Siri Kuhusu Biblia

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 265)

Kwa miaka mingi, imani ya watu ya kitamaduni (hiyo ya Ukristo, moja ya dini kuu tatu za dunia) imekuwa ni kusoma Biblia; kujitenga na Biblia sio imani kwa Bwana, kujitenga na Biblia ni kufuata imani tofauti tofauti na uzushi, na hata pale watu wanaposoma vitabu vingine, msingi wa vitabu hivi ni lazima uwe ni ufafanuzi wa Biblia. Ni kusema kwamba, kama unasema unamwamini Bwana, basi ni lazima usome Biblia, unapaswa kula na kunywa Biblia, na nje ya Biblia hupaswi kuabudu kitabu kingine ambacho hakihusishi Biblia. Ikiwa utafanya hivyo, basi unamsaliti Mungu. Kuanzia kipindi ambapo kulikuwa na Biblia, imani ya watu kwa Bwana imekuwa imani katika Biblia. Badala ya kusema watu wanamwamini Bwana, ni bora kusema kwamba wanaamini Biblia; badala ya kusema wameanza kusoma Biblia, ni bora kusema wameanza kuamini Biblia; na badala ya kusema wamerudi mbele ya Bwana, ingekuwa vyema kusema wamerudi mbele ya Biblia. Kwa njia hii, watu wanaiabudu Biblia kana kwamba ni Mungu, kana kwamba ni damu yao ya uzima na kuipoteza itakuwa ni sawa na kupoteza maisha yao. Watu wanaitazama Biblia kuwa ni kuu kama Mungu, na hata kuna wale wanaoiona kuwa ni kuu kuliko Mungu. Kama watu hawatakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu, ikiwa hawawezi kuhisi Mungu, wanaweza kuendelea kuishi—lakini punde tu watakapoipoteza Biblia, au kupoteza sura na maneno maarufu sana kutoka katika Biblia, basi inakuwa ni kana kwamba wamepoteza maisha yao. Na hivyo, pale ambapo watu wataanza kumwamini Bwana wanaanza kusoma Biblia, na kuikariri Biblia, na kadri ya sehemu kubwa ya Biblia wanayoweza kukariri, ndivyo hii inathibitisha kwamba wanampenda Bwana na ni watu wenye imani kuu. Wale ambao wameisoma Biblia na wanaweza kuizungumzia kwa wengine wote ni kaka na dada wazuri. Kwa miaka yote hii, imani ya watu na uaminifu kwa Bwana vimepimwa kulingana na kiwango cha ufahamu wao wa Biblia. Watu wengi hawaelewi kwa nini wanapaswa kumwamini Mungu, wala jinsi ya kumwamini Mungu, na hawafanyi chochote zaidi ya kutafuta kiupofu dondoo ili kufasiri sura za Biblia. Watu hawajawahi kufuata mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu; muda wote huo, hawajafanya chochote, bali kujifunza na kuchunguza Biblia kwa papara, na hakuna hata mmoja ambaye amepata kazi mpya ya Roho Mtakatifu nje ya Biblia, hakuna ambaye amewahi kujitenga na Biblia, wala kuthubutu kujitenga na Biblia. Watu wamejifunza Biblia kwa miaka yote hii, wamekuja na maelezo mengi sana, na kufanya kazi kubwa sana, pia wana maoni mengi tofauti kuhusu Biblia, ambayo yamekuwa ni mdahalo usiokwisha, kiasi kwamba ziadi ya madhehebu elfu mbili yameanzishwa hadi leo. Wote wanataka kutafuta ufafanuzi maalumu, au siri za kina zaidi katika Biblia, wanataka kuichunguza, na kuipata katika usuli wa kazi ya Yehova katika Israeli, au usuli wa kazi ya Yesu katika Yudea, au siri nyingi zaidi ambazo hakuna yeyote anayejua. Watu wanavyoichukulia Biblia ni shauku na imani, na hakuna anayeweza kufafanua kikamilifu kisa cha ndani au kiini cha Biblia. Kwa hivyo, leo watu bado wana hisia zisizoelezeka za kimiujiza linapokuja suala la Biblia, na hata wana shauku nayo zaidi, na wanaiamini hata zaidi. Leo, kila mtu anataka kutafuta unabii wa kazi ya siku za mwisho katika Biblia, wanataka kugundua ni kazi gani Mungu hufanya wakati wa siku za mwisho na kuna ishara gani ya siku za mwisho. Kwa njia hii, kuabudu kwao Biblia kunakuwa na maana sana, na kadri wanaposogelea siku za mwisho, ndivyo wanavyozidi kuonyesha imani pofu kwa unabii wa Biblia, hususani ule wa siku za mwisho. Kwa imani hiyo ya upofu katika Biblia, kwa imani hiyo katika Biblia, hawana shauku ya kutafuta kazi ya Roho Mtakatifu. Katika dhana za watu, wanadhani kwamba ni Biblia pekee ndiyo inayoweza kuleta kazi ya Roho Mtakatifu; ni katika Biblia pekee ndimo wanamoweza kupata nyayo za Mungu; ni katika Biblia pekee ndimo kulimofichika siri za kazi ya Mungu; ni kwenye Biblia pekee—na sio katika vitabu vinginevyo au watu—wanaoweza kufafanua kila kitu cha Mungu na ujumla wa kazi Yake; Biblia inaweza kuleta kazi ya mbinguni duniani; na Biblia inaweza kuanzisha na kuhitimisha enzi. Kwa dhana hizi, watu hawana shauku kutafuta kazi ya Roho Mtakatifu. Hivyo, licha ya kiasi gani Biblia ilikuwa ina msaada mkubwa kwa watu wa wakati wa nyuma, imekuwa ni kikwazo katika kazi ya Mungu ya hivi karibuni. Bila Biblia, watu wanaweza kutafuta nyayo za Mungu mahali kwingineko, bado leo, nyayo zake zimejumuishwa na Biblia, na kupanua kazi Yake ya hivi karibuni, imekuwa na ugumu mara mbili, na mapambano magumu. Hii yote ni kwa sababu ya sura na misemo maarufu kutoka katika Biblia, vilevile unabii mbalimbali wa Biblia. Biblia imekuwa sanamu katika akili za watu, limekuwa ni fumbo katika akili zao, na hawawezi kabisa kuamini kwamba Mungu anaweza kufanya kazi nje ya Biblia, hawawezi kuamini kwamba watu wanaweza kumpata Mungu nje ya Biblia, achilia mbali kuwa na uwezo wa kuamini kwamba Mungu angeweza kujitenga na Biblia wakati wa kazi ya mwisho na kuanza upya. Hili suala haliingii akilini mwa watu; hawawezi kuliamini, na wala hawawezi kulifikiria. Biblia imekuwa kikwazo kikubwa kwa watu kukubali kazi mpya ya Mungu, na imefanya kuwa vigumu kwa Mungu kuipanua kazi hii mpya.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (1)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 266)

Baada ya Mungu kufanya kazi ya Sheria, Agano la Kale lilibuniwa, na ni hapo ndipo watu walianza kusoma Biblia. Baada ya Yesu kukuja, alifanya kazi ya Neema, na mitume Wake waliliandika Agano Jipya. Hivyo ndivyo Agano la Kale na Agano Jipya ya Biblia yalibuniwa, na hata leo, wale wote wanaomwamini Mungu wamekuwa wakisoma Biblia. Biblia ni kitabu cha historia. Ni kweli, pia kinahusisha baadhi ya unabii wa manabii, na unabii huu, kwa namna yoyote ile si historia. Biblia inajumuisha sehemu kadhaa—sio unabii tu, au kazi ya Yehova tu, wala hakuna nyaraka za Paulo pekee. Unapaswa kujua ni sehemu ngapi ambazo Biblia inajumuisha; Agano la Kale linajumuisha Mwanzo, Kutoka…, na pia kuna vitabu vya unabii ambavyo manabii waliandika. Mwishoni, Agano la Kale linakamilika kwa kitabu cha Malaki. Linarekodi kazi ya Enzi ya Sheria, ambayo iliongozwa na Yehova; kuanzia Mwanzo hadi Kitabu cha Malaki, ni rekodi kamilifu ya kazi ya Enzi ya Sheria. Ni sawa na kusema, Agano Jipya linarekodi yote ambayo yalipitiwa na watu ambao waliongozwa na Yehova katika Enzi ya Sheria. Wakati wa Enzi ya Sheria ya Agano la Kale, idadi kubwa ya manabii iliinuliwa na Yehova, walizungumza unabii kwa niaba Yake, walitoa maelekezo kwa makabila mbalimbali na mataifa, na wakatoa unabii juu ya kazi ambayo Yehova angefanya. Watu hawa ambao wameinuliwa wote walipewa na Yehova Roho ya unabii: Waliweza kutazama njozi kutoka kwa Yehova, na kusikia sauti Yake, na hivyo walivuviwa Naye na wakaandika unabii. Kazi waliyoifanya ilikuwa udhihirisho wa sauti ya Yehova, udhihirisho wa unabii wa Yehova, na kazi ya Yehova wakati huo ilikuwa ni kuwaongoza watu kwa njia ya Roho Mtakatifu; Hakufanyika mwili, na watu hawakuona uso Wake. Hivyo, aliwainua manabii wengi kufanya kazi Yake, na akawapatia mashauri ambayo waliyapelekea katika kila kabila na ukoo wa Israeli. Kazi yao ilikuwa ni kusema unabii, na baadhi yao waliandika maelekezo ya Yehova kwa ajili yao ili kuwaonesha wengine. Yehova aliwainua watu hawa kuzungumza unabii, kutoa unabii wa kazi ya wakati ujao au kazi ambayo ilikuwa bado haijafanyika wakati huo, ili kwamba watu wangeweza kutazama maajabu na hekima ya Yehova. Vitabu hivi vya unabii vilikuwa tofauti kabisa na vitabu vingine vya Biblia; yalikuwa ni maneno yaliyozungumzwa au kuandikwa na wale waliopewa Roho ya unabii—na wale ambao walipata njozi au sauti kutoka kwa Yehova. Kuacha vitabu vya unabii, kila kitu kingine katika Agano la Kale ni rekodi zilizochukuliwa na watu baada ya Yehova kukamilisha kazi Yake. Vitabu hivi haviwezi kusimama badala ya unabii uliozungumzwa na manabii walioinuliwa na Yehova, kama ambavyo Mwanzo na Kutoka haviwezi kulinganishwa na Kitabu cha Isaya na Kitabu cha Danieli. Unabii ulikuwa unazungumzwa kabla ya kazi haijafanyika; wakati huo, vitabu vingine viliandikwa baada ya kuwa kazi imemalizika, kazi ambayo watu walikuwa wanaiweza. Manabii wa wakati huo walivuviwa na Yehova na kuzungumza unabii, walizungumza maneno mengi, na walitoa unabii wa mambo ya Enzi ya Neema, na vilevile uharibifu wa dunia katika siku za mwisho—kazi ambayo Yehova alipanga kufanya. Vitabu vilivyosalia vyote vinarekodi kazi iliyofanywa na Yehova katika Israeli. Hivyo, unaposoma Biblia, unakuwa unasoma kile ambacho Yehova alifanya katika Israeli; Biblia ya Agano la Kale kimsingi inarekodi kazi ya Mungu ya kuwaongoza Israeli, kumtumia Musa kuwaongoza Waisraeli kutoka Misri, aliyewaondoa katika shida za Farao, na kuwachukua na kuwapeleka jangwani, ambapo baada ya hapo wakaingia Kaanani na kila kitu baada ya hapa ilikuwa ni kuanza maisha yao Kaanani. Yote, isipokuwa hii ni rekodi za kazi ya Yehova katika Israeli yote. Kila kitu kilichorekodiwa katika Agano la Kale ni kazi ya Yehova katika Israeli, ni kazi Aliyoifanya Yehova katika nchi ambapo Aliwaumba Adamu na Hawa. Kuanzia wakati ambapo Mungu alianza rasmi kuwaongoza watu duniani baada ya Nuhu, yote ambayo yamerekodiwa katika Agano la Kale ni kazi ya Israeli. Na kwa nini hakuna kazi yoyote iliyorekodiwa ambayo ni nje ya Israeli? Kwa sababu nchi ya Israeli ni chimbuko la binadamu. Mwanzoni hakukuwa na nchi yoyote tofauti na Israeli, na Yehova hakufanya kazi katika sehemu nyingine yoyote. Kwa namna hii, kile kilichorekodiwa katika Agano la kale la Biblia ni kazi ya Mungu katika Israeli pekee wakati huo. Maneno yaliyozungumzwa na manabii, na Isaya, Danieli, Yeremia na Ezekieli … maneno yao yanatabiri kazi Yake nyingine duniani, yanatabiri kazi ya Yehova Mungu Mwenyewe. Yote haya yalitoka kwa Mungu, ilikuwa ni kazi ya Roho Mtakatifu, na tofauti na vitabu hivi vya manabii, mambo mengine yote ni rekodi ya uzoefu wa watu juu ya kazi ya Yehova wakati huo.

Kazi ya uumbaji ilitokea kabla ya binadamu kuwepo, lakini Kitabu cha Mwanzo kilikuja tu baada ya kuwepo binadamu; kilikuwa ni kitabu kilichoandikwa na Musa wakati wa Enzi ya Sheria. Ni kama vitu vilivyotokea miongoni mwenu leo: Baada ya kutokea, mnayaandika ili kuwaonyesha watu katika maisha ya baadaye, na kwa watu wa baadaye, mliyoyarekodi ni mambo yaliyotokea wakati uliopita—na si chochote zaidi ya historia. Mambo yaliyorekodiwa katika Agano la Kale ni kazi ya Yehova katika Israeli, na kile kilichorekodiwa katika Agano Jipya ni kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema; ni rekodi ya kazi iliyofanywa na Mungu katika enzi mbili tofauti. Agano la Kale linarekodi kazi ya Mungu wakati wa Enzi ya Sheria, na hivyo Agano la Kale ni kitabu cha kihistoria, wakati Agano Jipya ni zao la kazi ya Enzi ya Neema. Wakati kazi mpya ilipoanza, hii pia ilipitwa na wakati—na hivyo, Agano Jipya pia ni kitabu cha kihistoria. Kimsingi Agano Jipya halina mpangilio mzuri kama Agano la Kale, wala halirekodi mambo mengi. Maneno yote mengi yaliyozungumzwa na Yehova yamerekodiwa katika Agano la Kale la Biblia, ambapo baadhi tu ya maneno ya Yesu yamerekodiwa katika Injili Nne. Ni kweli, Yesu pia alifanya kazi nyingi sana, lakini haikurekodiwa kwa kina. Mambo machache yamerekodiwa katika Agano Jipya ni kwa sababu ya kiasi cha kazi ambayo Yesu aliifanya; kiwango cha kazi Yake katika miaka mitatu na nusu duniani na kazi ile ya mitume ilikuwa ni pungufu zaidi kuliko kazi ya Yehova. Na hivyo, kuna vitabu vichache zaidi katika Agano Jipya kuliko Agano la Kale.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (1)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 267)

Biblia ni kitabu cha aina gani? Agano la Kale ni kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria. Agano la Kale la Biblia linarekodi kazi yote ya Yehova wakati wa Enzi ya Sheria na kazi Yake ya uumbaji. Lote linarekodi kazi iliyofanywa na Yehova, na hatimaye linahitimisha maelezo ya kazi ya Yehova kwa kitabu cha Malaki. Agano la Kale linarekodi kazi mbili zilizofanywa na Mungu: Moja ni kazi ya uumbaji, na nyingine ni kuamrisha sheria. Zote ni kazi zilizofanywa na Yehova. Enzi ya Sheria inawakilisha kazi chini ya jina la Yehova Mungu; ni ujumla wa kazi iliyofanywa kimsingi chini ya jina la Yehova. Hivyo, Agano la Kale linarekodi kazi ya Yehova, na Agano Jipya linarekodi kazi ya Yesu, kazi ambayo kimsingi ilifanywa chini ya jina la Yesu. Umuhimu wa jina la Yesu na kazi Aliyoifanya imerekodiwa sanasana katika Agano Jipya. Wakati wa Agano la Kale Enzi ya Sheria, Yehova alijenga hekalu na madhabahu katika Israeli, Aliongoza maisha ya Waisraeli duniani, kuzingatia kwamba walikuwa watu Wake, kundi la kwanza la watu ambalo alilichagua duniani na ambao walikuwa wanautafuta moyo Wake, kundi la kwanza ambalo Yeye Mwenyewe aliliongoza; ni sawa na kusema, makabila kumi na mawili ya Israeli walikuwa ni wateule wa kwanza wa Yehova, na hivyo siku zote Alifanya kazi ndani yao, hadi ambapo kazi ya Yehova ya Enzi ya Sheria ilihitimishwa. Hatua ya pili ya kazi ilikuwa ni kazi ya Enzi ya Neema ya Agano Jipya, na ilifanyika kati ya watu wa Kiyahudi, kati ya mojawapo ya makabila kumi na mawili ya Israeli. Mawanda ya kazi hii yalikuwa madogo kwa sababu Yesu alikuwa Mungu aliyepata mwili. Yesu alifanya kazi katika eneo lote la Yudea pekee, na Alifanya tu kazi ya miaka mitatu na nusu; hivyo, kile kilichorekodiwa katika Agano la Kale kiko mbali zaidi kupitiliza kiwango cha kazi kilichorekodiwa katika Agano la Kale.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (1)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 268)

Ikiwa unatamani kuiona kazi ya Enzi ya Sheria, na kuona jinsi gani Waisraeli waliifuata njia ya Yehova, basi ni lazima usome Agano la Kale; ikiwa unatamani kuelewa kazi ya Enzi ya Neema, basi ni lazima usome Agano Jipya. Lakini unawezaje kuona kazi ya siku za mwisho? Ni lazima ukubali uongozi wa Mungu wa leo, na kuingia katika kazi ya leo, maana hii ni kazi mpya na hakuna ambaye ameirekodi katika Biblia hapo nyuma. Leo, Mungu amefanyika mwili, na Amewachagua wateule wengine katika nchi ya China. Mungu anafanya kazi ndani ya watu hawa, Anaendelea na kazi Yake duniani, Anaendelea kutoka katika kazi ya Enzi ya Neema. Kazi ya leo ni njia ambayo mwanadamu hajawahi kuiendea, na njia ambayo hakuna mtu ambaye amewahi kuiona. Ni kazi ambayo haijawahi kufanywa hapo kabla—ni kazi ya Mungu ya hivi karibuni kabisa duniani. Hivyo, kazi ambayo haijawahi kufanywa kabla sio historia, kwa sababu sasa ni sasa, na bado haijawa muda uliopita. Watu hawajui kwamba Mungu amefanya kazi kubwa, mpya duniani, na nje ya Israeli, yaani imevuka mawanda ya Israeli, na zaidi ya unabii wa manabii, ambayo ni kazi mpya na ya kushangaza nje ya unabii, na kazi mpya kabisa nje ya Israeli, na kazi ambayo watu hawawezi kuielewa au kufikiria. Inawezekanaje Biblia kuwa na rekodi za wazi za kazi kama hiyo? Ni nani ambaye angeweza kurekodi kila hatua ya kazi ya leo, bila kuondoa kitu? Ni nani angeweza kurekodi kazi hii kubwa na yenye hekima ambayo inakataa maagano ya kitabu cha kale? Kazi ya leo sio historia, na kama vile, ikiwa unatamani kutembea katika njia ya leo, basi mnapaswa kutengana na Biblia, unapaswa kwenda mbele zaidi ya vitabu vya unabii au historia ya Biblia. Baada ya hapo tu ndipo utaweza kutembea njia mpya vizuri, na baada ya hapo ndipo utaweza kuingia katika ufalme mpya na kazi mpya. Unapaswa kuelewa ni kwa nini leo unaambiwa usisome Biblia, kwa nini kuna kazi nyingine ambayo inajitenga na Biblia, kwa nini Mungu haonekani mpya na wa kina zaidi katika Biblia, kwa nini badala yake kuna kazi kubwa zaidi nje ya Biblia. Haya ndiyo yote mnayopaswa kuelewa. Unapaswa kuelewa tofauti kati ya kazi ya zamani na kazi mpya, na hata kama hausomi Biblia, unapaswa kuitenganisha; kama hautaweza, bado utakuwa unaiabudu Biblia, na itakuwa ni vigumu sana kwako kuingia katika kazi mpya na kupitia mabadiliko mapya. Kwa kuwa kuna njia ya juu, kwa nini mjifunze hiyo ya chini, njia ya kale? Kwa kuwa kuna matamshi mapya, na kazi mpya, kwa nini uishi katikati ya rekodi za kale za kihistoria? Matamshi mapya yanaweza kukupa, ambayo yanathibitisha kwamba hii ni kazi mpya; rekodi za kale haziwezi kukushibisha, au kutosheleza mahitaji yako ya sasa, kitu ambacho kinathibitisha kwamba ni historia, na sio kazi ya hapa na sasa. Njia ya juu zaidi ni njia mpya zaidi, na kazi mpya, bila kujali njia ya zamani ni ya juu kiasi gani, bado ni historia ya kumbukumbu ya watu, na haijalishi ina thamani kiasi gani kama rejeleo, bado ni njia ya kale. Ingawa imerekodiwa katika “kitabu kitakatifu,” njia ya kale ni historia; ingawa hakuna rekodi yake katika “kitabu kitakatifu,” njia mpya ni ya hapa na sasa. Kwa njia hii inaweza kukuokoa, na kwa njia hii inaweza kukubadilisha, maana hii ni kazi ya Roho Mtakatifu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (1)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 269)

Biblia ni kitabu cha kihistoria, na ikiwa ungekula na kunywa Agano la Kale wakati wa Enzi ya Neema—ikiwa ungeweka katika vitendo kile kilichokuwa kinatakiwa katika wakati wa Agano la Kale wakati wa Enzi ya Neema—Yesu angekukataa, na kukuhukumu; ikiwa ungetumia Agano la Kale katika kazi ya Yesu, basi ungekuwa Farisayo. Ikiwa, leo, utaweka pamoja Agano Jipya na la Kale kula na kunywa, na kuliweka katika vitendo, basi Mungu wa leo Atakuhukumu; utakuwa umebaki nyuma ya kazi ya leo ya Roho Mtakatifu! Ikiwa unakula na kunywa Agano la Kale na Agano Jipya, basi upo nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu! Wakati wa kipindi cha Yesu, Yesu aliwaongoza Wayahudi na wale wote ambao walimfuata Yeye kulingana na kazi ya Roho Mtakatifu katika Yeye wakati huo. Hakuichukulia Biblia kama msingi wa kile Alichofanya, bali Alizungumza kulingana na kazi Yake; Hakutilia maanani kile ambacho Biblia ilisema, wala hakutafuta katika Biblia njia ya kuongoza wafuasi Wake. Kuanzia pale Alipoanza kufanya kazi, Aliongoza njia ya toba—neno ambalo halikutajwa kabisa katika unabii wa Agano la Kale. Sio kwamba tu Hakutenda kulingana na Biblia, lakini pia Aliongoza njia mpya, na Akafanya kazi mpya. Na wala Hakurejelea kabisa Biblia Alipohubiri. Wakati wa Enzi ya Sheria, hakuna ambaye aliweza kufanya miujiza Yake ya kuponya wagonjwa na kutoa mapepo. Hivyo, pia, kazi Yake, mafundisho Yake, na mamlaka na nguvu za maneno Yake yalizidi mtu yeyote wakati wa Enzi ya Sheria. Yesu alifanya tu kazi Yake mpya, na ingawa watu wengi walimhukumu kwa kutumia Biblia—na hata wakatumia Agano la Kale kumsulubisha—kazi Yake ilipitiliza Agano la Kale; kama hii haikuwa hivyo, kwa nini watu walimwangika msalabani? Ilikuwa ni kwa sababu haikusema kitu katika Agano la Kale la mafundisho Yake, na uwezo Wake wa kuponya wagonjwa na kutoa mapepo? Kazi Yake ilikuwa ni kwa ajili ya kuongoza katika njia mpya, haikuwa ni kwa makusudi ya kufanya ugomvi dhidi ya Biblia, au kwa makusudi kujitenga na Agano la Kale. Alikuja tu kufanya huduma Yake, kuleta kazi mpya kwa wale waliomtamani sana na kumtafuta. Hakuja kufafanua Agano la Kale au kutetea kazi yake. Kazi Yake bado haikuwa ni kwa ajili ya kuruhusu Enzi ya Sheria kuendelea kukua, maana kazi Yake haikuzingatia Biblia kama msingi wake; Yesu alikuja kufanya tu kazi ambayo Alipaswa kufanya. Hivyo, Hakufafanua unabii wa Agano la Kale, wala Hakufanya kazi kulingana na maneno ya Enzi ya Sheria ya Agano la Kale. Alipuuzia kile ambacho Agano la Kale lilisema, Hakujalia kama lilikubaliana na kazi Yake au la, na Hakujali kile ambacho watu wengine walijua kuhusu kazi Yake, au namna walivyokuwa wakiihukumu. Aliendelea tu kufanya kazi ambayo Alipaswa kufanya, ingawa watu wengi walitumia unabii waliousema manabii wa Agano la Kale kumhukumu. Ilionekana kwa watu kana kwamba kazi Yake haikuwa na msingi, na kulikuwa na mengi ambayo yalikuwa hayapatani na rekodi za Agano la Kale. Je, haya hayakuwa makosa ya mwanadamu? Je, kuna haja ya kutumia mafundisho ya dini katika kazi ya Mungu? Je, ni lazima iwe kulingana na maneno ya unabii waliyosema manabii? Hata hivyo, kipi ni kikubwa: Mungu au Biblia? Kwa nini ni lazima kazi ya Mungu iwe kulingana na Biblia? Je, inaweza kuwa kwamba Mungu hana haki ya kuwa juu ya Biblia? Je, Mungu hawezi kujitenga na Biblia na kufanya kazi nyingine? Kwa nini Yesu na wanafunzi Wake hawakutunza Sabato? Ikiwa Angetunza Sabato na matendo mengine kulingana na amri za Agano la Kale, kwa nini Yesu Hakutunza Sabato baada ya kuja, lakini badala yake Aliitawadha miguu, Akafunika kichwa, Akavunja mkate, na kunywa divai? Je, sio kwamba haya yote hayapatikani katika amri za Agano la Kale? Ikiwa Yesu aliliheshimu Agano la Kale, kwa nini Aliyakataa mafundisho haya. Unapaswa kujua ni kipi kilitangulia, Mungu au Biblia! Kuwa Bwana wa Sabato, je, Asingeweza pia kuwa Bwana wa Biblia?

Kazi iliyofanywa na Yesu wakati wa Agano Jipya ilifungua kazi mpya: Hakufanya kazi kulingana na kazi ya Agano la Kale, wala Hakutumia maneno yaliyozungumzwa na Yehova wa Agano la Kale. Alifanya kazi yake mwenyewe, na Alifanya kazi mpya zaidi, na kazi ambayo ilikuwa ya juu kuliko sheria. Hivyo, Alisema: “Msidhani ya kwamba Nilikuja kuiharibu torati au manabii; Sikuja kuharibu, bali kutimiliza.” Hivyo, kulingana na kile Alichokitimiza, mafundisho mengi yalikuwa yamevunjwa. Siku ya Sabato Alipowachukua wanafunzi wake kuenda katika shamba la nafaka, walichuma na kula masuke: Alikuwa Anaivunja Sabato, na Akasema, “Mwana wa Adamu ndiye Bwana hata wa siku ya sabato.” Kwa wakati huo, kulingana na sheria za Waisraeli, yeyote ambaye alikuwa haitunzi Sabato angepigwa na mawe hadi kufa. Hata hivyo Yesu, wala Hakuingia hekaluni wala Hakuitunza Sabato, na kazi Yake haikuwa imefanywa na Yehova wakati wa Agano la Kale. Hivyo, kazi aliyoifanya Yesu inapita sheria ya Agano la Kale, ilikuwa ni ya juu kuipita, na haikuwa na ulinganifu nayo. Wakati wa Enzi ya Neema, Yesu hakufanya kazi kulingana na sheria ya Agano la Kale, Aliyakataa mafundisho hayo. Lakini Waisraeli waliishikilia Biblia vikali na wakamshutumu Yesu—je, huku hukuwa kuikataa kazi ya Yesu? Leo, dunia ya dini pia inaishikilia Biblia vikali, na watu wengine husema, “Biblia ni kitabu kitakatifu, na inapaswa kusomwa.” Baadhi ya watu husema, “Kazi ya Mungu inapaswa itetewe milele, Agano la Kale ni agano la Mungu na Waisraeli, na haliwezi kubadilishwa, na Sabato inapaswa kutunzwa siku zote!” Je, hawa sio wapuuzi? Kwa nini Yesu Hakutunza Sabato? Je, Alikuwa Anafanya dhambi? Nani anaweza kuelewa mambo hayo? Haijalishi jinsi watu wanavyoisoma Biblia, itakuwa ni vigumu kuijua kazi ya Mungu kwa kutumia uwezo wao wa ufahamu. Hawatapata maarifa halisi ya Mungu, na fikira zao zitakuwa za ujinga kupita kiasi, kiasi kwamba wataanza kumpinga Mungu. Kama ingekuwa sio kwa ajili ya Mungu kupata mwili leo, watu wangeangamizwa na fikira zao wenyewe, na wangekufa katikati ya kuadibu kwa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (1)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 270)

Biblia pia huitwa Agano la Kale na Agano Jipya. Je, mnajua “agano” linarejelea nini? “Agano” katika Agano la Kale linatokana na makubaliano ya Yehova na watu wa Israeli Alipowaua Wamisri na kuwaokoa Waisraeli kutoka kwa Farao. Bila Shaka, uthibitisho wa haya makubaliano ulikuwa damu ya mwanakondoo iliyopakwa kwenye linta, kupitia kwayo Mungu Alianzisha agano na mwanadamu, moja ambalo ilisemwa kuwa wale wote waliokuwa na damu ya mwanakondoo juu na pembeni mwa viunzi vya mlango walikuwa Waisraeli, walikuwa wateuliwa wa Mungu, na wote wangeokolewa na Yehova (kwa kuwa Yehova wakati ule Alikuwa karibu kuwaua wazaliwa wa kwanza wa kiume wa Misri wote na wazaliwa wa kwanza wa kondoo na ng’ombe). Agano hili lina viwango viwili vya maana. Hakuna mmoja wa watu au wanyama wa Misri angeokolewa na Yehova; Angewaua wazaliwa wa kwanza wa kiume na wazaliwa wa kwanza wa kondoo na ng’ombe wao wote. Kwa hivyo, katika vitabu vingi vya unabii kulitabiriwa kwamba Wamisri wangeadibiwa vikali kutokana na agano la Yehova. Hiki ndicho kiwango cha kwanza cha maana cha agano. Yehova Aliwaua wazaliwa wa kwanza wa kiume wa Misri na wazaliwa wa kwanza wa mifugo wao wote, na kuwaacha Waisraeli wote, jambo lililomaanisha kuwa wale wote waliokuwa wa nchi ya Israeli walipendwa na Yehova na wote wangeokolewa; Alidhamiria kufanya kazi ya muda mrefu ndani yao, na Alianzisha agano nao kwa kutumia damu ya mwanakondoo. Tangu wakati ule kuendelea, Yehova Asingewaua Waisraeli na Alisema kuwa daima wangekuwa wateuliwa Wake. Angeianza kazi Yake ya Enzi Nzima ya Sheria Miongoni mwa makabila kumi na mawili ya Israeli, Angeziweka wazi sheria Zake zote kwa Waisraeli, na kuchagua manabii na waamuzi kutoka kati yao, na wangekuwa katikati ya kazi Yake. Yehova Agano nao: Angefanya kazi tu miongoni mwa wateuliwa isipokuwa enzi ibadilike. Agano la Yehova lilikuwa lisilobadilika kwani lilitengenezwa kwa damu, na lilianzishwa na wateuliwa Wake. La muhimu zaidi, Alikuwa Ameteua mawanda na malengo yafaayo ya kazi Yake katika enzi nzima, na kwa hivyo watu waliliona agano kuwa la umuhimu sana. Hiki ndicho kiwango cha pili cha maana ya agano. Isipokuwa kitabu cha Mwanzo, ambacho kilikuwepo kabla ya kuanzishwa kwa agano, vitabu vingine vyote vya Agano la Kale vinaeleza kuhusu kazi ya Mungu miongoni mwa Waisraeli baada ya kuanzishwa kwa agano hili. Bila shaka, yapo maelezo ya hapa na pale ya Watu wa Mataifa, ila kwa ujumla, Agano la Kale linaeleza kuhusu kazi ya Mungu nchini Israeli. Kwa sababu ya Agano kati ya Yehova na Waisraeli, vitabu vilivyoandikwa katika Enzi ya Sheria vinaitwa “Agano la Kale.” Vimepatiwa jina hili kutokana na agano la Yehova na Waisraeli.

Agano Jipya lilipatiwa jina hilo kutokana na damu iliyomwagwa na Yesu msalabani na agano Lake na wale wote waliomwamini. Agano la Yesu lilikuwa hili: Watu hawakuwa na budi kumwamini ili dhambi zao zisamehewe kwa kumwagika kwa damu Yake, na kwa njia hiyo wangeokolewa na kuzaliwa upya kupitia Kwake, na kamwe wasingeendelea kuwa wenye dhambi; watu walipaswa kumwamini ili wapokee neema Yake, na hawangeteseka jehanamu baada ya kufa. Vitabu vyote vilivyoandikwa wakati wa Enzi ya Neema vilizuka baada ya hili agano, na vyote vinaeleza kuhusu kazi na matamshi yaliyomo. Havielezi zaidi ya wokovu wa kusulubishwa kwa Bwana Yesu au hili agano; vyote ni vitabu vilivyoandikwa na wapendwa katika Bwana waliokuwa na tajriba. Kwa hivyo hivi vitabu vilevile vimepatiwa jina kutokana na agano: Vinaitwa Agano Jipya. Haya Maagano mawili yanajumuisha tu Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria na hayana uhusiano na enzi ya mwisho. Hivyo basi, Biblia haina msaada mkubwa kwa watu wa leo wa siku za mwisho. Zaidi, hutumika kama marejeleo ya muda mfupi, ila kimsingi haina matumizi ya thamani kubwa. Ila watu wa dini bado wanaienzi kuliko kitu kingine chochote. Hawaijui Biblia; wanajua tu jinsi ya kuieleza Biblia na kimsingi hawajui asili yake. Mtazamo wao kuhusu Biblia ni: Kila kitu katika Biblia ni sahihi, haina upungufu au makosa. Kwa sababu kwanza wameshakubali kwamba Biblia iko sahihi, bila makosa, wanaichunguza na kuitathimini kwa shauku kubwa. Hatua ya leo ya kazi haikutabiriwa kwa Biblia. Hakukutajwa kazi ya ushindi katika sehemu za giza zaidi, kwani hii ni kazi mpya zaidi. Kwa sababu enzi ya kazi ni tofauti, hata Yesu Mwenyewe hakufahamu kuwa hatua hii ya kazi ingefanywa katika siku za mwisho—basi, watu wa siku za mwisho wangetathimini vipi kuigundua hii hatua ya kazi katika Biblia?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (2)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 271)

Si kila kitu katika Biblia ni rekodi ya maneno aliyoyasema Mungu. Kimsingi Biblia inaandika hatua mbili za awali za kazi ya Mungu, ambapo sehemu moja ni rekodi ya utabiri wa kale wa manabii, na sehemu nyingine ni uzoefu na maarifa yaliyoandikwa na watu waliotumiwa na Mungu katika enzi zote. Uzoefu wa kibinadamu umetiwa doa na maoni na maarifa ya kibinadamu, kitu ambacho hakiepukiki. Katika vitabu vingi vya Biblia kuna dhana nyingi za kibinadamu, upendelevu wa binadamu, na ufahamu wa ajabu wa binadamu. Ni kweli, maneno mengi ni matokeo ya kupatiwa nuru na kuangaziwa na Roho Mtakatifu, na ni ufahamu sahihi—lakini haiwezi kusemwa kuwa ni udhihirishaji sahihi kabisa wa ukweli. Maoni yao juu ya vitu fulani si chochote zaidi ya maarifa yaliyotokana na uzoefu binafsi, au kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu. Utabiri wa manabii ulikuwa umeagizwa na Mungu binafsi: Unabii wa mifano ya Isaya, Danieli, Ezra, Yeremia, na Ezekieli, ulitoka moja kwa moja kwa Roho Mtakatifu; watu hawa walikuwa ni waonaji maono, walipokea Roho ya Unabii, wote walikuwa ni manabii wa Agano la Kale. Wakati wa Enzi ya Sheria watu hawa, ambao walikuwa wamepokea ufunuo wa Yehova, walizungumza unabii mwingi, ambao ulisemwa na Yehova moja kwa moja. Na kwa nini Yehova alifanya kazi ndani yao? Kwa sababu watu wa Israeli walikuwa ni wateule wa Mungu: Kazi ya manabii ilipaswa kufanyika miongoni mwao, na walikuwa wamefuzu kupokea maono hayo. Kimsingi, wao wenyewe hawakuelewa ufunuo wa Mungu kwao. Roho Mtakatifu Alizungumza maneno hayo kupitia vinywa vyao ili watu wa baadaye waweze kuelewa mambo hayo, na kuona kwamba ni kweli ilikuwa ni kazi ya Roho wa Mungu, ya Roho Mtakatifu, na haikutoka kwa mwanadamu, na kuweza kuwathibitishia kazi ya Roho Mtakatifu. Wakati wa Enzi ya Neema, Yesu Mwenyewe Alifanya kazi hii yote badala yao, na hivyo watu hawakuzungumza tena unabii. Kwa hivyo Yesu alikuwa nabii? Yesu, kimsingi alikuwa ni nabii, lakini pia Alikuwa na uwezo wa kufanya kazi ya mitume—: Aliweza kusema unabii na kuhubiri na kufundisha watu katika nchi yote. Bado kazi Aliyoifanya na utambulisho Aliouwakilisha haukuwa unafanana. Alikuja kuwakomboa binadamu wote, kumkomboa mwanadamu kutoka dhambini; Alikuwa nabii, na mtume, lakini zaidi ya hapo Alikuwa Kristo. Nabii Anaweza kuzungumza unabii, lakini haiwezi kusemwa kwamba yeye ni Kristo. Wakati huo, Yesu alizungumza unabii mwingi, na hivyo inaweza kusemwa kwamba Alikuwa nabii, lakini haiwezi kusemwa kwamba Alikuwa nabii na hivyo sio Kristo. Hiyo ni kwa sababu Alimwakilisha Mungu Mwenyewe katika kutekeleza hatua ya kazi, na utambulisho Wake ulikuwa tofauti na ule wa Isaya: Alikuja kukamilisha kazi ya ukombozi, na hivyo Alitoa maisha ya mwanadamu, na Roho wa Mungu Alikuja Kwake moja kwa moja. Katika kazi Aliyoifanya, hakukuwa na uvuvio wa kutoka kwa Roho wa Mungu au maelekezo kutoka kwa Yehova. Badala yake, Roho alifanya kazi moja kwa moja—kitu ambacho kinatosha kuthibitisha kwamba Yesu Hakuwa sawa na nabii. Kazi Aliyoifanya ilikuwa ni kazi ya ukombozi, kazi iliyoifuatia ilikuwa ni kuzungumza unabii. Alikuwa ni nabii, mtume, na zaidi ya hapo Alikuwa ni Mkombozi. Wakati huo, watabiri, wangeweza tu kuzungumza unabii, na walikuwa hawana uwezo wa kumwakilisha Roho wa Mungu katika kufanya kazi nyingine yoyote. Kwa sababu Yesu alifanya kazi kubwa ambayo haijawahi kufanywa na binadamu, na Alifanya kazi ya kumkomboa mwanadamu, kwa hiyo Alikuwa tofauti na manabii wengine kama Isaya.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (3)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 272)

Leo, watu wanaamini kwamba Biblia ni Mungu, na kwamba Mungu ni Biblia. Na hivyo pia, wanaamini kwamba maneno yote ya Biblia ni maneno pekee ambayo Mungu alizungumza, na kwamba yote yalizungumzwa na Mungu. Wale wanaomwamini Mungu hata wanafikia hatua ya kufikiri kwamba ingawa vitabu vyote sitini na sita vya Agano la Kale na Agano Jipya viliandikwa na watu, vyote viliandikwa kwa uvuvio wa Mungu, na ni rekodi ya matamshi ya Roho Mtakatifu. Huu ni ufahamu wenye makosa wa mwanadamu, na hauafikiani kabisa na kweli. Kimsingi, mbali na vitabu vya unabii, sehemu kubwa ya Agano la Kale ni rekodi ya kihistoria. Baadhi ya nyaraka za Agano Jipya zinatokana na uzoefu wa watu, na baadhi zinatokana na kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu; nyaraka za Paulo, kwa mfano, zilitokana na kazi ya mwanadamu, zote zilitokana na kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu, na ziliandikwa kwa ajili ya makanisa, yalikuwa ni maneno ya kushawishi na kutia moyo kwa kaka na dada wa makanisa. Hayakuwa maneno yaliyozungumzwa na Roho Mtakatifu—Paulo asingeweza kuzungumza kwa niaba ya Roho Mtakatifu, na wala hakuwa nabii, sembuse kuona maono ambayo Yohana aliona. Nyaraka zake ziliandikwa kwa ajili ya makanisa ya Efeso, Filadefia, Galatia, na makanisa mengineyo. Na hivyo, nyaraka za Paulo za Agano Jipya ni nyaraka ambazo Paulo aliandika kwa ajili ya makanisa, na sio uvuvio wa Roho Mtakatifu, wala sio matamshi ya moja kwa moja ya Roho Mtakatifu. Ni maneno tu ya kushawishi, faraja, na kutia moyo ambayo aliyaandika kwa ajili ya makanisa wakati wa kazi yake. Na hivyo pia, ni rekodi zaidi ya kazi na muda ya Paulo. Ziliandikwa kwa ajili ya kaka na dada wote katika Bwana, na zilikuwa ni kwa ajili ya kuwafanya kaka na dada wa makani yote ya wakati huo kufuata ushauri wake na kudumu siku zote katika njia zote za Bwana Yesu. Kwa namna yoyote ile Paulo hakusema kuwa, iwe ni kwa makanisa ya wakati huo au makanisa ya wakati ujao, yote yanapaswa kula na kunywa vitu alivyoandika, wala hakusema kwamba maneno yake yote yalitoka kwa Mungu. Kulingana na mazingira ya kanisa wakati huo, aliwasiliana tu na kaka na dada, na aliwashawishi, na akawaimarisha imani kwao; na aliwahubiria na kuwakumbusha watu na kuwashawishi. Maneno yake yalijikita katika mzigo wake mwenyewe, na aliwasaidia watu kupitia maneno haya. Alifanya kazi ya mitume wa kanisa wa wakati huo, alikuwa mfanyakazi ambaye alitumiwa na Bwana Yesu, na kwa hivyo lazima achukue jukumu kwa ajili ya makanisa, na lazima afanye kazi ya makanisa, alipaswa kujifunza kuhusu hali za ndugu—na kwa sababu hii, aliandika nyaraka kwa kaka na dada wote katika Bwana. Yote aliyoyasema ambayo yaliyokuwa ni ya kuadilisha na mazuri kwa watu yalikuwa sahihi, lakini hayakuwa yanawakilisha matamshi ya Roho Mtakatifu, na hayakuweza kumwakilisha Mungu. Ni uelewa mbaya kupita kiasi, na makufuru makubwa sana kwa watu kuchukulia rekodi za uzoefu wa mwanadamu na nyaraka za mwanadamu kama maneno yaliyozungumzwa na Roho Mtakatifu kwa makanisa! Hiyo ni kweli kabisa tunapokuja katika nyaraka ambazo Paulo aliziandika kwa ajili ya makanisa, kwani nyaraka zake ziliandikwa kwa ajili ya kaka na dada kulingana na mazingira na hali ya kila kanisa kwa wakati huo, na yalikuwa ni kwa ajili ya kuwashawishi kaka na dada katika Bwana, ili waweze kupokea neema ya Bwana Yesu. Nyaraka zake zilikuwa ni kwa ajili ya kuwaamsha kaka na dada wa wakati huo. Inaweza kusemwa kuwa huu ulikuwa ni mzigo wake mwenyewe, na pia ulikuwa ni mzigo aliopewa na Roho Mtakatifu; hata hivyo, alikuwa ni mtume aliyeyaongoza makanisa ya wakati huo, ambaye aliandika nyaraka kwa ajili ya makanisa na kuwashawishi, huo ulikuwa wajibu wake. Utambulisho wake ulikuwa tu ni mtume anayefanya kazi, na alikuwa ni mtume tu aliyetumwa na Mungu; hakuwa mtabiri, wala mtoa unabii. Kwake, kazi yake mwenyewe na maisha ya kaka na dada yalikuwa na umuhimu mkubwa sana. Hivyo, asingeweza kuzungumza kwa niaba ya Roho Mtakatifu. Maneno yake hayakuwa maneno ya Roho Mtakatifu, wala yasingesemwa kuwa ni maneno ya Mungu, maana Paulo hakuwa chochote zaidi ya kiumbe wa Mungu, na hakika hakuwa Mungu aliyepata mwili. Utambulisho wake haukuwa sawa na ule wa Yesu. Maneno ya Yesu yalikuwa ni maneno ya Roho Mtakatifu, yalikuwa ni maneno ya Mungu, maana utambulisho wake ulikuwa ule wa Kristo—Mwana wa Mungu. Inawezekanaje Awe sawa na Paulo? Ikiwa watu wanaona nyaraka au maneno kama ya Paulo kama matamshi ya Roho Mtakatifu, na kuwaabudu kama Mungu, basi inaweza kusemwa tu kuwa ni watu wasiochagua kwa busara. Tukisema kwa ukali zaidi, haya sio makufuru? Inawezekanaje mwanadamu azungumze kwa niaba ya Mungu? Na inawezekanaje watu wapigie magoti rekodi za nyaraka zake na maneno aliyoyazungumza kana kwamba yalikuwa ni kitabu kitakatifu, au kitabu cha mbinguni? Je, inawezekana maneno ya Mungu kutamkwa kwa kawaida na mwanadamu? Inawezekanaje mwanadamu azungumze kwa niaba ya Mungu? Na hivyo, unasemaje—kwamba nyaraka alizoandika kwa ajili ya makanisa haziwezi kutiwa doa na mawazo yake mwenyewe? Inawezekanaje zisitiwe doa na mawazo ya kibinadamu? Aliandika nyaraka kwa makanisa kulingana na uzoefu wake binafsi, na maarifa yake binafsi. Kwa mfano, Paulo aliandika waraka kwa kanisa la Wagalatia ambao ulikuwa na maoni fulani, na Petro aliandika waraka mwingine, ambao ulikuwa na mtazamo mwingine. Ni upi kati ya hizo ulitoka kwa Roho Mtakatifu? Hakuna anayeweza kutoa jibu, hakika. Hivyo inaweza kusemwa tu kwamba wote wanawiwa na mzigo kwa makanisa, lakini barua zao zinawakilisha kimo chao, zinawakilisha vile wanavyowapatia na kuwasaidia kaka na dada, na vile wanavyowiwa na makanisa, na zinawakilisha tu kazi ya binadamu; hayakuwa ya Roho Mtakatifu kabisa. Ikiwa unasema kwamba nyaraka zake ni maneno ya Roho Mtakatifu, basi wewe ni mpumbavu, na unafanya makufuru! Nyaraka za Paulo na nyaraka nyingine za Agano Jipya ni sawa na kumbukumbu za viongozi mashuhuri wa kiroho wa hivi karibuni. Zipo sawa na vitabu vya Watchman Nee au uzoefu wa Lawrence, na kadhalika. Ni vile tu vitabu vya viongozi mashuhuri wa kiroho wa hivi karibuni havijajumuishwa katika Agano Jipya, lakini hulka ya watu hawa ni sawa: Kulikuwa na watu ambao walitumiwa na Roho Mtakatifu wakati fulani, na hawakuweza kumwakilisha Mungu moja kwa moja.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (3)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 273)

Injili ya Mathayo ya Agano Jipya inaandika ukoo wa Yesu. Mwanzoni, inasema kwamba Yesu alikuwa mzao wa Abrahamu na wa Daudi, na mwana wa Yusufu; sehemu inayofuata inasema kwamba Yesu alizaliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu, na kuzaliwa na bikira—kitu kinachomaanisha kwamba Hakuwa mwana wa Yusufu au mzao wa Abrahamu na wa Daudi. Hata hivyo, orodha ya ukoo inasisitiza kumhusisha Yesu na Yusufu. Sehemu inayofuata, orodha ya ukoo inaanza kurekodi mchakato ambao kwa huo Yesu alizaliwa. Inasema mimba ya Yesu ilitungwa kwa njia ya Roho Mtakatifu, kwamba Alizaliwa na bikira, na sio mwana wa Yusufu. Lakini katika orodha ya ukoo imeandikwa waziwazi kwamba Yesu alikuwa mwana wa Yusufu, na kwa kuwa orodha ya ukoo iliandikwa kwa ajili ya Yesu, inaandika vizazi arobaini na mbili. Inapokwenda katika ukoo wa Yusufu, inasema kwa haraka kwamba Yusufu alikuwa mume wa Mariamu, haya ni maneno kwa ajili ya kuthibitisha kwamba Yesu alikuwa mzao wa Abrahamu. Je, huu si mkanganyiko? Orodha hii ya ukoo inaonyesha waziwazi chimbuko la Yusufu, ni wazi kwamba hii ni orodha ya ukoo wa Yusufu, lakini Mathayo anasisitiza kwamba ni orodha ya ukoo wa Yesu. Je, hii haipingi ukweli kwamba Yesu alizaliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu? Hivyo, orodha ya ukoo iliyoandikwa na Mathayo sio mawazo ya kibinadamu? Hii ni dhihaka! Kwa namna hii, unaweza kujua kwamba kitabu hiki sio chote kimetoka kwa Roho Mtakatifu. Pengine, kuna baadhi ya watu wanaodhani kwamba Mungu lazima atakuwa na orodha ya ukoo duniani, na matokeo yake ni kwamba wanampachika Yesu kama kizazi cha arobaini na viwili cha Abrahamu. Hii ni dhihaka kabisa! Baada ya kuja duniani, Mungu angewezaje kuwa na orodha ya ukoo? Ikiwa unasema kwamba Mungu ana ukoo, je, humweki katika madaraja sawa miongoni mwa viumbe wa Mungu? Maana Mungu si wa ulimwengu, Yeye ni Bwana wa uumbaji, na ingawa yeye ni wa mwili, hana asili sawa na mwanadamu. Unawezaje kumweka Mungu katika daraja sawa na viumbe wa Mungu? Abrahamu hawezi kumwakilisha Mungu; alikuwa ni mhusika wa kazi ya Yehova wakati huo, alikuwa ni mtumishi mwaminifu tu aliyethibitishwa na Yehova, na alikuwa mmoja wa watu wa Israeli. Inawezekanaje awe babu wa Yesu?

Ni nani aliandika orodha ya ukoo wa Yesu? Ni Yesu Mwenyewe ndiye aliyeandika? Je, ni Yesu Mwenyewe ndiye Alisema, “Andika orodha Yangu ya ukoo”? Iliandikwa na Mathayo baada ya Yesu kuangikwa msalabani. Wakati huo, Yesu alikuwa amefanya kazi kubwa ambayo ilikuwa haifahamiki kwa mitume, na Hakutoa maelezo yoyote. Baada ya Yeye kuondoka, mitume walianza kuhubiri na kufanya kazi kila mahali, na kwa ajili ya hatua hiyo ya kazi, walianza kuandika nyaraka na vitabu vya injili. Vitabu vya injili ya Agano Jipya vilirekodiwa miaka ishirini hadi thelathini baada ya Yesu kusulubiwa msalabani. Kabla ya hapo, watu wa Israeli walisoma tu Agano la Kale. Hiyo ni sawa na kusema, mwanzoni mwa Enzi ya Neema watu walisoma Agano la Kale. Agano Jipya lilionekana tu wakati wa Enzi ya Neema. Agano Jipya halikuwepo wakati wa kazi ya Yesu; watu waliandika kazi Yake baada ya kuwa amefufuka na kupaa mbinguni. Baada ya hapo kulikuwa na Injili Nne, katika nyongeza hiyo pia kulikuwa na nyaraka za Paulo na Petro, na vile vile kitabu cha Ufunuo. Ni baada tu ya zaidi ya miaka mia tatu baada ya Yesu kupaa mbinguni, wakati vizazi vilivyofuata viliweka pamoja rekodi zao, ndipo kulikuwa na Agano Jipya. Ni baada tu ya kazi hii kukamilika ndipo kukapatikana Agano Jipya; halikuwepo hapo kabla. Mungu alikuwa amefanya kazi yote hiyo, mtume Paulo alifanya kazi yote hiyo, na baadaye nyaraka za Paulo na Petro ziliunganishwa, na njozi kuu zaidi iliyorekodiwa na Yohana katika kisiwa cha Patmo iliwekwa mwishoni, maana ilikuwa inatoa unabii wa kazi ya siku za mwisho. Hii yote ilikuwa ni mipango ya vizazi vilivyofuata na ni tofauti na matamshi ya leo. Kile kilichorekodiwa leo ni kulingana na hatua za kazi ya Mungu; kile ambacho watu wanashughulika nacho leo ni kazi ambayo imefanywa na Mungu Mwenyewe, na maneno yaliyotamkwa na Mungu Mwenyewe. Wewe—mwanadamu—hupaswi kuingilia; maneno, ambayo yanatoka moja kwa moja kwa Roho Mtakatifu, yamepangwa hatua kwa hatua, na ni tofauti na mpangilio wa rekodi za wanadamu. Inaweza kusemwa kuwa, kile walichorekodi kilikuwa ni kulingana na kiwango chao cha elimu na tabia. Kile walichokirekodi kilikuwa ni uzoefu wa wanadamu, na kila mmoja alikuwa na namna yake ya kurekodi na kuelewa, na kila rekodi ilikuwa tofauti. Hivyo, ikiwa unaiabudu Biblia kama Mungu wewe ni mjinga na mpumbavu wa kutupwa! Kwa nini usitafute kazi ya Mungu wa leo? Ni kazi ya Mungu tu ndiyo inayoweza kumwokoa mwanadamu. Biblia haiwezi kuwaokoa wanadamu, wanaweza kuisoma kwa maelfu kadhaa ya miaka na bado hakutakuwa na mabadiliko hata kidogo ndani yao, na kama unaiabudu Biblia hutaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (3)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 274)

Watu wengi wanaamini kwamba kuelewa na kuwa na uwezo wa kufasiri Biblia ni sawa na kutafuta njia ya kweli—lakini, kimsingi, je, vitu ni rahisi sana? Hakuna anayejua uhalisia wa Biblia: kwamba si kitu chochote zaidi ya rekodi ya kihistoria ya kazi ya Mungu, na agano la hatua mbili zilizopita za kazi ya Mungu, na haikupatii ufahamu wa malengo ya kazi ya Mungu. Kila mtu ambaye amesoma Biblia anajua kwamba inarekodi hatua mbili za kazi ya Mungu wakati wa Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Agano la Kale linaandika historia ya Israeli na kazi ya Yehova kuanzia wakati wa uumbaji hadi mwisho wa Enzi ya Sheria. Agano Jipya linarekodi kazi ya Yesu duniani, ambayo ipo katika Injili Nne, vilevile kazi ya Paulo; je, sio rekodi za kihistoria? Kuleta mambo ya zamani leo kunayafanya yawe historia, haijalishi yana ukweli kiasi gani, bado ni historia—na historia haiwezi kushughulikia masuala ya leo. Maana Mungu haangalii historia! Na hivyo, kama unaelewa tu Biblia, na huelewi chochote kuhusu kazi ambayo Mungu anakusudia kufanya leo, na kama unamwamini Mungu, na hutafuti kazi ya Roho Mtakatifu, basi hujui inamaanisha nini kumtafuta Mungu. Ikiwa unasoma Biblia kwa lengo la kujifunza historia ya Israeli, kutafiti historia ya uumbaji wa Mungu wa mbingu na dunia, basi humwamini Mungu. Lakini leo, kwa kuwa unamwamini Mungu, na kutafuta uzima, kwa kuwa unatafuta maarifa juu ya Mungu, na hutafuti nyaraka na mafundisho mfu, au ufahamu wa historia, unapaswa kutafuta mapenzi ya Mungu ya leo, na unapaswa kutafuta uongozi wa kazi ya Roho Mtakatifu. Kama ungekuwa mwanaakiolojia ungeweza kusoma Biblia—lakini wewe sio mwanaakiolojia, wewe ni mmoja wa wale wanaomwamini Mungu, na utakuwa bora zaidi ukitafuta mapenzi ya Mungu ya leo. Kwa kusoma Biblia, angalau utakuwa umeelewa sehemu ndogo ya historia ya Israeli, utajifunza kuhusu maisha ya Abrahamu, Daudi, na Musa, utajua kuhusu namna walivyomheshimu sana Yehova, namna ambavyo Yehova aliwachoma wale waliompinga, na jinsi alivyozungumza na watu wa enzi hiyo. Utaelewa tu kuhusu kazi ya Mungu katika wakati uliopita. Rekodi za Biblia zinahusiana na jinsi ambavyo watu wa awali wa Israeli walivyomheshimu sana Mungu na kuishi chini ya uongozi wa Yehova. Kwa sababu Waisraeli walikuwa ni wateuliwa wa Mungu, katika Agano la Kale unaweza kuona utii wote wa watu wa Israeli kwa Yehova, jinsi ambavyo wale wote waliomtii Yehova walivyokuwa wanaangaliwa na kubarikiwa Naye, unaweza kujifunza kwamba Mungu alipofanya kazi katika Israeli alikuwa mwingi wa rehema na mapenzi, vilevile alikuwa na moto uteketezao, na kwamba Waisraeli wote, kuanzia watu wa chini hadi wakubwa, walimheshimu sana Yehova, na hivyo nchi yote ilibarikiwa na Mungu. Hiyo ni historia ya Israeli iliyorekodiwa katika Agano la Kale.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (4)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 275)

Biblia ni rekodi ya kihistoria ya kazi ya Mungu katika Israeli, na inaandika utabiri mwingi wa manabii wa kale vilevile baadhi ya matamshi ya Yehova katika kazi Yake wakati huo. Hivyo, watu wote wanakitazama kitabu hiki kama kitakatifu (maana Mungu ni mtakatifu na mkuu). Kimsingi, hii yote ni matokeo ya uchaji wao kwa Yehova na vile walivyokuwa wanampenda Mungu. Watu wanarejelea kitabu hiki kwa namna hii kwa sababu tu viumbe wa Mungu wacha Mungu na wanampenda Muumba wao sana, na hata kuna wale ambao wanakiita kitabu hiki kitabu cha mbinguni. Kimsingi, ni rekodi tu za kibinadamu. Hakikupewa jina na Yehova Mwenyewe, wala Yehova Mwenyewe hakuongoza utengenezaji wake. Kwa maneno mengine, mwandishi wa kitabu hiki sio Mungu, bali ni wanadamu. Biblia Takatifu ni jina la heshima tu lililotolewa na mwanadamu. Jina hili halikuamuliwa na Yehova na Yesu baada ya Wao kujadiliana; si chochote zaidi ya mawazo ya kibinadamu. Maana kitabu hiki hakikuandikwa na Yehova, wala kuandikwa na Yesu. Badala yake, ni maelezo yaliyotolewa na manabii wengi wa kale, mitume na waonaji maono, ambayo baadaye yalipangiliwa na vizazi vilivyofuata na kuwa kitabu cha maandiko ya kale, ambayo kwa watu, yanaonekana kuwa matakatifu, kitabu ambacho wanaamini kimejumuisha siri nyingi ambazo hazieleweki na za kina ambazo zinasubiri kufunguliwa na vizazi vijavyo. Kwa namna hiyo, watu hata wanaamini kwamba kitabu hiki ni kitabu cha mbinguni. Ukijumlisha Injili Nne na Kitabu cha Ufunuo, mtazamo wa watu kuhusu kitabu hicho ni tofauti kabisa na vitabu vingine, na hivyo hakuna mtu anayethubutu kukichambua hiki “kitabu cha mbinguni” kwa sababu ni “kitakatifu” sana.

Kwa nini, mara tu baada ya watu kusoma Biblia wanakuwa na uwezo wa kupata njia sahihi ya kukiweka katika matendo? Kwa nini wanakuwa na uwezo wa kupata mengi ambayo yalikuwa hayafahamiki kwao? Leo, Ninaichambua Biblia kwa namna hii na haimaanishi kwamba Naichukia, au kukana thamani yake kwa ajili ya marejeleo. Ninakuelezea na kukufafanulia thamani ya asili na chanzo cha Biblia ili uweze kuondoka katika giza. Maana watu wana mitazamo mingi kuhusu Biblia, na mingi yao ina makosa; kusoma Biblia kwa namna hii sio tu kunawazuia kupata kile wanachopaswa kupata, lakini, muhimu zaidi, kunazuia kazi Niliyokusudia kufanya. Inaingilia kati kazi ya siku zijazo kwa kiasi kikubwa, na inatoa hasara tu, na wala sio faida. Hivyo, Ninachokufundisha ni hulka tu na kisa cha ndani cha Biblia. Sikwambii kwamba usisome Biblia, au uzunguke ukitangaza kwamba haina thamani kabisa, bali kwamba uweze kuwa na maarifa na mtazamo sahihi juu ya Biblia. Usiegemee upande mmoja sana! Ingawa Biblia ni kitabu cha historia kilichoandikwa na wanadamu, pia kinaandika kanuni nyingi ambazo kwazo watakatifu wa zamani na manabii walimhudumia Mungu, vilevile uzoefu wa hivi karibuni wa mitume katika kumhudumia Mungu—yote haya yalishuhudiwa na kujulikana kwa watu hawa, na inaweza kutumika kama rejeleo kwa ajili ya watu wa enzi hii katika kutafuta njia ya kweli. Hivyo, katika kusoma Biblia watu wanaweza pia kupata njia nyingi za maisha ambazo haziwezi kupatikana katika vitabu vingine. Njia hizi ni njia za maisha ya kazi ya Roho Mtakatifu ambazo manabii na mitume walizipitia katika enzi iliyopita, na maneno mengi ni ya thamani, na yanaweza kutoa kile ambacho watu wanataka. Hivyo, watu wote wanapenda kusoma Biblia. Kwa sababu kuna mambo mengi sana yaliyofichwa katika Biblia, mitazamo ya watu juu ya Biblia ni tofauti na mitazamo yao juu ya maandiko ya viongozi wa kiroho mashuhuri. Biblia ni rekodi na mkusanyiko wa uzoefu na maarifa ya watu ambao walimhudumia Yehova na Yesu katika enzi ya kale na mpya, na pia vizazi vya baadaye vimeweza kupata nuru, mwanga mkubwa na njia za kuweza kutembea kwazo. Sababu ya Biblia kuwa na hadhi ya juu kuliko maandiko ya kiongozi yeyote mkubwa wa kiroho ni kwa sababu maandiko yao yote yanatoka katika Biblia, uzoefu wao wote unatokana na Biblia, na wote wanaelezea Biblia. Na hivyo, ingawa watu wanaweza wakafaidika na vitabu kutoka kwa kiongozi yeyote wa kiroho mashuhuri, bado wanaiabudu Biblia, maana kwao, inaonekana ni ya juu sana na ya kina sana! Ingawa Biblia inaleta pamoja baadhi ya vitabu vya maneno ya uzima, kama vile nyaraka za Paulo na nyaraka za Petro, na ingawa watu wanaweza kusaidiwa na vitabu hivi, vitabu hivi bado vimepitwa na wakati, bado ni vitabu vya enzi ya kale, na haijalishi ni vizuri kiasi gani, vinafaa tu kwa ajili ya kipindi kimoja, na wala sio vya milele. Maana kazi ya Mungu siku zote inaendelea, na haiwezi kusimama tu katika kipindi cha Paulo na Petro, au siku zote ibaki katika Enzi ya Neema, enzi ambayo Yesu alisulubiwa. Na hivyo, vitabu hivi vinafaa tu katika Enzi ya Neema, na wala sio kwa ajili ya Enzi ya Ufalme wa siku za mwisho. Vinaweza tu kuwa na manufaa kwa waumini wa Enzi ya Neema, na sio kwa watakatifu wa Enzi ya Ufalme, na haijalishi ni vizuri kiasi gani, bado havifai kwa kipindi hiki. Ni sawa na kazi ya Yehova ya uumbaji au kazi Yake katika Israeli: Haijalishi kazi hii ilikuwa kubwa kiasi gani, bado imepitwa na wakati, na muda utaendelea kuja wakati umekwishapita. Kazi ya Mungu pia ni ile ile: Ni nzuri, lakini muda utafika ambapo itakoma; siku zote haitaendelea kubaki katikati ya kazi ya uumbaji, wala katikati ya kazi ile ya msalaba. Haijalishi kazi ya msalaba inashawishi kiasi gani, haijalishi ilikuwa ya ufanisi kiasi gani katika kumshinda Shetani, hata hivyo, kazi bado ni kazi, na enzi, hata hivyo bado ni enzi; kazi siku zote haiwezi kubaki katika msingi ule ule, wala nyakati haziwezi kukosa kubadilika, kwa sababu kulikuwa na uumbaji na lazima kuwepo na siku za mwisho. Hii haiepukiki! Hivyo, leo maneno ya uzima katika Agano Jipya—nyaraka za mitume, na Injili Nne—vimekuwa vitabu vya kihistoria, vimekuwa vitabu vya kale, na inawezekanaje vitabu vya kale kuwapeleka watu katika enzi mpya? Haijalishi ni kiasi gani vitabu hivi vinaweza kuwapatia watu uzima, haijalishi vina uwezo kiasi gani katika kuwaongoza watu kwenye msalaba, ndio kwamba havijapitwa na wakati? Havijaondokewa na thamani? Hivyo, Ninasema hupaswi kuviamini vitabu hivi bila kufikiri. Ni vya zamani sana, haviwezi kukupeleka katika kazi mpya, vinaweza kukulemea tu. Sio tu haviwezi kukuleta katika kazi mpya, na katika kuingia kupya, bali vinakupeleka katika makanisa ya dini ya kale na kama ni hivyo, havirudishi nyuma imani yako kwa Mungu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (4)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 276)

Leo, nani kati yenu anathubutu kusema kwamba maneno yote yaliyotamkwa na wale waliotumiwa na Roho Mtakatifu yalitoka kwa Roho Mtakatifu? Kuna anayethubutu kusema mambo kama haya? Ukisema mambo kama haya, basi mbona kitabu cha Ezra cha unabii kiliondolewa, na mbona jambo hilo pia likafanyiwa vitabu vya watakatifu na manabii wa kale? Kama yote yalitoka kwa Roho Mtakatifu, basi mbona mnathubutu kufanya maamuzi ambayo yanabadilika kama haya? Umehitimu kuchagua kazi ya Roho Mtakatifu? Hadithi nyingi kutoka Israeli pia zilitolewa. Na ukiamini kwamba maandishi haya yote ya kale yalitoka Roho Mtakatifu, basi mbona baadhi ya vitabu vilitolewa? Kama yote yalitoka kwa Roho Mtakatifu, yote yanapaswa kuwekwa, na kutumwa kwa ndugu na dada wa makanisa kuyasoma. Hayapaswi kuchaguliwa na kutolewa kwa matakwa ya mwanadamu; ni makosa kufanya hivyo. Kusema kwamba mazoefu ya Paulo na Yohana yalichanganywa na waliyoyaona binafsi hakumaanishi kwamba uzoefu na maarifa yao yalitoka kwa Shetani, ila tu walikuwa na mambo yaliyotoka kwa mazoefu na waliyoyaona wao binafsi. Maarifa yao yalilingana na asili ya mazoefu halisi ya wakati huo, na ni nani anayeweza kusema kwa ujasiri kwamba yote yalitoka kwa Roho Mtakatifu? Kama Injili Nne zote zilitoka kwa Roho Mtakatifu, basi ilikuwaje kwamba Mathayo, Marko, Luka na Yohana kila mmoja alisema jambo tofauti kuhusu kazi ya Yesu? Msipoamini haya, basi angalia akaunti tofauti kwa Biblia ya jinsi Petro alivyomkana Yesu mara tatu: Yote ni tofauti, na kila moja ina sifa yake yenyewe. Wengi walio wajinga husema, “Mungu wa mwili pia ni mwanadamu, kwa hivyo maneno Anayoyazungumza yanaweza kutoka kikamilifu kwa Roho Mtakatifu? Kama maneno ya Paulo na Yohana yalichanganywa na matakwa ya mwanadamu, basi maneno Anayoyasema kweli hayajachanganywa na matakwa ya mwanadamu?” Watu wanaosema mambo kama haya ni vipofu na wajinga! Soma Injili Nne kwa kina; soma iliyorekodi kuhusu alichofanya Yesu, na maneno Aliyoyasema. Kila akaunti ilikuwa kwa urahisi tofauti, na kila ilikuwa na mtazamo wake. Kama vilivyoandikwa na waandishi wa vitabu hivi vyote vilitoka kwa Roho Mtakatifu, basi yote yanapaswa kuwa sawa na thabiti. Basi mbona kuna tofauti?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Majina na Utambulisho

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 277)

Matamshi na kazi ya Yesu wakati huo hayakushikilia mafundisho, na hakufanya kazi Yake kulingana na kazi ya sheria ya Agano la Kale. Yalilingana na kazi iliyopaswa kufanywa kwa Enzi ya Neema. Alitenda kulingana na kazi Aliyokuwa ameleta mbele, kulingana na mipango Yake, na kulingana na huduma Yake; Hakufanya kazi kulingana na sheria ya Agano la Kale. Hakuna Alichofanya kilicholingana na Agano la Kale, na Hakuja kufanya kazi ili kutimiza maneno ya manabii. Kila hatua ya kazi ya Mungu haikuwa wazi ili kutimiza utabiri wa manabii wa zamani, na Hakuja kuyafuata mafundisho au kutambua makusudi utabiri wa manabii wa kale. Bado vitendo Vyake havikuvuruga utabiri wa manabii wa kale, wala havikuvuruga kazi Aliyokuwa amefanya awali. Hatua muhimu ya kazi Yake haikuwa kufuata mafundisho yoyote, na kufanya kazi ambayo Yeye Mwenyewe anapaswa kufanya. Yeye hakuwa nabii wala mwaguzi, ila mtendaji, aliyekuja kufanya hiyo kazi Aliyopaswa kufanya, na aliyekuja kufungua enzi Yake mpya na kufanya kazi Yake mpya. Bila shaka, Yesu alipokuja kufanya kazi Yake, pia Alitimiza maneno mengi yaliyosemwa na manabii wa zamani kwa Agano la Kale. Hivyo pia kazi ya leo imetimiza utabiri wa manabii wa zamani wa Agano la Kale. Ni vile tu Sishikilii hiyo “kalenda njano ya zamani,” hayo tu. Kwani kuna kazi zaidi ambayo lazima Nifanye, kuna maneno zaidi ambayo lazima Niwazungumzie, na kazi hii na maneno haya ni ya umuhimu mkubwa kuliko kueleza vifungu kutoka Biblia, kwa sababu kazi kama hiyo haina maana ama thamani kubwa kwenu, na haiwezi kuwasaidia, au kuwabadilisha. Ninanuia kufanya kazi mpya sio kwa ajili ya kutimiza kifungu chochote kutoka Biblia. Ikiwa Mungu alikuja duniani tu kutimiza maneno ya manabii wa Biblia, basi ni nani aliye mkuu, Mungu wa mwili ama hao manabii wa zamani. Na hata hivyo, hao manabii ni wasimamizi wa Mungu, ama Mungu ni msimamizi wa manabii? Unaweza kueleza haya maneno jinsi gani?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Majina na Utambulisho

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 278)

Wayahudi wa wakati huo wote walisoma kutoka Agano la Kale na walijua unabii wa Isaya kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa horini. Mbona basi, na maarifa haya, bado walimtesa Yesu? Hii siyo kwa sababu ya asili yao ya kuasi na kutojua kazi ya Roho Mtakatifu? Wakati huo, Mafarisayo waliamini kwamba kazi ya Yesu ilikuwa tofauti na ile waliyoijua ya mtoto mchanga wa kiume aliyetabiriwa; mwanadamu wa leo anamkataa Mungu kwa sababu kazi ya Mungu mwenye mwili haikubaliani na Biblia. Si kiini cha uasi wao dhidi ya Mungu ni moja na sawa? Unaweza kuwa yule ambaye anakubali tu bila swali kazi yote ya Roho Mtakatifu? Kama ni kazi ya Roho Mtakatifu, basi ni mkondo sawa, na unastahili kuukubali bila wasiwasi wowote hata kidogo; hufai ya kuchukua na kuchagua kipi cha kukubali. Ukipata ufahamu zaidi kutoka kwa Mungu na kujitahadhari zaidi Kwake, basi hili silo tendo lisilohitajika? Huna haja kutafuta uthibitisho zaidi kutoka kwa Biblia; iwapo ni ya Roho Mtakatifu huna budi kuikubali, kwani unamwamini Mungu kumfuata Mungu, sio kumchunguza. Hupaswi kutafuta ushuhuda zaidi ili Nionyeshe kwamba Mimi ni Mungu wako. Badala yake, unapaswa kupambanua kama Nina faida kwako; hiyo ndiyo muhimu. Hata kama umegundua ushuhuda usiopingika ndani ya Biblia, haiwezi kukuleta kikamilifu mbele Yangu. Wewe ndiye mmoja anayeishi ndani ya mipaka ya Biblia, na sio mbele Yangu; Biblia haiwezi kukusaidia kunijua, wala haiwezi kuimarisha upendo wako Kwangu. Ingawa Biblia ilitabiri kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa, hakuna yeyote angeweza kuelewa kupitia nani unabii ungetimia, kwani mwanadamu hakujua kazi ya Mungu, na hii ndiyo ilisababisha Mafarisayo kusimama dhidi ya Yesu. Wengine wanajua kwamba kazi Yangu iko katika maslahi ya mwanadamu, lakini bado wanaendelea kuamini kwamba Yesu na Mimi ni viumbe tofauti kabisa visivyopatana. Wakati huo, Yesu alizungumza tu na wanafunzi Wake mfululizo wa mahubiri katika Enzi ya Neema, kama jinsi ya kuweka vitendoni, jinsi ya kukusanyika pamoja, jinsi ya kuuliza kwa maombi, jinsi ya kuwatendea wengine, na mengineyo. Kazi Aliyoifanya ilikuwa hiyo ya Enzi ya Neema, na alielezea tu juu ya jinsi wanafunzi na waliomfuata wanapaswa kuweka vitendoni. Alifanya tu kazi ya Enzi ya Neema na hakuna hata moja ya siku za mwisho. Wakati Yehova aliandika sheria ya Agano la Kale kwa Enzi ya Sheria, mbona basi hakufanya kazi ya Enzi ya Neema? Mbona hakueleza wazi mapema kazi ya Enzi ya Neema? Hii haingekuwa ya manufaa kwa kukubali kwa mwanadamu? Alitabiri tu kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa na kuja mamlakani, lakini Hakutekeleza mapema kazi ya Enzi ya Neema. Kazi ya Mungu katika kila enzi ina mipaka ya wazi; Anafanya tu kazi ya enzi ya sasa na Hatekelezi hatua ifuatayo ya kazi mapema. Kwa njia hii tu kazi Yake ya kuwakilisha ya kila enzi inaweza kuletwa mbele. Yesu alizungumzia tu ishara za siku za mwisho, kuhusu jinsi ya kuwa mtulivu na jinsi ya kuokolewa, jinsi ya kutubu na kukiri, na pia jinsi ya kubeba msalaba na kuvumilia mateso; Kamwe hakuzungumza kuhusu jinsi mwanadamu katika siku za mwisho anapaswa kuingia ndani, ama jinsi ya kutafuta kukidhi matakwa ya Mungu. Hasa, haingekuwa tendo la imani ya uwongo kutafuta ndani ya Biblia kazi ya Mungu ya siku za mwisho? Nini unaweza kupambanua tu kwa kushika Biblia kwa mikono yako? Uwe mkalimani wa Biblia ama mhubiri, nani anaweza kujua mbeleni kazi ya leo?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 279)

Biblia imekuwa sehemu ya historia ya binadamu kwa miaka mingi. Zaidi ya hayo, watu huichukulia kuwa Mungu, kufikia kiwango ambapo katika siku za mwisho, imechukua nafasi ya Mungu, jambo ambalo linamchukiza Mungu. Hivyo, muda uliporuhusu, Mungu alihisi kulazimishwa kubainisha maelezo ya ndani na vyanzo vya Biblia; Asingefanya hivi, Biblia ingeendelea kushikilia nafasi ya Mungu mioyoni mwa watu, na watu wangetumia maneno ya Biblia kupima na kushutumu matendo ya Mungu. Kwa kuelezea asili, muundo na dosari za Biblia, Mungu hakuwa akikana kuwepo kwa Biblia hata kidogo, wala Hakuwa anaishutumu; badala yake, Alikuwa akitoa maelezo yaliyofaa na kustahili yaliyorejesha picha asilia ya Biblia, Akazungumzia suitafahamu za watu kuhusu Biblia, na kuwapa maoni sahihi ya Biblia, ili wasiiabudu Biblia tena, na wasipotee tena; yaani, ili wasichanganye tena imani yao pofu ya Biblia kuwa imani katika Mungu na ibada ya Mungu, wakihofia hata kukabili usuli na dosari zake za kweli. Mara tu watu wanapopata ufahamu wa Biblia usiochanganywa na mambo duni, wanaweza kuiweka kando bila majuto na kuyakubali maneno mapya ya Mungu kwa ujasiri. Hili ndilo lengo la Mungu katika sura hizi kadhaa. Ukweli ambao Mungu angetaka kuwaambia watu hapa ni kwamba hakuna nadharia ama ukweli ambao unaweza kuchukua nafasi ya kazi na maneno ya Mungu ya leo, na kwamba hakuna kitu kinachoweza kuwa mbadala wa Mungu. Ikiwa watu hawawezi kuepuka mtego wa Biblia, hawatawahi kuweza kuja mbele za Mungu. Ikiwa wanataka kuja mbele za Mungu, lazima kwanza waitakase mioyo yao na kuondoa chochote kinachoweza kuchukua nafasi Yake; kisha watamridhisha Mungu. Ingawa Mungu anaifafanua Biblia pekee hapa, usisahau kwamba kuna mambo mengi yenye makosa ambayo watu wanayaabudu kwa kweli kando na Biblia; mambo wasiyoyaabudu ni yale yanayotoka kwa Mungu kwa kweli pekee. Mungu anatumia tu Biblia kama mfano kuwakumbusha watu wasichukue njia mbaya, na wasivuke mipaka tena na kukanganyikiwa wanapomwamini Mungu na kukubali maneno Yake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Kristo Alipokuwa Akitembea Makanisani, Utangulizi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 280)

Nimefanya kazi kubwa miongoni mwa binadamu, na maneno ambayo Nimeeleza wakati huu yamekuwa mengi. Maneno haya ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, na yalikuwa yanaeleza ili binadamu aweze kulingana na Mimi. Ilhali Nimewapokea watu wachache tu duniani ambao wanalingana na Mimi, na hivyo Nimesema kwamba binadamu hathamini maneno Yangu, kwa kuwa binadamu halingani na Mimi. Kwa njia hii, kazi ambayo Naifanya sio tu kwa ajili ya mwanadamu aweze kuniabudu; muhimu zaidi, ni kwa ajili ya mwanadamu aweze kulingana na Mimi. Watu, ambao wamepotoshwa, wote huishi katika mtego wa Shetani, wao kuishi katika mwili, kuishi katika tamaa za ubinafsi, na hakuna hata mmoja kati yao anayelingana na Mimi. Kuna wale ambao wanasema kwamba wao wanalingana na Mimi, lakini ambao wote huabudu sanamu zisizo yakini. Ingawa wanakubali jina Langu kama takatifu, wao hutembea kwenye njia ambazo huenda kinyume na Yangu, na maneno yao yamejaa kiburi na kujiamini, kwa sababu, katika mizizi, wote wananipinga na hawalingani Nami. Kila siku wao hutafuta dalili Yangu katika Biblia, na kupata vifungu “vinavyofaa” hapa na pale wanavyovisoma bila kukoma, na ambavyo wao hukariri kama maandiko. Hawajui jinsi ya kulingana na Mimi, hawajui maana ya kuwa katika uadui na Mimi, na wanasoma tu maandiko kwa upofu. Wao huzuia ndani ya Biblia na Mungu asiye yakini ambaye hawajawahi kumwona, na hawana uwezo wa kumwona, na wao huitoa tu na kuiangazia wakati wao wa ziada. Wao wanaamini kuwepo Kwangu tu ndani ya eneo la Biblia. Kwa fikira zao, Mimi ni sawa na Biblia; bila Biblia Mimi sipo, na bila Mimi hakuna Biblia. Wao hawatilii maanani kuwepo Kwangu au matendo, lakini badala yake hujishughulisha na umakini mno na maalum kwa kila neno la Maandiko, na wengi wao hata huamini kwamba Mimi sipaswi kufanya jambo lolote Nipendalo kufanya ila tu kama lilitabiriwa na Maandiko. Wao hutia umuhimu mwingi sana kwa Maandiko. Inaweza kusemwa kwamba wao huona maneno na maonyesho yakiwa muhimu mno, kwa kiasi kwamba wao hutumia mistari ya Biblia kupima kila neno Ninalolisema, na kunilaani Mimi. Wanalotafuta si njia ya uwiano na Mimi, au njia ya uwiano na ukweli, lakini njia ya uwiano na maneno ya Biblia, na wanaamini kwamba chochote ambacho hakiambatani na Biblia, bila ubaguzi, si kazi Yangu. Je, si watu wa namna hiyo ni wazawa watiifu wa Mafarisayo? Mafarisayo Wayahudi walitumia sheria ya Musa kumhukumu Yesu. Hawakutafuta uwiano na Yesu wa wakati huo, bali waliifuata sheria kwa makini, kwa kiasi kwamba wao hatimaye walimpiga misumari Yesu asiye na hatia juu ya msalaba, baada ya kumshitaki Yeye kwa kukosa kufuata sheria za Agano la Kale na kutokuwa Masihi. Kiini chao kilikuwa ni nini? Haikuwa kwamba hawakutafuta njia ya uwiano na ukweli? Walitamani na kutilia maanani mawazo yao na kila neno la Maandiko, bila kuyajali mapenzi Yangu na hatua na mbinu za kazi Yangu. Hawakuwa watu waliotafuta ukweli, ila walikuwa watu walioshikilia maneno kwa ugumu; hawakuwa watu walioamini katika Mungu, bali walikuwa watu walioamini katika Biblia. Kimsingi, walikuwa walinzi wa Biblia. Ili kulinda maslahi ya Biblia, na kuzingatia hadhi ya Biblia, na kulinda sifa za Biblia, wao walitenda kiasi kwamba walimsulubisha Yesu mwenye huruma msalabani. Haya walifanya tu kwa ajili ya kuitetea Biblia, na kwa ajili ya kudumisha hali ya kila neno la Biblia katika mioyo ya watu. Hivyo waliona ni heri kuyaacha maisha yao ya baadaye na sadaka ya dhambi kwa sababu ya kumhukumu Yesu, ambaye hakuwa Anazingatia kanuni za Maandiko, mpaka kifo. Je hawakuwa watumishi kwa kila mojawapo ya maneno ya Maandiko?

Na je watu leo? Kristo amekuja kutoa ukweli, lakini wanaona ni afadhali wao kumfukuza Yeye kutoka kati ya wanadamu ili wapate kuingia mbinguni na kupokea neema. Wanaona ni afadhali kabisa kukataa kuja kwa ukweli, ili kulinda maslahi ya Biblia, na ni afadhali kumtundika Kristo ambaye Alirudi kwa mwili kwa misumari msalabani tena ili kuhakikisha kuwepo kwa Biblia milele. Jinsi gani mwanadamu anaweza kupokea wokovu Wangu, wakati moyo wake una nia mbaya namna hiyo, na asili yake inanipinga Mimi? Mimi huishi miongoni mwa wanadamu, ilhali bado wanadamu hawajui kuhusu kuwepo Kwangu. Ninapoangaza mwanga Wangu juu ya wanadamu, bado yeye hana ufahamu kuhusu kuwepo Kwangu. Wakati Ninatoa ghadhabu Yangu juu ya wanadamu, wao hukanusha kuwepo Kwangu kwa nguvu kubwa zaidi. Binadamu hutafuta uwiano na maneno, na Biblia, ilhali bado hakuna mwanadamu hata mmoja huja Kwangu kutafuta njia ya uwiano na ukweli. Binadamu huniheshimu sana Nikiwa mbinguni, na kujishughulisha hasa na kuwepo Kwangu mbinguni, ilhali hakuna anayenijali Nikiwa katika mwili, kwa maana Mimi Ninayeishi miongoni mwa wanadamu sina umuhimu kwao hata kidogo. Wale ambao hutafuta tu uwiano na maneno ya Biblia, na ambao hutafuta tu uwiano na Mungu asiye yakini, mbele Yangu ni fidhuli. Hiyo ni kwa sababu wanachokiabudu ni maneno yaliyokufa, na Mungu Aliye na uwezo wa kuwapa hazina isiyoambilika. Wanachoabudu ni Mungu anayedhibitiwa na mtu, na ambaye hayuko. Ni nini, basi, ambacho watu wa namna hiyo wanaweza kupokea kutoka Kwangu? Mwanadamu ni kiumbe duni sana kiasi kwamba maneno hayawezi kueleza hali yake. Wale wanaonipinga, wanaofanya madai yasiyo na kipimo dhidi Yangu, wasio na upendo kwa ukweli, wanaoniasi—wangewezaje kulingana na Mimi?

Wale wanaonipinga ni wale ambao hawalingani na Mimi. Vile vile wale wasiopenda ukweli, na wale wanaoniasi ndio walio wapinzani Wangu zaidi na hawalingani na Mimi. Wale wote ambao hawalingani na Mimi Nawawasilisha mikononi mwa yule mwovu. Ninawaacha wao kwa upotovu wa yule mwovu, Nawaachilia huru ili wafichue maovu yao, na hatimaye kuwakabidhi kwa yule mwovu ili waliwe. Mimi Sijali ni watu wangapi wananiabudu, ambayo ni kusema, Sijali ni watu wangapi wanaamini ndani Yangu. Kinachonijalisha ni watu wangapi wanalingana na Mimi. Hiyo ni kwa sababu wote wasiolingana na Mimi ni wale waovu wanaonisaliti; wao ni adui Zangu, Nami “Sitawatunza” adui Zangu katika nyumba Yangu. Wale ambao wanalingana na Mimi watanitumikia milele katika nyumba Yangu, na wale wanaojiweka katika uadui na Mimi watateseka milele katika adhabu Yangu. Wale wanaojali tu kuhusu maneno ya Biblia, wasiojali kuhusu ukweli au kutafuta nyayo Zangu—wao wananipinga, kwa kuwa wao wananizuilia Mimi kulingana na Biblia, na kuniwekea vizuizi ndani ya na Biblia, na hivyo ni wa kukufuru pakubwa dhidi Yangu. Jinsi gani watu wa aina hii wanaweza kuja mbele Zangu? Wao hawatilii maanani matendo Yangu, au mapenzi Yangu, au ukweli, badala yake wanashikilia maneno, maneno yanayoua. Jinsi gani watu kama hao wanaweza kulingana na Mimi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

Iliyotangulia: Tabia ya Mungu na Kile Anacho na Alicho

Inayofuata: Kufunua Mawazo ya Kidini

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp