Kujua Kazi ya Mungu (I)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 141)

Kuijua kazi ya Mungu katika nyakati hizi, kwa sehemu kubwa, ni kujua kile ambacho ni huduma kuu ya Mungu katika mwili katika siku za mwisho, na kile ambacho Amekuja kufanya duniani. Hapo mwanzoni Nimesema katika maneno Yangu kwamba Mungu Amekuja duniani (katika siku za mwisho) ili kuweka mfano kabla Hajaondoka. Ni kwa jinsi gani Mungu Ameuweka mfano huu? Kwa kuzungumza maneno, kwa kufanya kazi na kuzungumza katika nchi nzima. Hii ni kazi ya Mungu wakati wa siku za mwisho; Anazungumza tu ili dunia iwe ulimwengu wa maneno, ili kila mtu awe amepewa na kutiwa nuru maneno Yake, na ili roho ya mwanadamu iamshwe na aweze kuona vizuri kuhusu maono yake. Wakati wa siku za mwisho, Mungu katika mwili Amekuja duniani hasa kwa ajili ya kuzungumza maneno. Yesu Alipokuja, Alieneza injili ya ufalme wa mbinguni, na Akatimiza kazi ya wokovu wa msalaba. Alihitimisha Enzi ya Sheria, na Akakomesha mambo yote ya kale. Ujio wa Yesu ulihitimisha Enzi ya Sheria na kuanzisha Enzi ya Neema. Ujio wa Mungu katika mwili wa siku za mwisho umehitimisha Enzi ya Neema. Amekuja hasa kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake, kutumia maneno ili kumfanya mwanadamu mkamilifu, kumwangazia na kumpa nuru mwanadamu, na kumwondoa Mungu asiye yakini katika moyo wa mwanadamu. Hii sio hatua ya kazi ambayo Yesu Aliifanya Alipokuja. Yesu Alipokuja, Alifanya miujiza mingi, Aliponya wagonjwa na kutoa mapepo, na Alifanya kazi ya wokovu ya msalaba. Na matokeo yake ni kwamba, katika dhana za mwanadamu, mwanadamu anaamini kwamba hivi ndivyo Mungu Anapaswa kuwa. Maana Yesu Alipokuja, hakufanya kazi ya kuondoa taswira ya Mungu asiye yakini moyoni mwa mwanadamu; Alipokuja, Alisulubishwa, Aliponya wagonjwa na kutoa mapepo, na Alieneza injili ya ufalme wa mbinguni. Kwa upande mmoja, Mungu katika mwili katika siku za mwisho Anaondoa nafasi iliyochukuliwa na Mungu asiye yakini katika dhana za mwanadamu, ili taswira ya Mungu asiye yakini isiwepo kabisa katika moyo wa mwanadamu. Kwa kutumia maneno Yake halisi na kazi Yake halisi, Anazunguka katika nchi zote, na kazi Anayoifanya miongoni mwa wanadamu ni halisi kabisa na ya kawaida, kana kwamba mwanadamu anakuja kujua uhalisia wa Mungu na Mungu asiye yakini Anapoteza nafasi Yake moyoni mwake. Kwa upande mwingine, Mungu Anatumia maneno yaliyozungumzwa na mwili Wake ili kumfanya mwanadamu mkamilifu, na kukamilisha vitu vyote. Hii ndiyo kazi ambayo Mungu Ataikamilisha wakati wa siku za mwisho.

Kile mnachopaswa kujua:

1. Kazi ya Mungu si ya kimiujiza, na hampaswi kuhifadhi dhana juu yake.

2. Mnapaswa kuelewa kazi kuu ambayo Mungu katika mwili Amekuja kufanya wakati huu.

Hakuja kuponya wagonjwa, au kutoa mapepo, au kufanya miujiza, na Hajakuja kueneza injili ya toba, au kumpatia mwanadamu ukombozi. Hiyo ni kwa sababu Yesu Amekwishafanya kazi hii, na Mungu Harudii kazi ile ile. Leo, Mungu Amekuja kuhitimisha Enzi ya Neema, na kuzitupilia mbali desturi zote za Enzi ya Neema. Mungu wa vitendo Amekuja hasa kuonyesha kuwa Yeye ni halisi. Yesu Alipokuja Alizungumza maneno machache; hasa Alionyesha miujiza, Akafanya ishara na maajabu, na Akaponya wagonjwa na kutoa mapepo, au wakati mwingine Alizungumza unabii ili kumshawishi mwanadamu, na kumfanya mwanadamu aone kwamba ni kweli Alikuwa Mungu, na Alikuwa Mungu Asiyependelea. Hatimaye, Akakamilisha kazi ya msalaba. Mungu wa leo Haonyeshi ishara na maajabu, wala Haponyi wagonjwa na kutoa mapepo. Yesu Alipokuja, kazi Aliyoifanya iliwakilisha upande mmoja wa Mungu, lakini wakati huu Mungu Amekuja kufanya hatua ya kazi ambayo imetazamiwa, maana Mungu Harudii kazi ile ile; ni Mungu ambaye siku zote ni mpya na Hawezi kuzeeka kamwe, na hivyo yale yote unayoyaona leo ni maneno na kazi ya Mungu wa vitendo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuijua Kazi ya Mungu Leo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 142)

Mungu katika mwili wa siku za mwisho Amekuja hasa kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake, ili kuelezea yale yote ambayo ni ya lazima katika maisha ya mwanadamu, kuonyesha yale ambayo mwanadamu anapaswa kuingia kwayo, kumwonesha mwanadamu matendo ya Mungu, na kumwonesha mwanadamu hekima, uweza na uajabu wa Mungu. Kupitia njia nyingi ambazo Mungu Anazungumza, mwanadamu anatazama ukuu wa Mungu, aidha, unyenyekevu na usiri wa Mungu. Mwanadamu anatazama kwamba Mungu ni mkuu, lakini ni mnyenyekevu na msiri, na Anaweza kuwa mdogo kuliko vitu vyote. Baadhi ya maneno Yake yanazungumzwa moja kwa moja kutoka kwa mtazamo wa Roho, baadhi ya hayo moja kwa moja kutoka katika mtazamo wa mwanadamu, na baadhi kutoka katika mtazamo wa nafsi ya tatu. Katika hili, inaweza kuonekana kwamba namna ya kazi ya Mungu inatofautiana kwa kiasi kikubwa na ni kwa njia ya maneno ndipo Anamruhusu mwanadamu kuiona. Kazi ya Mungu wakati wa siku za mwisho ni ya kawaida na halisi, na hivyo kundi la watu wa siku za mwisho wanakumbwa na majaribu makubwa kuliko yote. Kwa sababu ya ukawaida na uhalisia wa Mungu, watu wote wameingia katika majaribu hayo; kwamba mwanadamu ameingia katika majaribu ya Mungu ni kwa sababu ya ukawaida na uhalisia wa Mungu. Wakati wa enzi ya Yesu, hakukuwa na dhana au majaribu. Kwa sababu kazi kubwa iliyofanywa na Yesu ilikuwa ni kulingana na dhana za mwanadamu, watu walimfuata, na hawakuwa na dhana juu Yake. Majaribu ya leo ni makubwa sana ambayo yamewahi kukabiliwa na mwanadamu, na inaposemwa kwamba watu hawa wametoka katika dhiki kuu, hii ndiyo dhiki inayoongelewa. Leo, Mungu Ananena ili kusababisha imani, upendo, ustahimilivu na utii kwa watu hawa. Maneno yaliyozungumzwa na Mungu katika mwili wa siku za mwisho ni kutokana na hulka ya asili ya mwanadamu, kulingana na tabia ya mwanadamu, na kulingana na kile ambacho mwanadamu anapaswa kuingia kwacho leo. Maneno ni halisi na ya kawaida: Hazungumzi juu ya kesho, wala Haangalii nyuma, jana; Anazungumza kile tu ambacho kinapaswa kuingiwa kwacho, kuwekwa katika vitendo, na kueleweka leo. Kama, wakati wa zama hizi, kutatokea mtu mwenye uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, na kutoa mapepo, kuponya wagonjwa, na kufanya miujiza mingi, na kama mtu huyu anadai kwamba yeye ni Yesu ambaye amekuja, basi hii itakuwa ni ghushi ya roho wachafu, na kumuiga Yesu. Kumbuka hili! Mungu Harudii kazi ile ile. Hatua ya kazi ya Yesu tayari imekwisha kamilika, na Mungu Hataichukua tena hatua hiyo ya kazi. Kazi ya Mungu haipatani na dhana za mwanadamu; kwa mfano, Agano la Kale lilitabiri juu ya ujio wa Masihi, lakini ilikuwa dhahiri kwamba Yesu Alikuja, hivyo itakuwa makosa kwa Masihi mwingine kuja tena. Yesu tayari Amekwishakuja mara moja, na yatakuwa ni makosa ikiwa Yesu Atakuja tena wakati huu. Kuna jina moja kwa kila enzi, na kila jina linaeleza sifa ya enzi. Katika dhana za mwanadamu, Mungu ni lazima siku zote Aonyeshe ishara na maajabu, ni lazima siku zote Aponye wagonjwa na kutoa mapepo, na siku zote ni lazima Awe tu kama Yesu, lakini Mungu wakati huu Hayupo kama hivyo kabisa. Ikiwa, wakati wa siku za mwisho, Mungu bado Angeonyesha ishara na maajabu, na bado Angetoa mapepo na kuponya wagonjwa—kama Angefanya vilevile ambavyo Yesu Alifanya—basi Mungu Angekuwa Anarudia kazi ile ile, na kazi ya Yesu isingekuwa na maana au thamani yoyote. Hivyo, Mungu Anatekeleza hatua moja ya kazi katika kila enzi. Mara tu kila hatua ya kazi Yake inapokamilika, baada ya muda mfupi inaigizwa na roho wachafu, na baada ya Shetani kuanza kufuata nyayo za Mungu, Mungu Anabadilisha na kutumia mbinu nyingine. Mara Mungu Anapokamilisha hatua ya kazi Yake, inaigizwa na roho wachafu. Lazima muelewe vizuri hili. Kwa nini kazi ya Mungu leo ni tofauti na kazi ya Yesu? Kwa nini Mungu leo Haonyeshi ishara na maajabu, Hatoi mapepo, na Haponyi wagonjwa? Ikiwa kazi ya Yesu ingekuwa sawa na kazi iliyofanywa katika Enzi ya Sheria, je, Angekuwa Amemwakilisha Mungu wa Enzi ya Neema? Je, Yeye Angekuwa Amemaliza kazi ya msalaba? Ikiwa, kama katika Enzi ya Sheria, Yesu Angeingia hekaluni na kuitunza Sabato, basi Asingeteswa na mtu yeyote na Angekumbatiwa na wote. Kama ingekuwa hivyo, je, Angesulubiwa? Je, Angekuwa Amemaliza kazi ya ukombozi? Je, ingekuwa na maana gani ikiwa Mungu katika mwili wa siku za mwisho Angeonyesha ishara na maajabu kama Yesu? Ikiwa tu Mungu Atafanya sehemu nyingine ya kazi Yake wakati wa siku za mwisho, kazi inayowakilisha sehemu ya mpango wa usimamizi Wake, ndipo mwanadamu anaweza kupata maarifa ya kina ya Mungu, na baada ya hapo tu ndipo mpango wa usimamizi wa Mungu unaweza kukamilika.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuijua Kazi ya Mungu Leo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 143)

Wakati wa siku za mwisho, Mungu Amekuja mahususi kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake. Anazungumza kutokana na mtazamo wa Roho, kutokana na mtazamo wa mwanadamu, na kutokana na mtazamo wa nafsi ya tatu; Anazungumza kwa namna tofauti, Akitumia njia moja kwa kipindi fulani, na Anatumia njia za kuzungumza ili kubadilisha dhana za mwanadamu na kuondoa taswira ya Mungu yakini katika moyo wa mwanadamu. Hii ndiyo kazi kuu iliyofanywa na Mungu. Kwa sababu mwanadamu anaamini kwamba Mungu Amekuja kuponya wagonjwa, kutoa mapepo, kufanya miujiza, na kumpatia mwanadamu baraka za vitu, Mungu Anatekeleza hatua hii ya kazi—kazi ya kuadibu na hukumu—ili kuweza kuondoa mambo hayo kutoka katika dhana za mwanadamu, ili mwanadamu aweze kuuelewa uhalisia na ukawaida wa Mungu, na ili kwamba taswira ya Yesu iweze kuondolewa moyoni mwake na kuwekwa taswira mpya ya Mungu. Mara tu taswira ya Mungu ndani ya mwanadamu inapozeeka, basi inakuwa sanamu. Yesu alipokuja na kutekeleza hatua hii ya kazi, Hakuwakilisha Mungu kikamilifu. Alifanya baadhi ya ishara na maajabu, Alizungumza maneno kadhaa, na hatimaye Akasulubishwa, na Aliwakilisha upande mmoja wa Mungu. Hakuweza kuwakilisha yale yote ambayo ni ya Mungu, bali Alimwakilisha Mungu katika kufanya upande mmoja wa kazi ya Mungu. Hiyo ni kwa sababu Mungu ni mkuu, na ni wa ajabu sana, na Haeleweki, na kwa sababu Mungu Anafanya upande mmoja tu wa kazi Yake katika kila enzi. Kazi inayofanywa na Mungu katika enzi hii ni hasa ya kutoa maneno kwa ajili ya uzima wa mwanadamu; kufunuliwa kwa tabia potovu ya mwanadamu na kiini cha asili ya mwanadamu; na uondoaji wa fikira za kidini, fikra za kinjozi, mitazamo iliyopitwa na wakati, vilevile maarifa na utamaduni wa mwanadamu. Hii ni lazima iwekwe wazi na kusafishwa kupitia maneno ya Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu Anatumia maneno na siyo ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Anatumia maneno Yake kumweka wazi mwanadamu, kumhukumu mwanadamu, kumwadibu mwanadamu, na kumkamilisha mwanadamu, ili katika maneno ya Mungu, mwanadamu aje kuona hekima na wema wa Mungu, na aje kuelewa tabia ya Mungu, ili kupitia maneno ya Mungu, mwanadamu aone matendo ya Mungu. Wakati wa Enzi ya Sheria, Yehova Alimwongoza Musa kutoka Misri kwa maneno Yake, na Akazungumza maneno fulani kwa Wanaisraeli; wakati huo, sehemu ya matendo ya Mungu yaliwekwa wazi, lakini kwa sababu ubora wa tabia ya mwanadamu ulikuwa finyu na hakuna kitu chochote ambacho kingeweza kufanya maarifa yake kukamilika, Mungu Aliendelea kuzungumza na kufanya kazi. Wakati wa Enzi ya Neema, mwanadamu aliweza kuona tena sehemu ya matendo ya Mungu. Yesu Aliweza kuonyesha ishara na maajabu, kuponya wagonjwa na kutoa mapepo, na kusulubishwa, siku tatu baadaye. Akafufuka na Akawatokea watu Akiwa katika mwili. Kumhusu Mungu, mwanadamu hakujua chochote zaidi ya hiki. Mwanadamu anajua tu kile ambacho Mungu Amemwonyesha, na kama Mungu Asingeonyesha chochote zaidi kwa mwanadamu, basi hicho kingekuwa kiwango cha mwanadamu kumwekea mipaka Mungu. Hivyo, Mungu Anaendelea kufanya kazi, ili maarifa ya mwanadamu juu Yake yaweze kuwa ya kina zaidi, na ili taratibu aweze kuijua hulka ya Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu anatumia maneno yake kumkamilisha mwanadamu. Tabia yako iliyoharibika imewekwa wazi kwa maneno ya Mungu, na dhana zako za kidini zinaondolewa na uhalisia wa Mungu. Mungu katika mwili wa siku za mwisho Amekuja hasa kwa ajili ya kutimiza maneno haya kwamba “Neno Lafanyika kuwa mwili, Neno Lakuwa mwili, na Neno Laonekana katika mwili,” na kama huna maarifa ya kina kuhusu hili, basi hutaweza kusimama imara. Wakati wa siku za mwisho, kimsingi Mungu Anakusudia kukamilisha hatua ya kazi ambayo kwayo Neno Anaonekana katika mwili, na hii ni sehemu moja ya mpango wa usimamizi wa Mungu. Hivyo, maarifa yenu yanapaswa kuwa wazi; bila kujali namna ambavyo Mungu Anafanya kazi, Mungu Hamruhusu mwanadamu kumwekea mipaka. Ikiwa Mungu Asingefanya kazi hii wakati wa siku za mwisho, basi maarifa ya mwanadamu juu Yake yasingeweza kwenda popote. Ungeweza kujua tu kwamba Mungu Anaweza kusulubiwa na Anaweza kuiangamiza Sodoma, na kwamba Yesu Anaweza kufufuliwa kutoka katika wafu na kumtokea Petro.... Lakini usingeweza kusema kwamba maneno ya Mungu yanaweza kutimiza yote, na yanaweza kumshinda mwanadamu. Ni kwa njia tu ya kupitia uzoefu wa maneno ya Mungu ndipo unaweza kuzungumza juu ya maarifa hayo, na kadri unapopitia uzoefu wa kazi ya Mungu zaidi, ndivyo maarifa yako yanavyokuwa ya kina zaidi kumhusu Yeye. Ni baada ya hapo tu ndipo utaacha kumwekea Mungu mipaka ndani ya dhana zako binafsi. Mwanadamu anakuja kumjua Mungu kwa kupitia kazi Yake, na hakuna njia nyingine sahihi ya kumjua Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuijua Kazi ya Mungu Leo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 144)

Leo, inapaswa kueleweka kwenu wote kwamba, katika siku za mwisho, ni kwa kiasi kikubwa ukweli wa “Neno linakuwa mwili” ambao unakamilishwa na Mungu. Kupitia kazi yake halisi duniani, Anafanya mwanadamu kumfahamu, na kushirikiana Naye, na kuona matendo Yake halisi. Anamsababisha mwanadamu kuona kwa wazi kwamba Yeye Anaweza kuonyesha ishara na maajabu na pia kuna nyakati ambapo Hawezi kufanya hivyo, na hii inategemea enzi. Kutokana na hili unaweza kuona kwamba Mungu sio kwamba Hawezi kuonyesha ishara na maajabu, lakini badala yake Anabadilisha kufanya kazi Kwake kulingana na kazi Yake, na kulingana na enzi. Katika hatua ya sasa ya kazi, Haonyeshi ishara na maajabu; kuonyesha kwake baadhi ya ishara na maajabu katika enzi ya Yesu, ilikuwa ni kwa sababu kazi Yake katika enzi hiyo ilikuwa tofauti. Mungu Hafanyi kazi hiyo leo, na baadhi ya watu wanaamini Hana uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, au wanafikiri kwamba kama Haonyeshi ishara na maajabu, basi Yeye si Mungu. Hii sio hoja ya uwongo? Mungu Anaweza kuonyesha ishara na maajabu, lakini Anafanya kazi katika enzi tofauti, na hivyo Hafanyi kazi hiyo. Kwa kuwa hii ni enzi tofauti, na kwa kuwa hii ni hatua tofauti ya kazi ya Mungu, matendo yaliyowekwa wazi na Mungu pia ni tofauti. Imani ya mwanadamu kwa Mungu sio imani katika ishara na maajabu, wala imani katika miujiza, bali ni imani katika kazi Yake halisi wakati wa enzi mpya. Mwanadamu anamjua Mungu kupitia namna ambavyo Mungu Anafanya kazi, na maarifa haya yanamfanya mwanadamu amwamini Mungu, ambavyo ni kusema, imani katika kazi na matendo ya Mungu. Katika hatua hii ya kazi, Mungu Anazungumza hasa. Usisubiri kuona ishara na maajabu; hutayaona! Maana hukuzaliwa katika Enzi ya Neema. Kama ungezaliwa katika Enzi ya Neema, ungeweza kuona ishara na maajabu, lakini umezaliwa katika siku za mwisho, na hivyo unaweza kuona tu uhalisia na ukawaida wa Mungu. Usitarajie kumwona Yesu wa kimiujiza wakati wa siku za mwisho. Unaweza kumwona tu Mungu katika mwili wa vitendo, Ambaye si tofauti na mwanadamu yeyote wa kawaida. Katika kila enzi, Mungu Anaweka wazi matendo mbalimbali. Katika kila enzi Anaweka wazi sehemu ya matendo ya Mungu, na kazi ya kila enzi inawakilisha sehemu moja ya tabia ya Mungu, na inawakilisha sehemu moja ya matendo ya Mungu. Matendo Anayoyaweka wazi yanatofautiana na enzi ambayo kwayo Anafanya kazi, lakini yote yanampatia mwanadamu maarifa ya Mungu ambayo ni ya kina, imani kwa Mungu ambayo ni yenye kuhusika na mambo halisi sana, na ambayo ni ya kweli zaidi. Mwanadamu anamwamini Mungu kwa sababu ya matendo yote ya Mungu, na kwa sababu Mungu ni wa ajabu ni mkuu sana, kwa sababu Yeye ni mwenyezi, na ambaye Hapimiki kina. Ikiwa unamwamini Mungu kwa kuwa Anaweza kufanya ishara na maajabu na Anaweza kuponya wagonjwa na kuwatoa mapepo, basi mtazamo wako si sahihi, na baadhi ya watu watakwambia, “Je, pepo wachafu pia hawawezi kufanya mambo hayo?” Je, hii sio kuielewa vibaya taswira ya Mungu kwa kuilinganisha na taswira ya Shetani? Leo, imani ya mwanadamu kwa Mungu ni kwa sababu ya matendo Yake mengi na kiasi kikubwa cha kazi Anachofanya na njia nyingi ambazo kwazo Ananena. Mungu Anatumia matamshi yake kumshinda mwanadamu na kumfanya mkamilifu. Mwanadamu anamwamini Mungu, kwa sababu ya matendo Yake mengi, na si kwa sababu Anaweza kuonyesha ishara na maajabu, na wanadamu wanamwelewa tu kwa sababu wanaona matendo Yake, Ni kwa kujua tu matendo halisi ya Mungu, namna Anavyofanya kazi, njia ambazo Anaonyesha hekima Yake, vile Anavyozungumza, na jinsi Anavyomfanya mwanadamu kuwa mkamilifu—ni kwa kujua tu vipengele hivi—ndipo unaweza kufahamu uhalisia wa Mungu na kuelewa tabia Yake, kujua kile Anachopenda, kile Anachochukia, namna Anavyomfanyia kazi mwanadamu. Kwa kuelewa yale ambayo Mungu Anayapenda na Asiyoyapenda, unaweza kutofautisha kati ya kile ambacho ni chanya na kile ambacho ni hasi, na kupitia maarifa yako juu ya Mungu kunakuwa na maendeleo katika maisha yako. Kwa ufupi unapaswa kuwa na maarifa ya kazi ya Mungu, na unapaswa kuweka sahihi mitazamo yako kuhusu kuwa na imani kwa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuijua Kazi ya Mungu Leo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 145)

Haijalishi unavyofuatilia, unapaswa kuelewa kazi ambayo Mungu anaifanya leo, na unapaswa kuelewa umuhimu wa kazi hii. Unapaswa kuelewa na kujua ni kazi gani ambayo Mungu anaileta, Atakapokuja katika siku za mwisho, ni tabia gani Anayoileta, na kile kitakachofanywa kikamilifu kwa mwanadamu. Ikiwa hujui au huielewi kazi ambayo Amekuja kufanya katika mwili, basi unawezaje kufahamu mapenzi Yake, na unawezaje kuwa mwandani Wake? Kwa kweli, kuwa mwandani wa Mungu si vigumu, lakini pia si rahisi. Ikiwa watu wanaweza kuuelewa na kutekeleza, basi kuwa isiyo na ugumu; ikiwa watu hawawezi kuuelewa vilivyo, basi inakuja kuwa ngumu zaidi, na, zaidi, wanakuwa rahisi kuwa wenye ufuatiliaji wao unawafanya wawe wasio yakini. Ikiwa, katika kumfuatilia Mungu, mwanadamu hana msimamo wake wa kusimamia, na hajui ni ukweli gani anapaswa kuufuata, basi ina maana kwamba hana msingi, na hivyo si rahisi kwake kusimama imara. Leo, kuna wengi ambao hawauelewi ukweli, ambao hawawezi kutofautisha kati ya wema na uovu au kipi cha kupenda na kipi cha kuchukia. Watu kama hawa ni vigumu kusimama imara. Kitu cha msingi katika imani kwa Mungu ni kuwa na uwezo wa kuweka ukweli katika matendo, kujali mapenzi ya Mungu, kujua kazi ya Mungu kwa mwanadamu anapokuja katika mwili na kanuni ambazo kwazo Anazungumza; usifuate wengi, na unapaswa kuwa na kanuni katika kile unachokiingia, na unapaswa kuzishika imara. Kuyashikilia imara mambo ambayo yameangaziwa na Mungu kwako ni msaada kwako. Usipofanya hivyo, leo utakwenda njia moja, kesho utakwenda njia nyingine, na hutapata kitu chochote halisi. Kuwa hivi hakuna manufaa yoyote katika maisha yako. Wale ambao hawauelewi ukweli siku zote wanawafuata wengine. Ikiwa watu wanasema kwamba hii ni kazi ya Roho Mtakatifu, basi, wewe pia utasema ni kazi ya Roho Mtakatifu; ikiwa watu watasema ni kazi ya roho mchafu, basi wewe pia utatilia mashaka, au utasema ni kazi ya roho mchafu. Siku zote unakuwa kama kasuku kwa maneno ya wengine, na huwezi kutofautisha kitu chochote wewe mwenyewe, wala huwezi kufikiri kwa ajili yako mwenyewe. Huyu ni mtu ambaye hana msimamo, ambaye hana uwezo wa kutofautisha—mtu wa aina hiyo ni masikini asiye na thamani. Wewe siku zote hurudia maneno ya wengine: Leo inasemwa kuwa hii ni kazi ya Roho Mtakatifu, lakini kuna uwezekano siku moja mtu atasema si kazi ya Roho Mtakatifu, na si chochote bali matendo ya mwanadamu—na bado huwezi kuelewa, na utakaposhuhudia watu wengine wanasema hivyo, nawe pia unasema kitu kile kile. Kwa kweli ni kazi ya Roho Mtakatifu, lakini unasema ni kazi ya mwanadamu; hujawa mmoja wa wale wanaoikufuru kazi ya Roho Mtakatifu? Katika hili, hujampinga Mungu kwa sababu huwezi kutofautisha? Nani ajuaye, labda siku moja mtu atatokea na kusema “hii ni kazi ya roho mchafu,” na utakaposikia maneno haya utapotea, na kwa mara nyingine tena unafungwa na maneno ya wengine. Kila wakati mtu anapochochea usumbufu huwezi kusimama katika msimamo wako, na hii ni kwa sababu huna ukweli ndani yako. Kuamini katika Mungu na kutafuta maarifa ya Mungu si jambo rahisi. Hayawezi kupatikana kwa kukusanyika pamoja na kusikiliza mahubiri, na huwezi kukamilishwa kwa kupenda tu. Lazima upitie uzoefu, na ujue, na kuongozwa na kanuni katika matendo yako, na kupata kazi za Roho Mtakatifu. Utakapopitia katika uzoefu, utakuwa na uwezo wa kutofautisha mambo mengi—utakuwa na uwezo wa kutofautisha kati ya mema na mabaya, kati ya haki na uovu, kati ya kile ambacho ni cha mwili na damu na kile ambacho ni cha kweli. Unapaswa kuwa na uwezo wa kutofautisha kati ya mambo haya yote, na kwa kufanya hivyo, haijalishi ni mazingira gani, hutapotea kamwe. Hiki tu ndicho kimo chako halisi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 146)

Kuijua kazi ya Mungu si jambo rahisi. Unapaswa kuwa na viwango na malengo katika utafutaji wako, unapaswa kujua jinsi ya kutafuta njia ya kweli, na jinsi ya kupima kujua kama ni njia ya kweli au si ya kweli, na kama ni kazi ya Mungu au kinyume chake. Kanuni ya msingi kabisa katika kuutafuta ukweli ni nini? Unapaswa kuangalia kama kuna kazi ya Roho Mtakatifu au la kwa njia hii, iwapo maneno haya ni maonyesho ya ukweli, yanamshuhudia nani, na ni kitu gani yanaweza kukupatia. Kutofautisha kati ya njia ya kweli na hizi njia za uongo kunahitaji njia kadhaa za maarifa ya msingi, ya msingi kabisa kati ya zote ni kusema iwapo kuna Kazi ya Roho Mtakatifu au la. Maana kiini cha imani ya mwanadamu katika Mungu ni imani katika Roho Mtakatifu. Hata imani yake katika Mungu mwenye mwili ni kwa sababu mwili huu ni mfano halisi wa Roho wa Mungu, ikiwa na maana kwamba imani hiyo bado ni imani katika Roho. Kuna tofauti kati ya Roho na mwili, lakini kwa kuwa mwili unatokana na Roho, na ndio Neno linakuwa mwili, hivyo kile ambacho mwanadamu anaamini katika ni uungu halisi wa Mungu. Na hivyo, katika kutofautisha kama ni njia sahihi au la, zaidi ya yote unapaswa kuangalia kama kuna kazi ya Roho Mtakatifu, na baada ya hapo unapaswa kuangalia kama kuna ukweli katika njia hii. Ukweli huu ni tabia ya maisha ya ubinadamu wa kawaida, ni sawa na kusema, kile ambacho Mungu alitaka kwa mwanadamu alipomuumba hapo mwanzo, yaani, ubinadamu wote wa kawaida (ikiwa ni pamoja na hisia za kibinadamu, umaizi, hekima, na maarifa ya msingi ya kuwa mwanadamu). Yaani, unapaswa kuangalia iwapo njia hii inaweza kumpeleka mwanadamu katika maisha ya ubinadamu wa kawaida au la, iwapo ukweli uliozungumzwa unahitajika kulingana na uhalisi wa ubinadamu wa kawaida au la, iwapo ukweli huu ni wa kiutendaji au hali, na iwapo ni wa wakati muafaka au la. Ikiwa kuna ukweli, basi unaweza kumpeleka mwanadamu katika uzoefu wa kawaida na halisi; aidha, mwanadamu anakuwa wa kawaida zaidi, hisia za kawaida za kibinadamu zinakuwa kamili zaidi, maisha ya mwanadamu katika mwili na maisha ya kiroho yanakuwa katika mpangilio mzuri zaidi, na mihemko ya mwanadamu inakuwa ya kawaida kabisa. Hii ni kanuni ya pili. Kuna kanuni nyingine moja zaidi, ambayo ni iwapo watu wana maarifa mengi juu ya Mungu au la, kama unapitia uzoefu wa kazi hiyo na ukweli unaweza kuchochea upendo wa Mungu ndani yao au na kuwasogeza karibu zaidi na Mungu. Katika hili, inaweza kupimwa iwapo ni njia sahihi au la. Kanuni ya msingi ni iwapo njia hii ni ya uhalisi badala ya kuwa ya kimiujiza, na iwapo inaweza kutoa maisha ya mwanadamu. Kama inakubaliana na kanuni hizi, hitimisho linaweza kuwekwa kwamba njia hii ni njia ya kweli. Ninasema maneno haya si kuwafanya mkubali njia nyingine katika uzoefu mtakaoupitia baadaye, wala si utabiri kwamba kutakuwa na kazi ya enzi nyingine mpya hapo baadaye. Ninayasema ili mweze kuwa na uhakika kwamba kazi ya leo ni kazi ya kweli, ili kwamba msiwe na uhakika nusu katika imani yenu katika kazi ya leo na kushindwa kuielewa kwa ndani. Kuna hata watu wengi ambao, licha ya kuwa na uhakika, bado wanafuata kwa mkanganyiko; uhakika kama huo hauna kanuni, na wanapaswa kuondolewa siku moja. Hata wale ambao wapo motomoto katika imani yao wanakuwa na uhakika katika mambo matatu na mambo matano wanakuwa hawana uhakika, kitu kinachoonyesha kuwa hawana msingi. Kwa sababu tabia yenu ni dhaifu sana na msingi wenu hauna kina, hivyo hamna uelewa wa kutofautisha. Mungu harudii kazi Yake, Hafanyi kazi ambayo si halisi, Hamtaki mwanadamu afanye mambo zaidi ya uwezo wake, na Hafanyi kazi ambayo inazidi akili ya mwanadamu. Kazi yote Anayofanya ipo ndani ya mawanda ya akili ya kawaida ya mwanadamu, na haizidi ufahamu wa ubinadamu wa kawaida, na kazi Yake ni kulingana na mahitaji ya kawaida ya mwanadamu. Ikiwa ni kazi ya Roho Mtakatifu, mwanadamu anakuwa wa kawaida zaidi, na ubinadamu wako unakuwa wa kawaida kabisa. Watu wanapata maarifa mengi ya tabia yao potovu ya kishetani, na iliyopotoka, na asili ya mwanadamu, na pia wanapata shauku kubwa ya kuuelewa ukweli. Hiyo ni kusema, maisha ya mwanadamu yanakua zaidi na zaidi, na tabia upotovu ya mwanadamu inakuwa na uwezo wa mabadiliko zaidi na zaidi—yote hiyo ni maana ya Mungu kuwa maisha ya mwanadamu. Kama njia haiwezi kufunua vitu hivyo ambavyo ni asili ya mwanadamu, haiwezi kubadilisha tabia ya mwanadamu, na, zaidi ya hayo, hauwezi kumleta mbele ya Mungu au kumpa ufahamu wa kweli juu ya Mungu, na hata kufanya ubinadamu wake kuwa duni zaidi na hisia zake kuwa si za kawaida zaidi, basi njia hii itakuwa si njia ya kweli, na inaweza kuwa ni kazi ya roho mchafu, au njia ya zamani. Kwa ufupi, haiwezi kuwa kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu. Mmemwamini Mungu kwa miaka yote hii, halafu bado hamna uwezo wa kutofautisha kati ya njia ya kweli na njia ya uongo au kuweza kuitafuta njia ya kweli. Watu wengi hawana haja na masuala haya; wanakwenda tu kule ambako wengi wanakwenda, na wanarudia kile ambacho watu wengi wanasema. Mtu kama huyu anawezaje kuwa mtu anayetafuta njia ya kweli? Na watu kama hao wanaweza kuipata njia ya kweli? Ukielewa kanuni hizi muhimu, basi chochote kitakachotokea hutadanganywa. Leo, ni muhimu sana kwamba mwanadamu awe na uwezo wa kutofautisha mambo; hiki ndicho kinapaswa kuwa katika ubinadamu wa kawaida, na kile ambacho mwanadamu anapaswa kuwa nacho katika uzoefu wake. Ikiwa hata leo, mwanadamu bado hawezi kutofautisha kitu katika ufuataji wake wa ukweli, na hisia zake za kibinadamu bado hazikui, basi mwanadamu ni mpumbavu sana, na njia yake ni makosa na imepotoka. Hakuna tofauti hata ndogo katika maisha yako leo, na ingawa ni ukweli, kama unavyosema, umepata njia ya kweli, ni kweli umeipata? Umeweza kuwa na uwezo wa kutofautisha kitu chochote? Kiini cha njia ya kweli ni nini? Katika njia ya kweli, bado hujapata njia ya kweli, hujapata kitu chochote cha ukweli, yaani, hujapata kile ambacho Mungu anataka kutoka kwako, hivyo hakujawa na tofauti katika upotovu wako. Ukiendelea kufuatilia kwa njia hii, hatimaye utaondolewa. Kwa kuwa umefuata mpaka wa leo, unapaswa uwe na uhakika kwamba njia uliyoichukua ni njia sahihi, na hupaswi kuwa na mashaka sana. Watu wengi siku zote wanakuwa hawana uhakika na wanashindwa kufuatilia ukweli kwa sababu ya masuala fulani madogo madogo. Watu kama hao ni wale ambao hawana ufahamu ya kazi ya Mungu, ni wale ambao wanamfuata Mungu katika mkanganyiko. Watu ambao hawaijui kazi ya Mungu hawawezi kuwa wandani Wake, au kuwa na ushuhuda Kwake. Ninawashauri wale ambao wanatafuta tu baraka na kufuata kile ambacho si dhahiri na dhahania wafuatilie ukweli mapema iwezekanavyo, ili kwamba maisha yao yaweze kuwa na maana. Msiendelee kujidanganya tena!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 147)

Kazi yote ya miaka 6,000 imebadilika kwa utaratibu kuambatana na nyakati. Mabadiliko katika kazi hii yamefanyika kulingana na hali za ulimwengu mzima. Kazi ya usimamizi ya Mungu imebadilika tu kwa utaratibu kulingana na mitindo ya kimaendeleo ya binadamu kwa ujumla; haikuwa imepangwa tayari mwanzoni mwa uumbaji. Kabla ya ulimwengu kuumbwa, au punde tu baada ya kuumbwa kwake, Yehova bado hakuwa amepanga hatua ya kwanza ya kazi, ile ya sheria; hatua ya pili ya kazi, ile ya neema; au hatua ya tatu ya kazi, ile ya kushinda, ambapo Angefanya kazi kwanza miongoni mwa kundi la watu—baadhi ya vizazi vya Moabu, na kupitia hili Angeweza kuushinda ulimwengu mzima. Hakuyaongea maneno haya baada ya kuumba ulimwengu; Hakuyaongea maneno haya baada ya Moabu, wala hata kabla ya Lutu. Kazi Yake yote ilifanywa bila kupangwa. Hivi ndivyo hasa kazi Yake nzima kwa usimamizi wa miaka elfu sita imeendelea; kwa vyovyote vile, kabla kuumba dunia, Hakuwa ameandika mpango kama huo kwa mtindo wa kitu kama “Chati ya Muhtasari wa Maendeleo ya Binadamu.” Katika kazi ya Mungu, Anaonyesha moja kwa moja kile Alicho; Hapigi bongo kuunda mpango. Bila shaka, manabii wengi wameongea unabii mwingi, lakini bado haiwezi kusemekana kwamba kazi ya Mungu siku zote imekuwa ya upangaji mpango dhahiri; unabii ulitolewa kulingana na kazi halisi ya Mungu. Kazi Zake zote ni kazi halisi zaidi. Hufanya kazi Yake kufutana na maendeleo ya kila enzi, na inazingatia jinsi mambao yanabadilika. Kwake Yeye, kutekeleza kazi ni sawa na kutoa dawa kutibu ugonjwa; Akiwa anafanya kazi Yake, Anaangalia na kuendelea na kazi Yake kulingana na kile Alichoona. Katika kila hatua ya kazi Yake, Anaweza kuonyesha hekima Yake ya kutosha na kuelezea uwezo Wake wa kutosha; Anafichua hekima Yake ya kutosha na mamlaka Yake ya kutosha kulingana na kazi ya enzi hiyo husika na kuruhusu yeyote kati ya watu waliorudishwa na Yeye wakati wa enzi hizo kuweza kuiona tabia Yake nzima. Anawaruzuku watu na kutekeleza kazi Anayofaa kufanya kulingana na kazi ambayo lazima ifanywe katika kila enzi; Anawaruzuku watu kulingana na kiwango ambacho Shetani amewapotosha. Ilikuwa namna hii wakati Yehova aliwaumba Adamu na Hawa mwanzoni ili kuwaruhusu kumdhihirisha Mungu katika dunia na kuwa na mashahidi wa Mungu miongoni mwa uumbaji, lakini Hawa alitenda dhambi baada ya kujaribiwa na nyoka; Adamu alifanya vivyo hivyo, na kwa pamoja wakiwa kwenye bustani wakalila tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Na hivyo basi, Yehova alikuwa na kazi ya ziada ya kutenda miongoni mwao. Aliuona uchi wao na kuifunika mili yao kwa nguo ziliyotengenezwa kutoka kwa ngozi za wanyama. Kufuatia haya, Alimwambia Adamu “Kwa sababu umesikiliza sauti ya mkeo, na umekula kutoka kwa mti ule, ambao Nilikuamuru, nikisema, usile kutoka kwa mti huo: udongo umelaaniwa kwa sababu yako … mpaka urudi udongoni, kwani ulitolewa hapo: kwa kuwa wewe ni mavumbi, na utarudi mavumbini.” Kwa mwanamke Akasema, “Nitazidisha sana sikitiko lako na kupata kwako watoto; utazaa watoto kwa sikitiko; na ashiki yako itakuwa kwa mume wako, na atatawala juu yako.” Kuanzia hapo kuendelea, aliwafukuza kutoka kwenye Bustani ya Edeni na kuwafanya waishi nje ya bustani, kama vile binadamu wa kisasa afanyavyo duniani. Mungu alipomwumba mwanadamu mwanzoni kabisa, Hakupanga kumfanya binadamu ajaribiwe na nyoka baada ya kuumbwa na kisha kuwalaani binadamu na nyoka. Kwa hakika hakuwa na mpango wa aina hii; ilikuwa tu maendeleo ya mambo yaliyompa kazi hii mpya miongoni mwa uumbaji Wake. Baada ya Yehova kutekeleza kazi Yake miongoni mwa Adamu na Hawa kwenye ardhi, binadamu waliendelea kuimarika kwa miaka elfu kadhaa mpaka “Yehova aliona kwamba uovu wa mwanadamu ulikuwa mkubwa ulimwenguni, na kuwa kila wazo la fikira za moyo wake lilikuwa ovu tu daima. Na Yehova akajuta kwamba alikuwa amemwumba mwanadamu ulimwenguni, na akawa na huzuni moyoni mwake. … Lakini Nuhu alipata neema katika macho ya Yehova.” Wakati huu Yehova alikuwa na kazi mpya zaidi, kwa ajili binadamu Aliowaumba walikuwa wamezidisha dhambi baada ya kujaribiwa na nyoka. Kwa mujibu wa hali hizi, Yehova aliichagua familia ya Nuhu kutoka miongoni mwa watu hawa na kuwanusuru, na kutekeleza kazi Yake ya kuuangamiza ulimwengu kwa gharika. Binadamu wameendelea kukua kwa njia hii mpaka siku ya leo, wakiendelea kupotoka kwa kukithiri, na wakati maendeleo ya binadamu yafikapo kilele, utakuwa ndio mwisho wa binadamu. Kuanzia mwanzo kabisa hadi mwisho wa ulimwengu, ukweli wa ndani wa kazi Yake siku zote umekuwa hivi. Hii ni sawa na namna ambavyo watu watakavyoainishwa kulingana na aina yao; hii ni mbali na hali ya kwamba kila mtu anayeamuliwa kabla kwa kikundi fulani; bali kila mtu anaainishwa polepole baada ya kupitia mchakato wa maendeleo. Mwishowe, yeyote ambaye hawezi kuokolewa kwa ukamilifu atarudishwa kwa mababu zake. Hamna kati ya kazi za Mungu miongoni mwa binadamu iliyokuwa tayari imetayarishwa wakati wa uumbaji wa ulimwengu; badala yake, ilikuwa ni maendeleo ya mambo yaliyomruhusu Mungu kutekeleza kazi Yake hatua kwa hatua kwa uhalisia zaidi na kwa kimatendo zaidi miongoni mwa binadamu. Hivi ni kama ambavyo Yehova Mungu hakumwumba nyoka ili kumjaribu mwanamke. Haukuwa mpango Wake mahususi, wala halikuwa jambo ambalo Alikuwa ameliamua kimakusudi kabla; mtu anaweza kusema kwamba hili halikutarajiwa. Hivyo basi ilikuwa ni kwa sababu ya hili ndiyo Yehova aliwatimua Adamu na Hawa kutoka kwenye Bustani ya Edeni na kuapa kutowahi kumwumba binadamu tena. Lakini hekima ya Mungu inagunduliwa tu na watu kwenye msingi huu, kama tu ile hoja Niliyotaja awali: “Hekima Yangu hutumika kutokana na njama za Shetani.” Haikujalisha ni vipi ambavyo binadamu walizidi kupotoka au vipi nyoka alivyowajaribu, Yehova bado alikuwa na hekima Yake; kwa hivyo, Amekuwa Akijihusisha katika kazi mpya tangu Alipouumba ulimwengu, na hamna hatua zozote za kazi hii zimewahi kurudiwa. Shetani ameendelea kutekeleza njama zake; binadamu wamekuwa wakipotoshwa siku zote na Shetani, na Yehova Mungu pia ameendelea kutekeleza kazi Yake ya hekima siku zote. Hajawahi kushindwa, na Hajawahi kusita kufanya kazi Yake kuanzia uumbaji wa ulimwengu mpaka sasa. Baada ya binadamu kupotoshwa na Shetani, Aliendelea siku zote kufanya kazi miongoni mwa watu ili kumshinda adui Wake anayewapotosha binadamu. Vita hivi vitaendelea kuanzia mwanzo hadi mwisho wa ulimwengu. Kwa kufanya kazi hii yote, Hajaruhusu tu binadamu, ambao wamepotoshwa na Shetani, kupokea wokovu Wake mkubwa, lakini pia amewaruhusu kuiona hekima Yake, uweza na mamlaka, na hatimaye Atawaruhusu binadamu kuiona tabia Yake ya haki—huku Akiwaadhibu waovu na kuwatuza wema. Amepambana na Shetani hadi siku hii ya leo na Hajawahi kushindwa, kwani Yeye ni Mungu mwenye hekima, na hekima Yake hutumika kutokana na njama za Shetani. Na kwa hivyo mbali na kufanya tu kila kitu mbinguni kitii mamlaka Yake; pia Hufanya kila kitu duniani kipumzike chini ya kigonda Chake na pia, Huwafanya wale waovu wanaoshambulia na kunyanyasa binadamu wajipate katika kuadibu Kwake. Matokeo yote ya kazi yanaletwa kutokana na hekima Yake. Alikuwa hajawahi kufichua hekima Yake kabla ya uwepo wa binadamu, kwani Hakuwa na maadui kule mbinguni, juu ya dunia, au kwenye ulimwengu kwa ujumla, na hakukuwa na nguvu za giza zilizoshambulia chochote katika maumbile. Baada ya malaika mkuu kumsaliti, Aliwaumba binadamu kwenye dunia, na ilikuwa ni kwa sababu ya binadamu ndiyo Alianza rasmi vita Vyake vya milenia nzima dhidi ya Shetani, malaika mkuu, vita ambavyo vilizidi kushamiri kwa kila hatua iliyopigwa. Uweza Wake na hekima vinapatikana katika kila mojawapo ya awamu hizi. Ni katika muda huu tu ndipo kila kitu kule mbinguni na duniani huweza kushuhudia hekima ya Mungu, uweza Wake, na hasa uhalisi wa Mungu. Angali anatekeleza kazi Yake kwa njia ile ya kihalisi leo; aidha, Anapoendelea kutekeleza kazi Yake anafichua pia uweza Wake na hekima Yake; Anawaruhusu kuona ule ukweli wa ndani katika kila hatua ya kazi, kuona hasa ni vipi mnaweza kuelezea uweza wa Mungu na hasa ni vipi mnavyoweza kuelezea uhalisia wa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 148)

Kazi ya Roho Mtakatifu siku zote inafanywa kwa hiari; wakati wowote Anapopanga kazi Yake, Roho Mtakatifu ataitekeleza. Kwa nini sikuzote Nasema kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni ya uhalisi? Kwamba siku zote ni mpya na haijawahi kuwa zee, na siku zote inakuwa na uhai zaidi? Kazi Yake bado haikuwa imepangwa wakati ulimwengu ulipoumbwa; hivi sivyo kamwe ilivyofanyika! Kila hatua ya kazi hufikia athari yake bora kwa wakati wake mwafaka, nazo haziingiliani kati. Kunao wakati mwingi ambapo mipango katika akili zako hazilingani kamwe na kazi ya hivi punde ya Roho Mtakatifu. Kazi Yake si rahisi kama wanavyofikiria watu, wala si ngumu kama watu wengi wanavyofikiria; inajumuisha kuwaruzuku watu wakati wowote na mahali popote kulingana na mahitaji yao ya sasa. Hakuna aliye wazi zaidi kuhusu kiini halisi cha watu kama Yeye, na ni kwa sababu hii mahususi ndiposa hakuna kinachoweza kufaa mahitaji ya kihalisi ya watu kama vile ambavyo kazi Yake inavyofanya. Hivyo basi, kutoka katika mtazamo wa kibinadamu, kazi Yake ilipangiwa milenia kadha mbele. Anavyofanya kazi miongoni mwenu sasa, kulingana na hali yenu, Yeye pia Anafanya kazi na kuongea wakati wowote na mahali popote. Wakati watu wako katika hali fulani, Yeye huongea maneno hayo ambayo hasa ndiyo wanayohitaji ndani yao. Ni kama hatua ya kwanza ya kazi Yake, nyakati za kuadibu. Baada ya nyakati za kuadibu, watu walionyesha tabia fulani, walikuwa na mienendo ya kuasi katika njia fulani, hali fulani nzuri ziliibuka, hali fulani hasi pia ziliibuka, na mipaka ya juu ya uhasi huu ikafikia kiwango fulani. Mungu alifanya kazi Yake kwa msingi wa mambo haya yote, na hivyo basi Alichukua haya yote ili kuweza kutimiza athari bora zaidi kwa ajili ya kazi Yake. Anatekeleza tu kazi Yake ya kuruzuku miongoni mwa watu kulingana na hali zao za sasa. Yeye Hutekeleza kila hatua ya kazi Yake kulingana na hali halisi za watu. Viumbe wote wamo mikononi Mwake; Angekosa kuujua? Kwa mujibu wa hali za watu, Mungu hutekeleza hatua inayofuata ya kazi inayofaa kufanywa, wakati na mahali popote. Kazi hii haikupangwa maelfu ya miaka kabla; hii ni dhana ya kibinadamu tu! Yeye hufanya kazi huku akiangalia athari za kazi Yake, na kazi Yake inaendelea kuwa ya kina na kukua; Anapoendelea kuangalia matokeo ya kazi Yake, Anatekeleza hatua inayofuata ya kazi Yake. Yeye hutumia mambo mengi ili kuingia kwenye mpito hatua kwa hatua na kufanya kazi Yake mpya kuonekana na watu baada ya muda. Aina hii ya kazi inaweza kuruzuku mahitaji ya watu, kwani Mungu anawajua watu vizuri mno. Hivi ndivyo Anavyotekeleza kazi Yake kutoka mbinguni. Vilevile, Mungu mwenye mwili anafanya kazi Yake kwa njia iyo hiyo, Akipangilia kulingana na uhalisi na kufanya kazi miongoni mwa binadamu. Hakuna yoyote kati ya kazi Zake iliyopangwa kabla ya ulimwengu kuumbwa, wala kupangwa kwa umakinifu kabla ya wakati. Miaka elfu mbili baada ya ulimwengu kuumbwa, Yehova aliona binadamu walikuwa wamepotoka sana kiasi cha kwamba Alikitumia kinywa cha nabii Isaya kutabiri kwamba baada ya Enzi ya Sheria kukamilika, Angetekeleza kazi Yake ya kukomboa binadamu katika Enzi ya Neema. Huu ulikuwa mpango wa Yehova, bila shaka, lakini mpango huu pia kufanywa kulingana na hali ambazo Aliangalia wakati huo; bila shaka Yeye hakuufikiria mara moja baada ya kumwumba Adamu. Isaya alitabiri tu, lakini Yehova hakuwa amefanya matayarisho ya mapema ya kazi hii wakati wa Enzi ya Sheria; badala yake, Alianza kazi hii katika mwanzo wa Enzi ya Neema, wakati mjumbe alipojitokeza katika ndoto ya Yusufu na kumpa yeye nuru, akimwambia kwamba Mungu angekuwa mwili, na hivyo kazi Yake ya kupata mwili ikaanza. Kama watu wanavyofikiria Mungu hakujitayarishia kazi Yake ya kuwa mwili baada ya kuumba ulimwengu; jambo hili liliamuliwa tu kulingana na kiwango cha maendeleo ya binadamu na hadhi ya vita Vyake na Shetani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 149)

Mungu anapokuja kuwa mwili, Roho Wake anamshukia binadamu; kwa maneno mengine, Roho wa Mungu anauvaa mwili. Anafanya kazi Yake duniani, na badala ya kuleta naye hatua mbalimbali zilizozuiliwa, kazi hii haina mipaka kamwe. Kazi ambayo Roho Mtakatifu hufanya katika mwili bado inaamuliwa na athari ya kazi Yake, na Yeye hutumia mambo haya kuamua urefu wa muda ambao Atafanya kazi akiwa katika mwili. Roho Mtakatifu hufichua moja kwa moja kila hatua ya kazi Yake; Yeye huchunguza kazi Yake anapozidi kuendelea; si jambo la kimwujiza kiasi cha kupanua ile mipaka ya kufikiriwa na binadamu. Hii ni kama kazi ya Yehova katika kuumba mbingu na nchi na vitu vyote; Aliweza kupanga na kufanya kazi wakati huo huo. Alitenga nuru kutoka kwenye giza, na asubuhi pamoja na jioni vyote vikawepo—hii ilichukua siku moja. Siku ya pili Aliumba mbingu, ambayo pia ilichukua siku moja na kisha Akaiumba nchi, bahari na viumbe vilivyojaa ndani, pia ikichukua siku nyingine moja. Hili liliendelea hivyo hadi siku ya sita, wakati Mungu alipomwumba binadamu na kumwacha asimamie viumbe hivi vyote juu ya nchi, mpaka siku ya saba, Alipokuwa amemaliza kuumba viumbe vyote, na akapumzika. Mungu alibariki siku ya saba na kuitenga kuwa siku takatifu. Aliiamulia siku hii takatifu baada ya kuviumba viumbe vyote, na wala si kabla ya kuviumba. Kazi hii pia ilitekelezwa kwa hiari; kabla ya kuviumba viumbe vyote, Hakuamua kuumba ulimwengu kwa siku sita na kupumzika siku ya saba; ukweli hauko hivi hata kidogo. Hakusema hili, wala Hakupanga hili. Kwa vyovyote vile Hakusema kwamba uumbaji wa viumbe vyote ungekamilishwa katika siku ya sita na kwamba Angepumzika katika siku ya saba; badala yake, Aliumba kulingana na kile kilichokuwa kikionekana kizuri Kwake. Punde Alipomaliza kuumba kila kitu, tayari ilikuwa ni siku ya sita. Kama ingekuwa ni siku ya tano Alipomaliza kuumba kila kitu, Angepangilia basi siku ya sita kuwa siku takatifu; hata hivyo, Alimaliza kuumba kila kitu katika siku ya sita, na hivyo basi siku ya saba ikawa siku takatifu, ambayo imepitishwa hadi siku ya leo. Hivyo basi, kazi Yake ya sasa inatekelezwa kwa njia ii hii. Yeye huongea na kuwaruzuku kulingana na hali zenu. Yaani, Roho huongea na kufanya kazi kulingana na hali za watu; Roho huangalia kila kitu na kufanya kazi wakati wowote na mahali popote. Kile Ninachofanya, kwa mfano, kuwawekea na kuwapa bila kiwazo ni kile mnachohitaji. Kwa hivyo hakuna kazi Yangu iliyo tofauti na uhalisi; yote ni halisi, kwani nyinyi nyote mnajua ya kwamba “Roho wa Mungu hulinda vyote.” Kama haya yote yalikuwa yameamuliwa kabla ya wakati, huoni kwamba mambo yangekuwa yamekwisha amuliwa? Unafikiri kwamba Mungu alifanya kazi kwa milenia sita nzima na kisha kuamulia kabla binadamu kama waasi, wapingaji, waongo na wadanganyifu, kama kuwa na upotovu wa mwili, tabia za kishetani, ashiki za macho na kujihusisha kwao kwa mambo yasiyofaa. Haya yote hayakupangwa na Mungu, lakini yalitokana na upotoshaji wa Shetani. Baadhi watasema, “Shetani naye hakuwa ndani ya mfumbato wa Mungu? Mungu alikuwa amepanga awali kwamba Shetani angepotosha binadamu kwa njia hii, na baada ya hapo Akatekeleza kazi Yake miongoni mwa binadamu.” Je, Mungu kwa kweli angepanga awali Shetani kuwapotosha binadamu? Anayo hamu mno ya kuwaruhusu binadamu kuishi maisha ya kawaida na kibinadamu; Angenyanyasa maisha ya binadamu? Kama hali ni hivyo, kumshinda Shetani na kuokoa binadamu si kungekuwa jitihada za bure bilashi? Je, uasi wa binadamu ungeamuliwaje kabla? Ulitokana na kunyanyaswa na Shetani kwa hali halisi; ungepangwa vipi awali na Mungu? Shetani aliye ndani ya mfumbato wa Mungu ambaye mnamwelewa na Shetani ndani ya mfumbato wa Mungu ambaye Ninamzungumzia ni tofauti sana. Kulingana na kauli zenu kwamba “Mungu ni mwenyezi, na Shetani yumo mikononi Mwake,” Shetani asingemsaliti Yeye. Je, wewe hujasema kwamba Mungu ni mwenyezi? Maarifa yenu ni ya kidhahania mno na hayaambatani na uhalisi; mwanadamu kamwe hawezi kuelewa fikira za Mungu, wala mwanadamu hawezi kamwe kuelewa busara ya Mungu! Mungu ni mwenyezi; huu si uwongo kamwe. Malaika mkuu alimsaliti Mungu kwa sababu Mungu alimpa sehemu ya mamlaka awali. Bila shaka, tukio hili halikutarajiwa, kama vile Hawa kushindwa na jaribio la nyoka. Hata hivyo, bila kujali ni vipi ambavyo Shetani hutekeleza usaliti wake, tofauti na Mungu, yeye si mwenyezi. Kama vile mlivyosema, Shetani ni mwenye nguvu; haijalishi ni nini atakachofanya, mamlaka ya Mungu humshinda siku zote. Hii ndiyo maana ya kweli katika ule msemo “Mungu ni mwenyezi, na Shetani yumo mikononi Mwake.” Hivyo basi, vita Vyake na Shetani lazima vitekelezwe hatua moja baada ya nyingine; aidha, Yeye hupanga kazi Yake katika kuitikia ujanja wa Shetani. Hivi ni kusema, kulingana na enzi, Anawaokoa watu na kufichua hekima na uweza Wake. Vilevile, kazi za siku za mwisho haikuamuliwa mapema, kabla ya Enzi ya Neema; kuamuliwa kabla hakufanywi kwa njia ya kawaida kama hii: mwanzo, kwa kuifanya tabia ya nje ya binadamu ibadilike; pili, kumweka chini ya uongozi binadamu apokee adabu na majaribio yake; tatu, kusababisha binadamu kupitia jaribio la kifo; nne, kumfanya binadamu apitie nyakati za kumpenda Mungu na aonyeshe uamuzi wa kiumbe kilichoumbwa; tano, kumruhusu binadamu kuweza kuona mapenzi ya Mungu na kumjua Yeye kikamilifu; na hatimaye, kisha kumkamilisha binadamu. Hakupanga mambo haya yote wakati wa Enzi ya Neema; badala yake, Alianza kuyapanga katika enzi ya sasa. Shetani yumo kazini, kama vile alivyo Mungu. Shetani huonyesha tabia yake potovu, huku naye Mungu huongea moja kwa moja na kufichua baadhi ya mambo muhimu. Hii ndiyo kazi inayofanywa leo, na kanuni ii hii ya kufanya kazi ilitumika zamani, baada ya ulimwengu kuumbwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 150)

Kwanza Mungu aliwaumba Adamu na Hawa, na pia Alimwumba nyoka. Miongoni mwa vitu vyote, nyoka ndiye aliyekuwa mwenye sumu nyingi sana; mwili wake ulikuwa na sumu, na Shetani aliitumia sumu hii ili kufaidika naye. Ni nyoka aliyemjaribu Hawa hadi akatenda dhambi. Adamu alitenda dhambi baada ya Hawa kutenda, na wawili hawa kisha waliweza kutofautisha kati ya mema na maovu. Kama Yehova angejua kwamba nyoka angemjaribu Hawa, na kwamba Hawa angemjaribu Adamu, kwa nini Akawaweka wote pale ndani ya bustani? Kama Aliweza kutabiri mambo haya kwa nini Akamwumba nyoka na kumweka ndani ya Bustani ya Edeni? Kwa nini Bustani ya Edeni ilikuwa na tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya? Alinuia wao walile hilo tunda? Yehova alipokuja, Adamu wala Hawa hawakuthubutu kumkabili Yeye, na ulikuwa tu wakati huu ambapo Yehova alijua kwamba walikuwa wamelila tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya na kushikwa katika ujanja wa yule nyoka. Hatimaye Alimlaani nyoka, na Akamlaani Adamu na Hawa pia. Wakati hao wawili walilila tunda lile la mti, Yehova hakujua kabisa kwamba walikuwa wakifanya hivyo. Binadamu walipotoka hadi kufikia kiwango cha kuwa na uovu na uasherati wa kimapenzi, hadi kufikia hatua ambayo mambo yote waliyokuwa nayo katika mioyo yao yalikuwa maovu na yasiyo ya haki; yote yalikuwa machafu. Yehova hivyo basi alijutia kuumba binadamu. Baadaye Alitekeleza kazi Yake ya kuharibu ulimwengu kwa gharika, ambayo Nuhu na watoto wake wa kiume walinusurika. Baadhi ya mambo kwa hakika hayajaendelea na kuwa ya mwujiza kama vile watu wanavyoweza kufikiria. Baadhi wanauliza: “Kwa sababu Mungu alijua malaika mkuu angemsaliti Yeye, kwa nini Alimwumba?” Huu ndio ukweli: Wakati dunia haikuwepo bado, malaika mkuu ndiye aliyekuwa malaika mkuu zaidi mbinguni. Alikuwa na mamlaka juu ya malaika wote kule mbinguni; haya ndiyo yaliyokuwa mamlaka ambayo Mungu alimpa. Kando na Mungu, yeye ndiye aliyekuwa malaika mkubwa zaidi mbinguni. Wakati Mungu alipouumba binadamu baadaye, malaika mkuu alitekeleza usaliti mkuu zaidi dhidi ya Mungu duniani. Nasema kwamba alimsaliti Mungu kwa sababu alitaka kuwasimamia binadamu na kuzidi mamlaka ya Mungu. Ni malaika mkuu ambaye alimjaribu Hawa hadi akatenda dhambi; alifanya hivyo kwa sababu alipenda kuanzisha ufalme wake duniani na kuwafanya binadamu wamsaliti Mungu na kumtii yeye badala yake. Aliona kwamba kulikuwa na vitu vingi ambavyo vilimtii; malaika walimtii sawa na vile ambavyo watu wa dunia walivyomtii. Ndege na wanyama, miti, misitu, milima, mito na vitu vyote vilivyo duniani vilikuwa chini ya utunzaji wa binadamu—yaani, Adamu na Hawa—huku nao Adamu na Hawa wakimtii. Malaika mkuu hivyo basi alitamani kuzidi mamlaka ya Mungu na kumsaliti Mungu. Baadaye aliwaongoza malaika wengi kumsaliti Mungu, ambao baadaye walikuja kuwa pepo wachafu mbalimbali. Je, maendeleo ya binadamu hadi siku ya leo hayajasababishwa na upotovu wa malaika mkuu? Binadamu wako tu namna walivyo leo kwa sababu malaika mkuu alimsaliti Mungu na kuwapotosha binadamu. Kazi hii ya hatua kwa hatua haiko karibu kuwa ya dhahania na rahisi kama vile watu wanavyofikiria hata kidogo. Shetani alitekeleza usaliti wake kwa sababu fulani, ilhali watu hawawezi kufahamu kitu rahisi kama hicho. Kwa nini Mungu akaziumba mbingu na dunia na vitu vyote, na pia kumwumba Shetani? Kwa sababu Mungu anamdharau Shetani sana, naye Shetani ni adui Wake, kwa nini akamwumba Shetani? Kwa kumwumba Shetani, hakuwa Anamwumba adui? Mungu kwa hakika hakuumba adui; badala yake, Alimwumba malaika, na baadaye malaika akamsaliti Yeye. Hadhi yake ilikuwa kubwa mno kiasi cha kwamba alitaka kumsaliti Mungu. Mtu anaweza kusema kwamba hii ilikuwa ni sadfa, lakini ulikuwa pia mwelekeo usioepukika. Ni sawa na vile ambavyo mtu bila kuepuka atakufa akiwa na umri fulani; mambo yameendelea tayari hadi kwa hatua fulani. Kunao hata wapumbavu wengine wanaosema: “Kwa sababu Shetani ni adui Yako, kwa nini Ukamwumba? Kwani hukujua kuwa malaika huyu mkuu angekusaliti Wewe? Kwani Huwezi kukazia macho kutoka kwa milele hadi milele? Kwani Wewe huijui asili yake? Kwa sababu Ulijua waziwazi kuwa angekusaliti Wewe, basi kwa nini Ukamfanya kuwa malaika mkuu? Hata kama mtu atapuuza suala la usaliti wake, bado aliwaongoza malaika wengi sana na akashuka hadi kwa ulimwengu wa binadamu wenye kufa ili kuwapotosha binadamu; hadi siku ya leo Umeshindwa kukamilisha mpango Wako wa usimamizi wa miaka elfu sita.” Je, maneno haya ni sahihi? Unapofikiria kwa njia hii, hujiweki katika matatizo mengi zaidi kuliko yanayohitajika? Wengine bado husema: Kama Shetani asingewapotosha binadamu hadi siku ya leo, Mungu asingewaokoa binadamu kwa njia hii. Katika mfano huu, hekima na uweza wa Mungu vyote vingekuwa havionekani; hekima Yake ingejionyesha wapi? Hivyo basi Mungu alikiumba kizazi cha binadamu kwa minajili ya Shetani; katika siku za baadaye, Mungu angefichua uweza Wake—vinginevyo, binadamu angewezaje kugundua hekima ya Mungu? Kama binadamu asingempinga Yeye na kumwasi Yeye, isingehitajika kwa vitendo Vyake kujionyesha. Kama viumbe wote wangemwabudu Yeye na kumtii Yeye, Asingekuwa na kazi ya kufanya. Hali hii ni mbali zaidi na uhalisi wa mambo, kwani hakuna chochote kichafu kuhusu Mungu, na hivyo basi Hawezi kuumba uchafu. Yeye hufichua vitendo Vyake sasa ili kuweza tu kuwashinda kabisa adui Zake, ili kuokoa binadamu, ambao Aliwaumba, ili kuyashinda mapepo na Shetani, ambao wanamchukia, wanamsaliti na wanampinga, ambao walikuwa chini ya utawala Wake na alikuwa Wake mwanzoni kabisa; Anataka kuwashinda hawa mapepo na katika kufanya hivyo kuufichua uweza Wake kwa vitu vyote. Binadamu na vitu vyote vilivyomo duniani sasa hivi vinamilikiwa na Shetani na katika umiliki wa waovu. Mungu anataka kuvifichua vitendo Vyake kwa vitu vyote ili watu waweze kumjua Yeye, na hivyo kuishia kumshinda Shetani na kuwaangamiza kabisa adui Zake. Uzima wa kazi hii unakamilishwa kupitia kufichua matendo Yake. Viumbe Vyake vyote vimemilikiwa na Shetani, na hivyo basi Angependa kuufichua uweza Wake kwa viumbe hivyo, na hivyo kumshinda Shetani. Kama Shetani asingekuwepo, Asingehitaji kuyafichua matendo Yake. Kama usingekuwa usumbufu wa Shetani, Angewaumba binadamu na kuwaongoza kuishi katika Bustani ya Edeni. Kwa nini Hakuwahi kufichua vitendo Vyake vyote kwa malaika au malaika mkuu kabla ya kusalitiwa na Shetani? Kama malaika na malaika mkuu wangalimjua Yeye, na pia kumtii Yeye pale mwanzoni, basi Asingetekeleza vile vitendo vya kazi visivyo na maana. Kwa sababu ya uwepo wa Shetani na mapepo, watu humpinga na wanajazwa hadi pomoni na tabia ya uasi, na hivyo basi Mungu angependa kufichua vitendo Vyake. Kwa sababu Angependa kupigana vita na Shetani, lazima Atumie mamlaka Yake kumshinda Shetani na kutumia vitendo Vyake vyote kumshinda Shetani; kwa njia hii, kazi Yake ya wokovu Anayotekeleza miongoni mwa binadamu itawafanya watu waone hekima na uweza Wake. Kazi anayofanya Mungu leo ni yenye maana na haifanani hata kidogo kile watu wengine husema: “Je, kazi hii Unayofanya haihitilafiani? Je, hujisumbui tu na huu mfululizo wa kazi? Ulimwumba Shetani, kisha ukamruhusu Akakusaliti na kukupinga Wewe. Uliwaumba binadamu, na kisha ukawakabidhi kwa Shetani, na Ukaruhusu Adamu na Hawa wajaribiwe. Kwa sababu uliyafanya mambo haya yote kimakusudi, kwa nini Unawachukia binadamu? Kwa nini Unamchukia Shetani? Mambo haya si ya kujitungia Mwenyewe? Kuna nini cha Wewe kuchukia?” Watu wengi wa kipumbavu watasema hayo. Wanatamani kumpenda Mungu, lakini mioyoni mwao wanalalamika kumhusu Mungu—ukinzani kweli! Wewe huelewi ukweli, unazo fikira nyingi sana za kimiujiza, na pia unadai kwamba hili ni kosa la Mungu—wewe ni mpumbavu kweli! Ni wewe unayechezacheza na ukweli; si kosa la Mungu! Baadhi ya watu hata watalalamika na kulalamika: “Ni wewe uliyemwumba Shetani, na ni Wewe uliyemrusha Shetani hadi katika ulimwengu wa mwanadamu na uliyemkabidhi binadamu kwake. Binadamu wana tabia ya kishetani; badala ya kuwasamehe, Unawachukia sana kwa kiwango fulani. Mwanzoni Uliwapenda binadamu kwa kiwango fulani, na sasa Unawachukia sana binadamu. Ni Wewe unayewachukia sana na kuwapenda binadamu—maelezo ya haya ni yapi? Je, huu si ukinzani?” Bila kujali ni vipi mnavyoangalia suala hili, hili ndilo lililofanyika mbinguni; malaika mkuu alimsaliti Mungu kwa njia hii, nao binadamu wakapotoshwa kwa njia hii, na wakaendelea mpaka leo kwa njia hii. Bila kujali ni vipi mnavyolisema, hii ndiyo hadithi yote. Hata hivyo, lazima muelewe kwamba Mungu anaifanya kazi ya leo ili kuwaokoa nyinyi, na ili kumshinda Shetani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 151)

Mungu hutumia usimamizi Wake wa watu kumshinda Shetani. Kwa kuwapotosha watu, Shetani hutamatisha majaaliwa ya watu na kuinyanyasa kazi ya Mungu. Kwa upande mwingine, kazi ya Mungu ndiyo wokovu wa binadamu. Ni hatua gani ya kazi ya Mungu mwenyewe ambayo hainuii kuwaokoa binadamu? Ni hatua gani hainuii kuwatakasa watu, kuwafanya atende haki na kuwafanya kuishi kwa njia ambayo huunda taswira inayoweza kupendwa? Shetani, hata hivyo, hafanyi hivi. Yeye huwapotosha binadamu; siku zote anatekeleza kazi zake za kuwapotosha binadamu kote ulimwenguni. Bila shaka, Mungu pia hufanya kazi Yake mwenyewe. Hamtilii maanani Shetani. Haijalishi ni kiasi kipi cha mamlaka ambacho Shetani anacho, mamlaka yake bado yalitoka kwa Mungu; Mungu kwa hakika hakumpa mamlaka Yake yote tu, na hivyo basi haijalishi ni nini afanyacho, hawezi kuzidi Mungu na siku zote yuko mikononi mwa Mungu. Mungu hakufichua vitendo Vyake vyovyote akiwa mbinguni. Alimpa Shetani kiwango kidogo tu cha mamlaka ili kumruhusu kutekeleza udhibiti wake dhidi ya malaika. Hivyo basi, haijalishi kile anachofanya, hawezi kuzidi mamlaka ya Mungu kwa sababu mamlaka ambayo Mungu alimpa awali ni finyu. Huku Mungu akifanya kazi, Shetani hunyanyasa. Katika siku za mwisho, atamaliza unyanyasaji wake; vilevile, kazi ya Mungu itakamilika, na aina ya mtu ambaye Mungu angependa kumkamilisha atakuwa amekamilika. Mungu huwaelekeza watu kwa njia nzuri; maisha Yake ni maji yenye uzima, yasiyopimika na yasiyo na mipaka. Shetani amempotosha binadamu hadi kiwango fulani; hatimaye, yale maji hai ya uzima yatamkamilisha binadamu, na haitawezekana kwa Shetani kuingilia kati na kutekeleza kazi yake. Hivyo basi, Mungu ataweza kuwapata kabisa watu wake. Shetani angali anakataa kukubali haya sasa; siku zote hupambana na Mungu, lakini Mungu hamtilii maanani. Amesema, Nitakuwa mshindi dhidi ya nguvu zote za giza za Shetani na dhidi ya ushawishi wote wa giza. Hii ndiyo kazi ambayo lazima ifanywe katika mwili, na ndiyo pia maana ya kupata mwili kwa Yesu Kristo. Ni kukamilisha hatua ya kazi ya kumshinda Shetani katika siku za mwisho, kuondoa vitu vyote vinavyomilikiwa na Shetani. Ushindi wa Mungu dhidi ya Shetani ni mtindo usioepukika! Shetani kwa hakika alishindwa kitambo sana. Wakati injili ilipoanza kuenezwa kote duniani mwa joka kubwa jekundu, yaani, wakati Mungu mwenye mwili alipoanza kufanya kazi na kazi hii ikafanywa kuendelea, Shetani aliweza kushindwa kabisa, kwani kupata mwili wa Kristo kulimaanisha kumshinda Shetani. Shetani aliona kwamba Mungu alikuwa kwa mara nyingine tena amekuwa mwili na alikuwa ameanza kutekeleza kazi Yake, na akaona kwamba hakuna nguvu ambazo zingeweza kukomesha kazi hii. Hivyo basi, alipigwa na bumbuazi alipoona kazi hii na hakuthubutu kufanya kazi yoyote nyingine zaidi. Kwanza Shetani alifikiria kwamba pia alimiliki hekima nyingi, na akaingilia kati na kunyanyasa kazi ya Mungu; hata hivyo, hakutarajia kwamba Mungu alikuwa kwa mara nyingine tena amekuwa mwili, na kwamba katika kazi Yake, Mungu alikuwa ametumia uasi Wake kuhudumu kama ufunuo na hukumu kwa binadamu; na hivyo basi kumshinda binadamu na kumshinda Shetani. Mungu ni mwenye busara kumshinda, na kazi Yake inamzidi Shetani kwa mbali. Hivyo basi, Niliwahi kutaja awali kwamba: Kazi Ninayoifanya inatekelezwa kutokana na ujanja wa Shetani. Mwishowe Nitafichua uweza Wangu na hali ya kutoweza kwa Shetani. Mungu anapofanya kazi Yake, Shetani anamfuata unyo unyo kutoka nyuma mpaka mwishowe anaangamizwa—hatajua hata kilichomgonga! Ataweza kutambua tu ukweli baada ya kuvunjwa na kupondwapondwa; na wakati huo atakuwa tayari amechomwa kwenye ziwa la moto. Hatakuwa ameshawishika kabisa wakati huo? Kwani hatakuwa na njama zozote zingine za kutumia!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 152)

Kazi ya Mungu miongoni mwa mwanadamu haitengani na mwanadamu, kwa kuwa mwanadamu ni chombo cha kazi hii na kiumbe wa pekee aliyeumbwa na Mungu anayeweza kutoa ushuhuda kwa Mungu. Maisha ya mwanadamu na shughuli zake zote havitengani na Mungu, na vyote vinaongozwa na mkono wa Mungu, na inaweza kusemwa kuwa hakuna mtu anayeweza kuishi bila Mungu. Hakuna anayeweza kupinga hili, kwani ndio ukweli. Kila Akifanyacho Mungu ni kwa faida ya mwanadamu, na kinalenga hila za Shetani. Kila anachokihitaji mwanadamu kinatoka kwa Mungu, na Mungu ndiye chanzo cha maisha ya mwanadamu. Hivyo basi, mwanadamu hana uwezo wa kujitenga na Mungu. Vilevile, Mungu Hajawahi kuwa na nia ya kujitenga na mwanadamu. Kazi Aifanyayo Mungu ni kwa ajili ya wanadamu wote na mawazo Yake daima ni mema. Kwa mwanadamu, kwa hivyo, kazi ya Mungu na mawazo ya Mungu kwa mwanadamu (yaani mapenzi ya Mungu) ni “maono” ambayo yanafaa kutambuliwa na mwanadamu. Maono kama hayo pia ni usimamizi wa Mungu, na kazi ambayo haiwezi kufanywa na mwanadamu. Mahitaji ambayo Mungu anatarajia kutoka kwa mwanadamu wakati wa kazi Yake, wakati uo huo, yanaitwa “vitendo” vya mwanadamu. Maono ni kazi ya Mungu Mwenyewe au ni mapenzi Yake kwa mwanadamu au madhumuni na umuhimu wa kazi Yake. Maono pia yanaweza kusemekana kuwa sehemu ya usimamizi, kwani usimamizi huu ni kazi ya Mungu, iliyokusudiwa kwa mwanadamu, kwa maana kwamba ni kazi ambayo Mungu anaifanya miongoni mwa wanadamu. Kazi hii ni ushahidi na njia ambayo kwayo mwanadamu anamfahamu Mungu na ni ya umuhimu wa hali ya juu kwa mwanadamu. Iwapo wanadamu hawatatilia maanani kuijua kazi ya Mungu na badala yake kutilia maanani mafundisho ya dini kuhusu imani kwa Mungu au kutilia maanani vitu vidogo visivyo na maana, hawatamjua Mungu, na, aidha, hawatakuwa wanautafuta moyo wa Mungu. Kazi ya Mungu inamsaidia sana mwanadamu kumfahamu Mungu na inaitwa maono. Maono haya ni kazi ya Mungu, mapenzi, madhumuni na umuhimu wa kazi ya Mungu na yote ni kwa manufaa ya mwanadamu. Vitendo vinamaanisha yale ambayo yanafaa kufanywa na mwanadamu, yale ambayo yanafaa yafanywe na viumbe wanaomfuata Mungu. Ni wajibu wa mwanadamu pia. Kinachotakiwa kufanywa na mwanadamu si kile alichokielewa tangu awali bali ni yale matakwa ya Mungu wakati wa kuifanya kazi Yake. Matakwa haya taratibu yanakuwa ya kina na kuinuliwa kadri Mungu anavyofanya kazi. Kwa mfano, katika Enzi ya Sheria, mwanadamu alilazimika kuifuata sheria na katika Enzi ya Neema mwanadamu alitakiwa kuubeba msalaba. Enzi ya Ufalme ni tofauti: Matakwa kwa mwanadamu ni mazito kuliko yale ya Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Kadiri maono yanavyoinuliwa zaidi ndivyo matakwa haya yanavyokuwa mazito, ya wazi zaidi na halisi. Vivyo hivyo, maono yanaendelea kuwa halisi. Maono haya mengi na halisi si fursa tu ya utiifu wa mwanadamu kwa Mungu, bali pia, zaidi ya hayo, yanamsaidia yeye kumfahamu Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 153)

Ikilinganishwa na enzi za awali, kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme ni ya vitendo zaidi, imekusudiwa zaidi dutu ya mwanadamu na mabadiliko katika tabia yake na uwezo zaidi wa kuwa na ushuhuda wa Mungu Mwenyewe kwa wale wote wamfuatao Mungu. Kwa maneno mengine, katika Enzi ya Ufalme, Mungu anapofanya kazi hujionyesha zaidi kwa mwanadamu, kuliko kipindi kingine chochote kile cha awali, ikiwa inamaanisha kuwa maono ambayo yanafaa kujulikana na mwanadamu ni ya juu kuliko yale ya enzi yoyote ile ya awali. Kwa kuwa kazi ya Mungu miongoni mwa mwanadamu imeingia maeneo ambayo haikuwa imefika, maono yanayojulikana na mwanadamu katika Enzi ya Ufalme ni ya juu zaidi katika kazi nzima ya usimamizi. Kazi ya Mungu imeingia katika maeneo ambayo haikuwa imewahi kufika, na kwa hivyo maono yanayojulikana na mwanadamu yamekuwa ya juu zaidi katika maono yote, na matokeo ya vitendo vya mwanadamu ni ya juu zaidi kuliko enzi za awali kwani utendaji wa mwanadamu hubadilika kulingana na mabadiliko ya maono na ukamilifu wa maono vilevile huonyesha ukamilifu wa vitendo vya mwanadamu. Punde tu usimamizi wa Mungu usitapo, vitendo vya mwanadamu navyo husimama, na bila kazi ya Mungu mwanadamu hatakuwa na jingine ila tu kujikita katika mafundisho ya zamani, vinginevyo hatakuwa na pa kukimbilia. Bila maono mapya, hapatakuwa na utendaji mpya kutoka kwa mwanadamu; bila kuwepo na maono kamili hapatakuwa na utendaji kamili wa mwanadamu; na bila maono ya juu hapatakuwa na utendaji wa juu wa mwanadamu. Utendaji wa mwanadamu huandamana na nyayo za Mungu na vivyo hivyo ufahamu na tajriba ya mwanadamu hubadilika sawa na kazi ya Mungu. Bila kujali mwanadamu ana uwezo kiasi gani, hawezi kujitenga na Mungu, na iwapo Mungu angaliacha kufanya kazi hata kwa muda kidogo, mwanadamu angalikufa ghafla kutokana na ghadhabu ya Mungu. Mwanadamu hana lolote la kujivunia, kwani haijalishi ufahamu wa mwanadamu ulivyo wa juu leo, haijalishi jinsi uzoefu wake ulivyo wa kina, hawezi kujitenga na kazi ya Mungu—kwani vitendo vya mwanadamu na yale yote anayoyaandama katika imani yake kwa Mungu, hayatengani na maono haya. Katika tukio la kazi ya Mungu, kuna maono ambayo mwanadami anapaswa kujua, na, kufuatia haya matarajio mwafaka huwekewa mwanadamu. Bila haya maono kama msingi, mwanadamu hawezi kuwa na uwezo wa utendaji na pia hangeweza kumfuata Mungu bila kuyumbayumba. Ikiwa mwanadamu hamjui Mungu au hayaelewi mapenzi ya Mungu, basi yote ayafanyayo ni bure na yasiyoweza kukubalika na Mungu. Hata mwanadamu awe na vipawa vingi kiasi gani, bado hawezi kujitenga na kazi ya Mungu na uongozi wa Mungu. Bila kujali uzuri na wingi wa matendo ya mwanadamu, bado hayawezi kuchukua nafasi ya kazi ya Mungu. Kwa hivyo basi, utendaji wa mwanadamu hauwezi kutenganishwa na maono katika hali yoyote ile. Wale ambao hawakubali maono mapya hawana vitendo vipya. Vitendo vyao havina uhusiano na ukweli kwani wanajifunga katika mafundisho ya dini na kufuata sheria zilizokufa; hawana maono mapya kabisa na kwa sababu hiyo hawatendi kulingana na enzi mpya. Wamepoteza maono na kwa kufanya hivyo wamepoteza kazi ya Roho Mtakatifu, hivyo basi kupoteza ukweli pia. Wasio na ukweli ni wazawa wa upuuzi, ni mifano ya Shetani. Bila kujali mtu ni wa aina gani, hawezi kuwepo bila maono ya kazi ya Mungu, hawezi kuishi pasipo na uwepo wa Roho Mtakatifu; punde tu mtu apotezapo maono, anaingia Kuzimu na kuishi gizani. Watu wasio na maono ni wale wamfuatao Mungu kipumbavu, ni wale wasio na kazi ya Roho Mtakatifu, na wanaishi kuzimu. Watu kama hawa huwa hawafuatilii ukweli, na hulitundika jina la Mungu kama bango. Wale ambao hawafahamu kazi ya Roho Mtakatifu, ambao hawamjui Mungu katika mwili, ambao hawajui hatua tatu za kazi katika uzima wa usimamizi wa Mungu—hawajui maono na hivyo wanaishi bila ukweli. Je, si wale wote wasiokuwa na ukweli ni watenda maovu? Wale wanaotaka kuweka ukweli katika vitendo, ambao wako tayari kuutafuta ufahamu wa Mungu, na ambao kwa kweli wanashirikiana na Mungu ni watu ambao maono yanakuwa msingi wao. Wanakubaliwa na Mungu kwa sababu wanashirikiana na Mungu na ushirika huu ndio ambao unafaa kuwekwa katika vitendo na mwanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 154)

Katika maono kuna njia nyingi zinazoelekea kwa vitendo. Matakwa ya utendaji yaliyopo kwa mwanadamu yamo pia ndani ya maono sawa tu na kazi ya Mungu inayopaswa kufahamika na mwanadamu. Katika mikutano maalum ya zamani au mikutano mikuu iliyokuwa katika sehemu mbalimbali, ni kipengele kimoja tu cha vitendo kilichozungumziwa. Vitendo kama hivyo ni vile vilivyotiwa katika vitendo katika Enzi ya Neema na hapakuwa na mfanano wowote na ufahamu wa Mungu kwani maono ya Enzi ya Neema yalikuwa tu maono ya kusulubiwa kwa Yesu, na hapakuwa na maono ya juu zaidi. Mwanadamu hakuhitajika kujua zaidi ya kazi Yake ya ukombozi wa mwanadamu kupitia kusulubiwa, na kwa hivyo katika Enzi ya Neema hapakuwa na maono mengine ya kufahamiwa na mwanadamu. Kwa njia hii, mwanadamu alikuwa na ufahamu mdogo sana wa Mungu na mbali na upendo na huruma za Yesu, kulikuwa na vitu vichache tu vya mwanadamu kuweka katika vitendo, vitu ambavyo vilikuwa tofauti na hali ya leo. Zamani, haikujalisha mkutano wake ulichukua umbo lipi, mwanadamu hakuwa na uwezo wa kuzungumzia ufahamu wa vitendo wa kazi ya Mungu, sembuse kuwepo na yeyote aliyeweza kusema kwa dhahiri njia iliyokuwa sawa ya utendaji kwa mwanadamu kuiingilia. Mwanadamu aliongeza tu mambo kidogo katika msingi wa stahamala na uvumilivu; hapakuwa na mabadiliko yoyote katika kiini cha vitendo vyake kwani katika enzi hiyo Mungu hakufanya kazi yoyote mpya na matakwa ya pekee Aliyomwekea mwanadamu yalikuwa stahamala na uvumilivu, au kuubeba msalaba. Mbali na vitendo kama hivyo, hapakuwa na maono ya juu zaidi kuliko yale ya kusulubishwa kwa Yesu. Zamani hapakutajwa maono mengine kwa sababu Mungu hakufanya kazi kubwa na kwa sababu Alimwekea mwanadamu matakwa machache. Kwa njia hii, haikujalisha mwanadamu alifanya nini, hakuweza kuivuka mipaka ya viwango hivi, viwango ambavyo vilikuwa rahisi na vya juu juu vya mwanadamu kuweka katika vitendo. Leo Nazungumzia maono mengine kwa kuwa leo kazi nyingi zaidi imefanywa, kazi ambayo ni mara kadha zaidi ya ile ya Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Yanayohitajika kwa mwanadamu, aidha, ni mara kadhaa juu zaidi kuliko enzi zilizopita. Iwapo mwanadamu hana uwezo wa kuijua kikamilifu kazi kama hiyo, basi haitakuwa na umuhimu mkubwa; inaweza kuchukuliwa kuwa mwanadamu atakuwa na ugumu kuifahamu kazi yenyewe kikamilifu ikiwa hawezi kuitengea maisha yake yote. Katika kazi ya ushindi, kuzungumzia tu njia ya vitendo kutaufanya ushindi wa mwanadamu kuwa jambo lisilowezekana. Mazungumzo ya maono tu bila matakwa yoyote kwa mwanadamu vilevile kutaufanya ushindi wa mwanadamu kuwa jambo lisilowezekana. Iwapo hapana kitu kingine kitakachoweza kuzungumziwa ila tu njia ya vitendo, basi ingekuwa vigumu kuuweza udhaifu wa mwanadamu, au kuondoa dhana za mwanadamu, na vilevile itakuwa vigumu kumshinda mwanadamu. Maono ni zana muhimu ya ushindi wa mwanadamu, na bado pasingelikuwepo na njia ya vitendo tofauti na maono basi mwanadamu asingelikuwa na njia ya kufuata wala jinsi ya kuingia. Hii imekuwa kanuni ya kazi ya Mungu toka mwanzo hadi mwisho: Katika maono kuna kile ambacho chaweza kuwekwa katika vitendo, na vivyo hivyo kuna maono kuongezea kwa kutenda. Kiwango cha mabadiliko katika maisha na tabia za mwanadamu huambatana na mabadiliko katika maono. Kama mwanadamu angetegemea tu juhudi zake, basi ingekuwa vigumu kwake kufikia kiwango cha juu cha mabadiliko. Maono huzungumzia kazi ya Mungu Mwenyewe na usimamizi wa Mungu. Utendaji hurejelea njia ya vitendo vya mwanadamu na kwa namna ya maisha ya mwanadamu; katika usimamizi wote wa Mungu, uhusiano baina ya maono na vitendo ni uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu. Maono yangetolewa au yangezungumziwa bila kuhusishwa na vitendo, ama kungekuwa tu na maono na vitendo vya mwanaadamu viondolewe, basi vitu kama hivyo visingechukuliwa kama usimamizi wa Mungu, wala isingesemwa kwamba kazi ya Mungu ni kwa ajili ya wanadamu; kwa namna hii, si tu kwamba wajibu wa mwanadamu ungeondolewa, bali pia kazi ya Mungu ingekosa kusudi. Iwapo tangu mwanzo hadi mwisho, mwanadamu angetarajiwa tu kutenda, bila kujihusisha na kazi ya Mungu, na, zaidi ya hayo, kama mwanadamu asingetarajiwa kuifahamu kazi ya Mungu, basi kazi hiyo isingeitwa usimamizi wa Mungu. Kama mwanadamu hangemjua Mungu, na hangejua mapenzi ya Mungu, na huendelea kufanya vitendo kidhahania bila kuwa na uwazi, basi asingekuwa kiumbe kilichohitimu. Hivyo basi, hivi vitu viwili ni vya lazima. Kama kungekuwepo kazi ya Mungu tu, ambayo ni kusema, kungekuwepo maono pekee na hakungekuwepo na ushirikiano au vitendo kutoka kwa mwanadamu, basi hivyo vitu visingeitwa usimamizi wa Mungu. Iwapo kungekuwa tu na vitendo na kuingia kwa mwanadamu, basi bila kujali kuingia kwa mtu kungekuwa kwa juu kiasi gani, haya, pia, hayangekubalika. Kuingia kwa mwanadamu kunafaa kubadilika taratibu kulingana na kazi na maono; hakuwezi kubadilika ghafla. Kanuni za vitendo vya mwanadamu haziko huru na bila vizuizi, lakini ziko ndani ya mipaka fulani. Kanuni hizo hubadilika kwa hatua sawa na maono ya kazi. Hivyo basi usimamizi wa Mungu hatimaye huishia katika kazi ya Mungu na vitendo vya mwanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 155)

Kazi ya usimamizi ilikuja tu kwa ajili ya wanadamu, yaani ilitolewa kwa ajili ya uwepo wa wanadamu. Usimamizi haukuwepo kabla ya uwepo wa wanadamu au mwanzo wakati mbingu na nchi na vilivyomo vilipoumbwa. Iwapo, katika kazi nzima ya Mungu, hakungekuwa na vitendo vinavyomfaidi mwanadamu, yaani kama Mungu asingeweka matakwa maalum kwa mwanadamu aliyepotoka (ikiwa kazi ifanywayo na Mungu haikuwa na njia nzuri ya vitendo vya mwanaadamu), basi kazi hii isingeitwa usimamizi wa Mungu. Iwapo kazi nzima ya Mungu ingehusisha tu kuwaambia wanadamu waliopotoka jinsi ya kuendeleza vitendo vyao, na Mungu hakuendeleza kazi yoyote ya mipango Yake, na Hakuonyesha uwepo wake wa daima au busara, basi bila kujali ni jinsi gani matakwa ya Mungu kwa mwanadamu yangewekwa juu, bila kujali Mungu aliishi muda mrefu kiasi gani miongoni mwa wanadamu, mwanadamu asingejua chochote juu ya tabia ya Mungu; kama ingekuwa hivyo, basi kazi hii isingeweza kukaribia kuitwa usimamizi wa Mungu. Kwa ufupi, kazi ya usimamizi wa Mungu ni kazi iliyofanywa na Mungu na kazi zote zilizofanywa chini ya uongozi wa Mungu na wale ambao wamepatikana na Mungu. Kazi kama hiyo inaweza kuchukuliwa kwa ufupisho kama usimamizi. Kwa maneno mengine, kazi ya Mungu miongoni mwa wanadamu na vilevile ni ushirikiano Wake na wale wanaomfuata kwa ujumla yanaitwa usimamizi. Hapa kazi ya Mungu inaitwa maono na ushirikianao wa mwanadamu unaitwa vitendo. Kadiri kazi ya Mungu ilivyo juu (yaani kadiri maono yalivyo juu), ndivyo tabia za Mungu zinakuwa wazi kwa mwanadamu, na kutoafikiana na mawazo ya mwanadamu, na ndivyo vitendo na ushirikiano wa mwanadamu huwa vya juu. Kadiri matakwa kwa mwanadamu yanavyokuwa ya juu, ndivyo kazi ya Mungu inavyotofautiana mawazo ya mwanadamu, matokeo yake yakiwa majaribu ya mwanadamu, na viwango anavyotarajiwa kuwa navyo, vilevile vinakuwa vya juu. Katika hatima ya kazi hii, maono yote yatakuwa yametimizwa, na yale yote mwanadamu anapaswa kuweka katika vitendo yatakuwa yamefikia kilele cha ukamilifu. Huu ndio wakati pia ambapo kila kitu kitawekwa katika kundi lake kwani kile kinachopaswa kufahamika na mwanadamu kitakuwa kimebainishwa kwake. Kwa hivyo maono yatakapofikia upeo wa juu, vivyo hivyo kazi nayo itakaribia hatima yake na vitendo vya mwanadamu vitakuwa vimefikia ufanisi wake. Vitendo vya mwanadamu vimekitwa katika kazi ya Mungu, na usimamizi wa Mungu unadhihirika tu kupitia vitendo na ushirikiano wa mwanadamu. Mwanadamu ni mfano wa kazi ya Mungu, na mlengwa wa kazi ya usimamizi mzima wa Mungu, na pia mazao ya kazi ya usimamizi wote wa Mungu. Iwapo Mungu angefanya kazi peke yake bila ushirika wa mwanadamu, basi pasingekuwepo na kitu cha kudhihirisha kazi Yake nzima na kwa hali hiyo kusingekuwa na umuhimu hata kidogo wa usimamizi wa Mungu. Kando na kazi ya Mungu, ni kwa Mungu kuchagua vyombo vinavyofaa ili kuonyesha kazi Yake tu, na kuthibitisha kudura na busara zake, ndiyo inawezekana kufikia dhumuni la usimamizi wa Mungu na kufikia dhumuni la kutumia kazi hii yote ili kumshinda kabisa Shetani. Na kwa hivyo mwanadamu ni sehemu muhimu katika kazi ya usimamizi ya Mungu, na mwanadamu ndiye pekee anayeweza kuifanya kazi ya usimamizi ya Mungu izae matunda na kufikia lengo Lake kuu; mbali na mwanadamu, hakuna kiumbe kingine chenye uhai kinachoweza kuchukua nafasi hiyo. Ikiwa mwanadamu atakuwa dhihirisho kamili la kazi ya usimamizi, basi uasi wa wanadamu wenye maovu lazima utokomezwe. Hii inahitaji kuwa mwanadamu apewe utendaji ufaao kwa kila muktadha, na kwamba Mungu afanye kazi inayotangamana miongoni mwa wanadamu. Ni kwa njia hii tu ndipo kutakuwa na kundi la watu waliokubaliwa ambao ni dhihirisho la kazi ya usimamizi. Kazi ya Mungu miongoni mwa wanadamu haiwezi kuwa ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe kupitia kazi ya Mungu peke yake; ushuhuda huo vilevile unahitaji wanadamu ambao wanafaa ili kazi yake iafikiwe. Mwanzo Mungu atawatayarisha watu hawa ambao kupitia kwao kazi Yake itadhihirika na ushuhuda Wake utachukuliwa miongoni mwa viumbe. Kwa hili, Mungu atakuwa ameafiki lengo la kazi Yake. Mungu hafanyi kazi peke Yake kumshinda Shetani kwa sababu Mungu hawezi kujishuhudia Mwenyewe moja kwa moja miongoni mwa viumbe wote. Angefanya hivyo, ingekuwa vigumu kumshawishi mwanadamu, kwa hivyo Mungu lazima Afanye kazi kwa mwanadamu ili kumshinda na ndipo Atakapoweza kupata ushuhuda miongoni mwa viumbe vyote. Mungu angefanya kazi peke Yake bila kushirikiana na mwanadamu, au kama mwanadamu asingetakiwa kushirikiana, basi mwanadamu asingeitambua tabia ya Mungu na daima asingefahamu nia ya Mungu; na kwa hali hii haiwezi kuitwa usimamizi wa Mungu. Mwanadamu mwenyewe angejizatiti, na kutafuta, na kufanya bidii, bila kuifahamu kazi ya Mungu, basi mwanadamu angekuwa anafanya mizaha. Bila kazi ya Roho Mtakatifu, akifanyacho mwanadamu ni cha Shetani, ni muasi na mtenda maovu; Shetani anadhihirika katika yote yafanywayo na mwanadamu mwenye maovu na hamna kinachoafikiana na Mungu, na yote ni dalili ya Shetani. Hakuna kati ya vilivyozungumziwa kisichokuwa na maono na vitendo. Katika msingi wa maono, mwanadamu hupata vitendo na njia ya utiifu, ili kwamba aweze kuweka kando mawazo yake ili apate vile ambavyo hajawahi kuwa navyo hapo awali. Mungu huhitaji mwanadamu ashirikiane naye, kwamba mwanadamu asikilize matakwa Yake, na mwanadamu ashikilie kazi ifanywayo na Mungu Mwenyewe na kuupitia uwezo mkubwa wa Mungu na kuifahamu tabia ya Mungu. Kwa kifupi, haya ndiyo usimamizi wa Mungu. Ushirika wa Mungu na mwanadamu ndio usimamizi, na ni usimamizi mkuu zaidi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 156)

Kile kinachohusisha maono kimsingi hurejelea kazi ya Mungu Mwenyewe, na kile kinachohusisha vitendo ni sharti kifanywe na mwanadamu, na hakina uhusiano na Mungu. Kazi ya Mungu hukamilishwa na Mungu Mwenyewe, na vitendo vya mwanadamu hufikiwa na mwanadamu mwenyewe. Kile ambacho ni sharti kifanywe na Mungu Mwenyewe hakihitajiki kufanywa na mwanadamu, na kile kitendwacho na mwanadamu hakihusiani na Mungu. Kazi ya Mungu ni huduma Yake Mwenyewe na haina uhusiano na mwanadamu. Hii kazi haihitaji kufanywa na mwanadamu, na hata zaidi, mwanadamu hatakuwa na uwezo wa kufanya kazi ambayo ni ya kufanywa na Mungu. Kile ambacho kinafaa kutendwa na mwanadamu ni sharti kitimizwe na mwanadamu, iwe ni kujitoa kafara au kuwasilishwa kwake kwa Shetani ili kushuhudia—haya ni lazima yatimizwe na mwanadamu. Mungu Mwenyewe anatimiza kazi Yake yote, na kile ambacho ni wajibu wa mwanadamu, mwanadamu hufunuliwa na kazi iliyobaki huachiwa mwanadamu. Mungu hafanyi kazi ya ziada. Anafanya ile kazi iliyo katika huduma Yake na kumuonyesha mwanadamu na kumfunulia njia tu bali hampambanulii njia; hili lazima lieleweke kwa mwanadamu. Kuweka ukweli katika vitendo kunamaanisha kuweka neno la Mungu katika vitendo, na haya yote ni wajibu wa mwanadamu, ni kile kinachofaa kufanywa na mwanadamu, na wala halihusiani na Mungu. Iwapo mwanadamu atataka Mungu apitie masaibu na utakaso katika ukweli sawa na mwanadamu, basi mwanadamu atakuwa hatii. Kazi ya Mungu ni kuendeleza huduma Yake, na wajibu wa mwanadamu ni kutii uongozi wote wa Mungu, bila pingamizi yoyote. Kinachotakiwa kufikiwa na mwanadamu anawajibika kutimiza, bila kujali ni namna gani Mungu hufanya kazi au kuishi. Ni Mungu Mwenyewe tu ndiye anayeweza kumwekea mwanadamu matakwa, ambayo ni kusema, ni Mungu Mwenyewe tu ndiye anayestahili kumwekea mwanadamu matakwa. Mwanadamu hastahili kuwa na jingine, hastahili kufanya chochote ila tu kutii kikamilifu na kutenda; hii ndiyo busara ambayo mwanadamu anapaswa kuwa nayo. Punde kazi ifaayo kufanywa na Mungu Mwenyewe itakapokamilika, mwanadamu anatakiwa kuipitia, hatua kwa hatua. Iwapo mwishowe, baada ya usimamizi wote wa Mungu kukamilika, mwanadamu atakuwa hajafanya anachotakiwa na Mungu kufanya, basi mwanadamu anafaa aadhibiwe. Ikiwa mwanadamu hatimizi matakwa ya Mungu, basi hili ni kwa sababu ya uasi wa mwanadamu; haimaanishi kuwa Mungu hajakuwa makini vya kutosha katika kazi Yake. Wale wote wasioweka neno la Mungu katika vitendo, ambao hawatimizi matakwa ya Mungu na wale wote wasiokuwa na uaminifu na kutimiza wajibu wao—wataadhibiwa wote. Leo hii mnachohitajika kufikia si madai ya ziada, ila ni wajibu wa mwanadamu, na kile kinachofaa kufanywa na kila mtu. Kama hamuwezi hata kufanya wajibu wenu, au kuufanya vizuri, hamuoni mnajiletea masaibu nyinyi wenyewe? Hamwuoni mnajitakia kifo? Mtatarajiaje maisha ya baadaye na matarajio? Kazi ya Mungu ni kwa ajili ya wanadamu, na ushirika wa mwanadamu ni kwa minajili ya usimamizi wa Mungu. Baada ya Mungu kufanya yale yote Anayopaswa kufanya, mwanadamu anapaswa kufanya vitendo bila kukoma, na kushirikiana na Mungu. Mwanadamu hapaswi kulegeza kamba katika kazi ya Mungu, lazima aonyeshe uaminifu na asijitie katika mawazo mengi au kukaa akisubiri kifo bila kufanya kitu. Mungu Mwenyewe anaweza kujitolea kwa mwanadamu, basi ni kwa nini mwanadamu asiweze kuwa mwaminifu kwa Mungu? Mawazo na moyo wa Mungu vipo kwa mwanadamu, basi ni kwa nini mwanadamu asijitolee katika ushirika? Mungu huwafanyia wanadamu kazi, basi ni kwa nini mwanadamu asifanye wajibu wake kwa minajili ya usimamizi wa Mungu? Kazi ya Mungu imefika umbali huu, bado mnaona ila hutendi, mnasikia ila hamsogei. Je, si watu kama hawa wanafaa kuangamizwa kabisa? Tayari Mungu amejitolea kikamilifu kwa ajili ya mwanadamu, basi ni kwa nini siku hizi mwanadamu hafanyi wajibu wake kwa dhati? Kwa Mungu, kazi Yake ni ya kipaumbele Kwake, na kazi ya usimamizi Wake ni ya umuhimu wa hali ya juu. Kwa mwanadamu, kuweka maneno ya Mungu katika vitendo na kutimiza mahitaji ya Mungu ndiyo kipaumbele kwake. Ni lazima nyote myafahamu haya. Maneno mliyoambiwa yamefika kiini halisi cha nafsi yenu, na kazi ya Mungu imefika katika maeneo ambayo hayakuwa yamefikiwa awali. Watu wengi bado hawafahamu ukweli na uongo wa njia hii; bado wanasubiri na kutazama na hawafanyi wajibu wao. Badala yake huchunguza kila neno na tendo la Mungu, wanalenga juu ya Anachokula na Anachokivaa na mawazo yao huwa hata ya kuhuzunisha zaidi. Si watu wa aina hii wanafanya msukosuko bure? Hawa wanawezaje kuwa watu wamtafutao Mungu? Na wanawezaje kuwa watu wenye dhamira ya kunyenyekea kwa Mungu? Wanasahau uaminifu na wajibu wao na badala yake kujishughulisha na mahali alipo Mungu. Wanaghadhabisha! Ikiwa mwanadamu amefahamu yale yote anayopaswa kufahamu na kuweka katika vitendo yale yote anayopaswa, basi Mungu atampa mwanadamu baraka Zake, kwa sababu kile ambacho Yeye huhitaji kutoka kwa mwanadamu ni wajibu wa mwanadamu, na kile ambacho mwanadamu anastahili kufanya. Ikiwa mwanadamu hawezi kufahamu yale yote anayopaswa kufahamu na hawezi kutia katika vitendo yale anayopasa kuweka katika vitendo, basi mwanadamu ataadhibiwa. Wasioshirikiana na Mungu wana uhasama Naye, wasioikubali kazi mpya wanaipinga, hata kama watu kama hao hawafanyi chochote ambacho ni cha pingamizi dhahiri. Wale wote wasioweka ukweli unaohitajika na Mungu katika vitendo ni watu wanaopinga kwa makusudi na ni waasi wa maneno ya Mungu hata kama watu kama hawa hutilia maanani maalum kwa kazi ya Roho Mtakatifu. Watu wasiotii maneno ya Mungu na kumnyenyekea Mungu ni waasi, na wapinzani wa Mungu. Watu wasiofanya wajibu wao ni wale wasioshirikiana na Mungu, na watu wasioshirikiana na Mungu ni wale wasioikubali kazi ya Roho Mtakatifu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 157)

Wakati kazi ya Mungu inafikia hatua fulani, na usimamizi Wake kufikia hatua fulani, wale wanaoutafuta moyo Wake wote huwa na uwezo wa kutimiza matakwa yake. Mungu humwekea mwanadamu matakwa kulingana na viwango Vyake mwenyewe, na kulingana na kile ambacho mwanadamu anaweza kufanikisha. Akiwa anazungumzia usimamizi Wake, Yeye humwonyesha njia mwanadamu, na kumpa mwanadamu namna ya kudumu. Usimamizi wa Mungu na vitendo vya mwanadamu vipo katika hatua sawia kikazi, na yote yanafanyika kwa wakati mmoja. Mazungumzo kuhusu usimamizi wa Mungu yanagusia mabadiliko katika tabia ya mwanadamu, na yanazungumzia kuhusu yale yafaayo kufanywa na mwanadamu, na mabadiliko katika tabia ya mwanadamu, hugusia kazi ya Mungu; hakuna wakati ambao haya mawili yanaweza kutenganishwa. Vitendo vya mwanadamu vinabadilika, hatua kwa hatua. Hii ni kwa sababu matakwa ya Mungu kwa mwanadamu yanabadilika na vilevile kwa sababu kazi ya Mungu hubadilika na kusonga mbele kila wakati. Iwapo vitendo vya mwanadamu vitasalia ndani ya mafundisho, hii inathibitisha kwamba amepungukiwa na kazi na mwongozo wa Mungu; ikiwa vitendo vya mwanadamu havitabadilika kamwe au kuwa na kina zaidi, basi hili ni thibitisho kwamba vitendo vya mwanadamu hutendeka kulingana na mapenzi ya mwanadamu, na si vitendo vya ukweli; ikiwa mwanadamu hana njia ya kufuata, basi tayari ameanguka mikononi mwa Shetani, na sasa amedhibitiwa na Shetani, ambayo inamaanisha kwamba amedhibitiwa na roho mchafu. Ikiwa vitendo vya mwanadamu haviendi ndani zaidi, basi kazi ya Mungu haitakua, na kama hakuna mabadiliko katika kazi ya Mungu, basi kuingia kwa mwanadamu kutakwama; hili haliepukiki. Katika kazi nzima ya Mungu, mwanadamu angejifunga katika sheria za Yehova basi kazi ya Mungu isingeendelea na zaidi ingekuwa vigumu kutamatisha enzi nzima. Iwapo mwanadamu angeshikilia msalaba daima na kuishi katika uvumilivu na unyenyekevu, basi kazi ya Mungu isingeendelea. Miaka elfu sita ya usimamizi haiwezi kusitishwa miongoni mwa watu wanaoshikilia tu sheria au kushikilia msalaba na kuishi katika uvumilivu na unyenyekevu tu. Badala yake, kazi nzima ya usimamizi wa Mungu inahitimishwa miongoni mwa watu wa siku za mwisho wanaomfahamu Mungu na ambao wamekombolewa kutoka kwa Shetani na wamejinasua kabisa kutoka katika vishawishi vya Shetani. Huu ni mwelekeo wa kazi ya Mungu usioepukika. Kwa nini inasemekana kwamba vitendo vya walio katika makanisa ya kidini vimepitwa na wakati? Ni kwa kuwa wanayoyaweka katika vitendo ni tofauti na kazi ya leo. Katika Enzi ya Neema, walichotenda kilikuwa sahihi, ila kwa kuwa enzi yenyewe imepita na kazi ya Mungu kubadilika, vitendo vyao hatua kwa hatua vimepitwa na wakati. Vimeachwa nyuma na kazi mpya na mwangaza mpya. Ikiwa imesimama juu ya msingi wake asili, kazi ya Roho Mtakatifu imepiga hatua kadhaa kwa kina. Na bado watu hao wamebaki katika hatua ya asili ya kazi ya Mungu na bado wanapenyeza katikati ya vitendo na mwangaza wa zamani. Kazi ya Mungu yaweza kubadilika pakubwa kwa miaka mitatu au mitano, hivyo si mabadiliko hata makubwa zaidi yaweza kuja kwa kipindi cha miaka zaidi ya 2000? Ikiwa mwanadamu hana vitendo vipya ama mwangaza mpya, inamaanisha hajaenda sawia na kazi ya Roho Mtakatifu. Hili ni anguko la mwanadamu; uwepo wa kazi mpya ya Mungu hauwezi kukanwa kwa sababu, leo hii, wale waliokuwa na kazi ya Roho Mtakatifu hapo awali bado wanashikilia vitendo vilivyopitwa na wakati. Kazi ya Roho Mtakatifu daima inasonga mbele, na wote walio katika mkondo wa Roho Mtakatifu wanafaa waendelee mbele na kubadilika, hatua kwa hatua. Hawapaswi kukwama katika hatua moja. Ni wale tu wasioifahamu kazi ya Roho Mtakatifu ndio wanaweza kubaki katika hatua ya kazi ya Mungu ya awali na wasikubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu. Ni wale tu walio waasi ndio watakosa uwezo wa kuipokea kazi ya Roho Mtakatifu. Ikiwa vitendo vya mwanadamu haviendani na mwendo wa kazi mpya ya Roho Mtakatifu, basi vitendo vya mwanadamu hakika vimetengana na kazi ya leo na kwa hakika havilingani na kazi ya leo. Watu waliopitwa na wakati kama hawa hawawezi kutimiza mapenzi ya Mungu, sembuse kuwa wale watu watakaomshuhudia Mungu hatimaye. Aidha, kazi nzima ya usimamizi haiwezi kutimilika miongoni mwa kundi la watu kama hao. Kwa wale walioshikilia sheria za Yehova kipindi fulani, na wale walioumia wakati fulani chini ya msalaba, ikiwa hawawezi kukubali hatua ya kazi ya siku za mwisho, basi yale yote waliyofanya ni bure na yasiyofaa. Dhihirisho la wazi zaidi wa kazi ya Roho Mtakatifu ni kwa kuyakumbatia ya sasa, sio kushikilia ya zamani. Wale ambao hawajiendelezi na kazi ya leo, na wale ambao wametengwa na utendaji wa leo, ni wale wanaopinga na hawaikubali kazi ya Roho Mtakatifu. Watu kama hao wanaipinga kazi ya Mungu ya sasa. Ijapokuwa wanashikilia nuru ya zamani, hili halimaanishi kwamba inaweza kukanwa kwamba hawajui kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa nini kumekuwepo na mjadala huu wote kuhusu mabadiliko katika vitendo vya mwanadamu, kuhusu tofauti za utendaji kati ya zamani na sasa, kuhusu jinsi utendaji ulivyokuwa katika enzi za awali na jinsi ulivyo sasa? Migawanyiko kama hiyo katika vitendo vya mwanadamu hujadiliwa kwa sababu kazi ya Roho Mtakatifu daima inasonga mbele na kwa hivyo vitendo vya mwanadamu vinapaswa kubadilika daima. Ikiwa mwanadamu atasalia amekwama katika hatua moja tu, basi hili linaonyesha kuwa haendi sawia na kazi mpya na mwangaza mpya wa Mungu; haimaanishi kuwa mpango wa usimamizi wa Mungu haujabadilika. Walio nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu daima hudhani wako sahihi, lakini kwa hakika, kazi ya Mungu ndani yao ilisita zamani na kazi ya Roho Mtakatifu haimo ndani yao. Kazi ya Mungu imeshahamishiwa kwa kundi jingine la watu, kundi ambalo kwalo Anapania kukamilishia kazi Yake mpya. Kwani walio katika dini hawawezi kuikubali kazi mpya ya Mungu, na kushikilia tu kazi kongwe za zamani, hivyo Mungu amewaacha watu hawa na anafanya kazi Yake mpya kwa watu wanaoikubali kazi hii mpya. Hawa ni watu wanaoshiriki katika kazi Yake mpya, na usimamizi Wake utatimilika kwa njia hii tu. Usimamizi wa Mungu daima unasonga mbele na vitendo vya mwanadamu daima vinapanda juu. Mungu daima anafanya kazi na mwanadamu mara zote ni mhitaji ili kwamba wote wanafikia upeo wao, Mungu na mwanadamu wamo katika muungano kikamilifu. Haya ni maonyesho ya kutimilika kwa kazi ya Mungu, na ndiyo matokeo ya mwisho ya kazi nzima ya usimamizi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 158)

Katika kila hatua ya kazi ya Mungu yapo pia matakwa sawia kwa mwanadamu. Wale wote walio katika mkondo wa Roho Mtakatifu wanamilikiwa na uwepo na nidhamu ya Roho Mtakatifu na wasiokuwemo katika mkondo wa Roho Mtakatifu wako chini ya utawala wa Shetani na hawana kazi yoyote ya Roho Mtakatifu. Walio katika mkondo wa Roho Mtakatifu ni wale wanaoikubali kazi mpya ya Mungu, wanaoshiriki katika kazi mpya ya Mungu. Iwapo walio ndani ya mkondo huu hawana uwezo wa kushirikiana, na hawawezi kuweka ukweli unaotakiwa na Mungu katika vitendo wakati huu, basi watafundishwa nidhamu, na hali ikiwa mbaya zaidi kuachwa na Roho Mtakatifu. Wale ambao wanakubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wataishi katika mkondo wa Roho Mtakatifu, wapokee utunzaji na ulinzi wa Roho Mtakatifu. Wale ambao wako tayari kuweka ukweli katika vitendo wanapewa nuru na Roho Mtakatifu na wale wasiotaka kuweka ukweli katika vitendo wanafundishwa nidhamu na Roho Mtakatifu na huenda hata wakaadhibiwa. Bila kujali wao ni aina gani ya watu, ilimradi tu wamo katika mkondo wa Roho Mtakatifu, Mungu atawawajibikia wote wanaoikubali kazi Yake mpya kwa minajili ya jina Lake. Wale wanaolitukuza jina Lake na wako radhi kuweka maneno Yake katika vitendo watapokea baraka Zake; wale wasiomtii na wasioyaweka maneno Yake katika vitendo watapokea adhabu Yake. Watu walio katika mkondo wa Roho Mtakatifu ni wale wanaoikubali kazi mpya, na kwa sababu wameikubali kazi mpya, wanafaa kuwa na ushirika wa kufaa na Mungu na hawafai kuwa kama waasi wasiofanya wajibu wao. Hili ndilo sharti la pekee la Mungu kwa mwanadamu. Sio hivyo kwa watu wasioikubali kazi mpya: Wako nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu, na nidhamu na lawama ya Roho Mtakatifu hayatumiki kwao. Kila siku hawa watu wanaishi ndani ya mwili, wanaishi ndani ya akili zao, na yote wayafanyayo ni kulingana na mafundisho ya kidini yaliyozalishwa na uchanganuzi pamoja na utafiti wa bongo zao. Si matakwa ya kazi mpya ya Roho Mtakatifu sembuse ushirika na Mungu. Wale wasioikubali kazi mpya ya Mungu hawana uwepo wa Mungu na, zaidi, wanakosa baraka na ulinzi wa Mungu. Maneno na matendo yao mengi yanashikilia matakwa ya zamani ya kazi ya Roho Mtakatifu; ni mafundisho ya kidini, si ukweli. Mafundisho na taratibu kama hizo ni thibitisho la kutosha kuwa kukutana pamoja kwa watu hawa si linguine ila dini; si watu walioteuliwa au vyombo vya kazi ya Mungu. Mkutano wa wale wote walio miongoni mwao unaweza tu kuitwa mkutano mkubwa wa watu wa dini, na bali hauwezi kuitwa kanisa. Huu ni ukweli usioweza kubadilishwa. Hawana kazi mpya ya Roho Mtakatifu; wakifanyacho kinaonekana chenye kunuka dini, wanachoishi kwa kudhihirisha katika maisha yao kinaonekana kimejaa dini; hawana uwepo na kazi ya Roho Mtakatifu, sembuse kustahiki kupokea nidhamu au nuru ya Roho Mtakatifu. Watu hawa wote ni miili isiyo na uhai, na funza wasio na mambo ya kiroho. Hawana ufahamu wa uasi na pingamizi wa mwanadamu, hawana ufahamu wa uovu wote wa mwanadamu, sembuse kujua kazi yote ya Mungu na mapenzi ya sasa ya Mungu. Wote ni watu wapumbavu, waovu, ni watu duni wasiostahili kuitwa waumini! Hakuna wafanyacho kinachohusiana na usimamizi wa Mungu, sembuse kuweza kuidhoofisha mipango ya Mungu. Maneno na matendo yao yanaudhi sana, yanasikitisha mno, na hayafai kutajwa kabisa. Hakuna chochote wakifanyacho walio nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu kinahusiana na kazi mpya ya Roho Mtakatifu hata kidogo. Kwa sababu hii, haijalishi wanafanya nini, hawana nidhamu ya Roho Mtakatifu na zaidi, hawana nuru ya Roho Mtakatifu. Kwani wao ni watu wasiopenda ukweli, na wamechukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu. Wanaitwa watenda maovu kwani wanatembea katika mwili, na kufanya chochote kiwafurahishacho kwa kisingizio cha bango la Mungu. Mungu anapofanya kazi, wao wanakuwa maadui Kwake kwa makusudi, na kumkimbia Yeye. Kutoweza kushirikiana kwa mwanadamu na Mungu ni uasi wa hali ya juu, kwa hivyo wale watu wanaokimbia kinyume na Mungu makusudi si watapokea hakika malipo yao ya haki?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 159)

Ni lazima myafahamu maono ya kazi ya Mungu na mpate mwelekeo wa kazi Yake. Huku ni kuingia kwa njia nzuri. Punde unapong’amua ukweli wa maono kwa usahihi, kuingia kwako kutakuwa salama; bila kujali kazi Yake hubadilika kiasi gani, utaendelea kuwa imara moyoni mwako, utakuwa wazi kuhusu maono, na utakuwa na lengo la kuingia na kufuatilia kwako. Kwa njia hiyo, uzoefu na ufahamu ulio ndani yako utakua kwa kina na kutakaswa zaidi. Punde unapong’amua taswira nzima kwa ukamilifu, hutapoteza kitu maishani na hutapotea. Kama hutazijua hatua hizi za kazi, utapata hasara kwa kila mojawapo. Huwezi kugeuka baada ya siku chache tu na hutaweza kuipata njia mwafaka hata katika majuma machache. Je, si hili linakurudisha nyuma? Kuna zaidi katika kuingia kwa njia nzuri dhahiri na vitendo ambavyo mnapaswa kuving’amua, na vilevile unapaswa kuelewa mambo kadha katika maono ya kazi Yake kama vile umuhimu wa kazi Yake ya ushindi, njia ya kufanywa mkamilifu katika siku za usoni, kinachofaa kupatikana kupitia uzoefu wa majaribu na masaibu, umuhimu wa hukumu na kuadibu, kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu, na kanuni za ukamilifu na ushindi. Huu wote ndio ukweli wa maono. Hayo mengine ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme pamoja na ushuhuda wa baadaye. Huu pia ni ukweli kuhusiana na maono, na ni wa msingi na muhimu sana pia. Kwa sasa, kuna mengi sana mnayopaswa kuingia kwayo na kutenda, na kwa sasa yana safu nyingi na maelezo ya kina. Kama huna ufahamu wa ukweli huu, ni thibitisho kwamba bado hujaingia. Mara nyingi, ufahamu wa mwanadamu kuhusu ukweli huwa wa juujuu; mwanadamu hushindwa kuweka ukweli wa kimsingi katika vitendo na hajui jinsi ya kushughulikia hata maswala madogo. Sababu ya mwanadamu kushindwa kutenda ukweli ni tabia yake ya uasi, na kwa sababu ufahamu wake kuhusu kazi ya sasa ni wa juu juu na wa kuegemea upande mmoja. Kwa hivyo, si kazi rahisi kwa mwanadamu kufanywa mkamilifu. Uasi wako ni wa hali ya juu sana, na unashikilia sana hali yako ya zamani; huwezi kusimama katika upande wa ukweli, na huwezi kutenda hata ukweli ulio wazi. Wanadamu kama hao hawawezi kuokolewa na ni wale ambao hawajashindwa. Kama kuingia kwako hakuna kina au malengo, kukua kwako kutakujia polepole. Kama kuingia kwako hakuna uhalisi hata kidogo, basi kufuatilia kwako kutakuwa bure. Kama hujui kiini cha ukweli, hutabadilishwa. Ukuaji katika maisha ya mwanadamu na mabadiliko katika tabia zake hupatikana kwa kuingia ndani ya ukweli na, zaidi ya hili, kwa kuingia katika uzoefu wa kina. Ukiwa na uzoefu wa kina katika wakati wa kuingia kwako, na ukiwa na ufahamu halisi kuhusu kuingia, tabia yako itabadilika haraka. Hata kama kwa sasa hujapata nuru sana katika vitendo, unafaa angalau upate nuru ya maono ya kazi. La sivyo utashindwa kuingia, na hutaweza kufanya hivyo isipokuwa uufahamu ukweli. Ni baada ya kuangaziwa nuru na Roho Mtakatifu katika uzoefu wako ndipo utakapopata ufahamu wa kina kuhusu ukweli na uingie kwa kina. Ni sharti uifahamu kazi ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 160)

Baada ya uumbaji wa mwanadamu hapo mwanzoni, Waisraeli ndio waliokuwa kielelezo cha kazi, na Israeli nzima ilikuwa ngome ya kazi ya Yehova duniani. Kazi ya Yehova ilikuwa imwongoze mwanadamu moja kwa moja na kumchunga kwa kuweka wazi sheria ili kwamba mwanadamu aweze kuishi maisha ya kawaida na kumwabudu Yehova kwa njia ya kawaida duniani. Katika Enzi ya Sheria Mungu alikuwa Asiyeonekana wala kuguswa na mwanadamu. Alikuwa tu Anawaongoza wanadamu waliokuwa mwanzo wamepotoshwa na Shetani, na Alikuwepo kuwaagiza na kuwaongoza wanadamu, kwa hivyo maneno yote Aliyoyanena yalikuwa ya kisheria, amri na maarifa ya kawaida ya kuishi maisha kama mwanadamu, na wala sio kuhusu ukweli unaomruzuku mwanadamu. Waisraeli chini ya uongozi Wake hawakuwa wale waliopotoshwa zaidi na Shetani. Kazi Yake ya sheria ilikuwa tu hatua ya kwanza kabisa katika kazi ya ukombozi, mwanzo hasa wa kazi ya wokovu, na haikuwa inahusiana kamwe na mabadiliko katika tabia za kimaisha za mwanadamu. Kwa hivyo, mwanzoni mwa kazi ya ukombozi hapakuwa na haja Kwake kuwa katika mwili kwa ajili ya kazi Yake katika Israeli. Ndiyo maana Alihitaji kiungo, yaani, chombo ambacho kwacho Angemfikia mwanadamu. Kwa hivyo kukazuka miongoni mwa viumbe waliozungumza na kufanya kazi kwa niaba ya Yehova, na hivi ndivyo wana wa wanadamu na manabii walikuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu. Wana wa Adamu walifanya kazi miongoni mwa wanadamu kwa niaba ya Yehova. Ili waitwe na Yeye inamaanisha kuwa hao watu walipanga sheria kwa niaba ya Yehova na walikuwa miongoni mwa watu wa Israeli; na watu kama hao walikuwa makasisi walioangaliwa na kulindwa na Yehova, na Roho wa Yehova alifanya kazi ndani yao; walikuwa viongozi miongoni mwa wanadamu na wahudumu wa Yehova wa moja kwa moja. Manabii kwa upande mwingine ndio waliokuwa na jukumu la kunena na mataifa na makabila yote kwa niaba ya Yehova. Ndio vilevile waliotoa unabii kuhusu kazi ya Yehova. Wawe wanadamu au manabii, wote waliinuliwa na Roho wa Yehova Mwenyewe na walikuwa na kazi ya Yehova ndani yao. Miongoni mwa wanadamu, walikuwa ndio wale waliomwakilisha Yehova moja kwa moja; walifanya kazi tu kwa kuwa waliinuliwa na Yehova wala si kwa kuwa walikuwa miili ambamo Roho mtakatifu Mwenyewe alikuwa kapata mwili. Kwa hivyo, ingawa wao walifanya kazi na kuongea kwa niaba ya Mungu, hao wana wa mwanadamu na manabii wa Enzi ya Sheria hawakuwa mwili wa Mungu mwenye mwili. Hii ilikuwa kinyume hasa katika Enzi ya Neema na hatua ya mwisho, kwani kazi ya ukombozi na hukumu ya mwanadamu vilifanywa na Mungu katika mwili Mwenyewe, na hapakuwa na haja ya kukuza manabii na wanadamu kufanya kazi kwa niaba Yake. Machoni pa mwanadamu, hamna tofauti kubwa kati ya kiini na mbinu za kazi zao. Ni kwa sababu hii ndiyo mwanadamu anachanganya kati ya kazi ya Mungu mwenye mwili na ile ya manabii na wanadamu. Kimsingi, umbo la Mungu mwenye mwili lilikuwa sawa na lile la manabii na wanadamu. Mungu mwenye mwili alikuwa wa kawaida na halisi zaidi kuliko manabii. Kwa hivyo mwanadamu anashindwa kabisa kuwatofautisha. Mwanadamu huangazia maumbile peke yake bila kugundua kuwa japo wote hufanya kazi na kuongea, kuna tofauti kubwa kati yao. Kwa sababu uwezo wa mwanadamu wa kung’amua ni duni, mwanadamu anashindwa kung’amua mambo ya kimsingi na hata zaidi hawezi kubainisha kitu changamano. Maneno na kazi za manabii na za wale waliotumiwa na Roho Mtakatifu zote zilikuwa zinafanya wajibu wa mwanadamu, kutekeleza jukumu lake kama kiumbe na kufanya ambacho mwanadamu anapaswa kufanya. Hata hivyo, maneno na kazi za Mungu mwenye mwili ilikuwa ni kuendeleza huduma Yake. Ingawa umbo Lake lilikuwa lile la kiumbe, kazi Yake haikuwa kutimiza majukumu Yake bali Huduma Yake. Dhana “wajibu” inarejelea viumbe ilhali “huduma” inarejelea mwili wa Mungu mwenye mwili. Kuna tofauti kubwa kati ya haya mawili, na haya mawili hayabadilishani nafasi. Kazi ya mwanadamu ni kufanya wajibu wake, ilhali kazi ya Mungu ni kusimamia, na kuendeleza huduma Yake. Kwa hivyo, ingawa mitume wengi walitumiwa na Roho Mtakatifu na manabii wengi wakajazwa na Yeye, kazi zao na maneno yao yalikuwa tu kutimiza wajibu wao kama viumbe. Ingawa unabii wao ungeweza kuwa mkubwa kuliko maisha kama yanavyozungumziwa na Mungu mwenye mwili, na hata ubinadamu wao ulikuwa wa hali ya juu kuliko wa Mungu kuwa mwenye mwili, walikuwa bado wanafanya wajibu wao na wala si kutimiza huduma yao. Wajibu wa mwanadamu unarejelea majukumu yake, na ni kitu kinachoweza kupatwa kwa mwanadamu. Hata hivyo, huduma ifanywayo na Mungu mwenye mwili inahusiana na usimamizi Wake, na haiwezi kufanikishwa na mwanadamu. Hata kama Mungu mwenye mwili hunena, kufanya kazi, au kutenda miujiza, Anafanya kazi kubwa katika usimamizi Wake, kazi ambayo haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kazi ya mwanadamu ni kufanya tu wajibu wake kama kiumbe katika hatua fulani ya usimamizi wa Mungu. Bila usimamizi kama huo, yaani, ikiwa huduma ya Mungu mwenye mwili itapotea, pia wajibu wa viumbe utapotea. Kazi ya Mungu kuendeleza huduma Yake ni kumsimamia mwanadamu, ilhali mwanadamu afanyapo wajibu wake ni kutimiza wajibu wake ili kuafikia masharti ya Muumba na haiwezi kwa vyovyote vile kuchukuliwa kwamba ameendeleza huduma ya mtu yeyote. Kwa kiini asili cha Mungu, yaani, Roho, kazi ya Mungu ni usimamizi wake, bali kwa Mungu mwenye mwili akiwa na umbile la nje la kiumbe, kazi yake ni kuendeleza huduma Yake. Kazi yoyote Aifanyayo ni ya kuendeleza huduma Yake, na mwanadamu anaweza tu kufanya awezalo ndani ya upeo Wake wa usimamizi na chini ya uongozi Wake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 161)

Katika Enzi ya Neema, Yesu pia Alinena mengi na kufanya kazi nyingi. Alikuwaje tofauti na Isaya? Alikuwaje tofauti na Danieli? Je, Alikuwa nabii? Ni kwa nini inasemekana kwamba Yeye ni Kristo? Kuna tofauti gani baina yao? Wote walikuwa wanadamu walionena maneno, na maneno yao yalionekana sawa kwa wanadamu. Wote walinena na kufanya kazi. Manabii wa Agano la Kale walitoa unabii, na vivyo hivyo, pia na Yesu. Ni kwa nini iwe hivi? Tofauti hapa inapatikana katika aina ya kazi zao. Ili kutambua suala hili, huwezi kuangazia asili ya mwili na hufai kuangazia upurukushani wa maneno ya mtu. Daima ni sharti kwanza uangazie kazi yake na athari ambayo kazi yake inafanikisha ndani ya mwanadamu. Unabii uliotolewa na manabii wakati ule, haukuyaruzuku maisha ya mwanadamu, na ujumbe uliopokelewa na watu kama Isaya na Danieli ulikuwa tu unabii na si njia ya uzima. Ingekuwa si kuonekana moja kwa moja kwa Yehova, hakuna ambaye angefanya hiyo kazi, ambayo haiwezekani kwa wanadamu. Yesu pia Alisema mengi, lakini maneno yake yalikuwa njia ya uzima ambayo kwayo mwanadamu angepata njia ya kutenda. Hii ni kusema kuwa, kwanza, Angeukimu uzima wa mwanadamu, kwa kuwa Yesu ni uzima; pili, Angeweza kuugeuza upotovu wa mwanadamu; tatu, kazi Yake ingeweza kuifuata ile ya Yehova ili kuendeleza enzi; nne, Angeweza kutambua mahitaji ya mwanadamu kwa ndani na kufahamu anachokosa mwanadamu; tano, Angeweza kuanzisha enzi mpya na kutamatisha enzi ya zamani. Ndiyo maana Anaitwa Mungu na Kristo; Yeye si tofauti na Isaya tu; bali pia na manabii wengine wote. Chukua Isaya kama ulinganisho wa kazi za manabii. Kwanza, asingeweza kuukimu uzima wa mwanadamu; pili, asingeweza kuanzisha enzi mpya. Alikuwa akifanya kazi chini ya uongozi wa Yehova wala si kuanzisha enzi mpya. Tatu, alichokizungumza yeye mwenyewe kilikuwa nje ya ufahamu wake. Alikuwa akipata ufunuo moja kwa moja kutoka kwa Roho wa Mungu, na wengine wasingeelewa hata baada ya kuusikiliza ufunuo huo. Haya machache yanatosha kuthibitisha kuwa kazi yake haikuwa zaidi ya unabii, si zaidi ya kazi iliyofanywa kwa niaba ya Yehova. Hata hivyo, asingeweza kumwakilisha Yehova kikamilifu. Alikuwa mtumishi wa Yehova, chombo katika kazi ya Yehova. Aidha alikuwa anafanya kazi katika Enzi ya Sheria tu na katika mawanda ya kazi ya Yehova; hakufanya kazi nje ya Enzi ya Sheria. Kinyume na haya, kazi ya Yesu ilikuwa tofauti. Alivuka mipaka ya kazi ya Yehova; Alifanya kazi kama Mungu mwenye mwili na kupitia mateso ili amkomboe mwanadamu. Hiyo ni kusema kuwa Alifanya kazi mpya nje ya ile iliyofanywa na Yehova. Huku kulikuwa kukaribisha kwa enzi mpya. Jambo jingine ni kuwa Aliweza kuyazungumzia mambo ambayo mwanadamu asingeweza kupata. Kazi Yake ilikuwa kazi ndani ya usimamizi wa Mungu na ilijumuisha wanadamu wote. Hakufanya kazi miongoni mwa watu wachache tu, na wala kazi yake haikuwa kuwaongoza watu wachache tu. Kuhusu jinsi Mungu alivyopata mwili kuwa mwanadamu, jinsi Roho alivyotoa ufunuo wakati ule, na jinsi Roho alivyomshukia mwanadamu kufanya kazi, haya ni mambo ambayo mwanadamu hawezi kuona au kugusa. Haiwezekani kabisa ukweli huu kuwa thibitisho kuwa Yeye ni Mungu mwenye mwili. Kwa sababu hii, tofauti inaweza kupatikana tu kwenye maneno na kazi ya Mungu ambayo ni mambo dhahiri kwa mwanadamu. Hili tu ndilo halisi. Hii ni kwa sababu masuala ya Roho hayaonekani kwako na yanafahamika wazi na Mungu Mwenyewe peke Yake, wala hata mwili wa Mungu haufahamu yote; unaweza kuthibitisha tu kama Yeye ni Mungu[a] kutokana na kazi Aliyoifanya tu. Kutokana na kazi Yake, inaweza kuonekana kuwa, kwanza, Anaweza kufungua enzi mpya; pili, Yeye ana uwezo wa kuyaruzuku maisha ya mwanadamu na kumwonyesha mwanadamu njia ya kufuata. Hii inatosha kuthibitisha kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe. Angalau kazi Aifanyayo yaweza kumwakilisha kikamilifu Roho Mtakatifu wa Mungu na kutokana na kazi hiyo inaonekana kuwa Roho wa Mungu yupo ndani Yake. Kwa kuwa kazi iliyofanywa na Mungu mwenye mwili ilikuwa kuanzisha enzi mpya, kuongoza kazi mpya, na kuanzisha na kufungua mazingira mapya, haya mambo machache tu yanatosha kuthibitisha kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe. Hili kwa hivyo linamtofautisha na Isaya, Danieli, na manabii wengine wakuu. Isaya, Danieli na wengine wote walikuwa ni watu walioelimika na kustaarabika vilivyo; walikuwa watu wa kipekee chini ya uongozi wa Yehova. Mwili wa Mungu mwenye mwili pia ulikuwa na maarifa na haukupungukiwa na akili ila ubinadamu Wake ulikuwa wa kawaida. Alikuwa mwanadamu wa kawaida na jicho la mwanadamu lisingeweza kubaini ubinadamu wowote wa pekee kumhusu au kugundua kitu chochote katika ubinadamu Wake tofauti na wa wale wengine. Kamwe hakuwa kabisa wa kimiujiza au wa kipekee na hakuwa na elimu ya juu, ujuzi au nadharia kupita kiasi. Maisha Aliyoyazungumzia na njia Aliyoenenda hakuipata kinadharia, kielimu, kitajriba au kupitia malezi ya kifamilia. Badala yake, ilikuwa kazi ya moja kwa moja ya Roho, ambayo ni kazi ya mwili. Ni kwa kuwa mwanadamu ana mawazo makuu kumhusu Mungu, na hasa kwa kuwa fikira hizi hutungwa kutokana na vipengele vingi visivyo yakini na vya kimiujiza hivi kwamba, katika macho ya mwanadamu, Mungu wa kawaida mwenye udhaifu wa kibinadamu, ambaye hawezi kutenda miujiza, kwa hakika si Mungu. Je, si hizi ni fikra potovu za mwanadamu? Mwili wa Mungu mwenye mwili usingekuwa wa kawaida, basi ingesemekanaje kwamba Alipata mwili? Kupata mwili ni kuwa mtu wa kawaida; iwapo angekuwa wa kupita uwezo wa binadamu, basi Asingeweza kuwa wa kimwili. Kuthibitisha kuwa Yeye ni wa kimwili, Mungu mwenye mwili alihitaji kuwa na mwili wa kawaida. Hili lilikusudiwa tu kutimiza umuhimu wa kupata mwili. Hata hivyo, mambo hayakuwa hivyo kwa manabii na wanadamu. Walikuwa wanadamu waliopewa vipawa na kutumiwa na Roho Mtakatifu; machoni mwa mwanadamu, ubinadamu wao ulikuwa wa hali ya juu, walitenda matendo mengi yaliyovuka mipaka ya ubinadamu wa kawaida. Kwa sababu hii mwanadamu aliwachukulia kama Mungu. Sasa ni sharti nyote mlione hili kwa uwazi zaidi, kwani limekuwa jambo ambalo liliwakanganya sana wanadamu wote katika enzi zilizopita. Aidha, kuwa mwili ndicho cha ajabu zaidi kwa vitu vyote, na Mungu mwenye mwili ni vigumu zaidi kukubaliwa na mwanadamu. Ninachokisema kinasaidia katika kutimiza majukumu yenu na kuelewa kwenu kwa fumbo la kupata mwili. Haya yote yanahusiana na usimamizi wa Mungu, kwa maono. Ufahamu wenu wa hili jambo utakuwa wa faida zaidi kwa kupata ufahamu wa maono, yaani kazi ya usimamizi. Kwa njia hii, mtafahamu zaidi pia wajibu ambao wanadamu mbalimbali wanafaa kutekeleza. Ingawa maneno haya hayawaonyeshi njia moja kwa moja, bado ni msaada mkubwa kwa kuingia kwenu, kwa kuwa maisha yenu ya sasa yamepungukiwa sana na maono na hili litakuwa kikwazo kikubwa kinachozuia kuingia kwenu. Kama hamjaweza kuyafahamu masuala haya, basi hakutakuwa na motisha ya kuchochea kuingia kwenu. Na kufuatilia kama huku kunawezaje kuwawezesha kutimiza wajibu wenu vyema zaidi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu

Tanbihi:

a. Maandiko asili hayana kauli “kama Yeye ni Mungu.”

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 162)

Watu wengine watauliza, “Nini tofauti kati ya kazi aliyoifanya Mungu wa mwili na ile ya manabii na mitume wa zamani? Daudi pia aliitwa Bwana, na hivyo pia akawa Yesu; ingawa kazi waliyoifanya ilikuwa tofauti, waliitwa kitu kimoja. Mbona, unauliza, hawakuwa na utambulisho mmoja? Kile Yohana alichoshuhudia kilikuwa maono, moja iliyotoka pia kwa Roho Mtakatifu, na aliweza kuyasema maneno ambayo Roho Mtakatifu alikusudia kuyasema; kwa nini utambulisho wa Yohana ni tofauti na ule wa Yesu?” Maneno aliyoyasema Yesu yaliweza kumwakilisha Mungu kikamilifu, na kuwakilisha kikamilifu kazi ya Mungu. Kile alichokiona Yohana kilikuwa maono, na hakuweza kuwakilisha kikamilifu kazi ya Mungu. Ni kwa nini Yohana, Petro na Paulo walizungumza maneno mengi—kama alivyofanya Yesu—lakini bado hawakuwa na utambulisho sawa na Yesu? Ni hasa kwa sababu kazi waliyoifanya ilikuwa tofauti. Yesu aliwakilisha Roho wa Mungu, na Alikuwa Roho wa Mungu Akifanya kazi moja kwa moja. Alifanya kazi ya enzi mpya, kazi ambayo hakuna aliyekuwa amefanya mbeleni. Yeye Alifungua njia mpya, Alimwakilisha Yehova, na Alimwakilisha Mungu Mwenyewe. Ilhali kwa Petro, Paulo na Daudi, bila kujali walichoitwa, waliwakilisha tu utambulisho wa kiumbe wa Mungu, na walitumwa na Yesu na Yehova. Kwa hivyo bila kujali kiasi cha kazi walichofanya, bila kujali jinsi walivyofanya miujiza kubwa, walikuwa bado tu viumbe wa Mungu, na hawakuweza kuwakilisha Roho Mtakatifu. Walifanya kazi kwa jina la Mungu ama baada ya kutumwa na Mungu; zaidi ya hayo, walifanya kazi katika enzi iliyoanzishwa na Yesu ama Yehova, na kazi waliyoifanya haikutengwa. Walikuwa, hatimaye, viumbe wa Mungu tu. Katika Agano la Kale, manabii wengi walizungumza utabiri, ama kuandika vitabu vya unabii. Hakuna aliyesema kuwa yeye ni Mungu, lakini punde tu Yesu Alipoanza kufanya kazi, Roho wa Mungu Alimshuhudia kuwa Yeye ni Mungu. Mbona hivyo? Kwa sasa, unapaswa kujua tayari! Awali, mitume na manabii waliandika nyaraka mbalimbali, na kufanya unabii mwingi. Baadaye, watu walichagua baadhi zao kuweka katika Biblia, na baadhi zikapotea. Kwa vile kuna watu wanaosema kuwa vitu vyote wanavyozungumza vimetoka kwa Roho Mtakatifu, mbona baadhi yavyo vinachukuliwa kuwa nzuri, na baadhi yavyo vinachukuliwa kuwa mbaya? Na mbona baadhi vilichaguliwa, na sio vingine? Kama kweli yalikuwa maneno Aliyoyasema Roho Mtakatifu, ingekuwa lazima kwa watu kuyachagua? Kwa nini akaunti ya maneno yaliyosemwa na Yesu na kazi Aliyoifanya ni tofauti katika kila moja ya Injili Nne? Makosa sio ya waliyoyarekodi? Watu wengine watauliza, “Sababu nyaraka zilizoandikwa na Paulo na waandishi wengine wa Agano Jipya na kazi walizozifanya zilitokana kidogo na matakwa ya mwanadamu, na zilichanganywa na dhana za mwanadamu, basi hakuna uchafu wa binadamu katika maneno ambayo Wewe (Mungu) unazungumza leo? Je, kweli hayana dhana hata moja za mwanadamu?” Hii hatua ya kazi aliyoifanya Mungu ni tofauti kabisa na zile walizozifanya Paulo na wengi wa mitume na manabii. Sio tu kwamba kuna tofauti na utambulisho, lakini, hasa, kuna tofauti kati ya kazi inayofanywa. Baada ya Paulo kupigwa chini na kuanguka mbele ya Bwana, aliongozwa na Roho Mtakatifu kufanya kazi, na akawa mtume. Na hivyo akaandikia makanisa nyaraka, na hizi nyaraka zote zilifuata mafundisho ya Yesu. Paulo alitumwa na Bwana kufanya kazi kwa jina la Bwana Yesu, lakini Mungu Mwenyewe alipokuja, Hakufanya kazi kwa jina lolote na Hakuwakilisha yeyote isipokuwa Roho wa Mungu katika kazi Yake. Mungu alikuja kufanya kazi Yake moja kwa moja: Hakukamilishwa na mwanadamu, na kazi Yake haikufanywa juu ya mafundisho ya mwanadamu yeyote. Katika hatua hii ya kazi Mungu haongozi kwa kuzungumza juu ya uzoefu Wake binafsi, ila Hufanya kazi Yake moja kwa moja, kulingana na Alicho nacho. Kwa mfano, jaribio la watoa huduma, nyakati za kuadibu, jaribio la kifo, nyakati za kumpenda Mungu…. Hii yote ni kazi ambayo haijawahi kufanywa mbeleni, na ni kazi ya enzi ya sasa, badala ya uzoefu wa binadamu. Kwa maneno Nimesema, ni yapi mazoefu ya mwanadamu? Je, yote hayatoki moja kwa moja kwa Roho Mtakatifu, na hayatolewi nje na Roho Mtakatifu? Ni vile tu aina yako ni maskini sana hadi huwezi kuona kupitia ukweli! Maisha ya vitendo Ninayozungumzia ni ya kuongoza njia, na hayajawahi zungumziwa na yeyote mbeleni, wala hakuna aliye na uzoefu wa njia hii, wala kujua ukweli huu. Kabla Niliyatamka maneno haya, hakuna aliyewahi kuyasema. Hakuna aliyezungumzia mazoefu haya, wala hakuna aliyewahi kusema maelezo hayo, na, zaidi ya hayo, hakuna aliyewahi kuonyesha hali kama hizo kufichua mambo haya. Hakuna aliyewahi kuongoza njia Ninayoongoza leo, na kama ingeongozwa na mwanadamu, basi isingekuwa njia mpya. Chukua Paulo na Petro, kwa mfano. Hawakuwa na uzoefu wao binafsi kabla ya Yesu aiongoze njia. Ilikuwa tu baada ya Yesu kuongoza njia ndipo walipopata uzoefu wa maneno aliyoyasema Yesu, na njia aliyoiongoza; kutoka hapa walipata mazoefu mengi, na kuziandika nyaraka, Na hivyo, uzoefu wa mwanadamu sio sawa na kazi Ya Mungu, na kazi ya Mungu sio sawa na maarifa yalivyoelezwa na dhana na uzoefu wa mwanadamu. Nimesema, tena na tena, kuwa leo Ninaongoza njia mpya, na kufanya kazi mpya, na kazi na matamshi Yangu ni tofauti na yale ya Yohana na wale manabii wengine wote. Kamwe, Sijawahi pata uzoefu kwanza, na kisha kuyazungumzia kwenu—hiyo sio ukweli hata kidogo. Kama ingekuwa hivyo, haingewachelewesha kitambo sana? Zamani, maarifa waliyoyazungumzia wengi yalipandishwa cheo pia, lakini maneno yao yote yalisemwa tu kulingana na hayo ya wanaoitwa takwimu wa kiroho. Hawakuiongoza njia, lakini walitoka kwa uzoefu wao, walitoka kwa walichokiona, na kwa maarifa yao. Zingine zilikuwa dhana zao, na mengine yalikuwa mazoefu waliyofupisha. Leo, asili ya kazi Yangu ni tofauti kabisa na yao. Sijapata uzoefu wa kuongozwa na wengine, wala Sijakubali kukamilishwa na wengine. Zaidi ya hayo, yote Nimesema na kushiriki ni tofauti na yale ya wengine, na hayajawahi kuzungumzwa na mwingine yeyote. Leo, bila kujali ninyi ni nani, kazi yenu inafanywa kulingana na maneno Nisemayo. Bila haya matamshi na kazi, nani angeweza kupata uzoefu wa mambo haya (majaribu ya watendaji huduma, nyakati za kuadibu…), na nani ataweza kuzungumzia maarifa kama haya? Kweli huna uwezo wa kuona haya? Bila kujali hatua ya kazi, punde tu maneno Yangu yasemwapo, mnaanza kushiriki kulingana na maneno Yangu, na kufanya kazi kulingana nayo, na sio njia ambayo yeyote kati yenu amefikiria. Baada ya kuja mbali hivi, huna uwezo wa kuona swali wazi na rahisi hivi? Sio njia iliyowazwa na yeyote, wala haijalinganishwa na mtu yeyote wa kiroho. Ni njia mpya, na hata maneno mengi yaliyosemwa mara kwanza na Yesu hayatumiki tena. Ninachozungumza ni kazi ya kufungua enzi mpya, na ni kazi inayosimama peke yake; kazi Nifanyayo, na maneno Nizungumzayo, yote ni mapya. Si hii ndiyo kazi mpya ya leo? Kazi ya Yesu pia ilikuwa hivi. Kazi Yake pia ilikuwa tofauti na hizo za watu wengine hekaluni, na pia ilitofautiana na kazi za Mafarisayo, na wala haikufanana na zilizofanywa na watu wote wa Israeli. Baada ya kuishuhudia, watu walishindwa kuamua: “Kweli ilifanywa na Mungu?” Yesu hakuzingatia sheria ya Yehova; Alipokuja kumfunza mwanadamu, yote Aliyoyanena yalikuwa mapya na tofauti na yale yaliyosemwa na watakatifu wa zamani na manabii wa Agano la Kale, na kwa sababu hii, watu walisalia bila uhakika. Hii ndiyo humfanya mwanadamu kuwa mgumu sana kushughulika naye. Kabla ya kukubali hii hatua mpya ya kazi, njia ambayo wengi wenu walitembelea ilikuwa ya kutenda na kuingia katika msingi wa watu hao wa kiroho. Lakini leo, kazi Ninayoifanya ni tofauti sana, na hivyo hamna uwezo wa kuamua kama ni sawa ama sio. Sijalishwi na njia uliyopitia mbeleni, wala Sijali ulikula “chakula” cha nani, ama uliyemchukua kama “babako.” Sababu Nimekuja na kuleta kazi mpya ya kumwongoza mwanadamu, wote wanaonifuata lazima watende kulingana na Ninachosema. Bila kujali jinsi ulivyotoka “familia” ya nguvu, lazima unifuate, hupaswi kutenda kulingana na mazoea yako ya awali, “Baba wa kambo” wako anapaswa kushuka nawe unapaswa kuja mbele ya Mungu wako kupata mgao wako halali. Uzima wako wote umo mikononi Mwangu, nawe hupaswi kuwa na imani kipofu nyingi kwa baba wako wa kambo, hawezi kukutawala kabisa. Kazi ya leo inasimama peke yake. Yote Nisemayo leo ni wazi hayajalinganishwa na msingi wa zamani; ni mwanzo mpya, na ukisema kuwa umetengenezwa na mkono wa mwanadamu, basi wewe ni mtu aliye kipofu sana kwamba huwezi kuokolewa!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Majina na Utambulisho

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 163)

Isaya, Ezekieli, Musa, Daudi, Ibrahimu na Danieli walikuwa viongozi ama manabii kati ya wateule wa Israeli. Mbona hawakuitwa Mungu? Mbona Roho Mtakatifu hakuwashuhudia? Mbona Roho Mtakatifu alimshuhudia Yesu punde tu Alipoanza kazi yake na kuanza kuzungumza maneno Yake? Na mbona Roho Mtakatifu hakuwashuhudia wengine? Wao, wanadamu waliokuwa na mwili, wote waliitwa “Bwana.” Bila kujali waliyoitwa, kazi yao inawakilisha utu wao na kiini chao, na utu wao na kiini chao kinawakilisha utambulisho wao. Kiini chao hakina uhusiano na majina yao, inawakilishwa na waliyoonyesha, na waliyoishi kwa kudhihirisha. Kwa Agano la Kale, hakuwa na chochote tofauti na kuitwa Bwana, na mtu angeitwa kwa njia yoyote, lakini kiini na utambulisho wake wa asili ulikuwa haubadiliki. Kati ya hao Kristo wa uwongo, manabii waongo na wadanganyifu, hakuna wanaoitwa “Mungu” pia? Na mbona hao sio Mungu? Kwa sababu hawana uwezo wa kufanya kazi ya Mungu. Mizizini, wao ni wanadamu, wanaowadanganya watu, sio Mungu, na hivyo hawana utambulisho wa Mungu. Daudi pia hakuitwa Bwana miongoni mwa makabila kumi na mawili? Yesu pia aliitwa Bwana: mbona ni Yesu pekee aliyeitwa Mungu wa mwili? Yeremia pia hakujulikana kama Mwana wa Adamu? Na Yesu pia hakujulikana kama Mwana wa Adamu? Mbona Yesu alisulubiwa kwa niaba ya Mungu? Si kwa sababu kiini chake kilikuwa tofauti? Si kwa sababu kazi aliyoifanya ilikuwa tofauti? Je, jina lina umuhimu? Ingawa Yesu pia aliitwa Mwana wa Adamu, Alikuwa kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya kwanza. Alikuwa amekuja kuchukua mamlaka, na kukamilisha kazi ya ukombozi. Hii inathibitisha kuwa utambulisho na kiini cha Yesu kilikuwa tofauti na kile cha wengine walioitwa pia wana wa wanadamu. Leo, nani kati yenu anathubutu kusema kwamba maneno yote yaliyotamkwa na wale waliotumiwa na Roho Mtakatifu yalitoka kwa Roho Mtakatifu? Kuna anayethubutu kusema mambo kama haya? Ukisema mambo kama haya, basi mbona kitabu cha Ezra cha unabii kiliondolewa, na mbona jambo hilo pia likafanyiwa vitabu vya watakatifu na manabii wa kale? Kama yote yalitoka kwa Roho Mtakatifu, basi mbona mnathubutu kufanya maamuzi ambayo yanabadilika kama haya? Umehitimu kuchagua kazi ya Roho Mtakatifu? Hadithi nyingi kutoka Israeli pia zilitolewa. Na ukiamini kwamba maandishi haya yote ya kale yalitoka Roho Mtakatifu, basi mbona baadhi ya vitabu vilitolewa? Kama yote yalitoka kwa Roho Mtakatifu, yote yanapaswa kuwekwa, na kutumwa kwa ndugu na dada wa makanisa kuyasoma. Hayapaswi kuchaguliwa na kutolewa kwa matakwa ya mwanadamu; ni makosa kufanya hivyo. Kusema kwamba mazoefu ya Paulo na Yohana yalichanganywa na waliyoyaona binafsi hakumaanishi kwamba uzoefu na maarifa yao yalitoka kwa Shetani, ila tu walikuwa na mambo yaliyotoka kwa mazoefu na waliyoyaona wao binafsi. Maarifa yao yalilingana na asili ya mazoefu halisi ya wakati huo, na ni nani anayeweza kusema kwa ujasiri kwamba yote yalitoka kwa Roho Mtakatifu? Kama Injili Nne zote zilitoka kwa Roho Mtakatifu, basi ilikuwaje kwamba Mathayo, Marko, Luka na Yohana kila mmoja alisema jambo tofauti kuhusu kazi ya Yesu? Msipoamini haya, basi angalia akaunti tofauti kwa Biblia ya jinsi Petro alivyomkana Yesu mara tatu: Yote ni tofauti, na kila moja ina sifa yake yenyewe. Wengi walio wajinga husema, “Mungu wa mwili pia ni mwanadamu, kwa hivyo maneno Anayoyazungumza yanaweza kutoka kikamilifu kwa Roho Mtakatifu? Kama maneno ya Paulo na Yohana yalichanganywa na matakwa ya mwanadamu, basi maneno Anayoyasema kweli hayajachanganywa na matakwa ya mwanadamu?” Watu wanaosema mambo kama haya ni vipofu na wajinga! Soma Injili Nne kwa kina; soma iliyorekodi kuhusu alichofanya Yesu, na maneno Aliyoyasema. Kila akaunti ilikuwa kwa urahisi tofauti, na kila ilikuwa na mtazamo wake. Kama vilivyoandikwa na waandishi wa vitabu hivi vyote vilitoka kwa Roho Mtakatifu, basi yote yanapaswa kuwa sawa na thabiti. Basi mbona kuna tofauti? Si mwanadamu ni mjinga sana, kutoweza kuona haya? Ukiulizwa kutoa ushuhuda kwa Mungu, ni ushuhuda upi unaoweza kutoa? Njia hii ya kumjua Mungu inaweza kumshuhudia? Wengine wakikuuliza, “Kama rekodi ya Yohana na Luka yalichanganywa na matakwa ya mwanadamu, basi maneno yanayosemwa na Mungu wenu hayajachanganywa na matakwa ya mwanadamu?” utaweza kupeana jibu wazi? Baada ya Luka na Mathayo kuyasikia maneno ya Yesu, na kuona kazi ya Yesu, walizungumzia maarifa yao, kwa namna ya kumbukumbu walisema kwa kina baadhi ya mambo aliyoyafanya Yesu. Unaweza kusema kwamba maarifa yao yalifichuliwa kabisa na Roho Mtakatifu? Nje ya Biblia, kulikuwa na watu wengi wa kiroho wa maarifa ya juu kuwaliko; mbona maneno yao hayajachukuliwa na vizazi vya baadaye? Wao hawakutumika pia na Roho Mtakatifu? Jua kwamba kwa kazi ya leo, Sizungumzii juu ya kuona kwangu kunaolingana na msingi wa kazi ya Yesu, wala Sizungumzi juu ya maarifa Yangu dhidi ya usuli wa kazi ya Yesu. Ni kazi ipi Aliyofanya Yesu wakati huo? Na ni kazi ipi Ninayofanya leo? Ninachofanya na kusema hayana historia. Njia Nitembeleayo leo haijawahi kukanyagiwa mbeleni, haikuwahi tembelewa na watu wa enzi na vizazi vya kale. Leo, imefunguliwa, na hii sio kazi ya Roho? Hata kama ilikuwa kazi ya Roho Mtakatifu, viongozi wote wa kale walifanya kazi yao juu ya msingi wa wengine. Hata hivyo, kazi ya Mungu Mwenyewe ni tofauti. Hatua ya kazi ya Yesu ilikuwa sawa: Aliifungua njia mpya. Alipokuja Alihubiri injili ya ufalme wa mbinguni, na kusema kwamba mwanadamu anapaswa kutubu na kukiri. Baada ya Yesu kukamilisha kazi yake, Petro na Paulo na wengineo walianza kuendeleza kazi ya Yesu. Baada ya Yesu kusulubiwa na kupaa mbinguni, walitumwa na Roho Mtakatifu kueneza njia ya msalaba. Ingawa maneno ya Paulo yalipandishwa cheo, pia yalilingana na msingi uliolazwa na kile Yesu alisema, kama uvumilivu, upendo, mateso, kufunika kichwa, ubatizo, ama mafundisho mengine yakufuatwa. Haya yote yalikuwa juu ya msingi wa maneno ya Yesu. Hawakuwa na uwezo wa kufungua njia mpya, kwani wote walikuwa wanadamu waliotumiwa na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Majina na Utambulisho

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 164)

Matamshi na kazi ya Yesu wakati huo hayakushikilia mafundisho, na hakufanya kazi Yake kulingana na kazi ya sheria ya Agano la Kale. Yalilingana na kazi iliyopaswa kufanywa kwa Enzi ya Neema. Alitenda kulingana na kazi Aliyokuwa ameleta mbele, kulingana na mipango Yake, na kulingana na huduma Yake; Hakufanya kazi kulingana na sheria ya Agano la Kale. Hakuna Alichofanya kilicholingana na Agano la Kale, na Hakuja kufanya kazi ili kutimiza maneno ya manabii. Kila hatua ya kazi ya Mungu haikuwa wazi ili kutimiza utabiri wa manabii wa zamani, na Hakuja kuyafuata mafundisho au kutambua makusudi utabiri wa manabii wa kale. Bado vitendo Vyake havikuvuruga utabiri wa manabii wa kale, wala havikuvuruga kazi Aliyokuwa amefanya awali. Hatua muhimu ya kazi Yake haikuwa kufuata mafundisho yoyote, na kufanya kazi ambayo Yeye Mwenyewe anapaswa kufanya. Yeye hakuwa nabii wala mwaguzi, ila mtendaji, aliyekuja kufanya hiyo kazi Aliyopaswa kufanya, na aliyekuja kufungua enzi Yake mpya na kufanya kazi Yake mpya. Bila shaka, Yesu alipokuja kufanya kazi Yake, pia Alitimiza maneno mengi yaliyosemwa na manabii wa zamani kwa Agano la Kale. Hivyo pia kazi ya leo imetimiza utabiri wa manabii wa zamani wa Agano la Kale. Ni vile tu Sishikilii hiyo “kalenda njano ya zamani,” hayo tu. Kwani kuna kazi zaidi ambayo lazima Nifanye, kuna maneno zaidi ambayo lazima Niwazungumzie, na kazi hii na maneno haya ni ya umuhimu mkubwa kuliko kueleza vifungu kutoka Biblia, kwa sababu kazi kama hiyo haina maana ama thamani kubwa kwenu, na haiwezi kuwasaidia, au kuwabadilisha. Ninanuia kufanya kazi mpya sio kwa ajili ya kutimiza kifungu chochote kutoka Biblia. Ikiwa Mungu alikuja duniani tu kutimiza maneno ya manabii wa Biblia, basi ni nani aliye mkuu, Mungu wa mwili ama hao manabii wa zamani. Na hata hivyo, hao manabii ni wasimamizi wa Mungu, ama Mungu ni msimamizi wa manabii? Unaweza kueleza haya maneno jinsi gani?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Majina na Utambulisho

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 165)

Kila hatua ya kazi ya Mungu hufuata mkondo mmoja na sawa, na hivyo katika mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita, kila hatua imefuatwa kwa karibu na ifuatayo, kutoka msingi wa dunia hadi leo. Kama hakungekuwa na mtu wa kupisha njia, hakungekuwa na mtu wa kuja baadaye; Kwani kuna wale wanaokuja baadaye, kuna wale wanaopisha njia. Kwa njia hii kazi imepitishwa chini, hatua kwa hatua. Hatua moja inafuata ingine, na bila mtu wa kufungua njia, haitawezekana kuanza kazi, na Mungu angekosa namna ya kupeleka kazi Yake mbele. Hakuna hatua inayopingana na nyingine, na kila hatua inafuata nyingine katika mlolongo kuunda mkondo; hii yote inafanywa na Roho Yule Yule. Lakini bila kujali iwapo mtu atafungua njia ama kuendeleza kazi ya mwingine, hii haiamui utambulisho wake. Hii si sawa? Yohana aliifungua njia, na Yesu akaendeleza kazi yake, hivyo hii inathibitisha kwamba utambulisho wa Yesu ni chini kuliko wa Yohana? Yehova alifanya kazi Yake kabla Yesu, hivyo unaweza kusema kuwa Yehova ni mkubwa kumliko Yesu? Iwapo waliopasha njia ama kuendeleza kazi za wengine sio muhimu; kilicho muhimu ni kiini cha kazi zao, na utambulisho unaowakilishwa. Hii si sawa? Kwa vile Yesu alinuia kufanya kazi miongoni mwa wanadamu, ilimbidi Awainue wale ambao wangefanya kazi ya kupasha njia. Yohana alipoanza tu kuhubiri, alisema, “Itayarisheni ninyi njia ya Bwana, yafanyeni mapito Yake kuwa nyoofu.” “Ninyi tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni uko karibu.” Aliongea hivi tangu mwanzoni, na mbona aliweza kuyasema maneno haya? Kwa suala la utaratibu ambao maneno haya yalisemwa, ni Yohana aliyezungumzia kwanza injili ya ufalme wa mbinguni, na Yesu aliyezungumza baadaye. Kulingana na dhana za mwanadamu, ni Yohana aliyeifungua njia mpya, na bila shaka Yohana alikuwa mkubwa kumliko Yesu. Lakini Yohana hakusema yeye ni Kristo, na Mungu hakumshuhudia kama Mwana mpendwa wa Mungu, lakini Alimtumia tu kufungua na kuandaa njia ya Bwana. Alimpisha Yesu njia, lakini hangefanya kazi kwa niaba ya Yesu. Kazi zote za mwanadamu pia zilidumishwa na Roho Mtakatifu.

Katika enzi ya Agano la Kale, ni Yehova aliyeongoza njia, na kazi ya Yehova iliwakilisha enzi nzima ya Agano la Kale, na kazi zote zilizofanywa Israeli. Musa tu alizingatia hizi kazi duniani, na kazi zake zinachukuliwa kuwa ushirikiano uliotolewa na mwanadamu. Wakati huo, Yehova ndiye aliyezungumza, na Akimwita Musa, na Alimwinua Musa miongoni mwa watu wa Israeli, na kumfanya awaongoze nyikani na kuendelea hadi Kanaani. Hii haikuwa kazi ya Musa mwenyewe, lakini hiyo iliyoagizwa kibinafsi na Yehova, na hivyo Musa hawezi kuitwa Mungu. Musa pia aliiweka chini sheria, lakini sheria hii iliamrishwa kibinafsi na Yehova. Ni kwamba tu alifanya Musa kuitaja. Yesu pia alitengeneza amri, na kuondoa sheria ya Agano la Kale na kuweka amri ya enzi jipya. Mbona Yesu ni Mungu Mwenyewe? Kwa sababu haya si mambo sawa. Wakati huo, kazi aliyoifanya Musa haikuwakilisha enzi, wala haikufungua njia mpya; alielekezwa mbele na Yehova, na alikuwa tu anatumiwa na Mungu, Yesu alipokuja, Yohana alikuwa amefanya hatua ya kazi ya kupisha njia, na alikuwa ashaanza kueneza injili ya ufalme wa mbinguni (Roho Mtakatifu alikuwa ameanza hii). Yesu alipokuja, Alifanya moja kwa moja kazi Yake Mwenyewe, lakini kulikuwa na tofauti kubwa kati ya kazi Yake na kazi ya Musa. Isaya pia alizungumzia unabii mwingi, lakini mbona yeye hakuwa Mungu Mwenyewe? Yesu hakuzungumzia unabii mwingi lakini mbona Alikuwa Mungu Mwenyewe? Hakuna aliyethubutu kusema kwamba kazi zote za Yesu wakati huo zilitoka kwa Roho Mtakatifu, wala hawathubutu kusema zote zilitoka kwa matakwa ya mwanadamu, ama kwamba zilikuwa kabisa kazi za Mungu Mwenyewe. Mwanadamu hakuwa na njia yoyote ya kuchambua mambo haya. Inaweza kusemwa kwamba Isaya alifanya kazi kama hiyo, na kuzungumzia unabii huo, na yote yalitoka kwa Roho Mtakatifu; hayakutoka moja kwa moja kwa Isaya mwenyewe, lakini yalikuwa ufunuo kutoka kwa Yehova. Yesu hakufanya kazi nyingi sana, na Hakusema maneno mengi sana, wala Hakuzungumzia unabii mwingi. Kwa mwanadamu, mahubiri Yake hayakuonekana hasa ya kupandishwa cheo, lakini alikuwa Mungu Mwenyewe, na mwanadamu hawezi kueleza haya. Hakuna aliyewahi kumwamini Yohana, ama Isaya, ama Daudi, wala hakuna aliyewahi kuwaita Mungu, ama Daudi Mungu ama Yohana Mungu, hakuna aliyewahi kuzungumza hivi, na ni Yesu tu aliyewahi kuitwa Kristo. Uainishaji huu umefanywa kulingana na ushahidi wa Mungu, kazi Aliyoifanya, na huduma Aliyoifanya. Kuhusu watu wakuu wa Biblia—Ibrahimu, Daudi, Yoshua, Danieli, Isaya, Yohana na Yesu—kupitia kazi waliyoifanya, unaweza kusema ni nani aliye Mungu Mwenyewe, na ni watu wapi walio manabii, na ni wapi walio mitume. Ni nani aliyetumiwa na Mungu, na nani aliyekuwa Mungu Mwenyewe, inatofautishwa na kuamuliwa na asili na aina za kazi walizozifanya. Iwapo huwezi kusema tofauti, basi hii inadhihirisha kwamba hujui maana ya kumwamini Mungu. Yesu ni Mungu kwa sababu Alizungumza maneno mengi, na kufanya kazi nyingi hasa maonyesho Yake ya miujiza nyingi. Vivyo hivyo, Yohana, pia alifanya kazi nyingi, na kuzungumza maneno mengi, Musa pia; mbona hawakuitwa Mungu? Adamu aliumbwa moja kwa moja na Mungu; mbona hakuitwa Mungu, badala tu ya kuitwa kiumbe? Mtu akikwambia, “Leo, Mungu amefanya kazi nyingi sana, na kuzungumza maneno mengi; Yeye ni Mungu Mwenyewe. Basi, vile Musa alivyozungumza maneno mengi, lazima yeye pia ni Mungu Mwenyewe!” inapaswa uwarudishie swali, “Wakati huo, mbona Mungu alimshuhudia Yesu, na sio Yohana, kama Mungu Mwenyewe? Je, Yohana hakumtangulia Yesu? Ni ipi iliyokuwa kubwa, kazi ya Yohana ama Yesu? Kwa mwanadamu, kazi ya Yohana inakaa mkubwa kuliko ya Yesu, lakini mbona Roho Mtakatifu alimshuhudia Yesu, na sio Yohana?” Hiki kitu kimoja kinafanyika leo! Mwanzoni, Musa alipowaongoza watu wa Israeli, Yehova alimwongelesha kutoka miongoni mwa mawingu. Musa hakuzungumza moja kwa moja lakini badala yake aliongozwa moja kwa moja na Yehova. Hii ilikuwa kazi ya Israeli ya Agano la Kale. Ndani ya Musa hamkuwa na Roho, ama nafsi ya Mungu. Hangeweza kufanya kazi hiyo, na hivyo kuna tofauti kubwa kati ya aliyoifanya na Yesu. Na hiyo ni kwa sababu kazi walizozifanya zilikuwa tofauti! Iwapo mtu anatumiwa na Mungu, ama ni nabii, mtume, ama Mungu Mwenyewe, unaweza kubainishwa na asili ya kazi yake, na hii itakomesha mashaka yenu, Kwa Biblia, imeandikwa kwamba Kondoo peke yake ndiye anayeweza kuivunja mihuri saba. Kupitia zama zote kumekuwa na wachambuzi wengi wa maandiko miongoni mwa watu wakuu, na hivyo unaweza kusema kwamba wote ni Kondoo? Unaweza kusema kwamba maelezo yao yote yalitoka kwa Mungu? Walikuwa tu wachambuzi; hawana utambulisho wa Kondoo. Wanastahilije kuivunja mihuri saba? Ni ukweli kwamba “Kondoo peke yake anaweza kuivunja mihuri saba,” Lakini Hakuji tu kuivunja mihuri saba; hakuna umuhimu wa kazi hii, inafanywa kwa bahati. Yeye yu wazi kabisa kuhusu kazi Yake Mwenyewe; ni muhimu Kwake kutumia muda mwingi kutafsiri maandiko? Ni lazima “Enzi ya Mwanakondoo Akitafsiri Maandiko” iongezwe kwa kazi ya miaka elfu sita? Anakuja kufanya kazi mpya, lakini pia Anatoa ufunuo kadhaa kuhusu kazi za nyakati za zamani, kufanya watu waelewe ukweli wa kazi ya miaka elfu sita. Hakuna haja ya kueleza vifungo vingi kutoka Biblia; kazi ya leo ndiyo iliyo kuu, hiyo ni muhimu. Unapaswa kujua kwamba Mungu haji hasa kuivunja muhiri saba, ila kufanya kazi ya wokovu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Majina na Utambulisho

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 166)

Katika Enzi ya Neema, Yohana alimwandalia Yesu njia. Hangeweza kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe ila alitimiza tu kazi ya mwanadamu. Ingawa Yohana alikuwa mtangulizi wa Bwana; hangeweza kumwakilisha Mungu; alikuwa tu binadamu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu. Kufuatia ubatizo wa Yesu, “Roho Mtakatifu alimshukia Yeye kwa mfano wa njiwa.” Kisha Akaanza kazi Yake, hivyo, Alianza kufanya huduma ya Kristo. Hiyo ndiyo maana Alichukua utambulisho wa Mungu, kwa sababu Alitoka Kwa Mungu. Haijalishi jinsi imani Yake ilivyokuwa kabla ya hii—labda wakati mwingine ilikuwa dhaifu, au wakati mwingine ilikuwa na nguvu—hayo ndiyo yalikuwa maisha Yake ya kawaida ya binadamu kabla Afanye huduma Yake. Baada ya kubatizwa (kuteuliwa), mara moja Alikuwa na nguvu na utukufu wa Mungu pamoja Naye, na hivyo Akaanza Kufanya huduma Yake. Angetenda ishara na maajabu, Atende miujiza, Alikuwa na nguvu na mamlaka, kwani Alifanya kazi kwa niaba ya Mungu Mwenyewe; Alifanya kazi ya Roho badala Yake na kuonyesha sauti ya Roho Mtakatifu; kwa hivyo Alikuwa Mungu Mwenyewe. Hili halina pingamizi. Yohana alitumiwa na Roho Mtakatifu. Hangemwakilisha Mungu, na hakungekuwa na uwezekano wa yeye kumwakilisha Mungu. Kama angetaka kufanya hivyo, Roho Mtakatifu hangelikubali, kwani hangeweza kufanya kazi ambayo Mungu Mwenyewe alinuia kukamilisha. Labda kulikuwa na mengi ndani yake yaliyokuwa ya mapenzi ya mwanadamu, ama kitu kilichokuwa cha mwacha maadili; hakuna hali yoyote ambapo angemwakilisha Mungu moja kwa moja. Makosa Yake na mambo yasiyo sahihi yalimwakilisha yeye pekee, lakini kazi Yake ilikuwa uwakilishi wa Roho Mtakatifu. Ilhali, huwezi kusema kuwa yeye mzima alimwakilisha Mungu. Je upotovu na kuwa kwake na makosa kungemwakilisha Mungu pia? Kuwa na makosa katika kumwakilisha mwanadamu ni kawaida, lakini kama alikuwa na upotovu katika kumwakilisha Mungu, basi si hiyo ingekuwa kutomheshimu Mungu? Je hilo halingekuwa kufuru dhidi ya Roho Mtakatifu? Roho Mtakatifu hawezi kumruhusu mwanadamu asimame mahali pa Mungu anavyotaka, hata kama anasifiwa na wengine. Kama yeye si Mungu, basi hataweza kubaki akiwa amesimama mwishowe. Roho Mtakatifu hamkubali mwanadamu amwakilishe Mungu vile mwanadamu atakavyo! Kwa mfano, Roho Mtakatifu alimshuhudia Yohana na pia kumtambulisha kuwa mmoja wa wale watakaomwandalia Yesu njia, lakini kazi iliyofanywa ndani Yake na Roho Mtakatifu ilikuwa imepimwa vizuri. Kilichotakiwa kwa Yohana ilikuwa awe wa kutayarisha njia ya Yesu tu, kumtayarishia Yesu njia. Hiyo ni kusema, Roho Mtakatifu Aliiunga mkono kazi yake katika kutengeneza njia na kumruhusu afanye kazi ya aina hiyo pekee, hakuna mwingine. Yohana alimwakilisha Eliya, na alimwakilisha nabii aliyetengeneza njia. Hili liliungwa mkono na Roho Mtakatifu; bora kazi yake iwe kutengeneza njia, Roho Mtakatifu aliiunga mkono. Hata hivyo, kama angeweka madai kwamba yeye ni Mungu Mwenyewe na amekuja kumaliza kazi ya ukombozi, Roho Mtakatifu lazima amwadhibu. Haijalishi ukuu wa kazi ya Yohana, na ingawa iliungwa mkono na Roho Mtakatifu, kazi Yake ilibaki katika mipaka. Ni ukweli hakika kuwa kazi yake iliungwa mkono na Roho Mtakatifu, lakini nguvu aliyopewa katika wakati huo iliwekewa mipaka tu katika kutengeneza njia. Hangeweza, hata kidogo, kufanya kazi nyingine, kwani alikuwa tu Yohana aliyetengeneza njia, ila si Yesu. Kwa hivyo ushuhuda wa Roho Mtakatifu ni muhimu, lakini kazi ambayo mwanadamu anaruhusiwa kufanya na Roho Mtakatifu ni muhimu zaidi. Je, Yohana hakushuhudiwa sana? Kazi yake haikuwa kuu pia? Lakini kazi aliyofanya haingeshinda ile ya Yesu, kwani alikuwa mwanadamu tu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu na hangeweza kumwakilisha Mungu moja kwa moja, na kwa hiyo kazi aliyofanya ilikuwa yenye mipaka. Baada ya yeye kuimaliza kazi ya kuandaa njia, Roho Mtakatifu hakuthibitisha ushuhuda wake tena, hakuna kazi mpya iliyomfuata yeye tena, na aliondoka kazi ya Mungu Mwenyewe ilipoanza.

Kuna wengine ambao wamepagawa na roho wachafu na wanalia kwa kusisitiza wakisema, “Mimi ni Mungu!” Lakini mwishowe, hufichuliwa, kwani wanafanya kazi kwa niaba ya kiumbe asiyefaa. Wanawakilisha Shetani na Roho Mtakatifu hajali kuwahusu hata kidogo. Hata ujiinue vipi, ama kwa nguvu kivipi, wewe bado ni kiumbe aliyeumbwa na wewe unamilikiwa na Shetani. Mimi sipigi mayowe Nikisema, “Mimi ni Mungu, Mimi ni Mwana Mpendwa wa Mungu!” Lakini kazi Nifanyayo ni ya Mungu. Kuna haja Nipige mayowe? Hakuna haja ya kujiinua. Mungu hufanya kazi Yake Mwenyewe na hahitaji mwanadamu kumpa ruhusa ama cheo kubwa, na kazi Yake inatosha kuwakilisha utambulisho Wake na cheo. Kabla ya ubatizo Wake, si Yesu alikuwa Mungu Mwenyewe? Je, Yeye hakuwa mwili wa Mungu? Hakika haiwezi kusemekana kuwa Alikuwa Mwana wa pekee wa Mungu baada ya kushuhudiwa? Je, hakukuwa na mwanadamu jina lake Yesu kitambo kabla Aanze kazi Yake? Huwezi kuleta njia mpya ama kumwakilisha Roho. Huwezi kueleza kazi ya Roho ama maneno Anenayo. Huwezi kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe ama ile ya Roho. Huwezi kuelezea hekima, ajabu na mambo ya Mungu yasiyoeleweka, ama tabia yote ambayo Mungu humwadibu mwanadamu kupitia kwayo. Kwa hivyo madai yako ya kila mara ya kusema kuwa wewe ni Mungu hayajalishi; unalo tu jina lakini huna dutu. Mungu Mwenyewe Amekuja, lakini hakuna anayemtambua, ilhali Anaendelea na kazi Yake na Anafanya hivyo kwa uwakilishi wa Roho. Haijalishi unamwita mwanadamu ama Mungu, Bwana ama Kristo, ama umwite dada, yote ni sawa. Lakini kazi Afanyayo ni ile ya Roho na Anawakilisha kazi ya Mungu Mwenyewe. Hajali ni jina gani mwanadamu anamwita. Je, jina hilo linaweza kuamua kazi Yake? Bila kujali unachomwita, kutoka kwa mtazamo wa Mungu, Yeye ni kupata mwili kwa Roho wa Mungu; Anawakilisha Roho na amekubaliwa na Yeye. Huwezi kutengeneza njia ya enzi mpya, na huwezi kuhitimisha enzi nzee na huwezi kukaribisha enzi mpya ama kufanya kazi mpya. Kwa hivyo, huwezi kuitwa Mungu!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (1)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 167)

Hata mwanadamu anayetumiwa na Roho Mtakatifu hawezi kumwakilisha Mungu Mwenyewe. Na mwanadamu huyu hawezi tu kumwakilisha Mungu bali pia kazi yake haiwezi kumwakilisha Mungu moja kwa moja. Hivyo ni kusema uzoefu wa mwanadamu hauwezi kuwekwa moja kwa moja katika usimamizi wa Mungu, na hauwezi kuwakilisha usimamizi wa Mungu. Kazi yote ambayo Mungu Mwenyewe hufanya ni kazi Anayolenga Kufanya katika mpango Wake wa usimamizi na inahusiana na usimamizi mkuu. Kazi ifanywayo na mwanadamu (mwanadamu anayetumiwa na Roho Mtakatifu) hukidhi uzoefu wake binafsi. Anapata njia mpya ya uzoefu mbali na ile iliyotembelewa na wale waliomtangulia na anawaongoza ndugu zake chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Kinachotolewa na watu hawa ni uzoefu wao ama maandishi ya kiroho ya watu wa kiroho. Ingawa wanatumiwa na Roho Mtakatifu, kazi ya watu kama hao haina uhusiano na kazi ya usimamizi mkuu katika mpango wa miaka elfu sita. Wamesimamishwa na Roho Mtakatifu katika wakati tofauti kuongoza watu katika mkondo wa Roho Mtakatifu hadi wakamilishe kazi yao ama maisha yao yafike mwisho. Kazi wanayofanya ni kutayarisha njia ifaayo kwa ajili ya Mungu Mwenyewe ama kuendeleza kitu kimoja kwa usimamizi wa Mungu Mwenyewe katika dunia. Watu hao hawawezi kufanya kazi kuu katika usimamizi Wake, na hawawezi kufungua njia mpya, ama kumaliza kazi yote ya Mungu kutoka enzi ya kitambo. Kwa hivyo, kazi wafanyayo inawakilisha kiumbe aliyeumbwa pekee akifanya kazi Yake na hawezi kuwakilisha Mungu Mwenyewe Akifanya huduma Yake. Hii ni kwa sababu kazi wanayofanya haifanani na ile inayofanywa na Mungu Mwenyewe. Kazi ya kukaribisha enzi mpya haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba ya Mungu. Haiwezi kufanywa na mwingine ila Mungu Mwenyewe. Kazi yote inayofanywa na mwanadamu ni kufanya wajibu wake kama mmoja wa viumbe na inafanywa akiguswa au kupewa nuru na Roho Mtakatifu. Uongozi ambao watu hao hupeana ni jinsi ya kuzoea katika kila siku ya maisha ya mwanadamu na jinsi mwanadamu anapaswa kutenda kwa maelewano na mapenzi ya Mungu. Kazi ya mwanadamu haihusishi usimamizi wa Mungu ama kuwakilisha kazi ya Roho. Kama mfano, kazi ya Witness Lee na Watchman Nee ilikuwa ni kuongoza njia. Njia iwe mpya au nzee, kazi ilifanywa kwa misingi ya kanuni ya kutozidi Biblia. Haijalishi kama makanisa ya mitaa yalirejeshwa yalivyokuwa awali au yalijengwa, kazi yao ilikuwa ni kuanzisha makanisa. Kazi waliyofanya iliendeleza kazi ambayo Yesu Kristo na mitume Wake walikuwa hawajamaliza au kuendeleza zaidi kwenye Enzi ya Neema. Kile walichofanya katika kazi yao kilikuwa ni kurejesha kile ambacho Yesu Kristo Alikuwa Ameomba katika kazi Yake ya vizazi vitakavyokuja baada Yake Yeye, kama vile kuhakikisha kwamba vichwa vyao vimefunikwa, ubatizo, umegaji mkate, au unywaji wa mvinyo. Inaweza kusemekana kwamba kazi yao ilikuwa kubakia tu kwenye Biblia na kutafuta njia zinazotokana tu na Biblia. Hawakupiga hatua yoyote mpya kamwe. Hivyo basi, mtu anaweza kuona tu ugunduzi wa njia mpya ndani ya Biblia, pamoja na mazoea bora zaidi na yenye uhalisia zaidi. Lakini mtu hawezi kupata katika kazi yao mapenzi ya sasa ya Mungu, isitoshe hawezi kupata kazi mpya ambayo Mungu Atafanya kwenye siku za mwisho. Hii ni kwa sababu njia ambayo walitembelea ilikuwa bado ile nzee; hakukuwa na maendeleo yoyote na kitu chochote kipya. Waliendelea kuufuata ukweli wa “kule kusulubishwa kwa Yesu,” mazoea ya “kuwaomba watu kutubu na kukiri dhambi zao,” msemo kwamba “yule atakayevumilia hata mwisho ataokoka,” na msemo kwamba “mwanamume ndiye kichwa cha mwanamke, na mwanamke lazima amtii mume wake.” Aidha, waliendeleza dhana ya kitamaduni kwamba “akina dada hawawezi kuhubiri, na wanaweza tu kutii.” Ikiwa njia kama hiyo ya uongozi ingeendelea, basi Roho Mtakatifu asingewahi kuweza kutekeleza kazi mpya, kuwaweka binadamu huru kutokana na mafundisho, au kuwaongoza binadamu kwenye himaya ya uhuru na urembo. Hivyo basi, hatua hii ya kazi ya mabadiliko ya enzi lazima ifanywe na kuzungumzwa na Mungu Mwenyewe, la sivyo hakuna mwanadamu anayeweza kufanya hivyo badala Yake. Mpaka hapa, kazi yote ya Roho Mtakatifu iliyo nje ya mfululizo huu imesimama, na wale waliotumiwa na Roho Mtakatifu wamepoteza mwelekeo wao. Kwa hivyo, kwa sababu kazi ya wanadamu wanaotumiwa na Roho Mtakatifu si sawa na kazi ifanywayo na Mungu Mwenyewe, utambulisho wao na wanayefanya kazi kwa niaba yake ni tofauti. Hii ni kwa sababu kazi ambayo Roho Mtakatifu Analenga Kufanya ni tofauti, na hapo kutoa utambulisho tofauti na hadhi kwa wale wote wafanyao kazi. Wanadamu wanaotumiwa na Roho Mtakatifu wanaweza kufanya kazi mpya na wanaweza kutoa kazi iliyofanywa katika enzi iliyopita, lakini kazi yao haiwezi kueleza tabia na mapenzi ya Mungu kwa enzi mpya. Wanafanya kazi ili kuondoa kazi ya enzi iliyopita tu, sio kufanya kazi mpya kuwakilisha moja kwa moja tabia ya Mungu Mwenyewe. Hivyo, haijalishi matendo mangapi yaliyopitwa na wakati wanakomesha ama matendo mapya wanaanzisha, bado wanawakilisha mwanadamu na viumbe vilivyoumbwa. Mungu Mwenyewe Akifanya kazi, hata hivyo, Hatangazi wazi kukomeshwa kwa matendo ya enzi ya zamani au kutangaza moja kwa moja kuanzishwa kwa enzi mpya. Yeye hufanya kazi Yake moja kwa moja na kwa njia ya moja kwa moja. Yeye hufanya kazi Anayolenga kufanya moja kwa moja; hivyo, yeye hueleza moja kwa moja kazi Aliyoleta, Anafanya kazi Yake moja kwa moja Alivyolenga hapo awali, Akieleza uwepo Wake na tabia Yake. Mwanadamu anavyoona, tabia Yake na kazi Yake pia hazifanani na zile ya kitambo. Hata hivyo, kutoka kwa mtazamo wa Mungu Mwenyewe, huku ni kuendelea na ujenzi zaidi wa kazi Yake. Mungu Mwenyewe Akifanya kazi, Anaeleza neno Lake na Analeta kazi mpya moja kwa moja. Tofauti ni, mwanadamu akifanya kazi, ni kwa ukombozi na kusoma, ama ni kwa maendeleo ya maarifa na mpangilio wa mazoezi iliyojengwa juu ya msingi wa kazi za wengine. Hiyo ni kusema, umuhimu wa kazi inayofanywa na mwanadamu ni ya kuweka mkataba na “kutembea njia za kitambo kwa vitu mpya.” Hii inamanisha kuwa hata njia ambayo inatembelewa na watu wanaotumiwa na Roho Mtakatifu imejengwa juu ya yale yalifunguliwa na Mungu Mwenyewe. Kwa hivyo mwanadamu ni baada ya yote mwanadamu, na Mungu ni Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (1)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 168)

Yohana alizaliwa kwa ahadi, kama vile Isaka alivyozaliwa kwa Abrahamu. Alimwandalia Yesu njia na alifanya kazi nyingi, lakini hakuwa Mungu. Badala yake, anafikiriwa kuwa ni nabii kwa sababu alimwandalia tu Yesu njia. Kazi yake ilikuwa kuu pia, na ni baada ya yeye kuandaa njia tu ndipo Yesu akaanza kazi Yake kwa urasimu. Kimsingi, yeye alimfanyia tu Yesu kazi, na kazi yake ilikuwa katika huduma ya kazi ya Yesu. Baada ya yeye kuiandaa njia, Yesu akaanza kazi Yake, kazi iliyokuwa mpya zaidi, dhahiri zaidi, na katika utondoti mkubwa zaidi. Yohana alifanya tu kazi ya mwanzo; nyingi ya kazi mpya ilifanywa na Yesu. Yohana alifanya kazi mpya pia, lakini sio yeye aliyeianzisha enzi mpya. Yohana alizaliwa kwa ahadi, na jina lake kupewa na malaika. Katika wakati huo wengine walitaka kumpa jina la baba yake Zakaria, lakini mama yake alinena akisema, “Mtoto huyu hawezi kuitwa kwa jina hilo. Anapaswa kuitwa Yohana.” Haya yote yalielekezwa na Roho Mtakatifu. Jina la Yesu pia lilikuwa limeelekezwa na Roho Mtakatifu, na Alizaliwa wa Roho Mtakatifu, na kwa ahadi ya Roho Mtakatifu. Yesu Alikuwa Mungu, Kristo, na Mwana wa mtu. Kazi ya Yohana ilikuwa kuu pia, lakini mbona hakuitwa Mungu? Ni nini tofauti kati ya kazi iliyofanywa na Yesu na ile iliyofanywa na Yohana? Je, sababu pekee ni kwa kuwa Yohana ndiye aliyetengeneza njia ya Yesu? Au ni kwa sababu ilikuwa imepangwa na Mungu? Ingawa Yohana alisema kuwa, “Ninyi tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni uko karibu,” na kuhubiri pia injili ya ufalme wa mbinguni, kazi yake haikuwa yenye kina na ilijumuisha tu mwanzo. Kinyume, Yesu Alikaribisha enzi mpya na kuikamilisha enzi ya kitambo, lakini pia Alitimiza sheria ya Agano la Kale pia. Kazi Aliyofanya ni kubwa kuliko ile ya Yohana, na Alikuja kuwakomboa wanadamu wote—Alifanya hatua hii ya kazi. Yohana alitayarisha tu njia. Ingawa kazi yake ilikuwa kubwa, maneno yake mengi, na wale wafuasi waliomfuata wengi, kazi yake haikufanya kitu kingine ila kuletea mwanadamu mwanzo mpya. Mwanadamu hakupokea maisha, njia, ama ukweli wa ndani kutoka kwake, wala mwanadamu hakupata kupitia kwake ufahamu wa mapenzi ya Mungu. Yohana alikuwa nabii mkuu (Eliya) aliyeanza msingi mpya wa kazi ya Yesu na kutayarisha aliyeteuliwa; alikuwa mtangulizi wa Enzi ya Neema. Mambo kama haya hayawezi kutambuliwa kirahisi kwa kuchunguza kuonekana kwao kwa kawaida. Hasa sana, Yohana alifanya kazi kubwa; zaidi ya hayo, alizaliwa kutoka kwa ahadi ya Roho Mtakatifu, na kazi yake ikashikiliwa na Roho Mtakatifu. Hivyo, kutofautisha kati ya utambulisho wao inaweza kufanywa tu kupitia kazi yao, kwa kuwa sura tu ya nje ya mwanadamu haiwezi kuonyesha dutu yake, na mwanadamu hawezi kuhakikisha ushuhuda wa kweli wa Roho Mtakatifu. Kazi iliyofanywa na Yohana na ile iliyofanywa na Yesu si sawa na ilikuwa ya asili tofauti. Hii ndiyo inafaa kuonyesha kama yeye ni Mungu ama sio Mungu. Kazi ya Yesu ilikuwa kuanza, kuendelea, kuhitimisha na kukamilisha. Kila moja ya hatua hizi zilichukuliwa na Yesu, ilhali kazi ya Yohana haikuwa zaidi ya kuanzisha. Hapo mwanzo, Yesu Alieneza injili na kuhubiri njia ya kutubu, na Akaendelea mpaka kumbatiza mwanadamu, kuponya magonjwa, na kukemea mapepo. Mwishowe, Alimkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi na kukamilisha kazi Yake ya enzi yote. Alimhubiria mwanadamu na kueneza injili ya ufalme wa mbinguni katika sehemu zote. Hii ilikuwa sawa na Yohana, tofauti ikiwa kwamba Yesu Alikaribisha enzi mpya na kuleta Enzi ya Neema kwa mwanadamu. Kutoka kwa Mdomo Wake lilitoka neno jinsi mwanadamu anavyopaswa kutenda na njia mwanadamu anayopaswa kufuata Enzi ya Neema, na mwishowe, Akamaliza kazi ya Wokovu. Kazi kama hiyo haingeweza kutekelezwa na Yohana. Kwa hivyo, ni Yesu ndiye Aliyefanya Kazi Ya Mungu Mwenyewe, na ni Yeye ndiye Mungu Mwenyewe na Anamwakilisha Mungu moja kwa moja. Dhana za mwanadamu zinasema kwamba wale wote waliozaliwa kwa ahadi, waliozaliwa kwa Roho, waliothibitishwa na Roho Mtakatifu, na waliozifungua njia mpya ni Mungu. Kwa kadri ya fikira hii, Yohana pia angekuwa Mungu, na Musa, Abrahamu, na Daudi…, wao pia wangekuwa Mungu. Je, huu sio mzaha mkubwa?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (1)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 169)

Wengine wanaweza kushangaa, mbona enzi ikaribishwe na Mungu Mwenyewe? Kiumbe kilichoumbwa hakiwezi kusimama kwa niaba Yake? Nyote mnafahamu kuwa Mungu Anakuwa mwili hasa kwa ajili ya kuikaribisha enzi mpya, na, kwa hakika, Anapoikaribisha enzi mpya, Atakuwa Ameikamilisha enzi ya kale wakati uo huo. Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho; ni Yeye Mwenyewe ndiye Anayeanzisha kazi Yake na hivyo lazima iwe ni Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani na huishinda dunia. Kila wakati Yeye Mwenyewe Anapofanya kazi miongoni mwa mwanadamu, ni mwanzo wa mapigano mapya. Bila mwanzo wa kazi mpya, kwa kawaida hakutakuwa na kikomo kwa enzi ya kale. Na bila kikomo kwa enzi ya kale ina maana kuwa vita na Shetani havijafika mwisho. Ni kama tu Mungu Mwenyewe Anakuja miongoni mwa mwanadamu na kutenda kazi mpya ndipo mwanadamu atakapoweza kujitoa kutoka katika umiliki wa Shetani na kupata maisha na mwanzo mpya. Vinginevyo, mwanadamu ataishi milele katika wakati wa kale na milele kuishi katika ushawishi wa kale wa Shetani. Katika kila enzi inayoongozwa na Mungu, sehemu ya mwanadamu huwekwa huru, na hivyo, mwanadamu huendelea na kazi ya Mungu kuelekea enzi mpya. Ushindi wa Mungu ni ushindi kwa wale ambao humfuata Yeye. Kama binadamu wa kuumbwa angepewa usukani wa kutimiza enzi, basi iwe kutoka kwa mtazamo wa mwanadamu ama Shetani, hii ni kama kupinga au kusaliti Mungu, na hivyo kazi ya mwanadamu ingegeuka kuwa chombo kwa Shetani. Mwanadamu anapotii na kumfuata Mungu katika enzi iliyokaribishwa na Mungu Mwenyewe tu ndipo Shetani angeshawishiwa kabisa, kwani hiyo ndiyo kazi ya kiumbe aliyeumbwa. Kwa hivyo Nasema kuwa mnafaa tu kufuata na kutii, na hakuna kingine kitakachoulizwa kutoka kwenu. Hiyo ndiyo maana ya kusema kila mmoja kuendeleza kazi na kufanya kazi Yake. Mungu hufanya kazi Yake Mwenyewe na Yeye hahitaji mwanadamu kufanya kazi Yake kwa niaba Yake, na wala hajishughulishi katika kazi ya viumbe. Mwanadamu anafanya kazi yake na haingilii kati kazi ya Mungu, na huo ndio utii wa kweli na ushahidi kuwa Shetani ameshindwa. Baada ya Mungu Mwenyewe kukaribisha enzi mpya, Yeye Mwenyewe hafanyi kazi tena kati ya mwanadamu. Ni wakati huo tu ndipo mwanadamu anaingia rasmi katika enzi mpya kufanya kazi yake na kutekeleza misheni yake kama kiumbe aliyeumbwa. Hivyo ndivyo zilivyo kanuni za kazi zisizowezwa kukiukwa na yeyote. Kufanya kazi katika njia hii pekee ndio yenye busara. Kazi ya Mungu hufanywa na Mungu Mwenyewe. Ni Yeye ndiye Anayeweka kazi katika mwendo, na pia Yeye ndiye Anayemaliza. Ni Yeye ndiye hupanga kazi, na pia Yeye ndiye Anayesimamia, na zaidi ya hayo, ni Yeye ndiye Anayeleta kazi kuzaa matunda. Ni ilivyoandikwa katika Biblia, “Mimi ndiye Mwanzo na Mwisho: Mimi ndiye Mpanzi na Mvunaji.” Yote yanayohusiana na usimamizi wa kazi Yake yanafanywa na mkono Wake. Yeye ndiye Mtawala wa mpango wa miaka elfu sita; hakuna anayeweza kufanya kazi Yake kwa niaba Yake ama kuleta kazi Yake hadi mwisho, kwani Yeye ndiye Aliye katika uongozi wa yote. Kwa kuwa Aliumba dunia, Ataongoza ulimwengu mzima kuishi katika nuru Yake, na Atamaliza enzi yote na kuleta mpango Wake wote kwa mafanikio!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (1)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 170)

Tabia yote ya Mungu imefichuliwa katika mpango wote wa uongozi wa miaka elfu sita. Haikufichuliwa tu katika Enzi ya Neema, ni katika Enzi ya Sheria tu, na zaidi ya hayo, ni katika wakati huu wa siku za mwisho. Kazi iliyofanywa katika siku za mwisho inawakilisha hukumu, ghadhabu na kuadibu. Kazi ifanywayo katika siku za mwisho haiwezi kuwekwa mbadala wa kazi ya Enzi ya Sheria ama ile ya Enzi ya Neema. Ingawa, hatua zote tatu zinaungana kuwa kitu kimoja na yote ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja. Kawaida, utekelezaji wa kazi hizi umegawanyishwa katika enzi tofauti. Kazi iliyofanywa katika siku za mwisho inaleta kila kitu mpaka tamati; ile iliyofanywa katika Enzi ya Sheria ilikuwa ya mwanzo; na ile iliyofanywa katika Enzi ya Neema ilikuwa ya ukombozi. Na kuhusu maono ya kazi katika mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita, hakuna anayeweza kupata ufahamu au kuelewa. Maono kama hayo yamebaki kuwa mafumbo kila wakati. Katika siku za mwisho, kazi ya neno pekee inafanyika ili kuukaribisha Wakati wa Ufalme lakini haiwakilishi enzi zile zingine. Siku za mwisho sio zaidi ya siku za mwisho na sio zaidi ya Enzi ya Ufalme, na haziwakilishi Enzi ya Neema au Enzi ya Sheria. Siku za mwisho ni wakati ambapo kazi zote ndani ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita inafichuliwa kwenu. Mafumbo kama hayo hayawezi kufichuliwa na mwanadamu yeyote. Haijalishi mwanadamu ana maarifa makubwa ya Biblia vipi, yanabaki tu kuwa maneno na si kitu zaidi, kwani mwanadamu haelewi kiini cha Biblia. Mwanadamu anaposoma Biblia, anaweza kupokea baadhi ya ukweli, kueleza baadhi ya maneno ama kuchunguza vifungu maarufu na nukuu, lakini hatawahi kuwa na uwezo wa kunasua maana iliyoko katika maneno hayo, kwani yote aonayo mwanadamu ni maneno yaliyokufa pekee, sio matendo ya kazi ya Yehova na Yesu, na mwanadamu hawezi kufumbua mafumbo ya kazi ya aina hiyo. Kwa hivyo, fumbo la mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita ni fumbo kuu, iliyofichwa zaidi na isiyoshawishika kwa mwanadamu. Hakuna anayeweza kuelewa moja kwa moja mapenzi ya Mungu, ama, Mungu Mwenyewe aeleze na kumfichulia mwanadamu, vinginevyo, yatabaki kuwa mafumbo milele kwa mwanadamu na kubaki mafumbo yaliyofungwa milele. Usiwajali wale walio katika ulimwengu wa kidini; kama hamngeambiwa leo, pia nyinyi hamngeweza kuelewa. Kazi hii ya miaka elfu sita ni ya fumbo zaidi kuliko unabii wote wa manabii. Ni fumbo kuu zaidi tangu uumbaji, na hakuna nabii wa awali ambaye amewahi kuweza kulielewa, kwani fumbo hili hufumbuliwa tu katika enzi ya mwisho na kamwe halijawahi kufichuliwa hapo awali. Mkielewa fumbo hili na muweze kulipokea kwa ukamilifu, wale watu wote wa kidini watashindwa kwa fumbo hili. Hili pekee ndilo kuu zaidi ya maono, lile ambalo mwanadamu hutamani sana kulielewa lakini pia lile ambalo si wazi zaidi kwake. Mlipokuwa katika Enzi ya Neema, hamkujua kazi ambayo ilifanywa na Yesu wala ile ambayo ilifanywa na Yehova. Watu hawakuelewa chochote kuhusu kwa nini Yehova alitangaza sheria, kwa nini Aliwaambia watu wazitii sheria au kwa nini ilikuwa lazima kwa hekalu kujengwa, na sembuse watu kuelewa kwa nini Waisraeli waliongozwa kutoka Misri hadi jangwani na kisha hadi Kanaani. Ni mpaka siku hii ndipo mambo haya yamefichuliwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 171)

Hakuna mtu anayeweza kuishi kwa kujitegemea isipokuwa wale ambao wanapewa uelekeo na mwongozo maalumu na Roho Mtakatifu, kwani wanahitaji huduma na uchungaji wa wale wanaotumiwa na Mungu. Hivyo, katika kila enzi Mungu huwainua watu tofauti ambao hujishughulisha na kuchunga makanisa kwa ajili ya kazi Yake. Ambalo ni kusema, kazi ya Mungu lazima ifanywe kupitia wale ambao Huwaonyesha fadhili na kuwakubali; Roho Mtakatifu lazima atumie sehemu ndani yao inayostahili kutumiwa ili kufanya kazi, na wao hufanywa wa kufaa kutumiwa na Mungu kupitia kukamilishwa na Roho Mtakatifu. Kwa sababu uwezo wa mwanadamu wa kuelewa unapungukiwa sana, lazima afanyiwe uchungaji na wale wanaotumiwa na Mungu; ilikuwa vivyo hivyo na Mungu kumtumia Musa, ambaye kwake Alipata mengi yaliyostahili kwa matumizi wakati huo, na ambayo Aliyatumia kufanya kazi ya Mungu wakati wa hatua hiyo. Katika hatua hii, Mungu anamtumia mwanadamu huku Akitumia pia kwa manufaa Yake sehemu yake inayoweza kutumiwa na Roho Mtakatifu ili kufanya kazi, na Roho Mtakatifu humwongoza na wakati ule ule hukamilisha sehemu iliyobaki, isiyoweza kutumika.

Kazi inayotekelezwa na yule anayetumiwa na Mungu ni kwa ajili ya kushirikiana na kazi ya Kristo au Roho Mtakatifu. Mtu huyu anainuliwa na Mungu miongoni mwa wanadamu, yuko pale kuongoza wateule wote wa Mungu, na pia yeye anainuliwa na Mungu ili kufanya kazi ya ushirikiano wa mwanadamu. Na mtu kama huyu, ambaye anaweza kufanya kazi ya ushirikiano wa mwanadamu, matakwa mengi zaidi ya Mungu kwa mwanadamu na kazi ambayo Roho Mtakatifu lazima Afanye miongoni mwa wanadamu inaweza kutimizwa kupitia kwake. Njia nyingine ya kulisema ni hivi: Lengo la Mungu katika kumtumia mtu huyu ni ili wote wanaomfuata Mungu waweze kuelewa bora mapenzi ya Mungu, na waweze kufikia matakwa zaidi ya Mungu. Kwa vile watu hawawezi kuyaelewa maneno ya Mungu na mapenzi ya Mungu moja kwa moja, Mungu amemuinua mtu fulani ambaye anatumiwa kutekeleza kazi kama hiyo. Mtu huyu anayetumiwa na Mungu anaweza kuelezwa kama chombo ambacho Mungu hutumia kuwaongoza watu, kama “mfasiri” anayewasiliana kati ya Mungu na watu. Hivyo, mtu kama huyo hayuko kama yeyote kati ya wale wanaofanya kazi katika nyumba ya Mungu au ambao ni mitume Wake. Kama wao, anaweza kusemekana kuwa mtu anayemhudumia Mungu, lakini katika kiini cha kazi yake na usuli wa kutumiwa kwake na Mungu anatofautiana sana na wafanyakazi wengine na mitume. Kuhusu kiini cha kazi yake na usuli wa kutumiwa kwake, mwanadamu anayetumiwa na Mungu huinuliwa na Yeye, hutayarishwa na Mungu kwa kazi ya Mungu, na yeye hushirikiana katika kazi ya Mungu Mwenyewe. Hakuna mtu anayeweza kufanya kazi yake badala yake—huu ni ushirikiano wa mwanadamu ambao ni wa lazima pamoja na kazi takatifu. Kazi inayotekelezwa na wafanyakazi wengine au mitume, wakati ule ule, ni uchukuzi na utekelezaji tu wa hali nyingi za matayarisho ya makanisa wakati wa kila kipindi, ama sivyo kazi ya utoaji wa kawaida wa uzima ili kudumisha uzima wa kanisa. Wafanyakazi hawa na mitume hawateuliwi na Mungu, seuze kuweza kuitwa wale wanaotumiwa na Roho Mtakatifu. Wao huchaguliwa kutoka miongoni mwa makanisa na, baada ya kufunzwa na kukuzwa kwa kipindi cha wakati, wale wanaofaa hubaki, huku wale wasiofaa hurudishwa walikotoka. Kwa vile watu hawa huchaguliwa kutoka miongoni mwa makanisa, wengine huonyesha tabia yao halisi baada ya kuwa viongozi, na wengine hata hufanya mambo mengi mabaya na huishia kufutwa. Mtu anayetumiwa na Mungu, kwa upande mwingine, ni mtu ambaye ametayarishwa na Mungu, na aliye na ubora fulani wa tabia, na ana ubinadamu. Ametayarishwa na kukamilishwa mapema na Roho Mtakatifu, na anaongozwa kabisa na Roho Mtakatifu, na, inapofikia kazi yake hasa, yeye huongozwa na kuamriwa na Roho Mtakatifu—kutokana na hilo hakuna mkengeuko katika njia ya kuwaongoza wateule wa Mungu, kwani Mungu kwa hakika huwajibikia kazi Yake mwenyewe, na Mungu hufanya kazi Yake nyakati zote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Mungu Kumtumia Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 172)

Kazi katika mkondo wa Roho Mtakatifu, bila kujali ni kazi ya Mungu mwenyewe au ni kazi ya watu wanaotumiwa, ni kazi ya Roho Mtakatifu. Kiini cha Mungu Mwenyewe ni Roho, ambaye anaweza kuitwa Roho Mtakatifu au Roho mwenye nguvu mara saba. Kwa jumla, Wao ni Roho wa Mungu. Ni kwamba tu Roho wa Mungu anaitwa majina tofauti katika enzi tofauti tofauti. Lakini kiini Chao bado ni kimoja. Hivyo, kazi ya Mungu Mwenyewe ni kazi ya Roho Mtakatifu; kazi za Mungu mwenye mwili hazitofautiani na kazi za Roho Mtakatifu. Kazi ya wanadamu wanaotumiwa pia ni kazi ya Roho Mtakatifu. Ni kwamba tu kazi ya Mungu ni onyesho kamili la Roho Mtakatifu, ambalo ni ukweli kabisa, ilhali kazi ya watu wanaotumiwa inachanganyika na mambo mengi ya kibinadamu, na wala si uonyeshaji wa moja kwa moja wa Roho Mtakatifu, wala uonyeshaji kamili. Kazi ya Roho Mtakatifu ina mawanda mapana na wala haizuiliwi na hali yoyote ile. Kazi hiyo inatofautiana kwa watu tofauti tofauti, na kutoa viini tofauti tofauti vya kufanya kazi. Kazi pia inatofautiana katika enzi mbali mbali, kama pia ilivyo kazi tofauti katika nchi mbalimbali. Bila shaka, ingawa Roho Mtakatifu hufanya kazi katika njia nyingi tofauti tofauti na kulingana na kanuni nyingi, haijalishi kazi imefanyikaje au kwa watu wa aina gani, kiini ni tofauti daima, na kazi Anazofanya kwa watu tofauti zote zina kanuni na zote zinaweza kuwakilisha kiini cha mhusika anayefanyiwa kazi. Hii ni kwa sababu kazi ya Roho Mtakatifu ni mahususi kabisa kwa mapana yake na inapimika. Kazi inayofanywa katika mwili uliopatikana si sawa na kazi inayofanywa kwa watu, na kazi hii pia inatofautiana kulingana na ubora mbali mbali wa tabia za watu. Kazi inayofanywa katika mwili uliopatikana si sawa na kazi inayofanywa kwa watu, na katika mwili uliopatikana Hafanyi kazi ile ile kama aliyoifanya kwa watu. Kwa ufupi, haijalishi Anafanya kazi jinsi gani, kazi katika vitu mbalimbali haifanani, na kanuni ambazo Anazitumia kufanya kazi zinatofautiana kulingana na hali na asili ya watu mbalimbali. Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa watu tofauti tofauti kulingana na kiini chao cha asili na haweki mahitaji ambayo ni zaidi ya kiini chao cha asili, na wala Hafanyi kazi zaidi ya ubora halisi wa tabia yao. Kwa hivyo, kazi ya Roho Mtakatifu kwa mwanadamu inawaruhusu watu kuona kiini cha lengo la kazi hiyo. Kiini asili cha mwanadamu hakibadiliki; ubora halisi wa tabia ya mwanadamu ina mipaka. Kama Roho Mtakatifu anawatumia watu au anafanya kazi kwa watu kazi, kazi hiyo siku zote inafanywa kulingana na tabia za watu ili waweze kunufaika kutoka kwayo. Roho Mtakatifu anapofanya kazi kwa wanadamu wanaotumiwa, karama zao na tabia zao halisi zinatumiwa pia na wala haziachwi. Tabia zao halisi zinatumiwa zote kwa ajili ya kutoa huduma kwa kazi. Tunaweza kusema kuwa Anafanya kazi kwa kutumia sehemu zilizopo za wanadamu ili kupata matokeo yatendayo kazi. Kinyume chake, kazi inayofanyika katika mwili uliopatikana ni yenye kumwonyesha Roho moja kwa moja na wala haichanganywi na akili na mawazo ya mwanadamu, haifikiwi na karama za mwanadamu, uzoefu wa mwanadamu au hali ya ndani ya mwanadamu. Kazi nyingi mno ya Roho Mtakatifu yote inalenga kumnufaisha na kumwadilisha mwanadamu. Lakini baadhi ya watu wanaweza kukamilishwa wakati wengine hawana vigezo vya kuweza kukamilishwa, ambayo ni kusema, hawawezi kukamilishwa na ni vigumu sana kuokolewa, na ingawa wanaweza kuwa walishakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu, mwishowe wanaondolewa. Hii ni sawa na kusema kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni kuwaadilisha watu, hii haimaanishi kwamba wale wote waliokwisha kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu wanapaswa kukamilishwa kikamilifu, kwa sababu njia wanayoifuatilia watu wengi si njia ya kukamilishwa. Wana kazi moja tu ya Roho Mtakatifu, na wala si ushirikiano wa kibinafsi wa binadamu au njia sahihi za kibinadamu. Kwa njia hii, kazi ya Roho Mtakatifu kwa watu hawa inakuwa kazi katika huduma ya wale ambao wanakamilishwa. Kazi ya Roho Mtakatifu haiwezi kuonwa moja kwa moja na watu au kuguswa moja kwa moja na watu wenyewe. Inaweza kuonyeshwa tu kwa njia ya msaada wa watu wenye karama ya kufanya kazi, ikiwa na maana kwamba kazi ya Roho Mtakatifu inatolewa kwa wafuasi kwa njia ya onyemaonyesho wanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 173)

Kazi ya Roho Mtakatifu inakamilishwa na kukamilika kupitia watu wa aina nyingi na hali nyingi tofauti tofauti. Ingawa kazi ya Mungu mwenye mwili inaweza kuwakilisha kazi ya enzi zote, na inaweza kuwakilisha uingiaji wa watu katika enzi nzima, kazi kwa watu wengi bado inahitajika kufanywa na wanadamu wanaotumiwa na Roho Mtakatifu na sio na Mungu mwenye mwili. Kwa hivyo, kazi ya Mungu, au huduma ya Mungu mwenyewe, ni kazi ya Mungu mwenye mwili na haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kazi ya Roho Mtakatifu imekamilishwa kupitia watu wa aina mbalimbali na haiwezi kukamilishwa na mtu mahususi mmoja tu, au kufafanuliwa kikamilifu kupitia mtu mmoja mahususi. Wale ambao wanaongoza kanisa pia hawawezi kuiwakilisha kazi ya Roho Mtakatifu kikamilifu; wanaweza kufanya tu kazi fulani ya kuongoza. Kwa njia hii, kazi ya Roho Mtakatifu inaweza kugawanywa katika sehemu tatu: Kazi ya Mungu mwenyewe, kazi ya wanadamu wanaotumiwa, na kazi kwa wale wote walioko katika mkondo wa Roho Mtakatifu. Miongoni mwa hizo tatu, kazi ya Mungu ni kuongoza enzi nzima; kazi ya wanadamu wanaotumiwa ni kuwaongoza wafuasi wote wa Mungu kwa kutumwa au kupokea maagizo kwa ajili ya kazi ya Mungu mwenyewe; na wanadamu hawa ndio wanaoshirikiana na kazi ya Mungu; kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu kwa wale waliopo katika mkondo wake ni kudumisha kazi Yake yote, yaani, kudumisha usimamizi wote na kudumisha ushuhuda Wake, na wakati uo huo kuwakamilisha wale wanaoweza kukamilishwa. Sehemu hizi tatu ni kazi kamili ya Roho Mtakatifu, lakini bila kazi ya Mungu Mwenyewe, kazi yote ya usimamizi inaweza kutuama. Kazi ya Mungu Mwenyewe inahusisha kazi ya wanadamu wote, na pia inawakilisha kazi ya enzi nzima. Hii ni kusema kwamba, kazi ya Mungu mwenyewe inawakilisha harakati na mwelekeo wa kazi yote ya Roho Mtakatifu, ilhali kazi ya mitume inafuata kazi ya Mungu na wala haiongozi enzi, na wala haiwakilishi mitindo ya kazi ya Roho Mtakatifu katika enzi nzima. Huwa wanafanya tu kazi ambayo mwanadamu anapaswa kufanya, ambayo haihusishi kabisa kazi ya usimamizi. Kazi ya Mungu ni mradi ndani ya kazi ya usimamizi. Kazi ya mwanadamu ni wajibu tu wa wanadamu kuweza kutumika na wala haina uhusiano na kazi ya usimamizi. Kwa sababu ya utambulisho na uwakilishaji tofauti wa kazi hii, licha ya ukweli kwamba zote ni kazi za Roho Mtakatifu, kuna tofauti za wazi na bainifu kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu. Aidha, kiwango cha kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu kwa watu wenye tambulisho tofauti inatofautiana. Hizi ni kanuni na mawanda ya kazi ya Roho Mtakatifu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 174)

Kazi ya mwanadamu inawakilisha uzoefu wake na ubinadamu wake. Kile ambacho mwanadamu anatoa na kazi ambayo anafanya vinamwakilisha yeye. Kuona kwa mwanadamu, kufikiri kwa mwanadamu, mantiki ya mwanadamu na uwezo wake mkubwa wa kufikiri vyote vinajumuishwa katika kazi yake. Kimsingi, uzoefu wa mwanadamu, unaweza zaidi kuwakilisha kazi yake na kile ambacho mtu amekipitia kitakuwa ni sehemu ya kazi yake. Kazi ya mwanadamu inaweza kuonyesha uzoefu wake. Pale ambapo baadhi ya watu wanapitia hali ya kukaa tu bila kujishughulisha, sehemu kubwa ya ushirika wao inakuwa na vipengele vya uhasi. Kama uzoefu wao kwa kipindi cha muda ni mzuri na wanapita katika njia ya upande mzuri, kile wanachoshiriki kinatia moyo sana, na watu wanaweza kupokea mambo mazuri kutoka kwao. Mfanyakazi akiwa katika hali ya kukaa tu kwa kipindi cha muda, ushirika wake siku zote utakuwa na vipengele vya uhasi. Ushirika wa aina hii ni wa kuvunja moyo, na wengine watavunjika mioyo bila kujua kwa kufuata ushirika wa yule mfanyakazi. Hali ya wafuasi inabadilika kutegemea na hali ya kiongozi. Vile ambavyo mfanyakazi alivyo ndani, ndicho kile anachoonyesha, na kazi ya Roho Mtakatifu mara nyingi inabadilika kulingana na hali ya mwanadamu. Anafanya kazi kulingana na uzoefu wa mwanadamu na wala hamshurutishi mwanadamu bali anamsihi mwanadamu kulingana na hali yake ya kawaida ya uzoefu wake. Hii ni kusema kwamba ushirika wa mwanadamu unatofautiana na neno la Mungu. Kile ambacho mwanadamu hushiriki kinaeleza vile anavyotazama mambo na uzoefu wake, kinaonyesha kile wanachokiona na kupitia uzoefu kwa msingi wa kazi ya Mungu. Wajibu wao ni kutafuta, baada ya Mungu kufanya kazi au kuzungumza, kile wanachopaswa kufanya au kuingia kwacho, halafu kukiwasilisha kwa wafuasi. Hivyo, kazi ya mwanadamu inawakilisha kuingia au matendo yake. Bila shaka, kazi hiyo imechanganyika na masomo ya kibinadamu na uzoefu au mawazo ya kibinadamu. Haijalishi namna ambavyo Roho Mtakatifu anafanya kazi, ama Anavyomfanyia kazi mwanadamu au Mungu mwenye mwili, siku zote watenda kazi ndio wanaoonyesha vile walivyo. Ingawa ni Roho Mtakatifu ambaye hufanya kazi, kazi hiyo imejengwa katika msingi wa mwanadamu alivyo kiasili, kwa sababu Roho Mtakatifu hafanyi kazi pasipo msingi. Kwa maneno mengine, kazi haifanyiki pasipokuwa na kitu, lakini siku zote hufanyika kulingana na mazingira halisi na hali halisi. Ni kwa njia hii pekee ndiyo tabia ya mwanadamu inaweza kubadilishwa, kwamba mitazamo yake ya zamani na mawazo yake ya zamani yanaweza kubadilishwa. Kile ambacho mwanadamu huonyesha ni kile anachokiona, kupitia uzoefu na kukitafakari. Hata kama ni mafundisho au fikira, haya yote hufikiwa na fikira za mwanadamu. Bila kujali ukubwa wa kazi ya mwanadamu, haiwezi kuzidi mawanda ya uzoefu wa mwanadamu, kile ambacho mwanadamu huona, au kile ambacho mwanadamu anaweza kukitafakari au kuingia akilini mwake. Kile ambacho Mungu anaonyesha ndivyo hivyo Mungu Mwenyewe alivyo, na hii ni nje ya uwezo wa mwanadamu, yaani, nje ya uwezo wa kufikiri kwa mwanadamu. Anaonyesha kazi Yake ya kuwaongoza wanadamu wote, na hii haihusiani na undani wa uzoefu wa mwanadamu, badala yake inahusu usimamizi Wake. Mwanadamu anaonyesha uzoefu wake wakati Mungu anaonyesha nafsi Yake—nafsi hii ni tabia Yake ya asili na iko nje ya uwezo wa mwanadamu. Uzoefu wa mwanadamu ni kuona kwake na kupata maarifa kulingana na uonyeshaji wa Mungu wa nafsi Yake. Kuona kama huko na maarifa kama hayo yanaitwa asili ya mwanadamu. Yanaonyeshwa kwa msingi wa tabia asili ya mwanadamu na ubora wa tabia yake halisi; hivyo pia vinaitwa nafsi ya mwanadamu. Mwanadamu anaweza kushiriki kile anachokipitia na kukiona. Kile ambacho hajawahi kukipitia au kukiona au akili yake haiwezi kukifikia, yaani, vitu ambavyo havipo ndani yake, hawezi kuvishiriki. Ikiwa kile ambacho mwanadamu anakionyesha sio uzoefu wake, basi ni mawazo yake au mafundisho ya kidini. Kwa ufupi, hakuna ukweli wowote katika maneno yake. Kama hujawahi kukutana na maswala ya jamii, hutaweza kushiriki kwa uwazi kwenye mahusiano changamani katika jamii. Kama huna familia na watu wengine wanazungumza juu ya masuala ya familia, huwezi kuelewa kiasi kikubwa cha kile walichokuwa wakisema. Kwa hivyo, kile ambacho mwanadamu anakifanyia ushirika na kazi anayofanya vinawakilisha asili yake ya ndani. Ikiwa mtu anafanya ushirika kuhusu ufahamu wake wa kuadibu na hukumu, lakini huna uzoefu wake, usithubutu kukana maarifa yake, badala yake kuwa na uhakika wa anachokisema kwa asilimia mia moja. Hii ni kwa sababu kile anachokifanyia ushirika ni kitu ambacho hujawahi kupata uzoefu wake, kitu ambacho hujawahi kukifahamu, na akili yako haiwezi kukitafakari. Unaweza tu kujifunza kutoka kwa ufahamu wake njia za maisha yajayo yanayohusiana na kuadibu na hukumu. Lakini njia hii inaweza kufanya kazi tu kama ufahamu uliojikita katika fundisho na haiwezi kuchukua nafasi ya ufahamu wako, na zaidi sana uzoefu wako. Pengine unafikiri kwamba kile anachokisema ni sahihi, lakini unapokipitia, unagundua kwamba hakitekelezeki katika mambo mengi. Pengine unahisi kwamba maarifa fulani unayoyasikia hayatekelezeki kabisa; unakuwa na mtazamo kuhusu maarifa hayo kwa wakati fulani, na ingawa unayakubali, unafanya hivyo shingo upande. Lakini unapopata uzoefu, maarifa yanayokupa mtazamo ndiyo yanayoongoza matendo yako. Na kadiri unavyotenda, ndivyo unavyozidi kuelewa thamani halisi na maana ya maneno yake. Baada ya kuwa na uzoefu, sasa unaweza kuzungumza juu ya maarifa unayopaswa kuwa nayo kuhusu vitu ulivyovipitia. Aidha, unaweza pia kutofautisha kati ya wale ambao maarifa yao ni halisi na ya utendaji na wale ambao maarifa yao yamejikita katika mafundisho ya kidini na hayana thamani. Kwa hivyo, kama maarifa ambayo unayazungumzia yanapatana na ukweli kwa kiasi kikubwa yanategemea na iwapo una uzoefu wa vitendo. Pale palipo na ukweli katika uzoefu wako, maarifa yako yatakuwa yanatekelezeka na yenye thamani. Kupitia uzoefu wako, pia unaweza kupata utambuzi na umaizi, kukuza maarifa yako, na kuongeza hekima yako na akili ya kuzaliwa katika kujiongoza. Maarifa yanayozungumzwa na watu ambao hawana ukweli ni fundisho la kidini tu, bila kujali yana nguvu kiasi gani. Mtu wa aina hii anaweza kuwa mwenye akili sana yanapokuja masuala ya kimwili lakini hawezi kutofautisha yanapokuja masuala ya kiroho. Hii ni kwa sababu watu kama hao hawana uzoefu wowote katika masuala ya kiroho. Hawa ni watu ambao hawajapata nuru katika masuala ya kiroho na hawaelewi mambo ya kiroho. Haijalishi aina ya maarifa unayoonyesha, ilimradi ni asili yako, basi ni uzoefu wako binafsi, maarifa yako halisi. Kile ambacho watu wenye mafundisho tu huzungumzia, yaani, wale ambao hawana ukweli au uhalisi, huzungumzia yaweza kusemwa kuwa ni asili yao, kwa sababu mafundisho yao yamefikiwa kwa njia ya kutafakari sana na ni matokeo ya akili yao kutafakari kwa kina, lakini ni mafundisho tu, si kitu chochote zaidi ya fikira.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 175)

Uzoefu wa aina tofauti za watu unawakilisha vitu vilivyomo ndani yao. Wale wote ambao hawana uzoefu wa kiroho hawawezi kuzungumza juu ya maarifa ya ukweli, maarifa sahihi kuhusu aina mbalimbali za masuala ya kiroho. Kile ambacho mtu anakionyesha ndivyo alivyo ndani—hili ni hakika. Ikiwa mtu anatamani kuwa na maarifa ya masuala ya kiroho na ukweli, anapaswa kuwa na uzoefu halisi. Ikiwa huwezi kuzungumza wazi juu ya masuala ya kawaida yanayohusiana na maisha ya mwanadamu, basi utawezaje kuzungumzia masuala ya kiroho? Wale wanaoweza kuyaongoza makanisa, kuwaruzuku watu maisha, na kuwa mtume kwa watu, wanapaswa kuwa na uzoefu halisi, ufahamu sahihi wa masuala ya kiroho, kuelewa vyema na kuwa na uzoefu wa ukweli. Watu wa namna hiyo tu ndio wanaostahili kuwa watenda kazi au mitume wanaoyaongoza makanisa. Vinginevyo, wanaweza kutufuata tu kidogo na hawawezi kuongoza, sembuse kuwa mtume mwenye uwezo wa kuwapatia watu uhai. Hii ni kwa sababu kazi ya mitume siyo kukimbia au kupigana; ni kufanya kazi ya kutoa huduma ya maisha na kuwaongoza wengine katika kubadili tabia zao. Wale wanaofanya kazi hii wanaagizwa kubeba mzigo mkubwa, ambao si kitu ambacho kila mtu anaweza kufanya. Kazi ya aina hii inaweza tu kufanywa na wale ambao wana maisha ya uwepo, yaani, wale ambao wana uzoefu wa ukweli. Haiwezi kufanywa na kila mtu ambaye anaweza kukata tamaa, anaweza kukimbia au yupo tayari kutumia pesa; watu ambao hawana uzoefu wa ukweli, wale ambao hawajapogolewa au kuhukumiwa, hawawezi kufanya kazi ya aina hii. Watu ambao hawana uzoefu, yaani, watu wasio na ukweli, hawawezi kuona ukweli kwa uwazi kwa kuwa wao wenyewe hawako katika hali hii. Hivyo, mtu wa aina hii si kwamba hawezi tu kufanya kazi ya kuongoza bali atakuwa mlengwa wa kuondolewa ikiwa hatakuwa na ukweli kwa muda mrefu. Kuona unakokuzungumzia kunaweza kuthibitisha ugumu ulioupitia maishani, katika masuala ambayo kwayo umeadibiwa na katika mambo ambayo umehukumiwa kwayo. Hii pia ni kweli katika majaribu: Vitu ambavyo mtu anasafishwa kwavyo, vitu ambavyo kwavyo mtu ni mdhaifu, hivi ni vitu ambavyo mtu ana uzoefu kwavyo, vitu ambavyo mtu anaelewa njia zake. Kwa mfano, kama mtu amekatishwa tamaa katika ndoa, muda mwingi atakuwa anafanya ushirika, “Asante Mungu, msifu Mungu, ni lazima nitimize matakwa ya Mungu, na kuyatoa maisha yangu yote, kuikabidhi ndoa yangu kikamilifu katika mikono ya Mungu. Niko radhi kuyatoa maisha yangu yote kwa Mungu.” Vitu vyote ndani ya mwanadamu vinaweza kuonyesha kile alicho kupitia katika ushirika. Mwendo wa usemi wa mtu, kama anazungumza kwa sauti kubwa au kwa sauti ya chini, masuala kama hayo ambayo si masuala ya uzoefu hayawezi kuwakilisha kile alicho nacho na kile alicho. Yanaweza kueleza tu iwapo tabia yake ni nzuri au mbaya, au kama asili yake ni nzuri au mbaya lakini haiwezi kulinganishwa na kama ana uzoefu. Uwezo wa mtu kujionyesha anapozungumza, ama ujuzi au kasi ya kuzungumza, ni suala tu la utendaji na haliwezi kuchukua nafasi ya uzoefu wake. Unapozungumza juu ya uzoefu wako binafsi, unafanya ushirika wa kile ambacho unakipatia umuhimu na vitu vyote ndani yako. Usemi Wangu unawakilisha asili Yangu, lakini kile Ninachokisema kiko nje ya uwezo wa mwanadamu. Kile Nikisemacho sio kile ambacho mwanadamu anakipitia, na sio kitu ambacho mwanadamu anaweza kukiona, pia si kitu ambacho mwanadamu anaweza kukigusa, lakini ndicho Nilicho. Baadhi ya watu wanakiri tu kwamba kile Ninachokifanyia ushirika ndicho kile Nimekipitia, lakini hawatambui kwamba ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho. Ni kweli, kile Ninachokisema ndicho kile Nimekipitia. Ni Mimi Ndiye Niliyefanya kazi ya usimamizi kwa kipindi cha zaidi ya miaka elfu sita. Nimepitia kila kitu kuanzia mwanzo wa uumbaji wa mwanadamu hadi leo; Nitashindwaje kukizungumzia? Linapokuja suala la asili ya mwanadamu, Nimeliona waziwazi, na Nimeliangalia toka zamani; sasa Nitashindwaje kuliongelea? Kwa kuwa nimeiona asili ya mwanadamu kwa uwazi, Nina sifa za kumrudi mwanadamu na kumhukumu, kwa sababu mwanadamu mzima ametoka Kwangu lakini ameharibiwa na Shetani. Kwa ukweli, Nimehitimu kutathmini kazi ambayo Nimeifanya. Ingawa kazi hii haijafanywa na mwili Wangu, ni uonyeshaji wa moja kwa moja wa Roho, na hiki ndicho Nilicho nacho na kile Nilicho. Kwa hivyo, Ninaweza kuonyesha na kufanya kazi ambayo Napaswa kufanya. Kile ambacho mwanadamu anakisema ni kile alichokipitia. Ni kile ambacho wamekiona, kile ambacho akili zao zinaweza kukifikia, na kile ambacho milango yao ya fahamu inaweza kuhisi. Hicho ndicho wanachoweza kukifanyia ushirika. Maneno yaliyosemwa na mwili wa Mungu ni onyesho la moja kwa moja la Roho na huonyesha kazi ambayo imefanywa na Roho. Mwili haujaipitia au kuiona, lakini bado huonyesha asili Yake kwa sababu kiini cha mwili ni Roho, na huonyesha kazi ya Roho. Ingawa mwili hauwezi kuifikia, ni kazi ambayo tayari imefanywa na Roho. Baada ya kufanyika mwili, kupitia uonyeshaji wa mwili, Anawasaidia watu kujua asili ya Mungu na kuwafanya watu kuiona tabia ya Mungu na kazi ambayo Ameifanya. Kazi ya mwanadamu inawawezesha watu kuelewa kwa uwazi kuhusu kile wanachopaswa kuingia kwacho na wanachopaswa kukielewa; inahusisha kuwaongoza watu kupata ufahamu na kuujua ukweli. Kazi ya mwanadamu ni kuwaendeleza watu; kazi ya Mungu ni kufungua njia mpya na kufungua enzi mpya kwa ajili ya binadamu, na kuwafunulia watu kile ambacho hakijafahamika kwa watu wenye mwili wa kufa, ikiwasaidia kuelewa tabia Yake. Kazi ya Mungu ni kuwaongoza wanadamu wote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 176)

Kazi ya Roho Mtakatifu ni kuhusu kuwasaidia watu kupata faida; ni kuwaadilisha watu; hakuna kazi ambayo haiwanufaishi watu. Haijalishi kama ukweli ni wa kina au usio wa kina, na haijalishi tabia ya wale wanaopokea ukweli huo ilivyo, chochote ambacho Roho Mtakatifu anafanya, yote hayo huwanufaisha watu. Lakini kazi ya Roho Mtakatifu haiwezi kufanywa moja kwa moja; ni lazima ifanywe na wanadamu wanaoshirikiana na Yeye. Ni kwa njia hii pekee ndiyo matokeo ya kazi ya Roho Mtakatifu yanaweza kupatikana. Bila shaka, inapokuwa ni kazi ya moja kwa moja ya Roho Mtakatifu, haijachanganywa na kitu chochote kabisa; lakini inapotumia mwanadamu kama chombo, inakuwa imechanganywa sana na sio kazi halisi ya Roho Mtakatifu. Kwa njia hii, ukweli hubadilika katika viwango tofauti. Wafuasi hawapokei nia halisi ya Roho Mtakatifu bali wanapokea muungano wa kazi ya Roho Mtakatifu na uzoefu na maarifa ya mwanadamu. Sehemu ya kazi ya Roho Mtakatifu inayopokelewa na wafuasi ni sahihi. Uzoefu na maarifa ya mwanadamu yanayopokewa yanatofautiana kwa sababu watenda kazi ni tofauti. Watenda kazi wanapokuwa na nuru na uongozi wa Roho Mtakatifu, wanakuwa wanapata uzoefu kulingana na nuru na uongozi huu. Ndani ya uzoefu huu kuna akili ya mwanadamu na uzoefu, vile vile asili ya ubinadamu, ambapo wanapata maarifa na kuona vile walivyopaswa kuona. Hii ndiyo njia ya kutenda baada ya mwanadamu kuujua ukweli. Namna hii ya kutenda siku zote haifanani kwa sababu watu wana uzoefu tofauti na vitu ambavyo watu wanavipitia ni tofauti. Kwa njia hii, nuru ile ile ya Roho Mtakatifu inaleta maarifa tofauti na desturi kwa sababu wale wanaopokea nuru hiyo ni tofauti. Baadhi ya watu hufanya makosa madogo wakati wa utendaji ilhali wengine hufanya makosa makubwa, na baadhi hawafanyi chochote ila ni makosa tu. Hii ni kwa sababu uwezo wa kuelewa mambo unatofautiana na kwa sababu tabia zao halisi pia zinatofautiana. Baadhi ya watu wanaelewa hivi baada ya kuusikia ujumbe, na baadhi ya watu wanauelewa vile baada ya kuusikia ukweli. Baadhi ya watu wanapotoka kidogo; na baadhi hawaelewi kabisa maana ya ukweli. Kwa hiyo, kwa jinsi yoyote mtu aelewavyo ndivyo atakavyowaongoza wengine; hii ni kweli kabisa, kwa sababu kazi yake inaonyesha asili yake tu. Watu wanaoongozwa na watu wenye ufahamu sahihi wa ukweli pia watakuwa na ufahamu sahihi wa ukweli. Hata kama kuna watu ambao uelewa wao una makosa, ni wachache sana, na sio watu wote watakuwa na makosa. Ikiwa mtu ana makosa katika anavyouelewa ukweli, wale wanaomfuata bila shaka pia watakuwa na makosa. Watu hawa watakuwa na makosa katika kila namna. Kiwango cha kuuelewa ukweli miongoni mwa wafuasi kinategemea kwa kiasi kikubwa watenda kazi. Bila shaka, ukweli kutoka kwa Mungu ni sahihi na hauna makosa, na ni hakika. Lakini, watenda kazi hawako sahihi kikamilifu na hatuwezi kusema kwamba ni wa kutegemewa kabisa. Ikiwa watenda kazi wana njia ya kuuweka ukweli katika njia ya matendo, basi wafuasi pia watakuwa na njia ya kuutenda. Ikiwa watenda kazi hawawezi kuuweka ukweli katika matendo bali wanashikilia mafundisho tu, wafuasi hawatakuwa na uhalisia wowote. Ubora wa tabia na asili ya wafuasi vinaukiliwa na kuzaliwa na havihusiani na watenda kazi. Lakini kiwango ambacho kwacho wafuasi wanauelewa ukweli na kumfahamu Mungu kinategemeana na watenda kazi (hii ni kwa baadhi ya watu tu). Vyovyote alivyo mtenda kazi, hivyo ndivyo wafuasi anaowaongoza watakavyokuwa. Kile ambacho mtenda kazi anakionyesha ni asili yake mwenyewe, bila kuacha chochote. Yale anayowaambia wafuasi wake watende ndiyo yeye mwenyewe yuko radhi kuyafikia au ni yale anayoweza kutimiza. Watenda kazi wengi huwaambia wafuasi wao kufuata mambo fulani kulingana na yale wao wenyewe wanayoyafanya, licha ya kuwepo mengi ambayo watu hawawezi kuyafikia kabisa. Kile ambacho watu hawawezi kufanikisha kinakuwa kizuizi katika kuingia kwao.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 177)

Kuna mkengeuko mdogo zaidi katika kazi ya wale ambao wamepitia kupogolewa, kushughulikiwa, hukumu na kuadibu, na uonyeshaji wa kazi zao ni sahihi zaidi. Wale wanaotegemea asili yao katika kufanya kazi wanafanya makosa makubwa sana. Kuna uasili mwingi sana katika kazi ya watu ambao si wakamilifu, kitu ambacho kinaweka kizuizi kikubwa katika kazi ya Roho Mtakatifu. Bila kujali jinsi ubora wa tabia ya mtu ulivyo mzuri, lazima pia apitie upogoaji, ashughulikiwe, na kuhukumiwa kabla aweze kufanya kazi ya agizo la Mungu. Kama hajapitia hukumu kama hiyo, kwa namna yoyote nzuri ile atakavyofanya, haiwezi kuambatana na kanuni za ukweli na ni uasili kabisa na uzuri wa mwanadamu. Kazi ya wale ambao wamepitia kupogolewa, kushughulikiwa, na hukumu ni sahihi zaidi kuliko kazi ya wale ambao hawajapogolewa, kushughulikiwa, na hukumiwa. Wale ambao hawajapitia hukumu hawaonyeshi chochote isipokuwa mawazo ya kibinadamu, yakiwa yamechanganyika na ufahamu wa kibinadamu na talanta za ndani. Sio maonyesho sahihi wa mwanadamu wa kazi ya Mungu. Watu wanaowafuata wanaletwa mbele yao kwa tabia yao ya ndani. Kwa sababu wanaonyesha vitu vingi vya kuona na uzoefu wa mwanadamu, ambavyo takribani havina muungano na nia ya asili ya Mungu, na hutofautiana sana nayo, kazi ya mtu wa aina hii haiwezi kuwaleta watu mbele ya Mungu, bali badala yake huwaleta mbele ya mwanadamu. Hivyo, wale ambao hawajapitia hukumu na kuadibu, hawana sifa za kufanya kazi ya agizo la Mungu. Kazi ya mtenda kazi mwenye sifa inaweza kuwaleta watu katika njia sahihi na kuwaruhusu kuzama kwa kina katika ukweli. Kazi anayofanya inaweza kuwaleta watu mbele ya Mungu. Aidha, kazi anayofanya inaweza kutofautiana kutoka kwa mtu hadi mtu mwingine na wala haifungwi na kanuni, inawapa watu uhuru. Aidha, wanaweza kukua katika uzima kwa taratibu, wakiendelea kukua na kuzama ndani kabisa katika ukweli. Kazi ya mtenda kazi asiyehitimu haifikii kiwango hiki; kazi yake ni ya kipumbavu. Anaweza kuwaleta watu katika kanuni tu; kile anachowataka watu kufanya hakitofautiani kati ya mtu na mtu mwingine; hafanyi kazi kulingana na mahitaji halisi ya watu. Katika kazi ya aina hii kunakuwa na kanuni nyingi sana na mafundisho mengi sana, na haiwezi kuwaleta watu katika uhalisia au katika hali ya kawaida ya kukua katika uzima. Inaweza kuwawezesha watu tu kusimama kwa kanuni chache zisizokuwa na maana. Uongozi wa namna hii unaweza tu kuwapotosha watu. Anakuongoza ili uwe kama yeye; anaweza kukuleta katika kile anacho na kile alicho. Kwa wafuasi kutambua endapo viongozi wana sifa, jambo la muhimu ni kuangalia njia wanayoiongoza na matokeo ya kazi yao, na kuangalia iwapo wafuasi wanapokea kanuni kulingana na ukweli, na kama wanapokea namna ya kutenda kunakowafaa wao ili waweze kubadilishwa. Unapaswa kutofautisha kati ya kazi tofauti za aina tofauti za watu; haupaswi kuwa mfuasi mpumbavu. Hili linaathiri suala la kuingia kwako. Kama huwezi kutofautisha ni uongozi wa mtu yupi una njia na upi hauna, utadanganywa kwa urahisi. Haya yote yana athari ya moja kwa moja katika maisha yako. Kuna mambo mengi ya asili katika kazi ya mtu ambaye hajakamilishwa; matakwa mengi ya kibinadamu yamechanganywa humo. Hali yao ni ya asili, kile walichozaliwa nacho, si maisha baada ya kupitia kushughulikiwa au uhalisia baada ya kubadilishwa. Ni kwa namna gani mtu wa aina hii ya mtu anaweza kuunga mkono utafutaji wa uzima? Maisha halisi ya mwanadamu ni akili au talanta yake ya ndani. Aina hii ya akili au talanta ni kinyume cha kile hasa ambacho Mungu anamtaka mwanadamu afanye. Ikiwa mwanadamu hajakamilishwa na tabia yake potovu haijapogolewa na kushughulikiwa, kutakuwa na pengo kubwa kati ya kile anachokionyesha na ukweli; utachanganywa na vitu visivyoeleweka vizuri kama vile tafakari zake na uzoefu wa upande mmoja, n.k. Aidha, bila kujali jinsi anavyofanya kazi, watu wanahisi kwamba hakuna lengo la jumla na hakuna ukweli ambao unafaa kwa kuingia watu wote. Matakwa mengi yanawekwa kwa watu wakitakiwa kufanya kile ambacho ni nje ya uwezo wao, kumwingiza bata katika kitulio cha ndege. Hii ni kazi ya matakwa ya binadamu. Tabia potovu ya mwanadamu, mawazo yake na fikira vinaenea katika sehemu zote za mwili wake. Mwanadamu hakuzaliwa na tabia ya kutenda ukweli, na wala hana tabia ya kuuelewa ukweli moja kwa moja. Ikiongezwa kwa upotovu ya mwanadamu—mtu wa aina hii ya asili anapofanya kazi, je, si yeye husababisha ukatizaji? Lakini mwanadamu ambaye amekamilishwa ana uzoefu wa ukweli ambao watu wanapaswa kuuelewa, na maarifa ya tabia yao potovu, ili kwamba vitu visivyoeleweka vizuri na visivyokuwa halisi katika kazi yake vididimie kwa taratibu, ughushi wa binadamu upungue, na kazi na huduma yake yakaribie zaidi viwango vinavyohitajika na Mungu. Hivyo, kazi yake imeingia katika uhalisi wa ukweli na pia imekuwa halisi zaidi. Mawazo katika akili ya mwanadamu yanazuia kazi ya Roho Mtakatifu. Mwanadamu ana fikira nzuri na mwenye mantiki ya maana na uzoefu mkongwe katika kukabiliana na mambo. Kama haya yote hayatapitia kupogolewa na kusahihishwa, yote yanakuwa vizuizi katika kazi. Hivyo kazi ya mwanadamu haiwezi kufikia kiwango cha juu cha usahihi, hususan kazi ya watu ambao hawajakamilishwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 178)

Kazi ya mwanadamu ina mipaka na kadiri inavyoweza kufika. Mtu mmoja anaweza tu kufanya kazi ya wakati fulani na hawezi kufanya kazi ya enzi nzima—vinginevyo, angewaongoza watu katika kanuni. Kazi ya mwanadamu inaweza kufaa tu katika kipindi au awamu fulani. Hii ni kwa sababu uzoefu wa mwanadamu una mawanda. Mtu hawezi kulinganisha kazi ya mwanadamu na kazi ya Mungu. Njia za mwanadamu kutenda na maarifa yake ya ukweli yote yanatumika tu katika mawanda fulani. Huwezi kusema kwamba njia ambayo mwanadamu anaiendea ni matakwa ya Roho Mtakatifu kabisa, kwa sababu mwanadamu anaweza kupewa nuru na Roho Mtakatifu tu na hawezi kujazwa kikamilifu na Roho Mtakatifu. Vitu ambavyo mwanadamu anaweza kuvipitia vyote vipo ndani ya mawanda ya ubinadamu na haviwezi kuzidi mawanda ya fikira katika akili ya kawaida ya mwanadamu. Wale wote wanaoweza kuishi kwa kudhihirisha uhalisi wa ukweli hupitia ndani ya mawanda haya. Wanapoupitia ukweli, siku zote ni uzoefu wa maisha ya kawaida ya mwanadamu chini ya nuru ya Roho Mtakatifu, sio kupitia uzoefu kwa namna ambayo inakengeuka kutoka kwa maisha ya kawaida ya mwanadamu. Wanapitia uzoefu wa ukweli ambao unatiwa nuru na Roho Mtakatifu katika msingi wa kuishi maisha yao ya kibinadamu. Aidha, ukweli huu unatofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, na kina chake kinahusiana na hali ya mtu huyo. Mtu anaweza kusema kwamba njia anayoipitia ni maisha ya kawaida ya kibinadamu ya mwanadamu kufuatilia ukweli na kwamba hiyo ndiyo njia ambayo mtu wa kawaida ambaye amepata nuru ya Roho Mtakatifu anaipita. Huwezi kusema kwamba njia wanayoipitia ni njia ambayo inafuatwa na Roho Mtakatifu. Katika uzoefu wa kawaida wa binadamu, kwa sababu watu wanaoutafuta ukweli hawafanani, kazi ya Roho Mtakatifu pia haifanani. Aidha, kwa sababu mazingira wanayoyapitia na kiwango cha uzoefu wao havifanani, kwa sababu ya mchanganyiko wa akili na mawazo yao, uzoefu wao pia umechanganyika kwa kiwango tofauti. Kila mtu anaelewa ukweli kulingana na hali yake tofauti ya kibinafsi. Ufahamu wao wa maana halisi ya ukweli hauko kamili, na ni kipengele chake kimoja tu au vichache. Mawanda ambayo ukweli unaeleweka kwa mwanadamu siku zote umejikita katika hali tofauti tofauti za watu, na hivyo hazifanani. Kwa njia hii, maarifa yanayoonyesha ukweli ule ule na watu tofauti havifanani. Huu kusema, uzoefu wa mwanadamu siku zote una mipaka, na hauwezi kuwakilisha kikamilifu matakwa ya Roho Mtakatifu, na kazi ya mwanadamu haiwezi kuchukuliwa kama kazi ya Mungu, hata kama kile kinachoonyeshwa na mwanadamu kinafanana kwa karibu sana na mapenzi ya Mungu, hata kama uzoefu wa mwanadamu unakaribiana sana na kazi ya ukamilifu itakayofanywa na Roho Mtakatifu. Mwanadamu anaweza kuwa tu mtumishi wa Mungu, akifanya kazi ambayo Mungu amemwaminia. Mwanadamu anaweza kuonyesha maarifa tu chini ya nuru ya Roho Mtakatifu na ukweli alioupata kutokana na uzoefu wake binafsi. Mwanadamu hana sifa na hana vigezo vya kuwa njia ya Roho Mtakatifu. Hana uwezo wa kusema kuwa kazi ya mwanadamu ni kazi ya Mungu. Mwanadamu ana kanuni za kufanya kazi za mwanadamu, na wanadamu wote wana uzoefu tofauti na wana hali zinazotofautiana. Kazi ya mwanadamu inajumuisha uzoefu wake wote chini ya nuru ya Roho Mtakatifu. Uzoefu huu unaweza tu kuwakilisha asili ya mwanadamu na hauwakilishi asili ya Mungu, au mapenzi ya Roho Mtakatifu. Kwa hivyo, njia anayoipita mwanadamu haiwezi kusemwa kuwa njia anayoipita Roho Mtakatifu, kwa sababu kazi ya mwanadamu haiwezi kuwakilisha kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu na uzoefu wa mwanadamu sio matakwa ya Roho Mtakatifu. Kazi ya mwanadamu ina hatari ya kuangukia katika kanuni, na mbinu za kazi yake zimefinywa katika uelewa wake finyu na hawezi kuwaongoza watu katika njia huru. Wafuasi wengi wanaishi ndani ya mawanda finyu, na uzoefu wao pia unakuwa ni finyu. Uzoefu wa mwanadamu siku zote ni finyu; mbinu ya kazi yake pia ni finyu na haiwezi kulinganishwa na kazi ya Roho Mtakatifu au kazi ya Mungu Mwenyewe—hii ni kwa sababu uzoefu wa mwanadamu, hatimaye, ni finyu. Hata hivyo Mungu anafanya kazi Yake, hakuna kanuni kwa kazi yake; vyovyote vile inavyofanywa, haifungwi na njia moja. Hakuna kanuni za aina yoyote ile katika kazi ya Mungu—kazi Yake yote ni huru na ni bure. Haijalishi ni muda kiasi gani mwanadamu anatumia kumfuata Yeye, hawawezi kutengeneza sheria zozote za njia anavyofanya kazi. Ingawaje kazi Yake inaongozwa na kanuni, siku zote inafanywa katika njia mpya na siku zote inakuwa na maendeleo mapya ambayo yanazidi uwezo wa mwanadamu. Katika kipindi fulani, Mungu anaweza kuwa na njia nyingi tofauti tofauti za kazi na njia tofauti za kuongoza, Akiruhusu watu siku zote kuwa na kuingia kupya na mabadiliko mapya. Huwezi kuelewa sheria za kazi Yake kwa sababu siku zote Anafanya kazi katika njia mpya. Ni kwa njia hii tu ndiyo wafuasi wa Mungu hawawezi kuanguka katika kanuni. Kazi ya Mungu Mwenyewe siku zote inaepuka mitazamo ya watu na kupinga mitazamo yao. Ni wale tu ambao wanamfuata Yeye kwa moyo wote ndio wanaoweza kubadilishwa tabia zao na wanaweza kuishi kwa uhuru bila kuwa chini ya kanuni zozote au kufungwa na mitazamo yoyote ya kidini. Madai ambayo kazi ya mwanadamu inawawekea watu yamejikita katika uzoefu wake mwenyewe na kile ambacho yeye mwenyewe anaweza kutimiza. Kiwango cha matakwa haya kimejifunga ndani ya mawanda fulani, na mbinu za kutenda pia ni finyu sana. Kwa hivyo wafuasi bila kutambua huishi ndani ya matakwa finyu; kadiri muda unavyokwenda, yanakuwa kanuni na taratibu za kidini. Ikiwa kazi ya kipindi fulani inaongozwa na mtu ambaye hajapitia kukamilishwa na Mungu na hakupokea hukumu, wafuasi wake wote watakuwa wadini na wataalamu wa kumpinga Mungu. Kwa hivyo, ikiwa mtu fulani ni kiongozi aliyehitimu, mtu huyo anapaswa kuwa amepitia hukumu na kukubali kukamilishwa. Wale ambao hawajapitia mchakato wa hukumu, hata kama wanaweza kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu, wanaonyesha vitu ambavyo si dhahiri na visivyokuwa halisi. Kadiri muda unavyozidi kwenda, watawaongoza watu katika kanuni zisizoeleweka vizuri na za kimuujiza. Kazi ambayo Mungu anafanya haiambatani na mwili wa mwanadamu; haiambatani na mawazo ya mwanadamu bali inapinga mitazamo ya mwanadamu; haijachanganyika na mitazamo ya kidini isiyoeleweka vizuri. Matokeo ya kazi Yake hayawezi kupatikana kwa mwanadamu ambaye hajakamilishwa na Yeye na yapo nje ya uwezo wa fikira za mwanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 179)

Kazi katika akili ya mwanadamu inafikiwa kwa urahisi sana na mwanadamu. Wachungaji na viongozi katika ulimwengu wa kidini, kwa mfano, wanategemea karama zao na nafasi zao katika kufanya kazi zao. Watu wanaowafuata kwa muda mrefu wataambukizwa na karama zao na kuvutwa na vile walivyo. Wanalenga karama za watu, uwezo na maarifa ya watu, na wanamakinikia mambo ya kimiujiza na mafundisho mengi yasiyokuwa na uhalisi (kimsingi, haya mafundisho ya kina hayawezi kutekelezeka). Hawalengi mabadiliko ya tabia za watu, badala yake wanalenga kuwafundisha watu uwezo wao wa kuhubiri na kufanya kazi, kuboresha maarifa ya watu na mafundisho yao mengi ya kidini. Hawalengi kuona ni kwa kiasi gani tabia ya watu imebadilika au ni kwa kiasi gani watu wanauelewa ukweli. Wala hawajali kuhusu viini vya watu, wala kujua hali za watu za kawaida na zisizo za kawaida. Hawapingi mitazamo ya watu au kufichua fikira zao, sembuse kuwapogoa watu kwa ajili ya upungufu wao wa dhambi. Wengi wanaowafuata wanahudu kwa vipaji vyao, na yote wanayotoa ni fikira za kidini na nadharia za theolojia, ambazo haziambatani na uhalisi na haziwezi kabisa kuwapa watu uzima. Kwa kweli, kiini cha kazi yao ni kulea talanta, kumlea mtu kuwa mhitimu mwenye talanta aliyemaliza mafunzo ya kidini ambaye baadaye anakwenda kufanya kazi na kuongoza. Kwa miaka elfu sita ya kazi ya Mungu unaweza kupata sheria zozote kuihusu? Kuna kanuni na vizuizi vingi katika kazi ambayo mwanadamu hufanya, na ubongo wa mwanadamu umejazwa na mafundisho mengi ya kidini. Hivyo mwanadamu anachokionyesha ni kiasi cha maarifa na utambuzi ndani ya uzoefu wake wote. Mwanadamu hawezi kuonyesha kitu chochote zaidi ya hiki. Uzoefu au maarifa ya mwanadamu hayaibuki kutoka ndani ya karama zake za ndani au tabia yake; vinaibuka kwa sababu ya uongozi wa Mungu na uchungaji wa moja kwa moja wa Mungu. Mwanadamu ana ogani tu ya kupokea uongozi huu na sio ogani ya kuonyesha moja kwa moja uungu. Mwanadamu hana uwezo wa kuwa chanzo, anaweza kuwa tu chombo ambacho hupokea maji kutoka kwa chanzo; hii ni silika ya mwanadamu, ogani ambayo mtu anapaswa kuwa nayo kama mwanadamu. Ikiwa mtu anapoteza ogani ya kukubali neno la Mungu na kupoteza silika ya kibinadamu, mtu huyo anapoteza pia kile ambacho ni cha thamani sana, na anapoteza wajibu wa mwanadamu aliyeumbwa. Ikiwa mtu hana maarifa au uzoefu wa neno la Mungu au kazi Yake, mtu huyo anapoteza wajibu wake, wajibu anaopaswa kuutimiza kama kiumbe aliyeumbwa, na kupoteza heshima ya kiumbe aliyeumbwa. Ni silika ya Mungu kuonyesha uungu ni nini, kama unaonyeshwa katika mwili au moja kwa moja na Roho Mtakatifu; hii ni huduma ya Mungu. Mwanadamu anaonyesha uzoefu wake mwenyewe au maarifa (yaani, anaonyesha kile alicho) wakati wa kazi ya Mungu au baada yake; hii ndiyo silika ya mwanadamu na wajibu wa mwanadamu, ndicho kitu ambacho mwanadamu anapaswa kukifikia. Ingawa maonyesho ya mwanadamu ni duni sana kuliko kile ambacho Mungu anaonyesha, na kuna kanuni nyingi katika kile ambacho mwanadamu huonyesha, mwanadamu anapaswa kutimiza wajibu anaopaswa kutimiza na kufanya kile anachopaswa kufanya. Mwanadamu anapaswa kufanya kitu chochote kinachowezekana kwa mwanadamu kufanya ili kutimiza wajibu wake, na hapaswi kuacha kitu hata kidogo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 180)

Mnapaswa kujua jinsi ya kutofautisha kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu. Mnaweza kuona nini katika kazi ya mwanadamu? Kuna vitu vingi ambavyo ni uzoefu wa mwanadamu katika kazi ya mwanadamu; kile ambacho mwanadamu anakionyesha kile alicho. Kazi ya Mungu pia inaonyesha kile Alicho, lakini kile Alicho ni tofauti na mwanadamu alivyo. Kile mwanadamu alicho ni kiwakilishi cha uzoefu na maisha ya mwanadamu (kile ambacho mwanadamu anakipitia au kukabiliana nacho katika maisha yake, au falsafa za kuishi alizo nazo), na watu wanaoishi katika mazingira tofauti huonyesha nafsi tofauti. Kama una uzoefu wa kijamii au la na jinsi ambavyo unaishi na kupitia uzoefu katika familia yako inaweza kuonekana katika kile unachokionyesha, wakati ambapo huwezi kuona kutoka kwa kazi ya Mungu mwenye mwili kama Ana uzoefu wa maisha ya kijamii au Hana. Anatambua vizuri asili ya mwanadamu, Anaweza kufunua aina za matendo yote yanayohusiana na kila aina ya watu. Ni mzuri hata katika kufunua tabia ya dhambi ya mwanadamu na tabia yake ya uasi. Haishi miongoni mwa watu wa kidunia, lakini Anatambua asili ya watu wenye mwili wa kufa na upotovu wote wa watu wa duniani. Hicho ndicho Alicho. Ingawa Hashughuliki na dunia, Anajua kanuni za kushughulika na dunia, kwa sababu Anaielewa vizuri asili ya mwanadamu. Anajua kuhusu kazi ya Roho ambayo jicho la mwanadamu haliwezi kuiona na kwamba masikio ya mwanadamu hayawezi kusikia, wanadamu wa leo na wanadamu wa enzi zote. Hii inajumuisha hekima ambayo sio falsafa ya kuishi na makuu ambayo ni ngumu kwa watu kuelewa. Hiki ndicho Alicho, kuwekwa wazi kwa watu na pia kufichika kwa watu. Kile Anachoonyesha sio kile ambacho mwanadamu asiye wa kawaida alicho, bali ni tabia za asili na uungu wa Roho. Hasafiri ulimwenguni mzima lakini anajua kila kitu kuhusu ulimwengu. Anawasiliana na “sokwe” ambao hawana maarifa au akili, lakini Anaonyesha maneno ambayo ni ya kiwango cha juu kuliko maarifa na juu ya watu wakubwa duniani. Anaishi miongoni mwa kundi la wanadamu wapumbavu na wasiojali ambao hawana ubinadamu na ambao hawaelewi mila na desturi za ubinadamu na maisha, lakini Anaweza kumwambia mwanadamu kuishi maisha ya kawaida, na kwa wakati uo huo kufichua ubinadamu duni na wa chini wa binadamu. Haya yote ndiyo kile Alicho, mkuu kuliko vile ambacho mwanadamu yeyote wa damu na nyama alicho. Kwake Yeye, si lazima kupitia maisha ya kijamii magumu na changamani, ili Aweze kufanya kazi Anayotaka kufanya na kwa kina kufichua asili ya mwanadamu aliyepotoka. Maisha duni ya kijamii ambayo hayauadilishi mwili Wake. Kazi Yake na maneno Yake hufichua tu kutotii kwa mwanadamu na hayampi mwanadamu uzoefu na masomo kwa ajili ya kushughulika na ulimwengu. Hahitaji kuipeleleza jamii au familia ya mwanadamu wakati Anapompa mwanadamu uzima. Kumweka wazi na kumhukumu wanadamu sio maonyesho wa uzoefu wa mwili Wake; ni kufichua vile mwanadamu asivyokuwa na haki baada ya kufahamu kutotii kwa mwanadamu na kuchukia upotovu wa mwanadamu. Kazi yote Anayoifanya ni kufichua tabia Yake kwa mwanadamu na kuonyesha asili Yake. Ni Yeye tu ndiye anayeweza kuifanya kazi hii, sio kitu ambacho mtu mwenye mwili na damu anaweza kukipata.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 181)

Kazi ambayo Mungu anafanya haiwakilishi uzoefu wa mwili Wake; kazi ambayo mwanadamu anafanya inawakalisha uzoefu wa mwanadamu. Kila mtu anazungumza kuhusu uzoefu wake binafsi. Mungu anaweza kuonyesha ukweli moja kwa moja, wakati mwanadamu anaweza tu kuonyesha uzoefu unaolingana na huo baada ya kupata uzoefu wa ukweli. Kazi ya Mungu haina masharti na haifungwi na muda au mipaka ya kijiografia. Anaweza kuonyesha kile Alicho wakati wowote, mahali popote. Anafanya kazi vile Anavyopenda. Kazi ya mwanadamu ina masharti na muktadha; vinginevyo hana uwezo wa kufanya kazi na hawezi kuonyesha ufahamu wake wa Mungu au uzoefu wake wa ukweli. Unatakiwa tu kulinganisha tofauti baina yao ili kuonyesha kama ni kazi ya Mungu mwenyewe au kazi ya mwanadamu. Kama hakuna kazi inayofanywa na Mungu Mwenyewe, na kuna kazi tu ya mwanadamu, utajua tu kwamba mafundisho ya mwanadamu ni makuu, zaidi ya uwezo wa mtu yeyote yule; toni yao ya kuzungumza, kanuni zao katika kushughulikia mambo na uwezo wao katika kufanya kazi ni zaidi ya uwezo wa wengine. Nyinyi nyote mnavutiwa na watu hawa wa ubora mzuri wa tabia na maarifa ya juu, lakini hamwezi kuona kutoka katika kazi na maneno ya Mungu jinsi ubinadamu Wake ulivyo wa juu. Badala yake, Yeye ni wa kawaida, na Anapofanya kazi, Yeye ni wa kawaida na halisi lakini pia hapimiki kwa watu wenye mwili wa kufa, kitu ambacho kinawafanya watu wahisi kumheshimu sana. Pengine uzoefu wa mtu katika kazi yake ni mkubwa sana, au mawazo na fikira zake ni za juu sana, na ubinadamu wake ni mzuri hasa; hivi vinaweza kutamaniwa na watu tu, lakini visiamshe kicho na hofu yao. Watu wote wanawatamani wale ambao wana uwezo wa kufanya kazi na ambao wana uzoefu wa kina na wanaweza kuutenda ukweli, lakini hawawezi kuvuta kicho, bali kutamani na kijicho. Lakini watu ambao wamepitia uzoefu wa kazi ya Mungu hawamtamani Mungu, badala yake wanahisi kwamba kazi Yake haiwezi kufikiwa na mwanadamu na haiwezi kueleweka na mwanadamu, na kwamba ni nzuri na ya kushangaza. Watu wanapopitia uzoefu wa kazi ya Mungu, ufahamu wao wa kwanza kumhusu ni kwamba Yeye ni asiyeeleweka, ni mwenye hekima na wa ajabu na wanamcha bila kujua na kuihisi siri ya kazi Anayoifanya, ambayo inapita akili ya mwanadamu. Watu wanataka tu kuwa na uwezo wa kukidhi matakwa Yake, kuridhisha matamanio Yake; hawatamani kumpita Yeye, kwa sababu kazi anayoifanya inazidi fikira za mwanadamu na haiwezi kufanywa na mwanadamu kama mbadala. Hata mwanadamu mwenyewe hayajui mapungufu yake, wakati Amefungua njia mpya na kumleta mwanadamu katika dunia mpya zaidi na nzuri zaidi, kwamba mwanadamu amefanya maendeleo mapya na kuwa na mwanzo mpya. Kile ambacho watu wanahisi kumhusu Mungu, sio matamanio, au sio matamanio tu. Uzoefu wake wa kina ni kicho na upendo, hisia zake ni kwamba Mungu kweli ni wa ajabu sana. Anafanya kazi ambayo mwanadamu hawezi kufanya na kusema mambo ambayo mwanadamu hawezi kusema. Watu ambao wamepitia kazi ya Mungu daima wana hisia isiyoweza kuelezeka. Watu wenye uzoefu wa kina kutosha wanaweza kuelewa ukweli wa Mungu; wanaweza kuhisi uzuro Wake, kwamba kazi Yake ni ya hekima sana, ya ajabu sana, na hivyo hii inazalisha nguvu isiyokoma ndani yao. Si woga au upendo wa mara moja moja na heshima, bali hisia za ndani za upendo wa Mungu na uvumilivu kwa mwanadamu. Hata hivyo, watu ambao wamepata uzoefu wa kuadibu na hukumu Yake wanamhisi kuwa Yeye mtukufu na asiyekosewa. Hata watu ambao wamepitia uzoefu mkubwa wa kazi Yake pia hawawezi kumwelewa; watu wote wanaomcha wanajua kwamba kazi Yake hailingani na fikira za watu lakini siku zote inakwenda kinyume na fikira zao. Haihitaji watu wamtamani kabisa au kuwa na kuonekana kwa kujikabidhi Kwake, badala yake anataka wawe na uchaji wa kweli na kutii kikamilifu. Katika nyingi ya kazi Yake, mtu yeyote mwenye uzoefu wa kweli anahisi heshima Kwake, ambayo ni ya juu kuliko matamanio. Watu wameiona tabia Yake kwa sababu ya kazi Yake ya kuadibu na hukumu, na kwa hiyo wanamcha mioyoni mwao. Mungu anapaswa kuchiwa na kutiiwa, kwa sababu uungu Wake na tabia Yake havifanani kama ule wa watu walioumbwa na vikuu juu ya vile vya watu walioumbwa. Mungu hategemei chochote kuwepo na ni wa milele, Yeye siye kiumbe Aliyeumbwa, na ni Mungu tu anayestahili uchaji na utiifu; mwanadamu hana sifa ya kupewa hivi. Hivyo, watu wote waliopitia uzoefu wa kazi Yake na kweli wanamjua wanampatia heshima. Hata hivyo, wale ambao hawaachani fikira zao kumhusu, yaani, wale ambao hawamwoni kuwa Mungu, hawana uchaji wowote Kwake, na hata ingawa wanamfuata hawajashindwa; ni watu wasiotii kwa asili yao. Anafanya kazi hii ili apate matokeo kwamba viumbe vyote vilivyoumbwa vinaweza kumcha Muumbaji, vimwabudu Yeye, na kujikabidhi katika utawala Wake bila masharti. Haya ni matokeo ya mwisho ambayo kazi Yake yote inalenga kuyapata. Ikiwa watu ambao wamepitia kazi hiyo hawamchi Mungu, hata kidogo, kama kutotii kwao kwa zamani hakutabadilika kabisa, basi watu hawa ni hakika wataondolewa. Kama mtazamo wa mwanadamu kwa Mungu ni kumtamani au kuonyesha heshima kwa mbali na sio kumpenda, hata kidogo, hivi ndivyo mtu bila moyo wa kumpenda Mungu anapofikia, na mtu wa aina hiyo anakosa hali za kumwezesha kukamilishwa. Ikiwa kazi nyingi vile haiwezi kupata upendo wa kweli wa mtu, hii ina maana kwamba mtu huyo hajampata Mungu na kwa uhalisi hatafuti kuujua ukweli. Mtu ambaye hampendi Mungu hapendi ukweli na hivyo hawezi kumpata Mungu, sembuse kupata ukubali wa Mungu. Watu kama hao, bila kujali jinsi wanavyopata uzoefu wa Roho Mtakatifu, na bila kujali jinsi gani wanapitia uzoefu wa hukumu, bado hawawezi kumcha Mungu. Hawa ni watu ambao asili yao haiwezi kubadilishwa, ambao wana tabia ya uovu uliokithiri. Wale wote ambao hawamchi Mungu wataondolewa, na kuwa walengwa wa hukumu, na kuadhibiwa kama tu wale ambao wanafanya uovu, watateseka hata zaidi ya wale ambao wamefanya matendo maovu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 182)

Hata hivyo, kazi ya Mungu ni tofauti na kazi ya mwanadamu, na aidha, maonyesho Yake yanawezaje kuwa sawa na ya mwanadamu? Mungu ana tabia Yake Mwenyewe ya pekee, ilhali mwanadamu ana wajibu ambao anapaswa kutimiza. Tabia ya Mungu inaonyeshwa katika kazi Yake, ilhali wajibu wa mwanadamu unadhihirishwakatika uzoefu wa mwanadamu na kuonyeshwa katika kazi za mwanadamu. Kwa hiyo inakuwa dhahiri kupitia kazi inayofanywa iwapo jambo fulani ni maonyesho ya Mungu ama maonyesho ya mwanadamu. Halihitaji kufafanuliwa na Mungu Mwenyewe, wala halihitaji mwanadamu ajitahidi kushuhudia; aidha, halimhitaji Mungu Mwenyewe kumkandamiza mtu yoyote. Yote haya yanakuja kama ufunuo wa kawaida; hayalazimishwi wala silo jambo ambalo mwanadamu anaweza kuingilia kati. Wajibu wa mwanadamu unaweza kujulikana kupitia uzoefu wake, na hauhitaji watu wafanye kazi yoyote ya ziada inayohusu uzoefu wao. Nafsi yote ya mwanadamu inaweza kufichuliwa wakati anapotimiza wajibu wake, wakati Mungu anaweza kuonyesha tabia Yake ya asili anapotekeleza kazi Yake. Ikiwa ni kazi ya mwanadamu basi haiwezi kufichika. Ikiwa ni kazi ya Mungu, basi haiwezekani hata zaidi kwa tabia ya Mungu kufichwa na yeyote, sembuse kudhibitiwa na mwanadamu. Hakuna mwanadamu anayeweza kusemekana kuwa Mungu, wala kazi na maneno yake kuonekana kuwa matakatifu ama kuchukuliwa kuwa yasiyobadilika. Mungu anaweza kusemekana kuwa mwanadamu kwa sababu Amejivika mwili, lakini kazi Yake haiwezi kuchukuliwa kuwa kazi ya mwanadamu ama wajibu wa mwanadamu. Aidha, matamshi ya Mungu na nyaraka za Paulo hayawezi kulinganishwa, wala hukumu na kuadibu kwa Mungu na maneno ya mwanadamu ya kuagiza kuzungumziwa kuwa sawa. Kwa hiyo, kuna kanuni zinazotofautisha kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu. Zinatofautishwa kulingana na viini vyao, sio kwa upana wa kazi ama ustadi wake wa muda. Watu wengi hufanya makosa ya kanuni kuhusiana na hili. Hii ni kwa sababu mwanadamu anaangalia mambo ya nje, ambayo anaweza kutimiza, ilhali Mungu anaangalia kiini, ambacho hakiwezi kuonekana na macho ya mwanadamu. Ukichukulia maneno na kazi ya Mungu kama wajibu wa mtu wa kawaida, na kuona kazi kubwa ya mwanadamu kama kazi ya Mungu aliyejivika mwili badala ya wajibu ambao mwanadamu anatimiza, je, basi hujakosea kimsingi? Barua na wasifu wa mwanadamu vinaweza kuandikwa kwa urahisi, lakini kwa msingi tu wa kazi ya Roho Mtakatifu. Hata hivyo, matamshi na kazi ya Mungu haviwezi kufanikishwa kwa urahisi na mwanadamu ama kutimizwa kwa hekima na fikira za binadamu, na watu hawawezi kuvieleza kikamilifu baada ya kuvichunguza. Masuala haya ya kimsingi yasipowaletea hisia yoyote, basi ni dhahiri kwamba imani yenu si ya kweli ama safi sana. Inaweza tu kusemekana kwamba imani yenu imejaa mashaka, na imekanganyikiwa na ni isiyo na maadili. Bila hata kuelewa masuala ya msingi kabisa ya Mungu na mwanadamu, je, imani kama hii haijakosa utambuzi kabisa?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Msimamo Wako Kuhusu Nyaraka Kumi na Tatu ni Upi?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 183)

Yesu Alikuwa duniani kwa miaka thelathini na tatu na nusu, Alikuja kufanya kazi ya usulubisho na kupitia usulubisho, Mungu Alipata sehemu moja ya utukufu. Mungu Alipokuja katika mwili, Aliweza kunyenyekea na kujificha, na Aliweza kustahimili mateso makubwa. Japokuwa Alikuwa Mungu Mwenyewe, bado Alipitia kila aina ya fedheha, na kila aina ya matusi, na Alipitia uchungu mkubwa kwa kuangikwa msalabani ili kukamilisha kazi ya ukombozi. Baada ya hatua hii ya kazi kutamatishwa, japokuwa watu waliona kuwa Mungu Alikuwa Amepata utukufu mkubwa, huu haukuwa ukamilifu wa utukufu Wake; ilikuwa tu sehemu moja ya utukufu Wake ambao Alikuwa Amepata kutoka kwa Yesu. Japokuwa Yesu Aliweza kupitia magumu ya kila aina, kuwa Mnyenyekevu na kujificha, kusulubishwa kwa ajili ya Mungu, Mungu Alipata tu sehemu moja ya utukufu Wake, na utukufu Wake ulipatikana Israeli. Mungu bado Ana sehemu nyingine ya utukufu: kuja duniani kufanya kazi na kufanya kundi la watu kuwa wakamilifu. Wakati wa hatua ya kazi ya Yesu, Alifanya baadhi ya mambo ambayo si ya kawaida, ila ile hatua ya kazi kwa yoyote ile haikuwa tu ili kufanya ishara na maajabu. Kimsingi ilikuwa kuonyesha kuwa Yesu Angeweza kuteseka na kusulubishwa kwa ajili ya Mungu, kwamba Yesu Angeweza kupitia uchungu mkubwa kwa kuwa Alimpenda Mungu, na kwamba japokuwa Mungu Alimtelekeza, bado Alikuwa radhi kuyatoa maisha Yake kwa ajili ya mapenzi ya Mungu. Baada ya Mungu kukamilisha kazi Yake Israeli na Yesu Kuangikwa msalabani, Mungu Alitukuzwa, na Mungu Alikuwa na ushuhuda mbele ya Shetani. Hamjui na wala hamjaona jinsi Mungu Amekuwa mwili nchini Uchina, basi mnaonaje kuwa Mungu Ametukuzwa? Mungu Anapofanya kazi nyingi ya ushindi kwenu, na mnasimama imara, basi hii hatua ya kazi ya Mungu inakuwa ya mafanikio, na hii ni sehemu ya utukufu wa Mungu. Mnaliona hili tu na bado hamjafanywa na Mungu kuwa wakamilifu, bado hamjaitoa roho yenu kwa Mungu kikamilifu. Bado hamjauona huu utukufu kwa ukamilifu; mnaona tu kwamba Mungu Ameushinda moyo wenu tayari, kwamba hammuachi kamwe na kwamba mtamfuata Mungu mpaka mwisho na moyo wenu hautabadilika, na huo ndio utukufu wa Mungu. Ni katika kitu gani mnauona utukufu wa Mungu? Kwenye athari za kazi Yake kwa wanadamu. Watu huona kuwa Mungu anapendeza sana, wana Mungu mioyoni mwao, na hawako radhi kumuacha, na huu ni utukufu wa Mungu. Wakati ambapo uthabiti wa ndugu na dada wa makanisa unapotokea, na wanaweza kumpenda Mungu kutoka mioyoni mwao, na kuuona ukuu wa kazi inayofanywa na Mungu, ukuu usiomithilika wa maneno Yake, waonapo kwamba maneno yake yanabeba mamlaka na kwamba anaweza kuanzisha kazi Yake katika miji iliyohamwa katika bara ya Uchina, wakati ambapo, japo watu ni wanyonge, mioyo yao inasujudu mbele ya Mungu na wako radhi kuyakubali maneno ya Mungu, na wakati ambapo, japo ni wanyonge na wasiofaa, wanaweza kuona kuwa maneno ya Mungu ni ya kupendeza sana na yastahili utunzaji wao basi huu ndio utukufu wa Mungu. Siku ikija ambayo watu watafanywa wakamilifu na Mungu, na wanaweza kujisalimisha mbele Yake, na kuweza kumtii Mungu kabisa, na kuyawacha matarajio na majaliwa yao mikononi mwa Mungu, basi sehemu ya pili ya utukufu wa Mungu itakuwa imepatikana kikamilifu. Hii ni kusema kuwa wakati ambapo kazi ya Mungu wa vitendo itakapokuwa imekamilishwa kabisa, kazi Yake katika bara ya Uchina itafika kikomo; kwa maneno mengine, wakati wale walioamuliwa kabla na kuchaguliwa na Mungu watakapokuwa wamefanywa wakamilifu, Mungu Atatukuzwa. Mungu Alisema kwamba Ameleta sehemu ya pili ya utukufu Wake Mashariki, na bado hili halionekani kwa macho. Mungu Ameleta kazi Yake Mashariki: tayari Amekuja Mashariki, na huu ni utukufu wa Mungu. Leo ingawa kazi yake haijakamilika bado, kwa sababu Mungu Ameamua kufanya kazi, bila shaka itakamilika. Mungu Ameamua kuwa Ataikamilishia kazi yake Uchina, na Ameamua kuwafanya kuwa wakamilifu. Hivyo Hawapatii njia nyingine—tayari Ameishinda mioyo yenu, na lazima utaendelea upende usipende, na mnapokubaliwa na Mungu, Mungu Anatukuzwa. Leo hii bado Mungu Hajatukuzwa kikamilifu, kwa sababu bado hujafanywa kuwa wakamilifu. Ingawa moyo wako umerudi kwa Mungu, bado kuna udhaifu mwingi katika mwili wako, hauna uwezo wa kumridhisha Mungu, huwezi kushughulishwa na mapenzi ya Mungu, na bado mna vitu vingi hasi ambavyo ni sharti muondokane navyo nab ado lazima mpitie majaribu na usafishaji mwingi. Ni kwa njia hiyo tu ndiyo tabia zenu za maisha zinaweza kubadilika na mnaweza kupatwa na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mazungumzo Mafupi Kuhusu “Ufalme wa Milenia Umefika”

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 184)

Wakati huo kazi ya Yesu ilikuwa ni ukombozi wa wanadamu wote. Dhambi za wote ambao walimwamini zilisamehewa; ilimradi wewe ulimwamini, Angeweza kukukomboa wewe; kama wewe ulimwamini Yeye, wewe hukuwa tena mwenye dhambi, wewe ulikuwa umeondolewa dhambi zako. Hii ndiyo ilikuwa maana ya kuokolewa, na kuhesabiwa haki kwa imani. Hata hivyo, kati ya wale walioamini, kulibaki na kitu ambacho kilikuwa na uasi na pingamizi kwa Mungu, na ambacho kilibidi kiondolewe polepole. Wokovu haukuwa na maana kuwa mwanadamu alikuwa amepatwa na Yesu kabisa, lakini ni kuwa mwanadamu hakuwa tena mwenye dhambi, na kuwa alikuwa amesamehewa dhambi zake; mradi tu uliamini, wewe kamwe hungekuwa mwenye dhambi. Wakati huo, Yesu alifanya kazi kubwa ambayo haikueleweka kwa wanafunzi Wake, na kusema mengi kwamba watu hawakuelewa. Hii ni kwa sababu, wakati huo, Hakutoa maelezo. Kwa hivyo, miaka kadhaa baada ya Yeye kuondoka, Mathayo aliunda kizazi chake, na wengine pia walifanya kazi kubwa ambayo ilikuwa ya mapenzi ya mwanadamu. Yesu hakuja kumkamilisha na kumpata mwanadamu, lakini kufanya awamu moja ya kazi: kuleta injili ya ufalme wa mbinguni na kukamilisha kazi ya kusulubiwa—na punde tu Yesu Aliposulubishwa, kazi Yake ilifika mwisho kamili. Lakini kwa awamu iliyoko sasa—kazi ya ushindi—maneno mengi zaidi lazima yasemwe, kazi nyingi zaidi lazima ifanywe, na lazima kuwe na hatua nyingi. Hivyo pia ni lazima siri za kazi ya Yesu na Yehova zitafichuliwa, ili wanadamu wote waweze kuwa na ufahamu na uwazi wa imani yao, kwa kuwa hii ni kazi ya siku za mwisho, na siku za mwisho ni mwisho wa kazi ya Mungu, wakati wa kuhitimisha kazi hii. Hii awamu ya kazi itakufafanulia sheria ya Yehova na ukombozi wa Yesu, na ni hasa ili uweze kuelewa kazi nzima ya mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita, na kuelewa umuhimu na kiini cha mpango huu wa usimamizi wa miaka elfu sita, na kuelewa kusudi la kazi zote Alizozifanya Yesu na maneno Aliyoyasema, na hata upofu wako wa imani kwenye na katika ibada ya Biblia. Yote haya yatakuwezesha kuelewa kabisa. Wewe utakuja kufahamu kazi anayoifanya Yesu na kazi ya Mungu leo; utaelewa na kushuhudia ukweli wote, uzima, na njia. Katika awamu ya kazi Aliyoifanya Yesu, kwa nini Yesu Aliondoka bila kufanya kazi ya ukamilishaji? Kwa sababu awamu ya kazi ya Yesu haikuwa kazi ya kukamilisha. Wakati Yeye Alisulubishwa msalabani, maneno Yake pia yalifika mwisho; baada ya kusulubiwa kwake, kazi Yake kwa hivyo ilimalizika. Awamu ya sasa ni tofauti. Ni baada tu ya maneno hayo kusemwa hadi mwisho na kazi nzima ya Mungu iwe imehitimika ndipo kazi yake itakapokuwa imemalizika. Wakati wa awamu ya kazi ya Yesu, kulikuwa na maneno mengi yaliyobakia bila kusemwa, au ambayo hayakuwa yameelezwa kikamilifu kwa ufasaha. Waama, Yesu hakujali Alichosema au kile ambacho hakusema, kwa kuwa huduma yake haikuwa huduma ya maneno; na hivyo baada ya Yeye kusulubishwa msalabani Aliondoka. Awamu hiyo ilikuwa hasa kwa ajili ya kusulubiwa, na ni tofauti na awamu ya sasa. Awamu ya kazi hii ni hasa kwa ajili ya kukamilisha, kufumbua, na kuleta kazi yote kwenye hitimisho. Kama maneno hayasemwi hadi tamati yake kabisa, hakutakuwa na mbinu ya kuhitimisha kazi hii, kwa kuwa awamu hii ya kazi yote inafikishwa mwisho na kukamilika kwa kutumia maneno. Wakati huo, Yesu Alifanya kazi kubwa isiyoeleweka na mwanadamu. Akaondoka kimyakimya, na leo bado kunao wengi wasioelewa maneno Yake, ambao ufahamu wao ni potofu lakini bado unaaminika nao kwamba ni sahihi, ambao hawajui kuwa wao si sahihi. Mwishoni, awamu hii ya sasa itafikisha kazi ya Mungu mwisho ulio kamilifu, na kutoa hitimisho Lake. Wote watakuja kufahamu na kujua mpango wa usimamizi wa Mungu. Dhana zilizo ndani ya mwanadamu, nia yake, fahamu yake potofu, dhana zake kuhusu kazi ya Yehova na Yesu, maoni yake kuhusu watu wa Mataifa mengine na michepuko yake ingine na makosa yake yatarekebishwa. Na mwanadamu ataelewa njia yote ya haki ya uzima, na kazi yote anayofanya Mungu, na ukweli wote. Wakati hayo yatafanyika, awamu hii ya kazi itafikia kikomo. Kazi ya Yehova ilikuwa uumbaji wa ulimwengu, ilikuwa mwanzo; awamu hii ya kazi ni mwisho wa kazi, na ni hitimisho. Hapo mwanzo, kazi ya Mungu ilifanyika miongoni mwa wateule wa Israeli, na ilikuwa mapambazuko ya kipindi kipya katika pahali patakatifu zaidi ya popote. Awamu ya mwisho ya kazi inafanywa katika nchi ambayo ni chafu zaidi ya zote, kuhukumu ulimwengu na kuleta enzi kwenye kikomo. Katika awamu ya kwanza kazi ya Mungu ilifanyika katika maeneo yenye kung’aa kuliko maeneo yote, na awamu ya mwisho inafanyika katika maeneo yaliyo katika giza kuliko maeneo yote, na giza hili litaondolewa, na mwanga kufunguliwa, na watu wote kushindwa. Wakati watu wa maeneo haya yaliyo chafu kuliko yote na yaliyo na giza watakuwa wameshindwa na idadi yote ya watu wametambua kuwa Mungu yupo, na ya kuwa ni Mungu wa kweli, na kila mtu Amemwamini kabisa, basi ukweli huu utatumika kutekeleza kazi ya ushindi katika ulimwengu mzima. Awamu hii ya kazi ni ya ishara: Punde tu kazi ya kipindi hiki itakapomalizika, kazi ya miaka 6,000 ya usimamizi itafikia mwisho kabisa. Mara baada ya wale walioko katika maeneo yaliyo na giza kuliko yote watakapokuwa wameshindwa, bila shaka itakuwa hivyo pia kila mahali pengine. Kwa hivyo, kazi ya ushindi tu katika China inabeba ishara ya maana. China inajumuisha nguvu zote za giza, na watu wa China wanawakilisha wale wote ambao ni wa mwili, wa Shetani, na wa mwili na damu. Ni watu wa China ndio wamepotoshwa sana na joka kubwa jekundu, ambao wana upinzani wenye nguvu dhidi ya Mungu, ambao wana ubinadamu ulio mbovu zaidi na ulio mchafu, na kwa hivyo hao ni umbo asili la wanadamu wote wenye matendo maovu. Hii si kusema kwamba nchi nyingine hazina shida kabisa; dhana za mwanadamu ni sawa zote, na ingawa watu wa nchi hizi wanaweza kuwa na uhodari mzuri, ikiwa hawamjui Mungu, basi ni lazima iwe kwamba wanampinga. Kwa nini Wayahudi pia walimpinga na kumwasi Mungu? Kwa nini Mafarisayo pia walimpinga? Kwa nini Yuda alimsaliti Yesu? Wakati huo, wengi wa wanafunzi hawakumjua Yesu. Kwa nini, baada ya Yesu kusulubiwa na kufufuliwa tena, watu bado hawakumwamini? Je, uasi wa mwanadamu sio sawa wote? Ni tu kwamba watu wa China wamefanyika mfano, na watakaposhindwa watakuwa mfano na kielelezo, na watatumika kama kumbukumbu kwa wengine. Kwa nini mimi daima Nimesema yakuwa nyinyi ni kiungo cha mpango wangu wa usimamizi? Ni katika watu wa China ambapo upotovu, uchafu, udhalimu, upinzani, na uasi unadhihirishwa kikamilifu zaidi na kufichuliwa kwa hali zao mbalimbali. Kwa upande mmoja, wao ni wa kimo cha umaskini, na kwa upande mwingine, maisha yao na mawazo yao ni ya nyuma kimaendeleo, na tabia zao, mazingira ya kijamii, familia ya kuzaliwa—yote ni ya umaskini na ya nyuma kimaendeleo kuliko yote. Hadhi yao, pia, ni ya chini. Kazi katika eneo hili ni ya ishara, na baada ya kazi hii ya majaribio hufanywa kwa ukamilifu wake, na kazi yake inayofuata itakwenda vizuri zaidi. Kama awamu hii ya kazi inaweza kukamilika, basi kazi inayofuata itakamilika bila shaka. Mara baada ya awamu ya kazi hii kutimizwa, na mafanikio makubwa kufikiwa kikamilifu, kazi ya ushindi katika ulimwengu mzima itakua imefikia kikomo kamili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (2)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 185)

Kufanya kazi sasa kwa uzao wa Moabu ni kuwaokoa wale ambao wameanguka katika giza zaidi. Ingawa walikuwa wamelaaniwa, Mungu yuko tayari kupata utukufu kutoka kwao. Hii ni kwa sababu hapo awali, wote walikuwa watu waliomkosa Mungu mioyoni mwao—kuwafanya tu kuwa wale wanaomtii na kumpenda Yeye ni ushindi wa kweli, na matunda hayo ya kazi ni ya thamani sana na yenye kuridhisha zaidi. Huku tu ni kupata utukufu—huu ndio utukufu ambao Mungu anataka kuupata katika siku za mwisho. Ingawa watu hawa ni wa nafasi ya chini, sasa wanaweza kupata wokovu mkubwa mno, ambao kwa kweli ni kupandishwa hadhi na Mungu. Kazi hii ni ya maana sana, na ni kwa njia ya hukumu ndipo Anawapata watu hawa. Yeye hawaadhibu kwa makusudi, lakini Amekuja kuwaokoa. Kama angekuwa Anafanya kazi ya kushinda katika Israeli wakati wa siku za mwisho ingekuwa ni bure; hata kama ingezaa matunda, haingekuwa na thamani yoyote au umuhimu wowote mkubwa, na Yeye hangeweza kupata utukufu wote. Anafanya kazi kwenu, yaani, wale ambao wameanguka katika maeneo yenye giza zaidi, wao walio nyuma zaidi kimaendeleo. Watu hawa hawakiri kuwa kuna Mungu na kamwe hawajapata kujua kwamba kuna Mungu. Viumbe hawa wamepotoshwa na Shetani hadi kiwango ambapo wamemsahau Mungu. Wamepofushwa na Shetani na hawajui kabisa kwamba kuna Mungu mbinguni. Katika mioyo yenu nyote mnaabudu sanamu, mnamwabudu Shetani—je, si ninyi ni watu wa hali ya chini zaidi, watu walio nyuma zaidi kimaendeleo? Ninyi ni wa hali ya chini kabisa ya mwili, mnakosa uhuru wowote wa kibinafsi, na mnapitia shida pia. Ninyi pia ni watu mlio katika ngazi ya chini kabisa katika jamii hii, bila hata uhuru wa imani. Huu ni umuhimu wa kufanya kazi kwenu. Kufanya kazi kwenu sasa, uzao wa Moabu, sio kuwafedhehesha kwa makusudi, lakini ni kufichua umuhimu wa kazi. Ni kuwainua sana. Ikiwa mtu ana mantiki na utambuzi, atasema: “Mimi ni uzao wa Moabu. Kweli sistahili kuinuliwa kukuu huku na Mungu ambako nimepokea sasa, au baraka hizi nyingi. Kwa mujibu wa yale ninayofanya na kusema, na kulingana na hali na thamani yangu—sistahili kabisa hizo baraka nyingi kutoka kwa Mungu. Waisraeli wana upendo mkubwa kwa Mungu, na neema wanayoifurahia imefadhiliwa kwao na Yeye, lakini hali yao ni ya juu zaidi kuliko yetu. Abrahamu alijitolea sana kwa Yehova, na Petro alijitolea sana kwa Yesu—ibada yao ilishinda yetu kwa mara mia, na kwa msingi wa matendo yetu hatufai kabisa kufurahia neema ya Mungu.” Huduma ya watu hawa nchini China haiwezi kuletwa mbele za Mungu hata kidogo. Ni fujo kamili tu, na kwamba sasa mnafurahia neema nyingi za Mungu ni kuinuliwa na Mungu kabisa! Je, ni wakati upi mmeitafuta kazi ya Mungu? Je, mmeyatoa maisha yenu kwa Mungu lini? Ni wakati gani mmeiacha familia yako kwa urahisi, wazazi wenu, na watoto wenu? Hakuna hata mmoja wenu aliyelipa gharama kubwa! Kama haingekuwa kwa Roho Mtakatifu kukufanya uonekane, wangapi wenu wangeweza kutoa dhabihu kila kitu? Ni kwa sababu tu mmelazimishwa na kushurutishwa ndipo mmefuata hadi leo. Ibada yenu iko wapi? Utiifu wenu uko wapi? Kulingana na matendo vyenu, mngepaswa kuangamizwa muda mrefu uliopita—mngeondolewa kabisa. Nini kinawafanya mstahili kufurahia baraka nyingi mno? Hamstahili hata kidogo! Nani kati yenu amebuni njia yake mwenyewe? Ni nani kati yenu ameipata njia ya ukweli mwenyewe? Ninyi nyote ni wavivu na walafi, fidhuli msio na maana ambao mnasherehekea katika faraja kwa tamaa! Mnafikiri ninyi ni wakubwa sana? Je, nini mlicho nacho cha kujivunia? Hata kama Singesema ninyi ni uzao wa Moabu, je, asili yenu, mahali penu pa kuzaliwa ni ya fahari sana? Hata kama Singesema ninyi ni uzao wake, je, si ninyi nyote ni uzao wa Moabu kwa kweli? Ukweli wa mambo unaweza kubadilishwa? Je, kufichua asili yenu sasa kunaenda dhidi ya ukweli wa mambo? Angalieni jinsi mlivyo wanyonge, maisha yenu, na tabia—je, hamjui kwamba ninyi ni wa chini kabisa kati ya walio chini miongoni mwa wanadamu? Nini mlicho nacho cha kujisifia? Angalia nafasi yenu katika jamii. Je, si mko katika kiwango cha chini kabisa? Je, mnadhani kwamba Nimenena vibaya? Ibrahimu alimtoa Isaka. Nini ambacho mmetoa? Ayubu ilitoa kila kitu. Nini ambacho mmetoa? Watu wengi sana wameyatoa maisha yao, wakafa, wakamwaga damu yao ili kutafuta njia ya kweli. Je, mmelipa gharama hiyo? Kwa kulinganisha, hamna sifa zinazostahili hata kidogo kufurahia neema hiyo kubwa, kwa hivyo ni sawa kusema leo kwamba ninyi ni uzao wa Moabu? Msijione kuwa wakuu sana. Huna chochote cha kujisifia. Wokovu mkubwa kama huo, neema hiyo kubwa imepewa kwenu bure. Hamjatoa chochote, lakini mmeifurahia neema bure. Je, hamuoni haya? Je, njia hii ya ukweli ni jambo ambalo ninyi wenyewe mlipata kupitia kutafuta? Je, si ni Roho Mtakatifu aliyewalazimisha kuikubali? Kamwe hamkuwa na moyo wa kutafuta na hasa hamkuwa na mioyo ya kuutafuta ukweli, ya kuutamani ukweli. Mmekuwa tu mkistarehe na kuufurahia, na mmeupata ukweli huu bila jitihada kwa upande wenu. Mna haki gani ya kulalamika? Je, unadhani kuwa wewe ni wa thamani kubwa zaidi? Ikilinganishwa na wale ambao walitoa dhabihu maisha yao na kumwaga damu yao, nini mnachopaswa kulalamikia? Kuwaangamiza hivi sasa litakuwa ni jambo linalotarajiwa! Kando na kutii na kufuata, hamna chaguzi zingine. Ninyi hamstahili kabisa! Wengi wa wale kati yenu waliitwa, lakini kama mazingira hayangewalazimisha au kama hamngeitwa, hamngekuwa tayari kabisa kutokea wazi. Nani yuko tayari kutelekeza mambo kwa namna hii? Ni nani yuko tayari kuacha anasa za mwili? Ninyi nyote ni watu ambao husherehekea kwa ulafi katika faraja na kutafuta maisha ya anasa! Mmepata baraka nyingi mno—nini kingine mnacho cha kusema? Mna malalamiko yapi? Mmefurahia baraka nyingi mno na neema kuu mno mbinguni, na kazi sasa imefichuliwa kwenu ambayo haikuwahi kufanywa duniani awali. Je, si hii ni baraka? Kwa sababu mmempinga na kuasi dhidi ya Mungu, sasa mmepitia kuadibu kiasi hiki. Kwa sababu ya kuadibu huku mmeziona rehema na upendo wa Mungu, na hata zaidi mmeziona haki na utakatifu Wake. Kwa sababu ya kuadibu huku na kwa sababu ya uchafu wa wanadamu, mmeiona nguvu kuu ya Mungu, na mmeuona utakatifu na ukuu Wake. Je, si huu ni ukweli adimu mno? Je! Si haya ni maisha yenye maana? Kazi ambayo Mungu hufanya ina maana tele! Hivyo nafasi yenu ilivyo chini zaidi, ndivyo inavyoonyesha zaidi kuinuliwa na Mungu, na ndivyo inavyothibitisha zaidi jinsi kazi Yake ilivyo na thamani kwenu leo. Ni hazina yenye thamani mno hasa! Haiwezi kupatikana popote pengine! Kwa muda mrefu hakuna mtu aliyefurahia wokovu mkubwa hivi. Ukweli kwamba nafasi yenu ni ya chini inaonyesha jinsi wokovu wa Mungu ulivyo mkuu, na inaonyesha kwamba Mungu ni mwaminifu kwa wanadamu—Yeye huokoa, sio kuangamiza.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 186)

Mungu alipokuja duniani Yeye hakuwa wa ulimwengu na Yeye hakuwa mwili ili apate kuufurahia ulimwengu. Mahali ambapo kufanya kazi kungefichua tabia Yake vizuri sana na pawe mahali pa maana zaidi ni mahali Alipozaliwa. Kama ni nchi takatifu au yenye uchafu, na bila kujali Anapofanya kazi, Yeye ni mtakatifu. Kila kitu duniani kiliumbwa na Yeye; Ni kwamba tu kila kitu kimepotoshwa na Shetani. Hata hivyo, vitu vyote bado ni Vyake; vyote viko mikononi Mwake. Kuja Kwake katika nchi yenye uchafu kufanya kazi ni kufichua utakatifu Wake; Yeye hufanya hivi kwa ajili ya kazi Yake, yaani, Yeye huvumilia aibu kubwa kufanya kazi kwa njia hii ili kuwaokoa watu wa nchi hii yenye uchafu. Hii ni kwa ajili ya ushuhuda na ni kwa ajili ya wanadamu wote. Kile aina hii ya kazi inawaruhusu watu kuona ni haki ya Mungu, na ina uwezo zaidi wa kuonyesha mamlaka ya juu kabisa ya Mungu. Ukuu na uadilifu Wake vinaonyeshwa kupitia wokovu wa kundi la watu wa hali ya chini ambao hakuna mtu anayewapenda. Kuzaliwa katika nchi yenye uchafu haimaanishi kabisa kuwa Yeye ni duni; inawaruhusu tu viumbe vyote kuuona utuu Wake na upendo wake wa kweli kwa wanadamu. Zaidi Anavyofanya kwa njia hii, zaidi inavyofichua upendo Wake safi zaidi kwa mwanadamu, upendo wake usio na dosari. Mungu ni mtakatifu na mwenye haki. Hata ingawa Alizaliwa katika nchi yenye uchafu, na ingawa Anaishi na watu hao ambao wamejawa uchafu, kama vile Yesu alivyoishi na wenye dhambi katika Enzi ya Neema, si kazi Yake yote kwa ajili ya kuishi kwa wanadamu wote? Je, si yote ni ili mwanadamu aweze kuupata wokovu mkuu? Miaka elfu mbili iliyopita Aliishi na wenye dhambi kwa miaka kadhaa. Hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya ukombozi. Leo, Anaishi na kikundi cha watu wachafu, wa hali ya chini. Hii ni kwa ajili ya wokovu. Je, si kazi Yake yote ni kwa ajili yenu, wanadamu hawa? Kama haingekuwa ili kuwaokoa wanadamu, kwa nini Angeishi na kuteswa pamoja na wenye dhambi kwa miaka mingi sana baada ya kuzaliwa horini? Na kama haingekuwa ili kuwaokoa wanadamu, kwa nini Angeurudia mwili kwa mara ya pili, kuzaliwa katika nchi hii ambako mapepo hukusanyika, na kuishi na watu hawa ambao wamepotoshwa kwa kina na Shetani? Je, si Mungu ni mwaminifu? Ni aina gani ya kazi Yake ambayo haijakuwa kwa ajili ya wanadamu? Ni aina gani ambayo haijakuwa kwa ajili ya kudura yako? Mungu ni mtakatifu. Hili haliwezi kubadilika! Yeye hanajisiwi na uchafu, ingawa Amekuja katika nchi yenye uchafu; yote haya yanamaanisha tu kwamba upendo wa Mungu kwa wanadamu ni wenye kuwajali wengine sana, mateso na aibu Anayoyavumilia ni makubwa sana! Hamjui kwamba Yeye hupitia aibu kubwa sana kwa ajili yenu wote na kwa ajili ya kudura yenu? Je, hamjui hivyo? Yeye hawaokoi watu wakuu au wana wa familia tajiri na zenye uwezo, lakini Yeye huwaokoa hasa wale ambao ni wa hali za chini na wanaodharauliwa na wengine. Je, si haya yote ni utakatifu Wake? Je, si haya yote ni haki Yake? Afadhali Azaliwe katika nchi yenye uchafu na kuteseka aibu yote kwa ajili ya kuishi kwa wanadamu wote. Mungu ni halisi sana—Hafanyi kazi ya uwongo. Je, si kila hatua ya kazi Yake imefanyika kwa utendaji hivi? Ingawa watu wote wanamkashifu na kusema kuwa Anakaa mezani pamoja na wenye dhambi, ingawa watu wote wanamdhihaki na kusema kuwa Anaishi na wana wa uchafu, na watu wa hali ya chini sana, bado Anajitolea bila ubinafsi, na bado Anakataliwa kwa njia hii kati ya wanadamu. Je, si mateso Anayoyahimili ni makubwa zaidi kuliko yenu? Je, si kazi Yake ni zaidi ya gharama ambayo mmelipa? Mlizaliwa katika nchi ya uchafu lakini mmepata utakatifu wa Mungu. Mlizaliwa katika nchi ambako mapepo hukusanyika lakini mmepokea ulinzi mkubwa. Je, mna uchaguzi gani mwingine? Ni malalamiko yapi mliyo nayo? Je, si mateso ambayo Amevumilia ni makubwa zaidi kuliko mateso ambayo mmevumilia? Amekuja duniani na hajawahi kufaidi furaha za ulimwengu wa kibinadamu. Anayachukia mambo hayo. Mungu hakuja duniani kufurahia manufaa ya kibinadamu kutoka kwa mwanadamu, wala haikuwa kufurahia mambo mazuri ya wanadamu kula na kuvalia. Hazingatii mambo haya; Alikuja duniani kuteseka kwa ajili ya mwanadamu, si kufurahia mambo mazuri ya kidunia. Alikuja kuteseka, Alikuja kufanya kazi, na kukamilisha mpango Wake wa usimamizi. Hakuchagua mahali pazuri, kuishi katika ubalozi au hoteli ghali mno, wala Hana watumishi kadhaa kumtumikia. Kutokana na kile mmeona, hamjui kama Alikuja kufanya kazi au kufurahia? Je, macho yenu hayafanyi kazi? Amewapa kiasi gani? Kama Angezaliwa katika mahali pazuri Angeweza kuupata utukufu? Je, Angeweza kufanya kazi? Je! Huko kungekuwa na umuhimu wowote? Angeweza kuwashinda kabisa wanadamu? Angeweza kuwaokoa watu kutoka katika nchi ya uchafu? Kulingana na mawazo ya kibinadamu, “Mungu, kwa kuwa Wewe ni mtakatifu, kwa nini Ulizaliwa katika mahali penye uchafu mno kama hapa? Unatuchukia na kutukirihi sisi wanadamu wachafu; Unachukia upinzani wetu na uasi wetu, hivyo kwa nini Unaishi nasi? Wewe ni Mungu mkuu. Ungeweza kuzaliwa mahali popote, kwa hivyo mbona ilibidi uzaliwe katika nchi hii chafu? Unatuadibu na kutuhukumu kila siku na Unajua wazi kwamba sisi ni uzao wa Moabu, basi kwa nini bado Unaishi kati yetu? Kwa nini Ulizaliwa katika familia ya uzao wa Moabu? Kwa nini Ulifanya hivyo?” Aina hii ya ufahamu wenu inakosa mantiki! Ni aina hii ya kazi tu ambayo inawaruhusu watu kuuona ukuu Wake, unyenyekevu na kujificha Kwake. Yuko tayari kutoa kila kitu kwa ajili ya kazi Yake, na Amevumilia mateso yote kwa ajili ya kazi Yake. Anafanya kwa ajili ya wanadamu, na hata zaidi kumshinda Shetani ili viumbe vyote viweze kutii chini ya utawala Wake. Hii tu ni kazi ya maana, yenye thamani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 187)

Katika wakati ambapo Yesu Alifanya kazi Uyahudi, Aliifanya wazi, lakini sasa, Nazungumza na Kufanya kazi kati yenu kwa siri. Wasioamini hawana ufahamu wowote. Kazi Yangu kati yenu imetengwa kutoka kwa nyingine. Maneno haya, kuadibu huku na hukumu hii, vinajulikana tu kwako na sio mwingine. Kazi hii yote inatendeka kati yenu na kuonekana tu kwenu; hakuna yeyote asiyeamini anayefahamu haya, kwani muda haujafika. Wanadamu hao wako karibu kufanywa wakamilifu baada ya kuvumilia adibu, lakini wale walio nje hawajui lolote juu yake. Kazi hii imefichwa sana! Kwao, Mungu mwenye mwili ni siri, lakini kwa wale walio katika mkondo, Anaweza kuchukuliwa kuwa wazi. Ingawa kwa Mungu yote ni wazi, yote yanakuwa wazi na yote yanaachiliwa, haya tu ni ya ukweli kwa wale wanaomwamini, na hakuna kitu kinachofanywa kujulikana kwa wale wasioamini. Kazi inayofanywa kwa sasa miongoni mwenu na huko Uchina imefungwa vikali, ili kuwazuia wasijue. Wakipata kujua, kinachowangojea ni shutuma na mateso. Hawataamini. Kufanya kazi katika taifa la joka kuu jekundu, mahali palipo nyuma zaidi, sio kazi rahisi. Kama kazi hii ingewekwa wazi na kujulikana, basi ingekuwa vigumu kuendelea. Hatua hii ya kazi haiwezi kuendelea katika sehemu hii. Wangestahimili vipi kama kazi hii ingeendelezwa kwa uwazi? Hii haingeleta hata hatari kubwa zaidi? Kama kazi hii haingefichwa, na badala Yake kuendelea kama wakati wa Yesu Alivyowaponya wagonjwa na kufukuza mapepo kwa njia ya kustaajabisha, basi si ingekuwa tayari “imeshanyakuliwa” na ibilisi? Je, wangestahimili uwepo wa Mungu? Kama sasa ningeingia kwenye sinagogi kuwahadhiria wanadamu, je, si ningekuwa nimeshapasuliwa katika vipande kitambo? Na ikiwa hivyo, kazi Yangu itawezaje kuendelea kufanyika? Sababu ambayo ishara na miujiza haitendeki wazi wazi ni kwa ajili ya kujificha. Kwa hivyo kazi Yangu haiwezi kuonekana, kujulikana wala kugunduliwa na wasioamini. Iwapo hatua hii ya Kazi ingefanyika kwa njia sawa na kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema, haingekuwa thabiti sana. Kwa hivyo, kazi hii kufichwa namna hii ni ya manufaa kwenu na kwa kazi yote. Wakati kazi ya Mungu duniani inafika kikomo, kumaanisha, wakati kazi hii katika siri inakamilika, hatua hii ya kazi italipuka na kuwa wazi. Watu wote watajua kwamba kuna kundi la washindi ndani ya taifa la Uchina; kila mwanadamu atafahamu kuwa Mungu katika mwili yuko Uchina na kwamba kazi Yake imefika kikomo. Hapo tu ndipo kutampambazukia mwanadamu: Ni kwa nini taifa la Uchina halijaonyesha kudhoofika wala kuporomoka? Inaonekana kuwa Mungu anaendeleza kazi Yake binafsi katika taifa la China na amefanya kuwa kamilifu kundi la watu na kuwafanya washindi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (2)

Iliyotangulia: Kujua Kazi ya Mungu

Inayofuata: Kujua Kazi ya Mungu (II)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp