Kufunua Mawazo ya Kidini

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 281)

Mungu na mwanadamu hawawezi kuzungumziwa kama wa kulingana. Dutu ya Mungu na kazi Yake ni vitu visivyoeleweka na kufahamika kwa mwanadamu. Ikiwa Mungu hawezi kufanya kazi Yake binafsi na kuzungumza maneno Yake katika ulimwengu wa mwanadamu, basi mwanadamu hangeweza kuelewa mapenzi ya Mungu, na kwa hivyo, hata wale waliotoa maisha yao yote kwa ajili ya Mungu hawataweza kupata idhini ya Mungu. Bila kazi ya Mungu, haijalishi jinsi gani mwanadamu anatenda mema, haitahesabika kama chochote, kwa maana fikira za Mungu daima zitakuwa juu ya fikira za mwanadamu, na hekima ya Mungu haieleweki kwa mwanadamu. Na kwa hivyo Nasema kwamba wale ambao “wanaona kwa wazi”. Mungu na kazi Yake ni wasioweza kufanikisha chochote, wao wote ni wenye kiburi na wapumbavu. Mwanadamu hafai kufafanua kazi ya Mungu; zaidi ya hayo, mwanadamu hawezi kufafanua kazi ya Mungu. Katika macho ya Mungu, mwanadamu ni mdogo kushinda mchwa, kwa hivyo mwanadamu atawezaje kuelewa kazi ya Mungu? Wale wasemao daima, “Mungu hafanyi kazi kwa njia hii ama ile” au “Mungu yuko hivi ama vile”—je hawa wote si wenye kiburi? Tunafaa sote kujua kwamba watu, ambao ni wa mwili, wote wamepotoshwa na Shetani. Ni katika hali yao asili kumuasi Mungu, na hawako katika usawa na Mungu, sembuse kuweza kutoa mawaidha kwa kazi ya Mungu. Jinsi Mungu anavyomwelekeza mwanadamu ni kazi ya Mungu mwenyewe. Mwanadamu anafaa kunyenyekea, na hafai kuwa na wazo hili ama lile, kwani mwanadamu ni mchanga tu. Kwa sababu tunajaribu kumtafuta Mungu, hatufai kuwekelea dhana zetu katika kazi ya Mungu ili Mungu Aziwaze, na zaidi hatufai kutumia tabia zetu potovu kwa kupinga kazi ya Mungu kwa makusudi. Je hili halitatufanya wapinga Kristo? Je, watu kama hawa watawezaje kusema kuwa wanamwamini Mungu? Kwa maana tunaamini kuwa kuna Mungu, na kwa maana tunatamani kumtosheleza na kumwona, tunapaswa kutafuta njia ya ukweli, na tunapaswa kutafuta njia ya kulingana na Mungu. Hatupaswi kuwa katika upinzani sugu kwa Mungu; Matendo kama haya yatakuwa na matokeo gani mazuri?

Leo hii, Mungu Anayo kazi mpya. Unaweza kuyakataa maneno haya, yanaweza kuhisi yasiyo ya kawaida kwako, lakini Nakushauri usifichue asili yako halisi, kwa maana wale tu walio na njaa ya kweli na kiu cha haki mbele za Mungu ndio wanaweza kupata ukweli, na wale wanaomcha Mungu kwa ukweli tu ndio wanaweza kupata nuru na kuongozwa na Mungu. Hakuna litakalotoka kwa kutafuta ukweli kupitia ugomvi. Ni kwa kutafuta kwa utulivu ndio tunaweza kupata matokeo. Ninaposema kwamba “leo, Mungu Anayo kazi mpya,” Ninaashiria Mungu kurudi katika mwili. Pengine huyajali maneno haya, pengine unayachukia, au pengine una haja kubwa sana nayo. Haijalishi ni hali gani, Natumai kuwa wote walio na tamaa ya kweli ya kuonekana kwa Mungu wataweza kuukabili ukweli huu na kutafakari juu yake kwa makini. Ni vyema usiamue jambo upesi bila kuzingatia suala zima. Hivi ndivyo watu wenye hekima wanapaswa kutenda.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 282)

Katika imani yako kwa Mungu, utamjuaje Mungu? Unapaswa kumjua Mungu kupitia maneno na kazi ya leo ya Mungu, bila upotovu au uwongo, na hata kabla jambo lolote lile ni sharti uijue kazi ya Mungu. Huu ndio msingi wa kumjua Mungu. Huo uwongo wa aina mbalimbali unaokosa ukubalifu wa maneno ya Mungu ni dhana za kidini, ni ukubalifu ambao ni potovu na wenye makosa. Ujuzi mkubwa zaidi wa watu mashuhuri wa kidini ni kuyachukua maneno ya Mungu yaliyokuwa yakikubalika zamani na kuyalinganisha na maneno ya Mungu ya leo. Unapomhudumia Mungu wa leo, ikiwa unashikilia vitu vilivyoangaziwa nuru na Roho Mtakatifu hapo zamani, basi huduma yako itasababisha hitilafu na vitendo vyako vitakuwa vimepitwa na wakati na havitakuwa tofauti na ibada ya kidini. Ikiwa unaamini kuwa wanaomhudumia Mungu wanafaa kuwa wanyenyekevu na wavumilivu…, na ukiweka ufahamu wa aina hii katika vitendo leo hii, basi vitendo kama hivi ni dhana ya kidini, na vitendo kama hivyo ni maigizo ya kinafiki. “Dhana za kidini” inarejelea vitu vilivyopitwa na wakati (kutia ndani ukubalifu wa maneno yaliyonenwa na Mungu zamani na kufichuliwa na Roho Mtakatifu), na vikiwekwa katika vitendo leo, basi vitahitilafiana na kazi ya Mungu na havitamfaidi mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kuyatakasa dhana za kidini yaliyomo ndani yake, basi yatakuwa kizuizi kizito katika kumuhudumia Mungu. Walio na dhana za kidini hawana njia ya kuendelea sawia na hatua za kazi ya Roho Mtakatifu, watakuwa nyuma hatua moja, halafu mbili—kwani hizi dhana za kidini humfanya mwanadamu kuwa mtu wa kujitukuza na mwenye kiburi. Mungu hahisi kumbukumbu kwa ajili ya Alichokinena na kukifanya hapo zamani; kama kimepitwa na wakati, basi Anakiondoa. Hakika unaweza kuziacha dhana zako? Ukiyakatalia maneno aliyoyanena Mungu hapo zamani, je hili linadhihirisha kuwa unaijua kazi ya Mungu? Kama huwezi kukubali mwangaza wa Roho Mtakatifu leo na badala yake unashikilia mwangaza wa zamani, hili laweza kuthibitisha kuwa unafuata nyayo za Mungu? Je, bado huwezi kuziacha dhana za kidini? Ikiwa ndivyo ilivyo, basi utakuwa mpinga Mungu.

Mwanadamu akiacha dhana za kidini, basi hatatumia akili yake kuyapima maneno na kazi ya Mungu leo hii, na badala yake atatii moja kwa moja. Japokuwa kazi ya Mungu ya leo inaonekana wazi tofauti na ya zamani, unaweza kuiacha mitazamo ya zamani na kutii moja kwa moja kazi ya Mungu leo hii. Kama unaweza kuwa na ufahamu kama huu kwamba unaionea fahari nafasi ya kazi ya Mungu leo bila kujali Alivyofanya kazi zamani, basi wewe ni mtu aliyeyaacha dhana zake, anayemtii Mungu na anayeweza kuitii kazi na maneno ya Mungu na kufuata nyayo za Mungu. Katika hili, kwa hakika, utakuwa mtu anayemtii Mungu. Huichambui au kuitafiti kazi ya Mungu; ni kana kwamba Mungu amesahau kazi Yake ya zamani, nawe pia ukaisahau. Sasa ni sasa, na zamani ni zamani, na kwa sababu leo Mungu ameyaweka kando Aliyoyafanya zamani, haifai uendelee kuyashikilia. Hapo ndipo utakuwa mtu anayemtii kabisa anayemsikia Mungu na aliyeacha kabisa dhana zake za kidini.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Ndio Wanaoweza Kumhudumia Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 283)

Kwa sababu kazi ya Mungu mara zote huwa na masuala mapya, kuna kazi ambayo inakuwa iliyopitwa na wakati na nzee kazi mpya inapoibuka. Hizi aina tofauti tofauti za kazi, nzee na mpya, hazikinzani, bali zinatoshelezana, kila hatua ikifuata iliyotangulia. Kwa kuwa kuna kazi mpya, mambo ya zamani, kwa hakika, ni sharti yaondolewe. Kwa mfano, baadhi ya vitendo vilivyokita mizizi na misemo ya mwanadamu iliyozoeleka, kuongeza juu miaka mingi ya mazoea na mafundisho ya mwanadamu, ilimuumbia mwanadamu kila aina ya dhana. Maelezo ya mwanadamu kuhusu dhana kama hizi ni kwamba bado Mungu hajafichua uso Wake halisi na tabia Yake asili kwa mwanadamu, pamoja na kuenea kwa nadharia za kale kwa miaka mingi yamekuwa ya kupendelea uundaji wa mwanadamu wa fikira kama hizo. Inaweza kusewa kwamba, katika kipindi cha imani ya mwanadamu kwa Mungu, ushawishi wa fikira mbalimbali umesababisha kutengenezwa na kubadilika kwa ufahamu wote wa fikira kumhusu Mungu ndani ya watu, jambo ambalo limewafanya watu wengi wa kidini wanaomtumikia Mungu wageuke kuwa adui Zake. Hivyo, kadiri fikira za watu za kidini zinavyokuwa thabiti, ndivyo wanavyozidi kumpinga Mungu, na ndivyo wanavyozidi kuwa maadui wa Mungu. Kazi ya Mungu daima huwa mpya, si kongwe na huwa haitengenezi mafundisho ya kidini na badala yake inabadilika kila mara na kuwa mpya kwa kiwango fulani. Kazi hii ni onyesho la tabia ya asili ya Mungu Mwenyewe. Vilevile ni kanuni ya asili ya kazi ya Mungu na mojawapo ya njia ambazo Mungu hutimiza usimamizi Wake. Iwapo Mungu asingefanya kazi kwa njia hii, mwanadamu asingebadilika au kuweza kumfahamu Mungu, na Shetani asingeshindwa. Hivyo basi, kila mara katika kazi Yake, kunatokea mabadiliko ambayo yanaonekana hayatabiriki, ila ambayo, kwa hakika, yana kipindi chake. Njia mwanadamu anavyomwamini Mungu hata hivyo ni tofauti. Anashikilia mifumo ya zamani ya kidini na kadiri yalivyo ya zamani, ndivyo yanavyokuwa ya kupendeza kwake. Akili ya kipumbavu ya mwanadamu, akili isiyobadilika kama mawe inawezaje kukubali kazi nyingi isiyoeleweka mpya na maneno ya Mungu? Mwanadamu anamchukia Mungu ambaye ni mpya kila siku na si wa zamani; anampenda tu Mungu wa zamani, ambaye ni mzee kwa umri, aliyejaa mvi na Asiyekwama papo hapo. Hivyo, kwa sababu Mungu na mwanadamu kila mmoja analo alipendalo, mwanadamu amekuwa adui wa Mungu. Kwa kiwango kikubwa, huu utata upo hata leo, wakati ambao Mungu amekuwa akifanya kazi mpya kwa takribani miaka 6000. Hawawezi kusaidika. Labda ni kwa sababu ya usumbufu wa mwanadamu, au kutokiukwa kwa kazi ya Mungu—ila hawa wahubiri bado wanashikilia vitabu vizee na karatasi ilhali Mungu anaendelea na kazi Yake ambayo haijakamilika ya usimamizi kana kwamba hana msaidizi. Japo huu utata unaleta uadui kati ya mwanadamu na Mungu, kiasi kwamba hawapatanishiki, Mungu haujali ukinzani huu. Hata hivyo mwanadamu bado anashikilia imani na dhana zake, na kamwe haiachilii. Ila kitu kimoja kiko wazi: Japo mwanadamu haachi misimamo yake, Mungu mara zote anapiga hatua na kubadilisha misimamo Yake kulingana na muktadha na hatimaye ni mwanadamu atakayeshindwa bila mapambano. Mungu ndiye adui mkubwa zaidi wa maadui wake walioshindwa na vilevile ni bingwa wa wale miongoni mwa wanadamu ambao wameshindwa na wale ambao bado hawajashindwa. Ni nani anaweza kushindana na Mungu na ashinde? Dhana za mwanadamu zinaonekana kutoka kwa Mungu kwani wengi wao walizaliwa kipindi cha kazi ya Mungu. Na bado Mungu hamsamehei mwanadamu kwa sababu ya hili na hata zaidi Hammiminii sifa mwanadamu kwa “kumzalishia Mungu” mazao baada ya mazao ambayo yamo nje ya kazi ya Mungu. Badala yake, Yeye hughadhabishwa sana na fikira na imani za zamani za uungu, za mwanadamu na hata hachukui hatua kufikira tarehe ambayo hizi fikira zilitokea mara ya kwanza. Hakubali kamwe kwamba hizi dhana zinaletwa na kazi Yake kwani dhana za mwanadamu husambazwa na mwanadamu; chanzo chao ni fikira na akili za mwanadamu, na si Mungu, ila ni Shetani. Madhumuni ya Mungu mara zote ni kuona kazi Yake ikiwa mpya na hai, si kongwe na iliyokufa, na kile Anachotaka mwanadamu ashikilie kwa nguvu kinabadilika kulingana na enzi na kipindi, na si cha kudumu milele na kisichobadilika. Hii ni kwa sababu Yeye ni Mungu ambaye husababisha mwanadamu kuishi na kuwa mpya, tofauti na ibilisi anayemsababishia mwanadamu kufa na kuwa mzee. Je, bado hamlielewi hili? Una dhana kuhusu Mungu na umeshindwa kuziacha kwa kuwa hutafakari. Si kwa sababu kuna maana kidogo sana ndani ya kazi ya Mungu, wala kwa sababu kazi ya Mungu inatofautiana na matakwa ya binadamu, wala kwamba Mungu mara zote ni “mzembe katika wajibu Wake.” Huwezi kuacha dhana zako kwa kuwa umepungukiwa na utiifu, na huna sifa hata kidogo za kiumbe wa Mungu, na si kwamba Mungu anakufanyia mambo kuwa magumu. Yote haya umejisababishia na hayana uhusiano na Mungu; mateso na misukosuko yote husababishwa na mwanadamu. Dhamira za Mungu mara zote huwa nzuri: hakusudii kukufanya uzitoe dhana, ila angependa ubadilike na uwe mpya kadiri enzi zinavyopita. Ila bado huwezi kutofautisha chokaa na jibini na kila mara ama unachunguza au unachanganua. Si kwamba Mungu anakufanyia mambo kuwa magumu, ila ni kuwa humheshimu Mungu na uasi wako umezidi. Kiumbe mdogo anathubutu kuchukua sehemu ndogo ya kile alichopewa mwanzo na Mungu, na kisha kubadilika na kukitumia kumvamia Mungu—je, huu si uasi wa mwanadamu? Ni haki kusema kuwa binadamu hawana sifa kabisa za kutoa maoni yao mbele za Mungu, na sembuse hawana sifa za kuonyesha hadharani maneno yao yasiyo na thamani, yanukayo, yaliyooza wapendavyo—bila kutaja chochote kuhusu hizo fikira zilizooza. Haina maana?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Ndio Wanaoweza Kumhudumia Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 284)

Kazi ya Mungu inaendelea kusonga mbele, na ingawa madhumuni ya kazi Yake bado hayajabadilika, njia anazozitumia kufanya kazi zinabadilika mara kwa mara, na hivyo pia wale wanaomfuata Mungu. Zaidi iwapo kazi ya Mungu, zaidi mwanadamu anakuja kumjua kwa kina Mungu, na tabia ya mwanadamu inabadilika ipasavyo pamoja na kazi Yake. Hata hivyo, ni kwa sababu kazi ya Mungu milele inabadilika ndio wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu na wale wanadamu wajinga wasiojua ukweli wanakuwa wapinzani wa Mungu. Kazi ya Mungu kamwe haifuati dhana za mwanadamu, kwani kazi Yake daima ni mpya na siyo nzee. Kamwe Hairudii kazi ya zamani lakini badala Anasonga mbele na kazi ambayo haijafanywa hapo awali. Kwa sababu Mungu harudii kazi Yake na mwanadamu daima anahukumu kazi ya Mungu leo kulingana na kazi Yake ya zamani, ni vigumu sana kwa Mungu kutekeleza kila hatua ya kazi ya enzi mpya. Mwanadamu ana vizuizi vingi sana! Kufikiria kwa mwanadamu ni kwa akili finyu! Hakuna mwanadamu anayeijua kazi ya Mungu, lakini bado wote wanafafanua kazi hiyo. Mbali na Mungu, mwanadamu anapoteza uhai, ukweli na baraka za Mungu, lakini bado mwanadamu hajapokea uhai wala ukweli, na hata baraka kubwa Mungu anazowapa wanadamu. Wanadamu wote wanataka kumpata Mungu lakini bado hawawezi kuvumilia mabadiliko yoyote kwa kazi ya Mungu. Wale wasiokubali kazi mpya ya Mungu wanaamini kwamba kazi ya Mungu haibadiliki, na kwamba kazi ya Mungu milele inabakia kusimama. Kwa imani yao, yote yanayohitajika kupata wokovu wa milele kutoka kwa Mungu ni kuhifadhi sheria, na iwapo watatubu na kukiri dhambi zao, dhamira ya Mungu milele itaridhika. Wana maoni kwamba Mungu anaweza tu kuwa Mungu chini ya sheria na Mungu aliyesulubiwa kwa sababu ya mwanadamu; pia ni maoni yao kwamba Mungu hastahili na Hawezi kuzidi kiwango cha Biblia. Ni hasa maoni haya yaliyowafunga imara kwa sheria ya zamani na kuendelea kuwafumba kwa kanuni ngumu. Hata zaidi wanaamini kwamba kazi yoyote ile mpya ya Mungu, ni lazima ithibitishwe na unabii, na kwamba katika kila hatua ya hiyo kazi, wote wanaomfuata na roho ya kweli lazima pia waonyeshwe ufunuo, vinginevyo kazi hiyo haiwezi kuwa ya Mungu. Tayari si kazi rahisi kwa mwanadamu kuja kumjua Mungu. Ikichukuliwa pamoja na moyo wa ujinga wa mwanadamu na asili yake ya kuasi ya kujiona muhimu na kujivunia, basi ni vigumu zaidi kwa mwanadamu kukubali kazi mpya ya Mungu. Mwanadamu haitafiti kazi mpya ya Mungu kwa utunzaji wala haikubali na unyenyekevu; badala yake, mwanadamu anachukua mtazamo wa dharau, kusubiri ufunuo na mwongozo wa Mungu. Hii siyo tabia ya mwanadamu anayeasi dhidi ya na kumpinga Mungu? Ni jinsi gani wanadamu kama hawa wanaweza kupata idhini ya Mungu?

Wakati huo, Yesu alisema kuwa kazi ya Yehova ilikuwa imebaki nyuma kwa Enzi ya Neema, kama Nisemavyo leo kwamba kazi ya Yesu imebaki nyuma. Kama kungekuwa tu na Enzi ya Sheria na siyo Enzi ya Neema, Yesu hangeweza kusulubiwa na hangeweza kuwakomboa wanadamu wote; kungekuwa tu na Enzi ya Sheria, kungekuwa na uwezekano wa mwanadamu kuendelea hadi siku ya leo? Historia inaendelea mbele; historia sio asili ya sheria ya kazi ya Mungu? Hii sio picha ya usimamizi Wake wa mwanadamu ndani ya ulimwengu mzima? Historia inaendelea mbele, na pia kazi ya Mungu, na matakwa ya Mungu yanaendelea kubadilika. Haingewezekana kwa Mungu kudumisha hatua moja ya kazi kwa miaka elfu sita, kwani kila mwanadamu anajua kwamba Yeye daima ni mpya na kamwe si mzee. Hangeweza kuendelea kuendeleza kazi sawa na kusulubiwa, na mara moja, mara mbili, mara tatu…. kupigwa misumari kwa msalaba. Huu ni mtazamo wa mwanadamu mjinga. Mungu haendelezi kazi sawa, na kazi Yake daima inabadilika na daima ni mpya, jinsi kila siku Nazungumza nanyi maneno mapya na kufanya kazi mpya. Hii ndiyo kazi Ninayofanya, umuhimu wake ukiwa kwa maneno “mpya” na “ajabu.” “Mungu habadiliki, na Mungu daima Atakuwa Mungu”; usemi huu hakika ni ukweli. Kiini cha Mungu hakibadiliki, Mungu daima ni Mungu, na Hawezi kamwe kuwa Shetani, lakini haya hayathibitishi kwamba kazi Yake ni ya daima na kabambe kama kiini Chake. Unatangaza kwamba Mungu yuko hivyo, lakini ni jinsi gani basi unaweza kueleza kwamba Mungu daima ni mpya na kamwe si mzee? Kazi ya Mungu inaendelea kuenea, na mapenzi ya Mungu yanaendelea kujitokeza na kufanywa kujulikana na mwanadamu. Wakati mwanadamu anakuwa na uzoefu wa kazi ya Mungu, tabia yake inaendelea kubadilika, na maarifa yake yanaendelea kubadilika. Basi mabadiliko haya yanatokea wapi? Siyo kwa kazi ya Mungu inayobadilika milele? Kama tabia ya mwanadamu inaweza kubadilika, mbona mwanadamu hawezi kuruhusu kazi Yangu na maneno Yangu pia kuendelea kubadilika? Ni lazima Nikabiliwe na vikwazo vya mwanadamu? Hutegemei tu maneno ya hila?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 285)

Wayahudi wa wakati huo wote walisoma kutoka Agano la Kale na walijua unabii wa Isaya kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa horini. Mbona basi, na maarifa haya, bado walimtesa Yesu? Hii siyo kwa sababu ya asili yao ya kuasi na kutojua kazi ya Roho Mtakatifu? Wakati huo, Mafarisayo waliamini kwamba kazi ya Yesu ilikuwa tofauti na ile waliyoijua ya mtoto mchanga wa kiume aliyetabiriwa; mwanadamu wa leo anamkataa Mungu kwa sababu kazi ya Mungu mwenye mwili haikubaliani na Biblia. Si kiini cha uasi wao dhidi ya Mungu ni moja na sawa? Unaweza kuwa yule ambaye anakubali tu bila swali kazi yote ya Roho Mtakatifu? Kama ni kazi ya Roho Mtakatifu, basi ni mkondo sawa, na unastahili kuukubali bila wasiwasi wowote hata kidogo; hufai ya kuchukua na kuchagua kipi cha kukubali. Ukipata ufahamu zaidi kutoka kwa Mungu na kujitahadhari zaidi Kwake, basi hili silo tendo lisilohitajika? Huna haja kutafuta uthibitisho zaidi kutoka kwa Biblia; iwapo ni ya Roho Mtakatifu huna budi kuikubali, kwani unamwamini Mungu kumfuata Mungu, sio kumchunguza. Hupaswi kutafuta ushuhuda zaidi ili Nionyeshe kwamba Mimi ni Mungu wako. Badala yake, unapaswa kupambanua kama Nina faida kwako; hiyo ndiyo muhimu. Hata kama umegundua ushuhuda usiopingika ndani ya Biblia, haiwezi kukuleta kikamilifu mbele Yangu. Wewe ndiye mmoja anayeishi ndani ya mipaka ya Biblia, na sio mbele Yangu; Biblia haiwezi kukusaidia kunijua, wala haiwezi kuimarisha upendo wako Kwangu. Ingawa Biblia ilitabiri kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa, hakuna yeyote angeweza kuelewa kupitia nani unabii ungetimia, kwani mwanadamu hakujua kazi ya Mungu, na hii ndiyo ilisababisha Mafarisayo kusimama dhidi ya Yesu. Wengine wanajua kwamba kazi Yangu iko katika maslahi ya mwanadamu, lakini bado wanaendelea kuamini kwamba Yesu na Mimi ni viumbe tofauti kabisa visivyopatana. Wakati huo, Yesu alizungumza tu na wanafunzi Wake mfululizo wa mahubiri katika Enzi ya Neema, kama jinsi ya kuweka vitendoni, jinsi ya kukusanyika pamoja, jinsi ya kuuliza kwa maombi, jinsi ya kuwatendea wengine, na mengineyo. Kazi Aliyoifanya ilikuwa hiyo ya Enzi ya Neema, na alielezea tu juu ya jinsi wanafunzi na waliomfuata wanapaswa kuweka vitendoni. Alifanya tu kazi ya Enzi ya Neema na hakuna hata moja ya siku za mwisho. Wakati Yehova aliandika sheria ya Agano la Kale kwa Enzi ya Sheria, mbona basi hakufanya kazi ya Enzi ya Neema? Mbona hakueleza wazi mapema kazi ya Enzi ya Neema? Hii haingekuwa ya manufaa kwa kukubali kwa mwanadamu? Alitabiri tu kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa na kuja mamlakani, lakini Hakutekeleza mapema kazi ya Enzi ya Neema. Kazi ya Mungu katika kila enzi ina mipaka ya wazi; Anafanya tu kazi ya enzi ya sasa na Hatekelezi hatua ifuatayo ya kazi mapema. Kwa njia hii tu kazi Yake ya kuwakilisha ya kila enzi inaweza kuletwa mbele. Yesu alizungumzia tu ishara za siku za mwisho, kuhusu jinsi ya kuwa mtulivu na jinsi ya kuokolewa, jinsi ya kutubu na kukiri, na pia jinsi ya kubeba msalaba na kuvumilia mateso; Kamwe hakuzungumza kuhusu jinsi mwanadamu katika siku za mwisho anapaswa kuingia ndani, ama jinsi ya kutafuta kukidhi matakwa ya Mungu. Hasa, haingekuwa tendo la imani ya uwongo kutafuta ndani ya Biblia kazi ya Mungu ya siku za mwisho? Nini unaweza kupambanua tu kwa kushika Biblia kwa mikono yako? Uwe mkalimani wa Biblia ama mhubiri, nani anaweza kujua mbeleni kazi ya leo?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 286)

Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima. Na hivyo, hata leo bado wanamngoja Masiha, kwani hawana maarifa ya njia ya uzima, na hawajui ukweli ni nini. Ni vipi, hebu nielezeni, watu wapumbavu, wakaidi na washenzi kama hawa wangeweza kupata baraka za Mungu? Wangewezaje kumwona Masiha? Walimpinga Yesu kwa sababu hawakujua mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu hawakuijua njia ya ukweli uliozungumziwa na Yesu, na zaidi, kwa sababu hawakumwelewa Masiha. Na kwa kuwa hawakuwa wamewahi kumwona Masiha na hawakuwa wamewahi kuwa pamoja na Masiha, walifanya kosa la kuning’inia bila mafanikio kwa jina la Masiha huku wakipinga dutu ya Masiha kwa kila njia iwezekanayo. Mafarisayo hawa kwa dutu walikuwa wakaidi, wenye kiburi na hawakutii ukweli. Kanuni ya imani yao kwa Mungu ni: Haijalishi mahubiri Yako ni makubwa vipi, haijalishi mamlaka Yako ni makubwa vipi, Wewe si Kristo iwapo Huitwi Masiha. Je, maoni haya si ya upuuzi na ya kudhihaki? Nawauliza tena: Je, si rahisi sana kwenu kufanya makosa ya Mafarisayo wa mbeleni zaidi, kwa kuwa hamna ufahamu hata kidogo kumhusu Yesu? Je, unaweza kuitambua njia ya ukweli? Je, unaweza kutoa uhakika kweli kuwa hutampinga Kristo? Je, una uwezo wa kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu? Kama hujui iwapo utampinga Kristo, basi Nasema kuwa tayari unaishi kwenye ukingo wa kifo. Wale wote ambao hawakumfahamu Masiha walikuwa na uwezo wa kumpinga Yesu, wa kumkataa Yesu, wa kumpaka Yeye tope. Watu wote wasiomwelewa Yesu wako na uwezo wa kumkana, na kumtusi. Zaidi, wako na uwezo wa kuona kurejea kwa Yesu kama uwongo wa Shetani, na watu zaidi watamshutumu Yesu aliyerudi kwa mwili. Je, haya yote hayawafanyi muogope? Mtakachokumbana nacho kitakuwa kumkufuru Roho Mtakatifu, kuharibiwa kwa maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa, na kukataliwa kwa dharau ya yale yote ambayo yamedhihirishwa na Yesu. Mnaweza kupata nini kutoka kwa Yesu kama mmetatizwa kwa namna hii? Mtaielewaje kazi ya Yesu atakaporudi kwa mwili kwa wingu jeupe, kama mnakataa katakata kuona makosa yenu? Nawaambieni hili: Watu wasioukubali ukweli, ilhali wanangoja kufika kwa Yesu juu ya wingu jeupe kwa upofu, kwa hakika watamkufuru Roho Mtakatifu, na ni kundi ambalo litaangamizwa. Mnatamani tu neema ya Yesu, na kutaka tu kufurahia ulimwengu wa mbinguni wenye raha, ilhali hamjawahi kutii maneno yaliyonenwa na Yesu, na hamjawahi kupokea ukweli utakaoonyeshwa na Yesu atakaporudi katika mwili. Mtashikilia nini badala ya ukweli wa kurejea kwa Yesu juu ya wingu jeupe? Je, ni ukweli ambao ndani yake mnashinda mkitenda dhambi, na kisha kuzikiri, tena na tena? Mtatoa nini kama kafara kwa Yesu Anayerejea juu ya wingu jeupe? Je, ni miaka ya kazi ambayo mnajiinua nayo? Ni nini mtakachoinua kumfanya Yesu Anayerejea kuwaamini? Je, ni hiyo asili yenu ya kiburi, ambayo haitii ukweli wowote?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 287)

Uaminifu wenu uko kwa maneno pekee, maarifa yenu ni ya kiakili tu na ya dhana, kazi yenu ni kwa sababu ya kupata baraka za mbinguni, na kwa hivyo imani yenu inafaa kuwa vipi? Hata leo, bado mnapuuza kila neno la ukweli. Hamjui Mungu ni nini, hamjui Kristo ni nini, hamjui jinsi ya kumcha Yehova, hamjui jinsi ya kuingia katika kazi ya Roho Mtakatifu, na hamjui jinsi ya kutofautisha kati ya kazi ya Mungu Mwenyewe na uongo wa mwanadamu. Unajua tu kukashifu neno lolote la ukweli linaloelezwa na Mungu lisilolingana na mawazo yako. Unyenyekevu wako uko wapi? Utiifu wako uko wapi? Uaminifu wako uko wapi? Tamaa yako ya kupata ukweli iko wapi? Uchaji Mungu wako uko wapi? Nawaambieni, wale wanaoamini katika Mungu kwa sababu ya ishara hakika ni kikundi ambacho kitapata kuangamizwa. Wale wasio na uwezo wa kukubali maneno ya Yesu Ambaye Amerudi kwa mwili kwa hakika ni vizazi vya kuzimu, vizazi vya malaika mkuu, kikundi ambacho kitakabiliwa na kuangamizwa kwa milele. Watu wengi wanaweza kukosa kujali kuhusu kile Ninachosema, lakini bado Nataka kumwambia kila anayedaiwa kuwa mtakatifu wa Mungu anayemfuata Yesu kwamba, mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu ndio utakuwa mwonekano wa umma wa Jua la haki. Pengine huo utakuwa wakati wa furaha kubwa kwako, ilhali lazima ujue kuwa wakati utakaposhuhudia Yesu Akishuka kutoka mbinguni ndio pia wakati ambapo utaenda chini kuzimu kuadhibiwa. Huo ndio utakuwa wakati wa mwisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi na ndio utakuwa wakati ambapo Mungu atawatunukia wazuri na kuwaadhibu waovu. Kwani hukumu ya Mungu itakuwa imeisha kabla ya mwanadamu kuona ishara, wakati kuna onyesho la ukweli tu. Wale wanaokubali ukweli na hawatafuti ishara, na hivyo wametakaswa, watakuwa wamerudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu na kuingia katika kumbatio la Muumba. Ni wale tu ambao wanashikilia imani kwamba “Yesu Asiyeshuka juu ya wingu jeupe ni Kristo wa uongo” watakabiliwa na adhabu ya milele, kwani wanaamini tu katika Yesu ambaye Anaonyesha ishara, lakini hawamkubali Yesu Anayetangaza hukumu kali na Anatoa njia ya kweli ya uzima. Na hivyo itakuwa tu kuwa Yesu Atawashughulikia tu Atakaporejea wazi wazi juu ya wingu jeupe. Ni wakaidi sana, wanajiamini sana, wenye kiburi sana. Wapotovu kama hawa watatunukiwa vipi na Yesu? Kurejea kwa Yesu ni wokovu mkuu kwa wale ambao wana uwezo wa kuukubali ukweli, lakini kwa wale wasioweza kuukubali ukweli ni ishara ya kuhukumiwa. Mnafaa kuchagua njia yenu wenyewe, na hampaswi kukufuru Roho Mtakatifu na kuukataa ukweli. Hampaswi kuwa wajinga wala watu walio na kiburi, lakini watu ambao wanatii uongozi wa Roho Mtakatifu na wanangoja kwa hamu na kuutafuta ukweli; kwa njia hii tu ndiyo mtapata kufaidika. Nawashauri mtembee katika njia ya kuamini katika Mungu kwa uangalifu. Msiwe wepesi wa kuamua mambo bila kuzingatia suala zima; kilicho zaidi, msiwe wenye kuchukulia mambo bila uzito na wenye msiofikiria katika imani yenu kwa Mungu. Mnafaa kujua kwamba, angalau, wale wanaoamini Mungu wanafaa kuwa wanyenyekevu na wenye kucha. Wale ambao wamesikia ukweli ilhali wanaudharau ni wajinga na wapumbavu. Wale ambao wameusikia ukweli ilhali bila kujali wanaamua mambo bila kuzingatia kila kitu ama kuukashifu wamejawa na kiburi. Hakuna anayeamini katika Yesu anastahili kuwalaani au kuwahukumu wengine. Nyote mnafaa kuwa watu walio wenye mantiki na wanaoukubali ukweli. Pengine, baada ya kusikia njia ya kweli na kusoma neno la uzima, unaamini kuwa neno moja tu kati ya maneno haya elfu kumi ndiyo yanayolingana na dhana zako na Biblia, na kisha unafaa kuendelea kutafuta katika moja kati ya elfu kumi ya maneno haya. Bado Nawashauri muwe wanyenyekevu, msijiamini sana, na msijiinue juu sana. Moyo wako ukiwa na uchaji mdogo kama huu kwa Mungu, utapata mwanga mkuu. Ukichunguza kwa makini na kurudia kutafakari maneno haya, utapata kuelewa iwapo ni ukweli au la, na iwapo ni ya uzima au la. Pengine, baada ya kusoma tu sentensi chache, watu wengine watakashifu kwa upofu maneno haya, wakisema, “Hiki sicho chochote ila nuru kiasi ya Roho Mtakatifu,” ama, “Huyu ni Kristo wa uongo ambaye amekuja kuwadanganya watu.” Wale wanaosema vitu kama hivyo wamepofushwa na ujinga! Unaelewa kiasi kidogo sana kuhusu kazi na hekima ya Mungu, na Nakushauri uanze tena kutoka mwanzo! Hamfai kuyakashifu kwa upofu maneno yaliyonenwa na Mungu kwa sababu ya kutokea kwa Makristo wa uongo katika siku za mwisho, na hampaswi kuwa watu wanaomkufuru Roho Mtakatifu kwa sababu mnaogopa kudanganywa. Je, hiyo haitakuwa hali kubwa ya kuhuzunisha? Iwapo, baada ya uchunguzi mwingi, bado unaamini kuwa maneno haya si ukweli, si njia, na si maonyesho ya Mungu, basi utaadhibiwa hatimaye, na kuwa bila baraka. Iwapo huwezi kukubali ukweli kama huu ulionenwa wazi sana na kwa kawaida sana, basi wewe si ni asiyefaa kwa wokovu wa Mungu? Je, wewe si mtu ambaye hana bahati ya kutosha kurejea mbele za kiti cha enzi cha Mungu? Waza kuhusu hili! Usiwe mwenye pupa wala wa haraka, na usiichukulie imani kwa Mungu kama mchezo. Fikiria kwa ajili ya hatima yako, kwa ajili ya matarajio yako, kwa ajili ya maisha yako, na usifanye mchezo na nafsi yako. Je, unaweza kuyakubali maneno haya?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 288)

Wakati huo, sehemu ya kazi ya Yesu ilikuwa kwa mujibu wa Agano la Kale, pia na sheria za Musa na maneno ya Bwana wakati wa kipindi cha Enzi ya Sheria. Yote hayo Yesu Alitumia kufanya sehemu ya kazi yake. Alihubiri kwa watu na kuwafundisha kwenye masinagogi, na yeye Alitumia utabiri wa manabii katika Agano la Kale kuwakemea Mafarisayo waliokuwa na uhasama Naye, na Alitumia maneno katika Maandiko kufichua uasi wao na hivyo kuwahukumu. Kwa maana wao walidharau mambo ambayo Yesu Aliyafanya; hasa, nyingi ya kazi ya Yesu haikufuatana na sheria katika Maandiko, na zaidi ya hayo, kile Alichofundisha kilikuwa kikuu kuliko maneno yao wenyewe, na hata kikubwa kuliko kile ambacho kilikuwa kimetabiriwa na manabii katika Maandiko. Kazi ya Yesu ilikuwa kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu na kusulubiwa tu. Kwa hivyo, hakukuwa na haja Kwake kusema maneno zaidi ili kumshinda mtu yeyote. Mengi ya yale Aliyomfundisha mwanadamu yalitolewa kutoka kwa Maandiko, na hata kama kazi yake haikuzidi Maandiko, bado Aliweza kutimiza kazi ya kusulubiwa. Yake haikuwa kazi ya neno, wala kwa ajili ya kumshinda mwanadamu, lakini kwa minajili ya kumkomboa mwanadamu. Yeye Alihusika kama dhabihu ya dhambi tu kwa mwanadamu, na hakuhusika kama chanzo cha Neno kwa mwanadamu. Hakufanya kazi ya watu wa Mataifa mengine, ambayo ilikuwa kazi ya kumshinda mwanadamu, bali Alifanya kazi ya kusulubiwa, kazi ambayo ilifanywa miongoni mwa wale ambao waliamini kulikuwa na Mungu. Japokuwa kazi yake ilifanywa juu ya msingi wa Maandiko, na Alitumia yale yaliyotabiriwa na manabii wa kale kuwahukumu Mafarisayo, hii ilikuwa ya kutosha kukamilisha kazi ya kusulubiwa. Kama kazi ya leo ingekuwa bado inafanyika juu ya misingi ya utabiri wa manabii wa kale katika Maandiko, basi haingewezekana nyinyi kushindwa, kwa kuwa Agano la Kale halina kumbukumbu ya uasi na dhambi zenu nyinyi watu wa China, hakuna historia ya dhambi zenu. Kwa hivyo, kama kazi hii bado ingedumu katika Biblia, hamngeweza kutoa matunda. Biblia inaandika lakini kwa uchache historia ya wana wa Israeli, ambayo haina uwezo wa kusadikisha iwapo nyinyi ni waovu ama wema, ama ya kukuhukumu. Hebu Fikiria kama Ningekuwa wa kuwahukumu nyinyi kadri ya historia ya wana wa Israeli—bado mngenifuata Mimi kama mnavyonifuata hivi leo? Je, mnajua jinsi ambavyo nyinyi m wagumu? Kama hakuna maneno ambayo yalisemwa wakati wa awamu hii, basi itakuwa vigumu kukamilisha kazi ya ushindi. Kwa sababu Mimi sijakuja kugongomewa msumari msalabani, sharti Mimi niseme maneno ambayo ni tofauti na yatokayo kwa Biblia, ilimradi muweze kushindwa. Kazi iliyofanywa na Yesu ilikuwa tu hatua moja juu zaidi ya Agano la Kale; ilitumiwa kuianza enzi, na kuiongoza enzi hiyo. Kwa nini Alisema, “Sikuja kuharibu sheria, bali kuitimiza”? Lakini katika kazi Yake kulikuwa na mengi ambayo yalitofautiana na sheria zilizotumika na amri zilizofuatwa na Waisraeli wa Agano la Kale, kwani Hakuja kuitii sheria, bali kuitimiza. Mchakato wa kuitimiza ulikuwa pamoja na mambo mengi halisi: Kazi Yake ilikuwa ya vitendo zaidi na halisi, na, aidha, ilikuwa hai, na hakukuwa tu kufuata masharti bila kufikiri. Je, Waisraeli hawakuitii Sabato? Yesu alipokuja Hakuitii Sabato, kwani Alisema kwamba Mwana wa Adamu alikuwa Bwana wa Sabato, na wakati ambapo Bwana wa Sabato alikuja, Angefanya Alivyopenda. Alikuwa Amekuja kutimiza sheria za Agano la Kale na kuzibadilisha sheria. Yote ambayo hufanywa leo ni kwa msingi wa siku hizi, lakini bado yako juu ya msingi wa kazi ya Bwana katika Enzi ya Sheria, na hayavuki mipaka ya eneo hili. Kuulinda ndimi zenu, na kutozini, kwa mfano—Je, hizi si sheria za Agano la Kale? Leo, kile kinachotakikana kwenu sio chenye upeo wa amri kumi tu, lakini ni kuwa na amri na sheria ambazo zina ukuu kuliko hizo zilizokuja hapo awali, ila hii haina maana kuwa kile kilichokuja hapo awali kimeondolewa, kwa kuwa kila awamu ya kazi ya Mungu hufanywa juu ya msingi wa awamu ambayo ilikuja hapo awali. Na kuhusu kile ambacho Yehova aliwasilisha kwa Israeli, kama vile kuwahitaji watu kutoa sadaka, kuwaheshimu wazazi wao, kutoabudu sanamu, kutowadhulumu au kutukana wengine, kutozini, kutovuta sigara au kutokunywa pombe, na kutokula nyamafu au kunywa damu, je, huo si muundo msingi wa utendaji wenu hata leo? Kazi iliyotekelezwa hadi leo iko juu ya msingi wa mambo ya zamani. Ingawa sheria za zamani hazitajwi tena, nawe umewekewa madai mapya, sheria hizi mbali na kufutwa, badala yake, zimeinuliwa katika hadhi ya juu zaidi. Kusema kwamba zimefutwa kuna maana kwamba enzi ya awali imepitwa na wakati, wakati kuna amri zingine ambazo lazima uzitii milele yote. Amri za zamani tayari zimetiwa katika vitendo, tayari zimekuwa nafsi ya mwanadamu, na hakuna haja ya kurudia kusema amri za kutovuta sigara, kutokunywa pombe, na kadhalika. Juu ya msingi huu, amri mpya zimeagizwa kufuatana na mahitaji yenu leo, kufuatana na kimo chenu, na kufuatana na kazi ya leo. Kutangaza amri kwa ajili ya enzi mpya hakumaanishi kufuta amri za enzi ya kale, bali kuziinua juu zaidi ya msingi huu, kuyafanya matendo ya mwanadamu kuwa kamili zaidi, na kufuatana na uhalisi zaidi. Kama, leo, mngetakiwa tu kufuata amri na kutii sheria za Agano la Kale, kwa namna sawa na wana wa Israeli, na kama, hata, nyinyi mlitakiwa mkariri sheria ambazo ziliwekwa na Bwana, hakungekuwa na uwezekano kwamba mngeweza kubadilika. Kama mngekuwa tu mnatakiwa kutii zile amri chache zilizo na mipaka ama kukariri sheria zisizohesabika, asili zenu za zamani zingebaki zimekita mizizi, na hakungekuwa na mbinu ya kuzing’oa. Hivyo mngeendelea kuzidi kupotoshwa, na hakuna hata mmoja wenu angeweza kuwa mtiifu. Ambayo ni kusema kwamba amri chache rahisi au sheria zisizohesabika hazina uwezo wa kuwasaidia kujua matendo ya Yehova. Nyinyi si sawa na wana wa Israeli: kwa kufuata sheria na kukariri amri waliweza kushuhudia matendo ya Yehova, na kumpa Yeye pekee ibada yao, lakini hamwezi kufanikisha hili, na amri chache za Agano la Kale haziwezi tu kuwafanya nyinyi kupeana mioyo yenu, au kuwalinda, lakini badala yake itawafanya muwe wazembe, na kuwateremsha mpaka Kuzimu. Kwa sababu kazi Yangu ni kazi ya ushindi, na inalenga uasi wenu na asili yenu ya zamani. Maneno yenye huruma ya Yehova na Yesu yanapungukiwa mno na maneno makali ya hukumu leo. Bila maneno makali kama haya, ingekuwa vigumu kuwashinda ninyi “wataalam,” ambao mmekua wasiotii kwa miaka elfu nyingi. Sheria za Agano la Kale zilipoteza nguvu zake kwenu kwa muda mrefu uliopita, na hukumu ya leo ni ya kuogofya mno kuliko sheria za zamani. Ya kuwafaa nyinyi zaidi ni hukumu, na wala si vikwazo duni vya sheria, kwa kuwa ninyi si wanadamu wa mwanzo kabisa, lakini wanadamu ambao wamekuwa fisadi kwa miaka elfu nyingi. Kile ambacho mwanadamu lazima atimize sasa ni kulingana na hali halisi ya mwanadamu leo, kulingana na tabia bora na kimo halisi cha mwanadamu wa siku hizi, na hakihitaji kwamba wewe ufuate mafundisho ya dini. Hii ni kwa minajili ya mabadiliko yaweze kupatikana katika asili zako za zamani, na ili uweze kutupa kando dhana zako.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (1)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 289)

Historia inasonga mbele daima, na kazi ya Mungu inasonga mbele daima. Ili mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita ufike upeo wake, lazima uendelee kusonga mbele. Kila siku ni sharti Yeye afanye kazi mpya, kila mwaka lazima Yeye afanye kazi mpya, ni sharti Yeye azindue njia mpya, azindue enzi mpya, aanzishe kazi mpya na kubwa zaidi, na ni sharti alete majina mapya na kazi mpya. Roho wa Mungu daima hufanya kazi mpya, na kamwe Hashikilii njia za zamani au masharti. Kazi Yake pia kamwe haikomi, na inatendeka wakati wote. Ukisema kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni isiyobadilika, basi kwa nini Yehova aliwaruhusu makuhani kumhudumia Yeye hekaluni, lakini Yesu hakuingia hekaluni licha ya ukweli kwamba Alipokuja watu pia walisema kwamba Alikuwa kuhani mkuu, na kwamba Alikuwa wa nyumba ya Daudi na pia kuhani mkuu, na Mfalme mkuu? Na kwa nini Hakutoa dhabihu? Kuingia hekaluni au la—hii yote sio kazi ya Mungu Mwenyewe? Iwapo, kama mwanadamu anavyofikiria, Yesu Atakuja, akiwa anaitwa Yesu wakati wa siku za mwisho, na bado juu ya wingu jeupe, akishuka miongoni mwa wanadamu kwa mfano wa Yesu: huko hakutakuwa kurudia kazi yake? Je, si Roho Mtakatifu Atakuwa Ameshikamana na ya kale? Yote yale ambayo mwanadamu anaamini ni mawazo, na yote ambayo mwanadamu anakubali ni kulingana na maana halisi, na ni kwa mujibu wa mawazo yale; yanakinzana na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu, na hayafuatani na nia ya Mungu. Mungu pia hawezi kufanya hivyo; Mungu si mpumbavu na mjinga kiasi hicho, na kazi Yake si rahisi kama unavyofikiria. Kwa kutegemeza mambo yote yanayofikiriwa na mwanadamu, Yesu Atarejea juu ya wingu na Atateremka kati yenu. Mtamwona Yeye ambaye, akiwa amepaa juu ya wingu, atawaambia kwamba yeye ni Yesu. Nanyi pia mtatazama alama za misumari katika mikono yake, na mtamjua Yeye ni Yesu. Naye ndiye Atakayewaokoa tena, na Atakuwa Mungu wenu Mwenye nguvu. Yeye ndiye Atakayewaokoa, na kuwakabidhi ninyi jina jipya, na kumpa kila mtu jiwe jeupe, ambapo baadaye mtakubaliwa kuingia katika ufalme wa mbinguni na kulakiwa kwenye paradiso. Je, imani kama hizo si fikira za mwanadamu? Je, Mungu hufanya kazi kulingana na fikira za mwanadamu, au, je, Yeye hufanya kazi kinyume cha fikira za mwanadamu? Je, si fikira zote za mwanadamu zatoka kwa Shetani? Je, mwanadamu hajapotoshwa na Shetani? Kama Mungu Alifanya kazi yake kulingana na fikira ya mwanadamu, je, si Mungu Angekuwa Shetani? Je, si Angekuwa wa aina sawa na viumbe Wake wenyewe? Kwa kuwa viumbe Wake wamepotoshwa na Shetani hadi mwanadamu amekuwa mfano halisi ya Shetani, kama Mungu Angefanya kazi kwa mujibu wa vitu vya Shetani, si angekuwa katika ligi ya Shetani. Mwanadamu anawezaje kupima kina cha kazi ya Mungu? Na kwa hivyo, Mungu hafanyi kazi kwa mujibu wa fikira ya mwanadamu, na hangefanya kazi kwa njia unazofikiria. Kuna wale ambao husema kwamba Mungu mwenyewe Alisema kuwa Atawasili kwa wingu. Ni ukweli kuwa Mungu mwenyewe Alisema hivyo, lakini, je, hujui kuwa siri za Mungu haziwezi kueleweka na mwanadamu? Je, unajua kuwa maneno ya Mungu hayawezi kuelezwa na mwanadamu? Na wewe una hakika, bila tashwishi yoyote, kuwa ulipewa nuru na kuangaziwa na Roho Mtakatifu? Je, si Roho Mtakatifu Aliyekuonyesha moja kwa moja kwa namna hii? Je, haya ni maelekezo ya Roho Mtakatifu, au ni fikira zako? Ulisema, “Haya yalisemwa na Mungu mwenyewe.” Lakini hatuwezi kutumia fikira zetu na akili zetu kupima maneno ya Mungu. Na kuhusu maneno ya Isaya, je, unaweza kueleza maneno yake kwa kujiamini kikamilifu? Je, wewe unathubutu kueleza maneno yake? Kwa sababu huthubutu kueleza maneno ya Isaya, mbona unathubutu kueleza maneno ya Yesu? Nani ameinuliwa kuliko mwingine, Yesu au Isaya? Kwa vile jibu ni Yesu, kwa nini unaeleza maneno yaliyosemwa na Yesu? Je, Mungu Angeweza kukwambia kuhusu kazi yake mapema? Hakuna kiumbe kinachoweza kufahamu, wala hata wajumbe walio mbinguni, wala hata Mwana wa Adamu, kwa hivyo wewe ungejuaje? Mwanadamu ana upungufu mkuu. Kilicho muhimu kwenu sasa ni kufahamu awamu tatu za kazi. Kutoka kwa kazi ya Yehova mpaka ile ya Yesu, na kutoka kwa kazi ya Yesu hadi kwa kazi iliyoko kwa awamu hii ya sasa, awamu hizi tatu zinajumlisha upana wote wa usimamizi wa Mungu, na zote ni kazi za Roho mmoja. Kutoka Alipoumba ulimwengu, Mungu Amekuwa Akisimamia wanadamu. Yeye ndiye Mwanzo na ndiye Mwisho; Yeye ndiye wa Kwanza na wa Mwisho, na Yeye ndiye mwanzilishi wa enzi na Yeye ndiye huleta enzi kwenye kikomo. Awamu tatu za kazi, katika enzi tofauti na maeneo mbalimbali, hakika yanafanywa na Roho mmoja. Wote ambao wanatenganisha awamu hizi tatu wanampinga Mungu. Sasa, lazima uelewe kwamba kazi yote kutoka awamu ya kwanza hadi leo ni kazi ya Mungu mmoja, ni kazi ya Roho mmoja, ambapo hakuna shaka.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 290)

Kwa kuwa mwanadamu anamwamini Mungu, ni sharti afuate kwa ukaribu nyayo Zake, hatua kwa hatua; anapaswa “kumfuata Mwanakondoo popote Aendapo.” Hawa tu ndio watu wanaotafuta njia ya kweli, na wao tu ndio wanaoifahamu kazi ya Roho Mtakatifu. Watu wanaofuata tu kanuni na mafundisho ya dini kiutumwa ni wale ambao wameondolewa na kazi ya Roho Mtakatifu. Katika kila kipindi cha wakati, Mungu ataanza kazi mpya, na katika kila kipindi, patakuwepo na mwanzo mpya kwa mwanadamu. Laiti mwanadamu ashikilie tu ukweli kwamba “Yehova ni Mungu” na “Yesu ni Kristo,” ambao ni ukweli unaozingatiwa katika enzi moja tu, basi mwanadamu hatawahi kwenda sambamba na kazi ya Roho Mtakatifu, na daima hataweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Bila kujali jinsi Mungu anavyofanya, mwanadamu anafaa kufuata bila shaka lolote, na afuate kwa ukaribu. Kwa jinsi hii basi itakuwaje mwanadamu aondolewe na Roho Mtakatifu? Bila kujali kile anachofanya Mungu, kama mwanadamu ana uhakika ni kazi ya Roho Mtakatifu, na kushirikiana katika kazi ya Roho Mtakatifu bila mashaka yoyote, na kujaribu kufikia mahitaji ya Mungu, basi ataadhibiwaje? Kazi ya Mungu kamwe haijasimama, hatua Zake hazijakwama na kabla kukamilisha kazi Yake ya usimamizi, siku zote Mungu amekuwa mwenye kazi nyingi, na kamwe hajasimama. Lakini mwanadamu ni tofauti: Kutokana na kupata kiwango cha chini cha nguvu za Roho Mtakatifu, yeye huchukulia kwamba hakuna chochote kitakachobadilika; baada ya kupata ufahamu kidogo, hajipi msukumo wa kufuata nyayo za kazi mpya ya Mungu; licha ya kwamba ameona kiasi kazi ya Mungu, yeye anamchukulia Mungu kama kifaa, aina fulani ya umbo la sanamu ya mti, na anaamini kwamba Mungu atasalia kuwa hivyo daima kwani hali imekuwa hii tangu hapo awali na hata katika siku zijazo; akiwa amepata ufahamu wa kijuujuu, mwanadamu ni mwenye kiburi hivi kwamba hujisahau na kuanza kutangaza kwa fujo tabia ya Mungu na hali ya Mungu ambayo haipo; na akiwa na uhakika juu ya hatua moja ya Roho Mtakatifu, pasi kujali ni mtu wa aina gani ambaye anatangaza kazi mpya ya Mungu, mwanadamu huwa haikubali. Hawa ni watu ambao hawawezi kuikubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu; ni watu wenye kushikilia ukale sana, na hawawezi kukubali mambo mapya. Watu kama hawa ni watu wanaomwamini Mungu lakini wakati uo huo wanamkataa Mungu. Mwanadamu anaamini kwamba wana wa Israeli walikosea “tu kumuamini Yehova na kukosa kumuamini Yesu,” huku watu wengi wakiiga jukumu ambapo “humwamini Yehova tu na kumkataa Yesu” na “kusubiri kwa hamu kurejea kwa Masihi lakini wanamkataa Masihi ambaye ni Yesu”. Ndiyo maana, basi, watu wengi bado wanaishi chini ya mamlaka ya Shetani baada ya kukubali hatua moja tu ya Roho Mtakatifu na bado hawapokei baraka za Mungu. Je, si hii ni kutokana na uasi wa mwanadamu? Wakristo ulimwenguni kote ambao hawajazingatia kazi mpya ya sasa wote wameshikilia imani kwamba wao ni wenye bahati na kwamba Mungu atawatimizia kila mojawapo ya malengo yao. Lakini hawawezi kueleza mbona Mungu atawapeleka katika mbingu ya tatu na wala hawafahamu jinsi Yesu atakavyokuja juu ya wingu jeupe na kuwachukua, wala kusema kwa uhakika kamili kama kweli Yesu atawasili akiwa juu ya wingu jeupe siku ambayo wanaiwaza. Wote wana wasiwasi, na kukanganywa; wao wenyewe hata hawafahamu kama Mungu atachukua kila mmoja wao, watu wachache sana, wanaotoka katika madhehebu yote. Kazi ambayo Mungu anafanya kwa sasa, enzi ya sasa, mapenzi ya Mungu—ni vitu ambavyo watu hawavifahamu, na hawana cha kufanya bali kusubiri na kuhesabu siku katika vidole vyao. Ni wale tu wanaofuata nyayo za Mwanakondoo hadi mwisho kabisa ndio wanaoweza kufaidi baraka za mwisho, huku wale “watu werevu,” ambao hawawezi kumfuata hadi mwisho ilhali wanaamini wamepata yote, ndio wasiokuwa na uwezo wa kushuhudia kuonekana kwa Mungu. Wote huamini wao ndio werevu zaidi duniani, na wanasitisha maendeleo ya kazi ya Mungu bila sababu yoyote kabisa, na huonekana kuamini pasi na shaka kwamba Mungu atawachukua mbinguni, wao “wenye uaminifu wa juu zaidi kwa Mungu, humfuata Mungu, na hutii neno la Mungu”. Hata ingawa wana “uaminifu wa hali ya juu” kwa maneno yaliyozungumzwa na Mungu; maneno yao na matendo yao bado hukera kwa sababu wao huipinga kazi ya Roho Mtakatifu, na kufanya uongo na uovu. Wale wasiofuata hadi mwisho kabisa, ambao hawazingatii kazi ya Roho Mtakatifu, na ambao wanashikilia kazi ya zamani hawajakosa tu kupata uaminifu kwa Mungu, bali kwa kinyume, wamekuwa wale wanaompinga Mungu, wamekuwa wale ambao wamekanwa na enzi mpya, na watakaoadhibiwa. Kuna wa kuhurumiwa zaidi kuliko wao? Wengi hata wanaamini kuwa wale wanaokana sheria ya zamani na kukubali kazi mpya hawana dhamiri. Watu hawa, ambao huongea tu kuhusu “dhamiri,” na hawajui kazi ya Roho Mtakatifu, hatimaye watapata kuwa matarajio yao yamekatizwa na dhamiri yao yenyewe. Kazi ya Mungu haizingatii mafundisho, na ingawa ni kazi Yake Mwenyewe, bado Mungu haishikilii. Kile kinachopaswa kukataliwa kinakataliwa, kile kinachopaswa kuondolewa kinaondolewa. Lakini mwanadamu anajiweka kwenye uadui wa Mungu kwa kushikilia sehemu moja ndogo ya kazi ya usimamizi wa Mungu. Si huu ndio upuuzi wa mwanadamu? Si huu ndio ujinga wa mwanadamu? Kadri watu wanakuwa waoga na wenye tahadhari sana kwa sababu wanachelea kutopata baraka za Mungu, ndivyo wanavyopungukiwa zaidi na uwezo wa kupata baraka zaidi, na wa kupata ile baraka ya mwisho. Watu wale wanaoshikilia kiutumwa sheria huwa wanadhihirisha uaminifu wa hali ya juu kwa sheria, na kadri wanavyodhihirisha uaminifu jinsi hiyo kwa sheria, ndivyo wanavyokuwa waasi wanaompinga Mungu. Kwa kuwa sasa ni Enzi ya Ufalme na wala si Enzi ya Sheria, na kazi ya leo na kazi ya zamani haziwezi kulinganishwa, wala kazi ya zamani haiwezi kulinganishwa na kazi ya sasa. Kazi ya Mungu imebadilika, na vitendo vya mwanadamu pia vimebadilika; si kushikilia sheria au kuubeba msalaba. Basi, uaminifu wa watu kwa sheria na msalaba hautapata kibali cha Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 291)

Kusudi la kukushinda leo ni kukufanya utambue kuwa Mungu ni Mungu wako, na Mungu wa wengine, na muhimu zaidi ni Mungu wa wote wanaompenda, na Mungu wa viumbe wote. Ni Mungu wa Israeli na Mungu wa Misri. Ni Mungu wa Waingereza na Mungu wa Wamarekani. Si Mungu wa Adamu na Hawa tu, bali pia Mungu wa kizazi cha Adamu na Hawa. Ni Mungu wa kila Kitu mbinguni na duniani. Familia ya Waisraeli na familia zote za Mataifa zimo mikononi mwa Mungu. Hakufanya kazi katika nchi ya Israeli pekee kwa miaka elfu kadhaa na kuzaliwa Uyahudi, ila leo Anashuka Uchina, nchi hii ambapo joka kuu jekundu limejikunja. Ikiwa kuzaliwa Uyahudi kunamfanya Mfalme wa Wayahudi, basi si kushuka kwake miongoni mwenu leo kunamfanya Mungu wenu? Aliwaongoza Waisraeli na alizaliwa Yudea na vilevile amezaliwa katika nchi ya Mataifa. Je, kazi Yake yote haifanywi kwa ajili ya wanadamu wote Aliowaumba? Je, Anawapenda Waisraeli mara mia moja na kuwachukia Mataifa mara elfu moja? Je, hayo siyo mawazo yenu? Ni ninyi ambao hamtambui Mungu; si kwamba Mungu Hakuwa Mungu wenu. Ni ninyi mnaomkataa Mungu; si kwamba Mungu hapendi kuwa Mungu wenu. Ni nani kati ya walioumbwa hayuko mikononi mwa mwenye Uweza? Kwa kuwashinda leo, je, lengo si kuwafanya mtambue kuwa Mungu ni Mungu wenu? Iwapo bado mnashikilia kuwa Mungu ni Mungu wa Waisraeli tu, na kuendelea kushikilia kuwa nyumba ya Daudi huko Israeli ni asili ya uzao wa Mungu na kuwa hakuna taifa tofauti na Israeli limewezeshwa “kumzaa” Mungu, na hata zaidi kuwa hakuna familia ya Mataifa yenye uwezo wa kupokea kazi ya Yehova—ikiwa bado unafikiria hivi, je, haikufanyi kuwa mshikiliaji wa ukaidi? Usikazie macho Israeli kila wakati. Mungu Yuko hapa miongoni mwenu leo. Vilevile msitazamie mbingu tu. Acheni kutamani Mungu wenu Aliye mbinguni! Mungu ametua miongoni mwenu, basi Anawezaje kuwa mbinguni? Hujaamini katika Mungu kwa muda mrefu, ilhali una mawazo mengi kuhusu Mungu, kiasi kwamba unathubutu kutofikiri hata kwa sekunde moja kuwa Mungu wa Waisraeli Anaweza kuwatunukia na uwepo wake. Wala hamthubutu kufikiri jinsi mnavyoweza kumwona Mungu Akijitokeza binafsi, ikitiliwa maanani jinsi mlivyo wachafu. Aidha hamjawahi kufikiri jinsi Mungu anavyoweza kushuka miongoni mwa Mataifa. Anapaswa kushuka juu ya Mlima Sinai au Mlima wa Mizeituni na kuonekana kwa Waisraeli. Je, si watu wa Mataifa (yaani watu wa nje ya Israeli) ndio walengwa wa chuki Yake? Anawezaje kufanya kazi miongoni mwao? Haya yote ni mawazo yaliyokita mizizi ndani yenu ambayo mmeyakuza kwa miaka mingi. Kusudi la kuwashinda leo ni kuyaharibu haya mawazo yenu. Kwa njia hiyo mmeweza kumwona Mungu akijionyesha Mwenyewe miongoni mwenu—si katika Mlima Sinai au Mlima wa Mizeituni, bali miongoni mwa watu ambao Hajawahi kuwaongoza hapo awali. Baada ya Mungu kufanyia hatua mbili za kazi Yake Israeli, Waisraeli na watu wa Mataifa walishikilia wazo hili: Japo ni kweli Mungu aliumba viumbe wote, yuko radhi kuwa Mungu wa Waisraeli tu, si Mungu wa Mataifa. Waisraeli wanaamini yafuatayo: Mungu anaweza tu kuwa Mungu wetu, sio Mungu wenu Mataifa, na kwa sababu humchi Yehova, Yehova—Mungu wetu—Anawachukia. Zaidi, Wayahudi hao huamini hili: Bwana Yesu alichukua sura yetu Wayahudi na ni Mungu aliye na alama ya Wayahudi. Mungu anafanyia kazi miongoni mwetu. Sura ya Mungu na sura zetu zinafanana; sura zetu na sura ya Mungu zinakaribiana. Bwana Yesu ni Mfalme wetu Wayahudi; watu wa Mataifa hawajawezeshwa kupokea wokovu mkubwa kiasi hicho. Bwana Yesu ni sadaka ya dhambi kwetu Wayahudi. Ni kwa misingi ya hatua hizi mbili za kazi ndipo Waisraeli na Wayahudi walijijengea haya mawazo mengi. Wanamdai Mungu kuwa wao tu, bila kukubali kwamba Mungu vilevile ni Mungu wa Mataifa. Kwa njia hii, Mungu alikuwa pengo katika mioyo ya watu wa Mataifa. Hii ni kwa sababu kila mtu aliamini kuwa Mungu hataki kuwa Mungu wa watu wa Mataifa na kuwa Anawapenda tu Waisraeli—Wateule wake—na Anawapenda Wayahudi hasa wafuasi waliomfuata. Je, wajua kuwa kazi aliyoifanya Yehova na Yesu ilikuwa ni kwa ajili ya uzima wa wanadamu wote? Je, sasa unatambua kuwa Mungu ni wa wale wote waliozaliwa nje ya Israeli? Je, Mungu Hayumo miongoni mwenu leo? Hii haiwezi kuwa ndoto, ama vipi? Je, hamkubali uhalisi huu? Mnathubutu kutoamini au kulifikiria. Licha ya jinsi mnavyolitazama, je, Mungu hayumo miongoni mwenu? Je, bado mnaogopa kuyaamini maneno haya? Kuanzia leo, je, wote walioshindwa, na wale wote wanaotaka kuwa wafuasi wa Mungu, si wateule wa Mungu? Je, nyote mlio wafuasi leo, si wateule nje ya Israeli? Je, nafasi yenu si sawa na ya Waisraeli? Je, hili silo mnalopaswa kutambua? Je, hili si lengo la kazi ya kukushinda? Kwa kuwa mwaweza kumwona Mungu, basi Atakuwa Mungu wenu milele, tangu mwanzo hadi siku za baadaye. Hatawaacha, mradi tu nyinyi nyote mko radhi Kumfuata na kuwa viumbe Wake waaminifu na watiifu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (3)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 292)

Ni katika kuweka dhana zako za kale kando tu ndipo utakapoweza kupata maarifa mapya, ilhali maarifa ya zamani si lazima yawe dhana za zamani. “Dhana” inamaanisha vitu vinavyodhaniwa na mwanadamu ambavyo viko mbali na uhalisi. Kama maarifa ya zamani yalikuwa yamepitwa na wakati katika enzi ya kale, na yalimzuia mwanadamu kuingia katika kazi mpya, basi maarifa kama yale pia ni dhana. Ikiwa mwanadamu ataweza kuchukua mwelekeo mzuri kwa maarifa kama yale, na anaweza pata kumjua Mungu kutoka kwa vipengele tofauti, kuunganisha ya zamani na mapya, basi maarifa ya kale yatamsaidia mwanadamu, na yatakuwa msingi wa mwanadamu kuingia katika enzi mpya. Funzo la kumjua Mungu linahitaji kwamba uwe stadi wa kanuni nyingi: jinsi ya kuingia kwenye njia ya kumjua Mungu, ukweli gani unapaswa kuelewa ili kumjua Mungu, na jinsi ya kuondoa dhana zako na asili yako ya kale ili kwamba uweze kutii mipango yote ya kazi mpya ya Mungu. Ukitumia kanuni hizi kama msingi wa kuingia kwenye somo la kumjua Mungu, basi maarifa yako yatakuwa na kina zaidi na zaidi. Kama una maarifa wazi ya hatua tatu za kazi—ambayo ni kusema kwamba, ya mpango mzima wa usimamizi wa Mungu—na ikiwa utaweza kupatanisha hatua mbili za awali na hatua ya sasa, na unaweza kuona kwamba ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja, basi utakuwa na msingi imara zaidi. Hatua tatu za kazi zilifanywa na Mungu mmoja; haya ndiyo maono makubwa zaidi, na ndiyo njia ya pekee ya kumjua Mungu. Hatua tatu za kazi zingefanywa tu na Mungu Mwenyewe, na hapana mwanadamu yeyote ambaye angeweza kufanya kazi kama hii kwa niaba Yake—ambayo ni kusema kuwa ni Mungu Mwenyewe pekee ambaye angeifanya kazi Yake toka mwanzo hadi leo. Ingawa hatua tatu za kazi ya Mungu zimefanywa katika enzi tofauti na maeneo tofauti, na ingawa kazi ya kila moja ni tofauti, yote ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja. Kati ya maono yote, hili ndilo kuu zaidi ambalo mwanadamu anapaswa kulijua, na ikiwa litaeleweka kabisa na mwanadamu, basi ataweza kusimama imara. Leo, tatizo kuu linalokumba dini na madhehebu kadhaa ni kwamba hazijui kazi ya Roho Mtakatifu, na hazina uwezo wa kutofautisha kati ya kazi ya Roho Mtakatifu na kazi isiyo ya Roho Mtakatifu—na kwa hivyo hawawezi kueleza kama hatua hii ya kazi, kama hatua mbili za awali, pia zimefanywa na Yehova Mungu. Ingawa watu wanamfuata Mungu, wengi hawawezi kueleza kama ni njia sahihi. Mwanadamu anahofia ikiwa hii ndiyo njia inayoongozwa na Mungu Mwenyewe, na kama Mungu kupata mwili ni jambo la hakika, na watu wengi bado hawana dokezo jinsi ya kupambanua ikifikia maneno kama haya. Wale wanaomfuata Mungu hawawezi kujua njia, na kwa hivyo habari zinazozungumzwa zinaathiri sehemu ndogo tu kati ya watu hawa na hayana uwezo wa kufaa kikamilifu, na kwa hivyo, hili basi linaathiri kuingia kwa maisha kwa watu kama hawa. Ikiwa mwanadamu anaweza kuona katika hatua tatu za kazi kuwa zilitekelezwa na Mungu Mwenyewe wakati tofauti, katika maeneo tofauti, na kwa watu tofauti; ikiwa mwanadamu anaweza kuona kuwa ingawa kazi ni tofauti, yote imefanywa na Mungu mmoja, na kwa kuwa ni kazi ambayo imefanywa na Mungu mmoja, basi lazima iwe sawa, na bila dosari, na kwamba ingawa hailingani na dhana za mwanadamu, hakuna kupinga kuwa ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja—ikiwa mwanadamu anaweza kusema kwa hakika kuwa ni kazi ya Mungu mmoja, basi dhana zake zitakuwa duni, na ambazo hazifai kutajwa. Kwa sababu maono ya mwanadamu hayako wazi, na mwanadamu anamjua tu Yehova kama Mungu, na Yesu kama Bwana, na ana mitazamo miwili kumhusu Mungu mwenye mwili wa leo, watu wengi wamejitoa kwa ajili ya kazi ya Yehova na Yesu, na wamezingirwa na dhana kuhusu kazi ya leo, watu wengi daima huwa na shaka na hawachukulii kazi ya leo kwa makini. Mwanadamu hana uelewa kuhusu hatua mbili za mwisho, ambazo hazikuonekana. Hio ni kwa sababu mwanadamu haelewi uhalisi wa hatua mbili za mwisho za kazi, na wala hakuzishuhudia binafsi. Ni kwa sababu haziwezi kuonekana ndiyo mwanadamu anawaza jinsi anavyopenda; bila kujali atakayodhania, hakuna ukweli wa kudhibitisha, na yeyote wa kurekebisha. Mwanadamu anaruhusu silika yake ya asili itawale, huku akikosa kujali na kuachilia mawazo yake yaende popote, kwa kuwa hakuna ukweli wa kudhibitisha, na kwa hivyo dhana za mwanadamu zinakuwa “ukweli,” bila kujali kama zina dhibitisho. Kwa hivyo mwanadamu anaamini Mungu wake aliyemuwazia akilini mwake, na hamtafuti Mungu wa uhalisi. Ikiwa mtu mmoja ana aina moja ya imani, basi kati ya watu mia moja kuna aina mia moja za imani. Mwanadamu ana imani kama hizi kwa maana hajaona uhalisi wa kazi ya Mungu, kwa sababu amesikia tu kwa masikio yake na hajaona kwa macho yake. Mwanadamu amesikia hekaya na hadithi—lakini amesikia kwa nadra kuhusu maarifa ya ukweli ya kazi ya Mungu. Hivyo ni katika dhana zao ndivyo watu ambao wamekuwa waumini kwa mwaka mmoja tu wanaamini Mungu, na hilo ni kweli pia kwa wale ambao wamemwamini Mungu katika maisha yao yote. Wale ambao hawawezi kuona ukweli daima hawawezi kuepuka imani ambayo wana dhana kwazo kumhusu Mungu. Mwanadamu anaamini kuwa amejiweka huru kutokana na vifungo vya dhana zake za kale, na ameingia eneo jipya. Je, mwanadamu hajui kuwa maarifa ya wale wasioweza kuona uso wa kweli wa Mungu kuwa ni dhana na tetesi? Mwanadamu anafikiria kuwa dhana zake ni sawa, na wala hayana kasoro, na hufikiri kuwa hizi dhana zimetoka kwa Mungu. Leo, mwanadamu anaposhuhudia kazi ya Mungu, anaachilia dhana zilizokuwa zimeongezeka kwa miaka mingi. Mawazo na dhana za awali zilikuwa vizuizi vya kazi ya hatua hii, na inakuwa vigumu kwa mwanadamu kuachana na dhana kama hizo na kupinga mawazo kama yale. Dhana kuhusu kazi hii ya hatua kwa hatua ya wengi wa wale wanaomfuata Mungu hadi leo zimekuwa za kuhuzunisha na watu hawa pole pole wamefanya uadui wa kikaidi na Mungu mwenye mwili hatua kwa hatua, na chanzo cha chuki ni mawazo na dhana za mwanadamu. Ni hasa kwa sababu ukweli haumruhusu mwanadamu kuwa na uhuru wa hiari ya mawazo yake, na, zaidi ya hayo, hauwezi kupingwa na mwanadamu kwa urahisi, na mawazo na dhana za mwanadamu hazistahimili uwepo wa ukweli, na hata zaidi ya hayo, kwa sababu mwanadamu hawezi kufikiria kuhusu usahihi na unyofu wa ukweli, na kwa nia moja tu huachilia mawazo yake, na hutumia dhana yake, kwamba dhana na mawazo ya mwanadamu zimekuwa adui wa kazi ya leo, kazi ambayo haiambatani na dhana za mwanadamu. Hili linaweza kusemwa kuwa kasoro ya dhana za mwanadamu, na wala si dosari ya kazi ya Mungu. Mwanadamu anaweza kufikiria lolote atakalo, lakini hawezi kupinga waziwazi hatua yoyote ya kazi ya Mungu au hata sehemu yoyote; ukweli wa kazi ya Mungu hauwezi kukiukwa na mwanadamu. Unaweza kuruhusu mawazo yako yatawale, na unaweza pia kujumuisha hadithi nzuri kuhusu kazi ya Yehova na Yesu, lakini kamwe huwezi kupinga ukweli wa kila hatua ya kazi ya Yehova na Yesu; hii ni kanuni, na pia ni amri ya utawala, na mnapaswa kuelewa umuhimu wa masuala haya. Mwanadamu anaamini kuwa hatua hii ya kazi hailingani na dhana za mwanadamu, na hivi sivyo katika hatua mbili zilizopita za kazi. Katika mawazo yake, mwanadamu anaamini kuwa kazi ya hatua mbili zilizopita kwa hakika si sawa na kazi ya leo—lakini je, umewahi kufikiria kuwa kanuni zote za kazi ya Mungu ni sawa, na kuwa kazi Yake huwa vitendo daima, na kuwa, bila kujali enzi, daima kutakuwa na halaiki ya watu wanaokataa na kuupinga ukweli wa kazi Yake? Wale wote ambao leo wanakataa na kuipinga hatua hii ya kazi bila shaka wangempinga Mungu wakati uliopita, kwa kuwa watu kama hawa daima watakuwa adui za Mungu. Watu wanaoujua ukweli wa kazi ya Mungu wataona hatua tatu za kazi kama kazi ya Mungu mmoja, na watatupilia mbali dhana zao. Hawa ni watu wanaomjua Mungu, na watu kama hawa ndio kwa kweli humfuata Mungu. Wakati ambapo usimamizi mzima wa Mungu utakaribia kufika mwisho, Mungu ataweka vitu vyote kulingana na aina. Mwanadamu aliumbwa kwa mikono ya Muumba, na mwishowe lazima kabisa Amrudishe mwanadamu chini ya utawala Wake; huu ndio mwisho wa hatua tatu za kazi. Hatua ya kazi ya siku za mwisho, na hatua mbili zilizopita katika Israeli na Yudea, ni mpango wa Mungu wa usimamizi katika dunia nzima. Hakuna anayeweza kupinga hili, na ni ukweli wa kazi ya Mungu. Ingawa watu hawajapata uzoefu ama kushuhudia nyingi za kazi hizi, ukweli unabaki kuwa ukweli, na hauwezi kukanwa na mwanadamu yeyote. Watu wanaomwamini Mungu katika nchi zote duniani watakubali hatua tatu za kazi. Kama wajua tu hatua moja ya kazi, na huelewi hatua nyingine mbili za kazi, na huelewi kazi ya Mungu katika wakati uliopita, basi huwezi kuongea ukweli wa mpango mzima wa usimamizi wa Mungu, na maarifa yako ya Mungu yameegemea upande mmoja, kwa kuwa katika imani yako katika Mungu humfahamu, ama kumwelewa, na kwa hivyo hustahili kutoa ushuhuda wa Mungu. Bila kujali kama maarifa yako ya sasa ya mambo haya yana kina kirefu ama cha juujuu tu, mwishowe, lazima muwe na maarifa, na ushawishike kabisa, na watu wote wataona uzima wa kazi ya Mungu na kunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Mwishoni mwa kazi hii, madhehebu yote yatakuwa moja, viumbe wote watarejea chini ya utawala wa Muumba, viumbe wote watamwabudu Mungu mmoja wa kweli, na dini zote ovu zitakuwa bure, na hazitaonekana tena.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 293)

Kufahamu madhumuni ya kazi ya Mungu, athari inayotimizwa kwa mwanadamu, na mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu, hiki ndicho kitu ambacho kila mwanadamu anayemfuata Mungu anapaswa kutimiza. Sasa wanachokosa watu wote ni ufahamu wa kazi ya Mungu. Mwanadamu haelewi wala kufahamu kabisa maana ya vitendo vya Mungu ndani ya mwanadamu, kazi yote ya Mungu, na mapenzi ya Mungu tangu kuumbwa kwa dunia. Huu upungufu hauonekani tu katika ulimwengu mzima wa kidini, lakini zaidi ya hayo kwa waumini wote wa Mungu. Siku itakapofika utakapomtazama Mungu kwa kweli na kutambua hekima ya Mungu; utakapotazama matendo yote ya Mungu na kutambua kile Mungu Alicho na kile Alicho nacho; utakapotazama wingi Wake, hekima, ajabu Yake, na kazi Yake yote kwa mwanadamu, basi hapo ndipo utakuwa umefikia imani ya mafanikio kwa Mungu. Mungu anaposemekana kuwa Anayejumuisha yote na mwenye wingi, ni nini kinachomaanishwa na kujumuisha yote? Na nini kinachomaanishwa na utele? Iwapo huelewi haya, basi huwezi kuchukuliwa kuwa muumini wa Mungu. Mbona Nasema wale walio katika dunia ya kidini hawaamini katika Mungu na ni waovu, walio sawa na ibilisi? Ninaposema ni watenda maovu, ni kwa sababu hawaelewi matakwa ya Mungu, wala kuona hekima Yake. Hakuna wakati wowote ambao Mungu anadhihirisha kazi Yake kwao; ni vipofu, wasioona matendo ya Mungu. Wao ndio walioachwa na Mungu na hawamiliki kabisa utunzaji na ulinzi wa Mungu, sembuse kazi ya Roho Mtakatifu. Wale wasio na kazi ya Mungu ni watenda maovu na humpinga Mungu. Wale Ninaosema wanampinga Mungu ni wale wasiomjua Mungu, wale wanaokiri Mungu na maneno matupu ilhali hawamjui, wale wanaomfuata Mungu lakini hawamtii, na wale wanaofurahia neema ya Mungu lakini hawawezi kumshuhudia. Bila ufahamu wa madhumuni ya kazi ya Mungu na kazi ya Mungu kwa mwanadamu, mwanadamu hawezi kuwa katika ulinganifu na moyo wa Mungu, na hawezi kumshuhudia Mungu. Sababu kwamba mwanadamu humpinga Mungu inatoka, kwa upande mmoja, katika tabia potovu ya mwanadamu, na kwa upande mwingine, kutokana na kutomfahamu Mungu na kutoelewa kanuni za kazi ya Mungu na mapenzi Yake kwa mwanadamu. Vipengele hivi viwili vinaunganishwa katika historia ya upinzani wa mwanadamu kwa Mungu. Wanafunzi katika imani wanampinga Mungu kwa sababu upinzani kama huu uko ndani ya asili yao, ilhali upinzani dhidi ya Mungu wa wale walio na miaka mingi katika imani unatokana na kutomfahamu Mungu, kuongeza kwa tabia yao potovu. Kwa muda kabla ya Mungu kuwa mwili, kipimo cha kama mwanadamu alimpinga Mungu kilikuwa iwapo alishika amri zilizotolewa na Mungu mbinguni. Kwa mfano, katika Enzi ya Sheria, wowote ambao hawakushika sheria za Yehova walikuwa ndio wale waliompinga Mungu; wowote walioiba sadaka ya Yehova, na wowote waliosimama dhidi ya wale waliofadhiliwa na Yehova walikuwa wale waliompinga Mungu na wale ambao wangepigwa mawe hadi kufa; wowote ambao hawakuwaheshimu mama na baba zao, na wowote waliompiga ama kumlaani mwingine ni wale ambao hawakufuata sheria. Na wote ambao hawakufuata sheria za Yehova walikuwa wale waliosimama dhidi Yake. Hii haikuwa hivyo tena katika Enzi ya Neema, wakati wale waliosimama dhidi ya Yesu walikuwa wale waliosimama dhidi ya Mungu, na wowote ambao hawakutii maneno yaliyotamkwa na Yesu ni wale waliosimama dhidi ya Mungu. Katika enzi hii, makusudio ya upinzani kwa Mungu yalifafanuliwa zaidi na kuwa halisi. Kwa wakati ambao Mungu bado hakuwa amegeuka mwili, kipimo cha iwapo mwanadamu alimpinga Mungu kilitegemea iwapo mwanadamu alimwabudu na kumheshimu Mungu aliye mbinguni asiyeonekana. Ufafanuzi wa upinzani kwa Mungu wakati huo haukuwa halisi, kwani mwanadamu wakati huo hangemwona Mungu wala kujua mfano wa Mungu ama jinsi Alivyofanya kazi na kuongea. Mwanadamu hakuwa na dhana za Mungu na alimwamini Mungu kwa njia isiyo dhahiri, kwani Hakuwa amejitokeza kwa mwanadamu. Kwa hivyo, vile mwanadamu alivyomwamini Mungu katika mawazo yake, Mungu hakumlaumu mwanadamu ama kuulizia mengi kutoka kwa mwanadamu, kwani mwanadamu hangemwona Mungu hata kidogo. Mungu anapopata mwili na kuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu, wote wanamtazama Mungu na kusikia maneno Yake, na wote wanaona vitendo ambavyo Mungu anafanya kutoka ndani ya mwili Wake wa nyama. Katika wakati huo, fikira zote za mwanadamu zinakuwa povu tu. Kwa wale wanaomwona Mungu anayejitokeza katika mwili, wote walio na utiifu ndani ya mioyo yao hawalaaniwi, ilhali wanaosimama dhidi Yake kimakusudi watachukuliwa kuwa wapinzani wa Mungu. Wanadamu kama hao ni maadui wa Kristo na ni maadui wanaosimama dhidi ya Mungu kimakusudi. Wale walio na dhana kumhusu Mungu lakini bado wanatii kwa furaha hawatalaaniwa. Mungu anamlaani mwanadamu kulingana na nia yake na vitendo vyake, kamwe sio kwa mawazo na fikira zake. Iwapo mwanadamu angelaaniwa kwa misingi hiyo, basi hakuna mmoja ambaye angeweza kutoroka kutoka katika mikono ya Mungu ya ghadhabu. Wale wanaosimama makusudi dhidi ya Mungu mwenye mwili wataadhibiwa kwa sababu ya kutotii kwao. Upinzani wao wa makusudi unatokana na dhana zao kumhusu, ambao unasababisha usumbufu wao kwa kazi ya Mungu. Wanadamu kama hao wanapinga na kuiharibu kazi ya Mungu wakijua. Hawana tu dhana za Mungu, lakini wanafanya kile kinachosumbua kazi Yake, na ni kwa sababu hii ndiyo wanadamu kama hao watahukumiwa. Wale wasioshiriki katika usumbufu wa kazi ya Mungu kimakusudi huwatahukumiwa kama wenye dhambi, kwani wanaweza kutii kwa bila kulazimishwa na kutosababisha vurugu na usumbufu. Wanadamu kama hao hawatahukumiwa. Hata hivyo, wakati wanadamu wamepata uzoefu wa miaka mingi ya kazi ya Mungu, kama bado wanaficha dhana zao za Mungu na kubaki wasioweza kujua kazi ya Mungu mwenye mwili, na licha ya miaka mingi ya uzoefu, wanaendelea kushikilia dhana nyingi za Mungu na bado hawawezi kuja kumjua Mungu, basi hata kama hawasababishi shida yoyote kukiwa na dhana nyingi za Mungu ndani ya mioyo yao, na hata kama dhana kama hizi hazionekani, wanadamu kama hao hawana huduma yoyote kwa kazi ya Mungu. Hawawezi kuhubiri injili wala kumshuhudia Mungu; wanadamu kama hao hawana manufaa na ni wapumbavu. Kwa sababu hawamjui Mungu na hawawezi kuondoa dhana zao za Mungu, wamelaaniwa. Inaweza kusemwa hivi: Si jambo geni kwa wanafunzi wa kidini kuwa na dhana za Mungu ama kutojua chochote kumhusu, lakini sio kawaida kwa wale walioamini kwa miaka mingi na kuwa na uzoefu mwingi wa kazi Yake kushikilia dhana kama hizi, na hata zaidi kwa wanadamu kama hao kutokuwa na ufahamu wa Mungu. Ni kwa sababu ya hali kama hii isiyo ya kawaida ndio wanadamu kama hao wanalaaniwa. Wanadamu wasio wa kawaida kama hao hawana manufaa; ni wale wanaompinga Mungu zaidi na waliofurahia neema ya Mungu bure. Wanadamu wote kama hao wataondolewa mwishoni!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Watu Wote Wasiomjua Mungu Ni Watu Wanaompinga Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 294)

Wowote wasioelewa madhumuni ya kazi ya Mungu ni wale wanaompinga Mungu, na hata zaidi ya hayo ni wale waliofahamu madhumuni ya kazi ya Mungu lakini bado hawatafuti kumridhisha Mungu. Wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu waovu, kila mmoja akisimama juu kufundisha kuhusu Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga kwa hiari. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, pepo wakuu wanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Inagawa wao ni wenye “mwili imara,” wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza? Wale wanaojiheshimu mbele ya Mungu ni wanadamu wa chini kabisa, ilhali wanaojinyenyekeza ndio wa heshima zaidi. Na wale wanaojifikiria kujua kazi ya Mungu na kutangaza neno la Mungu kwa wengine kwa kishindo na tarumbeta nyingi wakati macho yao yako Kwake—hawa ndio wajinga zaidi kati ya wanadamu. Wanadamu kama hao ni wale wasio na ushahidi wa Mungu, na wale walio na kiburi na majivuno. Wale wanaoamini kwamba wana ufahamu mdogo wa Mungu licha ya uzoefu wao halisi na ufahamu wa vitendo ni wale Anaowapenda zaidi. Ni wanadamu kama hawa ndio walio na ushahidi wa kweli na wanaweza kweli kukamilishwa na Mungu. Wale wasioelewa mapenzi ya Mungu ni wapinzani wa Mungu; wale wanaoelewa mapenzi ya Mungu lakini bado hawauweki ukweli katika vitendo ni wapinzani wa Mungu; wale wanaokula na kunywa maneno ya Mungu lakini bado wanaenda dhidi ya kiini cha maneno ya Mungu ni wapinzani wa Mungu; wale walio na dhana za Mungu mwenye mwili na wanaasi makusudi ni wapinzani wa Mungu; wale wanaomhukumu Mungu ni wapinzani wa Mungu; na yeyote asiyeweza kumjua Mungu na kumshuhudia ni mpinzani wa Mungu. Kwa hivyo sikiliza ushawishi Wangu: Kama kweli una imani ya kutembea njia hii, basi zidi kuifuata. Iwapo huwezi kuepuka upinzani kwa Mungu, basi ni bora kwenda zako kabla hujachelewa. Vinginevyo, inaashiria mabaya badala ya mazuri, kwani asili yenu ni potovu sana. Huna uaminifu ama utii hata kidogo, ama moyo ulio na kiu ya haki na ukweli. Na wala huna upendo hata kidogo kwa Mungu. Inaweza kusemwa kuwa hali yako mbele ya Mungu imesambaratika kabisa. Huwezi kushika unachopaswa wala kusema unachopaswa. Huwezi kuweka katika vitendo kile ambacho unapaswa, na huwezi kutekeleza kazi unayopaswa. Huna uaminifu, dhamiri, utii ama azimio unalopasa. Hujavumilia mateso unayopaswa kuwa umevumilia, na huna imani unayopaswa kuwa nayo. Huna sifa yoyote kabisa; una heshima binafsi ya kuendelea kuishi? Nakuhimiza kwamba ni bora kufunga macho kwa mapumziko ya milele, hivyo kumtoa Mungu katika kujishughulisha nawe na kuvumilia mateso kwa ajili yako. Unaamini katika Mungu lakini bado hujui mapenzi Yake; unakula na kunywa maneno ya Mungu lakini bado huwezi kukidhi mahitaji Yake. Unaamini katika Mungu lakini bado humjui, na kuishi ingawa huna lengo la kujaribu kufikia. Huna maadili na huna madhumuni. Unaishi kama mwanadamu lakini huna dhamiri, uadilifu wowote wala hata uaminifu kidogo. Unafikiriwaje kuwa wanadamu? Unaamini katika Mungu lakini unamdanganya. Zaidi ya hayo, unachukua pesa za Mungu na kula sadaka Yake, na bado, mwishowe, huonyeshi fikira kwa hisia za Mungu ama dhamiri kwa Mungu. Huwezi hata kukidhi mahitaji ya Mungu ya chini zaidi. Kwa hivyo unawezaje kufikiriwa kuwa mwanadamu? Chakula unachokula na hewa unayopumua vimetoka kwa Mungu, unafurahia neema Yake, na bado mwishowe, huna hata ufahamu mdogo wa Mungu. Kinyume na hayo, umekuwa mtu asiye na maana anayempinga Mungu. Si basi wewe ni mnyama asiye bora kuliko mbwa? Kuna mnyama yeyote aliye mkatili kukuliko wewe?

Hao wahubiri na wazee wanaosimama katika mimbari ya juu wakimfundisha mwanadamu ni wapinzani wa Mungu na wako katika muungano na Shetani; wale kati yenu wasiosimama katika mimbari ya juu wakimfundisha mwanadamu hawatakuwa hata wapinzani wakubwa zaidi wa Mungu? Juu ya hayo, huna ushirikiano basi na Shetani? Wale wasioelewa madhumuni ya kazi ya Mungu hawajui kuwa na makubaliano na moyo wa Mungu. Bila shaka, haiwezi kuwa ukweli kwa wale wanaoyaelewa madhumuni ya kazi Yake? Kazi ya Mungu kamwe haina makosa; badala yake, ni kufuatilia kwa mwanadamu kuliko na dosari. Wale waliosawijika wanaompinga Mungu makusudi sio waovu zaidi na mahasidi kuliko hao wahubiri na wazee? Wanaompinga Mungu ni wengi, na miongoni mwa wanadamu hao wengi, kuna aina mbalimbali ya upinzani dhidi ya Mungu. Kwa kuwa kuna kila aina ya waumini, hivyo pia kuna kila aina ya wale wanaompinga Mungu kila tofauti na mwingine. Hakuna mmoja kati ya wale wasiotambua wazi madhumuni ya kazi ya Mungu anayeweza kuokolewa. Bila kujali jinsi mwanadamu anaweza kuwa alimpinga Mungu zamani, mwanadamu ajapo kufahamu madhumuni ya kazi ya Mungu na kujitolea juhudi zake ili kumridhisha Mungu, dhambi zake za awali zitafutiliwa mbali na Mungu. Bora tu mwanadamu anatafuta ukweli na kuuweka ukweli katika vitendo, Mungu hataweka akilini kile ambacho amefanya. Badala yake, ni kwa msingi wa kutenda ukweli kwa mwandamu ndiyo Mungu anamtetea mwanadamu. Hii ndiyo haki ya Mungu. Kabla ya mwanadamu kumwona Mungu ama kuwa na uzoefu wa kazi Yake, bila kujali jinsi mwanadamu anamtendea Mungu, Haliweki hili akilini. Hata hivyo, mara tu mwanadamu amwonapo Mungu, na kuwa na uzoefu wa kazi Yake, matendo yote na vitendo vyote vya mwanadamu vinaandikwa chini ndani ya “rekodi” na Mungu, kwani mwanadamu amemwona Mungu na kuishi ndani ya kazi Yake.

Wakati mwanadamu ameona kwa kweli kile Mungu alicho nacho na kile Alicho, aonapo ukuu Wake, na kweli amekuja kujua kazi ya Mungu, na zaidi ya hayo, tabia ya awali ya mwanadamu inabadilika, basi mwanadamu atakuwa ameitupilia mbali kabisa tabia yake ya uasi inayompinga Mungu. Inaweza kusemwa kwamba kila mwanadamu amempinga Mungu wakati mmoja na kila mwanadamu ameasi dhidi ya Mungu. Hata hivyo, kama una akili ya kummtii Mungu mwenye mwili, na kwa hivyo kuuridhisha moyo wa Mungu kwa uaminifu wako, unaweka katika vitendo ukweli unaopaswa, kutekeleza jukumu lako unavyopaswa, na kufuata kanuni unazopaswa, basi wewe ni mtu aliye tayari kutupilia mbali uasi wake kumridhisha Mungu na mtu anayeweza kukamilishwa na Mungu. Iwapo utakataa kutambua makosa yako na huna moyo wa kutubu; ukiendelea katika njia zako za uasi na huna kabisa moyo wa kufanya kazi na Mungu na kumridhisha Mungu, basi mjinga mkaidi kama wewe kwa hakika ataadhibiwa na hatawahi kuwa mmoja wa kukamilishwa na Mungu. Iwapo hivyo, wewe ni adui wa Mungu leo na kesho, na hivyo pia utabaki adui wa Mungu siku ifuatayo; utakuwa milele mpinzani wa Mungu na adui wa Mungu. Mungu atakuachaje? Ni asili ya mwanadamu kumpinga Mungu, lakini mwanadamu hawezi kwa makusudi kutafuta “siri” za kumpinga Mungu kwa sababu kubadili asili yake ni kazi isiyoshindika. Kama hali ni hiyo, basi ni bora uende zako kabla hujachelewa, isiwe kuadibu kwako wakati ujao kukawa kali zaidi, na isiwe asili yako kama ya mnyama ikaibuka na kuwa isiyotawalika mpaka mwili wako unaondolewa na Mungu mwishowe. Unaamini katika Mungu ili ubarikiwe; ikiwa mwishowe, balaa tu ndiyo itakayokupata, hiyo haitakuwa na thamani. Nawahimiza kuunda mpango mwingine; zoezi jingine litakuwa bora kuliko imani yenu kwa Mungu. Hakika kuna mengi kuliko njia hii moja? Hamngeweza kuendelea kuishi vile vile bila kutafuta ukweli? Mbona kuishi katika ukinzani na Mungu kwa namna hii?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Watu Wote Wasiomjua Mungu Ni Watu Wanaompinga Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 295)

Nimefanya kazi kubwa miongoni mwa binadamu, na maneno ambayo Nimeeleza wakati huu yamekuwa mengi. Maneno haya ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, na yalikuwa yanaeleza ili binadamu aweze kulingana na Mimi. Ilhali Nimewapokea watu wachache tu duniani ambao wanalingana na Mimi, na hivyo Nimesema kwamba binadamu hathamini maneno Yangu, kwa kuwa binadamu halingani na Mimi. Kwa njia hii, kazi ambayo Naifanya sio tu kwa ajili ya mwanadamu aweze kuniabudu; muhimu zaidi, ni kwa ajili ya mwanadamu aweze kulingana na Mimi. Watu, ambao wamepotoshwa, wote huishi katika mtego wa Shetani, wao kuishi katika mwili, kuishi katika tamaa za ubinafsi, na hakuna hata mmoja kati yao anayelingana na Mimi. Kuna wale ambao wanasema kwamba wao wanalingana na Mimi, lakini ambao wote huabudu sanamu zisizo yakini. Ingawa wanakubali jina Langu kama takatifu, wao hutembea kwenye njia ambazo huenda kinyume na Yangu, na maneno yao yamejaa kiburi na kujiamini, kwa sababu, katika mizizi, wote wananipinga na hawalingani Nami. Kila siku wao hutafuta dalili Yangu katika Biblia, na kupata vifungu “vinavyofaa” hapa na pale wanavyovisoma bila kukoma, na ambavyo wao hukariri kama maandiko. Hawajui jinsi ya kulingana na Mimi, hawajui maana ya kuwa katika uadui na Mimi, na wanasoma tu maandiko kwa upofu. Wao huzuia ndani ya Biblia na Mungu asiye yakini ambaye hawajawahi kumwona, na hawana uwezo wa kumwona, na wao huitoa tu na kuiangazia wakati wao wa ziada. Wao wanaamini kuwepo Kwangu tu ndani ya eneo la Biblia. Kwa fikira zao, Mimi ni sawa na Biblia; bila Biblia Mimi sipo, na bila Mimi hakuna Biblia. Wao hawatilii maanani kuwepo Kwangu au matendo, lakini badala yake hujishughulisha na umakini mno na maalum kwa kila neno la Maandiko, na wengi wao hata huamini kwamba Mimi sipaswi kufanya jambo lolote Nipendalo kufanya ila tu kama lilitabiriwa na Maandiko. Wao hutia umuhimu mwingi sana kwa Maandiko. Inaweza kusemwa kwamba wao huona maneno na maonyesho yakiwa muhimu mno, kwa kiasi kwamba wao hutumia mistari ya Biblia kupima kila neno Ninalolisema, na kunilaani Mimi. Wanalotafuta si njia ya uwiano na Mimi, au njia ya uwiano na ukweli, lakini njia ya uwiano na maneno ya Biblia, na wanaamini kwamba chochote ambacho hakiambatani na Biblia, bila ubaguzi, si kazi Yangu. Je, si watu wa namna hiyo ni wazawa watiifu wa Mafarisayo? Mafarisayo Wayahudi walitumia sheria ya Musa kumhukumu Yesu. Hawakutafuta uwiano na Yesu wa wakati huo, bali waliifuata sheria kwa makini, kwa kiasi kwamba wao hatimaye walimpiga misumari Yesu asiye na hatia juu ya msalaba, baada ya kumshitaki Yeye kwa kukosa kufuata sheria za Agano la Kale na kutokuwa Masihi. Kiini chao kilikuwa ni nini? Haikuwa kwamba hawakutafuta njia ya uwiano na ukweli? Walitamani na kutilia maanani mawazo yao na kila neno la Maandiko, bila kuyajali mapenzi Yangu na hatua na mbinu za kazi Yangu. Hawakuwa watu waliotafuta ukweli, ila walikuwa watu walioshikilia maneno kwa ugumu; hawakuwa watu walioamini katika Mungu, bali walikuwa watu walioamini katika Biblia. Kimsingi, walikuwa walinzi wa Biblia. Ili kulinda maslahi ya Biblia, na kuzingatia hadhi ya Biblia, na kulinda sifa za Biblia, wao walitenda kiasi kwamba walimsulubisha Yesu mwenye huruma msalabani. Haya walifanya tu kwa ajili ya kuitetea Biblia, na kwa ajili ya kudumisha hali ya kila neno la Biblia katika mioyo ya watu. Hivyo waliona ni heri kuyaacha maisha yao ya baadaye na sadaka ya dhambi kwa sababu ya kumhukumu Yesu, ambaye hakuwa Anazingatia kanuni za Maandiko, mpaka kifo. Je hawakuwa watumishi kwa kila mojawapo ya maneno ya Maandiko?

Na je watu leo? Kristo amekuja kutoa ukweli, lakini wanaona ni afadhali wao kumfukuza Yeye kutoka kati ya wanadamu ili wapate kuingia mbinguni na kupokea neema. Wanaona ni afadhali kabisa kukataa kuja kwa ukweli, ili kulinda maslahi ya Biblia, na ni afadhali kumtundika Kristo ambaye Alirudi kwa mwili kwa misumari msalabani tena ili kuhakikisha kuwepo kwa Biblia milele. Jinsi gani mwanadamu anaweza kupokea wokovu Wangu, wakati moyo wake una nia mbaya namna hiyo, na asili yake inanipinga Mimi? Mimi huishi miongoni mwa wanadamu, ilhali bado wanadamu hawajui kuhusu kuwepo Kwangu. Ninapoangaza mwanga Wangu juu ya wanadamu, bado yeye hana ufahamu kuhusu kuwepo Kwangu. Wakati Ninatoa ghadhabu Yangu juu ya wanadamu, wao hukanusha kuwepo Kwangu kwa nguvu kubwa zaidi. Binadamu hutafuta uwiano na maneno, na Biblia, ilhali bado hakuna mwanadamu hata mmoja huja Kwangu kutafuta njia ya uwiano na ukweli. Binadamu huniheshimu sana Nikiwa mbinguni, na kujishughulisha hasa na kuwepo Kwangu mbinguni, ilhali hakuna anayenijali Nikiwa katika mwili, kwa maana Mimi Ninayeishi miongoni mwa wanadamu sina umuhimu kwao hata kidogo. Wale ambao hutafuta tu uwiano na maneno ya Biblia, na ambao hutafuta tu uwiano na Mungu asiye yakini, mbele Yangu ni fidhuli. Hiyo ni kwa sababu wanachokiabudu ni maneno yaliyokufa, na Mungu Aliye na uwezo wa kuwapa hazina isiyoambilika. Wanachoabudu ni Mungu anayedhibitiwa na mtu, na ambaye hayuko. Ni nini, basi, ambacho watu wa namna hiyo wanaweza kupokea kutoka Kwangu? Mwanadamu ni kiumbe duni sana kiasi kwamba maneno hayawezi kueleza hali yake. Wale wanaonipinga, wanaofanya madai yasiyo na kipimo dhidi Yangu, wasio na upendo kwa ukweli, wanaoniasi—wangewezaje kulingana na Mimi?

Wale wanaonipinga ni wale ambao hawalingani na Mimi. Vile vile wale wasiopenda ukweli, na wale wanaoniasi ndio walio wapinzani Wangu zaidi na hawalingani na Mimi. Wale wote ambao hawalingani na Mimi Nawawasilisha mikononi mwa yule mwovu. Ninawaacha wao kwa upotovu wa yule mwovu, Nawaachilia huru ili wafichue maovu yao, na hatimaye kuwakabidhi kwa yule mwovu ili waliwe. Mimi Sijali ni watu wangapi wananiabudu, ambayo ni kusema, Sijali ni watu wangapi wanaamini ndani Yangu. Kinachonijalisha ni watu wangapi wanalingana na Mimi. Hiyo ni kwa sababu wote wasiolingana na Mimi ni wale waovu wanaonisaliti; wao ni adui Zangu, Nami “Sitawatunza” adui Zangu katika nyumba Yangu. Wale ambao wanalingana na Mimi watanitumikia milele katika nyumba Yangu, na wale wanaojiweka katika uadui na Mimi watateseka milele katika adhabu Yangu. Wale wanaojali tu kuhusu maneno ya Biblia, wasiojali kuhusu ukweli au kutafuta nyayo Zangu—wao wananipinga, kwa kuwa wao wananizuilia Mimi kulingana na Biblia, na kuniwekea vizuizi ndani ya na Biblia, na hivyo ni wa kukufuru pakubwa dhidi Yangu. Jinsi gani watu wa aina hii wanaweza kuja mbele Zangu? Wao hawatilii maanani matendo Yangu, au mapenzi Yangu, au ukweli, badala yake wanashikilia maneno, maneno yanayoua. Jinsi gani watu kama hao wanaweza kulingana na Mimi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 296)

Baada ya ukweli wa Yesu aliyepata mwili kutokea, mwanadamu aliamini hili: Si Baba pekee aliye mbinguni, bali pia Mwana, na hata Roho Mtakatifu. Hii ndiyo dhana ya kawaida aliyonayo mwanadamu, kwamba kuna Mungu wa aina hii mbinguni: Utatu ambao ni Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, wote katika nafsi moja. Wanadamu wote wana fikra hizi: Mungu ni Mungu mmoja, ila Anajumuisha sehemu tatu, kile ambacho wale wote waliofungwa kwa huzuni katika hizi dhana za kawaida wanachukulia kuwa kuna Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Ni sehemu hizo tatu pekee ambazo zimefanywa moja ambazo ni Mungu kamili. Bila Baba Mtakatifu, Mungu asingekuwa mkamilifu. Vivyo hivyo, wala Mungu asingekuwa mkamilifu bila Mwana au Roho Mtakatifu. Katika mawazo yao, wanaamini kuwa Baba au Mwana pekee hawezi kuwa Mungu. Ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu tu kwa pamoja wanaoweza kuwa Mungu Mwenyewe. Sasa, waumini wote wa kidini, na hata kila mfuasi miongoni mwenu, anashikilia hii imani. Ilhali, ikiwa hii imani ni sahihi, hakuna anayeweza kuelezea, kwani daima mmechanganyikiwa kuhusu masuala ya Mungu Mwenyewe. Japo hizi ni fikra tu, hamjui kama ni sawa au mbaya, kwani mmeathiriwa vibaya na mawazo ya kidini. Mmeyakubali kwa kina haya mawazo ya kidini yaliyozoeleka, na hii sumu imezama kwa kina ndani yenu. Hivyo basi, hata kwa hili mmeanguka katika huu ushawishi wenye madhara, kwani Utatu haupo. Yaani, Utatu wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu haupo. Hizi zote ni fikra za kawaida za mwanadamu, na imani za uongo za mwanadamu. Kwa karne nyingi, mwanadamu ameamini katika huu Utatu, ambao umebuniwa na mawazo katika akili za mwanadamu, ukatengenezwa na mwanadamu, na ambao haujawahi kuonekana na mwanadamu. Kwa miaka mingi, kumekuwa na watu maarufu wa kiroho ambao wameeleza “maana ya kweli” ya Utatu, ila maelezo hayo ya Utatu kama nafsi tatu dhahiri yamekuwa si yakini na hayapo wazi na watu wote wamepumbazwa na “ujenzi” wa Mungu. Hakuna mtu maarufu yeyote aliyewahi kutoa maelezo kamili; maelezo mengi yanafaa katika masuala ya mjadala na katika maandishi, ila hakuna hata mtu mmoja ambaye ana ufahamu kamili na wa wazi kuhusu maana ya Utatu. Hii ni kwa sababu huu Utatu huu mkuu ambao mwanadamu anashikilia moyoni kwa hakika haupo. Kwani hakuna aliyewahi kuiona sura ya Mungu au kubahatika kumtembelea katika makao Yake ili kuchunguza ni vitu gani vipo mahali ambapo Mungu anakaa, kubainisha wazi ni makumi mangapi ya maelfu, au mamia ya mamilioni ya vizazi yako katika “nyumba ya Mungu” au hata kuchunguza ni sehemu ngapi zimeuunga mwili wa asili wa Mungu Kinachofaa hasa kuchunguzwa ni: enzi ya Baba na Mwana, na vilevile Roho Mtakatifu; umbo la kila mmoja; hasa ni vipi Wanajitenganisha, na ni vipi Wanafanywa kuwa kitu kimoja. Kwa bahati mbaya, katika miaka hii yote, hakuna hata mtu mmoja ambaye ameweza kugundua ukweli wa haya mambo. Wote wanabuni tu, kwani hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kwenda mbinguni kwa matembezi na kurejea na “ripoti ya uchunguzi” kwa wanadamu wote ili kuripoti kuhusu ukweli wa mambo kwa wale waumini wote wa kidini wenye bidii na wacha Mungu wanaojishughulisha sana na Utatu Mtakatifu. Bila shaka, mwanadamu hawezi kulaumiwa kwa kubuni na fikra hizo, maana kwa nini Yehova Baba hakuambatana na Yesu Mwana alipomuumba mwanadamu? Ingekuwa hapo mwanzoni kuwa wote waliitwa Yehova, ingekuwa bora zaidi. Ikiwa kuna wa kulaumiwa, wacha lawama iwe kwa kuteleza kwa muda kwa Yehova Mungu, ambaye hakuwaita Mwana na Roho Mtakatifu mbele Zake wakati wa uumbaji, ila badala yake Akafanya kazi Yake peke Yake. Ikiwa Wote Wangefanya kazi wakati mmoja, basi wasingekuwa kitu kimoja? Ikiwa, tangu mwanzo kabisa hadi mwisho, kungekuwa na jina moja tu Yehova pasipo jina la Yesu tangu Enzi ya Neema, au ikiwa Angeitwa bado Yehova, je, Mungu asingeepushiwa na wanadamu taabu ya huu utengano? Kwa hakika, Yehova hawezi kulaumiwa kwa ajili ya haya yote; kama ni lawama, hebu na iwekwe kwa Roho Mtakatifu, ambaye kwa maelfu ya miaka Aliendelea na kazi yake kwa jina la Yehova, la Yesu, na hata la Roho Mtakatifu, Akiwachanganya na kuwakanganya wanadamu kiasi kwamba wanadamu wakashindwa kufahamu Mungu ni nani hasa. Iwapo Roho Mtakatifu angefanya kazi bila umbo au sura, aidha, bila jina kama vile Yesu, na mwanadamu asingemgusa wala kumuona, ila kusikia tu ngurumo za radi, basi si kazi hiyo ingekuwa ya manufaa zaidi kwa mwanadamu? Hivyo nini kinaweza kufanywa sasa? Fikra za mwanadamu zimerundikana juu kama mlima na kuenea kama bahari, kiasi kwamba Mungu wa sasa hawezi kuzistahimili kamwe na hajui la kufanya. Hapo nyuma wakati kulikuwa tu na Yehova, Yesu, na Roho Mtakatifu katikati ya hao wawili, mwanadamu tayari alikuwa amechanganyikiwa na jinsi ya kuvumilia, na sasa kuna ongezeko la mwenye Uweza, ambaye hata anasemekana kuwa sehemu ya Mungu. Ni nani anajua Yeye ni nani na Ameingiliana au kujificha kwa nani katika Utatu Mtakatifu kwa miaka mingapi? Mwanadamu anawezaje kulistahimili hili? Utatu Mtakatifu pekee ulitosha kumchukua mwanadamu milele kuueleza, lakini sasa kuna “Mungu mmoja katika nafsi nne.” Hili linaweza kuelezewa vipi? Unaweza kulieleza? Ndugu! Mmeaminije katika Mungu huyu mpaka leo? Ninawavulia kofia. Utatu uliweza kuvumilika; mliwezaje kuendelea kuwa na imani isiyotikisika namna hiyo katika huyu Mungu mmoja katika nafsi nne? Mmehimizwa muondoke na bado mnakataa. Ajabu iliyoje! Nyinyi ni watu wa ajabu! Mtu kweli anaweza kuendelea kuamini Mungu wanne na asiwaelewe; hamuoni kuwa huu ni muujiza? Sikujua kwamba mlikuwa na uwezo wa kutenda muujiza mkubwa kiasi hiki! Hebu Niwaambie hilo, kwa hakika, Mungu wa Utatu hayupo popote katika dunia hii. Mungu hana Baba wala Mwana, na sembuse Baba na Mwana hutumia kwa pamoja Roho Mtakatifu kama chombo. Huu wote ni uongo mkubwa zaidi na haupo kabisa katika dunia hii! Hata hivyo uongo huu una asili yake na haukosi msingi kabisa, kwani akili zenu si punguani, na mawazo yenu hayakosi mantiki. Badala yake, ziko sawa na yenye ubunifu kwa kiasi kikubwa, kwamba haziwezi kuzuiwa hata na Shetani yeyote. La kusikitisha ni kwamba mawazo haya ni uongo mtupu na hayapo kabisa! Hamjaona ukweli halisi haswa; mnabuni na kujiundia dhana, na kuzitengeneza kuwa hadithi ili kuteka imani ya wengine kwa uongo na kupata mamlaka miongoni mwa wanadamu wapumbavu wasio na busara, ili kwamba waamini katika “mafundisho yenu ya kitaaluma” makuu na mashuhuri. Je, huu ni ukweli? Je, hii ndiyo njia ya uzima ambayo wanadamu wanafaa kupokea? Huu ni upuuzi! Hakuna hata neno moja linafaa! Katika miaka hii yote, nyinyi mmegawanya Mungu namna hii, na kuendelea kugawanywa zaidi katika kila kizazi kiasi kwamba Mungu mmoja amegawanywa kuwa Mungu watatu. Na sasa haiwezekani kabisa kwa mwanadamu kumuunganisha Mungu kuwa mmoja kwani mmemgawanya zaidi. Ingekuwa si kazi yangu ya upesiupesi kabla ya muda kuyoyoma, haijulikani mngeishi hivi kwa muda gani! Kuendelea kumgawanya Mungu namna hii, Anawezaje kuendelea kuwa Mungu wenu? Je, bado mngeendelea kumtambua Mungu? Je, bado mngemkiri Yeye kama baba yenu na mumrudie? Ningechelewa hata kidogo, inaonekana kwamba mngewarudisha “Baba na Mwana,” Yehova na Yesu kwenda Israeli na mdai kwamba nyinyi wenyewe ni sehemu ya Mungu. Kwa bahati nzuri, sasa ni siku za mwisho. Hatimaye, siku Niliyoitarajia kwa hamu imewadia, na ni baada tu ya kuifanya hatua hii ya kazi kwa mikono Yangu ndipo kumgawanya kwenu Mungu Mwenyewe kumesitishwa. Isingekuwa hivi, mngezidisha, hadi kuwaweka Mashetani wote miongoni mwenu kwenye meza zenu kwa ajili ya ibada. Hii ndiyo njama yenu! Mbinu yenu ya kumgawanya Mungu! Je, mtaendelea kufanya hivyo sasa? Hebu Niwaulize: Kuna Mungu Wangapi? Ni Mungu Yupi atawaletea wokovu? Je, ni Mungu wa kwanza, wa pili au wa tatu mnayemwomba? Ni nani kati Yao mnayemwamini? Je, ni Baba? Au ni Mwana? Au ni Roho? Niambie ni nani unayemwamini. Ijapokuwa kwa kila neno unasema unamwamini Mungu, mnachokiamini hasa ni akili zenu! Hamna Mungu mioyoni mwenu kabisa! Na bado akilini mwenu mna “Utatu Mtakatifu” kadhaa. Hamkubaliani na hili?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 297)

Ikiwa hatua tatu za kazi zitakadiriwa kulingana na dhana hii ya Utatu, basi ni lazima kuwe na Mungu watatu kwani kazi iliyofanywa na kila mmoja si sawa. Ikiwa yeyote miongoni mwenu anasema kwamba hakika Utatu upo, basi eleza huyu Mungu mmoja katika nafsi tatu ni nini hasa. Baba Mtakatifu ni nini? Mwana ni nini? Roho Mtakatifu ni nini? Je, Yehova ni Baba Mtakatifu? Je, Yesu ni Mwana? Basi, Roho Mtakatifu je? Je, Baba si Roho? Je, kiini cha Mwana vilevile si Roho? Je, kazi ya Yesu haikuwa ya Roho Mtakatifu? Je, kazi ya Yehova haikufanywa wakati ule na Roho sawa tu na kazi ya Yesu? Mungu Anaweza kuwa na Roho wangapi? Kulingana na maelezo yako hizi nafsi tatu, yaani, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni mmoja; kama ni hivyo, kuna Roho watatu lakini kuwa na Roho watatu kunamaanisha kuwa kuna Mungu Watatu. Hii inamaanisha kuwa hakuna Mungu Mmoja wa kweli; Mungu wa aina hii anawezaje kuwa kiini asili cha Mungu? Kama unakubali kuwa kuna Mungu mmoja tu, basi Anawezaje kuwa na Mwana na awe Baba? Je, hizi si fikra zako mwenyewe? Kuna Mungu Mmoja tu, nafsi moja katika Mungu huyu, na Roho mmoja tu wa Mungu sawa tu na ilivyoandikwa katika Biblia kwamba “Kuna tu Roho Mtakatifu mmoja na Mungu mmoja tu.” Haijalishi kama Baba na Mwana unaowazungumzia wapo, kuna Mungu mmoja tu, na kiini cha Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu mnaowaamini ni kiini cha Roho Mtakatifu. Kwa maneno mengine, Mungu ni Roho, ila Ana uwezo wa kupata Mwili na kuishi miongoni mwa wanadamu na vilevile kuwa juu ya vitu vyote. Roho Wake anajumuisha kila kitu na Anapatikana kila mahala. Anaweza kuwa katika mwili na wakati huo huo awe ndani na juu ya ulimwengu. Kwa kuwa watu wanasema kwamba Mungu ndiye tu Mungu wa kweli, basi kuna Mungu mmoja, ambaye hawezi kugawanywa kwa mapenzi ya awaye yote! Mungu ni Roho mmoja tu, na nafsi moja; na huyo ni Roho wa Mungu. Ikiwa ni kama usemavyo, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, basi Hawa si watatu? Roho Mtakatifu ni kitu kimoja, Mwana ni kingine, na Baba vilevile ni kingine. Nafsi Zao ni tofauti na viini Vyao ni tofauti, iweje basi ziwe kila moja Yao ni sehemu ya Mungu mmoja? Roho Mtakatifu ni Roho; hili ni rahisi kueleweka kwa wanadamu. Ikiwa ni hivyo basi, Baba ni Roho zaidi. Hajawahi kushuka kuja duniani na Hajawahi kupata mwili; Yeye ni Yehova Mungu katika mioyo ya mwanadamu, na kwa hakika Yeye vilevile ni Roho. Basi kuna uhusiano gani kati Yake na Roho Mtakatifu? Je, ni uhusiano kati ya Baba na Mwana? Au ni uhusiano kati ya Roho Mtakatifu na Roho wa Mungu? Je, kiini cha kila Roho ni sawa? Au Roho Mtakatifu ni chombo cha Baba? Hili linaweza kuelezwaje? Aidha kuna uhusiano gani kati ya Mwana na Roho Mtakatifu? Je, ni uhusiano kati ya Roho wawili au ni uhusiano kati ya mwanadamu na Roho? Haya yote ni masuala ambayo hayawezi kuelezewa! Ikiwa Wote ni Roho mmoja, basi hapawezi kuwepo na mjadala kuhusu nafsi tatu, kwani zote zinamilikiwa na Roho mmoja. Kama Zingekuwa nafsi tofauti, basi Roho Zao Zingetofautiana katika nguvu zao na kamwe hawangekuwa Roho mmoja. Hii dhana ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni upuuzi mtupu! Hili linamweka Mungu katika vitengo na kumgawanya kuwa nafsi tatu, kila moja ikiwa na hadhi na Roho; basi Atawezaje kuwa Roho mmoja na Mungu mmoja? Hebu niambie, je, mbingu na dunia na vyote vilivyomo viliumbwa na Baba, Mwana, au na Roho Mtakatifu? Wengine husema Waliviumba kwa pamoja. Basi ni nani alimkomboa mwanadamu? Alikuwa Roho Mtakatifu, Mwana, au Baba? Wengine husema ni Mwana aliyewakomboa wanadamu. Basi Mwana ni nani katika kiini? Siye kupata mwili kwa Roho wa Mungu? Mungu aliyepata mwili anamwita Mungu aliye Mbinguni Baba katika mtazamo wa mwanadamu aliyeumbwa. Je, hufahamu kuwa Yesu alizaliwa kutokana na utungaji mimba kupitia Roho Mtakatifu. Ndani yake mna Roho Mtakatifu; lolote usemalo, Yeye bado ni mmoja na Mungu wa Mbinguni, kwani Yeye ni kupata mwili kwa Roho wa Mungu. Hili wazo la Mwana si kweli Kabisa. Ni Roho mmoja anayefanya Kazi yote; Mungu Mwenyewe pekee, yaani, Roho wa Mungu anafanya kazi Yake. Roho wa Mungu ni nani? Je, si Roho Mtakatifu? Je, si Roho Mtakatifu anayefanya kazi ndani ya Yesu? Ingekuwa kazi haikufanywa na Roho Mtakatifu (yaani Roho wa Mungu), je, kazi Yake ingemwakilisha Mungu Mwenyewe? Yesu alipomwita Mungu wa mbinguni kwa jina la Baba alipokuwa akiomba, hili lilifanywa katika mitazamo ya mwanadamu aliyeumbwa, kwa sababu Roho wa Mungu alikuwa amevaa mwili wa kawaida na Alikuwa na umbile la nje la mwanadamu aliyeumbwa. Hata ikiwa ndani yake mlikuwa na Roho wa Mungu, umbo Lake la nje bado lilikuwa lile la mtu wa kawaida; kwa maana nyingine, Alikuwa “Mwana wa Adamu” jambo ambalo watu wote, akiwemo Yesu Mwenyewe, walilizungumzia. Na kwa sababu Anaitwa Mwana wa Adamu, Yeye ni mtu (Mwanamke au mwanamume, kwa vyovyote vile mwenye umbo la nje la mwanadamu) aliyezaliwa katika familia ya kawaida ya watu wa kawaida. Kwa hivyo, Yesu kumwita Mungu wa mbinguni kwa jina la Baba kulikuwa sawa na mlivyomwita mara ya kwanza Baba; Alifanya hivyo kutokana na mtazamo wa Mwanadamu aliyeumbwa. Je, mnakumbuka Sala ya Bwana ambayo Yesu aliwafundisha kukariri? “Baba Yetu Uliye mbinguni….” Aliwaambia wanadamu wote wamwite Mungu wa Mbinguni kwa jina la Baba. Na kwa kuwa Naye pia alimwita Baba, alifanya hivyo kutoka kwa mtazamo wa mtu aliye katika daraja moja nanyi nyote. Kwa kuwa mlimuita Mungu wa mbinguni Baba, hili linaonyesha kuwa Yesu alijichukulia kuwa katika daraja sawa nanyi, kama mwanadamu duniani aliyeteuliwa na Mungu (yaani, Mwana wa Mungu). Kama mnamwita Mungu “Baba,” je, hii si kwa sababu nyinyi ni wanadamu walioumbwa? Haijalishi Yesu alikuwa na mamlaka makubwa kiasi gani duniani, kabla ya kusulubiwa, Alikuwa tu Mwana wa Adamu, akiongozwa na Roho Mtakatifu (yaani, Mungu), Akiwa miongoni mwa viumbe wa duniani, kwani bado Alikuwa hajaikamilisha kazi Yake. Kwa hivyo, kumwita kwake Mungu wa mbinguni Baba kulikuwa tu unyenyekevu na utiifu Wake. Yeye kumwita Mungu (yaani, Roho aliye mbinguni) kwa namna ile, hata hivyo, hakudhibitishi kuwa Yeye ni Mwana wa Roho wa Mungu aliye mbinguni. Badala yake, ni kuwa mtazamo wake ni tofauti, si kwamba ni nafsi tofauti. Uwepo wa nafsi tofauti ni uongo. Kabla ya kusulubiwa kwake, Yesu alikuwa Mwana wa Adamu aliyefungwa katika udhaifu wa kimwili, na Hakuwa na mamlaka kamilifu ya Roho. Hiyo ndiyo maana Angeweza tu kutafuta mapenzi ya Mungu Baba kutoka katika mtazamo wa kiumbe. Ni kama tu Alivyoomba mara tatu huko Gethsemane: “Si kama Nitakavyo, bali kama Utakavyo.” Kabla Atundikwe msalabani, Hakuwa zaidi ya Mfalme wa Wayahudi; alikuwa Kristo, Mwana wa Adamu, na wala si mwenye utukufu. Hiyo ndiyo maana, kutokana na mtazamo wa mwanadamu, Alimwita Mungu Baba. Sasa, huwezi kusema kuwa wote wamwitao Mungu Baba ni Wana. Ingekuwa kweli, basi wote si mngekuwa Mwana punde Yesu alipowafundisha Sala ya Bwana? Ikiwa bado hamjaridhika, basi niambieni hili, ni nani mmwitaye Baba? Ikiwa mnamrejelea Yesu, je, Baba ya Yesu ni nani kwenu? Baada ya Yesu kurudi mbinguni, hii dhana ya Baba na Mwana ilikoma. Hii dhana ilifaa tu kipindi ambacho Yesu alikuwa mwili; katika mazingira mengine yoyote, uhusiano ni ule wa kati ya Bwana wa uumbaji na kiumbe mnapomwita Mungu Baba. Hakuna wakati ambapo wazo hili la Utatu wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu linaweza kuwa na mashiko; ni uongo ambao ni nadra kuonekana na halipo!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 298)

Hili laweza kuwakumbusha watu maneno ya Mungu kutoka katika kitabu cha Mwanzo: “Na tumuumbe mwanadamu katika sura yetu, kwa mfanano wetu.” Ikichukuliwa kuwa Mungu anasema “na tumtengeneze” mtu kwa mfano “wetu,” basi “tu-” inaashiria wawili au wengi; na kwa kuwa anataja “tu-” basi hakuna tu Mungu mmoja. Kwa njia hii, mwanadamu alianza kufikiria udhahania wa nafsi bayana, na kutokana na maneno haya kulitokea dhana ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Basi, Baba anafananaje? Je, Mwana anafananaje? Na Roho Mtakatifu anafananaje? Yawezekana kuwa mwanadamu wa leo aliumbwa kwa mfano wa mtu mmoja aliyeunganishwa pamoja kutoka kwa nafsi tatu? Je, sura ya mwanadamu inafanana na ile ya Baba, Mwana, au Roho Mtakatifu? Mwanadamu ni mfano wa nani katika nafsi za Mungu? Mawazo ya mwanadamu ni ya kimakosa na upuuzi! Yanaweza tu Kumgawanya Mungu kuwa Mungu kadhaa. Wakati Musa aliandika kitabu cha Mwanzo, ni baada ya wanadamu kuumbwa baada ya uumbaji wa dunia. Mwanzo kabisa, dunia ilipoanza, Musa hakuwepo. Ni hadi baadaye kabisa ndipo Musa aliandika Biblia, basi angejuaje alichokinena Mungu kutoka mbinguni? Hakuwa na ufahamu wowote jinsi Mungu alivyoumba ulimwengu. Katika Agano la Kale la Biblia, hapakutajwa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, ni Mungu mmoja tu wa kweli, Yehova, akiifanya kazi yake nchini Israeli. Anaitwa majina tofauti kadri enzi zinavyobadilika, ila hili haliwezi kuthibitisha kuwa kila jina linarejelea mtu tofauti. Ingekuwa hivi, basi je, si kungekuwa na nafsi nyingi sana katika Mungu? Kilichoandikwa katika Agano la Kale ni kazi ya Yehova, hatua ya kazi ya Mungu Mwenyewe tangu mwanzo wa Enzi ya Sheria. Ilikuwa ni kazi ya Mungu, ambapo Alinena, ilikuwa, na Alipoamuru, ilitendeka. Hakuna hata wakati mmoja ambapo Yehova alisema kuwa alikuwa Baba aliyekuja kufanya kazi, wala Hakutabiri kuja kwa Mwana kuwakomboa wanadamu. Wakati wa Yesu ulipowadia, ilisemekana tu kwamba Mungu alikuwa Ameupata mwili kuwakomboa wanadamu, si kwamba ni Mwana aliyekuwa amekuja. Kwa sababu enzi hazifanani na kazi ambayo Mungu Mwenyewe hufanya vilevile inatofautiana, Anapaswa kufanya kazi Yake katika milki tofauti, kwa njia hii utambulisho Alionao vilevile unatofautiana. Mwanadamu anaamini kwamba Yehova ndiye Baba ya Yesu, ila hili halijakiriwa na Yesu ambaye alisema: “Hatukubainishwa kamwe kama Baba na Mwana; Mimi na Baba aliye Mbinguni ni kitu kimoja. Baba yu ndani Yangu Nami ni ndani Yake; wanadamu wanapomwona Mwana, wanamwona Baba.” Baada ya yote kusemwa, iwe Baba au Mwana, Wao ni Roho mmoja, Hawajagawanywa kuwa nafsi tofautitofauti. Mara tu wanadamu wanapojaribu kueleza, mambo hutatizwa na wazo la nafsi tofauti, na vilevile na uhusiano kati ya Baba, Mwana na Roho. Mwanadamu akizungumzia nafsi tofauti, je, hili halimfanyi Mungu kuwa kitu? Mwanadamu hata zaidi huziorodhesha nafsi hizi kama nafsi ya kwanza, ya pili, na ya tatu; haya yote ni mawazo ya mwanadamu yasiyofaa kurejelewa, hayana uhalisi kabisa! Ukimwuliza: “Kuna Mungu wangapi?” atasema kuwa Mungu ni Utatu Mtakatifu wa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu: Yule mmoja wa kweli. Ukiuliza tena: “Baba ni nani?” atasema: “Baba ni Roho wa Mungu aliye mbinguni; anatawala kila kitu, na kiongozi wa mbinguni.” “Je, Yehova ni Roho?” Atasema: “Ndiyo!” Ukimuuliza tena, “Mwana ni nani?” atasema kuwa Yesu ndiye Mwana, bila shaka. “Basi kisa cha Yesu ni kipi? Alitoka wapi?” Atasema: “Yesu alizaliwa na Maria kupitia kwa utungaji mimba wa Roho Mtakatifu.” “Je, kiini Chake si Roho vilevile? Je, kazi Yake si kiwakilishi cha Roho Mtakatifu? Yehova ni Roho, vivyo hivyo na kiini cha Yesu. Sasa katika siku za mwisho, bila shaka ni Roho Anayeendelea kufanya Kazi; Wangewezaje kuwa nafsi tofauti? Je, si Roho wa Mungu anafanya kazi ya Roho kutoka katika mitazamo tofauti?” Kwa hivyo, hakuna tofauti bayana kati ya nafsi. Yesu alipatikana kwa utungaji mimba wa Roho Mtakatifu, na bila shaka, Kazi Yake hasa ilikuwa ile ya Roho Mtakatifu. Katika hatua ya kwanza ya kazi iliyofanywa na Yehova, Hakuwa mwili au kuonekana kwa mwanadamu. Kwa hivyo mwanadamu hakuona uso Wake. Haijalishi Alikuwa mashuhuri au mrefu kiasi gani, bado Alikuwa Roho, Mungu Mwenyewe aliyemuumba mwanadamu mwanzoni. Yaani, alikuwa Roho wa Mungu. Aliponena na wanadamu kutoka mawinguni, alikuwa Roho tu. Hakuna hata mmoja aliyeuona Uso wake; ni katika Enzi ya Neema tu ambapo Roho wa Mungu alikuwa mwili na Alipata mwili kule Uyahudi ndipo mwanadamu aliona sura ya kupata mwili kama Myahudi. Hisia ya Yehova haingeweza kuhisika. Hata hivyo, Alipatikana kwa utungaji mimba wa Roho Mtakatifu, yaani, Alipatikana kwa utungaji mimba wa Roho wa Yehova Mwenyewe, na Yesu bado alizaliwa kama mfano halisi wa Roho wa Mungu. Alichokiona mwanadamu mwanzoni kilikuwa ni Roho Mtakatifu Akimshukia Yesu kama njiwa; Hakuwa Roho mwenye upekee kwa Yesu tu, badala yake alikuwa Roho Mtakatifu. Basi roho wa Yesu anaweza kutenganishwa na Roho Mtakatifu? Ikiwa Yesu ni Yesu, Mwana, na Roho Mtakatifu ni Roho Mtakatifu, basi wangewezaje kuwa kitu kimoja? Ingekuwa hivyo kazi isingefanywa. Roho ndani ya Yesu, Roho aliye mbinguni, na Roho wa Yehova wote ni mmoja. Anaweza kuitwa Roho Mtakatifu, Roho wa Mungu, Roho aliyezidishwa mara saba, na Roho mwenye vyote. Roho wa Mungu anaweza kufanya kazi nyingi. Ana uwezo wa kuumba na kuiangamiza dunia kwa kuleta mafuriko duniani; Anaweza kuwakomboa wanadamu, aidha, kuwashinda na kuwaangamiza wanadamu wote. Kazi hii yote inafanywa na Mungu Mwenyewe na haiwezi kufanywa na yeyote katika nafsi za Mungu kwa niaba Yake. Roho Wake anaweza kuitwa Yehova na Yesu, na vilevile mwenye Uweza. Yeye ni Bwana na Kristo. Anaweza pia kuwa Mwana wa Adamu. Yuko mbinguni na vilevile duniani; Yuko juu ya dunia na pia miongoni mwa umati. Yeye tu ndiye Bwana wa Mbingu na dunia! Tangu wakati wa uumbaji hadi sasa, kazi hii imekuwa ikifanywa na Roho wa Mungu Mwenyewe. Iwe ni kazi mbinguni au katika mwili, yote hufanywa na Roho Wake Mwenyewe. Viumbe wote, wawe mbinguni au duniani, wamo katika kiganja cha mkono Wake wenye nguvu; yote hii ni kazi ya Mungu na haiwezi kufanywa na yeyote kwa niaba Yake. Mbinguni Yeye ni Roho na vilevile Mungu Mwenyewe; miongoni mwa wanadamu, Yeye ni mwili ila anaendelea kuwa Mungu Mwenyewe. Japo Anaweza kuitwa mamia ya maelfu ya majina, Yeye bado ni Mungu Mwenyewe, na kazi yote ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho Wake. Ukombozi wa wanadamu wote kupitia kwa kusulubiwa Kwake ilikuwa kazi ya moja kwa moja ya Roho Wake, na vilevile tangazo kwa mataifa yote na nchi zote wakati wa siku za mwisho. Wakati wote Mungu anaweza kuitwa mwenye uweza na Mungu mmoja wa kweli, Mungu Mwenyewe mwenye vyote. Nafsi bayana hazipo, aidha dhana ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu haipo. Kuna Mungu mmoja mbinguni na duniani!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 299)

Mpango wa usimamizi wa Mungu umeenea katika miaka elfu sita na umegawanyika katika enzi tatu kutegemea tofauti katika kazi Yake: Enzi ya kwanza ni Enzi ya Sheria ya Agano la Kale; ya pili ni Enzi ya Neema; na ya tatu ni ile ya siku za mwisho—Enzi ya Ufalme. Katika kila enzi utambulisho tofauti huwasilishwa. Hili linafanywa kwa sababu ya utofauti wa kazi, yaani, mahitaji ya kazi. Hatua ya kwanza ya kazi wakati wa Enzi ya Sheria ilifanyiwa nchini Israeli, na hatua ya pili ya kuhitimisha kazi ya ukombozi ilifanyiwa Uyahudi. Kwa kazi ya ukombozi, Yesu alizaliwa kutokana na utungaji mimba wa Roho Mtakatifu na kama Mwana wa pekee. Haya yote yalitokana na mahitaji ya kazi. Katika siku za mwisho, Mungu anadhamiria kupanua kazi Yake katika watu wa Mataifa, na kuwashinda watu wa huko, ili kwamba jina lake liweze kuwa maarufu miongoni mwao. Anadhamiria kumwongoza mwanadamu katika kuelewa na kuingia katika ukweli wote. Kazi hii yote inafanywa na Roho mmoja. Ijapokuwa Anaweza kufanya hivyo kutoka mitazamo tofautitofauti, asili na kanuni za kazi zinabaki zile zile. Mara tu ukizifuata kanuni na asili ya kazi Waliyoifanya, basi utagundua kuwa yote ilikuwa kazi ya Roho mmoja. Hata hivyo, wengine wanaweza kusema: “Baba ni Baba; Mwana ni Mwana; Roho Mtakatifu ni Roho Mtakatifu, na mwishowe, Watafanywa kitu kimoja.” Je, Utawafanyaje kitu kimoja? Baba na Roho Mtakatifu Wawezaje kufanywa kitu kimoja? Ikiwa Walikuwa wawili kiasili, haijalishi Wamewekwa pamoja kwa namna gani, je, Hawataendelea kuwa sehemu mbili? Unaposema kuwa kuwafanya kuwa kitu kimoja, huko si kuunganisha sehemu mbili kutengeneza kitu kamili? Je, Hawakuwa sehemu mbili kabla ya kufanywa kitu kizima? Kila Roho ana kiini kinachotofautiana, na Roho wawili Hawawezi kufanywa kuwa kitu kimoja. Roho si chombo cha kutengenezwa, si kama chombo chochote katika ulimwengu. Kulingana na mitazamo ya wanadamu, Baba ni Roho mmoja, Mwana ni mwingine, na Roho Mtakatifu tena ni mwingine, halafu Roho Hawa huchanganyika sawa na glasi tatu za maji kuunda kitu kimoja kizima. Je, hizo si sehemu tatu zimefanywa kuwa kitu kimoja? Haya bila shaka ni maelezo ya kimakosa! Je, huku si kumgawa Mungu? Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu wanawezaje kufanywa kuwa kitu kimoja? Je, Wao si sehemu tatu zenye asili tofauti? Aidha kuna wale wasemao, “je, si Mungu alitaja wazi kuwa Yesu ni Mwanawe mpendwa?” Yesu ni Mwana mpendwa wa Mungu, ambaye anapendezwa naye—haya bila shaka yalitamkwa na Mungu Mwenyewe. Huyu alikuwa Mungu akijitolea ushuhuda Mwenyewe, ila kutoka katika mtazamo tofauti, ule wa Roho aliye mbinguni akitolea ushuhuda kupata Mwili Kwake. Yesu ni kupata mwili Kwake, si Mwanake mbinguni. Je, unaelewa? Je, maneno ya Yesu, “Mimi ni ndani ya Baba naye Baba yu ndani yangu,” hayaonyeshi kuwa Wao ni Roho mmoja? Na si kwa sababu ya kupata mwili kulikosababisha kutenganishwa Kwao kati ya mbinguni na duniani? Uhalisi ni kwamba Wao ni kitu kimoja; hata iweje, ni Mungu anajitolea ushuhuda Mwenyewe. Kutokana na kubadilika kwa enzi, mahitaji ya kazi, na hatua mbalimbali za mpango Wake wa usimamizi, vilevile jina wamwitalo wanadamu hubadilika. Alipokuja kufanya hatua ya kwanza ya kazi, Angeweza kuitwa tu Yehova, mchungaji wa Waisraeli. Katika hatua ya pili, Mungu mwenye mwili Angeweza kuitwa tu Bwana, na Kristo. Lakini wakati huo, Roho aliye mbinguni alikariri tu kwamba Alikuwa Mwana mpendwa wa Mungu, bila kutaja kuwa Alikuwa Mwana wa pekee wa Mungu. Hili halikufanyika kabisa. Mungu angewezaje kuwa na Mwana wa pekee? Basi, Mungu asingekuwa mwanadamu? Kwa kuwa Alikuwa Mwili, Aliitwa Mwana mpendwa wa Mungu na kutokana na hili, kukazuka uhusiano wa Baba na Mwana. Ni kwa sababu tu ya utengano kati ya mbingu na dunia. Yesu aliomba kutokana na msimamo wa mwili. Kwa sababu Alikuwa Amepata mwili wa ubinadamu wa kawaida, ni kutokana na msimamo wa mwili ndipo Alisema: “Umbo Langu la nje ni la kiumbe. Kwa sababu Nilijivisha mwili kuja duniani, sasa Niko mbali, mbali sana na mbinguni.” Kwa sababu hii, Angeomba tu kwa Baba kutokana na msimamo wa mwili. Huu ulikuwa wajibu Wake, ambao ni sharti Roho wa Mungu aliyepata mwili anapaswa kupewa. Haiwezekani kusema kwamba Hawezi kuwa Mungu kwa sababu tu Anamwomba Baba kutokana na msimamo wa mwili. Ijapokuwa Anaitwa Mwana mpendwa wa Mungu, Yeye bado ni Mungu Mwenyewe, ni vile tu Yeye ni mwili wa Roho, na kiini chake bado ni Roho. Kama wanavyoona wanadamu, wanashangaa ni kwa nini Anaomba ikiwa yeye ni Mungu Mwenyewe. Hii ni kwa sababu Yeye ni Mungu mwenye mwili, Mungu aishiye mwilini, bali si Roho aliye mbinguni. Kama anavyoona mwanadamu, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu wote ni Mungu. Ni kwamba tu wote watatu wanafanywa kuwa kitu kimoja na kudhaniwa kuwa Mungu wa Kweli, na kwa njia hii, uwezo Wake unakuwa mkuu kupindukia. Kuna wanaosema kuwa ni kwa njia hii tu anakuwa Roho aliyezidishwa mara saba. Mwana alipoomba baada ya kuja Kwake, alimwomba Roho. Kwa hakika, alikuwa Akiomba kutokana na msimamo wa kiumbe. Kwa kuwa mwili si kamili, Hakuwa mkamilifu na pia Alikuwa na udhaifu mwingi Alipokuja katika mwili, na Alisumbuka sana Alipoifanya kazi Yake katika mwili. Hii ndiyo maana Alimwomba Mungu Baba mara tatu kabla ya kusulubiwa Kwake, na hata mara nyingi zaidi kabla ya hapo. Aliomba miongoni mwa wanafunzi Wake; Aliomba peke Yake juu mlimani; Aliomba Akiwa Ameabiri dau la uvuvi; Aliomba Akiwa katika umati; Aliomba akiwa anaumega mkate; na kuomba akiwa Anawabariki wengine. Kwa nini Alifanya hivyo? Ilikuwa ni Roho Aliyemwomba; Alikuwa Akimwomba Roho, Alimwomba Mungu aliye mbinguni; kutokana na msimamo wa mwili. Hivyo basi kutoka katika msimamo wa mwanadamu, Yesu alikuwa Mwana katika hatua ile ya kazi. Katika hatua hii hata hivyo, Haombi. Kwa nini? Hii ni kwa sababu Anachokileta ni kazi ya neno, na hukumu na kuadibu kutumia neno. Hana haja ya maombi na huduma Yake ni ya kunena. Hajawekwa msalabani, na hashitakiwi na wanadamu kwa wale walio madarakani. Anafanya tu kazi Yake na yote yanakuwa sawa. Wakati Yesu alipoomba, Alikuwa akimwomba Mungu Baba ili ufalme wa mbinguni ushuke, ili mapenzi ya Baba yatimizwe, na ili kazi ifike. Katika hatua hii, ufalme wa mbinguni umeshuka, basi, Ana haja ya kuendelea kuomba? Kazi Yake ni kuihitimisha enzi, na hakuna tena enzi mpya, basi, kuna haja ya kuombea hatua inayofuata? Ninasikitika hakuna haja!

Kuna ukinzani mwingi katika maelezo ya mwanadamu. Kweli, haya ni mawazo ya mwanadamu; bila uchunguzi zaidi, ambayo nyote mngeamini kuwa yako sahihi. Je, hamjui hii dhana ya Mungu kama Utatu Mtakatifu ni mawazo ya mwanadamu tu? Hakuna ufahamu wa mwanadamu ulio mzima na kamili. Mara zote kuna madoa, na mwanadamu ana mawazo mengi mno; hili linaonyesha kuwa kiumbe hawezi kuieleza kazi ya Mungu. Kuna mengi sana katika akili ya mwanadamu, yote yakitokana na mantiki na tafakari, ambayo hukinzana na ukweli. Je, mantiki yako yaweza kuichangua kazi ya Mungu? Je, waweza kupata utambuzi wa kazi yote ya Yehova? Je, ni wewe kama mwanadamu uwezaye kubaini yote, au ni Mungu Mwenyewe awezaye kuona kutoka milele hadi milele? Je, ni wewe mwanadamu uwezaye kuona tangu milele ya zamani sana hadi milele ijayo, au Mungu ndiye Ana uwezo wa kufanya hivyo? Unasema nini? Unafaa vipi kumweleza Mungu? Maelezo yako yametegemezwa katika misingi gani? Wewe ni Mungu? Mbingu na dunia, na vyote vilivyomo viliumbwa na Mungu Mwenyewe. Si wewe uliyelifanya hili, basi ni kwa nini unatoa maelezo yasiyo sahihi? Sasa, unaendelea kuamini katika utatu mtakatifu? Hufikirii kuwa huu ni mzigo mkubwa kwa njia hii? Itakuwa bora kwako kuamini katika Mungu mmoja, si watatu. Ni bora zaidi kuwa mwepesi, kwani mzigo wa Bwana ni mwepesi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?

Iliyotangulia: Siri Kuhusu Biblia

Inayofuata: Kufunua Upotovu wa Wanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp