Kupata Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 99)

Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili. Hivyo, ili Mungu kuwa mwili, ni lazima kwanza Apate umbo la mwili, mwili wenye ubinadamu wa kawaida; hili ndilo hitaji la kimsingi zaidi. Kwa kweli, maana ya kupata mwili kwa Mungu ni kwamba Mungu Anaishi na kufanya kazi katika mwili, Mungu katika kiini Chake Anakuwa mwili, Anakuwa mwanadamu. Maisha Yake ya kimwili na kazi vinaweza kugawanywa katika hatua mbili. Kwanza ni maisha Anayoishi kabla ya kuanza kutekeleza huduma Yake. Anaishi katika familia ya kawaida ya binadamu, katika ubinadamu wa kawaida kabisa, Akifuata maadili na sheria za maisha ya wanadamu, Akiwa na mahitaji ya kawaida ya binadamu (chakula, nguo, makazi, na usingizi), na udhaifu wa kawaida wa binadamu na hisia za kawaida za binadamu. Kwa maneno mengine, katika hatua hii ya kwanza Anaishi maisha yasiyo na uungu, ubinadamu wa kawaida kabisa, Akijishughulisha na shughuli zote za wanadamu. Hatua ya pili ni ya maisha Anayoishi baada ya kuanza kutekeleza huduma Yake. Bado Yumo katika ubinadamu wa kawaida Akiwa na umbo la nje la binadamu bila kuonyesha ishara isiyo ya kawaida kwa nje. Lakini kimsingi Anaishi kwa ajili ya huduma Yake, na wakati huu ubinadamu Wake wa kawaida upo kikamilifu kuhudumia kazi ya kawaida ya uungu Wake; kwani wakati huo, ubinadamu Wake wa kawaida umekomaa kiasi cha kuweza kutekeleza huduma Yake. Kwa hivyo hatua ya pili ya maisha Yake ni ya kutekeleza huduma Yake katika ubinadamu Wake wa kawaida, ni maisha ya ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Sababu ya kuishi katika maisha ya kawaida kabisa ya ubinadamu katika hatua ya kwanza ya maisha Yake ni kwamba ubinadamu Wake bado ulikuwa haujalingana na ukamilifu wa kazi ya uungu, bado haujakomaa; ni baada tu ya kukomaa kwa ubinadamu Wake na kuwa na uwezo wa kustahimili huduma Yake, ndipo Anaweza kuanza kutekeleza huduma Yake. Kwa kuwa Yeye, kama mwili, Anahitaji kukua na kukomaa, hatua ya kwanza ya maisha Yake ni ile ya ubinadamu wa kawaida, ilhali katika hatua ya pili, kwa kuwa ubinadamu Wake una uwezo wa kuanza kazi Yake na kutekeleza huduma Yake, maisha ambayo Mungu mwenye mwili Anaishi katika kipindi cha huduma Yake ni ya ubinadamu na ya uungu kamili. Iwapo Mungu mwenye mwili Angeanza huduma Yake kwa dhati tangu kuzaliwa kwake, na kufanya ishara na maajabu ya mwujiza, basi Asingekuwa na kiini cha kimwili. Kwa hivyo, ubinadamu Wake upo kwa sababu ya kiini chake cha Kimwili; hakuwezi kuwepo na mwili bila ubinadamu, na mtu bila ubinadamu si mwanadamu. Kwa njia hii, ubinadamu wa mwili wa Mungu ni sifa ya ndani ya mwili wa Mungu. Kusema kwamba “Mungu Anapokuwa mwili Anakuwa na uungu kamili, na si binadamu kabisa,” ni kufuru, kwa kuwa kauli hii haipo kabisa, na hukiuka kanuni ya Yesu kupata mwili. Hata baada ya kuanza kutekeleza huduma Yake, bado Anaishi katika uungu Wake akiwa na umbo la nje la binadamu Anapofanya kazi Yake; ni kwamba tu wakati huo, ubinadamu Wake una kusudi la pekee la kuuwezesha uungu Wake kutekeleza kazi katika mwili wa kawaida. Kwa hivyo wakala wa kazi ni uungu unaosetiriwa katika ubinadamu Wake. Ni uungu na wala si ubinadamu Wake unaofanya kazi, lakini ni uungu uliojificha katika ubinadamu Wake; kimsingi kazi Yake inafanywa na uungu Wake kikamilifu, haifanywi na ubinadamu Wake. Ila mtekelezaji wa kazi ni mwili Wake. Mtu anaweza kusema kuwa Yeye ni mwanadamu na vilevile Mungu, kwani Mungu Anakuwa Mungu Anayeishi katika mwili, mwenye umbo la mwanadamu na kiini cha binadamu lakini pia na kiini cha Mungu. Kwa sababu ni mwanadamu mwenye kiini cha Mungu, Yuko juu ya wanadamu wote walioumbwa, juu ya mwanadamu yeyote anayeweza kutekeleza kazi ya Mungu. Kwa hivyo, miongoni mwa wale wote walio na umbo la binadamu kama Lake, miongoni mwa wale wote walio na ubinadamu, Yeye pekee ndiye Mungu mwenye mwili Mwenyewe—wengine wote ni wanadamu walioumbwa. Japokuwa wote wana ubinadamu, wanadamu walioumbwa hawana chochote ila ubinadamu, ilhali Mungu mwenye mwili ni tofauti: katika mwili Wake, si tu kwamba ana ubinadamu ila pia muhimu zaidi Ana uungu. Ubinadamu Wake waweza kuonekana katika mwonekano wa nje wa Mwili Wake na katika maisha Yake ya kila siku; ila uungu Wake ni vigumu kuonekana. Kwa kuwa uungu Wake huonyeshwa pale tu Anapokuwa na ubinadamu, na si wa kimuujiza kama watu wanavyoukisia kuwa, ni vigumu sana kwa watu kuuona. Hata leo hii ni vigumu sana kwa watu kuelewa kiini cha kweli cha Mungu mwenye mwili. Kwa kweli, hata baada ya Mimi kulizungumzia kwa mapana, Natarajia bado liwe fumbo kwa wengi wenu. Suala hili ni rahisi sana: kwa kuwa Mungu Anakuwa mwili, kiini Chake ni muungano wa ubinadamu na uungu. Muungano huu unaitwa Mungu Mwenyewe, Mungu Mwenyewe duniani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 100)

Maisha Aliyoishi Yesu duniani yalikuwa maisha ya kimwili ya kawaida. Aliishi katika ubinadamu wa kawaida wa mwili Wake. Mamlaka Yake—kufanya kazi Yake na kuzungumza neno Lake, au kuwaponya wagonjwa au kufukuza mapepo, kufanya hiyo kazi isiyo ya kawaida—hayakujitokeza, kwa kiasi kikubwa, hadi Alipoanza huduma Yake. Maisha Yake kabla ya umri wa miaka ishirini na tisa, kabla ya Yeye kuanza kutekeleza huduma Yake, yalikuwa uthibitisho tosha kuwa Alikuwa mwili wa kawaida. Kwa sababu ya hili, na kwa kuwa Alikuwa bado Hajaanza kutekeleza huduma Yake, watu hawakuona chochote cha uungu ndani Yake, hawakuona chochote zaidi ya ubinadamu wa kawaida, mwanadamu wa kawaida—kama vile wakati ule baadhi ya watu walimwamini kuwa mwana wa Yosefu. Watu walidhani kuwa Alikuwa mwana wa mwanadamu wa kawaida, hawakuwa na njia ya kugundua kuwa Alikuwa mwili wa Mungu; hata wakati Alipotenda miujiza mingi katika harakati za kutekeleza huduma Yake, watu wengi bado walisema Alikuwa mwana wa Yosefu, kwani Alikuwa Kristo mwenye umbo la nje la ubinadamu wa kawaida. Ubinadamu Wake wa kawaida pamoja na kazi yake vyote vilikuwepo ili kutimiza umuhimu wa kupata mwili kwa mara ya kwanza, kuthibitisha kuwa Mungu Alikuwa Amekuja katika mwili kwa ukamilifu, kuwa mwanadamu wa kawaida kabisa. Kuwa na ubinadamu wa kawaida kabla ya kuanza kazi Yake ulikuwa uthibitisho kuwa Alikuwa mwili wa kawaida; na kwa kuwa Alifanya kazi baadaye lilithibitisha pia kuwa Alikuwa mwili wa kawaida, kwa kuwa Alifanya ishara na miujiza, kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo katika mwili na ubinadamu wa kawaida. Sababu za kufanya miujiza ilikuwa kwamba mwili Wake ulikuwa umebeba mamlaka ya Mungu, ulikuwa mwili ambamo Roho wa Mungu Alikuwa Amesetiriwa. Alikuwa na mamlaka haya kwa sababu ya Roho wa Mungu, na haikumaanishi kuwa Hakuwa Mwili. Kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo ilikuwa kazi Aliyopaswa kutekeleza katika huduma Yake, onyesho la uungu Wake uliojificha ndani ya ubinadamu Wake, na haijalishi ni ishara za aina gani Alionyesha au Alidhihirisha vipi mamlaka Yake, bado Aliishi katika ubinadamu wa kawaida na bado Alikuwa mwili wa kawaida. Aliishi katika mwili wa kawaida mpaka wakati Alipofufuliwa baada ya kufa msalabani. Aliishi katika mwili wa kawaida. Akitoa neema, Akiwaponya wagonjwa, na kufukuza mapepo hayo yote yalikuwa sehemu ya huduma Yake, hiyo yote ilikuwa kazi Aliyotekeleza katika mwili Wake wa kawaida. Kabla ya kwenda msalabani, Hakuuacha mwili Wake wa kawaida, haijalishi Alikuwa Anafanya nini. Alikuwa Mungu Mwenyewe, Akifanya kazi ya Mungu, lakini kwa sababu Alikuwa Mwili wa Mungu, Alikula chakula na kuvaa nguo, Alikuwa na mahitaji ya kawaida ya binadamu, Alikuwa na fikira za kawaida za binadamu na akili za kawaida. Haya yote yalikuwa uthibitisho kwamba Alikuwa mwanadamu wa kawaida, ambayo yalithibitisha kuwa mwili wa Mungu ulikuwa mwili wenye ubinadamu wa kawaida, haukuwa wa rohoni. Kazi Yake ilikuwa kukamilisha kazi ya Mungu kupata mwili mara ya kwanza, kutimiza huduma ya kupata mwili mara ya kwanza. Umuhimu wa kupata mwili ni kwamba mtu wa kawaida Anatekeleza kazi ya Mungu Mwenyewe; yaani, kwamba Mungu Anatekeleza kazi Yake ya uungu katika ubinadamu na hivyo kumshinda Shetani. Kupata mwili kunamaanisha kwamba Roho wa Mungu Anakuwa Mwili, yaani, Mungu Anakuwa mwili; kazi Anayoifanya katika mwili ni kazi ya Roho, inayothibitika katika mwili, na kuonyeshwa kwa mwili. Hakuna mwingine ila tu mwili wa Mungu Anayeweza kutimiza huduma ya Mungu mwenye mwili; yaani, mwili wa Mungu kuwa mwili pekee, ubinadamu huu wa kawaida—na hakuna mwingine yeyote—anayeweza kuonyesha kazi ya uungu. Ikiwa, wakati wa kuja Kwake wa kwanza, Mungu Asingekuwa Amekuwa na ubinadamu wa kawaida kabla ya umri wa miaka ishirini na tisa—ikiwa mara tu Alipozaliwa Angeweza kufanya miujiza, ikiwa mara tu Alipojifunza kuongea Angeweza kuongea lugha ya mbinguni, ikiwa mara tu Alipokanyaga duniani Angeweza kuyaelewa mambo yote ya kidunia, kung’amua fikira za kila mtu na nia zao—mtu kama huyu asingeitwa mwanadamu wa kawaida, na mwili Wake usingeitwa mwili wa mwanadamu. Iwapo ingekuwa hivi kwa Kristo, basi maana na kiini cha kuwa mwili kwa Mungu ingepotea. Kuwa Yeye ana ubinadamu wa kawaida kunathibitisha kuwa Yeye ni Mungu Aliyejidhihirisha katika mwili; ukweli kwamba Anapitia ukuaji wa kawaida wa binadamu unaonyesha zaidi kuwa Yeye ni mwili wa kawaida; zaidi, kazi Yake ni uthibitisho tosha kuwa Yeye ni Neno la Mungu, Roho wa Mungu, kuwa mwili. Mungu Anakuwa mwili kwa sababu ya mahitaji ya kazi; kwa maneno mengine, hii hatua ya kazi inapaswa kufanywa kwa mwili, kufanywa katika ubinadamu wa kawaida. Hili ndilo sharti la “Neno kuwa mwili,” la “Neno kuonekana katika mwili,” na ndio ukweli wa Mungu kupata mwili mara Mbili. Watu huenda wakaamini kuwa maisha yote ya Yesu yaliambatana na miujiza, kwamba hadi mwisho wa kazi Yake duniani Hakudhihirisha ubinadamu wa kawaida, kwamba Hakuwa na mahitaji ya kawaida ya mwanadamu au udhaifu au hisia za binadamu, kwamba Hakuhitaji vitu vya kimsingi vya maisha au kuwa na fikira za kawaida za binadamu. Wanadhani tu kuwa Alikuwa mwanadamu asiyekuwa na akili ya kawaida, aliyevuka mipaka ya ubinadamu. Wanaamini kuwa kwa sababu Yeye ni Mungu, Hapaswi kufikiri na kuishi jinsi wanadamu wa kawaida hufanya, kwamba ni mtu wa kawaida tu, mwanadamu halisi, anayeweza kufikiri fikira za mwanadamu wa kawaida na kuishi maisha ya mwanadamu wa kawaida. Haya yote ni mawazo ya wanadamu na maoni ya wanadamu, ambayo yanakinzana na madhumuni asilia ya kazi ya Mungu. Kufikiri kwa mwanadamu wa kawaida kunadumisha mawazo ya kawaida ya mwanadamu na ubinadamu wa kawaida; ubinadamu wa kawaida unadumisha kazi za kawaida za mwili; na kazi za kawaida za mwili zinawezesha maisha ya kawaida ya mwili katika ukamilifu wake. Ni kwa kufanya kazi tu katika mwili kama huo ndipo Mungu Anaweza kutimiza kusudi la kupata mwili Kwake. Kama Mungu mwenye mwili angekuwa na umbo la nje tu la mwili, bila kufikiri fikira za kawaida za binadamu, basi mwili huu usingekuwa na mawazo ya binadamu, sembuse ubinadamu halisi. Ni vipi ambavyo mwili kama huu, usio na ubinadamu, ungeweza kutimiza huduma ambayo Mungu mwenye mwili Anapaswa kutekeleza? Akili za kawaida huwezesha vipengele vyote vya maisha ya binadamu; bila akili ya kawaida, mtu hawezi kuwa mwanadamu. Kwa maneno mengine, mtu asiyefikiria fikra za kawaida ni mgonjwa wa akili. Na Kristo ambaye Hana ubinadamu ila uungu pekee Hawezi kuitwa mwili wa Mungu. Basi, mwili wa Mungu unawezaje kukosa ubinadamu wa kawaida? Je, si kufuru kusema kwamba Kristo hana ubinadamu? Kila shughuli ambazo wanadamu wa kawaida hufanya hutegemea utendaji kazi wa akili ya kawaida ya mwanadamu. Bila hiyo, wanadamu wangekuwa na mienendo iliyopotoka; wangeshindwa hata kutofautisha kati ya nyeupe na nyeusi, wema na uovu; na hawangekuwa na maadili ya binadamu na kanuni za uadilifu. Vivyo hivyo, iwapo Mungu mwenye mwili Asingefikiri kama mwanadamu wa kawaida, basi Asingekuwa mwili halisi, mwili wa kawaida. Mwili usiofikiri kama huo haungeweza kuikabili kazi ya uungu. Haungeweza kushiriki kwa kawaida katika shughuli za za mwili wa kawaida, sembuse kuishi na wanadamu duniani. Hivyo basi, umuhimu wa Mungu kupata mwili, kiini kabisa cha Mungu kuja duniani, kingepotea. Ubinadamu wa Mungu kuwa mwili huwepo kudumisha kazi ya kawaida ya uungu katika mwili; fikira Zake za kawaida za binadamu zinadumisha ubinadamu Wake wa kawaida na shughuli Zake zote za kimwili. Mtu anaweza kusema kuwa fikira zake za kawaida za binadamu zipo ili kudumisha kazi yote ya Mungu katika mwili. Kama mwili huu usingekuwa na akili ya mwanadamu wa kawaida, basi Mungu Asingefanya kazi katika mwili, na Anachopaswa kufanya kimwili kisingetimilika. Japo Mungu mwenye mwili Ana akili ya mwanadamu wa kawaida, kazi Yake haijatiwa doa na mawazo ya binadamu; Anafanya kazi katika ubinadamu na akili ya kawaida chini ya masharti ya awali kuwa atakuwa na ubinadamu na akili ya kawaida, na si na mawazo ya kawaida ya binadamu. Haijalishi mawazo ya mwili Wake ni bora kiasi gani, kazi Yake haionyeshi alama ya mantiki au kufikiria. Kwa maneno mengine, kazi Yake haiwazwi na akili ya mwili Wake, ila ni onyesho la moja kwa moja la kazi ya uungu katika ubinadamu Wake. Kazi Yake yote ni huduma Anayostahili kutimiza, na haiwazwi hata chembe kwa akili Zake. Kwa mfano, kuponya wagonjwa, kufukuza mapepo na kusulubishwa hayakuwa mazao ya akili Zake za binadamu, yasingeweza kutimizwa na mwanadamu yeyote mwenye akili za binadamu. Vivyo hivyo, kazi ya ushindi ya leo ni huduma ambayo ni sharti itekelezwe na Mungu mwenye mwili, lakini si kazi ya mapenzi ya mwanadamu, ni kazi ambayo uungu Wake unapaswa kufanya, kazi ambayo hakuna mwanadamu wa mwili anaiweza. Kwa hivyo, Mungu mwenye mwili ni lazima Awe na akili za binadamu, ni lazima Awe na ubinadamu wa kawaida, kwa sababu ni lazima Atekeleze kazi Yake katika ubinadamu akiwa na akili za kawaida. Hiki ndicho kiini cha kazi ya Mungu mwenye Mwili, kiini chenyewe cha Mungu mwenye mwili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 101)

Kabla Yesu Hajatekeleza kazi yake, Aliishi tu katika ubinadamu Wake wa kawaida. Hakuna mtu ambaye angeweza kutambua kuwa Alikuwa Mungu, hakuna aliyegundua kuwa Alikuwa Mungu mwenye mwili; watu walimjua tu kama mwanadamu wa kawaida kabisa. Ubinadamu Wake wa kawaida ulikuwa uthibitisho kuwa Mungu Alipata mwili, na kwamba Enzi ya Neema ilikuwa enzi ya kazi ya Mungu mwenye mwili, si enzi ya kazi ya Roho. Ilikuwa uthibitisho kuwa Roho wa Mungu Alipatikana kikamilifu katika mwili, kwamba katika enzi ya kupata mwili kwa Mungu mwili Wake ungetekeleza kazi yote ya Roho. Kristo mwenye ubinadamu wa kawaida ni mwili ambao kwao Roho Hupatikana, Akiwa na ubinadamu wa kawaida, ufahamu wa kawaida, na fikira za wanadamu. “Kupatikana” kunamaanisha Mungu kuwa mwanadamu, Roho kuwa mwili; kuiweka wazi, ni wakati ambapo Mungu Mwenyewe Anaishi katika mwili wenye ubinadamu wa kawaida, na kupitia kwenye huo mwili, Anaonyesha kazi yake ya uungu—hii ndiyo maana ya kupatikana, au kupata mwili. Wakati wa kupata mwili Kwake mara ya kwanza, ilikuwa muhimu kwa Mungu kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo kwa sababu kazi Yake ilikuwa ni kukomboa. Ili kulikomboa kabila lote la mwanadamu, Alipaswa kuwa mwenye upendo na mwenye kusamehe. Kazi Aliyoifanya kabla ya kusulubiwa ilikuwa kuponya watu na kufukuza mapepo, ambayo iliashiria wokovu Wake wa mwanadamu kutoka katika dhambi na uchafu. Kwa sababu ilikuwa ni Enzi ya Neema, ilikuwa muhimu Kwake kuponya wagonjwa, na kwa njia hiyo Alionyesha ishara na miujiza, mambo ambayo yalikuwa kiwakilishi cha neema katika hiyo enzi; kwani Enzi ya Neema ilikitwa katika kutolewa kwa neema, ikiashiriwa na amani, furaha, na baraka ya vitu, vyote vikiwa zawadi za imani ya watu kwa Yesu. Hii ni kusema kuwa, kuponya wagonjwa, kufukuza mapepo na kutoa neema ulikuwa uwezo asilia wa mwili wa Yesu katika Enzi ya Neema, mambo haya yalikuwa ni kazi ya Roho iliyopatikana katika mwili. Lakini Alipokuwa Akitekeleza kazi kama hiyo, Alikuwa Akiishi katika mwili, Hakuenda nje ya mipaka ya mwili. Haijalishi ni matendo gani ya uponyaji Aliyotekeleza, bado Alikuwa na ubinadamu wa kawaida, bado Aliishi maisha ya kawaida ya binadamu. Sababu inayonifanya Niseme kuwa katika enzi ya kupata mwili kwa Mungu mwili ulitekeleza kazi yote ya Roho, ni kuwa haijalishi ni kazi gani Aliyoifanya, Aliifanya katika mwili. Lakini kwa sababu ya kazi Yake, watu hawakuchulia mwili Wake kuwa ulikuwa na kiini cha kimwili, kwani huu mwili ungefanya maajabu, na baadhi ya nyakati maalum ungefanya mambo ambayo yalivuka uwezo wa kimwili. Kwa hakika, haya matukio yote yalitokea Alipoanza huduma Yake, kama vile Yeye kujaribiwa kwa siku arobaini au kubadilishwa kule mlimani. Hivyo kwa Yesu, maana ya kupata mwili kwa Mungu haikukamilishwa, ila tu sehemu yake ilitimizwa. Maisha Aliyoishi katika mwili kabla ya kuanza kazi Yake yalikuwa ya kawaida tu katika hali zote. Alipoanza kazi Alidumisha umbo la nje la mwili Wake tu. Kwa sababu kazi Yake ilikuwa onyesho la uungu Wake, ilipita kazi ya kawaida ya mwili. Hata hivyo, Mwili wa Mungu ulikuwa tofauti na wanadamu wenye nyama na damu. Kwa hakika, katika maisha Yake ya kila siku, Alihitaji chakula, nguo, usingizi, na makao kama mtu yeyote yule, Alikuwa na mahitaji ya lazima ya kawaida, Alifikiri na kuwaza kama mwanadamu wa kawaida. Bado watu walimchukulia kuwa mwanadamu wa kawaida, isipokuwa tu kwamba kazi Aliyoifanya ilikuwa ya kupita akili. Kwa hakika, haijalishi Alifanya nini, Aliishi katika ubinadamu wa kawaida, na hata Alipotekeleza kazi, fikira zake zilikuwa za kawaida, mawazo yake yalikuwa ya wazi, hata zaidi ya wanadamu wa kawaida. Ilikuwa muhimu kwa Mungu mwenye mwili kufikiri kwa njia hii, kwani kazi ya uungu ilipaswa ionyeshwe na mwili ambao fikira zake zilikuwa za kawaida sana na mawazo yake wazi kabisa—ni kwa njia hii tu ndiyo mwili Wake ungeweza kuonyesha kazi ya uungu. Wakati wote wa miaka yote thelathini na tatu na nusu ambayo Yesu Aliishi duniani, Alidumisha ubinadamu Wake wa Kawaida, ila kwa sababu ya kazi Yake katika huduma Yake ya miaka mitatu na nusu, watu walidhani kuwa Alikuwa Amepita mipaka ya ubinadamu, kwamba Alikuwa wa rohoni zaidi kuliko hapo awali. Kwa kweli, ubinadamu wa kawaida wa Yesu haukubadilika kabla na baada ya Yeye kuanza huduma Yake; ubinadamu Wake ulikuwa sawa wakati wote, lakini kwa sababu ya tofauti kabla na baada ya Yeye kuanza huduma Yake, mitazamo miwili ilijitokeza kuhusiana na mwili Wake. Haijalishi watu walifikiria nini, Mungu mwenye mwili Alidumisha ubinadamu Wake asilia wa kawaida kipindi chote, kwani kwa sababu Mungu Alikuwa mwili, Aliishi katika mwili, mwili uliokuwa na ubinadamu wa kawaida. Hata ikiwa Alikuwa Anatekeleza huduma Yake au la, ubinadamu Wake wa kawaida usingeweza kufutika, kwani ubinadamu ndio kiini cha msingi cha mwili. Kabla Yesu hajaanza kutekeleza huduma Yake, mwili Wake ulibaki wa kawaida kabisa, ukishiriki katika shughuli zote za binadamu; Hakuonekana hata kidogo kuwa wa rohoni, Hakuonyesha ishara zozote za kimiujiza. Wakati ule Alikuwa tu mwanadamu wa kawaida sana Aliyemwabudu Mungu, japo dhamira Yake ilikuwa adilifu sana, ya kweli zaidi kuliko ya mtu yeyote. Hivi ndivyo ubinadamu Wake wa kawaida ulijionyesha wenyewe. Kwa kuwa Hakufanya kazi kabisa kabla ya kuianza huduma Yake, hakuna aliyemtambua, hakuna aliyegundua kuwa mwili Wake ulikuwa tofauti kabisa na miili ya watu wengine, kwa kuwa Hakutenda muujiza hata mmoja, Hakutenda hata chembe ya Kazi ya Mungu. Hata hivyo, baada ya kuanza kutekeleza kazi Yake, Alidumisha umbo la nje la ubinadamu wa kawaida na kuendelea kuishi katika mawazo ya kawaida ya binadamu, lakini kwa kuwa Alikuwa Ameanza kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe, kuanzisha huduma ya Kristo na kufanya kazi ambayo wanadamu hai, wanadamu wenye nyama na damu, wasingeweza kufanya, basi watu walidhani kuwa Hakuwa na ubinadamu wa kawaida na Hakuwa mwili wa kawaida kikamilifu ila mwili usio kamili. Kwa sababu ya yale Aliyotekeleza, watu walisema kuwa Alikuwa Mungu katika mwili Ambaye Hakuwa na ubinadamu wa kawaida. Huu ulikuwa ufahamu wa kimakosa, kwani watu hawakuelewa maana ya Mungu kupata mwili. Huu ufahamu mbaya ulitokana na ukweli kuwa kazi iliyoonyeshwa na Mungu katika mwili ilikuwa kazi ya uungu, iliyoonyeshwa kupitia kwa mwili wenye ubinadamu wa kawaida. Mungu Alikuwa Amevishwa katika mwili, Alikaa ndani ya mwili, na kazi Yake katika ubinadamu Wake iliuziba ukawaida wa ubinadamu Wake. Kwa sababu hii, watu walidhani kuwa Mungu hakuwa na ubinadamu bali uungu tu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 102)

Mungu katika kupata mwili Kwake mara ya kwanza Hakukamilisha kazi ya kupata mwili; Alikamilisha tu hatua ya kwanza ya kazi iliyokuwa lazima kwa Mungu kuifanya katika mwili. Kwa hivyo, ili kuimaliza kazi ya kupata mwili, Mungu Amerudi katika mwili kwa mara nyingine tena, Akiishi kulingana na ukawaida na uhalisia wote wa mwili, yaani, kuifanya kazi ya Mungu ijitokeze katika mwili wa kawaida kabisa, na kwa njia hiyo Anahitimisha kazi Aliyoiacha bila kukamilisha katika mwili. Mwili wa pili uliopatikana kimsingi ni sawa na ule wa kwanza, lakini ni halisi zaidi, wa kawaida kabisa kuliko ule wa kwanza. Kwa sababu hiyo, mateso unayoyapitia mwili wa pili uliopatikana ni makubwa kuliko yale ya ule wa kwanza, ila mateso haya ni kwa sababu ya huduma Yake katika mwili, ambayo ni tofauti na mateso ya mwanadamu mwovu. Vilevile yanachipuka kutokana na ukawaida na uhalisi wa mwili Wake. Kwa kuwa Anatekeleza huduma Yake katika mwili wa kawaida na halisi kabisa, mwili ni sharti upitie mateso mazito. Kadiri mwili ulivyo wa kawaida na halisi, ndivyo unateseka zaidi katika utekelezaji wa huduma Yake. Kazi ya Mungu inaonyeshwa katika mwili wa kawaida sana, mwili ambao si wa rohoni kamwe. Kwa kuwa mwili Wake ni wa kawaida, na ni lazima ubebe kazi ya kumwokoa mwanadamu, Anateseka hata zaidi kuliko ambavyo mwili wa rohoni unaweza kuteseka—mateso haya yote yanatokana na uhalisi na ukawaida wa mwili Wake. Kutokana na mateso yaliyopitiwa na hii miili miwili iliyopatikana wakati wa kutekeleza huduma Zao, mtu anaweza kuona kiini cha mwili uliopatikana. Kadiri mwili ulivyo wa kawaida, ndivyo Anapata mateso mazito Afanyapo kazi, kadri mwili unaofanya kazi unavyokuwa wa kweli, ndivyo maoni ya watu yanaendelea kuwa makali, na hatari zinazomkabili zinaendelea kuongezeka. Lakini, kadiri mwili ulivyo halisi, kadiri mwili unavyokuwa na hali kamili ya binadamu wa kawaida, ndivyo Anaweza zaidi kuifanya kazi ya Mungu katika mwili. Ulikuwa mwili wa Yesu ulioangikwa msalabani, mwili Wake Alioutoa kama kafara kwa dhambi; ni kupitia kwa mwili wenye ubinadamu wa kawaida ndipo Aliweza kumshinda Shetani na kumkomboa kabisa mwanadamu kutoka msalabani. Ni kupitia mwili kamili ndipo Mungu katika mwili mara ya pili Anatekeleza kazi ya ushindi na kumshinda Shetani. Ni mwili tu wa kawaida na halisi kabisa unaoweza kutekeleza kazi ya ushindi kwa ukamilifu wake na kutoa ushuhuda wa nguvu. Hii ni sawa na kusema kwamba ushindi juu ya mwanadamu inafanywa kuwa bora kupitia uhalisia na ukawaida wa mwili wa Mungu, si kupitia miujiza mikuu na ufunuo. Huduma ya huyu Mungu mwenye mwili ni ya kunena na kwa njia hiyo inamshinda mwanadamu na kumfanya mkamilifu; kwa maneno mengine, kazi ya Roho Aliyejitokeza katika mwili, wajibu wa mwili, ni kunena na kupitia kwa hili kumshinda, kumfichua, kumfanya kuwa kamilifu, na kumwondoa mwanadamu kabisa. Kwa hivyo, ni katika kazi ya kushinda ambapo kazi ya Mungu katika mwili itatimiziwa kwa ukamilifu. Kazi ya ukombozi ya kwanza ilikuwa mwanzo tu wa kazi ya kupata mwili kwa Yesu; mwili unaofanya kazi ya kushinda utaikamilisha kazi nzima ya kupata mwili kwa Yesu. Kijinsia, mmoja ni mwanamke na mwingine ni mwanamume; kwa hili, maana ya kupata mwili kwa Mungu imekamilishwa. Mawazo mabaya ya mwanadamu kumhusu Mungu yameondolewa: Mungu Anaweza kuwa mwanamke na mwanamume, na kimsingi Mungu mwenye mwili Hana jinsia. Alimuumba mwanamume na mwanamke, na Kwake, hakuna mgawanyiko wa jinsia. Katika hatua hii ya kazi, Mungu Hafanyi ishara na miujiza, ili kwamba kazi iweze kutimiza matokeo yake kupitia kwa maneno. Sababu ya jambo hili, aidha, ni kwa maana kazi ya Mungu mwenye mwili mara hii si kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo, ila kumshinda mwanadamu kupitia kunena, ikiwa na maana kwamba uwezo asili uliomo kwenye huu mwili uliopatikana wa Mungu ni kunena maneno na kumshinda mwanadamu, si kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo. Kazi Yake katika ubinadamu wa kawaida si kutenda miujiza, si kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo, ila ni kunena, na kwa hivyo Yesu kupata mwili kwa mara ya pili kunaonekana kwa watu kuwa kawaida zaidi ya mara ya kwanza. Watu wanaona kuwa Mungu kupata mwili si uongo; lakini huyu Mungu mwenye mwili ni tofauti na Yesu Aliyekuwa mwili, na japo wote ni Mungu wenye mwili, Hawako sawa kabisa. Yesu Alikuwa na ubinadamu wa desturi, ubinadamu wa kawaida, lakini Aliambatana na ishara nyingi na miujiza. Katika huyu Mungu mwenye mwili, macho ya mwanadamu hayataona ishara au miujiza, wala kuponya wagonjwa au kufukuza mapepo, wala kutembea juu ya bahari, wala kufunga kwa siku arobaini… Hafanyi kazi sawa na Aliyoifanya Yesu, si kwa kuwa mwili Wake kimsingi ni tofauti na ule wa Yesu, ila ni kwa sababu si huduma Yake kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo. Haharibu kazi Yake mwenyewe, Havurugi kazi Yake mwenyewe. Kwa kuwa anamshinda mwanadamu kwa maneno Yake halisi, haina haja ya kumhini kwa miujiza, na kwa hivyo hii hatua ni kukamilisha kazi ya kupata mwili. Mungu mwenye mwili umwonaye leo ni mwili kabisa, na hana hali ya rohoni ndani yake. Anakuwa mgonjwa sawa tu na watu wengine, Anahitaji chakula na nguo sawa tu na watu wengine, kwani ni mwili kabisa. Ikiwa wakati huu Mungu mwenye mwili Angetekeleza ishara na miujiza mikuu, ikiwa Angeponya wagonjwa, kufukuza mapepo, au Angeweza kuua kwa neno moja tu, kazi ya kushinda ingefanywaje? Kazi ingeenezwa vipi miongoni mwa watu wa Mataifa? Kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo ilikuwa kazi ya Enzi ya Neema, hatua ya kwanza katika kazi ya ukombozi, na sasa kwa kuwa Mungu Amemkomboa mwanadamu kutoka msalabani, Hatekelezi kazi hiyo kamwe. Ikiwa katika siku za mwisho “Mungu” sawa na Yesu Angeonekana, Ambaye Anaponya wagonjwa, Anafukuza mapepo na Anayesulubiwa kwa ajili ya wanadamu, “Mungu” huyo, japo Analingana na maelezo ya Mungu katika Biblia, na rahisi kwa mwanadamu kukubali, Hangeweza, katika kiini chake, kuwa mwili uliovaliwa na Roho wa Mungu, bali na roho mwovu. Kwani ni kanuni ya kazi ya Mungu kutorudia Alichokikamilisha. Hivyo basi kazi ya kupata mwili wa Mungu kwa mara ya pili ni tofauti na kule kwa kwanza. Katika siku za mwisho, Mungu Anafanikisha kazi ya kushinda katika mwili wa kawaida; Haponyi wagonjwa, Hatasulubishwa kwa ajili ya mwanadamu, ila tu Ananena maneno katika mwili, Anamshinda mwanadamu katika mwili. Ni mwili kama huo tu ndio mwili wa Mungu katika mwili; ni mwili kama huo tu ndio unaoweza kukamilisha Kazi ya Mungu katika mwili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 103)

Ikiwa katika hii hatua Mungu mwenye mwili Anapitia ugumu au Anatekeleza huduma Yake, Anafanya hivyo ili kukamilisha maana ya kupata mwili, kwani huku ndiko Mungu kupata mwili kwa mara ya mwisho. Mungu Anaweza kuwa mwili mara mbili tu. Hakuwezi kuwepo mara ya tatu. Kuwa mwili kwa mara ya kwanza Alikuwa ni wa kiume, wa pili ni wa kike, na kwa hivyo sura ya mwili wa Mungu imekamilika katika akili za mwanadamu; aidha, huku kuwa mwili mara mbili tayari kumemaliza kazi ya Mungu katika mwili. Mara ya kwanza, Mungu mwenye mwili Alikuwa na ubinadamu wa kawaida, ili kukamilisha maana ya kupata mwili. Mara hii vilevile Ana ubinadamu wa kawaida ila maana ya huku kupata mwili ni tofauti: ni kwa kina, na kazi Yake ni ya umuhimu mkubwa. Sababu ya Mungu kuwa mwili tena ni kukamilisha maana ya kupata mwili. Mungu Akiikamilisha kabisa hii hatua ya kazi Yake, maana nzima ya kupata mwili, yaani, kazi ya Mungu katika mwili, itakuwa imekamilika, na hakutakuwa na kazi nyingine ya kufanywa katika mwili. Yaani, tangu sasa Mungu Hatawahi tena kuja katika mwili kufanya kazi Yake. Ni kwa kuokoa na kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu pekee ndiko Mungu Hufanya kazi ya kupata mwili. Kwa maneno mengine, si jambo la kawaida kwa Mungu kuwa na mwili, ila tu ni kwa minajili ya kazi. Kwa kuja kufanya kazi Akiwa kwenye mwili, Anamwonyesha Shetani kuwa Mungu ni mwili, mtu wa kawaida—lakini Anaweza kuitawala dunia kwa ushindi, Anaweza kumshinda Shetani, kumkomboa mwanadamu na kumshinda mwanadamu! Lengo la kazi ya Shetani ni kuwapotosha wanadamu, ilhali lengo la Mungu ni kuwaokoa wanadamu. Shetani huwateka wanadamu katika shimo lisilo na mwisho, ilhali Mungu Huwaokoa kutoka humo shimoni. Shetani huwafanya wanadamu wote wamwabudu, ilhali Mungu Huwafanya wawe wafuasi wa utawala Wake, kwani Yeye ndiye Bwana wa viumbe wote. Kazi hii yote hutekelezwa kupitia Mungu kupata mwili mara mbili. Mwili Wake kimsingi ni muungano wa ubinadamu na uungu na huwa na ubinadamu wa kawaida. Kwa hivyo, bila Mungu kuwa mwili, Mungu Asingeweza kufikia matokeo katika ukombozi wa mwanadamu, na bila ubinadamu wa kawaida wa mwili Wake, kazi Yake katika mwili bado haingefikia matokeo. Kiini cha kupata mwili kwa Mungu ni kwamba lazima awe na ubinadamu wa kawaida; kwani ingekuwa vinginevyo, ingekuwa kinyume na madhumuni asili ya Mungu ya kupata mwili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 104)

Kwa nini Ninasema kuwa maana ya kupata mwili haikukamilishwa katika kazi ya Yesu? Ni kwa sababu Neno halikuwa Mwili kikamilifu. Kilichofanywa na Yesu kilikuwa tu sehemu moja ya kazi ya Mungu katika mwili; Alifanya tu kazi ya ukombozi na Hakufanya kazi ya kumpata mwanadamu kikamilifu. Kwa sababu hii, Mungu Amekuwa mwili mara nyingine tena katika siku za mwisho. Hatua hii ya kazi, pia inafanywa katika mwili wa kawaida, ikifanywa na mwanadamu wa kawaida kabisa, ambaye ubinadamu wake haupiti mipaka ya ubinadamu. Kwa maneno mengine, Mungu Amekuwa mwanadamu kamili, na ni mtu ambaye utambulisho wake ni ule wa Mungu, mwanadamu kamili, mwili kamili, Ambaye Anatekeleza kazi. Katika jicho la mwanadamu, Yeye ni mwili tu ambao haujapita mipaka ya ubinadamu hata kidogo, mwanadamu wa kawaida kabisa Anayeweza kuzungumza lugha ya mbinguni, Ambaye Haonyeshi ishara za kimiujiza, Hafanyi miujiza, sembuse kuweka wazi ukweli wa ndani kuhusu dini katika kumbi kuu za mikutano. Kazi ya kupata mwili kwa mara ya pili inaonekana kwa wanadamu kuwa tofauti kabisa na ile ya kwanza, kiasi kwamba kazi hizi mbili zinaonekana kutokuwa na uhusiano wowote, na hakuna chochote katika kazi ya kwanza kinachoweza kuonekana wakati huu. Japo kazi ya kupata mwili kwa mara ya pili ni tofauti na ile ya kwanza, hili halithibitishi kuwa chanzo Chao si kimoja na sawa. Iwapo chanzo Chao ni kimoja inategemea aina ya kazi iliyofanywa na miili na si katika maumbo Yao ya nje. Katika hatua tatu za kazi Yake, Mungu Amekuwa mwili mara mbili, na mara zote kazi ya Mungu kuwa mwili inaanzisha enzi mpya, inaanzisha kazi mpya; kuwa mwili kwa mara ya kwanza na pili kunakamilishana. Macho ya wanadamu hayawezi kugundua kuwa hii miili miwili kwa kweli imetokana na chanzo kimoja. Ni wazi kwamba hili liko nje ya uwezo wa macho ya wanadamu au akili za wanadamu. Ila katika kiini Chao, ni miili sawa, kwani kazi Yao inatokana na Roho mmoja. Iwapo hii miili miwili inatokana na chanzo kimoja haiwezi kuamuliwa kutokana na enzi na sehemu Ilipozaliwa, au vigezo vingine kama hivyo, ila kwa kazi ya uungu iliyoonyeshwa Nayo. Kupata mwili wa pili hakufanyi kazi yoyote iliyofanywa na Yesu, kwani kazi ya Mungu haifuati makubaliano, lakini kila wakati inafungua njia mpya. Kupata mwili wa pili hakulengi kuongeza au kuimarisha maono ya kupata mwili wa kwanza katika akili za watu, ila kuutimiza na kuukamilisha, kuongeza kina cha wanadamu kumwelewa Mungu, kuvunja sheria zote ambazo zipo katika mioyo ya watu, na kufuta picha za uongo kuhusu Mungu mioyoni mwao. Ni wazi kuwa hakuna hatua yoyote ya kazi ya Mungu mwenyewe inaweza kumpa mwanadamu ufahamu kamili wa Mungu; kila mojawapo inatoa kwa sehemu tu, si ufahamu mzima. Japo Mungu Ameonyesha tabia Yake kikamilifu, kwa sababu ya upungufu wa ufahamu wa wanadamu, ufahamu wake kuhusu Mungu si kamili. Haiwezekani, kutumia lugha ya wanadamu, kueleza tabia nzima ya Mungu; basi hatua moja tu ya kazi Yake itamwelezaje Mungu kikamilifu? Anafanya kazi katika mwili kwa kujisetiri katika ubinadamu Wake wa kawaida, na mtu anaweza kumjua tu kupitia kwa maonyesho ya uungu Wake, si kupitia kwa umbo Lake la kimwili. Mungu Anakuja katika mwili kumruhusu mwanadamu Amjue kupitia kazi Zake mbalimbali, na hakuna hatua mbili za kazi Yake zinafanana. Ni kwa njia hii tu mwanadamu anaweza kuwa na ufahamu kamili wa kazi ya Mungu katika mwili, si kwa kujifunga katika kipengele kimoja tu. Japo kazi ya hii miili miwili iliyopatikana ni tofauti, kiini cha hii miili, na chanzo cha kazi Yao vinafanana; ni kwamba tu Ipo ili kutekeleza hatua mbili tofauti za kazi, na inatokea katika enzi mbili tofauti. Licha ya jambo lolote, miili ya Mungu katika mwili inashiriki kiini kimoja na asili moja—huu ni ukweli ambao hauwezi kupingwa na yeyote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 105)

Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kiini cha Kristo ni Roho, yaani, uungu. Kwa hivyo, chemichemi Yake ni ile ya Mungu Mwenyewe; Dutu hii haitapinga kazi Yake Mwenyewe, na Yeye hangeweza kufanya kitu chochote kinachoharibu kazi Yake Mwenyewe, wala milele Yeye kutamka maneno yoyote ambayo yanakwenda kinyume na mapenzi Yake Mwenyewe. Kwa hiyo, Mungu mwenye mwili kamwe hangefanya kazi yoyote ambayo inasumbua usimamizi Wake Mwenyewe. Hili ndilo ambalo binadamu wote wanapaswa kuelewa. Kiini cha kazi ya Roho Mtakatifu ni kuokoa binadamu na ni kwa ajili ya usimamizi wa Mungu Mwenyewe. Vile vile, kazi ya Kristo ni kuokoa binadamu na ni kwa ajili ya mapenzi ya Mungu. Kutokana na kwamba Mungu Anapata mwili, Anatambua dutu Yake ndani ya mwili Wake, kama kwamba mwili Wake ni wa kutosha kufanya kazi Yake. Kwa hivyo, kazi zote za Roho wa Mungu zinabadilishwa na kazi ya Kristo wakati wa kupata mwili, na kwenye msingi wa kazi zote wakati wa kupata mwili ni kazi ya Kristo. Haiwezi kuchanganyika na kazi yoyote ile kutoka enzi nyingine yoyote. Na kwa kuwa Mungu Anakuwa mwili, Yeye Anafanya kazi katika utambulisho wa mwili Wake; kwa kuwa Yeye hukuja katika mwili, kisha Yeye humaliza katika mwili kazi hiyo Anayoazimia kufanya. Iwe ni Roho wa Mungu au ni Kristo, wote ni Mungu Mwenyewe, na Anafanya kazi hiyo Anayoazimia kufanya na hufanya huduma hiyo Anayopaswa kufanya.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 106)

Dutu ya Mungu yenyewe hushika na kutumia mamlaka, lakini Yeye Anao uwezo wa kuwasilisha kwa ukamilifu mamlaka ambayo hutoka Kwake. Iwe ni kazi ya Roho au kazi ya mwili, hakuna ambayo itazozana na nyingine. Roho wa Mungu ndiyo mamlaka juu ya viumbe vyote. Mwili na dutu ya Mungu pia inayo mamlaka, bali Mungu katika mwili Anaweza kufanya kazi yote inayotii mapenzi ya Baba wa mbinguni. Hii haiwezi kupatikana au kufanyika na binadamu yeyote. Mungu Mwenyewe ni mamlaka, lakini mwili Wake unaweza kunyenyekea kwa mamlaka Yake. Hii ndiyo maana ya ndani ya maneno: “Kristo hutii mapenzi ya Mungu Baba.” Mungu ni Roho na Anaweza kufanya kazi ya wokovu, kama vile Mungu Anavyoweza kuwa mwanadamu. Hata hivyo, Mungu Mwenyewe Anafanya kazi Yake Mwenyewe; Yeye wala hazuii wala kuathiri, wala kufanya kazi inayozipinganisha pande zote mbili, kwa kuwa kiini cha kazi iliyofanywa na Roho na mwili yote ni sawa. Iwe ni Roho au mwili, vyote hufanya kazi kutimiza nia moja na kusimamia kazi sawa. Ingawa Roho na mwili huwa na sifa mbili tofauti, dutu yao ni sawa; zote zina dutu ya Mungu Mwenyewe, na utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Mungu Mwenyewe hana mambo ya kuasi; dutu Yake ni nzuri. Yeye ni udhihirisho wa uzuri wote na wema, vile vile upendo wote. Hata katika mwili, Mungu hafanyi lolote linalomuasi Mungu Baba. Hata kwa gharama ya kutoa sadaka maisha Yake, Angekuwa kwa ukamilifu tayari na kutofanya uchaguzi mwingine. Mungu hana mambo ya ukamilifu wa kibinafsi na umuhimu wa kibinafsi, au yale wa kujiona na kiburi; Hana mambo yasiyo aminifu. Yote yanayomuasi Mungu yanatoka kwa Shetani; Shetani ni chanzo cha ubaya na uovu wote. Sababu kwamba mwanadamu anayo sifa sawa na zile za Shetani ni kwa sababu mwanadamu amelaghaiwa na kushughulikiwa na Shetani. Kristo hajawahi kupotoshwa na Shetani, hivyo Anazo tu tabia za Mungu na hakuna hata moja ya Shetani. Haijalishi ugumu wa kazi, au udhaifu wa mwili, Mungu, wakati Anapoishi katika mwili, kamwe hatafanya kitu chochote kitakachopinga kazi ya Mungu Mwenyewe, wala kuacha mapenzi ya Mungu Baba kwa njia ya uasi. Ni afadhali Ateseke maumivu ya mwili kuliko kwenda kinyume na matakwa ya Mungu Baba; ni kama vile Yesu Alisema katika sala, “Baba, kama inawezekana, kikombe hiki kiniondokee: hata hivyo si kama Mimi Nipendavyo, bali kama Wewe upendavyo.” Wanadamu watachagua, bali Kristo hawezi. Ingawa Anao utambulisho wa Mungu Mwenyewe, bado Yeye Anatafuta mapenzi ya Mungu Baba, na Anatimiza kile Alichokabidhiwa na Mungu Baba, kutoka kwa mtazamo wa mwili. Hili ni jambo ambalo haliwezi kupatikana kwa binadamu. Hilo ambalo huja kutoka kwa Shetani haliwezi kuwa na dutu ya Mungu, bali mojawapo ya yale ambayo hukosa kutii na kumpinga Mungu. Haliwezi kumtii Mungu kikamilifu, wala kutii mapenzi ya Mungu kwa hiari. Wanadamu wote isipokuwa Kristo wanaweza kufanya yaliyo ya kumpinga Mungu, na hakuna anayeweza moja kwa moja kufanya kazi aliyoaminiwa na Mungu; hakuna hata mmoja aliye na uwezo wa kuzingatia usimamizi wa Mungu kama wajibu wake wenyewe kutekeleza. Kuwasilisha mapenzi ya Mungu Baba ni kiini cha Kristo; uasi dhidi ya Mungu ni tabia ya shetani. Sifa hizo mbili hazipatani, na yeyote aliye na sifa za shetani hawezi kuitwa Kristo. Sababu ambayo binadamu hawezi kufanya kazi ya Mungu kwa niaba Yake ni kwa sababu mwanadamu hana kiini chochote cha Mungu. Binadamu humfanyia Mungu kazi kwa ajili ya maslahi binafsi ya binadamu na ya matarajio Yake ya baadaye, lakini Kristo Anafanya kazi ya kufanya mapenzi ya Mungu Baba.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 107)

Ubinadamu wa Kristo unaongozwa na uungu Wake. Ingawa yuko katika mwili, ubinadamu Wake si kama ule wa binadamu wa mwili kabisa. Anao upekee wa tabia Yake Mwenyewe, na hii pia huongozwa na uungu Wake. Uungu Wake hauna udhaifu; udhaifu wa Kristo unaelezea ule wa ubinadamu Wake. Kwa kiasi fulani, udhaifu huu huzuia uungu Wake, lakini mipaka hiyo ipo tu kati ya wigo fulani na wakati, na sio zisizo na mipaka. Linapokuja suala la muda wa kufanya kazi ya uungu Wake, hufanyika bila kujali ubinadamu Wake. Ubinadamu wa Kristo kabisa huongozwa na uungu Wake. Mbali na maisha ya kawaida ya ubinadamu Wake, matendo mengine yote ya ubinadamu Wake ni ya kushawishiwa, inayoathirika na kuelekezwa na uungu Wake. Ingawa Kristo Anao ubinadamu, haukatizi kazi ya uungu Wake. Hii hasa ni kwa sababu ubinadamu wa Kristo unaongozwa na uungu Wake; ingawa ubinadamu Wake haujakomaa katika mwenendo Wake mbele ya wengine, hauathiri kazi ya kawaida ya uungu Wake. Ninaposema kwamba ubinadamu Wake haujapotoshwa, Ninamaanisha kwamba ubinadamu wa Kristo unaweza moja kwa moja kuongozwa na uungu Wake, na kwamba Yeye ni mwenye hisia kubwa kuliko ile ya mwanadamu wa kawaida. Ubinadamu Wake unafaa zaidi kwa kuongozwa na uungu katika kazi Yake; ubinadamu Wake una uwezo wa kuonyesha kazi ya uungu, kama vile unao uwezo wa kutii kazi kama hiyo. Mungu Anapofanya kazi katika mwili, hajawahi kamwe kupoteza maono ya wajibu wa mwanadamu katika mwili Anaopaswa kutimiza; Anao uwezo wa kumwabudu Mungu mbinguni kwa moyo wa kweli. Anayo dutu ya Mungu, na utambulisho Wake ni mfano wa Mungu Mwenyewe. Ni kwamba tu Amekuja duniani na kuwa kiumbe aliyeumbwa, na ganda la nje la kiumbe, na sasa Amemiliki ubinadamu ambao hakuwa nao mwanzo; Yeye anao uwezo wa kumwabudu Mungu mbinguni. Hiki ni kiumbe cha Mungu Mwenyewe na hakiigwi na binadamu. Utambulisho Wake ni Mungu Mwenyewe. Ni kutokana na mtazamo wa mwili ndio Yeye huabudu Mungu; Kwa hivyo, maneno “Kristo huabudu Mungu mbinguni” si kwa makosa. Kile Anachouliza binadamu hasa ni nafsi Yake Mwenyewe; Yeye tayari Ameshafanikisha yote Anayotarajia kutoka kwa binadamu kabla ya kuwauliza wafanye hayo. Asingeweza kudai wengine wakati Yeye Mwenyewe Anapata kwao bure, kwa kuwa haya yote yanayotengeneza nafsi Yake. Bila kujali jinsi Yeye hufanya kazi Yake, wala Naye hangewahi kutenda kwa namna inayomuasi Mungu. Haijalishi Analomuuliza mwanadamu, hakuna mahitaji Yake yanayozidi uwezo wa mwanadamu kupata. Yote Afanyayo ni kufanya mapenzi ya Mungu na ni kwa ajili ya usimamizi Wake. Uungu wa Kristo ni zaidi ya wanadamu wote, kwa hivyo Yeye Anayo mamlaka ya juu ya viumbe vyote vilivyoumbwa. Mamlaka haya ni uungu Wake, yaani, nafsi na tabia ya Mungu Mwenyewe, ambayo huamua utambulisho Wake. Kwa hiyo, haijalishi jinsi ubinadamu Wake ni wa kawaida ni wazi kuwa Anao utambulisho wa Mungu Mwenyewe; haijalishi upande Anaosimama Akiongea na kwa vyovyote vile Yeye hutii mapenzi ya Mungu, haiwezi kusemwa kwamba Yeye si Mungu Mwenyewe. Wanadamu wajinga na wapumbavu mara nyingi huchukua ubinadamu wa kawaida wa Kristo kama dosari. Haijalishi jinsi Anavyofichua na kuonyesha nafsi ya uungu Wake, mwanadamu bado hawezi kukiri kwamba Yeye ni Kristo. Na zaidi kwamba Kristo Anaonyesha utii Wake na unyenyekevu, ndivyo wanadamu wengi wajinga humchukua Kristo kwa mzaha. Kuna hata wale ambao huelekeza Kwake mtizamo wa kutengwa na dharau, ilhali kuweka wale “wanadamu wakubwa” wa picha ya kujidai juu ya meza na kuwaabudu. Upinzani wa binadamu dhidi ya, na uasi wa Mungu huja kutokana na ukweli kwamba kiini cha Mungu mwenye mwili hutii mapenzi ya Mungu, vile vile kutokana ubinadamu wa kawaida wa Kristo; hapa ndipo kuna chanzo cha upinzani wa binadamu na uasi wake kwa Mungu. Kama Kristo hangekuwa mwenye umbo la ubinadamu wala nia ya kutafuta mapenzi ya Mungu Baba kutoka katika mtazamo wa kiumbe aliyeumbwa, lakini badala yake kumiliki ubinadamu mkuu, basi kuna uwezekano hakungekuwa na uasi katika mwanadamu yeyote. Sababu ya binadamu kuwa tayari kuamini katika Mungu Asiyeonekana mbinguni ni kwa sababu Mungu mbinguni hana ubinadamu na Yeye hana sifa ya kiumbe hata moja. Hivyo binadamu siku zote humchukua Yeye kwa heshima kubwa, lakini anayo tabia ya dharau kwa Kristo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 108)

Ingawa Kristo duniani Anaweza kufanya kazi kwa niaba ya Mungu Mwenyewe, hajakuja na nia ya kuonyesha watu wote mfano Wake katika mwili. Yeye hajakuja kwa watu wote kumwona; Anakuja kwa ajili ya kuwaruhusu binadamu kuongozwa na mkono Wake, na hivyo kuingia katika enzi mpya. Kazi ya mwili wa Kristo ni kwa ajili ya kazi ya Mungu Mwenyewe, yaani, kwa ajili ya kazi ya Mungu katika mwili, na si ili kuwawezesha binadamu kuelewa kikamilifu kiini cha mwili Wake. Haijalishi jinsi Anavyofanya kazi, haiwezi kuzidi yanayoweza kupatwa na mwili. Haijalishi jinsi Anavyofanya kazi, anafanya hivyo katika mwili na ubinadamu wa kawaida, na wala hafichui kwa kikamilifu kwa mwanadamu uso wa kweli wa Mungu. Zaidi ya hayo, kazi Yake katika mwili kamwe sio isiyo ya kawaida au isiyokadirika kama mwanadamu anavyodhani. Japokuwa Kristo Anamwakilisha Mungu Mwenyewe katika mwili na hufanya binafsi ambayo Mungu Mwenyewe Anapaswa kufanya, Yeye hakani kuwepo kwa Mungu mbinguni, wala kuyatangaza matendo Yake Mwenyewe kwa msisimko. Badala yake, Yeye kwa unyenyekevu Hubaki kwa siri ndani ya mwili Wake. Mbali na Kristo, wale ambao wanadai kwa udanganyifu kuwa Kristo hawana sifa Zake. Wakiwekwa sambamba dhidi ya tabia za kiburi na kujiinua za Kristo wa uongo, inakuwa dhahiri aina gani ya mwili ndiye Kristo wa kweli. Walivyo waongo zaidi, ndivyo Kristo wa uongo wanavyojionyesha wenyewe, na ndivyo wanavyoweza zaidi kufanya kazi za ishara na maajabu ya kuwahadaa binadamu. Kristo wa uongo hawana sifa za Mungu; Kristo hajachafuliwa na kipengele chochote cha dutu ya Kristo wa uongo. Mungu hupata mwili tu kukamilisha kazi ya mwili, na sio tu kuwaruhusu watu wote kumwona. Badala yake, Yeye huacha kazi Yake ithibitishe utambulisho Wake, na kuruhusu Anachofichua kushuhudia dutu Yake. Dutu Yake haikosi msingi; utambulisho Wake haukukamatwa na mkono Wake; huamuliwa kwa kazi Yake na dutu Yake. Ingawa Anacho kiini cha Mungu Mwenyewe na uwezo wa kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe, Yeye bado, hata hivyo, mwili ambao sio kama Roho. Yeye si Mungu na sifa za Roho; Yeye ni Mungu na ganda la mwili. Kwa hivyo, haijalishi jinsi ya ukawaida Wake na Alivyo mdhaifu, na vyovyote vile Anavyotafuta mapenzi ya Mungu Baba, uungu Wake ni usioweza kupingwa. Katika mwili wa Mungu haupo tu ubinadamu wa kawaida na udhaifu Wake; kunao hata zaidi uzuri na mambo yasiyoeleweka ya uungu Wake, na vile vile matendo Yake yote katika mwili. Kwa hiyo, ubinadamu na uungu kwa kweli vipo kwa matendo ndani ya Kristo. Hili sio jambo tupu au lisilo la kawaida kwa vyovyote vile. Yeye huja duniani na lengo kuu la kufanya kazi; ni muhimu kumiliki ubinadamu wa kawaida kutekeleza kazi duniani; la sivyo, haijalishi ukubwa wa nguvu ya uungu Wake, kazi Yake ya awali haiwezi kutiwa katika utumizi mzuri. Ingawa ubinadamu Wake ni wa umuhimu mkubwa, sio dutu Yake. Dutu Yake ni uungu; Kwa hiyo, wakati Anapoanza kufanya huduma Yake hapa duniani ndio wakati Yeye huanza kuonyesha nafsi ya uungu Wake. Ubinadamu Wake uko kwa ajili tu ya kuendeleza maisha ya kawaida ya mwili Wake ili uungu Wake uweze kufanya kazi kama kawaida katika mwili; ni uungu ndio unaoongoza kazi Yake kwa ukamilifu. Wakati Anapomaliza kazi Yake, Atakuwa Ametimiza mujibu wa huduma Yake. Wanachopaswa kujua wanadamuni ni ukamilifu wa kazi Yake, na ni kwa njia ya kazi Yake kuwa Yeye Humwezesha binadamu kumjua Yeye. Katika kipindi cha kazi Yake, Yeye huonyesha kikamilifu kabisa nafsi ya uungu Wake, ambayo si tabia iliyochafuliwa na ubinadamu, au nafsi iliyochafuliwa na mawazo na tabia za binadamu. Wakati utakapokuja ambapo huduma Yake yote imefika mwisho, Atakuwa tayari kwa kikamilifu na kikamilifu Amekwishaonyesha tabia hiyo Anayopaswa kueleza. Kazi Yake haifundishwi na mwanadamu yeyote; maonyesho ya tabia Yake pia ni huru kabisa, haudhibitiwi na akili au kutengenezwa na mawazo, bali hujitokeza kiasili. Hili haliwezi kutimizwa na binadamu yeyote. Hata kama mazingira ni magumu au hali haziruhusu, Yeye Anao uwezo wa kuonyesha tabia Yake kwa wakati muafaka. Yule Ambaye ni Kristo Anaonyesha nafsi ya Kristo, ilhali wale ambao sio hawana tabia za Kristo. Kwa hivyo, hata kama wote watampinga Yeye au kuwa na fikira Kwake, hakuna anayeweza kukana kwa misingi ya fikira ya mwanadamu kwamba tabia iliyoonyeshwa na Kristo ni ile ya Mungu. Wale wote ambao humfuata Kristo kwa moyo wa kweli au kumtafuta Mungu kwa nia watakubali kwamba Yeye ni Kristo kulingana na maonyesho ya uungu Wake. Wao kamwe hawangewahi kumkataa Kristo kwa misingi ya kipengele chochote Chake ambacho hakipatani na fikira za mwanadamu. Ingawa binadamu ni wapumbavu sana, wote wanajua hasa ni nini mapenzi ya binadamu na kile kitokacho kwa Mungu. Ni kwamba tu watu wengi kwa makusudi humpinga Kristo kutokana na makusudi yao wenyewe. Kama si kwa ajili ya haya, hakuna hata mwanadamu mmoja angekuwa na sababu ya kukataa kuwepo kwa Kristo, kwa kuwa uungu uliodhihirishwa na Kristo kwa hakika upo, na kazi Yake inaweza kushuhudiwa kwa macho ya wote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 109)

Kazi na maonyesho ya Kristo huamua dutu Yake. Yeye Anaweza kukamilisha kwa moyo wa kweli kile Alichoaminiwa kufanya. Anaweza kumwabudu Mungu mbinguni kwa moyo wa kweli, na kwa moyo wa kweli Atafute mapenzi ya Mungu Baba. Yote haya yanaamuliwa na dutu Yake. Na vile vile ufunuo Wake wa asili pia unaamuliwa na dutu Yake; sababu ya ufunuo Wake wa asili kuitwa hivyo ni kwa sababu ya maonyesho Yake siyo maigizo, au matokeo ya elimu na mwanadamu, au matokeo ya miaka mingi ya kukuzwa na mwanadamu. Hakujifunza au kujivika nayo Yeye Mwenyewe; badala yake, ni asili ndani Yake. Mwanadamu anaweza kukataa kazi Yake, maonyesho Yake, ubinadamu Wake, na maisha yote ya ubinadamu Wake wa kawaida, lakini hakuna hata mmoja anayeweza kukana kwamba Yeye humwabudu Mungu mbinguni kwa moyo wa kweli; hakuna anayeweza kukana kwamba Amekuja kutimiza mapenzi ya Baba wa mbinguni, na hakuna anayeweza kukana uaminifu Alio nao Anapomtafuta Mungu Baba. Ingawa mfano Wake si wa kupendeza hisia, ingawa hotuba Yake haujajawa na hewa ya ajabu, na kazi Yake sio ya kutikisa ulimwengu au mbingu vile mwanadamu anavyofikiria, Yeye hakika ni Kristo, Anayetimiza mapenzi ya Baba wa mbinguni kwa moyo wa kweli, Ananyenyekea kikamilifu kwa Baba wa mbinguni, na ni mtiifu mpaka wakati kifo. Hii ni kwa sababu dutu Yake ni dutu ya Kristo. Ukweli huu ni mgumu kwa mwanadamu kuamini lakini kwa kweli upo. Wakati huduma ya Kristo imetimia kikamilifu, mwanadamu ataweza kuona kutokana na kazi Zake kwamba tabia Yake na nafsi Yake yanawakilisha tabia na nafsi ya Mungu huko mbinguni. Wakati huo, ujumla wa kazi Zake zote utaweza kuthibitisha kwamba Yeye kweli ni Neno linalogeuka mwili, na si sawa na ule wa mwili na damu ya mwanadamu. Kila hatua ya kazi ya Kristo duniani ina umuhimu wakilishi Wake, lakini mwanadamu anayepitia kazi halisi ya kila hatua hawezi kufahamu umuhimu wa kazi Yake. Hii hasa ni vile katika hatua kadhaa za kazi zilizotekelezwa na Mungu katika kupata Kwake mwili mara ya pili. Wengi wa wale ambao wamesikia tu au kuona maneno ya Kristo tu lakini bado hawajawahi kumwona hawana fikira ya kazi Yake; wale ambao wamemwona Kristo na kusikia maneno Yake, na vile vile kupitia kazi Yake, huona ugumu kuikubali kazi Yake. Je, hii si kwa sababu ya kwamba kuonekana na ubinadamu wa kawaida kwa Kristo hakulingani na matarajio ya binadamu? Wale wanaokubali kazi Yake baada ya Kristo kwenda hawatakuwa na matatizo kama hayo, kwa kuwa wao wanaikubali kazi Yake na wala hawapati kukutana na ubinadamu wa kawaida wa Kristo. Mwanadamu hawezi kuacha fikira zake kuhusu Mungu na badala yake humchunguza kwa mkazo; hii ni kutokana na ukweli kwamba mwanadamu analenga tu juu ya kuonekana Kwake na anashindwa kutambua dutu Yake kwa kuzingatia kazi Yake na maneno Yake. Iwapo mwanadamu ataufumbia macho kuonekana kwa Kristo au kuepuka kujadili ubinadamu wa Kristo, na aongee tu juu ya uungu Wake, Ambao kazi Yake na maneno hayawezi kufikiwa na mwanadamu yeyote, basi fikira ya binadamu itapungua kwa nusu, hata kwa kiasi kwamba matatizo yote ya mwanadamu yatatatuliwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 110)

Yeye Aliye mwili wa Mungu Atakuwa na dutu ya Mungu, na Yule Aliye Mungu katika mwili Atakuwa na maonyesho ya Mungu. Kwa maana Mungu Hupata mwili, Ataleta mbele kazi Anayopaswa kufanya, na kwa maana Mungu Amepata mwili, Ataonyesha kile Alicho na Ataweza kuuleta ukweli kwa mwanadamu, kumpa mwanadamu uhai, na Amwonyeshe mwanadamu njia. Mwili usio na dutu ya Mungu kwa kweli sio Mungu mwenye mwili; kwa hili hakuna tashwishi. Kupeleleza kama kweli ni mwili wa Mungu mwenye Mwili, mwanadamu lazima aamue haya kutoka kwa tabia Yeye huonyesha na maneno Yeye hunena. Ambayo ni kusema, kama ni mwili wa Mungu mwenye mwili au la, na kama ni njia ya kweli au la, lazima iamuliwe kutokana na dutu Yake. Hivyo, katika kudadisi[a] iwapo ni mwili wa Mungu mwenye mwili, cha msingi ni kuwa makini kuhusu dutu Yake (Kazi Yake, maneno Yake, tabia Yake, na mengine mengi), bali sio hali ya sura Yake ya nje. Mwanadamu akiona tu sura Yake ya nje, na aipuuze dutu Yake, basi hilo linaonyesha upumbavu na ujinga wa mwanadamu. Sura ya nje haiamulii dutu; na zaidi, kazi ya Mungu haiwezi kamwei kuambatana na dhana za mwanadamu. Je, si sura ya nje ya Yesu ilikinzana na dhana za mwanadamu? Je sura Yake na mavazi Yake hayakuweza kutoa dalili yoyote ya utambulisho Wake? Je, si sababu ya Mafarisayo wa zamani kabisa kumpinga Yesu hasa ilikuwa ni kwa sababu waliiangalia tu sura Yake ya nje, na hawakuyaweka moyoni maneno Aliyoongea? Ni matumaini Yangu kuwa ndugu wanaotafuta kuonekana kwa Mungu hawatarudia tanzia ya kihistoria. Hampaswi kuwa Mafarisayo wa wakati huu na kumsulubisha Mungu msalabani tena. Mnafaa kufikiria kwa makini jinsi ya kukaribisha kurudi kwa Mungu, na kuwa na mawazo dhahiri ya jinsi ya kuwa mtu anayetii ukweli. Hili ni jukumu la kila mtu anayengoja Yesu arudi na mawingu. Tunafaa kusugua macho yetu ya kiroho, na tusiwe waathiriwa wa maneno yaliyojaa mambo ya kufurahisha masikio. Tunafaa kuwaza juu ya kazi ya Mungu ya matendo, na tunafaa kuangalia upande wa hakika wa Mungu. Msijisahau ama kupotelea ndotoni, mkitazamia daima ile siku ambayo Bwana Yesu atashuka kwa ghafla juu ya mawingu kuwachukua nyinyi ambao hamjawahi kumjua wala kumwona Yeye, na msiojua kutenda mapenzi Yake. Ni vyema kufikiri juu ya mambo ya kiutendaji!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji

Tanbihi:

a. Nakala halisi ya mwanzo inasema “na kwa.”

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 111)

Mungu mwenye mwili Anajidhihirisha mwenyewe kwa watu kadhaa wanaomfuata Anapofanya kazi Yeye binafsi, na sio kwa viumbe wote. Alijifanya mwili ili Akamilishe hatua ya kazi Yake, na sio ili amwonyeshe mwanadamu mfano Wake. Hata hivyo, kazi Yake lazima ifanywe na Yeye binafsi, kwa hivyo inalazimu Afanye kazi hiyo katika mwili. Kazi hii inapokamilika, Ataondoka duniani; Hawezi kusalia duniani kwa muda mrefu kwa hofu ya kuzuia kazi inayokuja. Anachokionyesha kwa halaiki ni tabia Yake ya haki na matendo Yake yote, na sio umbo la wakati Amejifanya mwili mara mbili, kwa maana mfano wa Mungu unaweza tu kuonyeshwa kupitia kwa tabia Yake, na si kubadilishwa na mfano wa mwili Wake wa nyama. Mfano wa mwili Wake wa nyama huonyeshwa kwa watu wachache tu, kwa wale wanaomfuata Anapofanya kazi katika mwili. Hiyo ndio maana kazi inayofanywa wakati huu inafanywa kwa siri. Ni kama tu vile Yesu alivyojionyeshwa kwa Wayahudi pekee yao Alipofanya kazi Yake, na hakujionyesha hadharani kwa mataifa mengine. Hivyo, pindi Alipomaliza kazi Yake, Aliondoka miongoni mwa wanadamu na hakukawia; kwa wakati uliofuata Hakujionyesha kwa nafsi Yake kwa mwanadamu, bali kazi iliendeshwa moja kwa moja na Roho Mtakatifu. Mara tu kazi ya Mungu katika mwili inapokamilika, Anaondoka katika dunia ya mwanadamu, na kamwe Hafanyi tena kazi sawa na ile Aliyofanya Akiwa katika mwili. Kazi inayofuata hufanywa na Roho Mtakatifu moja kwa moja. Wakati huu, mwanadamu hawezi kuona mfano Wa Mungu katika mwili; Yeye Hajionyeshi wazi kwa mwanadamu hata kidogo, na daima Anabaki mafichoni. Muda wa kazi ya Mungu mwenye mwili ni mchache, ambayo lazima ifanywe katika Enzi bayana, muda, taifa na kati ya watu bayana. Kazi kama hiyo inawakilisha tu kazi ya wakati wa Mungu katika mwili, na inalenga enzi fulani, ikiwakilisha kazi ya Roho wa Mungu katika enzi moja hasa, na sio ujumla wa kazi Yake. Kwa hivyo, umbo la Mungu mwenye mwili halitaonyeshwa kwa kila mwanadamu. Kinachoonyeshwa kwa halaiki ni haki ya Mungu na tabia Yake kwa ukamilifu, na wala sio mfano Wake Alipokuwa mwili mara mbili. Sio sura inayoonyeshwa kwa mwanadamu, wala mifano yote miwili ikijumlishwa. Kwa hivyo, ni muhimu kwamba mwili wa Mungu uondoke duniani baada ya kukamilisha kazi Anayohitajika kufanya, kwa kuwa Anakuja tu kufanya kazi Anayopaswa kufanya, na sio kuwaonyesha wanadamu mfano wa umbo Lake. Ingawa umuhimu wa kuingia katika mwili umeshatimizwa na Mungu mara mbili Akijifanya mwili na nyama, bado hatajionyesha wazi kwa taifa ambalo halijawahi kumwona mbeleni. Yesu hatajionyesha Mwenyewe kamwe mara nyingine kwa Wayahudi kama Jua la haki, wala Hataupanda Mlima wa Mizeituni na kuonekana kwa watu wote: yote ambayo Wayahudi huona ni taswira Yake wakati wa kipindi Chake katika Uyahudi. Hili ni kwa sababu kazi ya Yesu aliyepata mwili iliisha kitambo sana miaka elfu mbili iliyopita; Hatarudi Uyahudi katika sura ya Myahudi, sembuse kujionyesha katika sura ya Myahudi kwa nchi yoyote ya Mataifa, kwani sura ya Yesu aliyepata mwili ni sura ya Myahudi tu, na siyo sura ya Mwana wa Adamu ambayo Yohana alikuwa ameiona. Ingawa Yesu aliwaahidi wafuasi Wake kwamba Angerudi tena, Hatajionyesha tu Mwenyewe katika sura ya Myahudi kwa wote walio katika nchi za Mataifa. Mnapaswa kujua kwamba kazi ya Mungu katika mwili inafaa kufungua enzi mpya. Kazi hii ni ya muda wa miaka michache tu, na Hawezi kukamilisha kazi yote ya Roho wa Mungu. Hii ni sawia na vile umbo la Yesu kama Myahudi linaweza tu kuwakilisha mfano wa Mungu alivyofanya kazi katika Yudea, na Angefanya tu kazi ya msalabani. Wakati ambao Yesu Alikuwa katika mwili, Hangefanya kazi ya kutamatisha enzi au kumwangamiza mwanadamu. Kwa hivyo, baada ya kusulubiwa na kukamilisha kazi Yake, Alipaa juu na daima Akajificha kutoka kwa mwanadamu. Kutoka wakati huo kuendelea, wale waumini wa mataifa waliweza tu kuiona picha Yake ambayo walibandika kwenye kuta zao, na sio udhihirisho wa Bwana Yesu. Picha hii imechorwa na mwanadamu tu, na si mfano ambao Mungu Mwenyewe Alimwonyesha mwanadamu. Mungu Hatajionyesha kwa halaiki wazi wazi katika mfano ambao Yeye Alikuwa nao mara mbili Akiwa katika mwili. Kazi Anayofanya miongoni mwa wanadamu ni kuwaruhusu kuelewa tabia Yake. Yote haya yanaonyeshwa kwa mwanadamu kwa njia ya kazi za enzi tofauti; yanakamilishwa kupitia tabia ambazo Ameziweka wazi na kazi ambayo Amefanya, na bali si kupitia kwa udhihirisho wa Yesu. Hiyo ni kusema, umbo la Mungu halionyeshwi kwa mwanadamu kupitia katika mfano wa Mungu mwenye mwili, lakini ni kwa kupitia katika kazi iliyotekelezwa na Mungu mwenye mwili wa sura na umbo; na kupitia kazi Yake, mfano Wake unaonekana na tabia Yake inajulikana. Huu ndio umuhimu wa kazi Angependa kufanya katika mwili.

Wakati kazi ya Alipokuwa mwili mara mbili inakamilika, Anaanza kuonyesha tabia Yake ya haki katika mataifa, Akiruhusu halaiki ione mfano wa umbo Lake. Anapenda kudhihirisha tabia Yake, na kupitia katika hili Aweke wazi tamati za aina tofauti ya wanadamu, hapo kuifikisha mwisho kabisa enzi nzee. Kazi Yake katika mwili haitendeki katika sehemu pana (kama vile Yesu Alivyofanya kazi katika sehemu ya Yuda peke Yake, na leo hii Ninafanya kazi miongoni mwenu pekee) kwa sababu kazi Yake katika mwili ina mipaka na kingo. Anafanya tu kazi ya muda mchache katika mfano wa kawaida na mwili wa kawaida, badala ya kufanya kazi ya milele kupitia kwa Mungu mwenye mwili, ama kufanya kazi ya kuwaonekania watu wote wa mataifa. Kazi hii katika mwili lazima izuiliwe katika mawanda (kama vile kufanya kazi katika Yuda ama kati Yenu), kisha kupanua kazi iliyofanyika katika mipaka hii. Bila shaka, kazi ya upanuzi huu huendeshwa na Roho Mtakatifu moja kwa moja na haiwezi kuwa kazi ya mwili Wake wa nyama. Kwa maana kazi katika mwili iko na mipaka na haiwezi kuenea katika pembe zote za ulimwengu. Hauwezi kuyatekeleza haya. Kupitia kwa kazi katika mwili, Roho Wake hutekeleza kazi inayofuatia. Kwa hivyo, kazi inayofanywa katika mwili ni ya matayarisho inayotekelezwa ndani ya mipaka; Roho Wake kisha Anaendeleza kazi hii, na kuipanua.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (2)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 112)

Mungu huja tu katika dunia hii kufanya kazi ya kuongoza enzi; kufungua enzi mpya na kutamatisha enzi ya zamani. Hajakuja kuishi kulingana na maisha ya mwanadamu wa kawaida kwa kikamilifu, kupitia Mwenyewe raha na machungu ya maisha kama mwanadamu, au kumfanya mtu fulani mkamilifu kwa mkono Wake au kumtazama binafsi mtu Fulani anavyokua. Hii sio kazi Yake; kazi Yake ni kufunua tu enzi mpya na kutamatisha enzi iliyotangulia. Hiyo ina maana, Atafungua enzi mpya, akamilishe iliyotangulia, amshinde shetani kwa kufanya kazi Yake binafsi. Kila mara Anapotekeleza kazi Yeye Mwenyewe, ni kana kwamba Anakanyaga mguu wake katika uwanja wa vita Katika mwili, kwanza Anaishinda dunia kisha Anatawala juu ya Shetani; Anachukua utukufu wote na kufungua pazia kwa kazi ya enzi yote elfu mbili, na kuwapa binadamu wote duniani njia ya kweli ya kufuata, na maisha ya amani na furaha. Hata hivyo, Mungu hawezi kuishi na mwanadamu duniani kwa muda mrefu, kwa maana Mungu ni Mungu, ni si kama mwanadamu kamwe. Hawezi kuishi urefu wa maisha ya mwanadamu wa kawaida, hiyo ina maana, Hawezi kuishi duniani kama mwanadamu ambaye si wa kawaida, kwa maana Yuko na sehemu ndogo ya ubinadamu wa kawaida wa mtu wa kawaida kumuwezesha kuishi vile. Kwa maneno mengine, Mungu anawezaje kuanzisha familia, kuwa na kazi na kulea watoto duniani? Je, si hii itakuwa ni aibu? Kwamba Yeye amejaliwa na ubinadamu wa kawaida ni kwa minajili tu ya kutekeleza kazi Yake kwa njia ya kawaida, na sio kumwezesha Yeye kuwa na familia na kazi kama mtu wa kawaida. Hisia Zake za kawaida, mawazo ya kawaida, na kula kwa kawaida na nguo za mwili Wake yanatosha kuthibitisha kuwa Yuko na ubinadamu wa kawaida; hakuna haja Yake kuwa na familia au kazi ili athibitishe kwamba Yeye kweli yuko na ubinadamu wa kawaida. Hiyo haina maana hata kidogo! Mungu anakuja duniani, kumaanisha Neno linageuka kuwa mwili; Kwa urahisi Anamruhusu mwanadamu kulielewa neno Lake na kuliona neno Lake, hiyo ni, kumruhusu mwanadamu kuona kazi inayotekelezwa na mwili. Nia Yake sio kwamba wanadamu wauchukue mwili Wake kwa njia Fulani, bali kwamba mwanadamu awe mtiifu mpaka mwisho, kumaanisha, aweze kutii maneno yote yanayotoka katika kinywa Chake, na kunyenyekea na kukubali kazi yote Anayofanya. Yeye Anafanya kazi katika mwili tu; Yeye hamuulizi mwanadamu kwa kujua aabudu ukuu na utakatifu wa mwili Wake, bali anamwonyesha mwanadamu hekima ya kazi Yake na mamlaka yote Aliyo nayo. Kwa hivyo, ingawa Anao ubinadamu wa kipekee, Hafanyi matangazo yoyote, na Anatilia tu maanani kazi ambayo Anapaswa kufanya. Mnapaswa kujua ni kwa nini Mungu Alipata mwili na ilhali hatangazi wala kushuhudia juu ya ubinadamu Wake wa kawaida, lakini badala yake Anatekeleza tu kazi ambayo Angependa kufanya. Hii ndio sababu mnaona tu uwepo wa uungu katika Mungu mwenye mwili, kwa sababu Hatangazi kuwa Kwake katika mwili ndio mwanadamu aige. Wakati tu mwanadamu anamwongoza mwanadamu ndipo anapozungumzia kuhusu kile alicho kama binadamu, ndivyo apate heshima na utii wao vyema zaidi na hivyo kufanikisha uongozi wa wengine. Kinyume na hilo, Mungu huwashinda watu kupitia katika kazi Yake pekee (hiyo ni, kazi isiyoweza kufanywa na mwanadamu); hakuna shaka ya mwanadamu kuvutiwa na Yeye au kumfanya mwanadamu amwabudu. Yote Anayofanya ni kuweka tu katika mwanadamu hisia za uchaji Kwake au kumfanya mwanadamu aweze kujua kuhusu kutowezekana kwa kumchunguza Yeye. Hakuna haja ya Mungu kumpendeza mwanadamu. Kile anachohitaji ni kuwa wewe umheshimu na kumwabudu mara tu unaposhuhudia tabia Yake. Kazi ambayo Mungu hufanya ni Yake mwenyewe; haiwezi kufanywa na mwanadamu badala Yake, wala kuweza kutimizwa na mwanadamu. Ni Mungu Mwenyewe tu ndiye Anaweza kufanya kazi Yake mwenyewe na kuanzisha enzi mpya ili kumwongoza mwanadamu katika maisha mapya. Kazi ambayo Yeye hufanya ni kumwezesha mwanadamu kupokea maisha mapya na kuingia katika enzi mpya. Kazi nyingine yote hupokezwa kwa wale wanadamu wa ubinadamu wa kawaida na ambao wanapendwa na wengine. Kwa hivyo, katika Enzi ya Neema, Alimaliza kazi ya miaka elfu mbili katika miaka mitatu na nusu pekee wakati wa miaka Yake thelathini na mitatu ndani ya mwili. Wakati ambapo Mungu atakuja duniani kutekeleza kazi Yake, Yeye kila mara hukamilisha kazi ya miaka elfu mbili au ya enzi nzima katika muda mfupi sana wa miaka michache. Yeye hachelewi, na Hasimami; Yeye hufupisha tu kazi ya miaka mingi ili ikamilishwe katika miaka michache tu mifupi. Hili ni kwa sababu kazi ambayo Yeye hufanya Mwenyewe ni kuifungua tu njia mpya na kuiongoza enzi mpya.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (2)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 113)

Wakati ambapo Mungu huitekeleza kazi Yake, Yeye haji kujishughulisha katika ujenzi wowote au mabadiliko; Yeye huja kutimiza huduma Yake. Kila wakati Anapopata mwili, ni kwa ajili tu ya kufanikisha hatua ya kazi na kuifungua enzi mpya. Sasa Enzi ya Ufalme imefika, na mafundisho ya ufalme. Hatua hii ya kazi si kazi ya mwanadamu, si ya kumfanyia kazi mwanadamu kwa kiwango fulani; ni kuimaliza sehemu ya kazi ya Mungu tu. Kazi Yake si kazi ya mwanadamu, si kufikia matokeo fulani katika kumfanyia kazi mwanadamu kabla ya kuondoka duniani; ni kutimiza huduma Yake kwa ukamilifu na kuimaliza kazi ambayo Anapaswa kuifanya, ambayo ni kutengeneza mipango ya kufaa ya kazi Yake duniani, na hivyo kupata kutukuka. Kazi ya Mungu mwenye mwili ni tofauti na ile ya wale wanaotumiwa na Roho Mtakatifu. Mungu anapofanya kazi Yake duniani, Yeye anajali kutimilika kwa huduma Yake pekee Yake. Na kwa mambo mengine yasiyohusiana na huduma Yake, Yeye kimatendo hajishughulishi hata kidogo, hata kwa kiwango cha kuzipa mgongo shughuli hizo. Yeye hufanya tu kazi Anayopaswa kufanya, na hajishughulishi na kazi ambayo mwanadamu anapaswa kufanya. Kazi Anayofanya ni ile tu inahusiana na enzi Aliyomo na huduma Anayopaswa kukamilisha, kana kwamba mambo mengine yote si jukumu Lake. Yeye hajijazi na maarifa ya kawaida kuhusu jinsi ya kuishi kama mwanadamu, na Hajifunzi mahusiano ya jamii au mambo yoyote ambayo mwanadamu anaelewa. Hajishughulishi kamwe na mambo ambayo mwanadamu anapaswa kujua na Anafanya tu kitu ambacho ni jukumu Lake. Kwa hivyo, mwanadamu anavyoona, Mungu mwenye mwili ni mwenye upungufu katika mambo mengi mno, hata kwa kiasi kwamba Anavipa mgongo vingi ambavyo mwanadamu anapaswa kuwa navyo, na kwamba hana ufahamu wa mambo kama hayo. Mambo kama ufahamu wa maisha ya kawaida, na vile vile kanuni za tabia na kuhusiana na wengine, huonekana kuwa hazina uhusiano Kwake. Hata hivyo, huwezi kuona kutoka kwa Mungu mwenye mwili tabia zozote zisizo za kawaida. Hiyo ni kusema, ubinadamu Wake unadumisha maisha Yake kama mwanadamu wa kawaida na fikira za kawaida za ubongo Wake, na kumpa uwezo wa kutofautisha kati ya mazuri na mabaya. Hata hivyo, Hajajazwa na kingine chochote, yote ambayo ni ya wanadamu (walioumbwa) pekee. Mungu anapata mwili ili kukamilisha huduma Yake pekee. Kazi Yake inaelekezwa kwa enzi nzima na sio kwa mtu binafsi au mahali fulani. Kazi Yake inaelekezwa kwa ulimwengu mzima. Huu ndio mwelekeo wa kazi Yake na kanuni Anayofuata katika kazi Yake. Hii haiwezi kubadilishwa na yeyote, na mwanadamu hawezi kuhusika kwa sehemu yoyote. Kila wakati ambapo Mungu hupata mwili, Yeye huja pamoja na kazi ya enzi hiyo, na sio dhamira ya kuishi ubavuni mwa mwanadamu kwa miaka ishirini, thelathini, arobaini, au hata miaka sabini, themanini ili waweze kuelewa bora zaidi na kupata utambuzi Kwake. Hakuna haja ya hilo! Kufanya hivyo hakungeweza katu kuzidisha ufahamu ambao mwanadamu anao wa tabia ya asili ya Mungu; badala yake, kungeongeza tu kwa fikira zao na kufanya fikira na mawazo ya mwanadamu yawe kuukuu. Na kwa hiyo nyote mnapaswa kuelewa hasa ni nini kazi ya Mungu aliyepata mwili. Yawezekana kwamba hamyaelewi maneno Yangu: “Siji kuyapitia maisha ya mwanadamu wa kawaida”? Je, mmesahau maneno: “Mungu haji duniani kuishi maisha ya mwanadamu wa kawaida”? Hamlielewi kusudi la Mungu kupata mwili, wala hamjui maana ya “Mungu angekujaje duniani na dhamira ya kuyapitia maisha ya kiumbe aliyeumbwa?” Mungu anakuja tu duniani kukamilisha kazi Yake, na kwa hivyo Kazi Yake duniani ni ya muda mfupi. Haji duniani na nia ya Roho wa Mungu kukuza mwili Wake kuwa mkuu wa kipekee wa kanisa. Mungu anapokuja duniani, ni Neno ambalo kugeuka kuwa mwili; mwanadamu, hata hivyo, hajui kuhusu kazi Yake na kwa nguvu anaona Yeye kuwa sababu ya mambo. Lakini nyote mnapaswa kufahamu kuwa Mungu ni Neno lililogeuka kuwa mwili, na sio mwili uliokuzwa na Roho wa Mungu ili kusimamia nafasi ya Mungu kwa ufupi. Mungu Mwenyewe hakuzwi, ila ni Neno kugeuka mwili, na leo hii Anatekeleza kazi Yake kirasmi miongoni mwenu. Nyote mwajua na kukubali kwamba kupata mwili kwa Mungu ni ukweli, lakini mnajidai kuwa na ufahamu ambao kwa kweli hamna. Ninyi hamthamini kabisa kazi ya Mungu aliyepata mwili au umuhimu na kiini cha Yeye kupata mwili, na husimulia kwa urahisi tu maneno ambayo hunenwa na wengine. Je, unaamini kwamba Mungu aliyepata mwili ni kama unavyodhani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (3)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 114)

Mungu hugeuka mwili ili tu Aiongoze enzi na Aanzishe kazi mpya. Lazima muelewe hoja hii. Hii ni tofauti kabisa na kazi ya mwanadamu, na mawili haya hayawezi kuzungumzwa kwa pamoja. Mwanadamu anahitaji muda mrefu wa kukuzwa na kufanywa mkamilifu kabla mwanadamu aweze kutumiwa kutekeleza kazi, na ubinadamu wa hali ya juu unahitajika. Mwanadamu hapaswi kudumisha hali yake ya ubinadamu wa kawaida tu, bali pia mwanadamu zaidi ya hapo lazima aelewe kanuni nyingi na sheria za tabia kabla ya mengine, na zaidi ya hayo lazima ajifunze zaidi kuhusu hekima na maadili ya mwanadamu. Haya ndiyo mwanadamu lazima kujengwa nayo. Hata hivyo, hivi sivyo ilivyo na Mungu mwenye mwili, kwa maana kazi Yake haimwakilishi mwanadamu na wala si ya binadamu; bali ni dhihirisho la moja kwa moja la hali Yake na utekelezaji wa moja kwa moja wa kazi Anayopaswa kufanya. (Kwa kawaida, kazi Yake hufanyika wakati inapaswa kufanyika, na sio tu wakati wowote kiholela. Badala Yake, kazi Yake hufanyika wakati ambapo ni wakati wa kukamilisha huduma Yake). Yeye hajihusishi katika maisha ya mwanadamu wala katika kazi ya mwanadamu, hiyo inamaanisha, ubinadamu Wake haujengwi na yoyote kati ya haya (lakini hili haliathiri kazi Yake). Anatimiza huduma Yake tu ikiwa wakati umewadia wa kufanya hivyo; haijalishi hali Aliyomo, Yeye huendelea mbele na kazi Anayopaswa kufanya. Haijalishi mwanadamu anajua nini kumhusu, au maoni ya mwanadamu kumhusu, kazi Yake haiathiriki. Hii ni kama tu vile Yesu Alivyofanya kazi Yake; hakuna aliyejua Yeye ni nani, lakini Aliendelea tu mbele na kazi Yake. Mambo haya hayakumuathiri katika utendaji wa kazi Yake Aliyopaswa kufanya. Kwa hivyo, Hakukiri au kutangaza kuwa Yeye ni nani, na Yeye alimfanya mwanadamu Amfuate tu. Kwa kawaida, huu haukuwa tu uvumilivu wa Mungu; ilikuwa ni njia ambayo Yesu anafanya kazi katika mwili. Angeweza tu kufanya kazi kwa namna hii, kwani mwanadamu hangeweza kumtambua Yesu kwa jicho la kawaida. Na hata kama mwanadamu angeweza, mwanadamu hangeweza kusaidia katika kazi Yake. Zaidi ya hayo, hakugeuka mwili ili mwanadamu apate kujua mwili huu Wake; ilikuwa ni kwa ajili ya kufanya kazi Yake na kukamilisha huduma Yake. Kwa sababu hii, hakutilia maanani hali ya kufanya Ajulikane. Alipokamilisha kazi Aliyopaswa kufanya, utambulisho Wake na hadhi Yake vilijulikana wazi kwa mwanadamu. Mungu mwenye mwili hukaa kimya na hafanyi matangazo yoyote. Yeye hajishughulishi na mwanadamu au vile mwanadamu anaendelea katika kumfuata, na yeye husonga tu mbele katika kutimiza huduma Yake na kufanya kazi Anayopaswa kufanya. Hakuna Anayeweza kusimama mbele ya njia ya kazi Yake. Wakati muda unawadia wa kazi Yake kukamilika, ni muhimu kazi hiyo ikamilike na kufikishwa kikomo. Hakuna anayeweza kusema vinginevyo. Baada tu ya Yeye kuondoka kutoka kwa mwanadamu baada ya kukamilisha kazi Yake ndipo mwanadamu ataelewa kazi Anayofanya, ingawa hataifahamu kikamilifu. Na itachukua muda mrefu ndipo mwanadamu aelewe nia Yake Alipofanya kazi hiyo mara ya kwanza. Kwa maneno mengine, kazi ya enzi ambapo Mungu anageuka mwili imegawanywa katika sehemu mbili. Sehemu moja ni kupitia katika kazi na maneno ya Mungu mwenye mwili Mwenyewe. Pindi tu huduma ya mwili Wake imetimika kikamilifu, sehemu nyingine ya kazi inatakiwa kutekelezwa na Roho Mtakatifu; basi utakuwa wakati wa mwanadamu kutimiza wajibu wake, kwa maana Mungu ameshafungua njia tayari, na lazima itembelewe na mwanadamu mwenyewe. Hiyo ni kusema, Mungu anageuka kuwa mwili ili kutekeleza sehemu moja ya kazi Yake, na inaendelezwa kwa urithi na Roho Mtakatifu na vile vile wale watu wanaotumiwa na Roho Mtakatifu. Kwa hivyo mwanadamu anapaswa kujua kazi ya msingi inayopaswa kutekelezwa na Mungu mwenye mwili katika hatua hii ya kazi. Mwanadamu lazima aelewe hasa umuhimu wa Mungu kugeuka kuwa mwili na kazi Anayopaswa kufanya, badala ya kumuuliza Mungu ni nini kinachotakiwa kwa mwanadamu. Haya ni makosa ya mwanadamu, na vile vile fikira, na zaidi ya hayo, ni kutotii kwake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (3)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 115)

Mungu anakuwa mwili bila nia ya kumfanya mwanadamu apate kuujua mwili Wake, ama kukubali mwanadamu kutofautisha tofauti kati ya mwili wa Mungu mwenye mwili na ule wa mwanadamu; Mungu hapati mwili ili kufunza mwanadamu uwezo wa utambuzi, na zaidi nia ya mwanadamu kumwabudu Mungu mwenye mwili, ambayo kupitia kwayo atapata utukufu mkuu. Hakuna kati ya haya yaliyo mapenzi ya Mungu ya awali ya Mungu kuwa mwili. Mungu hawi mwili ili kulaani mwanadamu, kufichua mwanadamu akipenda, ama kufanya vitu kuwa vigumu kwa mwanadamu. Hakuna kati ya hayo lililo penzi la awali la Mungu. Kila wakati ambapo Mungu anakuwa mwili, ni kazi isiyo na budi. Ni kwa ajili ya kazi Yake kuu na usimamizi Wake mkuu ndio maana Anafanya hivyo, na si kwa sababu ambazo mwanadamu anafikiria. Mungu anakuja tu duniani Anavyohitajika na kazi Yake, na kila wakati ikiwa lazima. Haji duniani Akiwa na nia ya kuzurura, ila kutekeleza kazi ambayo Anapaswa kufanya. Mbona basi Ajipatie kazi hii ngumu na kujiweka katika hatari kubwa kufanya kazi hii? Mungu anakuwa mwili tu inapobidi, na kila wakati ikiwa na umuhimu wa kipekee. Kama ingekuwa tu kwa sababu ya kumfanya mwanadamu amuangalie na kufungua macho yao, basi kwa uhakika kabisa, hangekuja kati ya wanadamu kwa kubembeleza. Anakuja duniani kwa usimamizi Wake na kazi Yake kuu, na kuwa na uwezo wa kutwaa wanadamu zaidi. Anakuja kuwakilisha enzi na kumshinda Shetani, na ni katika mwili ndimo Anakuja kumshinda Shetani. Zaidi, Anakuja kuwaongoza binadamu wote katika maisha yao. Haya yote yanahusu uongozi Wake, na yanahusu kazi ya ulimwengu wote. Mungu angekuwa mwili ili tu kumruhusu mwanadamu kuja kuujua mwili Wake na kuyafungua macho ya mwanadamu, basi mbona Hangesafiri kwa kila taifa? Je hili sio jambo la wepesi zaidi? Lakini hakufanya hivyo, badala yake, Akachagua mahali palipofaa pa kuishi na kuanza kazi Aliyopaswa kufanya. Mwili huu pekee ni wa umuhimu mkuu. Anawakilisha enzi nzima, na Anatekeleza kazi ya enzi nzima; Analeta enzi ya zamani kufika tamati na kuikaribisha mpya. Haya yote ni mambo muhimu yanayohusu usimamizi wa Mungu, na ni umuhimu wa hatua ya kazi iliyotekelezwa na Mungu kuja duniani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (3)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 116)

Wokovu wa Mungu kwa mwanadamu haufanywi moja kwa moja kupitia njia ya Roho ama kama Roho, kwani Roho Wake hawezi kuguzwa ama kuonekana na mwanadamu, na hawezi kukaribiwa na mwanadamu. Kama Angejaribu kumwokoa mwanadamu moja kwa moja kwa njia ya Roho, mwanadamu hangeweza kupokea wokovu Wake. Na kama sio Mungu kuvalia umbo la nje la mwanadamu aliyeumbwa, mwanadamu hawangeweza kupokea wokovu huu. Kwani mwanadamu hawezi kumkaribia kwa njia yoyote ile, zaidi kama jinsi hakuna anayeweza kukaribia wingu la Yehova. Ni kwa kuwa mwanadamu wa kuumbwa tu, hivyo ni kusema, kuliweka neno Lake katika mwili Atakaogeukana kuwa, ndio ataweza kulifanya neno yeye Mwenyewe ndani ya wale wote wanaomfuata. Hapo ndipo mwanadamu atasikia mwenyewe neno Lake, kuona neno Lake, na kupokea neno Lake, kisha kupitia hili aokolewe kamili. Kama Mungu hangegeuka na kupata mwili, hakuna mtu mwenye mwili ambaye angepokea wokovu huo mkuu, wala hakuna mtu hata mmoja ambaye angeokolewa. Kama Roho wa Mungu angefanya kazi moja kwa moja kati ya mwanadamu, mwanadamu angepigwa ama kubebwa kabisa kama mfungwa na Shetani kwani mwanadamu hawezi kushirikiana na Mungu. Kupata mwili mara ya kwanza kulikuwa kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi kupitia mwili wa Yesu, hivyo, Aliokoa mwanadamu kutoka kwa msalaba, lakini tabia potovu ya kishetani ilibaki ndani ya mwanadamu. Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi. Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao, na kufanywa safi kabisa, na kupata mabadiliko ya tabia, hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu. Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu. Mungu Alianza kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema baada ya Enzi ya Sheria kufika mwisho. Ni mpaka siku za mwisho tu ambapo Mungu Ametakasa binadamu kikamilifu kwa kufanya kazi ya hukumu na kuadibu mwanadamu kwa kuwa muasi, ndipo Mungu atakamilisha kazi Yake ya wokovu na kupumzika. Kwa hivyo, katika hatua tatu za kazi, ni mara mbili tu ndipo Mungu amekuwa mwili ili kufanya kazi Yake kati ya mwanadamu Mwenyewe. Hiyo ni kwa sababu moja tu kati ya hatua tatu za kazi ni kuwaongoza wanadamu katika maisha yao, ilhali zingine mbili ni kazi ya wokovu. Mungu Anapokuwa mwili tu ndipo Atakapoishi pamoja na mwanadamu, kuzoea mateso ya dunia, na kuishi katika mwili wa kawaida. Ni kwa namna hii tu ndipo Ataweza kuwapa wanadamu njia ya vitendo wanayohitaji kama viumbe. Mwanadamu anapokea wokovu kamili kutoka kwa Mungu kwa sababu ya Mungu mwenye mwili, sio moja kwa moja kutoka kwa maombi yao kwenda mbinguni. Kwani mwanadamu ni mwenye mwili; mwanadamu hawezi kuona Roho wa Mungu na pia kutoweza kumkaribia. Kile tu mwanadamu anaweza kushiriki ni mwili wa Mungu; kupitia Yeye tu ndipo mwanadamu ataweza kuelewa njia zote, na ukweli wote, na kupokea wokovu kamili. Kupatikana kwa mwili mara ya pili kunatosha kumaliza dhambi za mwanadamu na kumtakasa mwanadamu. Hivyo, kupatikana kwa mwili mara ya pili kutafikisha tamati kazi yote ya Mungu mwenye mwili na kukamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili. Baada ya hapo, kazi ya Mungu mwenye mwili itakuwa imefika mwisho kabisa. Baada ya kupata mwili mara ya pili, hatakuwa mwili tena kwa kazi Yake. Kwani usimamizi Wake wote utakuwa umefika mwisho. Katika siku za mwisho, mwili Wake utakuwa umepata watu Wake teule kabisa, na yote mwanadamu katika siku za mwisho watakuwa wameainishwa kulingana na aina. Hatafanya kazi ya wokovu tena, wala Hatarudi kuwa mwili ili kutekeleza kazi yoyote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 117)

Kile ambacho mwanadamu amepata sasa—kimo cha mwanadamu leo, maarifa yao, upendo, uaminifu, utiifu, na pia kuona kwao—ni matokeo yanayopatikana kupitia hukumu ya neno. Kwamba unaweza kuwa na uaminifu na kubaki umesimama mpaka siku hii ipatikane kwa kupita neno. Hivi sasa mwanadamu anaona kuwa kazi ya Mungu kupata mwili ni ya ajabu kweli. Kuna mengi ambayo hayawezi kupatikana na mwanadamu, na kwamba ni mafumbo na maajabu. Kwa hivyo, wengi wamejiwasilisha. Wengine hawajawahi kujiwasilisha kwa mwanadamu yeyote kutoka siku za kuzaliwa kwao, ilhali wanapoyaona maneno ya Mungu siku hii, wanajiwasilisha kikamilifu bila kujua wamefanya vile, na hawajaribu kuchunguza au kusema chochote kingine. Binadamu wameanguka chini ya neno na wamesujudu chini ya hukumu ya neno. Kama Roho wa Mungu angemwongelesha wanadamu moja kwa moja, wote wangejiwasilisha kwa sauti hiyo, na kuanguka chini bila maneno ya ufunuo, vile Paulo alivyoanguka chini kukiwa na nuru alipokuwa akisafiri kwenda Damaski. Mungu angeendelea kufanya kazi kwa njia hii, mwanadamu hangeweza kutambua upotovu wake kupitia kwa hukumu ya neno na kupata wokovu. Ni kwa kupata mwili pekee ndiyo Mungu ataweza kuwasilisha maneno Yake Mwenyewe kwa masikio ya wale wote ambao wana masikio waweze kuyasikia maneno Yake na kupokea kazi Yake ya hukumu kupitia kwa neno. Hayo tu ndio matokeo yanayopokewa na neno Lake, badala ya kutokea kwa Roho ikimtisha mwanadamu kuwasilisha. Ni kupitia tu kwa kazi ya vitendo na ya ajabu ndio tabia ya mwanadamu, iliyofichika ndani zaidi kwa enzi nyingi, ifichuliwe kabisa ili mwanadamu aitambue na kuibadilisha. Hili ndiyo kazi ya vitendo ya Mungu mwenye mwili; Ananena na kutekeleza hukumu kwa njia ya vitendo ili kupata matokeo ya hukumu juu ya mwanadamu kupitia kwa neno. Haya ndiyo mamlaka ya Mungu mwenye mwili na umuhimu wa Mungu kupata mwili. Inafanyika kuonyesha mamlaka ya Mungu mwenye mwili, matokeo yanayopatikana na kazi ya neno, na kwamba Roho Amekuja kwa mwili; Anaonyesha mamlaka Yake kupitia hukumu juu ya mwanadamu kwa neno. Ingawa mwili Wake ni hali ya nje ya mwanadamu wa kawaida, ni matokeo ambayo neno Lake linapokea ndiyo yanamwonyesha mwanadamu kuwa Amejaa mamlaka, kwama ni Mungu Mwenyewe na kwamba maneno Yake ni maonyesho ya Mungu Mwenyewe. Hii inaonyesha wanadamu wote kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe, Mungu Mwenyewe Aliyekuwa mwili, kwamba hapaswi kukosewa na yeyote na kwamba hakuna anayeweza kuepuka hukumu Yake kupitia kwa neno, na hakuna nguvu ya giza inayoweza kutamalaki juu ya mamlaka Yake. Mwanadamu anamtii Yeye kabisa kwa sababu Yeye ni Neno aliyepata mwili, kwa sababu ya mamlaka Yake, na kwa sababu ya hukumu Yake kwa neno. Kazi iliyoletwa na mwili Wake uliokuwa mwili ni mamlaka ambayo Anamiliki. Anakuwa mwili kwani mwili pia unaweza kuwa na mamlaka, na Anaweza kutekeleza kazi kati ya wanadamu katika halii ya njia halisi, inayoonekana na kuguswa na mwanadamu. Kazi kama hii ni ya ukweli kuliko kazi ingine yoyote ifanywayo moja kwa moja na Roho wa Mungu Aliye na mamlaka yote, na matokeo Yake ni dhahiri pia. Hii ni kwa sababu mwili wa Mungu unaweza kuongea na kufanya kazi kwa njia halisi; hali ya nje ya mwili Wake haina mamlaka yoyote na inaweza kukaribiwa na mwanadamu. Dutu Yake inabeba mamlaka, lakini mamlaka Yake hayaonekani kwa yeyote. Anaponena na kufanya kazi, mwanadamu hana uwezo wa kutambua uwepo wa mamlaka Yake; hili ni nzuri kwa kazi Yake hata zaidi. Hii kazi yote inaweza kupata matokeo. Ingawa hakuna mwanadamu anayefahamu kuwa Anayo mamlaka ama kuona kuwa Hastahili kukosewa ama kuona hasira Yake, kupitia mamlaka Yake yaliyofichika na hasira na hotuba ya uma, Anapata matokeo yaliyotarajiwa ya neno Lake. Kwa maneno mengine, kupitia kwa tani ya sauti Yake, ukali wa hotuba Yake, na hekima ya maneno Yake, mwanadamu anashawishika kabisa. Kwa njia hii, mwanadamu anawasilisha kwa neno la Mungu mwenye mwili wa Mungu, ambaye anaonekana kutokuwa na mamlaka, hivyo kufikia lengo la Mungu la wokovu kwa mwanadamu. Huu ndio umuhimu mwingine wa kuingia Kwake katika mwili: kuongea na ukweli zaidi na kukubali ukweli wa neno Lake kuwa na athari juu ya mwanadamu ili kushuhudia nguvu ya neno la Mungu. Kwa hivyo kazi hii isingefanywa kupitia kupata mwili, isingekuwa na matokeo hata kidogo na isingeweza kuokoa watenda dhambi kikamilifu. Mungu Asipokuwa mwili, Atabaki kama Roho bila kuonekana au kuguswa na mwanadamu. Mwanadamu ni kiumbe wa mwili, na mwanadamu na Mungu ni wa dunia mbili tofauti na ina asili tofauti tofauti. Roho wa Mungu hana uwiano na mwili wa mwanadamu, na hakuna uhusiano unaoweza kuwepo kati yao; pia, mwanadamu hawezi kuwa roho. Hivyo, Roho wa Mungu lazima ageuke mmoja wa viumbe na kufanya kazi yake ya asili. Mungu anaweza kujipandisha mahali pa juu zaidi na pia aweze kunyenyekea na kuwa mwanadamu aliyeumbwa, kufanya kazi na kuishi kati ya wanadamu, lakini mwanadamu hawezi kupanda juu na kuwa roho na pia kuteremka chini. Kwa hivyo, Mungu lazima awe mwili ili atekeleze kazi Yake. Kama ilivyokuwa wakati wa kuingia katika mwili mara ya kwanza, mwili wa Mungu mwenye mwili pekee ndio unaoweza kumkomboa mwanadamu kupitia kusulubiwa, ilhali hakuna uwezo wa Roho wa Mungu kusulubiwa kama sadaka ya dhambi kwa mwanadamu. Mungu Angekuwa mwili moja kwa moja ili kuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu, lakini mwanadamu hangepanda mbinguni moja kwa moja kuchukua sadaka ambayo Mungu alikuwa amewaandalia. Hivyo, lazima Mungu asafiri kwenda na kurudi kati ya mbingu na nchi, badala ya kumwacha mwanadamu apande mbinguni kuchukua wokovu huu, kwani mwanadamu alikuwa ameanguka na, aidha, hangeweza kabisa kupaa mbinguni, ama hata kupata sadaka ya dhambi. Kwa hivyo, ilikuwa lazima kwa Yesu kuja kati ya wanadamu na binafsi kufanya kazi ambayo mwanadamu hangeweza kukamilisha. Kila wakati ambapo Mungu aligeuka kuwa mwili, ilikuwa lazima kabisa Afanye hivyo. Iwapo hatua yoyote ingetekelezwa moja kwa moja na Roho wa Mungu, Hangevumilia ukosefu wa hadhi unaoambatana na kupata mwili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 118)

Mungu alifanyika mwili kwa sababu lengo la kazi Yake si roho ya Shetani, au kitu chochote kisicho cha mwili, ila mwanadamu, ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa na Shetani. Ni kwa sababu hii hasa kwamba mwili wa mwanadamu umepotoshwa ndiyo maana Mungu amemfanya mwanadamu mwenye mwili kuwa mlengwa wa kazi Yake; aidha, kwa sababu mwanadamu ni mlengwa wa upotovu, Amemfanya mwanadamu kuwa mlengwa wa pekee wa kazi Yake katika hatua zote za kazi Yake ya wokovu. Mwanadamu ni kiumbe anayekufa, ni wa mwili na damu, na Mungu ndiye tu Anayeweza kumwokoa mwanadamu. Kwa namna hii, ni lazima Mungu awe mwili ambao una tabia zinazofanana na mwanadamu ili Aweze kufanya kazi Yake, ili kwamba kazi Yake iweze kupata matokeo mazuri zaidi. Mungu lazima awe mwili ili Aweze kufanya kazi Yake kwa ufanisi kwa sababu mwanadamu ni wa mwili, na hana uwezo wa kushinda dhambi au kujivua mwili. Ingawa kiini na utambulisho wa Mungu unatofautiana kwa kiasi kikubwa na kiini na utambulisho wa mwanadamu, bado kuonekana Kwake kunafanana na kuonekana kwa mwanadamu, Ana umbo la mwanadamu wa kawaida, na Anaishi maisha ya mwanadamu wa kawaida, na wale wanaomwona hawawezi kuona tofauti na mtu wa kawaida. Kuonekana huku kwa kawaida na ubinadamu wa kawaida vinatosha Kwake kwa ajili ya kufanya kazi Yake ya kiungu katika ubinadamu wa kawaida. Mwili Wake unamruhusu kufanya kazi Yake katika ubinadamu wa kawaida, na unamsaidia kufanya kazi Yake miongoni mwa wanadamu, na ubinadamu Wake wa kawaida, aidha, humsaidia kufanya kazi ya wokovu miongoni mwa wanadamu. Ingawa ubinadamu Wake wa kawaida umeleta msukosuko miongoni mwa wanadamu, msukosuko huo haujaathiri matokeo ya kawaida ya kazi Yake. Kwa ufupi, kazi ya ubinadamu Wake wa kawaida ni ya manufaa makubwa kwa mwanadamu. Ingawa watu wengi hawakubali ubinadamu Wake wa kawaida, kazi Yake bado inaweza kuwa ya ufanisi, na matokeo haya yanapatikana kutokana na ubinadamu Wake wa kawaida. Kuhusu hili hakuna shaka. Kutokana na kazi Yake ya mwili, mwanadamu anapata vitu mara kumi au dazeni kadhaa zaidi kuliko mitazamo iliyopo miongoni mwa mwanadamu kuhusu ubinadamu Wake wa kawaida, na mitazamo hiyo hatimaye itamezwa na kazi Yake. Na matokeo ambayo kazi Yake imefanikiwa, ambayo ni kusema, maarifa ambayo mwanadamu anayo juu Yake, yanazidi kwa mbali sana dhana za mwanadamu kumhusu. Hakuna namna ya kufikiri au kupima kazi Anayofanya katika mwili, maana mwili Wake si kama wa mwanadamu; ingawa sura za nje zinafanana kiini chao si sawa. Mwili Wake unatoa mitazamo mingi kuhusu Mungu miongoni mwa mwanadamu, bado mwili Wake unaweza pia kumruhusu mwanadamu kuwa na maarifa mengi, na anaweza hata kumshinda mwanadamu yeyote mwenye ganda la sawa nje. Maana Yeye si mwanadamu wa kawaida tu, bali ni Mungu mwenye umbo la nje kama la mwanadamu, na hakuna anayeweza kumwelewa au kumfahamu kikamilifu. Mungu asiyeonekana na kushikika anapendwa na kukaribishwa na wote. Kama Mungu ni Roho tu ambayo haionekani kwa mwanadamu, ni rahisi sana kwa mwanadamu kumwamini Mungu. Mwanadamu anaweza kuzipa uhuru fikra zake mwenyewe, anaweza kuchagua taswira yoyote anayotaka kama taswira ya Mungu ili kujifurahisha mwenyewe na kujifanya mwenyewe awe na furaha. Kwa njia hii, watu wanaweza kufanya yoyote yanoyompendeza zaidi Mungu wao mwenyewe, na kile ambacho Mungu huyu angempenda wakifanye, bila aibu yoyote. Aidha, mwanadamu huyu anaamini kwamba hakuna ambaye ni mwaminifu zaidi anayejitolea kwa Mungu kuliko yeye, na kwamba wengine wote ni mbwa wa Mataifa, na wasiokuwa waaminifu kwa Mungu. Inaweza kusemekana kwamba hiki ndicho kinachotafutwa na wale ambao imani yao kwa Mungu ni ya kidhahania na ambayo imejikita katika mafundisho; wanavyovitafuta vinafanana, tofauti ikiwa ndogo tu. Ni kwamba tu taswira za Mungu katika fikra zao ni tofauti, lakini viini vyao kimsingi vinafanana.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 119)

Sababu pekee ambayo Mungu mwenye mwili amefanyika mwili ni kwa sababu ya mahitaji ya mwanadamu aliyepotoka. Ni kwa sababu ya mahitaji ya mwanadamu na si ya Mungu, na mateso Yake na sadaka ni kwa ajili ya mwanadamu na si kwa manufaa ya Mungu Mwenyewe. Hakuna faida wala hasara au tuzo kwa Mungu; Hatavuna mavuno yoyote ya baadaye, bali ni kile ambacho hapo awali Aliwiwa. Yote Anayoyafanya na kujitolea kwa ajili mwanadamu si kwa sababu Atapata thawabu kubwa, bali ni kwa ajili ya mwanadamu. Ingawa kazi ya Mungu mwenye mwili inahusisha ugumu mwingi usiofikirika, matokeo ambayo yanapatikana mwishowe yanazidi kwa mbali sana kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu moja kwa moja. Kazi ya mwili inahusisha taabu nyingi sana, na mwili hauwezi kuwa na utambulisho mkubwa kama wa Roho, hauwezi kufanya matendo ya kimiujiza kama Roho, sembuse kuwa na mamlaka kama ya Roho. Lakini kiini cha kazi inayofanywa na mwili huu usiokuwa wa kawaida ni kuu zaidi kulinganisha na kazi inayofanywa moja kwa moja na Roho, na mwili huu Mwenyewe ndio jibu kwa mahitaji yote ya wanadamu wote. Kwa wale wanaotaka kuokolewa, thamani ya Roho ipo chini zaidi kulinganisha na ile ya mwili. Kazi ya Roho inaweza kuufikia ulimwengu wote, katika milima yote, mito, maziwa, na bahari, lakini kazi ya mwili kwa ufanisi zaidi inahusiana na kila mtu anayekutana na Yeye. Aidha, mwili wa Mungu katika umbo la kushikika unaweza kueleweka vizuri na kuaminiwa na mwanadamu, na unaweza kuimarisha maarifa ya mwanadamu kuhusu Mungu, na anaweza kumwachia mwanadamu mvuto wa kina wa matendo halisi ya Mungu. Kazi ya Roho imefungwa sirini, ni vigumu kwa viumbe wenye mwili wa kufa kuelewa, na vigumu zaidi kwao kuona, na hivyo wanaweza kutegemea tu vitu vya kufikirika. Hata hivyo, kazi ya mwili ni ya kawaida, na imejikita katika uhalisi, na ina hekima kubwa sana, na ni ukweli unaoweza kuonekana kwa macho ya mwanadamu; mwanadamu anaweza kupitia uzoefu wa hekima ya Mungu, na hana haja ya kuwa na fikira zake kubwa. Huu ndio usahihi na thamani halisi ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Roho anaweza tu kufanya vitu ambavyo havionekani kwa mwanadamu na vigumu kwake kufikiria, kwa mfano nuru ya Roho, mzunguko wa Roho na uongozi wa Roho, lakini kwa mwanadamu mwenye akili, hivi havitoi maana inayoeleweka. Vinatoa maana ya kusonga, au ya jumla tu, na havitoi maelekezo kwa maneno. Hata hivyo, kazi ya Mungu mwenye mwili, ni tofauti sana: Ina mwongozo sahihi wa maneno, ina nia ya wazi, ina malengo ya wazi yanayohitajika. Na hivyo mwanadamu hahitaji kupapasa, au kutumia fikra zake, au kufanya makisio. Huu ndio uwazi wa kazi katika mwili, na tofauti yake kubwa na kazi ya Roho. Kazi ya Roho inafaa tu kwa mawanda finyu, na haiwezi kuchukua kazi ya mwili. Kazi ya mwili inampa mwanadamu malengo halisi zaidi na yanayohitajika na maarifa yaliyo halisi zaidi na yenye thamani kuliko kazi ya Roho Mtakatifu. Kazi ambayo ina thamani kubwa kwa mwanadamu aliyepotoka ambayo inatoa maneno sahihi, malengo wazi ya kufuata, na ambayo inaweza kuonekana na kuguswa. Ni kazi yenye kuwezekana tu, na uongozi wa wakati ndio unaofaa kwa ladha ya mwanadamu, na kazi halisi ndiyo inayoweza kumwokoa mwanadamu kutoka katika tabia yake iliyopotoka na kusawijika. Hii inaweza kufanywa na Mungu mwenye mwili tu; ni Mungu mwenye mwili peke yake ndiye Anayeweza kumwokoa mwanadamu kutoka katika hali yake ya zamani ya kupotoka. Ingawa Roho ni kiini cha asili ya Mungu, kazi kama hii inaweza tu kufanywa na mwili Wake. Kama Roho angefanya kazi peke Yake, basi haingewezekana kwa kazi Yake kuwa ya ufanisi—huu ni ukweli ulio wazi kabisa. Ingawa watu wengi wamekuwa maadui wa Mungu kwa sababu ya mwili huu, Anapokamilisha kazi Yake, wale ambao wapo kinyume Chake hawataacha tu kuwa maadui Zake, bali kinyume Chake watakuwa mashahidi Wake. Watakuwa mashahidi watakaokuwa wameshindwa naye, mashahidi ambao wana ulinganifu na Yeye na ambao hawatenganishwi naye. Atamsababisha mwanadamu kujua umuhimu wa kazi Yake katika mwili kwa mwanadamu, na mwanadamu atajua umuhimu wa mwili huu katika maana ya uwepo wa mwanadamu, atajua thamani Yake halisi katika ukuaji wa maisha ya mwanadamu, aidha, atajua mwili huu utakuwa chemchemi ya uhai ambayo kwayo mwanadamu hataachana nayo. Ingawa Mungu mwenye mwili anatofautiana sana na utambulisho na nafasi ya Mungu, na anaonekana kwa mwanadamu kuwa hana ulinganifu na hadhi yake halisi, mwili huu, ambao hauna sura halisi ya Mungu, au utambulisho halisi wa Mungu, unaweza kufanya kazi ambayo Roho wa Mungu hawezi kuifanya moja kwa moja. Hiyo ndiyo maana ya kweli na thamani ya Mungu mwenye mwili, na ni umuhimu huu na thamani ambayo mwanadamu hawezi kuithamini na kuikubali. Ingawa wanadamu wote wanamtazamia Roho wa Mungu na wanamdharau Mungu mwenye mwili, bila kujali vile wanavyoona au kufikiri, maana na thamani halisi ya mwili inapita kwa mbali ile ya Roho. Bila shaka, hii ni kwa mujibu wa mwanadamu aliyepotoka. Kwa kuwa kila mtu anayetafuta ukweli na anatamani kumwona Mungu, Kazi ya Roho inaweza kutoa tu kuguswa au msukumo, na hisia ya kuona maajabu ambayo hayaelezeki na kufikirika, na hisia ambayo ni kuu, ya juu sana kuliko uwezo wa mwanadamu, na inayotamanika, lakini ambayo pia haifikiwi na haipatikani kwa wote. Mwanadamu na Roho wa Mungu wanaweza tu kutazamana kwa mbali, kana kwamba kuna umbali mrefu baina yao, na hawawezi kufanana kamwe, kana kwamba mwanadamu na Mungu wametenganishwa na mgawanyiko usioonekana. Kwa hakika, hizi ni fikra za uongo ambazo Roho amempa mwanadamu, ambayo ndiyo sababu Roho na mwanadamu sio wa aina moja, na Roho na mwanadamu hawawezi kuishi pamoja katika ulimwengu mmoja, na kwa sababu Roho hana kitu chochote cha mwanadamu. Kwa hivyo mwanadamu hana haja ya Roho, maana Roho hawezi kufanya kazi inayohitajika sana na mwanadamu moja kwa moja. Kazi ya mwili inampatia mwanadamu malengo halisi ya kufuata, maneno halisi, na hisia kwamba Yeye ni halisi na wa kawaida, kwamba ni mnyenyekevu na wa kawaida. Ingawa mwanadamu anaweza kumwogopa, kwa watu wengi Yeye ni rahisi kuhusiana naye: Mwanadamu anaweza kuuona uso Wake, na kuisikia sauti Yake, na hahitaji kumwangalia kwa kutokea mbali. Mwanadamu anahisi kuwa ni rahisi kuufikia mwili huu, sio wa mbali au usioeleweka, bali unaoonekana na kushikika, maana mwili huu upo katika ulimwengu mmoja na mwanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 120)

Kwa wale wote ambao wanaishi katika mwili, kubadilisha tabia zao kunahitaji kuwe na malengo ya kufuata, na kumjua Mungu kunahitaji kushuhudia matendo halisi na sura halisi ya Mungu. Yote haya yanaweza kufikiwa tu na Mungu mwenye mwili, na yote yanaweza kukamilishwa na mwili wa kawaida na halisi. Hii ndiyo maana kufanyika mwili ni muhimu, na kwa nini kunahitajika na wanadamu wote wapotovu. Kwa kuwa watu wanahitajika kumjua Mungu, taswira za Mungu wa kufikirika na wa kimiujiza inapaswa iondolewe kutoka katika mioyo yao, na kwa kuwa wanahitajika kutupilia mbali tabia yao iliyopotoka, kwanza wanapaswa kujua tabia yao iliyopotoka. Ikiwa mwanadamu anafanya kazi ili kuondoa taswira za Miungu wasio dhahiri kutoka katika mioyo ya watu, basi atashindwa kupata matokeo sahihi. Taswira za Miungu wasio dhahiri katika mioyo ya watu haziwezi kuwekwa hadharani, kutupwa, au kufukuzwa kabisa kwa maneno pekee. Kwa kufanya hivyo, mwisho wake haitawezekana kuondoa vitu hivi vilivyokita mizizi kwa watu. Ni kwa kubadilisha vitu hivi visivyo dhahiri na vya kimiujiza na Mungu anayeonekana tu na mwenye taswira halisi ya Mungu, na kuwafanya watu kuvielewa ndipo matokeo mazuri yanaweza kupatikana. Mwanadamu anatambua kwamba Mungu aliyekuwa anamtafuta huko nyuma ni asiye dhahiri na wa kimiujiza. Kile ambacho kinaweza kufanikisha matokeo haya sio uongozi wa moja kwa moja wa Roho, sembuse mafundisho ya mtu fulani, bali ni Mungu mwenye mwili. Dhana za mwanadamu zinakuwa wazi pale ambapo Mungu mwenye mwili atafanya kazi Yake rasmi, kwa sababu ukawaida na uhalisi wa Mungu mwenye mwili ni kinyume na nadharia za Mungu asiye dhahiri na wa kufikirika katika fikra za mwanadamu. Dhana asili za mwanadamu zinaweza tu kudhihirishwa kupitia tofauti zao na Mungu mwenye mwili. Bila ulinganisho na Mungu mwenye mwili, dhana za mwanadamu zisingefichuliwa; kwa maneno mengine, bila tofauti ya uhalisi vitu visivyo dhahiri visingefichuliwa. Hakuna anayeweza kutumia maneno ili kufanya kazi hii, na hakuna anayeweza kuizungumzia kazi hii kwa kutumia maneno. Ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anayeweza kufanya kazi Yake, na hakuna mtu mwingine anayeweza kufanya kazi hii kwa niaba Yake. Haijalishi lugha ya mwanadamu ni pevu kiasi gani, hawezi kuzungumzia uhalisi na ukawaida wa Mungu. Mwanadamu anaweza tu kumjua Mungu zaidi kwa utendaji, na anaweza tu kumwona kwa uwazi zaidi, ikiwa Mungu binafsi anafanya kazi miongoni mwanadamu na anaonyesha kikamilifu sura Yake na uungu Wake. Athari hii haiwezi kupatwa na mwanadamu yeyote yule mwenye mwili. Bila shaka, Roho wa Mungu pia hawezi kupata matokeo haya. Mungu anaweza kumwokoa mwanadamu kutoka katika ushawishi wa Shetani, lakini kazi hii haiwezi kukamilishwa moja kwa moja na Roho wa Mungu; badala yake, inaweza kufanywa tu na mwili ambao Roho wa Mungu anauvaa, na mwili wa Mungu mwenye mwili. Mwili huu ni mwanadamu na pia ni Mungu, ni mwanadamu aliye katika ubinadamu wa kawaida na pia ni Mungu ambaye ana uungu wote. Na hivyo, hata kama mwili huu sio Roho wa Mungu, na unatofautiana kwa kiasi kikubwa na Roho, bado ni Mungu mwenye mwili Mwenyewe ambaye Anamwokoa mwanadamu, ambaye ni Roho, pia ni mwili. Haijalishi Anaitwa majina gani, hatimaye bado ni Mungu Mwenyewe anayemwokoa mwanadamu. Maana Roho wa Mungu hatenganishwi na mwili, na kazi ya mwili pia ni kazi ya Roho wa Mungu; ni kwamba tu kazi hii haifanywi kwa kutumia utambulisho wa Roho, lakini inafanywa kwa kutumia utambulisho wa mwili. Kazi inayotakiwa kufanywa moja kwa moja na Roho haihitaji kufanyika mwili, na kazi ambayo inahitaji mwili kuifanya haiwezi kufanywa moja kwa moja na Roho, na inaweza kufanywa tu na Mungu mwenye mwili. Hiki ndicho kinachohitajika kwa kazi hii, na ndicho kinachohitajika na mwanadamu aliyepotoka. Katika hatua tatu za kazi ya Mungu, ni hatua moja tu ndiyo iliyofanywa moja kwa moja na Roho, na hatua mbili zilizobaki zimechukuliwa na Mungu mwenye mwili, na hazifanywi moja kwa moja na Roho. Kazi ya Enzi ya Sheria iliyofanywa na Roho haikuhusisha kubadilisha tabia potovu ya mwanadamu, na wala haikuwa na uhusiano wowote na maarifa ya mwanadamu kuhusu Mungu. Hata hivyo kazi ya Mungu mwenye mwili katika Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme, inahusisha tabia ya dhambi ya mwanadamu na maarifa yake juu ya Mungu, na ni sehemu ya maana na muhimu ya kazi ya wokovu. Kwa hiyo, mwanadamu aliyepotoka anahitaji zaidi wokovu wa Mungu mwenye mwili, na anahitaji zaidi kazi ya moja kwa moja ya Mungu mwenye mwili. Mwanadamu anamhitaji Mungu mwenye mwili ili kumchunga, kumsaidia, kumnywesha maji, kumlisha, kumhukumu na kumwadibu, na anahitaji neema zaidi na wokovu mkubwa kutoka kwa Mungu mwenye mwili. Ni Mungu katika mwili pekee ndiye anayeweza kuwa msiri wa mwanadamu, mchungaji wa mwanadamu, msaada wa mwanadamu uliopo kila mara, na hii yote ni ulazima wa kufanyika mwili leo na katika nyakati za nyuma.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 121)

Mwanadamu amepotoshwa na Shetani, na yeye ndiye kiumbe wa juu kabisa kuliko viumbe wote wa Mungu, hivyo mwanadamu anahitaji wokovu wa Mungu. Mlengwa wa wokovu wa Mungu ni mwanadamu, si Shetani, na kile kitakachookolewa ni mwili wa mwanadamu, na roho ya mwanadamu, na si mwovu. Shetani ni mlengwa wa uharibifu wa Mungu, mwanadamu ni mlengwa wa wokovu wa Mungu, na mwili wa mwanadamu umepotoshwa na Shetani, kwa hivyo kitu cha kwanza kuokolewa ni mwili wa mwanadamu. Mwili wa mwanadamu umepotoshwa kwa kiasi kikubwa, na umekuwa kitu cha kumpinga Mungu, ambacho kinapinga na kukana waziwazi uwepo wa Mungu. Mwili huu uliopotoka ni vigumu sana kushughulika nao, na hakuna kitu ambacho ni kigumu sana kushughulika nacho au kukibadilisha kuliko tabia potovu ya mwili. Shetani anaingia katika mwili wa mwanadamu ili kuchochea usumbufu, na anatumia mwili wa mwanadamu kuisumbua kazi ya Mungu, na kuharibu mpango wa Mungu, na hivyo mwanadamu amekuwa Shetani, na adui wa Mungu. Ili mwanadamu aweze kuokolewa, kwanza ni lazima achukuliwe mateka. Ni kwa sababu hii ndiyo maana Mungu anainuka na kuingia katika vita na Anaingia katika mwili ili afanye kazi ambayo Amekusudia kufanya, na kupambana na Shetani. Lengo Lake ni wokovu wa mwanadamu, mwanadamu ambaye amepotoshwa, na kushindwa na kuangamizwa kwa Shetani, ambaye ameasi dhidi Yake. Anamshinda Shetani kupitia kazi Yake ya kumshinda mwanadamu, na huku akimwokoa mwanadamu aliyepotoka. Hivyo, ni kazi ambayo inatimiza matatizo mawili kwa wakati mmoja. Anafanya kazi makusudi mawili mwili mara moja na Anazungumza katika mwili, na Anafanya kazi zote katika mwili ili aweze kujihusisha vizuri na mwanadamu, na kumdhibiti mwanadamu vizuri. Wakati wa mwisho ambapo Mungu atakuwa mwili, kazi Yake katika siku za mwisho itahitimishwa katika mwili. Atawaainisha wanadamu wote kulingana na aina, na kuhitimisha usimamizi wake wote, na pia kuhitimisha kazi Yake yote katika mwili. Baada ya kazi Yake yote duniani kuisha, Atakuwa mshindi kikamilifu. Kufanya kazi katika mwili, Mungu atakuwa amemshinda mwanadamu kikamilifu na atakuwa amempata mwanadamu kikamilifu. Hii haimaanishi kuwa usimamizi Wake wote utakuwa umekoma? Mungu anapohitimisha kazi Yake katika mwili, ilivyo kwamba Amemshinda Shetani kikamilifu, na Amekuwa mshindi, Shetani hatakuwa na fursa zaidi ya kumpotosha mwanadamu. Kazi ya Mungu mwenye mwili wa kwanza ilikuwa ni wokovu na msamaha wa dhambi za mwanadamu. Sasa ni kazi ya kumshinda na kumpata mwanadamu, ili kwamba Shetani asiweze tena kufanya kazi yake, na atakuwa amepotea kabisa, na Mungu atakuwa ameshinda kabisa. Hii ni kazi ya mwili, na ni kazi inayofanywa na Mungu Mwenyewe.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 122)

Kazi ya awali ya hatua tatu za kazi ya Mungu ilifanywa moja kwa moja na Roho, na wala si mwili. Hata hivyo, kazi ya mwisho ya hatua tatu za kazi ya Mungu, inafanywa na Mungu mwenye mwili, na wala haifanywi moja kwa moja na Roho. Kazi ya ukombozi ya hatua ya katikati pia imefanywa na Mungu mwenye mwili. Katika kazi yote ya usimamizi, kazi muhimu sana ni wokovu kutoka katika ushawishi wa Shetani. Kazi muhimu ni kumshinda kabisa mwanadamu aliyepotoka, na hivyo kurejesha heshima ya awali ya Mungu katika moyo wa mwanadamu, na kumruhusu kufikia maisha ya kawaida, ni sawa na kusema, maisha ya kawaida ya kiumbe wa Mungu. Kazi hii ni muhimu, na ni kiini cha kazi ya usimamizi. Katika hatua tatu za kazi ya wokovu, hatua ya kwanza ya kazi ya Enzi ya Sheria inatofautiana sana na kiini cha kazi ya usimamizi; ilikuwa tu ina kuonekana kwa mbali kwa kazi ya wokovu, na haikuwa mwanzo wa kazi ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu kutoka katika utawala wa Shetani. Hatua ya kwanza ya kazi ilifanywa na Roho kwa sababu, chini ya sheria, mwanadamu alijua tu kuzishika sheria, na hakuwa na ukweli zaidi, na kwa sababu kazi katika Enzi ya Sheria haikujihusisha na kubadilisha tabia ya mwanadamu, sembuse haikuwa inajihusisha na kazi ya jinsi ya kumwokoa mwanadamu kutoka katika utawala wa Shetani. Roho wa Mungu alikamilisha hatua hii rahisi ya kazi ambayo haikujihusisha na tabia iliyopotoka ya mwanadamu. Hatua hii ya kazi ilikuwa na uhusiano mdogo na kiini cha usimamizi na haikuwa na uhusiano mkubwa na kazi rasmi ya wokovu wa mwanadamu, na kwa hivyo haikumhitaji Mungu ili aweze kuifanya kazi Yake. Kazi inayofanywa na Roho ni dhahiri na haifahamiki, na ya kutisha kwa kina isiyofikiwa kwa mwanadamu; Roho hafai kikamilifu kwa ajili ya kufanya kazi ya wokovu moja kwa moja, na hafai kikamilifu kwa ajili ya kumpa mwanadamu uzima moja kwa moja. Kinachomfaa zaidi mwanadamu ni kubadilisha kazi ya Roho na kuwa katika hali ambayo inamkaribia mwanadamu, yaani, kile kinachomfaa mwanadamu zaidi ni Mungu kuwa mtu wa kawaida ili kufanya kazi Yake. Hili linahitaji Mungu apate mwili ili kuchukua kazi ya Roho, na kwa mwanadamu, hakuna njia inayofaa zaidi ya Mungu kufanya kazi. Kati ya hatua hizi tatu za kazi, hatua mbili zinafanywa na mwili, na hatua hizi mbili ni awamu muhimu ya kazi ya usimamizi. Kupata mwili huku kuwili kunakamilishana na kuafikiana. Hatua ya kwanza ya Mungu mwenye mwili iliweka msingi kwa ajili ya hatua ya pili, na tunaweza kusema kwamba kupata mwili huku kuwili kwa Mungu kunafanya hatua moja, na zote hazina ulinganifu. Hatua mbili hizi za kazi ya Mungu zinafanywa na Mungu katika utambulisho Wake katika mwili kwa sababu zina umuhimu sana katika kazi nzima ya usimamizi. Inaweza kusemwa kuwa, bila kazi ya Mungu mwenye mwili katika hatua mbili hizi, kazi nzima ya usimamizi ingefikia kikomo kwa ghafla, na kazi ya kumwokoa mwanadamu isingekuwa kitu isipokuwa maneno matupu. Haijalishi kazi hii ni muhimu au si muhimu lakini imejikita katika mahitaji ya mwanadamu, na uhalisi wa upotovu wa mwanadamu, na uzito wa kutotii kwa Shetani na usumbufu wake katika kazi. Mhusika sahihi ni yule anayeifanya kazi ametabiriwa na asili ya kazi inayofanywa na huyo mfanyakazi, na umuhimu wa kazi. Unapokuja umuhimu wa kazi hii, kwa misingi ya mbinu ya kutumia—kazi inayofanywa moja kwa moja na Roho wa Mungu, au kazi inayofanywa na Mungu mwenye mwili, au kazi inayofanywa kupitia mwanadamu—ya kwanza kuondolewa ni kazi inayofanywa kupitia mwanadamu, na kulingana na asili ya kazi, na asili ya kazi ya Roho dhidi ya ile ya mwili, hatimaye inaamuliwa kwamba kazi inayofanywa na mwili ni ya manufaa zaidi kwa mwanadamu kuliko kazi inayofanywa moja kwa moja na Roho, na inakuwa na manufaa zaidi. Hili ni wazo la Mungu wakati wa kuamua ama kazi ifanywe na Roho au ifanywe na mwili. Kuna umuhimu na msingi katika kila hatua ya kazi. Siyo fikra tu zisizo na msingi, na wala hazifanywi kiholela; kuna hekima fulani ndani yake. Huo ndio ukweli wa kazi zote za Mungu. Hasa, kuna mpango wa Mungu zaidi katika kazi kubwa kama hiyo kwa kuwa Mungu mwenye mwili akifanya kazi miongoni mwa wanadamu. Na kwa hivyo, hekima ya Mungu na uungu Wake wote unaakisiwa katika kila tendo Lake, fikira, na wazo katika kufanya kazi; huu ndio uungu wa Mungu ambao uko imara na wenye mpangilio. Fikira hizi na mawazo ya kutatiza ni ngumu kwa mwanadamu kuwaza, na mambo magumu kwa mwanadamu kuamini, aidha, magumu kwa mwanadamu kuyafahamu. Kazi inayofanywa na mwanadamu ni kulingana na kanuni ya ujumla, ambayo, kwa mwanadamu, ni ya kuridhisha sana. Lakini ikilinganisha na kazi ya Mungu, kuna tofauti kubwa sana; ingawa matendo ya Mungu ni makuu na kazi ya Mungu ni ya kiwango cha juu sana, nyuma yake kuna mipango na mipangilio midogo ya uhakika ambayo haiwezi kufikirika kwa mwanadamu. Kila hatua ya kazi Yake sio kulingana na kanuni tu, lakini pia inajumuisha vitu vingi ambavyo haviwezi kusemwa kwa lugha ya kibinadamu, na haya ni mambo ambayo hayaonekani kwa mwanadamu. Bila kujali kama ni kazi ya Roho au kazi ya Mungu mwenye mwili, kila kazi inajumuisha mpango wa kazi Yake. Hafanyi kazi bila kuwa na msingi, na hafanyi kazi isiyokuwa na maana. Roho anapofanya kazi moja kwa moja, ni kwa malengo Yake, na Anapokuwa mwanadamu (ambayo ni sawa na kusema, Anapobadilisha ganda Lake la nje) kufanya kazi, ni zaidi hata na lengo Lake. Kwa sababu ipi nyingine kwa urahisi Abadilishe utambulisho Wake vivi hivi tu? Kwa sababu ipi nyingine kwa urahisi Abadilike awe mtu ambaye anachukuliwa kuwa ni duni na kuteswa?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 123)

Kazi Yake katika mwili ni ya umuhimu mkubwa, ambao umezungumzwa kuhusiana na kazi, na Yule ambaye hatimaye anahitimisha kazi ni Mungu mwenye mwili, na sio Roho. Baadhi ya watu wanaamini kwamba Mungu wakati fulani anaweza kuja duniani na kumtokea mwanadamu, ambapo Atawahukumu wanadamu wote, akimjaribu mmoja baada ya mwingine bila mtu yeyote kupitwa. Wale wanaofikiri kwa namna hii hawafahamu hatua hii ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Mungu hamhukumu mwanadamu mmoja baada ya mwingine, na hamjaribu mwanadamu mmoja baada ya mwingine; kufanya hivyo hakungekuwa kazi ya hukumu. Je, upotovu wa wanadamu wote si ni sawa? Je, kiini cha wanadamu wote hakifanani? Kinachohukumiwa ni kiini cha mwanadamu kilichopotoka, kiini cha mwanadamu kilichopotoshwa na Shetani, na dhambi zote za mwanadamu. Mungu hahukumu makosa madogo madogo ya mwanadamu na yasiyokuwa na umuhimu. Kazi ya hukumu ni ya uwakilishi, na haifanywi mahususi kwa ajili ya mtu fulani. Badala yake, ni kazi ambayo kwayo kundi la watu wanahukumiwa ili kuiwakilisha hukumu ya wanadamu wote. Kwa Yeye mwenyewe kufanya kazi Yake katika kundi la watu, Mungu mwenye mwili anatumia kazi Yake ili kuwakilisha kazi ya wanadamu wote, ambayo inaenea taratibu. Kazi ya hukumu pia iko hivyo. Mungu hahukumu aina fulani ya mtu au kundi fulani la watu, bali anawahukumu wasio na haki wote miongoni mwa wanadamu—upinzani wa mwanadamu kwa Mungu, kwa mfano, au mwanadamu kutomcha Yeye, au kusababisha usumbufu katika kazi ya Mungu, na kadhalika. Kile kinachohukumiwa ni kiini cha mwanadamu cha kumpinga Mungu, na kazi hii ni kazi ya ushindi ya siku za mwisho. Kazi na neno la Mungu mwenye mwili lililoshuhudiwa na mwanadamu ni kazi ya hukumu mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi wakati wa siku za mwisho, ambacho kilibuniwa na mwanadamu katika kipindi cha siku za nyuma. Kazi ambayo sasa inafanywa na Mungu mwenye mwili ni hukumu yenyewe mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi. Mungu mwenye mwili wa leo ni Yule Mungu anayewahukumu wanadamu wote wakati wa siku za mwisho. Mwili huu na kazi, neno, na tabia Yake yote, vyote ni ujumla Wake. Ingawa mawanda ya kazi Yake ni finyu, na hayahusishi moja kwa moja ulimwengu wote, kiini cha kazi ya hukumu ni hukumu ya moja kwa moja kwa wanadamu wote; si kazi inayofanywa kwa ajili ya watu weteule Uchina tu, au kwa ajili ya idadi ndogo ya watu. Wakati wa kazi ya Mungu mwenye mwili, ingawa mawanda ya kazi hii hayahusishi ulimwengu mzima, inawakilisha kazi ya ulimwengu mzima na, baada ya kuhitimisha kazi ndani ya mawanda ya mwili Wake, Ataipanua kazi hii mara moja katika ulimwengu mzima, kwa namna ile ile, injili ya Yesu ilienea ulimwengu mzima baada ya kufufuka Kwake na kupaa mbinguni. Bila kujali endapo ni kazi ya Roho au ni kazi ya mwili, ni kazi ambayo inafanywa ndani ya mawanda finyu, lakini ambayo inauwakilisha ulimwengu mzima. Wakati wa siku za mwisho, Mungu anaonekana kufanya kazi Yake kwa kutumia utambulisho Wake wa Mungu mwenye mwili, na Mungu mwenye mwili ni Mungu anayemhukumu mwanadamu mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi. Bila kujali endapo ni Roho au mwili, Yule ambaye anafanya kazi ya hukumu ni Mungu anayemhukumu mwanadamu katika siku za mwisho. Hii inafasiliwa kwa kutegemeza kwa kazi Yake, na haifasiliwi kulingana na umbo Lake la nje au sababu nyinginezo. Ingawa mwanadamu ana dhana za maneno haya, hakuna anayeweza kukana ukweli wa hukumu ya Mungu mwenye mwili na kuwashinda wanadamu wote. Bila kujali ni jinsi gani binadamu anafikiri kuuhusu, ukweli ni, baada ya yote, ukweli tu. Hukuna anayeweza kusema “Kazi imefanywa na Mungu lakini mwili si Mungu.” Huu ni upuuzi, maana kazi hii haiwezi kufanywa na mtu yeyote isipokuwa Mungu mwenye mwili. Kwa kuwa kazi hii imekwishakamilika, kufuatia kazi hii, kazi ya hukumu ya Mungu kwa mwanadamu haitatokea kwa mara ya pili; Mungu katika kupata mwili Kwake mara ya pili amekwishaikamilisha kazi yote ya usimamizi, na hakutakuwa na hatua ya nne ya kazi ya Mungu. Kwa sababu yule anayehukumiwa ni mwanadamu, mwanadamu ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa, na sio roho ya Shetani ambayo inahukumiwa moja kwa moja, kazi ya hukumu haifanywi katika ulimwengu wa roho, bali miongoni mwa wanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 124)

Hakuna anayefaa zaidi na anayestahili, kuliko Mungu mwenye mwili kwa ajili ya kuhukumu upotovu wa mwili wa mwanadamu. Ikiwa hukumu ingefanywa moja kwa moja na Roho wa Mungu, basi isingekuwa inajumuisha wote. Aidha, kazi kama hiyo itakuwa vigumu kwa mwanadamu kuikubali, maana Roho hawezi kukutana uso kwa uso na mwanadamu, na kwa sababu hii, matokeo hayawezi kuwa ya haraka, sembuse mwanadamu hataweza kuona kwa uwazi kabisa tabia ya Mungu isiyokosewa. Shetani anaweza tu kushindwa kabisa ikiwa Mungu mwenye mwili anahukumu upotovu wa mwanadamu. Kuwa sawa na mwanadamu akiwa na ubinadamu wa kawaida, Mungu mwenye mwili anaweza kumhukumu mwanadamu asiye na haki; hii ni ishara ya utakatifu Wake wa ndani na hali Yake ya kutokuwa wa kawaida. Ni Mungu pekee ndiye anayestahili, na aliye katika nafasi ya kumhukumu mwanadamu, maana Ana ukweli, na mwenye haki, na kwa hivyo Ana uwezo wa kumhukumu mwanadamu. Wale ambao hawana ukweli na haki hawafai kuwahukumu wengine. Ikiwa kazi hii ingefanywa na Roho wa Mungu, basi usingekuwa ushindi dhidi ya Shetani. Roho kiasili huwa ameinuliwa sana kuliko viumbe wenye mwili wa kufa, na Roho wa Mungu ni mtakatifu kwa asili, na anaushinda mwili. Ikiwa Roho angefanya kazi hii moja kwa moja, Asingeweza kuhukumu kutotii kote kwa mwanadamu, na asingeweza kufichua hali nzima ya mwanadamu ya kutokuwa na haki. Kwa maana kazi ya hukumu pia inafanywa kwa mitazamo ya mwanadamu juu ya Mungu, na mwanadamu hajawahi kuwa na dhana yoyote juu ya Roho, na hivyo Roho hana uwezo wa kufunua hali ya mwanadamu ya kutokuwa na haki, wala kuweza kuweka wazi kabisa hali hiyo ya kutokuwa na haki. Mungu mwenye mwili ni adui wa wale wote wasiomjua. Kupitia kuhukumu dhana za mwanadamu na kumpinga, Anafunua hali yote ya kutotii ya mwanadamu. Matokeo ya kazi Yake katika mwili yapo dhahiri zaidi kuliko yale ya kazi ya Roho. Na hivyo, hukumu ya wanadamu wote haifanywi moja kwa moja na Roho, bali ni kazi ya Mungu mwenye mwili. Mungu mwenye mwili anaweza kuonekana na kuguswa na mwanadamu, na Mungu mwenye mwili anaweza kumshinda kabisa mwanadamu. Katika uhusiano wake na Mungu mwenye mwili, mwanadamu huwa anapiga hatua kutoka katika upinzani na kuwa mtii, kutoka katika mateso na kukubaliwa, kutoka katika mitazamo na kuwa na maarifa, na kutoka kukataliwa hadi upendo. Haya ni matokeo ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Mwanadamu anaokolewa tu kwa kukubali hukumu Yake, bali hatua kwa hatua tu atamwelewa taratibu kupitia neno la mdomo Wake, ametwaliwa na Yeye wakati wa upinzani wake Kwake, na anapata uzima kutoka Kwake wakati wa kukubali kuadibu Kwake. Hii yote ni kazi ya Mungu mwenye mwili, na sio kazi ya Mungu katika utambulisho Wake kama Roho. Kazi inayofanywa na Mungu mwenye mwili ni kazi kubwa sana, na ni kazi ya kina sana, na sehemu muhimu ya hatua tatu za kazi ya Mungu ni hatua mbili za kazi ya kupata mwili. Upotovu wa kina wa mwanadamu ni kikwazo kikubwa sana katika kazi ya Mungu mwenye mwili. Hasa, kazi inayofanywa kwa watu wa siku za mwisho ni ngumu sana, na mazingira ni ya uhasama, na ubora wa tabia ya kila aina ya mwanadamu ni duni sana. Lakini mwishoni mwa kazi hii, bado itapokea matokeo mazuri, bila dosari yoyote; haya ni matokeo ya kazi ya mwili, na matokeo haya yanashawishi sana kuliko kazi ile ya Roho. Hatua tatu za kazi ya Mungu zitahitimishwa katika mwili, na lazima zikamilishwe na Mungu mwenye mwili. Kazi muhimu sana imefanywa katika mwili, na wokovu wa mwanadamu ni lazima ufanywe na Mungu mwenye mwili. Ingawa binadamu wote wanahisi kwamba Mungu katika mwili hahusiani na mwanadamu, kwa kweli ni kuwa mwili huu unahusiana na majaliwa na uwepo wa wanadamu wote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 125)

Kila hatua ya kazi ya Mungu ni kwa ajili ya wanadamu wote, na inawalenga wanadamu wote. Ingawa ni kazi Yake katika mwili, bado inaelekezwa kwa binadamu wote; Yeye ni Mungu wa binadamu wote, na ni Mungu wa viumbe vyote vilivyoumbwa na ambavyo havijaumbwa. Ingawa kazi Yake katika mwili ipo ndani ya mawanda finyu, na kusudi la kazi hii pia lina mipaka, kila wakati Anapokuwa mwili kufanya kazi Yake, Yeye huchagua chombo cha kazi Yake ambacho ni wakilishi na ambacho kina uwakilishi mkubwa; Hachagui kikundi cha watu wa kawaida na wasiosifika kwa ajili ya kuwafanyiza kazi, lakini badala yake huwachagua kama wawakilishi wa kazi Yake kundi la watu wenye uwezo kuwa wawakilishi wa kazi Yake katika mwili. Kundi hili la watu linachaguliwa kwa sababu ya mawanda ya kazi Yake katika mwili ni finyu, na wamejiandaa mahususi kwa ajili ya Kufanyika Kwake kuwa mwili, na limechaguliwa hasa kwa ajili ya kazi Yake katika mwili. Uchaguzi wa Mungu wa walengwa wa kazi Yake si usio na msingi, bali kulingana na kanuni: Mlengwa wa kazi anapaswa kuwa na manufaa katika kazi ya Mungu mwenye mwili, na anapaswa kuwa na uwezo wa kuwawakilisha wanadamu wote. Kwa mfano, Wayahudi waliweza kuwawakilisha binadamu wote katika kupokea wokovu binafsi wa Yesu, na Wachina wanaweza kuwawakilisha wanadamu wote katika kuukubali ushindi binafsi wa Mungu mwenye mwili. Kuna msingi kwa Wayahudi kuwa wawakilishi wa binadamu wote, na kuna msingi kwa uwakilishi wa Wachina wa wanadamu wote katika kuukubali ushindi binafsi wa Mungu. Hakuna kinachofichua maana ya ukombozi kuliko kazi ya ukombozi iliyofanywa miongoni mwa Wayahudi, na hakuna kinachofichua uhakika na mafanikio ya kazi ya ushindi kuliko kazi ya ushindi iliyofanywa miongoni mwa Wachina. Kazi na neno la Mungu mwenye mwili vinaonekana kuelekezwa kwa kikundi kidogo tu cha watu, lakini kwa hakika, kazi Yake miongoni mwa kikundi hiki kidogo ni kazi ya ulimwengu wote, na neno Lake limeelekezwa kwa wanadamu wote. Baada ya kazi Yake katika mwili kufikia kikomo, wale wanaomfuata wataanza kueneza kazi ambayo Amefanya miongoni mwao. Kitu kizuri zaidi kuhusu kazi Yake katika mwili ni kwamba anaweza kuacha maneno sahihi na ushawishi, na mapenzi Yake mahususi kwa mwanadamu kwa wale wanaomfuata, ili kwamba hapo baadaye wafuasi Wake waweze kueneza kazi Yake yote katika mwili kwa usahihi zaidi na kwa udhabiti na mapenzi Yake kwa wanadamu wote kwa wanaoikubali njia hii. Ni kazi ya Mungu mwenye mwili pekee miongoni mwa wanadamu ndiyo inayokamilisha ukweli wa Mungu kuwepo na kuishi pamoja na mwanadamu. Ni kazi hii pekee ndiyo inayotimiza shauku ya mwanadamu kuutazama uso wa Mungu, kushuhudia kazi ya Mungu, na kusikia neno la Mungu. Mungu mwenye mwili anahitimisha enzi ambapo Yehova alionekana mgongo tu, na pia anahitimisha enzi ya mwanadamu kuamini katika Mungu asiye dhahiri. Kwa umahususi, kazi ya Mungu mwenye mwili wa mwisho inawaleta wanadamu wote katika enzi ambayo ni halisi zaidi, ya utendaji zaidi na nzuri zaidi. Hahitimishi tu enzi ya sheria na mafundisho ya kidini; la umuhimu zaidi, Anamfunulia mwanadamu Mungu ambaye ni halisi na wa kawaida ambaye ni mwenye haki na mtakatifu, ambaye anafungua kazi ya mpango wa usimamizi na kuonyesha siri za hatma ya mwanadamu, ambaye alimuumba mwanadamu na kuhitimisha kazi ya usimamizi, na ambaye amebakia sirini kwa maelfu ya miaka. Anaihitimisha enzi ya Mungu asiye yakini, Anaihitimisha enzi ambayo kwayo wanadamu wote wanatamani kuutafuta uso wa Mungu lakini wanashindwa, Anahitimisha enzi ambayo kwayo wanadamu wote wanamtumikia Shetani, na Anawaongoza wanadamu wote katika enzi mpya kabisa. Haya yote ni matokeo ya Mungu mwenye mwili kwa niaba ya Roho wa Mungu. Wakati Mungu anapofanya kazi katika mwili Wake, wale wanaomfuata wanakuwa hawatafuti tena vitu hivyo ambavyo vinaonekana kuishi na kutoishio, na wao wanaacha kukisia mapenzi ya Mungu asiye yakini. Mungu anapoeneza kazi Yake katika mwili, wale wanaomfuata wataieneza kazi ambayo Ameifanya katika mwili kwa dini na madhehebu yote, na watazungumza maneno Yake yote katika masikio ya wanadamu wote. Yote yale yanayosikizwa na wale wanaoipokea injili Yake yatakuwa ni ukweli wa kazi Yake, yatakuwa mambo ambayo mwanadamu ameyashuhudia na kuyaona binafsi, na utakuwa ukweli na sio uvumi. Ukweli huu ni ushahidi ambao Anauenezea kazi na pia ni zana ambazo Anazitumia katika kueneza kazi. Bila uwepo wa ukweli, injili Yake isingeweza kuenea katika nchi zote na maeneo yote; bila ukweli bali kwa fikira tu za mwanadamu, Asingeweza kufanya kazi ya kuushinda ulimwengu wote. Roho hagusiki na mwanadamu, na wala haonekani kuonekana na mwanadamu, na kazi ya Roho haiwezi kuacha ushahidi au ukweli wowote zaidi wa kazi ya Mungu kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu kamwe hataweza kuuona uso halisi wa Mungu, na siku zote ataamini katika Mungu asiye yakini ambaye hayupo. Mwanadamu hataweza kuutazama uso wa Mungu, hataweza kusikia maneno yaliyozungumzwa na Mungu moja kwa moja. Mawazo ya mwanadamu, hata hivyo, ni matupu, na hayawezi kuchukua nafasi ya uso halisi wa Mungu; tabia ya asili ya Mungu, na kazi ya Mungu Mwenyewe haiwezi kuigwa na mwanadamu. Mungu wa mbinguni asiyeonekana na kazi Yake inaweza kuletwa tu duniani na Mungu mwenye mwili ambaye binafsi Anafanya kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Hii ndiyo njia halisi ambayo Mungu anaonekana kwa mwanadamu, ambayo kwayo mwanadamu anamwona Mungu na kuujua uso wa kweli wa Mungu, na haiwezi kufanikishwa na Mungu asiyekuwa katika mwili. Baada ya Mungu kufanya kazi Yake hadi hatua hii, kazi Yake tayari imeshafanikiwa kuwa na matokeo mazuri, na imekuwa ni mafanikio kamili. Kazi binafsi ya Mungu mwenye mwili tayari imekwishakamilisha asilimia tisini ya kazi ya usimamizi Wake mzima. Mwili umetoa mwanzo mzuri katika kazi Yake yote, na muhtasari kwa ajili ya kazi Yake yote, na umetangaza kazi Yake yote na Ameifanya ya mwisho kupitia ujazaji tena wa kazi hii yote. Kuanzia sasa, hakutakuwepo na Mungu mwingine katika mwili kwa ajili ya kufanya hatua ya nne ya kazi ya Mungu, na hakutakuwa na kazi ya miujiza zaidi ya kupata mwili kwa tatu kwa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 126)

Kila hatua ya kazi ya Mungu katika mwili inawakilisha kazi Yake ya enzi yote, na haiwakilishi kipindi fulani kama kazi ya mwanadamu. Na hivyo mwisho wa kazi ya kufanyika Kwake mwili mara ya mwisho haimaanishi kwamba kazi Yake imefikia mwisho kabisa, kwa maana kazi Yake katika mwili inawakilisha enzi yote, na haiwakilishi kipindi tu ambacho Anafanya kazi Yake katika mwili tu. Ni kwamba tu Anakamilisha kazi Yake ya enzi yote wakati ambapo yupo katika mwili, ambayo baadaye inaenea sehemu zote. Baada ya Mungu mwenye mwili kutimiza huduma yake, atawakabidhi wale wote wanaoifuata kazi Yake ya baadaye. Kwa njia hii kazi Yake ya enzi yote itaendelezwa bila kusitishwa. Kazi ya enzi yote ya kufanyika kuwa mwili itachukuliwa tu kuwa imekamilika baada ya kuenea ulimwenguni kote. Kazi ya Mungu mwenye mwili huanzisha enzi mpya, na wale wanaoiendeleza kazi Yake ni watu wanaotumiwa naye. Kazi inayofanywa na mwanadamu yote ipo ndani ya huduma ya Mungu mwenye mwili, na haina uwezo wa kwenda zaidi ya mawanda haya. Ikiwa Mungu mwenye mwili haji kufanya kazi Yake, mwanadamu hana uwezo wa kuhitimisha enzi ya zamani, na hana uwezo wa kuikaribisha enzi mpya. Kazi inayofanywa na mwanadamu ipo tu ndani ya wajibu wake ambao unawezekana kibinadamu, na haiwakilishi kazi ya Mungu. Ni Mungu mwenye mwili pekee ndiye anayeweza kuja na kukamilisha kazi ambayo Anapaswa kuifanya, na mbali na Yeye, hakuna anayeweza kuifanya kazi hii badala Yake. Bila shaka, kile Ninachozungumzia ni kuhusiana na kazi ya kufanyika mwili. Huyu Mungu mwenye mwili, kwanza anachukua hatua ya kazi ambayo haipatani na mitazamo ya mwanadamu, baada ya hapo Anafanya kazi zaidi ambayo haipatani na mitazamo ya mwanadamu. Lengo la kazi hii ni kumshinda mwanadamu. Kwa upande mmoja, kupata mwili kwa Mungu hakupatani na dhana za mwanadamu, aidha, Anafanya kazi zaidi ambayo haipatani na dhana za mwanadamu, na kwa hivyo mwanadamu anakuza mawazo zaidi ya kukosoa kumhusu. Anafanya kazi ya ushindi miongoni mwa wanadamu ambaye ana dhana nyingi sana kumhusu. Bila kujali jinsi wanavyomchukulia, Atakapokuwa amekamilisha huduma Yake, wanadamu wote watakuwa chini ya utawala Wake. Ukweli wa kazi hii hauonekani tu miongoni mwa Wachina, bali wao wanawakilisha namna ambavyo wanadamu wote watakavyoshindwa. Matokeo yanayoonekana kwa watu hawa ni kitangulizi cha matokeo yatakayoonekana kwa wanadamu wote, na matokeo ya kazi Anayofanya wakati ujao yatazidi sana matokeo kwa watu hawa. Kazi ya Mungu katika mwili haihusishi mshindo mkubwa wa tarumbeta, wala imefunikwa katika maficho. Ni halisi na ya kweli, na ni kazi ambayo moja kujumlisha na moja ni sawa sawa na mbili. Hajafichwa kwa mtu yeyote, na wala haimdanganyi mtu yeyote. Kile ambacho watu wanaona ni vitu halisi, na kile ambacho mwanadamu anapata ni ukweli halisi na maarifa. Kazi itakapokamilika, mwanadamu atakuwa na maarifa mapya juu Yake, na wale ambao kweli wanamtafuta Mungu hawatakuwa na dhana zozote juu Yake. Haya siyo tu matokeo ya kazi Yake kwa Wachina, lakini pia inawakilisha matokeo ya kazi Yake katika kuwashinda wanadamu wote, kwa maana hakuna kitu ambacho ni cha manufaa zaidi katika kazi ya kuwashinda watu kuliko mwili huu, na kazi ya mwili huu, na kila kitu cha mwili huu. Vina manufaa katika kazi Yake leo, na vina manufaa katika kazi Yake hapo baadaye. Mwili huu utawashinda wanadamu wote na utawapata wanadamu wote. Hakuna kazi bora zaidi ambayo kwayo wanadamu wote watamwona Mungu, na kumtii Mungu, na kumfahamu Mungu. Kazi inayofanywa na mwanadamu inawakilisha tu mawanda finyu, na Mungu anapofanya kazi Yake hazungumzi na watu fulani, bali Anazungumza na wanadamu wote, na wale wote wanaoikubali kazi Yake. Mwisho Anaoutangaza ni mwisho wa wanadamu wote, na sio mwisho wa mtu fulani tu. Hamtendei mtu yeyote kwa umahususi, wala hampendelei mtu yeyote, na Anafanya kazi kwa ajili ya, na Anazungumza na wanadamu wote. Na kwa hiyo Mungu huyu katika mwili amekwisha waainisha wanadamu wote kulingana na aina yao, tayari amekwisha wauhukumu wanadamu wote, na amekwishapangilia hatima inayofaa kwa wanadamu wote. Ingawa Mungu anafanya kazi Yake China tu, kwa hakika Ameshaamua kazi ya ulimwengu mzima. Hawezi kusubiri hadi kazi Yake itakapoenea miongoni mwa wanadamu wote kabla ya kutoa matamko Yake na kuweka mipango hatua kwa hatua. Hivyo, sio kwamba utakuwa umechelewa sana? Sasa Anaweza kabisa kukamilisha kazi ya wakati ujao kabla ya wakati huo. Kwa sababu Yule anayefanya kazi ni Mungu mwenye mwili, Anafanya kazi isiyokuwa na mipaka ndani ya mawanda yenye mipaka, na baadaye Atamfanya mwanadamu atekeleze jukumu ambalo mwanadamu anapaswa kulitekeleza; hii ni kanuni ya kazi Yake. Anaweza kuishi tu na mwanadamu kwa muda, na hawezi kuambatana na mwanadamu hadi kazi ya enzi zote itakapokamilika. Ni kwa sababu Yeye ni Mungu kwamba Yeye hutabiri kazi Yake ya Wakati ujao kabla ya wakati. Baada ya hapo, Atawaainisha wanadamu wote kulingana na aina kwa maneno Yake, na mwanadamu ataingia katika kazi Yake ya hatua kwa hatua kulingana na neno Lake. Hakuna atakayekwepa, na wote wanapaswa kutenda kulingana na hili. Hivyo, katika wakati ujao, enzi itaongozwa na maneno Yake, na sio kuongozwa na Roho.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 127)

Mwili wa mwanadamu umepotoshwa na Shetani, na wengi wamepofushwa, na kuumizwa sana. Sababu muhimu sana ambayo inamfanya Mungu kufanya kazi katika mwili ni kwa sababu mlengwa wa wokovu Wake ni mwanadamu, ambaye ni wa mwili, na kwa sababu Shetani pia anatumia mwili wa mwanadamu kusumbua kazi ya Mungu. Vita na Shetani kwa hakika ni kazi ya kumshinda mwanadamu, na wakati uo huo mwanadamu pia ni mlengwa wa wokovu wa Mungu. Kwa njia hii, kazi ya Mungu mwenye mwili ni muhimu. Shetani aliupotosha mwili wa mwanadamu, na mwanadamu akawa mfano halisi wa Shetani, na akawa mlengwa wa kushindwa na Mungu. Kwa njia hii, kazi ya kupambana na Shetani na kumwokoa mwanadamu inatokea duniani, na Mungu ni lazima awe mwanadamu ili aweze kupambana na mwanadamu. Hii ni kazi yenye utendaji wa hali ya juu. Mungu anapofanya kazi katika mwili, kwa hakika Anapambana na Shetani katika mwili. Anapofanya kazi katika mwili, Anafanya kazi Yake katika ulimwengu wa kiroho, na Anafanya kazi Yake yote katika ufalme wa kiroho ili iwe halisi duniani. Anayeshindaniwa ni mwanadamu, asiye mtiifu Kwake, yule anayeshindwa ni mfano halisi wa Shetani (bila shaka, huyu pia ni mwanadamu), ambaye ana uadui na Yeye, na ambaye ataokolewa hatimaye ni mwanadamu. Kwa namna hii, ni muhimu zaidi Kwake kuwa mwanadamu ambaye ana ganda la nje la kiumbe, ili kwamba Awe na uwezo wa kupambana na Shetani katika uhalisi, kumshinda mwanadamu, ambaye si mtiifu Kwake na ambaye ana kuonekana kwa nje ambako kunafanana na Yeye, na kumwokoa mwanadamu, ambaye ana umbo la nje kama Lake na aliyeumizwa na Shetani. Adui Wake ni mwanadamu, mlengwa wa ushindi Wake ni mwanadamu, na mlengwa wa wokovu Wake ni mwanadamu, aliyeumbwa na Yeye. Hivyo ni lazima Awe mwanadamu, na kwa njia hii, kazi Yake inakuwa rahisi zaidi. Ana uwezo wa kumshinda Shetani na kumshinda mwanadamu, aidha, anaweza kumwokoa mwanadamu. Ingawa mwili huu ni wa kawaida na halisi, Yeye si mwili wa kawaida. Yeye si mwili ambao ni mwanadamu tu, bali mwili ambao una uanadamu na uungu. Hii ndiyo tofauti Yake na mwanadamu, na ni alama ya utambulisho wa Mungu. Ni mwili tu kama huu ndio unaweza kufanya kazi Anayokusudia kufanya, na kutimiza huduma ya Mungu katika mwili, na kukamilisha kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Isingekuwa hivyo, kazi Yake miongoni mwa wanadamu ingekuwa tupu na yenye dosari. Ingawa Mungu anaweza kupambana na roho wa Shetani na kuibuka mshindi, asili ya zamani ya mwanadamu aliyepotoka haiwezi kuondolewa, na wale ambao sio watiifu Kwake na wanaompinga hawawezi kuwa wahusika katika utawala Wake, ambayo kusema, Hawezi kamwe kumshinda mwanadamu, na hawezi kamwe kuwapata wanadamu wote. Kama kazi Yake duniani haiwezi kutatuliwa, basi usimamizi Wake hautafika mwisho, na wanadamu wote hawataweza kuingia katika pumziko. Kama Mungu hawezi kuingia katika pumziko pamoja na viumbe Wake wote, basi hakutakuwa na matokeo ya usimamizi huo, na utukufu wa Mungu kwa sababu hiyo utatoweka. Ingawa mwili Wake hauna mamlaka, kazi Anayofanya itapokea matokeo yake. Huu ndio mwelekeo usioepukika wa kazi Yake. Haijalishi kama mwili Wake una mamlaka au la, maadamu Ana uwezo wa kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe, basi Yeye ni Mungu Mwenyewe. Haijalishi mwili huu ni wa kawaida kiasi gani, Anaweza kufanya kazi Anayopaswa kufanya, maana mwili huu ni Mungu na wala si mwanadamu tu. Sababu ambayo mwili huu unaweza kufanya kazi ambayo mwanadamu hawezi kufanya ni kwamba kiini Chake cha ndani si kama cha mwanadamu yeyote yule, na sababu kuwa Anaweza kumwokoa mwanadamu ni kuwa utambulisho Wake ni tofauti na wa mwanadamu yeyote yule. Mwili huu ni muhimu sana kwa mwanadamu kwa sababu ni mwanadamu hata zaidi ni Mungu, kwa sababu Anaweza kufanya kazi ambayo hakuna mwanadamu wa kawaida anayeweza kufanya, na kwa sababu Anaweza kumwokoa mwanadamu aliyepotoka, ambaye anaishi pamoja na Yeye duniani. Ingawa Anafanana na mwanadamu, Mungu mwenye mwili ni wa muhimu sana kwa mwanadamu kuliko mtu yeyote wa thamani, kwa maana Anaweza kufanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na Roho wa Mungu, ni mwenye uwezo zaidi kuliko Roho wa Mungu kuwa na ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe, na ni mwenye uwezo zaidi kuliko Roho wa Mungu kuweza kumpata mwanadamu kabisa. Kwa sababu hii, ingawa mwili huu ni wa kawaida, mchango Wake kwa wanadamu na umuhimu Wake katika uwepo wa mwanadamu kunamfanya Awe wa thamani zaidi, na thamani halisi na umuhimu wa mwili huu hauwezi kupimwa na mwanadamu yeyote. Ingawa mwili huu hauwezi kumwangamiza Shetani moja kwa moja, Anaweza kutumia kazi Yake kumshinda mwanadamu na kumshinda Shetani, na kumfanya Shetani kutii kikamilifu katika utawala Wake. Ni kwa sababu Mungu amepata mwili ili kwamba Aweze kumshinda Shetani na aweze kumwokoa binadamu. Hamwangamizi Shetani moja kwa moja, bali Anakuwa mwili ili kuweza kufanya kazi ya kumshinda binadamu, ambaye amepotoshwa na Shetani. Kwa njia hii, Anakuwa na uwezo zaidi wa kuwa ushuhuda Kwake Mwenyewe miongoni mwa viumbe, na Anakuwa na uwezo zaidi wa kumwokoa mwanadamu aliyepotea. Ushindi wa Mungu mwenye mwili dhidi ya Shetani unabeba ushuhuda mkubwa, na una ushawishi mkubwa, kuliko uangamizaji wa Shetani wa moja kwa moja na Roho wa Mungu. Mungu katika mwili Ana uwezo zaidi wa kumsaidia mwanadamu kumjua Muumba, na Ana uwezo zaidi wa kuwa na ushuhuda Wake mwenyewe miongoni mwa viumbe.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 128)

Mungu amekuja duniani kufanya kazi Yake miongoni mwa watu, kujifichua Mwenyewe kwa mwanadamu na kumruhusu mwanadamu kumtazamia; je, hili ni jambo dogo? Kwa kweli ni kuu! Si kama jinsi mwanadamu anavyofikiria kwamba Mungu amekuja ili mwanadamu aweze kumtazamia, ili mwanadamu aweze kuelewa kwamba Mungu ni wa ukweli na wala si yule asiye yakini ama mtupu, na ya kuwa Mungu ni wa fahari lakini pia mnyenyekevu. Je, inawezekana kuwa rahisi hivyo? Ni hasa kwa sababu Shetani amepotosha mwili wa mwanadamu, na mwanadamu ndiye Mungu anakusudia kuokoa, ya kuwa Mungu ni sharti achukue mwili ili afanye vita na Shetani na amchunge mwanadamu binafsi. Hii pekee ndiyo yenye manufaa kwa kazi Yake. Miili hiyo miwili ya Mungu ya nyama imekuwepo ili kumshinda Shetani, na pia imekuwepo ili imuokoe mwanadamu kwa njia bora zaidi. Hilo ni kwa sababu yule anayefanya vita na Shetani anaweza tu kuwa Mungu, awe ni Roho wa Mungu au ni mwili wenye nyama wa Mungu. Kwa kifupi, yule anayefanya vita na Shetani hawezi kuwa ni malaika, sembuse kuwa mwanadamu, ambaye amepotoshwa na Shetani. Malaika hawana uwezo wa kuifanya, na mwanadamu ni dhaifu hata zaidi. Kwa hivyo, ikiwa Mungu anataka kufanyia kazi maisha ya mwanadamu, kama Yeye anataka kuja duniani binafsi kumwokoa mwanadamu, basi ni lazima Yeye binafsi apate mwili—yaani, lazima Yeye binafsi achukue mwili, na kwa utambulisho Wake wa asili na kazi ambayo ni lazima afanye, aje miongoni mwa wanadamu na kumwokoa mwanadamu binafsi. La sivyo, kama ingekuwa ni Roho wa Mungu au mwanadamu ndiye aliyefanya kazi hii, basi vita hivi daima vingeshindwa kutimiza matokeo yake, na kamwe havingekwisha. Wakati tu Mungu anapata mwili ili Yeye binafsi aende kwa vita dhidi ya Shetani miongoni mwa watu ndipo mwanadamu anapata nafasi ya wokovu. Aidha, hapo tu ndipo Shetani anaaibishwa, na kuwachwa bila nafasi zozote za kutumia au mipango yoyote ya kutekeleza. Kazi inayofanywa na Mungu aliyepata mwili haiwezi kutimizwa na Roho wa Mungu, na hata zaidi haiwezi kufanywa na mtu yeyote mwenye mwili kwa niaba ya Mungu, kwa kuwa kazi ambayo Yeye hufanya ni kwa ajili ya maisha ya mwanadamu, na ili kubadilisha tabia potovu ya mwanadamu. Kama mwanadamu angeshiriki katika vita hivi, yeye angekimbia tu kwa vurugu ya huzuni, na hangekuwa na uwezo kabisa wa kubadilisha tabia potovu ya mwanadamu. Angekuwa hana uwezo wa kumwokoa mwanadamu kutoka msalabani, ama wa kushinda wanadamu wote waasi, lakini angeweza tu kufanya kazi kidogo ya zamani ambayo haiendi zaidi ya kanuni, au vinginevyo kazi ambayo haihusiani na kushindwa kwa Shetani. Kwa hivyo, mbona ujisumbue? Kuna umuhimu gani wa kazi ambayo haiwezi kuwapata wanadamu, sembuse kumshinda Shetani? Na kwa hivyo, vita dhidi ya Shetani vinaweza kufanywa tu na Mungu Mwenyewe, na itakuwa tu vigumu kwa mwanadamu kupigana vita hivyo. Wajibu wa mwanadamu ni kutii na kufuata, kwa kuwa mwanadamu hana uwezo wa kufanya kazi kama vile kuumba mbingu na dunia, wala, zaidi ya hayo, hawezi kutekeleza kazi ya kupigana na Shetani. Mwanadamu anaweza tu kumtosheleza Muumba chini ya uongozi wa Mungu Mwenyewe, ambapo Shetani hushindiwa; hili ndilo jambo pekee ambalo mwanadamu anaweza kulitenda. Na kwa hivyo, kila wakati vita vipya vinapoanza, kila wakati kazi ya enzi mpya inapoanza, kazi hii inafanywa na Mungu binafsi, ambapo kupitia kazi hiyo Yeye huongoza enzi nzima, na kufungua njia mpya kwa ajili ya wanadamu wote. Pambazuko la kila enzi mpya ni mwanzo mpya katika vita na Shetani, ambapo kupitia hiyo mwanadamu anaingia akiwa mpya zaidi, ulimwengu wa kupendeza zaidi na enzi mpya ambayo inaongozwa na Mungu Mwenyewe. Mwanadamu ni bwana wa vitu vyote, lakini wote ambao wamepatwa watakuwa matunda ya vita dhidi ya Shetani. Shetani ndiye mpotoshaji wa vitu vyote, na ndiye mshindwa katika mwisho wa vita vyote, na pia ndiye atakayeadhibiwa kufuatia vita hivi. Miongoni mwa Mungu, mwanadamu na Shetani, ni Shetani pekee ndiye atachukiwa na kukataliwa. Wale waliopatwa na Shetani lakini hawarejeshwi na Mungu, wakati huo huo, watakuwa wale ambao watapokea adhabu kwa niaba ya Shetani. Kati ya hawa watatu, Mungu pekee ndiye anapaswa kuabudiwa na vitu vyote. Wale waliopotoshwa na Shetani lakini wanarejeshwa na Mungu na wale wanaofuata njia ya Mungu, wakati huo huo, wanakuwa wale ambao watapokea ahadi ya Mungu na kuhukumu wale waovu kwa niaba ya Mungu. Bila shaka Mungu atakuwa mshindi na Shetani bila shaka atashindwa, lakini miongoni mwa wanadamu kuna wale watakaoshinda na wale watakaoshindwa. Wale ambao watashinda ni wa washindi, na wale ambao watashindwa ni wale wa washindwa; huu ni uainishaji wa kila mmoja kufuatana na aina, na ni hitimisho la mwisho la kazi yote ya Mungu. Pia ni lengo la kazi yote ya Mungu, na kamwe haitabadilika. Msingi wa kazi kuu wa mpango wa usimamizi wa Mungu unalenga wokovu wa mwanadamu, na Mungu anakuwa mwili kimsingi kwa ajili ya msingi huu, kwa ajili ya kazi hii, na ili kumshinda Shetani. Mara ya kwanza Mungu kuwa mwili ilikuwa ili kumshinda Shetani: Yeye binafsi akawa mwili, na akasulubiwa msalabani binafsi, ili kukamilisha kazi ya vita vya kwanza, ambayo ilikuwa kazi ya ukombozi wa mwanadamu. Aidha, awamu hii ya kazi ilifanywa na Mungu binafsi, ambaye amekuwa mwili ili kufanya kazi yake miongoni mwa wanadamu, ili kusema neno lake binafsi na kumwezesha mwanadamu kumwona. Bila shaka, ni hakika kwamba Yeye hufanya kazi nyingine njiani, lakini sababu kuu ya kufanya kazi yake binafsi ni ili kumshinda Shetani, kushinda wanadamu wote, na kuwapata hawa watu. Na kwa hivyo, kazi ya Mungu kuwa na mwili ni jambo kuu kweli. Kama kusudi lake lilikuwa tu kumwonyesha mwanadamu kuwa Mungu ni mnyenyekevu na aliyefichika, na kuwa Mungu ni wa ukweli, kama ingelikuwa ni kwa ajili ya kufanya kazi hii, basi hakungekuwa na haja ya kuwa mwili. Hata kama Mungu hakuwa mwili, yeye angefichua unyenyekevu na usiri wake, ukuu wake na utakatifu, kwa mwanadamu moja kwa moja, lakini mambo kama hayo hayana uhusiano wowote na usimamizi wa mwanadamu. Mambo kama hayo hayana uwezo wa kumwokoa mwanadamu au kumfanya awe kamili, na hata hayawezi kumshinda Shetani. Kama kushindwa kwa Shetani kungehusisha Roho tu akipigana vita dhidi ya roho, basi kazi kama hii ingekuwa na thamani ndogo ya ukweli; haingeweza kumpata mwanadamu na ingeharibu hatima na matarajio ya mwanadamu. Kwa hivyo, kazi ya Mungu leo ni moja ambayo ina umuhimu kupindukia. Sio hivyo ili kwamba mwanadamu aweze kumwona, au ili macho ya mwanadamu yaweze kufunguliwa, au ili ampe msukumo kiasi na kutiwa moyo; kazi kama hii haina umuhimu. Kama unaweza tu kuongea kwa hekima ya sampuli hii, basi inathibitisha kuwa wewe haujui umuhimu wa ukweli wa Mungu kupata mwili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 129)

Kila hatua ya kazi iliyofanywa na Mungu ina umuhimu wake mkubwa. Yesu alipokuja zamani, Alikuwa mwanaume, lakini Mungu anapokuja wakati huu Yeye ni mwanamke. Kutokana na hili, unaweza kuona kwamba Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke kwa ajili ya kazi Yake na Kwake hakuna tofauti ya jinsia. Roho Wake anapowasili, Anaweza kuchukua mwili wowote kwa matakwa Yake na mwili huo unaweza kumwakilisha Yeye. Uwe wa kiume au kike, unaweza kumwakilisha Mungu alimradi tu ni mwili Wake wa nyama. Kama Yesu angeonekana kama kike alipokuja, kwa maneno mengine, iwapo mtoto wa kike, sio wa kiume, angezaliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu, hatua hiyo ya kazi ingekuwa imekamilika pia. Kama hali ingekuwa hivyo, basi hatua ya leo ya kazi ingelazimika kukamilishwa badala yake na mwanaume, lakini kazi ingekamilika pia. Kazi inayofanywa katika hatua hizi zote ni muhimu kwa kiwango sawa; hakuna hatua yoyote ya kazi inayojirudia au kupingana na nyingine. Wakati huo, Yesu alipokuwa akifanya kazi Yake aliitwa Mwana wa pekee, na “Mwana” inaashiria jinsia ya kiume. Basi kwa nini Mwana wa pekee halikutajwa katika hatua hii? Hii ni kwa sababu mahitaji ya kazi yamelazimisha badiliko la jinsia ambayo ni tofauti na ile ya Yesu. Kwa Mungu hakuna tofauti ya jinsia. Kazi Yake inafanywa kama Anavyotaka na katika kufanya kazi Yake hazuiliwi na kitu chochote kile, lakini hasa yupo huru. Hata hivyo, kila hatua ya kazi ina umuhimu wake mkubwa. Mungu alipata mwili mara mbili, na ni dhahiri kwamba kupata mwili Kwake katika siku za mwisho ni mara ya mwisho. Amekuja kufichua matendo Yake yote. Ikiwa katika hatua hii Hakupata mwili ili Yeye binafsi afanye kazi kwa ajili ya mwanadamu kushuhudia, mwanadamu milele angeshikilia fikra kwamba Mungu ni wa kuime tu, na si wa kike. Kabla ya hili, wanadamu wote waliamini kwamba Mungu angeweza kuwa tu mwanaume na kwamba mwanamke hawezi kuitwa Mungu, maana wanadamu wote walimchukulia mwanamume kuwa na mamlaka juu ya mwanamke. Waliamini kwamba hakuna mwanamke anayeweza kuchukua mamlaka, bali ni mwanamume tu. Aidha hata walisema kwamba mwanamume alikuwa ni mkuu wa mwanamke na kwamba mwanamke anapaswa kumtii mwanaume na asimshinde. Iliposemwa hapo nyuma kwamba mwanamume alikuwa mkuu wa mwanamke, ilielekezwa kwa Adamu na Hawa ambao walikuwa wamedanganywa na yule nyoka, na wala sio kwa mwanamume na mwanamke kama walivyoumbwa na Yehova hapo mwanzo. Bila shaka, mwanamke anapaswa kumtii na kumpenda mume wake, na mume anapaswa kujifunza kuilisha na kuiruzuku familia yake. Hizi ni sheria na kanuni zilizowekwa na Yehova ambazo kwazo wanadamu wanapaswa kuzifuata katika maisha yao ya hapa duniani. Yehova alimwambia mwanamke “Ashiki yako itakuwa kwa mume wako, na atatawala juu yako.” Alisema hivyo tu ili kwamba wanadamu (yaani, mwanamume na mwanamke) waweze kuishi maisha ya kawaida chini ya utawala wa Yehova, na tu ili kwamba maisha ya wanadamu yaweze kuwa na mfumo na yasipoteze mwelekeo. Kwa hivyo, Yehova alitengeneza kanuni zinazofaa ya namna ambavyo mwanamume na mwanamke wanavyopaswa kutenda, lakini hili lilihusu tu viumbe wote wanaoishi duniani na halikuhusiana na mwili wa Mungu wa nyama. Inawezekanaje Mungu awe sawa na viumbe Wake? Maneno Yake yalielekezwa tu kwa wanadamu wa viumbe Wake; Alianzishia mwanamume na mwanamke kanuni ili wanadamu waweze kuishi maisha ya kawaida. Hapo mwanzo, Yehova alipoumba wanadamu, Aliwaumba wanadamu wa aina mbili, mwanamume na mwanamke; na kwa hiyo, kuna mgawanyo wa kike na kiume katika miili Yake. Hakuamua juu ya kazi Yake kulingana na maneno aliyozungumza kwa Adamu na Hawa. Mara mbili Alipopata mwili kuliamuliwa kwa kuzingatia kabisa mawazo Yake alipowaumba wanadamu kwa mara ya kwanza, yaani, Alikamilisha kazi ya kupata Kwake mwili mara mbili, kwa msingi wa mwanamke na mwanamume kabla ya wao kupotoshwa. Ikiwa wanadamu wangechukua maneno yaliyozungumzwa na Yehova kwa Adamu na Hawa, ambao walikuwa wamedanganywa na yule nyoka, na kuyatumia katika kazi ya mwili wa Mungu, je, si Yesu pia angepaswa kumpenda mke Wake kama Alivyotakiwa? Je, kwa njia hii, Mungu bado ni Mungu? Na ikiwa ni hivyo, je, bado Angeweza kukamilisha kazi Yake? Ikiwa ni vibaya kwa mwili wa Mungu kuwa mwanamke, je, basi lisingekuwa kosa kubwa sana pia kwa Mungu kumuumba mwanamke? Ikiwa mwanadamu bado anaamini kwamba Mungu kupata mwili kama mwanamke ni vibaya, je, basi Yesu, ambaye hakuoa na hivyo hakuweza kumpenda mke Wake, angekuwa na makosa kama kupata mwili wa sasa? Kwa kuwa unatumia maneno yaliyozungumzwa na Yehova kwa Hawa ili kupima ukweli wa Mungu kupata mwili leo, basi unapaswa kutumia maneno ya Yehova kwa Adamu kumhukumu Bwana Yesu ambaye alipata mwili katika Enzi ya Neema. Je, hawa wawili sio sawa? Kwa kuwa unampima Bwana Yesu kulingana na mwanamume ambaye hakuwa amedanganywa na yule nyoka, basi hupaswi kuhukumu ukweli wa kupata mwili leo hii kulingana na mwanamke ambaye alikuwa amedanganywa na yule nyoka. Hili si haki! Ikiwa umefanya hukumu ya namna hiyo, inathibitisha kukosa urazini kwako. Yehova alipopata mwili mara mbili, jinsia ya mwili Wake ilikuwa inahusiana na mwanamume na mwanamke ambaye hakuwa amedanganywa na yule nyoka; Alipata mwili mara mbili kulingana na mwanamume na mwanamke ambaye hakuwa amedanganywa na yule nyoka. Usifikiri kwamba uanaume wa Yesu ulikuwa sawa na uanaume wa Adamu ambaye alidanganywa na yule nyoka. Hahusiani naye kabisa, na ni wanaume wawili wa asili tofauti. Hakika haiwezi kuwa kwamba uanaume wa Yesu unathibitisha Yeye ni mkuu wa wanawake wote lakini sio mkuu wa wanaume wote? Je, Yeye si Mfalme wa Wayahudi wote (ikiwa ni pamoja na wanaume na wanawake)? Yeye ni Mungu Mwenyewe, sio tu mkuu wa mwanamke bali mkuu wa mwanamume pia. Yeye ni Bwana wa viumbe vyote, na mkuu wa viumbe vyote. Unawezaje kuamua uanaume wa Yesu kuwa ishara ya mkuu wa mwanamke? Huku si kukufuru? Yesu ni mwanamume ambaye hajapotoshwa. Yeye ni Mungu; Yeye ni Kristo; Yeye ni Bwana. Anawezaje kuwa mwanamume kama Adamu ambaye alipotoshwa? Yesu ni mwili uliovaliwa na Roho wa Mungu aliye mtakatifu sana. Unawezaje kusema kuwa Yeye ni Mungu aliye na uanaume wa Adamu? Kama ni hivyo, kazi yote ya Mungu haingekuwa si sahihi? Je, Yehova angeweza kuuweka ndani ya Yesu uanaume wa Adamu ambaye alidanganywa na yule nyoka? Je, si kupata mwili kwa wakati huu ni tukio jingine la kazi ya Mungu mwenye mwili ambaye ni tofauti kijinsia na Yesu lakini aliye kama Yeye katika asili? Bado unathubutu kusema kwamba Mungu mwenye mwili hawezi kuwa mwanamke kwa kuwa mwanamke ndiye aliyedanganywa kwanza na yule nyoka? Bado unathubutu kusema kwamba, kwa kuwa mwanamke ndiye mwenye najisi sana na ni chanzo cha upotovu wa wanadamu, Mungu hawezi kabisa kupata mwili kama mwanamke? Bado unathubutu kuendelea kusema kwamba “mwanamke siku zote atamtii mwanamume na hawezi kamwe kudhihirisha au kumwakilisha Mungu moja kwa moja”? Hukuelewa hapo nyuma; lakini sasa bado unaweza kuendelea kukufuru kazi ya Mungu, hususan mwili wa nyama wa Mungu? Kama huwezi kuona hili kwa uwazi kabisa, ni vizuri zaidi ukawa makini na ulimi wako, la sivyo upumbavu na ujinga wako ufichuliwe na ubaya wako uwekwe wazi. Usidhani kwamba unaelewa kila kitu. Nakueleza kwamba yote uliyokwishayaona na kuyapitia hayakutoshelezi wewe kuelewa hata sehemu ndogo kabisa ya mpango Wangu wa usimamizi. Hivyo kwa nini basi unakuwa mwenye kiburi sana? Talanta ndogo hiyo uliyonayo na maarifa kidogo hayo uliyonayo hayatoshelezi kutumika na Yesu hata katika sekunde moja ya kazi Yake! Je, una uzoefu kiasi gani hasa? Yale uliyoyaona na yote uliyoyasikia katika maisha yako yote na yale uliyoyafikiria ni kidogo kuliko kazi Ninayoifanya kwa muda mfupi sana! Ni bora usichambue na kutafuta kosa. Haijalishi una kiburi kiasi gani, wewe bado ni kuimbe tu mdogo kuliko mchwa! Vyote vilivyomo katika tumbo lako ni vichache zaidi ya vile vilivyomo katika tumbo la mchwa! Usifikiri kwamba kwa kuwa tu umepata uzoefu na ukubwa kiasi, unaweza kuashiria kiburi na kuzungumza kwa maringo. Je, uzoefu wako na ukubwa wako sio matokeo ya maneno Niliyoyazungumza? Je, unaamini kwamba yalikuwa mbadala wa kufanya kwako kazi kwa bidii na kutokwa jasho? Siku hii, unaona kuwa nimepata mwili, na kwa sababu ya hili pekee unajawa na dhana nyingi hizo, na kutoka kwalo unakuwa na fikira nyingi isiyohesabika. Isingekuwa kwa kupata mwili Kwangu, bila kujali talanta ulizo nazo ni za ajabu kiasi gani, usingekuwa na dhana hizi nyingi; si ni kutoka hapa ndipo fikira zako zinatoka hapa? Kama si kupata mwili kwa Yesu mara hiyo ya kwanza, je, hata ungejua kuhusu kupata mwili? Je, si kwa sababu ya maarifa yako kutoka kwa kupata mwili mara ya kwanza ndio una ufidhuli kuthubutu kuhukumu kupata mwili kwa mara ya pili? Kwa nini ukuchunguze badala ya kuwa mfuasi mtiifu? Wakati umeingia katika mkondo huu na kuja mbele ya Mungu mwenye mwili, je, Angekuruhusu kuchunguza hili? Ni sawa kwako kuchunguza historia ya familia yako, lakini ukijaribu kuchunguza “historia ya familia” ya Mungu, inawezekanaje Mungu wa leo akuruhusu kufanya uchunguzi kama huo? Je, wewe si kipofu? Je, hujiletei dharau kwako mwenyewe?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 130)

Yesu pamoja na Mimi tunatoka kwa Roho Mmoja. Ingawa miili Yetu haina uhusiano, Roho Zetu ni moja; ingawa kile Tunachofanya na kazi Tulizo nazo hazifanani, kwa asili Tunafanana; Miili Yetu ina maumbo tofauti, lakini hii ni kwa sababu ya mabadiliko ya enzi na mahitaji tofauti ya kazi Yetu; huduma Zetu hazifanani, hivyo kazi Tunayoileta na tabia Tunayoifichua kwa mwanadamu pia ni tofauti. Ndiyo maana kile ambacho mwanadamu anakiona na kukielewa leo hii si kama kile cha wakati uliopita; ni hivyo kwa sababu ya mabadiliko ya enzi. Ingawa jinsia na maumbo ya miili Yao ni tofauti, na kwamba hawakuzaliwa katika familia moja, sembuse katika kipindi kimoja, hata hivyo Roho Zao ni moja. Ingawa miili Yao haina uhusiano wa damu au kimwili kwa namna yoyote ile, haipingiki kwamba Wao ni Mungu kupata mwili katika vipindi viwili tofauti vya nyakati. Ni ukweli usiopingika kwamba Wao ni miili ya nyama ya Mungu, ingawa hawatoki katika ukoo mmoja na hawatumii lugha moja ya binadamu (mmoja alikuwa mwanamume aliyezungumza lugha ya Wayahudi na mwingine ni mwanamke anayezungumza Kichina pekee). Ni kwa sababu hizi ndiyo Wameishi katika nchi tofauti kufanya kazi ambayo inampasa kila mmoja kufanya, na katika nyakati tofauti vilevile. Licha ya ukweli kwamba Wao ni Roho moja, wakiwa na asili inayofanana, hakuna mfanano wa wazi kabisa kati ya ngozi za nje za miili Yao. Wanashiriki tu ubinadamu sawa, lakini sura ya nje ya miili Yao na kuzaliwa Kwao hakufanani. Mambo haya hayana athari katika kazi Zao au maarifa aliyonayo mwanadamu juu Yao, maana, kimsingi, Wao ni Roho moja na hakuna anayeweza kuwatenganisha. Ingawa Hawana uhusiano wa damu, nafsi Zao zote zinaongoza Roho Zao, ambazo zinawapa kazi tofauti katika nyakati tofauti, na miili Yao kwa ukoo tofauti. Roho wa Yehova si baba wa Roho wa Yesu na Roho wa Yesu si mwana wa Roho wa Yehova: Ni Roho moja. Vile vile Kama vile Mungu mwenye mwili wa leo na Yesu. Ingawa Hawahusiani kwa damu, ni Wamoja; hii ni kwa sababu Roho Zao ni moja. Mungu anaweza kufanya kazi ya rehema na wema, vilevile na ile kazi ya hukumu ya haki na kumwadibu mwanadamu, na ile ya kuleta laana kwa mwanadamu; na hatimaye, Anaweza kufanya kazi ya kuuharibu ulimwengu na kuwaadhibu waovu. Je, hafanyi haya yote Mwenyewe? Je, hii si kudura ya Mungu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 131)

Mungu akiwa mkuu zaidi katika ulimwengu wote, na katika ulimwengu wa juu, Angeweza kujieleza Mwenyewe kwa ukamilifu kwa kutumia mfano wa mwili? Mungu hujivika Mwenyewe mwili ili kufanya hatua ya kazi Yake. Hakuna umuhimu mahsusi kwa sura ya mwili, na haina uhusiano na kupita kwa enzi, na haina uhusiano wowote na tabia ya Mungu. Kwa nini Yesu hakuruhusu sura Yake kubaki? Kwa nini hakumruhusu mtu kuchora sura Yake, ili iweze kupitishwa kwa vizazi vya baadaye? Kwa nini Hakuruhusu watu kukubali kwamba sura yake ilikuwa sura ya Mungu? Ingawa sura ya mwanadamu iliumbwa kwa mfano wa Mungu, ni kwa jinsi gani sura ya mwanadamu ingewakilisha mfano wa Mungu aliyeinuliwa? Mungu anapopata mwili, Yeye anashuka tu kutoka mbinguni na kuingia ndani ya mwili maalumu. Roho Wake ashuka kingia ndani ya mwili, kwa njia ambayo Yeye hufanya kazi ya Roho. Roho huonyeshwa katika mwili, na Roho hufanya kazi Yake katika mwili. Kazi iliyofanyika katika mwili inawakilisha Roho kwa ukamilifu, na mwili ni kwa ajili ya kazi, lakini hilo halimaanishi kwamba sura ya mwili ni mbadala wa sura halisi ya Mungu Mwenyewe; hili silo kusudi na umuhimu wa Mungu kupata mwili. Anapata mwili tu ili Roho apate mahali pa kuishi Akifanya kazi Yake, ili Apate kufanikisha kazi Yake katika mwili, ili watu waweze kuona matendo Yake, waelewe tabia Yake, kusikia maneno Yake, na kujua ajabu ya kazi Yake. Jina Lake linawakilisha tabia Yake, kazi Yake inawakilisha utambulisho Wake, lakini Hajawahi kusema kuwa kuonekana Kwake katika mwili kunawakilisha sura Yake; hiyo ni fikira tu ya mwanadamu. Na kwa hiyo, hoja muhimu za kupata mwili kwa Mungu ni jina Lake, kazi Yake, tabia Yake, na jinsia Yake. Yeye hutumia hivi kuwakilisha usimamizi wake katika enzi hii. Kuonekana Kwake katika mwili hakuna uhusiano na usimamizi Wake, na ni kwa ajili tu ya kazi Yake wakati huo. Hata hivyo haiwezekani kwa Mungu mwenye mwili kutokuwa na kuonekana maalumu, na kwa hiyo Anachagua jamii inayofaa ili kuamua kuonekana Kwake. Ikiwa kuonekana kwa Mungu kuna umuhimu wa uwakilishi, basi wale wote ambao wana sifa muhimu za uso sawa na Zake pia wanawakilisha Mungu. Hilo silo kosa la kupita kiasi? Picha ya Yesu ilichorwa na mwanadamu ili mwanadamu angeweza kumwabudu. Wakati huo, hakuna maagizo maalum yaliyotolewa na Roho Mtakatifu, na kwa hiyo mwanadamu alipitisha picha hiyo iliyodhaniwa hadi leo. Kwa kweli, kulingana na kusudi la Mungu, mwanadamu hakupaswa kufanya hivyo. Ni ari tu ya mwanadamu ambayo imesababisha picha ya Yesu kubaki hadi siku hii. Mungu ni Roho, na mwanadamu hataweza kamwe kuwa na uwezo wa kutoa muhtasari wa hasa sura Yake ni nini. Sura Yake inaweza tu kuwakilishwa na tabia Yake. Huwezi kufafanua kuonekana kwa pua Lake, kwa mdomo Wake, kwa macho Yake, na kwa nywele Zake. Wakati ufunuo ulipofika kwa Yohana, aliona sura ya Mwana wa Adamu: Kutoka mdomoni mwake ulikuwa upanga mkali ukatao kuwili, macho Yake yalikuwa kama miale ya moto, kichwa Chake na nywele vilikuwa vyeupe kama sufu, miguu Yake ilikuwa kama shaba iliyong’arishwa, na kulikuwa na mshipi wa dhahabu unaozunguka kifua Chake. Ingawa maneno yake yalikuwa wazi sana, sura ya Mungu aliyoieleza haikuwa sura ya kiumbe. Aliyoona ni maono tu, na sio sura ya mtu kutoka ulimwengu yakinifu. Yohana alikuwa ameona maono, lakini hakuwa ameshuhudia kuonekana kwa kweli kwa Mungu. Sura ya mwili wa Mungu uliopata mwili ni sura ya uumbaji, na haiwezi kuwakilisha tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake. Wakati Yehova alipoumba wanadamu, Alisema kuwa Alifanya hivyo kwa mfano Wake na Akaumba mume na mke. Wakati huo, Alisema Alifanya mume na mke katika mfano wa Mungu. Ingawa sura ya mwanadamu inafanana na sura ya Mungu, haimaanishi kuwa kuonekana kwa mwanadamu ni sura ya Mungu. Huwezi kutumia lugha ya mwanadamu kufanya muhtasari wa sura ya Mungu kwa ukamilifu, kwa maana Mungu ameinuliwa sana, ni mkubwa sana, wa ajabu sana na Asiyeeleweka!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 132)

Wakati huu, Mungu haji kufanya kazi kwa mwili wa kiroho ila kwa ule wa kawaida sana. Sio tu mwili wa kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili, lakini pia mwili ambao Mungu anarudia. Ni mwili wa kawaida sana. Ndani Yake, huwezi kuona chochote kilicho tofauti na cha wengine, lakini unaweza kupokea kutoka Kwake ukweli ambao hujawahi kusikia mbeleni. Mwili huu usio na umuhimu ni mfano halisi wa maneno yote ya kweli kutoka kwa Mungu, ambao hufanya kazi ya Mungu siku za mwisho, na maonyesho ya tabia nzima ya Mungu kwa mwanadamu kuja kujua. Je, hukutamani sana kumwona Mungu aliye mbinguni? Je, hutamani sana kumwelewa Mungu aliye mbinguni? Je, hutamani sana kuona hatima ya mwanadamu? Atakueleza hizi siri zote ambazo hakuna mwanadamu ameweza kukuambia, na pia Atakuelezea kuhusu ukweli usioelewa. Yeye ndiye lango la kuingia katika ufalme, na mwongozo wako katika enzi mpya. Mwili wa kawaida kama huu una siri nyingi zisizoeleweka. Matendo Yake labda hayaeleweki kwako, lakini lengo la kazi yote Anayoifanya limekutosha kuona kuwa Yeye si mwili wa kawaida anavyoamini mwanadamu. Kwani Anawakilisha mapenzi ya Mungu na pia utunzaji anaoonyesha Mungu kwa mwanadamu siku za mwisho. Ingawa huwezi kuyasikia maneno Anayozungumza yanayoonekana kutingisha mbingu na dunia wala kuona macho Yake kama moto mkali, na ingawa huwezi kuhisi nidhamu ya fimbo Yake ya chuma, unaweza kusikia kupitia maneno Yake ghadhabu ya Mungu na kujua kwamba Mungu Anaonyesha huruma kwa mwanadamu; unaweza kuona tabia ya haki ya Mungu na hekima Yake, na zaidi ya hayo, kutambua wasiwasi na utunzaji anao Mungu kwa wanadamu wote. Kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kuruhusu mwanadamu kumwona Mungu aliye mbinguni Akiishi miongoni mwa wanadamu duniani, na kumwezesha mwanadamu kuja kumjua, kumtii, kumheshimu, na kumpenda Mungu. Hii ndiyo maana Amerudi kwa mwili kwa mara ya pili. Ingawa kile anachokiona mwanadamu siku hii ni Mungu aliye sawa na mwanadamu, Mungu aliye na pua na macho mawili, na Mungu asiye wa ajabu, mwishowe, Mungu atawaonyesha kwamba bila kuwepo kwa huyu mwanadamu, mbingu na dunia zitapitia mabadiliko makuu; bila kuwepo kwa huyu mwanadamu, mbingu itapungukiwa na mwangaza, dunia itakuwa vurugu, na wanadamu wote wataishi katika njaa na mabaa. Atawaonyesha kuwa bila wokovu wa Mungu mwenye mwili katika siku za mwisho, basi Mungu Angekuwa Ashawaangamiza wanadamu wote kuzimu kitambo sana; bila kuwepo kwa mwili huu, basi daima mngekuwa viongozi wa wenye dhambi na maiti milele. Mnapaswa kujua kwamba bila kuwepo kwa mwili huu, wanadamu wote wangetazamia msiba usioepukika na kupata kuwa ngumu kuponyoka adhabu kali zaidi ya Mungu katika siku za mwisho. Bila kuzaliwa kwa mwili huu wa kawaida, nyinyi nyote mngekuwa katika hali ambayo uhai wala kifo havitakuja bila kujali jinsi mtakavyovitafuta; bila kuwepo kwa mwili huu, basi siku hii hamngeweza kupokea ukweli na kuja mbele ya kiti cha Mungu cha enzi. Badala yake, mngeadhibiwa na Mungu kwa sababu ya dhambi zenu zinazohuzunisha. Je, mnajua? Kama sio kwa kurudi kwa Mungu kwa mwili, hakuna ambaye angepata nafasi ya wokovu; na isipokuwa kwa kuja kwa mwili huu, Mungu angekuwa ameimaliza kitambo enzi ya zamani. Hivyo basi, mnaweza bado kuukataa kupata mwili kwa mara ya pili kwa Mungu? Sababu mnaweza kufaidika sana kutoka kwa huyu mwanadamu wa kawaida, basi mbona hamumkubali kwa urahisi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Ulikuwa Unajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 133)

Kazi ya Mungu ni ile usiyoweza kuelewa. Kama huwezi kufahamu kama uamuzi wako ni sahihi wala kujua kama kazi ya Mungu inaweza kufaulu, basi mbona usijaribu bahati yako na kuona iwapo huyu mwanadamu wa kawaida ni wa msaada mkubwa kwako, na iwapo Mungu amefanya kazi kubwa. Hata hivyo, lazima Nikuelezee kuwa wakati wa Nuhu, wanadamu walikuwa wamekula na kunywa, wakifunga ndoa na kupeana katika ndoa hadi kiwango ambacho Mungu asingevumilia kushuhudia, hivyo, Alituma chini mafuriko makubwa kuangamiza wanadamu na kuacha tu nyuma familia ya Nuhu ya watu wanane na aina yote ya ndege na wanyama. Katika siku za mwisho, hata hivyo, wale waliohifadhiwa na Mungu ni wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake hadi mwisho. Ingawa nyakati zote mbili zilikuwa za upotovu mkubwa Asizoweza kuvumilia kushuhudia Mungu, na mwanadamu katika enzi zote mbili alikuwa mpotovu kiasi cha kumkana Mungu kama Bwana, watu wote katika wakati wa Nuhu waliangamizwa na Mungu. Mwanadamu katika enzi zote mbili amemhuzunisha Mungu sana, lakini Mungu bado Amebakia mvumilivu na wanadamu katika siku za mwisho hadi sasa. Mbona hivi? Hamjawahi kufikiria haya? Kama kweli hamjui, basi wacha Niwaelezee. Sababu Mungu anaweza kushughulika na wanadamu kwa neema siku za mwisho si kwamba ni wapotovu kidogo zaidi kuliko wanadamu katika wakati wa Nuhu ama kwamba wamemwonyesha Mungu toba, sembuse si kwamba Mungu hawezi kuvumilia kuwaangamiza wanadamu katika siku za mwisho ambapo teknolojia imeendelea. Badala yake, ni kwamba Mungu ana kazi ya kufanya kwa kundi la wanadamu katika siku za mwisho na hii itafanywa na Mungu mwenye mwili Mwenyewe. Zaidi ya hayo, Mungu atachagua sehemu ya kundi hili kama vyombo Vyake vya wokovu, tunda la mpango Wake wa usimamizi, na kuleta wanadamu kama hawa naye katika enzi ifuatayo. Kwa hivyo, bila kujali, hii gharama iliyolipwa na Mungu yote imekuwa katika maandalizi ya kazi ya kupata mwili Kwake katika siku za mwisho. Ukweli kwamba mmefika siku ya leo ni kwa sababu ya huu mwili. Ni kwa sababu Mungu huishi ndani ya mwili ndiyo mna nafasi ya kuishi. Hii bahati yote nzuri imepatwa kwa sababu ya huyu mwanadamu wa kawaida. Siyo haya tu, lakini mwishowe kila taifa litamwabudu huyu mwanadamu wa kawaida, na pia kumpa shukrani na kumtii huyu mwanadamu asiye muhimu, kwa sababu ni ukweli, uzima, na njia Aliyoleta ndivyo vilivyowaokoa wanadamu wote, kutuliza migogoro kati ya mwanadamu na Mungu, ikafupisha umbali kati yao, na kufungua kiungo kati ya mawazo ya Mungu na mwanadamu. Pia ni Yeye ambaye Ameleta hata utukufu zaidi kwa Mungu. Mwanadamu wa kawaida kama huyu hastahili uaminifu na ibada yako? Mwili wa kawaida kama huu haufai kuitwa Kristo? Mwanadamu wa kawaida kama huyu hawezi kuwa maonyesho ya Mungu miongoni mwa wanadamu? Mwanadamu kama huyu anayesaidia wanadamu kuepuka maafa hastahili mapenzi yenu na nyinyi kumshikilia? Mkiukataa ukweli unaotamkwa kutoka mdomo Wake na pia kuchukia kuwepo Kwake miongoni mwenu, basi nini itakuwa majaliwa yenu?

Kazi yote ya Mungu katika siku za mwisho inafanywa kupitia huyu mwanadamu wa kawaida. Atakupa kila kitu, na juu ya hayo, Anaweza kuamua kila kitu kukuhusu. Mtu kama huyu anaweza kuwa mnavyoamini: mtu wa kawaida sana kiasi cha kutostahili kutajwa? Ukweli Wake hujatosha kuwashawishi kabisa? Ushuhuda wa vitendo Vyake hujatosha kuwashawishi kabisa? Ama ni kuwa njia Anayowaongozea haistahili nyinyi kuifuata? Ni nini kinachowasababisha kumchukia na kumtupilia mbali na kumwepuka? Ni Yeye anayeonyesha ukweli, ni Yeye anayetoa ukweli, na ni Yeye anayewawezesha kuwa na njia ya kusafiri. Inaweza kuwa kwamba bado hamwezi pata chembe cha kazi ya Mungu ndani ya ukweli huu? Bila kazi ya Yesu, mwanadamu hangeweza kushuka chini kutoka msalabani, lakini bila kupata mwili siku hii, wale wanaoshuka chini kutoka msalabani hawangewahi kusifiwa na Mungu ama kuingia katika enzi mpya. Bila kuja kwa huyu mwanadamu wa kawaida, basi hamngeweza kuwa na hii fursa ama kustahiki kuona uso wa ukweli wa Mungu, kwani nyinyi nyote ni wale ambao wangepaswa kuangamizwa kitambo sana. Kwa sababu ya kuja kwa Mungu mwenye mwili kwa mara ya pili, Mungu amewasamehe na kuwaonyesha huruma. Bila kujali, maneno ambayo lazima Niwaachie mwishowe ni haya: Huyu mwanadamu wa kawaida, ambaye ni Mungu mwenye mwili, ni wa umuhimu sana kwenu. Hili ndilo jambo kubwa ambalo Mungu tayari Amefanya miongoni mwa wanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Ulikuwa Unajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 134)

Je, unapaswa kujua nini kuhusu Mungu wa vitendo? Mungu wa vitendo Mwenyewe anajumuisha Roho, Nafsi, na Neno, na hii ndiyo maana ya kweli ya Mungu wa utendaji Mwenyewe. Kama unajua Nafsi pekee—kama unajua tabia na utu Wake—lakini hujui kazi ya Roho, au ambacho Roho hufanya katika mwili, na kuangazia Roho tu, na Neno, na kuomba mbele ya Roho, bila kujua kazi ya Roho wa Mungu katika Mungu wa vitendo, basi hii inadhihirisha kuwa humjui Mungu wa vitendo. Ufahamu wa Mungu wa vitendo unajumuisha kujua na kuyapitia maneno Yake, na kuelewa sheria na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu, na jinsi Roho wa Mungu anavyofanya kazi katika mwili. Kwa hivyo, pia, inajumuisha kujua kwamba kila tendo la Mungu katika mwili linaongozwa na Roho, na kwamba maneno Anenayo ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho. Hivyo, ukitaka kumjua Mungu wa vitendo, lazima kimsingi ujue jinsi ambavyo Mungu hufanya kazi katika ubinadamu na katika uungu; hili, wakati ule ule, linahusu maonyesho ya Roho, ambayo watu wote hujihusisha nayo.

Ni nini kilichomo katika maonyesho ya Roho? Wakati mwingine Mungu hufanya kazi miongoni mwa ubinadamu, na wakati mwingine katika uungu—lakini kwa jumla, Roho anatawala katika pande zote mbili. Hata iwe ni roho gani ndani ya watu, hivyo ndivyo huwa maonyesho yao ya nje. Roho anafanya kazi kawaida, lakini kuna pande mbili za uelekezaji Wake kwa Roho: Upande mmoja ni kazi Yake kwa ubinadamu, na upande mwingine ni kupitia uungu. Unafaa kujua haya wazi wazi. Kazi ya Roho hubadilika kulingana na matukio: Wakati kazi Yake ya binadamu inahitajika, Roho anaielekeza kazi hii ya binadamu, na wakati kazi ya uungu inahitajika, uungu hujitokeza moja kwa moja kuifanya. Kwa sababu Mungu hufanya kazi katika mwili na kujionyesha katika mwili, Anafanya kazi katika ubinadamu na katika uungu. Kazi Yake katika ubinadamu inaongozwa na Roho, na ili kuyaridhisha mahitaji ya kimwili ya watu, kuwezesha ushirikiano wao Naye, kuwafanya waone uhalisi na ukawaida wa Mungu, na kuwafanya waone kuwa Roho amekuja katika Mwili, na Yuko miongoni mwa wanadamu, Anaishi pamoja na wanadamu, na Hushirikiana na wanadamu. Kazi Yake ya uungu ni kwa ajili ya kuwapa watu uzima, na kuwaelekeza watu katika kila kitu kwa upande mzuri, na kubadili tabia za watu na kuwafanya waone kwa kweli kuonekana kwa Roho katika mwili. Kwa kiwango kikubwa, ukuaji katika maisha ya mwanadamu unapatikana moja kwa moja kupitia kazi ya Mungu na maneno katika uungu. Ikiwa tu watu wataikubali kazi ya Mungu ya uungu wataweza kubadili tabia zao, na hapo tu ndipo wataweza kushibishwa katika roho zao; ni ikiwa tu, ikiongezwa kwa hili, ndipo kutakuwa na kazi katika ubinadamu—uchungaji wa Mungu, usaidizi, na riziki kwa ubinadamu—ndipo matokeo ya kazi ya Mungu yanaweza kufanikishwa kikamilifu. Mungu wa vitendo Mwenyewe ambaye Anazungumziwa leo hufanya Kazi katika uungu na ubinadamu. Kupitia kwa kujitokeza kwa Mungu wa vitendo, kazi Yake ya kawaida ya binadamu na maisha na kazi Yake kamilifu ya uungu vinapatikana. Ubinadamu na uungu wake vimeungwa kuwa kitu kimoja, na kazi ya pande zote mbili inakamilishwa kupitia maneno; iwe katika ubinadamu au uungu, Ananena maneno. Mungu anapofanya Kazi katika ubinadamu, Anazungumza lugha ya ubinadamu, ili watu waweze kushiriki na kuelewa. Maneno Yake yanasemwa waziwazi, na ni rahisi kueleweka, kiasi kwamba yanaweza kutolewa kwa watu wote; bila ya kujali kuwa hawa watu wana ufahamu au hawajasoma vyema, wote wanaweza kupokea maneno ya Mungu. Kazi ya Mungu katika uungu vilevile inaweza kufanywa kupitia maneno, lakini imejawa na riziki, imejawa na uzima, haijatiwa dosari na mawazo ya mwanadamu, haihusishi mapenzi ya mwanadamu, na haina mipaka ya binadamu, iko nje ya mipaka ya ubinadamu wowote wa kawaida; vilevile, inafanywa katika mwili, lakini ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho. Kama watu wanaikubali kazi ya Mungu katika ubinadamu tu, basi watajiwekea mipaka katika upeo fulani, na hivyo milele watahitaji kushughulikiwa, kupogolewa, na kufundishwa nidhamu ili kwamba pawepo na mabadiliko kidogo ndani yao. Bila ya Kazi au uwepo wa Roho Mtakatifu, ingawa, watairudia mienendo yao ya awali; ni kupitia kazi ya uungu tu ndio haya maradhi na upungufu vitaweza kurekebishwa, hapo ndipo watu wanafanywa kuwa wakamilifu. Badala ya kushughulikia na kupogoa mara kwa mara, kinachohitajika ni matokeo mazuri, kwa kutumia maneno kufidia upungufu wote, kutumia maneno ili kufichua hali zote za watu, kutumia maneno kuyaelekeza maisha yao, kila matamshi yao, kila tendo lao, ili kuziweka wazi nia na motisha yao; hii ni kazi halisi ya Mungu wa vitendo. Na kwa hivyo, katika mwelekeo wako kwa Mungu wa vitendo unafaa kunyenyekea mbele ya ubinadamu Wake, ukimkubali na kumtambua, na zaidi, unapaswa kukubali na kutii kazi ya uungu na maneno. Kuonekana kwa Mungu katika mwili kunamaanisha kuwa kazi yote na maneno ya Roho wa Mungu yanafanywa katika ubinadamu wake wa kawaida, na kupitia mwili Wake uliopatikana. Kwa maneno mengine, Roho wa Mungu huelekeza kazi Yake ya ubinadamu na hutekeleza kazi Yake ya uungu katika mwili, na katika Mungu kupata mwili unaweza kuona kazi ya Mungu katika ubinadamu na kazi kamili ya uungu; huu ndio umuhimu wa utendaji hata zaidi wa kuonekana kwa Mungu wa vitendo katika mwili. Ukiweza kuliona hili wazi, utaweza kuhusisha sehemu zote za Mungu, na utaacha kuthamini sana kazi Yake ya uungu, na kuwa mwenye kupuuza sana kazi Yake katika ubinadamu, na hautazidi mipaka wala kupita njia za michepuo. Kwa jumla, maana ya Mungu wa vitendo ni kuwa kazi Yake ya ubinadamu na kazi Yake ya uungu, kama inavyoelekezwa na Roho, inaonyeshwa kupitia mwili Wake, ili watu waone kuwa Yeye ni wazi na mwenye kufanana na kiumbe chenye uhai, na ni halisi na wa hakika.

Kazi ya Roho wa Mungu katika ubinadamu ina awamu za mpito. Kwa kuwafanya ubinadamu wakamilifu, Anawawezesha ubinadamu Wake kupokea mwelekeo wa Roho, ambapo baadaye ubinadamu Wake unaweza kuyakimu na kuyaongoza makanisa. Hii ni aina moja ya maonyesho ya kazi ya kawaida ya Mungu. Hivyo, ukiweza kuona wazi kanuni za kazi ya Mungu katika ubinadamu, basi itakuwa vigumu kwako kuwa na dhana kuhusu kazi ya Mungu katika ubinadamu. Bila kujali kitu kingine chochote, Roho wa Mungu hawezi kukosea. Yuko sahihi, na Hana dosari; Hawezi kufanya kitu chochote kimakosa. Kazi ya uungu ni maonyesho ya moja kwa moja ya mapenzi ya Mungu, bila maingilio ya ubinadamu. Haipitii ukamilifu, ila inatoka moja kwa moja kwa Roho. Na bado, kufanya Kwake kazi katika uungu ni kwa sababu ya ubinadamu Wake wa kawaida; si miujiza, na kazi inaonekana kana kwamba imefanywa na mwanadamu wa kawaida; Kimsingi Mungu alitoka mbinguni kuja duniani ili kuonyesha maneno ya Mungu kupitia mwili, kukamilisha kazi ya Roho wa Mungu kwa kutumia mwili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 135)

Ufahamu wa watu leo kuhusu Mungu wa vitendo bado unaegemea upande mmoja, na ufahamu wao kuhusu umuhimu wa kupata mwili bado ni mdogo sana. Kuhusu suala la mwili wa Mungu, watu huona kupitia katka kazi na maneno Yake kwamba Roho wa Mungu ana mengi, kwamba yeye ni tajiri. Lakini, hata hivyo, ushuhuda wa Mungu hatimaye hutoka kwa Roho wa Mungu: Anachokifanya Mungu katika Mwili, ni kanuni gani anatumia, anachokifanya katika ubinadamu, na anachokifanya katika uungu. Watu lazima wawe na ufahamu wa hili. Leo unaweza kumwabudu huyu mtu, lakini kwa hakika unamwabudu Roho. Hiki ndicho kiwango cha chini kabisa kinachopaswa kufahamiwa kuhusu ufahamu wa watu kuhusu Mungu aliyepata mwili: kujua kiini cha Roho kupitia kwa mwili, kujua kazi ya uungu ya Roho katika mwili na kazi ya wanadamu katika mwili, kukubali maneno yote ya Roho na matamshi katika mwili, na kuona jinsi Roho wa Mungu anauelekeza mwili na kudhihirisha uwezo Wake katika mwili. Hivi ni kusema kuwa, mwanadamu anapata kumjua Roho aliye mbinguni kupitia kwa mwili; kuonekana kwa Mungu wa vitendo Mwenyewe miongoni mwa wanadamu kumemwondoa Mungu asiye yakini kutoka katika dhana za wanadamu; ibada ya watu kwa Mungu wa vitendo Mwenyewe imeongeza utiifu wao kwa Mungu; na kupitia kwa uungu wa kazi ya Roho wa Mungu katika Mwili, na kazi ya wanadamu katika miili, mwanadamu hupata ufunuo, na kuongozwa, na mabadiliko hupatikana katika tabia ya maisha yake. Hii tu ndiyo maana halisi ya ujio wa Roho katika mwili, kimsingi, ili kwamba watu waweze kushirikiana na Mungu, kumtegemea Mungu, na kuupata ufahamu wa Mungu.

Kwa kiasi kikubwa, ni mtazamo upi watu wanapaswa kuwa nao kuhusu Mungu wa vitendo? Unajua nini kuhusu kupata mwili, kuhusu kuonekana kwa Neno katika mwili, kuhusu kuonekana kwa Mungu katika mwili, na matendo ya Mungu wa vitendo? Mada kuu za kuzungumziwa leo ni zipi? Kupata mwili, ujio wa Neno katika mwili, kuonekana kwa Mungu katika mwili yote ni masuala ambayo ni lazima yaeleweke. Ni lazima mpate kuyaelewa haya masuala hatua kwa hatua na muwe na ufahamu ulio wazi kuyahusu katika uzoefu wenu wa maisha, kwa msingi wa kimo chenu na kwa msingi wa enzi. Mchakato ambamo watu huyapitia maneno ya Mungu ni sawa na mchakato ambamo wanafahamu kujitokeza kwa maneno ya Mungu katika mwili. Kadiri watu wanavyoyapitia maneno ya Mungu, ndivyo wanavyomjua Roho wa Mungu; kwa kuyapitia maneno ya Mungu, watu wanaelewa kanuni za kazi ya Roho na kupata kumjua Mungu wa vitendo Mwenyewe. Kwa hakika, Mungu akiwafanya watu wakamilifu na kuwachukua, Anawafanya wayajue matendo ya Mungu wa vitendo; Anatumia kazi ya Mungu wa vitendo kuwaonyesha watu umuhimu halisi wa kupata mwili, na kuwaonyesha kuwa Roho wa Mungu hakika ameonekana kwa mwanadamu. Watu wakichukuliwa na kufanywa wakamilifu na Mungu, maonyesho ya Mungu wa vitendo huwa amewashinda, maneno ya Mungu wa vitendo huwa yamewabadilisha, na kutoa uzima Wake ndani yao, kuwajaza na kile Alicho (iwe ni uwepo wake wa binadamu, au ule wa uungu), kuwajaza kwa kiini cha maneno Yake, na kuwafanya watu waishi kwa kudhihirisha maneno Yake. Mungu akiwapata watu, kimsingi Anafanya hivyo kwa kutumia maneno na matamko ya Mungu wa vitendo ili kuushughulikia upungufu wa watu, na kuhukumu na kufichua tabia zao za uasi, kuwafanya wapate wanachokihitaji, na kuwaonyesha kuwa Mungu yuko miongoni mwa wanadamu. Muhimu zaidi, kazi ifanywayo na Mungu wa vitendo ni kumwokoa kila mtu kutoka katika ushawishi wa Shetani, kuwatoa katika nchi ya uchafu, na kuziondoa tabia zao potovu. Umuhimu mkubwa zaidi wa watu kupatikana na Mungu wa vitendo ni kuwa na uwezo wa kumfanya Mungu wa vitendo kielelezo, na kuishi kulingana na ubinadamu wa kawaida, kuweza kutenda kulingana na maneno na mahitaji ya Mungu wa vitendo, bila upotofu au kuteleza, kutenda kama Asemavyo, na kuweza kufanikisha lolote Atakalo. Kwa njia hii, utakuwa umepatwa na Mungu. Ukipatwa na Mungu, hupati tu kazi ya Roho Mtakatifu; kidesturi, unaweza kuzidisha mahitaji ya Mungu wa utendaji. Kuwa tu na kazi ya Roho Mtakatifu hakumaanishi kuwa una uzima. Cha muhimu ni kama unaweza kuishi kwa kudhihirisha mahitaji ya Mungu wa vitendo, ambayo inahusiana na kama unaweza kupatikana na Mungu. Haya mambo ndiyo muhimu zaidi katika kazi ya Mungu wa vitendo katika mwili. Hivi ni kusema kuwa, Mungu analipata kundi la watu kwa kuonekana halisi na hakika katika mwili na kuwa wazi na mwenye kufanana na kiumbe chenye uhai, Akionekana na watu, hasa Akifanya kazi ya Roho katika mwili, na kwa kuwa kielelezo kwa watu wenye miili. Kimsingi, ujio wa Mungu katika mwili ni kuwawezesha watu kuona matendo halisi ya Mungu, kumfanya Roho asiye na umbo kuwa bayana katika mwili, na kuwapa watu fursa ya kumwona na kumgusa. Kwa njia hii, wanaokamilishwa Naye wataishi kwa kumfuata Yeye, watamfaidi na kuupendeza moyo Wake. Mungu angalinena kutoka mbinguni tu, na hakika asije duniani, basi bado watu hawangeweza kumjua, wangeweza tu kuyahubiri matendo ya Mungu kwa kutumia nadharia tupu, na hawangekuwa na maneno ya Mungu kama uhalisi. Mungu amekuja duniani kimsingi kuwa mfano na kielelezo kwa wale ambao wamepatwa na Mungu; ni kwa njia hii pekee ndio watu wanaweza kumjua Mungu kwa hakika, na kumgusa Mungu, na kumwona, na hapo ndipo wanaweza kupatikana na Mungu kwa kweli.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 136)

Kazi ya Mungu mwenye mwili inajumuisha sehemu mbili. Mara ya kwanza Alipofanyika kuwa mwili, watu hawakumwamini au kumfahamu na wakamsulubisha Yesu msalabani. Mara ya pili, pia, watu pia hawakuamini ndani Yake, wala kumfahamu, na kwa mara nyingine wakamsulubisha Kristo msalabani. Je, mwanadamu si adui wa Mungu? Kama mwanadamu hamjui Yeye, mwanadamu anawezaje kuwa mwandani wa Mungu? Na anawezaje kuwa na sifa za kumshuhudia Mungu? Je, si madai ya kumpenda Mungu, kumtumikia Mungu, kumtukuza Mungu yote ni udanganyifu? Kama unayatoa maisha yako kwa haya mambo yasiyokuwa na uhalisi, yasiyoweza kutekelezeka, huoni kama unafanya kazi bure? Unawezaje kuwa mwandani wa Mungu wakati hujui Mungu ni nani? Kufuatilia kama huko si kusio dhahiri na kwa dhahania? Je, sio kwa udanganyifu? Mtu anawezaje kuwa mwandani wa Mungu? Kuna maana gani kivitendo kuwa mwandani wa Mungu? Je, unaweza kuwa mwandani wa Roho wa Mungu? Je, unaweza kuona jinsi Roho alivyo mkubwa na alivyoinuliwa? Kuwa mwandani wa Mungu asiyeonekana, asiyeshikika—hili si jambo lisilo dhahiri na la dhahania? Maana ya utendaji ya kufuatilia huku ni gani? Je, sio udanganyifu mtupu tu? Kile unachokifuatilia ni kuwa mwandani wa Mungu, lakini bado ni mtumwa wa Shetani, maana humfahamu Mungu, na kumfuatilia “Mungu wa vitu vyote,” asiyekuwepo ambaye haonekani, hashikiki, na ni wa dhana zako mwenyewe. Kwa maana isiyo dhahiri, huyo “Mungu” ni Shetani, na kwa uhalisi, ni wewe mwenyewe. Unatafuta kuwa mwandani wako mwenyewe halafu bado unasema unatafuta kuwa mwandani wa Mungu—huko si ni kukufuru? Thamani ya ufutiliaji wa aina hii ni nini? Kama Roho wa Mungu hawezi kuwa mwili, basi kiini cha Mungu ni kitu kisichoonekana, Roho wa uzima asiyeshikika, asiyekuwa na umbo, hana vitu vya kushikika, hafikiki na mwanadamu hawezi kumtambua. Mwanadamu anawezaje kuwa mwandani wa Roho asiyekuwa na mwili, wa ajabu na asiyeweza kueleweka kama huyu? Huu sio utani? Fikira ya kipuuzi kama hiyo ni batili na haitekelezeki. Mwanadamu aliyeumbwa kwa asili yuko tofauti na Roho wa Mungu, sasa inawezekanaje wawili hawa kuwa wandani? Ikiwa Roho wa Mungu hakutambuliwa katika mwili, ikiwa Mungu hakuwa mwili na kujishusha Mwenyewe kwa kufanyika kiumbe, basi mwanadamu aliyeumbwa asingekuwa na sifa na kuwa na uwezo wa kuwa mwandani Wake, na licha ya wachamungu ambao wanaweza kuwa na nafasi ya kuwa wandani wa Mungu baada ya Roho zao kuingia mbinguni, watu wengi wasingeweza kuwa wandani wa Roho wa Mungu. Na ikiwa mwanadamu anataka kuwa mwandani wa Mungu mbinguni chini ya uongozi wa Mungu mwenye mwili, je, yeye si mwanadamu mpumbavu kupindukia? Mwanadamu anakuwa tu “mwaminifu” kwa Mungu asiyeonekana, na wala hamzingatii Mungu ambaye hawezi kuonekana, kwa maana ni rahisi sana kumfuata Mungu asiyeonekana—mwanadamu anaweza kufanya hivyo kwa vyovyote apendavyo. Lakini njia ya Mungu anayeonekana si rahisi. Mwanadamu ambaye anamtafuta Mungu asiye dhahiri hakika hawezi kumpata Mungu, maana vitu ambavyo si dhahiri na ni vya dhahania vyote vinafikiriwa na mwanadamu, na ambavyo mwanadamu hawezi kuvipata. Ikiwa Mungu ambaye alikuja kwenu angekuwa Mungu wa kifahari na aliyeinuliwa ambaye angekuwa hafikiki kwenu, sasa mngewezaje kutafuta mapenzi Yake? Na mngewezaje kumfahamu na kumwelewa? Ikiwa angefanya kazi Yake tu, na wala hakuwa na uhusiano na mwanadamu, au hakuwa na ubinadamu wa kawaida na hakuweza kufikiwa na mwanadamu mwenye mwili wa kufa, basi, hata kama Alifanya kazi kubwa kwa ajili yako, lakini hukuweza kuhusiana naye, na hukuweza kumwona, utawezaje kumfahamu? Kama isingekuwa kwa kuchukua mwili wa ubinadamu, mwanadamu asingeweza kumjua Mungu; ni kwa sababu tu ya Mungu mwenye mwili ndiyo mwanadamu amefuzu kuwa mwandani wa Mungu mwenye mwili. Mwanadamu huwa mwandani wa Mungu kwa sababu mwanadamu huhusiana naye, kwa sababu mwanadamu huishi naye na kuambatana naye, na kwa hivyo huja kumjua. Isingekuwa hivyo mwanadamu kumtafuta Mungu si kungekuwa ni bure? Hii ni kusema, si kwa sababu ya kazi ya Mungu ndiyo mwanadamu anaweza kuwa mwandani wa Mungu, bali ni kwa sababu ya uhalisi na ukawaida wa Mungu mwenye mwili. Ni kwa sababu tu Mungu huwa mwili ndiyo mwanadamu huwa na nafasi ya kufanya wajibu wake, na nafasi ya kumwabudu Mungu wa kweli. Je, si huu ni ukweli halisi na unaoweza kutekelezeka? Sasa, bado unatamani kuwa mwandani wa Mungu mbinguni? Ni pale tu ambapo Mungu anajinyenyekeza kwa kiwango fulani, ambavyo ni sawa na kusema, ni pale tu ambapo Mungu anafanyika kuwa mwili, ndipo mwanadamu anaweza kuwa mwandani na msiri Wake. Mungu ni wa Roho: Mwanadamu anawezaje kuwa na sifa ya kuwa mwandani wa Roho huyu, ambaye ameinuliwa sana na asiyeweza kueleweka? Ni pale tu ambapo Roho wa Mungu anaposhuka na kuwa mwili, anakuwa kiumbe anayefanana na mwanadamu, ndipo mwanadamu huweza kuelewa mapenzi Yake na kimsingi kumilikiwa naye. Yeye huzungumza na kufanya kazi katika mwili, hushiriki katika furaha, huzuni, na mateso ya mwanadamu, huishi katika dunia ile ile kama mwanadamu, humlinda mwanadamu, na kumwongoza, na kupitia katika hili humsafisha mwanadamu na kumruhusu mwanadamu kupata wokovu Wake na baraka Zake. Baada ya kuvipata vitu hivi, mwanadamu hupata kuyaelewa mapenzi ya Mungu kwa kweli, na ni hapo tu ndipo anaweza kuwa mwandani wa Mungu. Hii ndiyo inaweza kutekelezeka. Kama Mungu angekuwa haonekani na hashikiki, mwanadamu angewezaje kuwa mwandani Wake? Je, si hili ni fundisho lililo tupu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 137)

Wakati Mungu Anakuja duniani, Yeye Anafanya tu kazi Yake ndani ya uungu. Hili ndilo Roho wa mbinguni amemwaminia Mungu mwenye mwili. Anapokuja, anakwenda tu kuzungumza kila mahali, kutamka matamshi Yake kwa njia tofauti na kutoka kwa mitazamo tofauti. Yeye kimsingi Anachukulia kumruzuku mwanadamu na kumfundisha mwanadamu kama malengo Yake na kanuni Zake za kazi na hajihusishi na vitu kama uhusiano kati ya wanadamu au maelezo ya maisha ya wanadamu. Huduma Yake kuu ni kuzungumza kwa niaba ya Roho. Wakati Roho wa Mungu Anaonekana katika mwili kwa hali iliyo wazi, Yeye hukimu uzima wa mwanadamu na kuuweka wazi ukweli tu. Yeye hajihusishi katika kazi ya mwanadamu, yaani, Yeye hashiriki katika kazi ya binadamu. Binadamu hawezi kufanya kazi ya uungu, na Mungu hashiriki katika kazi za binadamu. Katika miaka yote tangu Mungu aje duniani kufanya kazi Yake, Yeye daima Ametumia wanadamu kuifanya. Lakini wanadamu hawa hawawezi kuchukuliwa kama Mungu mwenye mwili; wao wanaweza tu kuchukuliwa kama wanadamu wanaotumiwa na Mungu. Lakini Mungu wa leo Anaweza kuzungumza moja kwa moja kutoka katika mtazamo wa uungu, Akitoa nje sauti ya Roho, na kufanya kazi kwa niaba ya Roho. Wanadamu wote ambao Mungu Ametumia katika enzi zote vivyo hivyo ni mifano ya Roho wa Mungu Akifanya kazi ndani ya mwili wa nyama, hivyo basi kwa nini hawawezi kuitwa Mungu? Lakini Mungu wa leo pia ni Roho wa Mungu Anayefanya kazi moja kwa moja katika mwili, na Yesu pia Alikuwa Roho wa Mungu Aliyefanya kazi katika mwili; Wote hawa wawili wanaitwa Mungu. Basi tofauti ni gani? Katika enzi zote, wanadamu ambao Mungu Ametumia wote wana uwezo wa mawazo na mantiki ya kawaida. Wao wote wanajua kanuni za mienendo ya binadamu. Wamekuwa na mawazo ya kawaida ya binadamu, na wamemilikiwa na vitu vyote ambavyo watu wa kawaida wanapaswa kumiliki. Wengi wao wamekuwa na vipaji vya pekee na werevu wa kiasili. Katika kuwafinyanga watu hawa, Roho wa Mungu Anatumia vipaji vyao, ambavyo ni zawadi zao Alizowapa Mungu. Roho wa Mungu Anayeleta vipaji vyao katika kazi, Akitumia uwezo wao kumhudumia Mungu. Hata hivyo, kiini cha Mungu hakina itikadi na hakina fikira. Hakiungani na mawazo ya binadamu na hata kinakosa vitu ambavyo binadamu wa kawaida huwa navyo. Yaani, Mungu hata hafahamu vizuri kanuni za maadili ya binadamu. Hivi ndivyo ilivyo Mungu wa leo Anapokuja duniani. Kazi Yake na maneno Yake hayajachafuliwa na nia au fikira za binadamu, bali ni dhihirisho la moja kwa moja la nia za Roho, na Anafanya kazi moja kwa moja kwa niaba ya Mungu. Hii ina maana kuwa Roho hunena moja kwa moja, yaani, uungu hufanya kazi moja kwa moja, bila kuchanganya ndani hata nia kidogo za mwanadamu. Yaani, Mungu katika mwili Anajumuisha uungu moja kwa moja, Hana mawazo ya binadamu au itikadi, na Haelewi kanuni za maadili ya binadamu. Kama kungekuwa na kazi ya uungu tu (kumaanisha iwapo ingekuwa Mungu mwenyewe pekee ndiye Anayefanya kazi hiyo), kazi ya Mungu haingeweza kufanyika duniani. Kwa hivyo Mungu Anapokuja duniani, lazima Awe na wanadamu wachache Anaowatumia kufanya kazi katika ubinadamu pamoja na kazi ambayo Mungu hufanya katika uungu. Kwa maneno mengine, Yeye Anatumia kazi ya mwanadamu ili kusaidia kazi Yake takatifu. La sivyo, mwanadamu hangeweza kuja katika mawasiliano ya moja kwa moja na kazi ya uungu. Hivi ndivyo ilivyokuwa baina ya Yesu na wanafunzi wake. Wakati wa maisha Yake duniani Yesu alipiga marufuku sheria za zamani na kuanzisha amri mpya. Pia alizungumza maneno mengi. Yote haya yalifanyika katika uungu. Wale wengine, kama vile Petro, Paulo, na Yohana, wote waliweka kazi yao ya baadaye juu ya msingi wa maneno ya Yesu. Yaani, Mungu alikuwa akizindua kazi Yake katika enzi hiyo, Akikaribisha mwanzo wa Enzi ya Neema; yaani, Alileta enzi mpya, Akaiondoa ile ya zamani, na pia kutimiza maneno “Mungu ni Mwanzo na Mwisho”. Kwa maneno mengine, mwanadamu lazima afanye kazi ya mwanadamu juu ya msingi wa kazi ya Mungu. Yesu alipomaliza kusema yote Aliyohitajika kusema na kumaliza kazi Yake hapa duniani, alitoka katika mwanadamu. Baada ya haya, watu wote, wakifanya kazi, walifanya hivyo kwa mujibu wa kanuni zilizoonyeshwa katika maneno Yake na kutenda kwa mujibu wa ukweli Alioongea. Hawa wote walikuwa watu waliomfanyia Yesu kazi. Kama ingekuwa ni Yesu pekee Yake akifanya kazi, haijalishi kiasi gani Yeye Angezungumza, bado wanadamu hawangeweza kuwa na uhusiano na neno Lake, kwa sababu Yeye Alifanya kazi katika uungu na angeweza tu kuzungumza maneno ya uungu, na Hangeweza kueleza mambo hadi kiwango ambacho watu wa kawaida wangeweza kuelewa maneno Yake. Hivyo basi ilimpasa kuwa na mitume na manabii waliokuja kabla Yake kuongezea kazi Yake. Hii ni kanuni ya jinsi Mungu mwenye mwili Hufanya kazi—kwa kutumia mwili wa nyama kusema na kutenda ili kukamilisha kazi ya uungu, na kisha kwa kutumia wanadamu wachache au zaidi wanaopendeza moyo wa Mungu ili kuongezea kazi Yake. Yaani, Mungu Anatumia wanadamu wanaopendeza moyo Wake kuongoza na kunyunyiza binadamu ili watu wateule wa Mungu waweze kuingia katika uhalisi wa ukweli.

Kama, katika kupata mwili, Mungu anafanya kazi ya uungu tu bila kuwa na wanadamu wachache wa ziada wanaopendeza moyo Wake kushirikiana na Yeye, basi mwanadamu hangekuwa na uwezo kabisa wa kuelewa mapenzi ya Mungu au kuwasiliana na Mungu. Mungu lazima atumie wanadamu wa kawaida wanaopendeza moyo Wake ili kukamilisha kazi hii, kutunza na kuchunga makanisa, ili kufikia kiwango ambapo mchakato wa ufahamu wa mwanadamu, ubongo wake unaweza kubuni. Kwa maneno mengine, Mungu anatumia wanadamu wachache wanaopendeza moyo wake “kutafsiri” kazi anayofanya katika uungu Wake, ili iweze kufunuliwa, yaani, kubadilisha lugha ya Mungu kuwa lugha ya binadamu, hivyo kwamba wanadamu wote waweze kuielewa, wote waifahamu. Kama Mungu hangefanya hivyo, hakuna mwanadamu angeweza kuelewa lugha takatifu ya Mungu, kwa sababu idadi ya wanadamu wanaoupendeza moyo wa Mungu, ni chache mno, na uwezo wa mwanadamu kufahamu ni dhaifu. Hiyo ndiyo maana Mungu hutumia njia hii wakati wa kufanya kazi katika mwili wa nyama. Kama kungekuwa na kazi ya uungu peke yake, mwanadamu hangeweza kabisa kujua au kuwasiliana na Mungu, kwa sababu mwanadamu haelewi lugha ya Mungu. Mwanadamu anaweza kuelewa lugha hii tu kupitia tu kwa nguvu ya wanadamu wanaopendeza moyo wa Mungu kufafanua maneno Yake. Hata hivyo, kama kungekuwa na wanadamu kama hao pekee wakifanya kazi katika ubinadamu, hilo lingeweza tu kudumisha maisha ya kawaida ya mwanadamu; lisingeweza kubadilisha tabia ya mwanadamu. Kazi ya Mungu basi haingekuwa na mwanzo mpya; kungekuwa tu na nyimbo zile zile za zamani, maelezo yale yale ya kawaida ya zamani. Ni kupitia kwa nguvu ya Mungu mwenye mwili pekee, Anayesema yote yanayohitajika kusemwa na kufanya yote ambayo yanafaa kufanywa katika kipindi cha Yeye kupata mwili, ambapo baadaye watu hufanya kazi na kupata uzoefu kulingana na maneno Yake, ndipo tabia ya maisha yao itaweza kubadilika na waweze kusonga na nyakati. Yeye ambaye Anafanya kazi katika uungu Anawakilisha Mungu, ilhali wale wanaofanya kazi katika ubinadamu ni wanadamu wanaotumiwa na Mungu. Yaani, Mungu mwenye mwili ana tofauti kubwa na wanadamu wanaotumiwa na Mungu. Mungu mwenye mwili Anaweza kufanya kazi ya uungu, lakini wanadamu wanaotumiwa na Mungu hawawezi. Mwanzoni mwa kila enzi, Roho wa Mungu huongea binafsi kuzindua enzi mpya na kuleta mwanadamu kwenye mwanzo mpya. Wakati Yeye Amemaliza kuongea, hili linaashiria kwamba kazi ya Mungu katika uungu Wake imekamilika. Baada ya hapo, wanadamu wote hufuata mwongozo wa wale ambao wametumiwa na Mungu kuingia katika uzoefu wa maisha. Vile vile, hii pia ni enzi ambapo Mungu huleta mwanadamu katika enzi mpya na Anampa kila mwanadamu mwanzo mpya. Kwa hilo, kazi ya Mungu katika mwili inahitimishwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Mwenye Mwili na Watu Wanaotumiwa na Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 138)

Mungu haji duniani kufanya ubinadamu Wake wa kawaida uwe mkamilifu. Yeye haji kufanya kazi ya ubinadamu wa kawaida, ila kufanya kazi ya uungu katika ubinadamu wa kawaida. Kile ambacho Mungu huongea kama ubinadamu wa kawaida si kile ambacho mwanadamu anakifikiria kuwa. Mwanadamu hufafanua “ubinadamu wa kawaida” kama kuwa na mke, au mume, na watoto. Huu ni ushahidi kwamba mtu ni mwanadamu wa kawaida. Lakini Mungu haoni hivi. Anaona ubinadamu wa kawaida kama kuwa na mawazo ya kawaida ya binadamu, maisha ya kawaida ya binadamu, na kuzaliwa kwa watu wa kawaida. Lakini kuwa Kwake kawaida hakuhusishi kuwa na mke, au mume na watoto vile ambavyo mwanadamu anavyozungumzia hali ya kawaida. Yaani, kwa mwanadamu, ubinadamu wa kawaida ambao Mungu Anazungumzia ni kile mwanadamu angeona kama kukosekana wa ubinadamu, karibu ukose kuwa na hisia na kuonekana hauna mahitaji ya kimwili, kama vile Yesu, Ambaye kwa nje tu alikuwa mwanadamu wa kawaida na alichukua sura ya mwanadamu wa kawaida, lakini katika kiini hakuwa kabisa na vitu alivyo navyo mwanadamu wa kawaida. Kutokana na hili inaweza kuonekana kwamba dutu ya Mungu mwenye mwili haihusishi ubinadamu wote wa kawaida, lakini sehemu tu ya mambo ambayo wanadamu wanapaswa kuwa nayo, ili kuendeleza utaratibu wa maisha ya kawaida ya binadamu na kuruzuku uwezo wa kawaida wa binadamu wa akili. Lakini hivi vitu havihusiani na kile ambacho mwanadamu anaona kama ubinadamu wa kawaida. Ni vitu ambavyo Mungu mwenye mwili Anapaswa kuwa navyo. Hata hivyo, kuna baadhi ya wanadamu wanaoshikilia kwamba Mungu mwenye mwili Anaweza tu kuwa na ubinadamu wa kawaida iwapo Yeye ana mke, watoto na familia. Bila mambo haya, wanasema, Yeye si mwanadamu wa kawaida. Nakuuliza hivi basi, je, Mungu Ana mke? Je, inawezekana kwa Mungu kuwa na mume? Je, Mungu Anaweza kuwa na watoto? Je, hizi sio dhana zenye kosa tu? Hata hivyo, Mungu mwenye mwili hawezi kuchomoka kutoka katika nyufa kwenye miamba au kuanguka chini kutoka mbinguni. Anaweza tu kuzaliwa kwa familia ya kawaida ya binadamu. Hiyo ndiyo maana Anao wazazi na madada. Haya ndiyo mambo ambayo ubinadamu wa kawaida wa Mungu mwenye mwili lazima Awe nayo. Hivi ndivyo Yesu alivyokuwa. Yesu Alikuwa na baba na mama, na ndugu. Haya yote yalikuwa ya kawaida. Lakini kama Angekuwa na mke na watoto, basi Wake haungekuwa ubinadamu wa kawaida ambao Mungu alitaka Mungu mwenye mwili awe nao. Kama hali ingekuwa hivyo, Yeye Hangekuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa niaba ya uungu. Ilikuwa hasa kwa sababu Hakuwa na mke au watoto lakini Alizaliwa na wanadamu wa kawaida katika familia ya kawaida ndipo yeye alikuwa na uwezo wa kufanya kazi ya uungu. Ili kufafanua hili zaidi, kile ambacho Mungu anaona kama mwanadamu wa kawaida ni mwanadamu aliyezaliwa katika familia ya kawaida. Mwanadamu kama huyo tu ndiye anayestahili kufanya kazi ya Mungu. Kama, kwa upande mwingine, mtu huyo angekuwa na mke, watoto, au mume, mwanadamu huyo basi hangekuwa na uwezo wa kufanya kazi ya uungu kwa sababu angekuwa tu na ubinadamu wa kawaida ambao binadamu wanataka lakini si ubinadamu wa kawaida ambao Mungu anataka. Kile ambacho Mungu huona kuwa na kile ambacho Mungu huelewa ni tofauti sana mara nyingi, havifanani kabisa. Katika hatua hii ya kazi ya Mungu kuna mengi ambayo yanapingana na kutofautiana sana na fikra za wanadamu. Unaweza kusema kwamba hatua hii ya kazi ya Mungu hujumuisha uungu ukifanya kazi moja kwa moja, huku ukisaidiwa na ubinadamu. Kwa sababu Mungu anakuja duniani kufanya kazi Yake Mwenyewe badala ya kumruhusu mwanadamu aifanye, hiyo ndiyo maana Anajipa mwili wa nyama (katika mwanadamu wa kawaida asiye mkamilifu) ili kufanya kazi Yake. Anatumia mwili huu kuwapa wanadamu enzi mpya, kuwaambia wanadamu hatua inayofuata katika kazi Yake, na kuwataka watende kwa mujibu wa njia iliyoelezwa katika maneno Yake. Na hapo Mungu Anakamilisha kazi Yake katika mwili, na yuko karibu kuondoka kwa wanadamu, asiishi tena katika mwili wa ubinadamu wa kawaida, na badala yake kusonga mbali na mwanadamu ili kuendelea na sehemu nyingine ya kazi Yake. Kisha, kwa kutumia wanadamu wanaoupendeza moyo Wake, Anaendeleza kazi Yake hapa duniani miongoni mwa kundi hili la wanadamu, lakini katika ubinadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Mwenye Mwili na Watu Wanaotumiwa na Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 139)

Mungu mwenye mwili hawezi kukaa na mwanadamu milele kwa sababu Mungu Ana kazi zingine nyingi za kufanya. Yeye hawezi kufungwa katika mwili; lazima aondoe mwili ili kufanya kazi ambayo Anahitaji kufanya, ingawa Yeye hufanya kazi hiyo kwa mfano wa mwili. Wakati Mungu Anakuja duniani, Yeye hasubiri hadi Afikie umbo ambalo mwanadamu wa kawaida anapaswa kufika kabla ya kufa na kuwaacha wanadamu. Haijalishi mwili Wake ni mzee vipi, wakati kazi Yake imemalizika, Anaondoka na kumwacha mwanadamu. Hakuna kitu kama umri Kwake, Yeye hahesabu siku zake kulingana na maisha ya mwanadamu; badala yake Yeye hukamilisha maisha Yake katika mwili kulingana na hatua katika kazi Yake. Baadhi ya watu wanaweza kuhisi kwamba Mungu, kwa kuingia katika mwili, lazima akue mpaka afikie hatua fulani, Awe mwanadamu mzima, kufikia umri wa uzee, na kuondoka tu wakati mwili umeshindwa. Haya ni mawazo ya mwanadamu; Mungu hafanyi kazi kwa namna hiyo. Yeye Anakuja katika mwili kufanya kazi Anayostahili kufanya tu, bali si kuishi maisha ya kawaida ya mwanadamu ya kawaida ya kuzaliwa kwa wazazi, kuwa mtu mzima, kutengeneza familia na kuanza kazi, na kulea watoto, au kupitia panda shuka za maisha—shughuli zote za mtu wa kawaida. Mungu anapokuja duniani, huyu ni Roho wa Mungu akivaa mwili, akiingia katika mwili, lakini Mungu Haishi maisha ya mtu wa kawaida. Yeye huja tu kukamilisha sehemu moja katika mpango Wake wa usimamizi. Baada ya hapo Atawaacha wanadamu. Anapoingia katika mwili, Roho wa Mungu hakamilishi ubinadamu wa kawaida wa mwili. Badala Yake, kwa wakati ulioamuliwa kabla na Mungu, uungu unafanya kazi moja kwa moja. Kisha, baada ya kufanya yote ambayo Yeye anahitajika kufanya na kukamilisha huduma Yake kikamilifu, kazi ya Roho wa Mungu katika hatua hii imekamilika, na wakati huo maisha ya Mungu mwenye mwili yanaisha pia, bila kujali kama mwili Wake wa nyama umekamilisha maisha yake au la. Yaani, haijalishi mwili wa nyama unafika hatua gani ya maisha, muda ambao unaishi duniani, yote hutegemea kazi ya Roho. Haihusiani na kile mwanadamu anachoona kuwa ubinadamu wa kawaida. Chukua Yesu kama mfano. Yeye Aliishi katika mwili kwa miaka thelathini na mitatu na nusu. Kuhusiana na urefu wa maisha ya mwili wa binadamu, Yeye Hakupaswa kufariki Akiwa na umri huo na Hakupaswa kuondoka. Lakini Roho wa Mungu hakujali kuhusu hayo hata kidogo. Baada ya kazi Yake kumalizika, hapo mwili ulichukuliwa, ukitoweka pamoja na Roho. Hii ni kanuni ambayo Mungu hutumia kufanya kazi katika mwili. Na hivyo, kusema kwa uzito kabisa, ubinadamu wa Mungu mwenye mwili si lenye umuhimu wa kimsingi. Kusema tena, Yeye haji duniani kuishi maisha ya mtu wa kawaida. Yeye kwanza haasisi maisha ya kawaida ya binadamu na kisha Aanze kufanya kazi. Badala Yake, alimradi tu Amezaliwa katika familia ya kawaida ya binadamu, Yeye ana uwezo wa kufanya kazi ya Mungu, ambayo haijatiwa doa na nia zap mwanadamu, ambayo si ya mwili ambayo hakika haitumii njia za jamii au kuhusisha mawazo au fikra za mwanadamu, na aidha, isiyohusiana na falsafa za binadamu za kuishi. Hii ni kazi ambayo Mungu mwenye mwili ananuia kufanya, na pia ni umuhimu wa vitendo wa kupata mwili Kwake. Mungu anakuja katika mwili kimsingi kufanya hatua ya kazi inayohitaji kufanyika katika mwili, bila kupitia michakato mingine isiyo na maana, na, hana uzoefu wa mwanadamu wa kawaida. Kazi ambayo Mungu mwenye mwili anahitaji kufanya haihusishi uzoefu wa kawaida wa binadamu. Hivyo, Mungu Anakuja katika mwili ili kumaliza kazi Anayohitaji kukamilisha katika mwili. Yaliyobaki Hayamhusu. Hapitii michakato mingi isiyo ya maana hivyo. Mara kazi Yake inapokamilika, umuhimu wa kupata mwili Kwake pia unaisha. Kumaliza hatua hii kuna maana kwamba kazi ambayo Yeye Anahitajika kufanya katika mwili imekamilika, na huduma ya mwili Wake imekamilika. Lakini Yeye hawezi kuendelea kufanya kazi katika mwili kwa muda usio na mwisho. Yeye lazima aende mahali pengine kufanya kazi, mahali ambapo ni nje ya mwili. Ni kwa njia hii tu ndio kazi Yake inaweza kuwa kamili zaidi, na kupanuka vizuri zaidi. Mungu hufanya kazi kulingana na mpango Wake wa awali. Yeye Anajua vyema kazi Anayohitaji kufanya na kazi Aliyomaliza kama kiganja cha mkono Wake. Mungu humwongoza kila mwanadamu kutembelea njia ambayo Yeye tayari Ameamua. Hakuna anayeweza kuepuka hili. Ni wale tu ambao hufuata uongozi wa Roho wa Mungu ndio watakaokuwa na uwezo wa kuingia katika pumziko. Huenda ikawa kwamba, katika kazi ya baadaye, sio Mungu Atakayezungumza katika mwili ili kumwongoza mwanadamu, ila Roho anayegusika akiongoza maisha ya mwanadamu. Hapo tu ndipo mwanadamu atakuwa na uwezo thabiti wa kumgusa Mungu, kumwona Mungu, na kwa kikamilifu zaidi kuingia katika uhalisi ambao Mungu anataka, ili aweze kukamilishwa na Mungu wa vitendo. Hii ndiyo kazi ambayo Mungu ananuia kukamilisha, ambayo amepanga tangu zamani. Kutokana na hili, nyote mnapaswa kuona njia ambayo mnafaa kuchukua!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Mwenye Mwili na Watu Wanaotumiwa na Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 140)

Mungu aliyepata mwili Anaitwa Kristo, na hivyo Kristo ambaye Anaweza kuwapa binadamu ukweli anaitwa Mungu. Hakuna kitu kikuu kuliko hiki, kwa kuwa Anayo hali ya Mungu, na ana tabia za Mungu, na hekima katika kazi Yake, ambayo haiwezi kupatikana kwa binadamu. Wale wanaojiita Kristo, walakini hawawezi kufanya kazi ya Mungu, ni matapeli. Kristo sio tu udhihirisho wa Mungu duniani, bali pia, mwili hasa ulioigwa na Mungu kufanya na kutimiza kazi Yake kati ya wanadamu. Mwili huu si ule unaoweza kubadilishwa na mtu yeyote tu, lakini ambao unaweza kutosha kufanya kazi ya Mungu duniani, na kueleza tabia ya Mungu, na pia kumwakilisha Mungu, na kumpa binadamu maisha. Hivi karibuni au baadaye, wale wanaojifanya kuwa Kristo wataanguka wote, ingawa wanadai kuwa Kristo, hawana chochote cha hali ya Kristo. Na hivyo Mimi nasema kwamba hali halisi ya Kristo haiwezi kuelezwa na mwanadamu, bali inajibiwa na kuamuliwa na Mungu Mwenyewe. Kwa njia hii, kama kweli unataka kutafuta njia ya maisha, lazima kwanza ukiri kuwa ni kwa kuja duniani ndipo Anazirejesha njia za maisha kwa binadamu, na lazima kukiri ni katika siku za mwisho Yeye anakuja duniani kuhifadhia njia ya maisha kwa mwanadamu. Haya sio ya wakati wa nyuma; yanatendeka leo.

Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo kwayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maandiko, na waliofungwa na historia kamwe hawataweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hiyo ni kwa sababu yote walio nayo ni maji machafu ambayo yameshikiliwa kwa maelfu ya miaka badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. Wale ambao hawajaruzukiwa maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya kuchezewa na Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Kama wewe kamwe hujaribu kushikilia kwenye siku zilizopita, jaribu tu kuweka mambo kama yalivyo kwa kusimama kwa utulivu, na wala hujaribu kubadili hali kama ilivyo na kuacha historia, basi wewe hutakuwa daima dhidi ya Mungu? Hatua za kazi ya Mungu ni kubwa na zenye nguvu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—ilhali wewe unakaa na kwa uvivu ukisubiri uharibifu, na kujikita katika upumbavu wako na kutofanya chochote. Kwa njia hii, jinsi gani unaweza kuchukuliwa kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Jinsi gani unaweza kuhalalisha Mungu unayeshikilia kama Mungu ambaye ni daima mpya na si kamwe wa zamani? Na jinsi gani maneno ya vitabu vyako vya manjano yanaweza kukubeba hadi enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi ni barua ambazo zisizoweza kukuondolea kitu ila furaha ya muda mfupi, sio ukweli unaoweza kukupa maisha. Maandiko unayosoma ni yale tu ambayo yanaweza kuimarisha ulimi wako, sio maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua maisha ya binadamu, sembuse njia zinazoweza kukuongoza kuelekea kwa ukamilifu. Je, si tofauti hii hukupa sababu kwa ajili ya kutafakari? Je, si inakuruhusu kuelewa siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Bila kuja kwa Mungu, je, unaweza kujichukua mwenyewe kwenda mbinguni kufurahia pamoja na familia ya Mungu? Je, wewe bado unaota sasa? Basi, Napendekeza sasa acha kuota, na kuangalia Anayefanya kazi sasa, na Anayefanya kazi ya kuwaokoa binadamu siku za mwisho. Kama huwezi, wewe kamwe hutapata ukweli, na kamwe hutapata uzima.

Wale ambao wanataka kupata uzima bila kutegemea ukweli wa neno la Kristo ni watu wafidhuli mno duniani, na wale ambao hawawezi kukubali njia ya maisha inayoletwa na Kristo wamepotea ndotoni. Na hivyo nasema kwamba watu ambao hawakubali Kristo wa siku za mwisho watadharauliwa milele na Mungu. Kristo ni lango la binadamu kwa ufalme katika siku za mwisho, ambayo hakuna anayeweza kupita bila Yeye. Hakuna anayeweza kukamilishwa na Mungu ila kwa njia ya Kristo. Unaamini katika Mungu, na hivyo ni lazima ukubali neno Lake na kutii njia Yake. Lazima usifikiri juu ya kupata baraka tu bila kupokea ukweli, au kukubali utoaji wa maisha. Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili wale wote ambao kweli wanaamini katika Yeye waweze kupata maisha. Kazi Yake ni kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuingia enzi mpya, na ni njia ambayo lazima ichukuliwe na wale wote ambao wataingia enzi mpya. Kama huna uwezo wa kumtambua Yeye, na badala yake kumhukumu, kulikufuru jina Lake au hata kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele, na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu. Kwa maana Kristo Mwenyewe ni onyesho la Roho Mtakatifu, onyesho la Mungu, Yule ambaye Mungu amemkabidhi kufanya kazi Yake hapa duniani. Na hivyo nasema kwamba kama huwezi kukubali yote yanayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, basi unakufuru Roho Mtakatifu. Adhabu ambayo lazima ishuhudiwe na wale ambao wanakufuru Roho Mtakatifu ni hasa dhahiri kwa wote. Nawaambia tena kwamba kama mtampinga Kristo wa siku za mwisho, na kumkanusha, basi hakuna mtu ambaye anaweza kubeba matokeo ya hilo kwa niaba yako. Aidha, tangu siku hii na kuendelea huwezi kuwa na nafasi nyingine ya kupata kibali cha Mungu; hata kama utajaribu kujikomboa mwenyewe, kamwe tena hutautazama uso wa Mungu. Kwa kuwa unachopinga si binadamu, unachokataa si jambo dogo, bali ni Kristo. Je, unafahamu ghadhabu ya matokeo haya? Wewe hujafanya makosa madogo, bali umetenda uhalifu wa kutisha. Na hivyo Nashauri kila mtu kutoweka wazi meno yenu mbele ya ukweli, au kufanya shutuma bila ya kujali, kwa kuwa ni ukweli tu unaoweza kukuletea maisha, na hakuna kitu isipokuwa ukweli kinachoweza kukuruhusu kuzaliwa upya na kutazama uso wa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Iliyotangulia: Hukumu Katika Siku za Mwisho

Inayofuata: Kujua Kazi ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp