka kwako.

Mwa 18:18-19 Ibrahimu hakika atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa ndani yake. Kwani namjua, kuwa atawatawala watoto wake na nyumba yake kufuata yeye, na wataishika njia ya Yehova, kufanya haki na hukumu; ili Yehova aweze kumletea Ibrahimu yale ambayo amemwambia.

Mwa 22:16-18 Mimi nimeapa kwa nafsi yangu, akasema Yehova, kwa maana umefanya jambo hili, na hujamzuilia mwana wako, mwana wako wa pekee: Kuwa katika kubariki nitakupa baraka, na katika kuzidisha uzao wako nitazidisha mithili ya nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utakuwa na mlango wa maadui zao; Na kupitia uzao wako kila taifa la dunia litabarikiwa; kwa kuwa umeitumikia sauti yangu.

Ayu 42:12 Kwa hivyo Yehova akabariki mwisho wa Ayubu zaidi kuliko mwanzo wake: kwa sababu alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na elfu moja ya jozi za ng’ombe, na elfu moja ya punda wa kike.

Ni nini umeona katika vipengele hivi vitatu maandiko? Je, umeona kuwa kuna kanuni ambayo Mungu hutumia mamlaka Yake? Kwa mfano, Mungu aliutumia upinde wa mvua kuanzisha agano na binadamu, ambapo Aliuweka upinde wa mvua katika mawingu ili kumwambia binadamu kuwa Yeye Hatawahi tena kutumia gharika kuangamiza ulimwengu. Je, upinde wa mvua tunaouona leo, bado ndio uleule uliozungumziwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu? Je, asili na maana yake vimebadilika? Bila shaka, havijabadilika. Mungu alitumia mamlaka Yake ili kutekeleza kitendo hiki, na agano Aliloanzisha na binadamu limeendelea hadi leo, na muda ambao agano hili litabadilishwa, bila shaka, ni uamuzi wa Mungu. Baada ya Mungu kutamka “Nauweka upinde wangu wa mvua mawinguni,” siku zote Mungu alifuata agano hili, Alilifuata hadi leo. Unaona nini katika haya? Ingawa Mungu anamiliki mamlaka na nguvu, Ana msimamo sana na Anafuata kanuni katika vitendo Vyake, na Anashikilia maneno Yake. Msimamo Wake na kanuni za vitendo Vyake, vinaonyesha namna Muumba asivyoweza kukosewa na kutoweza kushindwa kwa mamlaka ya Muumba. Ingawa Anamiliki mamlaka ya juu, na kila kitu kinatawaliwa na Yeye, na japokuwa Anazo nguvu za kutawala vitu vyote, Mungu hajawahi kuharibu mpango Wake au kutatiza mpangilio Wake mwenyewe, na kila wakati Anapotumia mamlaka Yake, ni kulingana na umakinifu unaohitajika kwenye kanuni Zake mwenyewe na hasa kwa kufuata kile kilichotamkwa kutoka kwenye kinywa Chake, na kufuata hatua na majukumu ya mpango Wake. Bilas haka, kila kitu kinachotawaliwa na Mungu pia kinatii kanuni ambazo mamlaka ya Mungu yanatumika, na hakuna mwanadamu au kitu kisichojumuishwa kwenye mipangilio ya mamlaka Yake, wala hakuna anayeweza kubadilisha kanuni ambazo mamlaka Yake yanatumika. Machoni pa Mungu, wale wanaobarikiwa hupokea utajiri mzuri unaoletwa na mamlaka Yake, na wale wanaolaaniwa hupokea adhabu yao kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Chini ya ukuu wa mamlaka ya Mungu, hakuna binadamu au kitu ambacho hakijumuishwi katika utumiaji wa mamlaka Yake, wala hakuna kinachoweza kubadilisha kanuni hizi ambazo mamlaka Yake yanatekelezwa. Mamlaka ya Muumba hayabadilishwi kwa mabadiliko ya aina yoyote ile, na, vilevile, kanuni ambazo mamlaka Yake yanatumiwa hazibadiliki kwa sababu yoyote ile. Mbingu na ardhi vyote vinaweza kupitia misukosuko mingi, lakini mamlaka ya Muumba hayatabadilika; vitu vyote vitatoweka, lakini mamlaka ya Muumba hayatawahi kutoweka. Hiki ndicho kiini cha mamlaka ya Muumba ambayo hayabadiliki na yasiyokosewa kukosewa, na huu ndio upekee wenyewe wa Muumba!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 98)

Amri ya Mungu kwa Shetani

Ayubu 2:6 Na Yehova akamwambia kwa Shetani, Tazama, yeye yuko katika mkono wako; lakini uuhifadhi uhai wake.

Shetani Hajawahi Kuthubutu Kukiuka Mamlaka ya Muumba, na Kwa Sababu Hiyo, Vitu Vyote Vinaishi kwa Mpangilio

Hili ni dondoo kutoka katika Kitabu cha Ayubu, na “yeye” katika maneno haya inamrejelea Ayubu. Ingawa imeandikwa kwa muhtasari, sentensi hii inaelezea masuala mengi. Inafafanua mabadilishano fulani kati ya Mungu na Shetani kwenye ulimwengu wa kiroho, na inatwambia kuwa mlengwa wa maneno ya Mungu alikuwa ni Shetani. Pia inarekodi kile kilichosemwa hasa na Mungu. Maneno ya Mungu yalikuwa amri na shurutisho kwa Shetani. Maelezo mahususi ya shurutisho hili ni kuhusiana na kuuhifadhi uhai wa Ayubu na pale ambapo Mungu aliweka masharti ya jinsi ambavyo Shetani alipaswa kumtendea Ayubu—Shetani alilazimika kuuhifadhi uhai wa Ayubu. Kitu cha kwanza tunachojifunza kutoka kwenye sentensi hii ni kwamba matamshi haya yalitamkwa na Mungu kwa Shetani. Kulingana na maandiko halisi ya Kitabu cha Ayubu, yanatwambia usuli wa matamshi kama hayo: Shetani alitaka kumshutumu Ayubu, na hivyo lazima angepokea huo mkataba wa Mungu kabla hajamtia majaribuni. Alipokubali ombi la Shetani la kumjaribu Ayubu, Mungu aliweza kumtajia Shetani sharti lifuatalo: “Ayubu yuko mkononi mwako; lakini uuhifadhi uhai wake.” Ni nini asili ya maneno haya? Ni wazi kwamba ni amri, ni shurutisho. Baada ya kuelewa asili ya maneno haya, unafaa, bila shaka, kufahamu pia kwamba Aliyetoa shurutisho hili ni Mungu, na kwamba aliyepokea amri hii, na akaitii, ni Shetani. Bilas haka, katika shurutisho hili, uhusiano kati ya Mungu na Shetani uko wazi kwa yeyote ambaye anasoma maneno haya. Bila shaka, huu ndio uhusiano kati ya Mungu na Shetani katika ulimwengu wa kiroho, na tofauti kati ya utambulisho na hadhi ya Mungu na Shetani iliyoelezwa katika rekodi za mabadilishano ya mazungumzo ya Mungu na Shetani katika Maandiko, na, hadi leo, ni mfano mahususi na rekodi ya maandishi ambapo binadamu anaweza kujifunza tofauti kuu kati ya utambulisho na hadhi ya Mungu na Shetani. Katika hatua hii, ni lazima Niseme kwamba, rekodi ya maneno haya ni waraka muhimu sana katika ufahamu wa binadamu juu ya hadhi na utambulisho wa Mungu, na inatoa taarifa muhimu kwa maarifa ya mwanadamu kuhusu Mungu. Kupitia mabadilishano haya ya Mungu na Shetani katika ulimwengu wa kiroho, mwanadamu anaweza kuelewa kipengele kimoja mahususi zaidi katika mamlaka ya Muumba. Maneno haya ni ushuhuda mwingine wa kuonyesha mamlaka ya kipekee ya Muumba.

Kwa nje, Yehova Mungu yuko katika mazungumzo na Shetani. Kwa kuzingatia kiini, mtazamo ambao Yehova Mungu anaongea, na nafasi ambayo Anasimama ni ya juu zaidi kuliko ya Shetani. Hivi ni kusema kwamba Yehova Mungu anamwamuru Shetani na sauti ya kushurutisha, na Anamwambia Shetani ni nini anachopaswa kufanya na asichopaswa kufanya, kwamba tayari Ayubu yu mikononi mwake, na yuko huru kumfanya Ayubu vyovyote atakavyo—lakini asiuchukue uhai wa Ayubu. Ujumbe hapa ni kwamba, ingawa Ayubu amewekwa katika mikono ya Shetani, uhai wake haujakabidhiwa kwa Shetani; hakuna anayeweza kuuchukua uhai wa Ayubu kutoka mikononi mwa Mungu isipokuwa ameruhusiwa na Mungu. Mtazamo wa Mungu unaelezwa waziwazi katika amri hii kwa Shetani, na amri hii pia inadhihirisha na kufichua nafasi ambayo Yehova Mungu anazungumza na Shetani. Katika haya, Yehova Mungu hashikilii tu hadhi ya Mungu aliyeumba nuru, na hewa, na vitu vyote na viumbe hai, au ya Mungu anayeshikilia ukuu juu ya vitu vyote na viumbe hai, lakini pia ya Mungu ambaye Anawaamuru wanadamu, na kuamuru Jehanamu, Mungu ambaye anadhibiti uhai na kifo cha viumbe vyote vilivyo hai. Katika ulimwengu wa kiroho, ni nani mbali na Mungu ambaye angethubutu kutoa shurutisho kama hilo kwa Shetani? Na ni kwa nini Mungu Mwenyewe Alitoa agizo Lake kwa Shetani? Kwa sababu uhai wa binadamu, pamoja na ule wa Ayubu, unadhibitiwa na Mungu. Mungu hakumruhusu Shetani adhuru au achukue uhai wa Ayubu, hivyo ni kusema kwamba kabla ya Mungu kumruhusu Shetani kumjaribu Ayubu, Mungu bado alikumbuka kutoa shurutisho maalum kama hilo, na kwa mara nyingine Akamwamuru Shetani asiuchukue uhai wa Ayubu. Shetani hajawahi kuthubutu kukiuka mamlaka ya Mungu, na, vilevile, amesikiliza kwa umakinifu siku zote na kutii shurutisho na amri mahususi za Mungu, asiwahi thubutu kuzivunja, na, bila shaka asithubutu kubadilisha kwa hiari shurutisho zozote za Mungu. Hiyo ndiyo mipaka ambayo Mungu amemwekea Shetani, na hivyo Shetani hajawahi kuthubutu kuvuka mipaka hiyo. Je, huu si uwezo wa mamlaka ya Mungu? Je, huu si ushuhuda wa mamlaka ya Mungu? Shetani ana ufahamu wa wazi zaidi kuliko wanadamu kuhusu jinsi ya kuenenda mbele za Mungu, na jinsi ya kumtazama Mungu, hivyo, katika ulimwengu wa kiroho, Shetani anaona hadhi na mamlaka ya Mungu vizuri sana, na anatambua sana ule uwezo wa mamlaka ya Mungu na kanuni zinazoongoza utekelezaji wa mamlaka Yake. Hathubutu, kamwe, kutozitilia maanani kanuni hizo, wala hathubutu kukiuka kanuni hizo kwa vyovyote vile, au kufanya chochote ambacho kinakiuka mamlaka ya Mungu, na hathubutu kukabiliana na hasira ya Mungu kwa njia yoyote ile. Ingawa ni mwovu na mwenye kiburi kiasili, Shetani hajawahi kuthubutu kuvuka mipaka na viwango alivyowekewa na Mungu. Kwa mamilioni ya miaka, ametii kwa umakinifu mipaka hii, ametii kila amri na shurutisho lililotolewa na Mungu na hajawahi kuthubutu kuvuka alama hiyo. Ingawa ni mwovu, Shetani ni “mwerevu” zaidi kuliko mwanadamu aliyepotoka; anajua utambulisho wa Muumba, na anajua mipaka yake. Kutokana na vitendo vya Shetani vya kunyenyekea tunaweza kuona kwamba mamlaka na nguvu za Mungu ni maagizo ya mbinguni ambayo hayawezi kukiukwa na Shetani, na kwamba ni kwa sababu hasa ya upekee na mamlaka ya Mungu ndio maana vitu vyote vinabadilika na kuzaliana katika njia ya mpangilio, kwamba wanadamu wanaweza kuishi na kuongezeka ndani ya mkondo uliowekwa na Mungu, hakuna mtu au kitu chochote kinachoweza kuvuruga mpangilio huu, na hakuna mtu au kitu chochote kinachoweza kubadilisha sheria hii—kwani vyote vinatoka kwenye mikono ya Muumba na kwenye mpangilio na mamlaka ya Muumba.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 99)

Ni Mungu Pekee, Aliye na Utambulisho wa Muumba, Anayemiliki Mamlaka ya Kipekee

Ule utambulisho maalum wa Shetani umewafanya watu wengi waonyeshe kupendezwa sana na udhihirisho wake wa vipengele mbalimbali. Kuna hata watu wengi wapumbavu wanaoamini kwamba, kama vile Mungu, Shetani anamiliki mamlaka, kwani Shetani anaweza kuonyesha miujiza, na anaweza kufanya mambo ambayo mwanadamu hawezi kufanya. Kwa hivyo, mbali na kumwabudu Mungu, mwanadamu pia anahifadhi nafasi kwa Shetani moyoni mwake, na hata anamwabudu Shetani kama Mungu. Watu wote hawa ni wa kusikitikiwa na kuchukiwa. Ni wa kusikitikiwa kwa sababu ya ujinga wao, na ni wa kuchukiwa kwa sababu ya uzushi wao na asili yao ovu. Kwa wakati huu, Ninahisi kwamba ni muhimu niwafahamishe kuhusu maana ya mamlaka, yanaashiria nini, na yanawakilisha nini. Kwa mazungumzo ya jumla, Mungu Mwenyewe ni mamlaka, mamlaka Yake yanaashiria ukuu na kiini cha Mungu, na mamlaka ya Mungu Mwenyewe yanawakilisha hadhi na utambulisho wa Mungu. Kwa hiyo, je, Shetani atathubutu kusema kwamba yeye ni Mungu? Je, Shetani atathubutu kusema kwamba aliumba vitu vyote, na anashikilia ukuu juu ya vitu vyote? Bila shaka hawezi! Kwa sababu hawezi kuumba vitu vyote; mpaka leo, hajawahi kuumba chochote kilichoumbwa na Mungu, na hajawahi kuumba chochote chenye uhai. Kwa sababu hana mamlaka ya Mungu, hawezi kamwe kumiliki hadhi na utambulisho wa Mungu, na hii inaamuliwa na kiini chake. Je, anazo nguvu sawa na za Mungu? Bila shaka hana! Je, tunaitaje matendo ya Shetani, na miujiza inayoonyeshwa na Shetani? Je, ni nguvu? Je, inaweza kuitwa mamlaka? Bila shaka sivyo! Shetani anaongoza wimbi la uovu, na kuvuruga, kuharibu, na kuingilia kila kipengele cha kazi ya Mungu. Kwa miaka elfu kadhaa iliyopita, mbali na kuwapotosha na kuwanyanyasa wanadamu, na kumrubuni na kumdanganya mwanadamu hadi kufikia kiwango cha uovu, na kumkataa Mungu, ili mwanadamu atembee kwenye bonde la uvuli wa mauti, je, Shetani amefanya jambo lolote linalostahili hata kuadhimishwa, kupongezwa, au kuthaminiwa na mwanadamu? Kama Shetani angekuwa na mamlaka na nguvu, je, wanadamu wangepotoshwa naye? Kama Shetani angekuwa na mamlaka na nguvu, je, mwanadamu angepata madhara kutokana nayo? Kama Shetani anamiliki mamlaka na nguvu, je, mwanadamu angemwacha Mungu na kugeukia mauti? Kwa sababu Shetani hana mamlaka au nguvu, ni nini ambacho tunafaa kuhitimisha kuhusu kiini cha kila kitu anachofanya? Kunao wale wanaofafanua kila kitu ambacho Shetani anafanya kama hila tu, ilhali Ninaamini kwamba ufafanuzi kama huo haufai sana. Je, matendo maovu ya upotoshaji wake wa mwanadamu ni hila tu? Nguvu za maovu ambazo Shetani alimnyanyasia Ayubu, na tamanio lake la kikatili la kumnyanyasa na kumwangamiza, lisingeweza kutimizwa kwa hila tu. Tukiangalia nyuma, tunaona kwamba, mara moja, kondoo na ng’ombe wa Ayubu walitawanyishwa kila pahali katika milima na vilima, walitoweka; kwa muda mfupi tu, utajiri mwingi wa Ayubu ulitoweka. Je, inawezekana kwamba haya yote yalitimizwa kwa hila tu? Asili ya yale yote ambayo Shetani anafanya yanalingana na kuingiliana na mambo mabaya kama vile kudhoofisha, kuvuruga, kuharibu, kudhuru, uovu, nia mbaya, na giza, na kwa hivyo matukio haya yote ambayo si ya haki na ni maovu yanaunganishwa bila kutenganishwa na matendo ya Shetani, na hayawezi kutenganishwa na kiini kiovu cha Shetani. Haijalishi jinsi Shetani “alivyo na nguvu,” haijalishi jinsi Shetani alivyo jasiri na mwenye tamaa ya makuu, haijalishi jinsi uwezo wake ulivyo mkubwa katika kusababisha uharibifu, haijalishi jinsi zilivyo nyingi mbinu anazotumia kumpotosha na kumshawishi mwanadamu, haijalishi jinsi zilivyo mahiri hila na njama zake anazotumia kumtishia mwanadamu, haijalishi jinsi mfumo wa kuwepo kwake unavyoweza kubadilika, hajawahi kuweza kuumba hata kiumbe kimoja kilicho hai, hajawahi kuweza kuweka sheria au kanuni za kuwepo kwa vitu vyote, na hajawahi kutawala na kudhibiti kitu chochote, kiwe ni chenye uhai au kisichokuwa na uhai. Katika ulimwengu na anga, hakuna hata mtu au kitu kimoja kilichotokana na Shetani, au kilichopo kwa sababu ya Shetani; hakuna hata mtu au kitu kimoja ambacho kinatawaliwa na Shetani, au kudhibitiwa na Shetani. Kinyume chake ni kwamba, sio tu kuwa hana budi kuishi chini ya utawala wa Mungu, lakini, vilevile, lazima atii masharti na amri zote za Mungu. Bila ruhusa ya Mungu, ni vigumu sana kwa Shetani kugusa hata tone la maji au chembe ya mchanga juu ya nchi; bila ruhusa ya Mungu, Shetani hana hata uhuru wa kusogeza mchwa wanaotembea juu ya nchi, licha ya wanadamu, ambao waliumbwa na Mungu. Machoni pa Mungu, Shetani ni duni kuliko yungiyungi mlimani, kuliko ndege warukao angani, kuliko samaki wa baharini, na kuliko funza juu ya nchi. Jukumu lake miongoni mwa vitu vyote ni kutumikia vitu vyote, kuwatumikia wanadamu, na kuhudumia kazi ya Mungu na mpango Wake wa usimamizi. Haijalishi jinsi asili yake ilivyo na nia mbaya, na jinsi kiini chake kilivyo kiovu, kitu pekee anachoweza kufanya ni kutii jukumu lake: kuwa mtoa huduma kwa Mungu, na kutoa kipingamizi kwa Mungu. Hicho ndicho kiini na nafasi ya Shetani. Asili yake haijaunganishwa na maisha, haijaunganishwa na nguvu, haijaunganishwa na mamlaka; ni kitu tu cha kuchezea mikononi mwa Mungu, ni mashine tu ya kutoa huduma kwa Mungu!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 100)

Ni Mungu Pekee, Aliye na Utambulisho wa Muumba, Anayemiliki Mamlaka ya Kipekee

Mamlaka yenyewe yanaweza kufafanuliwa kama nguvu za Mungu. Kwanza, inaweza kusemwa kwa uhakika kwamba mamlaka na nguvu vyote ni chanya. Hazina uhusiano na kitu chochote kilicho kibaya, na hazina uhusiano na viumbe vyovyote vilivyoumbwa au vile ambavyo havikuumbwa. Nguvu za Mungu zinaweza kuumba kusemwa kwa uhakika kwamba mamlaka na nguvu vyote ni chanya. Hazina uhusiano na kitu chochote kilicho kibaya, na hazina uhusiano na nguvu, na haya yote yanaamuliwa na uzima wa Mungu. Mungu ni uzima, kwa hivyo Yeye ndiye chanzo cha viumbe vyote vyenye uhai. Zaidi ya hayo, mamlaka ya Mungu yanaweza kufanya viumbe vyote kutii kila neno la Mungu, yaani kuumbika kulingana na matamshi yanayotoka kwenye kinywa cha Mungu, na kuishi na kuongezeka kwa amri ya Mungu, kisha, Mungu anatawala na kuamuru viumbe vyote vyenye uhai, na hakutakuwa na kupotoka, milele na milele. Hakuna mtu au kitu chenye vitu hivi; ni Muumba pekee ndiye Anayemiliki na kubeba nguvu kama hizo, na hivyo yanaitwa mamlaka. Huu ndio upekee wa Muumba. Kwa hivyo, haijalishi kama ni neno lenyewe “mamlaka” au kiini cha mamlaka hayo, kila moja inaweza tu kuhusishwa na Muumba, kwa sababu ni ishara ya utambulisho wa kipekee na kiini cha Muumba, na inawakilisha utambulisho na hadhi ya Muumba; mbali na Muumba, hakuna mtu au kitu kinachoweza kuhusishwa na neno “mamlaka.” Hii ni tafsiri ya mamlaka ya kipekee ya Muumba.

Ingawa Shetani alimtazama Ayubu kwa macho ya tamaa, bila ruhusa ya Mungu hakuthubutu kugusa hata unywele mmoja kwenye mwili wa Ayubu. Ingawa Shetani kwa asili ni mwovu na mkatili, baada ya Mungu kutoa agizo lake kwake, Shetani hakuwa na chaguo ila kutii amri yaMungu. Na kwa hivyo, hata Ingawa Shetani alionekana kana kwamba ameshikwa na kichaa sawa na mbwa-mwitu miongoni mwa kondoo alipomjia Ayubu, hakuthubutu kusahau mipaka aliyowekewa wazi na Mungu, hakuthubutu kukiuka maagizo ya Mungu, na kwa hayo yote, Shetani hakuthubutu kutoka kwenye kanuni ya maneno ya Mungu—je, hii si kweli? Kutokana na hili inaweza kuonekana kwamba Shetani hathubutu kukiuka matamshi yoyote yale ya Yehova Mungu. Kwa Shetani, kila neno kutoka kwenye kinywa cha Mungu ni amri, na sheria ya mbinguni, na maonyesho ya mamlaka ya Mungu—kwani nyuma ya kila neno la Mungu kunadokezwa adhabu ya Mungu kwa wale wanaokiuka maagizo ya Mungu, na wale wasiotii na wanaopinga sheria za mbinguni. Shetani anajua wazi kwamba kama atakiuka maagizo ya Mungu, basi lazima akubali athari za kukiuka mamlaka ya Mungu na kupinga sheria za mbinguni. Na sasa athari hizi ni zipi? Sina haja ya kusema kwamba, athari hizi bila shaka, ni adhabu kutoka kwa Mungu. Vitendo vya Shetani kwa Ayubu vilikuwa ni mfano mdogo tu wa upotoshaji wake kwa mwanadamu, na Shetani alipokuwa akitekeleza vitendo hivi, mipaka ambayo Mungu aliweka na maagizo ambayo Alitoa kwa Shetani ilikuwa ni mfano mdogo tu wa kanuni zilizo nyuma ya kila kitu anachofanya. Aidha, wajibu na nafasi ya Shetani katika suala hili ulikuwa tu mfano mdogo wa wajibu na nafasi yake katika kazi ya usimamizi wa Mungu, na utiifu kamili wa Shetani kwa Mungu wakati alipomjaribu Ayubu, ulikuwa tu mfano mdogo wa namna ambavyo Shetani hakuthubutu kuweka hata upinzani mdogo kwa Mungu katika kazi ya usimamizi wa Mungu. Ni onyo gani ambalo mifano hii midogo inakupa? Miongoni mwa vitu vyote, ikiwa ni pamoja na Shetani, hakuna mtu au kitu kinachoweza kukiuka sheria na kanuni za mbinguni zilizowekwa wazi na Muumba, na hakuna mtu au kitu kinachothubutu kukiuka sheria na kanuni hizi za mbinguni, kwani hakuna mtu au kitu kinachoweza kubadilisha au kuepuka adhabu ambayo Mungu anawawekea wale wanaokosa kumtii. Ni Muumba tu anayeweza kuanzisha sheria na kanuni za mbinguni, ni Muumba tu aliye na nguvu za kuanza kuzitekeleza na nguvu za Muumba ndizo haziwezi kukiukwa na mtu au kitu chochote. Haya ndiyo mamlaka ya kipekee ya Muumba, mamlaka haya yako juu zaidi miongoni mwa vitu vyote, na hivyo, haiwezekani kusema kwamba “Mungu ndiye mkuu na Shetani ni namba mbili.” Isipokuwa Muumba anayemiliki mamlaka ya kipekee, hakuna Mungu mwingine.

Je, sasa una maarifa mapya kuhusu mamlaka ya Mungu? Kwanza, je, kuna tofauti kati ya mamlaka ya Mungu yaliyotajwa hivi punde na nguvu za binadamu? Na tofauti ni nini? Baadhi ya watu wanasema kwamba hakuna ufanano wowote kati ya hizo mbili. Hiyo ni sahihi! Ingawa watu wanasema hakuna ufanano kati ya hizo mbili, katika fikira na dhana za binadamu, nguvu za binadamu mara nyingi zinadhaniwa kuwa mamlaka, na haya mawili yanalinganishwa sambamba mara nyingi. Ni nini kinachoendelea hapa? Je, si watu wanafanya kosa la kubadilisha moja kwa nyingine bila kujua? Vitu hivi viwili havina uhusiano wowote na hakuna ufanano wowote kati yavyo, ilhali watu bado hawawezi kuelewa. Je, hili linapaswa kutatuliwaje? Kama unapenda kwa kweli kupata suluhu, njia ya pekee ni kuelewa na kujua mamlaka ya kipekee ya Mungu. Baada ya kuelewa na kujua mamlaka ya Muumba, hutataja kwa mkupuo mmoja nguvu za binadamu na mamlaka ya Mungu.

Nguvu za binadamu zinarejelea nini? Kwa ufupi, ni uwezo au mbinu inayowezesha tabia potovu, matamanio na malengo ya binadamu kuweza kupanuliwa au kutimizwa hadi kiwango cha juu zaidi. Je, hii inaweza kuhesabiwa kama mamlaka? Haijalishi ni vipi ambavyo malengo na matamanio ya binadamu yalivyo makubwa au yenye faida, mtu huyu hawezi kusemekana amemiliki mamlaka; kwa kiasi kikubwa, haya majivuno na ufanisi ni maonyesho tu ya upumbavu wa Shetani miongoni mwa binadamu; zaidi sana, ni upuuzi ambao Shetani anaendeleza kama babu yake mwenyewe ili kutimiza maono yake ya kuwa Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 101)

Ni Mungu Pekee, Aliye na Utambulisho wa Muumba, Anayemiliki Mamlaka ya Kipekee

Mamlaka ya Mungu yanaashiria nini? Je, yanaashiria ule utambulisho wa Mungu Mwenyewe? Je, yanaashiria nguvu za Mungu Mwenyewe? Je, yanaashiria hadhi ya kipekee ya Mungu Mwenyewe? Miongoni mwa mambo yote, ni katika kitu gani umeona mamlaka ya Mungu? Je, uliyaona vipi? Kwa mujibu wa ile misimu minne inayopitiwa na binadamu, je, kuna mtu yeyote anayeweza kubadilisha sheria ya mabadiliko kati ya machipuko, kiangazi, vuli na kipupwe? Wakati wa machipuko, miti inaweza kuchomoza na kuchanua; katika kiangazi, inafunikwa na majani; katika vuli inazaa matunda na katika kipupwe majani yanaanguka. Je, yupo anayeweza kubadilisha sheria hii? Je, hii inaonyesha kipengele kimoja cha mamlaka ya Mungu? Mungu alisema “Iwe Nuru,” na ikawa nuru. Je, nuru hii ingali ipo? Nuru hii inakuwepo kwa sababu ya nini? Inakuwepo kwa sababu ya maneno ya Mungu, bila shaka, na kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Je, hewa iliyoumbwa na Mungu bado ipo? Je, hewa ambayo binadamu anapumua inatoka kwa Mungu? Je, kuna yeyote anayeweza kuchukua vitu vinavyotoka kwa Mungu? Je, kuna yeyote anayeweza kubadilisha asili na kazi zao? Je, kuna yeyote anayeweza kubadilisha mpangilio wa usiku na mchana kama ulivyopangwa na Mungu, na sheria ya usiku na mchana kama ilivyoamrishwa na Mungu? Je, Shetani anaweza kufanya kitu kama hicho? Hata kama hulali wakati wa usiku, na unachukulia usiku kuwa wakati wa mchana, basi bado ni wakati wa usiku; unaweza kubadilisha mazoea yako ya kila siku, lakini huwezi kubadilisha sheria ya mabadilishano kati ya usiku na mchana—ukweli huu hauwezi kubadilishwa na mtu yeyote, sivyo? Je, kuna yeyote anayeweza kumfanya simba alime ardhi kama ng’ombe? Je, kuna mtu yeyote anayeweza kumbadilisha tembo kuwa punda? Je, kuna mtu yeyote anayeweza kumfanya kuku apae hewani kama tai? Je, kuna yeyote anayeweza kumfanya mbwa-mwitu alenyasi kama kondoo? (La.) Je, yupo anayeweza kumfanya samaki aliye majini kuishi kwenye ardhi kavu? Hilo haliwezi kufanywa na wanadamu. Na kwa nini haiwezekani? Ni kwa sababu Mungu aliwaamuru samaki kuishi ndani ya maji, na kwa hivyo wanaishi ndani ya maji. Kwenye ardhi kavu hawataweza kuishi kwani watakufa; hawawezi kukiuka mipaka ya amri ya Mungu. Vitu vyote vina sheria na mipaka ya kuwepo kwao, na kila mojawapo kina silika zake binafsi. Haya yameamriwa na Muumba, na hayawezi kubadilishwa na kukiukwa na binadamu yeyote. Kwa mfano, simba siku zote ataishi porini, umbali fulani kutoka kwenye jumuia ya binadamu, na hatawahi kuwa mtulivu na mwaminifu kama vile ng’ombe alivyo na anavyoishi na kumfanyia binadamu kazi. Ingawa ndovu na punda ni wanyama, na wote wana miguu minne, na ni viumbe vinavyopumua hewa, wao ni aina tofauti, kwa kuwa waligawanywa katika aina aina tofauti na Mungu, kila mmoja wao anazo silika zake binafsi, na hivyo hawatawahi kubadilishana. Ingawa kuku ana miguu miwili, na mabawa kama vile alivyo tai, hatawahi kuweza kupaa hewani; kama amejaribu sana anaweza tu kupaa hadi kwenye mti—na hili linaamuliwa na silika yake. Sina haja kusema, haya yote ni kwa sababu ya amri za mamlaka ya Mungu.

Katika maendeleo ya mwanadamu leo, sayansi ya mwanadamu inaweza kusemwa kwamba imeongezeka, na mafanikio ya uchunguzi wa kisayansi wa binadamu unaweza kufafanuliwa kama wa kuvutia. Uwezo wa kibinadamu, lazima isemwe, unazidi kuwa mkubwa zaidi, lakini kuna utafiti mmoja wa kisayansi ambao mwanadamu hajaweza kuufanya: Mwanadamu ameunda ndege, vifaa vya angani, na hata bomu la atomiki, mwanadamu ameenda angani, ametembea mwezini, amevumbua Intaneti, na ameishi maisha ya kiwango cha juu cha teknolojia, ilhali mwanadamu hawezi kuumba kiumbe hai kinachopumua. Silika za kila kiumbe kilicho hai na sheria ambazo zinatawala kuishi kwao na mzunguko wa maisha na kifo cha kila kiumbe kilicho hai—vyote hivi haviwezekani na havidhibitiki na sayansi ya mwanadamu. Wakati huu, lazima isemwe kwamba haijalishi ni viwango gani vya juu zaidi vitakavyofikiwa na sayansi ya binadamu, haviwezi kulinganishwa na fikira zozote za Muumba na haiwezekani kutambua miujiza ya uumbaji wa Muumba na uwezo wa mamlaka Yake. Kuna bahari nyingi sana juu ya nchi, ilhali hazijawahi kukiuka mipaka yao na kuja kwenye ardhi kwa nguvu, na hiyo ni kwa sababu Mungu aliweka mipaka kwa kila moja ya bahari hizo; zilikaa popote pale Alipoziamuru kukaa; na bila ya ruhusa ya Mungu haziwezi kuzunguka kwa uhuru. Bila ruhusa ya Mungu, haziwezi kuingiliana, na zinaweza kusonga tu pale ambapo Mungu anasema hivyo, na pale ambapo zinaenda na kubakia inaamuliwa na mamlaka ya Mungu.

Ili kuiweka kwa uwazi zaidi, “mamlaka ya Mungu” ina maana kwamba ni wajibu wa Mungu. Mungu anayo haki ya kuamua namna ya kufanya kitu na kinafanywa kwa vyovyote vile Anavyopenda. Sheria ya vitu vyote ni juu ya Mungu, na sio juu ya mwanadamu; wala haiwezi kubadilishwa na mwanadamu. Haiwezi kubadilishwa kwa mapenzi ya mwanadamu, lakini inaweza badala yake kubadilishwa kwa fikira za Mungu, na hekima ya Mungu, na amri za Mungu, na huu ni ukweli usiopingika kwa binadamu yeyote. Mbingu na nchi na viumbe vyote, ulimwengu, mbingu yenye nyota, misimu minne ya mwaka, kile kinachoonekana na kisichoonekana kwa mwanadamu-vyote vipo, vinafanya kazi, na vinabadilika bila ya kosa hata dogo, chini ya mamlaka ya Mungu, kulingana na maagizo ya awali ya Mungu, kulingana na amri za Mungu, na kulingana na sheria za mwanzo wa uumbaji. Hakuna mtu au kitu hata kimoja kinachoweza kubadilisha sheria zao, au kubadilisha mkondo wa asili ambao sheria hizi zinafanya kazi; zilianza kutumika kwa sababu ya mamlaka ya Mungu, na zitaangamia kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Haya ndiyo mamlaka yenyewe ya Mungu. Sasa kwa sababu haya yote yamesemwa, je, unahisi kwamba mamlaka ya Mungu ni ishara ya utambulisho na hadhi ya Mungu? Je, mamlaka ya Mungu yanaweza kumilikiwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au ambacho hakijaumbwa? Je, yanaweza kuigwa, kufananishwa, au kubadilishwa na mtu yeyote, na kitu chochote, au kifaa chochote?

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 102)

Utambulisho wa Muumba ni wa Kipekee, na Hupaswi Kufuata Wazo la Imani ya Miungu Wengi

Ingawa mbinu na uwezo wa Shetani ni mkubwa zaidi kuliko ule wa mwanadamu, ingawa anaweza kufanya mambo ambayo mwanadamu hawezi kuyafanya, bila kujali kama unaonea wivu au unatamani kile ambacho Shetani anafanya, bila kujali kama unachukia au unachukizwa na kile anachofanya, bila kujali kama unaweza au huwezi kuona hicho, bila kujali kiwango ambacho Shetani anaweza kutimiza, au ni watu wangapi anaoweza kuwadanganya ili wamwabudu na kumtolea kafara, na bila kujali jinsi unavyomfafanua, hauwezi kusema kwamba Shetani ana mamlaka na nguvu za Mungu. Unapaswa kujua kwamba Mungu ni Mungu, tunaye Mungu mmoja tu, na zaidi ya yote unafaa kujua kwamba ni Mungu tu aliye na mamlaka, na kwamba Anazo nguvu za kudhibiti na kutawala vitu vyote. Eti kwa sababu Shetani anao uwezo wa kuwadanganya watu, na anaweza kujifanya kuwa Mungu, na anaweza kuiga ishara na miujiza inayofanywa na Mungu, na amefanya mambo yanayofanana na yale ya Mungu, wewe unasadiki kimakosa kwamba Mungu si wa kipekee, kwamba kuna Miungu mingi, kwamba Miungu hii tofauti ina ujuzi mkubwa au mdogo tu, na kwamba kuna utofauti katika upana wa nguvu wanazotumia. Unapangilia ukuu wao katika mpangilio wa kuwasili kwao, na kulingana na umri wao, na unasadiki kimakosa kwamba kuna miungu mingine mbali na Mungu, na unafikiri kwamba nguvu na mamlaka ya Mungu si ya kipekee. Kama unazo fikira kama hizo, kama hutambui upekee wa Mungu, husadiki ni Mungu pekee anayemiliki mamlaka, na kama utadumu tu katika kushikilia imani ya kuabudu miungu wengi, basi Nasema kwamba wewe ni duni kabisa kuliko viumbe wote, wewe ni mfano halisi wa Shetani, na wewe ni mtu kamili wa maovu! Je, unaelewa kile Ninachojaribu kukufundishaa kwa kusema maneno haya? Haijalishi ni wakati gani, mahali, au historia yako, hupaswi kumchanganya Mungu na mtu mwingine yeyote, kitu, au kifaa chochote. Bila kujali jinsi unavyohisi kwamba mamlaka ya Mungu na kiini cha Mungu Mwenyewe haviwezi kujulikana wala kuweza kufikiwa, haijalishi ni kiwango kipi cha matendo na maneno ya Shetani yanavyokubaliana na mawazo na fikira zako, haijalishi ni vipi ambavyo mambo haya yanakutosheleza wewe, usiwe mjinga, usichanganye vipengele hivi, usikatae uwepo wa Mungu, usikatae utambulisho na hadhi ya Mungu, usimsukume Mungu nje ya mlango na kumleta Shetani kuchukua nafasi ya “Mungu” aliye ndani ya moyo wako na kuwa Mungu wako. Sina shaka kwamba una uwezo wa kufikiria matokeo ya kufanya hivyo!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 103)

Ingawa Binadamu Amepotoka, Bado Anaishi Chini ya Ukuu wa Mamlaka ya Muumba

Shetani amekuwa akiwapotosha wanadamu kwa maelfu ya miaka. Ametenda maovu mengi sana, amepotosha kizazi baada ya kizazi, na amefanya uhalifu wa kutisha duniani. Amemdhulumu mwanadamu, kumpotosha mwanadamu, kumshawishi mwanadamu kumpinga Mungu, na amefanya matendo maovu ambayo yamesumbua na kuharibu mpango wa usimamizi wa Mungu mara kwa mara. Hata hivyo, chini ya mamlaka ya Mungu, vitu vyote na viumbe vyenye uhai vinaendelea kutii kanuni na sheria zilizowekwa wazi na Mungu. Ikilinganishwa na mamlaka ya Mungu, asili ovu ya Shetani na kuenea kwake ni vitu vibaya mno, vinakera mno na ni vya kuleta aibu na ni vidogo mno na vinyonge. Hata Ingawa Shetani anatembea kati ya vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, hawezi kutekeleza mabadiliko madogo zaidi kwa watu, vitu, na vifaa vilivyoamriwa na Mungu. Miaka elfu kadhaa imepita, na mwanadamu angali anafurahia nuru na hewa aliyopewa na Mungu, angali anapumua pumzi iliyotolewa na Mungu Mwenyewe, angali anafurahia maua, ndege, samaki na wadudu walioumbwa na Mungu, na kufurahia vitu vyote vilivyotolewa na Mungu; mchana na usiku bado zinabadilishana bila kukoma; hiyo misimu minne inabadilishana kama kawaida; nao batabukini wanaopaa wanaondoka msimu huu wa kipupwe, lakini bado watarudi kwenye msimu ujao wa machipuko; samaki ndani ya maji hawajawahi kuondoka kwenye mito, maziwa—maskani yao; wadudu aina ya nyenje juu ya nchi wanaimba kwa mioyo yao kwenye siku za kiangazi; chenene kwenye nyasi wanaimba kwa sauti za polepole huku wakikaribisha msimu wa vuli, wale batabukini wanaanza kutembea kwa makundi, huku nao tai wanabakia peke yao; makundi ya simba yanajitosheleza yenyewe kwa kuwinda; nao kulungu hawatoki kwenye nyasi na maua…. Kila aina ya kiumbe kilicho hai miongoni mwa viumbe vyote kinaondoka na kurudi, kisha kinaondoka tena, mabadiliko milioni moja yanatokea kwa kufumba na kufumbua—lakini kile kisichobadilika ni silika zao na sheria za kuishi. Wanaishi chini ya riziki na usitawishaji wa Mungu, na hakuna mtu anayeweza kubadilisha silika zao, na vilevile hakuna mtu yeyote anayeweza kukiuka sheria hizi za kuishi. Ingawa mwanadamu, anayeishi miongoni mwa vitu vyote, amepotoshwa na kudanganywa na Shetani, mwanadamu bado hawezi kuacha maji yaliyoumbwa na Mungu, na, na, hewa iliyoumbwa na Mungu, na vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, na binadamu bado anaishi na kuzaliana kwenye anga hii iliyoumbwa na Mungu. Silika za mwanadamu bado hazijabadilika. Binadamu bado anategemea macho yake kuona, masikio yake kusikia, ubongo wake kufikiria, moyo wake kuelewa, miguu na nyayo zake kutembea, mikono yake kufanya kazi, na kadhalika; silika zote ambazo Mungu alimpa binadamu ili aweze kukubali utoaji wa Mungu umebaki bila kubadilishwa, uwezo ambao kupitia huo mwanadamu anashirikiana na Mungu haujabadilika, uwezo wa mwanadamu wa kutenda wajibu wa kiumbe kilichoumbwa haujabadilishwa, mahitaji ya kiroho ya mwanadamu hayajabadilika, tamanio la mwanadamu kuweza kujua asili yake haijabadilika, shauku ya mwanadamu kuweza kuokolewa na Muumba haijabadilika. Hizi ndizo hali za sasa za mwanadamu, anayeishi chini ya mamlaka ya Mungu, na ambaye amevumilia maangamizo mabaya yaliyoletwa na Shetani. Ingawa mwanadamu amepitia unyanyasaji wa Shetani, na yeye si Adamu na Hawa tena ambao waliumbwa hapo mwanzo, badala yake amejaa mambo ambayo yana uadui na Mungu kama vile maarifa, fikira, dhana na kadhalika, na amejaa tabia potovu za kishetani, machoni pa Mungu, mwanadamu bado ni mwanadamu yule yule Aliyemuumba. Mwanadamu bado yuko chini ya ukuu na mipangilio ya Mungu, na bado anaishi ndani ya mkondo uliowekwa na Mungu, na hivyo machoni pa Mungu, mwanadamu ambaye amepotoshwa na Shetani amefunikwa tu na uchafu na tumbo linalonguruma, na miitikio ambayo ni ya polepole kidogo, kumbukumbu ambayo si nzuri kama ilivyokuwa, na ni ya zamani kidogo—lakini kazi na silika zote za binadamu bado hazijapata madhara kamwe. Hawa ndio wanadamu ambao Mungu anakusudia kuwaokoa. Wanadamu hawa wanahitaji tu kusikia mwito wa Muumba na kusikia sauti ya Muumba, naye atasimama na kukimbia kutafuta ni wapi sauti imetokea. Mwanadamu huyu lazima tu aweze kuona sura ya Muumba na atapuuzia mengine yote, na kuacha kila kitu, ili kuweza kujitolea mwenyewe kwa Mungu, na hata atayatenga maisha yake kwa ajili Yake. Wanadamu wanapofahamu kutoka mioyoni mwao sauti ya moyo wa Muumba, watamkataa Shetani na kuja upande wa Muumba; wakati mwanadamu atakuwa ametakasa kabisa uchafu kutoka kwenye mwili wake, na amepokea kwa mara nyingine tena utolewaji na utunzaji wa Muumba, kumbukumbu ya mwanadamu itarejeshwa na kwa wakati huu mwanadamu atakuwa amerejea kwa kweli katika utawala wa Muumba.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 104)

Kwa Kumpinga Mungu kwa Ukaidi, Mwanadamu Anaangamizwa na Ghadhabu ya Mungu

Mwa 19:1-11 Na jioni malaika wawili walikuja Sodoma; naye Lutu aliketi katika lango la Sodoma: na baada ya Lutu kuwaona aliinuka kwenda kuwakaribisha; na akasujudu; Naye akasema, Tazama saa hii, bwana zangu, ingieni ndani, nawaomba, ndani ya nyumba ya mtumishi wenu, na mbaki usiku mzima, na msafishe miguu yenu, na mtaamka mapema, na mshike njia zenu. Nao wakasema, La; lakini tutaketi katika uwanja usiku mzima. Na akawaomba sana; na wakamjia na kuingia katika nyumba yake; na akawaandalia karamu, na kupika mikate bila chachu, na wakala. Lakini kabla ya wao kujilaza, watu kutoka mjini, hata wenyeji wa Sodoma, waliizunguka nyumba hiyo, wazee na pia vijana, watu wote kutoka kila sehemu: Na wakamwita Lutu, na kumwambia, Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako leo usiku? Walete kwetu, ili tupate kuwajua. Naye Lutu akatoka mlangoni mahali walipokuwa, na akafunga mlango nyuma yake, Na kusema, nawaomba, ndugu, msitende maovu hivyo. Tazameni sasa, ninao mabinti wawili ambao ni mabikira; mniruhusu, nawaomba, niwalete nje kwenu, na mwafanyie mwonavyo kuwa vizuri katika macho yenu: ila kwa hawa wanaume msifanye chochote: kwani wamekuja chini ya kivuli cha paa langu. Na walisema. Ondoka. Na wakasema tena, Mtu huyu mmoja aliingia kwetu kukaa kwa muda, naye anatamani kuhukumu: sasa tutakushughulikia kwa njia mbaya zaidi, kuliko wao. Na wakamshinikiza sana mtu huyo, hadi Lutu, na wakawa karibu kuuvunja mlango. Lakini watu wale wakanyosha mbele mikono yao, na kumvuta Lutu katika nyumba waliyokuwemo, na kuufunga mlango. Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta mlango.

Mwa 19:24-25 Kisha Yehova alinyesha kwa Sodoma na Gomora kibiriti na moto kutoka kwa Yehova mbinguni; Na Akaiangusha hiyo miji, na mabonde yote, na wenyeji wote wa miji hiyo, na kile kilichomea kutoka ardhini.

Kutoka kwenye mafungu haya, si vigumu kuona kwamba dhambi ya Sodoma na kupotoka kwake tayari vilikuwa vimefikia kiwango kilichochukiza binadamu na Mungu, na kwamba machoni pa Mungu mji huo ulifaa kuangamizwa. Lakini ni nini kilichotokea ndani ya mji huo hapo awali kabla haujaangamizwa? Ni msukumo upi tunaoweza kupata kutoka kwenye matukio haya? Je, mtazamo wa Mungu katika matukio haya unatuonyesha nini kuhusu tabia yake? Ili kuelewa hadithi nzima, hebu na tuweze kusoma kwa makini kile kilichorekodiwa katika Maandiko …

Kupotoka kwa Sodoma: Kunamkasirisha Mwanadamu, Kunamghadhibisha Mungu

Kwenye usiku huo, Lutu alipokea wajumbe wawili kutoka kwa Mungu na akawatayarishia karamu. Baada ya kula, kabla hawajalala, watu kutoka kila pahali kwenye mji walizunguka makazi ya Lutu na kumwita nje Lutu. Maandiko yanawarekodi wakisema, “Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako leo usiku? Walete kwetu, ili tupate kuwajua.” Je, ni nani waliosema maneno haya? Je, yalielekezwa kwa nani? Haya yalikuwa maneno ya watu wa Sodoma, walipiga mayowe nje ya makazi ya Lutu wakinuia kumwita Lutu. Je, unahisi vipi ukiyasikia maneno haya? Je, unaghadhibishwa? Je, maneno haya yanakukera? Je, unachemkwa na hasira kali? Je, Huoni kwamba maneno haya yanamdhihirisha Shetani? Kupitia kwa maneno haya, je, unaweza kuhisi uovu na giza vilivyomo kwenye mji huu? Je, unaweza kuhisi ukatili na unyama wa tabia za watu hawa kupitia kwa maneno yao? Je, unaweza kuhisi kina cha kupotoka kwao kupitia kwa tabia yao? Kupitia kwa maudhui ya maneno yao, si vigumu kuona kwamba asili yao ya dhambi na tabia yao iliyopotoka ilikuwa imefikia kiwango kilichokuwa zaidi ya uwezo wao kuidhibiti. Isipokuwa Lutu, kila mtu katika mji huu hakuwa tofauti na Shetani; kule kuona tu mtu mwingine kuliwafanya watu hawa watake kuwadhuru na kuwateketeza …. Mambo haya hayampatii tu mtu hisia ya asili potovu na ya kutisha ya mji huu, lakini pia yanamwonyesha harufu ya kifo iliyouzunguka mji huu; yanampa pia mtu hisia za uovu wake na umwagaji wa damu.

Akikabiliana uso kwa uso na kundi la watu wakatili wasio na utu, watu waliokuwa wamejaa tamaa ya kuteketeza nafsi za wanadamu, je, Lutu aliwaambia nini? Kulingana na Maandiko: “Nawaomba … msitende maovu hivyo. Tazameni sasa, ninao mabinti wawili ambao ni mabikira; mniruhusu, nawaomba, niwalete nje kwenu, na mwafanyie mwonavyo kuwa vizuri katika macho yenu: ila kwa hawa wanaume msifanye chochote: kwani wamekuja chini ya kivuli cha paa langu.” Lutu alimaanisha yafuatayo katika maneno yake: Alikuwa radhi kuwatoa binti zake wawili ili kuwalinda wale wajumbe. Kwa sababu yoyote ile inayofaa, watu hawa walipaswa kukubaliana na masharti ya Lutu na kuwaacha wale wajumbe wawili peke yao; kwani hata hivyo, wajumbe hao walikuwa watu wageni kabisa kwao, watu ambao hawakuwa na chochote katu kuhusiana na wao; wajumbe hawa wawili walikuwa hawajawahi kudhuru masilahi yao. Hata hivyo, kwa kuchochewa na asili yao ya dhambi, hawakuliachia suala hili hapo. Badala yake, walizidisha tu jitihada zao. Hapa mojawapo ya mabishano yao yanaweza bila shaka kumpatia mtu ufahamu zaidi kuhusu asili ya kikatili iliyopo ndani ya watu hawa; wakati uo huo yanatujuza na kutufanya tuelewe sababu ya Mungu kutaka kuuangamiza mji huu.

Kwa hivyo walisema nini baadaye? Kama vile Biblia inavyosoma: “Toka. Na wakasema tena, Mtu huyu mmoja aliingia kwetu kukaa kwa muda, naye anatamani kuhukumu: sasa tutakushughulikia kwa njia mbaya zaidi, kuliko wao. Na wakamshinikiza sana mtu huyo, hadi Lutu, na wakawa karibu kuuvunja mlango.” Kwa nini walitaka kuuvunja mlango? Sababu ni kwamba walikuwa na hamu ya kuwaletea madhura wale wajumbe wawili. Wale wajumbe walikuwa wakifanya nini Sodoma? Kusudio lao la kuja hapo lilikuwa ni kumwokoa Lutu na familia yake; hata hivyo, watu wa mji huo walifikiri kimakosa kwamba walikuwa wamekuja kuchukua nyadhifa zao rasmi. Bila ya kuulizia kusudio la wajumbe hao, watu wa mji huo waliegemeza tamaa yao ya kuwadhuru kikatili wajumbe hao wawili kwa makisio yao tu; walitaka kuwadhuru watu hao wawili ambao hawakuwa na uhusiano wowote nao. Ni wazi kwamba watu wa mji huu walikuwa wamepoteza kabisa ubinadamu na akili zao razini. Kiwango cha wendawazimu wao na kukosa ustaarabu kwao kilikuwa tayari si tofauti na asili potovu ya Shetani ya kudhuru na kudanganya binadamu.

Walipodai watu hawa kutoka kwa Lutu, je, Lutu alifanya nini? Kutoka kwenye maandiko hayo tunajua kwamba Lutu hakuwakabidhi wajumbe hawa kwa watu hawa. Je, Lutu aliwajua wajumbe hawa wawili wa Mungu? Bila shaka la! Lakini kwa nini aliweza kuwaokoa watu hawa wawili? Je, alijua ni nini walichokuwa wamekuja kufanya? Ingawa hakujua sababu ya wao kuja, alijua kwamba walikuwa ni watumishi wa Mungu, na kwa hivyo aliwapokea. Kwamba aliweza kuwaita watumishi hawa wa Mungu mabwana yaonyesha kwamba Lutu kwa kawaida alikuwa ni mfuasi wa Mungu, tofauti na wale wengine waliokuwa ndani ya Sodoma. Kwa hivyo, wakati wajumbe wa Mungu walipomjia, alihatarisha maisha yake binafsi ili kuwapokea watumishi hao wawili; aidha, aliwatoa binti zake wawili kuwabadilisha na watumishi hao wawili ili kuwalinda watumishi hao. Hiki ndicho kilikuwa kitendo cha haki cha Lutu; vilevile lilikuwa onyesho linaloonekana waziwazi kuhusu asili na kiini cha Lutu, na ndiyo pia sababu ya Mungu kuwatuma watumishi Wake ili kumwokoa Lutu. Wakati alipokabiliwa na changamoto, Lutu aliwalinda watumishi hawa wawili bila kujali chochote kingine; alitaka hata awatoe mabinti zake wawili kwa mabadilishano ili mradi tu watumishi hawa wapate usalama. Mbali na Lutu, je, kulikuwa na mtu mwingine yeyote ndani ya mji huo ambaye angefanya jambo kama hili? Ukweli unathibitisha kwamba: hakuna! Kwa hivyo, ni wazi kabisa kwamba kila mtu katika Sodoma, isipokuwa Lutu, alikuwa mlengwa wa maangamizo na walipaswa kuangamizwa.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 105)

Mwa 19:1-11 Na jioni malaika wawili walikuja Sodoma; naye Lutu aliketi katika lango la Sodoma: na baada ya Lutu kuwaona aliinuka kwenda kuwakaribisha; na akasujudu; Naye akasema, Tazama saa hii, bwana zangu, ingieni ndani, nawaomba, ndani ya nyumba ya mtumishi wenu, na mbaki usiku mzima, na msafishe miguu yenu, na mtaamka mapema, na mshike njia zenu. Nao wakasema, La; lakini tutaketi katika uwanja usiku mzima. Na akawaomba sana; na wakamjia na kuingia katika nyumba yake; na akawaandalia karamu, na kupika mikate bila chachu, na wakala. Lakini kabla ya wao kujilaza, watu kutoka mjini, hata wenyeji wa Sodoma, waliizunguka nyumba hiyo, wazee na pia vijana, watu wote kutoka kila sehemu: Na wakamwita Lutu, na kumwambia, Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako leo usiku? Walete kwetu, ili tupate kuwajua. Naye Lutu akatoka mlangoni mahali walipokuwa, na akafunga mlango nyuma yake, Na kusema, nawaomba, ndugu, msitende maovu hivyo. Tazameni sasa, ninao mabinti wawili ambao ni mabikira; mniruhusu, nawaomba, niwalete nje kwenu, na mwafanyie mwonavyo kuwa vizuri katika macho yenu: ila kwa hawa wanaume msifanye chochote: kwani wamekuja chini ya kivuli cha paa langu. Na walisema. Ondoka. Na wakasema tena, Mtu huyu mmoja aliingia kwetu kukaa kwa muda, naye anatamani kuhukumu: sasa tutakushughulikia kwa njia mbaya zaidi, kuliko wao. Na wakamshinikiza sana mtu huyo, hadi Lutu, na wakawa karibu kuuvunja mlango. Lakini watu wale wakanyosha mbele mikono yao, na kumvuta Lutu katika nyumba waliyokuwemo, na kuufunga mlango. Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta mlango.

Mwa 19:24-25 Kisha Yehova alinyesha kwa Sodoma na Gomora kibiriti na moto kutoka kwa Yehova mbinguni; Na Akaiangusha hiyo miji, na mabonde yote, na wenyeji wote wa miji hiyo, na kile kilichomea kutoka ardhini.

Sodoma Yaangamizwa kwa Kuikosea Ghadhabu ya Mungu

Wakati watu wa Sodoma walipowaona watu hawa wawili, hawakuuliza sababu ya wao kuja wala hakuna yule aliyeuliza kama walikuwa wamekuja kueneza mapenzi ya Mungu. Kinyume cha mambo, walikusanyika na kuwa umati wa watu na, bila kusubiri ufafanuzi wowote, walikuja kuwakamata watumishi hawa wawili ni kana kwamba walikuwa mbwa koko au mbwa mwitu. Je, Mungu aliyatazama mambo haya wakati yalipokuwa yakifanyika? Je, Mungu alikuwa akifikiria nini katika moyo Wake kuhusiana na tabia hii ya binadamu, aina ya jambo kama hili? Mungu aliamua kuangamiza mji huu; Asingesita wala kusubiri, wala Asingeendelea kuonyesha subira yake. Siku yake ilikuwa imetimia, na kwa hivyo Aliweza kuweka wazi kazi Aliyopenda kufanya. Hivyo basi, Mwanzo 19:24-25 inasema, “Kisha Yehova alinyesha kwa Sodoma na Gomora kibiriti na moto kutoka mbinguni kwa Yehova; Na Akaiangusha hiyo miji, na mabonde yote, na wenyeji wote wa miji hiyo, na kile kilichomea kutoka ardhini.” Mistari hii miwili inawaambia watu mbinu ambayo kwayo Mungu aliuangamiza mji huu; pia inawaambia watu kile ambacho Mungu alikiangamiza. Kwanza, Biblia inasimulia kwamba Mungu aliteketeza mji kwa moto, na kwamba kiwango cha moto kilitosha kuwaangamiza watu wote na kila kitu kilichomea kwenye ardhi. Hii ni kusema kwamba, moto ulioangushwa kutoka mbinguni haukuangamiza tu mji; uliangamiza pia watu wote na vitu vilivyo hai ndani yake, vyote bila kuacha chochote nyuma. Baada ya mji kuangamizwa, ardhi ilikuwa tupu bila kitu chochote kilicho hai. Hakukuwa tena na maisha, wala dalili zozote za maisha. Mji ulikuwa umebadilika na kuwa ardhi iliyoharibiwa, mahali patupu palipojaa kimya cha kutisha. Kusingekuwa na matendo maovu zaidi dhidi ya Mungu mahali hapa; kusingekuwa na uchinjaji zaidi au umwagikaji wa damu.

Kwa nini Mungu alitaka kuuchoma mji huu kabisa? Ni nini unachoweza kuona hapa? Je, inawezekana kwamba Mungu hangeweza kustahimili kuona wanadamu na vitu vyote alivyoviumba vikiharibiwa hivi? Kama unaweza kutambua ghadhabu ya Yehova Mungu kutokana na moto ule ambao uliangushwa kutoka mbinguni, basi si vigumu sana kuona kiwango Chake cha hasira kali kutoka kwenye lengo la maangamizo Yake pamoja na kiwango ambacho mji huo uliweza kuangamizwa. Wakati Mungu anadharau mji, Ataweza kutekeleza adhabu Yake juu ya mji huo. Wakati Mungu anachukizwa na mji, Ataweza kutoa maonyo mbalimbali akifahamisha watu kuhusu ghadhabu Yake. Hata hivyo, wakati Mungu anaamua kukomesha na kuangamiza mji—yaani, wakati hasira na heshima Yake vimekosewa—Hataweza tena kutoa maonyo au adhabu nyingine. Badala yake, Ataweza kuuangamiza moja kwa moja. Ataufanya kutoweka kabisa. Hii ndiyo tabia ya haki ya Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 106)

Mwa 19:1-11 Na jioni malaika wawili walikuja Sodoma; naye Lutu aliketi katika lango la Sodoma: na baada ya Lutu kuwaona aliinuka kwenda kuwakaribisha; na akasujudu; Naye akasema, Tazama saa hii, bwana zangu, ingieni ndani, nawaomba, ndani ya nyumba ya mtumishi wenu, na mbaki usiku mzima, na msafishe miguu yenu, na mtaamka mapema, na mshike njia zenu. Nao wakasema, La; lakini tutaketi katika uwanja usiku mzima. Na akawaomba sana; na wakamjia na kuingia katika nyumba yake; na akawaandalia karamu, na kupika mikate bila chachu, na wakala. Lakini kabla ya wao kujilaza, watu kutoka mjini, hata wenyeji wa Sodoma, waliizunguka nyumba hiyo, wazee na pia vijana, watu wote kutoka kila sehemu: Na wakamwita Lutu, na kumwambia, Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako leo usiku? Walete kwetu, ili tupate kuwajua. Naye Lutu akatoka mlangoni mahali walipokuwa, na akafunga mlango nyuma yake, Na kusema, nawaomba, ndugu, msitende maovu hivyo. Tazameni sasa, ninao mabinti wawili ambao ni mabikira; mniruhusu, nawaomba, niwalete nje kwenu, na mwafanyie mwonavyo kuwa vizuri katika macho yenu: ila kwa hawa wanaume msifanye chochote: kwani wamekuja chini ya kivuli cha paa langu. Na walisema. Ondoka. Na wakasema tena, Mtu huyu mmoja aliingia kwetu kukaa kwa muda, naye anatamani kuhukumu: sasa tutakushughulikia kwa njia mbaya zaidi, kuliko wao. Na wakamshinikiza sana mtu huyo, hadi Lutu, na wakawa karibu kuuvunja mlango. Lakini watu wale wakanyosha mbele mikono yao, na kumvuta Lutu katika nyumba waliyokuwemo, na kuufunga mlango. Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta mlango.

Mwa 19:24-25 Kisha Yehova alinyesha kwa Sodoma na Gomora kibiriti na moto kutoka kwa Yehova mbinguni; Na Akaiangusha hiyo miji, na mabonde yote, na wenyeji wote wa miji hiyo, na kile kilichomea kutoka ardhini.

Baada ya Upinzani wa Mara kwa Mara wa Sodoma na Uadui Wao Dhidi Yake, Mungu Anaufuta Kabisa

Kwa mtazamo wa kibinadamu, Sodoma ulikuwa ni mji ambao ungeweza kutosheleza kabisa tamaa za wanadamu na maovu ya wanadamu. Walivutiwa na kutekwa akili zao, kwa muziki na kucheza densi usiku baada ya usiku, ufanisi wake uliwasukuma wanaume wavutiwe sana na kutiwa wazimu. Maovu yake yalidhuru mioyo ya watu na wakapumbazwa hadi kufikia kukengeuka vibaya. Huu ulikuwa ni mji ambao roho wachafu na roho waovu walicharuka hewani; ulijaa dhambi na mauaji na harufu ya damu iliyovunda. Ulikuwa mji ambao ulitisha watu kabisa, mji ambao mtu angejitoa kwake kwa hofu. Hakuna mtu katika mji huu—awe wa kiume au wa kike, awe mchanga au mzee—aliyetafuta njia ya kweli; hakuna aliyetamani mwangaza au kutaka kuachana na dhambi. Kila mmoja aliishi chini ya udhibiti wa Shetani, upotovu na uwongo. Kila mmoja alikuwa ameupoteza ubinadamu wake; walikuwa wamepoteza hisia zao, na walikuwa wamepoteza shabaha asilia ya kuweko kwa binadamu. Walitenda matendo maovu yasiyohesabika ya upinzani dhidi ya Mungu; walikataa mwongozo wake na kupinga mapenzi Yake. Yalikuwa matendo yao maovu ambayo yaliwapeleka watu hawa, mji na kila kiumbe kilichokuwa ndani ya mji huu, hatua kwa hatua, kwenye njia ya maangamizo.

Ingawa vifungu hivi viwili havirekodi maelezo yanayofafanua kiwango cha kupotoka cha watu wa Sodoma, badala yake yanarekodi mwenendo wao kwa watumishi wawili wa Mungu kufuatia kuwasili kwao mjini, kuna ukweli rahisi unaoweza kufichua kiwango ambacho watu wa Sodoma walikuwa wamepotoka, jinsi walivyojaa maovu na kumpinga Mungu. Kwa mujibu wa haya, ukweli wa mambo na hali halisi ya watu wa mji huu vinafichuliwa pia. Mbali na kutokubali maonyo ya Mungu, hawakuogopa pia adhabu Yake. Kinyume cha mambo ni kwamba, walifanyia mzaha ghadhabu ya Mungu. Walimpinga Mungu bila sababu. Haijalishi ni nini Alichofanya au ni vipi Alivyokifanya, asili yao ya tamaa ilizidi kuongezeka, na wakampinga Mungu mara kwa mara. Watu wa Sodoma walikuwa wanachukia kuwepo kwa Mungu, wanachukia ujio wa Mungu, wanachukia adhabu ya Mungu, na hata zaidi, wanachukia maonyo ya Mungu kwao. Hawakuona kingine chochote chenye thamani karibu nao. Waliwapotosha na kuwadhuru watu wote walioweza kupotoshwa na kupata madhara, na wakawatendea watumishi wa Mungu vivyo hivyo. Kuhusiana na matendo yote maovu yaliyotendwa na watu hawa wa Sodoma, kuwadhuru watumishi wa Mungu kulikuwa mfano tu wa tone baharini ya kile walichokuwa wakifanya, na asili yao potovu ambayo imefichuliwa kwa kweli inaonekana tu kuwa ni ndogo zaidi kuliko hata tone moja ndani ya bahari kubwa. Kwa hivyo, Mungu alichagua kuwaangamiza kwa moto. Mungu hakutumia gharika, wala hakutumia tufani, tetemeko la ardhi, tsunami au njia nyingine yoyote ya kuuangamiza mji huu. Je, kulimaanisha nini Mungu kuangamiza mji huu kwa kutumia moto Kulimaanisha uangamizaji kamili wa mji huo; kulimaanisha kwamba mji huu ungetoweka kabisa kutoka ulimwenguni na ungekoma kabisa katika kuwepo kwake. Hapa, “kuangamiza” hakurejelei tu kule kutoweka kwa umbo na muundo au sura ya nje ya mji huo; kunamaanisha pia kwamba nafsi za watu ndani ya mji huo zilikoma kuwepo, zikiwa zimeangamizwa kabisa. Kwa ufupi, watu wote, matukio na vitu vyote vilivyohusiana na mji huu viliangamizwa. Kusingekuwa na maisha ya baadaye ama roho zao kupata mwili tena; Mungu alikuwa amewafuta kabisa kutoka kwa wanadamu, uumbaji Wake, mara moja na tena milele. Yale “matumizi ya moto” yalimaanisha kusitisha dhambi, na yalimaanisha mwisho wa dhambi; dhambi hii ingekoma kuwepo na kuenea. Ilimaanisha kwamba uovu wa Shetani ulikuwa umepoteza mahali pake pa kunawiri pamoja na eneo la kaburi ambalo lilimpatia Shetani mahali pa kukaa na kuishi. Kwenye vita kati ya Mungu na Shetani, Mungu anapotumia moto ni alama ya ushindi Wake ambayo Shetani anatajiwa. Kuangamizwa kwa Sodoma ni hatua kubwa ya kuzuia maono ya Shetani ya kumpinga Mungu kwa kuwapotosha na kuwadanganya wanadamu. Pia ni ishara ya aibu katika historia ya maendeleo ya binadamu ambapo binadamu alikataa mwongozo wa Mungu na akajiachilia kutenda maovu. Aidha, ni rekodi ya ufunuo wa kweli wa tabia ya haki ya Mungu.

Wakati ule moto ambao Mungu aliutuma kutoka mbinguni ulikuwa umeteketeza kabisa Sodoma hata zaidi ya majivu, ilimaanisha kwamba mji huu ulioitwa “Sodoma” ungekoma kuwepo, na ilimaanisha kwamba kila kitu ndani ya mji huo hakingeonekana tena. Mji uliangamizwa kwa ghadhabu ya Mungu; ulitoweka kutokana na hasira na ukuu wa Mungu. Kwa sababu ya tabia ya haki ya Mungu Sodoma ilipokea adhabu yake ya haki; kutokana na tabia ya haki ya Mungu, ilipokea mwisho wake wa haki. Mwisho wa kuwepo kwa Sodoma ulitokana na maovu yake, na ulitokana pia na tamanio la Mungu kutowahi kuutazamia mji huu tena, pamoja na watu wote walioishi ndani ya mji huo au maisha yoyote yaliyowahi kukua ndani ya mji huo. “Tamanio la Mungu la kutowahi kuutazama tena mji huo” ni ghadhabu Yake, pamoja na ukuu Wake. Mungu aliuteketeza mji kwa sababu maovu na dhambi zake vilimsababisha Yeye kuhisi ghadhabu, maudhi na chuki katika mji huu na tamanio lake la kutowahi kuuona tena au watu wowote wa mji huo na viumbe vyote vilivyo hai vilivyokuwa ndani ya mji huo. Baada ya mji huo kumalizika kuteketea, huku yakiwa yameachwa nyuma majivu pekee, ilikuwa kwa kweli mji huo umekoma kuwepo mbele ya macho ya Mungu; hata kumbukumbu za Mungu kuuhusu ziliondolewa, zilifutwa. Hii inamaanisha kwamba moto ulioangushwa kutoka mbinguni haukuangamiza tu mji wote wa Sodoma na watu waliokua wamejaa maovu ndani yake, wala haukuangamiza tu vitu vyote vilivyokuwa ndani ya mji huo ambavyo vilikuwa vimetiwa doa na dhambi; zaidi pia, moto huu uliharibu kumbukumbu za maovu na upinzani wa wanadamu dhidi ya Mungu. Hili ndilo lilikuwa kusudi la Mungu la kuuteketeza mji ule.

Binadamu walikuwa wamepotoka kupindukia. Watu hawa hawakujua Mungu alikuwa nani au kule walikokuwa wametokea. Kama ungemtaja Mungu, watu hawa wangekushambulia, kukutukana na wangekufuru. Hata wakati ambao watumishi wa Mungu walikuwa wamekuja kueneza onyo Lake, watu hawa waliopotoka hawakuweza kuonyesha ishara zozote za toba na hawakuacha mwenendo wao wa maovu, lakini kinyume cha mambo ni kwamba, waliweza bila ya haya, kuwadhuru watumishi wa Mungu. Kile walichoonyesha na kufichua kilikuwa asili na kiini chao halisi cha uadui mkubwa kwa Mungu. Tunaweza kuona kwamba upinzani wa watu hawa waliopotoka dhidi ya Mungu ulikuwa zaidi ya ufunuo wa tabia yao potovu, kama vile tu ilivyokuwa zaidi ya tukio la kashfa au dhihaka inayotokana na ukosefu wa ufahamu wa ukweli. Ujinga wala kutojua havikusababisha mwenendo huu wa maovu; haikuwa kwa sababu watu hawa walikuwa wamedanganywa, na bila shaka si kwa sababu walikuwa wamepotoshwa. Mwenendo wao ulikuwa umefikia kiwango cha uhasama wa wazi wa kupinga na kuasi dhidi ya Mungu. Bila shaka, aina hii ya tabia ya binadamu ingempa hasira kali Mungu, na ingesababisha hasira kali kwenye tabia Yake—tabia ambayo haitakiwi kukosewa. Kwa hivyo, Mungu aliachilia kwa njia ya moja kwa moja na kwa uwazi hasira Yake na adhama Yake; huu ni ufunuo wa kweli wa tabia Yake ya haki. Akiwa amekabiliwa na mji uliofurika na dhambi, Mungu alitamani kuuangamiza kwa njia ya haraka zaidi iliyowezekana; Alitaka kuwaangamiza kabisa watu waliokuwa ndani yake na dhambi zao zote, ili kuwafanya watu wa mji huu wakome kuwepo na kukomesha dhambi ndani ya mahali hapa isiongezeke. Njia ya haraka zaidi na kamilifu zaidi ya kufanya hivyo ilikuwa ni kuuteketeza kwa moto. Mtazamo wa Mungu kwa watu wa Sodoma haukuwa ule wa kuwaacha au kutowajali; bali, Alitumia hasira Yake, adhama na mamlaka kuwaadhibu, kuwaweka chini na kuwaangamiza kabisa watu hawa. Mtazamo wake kwao haukuwa tu ule wa kuwaangamiza kimwili bali pia kuwaangamiza kinafsi, ukomeshaji wa milele. Hii ndiyo athari ya kweli ya tamanio la Mungu kwao “kuweza kukoma kuwepo.”

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 107)

Ingawaje Hasira ya Mungu Imefichwa na Haijulikani kwa Binadamu, Haivumilii Kosa Lolote

Mungu huwashughulikia wanadamu wajinga na wapumbavu kwa huruma na uvumilivu. Lakini, kwa upande mwingine ghadhabu ya Mungu imefichwa mara nyingi na katika matukio mengi, na haijulikani kwa watu. Kutokana na hayo, ni vigumu sana kwa binadamu kumwona Mungu akionyesha hasira Yake, na ni vigumu pia kuelewa hasira Yake. Kwa hivyo, binadamu huchukulia hasira ya Mungu kuwa ndogo. Wakati mwanadamu anapokabiliwa na kazi ya mwisho ya Mungu na hatua ya mwisho ya uvumilivu na msamaha kwa mwanadamu—yaani, wakati tukio la mwisho la Mungu la rehema na onyo Lake la mwisho linapowajia wanadamu—ikiwa watu bado wanatumia mbinu zilezile kumpinga Mungu na hawafanyi jitihada zozote za kutubu, kurekebisha njia zao au kukubali rehema Zake, basi Mungu hataweka tena uvumilivu na subira Yake juu yao. Kinyume cha mambo ni kwamba, Mungu atabatilisha rehema Zake wakati huu. Kufuatia haya, Ataituma tu ghadhabu Yake. Anaweza kudhihirisha ghadhabu Yake kwa njia tofauti, kama vile tu Anavyoweza kutumia mbinu tofauti kuwaadhibu na kuwaangamiza watu.

Matumizi ya Mungu ya moto kuuangamiza mji wa Sodoma ndio mbinu Yake ya haraka zaidi ya kuondoa kabisa binadamu au kitu. Kuwachoma watu wa Sodoma kuliangamiza zaidi ya miili yao ya nyama; kuliangamiza uzima wa roho zao, nafsi zao na miili yao, na kuhakikisha kwamba watu waliokuwa ndani ya mji wangekoma kuwepo kwenye ulimwengu wa anasa na hata ulimwengu usioonekana na mwanadamu. Hii ni njia mojawapo ambayo Mungu hufichua na kuonyesha hasira Yake. Mfano huu wa ufunuo na maonyesho ni kipengele kimoja cha dutu ya ghadhabu ya Mungu, kama vile ilivyo kwa kawaida pia ufunuo wa kiini cha tabia ya haki ya Mungu. Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake, Anaacha kufichua rehema au wema wowote, na wala haonyeshi tena uvumilivu au subira Yake; hakuna mtu, kitu au sababu inayoweza kumshawishi kuendelea kuwa na subira, kutoa rehema Zake tena, na kumpa binadamu uvumilivu wake kwa mara nyingine. Badala ya mambo haya, bila kusita hata kidogo, Mungu atashusha hasira Yake na adhama, kufanya kile Anachotamani, na Atafanya mambo haya kwa haraka na kwa njia safi kulingana na matamanio Yake binafsi. Hii ndiyo njia ambayo Mungu hushusha hasira na adhama Yake, ambavyo binadamu hatakiwi kuvikosea, na pia ni maonyesho ya kipengele kimoja cha tabia Yake ya haki. Wakati watu wanamshuhudia Mungu akionyesha wasiwasi na upendo kwa binadamu, hawawezi kugundua hasira Yake, kuona ukuu Wake au kuhisi kutovumilia Kwake kosa. Mambo haya siku zote yamewaongoza watu kusadiki kwamba tabia ya haki ya Mungu ni ile ya huruma, uvumilivu na upendo tu. Hata hivyo, wakati mtu anapoona Mungu akiuangamiza mji au akichukia binadamu, hasira Yake katika kuangamiza binadamu na adhama Yake huruhusu watu kuona kidogo upande ule mwingine wa tabia Yake ya haki. Huku ni kutovumilia kosa kwa Mungu. Tabia ya Mungu ambayo haivumilii kosa lolote inapita fikira za kiumbe chochote kilichoumbwa, na miongoni mwa viumbe visivyoumbwa, hakuna chenye uwezo wa kuiingilia au kuiathiri; hata zaidi, haiwezi kughushiwa au kuigwa. Kwa hivyo, kipengele hiki cha tabia ya Mungu ndicho ambacho cha tabia ya Mungu ndicho ambacho binadamu anafaa kukijua zaidi. Ni Mungu Mwenyewe Pekee ndiye aliye na aina hii ya tabia, na Mungu Mwenyewe pekee ndiye anayemiliki aina hii ya tabia. Mungu anamiliki aina hii ya tabia kwa sababu Anachukia maovu, giza, maasi na vitendo viovu vya Shetani—vya kuwapotosha na kuwaangamiza wanadamu—kwa sababu Anachukia vitendo vyote vya dhambi vinavyompinga Yeye na kwa sababu ya kiini Chake kitakatifu na kiisicho na doa. Ni kwa sababu ya hali ndiyoHataacha viumbe vyovyote kati ya vile vilivyoumbwa au ambavyo havikuumbwa vimpinge waziwazi au kushindana na Yeye. Hata mtu ambaye Aliwahi kumwonea huruma, au wale ambao Aliwachagua, endapo tu wataikasirisha tabia Yake na kukiuka kanuni Zake za subira na uvumilivu, Yeye bila huruma na bila kusita Ataachilia na kufichua tabia Yake ya haki ambayo haiwezi kuvumilia kosa lolote.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 108)

Hasira ya Mungu Ni Usalama wa Nguvu Zote za Haki na Mambo Yote Mazuri

Mungu kutoweza kuvumilia kosa ndicho kiini Chake cha kipekee; hasira ya Mungu ndiyo tabia Yake ya kipekee; ukuu wa Mungu ndiyo kiini Chake cha kipekee. Kanuni inayoelezea ghadhabu ya Mungu inaonyesha utambulisho na hadhi ambayo Yeye tu ndiye anayemiliki. Ni dhahiri kwamba pia ni ishara ya hali halisi ya Mungu Mwenyewe wa kipekee. Tabia ya Mungu ni asili Yake Mwenyewe, ambayo haibadiliki hata kidogo na kupita kwa wakati, na wala haibadilishwi na mabadiliko ya eneo la kijiografia. Tabia Yake ya asili ndiyo kiini Chake halisi cha kweli. Bila kujali ni nani Anayemfanyia kazi Yake juu yake, kiini Chake hakibadiliki, na wala tabia Yake ya haki haibadiliki. Wakati mtu anapomghadhibisha Mungu, kile Anachomshushia ni tabia Yake ya asili; wakati huu kanuni inayoelezea ghadhabu Yake haibadiliki, wala utambulisho na hadhi Yake ya kipekee. Haghadhibishwi kwa sababu ya mabadiliko katika kiini Chake au kwa sababu ya tabia Yake kusababisha dalili tofauti, lakini ni kwa sababu upinzani wa binadamu dhidi Yake huikosea tabia Yake. Uchochezi waziwazi wa binadamu kwa Mungu ni changamoto kubwa katika utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu. Kwa mtazamo wa Mungu, wakati binadamu anapompinga Yeye, binadamu huyo anashindana na Yeye na anaijaribu ghadhabu Yake. Wakati binadamu anapompinga Mungu, wakati binadamu anaposhindana na Mungu, wakati binadamu anapoijaribu mara kwa mara ghadhabu ya Mungu—na pia wakati ambapo dhambi inaenea—ghadhabu ya Mungu itaweza kufichuka kwa kawaida na kujitokeza yenyewe. Kwa hivyo, maonyesho ya Mungu ya hasira Yake yanaashiria kwamba nguvu zote za maovu zitakoma kuwepo; yanaashiria kwamba nguvu zote za adui zitaangamizwa. Huu ndio upekee wa tabia ya haki ya Mungu, na ndio upekee wa hasira ya Mungu. Wakati heshima na utakatifu wa Mungu unapopingwa, wakati nguvu za haki zinapozuiliwa na kutoonekana na binadamu, Mungu atashusha hasira Yake. Kwa sababu ya kiini cha Mungu, nguvu hizo zote ulimwenguni zinazoshindana na Mungu, zinazompinga Yeye na zinapozuiliwa na kutoonekana na zinamilikiwa na Shetani. Kwa sababu Mungu ni wa haki, wa nuru na mtakatifu Asiye na dosari, vitu vyote viovu, vilivyopotoka na vinavyomilikiwa na Shetani vitatoweka baada ya kuachiliwa kwa hasira ya Mungu.

Ingawa kumwagwa kwa hasira ya Mungu ni kipengele kimojawapo cha onyesho la tabia Yake ya haki, hasira ya Mungu kwa vyovyote vile haibagui walengwa wake au isiyo na kanuni. Kinyume cha mambo ni kwamba, Mungu si mwepesi wa hasira hata kidogo, na wala Yeye hakimbilii kufichua ghadhabu Yake na ukuu Wake kirahisi. Aidha, hasira ya Mungu inadhibitiwa na kupimwa kwa kiwango fulani; hailinganishwi kamwe na namna ambavyo binadamu atakavyowaka kwa hasira kali au kutoa ghadhabu zake. Mazungumzo mengi kati ya binadamu na Mungu yamerekodiwa kwenye Biblia. Maneno ya baadhi ya watu hawa binafsi yalikuwa ya juujuu, yasiyo na ujuzi na yasiyofaa, lakini Mungu hakuwaangusha chini, wala Hakuwashutumu. Hususan, wakati wa majaribio ya Ayubu, je, Yehova Mungu aliwachukuliaje marafiki watatu wa Ayubu na wale wengine baada ya Yeye kusikia maneno waliyomwambia Ayubu? Je, Aliwashutumu? Je, Aligeuka na kushikwa na hasira kali kwao? Hakufanya kitu kama hicho! Badala yake Alimwambia Ayubu aweze kusihi kwa niaba yao na kuwaombea, na Mungu Mwenyewe hakuyachukua makosa yao moyoni Mwake. Matukio haya yote yanawakilisha mtazamo wa kimsingi ambao Mungu huwachukulia binadamu waliopotoka, na wasiojua. Kwa hivyo, kuachiliwa kwa ghadhabu ya Mungu si onyesho la hali Yake, wala si njia Yake ya kuonyesha hisia Zake. Hasira ya Mungu si mlipuko mkubwa wa hasira kali kama vile binadamu anavyoielewa. Mungu haachilii hasira Yake kwa sababu hawezi kuidhibiti hali ya moyo Wake binafsi au kwa sababu ghadhabu Yake imefikia kilele na lazima itolewe. Kinyume cha mambo ni kwamba, hasira Yake ni maonyesho na udhihirisho kamili wa tabia Yake ya haki, na ni ishara ya ufunuo wa kiini Chake kitakatifu. Mungu ni mwenye hasira, Asiyevumilia kukosewa—hivi si kusema kwamba ghadhabu ya Mungu haitofautishi sababu za kufanya hivyo au haifuati kanuni; ni binadamu waliopotoka ambao wana umiliki wa kipekee wa kutokuwa na kanuni, mlipuko wa hasira kali bila mpango usiotofautisha hali hii kati ya sababu mbalimbali. Mara tu binadamu anapokuwa na hadhi, mara nyingi atapata ugumu wa kudhibiti hali ya moyo wake, na kwa hivyo atafurahia kutumia nafasi mbalimbali kueleza kutotosheka kwake na kutoa nje hisia zake; mara nyingi atawaka kwa hasira kali bila sababu yoyote, ili kuonyesha uwezo wake na kuwafanya wengine kujua kwamba hadhi yake na utambulisho wake ni tofauti na ule wa watu wa kawaida. Bila shaka, watu waliopotoka wasiokuwa na hadhi yoyote mara kwa mara pia watapoteza udhibiti wao. Ghadhabu yao mara nyingi husababishwa na uharibifu wa manufaa yao ya kibinafsi. Ili kulinda hadhi yake binafsi na heshima, mara kwa mara atatoa nje hisia zake na kufichua asili yake yenye kiburi. Mwanadamu atawaka kwa hasira na kutoa hisia zake ili kutetea na kudumisha uwepo wa dhambi, na vitendo hivi ni njia ambazo mwanadamu huonyesha kutoridhika kwake; wamejawa na uchafu, njama na fitina, upotovu na uovu wa wanadamu, na zaidi ya kitu kingine chochote, wamejawa na malengo na tamaa mbaya za wanadamu. Wakati haki inaposhindana na maovu, hasira ya mwanadamu haitawaka ili kutetea uwepo wa haki; kinyume chake ni kwamba, wakati nguvu za haki zinatishwa, zinateswa na kushambuliwa, mtazamo wa binadamu ni ule wa kutotilia maanani, kukwepa, au kuliondoa. Hata hivyo, wakati anapokabiliwa na nguvu za maovu, mtazamo wa binadamu ni ule wa kutunza, na kunyenyekea mno. Hivyo basi, mwanadamu anapolipukwa na hasira ni kimbilio la nguvu za maovu, maonyesho ya mwenendo wa maovu uliokithiri na usiozuilika kwa mwandamu. Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake, hata hivyo, nguvu zote za maovu zitasitishwa; dhambi zote zinazomdhuru mwanadamu zitasitishwa; nguvu zote za uadui zinazozuia kazi ya Mungu zitawekwa wazi, zitatenganishwa na kulaaniwa; washirika wote wa Shetani ambao wanampinga Mungu wataadhibiwa, na kuondolewa. Badala yake, kazi ya Mungu itaendelea huru bila vizuizi vyovyote; mpango wa usimamizi wa Mungu utaendelea kuimarika hatua kwa hatua kulingana na utaratibu uliopo; na watu walioteuliwa na Mungu watakuwa huru dhidi ya kusumbuliwa na Shetani na kupotshwa naye; wale wanaomfuata Mungu watafurahia uongozi na ruzuku ya Mungu katika mazingira yenye utulivu na amani. Hasira ya Mungu ni ulinzi unaozuia nguvu zote za maovu dhidi ya kuzidishwa na kuenezwa kwa nguvu, na pia ni ulinzi unaolinda kuwepo na kuenezwa kwa mambo yote ya haki na mazuri na daima dawamu unayalinda mambo haya dhidi ya kukandamizwa na kuangamizwa.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 109)

Hasira ya Mungu Ni Usalama wa Nguvu Zote za Haki na Mambo Yote Mazuri

Je, unaweza kuona kiini cha ghadhabu ya Mungu katika kuangamiza Kwake Sodoma? Je, kuna kitu chochote kililochanganyika kwenye hasira Yake kali? Je, hasira kali ya Mungu ni safi? Kwa kutumia maneno ya kibinadamu, je, hasira kali ya Mungu imetiwa unajisi? Je, kunayo hila yoyote katika hasira Yake? Je, kuna njama yoyote? Je, kuna siri yoyote iliyofichwa? Ninaweza kukuambia kwa uwazi na kwa kweli: Hakuna sehemu yoyote ya ghadhabu ya Mungu ambayo inaweza kumsababishia mtu kuitilia shaka. Ghadhabu yake haina kasoro, ni hasira ambayo haijatiwa unajisi na haina nia au kusudi lingine lolote. Sababu zilizo nyuma ya ghadhabu Yake ni safi, hazina lawama na haziwezi kukosolewa. Ni ufunuo wa asili na onyesho la kiini Chake kitakatifu; ni kitu ambacho hakuna hata kiumbe kimoja kilichoumbwa kinachoimiliki. Hii ni sehemu ya kipekee ya tabia ya haki ya Mungu, na pia ni tofauti kubwa kati ya kiini cha Muumba na viumbe vilivyoumbwa.

Haijalishi kama mtu anakuwa na ghadhabu akiwa mbele ya wengine au wakiwa hawako naye, kila mtu anayo nia na kusudi tofauti. Pengine wanajenga heshima zao, au pengine wanatetea masilahi yao binafsi, na kuendeleza taswira zao au kulinda sura zao. Baadhi yao huendeleza hali ya kuzuia ghadhabu yao, huku nao wengine wanakimbilia na wanapandwa na hasira kali kila wanapotaka bila kujizuia hata kidogo. Kwa ufupi, ghadhabu ya binadamu inatokana na tabia yake iliyopotoka. Haijalishini kusudi gani, ni la mwili na ni la asili; halina uhusiano wowote na haki au ukiukaji wa haki kwa sababu hakuna kitu katika asili ya binadamu na kiini chake ambacho kinalingana na ukweli. Kwa hivyo, hasira ya binadamu wapotovu na hasira ya Mungu vyote havifai kutajwa kwa kiwango sawa. Bila ubaguzi, tabia ya mwanadamu aliyepotoshwa na Shetani huanza na tamanio la kulinda upotovu, na kwa hakika ina msingi katika upotovu; hii ndiyo sababu, hasira ya mwanadamu haiwezi kutajwa kwa kiwango sawa na ghadhabu ya Mungu, haijalishi jinsi hasira ya mwanadamu inaweza kuonekana kinadharia. Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake kali, nguvu za uovu hudhibitiwa, mambo ya giza yanaangamizwa, huku mambo ya haki na mazuri yakifurahia utunzaji wa Mungu, ulinzi, na yote yanaruhusiwa kuendelea. Mungu hushusha hasira Yake kwa sababu ya mambo dhalimu, mabaya na ya giza, yanayozuia, yanayotatiza au kuangamiza shughuli na maendeleo ya kawaida ya mambo ya haki na mazuri. Lengo la hasira ya Mungu si kulinda hadhi na utambulisho Wake mwenyewe, bali ni kulinda uwepo wa mambo ya haki, mazuri, ya kupendeza na kuvutia, ili kulinda sheria na mpangilio wa kuwepo kwa kawaida kwa binadamu. Hiki ndicho chanzo asilia cha hasira ya Mungu. Hasira kali ya Mungu ni ufunuo sahihi sana wa asili na ufunuo wa kweli wa tabia Yake. Hakuna nia potovu katika ghadhabu Yake, na wala hakuna udanganyifu au njama zozote, achilia mbali tamaa, hila, udhalimu, vurugu, uovu au tabia zingine zozote ambazo binadamu wote waliopotoka huwa nazo. Kabla ya Mungu kushusha hasira Yake kali, huwa tayari Ametambua kiini cha kila suala kwa uwazi na ukamilifu zaidi, na huwa tayari Amepangilia ufafanuzi na hitimisho sahihi na zilizo wazi. Hivyo basi, lengo la Mungu katika kila kitu Anachofanya ni wazi kabisa, kama vile ulivyo mtazamo Wake. Yeye si mtu aliyechanganyikiwa; Yeye si kipofu; Yeye si mtu wa kuamua ghafla; Yeye si mzembe; na zaidi, Yeye si mtu asiyefuata kanuni. Hiki ndicho kipengele cha kivitendo cha ghadhabu ya Mungu, na ni kwa sababu ya kipengele hiki cha kivitendo cha ghadhabu ya Mungu kwamba ubinadamu umefikia uwepo wake wa kawaida. Bila ya hasira ya Mungu, binadamu wangeishia kuishi katika mazingira yasiyo ya kawaida; viumbe vyote vyenye haki, vyema na vizuri vingeangamizwa na kukoma kuwepo. Bila ya hasira ya Mungu, sheria na amri za kuwepo kwa viumbe vingekiukwa au hata kupinduliwa kabisa. Tangu uumbwaji wa binadamu, Mungu ameendelea kutumia tabia Yake ya haki ili kulinda na kudumisha maisha ya kawaida ya binadamu. Kwa sababu tabia Yake ya haki inayo hasira na uadhama, watu wote waovu, mambo, vifaa na vitu vyote vinavyotatiza na kuharibu uwepo wa kawaida wa binadamu vinaadhibiwa, vinadhibitiwa na kuangamizwa kwa sababu ya hasira Yake. Katika kipindi cha milenia kadhaa zilizopita, Mungu ameendelea kutumia tabia Yake ya haki kuangusha na kuangamiza kila aina za roho chafu na za giza ambazo zinampinga Mungu na ambao wanachukua nafasi ya wasaidizi na watumishi wa Shetani katika kazi ya Mungu ya kuwasimamia binadamu. Hivyo basi, kazi ya Mungu ya wokovu wa binadamu siku zote imeimarika kulingana na mpango Wake. Hivi ni kusema kwamba kwa sababu ya uwepo wa hasira ya Mungu, sababu za haki zaidi miongoni mwa wanadamu hazijawahi kuharibiwa.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 110)

Ingawa Shetani Anaonekana Mwenye Utu, Haki na Maadili, Ni Mkatili na Mwovu katika Kiini Chake

Shetani hupata umaarufu wake kupitia kwa kuwadanganya watu. Mara nyingi hujiweka kama kiongozi na kuchukua wajibu wa kielelezo cha haki. Akisingizia kuwa anatetea haki, anaishia kumdhuru binadamu, kudanganya nafsi zao, na kutumia mbinu zote ili kuweza kuteka nyara hisia na fikira za binadamu, kuwapotosha na kuwachochea. Shabaha yake ni kumfanya binadamu aidhinishe na kuufuata mwenendo wake wa maovu, kumfanya binadamu kujiunga naye katika kupinga mamlaka na ukuu wa Mungu. Hata hivyo, wakati mtu anapokuwa mwerevu na kutambua njama zake, mipango na sifa zake hizo na hataki kuendelea kudhalilishwa na kudanganywa naye hivyo au kuendelea kuwa mtumwa wa Shetani, au kuadhibiwa na kuangamizwa pamoja na Shetani, Shetani naye hubadilisha sifa zake za awali za kuwa mwema na kuondoa baraka zake bandia ili kufichua uso wake wa kweli wenye maovu, ubaya, sura mbaya na wa kikatili. Shetani hawezi kupenda jambo lolote isipokuwa kuwaangamiza wale wote wanaokataa kumfuata yeye na wale wanaopinga nguvu zake za giza. Wakati huu Shetani hawezi tena kuvaa sura ya uaminifu, na utulivu; badala yake, sifa zake za kweli za sura mbaya na za kishetani zilizokuwa zimefichwa kwenye mavazi ya kondoo zinafichuliwa. Mara tu njama za Shetani zinapomulikwa, na sifa zake za kweli kufichuliwa, yeye huingia kwenye hisia za hasira kali na kuonyesha ukatili wake; tamanio lake la kuwadhuru na kuwameza watu ndipo litazidi zaidi. Anakasirika kwasababu ya mwamko wa mwanadamu katika kufuata ukweli; anataka kuwa na kisasi kingi dhidi ya binadamu kwa maazimio yake ya kutamani kuwa na uhuru na nuru na kutokuwa mateka katika gereza lake. Hasira yake kali inanuiwa kutetea maovu yake, na pia ni ufunuo wa kweli wa asili yake ya kikatili.

Katika kila suala, tabia ya Shetani hufichua asili yake ya uovu. Kati ya matendo yote maovu ambayo Shetani ameyafanya juu ya mwanadamu—kuanzia kwa jitihada zake za awali za kumdanganya binadamu ili aweze kumfuata, hadi unyonyaji wake wa binadamu, ambapo anamkokota binadamu hadi kwenye matendo maovu, hadi ulipizaji wa kisasi wa Shetani kwa binadamu baada ya sifa zake za kweli kuweza kufichuliwa na binadamu kuweza kumtambua na kumwacha—hakuna hata kimoja kati ya vitendo hivi kinachoshindwa kufichua kiini kiovu cha Shetani; hakuna hata kimoja kinachoshindwa kuthibitisha ukweli kwamba Shetani hana uhusiano na mambo mazuri; hakuna hata kimoja kinachoshindwa kuthibitisha kwamba Shetani ndiye chanzo cha mambo yote maovu. Kila mojawapo ya matendo yake inayalinda maovu yake, inadumisha uendelevu wa vitendo vyake viouvu inaenda kinyume cha haki na mambo mazuri, inaharibu sheria na mpangilio wa uwepo wa kawaida wa binadamu. Matendo haya ya Shetani ni uadui kwa Mungu, na yataangamizwa na ghadhabu ya Mungu. Ingawa Shetani anayo hasira yake kali, hasira yake ni njia tu ya kudhihirisha asili yake mbaya. Sababu inayomfanya Shetani akasirike na kuwa mkali ni kwa sababu njama zake zilizofichika zimefichuliwa; mipango yake haiwezi tena kufanikiwa kwa urahisi; malengo yake ya kijinga na tamaa yake mbaya ya kuchukua nafasi ya Mungu na kujifanya kuwa Mungu, vyote vimekwama na kuzuiliwa; shabaha yake ya kudhibiti binadamu wote imeishia patupu na haiwezi tena kutimizwa. Kuitisha kwa Mungu hasira Yake mara kwa mara ndiko kumesitisha mipango ya Shetani dhidi ya kukamilika na kukatiza kuenea na kusambaa kwa maovu ya Shetani; kwa hivyo, Shetani anaogopa na kuchukia hasira ya Mungu. Kila wakati ambao hasira ya Mungu inaachiliwa huwa haifichui tu sura ya kweli ya Shetani iliyo mbaya; bali pia inafichua na kuweka wazi tamaa mbaya ya Shetani. Wakati uo huo, sababu za hasira kali ya Shetani dhidi ya binadamu zinafichuliwa kabisa. Mlipuko wa hasira ya Shetani ni ufunuo wa kweli wa asili yake mbovu, ufichuzi wa njama zake. Bila shaka, kila wakati Shetani anapopandwa na hasira kali, huwa ni dalili ya maangamizo ya mambo maovu; huashiria ulinzi na mwendelezo wa mambo mazuri, na huashiria asili ya hasira ya Mungu—ile ambayo haiwezi kukosewa!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 111)

Mtu Hapaswi Kutegemea Uzoefu na Fikira Ili Kujua Tabia ya Haki ya Mungu

Ukijipata unakabiliwa na hukumu na kuadibiwa na Mungu, je, utasema kwamba neno la Mungu limeghushiwa? Je, utasema kwamba kunayo hadithi inayoelezea kuhusu ghadhabu ya Mungu, na kwamba ghadhabu Yake imetiwa unajisi? Je, utamchafulia Mungu jina, ukisema kwamba tabia Yake si ya haki kwa ujumla? Wakati unaposhughulikia kila mojawapo ya vitendo vya Mungu, lazima uwe na uhakika kwamba tabia ya haki ya Mungu iko huru dhidi ya vipengele vingine vyovyote, kwamba ni takatifu na haina dosari; vitendo hivi vinajumuisha binadamu kuweza kuangushwa chini, kuadhibiwa na kuangamizwa na Mungu. Bila kuacha, kila kimojawapo cha vitendo vya Mungu kinatekelezwa kulingana na tabia yake ya asili na mpango Wake—hii haijumuishi maarifa ya binadamu, mila na falsafa—na kila kimojawapo cha vitendo vya Mungu ni maonyesho ya tabia Yake na kiini Chake, kisichohusiana na chochote kinachomilikiwa na binadamu aliyepotoka. Mwanadamu ana dhana kwamba upendo, huruma na uvumilivu wa Mungu pekee kwa binadamu ndivyo visivyokuwa na dosari, visivyoghoshiwa na vilivyo vitakatifu. Hata hivyo, hakuna anayejua kwamba ghadhabu ya Mungu na hasira Yake vilevile vyote havijatiwa unajisi; aidha, hakuna yule aliyefikiria maswali kama vile: kwa nini Mungu havumilii kosa lolote au kwa nini ghadhabu Yake ni kubwa mno. Kinyume ni kwamba, baadhi ya watu hukosa kuelewa hasira ya Mungu na kudhania kuwa ni hasira kali sawa na ile ya binadamu waliopotoka: wanaelewa ghadhabu ya Mungu kuwa ni sawa na hasira za binadamu waliopotoka; wao hata hudhania kimakosa kwamba ghadhabu ya Mungu ni sawa tu na ufunuo wa kiasili wa tabia potovu ya binadamu. Wanasadiki kimakosa kwamba ghadhabu ya Mungu inapoachiliwa ni sawa tu na ghadhabu ya binadamu waliopotoka, jambo linalotokana na kutoridhika; wanasadiki hata kwamba Mungu anapoachilia ghadhabu Yake ni maonyesho ya hali Yake ya moyo. Baada ya ushirika huu, Ninatumai kwamba kila mmoja wenu hatakuwa tena na shaka, fikira au kukisia kuhusiana na tabia ya haki ya Mungu, na Natumai baada ya kusikiliza maneno Yangu mnaweza kuwa na utambuzi wa kweli wa ghadhabu ya tabia ya haki ya Mungu katika mioyo yenu, kwamba mnaweza kuweka kando ufahamu wowote potofu wa hapo awali kuhusiana na ghadhabu ya Mungu, na kwamba mnaweza kubadilisha imani zenu zilizopotoka na maoni yenu potovu kuhusiana na kiini cha ghadhabu ya Mungu. Vilevile, Natumai kwamba mnaweza kuwa na ufafanuzi sahihi wa tabia ya Mungu katika mioyo yenu, kwamba hamtakuwa tena na mashaka yoyote kuhusiana na tabia ya haki ya Mungu, na kwamba hamtaweka mawazo ama fikira zozote za kibinadamu kuhusiana na tabia ya kweli ya Mungu. Tabia ya haki ya Mungu ni kiini cha kweli cha Mungu mwenyewe. Si kitu kilichotungwa au kuundwa na binadamu. Tabia Yake ya haki ni tabia Yake na haina uhusiano au muunganiko wowote na kiumbe chochote kilichoumbwa. Mungu Mwenyewe ni Mungu Mwenyewe. Hatawahi kuwa sehemu ya uumbaji, na hata kama Atakuwa mwanachama miongoni mwa viumbe vilivyoumbwa, tabia Yake ya asili na kiini Chake havitabadilika. Hivyo basi, kumjua Mungu si sawa na kujua kitu; kumjua Mungu si kuchunguza kitu, na wala si sawa na kumwelewa mtu. Kama mwanadamu atatumia dhana au mbinu yake ya kujua kifaa au kumwelewa mtu ili kumjua Mungu, basi hutawahi kuweza kutimiza maarifa ya Mungu. Kumjua Mungu hakutegemei uzoefu au kufikiria kwako, na hivyo basi hufai kulazimisha uzoefu wako au kufikiria kwako kwa Mungu. Haijalishi uzoefu au kufikiria kwako ni kwa kipekee namna gani, huko kote bado ni finyu; na hata zaidi, kufikiria kwako hakulingani na hoja, isitoshe hakulingani na ukweli, na pia hakulingani na tabia na kiini cha kweli cha Mungu. Hutawahi kamwe kufanikiwa kama utategemea mawazo yako ili kuelewa kiini cha Mungu. Njia ya pekee ni hii: kukubali yote yanayotoka kwa Mungu, kisha kwa utaratibu uweze kuyapitia na kuyaelewa. Kutakuwa na siku ambayo Mungu atakupa nuru ili uweze kuelewa kwa kweli na kumjua Yeye kwa sababu ya ushirikiano wako na kwa sababu ya njaa na kiu yako ya kupenda ukweli.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 112)

Binadamu Hupata Huruma na Uvumilivu wa Mungu Kupitia kwa Toba ya Dhati

Onyo la Yehova Mungu Lawafikia Waninawi

Hebu tuendelee hadi kwenye fungu la nne, sura ya tatu ya kitabu cha Yona: “Naye Yona akaanza kuingia ndani ya mji huo safari ya siku moja, na akatoa sauti kubwa, na kusema, Imebaki siku arobaini, na Ninawi utashindwa.” Haya ndiyo maneno ambayo Mungu alipitisha moja kwa moja kwake Yona ili aweze kuwaambia Waninawi. Bila shaka, haya ndiyo maneno ambayo Yehova alipenda kusema kwa Waninawi. Maneno haya yanatwambia kwamba Mungu alianza kukerwa na kuchukizwa na watu wa mji huu kwa sababu ya maovu yao yaliyokuwa yamefika machoni pa Mungu, na hivyo basi, Alitaka kuuangamiza mji huo. Hata hivyo, kabla ya Mungu kuuangamiza mji, Aliwatangazia Waninawi, na hapo kwa hapo Akawapa fursa ya kutubu maovu yao na kuanza upya. Fursa hii ingedumu kwa siku arubaini. Kwa maneno mengine, kama watu waliokuwa ndani ya mji huu wasingetubu, na kukubali dhambi au maovu yao wenyewe na kusujudu mbele ya Yehova Mungu ndani ya siku arubaini, Mungu angeangamiza mji huu kama Alivyoangamiza Sodoma. Hivi ndivyo ambavyo Yehova Mungu alipenda kuwaambia watu wa Ninawi. Ni wazi kwamba, hili halikuwa tangazo rahisi. Halikuweza tu kuonyesha hasira ya Yehova Mungu, lakini pia lilionyesha mtazamo Wake kwa wale Waninawi; wakati uo huo tangazo hili rahisi lilitumika kama onyo kali kwa watu waliokuwa wakiishi ndani ya mji huo. Onyo hili liliwaambia kwamba matendo yao maovu yalikuwa yamewafanya kuchukiwa na Yehova Mungu na liliwaambia kwamba matendo yao maovu yangewaleta kwenye ukingo wa maangamizo yao wenyewe; kwa hivyo, maisha ya kila mmoja kule Ninawi yalikuwa karibu kuangamia.

Tofauti Kubwa Iliyopo Kati ya Mwitikio wa Ninawi na Sodoma kwa Onyo la Yehova Mungu

Kupinduliwa kunamaanisha nini? Kwa muktadha wa mazungumzo, kunamaanisha kutoweka. Lakini kwa njia gani? Ni nani angefanya mji mzima kupinduliwa? Haiwezekani kwa binadamu kufanya kitendo kama hicho, bila shaka. Watu hawa hawakuwa wajinga; mara tu waliposikia matangazo haya, walipata wazo hilo. Walijua kwamba yalikuwa yametoka kwa Mungu; walijua kwamba Mungu angetekeleza kazi Yake; walijua kwamba maovu yao yalikuwa yamemkasirisha Yehova Mungu na kwa hivyo hasira ya Yehova Mungu ikawajia, na Alitaka kuwaangamiza wao pamoja na mji wao. Je, watu wa mji huo walichukulia vipi suala hilo baada ya kusikiliza onyo la Yehova Mungu? Biblia inafafanua kwa undani namna ambavyo watu hawa walivyoitikia, kuanzia kwa mfalme wao hadi kwa binadamu wa kawaida. Kama ilivyorekodiwa kwenye Maandiko: “Basi watu wa hapo Ninawi wakamwamini Mungu, na wakatangaza mfungo, na wakavalia nguo za magunia, kuanzia aliyekuwa mkubwa zaidi kwao mpaka aliyekuwa mdogo zaidi. Kwa kuwa habari ilimfikia mfalme wa Ninawi, na akainuka kutoka kwa kiti chake che enzi, na akaivua nguo yake, na kuvaa nguo ya gunia, na kukaa chini katika majivu. Na akafanya kutangazwe Ninawi kupitia amri yake mfalme na wakubwa wake, ikisema, Mtu wala mnyama, wala kundi la ng’ombe, wala kundi la kondoo wasionje chochote: wasikule, wala kunywa maji: Ila mwanadamu na mnyama wavikwe kwa nguzo za magunia, na kulia kwa nguvu kwa Mungu: ndiyo, na wawageuze watu wote kutoka kwa njia ovu, na kutoka kwa vurugu iliyo mikononi mwao. …”

Baada ya kusikia tangazo la Yehova Mungu, watu wa Ninawi walionyesha mtazamo uliokuwa kinyume kabisa na ule wa watu wa Sodoma—watu wa Sodoma walimpinga Mungu waziwazi, huku wakiendelea kuongeza uovu kwa uovu, lakini baada ya kusikia maneno haya, Waninawi hawakupuuza suala hilo, wala hawakuweza kulipinga; badala yake walimsadiki Mungu na kutangaza kufunga. “Walisadiki” inarejelea nini hapa? Neno lenyewe linamaanisha imani na unyenyekevu. Kama tutatumia tabia halisi ya Waninawi kuelezea neno hili, inamaanisha kwamba waliamini Mungu anaweza na angeweza kufanya vile Alivyosema, na kwamba walikuwa radhi kutubu. Je, watu wa Ninawi walihisi hofu mbele ya janga lililokuwa karibu kutokea? Imani yao ndiyo iliyotia hofu katika mioyo yao. Kwa kweli, ni nini tunachoweza kutumia kuthibitisha Imani na hofu ya Waninawi? Ni sawa na vile Biblia inavyosema: “na wao wakatangaza kufunga, na wakavalia nguo za magunia, kuanzia wale walio wakubwa zaidi na hata kwa wale walio wadogo zaidi.” Hivi ni kusema kwamba Waninawi waliamini kweli, na kwamba kutoka kwenye imani hii hofu iliibuka, ambayo sasa ilisababisha kufunga na kuvaliwa kwa nguo za magunia. Hivi ndivyo walivyoonyesha mwanzo wa toba yao. Tofauti kabisa na watu wa Sodoma, Waninawi hawakumpinga Mungu tu, bali walionyesha pia waziwazi toba yao kupitia kwa tabia na matendo yao. Bila shaka, hii haikutumika tu kwa watu wa kawaida wa Ninawi; hata mfalme wao hakubakizwa.

Toba ya Mfalme wa Ninawi Inapata Sifa ya Yehova Mungu

Wakati mfalme wa Ninawi alipozisikia habari hizi, aliinuka kutoka kwenye kiti chake cha enzi, akavua nguo zake, akavalia nguo za magunia na kukalia jivu. Kisha akatangaza kwamba hakuna mtu kwenye mji huo ambaye angeruhusiwa kuonja chochote, na kuwa hakuna mifugo, wanakondoo na ng’ombe ambao wangekunywa maji na kula nyasi. Binadamu na mifugo kwa pamoja walitakikana kujifunika nguo za magunia; nao watu wangemsihi Mungu kwa uaminifu. Mfalme pia alitangaza kwamba watu wote wangetupilia mbali njia zao za maovu na kukataa udhalimu ulioko mikononi mwao. Tukifanya uamuzi kutoka kwenye misururu ya vitendo hivi, mfalme wa Ninawi alionyesha toba yake ya dhati. Misururu ya vitendo alivyovifanya—kutoka kwenye kiti chake cha ufalme, kulitupa joho lake la kifalme, kuvalia nguo za magunia na kukalia majivu—kulionyesha watu kwamba mfalme wa Ninawi aliweka kando hadhi yake ya kifalme na kuvalia nguo za magunia pamoja na watu wa kawaida wa nchi. Hii ni kusema kwamba mfalme wa Ninawi hakuweza kushikilia wadhifa wake wa kifalme ili aendelee na njia zake za maovu au udhalimu katika mikono yake baada ya kusikia tangazo kutoka kwa Yehova Mungu; badala yake, aliweka pembeni mamlaka aliyoyashikilia na kutubu mbele za Yehova Mungu. Kwenye kipindi hiki cha muda, mfalme wa Ninawi hakuwa akitubu akiwa mfalme; alikuwa amekuja mbele za Mungu kuungama na kutubu dhambi zake akiwa kama binadamu wa kawaida wa Mungu. Aidha, aliuambia mji mzima kuungama na kutubu dhambi zao mbele za Yehova Mungu kwa njia sawa na yeye; vilevile, alikuwa na mpango mahususi wa namna ya kufanya hivyo kama inavyoonekana kwenye Maandiko: “Mtu wala mnyama, wala kundi la ng’ombe, wala kundi la kondoo wasionje chochote: wasikule, wala kunywa maji: … na kulia kwa nguvu kwa Mungu: ndiyo, na wawageuze watu wote kutoka kwa njia ovu, na kutoka kwa vurugu iliyo mikononi mwao.” Kama kiongozi wa mji, mfalme wa Ninawi alimiliki hadhi na nguvu za kimamlaka na angefanya chochote alichopenda. Alipokabiliwa na tangazo la Yehova Mungu, angeweza kupuuza suala hilo au kutubu na kuungama tu dhambi zake pekee; kuhusiana na kama watu wa mji wangechagua kutubu au la, angepuuza suala hili kabisa. Hata hivyo, mfalme wa Ninawi hakufanya hivyo kamwe. Mbali na kuinuka kutoka kwenye kiti chake cha enzi, kuvalia nguo za magunia na kujipaka majivu na kuungama na kutubu dhambi zake mbele za Yehova Mungu, aliweza pia kuwaamuru watu na mifugo ndani ya mji huo kufanya hivyo. Aliweza hata kuamuru watu “kumlilia Mungu kwa nguvu.” Kupitia misururu hii ya vitendo, mfalme wa Ninawi aliweza kukamilisha kwa kweli kile ambacho kiongozi anafaa kufanya; misururu ya vitendo vyake ndivyo vilivyokuwa vigumu kwa mfalme yeyote katika historia ya binadamu kuvitimiza, na kwa hakika, hakuna mfalme mwingine aliyewahi kufanikisha mambo haya. Matendo haya yanaweza kuitwa shughuli isiyo na kifani katika historia ya binadamu; yanastahili kukumbukwa na kuigwa na binadamu. Tangu mwanzo wa mwanadamu, kila mfalme alikuwa amewaongoza wafuasi wake kukinzana na kumpinga Mungu. Hakuna yule aliyewahi kuwaongoza wafuasi wake wamsihi Mungu ili kutafuta ukombozi kwa ajili ya maovu yao, kupokea msamaha wa Yehova Mungu na kuepuka adhabu kali. Mfalme wa Ninawi, hata hivyo, aliweza kuwaongoza raia wake kumlilia Mungu, kuacha njia zao mbalimbali za maovu na kutupilia mbali udhalimu ulio mikononi mwao. Aidha, aliweza pia kuweka kando kiti chake cha enzi, na badala yake, Yehova Mungu alibadilisha na kughairi na kugeuza hasira Yake, na kuwaruhusu watu wa mji huu kuishi na kuwalinda dhidi ya kuangamia. Matendo ya mfalme yanaweza kuitwa tu muujiza wa nadra katika historia ya binadamu; yanaweza hata kuitwa mfano wa kuigwa wa ubinadamu uliopotoka unaoungama na kutubu dhambi zao mbele za Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 113)

Yona 3 Neno lake Yehova likakuja kwake Yona kwa mara ya pili, likisema, Inuka, nenda Ninawi, mji huo mkuu; na uuhubirie mahubiri ninayokuambia. Kwa hivyo Yona akainuka, na kuenda Ninawi, kulingana na neno la Yehova. Sasa Ninawi ulikuwa mji mkuu wa safari ya siku tatu. Naye Yona akaanza kuingia ndani ya mji huo safari ya siku moja, na akatoa sauti kubwa, na kusema, Imebaki siku arobaini, na Ninawi utashindwa. Basi watu wa hapo Ninawi wakamwamini Mungu, na wakatangaza mfungo, na wakavalia nguo za magunia, kuanzia aliyekuwa mkubwa zaidi kwao mpaka aliyekuwa mdogo zaidi. Kwa kuwa habari ilimfikia mfalme wa Ninawi, na akainuka kutoka kwa kiti chake che enzi, na akaivua nguo yake, na kuvaa nguo ya gunia, na kukaa chini katika majivu. Na akafanya kutangazwe Ninawi kupitia amri yake mfalme na wakubwa wake, ikisema, Mtu wala mnyama, wala kundi la ng’ombe, wala kundi la kondoo wasionje chochote: wasikule, wala kunywa maji: Ila mwanadamu na mnyama wavikwe kwa nguzo za magunia, na kulia kwa nguvu kwa Mungu: ndiyo, na wawageuze watu wote kutoka kwa njia ovu, na kutoka kwa vurugu iliyo mikononi mwao. Nani anayejua iwapo Mungu atabadili na kughairi, na kuiacha ghadhabu Yake iliyo kali, ili tusiangamie? Naye Mungu aliona vitendo vyao, kwamba walikuwa wameiacha njia yao ovu; na Mungu akaghairi lile neno ovu, ambalo Alikuwa amesema Angeliwafanyia; na Aakulifanya.

Mungu Aona Kutubu kwa Dhati katika Vina vya Mioyo ya Waninawi

Baada ya kusikiliza tangazo la Mungu, mfalme wa Ninawi na raia Wake walitekeleza misururu ya vitendo. Je, ni nini asili ya tabia na matendo yao? Kwa maneno mengine, ni nini kiini cha mwenendo wao kwa ujumla wake? Kwa nini walifanya kile walichokifanya? Katika macho ya Mungu walikuwa wametubu kwa dhati, si tu kwa sababu walikuwa wamemsihi Mungu kwa dhati na kuungama dhambi zao mbele Yake, lakini pia kwa sababu walikuwa wameacha mwenendo wao wenye maovu. Walitenda kwa njia hii kwa sababu baada ya kusikia maneno ya Mungu, waliogopa sana na kuamini kwamba Angefanya kama Alivyosema. Kwa kufunga, kuvalia nguo za magunia na kuketi kwenye majivu, walipenda kuonyesha namna walivyokuwa radhi kubadilisha njia zao na kujizuia na maovu, kumwomba Yehova Mungu azuie hasira Yake, wakimsihi Yehova Mungu Atupilie mbali uamuzi Wake, pamoja na msiba mkuu ambao ulikuwa karibu kuwakabili. Kupitia uchunguzi wa tabia yao yote, tunaona ya kwamba tayari walielewa kwamba vitendo vyao vya awali vilimchukiza Yehova Mungu na kwamba walielewa sababu iliyomfanya kutaka kuwaangamiza hivi karibuni. Kwa sababu hizi, wote walipenda kutubu kabisa, kugeuka na kuacha njia zao za maovu na kuacha udhalimu ulio mikononi mwao. Kwa maneno mengine, pindi tu walipotambua tangazo la Yehova Mungu, wote walihisi woga katika mioyo yao; hawakuendelea tena na mwenendo wao wa maovu wala kuendelea kutenda vitendo ambavyo Yehova Mungu alivichukia. Vilevile, walimsihi Yehova Mungu kusamehe dhambi zao za kale na kutowatendea kulingana na vitendo vyao vya kale. Walikuwa radhi kutowahi kujihusisha tena katika maovu na kutenda kulingana na maagizo ya Yehova Mungu, ikiwa tu ingewezekana kutomkasirisha tena Yehova Mungu. Toba yao ilikuwa ya dhati na ya kweli. Ilitoka kwenye kina cha mioyo yao na haikuwa ya kunafiki, wala haikuwa ya muda.

Mara tu watu wote wa Ninawi, kuanzia mfalme hadi watu wa kawaida, walipojua kwamba Yehova Mungu alikuwa amewakasirikia, kila moja ya vitendo vyao, tabia zao zote, pamoja na kila uamuzi na uchaguzi walioufanya vilikuwa wazi na dhahiri mbele za Mungu. Moyo wa Mungu ulibadilika kulingana na tabia zao. Je, mtazamo wa Mungu ulikuwa ni upi kwa wakati huo? Biblia inaweza kukujibia swali hili. Maneno yafuatayo yalirekodiwa katika maandiko: “Naye Mungu aliona vitendo vyao, kwamba walikuwa wameiacha njia yao ovu; na Mungu akaghairi lile neno ovu, ambalo Alikuwa amesema Angeliwafanyia; na Hakulifanya.” Ingawa Mungu alibadilisha fikira Zake, hakukuwa na chochote kigumu kuhusu mtazamo wa fikira Zake. Aliweza kubadilika kutoka katika kuonyesha hasira Yake hadi kutuliza hasira Yake, na kisha kuamua kutouleta msiba mkuu katika mji wa Ninawi. Sababu ya uamuzi wa Mungu wa—kuwaokoa Waninawi dhidi ya msiba wao mkuu—ilikuwa ya haraka mno, ni kwa sababu Mungu aliangalia moyo wa kila mmoja wa wale Waninawi. Aliona kwamba katika kina cha mioyo yao waliweza: kuungama na kutubu kwa dhati dhambi zao, imani yao ya dhati kwake Yeye, hisia zao za kina za jinsi matendo yao maovu yalivyoikasirisha tabia Yake, na hofu iliyotokana na adhabu ya Yehova Mungu iliyokuwa inawakaribia. Wakati uo huo, Yehova Mungu aliweza kusikia maombi kutoka kwenye kina cha mioyo yao wakimsihi kusitisha hasira Yake dhidi yao ili waweze kuepuka msiba huu mkuu. Wakati Mungu alipoangalia hoja hizi zote, kwa utaratibu hasira yake ilitoweka. Licha ya vile hasira yake ilivyokuwa kubwa hapo awali, alipoona kutubu kwao kwa dhati ndani ya kina cha mioyo ya watu hawa, moyo Wake uliguswa na hili, na kwa hivyo Hakuweza kuvumilia kuwaletea msiba mkuu, na Alisitisha hasira yake kwao. Badala yake Aliendelea kuwaonyesha huruma Yake na uvumilivu kwao na akaendelea kuwaongoza na kuwakimu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 114)

Yona 3 Neno lake Yehova likakuja kwake Yona kwa mara ya pili, likisema, Inuka, nenda Ninawi, mji huo mkuu; na uuhubirie mahubiri ninayokuambia. Kwa hivyo Yona akainuka, na kuenda Ninawi, kulingana na neno la Yehova. Sasa Ninawi ulikuwa mji mkuu wa safari ya siku tatu. Naye Yona akaanza kuingia ndani ya mji huo safari ya siku moja, na akatoa sauti kubwa, na kusema, Imebaki siku arobaini, na Ninawi utashindwa. Basi watu wa hapo Ninawi wakamwamini Mungu, na wakatangaza mfungo, na wakavalia nguo za magunia, kuanzia aliyekuwa mkubwa zaidi kwao mpaka aliyekuwa mdogo zaidi. Kwa kuwa habari ilimfikia mfalme wa Ninawi, na akainuka kutoka kwa kiti chake che enzi, na akaivua nguo yake, na kuvaa nguo ya gunia, na kukaa chini katika majivu. Na akafanya kutangazwe Ninawi kupitia amri yake mfalme na wakubwa wake, ikisema, Mtu wala mnyama, wala kundi la ng’ombe, wala kundi la kondoo wasionje chochote: wasikule, wala kunywa maji: Ila mwanadamu na mnyama wavikwe kwa nguzo za magunia, na kulia kwa nguvu kwa Mungu: ndiyo, na wawageuze watu wote kutoka kwa njia ovu, na kutoka kwa vurugu iliyo mikononi mwao. Nani anayejua iwapo Mungu atabadili na kughairi, na kuiacha ghadhabu Yake iliyo kali, ili tusiangamie? Naye Mungu aliona vitendo vyao, kwamba walikuwa wameiacha njia yao ovu; na Mungu akaghairi lile neno ovu, ambalo Alikuwa amesema Angeliwafanyia; na Aakulifanya.

Kama Imani Yako kwa Mungu ni ya Kweli, Utapokea Utunzaji Wake Mara Nyingi

Mungu kubadilisha nia Zake kwa watu wa Ninawi hakukuhusisha kusitasita au kutoeleweka kokote. Badala yake kulikuwa ni mabadiliko kutoka kwa hasira tupu hadi uvumilivu mtupu. Huu ni ufunuo wa kweli wa kiini cha Mungu. Mungu kamwe si wa kusitasita au asiye na uamuzi katika vitendo Vyake; kanuni na makusudio yaliyo katika matendo Yake yote ni wazi na dhahiri, yasiyo na dosari wala doa, yasiyo kabisa na hila ama njama zozote zilizochanganywa ndani. Kwa maneno mengine, kiini cha Mungu hakina giza wala maovu. Mungu aliwakasirikia Waninawi kwa sababu vitendo vyao viovu vilikuwa vimefikia macho Yake; wakati ule hasira Yake ilitokana na kiini Chake. Hata hivyo, wakati hasira ya Mungu ilitoweka na akatoa uvumilivu Wake kwa watu wa Ninawi kwa mara nyingine tena, kila kitu Alichofichua kilikuwa bado ni kiini Chake. Mabadiliko haya yote yalitokana na mabadiliko katika mtazamo wa mwanadamu kwa Mungu. Katika kipindi hiki chote cha muda, tabia ya Mungu isiyokosewa haikubadilika; kiini cha Mungu cha uvumilivu hakikubadilika; kiini cha Mungu cha upendo na huruma hakikubadilika. Wakati watu wanapotekeleza vitendo viovu na kumkosea Mungu atawashushia ghadhabu Yake. Wakati watu wanatubu kwa kweli, moyo wa Mungu utabadilika, na hasira Yake itakoma. Wakati watu wanapoendelea kumpinga Mungu kwa ukaidi, hasira Yake kali haitakoma; hasira Yake itawalemea hatua kwa hatua mpaka watakapoangamizwa. Hiki ndicho kiini cha tabia ya Mungu. Haijalishi kama Mungu anaonyesha hasira au huruma na wema, mwenendo wa binadamu, tabia na mtazamo wake kwa Mungu ndani ya kina cha moyo wake vinaamrisha kile ambacho kinaonyeshwa kupitia kwa ufunuo wa tabia ya Mungu. Kama Mungu anaendelea kumfanya mtu apitie hasira Yake, moyo wa mtu huyu bila shaka humpinga Mungu. Ni kwa sababu mtu huyu hajawahi kutubu kwa kweli, kuinamisha kichwa chake mbele ya Mungu au kumiliki imani ya kweli kwa Mungu, hajawahi kupata huruma na uvumilivu wa Mungu. Kama mtu hupokea utunzaji wa Mungu mara nyingi na hupokea huruma na uvumilivu Wake mara nyingi, basi mtu huyo bila shaka ana imani ya kweli kwa Mungu ndani ya moyo wake, na moyo wake haumpingi Mungu. Mtu huyu mara nyingi anatubu kwa kweli mbele ya Mungu; kwa hivyo, hata kama nidhamu ya Mungu mara nyingi humshukia mtu huyu, hasira Yake haitamshukia.

Maelezo haya mafupi yanaruhusu watu kuuona moyo wa Mungu, kuona uhalisi wa kiini Chake, kuona kwamba ghadhabu ya Mungu na mabadiliko katika moyo Wake yana sababu. Ingawa kuna tofauti kubwa ambayo Mungu aliionyesha Alipoghadhabishwa na wakati Alipobadilisha moyo Wake, jambo hili linaweza kuwafanya watu kuamini kwamba kuna pengo kubwa ama tofauti kubwa inayoweza kuwepo kati ya vipengele hivi viwili vya kiini cha Mungu—ghadhabu Yake na uvumilivu Wake—mtazamo wa Mungu kwa kule kutubu kwa Waninawi kwa mara nyingine kunaruhusu watu kuweza kuona ule upande mwingine wa tabia halisi ya Mungu. Mabadiliko katika moyo wa Mungu yanaruhusu kwa kweli binadamu kwa mara nyingine kuuona ukweli wa huruma na wema wa Mungu na kuona ufunuo wa kweli wa kiini cha Mungu. Binadamu hawana budi kutambua kwamba rehema za Mungu na wema Wake si hadithi za uwongo tu, wala si uzushi. Hii ni kwa sababu hisia za Mungu kwa wakati huo zilikuwa za kweli; Mabadiliko ya moyo wa Mungu yalikuwa ya kweli; Mungu kwa kweli aliwapa binadamu kwa mara nyingine tena rehema na uvumilivu Wake.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 115)

Yona 3 Neno lake Yehova likakuja kwake Yona kwa mara ya pili, likisema, Inuka, nenda Ninawi, mji huo mkuu; na uuhubirie mahubiri ninayokuambia. Kwa hivyo Yona akainuka, na kuenda Ninawi, kulingana na neno la Yehova. Sasa Ninawi ulikuwa mji mkuu wa safari ya siku tatu. Naye Yona akaanza kuingia ndani ya mji huo safari ya siku moja, na akatoa sauti kubwa, na kusema, Imebaki siku arobaini, na Ninawi utashindwa. Basi watu wa hapo Ninawi wakamwamini Mungu, na wakatangaza mfungo, na wakavalia nguo za magunia, kuanzia aliyekuwa mkubwa zaidi kwao mpaka aliyekuwa mdogo zaidi. Kwa kuwa habari ilimfikia mfalme wa Ninawi, na akainuka kutoka kwa kiti chake che enzi, na akaivua nguo yake, na kuvaa nguo ya gunia, na kukaa chini katika majivu. Na akafanya kutangazwe Ninawi kupitia amri yake mfalme na wakubwa wake, ikisema, Mtu wala mnyama, wala kundi la ng’ombe, wala kundi la kondoo wasionje chochote: wasikule, wala kunywa maji: Ila mwanadamu na mnyama wavikwe kwa nguzo za magunia, na kulia kwa nguvu kwa Mungu: ndiyo, na wawageuze watu wote kutoka kwa njia ovu, na kutoka kwa vurugu iliyo mikononi mwao. Nani anayejua iwapo Mungu atabadili na kughairi, na kuiacha ghadhabu Yake iliyo kali, ili tusiangamie? Naye Mungu aliona vitendo vyao, kwamba walikuwa wameiacha njia yao ovu; na Mungu akaghairi lile neno ovu, ambalo Alikuwa amesema Angeliwafanyia; na Aakulifanya.

Toba ya Kweli Ndani ya Mioyo ya Waninawi Inawapa Rehema za Mungu na Kubadilisha Hatima Zao Wenyewe

Je, kulikuwa na mkanganyiko wowote kati ya mabadiliko ya moyo wa Mungu na hasira Yake? Bila shaka la! Hii ni kwa sababu uvumilivu wa Mungu wakati ule maalum ulikuwa na sababu yake. Je, sababu yake yaweza kuwa nini? Ni ile iliyotolewa katika Biblia: “Kila mtu aligeuka kutoka kwenye njia yake ovu” na “kuacha vurugu iliyokuwa mikononi mwake.”

Hii “njia ovu” hairejelei kiasi kidogo cha vitendo viovu, lakini inarejelea chanzo cha maovu katika tabia ya watu. “Kugeuka kutoka kwenye njia yake ovu” kunamaanisha kwamba wale wanaozungumziwa hawatawahi kutekeleza vitendo hivi tena. Kwa maneno mengine, hawatawahi kutenda kwa njia hii ovu tena; mbinu, chanzo, kusudio, nia na kanuni za vitendo vyao vyote vimebadilika; hawatawahi tena kutumia mbinu na kanuni hizi kuleta nafuu na furaha mioyoni mwao. Kule “kuacha” katika “kuacha vurugu iliyo mikononi mwake” kunamaanisha kuweka chini au kuweka pembeni, kujitenga kabisa na mambo ya kale na kutorudi nyuma tena. Wakati watu wa Ninawi walipoacha udhalimu uliokuwa mikononi mwao, hii ilithibitisha na vilevile iliwakilisha toba yao ya kweli. Mungu huangalia kwa makini sehemu ya nje ya watu na vilevile mioyo yao. Wakati Mungu alipoangalia kwa makini toba ya kweli katika mioyo ya Waninawi bila shaka Aliona pia kwamba walikuwa wameacha njia zao ovu na kuacha udhalimu uliokuwa mikononi mwao, Alibadilisha moyo Wake. Hivi ni kusema kwamba mwenendo na tabia ya watu hawa na njia mbalimbali za kufanya mambo, pamoja na ungamo na toba ya dhambi ya kweli zilizokuwa mioyoni mwao, kulisababisha Mungu kubadilisha moyo Wake, kubadilisha nia Zake, kufuta uamuzi Wake na kutowaadhibu wala kuwaangamiza. Kwa hivyo, watu wa Ninawi waliweza kufikia hatima tofauti. Waliyakomboa maisha yao binafsi na wakati uo huo wakapata huruma na uvumilivu wa Mungu, na wakati huo Mungu pia alifuta hasira Yake.

Huruma na Uvumilivu wa Mungu si Nadra—Toba ya Kweli ya Mwanadamu Ndiyo Nadra

Licha ya vile ambavyo Mungu alikuwa na ghadhabu kwa Waninawi, mara tu walipotangaza kufunga na kuvalia nguo za magunia pamoja na kuketi kwenye majivu, moyo Wake ulianza kutulia taratibu, na Akaanza kubadilisha moyo Wake. Wakati Alipowatangazia kwamba Angeangamiza mji wao—ule muda kabla ya kuungama na kutubu kwao kwa dhambi zao—Mungu alikuwa bado ana ghadhabu juu yao. Baada ya wao kupitia mfululizo wa vitendo vya kutubu, ghadhabu ya Mungu kwa watu wa Ninawi ilibadilika polepole kuwa huruma na uvumilivu kwao. Hakuna kitu kinachohitilafiana kuhusu ufunuo wenye ulinganifu wa vipengele hivi viwili vya tabia ya Mungu katika tukio moja. Kwa hivyo, ni kwa jinsi gani mtu anapaswa kuelewa na kujua kwamba hazihitilafiani? Mungu alionyesha na kufichua viini hivi viwili tofauti kabisa kwa mfululizo wakati watu wa Ninawi walipokuwa wakitubu na Akawaruhusu watu kuona uhalisi na kutokosewa kwa kiini cha Mungu. Mungu alitumia mtazamo Wake kuambia watu yafuatayo: Si kwamba Mungu hawavumilii watu, au hataki kuwaonyesha huruma; ni kwamba wao hutubu kwa kweli kwa nadra sana mbele za Mungu, na ni nadra kwa watu kugeuka kwa kweli kutoka kwa njia zao ovu na kuacha udhalimu ulio mikononi mwao. Kwa maneno mengine, wakati Mungu ameghadhabishwa na binadamu, Anatumaini kwamba binadamu ataweza kutubu kwa kweli na Anatumaini kumwona binadamu akitubu kwa kweli, ambapo Ataendelea kumpa binadamu huruma na uvumilivu Wake kwa ukarimu. Hivi ni kusema kwamba mwenendo mbovu wa mwanadamu ndio husababisha hasira ya Mungu, huku nazo rehema na uvumilivu wa Mungu zikipewa wale wanaomsikiliza Mungu na kutubu kwa kweli mbele Yake, kwa wale wanaoweza kugeuka kutoka kwa njia zao ovu na kuacha udhalimu ulio mikononi mwao. Mtazamo wa Mungu ulifichuliwa waziwazi sana katika jinsi Alivyowatendea Waninawi: Huruma na uvumilivu wa Mungu si vigumu kuvipokea hata kidogo; Anahitaji toba ya kweli ya mtu. Mradi tu watu wageuka kutoka kwa njia zao ovu na kuacha udhalimu ulio mikononi mwao, Mungu atabadilisha moyo Wake na kubadilisha mtazamo Wake kwao.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 116)

Tabia ya Haki ya Muumba ni ya Kweli na Wazi

Wakati Mungu alibadilisha moyo Wake kwa minajili ya watu wa Ninawi, je, huruma na uvumilivu Wake ulikuwa wa bandia? Bila shaka la! Basi mabadiliko kati ya vipengele hivi viwili vya tabia ya Mungu katika hili suala moja yanakuruhusu kuona nini? Tabia ya Mungu ni kamili kabisa; haijagawanywa hata kidogo. Haijalishi kama Anaonyesha ghadhabu au huruma na uvumilivu kwa watu, haya yote ni maonyesho ya tabia Yake ya haki. Tabia ya Mungu ni ya kweli na wazi. Yeye hubadilisha fikira na mitazamo Yake kulingana na maendeleo ya mambo. Mabadiliko ya mtazamo Wake kwa Waninawi yanawaambia binadamu kwamba Anazo fikira na mawazo Yake mwenyewe; Yeye si roboti au sanamu ya udongo, bali Yeye ni Mungu Mwenyewe aliye hai. Angeweza kuwa na ghadhabu kwa watu wa Ninawi, sawa tu na vile ambavyo Angeweza kusamehe dhambi zao za kale kulingana na mitazamo yao; Angeweza kuamua kuwaletea Waninawi msiba na Angeweza kubadilisha uamuzi Wake kwa sababu ya kutubu kwao. Watu hupenda kutumia sheria bila kupinda na kutumia sheria kama hizo ili kumwekea mipaka na kumfafanua Mungu, sawa tu na vile watu wanavyopendelea kutumia kanuni kujaribu kuelewa tabia ya Mungu. Kwa hivyo, katika uwanja wa fikira za binadamu, Mungu hafikirii wala Yeye hana mawazo yoyote halisi. Kwa uhalisi, fikira za Mungu zinabadilika siku zote kulingana na mabadiliko katika mambo, na mazingira; huku fikira hizi zikiwa zinabadilika, vipengele tofauti vya kiini cha Mungu vitafichuliwa. Katika kipindi hiki cha mabadiliko, wakati ule Mungu hubadilisha moyo Wake, Yeye humfichulia mwanadamu ukweli wa uwepo wa maisha Yake na kufichua kwamba tabia Yake ya haki ni halisi na wazi. Aidha, Mungu hutumia ufunuo Wake mwenyewe wa kweli kuthibitisha kwa mwanadamu ukweli wa uwepo wa hasira Yake, huruma Yake, wema Wake na uvumilivu Wake. Kiini Chake kitafichuliwa wakati wowote na mahali popote kulingana na maendeleo ya mambo. Anamiliki hasira ya simba na huruma na uvumilivu wa mama. Tabia Yake ya haki hairuhusiwi kutiliwa shaka, kukiukwa, kubadilishwa au kupotoshwa na mtu yeyote. Miongoni mwa masuala yote na mambo yote, tabia ya haki ya Mungu, yaani, hasira ya Mungu na huruma ya Mungu, vyote vinaweza kufichuliwa wakati wowote na mahali popote. Anaonyesha waziwazi vipengele hivi kwa kila sehemu ya viumbe vyote, na Anavitekeleza kila wakati kwa uwazi. Tabia ya haki ya Mungu haiwekewi mipaka na muda au eneo, au kwa maneno mengine, tabia ya haki ya Mungu haionyeshwi bila kufikiri au kufichuliwa kulingana na mipaka ya muda au eneo. Badala yake, tabia ya haki ya Mungu inaonyeshwa kwa njia huru na kufichuliwa mahali popote na wakati wowote. Unapoona Mungu akibadilisha moyo Wake na kukoma kuonyesha hasira Yake na kujizuia dhidi ya kuuangamiza mji wa Ninawi, je, unaweza kusema kwamba Mungu ni mwenye huruma na upendo tu? Je, unaweza kusema kwamba hasira ya Mungu inajumuisha maneno matupu? Wakati Mungu anapoonyesha hasira kali na kuiondoa huruma Yake, je, unaweza kusema kwamba Hana hisia zozote za upendo wa kweli kwa binadamu? Mungu huonyesha hasira kali kutokana na vitendo viovu vya watu, hasira Yake haina dosari. Moyo wa Mungu unavutiwa na toba ya watu, na ni toba hii ambayo hubadilisha moyo Wake. Anapohisi kuguswa, Anapokuwa na mabadiliko katika moyo Wake pamoja na huruma na uvumilivu Wake kwa binadamu, vyote havina kosa kabisa; ni safi, havina kasoro, havina doa na havijachafuliwa. Uvumilivu wa Mungu ni uvumilivu mtupu; Huruma Yake ni huruma tupu. Tabia Yake itafichua hasira, pamoja na huruma na uvumilivu, kulingana na kutubu kwa binadamu na mwenendo wake tofauti. Haijalishi kile ambacho Anafichua na kuonyesha, yote hayo hayana kasoro; yote ni ya moja kwa moja; kiini Chake ni tofauti na ile ya kiumbe chochote kilichoumbwa. Wakati Mungu anapoeleza kanuni zinazohusu matendo Yake, mawazo Yake, fikira Zake, na kila uamuzi Anaoufanya, pamoja na kila hatua Anazozichukua, huwa hazina doa au dosari zozote. Kama jinsi ambavyo Mungu huamua na jinsi Atendavyo, ndivyo Anavyokamilisha shughuli Zake. Aina hizi za matokeo ni sahihi na hazina dosari kwa sababu chanzo chake hakina dosari na doa lolote. Hasira ya Mungu haina dosari. Vilevile, huruma na uvumilivu wa Mungu, ambazo hazimilikiwi na kiumbe yeyote ni takatifu na hazina kosa, na zinaweza kustahimili fikira na uzoefu.

Baada ya kuelewa hadithi ya Ninawi, je, sasa mnauona upande ule mwingine wa kiini cha tabia ya haki ya Mungu? Je, mnauona upande ule mwingine wa tabia ya haki na ya kipekee ya Mungu? Je, kunaye mtu yeyote miongoni mwa binadamu anayemiliki aina hii ya tabia? Je, kunaye mtu yeyote anayemiliki aina hii ya hasira kama ile ya Mungu? Je, kunaye mtu yeyote anayemiliki huruma na uvumilivu kama ule wa Mungu? Ni nani miongoni mwa viumbe anayeweza kuitisha ghadhabu kuu namna hii na kuamua kuangamiza au kuleta maafa juu yawanadamu? Na ni nani anazo sifa zinazostahili kutoa huruma kuvumilia na kumsamehe binadamu na hivyo basi kubadilisha uamuzi wake wa kuangamiza binadamu? Muumba huonyesha tabia Yake ya haki kupitia mbinu na kanuni Zake za kipekee; na Hayuko chini ya udhibiti au vizuizi vilivyowekwa na watu, matukio au vitu vyovyote. Akiwa na tabia Yake ya kipekee, hakuna mtu anayeweza kubadilisha fikira na mawazo Yake, wala hakuna yule anayeweza kumshawishi Yeye na kubadilisha maamuzi Yake yoyote. Tabia zote na mawazo yote yaliyopo katika viumbe vyote vilivyoumbwa vipo chini ya hukumu ya tabia Yake ya haki. Hakuna anayeweza kudhibiti kama atatumia hasira au huruma; ni kiini cha Muumba tu—au kwa maneno mengine, tabia ya haki ya Muumba—inaweza kuamua hili. Hii ndiyo asili ya kipekee ya tabia ya haki ya Muumba!

Baada ya kuchambua na kuelewa mabadiliko katika mtazamo wa Mungu kwa watu wa Ninawi, je, unaweza kutumia neno “upekee” kufafanua huruma inayopatikana katika tabia ya haki ya Mungu? Hapo awali tulisema kwamba hasira ya Mungu ni kipengele kimoja cha kiini cha tabia Yake ya haki na ya kipekee. Sasa Nitafafanua vipengele viwili, hasira ya Mungu na huruma ya Mungu, kama tabia Yake ya haki. Tabia ya haki ya Mungu ni takatifu; ni isiyokosewa na isiyoweza kutiliwa shaka; ni kitu kisichomilikiwa na yeyote miongoni mwa viumbe vilivyoumbwa au vile ambavyo havikuumbwa. Ni ya kipekee na maalum kwa Mungu pekee. Hivi ni kusema kwamba hasira ya Mungu ni takatifu na isiyoweza kukosewa Vivyo hivyo, kipengele kile kingine cha tabia ya haki ya Mungu—huruma ya Mungu—ni takatifu na haiwezi kukosewa. Hakuna yeyote kati ya viumbe vile vilivyoumbwa au vile ambavyo havikuumbwa, anayeweza kuchukua nafasi Yake au kumwakilisha Mungu katika matendo Yake, wala hakuna yeyote ambaye angeweza kuchukua nafasi Yake au kumwakilisha Yeye katika kuangamiza Sodoma au wokovu wa Ninawi. Haya ndiyo maonyesho ya kweli ya tabia ya haki ya kipekee ya Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 117)

Hisia za Dhati za Muumba kwa Wanadamu

Watu mara nyingi husema kwamba si jambo rahisi kumjua Mungu. Mimi, hata hivyo, nasema kwamba kumjua Mungu si jambo gumu kamwe, kwani Mungu mara kwa mara huruhusu binadamu kushuhudia matendo Yake. Mungu hajawahi kusitisha mazungumzo Yake na mwanadamu; Yeye hajawahi kujificha kutoka kwa binadamu, wala Yeye hajajificha. Fikira Zake, mawazo Yake, maneno Yake na matendo Yake vyote vimefichuliwa kwa mwanadamu. Kwa hivyo, mradi tu mwanadamu angependa kumjua Mungu, anaweza kumwelewa hatimaye na kumjua Yeye kupitia aina zote za mambo na mbinu. Sababu inayomfanya binadamu kufikiria kwa kutojua kwamba Mungu amemwepuka kimakusudi, kwamba Mungu amejificha kimakusudi kutoka kwa binadamu, kwamba Mungu hana nia yoyote ya kumruhusu mwanadamu kumwelewa na kumjua Yeye, ni kwa sababu hamjui Mungu ni nani, na wala hataki kumuelewa Mungu; na hata zaidi, hajali kuhusu fikira, matamshi au matendo ya Muumba…. Kusema kweli, kama mtu atatumia tu muda wake wa ziada vizuri katika kuzingatia na kuelewa matamshi au matendo ya Muumba na kuuweka umakinifu mchache kwa fikira za Muumba na sauti ya moyo Wake, haitakuwa vigumu kwa wao kutambua ya kwamba fikira, maneno na matendo ya Muumba, vyote vinaonekana na viko wazi. Vilevile, itachukua jitihada kidogo kutambua kwamba Muumba yuko miongoni mwa binadamu wakati wote, kwamba siku zote Anazungumza na binadamu na vitu vyote, na kwamba Anatekeleza matendo mapya kila siku. Kiini Chake na tabia Yake vimeonyeshwa katika mazungumzo Yake na binadamu; fikira na mawazo Yake vyote vinafunuliwa kabisa katika matendo Yake; Anaandamana na mwanadamu na kumtazama wakati wote. Yeye anatumia maneno Yake asiyotamka kuwaambia wanadamu na vitu vyote kwa utulivu: “Mimi niko mbinguni, na Mimi nimo miongoni mwa vitu vyote. Ninaangalia, Ninasubiri; Niko kando yako….” Mikono Yake ni yenye joto na nguvu; nyayo Zake ni nyepesi; sauti Yake ni laini na yenye neema, umbo Lake hupita na kugeuka, likiwakumbatia wanadamu wote; uso Wake ni mzuri na mpole. Hajawahi kuondoka, hajawahi kutoweka. Usiku na mchana, Yeye yuko na mwanadamu siku zote, Asiyeondoka upande wao kamwe. Utunzaji Wake wa kujitolea na mapenzi Yake ya kipekee kwa binadamu, pamoja na kujali Kwake kwa kweli na upendo kwa binadamu, yalionyeshwa kidogo kidogo Alipouokoa mji wa Ninawi. Hasa, mabadilishano ya mazungumzo kati ya Yehova Mungu na Yona yalifunua kikamilifu upole wa Muumba kwa mwanadamu ambaye Yeye Mwenyewe Alimuumba. Kupitia katika maneno hayo, unaweza kufahamu kwa kina hisia za dhati za Mungu kwa binadamu …

Kifungu kifuatacho kilirekodiwa kwenye kitabu cha Yona 4:10-11: “Kisha Yehova akasema, Umekitunza sana kibuyu, ambacho hujakifanyia kazi, wala kukikuza; ambacho kilimea kwa usiku mmoja, na kufa kwa usiku mmoja: Nami, je, sipaswi kulitunza Ninawi, mji ule mkuu, ulio na zaidi ya watu elfu mia na ishirini humo ambao hawawezi kupambanua kati ya mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; na pia mifugo mingi?” Haya ni maneno halisi ya Yehova Mungu, kutoka katika mazungumzo kati ya Mungu na Yona. Ingawa mazungumzo haya ni mafupi, yamejaa kutotaka kwa Muumba kumwacha mwanadamu na utunzaji Wake kwa binadamu. Maneno haya yanaonyesha mtazamo na hisia za kweli ambazo Mungu anashikilia ndani ya moyo Wake kwa viumbe Wake aliowaumba. Maneno haya pia ni Mungu akieleza nia Zake za kweli kwa binadamu, kwa njia iliyo dhahiri ambayo binadamu husikia kwa nadra sana. Mabadilishano ya mazungumzo haya yanawakilisha mtazamo ambao Mungu alishikilia kwa watu wa Ninawi—lakini mtazamo huu ni upi? Ni mtazamo Alioshikilia kuhusu watu wa Ninawi kabla na baada ya kutubu kwao. Mungu huchukulia binadamu kwa njia sawa. Ndani ya maneno haya mtu anaweza kupata fikira Zake, pamoja na tabia Yake.

Je, ni fikira zipi za Mungu zinafichuliwa katika maneno haya? Ukizingatia maelezo kwa makini unaposoma, haitakuwa vigumu kutambua kwamba Anatumia neno “huruma”; matumizi ya neno hili yanaonyesha mtazamo wa kweli wa Mungu kwa binadamu.

Kwa kiwango cha maana halisi, watu wanaweza kufasiri neno “huruma” kwa njia tofauti: Kwanza, inamaanisha “kupenda na kulinda, kuhisi huruma kuhusu kitu fulani”; pili, inamaanisha “kupenda kwa dhati”; na ya mwisho, inamaanisha “kutokuwa radhi kukiumiza kitu fulani na kutoweza kuvumilia kufanya hivyo.” Kwa ufupi, inaashiria hisia za kujali na upendo wa dhati, pamoja na kutokuwa radhi kukata tamaa na kumwacha mtu au kitu; unamaanisha huruma ya Mungu na uvumilivu kwa mwanadamu. Ingawa Mungu alitumia neno hili, ambalo huzungumzwa kwa kawaida na wanadamu, matumizi ya neno hili yanaweka wazi sauti ya moyo wa Mungu na mtazamo Wake kwa mwanadamu.

Ingawa mji wa Ninawi ulikuwa umejaa watu waliopotoka, walio waovu, na wenye udhalimu kama wale wa Sodoma, kutubu kwao kulisababisha Mungu kubadilisha moyo Wake na kuamua kutowaangamiza. Kwa sababu mwitikio wao kwa maneno na maagizo ya Mungu ulionyesha mtazamo ambao ulitofautiana kabisa na ule wa wananchi wa Sodoma, na kwa sababu ya utiifu wao wa dhati kwa Mungu na kutubu kwa uaminifu dhambi zao, pamoja na tabia yao ya kweli na ya dhati katika mambo yote, Mungu kwa mara nyingine tena alionyesha huruma Yake ya moyoni naye akaweza kuwapa. Kile ambacho Mungu huwapa binadamu na huruma Yake kwa binadamu haiwezekani kwa yeyote yule kuiga, na haiwezekani kwa mtu yeyote kumiliki huruma au uvumilivu wa Mungu, wala hisia Zake za dhati kwa binadamu. Je, yupo yeyote unayemwona kuwa mwanamume au mwanamke mkuu, au hata mwanadamu mkuu zaidi, ambaye angeweza, kutoka katika mtazamo mkuu, kuongea kama mwanamume au mwanamke mkuu au kwenye sehemu ya mamlaka ya juu, kutoa aina hii ya kauli kwa mwanadamu au viumbe? Ni nani miongoni mwa wanadamu anayeweza kujua hali za maisha ya binadamu kama viganja vya mikono yao? Ni nani anayeweza kubeba mzigo na jukumu la uwepo wa mwanadamu? Nani aliye na sifa ya kutangaza kuangamizwa kwa mji? Na ni nani aliye na sifa ya kuusamehe mji? Ni nani anayeweza kusema kwamba anauthamini uumbaji Wake wote? Ni Muumba pekee! Muumba pekee ndiye Anayethamini jamii hii ya wanadamu. Muumba pekee ndiye Anaewaonyesha wanadamu hawa huruma na upendo. Ni Muumba pekee ndiye aliye na upendo wa kweli, usioweza kutenganishwa kwa wanadamu hawa. Vivyo hivyo, ni Muumba pekee ndiye Anayeweza kuwahurumia wanadamu hawa, na kuvithamini viumbe Vyake vyote. Moyo Wake unavutwa na kuumizwa kwa kila kitendo cha mwanadamu: Anagadhibishwa, Anahuzunishwa na kuumizwa kwa uovu na upotovu wa mwanadamu; Anakuwa radhi, Anafurahishwa, Anasamehe na kushangilia kutokana na toba na imani ya mwanadamu; kila moja ya mawazo Yake na fikira Zake vipo kwa ajili ya wanadamu na yanawazunguka wanadamu; kile Alicho na Anacho kinaonyeshwa kikamilifu kwa ajili ya wanadamu; hisia Zake zote zinahusiana sana na uwepo wa wanadamu. Kwa ajili ya wanadamu, Anasafiri na kukimbia huku na kule; Anatoa kwa ukimya kila sehemu ya maisha Yake; na Anajitolea kila dakika na sekunde ya maisha Yake…. Hajawahi kujua jinsi ya kuyathamini maisha Yake Mwenyewe, lakini daima Amewatunza wanadamu Aliowaumba kwa mikono Yake Mwenyewe…. Anatoa kila Alichonacho kwa wanadamu hawa…. Anatoa rehema na uvumilivu Wake bila masharti na bila kutarajia malipo. Anafanya hivi tu ili kwamba wanadamu waweze kuendelea kuishi mbele ya macho Yake, wakipokea utoaji Wake wa maisha. Anafanya hivi tu ili kwamba wanadamu waweze siku moja kujisalimisha mbele Zake na kutambua kwamba Yeye ndiye Anayetosheleza maisha ya wanadamu na kutoa uhai wa viumbe vyote.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 118)

Yona 4 Lakini lilimwudhi Yona mno, naye alikuwa na hasira sana. Na akaomba kwa Yehova, na kusema, Nakuomba, Ee Yehova, hivi sivyo nilivyonena, nilipokuwa bado katika nchi yangu? Kwa hivyo nilitorokea Tarshishi kabla: kwa sababu nilijua kwamba Wewe ni Mungu wa neema, na mwenye huruma, asiyekasirika haraka, na wa rehema kubwa, na Wewe unaghairi maovu. Kwa hivyo sasa, Ee Yehova, chukua, nakusihi, uhai wangu kutoka kwangu; kwa sababu ni heri nikufe kuliko kuishi. Kisha Yehova akasema, Je, unafanya vizuri kukasirika? Hivyo Yona akatoka nje ya mji, na kuketi katika upande wa mashariki wa mji, na huko akajitengenezea kibanda, na akaketi chini yake katika kivuli, mpaka aweze kuona kile kingefanyikia mji huo. Naye Yehova Mungu akatayarisha mtango, na akaufanya ukuje juu yake Yona, ili uweze kuwa kivuli juu ya kichwa chake, na kumwokoa kutoka katika huzuni yake. Kwa hivyo Yona akawa na furaha sana juu ya ule mtango. Lakini Mungu akatayarisha buu siku iliyofuata wakati kulipopambazuka, nalo likaula ule mtango hadi ukanyauka. Na hivyo ikatimia, wakati jua lilipopanda, kwamba Mungu akautayarisha upepo mkali wa mashariki; na jua likapiga kichwa chake Yona, kiasi kwamba alizimia, naye akatamani afe, na akasema, Ni heri mimi nife kuliko niishi. Mungu akasema kwa Yona, Je, unafanya vizuri kukasirika kwa sababu ya mtango? Na yeye akasema, naam, nafanya vizuri kukasirika, hata mpaka kufa. Kisha Yehova akasema, Umekitunza sana kibuyu, ambacho hujakifanyia kazi, wala kukikuza; ambacho kilimea kwa usiku mmoja, na kufa kwa usiku mmoja: Nami, je, sipaswi kulitunza Ninawi, mji ule mkuu, ulio na zaidi ya watu elfu mia na ishirini humo ambao hawawezi kupambanua kati ya mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; na pia mifugo mingi?

Muumba Aonyesha Hisia Zake za Kweli Kwa Binadamu

Mazungumzo haya kati ya Yehova Mungu na Yona bila shaka ni onyesho la hisia za kweli za Muumba juu ya binadamu. Kwa upande mmoja yanafahamisha watu kuhusu ufahamu wa Muumba wa viumbe vyote chini ya ukuu Wake; kama vile Yehova Mungu alivyosema, “Nami sipaswi kuonea Ninawi huruma, mji ule mkuu, ulio na zaidi ya watu elfu mia na ishirini ndani yake ambao hawawezi kutambua kati ya mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; na pia mifugo wengi?” Kwa maneno mengine, ni kwamba ufahamu wa Mungu juu ya mji wa Ninawi si wa kukadiria. Sio kwamba anajua tu idadi ya viumbe vilivyo hai ndani ya mji (wakiwemo watu na mifugo), bali Alijua pia ni wangapi wasioweza kutambua kati ya mikono yao ya kulia na kushoto—yaani, ni watoto na vijana wangapi waliokuwepo. Huu ni uthibitisho kamili wa ufahamu mpana wa Mungu juu ya wanadamu. Kwa upande mwingine mazungumzo haya yanafahamisha watu kuhusu mtazamo wa Muumba kwa binadamu, yaani, umuhimu wa wanadamu katika moyo wa Muumba. Ni vile tu Yehova Mungu alivyosema: “Umekitunza sana kibuyu, ambacho hujakifanyia kazi, wala kukikuza; ambacho kilimea kwa usiku mmoja, na kufa kwa usiku mmoja: Nami, je, sipaswi kulitunza Ninawi, mji ule mkuu…?” Maneno haya yalisemwa na Yehova Mungu dhidi ya Yona, lakini yote yalikuwa kweli.

Ingawaje Yona alikuwa ameaminiwa kutangaza matamshi ya Yehova Mungu kwa watu wa Ninawi, hakuelewa nia za Yehova Mungu, wala hakuelewa wasiwasi na matarajio Yake kwa watu wa mji huu. Kupitia kwa kemeo hili Mungu alinuia kumwambia kwamba binadamu walikuwa ni zao la mikono Yake mwenyewe, na kwamba Mungu alikuwa ametia jitihada za dhati kwa kila mtu; kwamba Mungu ameweka matarajio Yake kwa kila mtu, kwamba kila mtu anafurahia maisha yanayotolewa na Mungu, na kwamba kwa kila mtu, Mungu alikuwa amelipa gharama ya dhati. Kemeo hili lilimfahamisha Yona kwamba Mungu aliwahurumia wanadamu, ambao walikuwa ni kazi ya mikono Yake mwenyewe, kama vile tu ambavyo Yona mwenyewe aliuhurumia ule mtango. Mungu kwa vyovyote vile asingewaacha kwa urahisi kabla ya ule muda wa mwisho unaowezekana; vilevile, kulikuwa na watoto wengi na mifugo isiyo na hatia ndani ya mji. Wakati wa kushughulikia wanadamu hawa wenye umri mdogo walio zao la uumbaji wa Mungu, ambao bado hawawezi hata kutofautisha kati ya mikono yao ya kushoto na ile ya kulia, na walio katika umri wa ujinga, Mungu asingeweza hata zaidi kukatisha maisha yao kwa urahisi na kuamua mwisho wao kwa haraka hivyo. Mungu alitumai kuwaona wakikua; Alitumai kwamba wasingetembea njia ile ile kama wakubwa wao, kwamba wasingeweza kusikia tena onyo la Yehova Mungu, na kwamba wangeshuhudia mambo ya kale ya Ninawi. Na hata zaidi Mungu alitumai kuiona Ninawi baada ya kuweza kutubu, kuuona mustakabali wa Ninawi kufuatia kutubu kwake, na muhimu zaidi, kuiona Ninawi ikiishi katika huruma za Mungu kwa mara nyingine tena. Kwa hivyo, machoni pa Mungu, wale wanadamu walioumbwa ambao bado hawakuweza kutofautisha kati ya mikono yao ya kulia na kushoto walikuwa mustakabali wa Ninawi. Wangeweza kubeba na kusimulia hadithi ya kale ya Ninawi iliyostahili dharau, na pia wangebeba wajibu muhimu wa kushuhudia wakati uliopita na ule ujao wa Ninawi chini ya uongozi wa Yehova Mungu. Katika tangazo hili la hisia Zake za kweli, Yehova Mungu aliwasilisha huruma ya Muumba kuhusu binadamu kwa ujumla wake. Lilionyesha binadamu kwamba “ile huruma ya Muumba” si kauli tupu tu, wala si ahadi isiyotimizika; ilikuwa na kanuni, mbinu na malengo madhubuti. Mungu ni wa kweli na halisi, na hatumii uwongo au utapeli wowote, na kwa njia hii hii huruma Yake hutolewa bila kikomo kwa wanadamu katika kila wakati na enzi. Hata hivyo, hadi siku hii, mabadilishano ya mazungumzo ya Muumba na Yona ndiyo kauli moja, na ya kipekee ya matamshi yanayoelezea ni kwa nini Anaonyesha huruma kwa binadamu, jinsi Anavyoonyesha huruma kwa binadamu, ni vipi Alivyo na uvumilivu kwa binadamu na hisia Zake za kweli kuhusu binadamu. Mazungumzo haya ya Yehova Mungu kwa ufupi na uwazi yanaonyesha fikira Zake kamili kuhusu binadamu; ni maonyesho ya kweli ya mtazamo wa moyo Wake kwa binadamu, na pia ni uthibitisho kamili wa utoaji Wake wa huruma nyingi juu ya binadamu. Huruma yake haitolewi tu kwa vizazi vya wazee wa binadamu, lakini pia hutolewa kwa washiriki wachanga wa binadamu, kama vile tu ambavyo imekuwa siku zote, kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Ingawa ghadhabu ya Mungu mara kwa mara hushuka kwenye pembe fulani na enzi fulani za binadamu, huruma za Mungu hazijawahi kukoma. Kupitia kwa huruma Yake, Yeye huongoza na kuelekeza kizazi kimoja cha uumbaji Wake hadi kingine, huruzuku na kukimu kizazi kimoja cha uumbaji hadi kingine, kwa sababu hisia Zake za kweli kwa binadamu hazitawahi kubadilika. Kama vile tu Yehova Mungu alivyosema: “Nami sipaswi kuonea Ninawi huruma…?” Siku zote amefurahia uumbaji Wake mwenyewe. Hii ndiyo huruma ya tabia ya haki ya Muumba, na ndio pia upekee usio na kasoro wa Muumba!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Maneno ya Mungu ya Kila Siku  (Dondoo 119)

Aina Tano za Watu

Nitaainisha wafuasi wa Mungu katika makundi kadhaa, kulingana na ufahamu wao wa Mungu, pamoja na ufahamu na uzoefu wao kuhusu tabia Yake ya haki, ili uweze kujua hatua uliyomo kwa sasa, pamoja na kimo chako cha sasa. Kuhusiana na maarifa ya watu juu ya Mungu na ufahamu wao wa tabia Yake ya haki, hatua na vimo tofauti ambavyo watu wanashikilia kwa ujumla vinaweza kugawanywa katika aina tano. Mada hii imeelezewa kwa msingi wa kumjua Mungu wa kipekee na tabia Yake ya haki; kwa hivyo, unaposoma maudhui yafuatayo, unafaa kujaribu kwa makini kuchambua ni kiwango kipi haswa cha ufahamu na maarifa ulichonacho kuhusiana na upekee wa Mungu na tabia Yake ya haki, na kisha utumie hayo kujua ni hatua gani ambayo kwa kweli unapatikana ndani, kimo chako ni kikubwa vipi kwa kweli, na wewe ni mtu wa aina gani kwa kweli.

Aina ya Kwanza: Hatua ya Mtoto Mchanga Aliyevikwa Nguo za Kitoto

Mtoto mchanga aliyevikwa nguo za kitoto ni nani? Mtoto mchanga aliyevikwa nguo za kitoto ni mtoto mchanga ambaye ndio amekuja tu katika ulimwengu huu, amezaliwa. Huu ndio wakati ambao watu wako katika awamu ndogo zaidi na isiyo na ukomavu.

Watu katika awamu hii kimsingi hawamiliki utambuzi au ufahamu wowote wa masuala ya imani katika Mungu. Wamechanganyikiwa na hawajui kila kitu. Watu hawa huenda wamemsadiki Mungu kwa muda mrefu au kwa muda usiokuwa mrefu, lakini hali yao ya kuchakanganywa na kutojua kimo chao halisi kinawaweka kwenye awamu ya mtoto mchanga ambaye amevikwa kwa nguo za kitoto. Ufafanuzi sahihi wa hali hii ya mtoto mchanga aliyevikwa nguo za kitoto ni kama vile: Haijalishi ni kwa muda gani mtu wa aina hii amemwamini Mungu, siku zote atakuwa mpumbavu, atachanganyikiwa na atakosa busara; hajui ni kwa nini anamwamini Mungu, wala hamjui Mungu ni nani au Mungu ni nini. Ingawa wanamfuata Mungu, hakuna ufafanuzi sahihi wa Mungu ndani ya mioyo yao, na hawawezi kuamua kama Yule wanayemfuata ni Mungu, achilia mbali kama kweli wanafaa kumwamini Mungu na kumfuata. Hii ndiyo hali halisi ya mtu wa aina hii. Fikira za watu hawa zimezingirwa na ukungu, na kama nitasema wazi, imani yao ni ile ya mkanganyo. Siku zote wanakuwa katika hali ya kutokuelewa na utupu; wanakuwa wapumbavu, wanachanganyikiwa, na wanakosa busara, hivi ndivyo vitu vinavyofanya muhtasari wa hali zao. Hawajawahi kuona wala kuhisi uwepo wa Mungu, na hivyo basi, kuzungumza nao kuhusu kumjua Mungu ni sawa tu na kuwafanya wasome kitabu kilichoandikwa kwa maandishi ama ishara zisizoeleweka; hawataelewa wala kuyakubali. Kwao, kumjua Mungu ni sawa na kusikia hadithi ya ajabu. Huku mawazo yao yakiwa yamejaa ukungu, wanaamini kwa hakika kwamba kumjua Mungu ni kupoteza muda na jitihada. Huyu ndiye mtu wa aina ya kwanza: mtoto mchanga aliyevikwa nguo za kitoto.

Aina ya Pili: Hatua ya Mtoto Mchanga Anayenyonya

Akilinganishwa na mtoto mchanga aliyevikwa nguo za kitoto, mtu wa aina hii amepata maendeleo fulani. Kwa bahati mbaya, bado hawana ufahamu wowote wa Mungu. Bado hawana ufahamu wazi wa Mungu na utambuzi wa Mungu, na hawaelewi vizuri sana ni kwa nini wanapaswa kumwamini Mungu, lakini katika mioyo yao wana madhumuni yao wenyewe na mawazo yaliyo wazi. Hawajishughulishi katika suala la ikiwa ni sahihi kumwamini Mungu. Lengo na madhumuni wanayotafuta kupitia imani katikaMungu ni kufurahia neema Yake, kuwa na furaha na amani, kuishi maisha yenye utulivu, kuwa na utunzaji na ulinzi wa Mungu na kuishi katika baraka za Mungu. Hawajali kiwango ambacho wanamjua Mungu; hawana msukumo wa kutafuta kuelewa kuhusu Mungu, wala hawashughuliki na kile ambacho Mungu anafanya au kile ambacho Angependa kufanya. Wanatafuta tu bila mwelekeo kufurahia neema Yake na kupata baraka Zake nyingi; wanatafuta kupokea baraka mara mia moja katika wakati wa sasa, na uzima wa milele katika wakati ujao. Mawazo yao, kiasi wanachojitumia wao wenyewe kujitolea kwao, pamoja na kuteseka kwao, vyote vinalo lengo moja: kupokea neema na baraka za Mungu. Hawana shughuli na kitu kingine chochote. Mtu wa aina hii ana uhakika tu kwamba Mungu anaweza kuwalinda wakawa salama na kuwapa neema Yake. Mtu anaweza kusema kwamba hawapendezwi na wala hawana uelewa sana kuhusiana na kwa nini Mungu angependa kumwokoa binadamu au matokeo ambayo Mungu angependa kupata kutokana na matamshi na kazi Yake. Hawajawahi kutia jitihada za kujua kiini cha Mungu na tabia Yake ya haki, wala hawawezi kujipa moyo na kuwa na nia ya kufanya hivyo. Hawana mwelekeo wa kuzingatia mambo haya, na, wala hawapendi kuyajua. Hawapendi hata kuulizia kuhusu kazi ya Mungu, mahitaji ya Mungu kwa binadamu, mapenzi ya Mungu au kitu kingine chochote kinachohusiana na Mungu; wala hawawezi kuwa na msukumo wa kuulizia mambo haya. Hii ni kwa sababu wanaamini kwamba mambo haya hayahusiani na kufurahia kwao neema ya Mungu; wanajali tu Mungu anayeweza kuwapa neema na ambaye ana uhusiano na masilahi yao ya kibinafsi. Kamwe hawana haja na kitu kingine chochote, na kwa hivyo hawawezi kuingia kwenye uhalisi wa ukweli, licha ya miaka mingapi ambayo wamemwamini Mungu. Bila kuwepo mtu yeyote wa kuwanywesha mara kwa mara au kuwalisha, ni vigumu kwao kuendelea na njia ya imani katika Mungu. Kama hawawezi kufurahia furaha yao na amani ya awali au kufurahia neema ya Mungu, basi wana uwezekano mkubwa wa kujiondoa. Huyu ndiye mtu wa aina ya pili: mtu anayekuwepo kwenye awamu ya mtoto mchanga wa kunyonya.

Aina ya Tatu: Hatua ya Mtoto Mchanga Anayeachishwa Kunyonya, au Hatua ya Mtoto Mdogo

Kundi hili la watu humiliki ufahamu fulani wenye uwazi. Watu hawa wanao ufahamu kwamba kufurahia neema ya Mungu hakumaanishi kwamba wao wenyewe wanamiliki uzoefu wa kweli; na wanafahamu kwamba hata kama hawatachoka kamwe kutafuta furaha na amani, kutafuta neema, au kama wanaweza kutoa ushuhuda kwa kushiriki uzoefu wao katika kufurahia neema ya Mungu au kwa kumsifu Mungu kwa baraka Alizowapa, mambo haya hayamaanishi kwamba wana uzima, wala hayamaanishi kwamba wanao uhalisi wa ukweli. Tukianzia katika ufahamu wao, wanaacha kuwa na matumaini yasiyo na mipaka kwamba wataandamana tu na neema ya Mungu; badala yake, wakati wanapofurahia neema ya Mungu, wanapenda wakati uo huo kufanya kitu kwa ajili ya Mungu; wako radhi kutekeleza wajibu wao, kuvumilia ugumu kidogo na uchovu, kuwa na kiwango fulani cha ushirikiano na Mungu. Hata hivyo, kwa sababu ufuatiliaji wao wa imani yao katika Mungu umepotoka sana, kwa sababu nia za kibinafsi na matamanio waliyo nayo ni yenye nguvu sana, kwa sababu tabia yao ni yenye kiburi kupita kiasi, ni vigumu sana kwao kutosheleza nia zaMungu au kuwa watiifu kwa Mungu; hivyo basi, wao mara nyingi hawawezi kutambua matamanio yao ya kibinafsi au kuheshimu ahadi zao kwa Mungu. Mara nyingi wanajikuta katika hali zinazopingana: Wanatamani sana kumridhisha Mungu kwa kiwango kikubwa zaidi kinachowezekana, ilhali wanatumia uwezo wao wote kumpinga Yeye; mara nyingi wanaweka nadhiri kwa Mungu lakini kwa haraka sana wanaishia kuzivunja nadhiri zao. Hata mara nyingi zaidi wanajikuta katika hali zingine zinazopingana: Wanamwamini Mungu kwa dhati, ilhali wanamkana Yeye na kila kitu kinachotoka Kwake; wanatumai kwa hamu kwamba Mungu atawapa nuru, atawaongoza, atawaruzuku na kuwasaidia, ilhali bado wanatafuta njia yao wenyewe ya kutokea. Wanatamani kumwelewa na kumjua Mungu, ilhali hawako radhi kuwa na uhusiano wa karibu na Yeye. Badala yake, siku zote wanamwepuka Mungu; mioyo yao haiko wazi kumkaribisha. Ingawa wana ufahamu wa juu juu na uzoefu wa maana halisi ya matamshi ya Mungu na ya ukweli, na dhana ya juujuu ya Mungu na ukweli, bila kujua bado hawawezi kuthibitisha au kubainisha kama Mungu ndiye ukweli, wala hawawezi kuthibitisha kama Mungu kweli ni mwenye haki. Pia hawawezi kubainisha uhalisi wa tabia na kiini cha Mungu, achilia mbali uwepo Wake wa kweli. Imani yao katika Mungu siku zote ina mashaka na kutokuelewa kwingi, na pia ina mawazo na dhana. Wanapofurahia neema ya Mungu, pia kwa kusita wanapitia au kutenda baadhi ya ukweli ambao wanaona kuwa unaweza kutekelezeka ili kuimarisha imani yao, kuongeza uzoefu wao katika kumwamini Mungu, kuthibitisha uelewa wao wa kumwamini Mungu, na kutosheleza ubatili wao kwa kutembea juu ya njia ya uzima ambayo wao wenyewe waliianzisha na kutimiza vitendo vya haki vya wanadamu. Wakati huo huo, wao pia hufanya mambo haya ili kukidhi matamanio yao wenyewe ya kupata baraka, ambayo ni sehemu ya dau wanalofanya kwa matumaini ya kupokea baraka kubwa zaidi za binadamu, na ili kutimiza matamanio yao makubwa na hamu ya maisha yao yoteya kutopumzika mpaka pale ambapo wamempata Mungu. Watu hawa kwa nadra sana wanaweza kupokea nuru ya Mungu, kwani tamanio lao na nia yao ya kufaidi baraka ni muhimu sana kwao. Hawana tamanio la kuacha na hawawezi kuvumilia kutupilia mbali hili. Wanaogopa kwamba bila ya tamanio la kupata baraka, bila ya matamanio ya muda mrefu ya kutopumzika hadi wampate Mungu, wataweza kupoteza msukumo wa kumwamini Mungu. Kwa hivyo, hawapendi kukabiliana na uhalisi. Hawapendi kukabiliana na matamshi ya Mungu au kazi ya Mungu. Hawapendi kukabiliana na tabia au kiini cha Mungu, sembuse kuzungumzia hata mada ya kumjua Mungu. Hii ni kwa sababu mara tu Mungu, kiini Chake na tabia Yake ya haki vinapobadilisha maono yao, ndoto zao zitatoweka hivyo bila kuonekana; imani yao inayodhaniwa kuwa safi na “sifa njema” zilizokusanywa baada ya miaka ya kazi ngumu zitatoweka zote na kutokuwa na manufaa yoyote; “eneo” lao ambalo wameshinda kupitia kwa jasho na damu yao kwa miaka mingi litakuwa karibu kusambaratika. Hii itamaanisha kwamba miaka yao mingi ya kazi ngumu na jutihada vyote vimekuwa bure, na kwamba lazima waanze tena bila ya kuwa na chochote. Haya ndiyo maumivu makali sana kwao kuyavumlia katika mioyo yao, na ni matokeo ambayo hawangetamani kuyaona hata kidogo; hivyo basi, siku zote wamefungwa katika kizuizi cha aina hii, wakikataakurudi nyuma. Huyu ndiye mtu wa aina ya tatu: mtu anayekuwa katika awamu hii ya mtoto mchanga aliyeachishwa kunyonya.

Aina tatu za watu waliofafanuliwa hapo juu—kwa maneno mengine, watu wanaopatikana katika hatua hizi tatu—hawamiliki imani yoyote ya kweli katika utambulisho na hadhi ya Mungu au katika tabia Yake ya haki, na wala hawana utambuzi wowote wa wazi, wa uhakika au uthibitisho wa mambo haya. Kwa hivyo, ni vigumu sana kwa aina hizi tatu za watu kuingia kwenye uhalisi wa ukweli, na ni vigumu pia kwa wao kupokea huruma, ufahamu au mwangaza wa Mungu kwa sababu ya namna ambavyo wanamwamini Mungu na mtazamo wao potofu kwa Mungu unamfanya Yeye kutoweza kutekeleza kazi yoyote ndani ya mioyo yao. Mashaka yao, dhana zao potofu na mawazo yao juu ya Mungu yanazidi imani yao na ufahamu wao juu ya Mungu. Hizi ni aina tatu za watu walio katika hatari kubwa, na ni hatua tatu hatari sana. Wakati mtu anapoendeleza mtazamo wa shaka kwa Mungu, kiini cha Mungu, utambulisho wa Mungu, kwa suala la iwapo Mungu ndiye ukweli na uhalisi wa kuwepo Kwake, na wakati ambapo mtu hawezi kuwa na uhakika katika mambo haya, ni vipi ambavyo mtu anaweza kukubali kila kitu kinachotoka kwa Mungu? Mtu anawezaje kukubali ukweli kwamba Mungu ndiye ukweli, njia na uzima? Mtu anawezaje kukubali kuadibu na hukumu ya Mungu? Mtu anawezaje kukubali wokovu wa Mungu? Ni vipi ambavyo mtu wa aina hii anaweza kupokea mwongozo na ruzuku ya kweli kutoka kwa Mungu? Wale ambao wanapatikana katika awamu hizi tatu wanaweza kumpinga Mungu, kupitisha hukumu kwa Mungu, kumkufuru Mungu au kumsaliti Mungu wakati wowote. Wanaweza kuacha njia ya kweli na kumwacha Mungu wakati wowote. Mtu anaweza kusema kwamba watu katika hatua hizi tatu wapo katika kipindi cha hatari sana, kwani hawajaingia kwenye njia sahihi ya kumwamini Mungu.

Aina ya Nne: Hatua ya Mtoto Anayekomaa, au Kipindi cha Utoto

Baada ya mtu kuachishwa kunyonya—yaani, baada ya wao kufurahia kiasi cha kutosha cha neema—wanaanza kuchunguza ni nini maana ya kumwamini Mungu, wanaanza kutamani kuelewa maswali tofauti, kama vile kwa nini binadamu anaishi, binadamu anafaa kuishi vipi, na kwa nini Mungu hutekeleza kazi Yake kwa binadamu. Wakati ambapo mawazo haya yasiyo wazi na mawazo yaliyokanganyikiwa hujitokeza ndani yao, na kuwepo ndani yao, wanaendelea kupokea kunyunyizwa, na wao wanaweza pia kutekeleza wajibu wao. Kwenye kipindi hiki, hawana tena shaka kuhusiana na ukweli wa uwepo wa Mungu, na wanao ufahamu sahihi wa ni nini maana ya kumwamini Mungu. Kwenye msingi huu wao hupata maarifa ya Mungu hatua kwa hatua, na polepole wanapata baadhi ya majibu ya mawazo yao yasiyo wazi na mawazo yaliyokanganyika kuhusiana na tabia ya Mungu na kiini Chake. Kwa upande wa mabadiliko yao katika tabia pamoja na maarifa yao kuhusu Mungu, watu katika awamu hii huanza kushika njia sahihi na kuingia kwenye kipindi cha mabadiliko. Ni katika awamu hii ambapo watu huanza kuwa na maisha. Dalili za wazi za kumiliki uzima ni utatuzi wa taratibu wa maswali mbalimbali yanayohusiana na kumjua Mungu ambayo watu wanakuwa nayo katika mioyo yao—kama vile kutoelewana, mawazo, fikira, na ufafanuzi usio wazi wa Mungu—na sio tu kwamba wanakuja kweli kuamini na kutambua uhalisi wa uwepo wa Mungu, lakini pia wanakuja kumiliki ufafanuzi sahihi wa Mungu na kuwa na nafasi sahihi ya Mungu katika mioyo yao, na kumfuata Mungu kwa kweli kunachukua nafasi ya imani yao isiyo dhahiri. Katika hatua hii, watu wanaanza hatua kwa hatua kujua dhana zao potofu kwa Mungu, mambo yasiyo sahihi waliyofuatilia na njia za imani zisizo sahihi. Wanaanza kutamani ukweli, kutamani kupitia hukumu ya Mungu, kurudiwa na nidhamu, kutamani mabadiliko katika tabia yao. Kwa utaratibu wanaanza kuacha aina zote za dhana na fikira kuhusu Mungu katika hatua hii; wakati uo huo wanabadilisha na kurekebisha maarifa yasiyo sahihi kuhusu Mungu na kupata baadhi ya maarifa muhimu na sahihi kuhusu Mungu. Ingawa sehemu ya maarifa inayomilikiwa na watu katika awamu hii si mahususi au sahihi sana, kwa kiwango cha chini zaidi wanaanza kwa utaratibu kuacha dhana zao, maarifa ya kimakosa na kutoelewa mambo kuhusu Mungu; hawaendelezi tena dhana zao binafsi na fikira zao kuhusu Mungu. Wanaanza kujifunza namna ya kuacha—kuacha mambo yanayopatikana miongoni mwa dhana zao binafsi, kutoka kwa maarifa yao na kutoka kwa Shetani; wanaanza kuwa radhi kutii mambo sahihi na mazuri, hata kwa mambo yanayotoka kwenye matamshi ya Mungu na yanayopatana na ukweli. Wanaanza pia kujaribu kupata matamshi ya Mungu, kujua kibinafsi na kutekeleza matamshi Yake, kukubali matamshi Yake kama kanuni za matendo yao na kama msingi wa kubadilisha tabia yao. Kwenye kipindi hiki, watu bila kufahamu wanakubali hukumu na kuadibu kwa Mungu, wanakubali bila fahamu matamshi ya Mungu kuwa maisha yao. Huku wakikubali hukumu ya Mungu, kuadibu kwa Mungu, na kukubali matamshi ya Mungu, wanaendelea kupata ufahamu zaidi na kuweza kuhisi kwamba Mungu wanayemwamini ndani ya mioyo yao yuko kweli. Katika maneno ya Mungu, katika uzoefu wao na maisha yao, wanazidi kuhisi kwamba Mungu siku zote amesimamia hatima ya binadamu, kumwongoza binadamu na kumruzuku binadamu. Kupitia kwa ushirikiano wao na Mungu, wanaanza kwa utaratibu kuthibitisha uwepo wa Mungu. Kwa hivyo, kabla ya wao kutambua hilo, tayari wameidhinisha bila kujua na kuanza kuamini kwa dhati katika kazi ya Mungu, na wameidhinisha matamshi ya Mungu. Baada ya watu kuidhinisha matamshi ya Mungu, na kuidhinisha kazi ya Mungu, daima wao watajikana wenyewe, watakana dhana zao wenyewe, watakana maarifa yao wenyewe, watakana fikira zao wenyewe, na wakati huo huo pia bila kukoma watatafuta ukweli ni nini na mapenzi ya Mungu ni nini. Maarifa ya watu kuhusu Mungu ni ya juujuu sana kwenye kipindi hiki cha maendeleo—hawawezi hata kufafanua kwa uwazi maarifa haya kwa kutumia matamshi, wala hawawezi hata kufafanua kimahususi—na wanao tu ufahamu unaotegemea mtazamo; hata hivyo, wakati hatua hii inawekwa sambamba na zile awamu tatu zilizotangulia, maisha ya watu wasiokomaa katika kipindi hiki tayari yameanza kupokea unyunyiziaji na utolewaji wa matamshi ya Mungu, na hivyo tayari yameanza kuchipua. Maisha yao ni kama mbegu iliyofukiwa ardhini; baada ya kupokea unyevunyevu na virutubisho, lazima itapenyeza kupitia kwenye udongo; kuota kwake kunawakilisha kuzaliwa kwa maisha mapya. Kuzaliwa huku kwa maisha mapya kunaruhusu mtu kuona viashiria vya maisha. Kupitia kwa maisha, watu wataweza kukua. Kwa hivyo, juu ya misingi hii—hatua kwa hatua wataingia kwenye njia sahihi ya kuamini katika Mungu, wakiacha dhana zao wenyewe, wakipata mwongozo wa Mungu—maisha ya watu yataweza kukua bila shaka hatua kwa hatua. Ni katika msingi gani ndipo ukuaji huu unapimwa? Unapimwa kulingana na uzoefu wao na maneno ya Mungu na ufahamu wao wa kweli kuhusu tabia ya haki ya Mungu. Ingawa wanaona ni vigumu sana kutumia maneno yao wenyewe ili kufafanua kwa usahihi maarifa yao kuhusu Mungu na kiini Chake katika kipindi hiki cha ukuaji, kundi hili la watu haliko radhi tena kufuatilia kimsingi furaha kupitia kwa kufurahia neema ya Mungu, au kuamini katika Mungu ili kufuata kusudi lao la kupokea neema Yake. Badala yake, wako radhi kutafuta kuishi kwa neno la Mungu, ili kuwa walengwa wa wokovu wa Mungu. Vilevile, wanamiliki ujasiri na wako tayari kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu. Hii ndiyo alama ya mtu aliye katika hatua ya ukuaji.

Ingawa watu katika hatua hii wanayo maarifa fulani kuhusu tabia ya haki ya Mungu, maarifa yao si dhahiri na hayana uwazi. Huku wakiwa hawawezi kufafanua wazi hali hii, wanahisi kwamba tayari wamefaidi kitu fulani ndani kwa ndani, kwani wamepata kiasi fulani cha maarifa na ufahamu wa tabia ya haki ya Mungu kupitia kwa kuadibu kwa Mungu na hukumu yake; hata hivyo yote haya ni kana kwamba ni ya juujuu, na bado yapo katika hatua ya msingi. Kundi hili la watu lina mtazamo mahususi kuhusiana na neema ya Mungu. Mtazamo huu mahususi unaelezewa kupitia kwenye mabadiliko ya malengo wanayoyatafuta na njia ambayo wanayatafutia. Tayari wameona—katika maneno na kazi ya Mungu, katika kila aina ya mahitaji Yake kwa mwanadamu na katika ufunuo Wake kwa mwanadamu—kwamba kama bado hawatafuatilia ukweli, kama bado hawatafuti kuingia kwenye uhalisia, kama bado hawatafuti kumridhisha na kumjua Mungu wanapopitia maneno Yake, basi watapoteza umuhimu wa kuamini katika Mungu. Wanaona kwamba haijalishi ni kiwango kipi ambacho wanafurahia neema ya Mungu, hawawezi kubadilisha tabia zao, kumridhisha Mungu na kumjua Mungu, na kwamba kama watu wataendelea kuishi chini ya neema ya Mungu, basi hawatawahi kupata ukuaji, kupata uzima au kuweza kupokea wokovu. Kwa muhtasari, kama mtu hawezi kupitia maneno ya Mungu kwa njia ya kweli na hawezi kumjua Mungu kupitia kwa maneno Yake, mtu huyo daima dawamu atabakia katika awamu ile ya mtoto mchanga na hatawahi kupiga hatua yoyote mbele kwenye ukuaji wa maisha yake. Iwapo siku zote utabakia kwenye hatua ya mtoto mchanga, kama kamwe huingii kwenye uhalisi wa neno la Mungu, kama kamwe huna neno la Mungu kama maisha yako, kama kamwe huna imani na maarifa ya kweli kuhusu Mungu, je, kunao uwezekano wowote kwako wewe kufanywa kuwa kamili na Mungu? Hivyo basi, yeyote anayeingia katika uhalisi wa neno la Mungu, yeyote anayekubali neno la Mungu kuwa maisha yake, yeyote anayeanza kukubali kuadibu na hukumu ya Mungu, yeyote ambaye tabia yake potovu inaanza kubadilika, na yeyote aliye na moyo unaotamani ukweli, analo tamanio la kumjua Mungu, analo tamanio la kukubali wokovu wa Mungu—watu hawa ndio wale wanaomiliki uzima kwa kweli. Hii kwa kweli ndiyo aina ya nne ya mtu, ile ya mtoto anayekomaa, mtu aliye katika hatua ya utoto.

Aina ya Tano: Hatua ya Maisha Yaliyokomaa, au Hatua ya Mtu Mzima

Baada ya kupitia hatua ya utoto, hatua hii ya ukuaji imejaa misukosuko ya kujirudia rudia, maisha ya watu tayari yameimarishwa, hatua zao za kusonga mbele hazisimami tena, wala hakuna yeyote anayeweza kuwazuia. Ingawanjia iliyo mbele ingali na mabonde na misukosuko, si wanyonge tena au wenye woga; hawayumbiyumbi tena huko mbele au kupoteza mwelekeo wao. Misingi yao imekita mizizi ndani ya uzoefu halisi wa neno la Mungu. Mioyo yao imevutwa na hadhi na ukuu wa Mungu. Wanatamani kufuata nyayo za Mungu, kujua kiini cha Mungu, kumjua Mungu kwa ukamilifu Wake wote.

Watu katika hatua hii tayari wanajua waziwazi ni nani wanayemwamini, na wanajua wazi kwa nini wanapaswa kumwamini Mungu na maana ya maisha yao wenyewe, na pia wanajua wazi kwamba kila kitu ambacho Mungu anaeleza ni ukweli. Katika uzoefu wao wa miaka mingi, wametambua kwamba bila hukumu na kuadibu kwa Mungu, mtu hataweza kamwe kumridhisha au kumjua Mungu, na kamwe hawezi kuja mbele za Mungu kwa kweli. Ndani ya mioyo ya watu hawa kuna shauku kubwa ya kujaribiwa na Mungu, ili waweze kuona tabia ya haki ya Mungu wanapojaribiwa, na kufikia upendo safi zaidi, na wakati huo huo waweze kumwelewa na kumjua Mungu kwa njia ya kweli zaidi. Watu katika hatua hii tayari wameaga kabisa hatua ya mtoto mchanga, na hatua ya kufurahia neema ya Mungu na kula mkate na kushiba. Hawaweki tena matumaini mengi ya kupita kiasi juu ya kumfanya Mungu awavumilie na kuwaonea huruma; badala yake, wanao ujasiri wa kupokea na kutumai kupata kuadibu na hukumu ya Mungu isiyokoma, ili waweze kujitenga na tabia zao potovu na kumridhisha Mungu. Maarifa yao kwa Mungu, kufuatilia kwao au malengo yao ya mwisho ya ufuatiliaji wao: mambo haya yote yako wazi kabisa katika mioyo yao. Kwa hivyo, watu katika hatua ya watu wazima tayari wameaga kwaheri kabisa hatua ya imani isiyo dhahiri, hatua ambayo wanategemea neema kupata wokovu, kwenye hatua ya maisha yasiyo na ukomavu unaoweza kustahimili majaribu, kwenye hatua ya kutokuwa na uhakika, kwenye hatua ya kupapasa, kwenye hatua ya kukosa njia ya kutembea mara kwa mara, kwenye kipindi kisichokuwa thabiti cha kubadilisha kati ya joto na baridi kwa ghafla, na kwenye hatua ambayo mtu anamfuata Mungu huku akiwa ameyafumba macho yake. Mtu wa aina hii hupokea nuru na mwangaza wa Mungu mara kwa mara, na pia mara kwa mara hujihusisha katika ushirikiano na mawasiliano ya kweli na Mungu. Mtu anaweza kusema kwamba watu wanaoishi katika hatua hii tayari wameng’amua sehemu ya mapenzi ya Mungu; wanaweza kupata kanuni za ukweli katika kila kitu wanachofanya; wanajua namna ya kutosheleza tamanio la Mungu. Isitoshe, wamepata pia njia ya kumjua Mungu na wameanza kutoaushuhuda wa maarifa yao kwa Mungu. Wakati wa mchakato huu wa ukuaji wa taratibu, wanapata ufahamu wa taratibu na maarifa ya nia za Mungu: ya nia za Mungu katika kumuumba mwandamu, na nia za Mungu katika kumsimamia mwanadamu. Pia hatua kwa hatua wanapata ufahamu na maarifa ya tabia ya haki ya Mungu katika suala la kiini. Hakuna dhana za kibinadamu au mawazo yanayoweza kubadilisha maarifa haya. Ingawa mtu hawezi kusema kwamba katika hatua ya tano maisha ya mtu yamekomaa kabisa au kumwita mtu huyu mwenye haki au mkamilifu, mtu wa aina hii hata hivyo tayari amepiga hatua kuelekea kwenye hatua ya ukomavu katika maisha; mtu huyu tayari anaweza kuja mbele za Mungu, kusimama ana kwa ana na neno la Mungu na kuwa ana kwa ana na Mungu. Kwa sababu mtu wa aina hii tayari amepitia maneno mengi ya Mungu, amepitia majaribu yasiyohesabika na amepitia matukio yasiyohesabika ya nidhamu, hukumu na kuadibu kutoka kwa Mungu, unyenyekevu wake kwa Mungu si wa kutegemea chochote bali ni kamili. Maarifa yao juu ya Mungu yamebadilika kutoka katika hali ya kutokufahamu hadi kwenye maarifa yaliyo wazi na sahihi, kutoka yale ya juujuu hadi yale ya kina, kutoka kwenye hali ya utata na kutokuwa bainifu hadi hali ya umakinifu na thabiti, na wamebadilika kutoka kwenye kutafutatafuta kwa kupapasa na kutafuta kwa ulegevu hadi katika hali ya kuwa na maarifa kwa hakika na kushuhudia ukweli kwa vitendo. Inaweza kusemwa kwamba watu katika awamu hii wamemiliki uhalisi wa ukweli wa neno la Mungu, kwamba wamepitia kwenye njia ya kukamilishwa kama vile Petro alivyopita. Huyu ndiye mtu wa aina ya tano, yule anayeishi katika hali ya kuwa mkomavu—awamu ya kuwa mtu mzima.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Iliyotangulia: Kumjua Mungu (II)

Inayofuata: Kumjua Mungu (IV)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp