Hukumu Katika Siku za Mwisho
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 77)
Kabla ya mwanadamu kukombolewa, sumu nyingi ya Shetani ilikuwa imepandwa ndani yake tayari. Baada ya miaka mingi ya upotovu wa Shetani, mwanadamu tayari ana asili ndani yake inayompinga Mungu. Hivyo, mwanadamu atakapokombolewa, hakitakuwa kitu kingine ila ni ukombozi, ambapo mwanadamu ananunuliwa kwa gharama kuu, lakini asili ya sumu ndani yake haijaondolewa. Mwanadamu ambaye amechafuliwa lazima apitie mabadiliko kabla ya kuwa wa kustahili kumtumikia Mungu. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuacha nje upotovu wake na kufanywa safi. Badala ya kuichukua hatua hii ya kazi kuwa ile ya wokovu, itafaa zaidi kusema kuwa ni kazi ya utakaso. Kwa kweli hatua hii ni ile ya ushindi na pia hatua ya pili ya wokovu. Mwanadamu anatwaliwa na Mungu kupitia hukumu na kuadibu na neno; kwa kutumia neno kusafisha, hukumu na kufichua, uchafu wote, fikira, nia, na matumaini ya mtu mwenyewe katika moyo wa mwanadamu zinafuliwa. Ingawa mwanadamu amekombolewa na kusamehewa dhambi zake, inachukuliwa kuwa Mungu hakumbuki makosa ya mwanadamu na kutomtendea mwanadamu kulingana na makosa yake. Hata hivyo, mwanadamu anapoishi katika mwili na hajaachiliwa huru kutoka kwa dhambi, ataendelea tu kutenda dhambi, akiendelea kufunua tabia yake potovu ya kishetani. Haya ndiyo maisha ambayo mwanadamu anaishi, mzunguko usiokoma wa dhambi na msamaha. Wengi wa wanadamu wanatenda dhambi mchana kisha wanakiri jioni. Hivi, hata ingawa sadaka ya dhambi ni ya manufaa kwa binadamu milele, haitaweza kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye dhambi. Ni nusu tu ya kazi ya wokovu ndiyo imemalizika, kwani mwanadamu bado yuko na tabia potovu. Kwa mfano, wakati ambapo watu walijua kwamba walitoka kwa Moabu, walitoa maneno ya malalamiko, hawakutafuta tena uzima, na wakawa hasi kabisa. Je, hili halionyeshi kwamba bado hawawezi kutii kwa ukamilifu kutawaliwa na Mungu? Je, hii siyo tabia ya kishetani ya upotovu kabisa? Ulipokuwa hupitii kuadibu, mikono yako iliinuliwa juu zaidi ya wengine wote, hata ile ya Yesu. Na ulilia kwa sauti kubwa: “Kuwa mwana mpendwa wa Mungu! Kuwa mwandani wa Mungu! Ni heri tufe kuliko kumtii Shetani! Muasi Shetani wa zamani! Liasi joka kuu jekundu! Acha joka kuu jekundu lianguke kabisa kutoka mamlakani! Acha Mungu atufanye kamili!” Vilio vyako vilikuwa vikubwa zaidi ya wengine. Lakini kisha ukaja wakati wa kuadibu na, mara tena, tabia ya upotovu ya watu ilifichuliwa. Kisha, vilio vyao vikakoma, na hawakuwa tena na azimio. Huu ni upotovu wa mwanadamu; unaingia ndani zaidi kuliko dhambi, ulipandwa na Shetani na umekita mizizi ndani zaidi ya mwanadamu. Sio rahisi kwa mwanadamu kuzifahamu dhambi zake; mwanadamu hawezi kufahamu asili yake iliyokita mizizi. Ni kupitia tu katika hukumu na neno ndipo mabadiliko haya yatatokea. Hapo tu ndipo mwanadamu ataendelea kubadilika kutoka hatua hiyo kuendelea.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 78)
Ikifika kwa neno “hukumu,” utawaza juu ya maneno ambayo Yehova alizungumza kila mahali na pia maneno ya kukaripia ambayo Yesu aliwaambia Mafarisayo. Ingawa maneno haya ni yenye ukali, sio hukumu ya Mungu kwa mwanadamu; maneno tu ambayo yamezungumzwa na Mungu katika mazingira tofauti, yaani, mandhari tofauti, maneno haya ni tofauti kabisa na yale maneno anayonena Kristo wakati Anamhukumu mwanadamu siku za mwisho. Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu. Usipouchukulia ukweli huu kuwa muhimu na kila mara kufikiria kuuepuka au kutafuta njia nyingine isipokuwa ukweli, basi ninasema kuwa wewe ni mtenda dhambi mkubwa. Iwapo una imani kwa Mungu, lakini hutafuti ukweli au mapenzi ya Mungu, wala hupendi njia inayokuleta karibu na Mungu, basi nakwambia kuwa wewe ni yule anayejaribu kuepuka hukumu, na kwamba wewe ni kibaraka na msaliti anayekikimbia kiti kikuu cheupe cha enzi. Mungu hatawasamehe waasi wowote wanaotoroka machoni Pake. Wanadamu wa aina hii watapokea adhabu kali zaidi. Wale wanaokuja mbele za Mungu ili wahukumiwe, na zaidi ya hayo wametakaswa, wataishi milele katika ufalme wa Mungu. Bila shaka, hili ni jambo ambalo liko katika siku za usoni.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 79)
Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli, hakuna shaka kuwa Mungu bado Anaonekana kama kiumbe aliyepata mwili kufanya kazi hii miongoni mwa wanadamu. Hiyo ni kumaanisha, wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya hukumu ya Mungu. Wengi wana hisia mbaya kuhusu kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili, kwa maana mwanadamu huona vigumu kuamini ya kwamba Mungu angefanya kazi ya hukumu akiwa na mwili. Hata hivyo, lazima Nikueleze kwamba mara nyingi kazi ya Mungu huzidi sana matarajio ya mwanadamu na ni vigumu kwa mawazo yao kukubali. Kwa maana wanadamu ni mabuu tu kwenye ardhi, ilhali Mungu ni mkuu Anayejaza ulimwengu mzima; mawazo ya mwanadamu ni kama shimo la maji machafu ambayo yanazalisha mabuu peke yake, ilhali kila hatua ya kazi inayoelekezwa na mawazo ya Mungu ni utoneshaji wa hekima ya Mungu. Mwanadamu hutaka kila wakati kushindana na Mungu, ambalo kwalo Nasema ni wazi nani atapata hasara mwishowe. Nawasihi nyote msijichukulie kuwa wa maana zaidi kushinda dhahabu. Ikiwa wengine wanaweza kukubali hukumu ya Mungu, ni kwa nini wewe usiikubali? Ni vipi ambavyo ninyi ni bora zaidi kuliko wengine? Iwapo wengine wanaweza kuinamisha vichwa vyao mbele ya ukweli, ni kwa nini usifanye vile pia? Mwelekeo mkuu wa kazi ya Mungu hauwezi kukomeshwa. Hatarudia kazi ya hukumu tena kwa sababu tu ya “mchango” ambao umetoa, na utajawa na majuto mengi kwa kupoteza nafasi nzuri kama hiyo. Usipoyaamini maneno Yangu, basi kingoje tu kiti cheupe kikuu cha enzi kilicho angani kipitishe hukumu juu yako! Lazima ujue kwamba Waisraeli wote walimkataa kwa dharau na kumkana Yesu, ilhali uhakika wa ukombozi wa Yesu kwa wanadamu ulizidi kusambaa mpaka mwisho wa ulimwengu. Je, hili silo jambo ambalo Mungu tayari Amelitimiza? Iwapo bado unangoja Yesu aje kukupeleka mbinguni, basi Nasema kuwa wewe ni kipande sugu cha mti mkavu[a]. Yesu hatamkubali mfuasi bandia kama wewe asiye mwaminifu kwa ukweli na anayetafuta baraka pekee. Hasha, Hataonyesha huruma Anapokutupa kwenye ziwa la moto uungue kwa makumi ya maelfu ya miaka.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli
Tanbihi:
a. Kipande cha mti mkavu: nahau ya Kichina inayomaanisha “hali isiyo na matumaini.”
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 80)
Je, sasa unaelewa hukumu ni nini na ukweli ni nini? Ikiwa umeelewa, basi Nakusihi ujisalimishe kwa hukumu kwa utii, la sivyo hutapata kamwe fursa ya kusifiwa na Mungu au kupelekwa na Mungu katika ufalme Wake. Wale wanaokubali hukumu pekee yake na hawawezi kamwe kutakaswa, yaani, wale wanaotoroka wakati kazi ya hukumu inapoendelea, watachukiwa na kukataliwa na Mungu milele. Dhambi zao ni nyingi zaidi, na za kusikitisha zaidi, kuliko zile za Mafarisayo, kwa maana wamemsaliti Mungu na ni waasi dhidi ya Mungu. Wanadamu wa aina hii wasiostahili hata kufanya huduma watapokea adhabu kali zaidi, aidha adhabu inayodumu milele. Mungu hatamsamehe msaliti yeyote ambaye kwa wakati mmoja alidhihirisha uaminifu kwa Mungu kwa maneno tu ilhali alimsaliti Mungu. Wanadamu kama hao watapata adhabu ya malipo kupitia adhabu ya roho, nafsi, na mwili. Je, huu si ufichuzi wa tabia yenye haki ya Mungu? Je, hili silo kusudi la Mungu katika kumhukumu mwanadamu na kumfichua mwanadamu? Wakati wa hukumu, Mungu huwapeleka wote wanaofanya aina zote za uovu mahali palipojaa roho waovu, Akiacha miili yao ya nyama iharibiwe vile wapendavyo roho hao waovu. Miili yao inatoa harufu mbaya ya maiti, na adhabu kama hiyo ndiyo inayowafaa. Mungu huandika kwenye vitabu vyao vya kumbukumbu kila mojawapo ya dhambi za waumini hawa wanafiki wasio waaminifu, mitume wanafiki, na wafanyakazi bandia; kisha, wakati unapowadia, Anawatupa katikati ya roho wachafu, Akiacha miili yao ichafuliwe na roho hao wachafu wanavyopenda, na matokeo yake ni kwamba hawatawahi kamwe kuzaliwa upya katika miili mipya na hawatauona mwanga kamwe. Wale wanafiki waliotoa huduma wakati mmoja lakini hawawezi kuwa waaminifu mpaka mwisho wanahesabiwa na Mungu miongoni mwa waovu, ili watembee katika baraza la waovu, na kuungana na halaiki ya wasio na mpangilio; mwishowe, Mungu atawaangamiza. Mungu huwatenga na Hawatambui wote ambao hawajawahi kuwa waaminifu kwa Kristo au kuweka juhudi yoyote, na Atawaangamiza wote wakati wa mabadiliko ya enzi. Hawatakuwepo tena duniani, sembuse kupata njia ya kuingia katika ufalme wa Mungu. Wale ambao hawajawahi kuwa wa kweli kwa Mungu lakini wamelazimishwa na hali kumshughulikia Mungu kwa uzembe wanahesabiwa miongoni mwa wale wanaotoa huduma kwa watu wa Mungu. Ni idadi ndogo tu ya wanadamu wa aina hii ndio wanaweza kuendelea kuishi, huku wengi wao wataangamia pamoja na wasiohitimu hata kufanya huduma. Hatimaye, Mungu ataleta kwenye ufalme Wake wale wote walio na mawazo kama Yake, watu na wana wa Mungu na vilevile waliojaaliwa na Mungu kuwa makuhani. Hili ndilo tone Analopata Mungu kutokana na kazi Yake. Na kwa wale wasio katika sehemu zozote zilizotengwa na Mungu, watahesabiwa miongoni mwa wasioamini. Na kwa hakika mnaweza kuwaza jinsi hatima yao itakavyokuwa. Tayari Nimewaambia yote Ninayopaswa kusema; njia mnayochagua itakuwa uamuzi wenu kufanya. Mnachopaswa kuelewa ni hiki: Kazi ya Mungu kamwe haimsubiri yeyote asiyeweza kwenda sambamba na Mungu, na tabia ya Mungu ya haki haimwonyeshi mwanadamu yeyote huruma.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 81)
Mungu harudii kazi yake katika kila enzi mpya. Kwa kuwa siku za mwisho zimewadia, Yeye Atafanya kazi ya siku za mwisho na kufichua tabia yake yote siku za mwisho. Siku za mwisho ni enzi tofauti, enzi ambayo Yesu Alisema lazima mteseke kwa maafa, na ukabiliwe na mitetemeko ya ardhi, njaa, na baa, ambavyo vitaonyesha kuwa hii ni enzi mpya, na sio tena Enzi ya Neema ya zamani. Kama, watu wanavyosema, Mungu daima habadiliki, tabia yake daima ni ya huruma na ya upendo, kwamba Yeye anampenda mwanadamu jinsi Anavyojipenda, na Anampa kila mwanadamu wokovu na kamwe hamchukii mwanadamu, basi Angekuwa na uwezo wa kukamilisha kazi yake? Wakati Yesu Alikuja, Alisulubishwa msalabani, na Yeye Alijitoa kama sadaka kwa sababu ya wote wenye dhambi na kwa kujitoa Yeye mwenyewe madhabahuni. Yeye tayari Alikuwa Amemaliza kazi ya ukombozi na tayari Alikuwa Ametamatisha Enzi ya Neema, na hivyo ni nini kiini cha kurudia kazi ya enzi hiyo katika siku za mwisho? Je, kufanya kitu kimoja haitakuwa kukana kazi ya Yesu? Iwapo Mungu hatafanya kazi ya kusulubiwa awamu hii itakapofika, lakini Yeye Asalie mwenye mapenzi na Mungu wa huruma, je, anaweza kufikisha enzi hii mwisho? Je, Mungu mwenye upendo na mwenye huruma, si Angeweza kuhitimisha enzi hii? Katika kazi yake ya kuhitimisha enzi, tabia ya Mungu ni ile ya kuadibu na hukumu, ambayo inafichua yote ambayo si ya haki, na kuhukumu wanadamu hadharani, na kukamilisha wale ambao wanampenda kwa ukweli. Ni tabia tu kama hii ndiyo ambayo inaweza kufikisha enzi hii mwisho. Siku za mwisho tayari zimewadia. Kila kitu kitatengashwa kulingana na aina, na kitagawanywa katika makundi tofauti kulingana na asili yake. Huu ni wakati ambapo Mungu Atafichua matokeo na hatima ya binadamu. Kama mwanadamu hatashuhudia kuadibu na hukumu yake, basi hakutakuwepo na mbinu ya kufichua uasi na udhalimu wao mwanadamu. Ni kwa njia ya kuadibu na hukumu ndipo mwisho wa mambo yote yatafunuliwa. Mwanadamu huonyesha tu ukweli ulio ndani yake anapoadibiwa na kuhukumiwa. Mabaya yataekwa na mabaya, mema na mema, na wanadamu watatenganishwa kulingana na aina. Kupitia kuadibu na hukumu, mwisho wa mambo yote utafichuliwa, ili mabaya yaadhibiwe na mazuri yatunukiwe zawadi, na watu wote watakuwa wakunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Kazi hii yote inapaswa kutimizwa kupitia kuadibu kwa haki adhibu na hukumu. Kwa sababu upotovu wa mwanadamu umefika upeo wake na uasi wake umekua mbaya mno, ni haki ya tabia ya Mungu tu, ambayo hasa ni ya kuadibu na hukumu, na imefichuliwa kwa kipindi cha siku za mwisho, inayoweza kubadilisha na kukamilisha mwanadamu. Ni tabia hii pekee ambayo itafichua maovu na hivyo kuwaadhibu watu wote dhalimu. Kwa hivyo, tabia kama hii imejazwa umuhimu wa enzi, na ufunuo na maonyesho ya tabia yake ni kwa ajili ya kazi ya kila enzi mpya. Mungu hafichui tabia yake kiholela na bila umuhimu. Kama, wakati wa mwisho wa mwanadamu umefichuliwa katika kipindi cha siku za mwisho, Mungu bado anamfadhili binadamu kwa huruma na upendo usioisha, kama yeye bado ni wa kupenda mwanadamu, na kutompitisha mwanadamu katika hukumu ya haki, bali anamwonyesha stahamala, uvumilivu, na msamaha, kama bado Yeye anamsamehe mwanadamu bila kujali ubaya wa makosa anayofanya, bila hukumu yoyote ya haki: basi usimamizi wa Mungu ungetamatishwa lini? Ni wakati gani tabia kama hii itaweza kuwaongoza wanadamu katika hatima inayofaa? Chukua, kwa mfano, hakimu ambaye daima ni mwenye upendo, mwenye roho safi na mpole. Anawapenda watu bila kujali dhambi wanazozifanya, na ni mwenye upendo na stahamala kwa watu bila kujali hao ni nani. Kisha ni lini ambapo ataweza kufikia uamuzi wa haki? Katika siku za mwisho, ni hukumu ya haki tu inaweza kumtenganisha mwanadamu kulingana na aina yake na kumleta mwanadamu katika ufalme mpya. Kwa njia hii, enzi nzima inafikishwa mwisho kupitia kwa tabia ya Mungu iliyo ya haki ya hukumu na kuadibu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 82)
Kazi Yake katika mwili ni ya umuhimu mkubwa, ambao umezungumzwa kuhusiana na kazi, na Yule ambaye hatimaye anahitimisha kazi ni Mungu mwenye mwili, na sio Roho. Baadhi ya watu wanaamini kwamba Mungu wakati fulani anaweza kuja duniani na kumtokea mwanadamu, ambapo Atawahukumu wanadamu wote, akimjaribu mmoja baada ya mwingine bila mtu yeyote kupitwa. Wale wanaofikiri kwa namna hii hawafahamu hatua hii ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Mungu hamhukumu mwanadamu mmoja baada ya mwingine, na hamjaribu mwanadamu mmoja baada ya mwingine; kufanya hivyo hakungekuwa kazi ya hukumu. Je, upotovu wa wanadamu wote si ni sawa? Je, kiini cha wanadamu wote hakifanani? Kinachohukumiwa ni kiini cha mwanadamu kilichopotoka, kiini cha mwanadamu kilichopotoshwa na Shetani, na dhambi zote za mwanadamu. Mungu hahukumu makosa madogo madogo ya mwanadamu na yasiyokuwa na umuhimu. Kazi ya hukumu ni ya uwakilishi, na haifanywi mahususi kwa ajili ya mtu fulani. Badala yake, ni kazi ambayo kwayo kundi la watu wanahukumiwa ili kuiwakilisha hukumu ya wanadamu wote. Kwa Yeye mwenyewe kufanya kazi Yake katika kundi la watu, Mungu mwenye mwili anatumia kazi Yake ili kuwakilisha kazi ya wanadamu wote, ambayo inaenea taratibu. Kazi ya hukumu pia iko hivyo. Mungu hahukumu aina fulani ya mtu au kundi fulani la watu, bali anawahukumu wasio na haki wote miongoni mwa wanadamu—upinzani wa mwanadamu kwa Mungu, kwa mfano, au mwanadamu kutomcha Yeye, au kusababisha usumbufu katika kazi ya Mungu, na kadhalika. Kile kinachohukumiwa ni kiini cha mwanadamu cha kumpinga Mungu, na kazi hii ni kazi ya ushindi ya siku za mwisho. Kazi na neno la Mungu mwenye mwili lililoshuhudiwa na mwanadamu ni kazi ya hukumu mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi wakati wa siku za mwisho, ambacho kilibuniwa na mwanadamu katika kipindi cha siku za nyuma. Kazi ambayo sasa inafanywa na Mungu mwenye mwili ni hukumu yenyewe mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi. Mungu mwenye mwili wa leo ni Yule Mungu anayewahukumu wanadamu wote wakati wa siku za mwisho. Mwili huu na kazi, neno, na tabia Yake yote, vyote ni ujumla Wake. Ingawa mawanda ya kazi Yake ni finyu, na hayahusishi moja kwa moja ulimwengu wote, kiini cha kazi ya hukumu ni hukumu ya moja kwa moja kwa wanadamu wote; si kazi inayofanywa kwa ajili ya watu weteule Uchina tu, au kwa ajili ya idadi ndogo ya watu. Wakati wa kazi ya Mungu mwenye mwili, ingawa mawanda ya kazi hii hayahusishi ulimwengu mzima, inawakilisha kazi ya ulimwengu mzima na, baada ya kuhitimisha kazi ndani ya mawanda ya mwili Wake, Ataipanua kazi hii mara moja katika ulimwengu mzima, kwa namna ile ile, injili ya Yesu ilienea ulimwengu mzima baada ya kufufuka Kwake na kupaa mbinguni. Bila kujali endapo ni kazi ya Roho au ni kazi ya mwili, ni kazi ambayo inafanywa ndani ya mawanda finyu, lakini ambayo inauwakilisha ulimwengu mzima. Wakati wa siku za mwisho, Mungu anaonekana kufanya kazi Yake kwa kutumia utambulisho Wake wa Mungu mwenye mwili, na Mungu mwenye mwili ni Mungu anayemhukumu mwanadamu mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi. Bila kujali endapo ni Roho au mwili, Yule ambaye anafanya kazi ya hukumu ni Mungu anayemhukumu mwanadamu katika siku za mwisho. Hii inafasiliwa kwa kutegemeza kwa kazi Yake, na haifasiliwi kulingana na umbo Lake la nje au sababu nyinginezo. Ingawa mwanadamu ana dhana za maneno haya, hakuna anayeweza kukana ukweli wa hukumu ya Mungu mwenye mwili na kuwashinda wanadamu wote. Bila kujali ni jinsi gani binadamu anafikiri kuuhusu, ukweli ni, baada ya yote, ukweli tu. Hukuna anayeweza kusema “Kazi imefanywa na Mungu lakini mwili si Mungu.” Huu ni upuuzi, maana kazi hii haiwezi kufanywa na mtu yeyote isipokuwa Mungu mwenye mwili. Kwa kuwa kazi hii imekwishakamilika, kufuatia kazi hii, kazi ya hukumu ya Mungu kwa mwanadamu haitatokea kwa mara ya pili; Mungu katika kupata mwili Kwake mara ya pili amekwishaikamilisha kazi yote ya usimamizi, na hakutakuwa na hatua ya nne ya kazi ya Mungu. Kwa sababu yule anayehukumiwa ni mwanadamu, mwanadamu ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa, na sio roho ya Shetani ambayo inahukumiwa moja kwa moja, kazi ya hukumu haifanywi katika ulimwengu wa roho, bali miongoni mwa wanadamu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 83)
Hakuna anayefaa zaidi na anayestahili, kuliko Mungu mwenye mwili kwa ajili ya kuhukumu upotovu wa mwili wa mwanadamu. Ikiwa hukumu ingefanywa moja kwa moja na Roho wa Mungu, basi isingekuwa inajumuisha wote. Aidha, kazi kama hiyo itakuwa vigumu kwa mwanadamu kuikubali, maana Roho hawezi kukutana uso kwa uso na mwanadamu, na kwa sababu hii, matokeo hayawezi kuwa ya haraka, sembuse mwanadamu hataweza kuona kwa uwazi kabisa tabia ya Mungu isiyokosewa. Shetani anaweza tu kushindwa kabisa ikiwa Mungu mwenye mwili anahukumu upotovu wa mwanadamu. Kuwa sawa na mwanadamu akiwa na ubinadamu wa kawaida, Mungu mwenye mwili anaweza kumhukumu mwanadamu asiye na haki; hii ni ishara ya utakatifu Wake wa ndani na hali Yake ya kutokuwa wa kawaida. Ni Mungu pekee ndiye anayestahili, na aliye katika nafasi ya kumhukumu mwanadamu, maana Ana ukweli, na mwenye haki, na kwa hivyo Ana uwezo wa kumhukumu mwanadamu. Wale ambao hawana ukweli na haki hawafai kuwahukumu wengine. Ikiwa kazi hii ingefanywa na Roho wa Mungu, basi usingekuwa ushindi dhidi ya Shetani. Roho kiasili huwa ameinuliwa sana kuliko viumbe wenye mwili wa kufa, na Roho wa Mungu ni mtakatifu kwa asili, na anaushinda mwili. Ikiwa Roho angefanya kazi hii moja kwa moja, Asingeweza kuhukumu kutotii kote kwa mwanadamu, na asingeweza kufichua hali nzima ya mwanadamu ya kutokuwa na haki. Kwa maana kazi ya hukumu pia inafanywa kwa mitazamo ya mwanadamu juu ya Mungu, na mwanadamu hajawahi kuwa na dhana yoyote juu ya Roho, na hivyo Roho hana uwezo wa kufunua hali ya mwanadamu ya kutokuwa na haki, wala kuweza kuweka wazi kabisa hali hiyo ya kutokuwa na haki. Mungu mwenye mwili ni adui wa wale wote wasiomjua. Kupitia kuhukumu dhana za mwanadamu na kumpinga, Anafunua hali yote ya kutotii ya mwanadamu. Matokeo ya kazi Yake katika mwili yapo dhahiri zaidi kuliko yale ya kazi ya Roho. Na hivyo, hukumu ya wanadamu wote haifanywi moja kwa moja na Roho, bali ni kazi ya Mungu mwenye mwili. Mungu mwenye mwili anaweza kuonekana na kuguswa na mwanadamu, na Mungu mwenye mwili anaweza kumshinda kabisa mwanadamu. Katika uhusiano wake na Mungu mwenye mwili, mwanadamu huwa anapiga hatua kutoka katika upinzani na kuwa mtii, kutoka katika mateso na kukubaliwa, kutoka katika mitazamo na kuwa na maarifa, na kutoka kukataliwa hadi upendo. Haya ni matokeo ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Mwanadamu anaokolewa tu kwa kukubali hukumu Yake, bali hatua kwa hatua tu atamwelewa taratibu kupitia neno la mdomo Wake, ametwaliwa na Yeye wakati wa upinzani wake Kwake, na anapata uzima kutoka Kwake wakati wa kukubali kuadibu Kwake. Hii yote ni kazi ya Mungu mwenye mwili, na sio kazi ya Mungu katika utambulisho Wake kama Roho. Kazi inayofanywa na Mungu mwenye mwili ni kazi kubwa sana, na ni kazi ya kina sana, na sehemu muhimu ya hatua tatu za kazi ya Mungu ni hatua mbili za kazi ya kupata mwili. Upotovu wa kina wa mwanadamu ni kikwazo kikubwa sana katika kazi ya Mungu mwenye mwili. Hasa, kazi inayofanywa kwa watu wa siku za mwisho ni ngumu sana, na mazingira ni ya uhasama, na ubora wa tabia ya kila aina ya mwanadamu ni duni sana. Lakini mwishoni mwa kazi hii, bado itapokea matokeo mazuri, bila dosari yoyote; haya ni matokeo ya kazi ya mwili, na matokeo haya yanashawishi sana kuliko kazi ile ya Roho. Hatua tatu za kazi ya Mungu zitahitimishwa katika mwili, na lazima zikamilishwe na Mungu mwenye mwili. Kazi muhimu sana imefanywa katika mwili, na wokovu wa mwanadamu ni lazima ufanywe na Mungu mwenye mwili. Ingawa binadamu wote wanahisi kwamba Mungu katika mwili hahusiani na mwanadamu, kwa kweli ni kuwa mwili huu unahusiana na majaliwa na uwepo wa wanadamu wote.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 84)
Leo Mungu anawahukumu, na kuwaadibu, na kuwashutumu, lakini jueni kwamba shutuma yako ni ili kukufanya kuweza kujijua. Shutuma, laana, hukumu, kuadibu—haya yote ni ili kwamba uweze kujijua, ili tabia yako iweze kubadilika, na, zaidi ya hayo, ili uweze kujua thamani yako, na kutambua kwamba vitendo vyote vya Mungu ni vyenye haki, na kulingana na tabia Yake na mahitaji ya kazi Yake, kwamba Anafanya kazi kulingana na mpango Wake kwa wokovu wa mwanadamu, na kwamba Yeye ndiye Mungu mwenye haki anayempenda mwanadamu, na kumwokoa mwanadamu, na Anayemhukumu na kumwadibu mwanadamu. Kama utajua tu kwamba wewe ni mwenye hadhi ya chini, kwamba umepotoka na hutii, lakini hujui kwamba Mungu angependa kuweka wazi wokovu Wake kupitia kwa hukumu na kuadibu ambako Anafanya ndani yako leo, basi huna njia yoyote ya kupitia haya, isitoshe huwezi kuendelea mbele. Mungu hajaja kuua, au kuangamiza, lakini kuhukumu, kulaani, kuadibu, na kuokoa. Kabla ya hitimisho ya mpango Wake wa usimamizi wa miaka 6,000—kabla ya Yeye kuweka wazi mwisho wa kila aina ya binadamu—kazi ya Mungu ulimwenguni utakuwa kwa ajili ya wokovu, yote haya ni ili kuwafanya wale wanaompenda Yeye kukamilika kabisa, na kuwarejesha katika utawala Wake. Bila kujali jinsi ambavyo Mungu huwaokoa watu, yote hufanywa kwa kuwafanya wajitenge na asili yao ya zamani ya kishetani; yaani, Yeye huwaokoa kwa kuwafanya watafute uzima. Wasipotafuta uzima basi hawatakuwa na njia yoyote ya kukubali wokovu wa Mungu. Wokovu ni kazi ya Mungu Mwenyewe na kutafuta uzima ni kitu ambacho mwanadamu anapaswa kumiliki ili kupokea wokovu. Kwenye macho ya mwanadamu, wokovu ni upendo wa Mungu, na upendo wa Mungu hauwezi kuwa kuadibu, kuhukumu, na kulaani; wokovu lazima uwe na upendo, huruma, na, zaidi ya hayo, maneno ya faraja, na lazima wokovu uwe na baraka zisizo na mipaka kutoka kwa Mungu. Watu husadiki kwamba wakati Mungu anapomwokoa mwanadamu Anafanya hivyo kwa kumgusa kwa baraka na neema Zake, ili kwamba waweze kumpa Mungu mioyo yao. Hivyo ni kusema, Yeye kumgusa mwanadamu ni kumwokoa. Aina hii ya wokovu inafanywa kwa kufanya makubaliano. Pale tu ambapo Mungu atampa yeye mara mia ndipo mwanadamu atatiimbele ya jina la Mungu, na kulenga kuwa na mienendo mizuri mbele ya Mungu na kumletea Yeye utukufu. Haya si mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu. Mungu amekuja kufanya kazi ulimwenguni ili kumwokoa mwanadamu aliyepotoka—hakuna uongo katika haya; kama upo, Asingefanya kazi Yake yeye Mwenyewe. Kitambo, mbinu Zake za wokovu zilikuwa kuonyesha upendo na huruma mkuu, kiasi cha kwamba Alijitolea Yake yote kwa Shetani ili naye aweze kuwapata wanadamu wote. Leo haifanani kamwe na kitambo: Wokovu uliopewa leo unatokea wakati wa siku za mwisho, wakati wa uainishaji wa kila mmoja kulingana na aina yake; mbinu za wokovu wako si upendo wala huruma, lakini kuadibu na hukumu ili mwanadamu aweze kuokolewa kabisa. Hivyo basi, kila kitu unachopokea ni kuadibu, hukumu, na kupiga bila huruma, lakini jua kwamba katika kupiga huku kusiko na huruma hakuna hata adhabu ndogo zaidi, jua kwamba licha ya namna ambavyo maneno haya yanavyoweza kuwa makali, kile kinachokupata ni maneno machache yanayoonekana kutokuwa na huruma kabisa kwako, na jua kwamba, licha ya namna ambavyo hasira Yangu itakavyokuwa, kile kitakachokujia bado ni maneno ya mafunzo, na sinuii kukudhuru, au kukuua. Je, haya yote ni ukweli, sivyo? Jua kwamba leo, iwe hukumu ya haki au usafishaji na adhabu visivyo na huruma, yote haya ni kwa minajili ya wokovu. Haijalishi kama leo kila anaainishwa kulingana na aina yake, ama makundi ya wanadamu yanafichuliwa, matamko yote ya Mungu na kazi ni kwa ajili ya kuwaokoa wale wanaompenda Mungu kwa dhati. Kuhukumu kwa haki ni kwa ajili ya kumtakasa mwanadamu, utakasaji usio na huruma ni kwa ajili ya kumsafisha mwanadamu, maneno makali au kuadibu yote ni kwa ajili ya kutakasa, na kwa minajili ya wokovu. Na hivyo, mbinu ya leo ya wokovu haifanani na ya kitambo. Leo, kuhukumu kwa haki kunakuokoa wewe, na ni zana nzuri pia ya kumuainisha kila mmoja wenu kulingana na aina, na kuadibu kusiko na huruma kunawaletea wokovu mkubwa—na ni kipi ambacho unahitajika kusema mbele ya kuadibu na kuhukumu huku? Je, hujafurahia wokovu kutoka mwanzo hadi mwisho? Nyote mmeona Mungu mwenye mwili na kutambua kudura na hekima Yake; zaidi ya hayo, umepitia hali ya kupigwa na kufundishwa nidhamu mara kwa mara. Lakini je, hujapokea pia neema kubwa? Je, baraka zako si kubwa zaidi kuliko za mtu yeyote mwingine? Neema zako ni nyingi zaidi kuliko utukufu na utajiri uliofurahiwa na Sulemani! Hebu fikiria: Kama nia Yangu ya kuja ulimwenguni ingekuwa ni kushutumu na kukuadhibu wewe, na wala si kukuokoa, je, siku zako zingedumu kwa muda mrefu? Mngeweza, enyi viumbe wenye dhambi wa mwili na damu, kuishi hadi leo? Kama ingekuwa tu ni kwa ajili ya kuwaadhibu nyinyi, kwa nini Nikawa mwili na kuanza kushughulikia shughuli kubwa kama hiyo? Je, kuwaadhibu ninyi wanadamu wa kufa hakuwezi kufanywa kwa kutamka neon moja tu? Ningekuwa bado na haja ya kuwaangamiza baada ya kuwashutumu kwa makusudi? Je, bado hamwamini haya maneno Yangu? Ningeweza kumwokoa mwanadamu kupitia tu kwa upendo na huruma? Au Ningetumia tu kusulubishwa kwa minajili ya kumwokoa mwanadamu? Je, tabia Yangu yenye haki si nzuri zaidi ya kumfanya mwanadamu kuwa mtiifu kabisa? Je, haiwezi kabisa kumwokoa mwanadamu zaidi?
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu ya Kumletea Mwanadamu Wokovu
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 85)
Ingawa maneno Yangu yanaweza kuwa makali, yote yanasemwa kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, kwa kuwa Ninazungumza tu maneno na sio kuuadhibu mwili wa mwanadamu. Maneno haya humsababisha mwanadamu kuishi katika nuru, kujua kwamba mwanga upo, kujua kwamba mwanga ni wa thamani, hata zaidi kujua jinsi maneno haya yalivyo na manufaa kwa mtu, na kujua kwamba Mungu ni wokovu. Ingawa Nimesema maneno mengi ya kuadibu na hukumu, hayajafanywa kwako katika vitendo. Nimekuja kufanya kazi Yangu, kuzungumza maneno Yangu na, ingawa maneno Yangu yanaweza kuwa magumu, yanasemwa kwa hukumu ya upotovu na uasi wako. Madhumuni Yangu ya kufanya hili yanabaki kumwokoa mtu kutoka kwa utawala wa Shetani, kutumia maneno Yangu ili kumwokoa mwanadamu; Kusudi Langu sio kumdhuru mwanadamu kwa maneno Yangu. Maneno Yangu ni makali ili matokeo yaweze kupatikana kutoka katika Kazi Yangu. Ni katika kufanya kazi kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kujijua na anaweza kujitenga mbali na tabia yake ya uasi. Umuhimu mkubwa zaidi wa kazi ya maneno ni kuwaruhusu watu kuweza kutia katika matendo ukweli baada ya kuuelewa ukweli, kutimiza mabadiliko katika tabia yao, na kutimiza maarifa kuhusu wao wenyewe na kazi ya Mungu. Mbinu za kufanya kazi tu kupitia kwa kuongea ndizo zinazoweza kuleta mawasiliano kuhusu uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu, maneno tu ndiyo yanayoweza kuelezea ukweli. Kufanya kazi kwa njia hii ndiyo mbinu bora zaidi ya kumshinda mwanadamu; mbali na matamko ya maneno, hakuna mbinu nyingine inayoweza kumpatia mwanadamu uelewa wa wazi zaidi wa ukweli na kazi ya Mungu, na hivyo basi katika awamu Yake ya mwisho ya kazi, Mungu anazungumza naye mwanadamu ili kuweza kuwa wazi kwa mwanadamu kuhusu ukweli na siri zote ambazo haelewi, na hivyo basi kumruhusu kufaidi njia ya kweli na uzima kutoka kwa Mungu na kisha kutosheleza mapenzi ya Mungu. Madhumuni ya kazi ya Mungu juu ya mwanadamu ni ili aweze kukidhi mapenzi ya Mungu na yote yamefanywa kumwokoa mwanadamu, kwa hivyo wakati wa wokovu wake wa mwanadamu Yeye hafanyi kazi ya kumwadibu mtu. Wakati wa wokovu wa mwanadamu, Mungu haadhibu maovu au kulipa mema, wala Yeye hafunui hatima ya aina zote za watu. Badala yake, ni baada tu ya hatua ya mwisho ya kazi Yake kukamilishwa ndipo basi Atafanya kazi ya kuadhibu maovu na kulipa mazuri, na kisha basi ndipo Atafunua mwisho wa aina zote za watu. Wale ambao wanaadhibiwa hakika hawataweza kuokolewa, wakati wale waliookolewa watakuwa wale ambao wamepata wokovu wa Mungu wakati wa wokovu Wake wa mwanadamu. Wakati wa kazi ya Mungu ya wokovu, wale wote ambao wanaweza kuokolewa wataokolewa kwa upeo wa juu zaidi, hakuna hata mmoja wao atakayeachwa, kwa kuwa kusudi la kazi ya Mungu ni kumwokoa mwanadamu. Wote ambao, wakati wa wokovu wa Mungu wa mwanadamu, hawawezi kufikia mabadiliko katika tabia zao, wote ambao hawawezi kumtii Mungu kabisa, wote watakuwa walengwa wa adhabu. Hatua hii ya kazi—kazi ya maneno—humwekea wazi mwanadamu njia na siri zote ambazo haelewi, ili mwanadamu aweze kuelewa mapenzi ya Mungu na mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu, ili aweze kuwa katika ile hali ya kutia katika matendo maneno ya Mungu na kutimiza mabadiliko hayo katika tabia yake. Mungu huyatumia maneno tu kufanya kazi Yake, na hawaadhibu watu kwa sababu ni waasi kidogo, kwa sababu sasa ndio wakati wa kazi ya wokovu. Kama kila mtu ambaye alikuwa muasi angeadhibiwa, basi hakuna mtu ambaye angepata fursa ya kuokolewa; wote wangeadhibiwa na kuanguka kuzimuni. Kusudi la maneno ya yanayomhukumu mtu ni kumwezesha kujitambua na kumtii Mungu; sio kwao kuadhibiwa kwa njia ya hukumu ya maneno. Wakati wa kazi ya maneno, watu wengi watafunua uasi wao na kutotii kwao, na wataweka wazi kutotii kwao kwa Mungu mwenye mwili. Lakini Yeye hatawaadhibu watu hawa wote kwa sababu ya hili, badala yake Atawatupa kando wale ambao wamepotoka kabisa na ambao hawawezi kuokolewa. Atautoa mwili wao kwa Shetani, na katika hali kadhaa, kumaliza mwili wao. Wale ambao wanaachwa wataendelea kufuata na kupitia kushughulikiwa na kupogolewa. Ikiwa wanapofuata hawawezi kukubali kushughulikiwa na kupogolewa na wanazidi kupotoka, basi watu hawa watapoteza nafasi zao za wokovu. Kila mtu ambaye amekubali ushindi wa maneno atakuwa na nafasi nzuri ya wokovu. Wokovu wa Mungu wa kila mmoja wa watu hawa huwaonyesha upole Wake mkubwa, kumaanisha kwamba wanaonyeshwa uvumilivu mkubwa. Mradi watu warudi kutokakatika njia mbaya, mradi kama waweze kutubu, basi Mungu atawapa fursa ya kupata wokovu wake. Watu wanapoasi dhidi ya Mungu kwanza, Mungu hana hamu ya kuwaua, lakini badala yake Anafanya yote Anayoweza kuwaokoa. Ikiwa mtu kwa kweli hana nafasi ya wokovu, basi Mungu atamtupa pembeni. Kwamba Mungu si mwepesi wa kumwadhibu mtu ni kwa sababu Anataka kuwaokoa wale wote ambao wanaweza kuokolewa. Yeye huwahukumu, huwapa nuru na kuwaongoza watu tu kwa maneno, na Hatumii fimbo kuwaua. Kutumia maneno kuwaokoa watu ni kusudi na umuhimu wa hatua ya mwisho ya kazi.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu ya Kumletea Mwanadamu Wokovu
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 86)
Mungu anafanya kazi ya hukumu na kuadibu ili kwamba mwanadamu amjue, na kwa ajili ya ushuhuda Wake. Bila hukumu Yake ya tabia potovu ya mwanadamu, basi mwanadamu hangeweza kujua tabia Yake ya haki isiyoruhusu kosa lolote, na hangeweza kubadili ufahamu Wake wa Mungu kuwa mpya. Kwa ajili ya ushuhuda Wake, na kwa ajili ya usimamizi Wake, Anafanya ukamilifu Wake kuwa wazi kwa kila mtu, hivyo kumwezesha mwanadamu kupata ufahamu wa Mungu, na kubadili tabia yake, na kuwa na ushuhuda mkuu kwa Mungu kupitia kuonekana kwa Mungu wa hadharani. Mabadiliko yanafanikishwa kwa tabia ya mwanadamu kupitia njia tofauti ya kazi ya Mungu; bila mabadiliko ya aina hii katika tabia ya mwanadamu, mwanadamu hangeweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na hangekuwa wa kuupendeza moyo wa Mungu. Mabadiliko katika tabia ya mwanadamu yanaashiria kwamba mwanadamu amejiweka huru kutokana na minyororo ya Shetani, amejiweka huru kutokana na ushawishi wa giza, na kwa kweli amekuwa mfano na kifaa cha kujaribiwa cha kazi ya Mungu, amekuwa shahidi wa kweli wa Mungu na mtu aliye wa kuupendeza moyo wa Mungu. Leo hii, Mungu mwenye mwili Amekuja kufanya kazi Yake duniani, na Anahitaji kwamba mwanadamu apate ufahamu kumhusu, aweze kumtii, awe na ushuhuda Kwake—aweze kujua kazi Yake ya matendo na ya kawaida, atii maneno Yake yote na kazi ambayo haiambatani na mawazo ya mwanadamu, na kuwa na ushuhuda kwa kazi Yake yote ya kumwokoa mwanadamu, na matendo yote Anayofanya ya kumshinda mwanadamu. Wale walio na ushuhuda kwa Mungu lazima wawe na ufahamu wa Mungu; ni aina hii tu ya ushuhuda ndio ulio sahihi, na wa kweli, na ni aina hii tu ya ushuhuda ndio unaoweza kumpa Shetani aibu. Mungu Anawatumia wale waliomjua baada ya kupitia hukumu Yake na kuadibu, ushughulikiaji na upogoaji, kuwa na ushuhuda Kwake. Anawatumia wale waliopotoshwa na Shetani kumtolea Yeye ushuhuda, na vilevile Anawatumia wale ambao tabia yao imebadilika, na wale basi ambao wamepokea baraka Zake, kumtolea ushuhuda. Yeye hana haja na mwanadamu kumsifu kwa maneno tu, wala hana hitaji lolote la sifa na ushuhuda kutoka kwa namna ya Shetani, ambao hawajaokolewa na Yeye. Ni wale tu wanaomjua Mungu ndio wanaohitimu kumtolea Mungu ushuhuda, na ni wale tu ambao tabia zao zimebadilika ndio wanaofaa kumshuhudia Mungu, na Mungu hatamruhusu mwanadamu kwa makusudi aliletee jina Lake aibu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 87)
Ni kupitia nini ndiyo ukamilishaji wa Mungu kwa mwanadamu hutimizwa? Kupitia tabia Yake yenye haki. Tabia ya Mungu hasa huwa na haki, ghadhabu, uadhama, hukumu, na laana, na ukamilishaji Wake wa mwanadamu hasa ni kupitia hukumu. Watu wengine hawaelewi, na huuliza ni kwa nini Mungu anaweza tu kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu kupitia hukumu na laana. Wao husema, “Kama Mungu angemlaani mwanadamu, si mwanadamu angekufa? Kama Mungu angemhukumu mwanadamu, si mwanadamu angelaaniwa? Basi anawezaje hata hivyo kufanywa mkamilifu?” Hayo ndiyo maneno ya watu wasioijua kazi ya Mungu. Kile ambacho Mungu hulaani ni uasi wa mwanadamu, na kile Anachohukumu ni dhambi za mwanadamu. Ingawa Yeye hunena kwa ukali, na bila kiwango cha hisi hata kidogo, Yeye hufichua yote yaliyo ndani ya mwanadamu, na kupitia maneno haya makali Yeye hufichua kile kilicho muhimu ndani ya mwanadamu, lakini kupitia hukumu kama hiyo, Yeye humpa mwanadamu ufahamu mkubwa wa kiini cha mwili, na hivyo mwanadamu hujitiisha chini ya utii mbele za Mungu. Mwili wa mwanadamu ni wa dhambi, na wa Shetani, ni wa kutotii, na chombo cha kuadibu kwa Mungu—na kwa hiyo, ili kumruhusu mwanadamu kujijua, maneno ya hukumu ya Mungu lazima yamfike na lazima kila aina ya usafishaji itumike; ni wakati huo tu ndiyo kazi ya Mungu inaweza kuwa ya kufaa.
Kutokana na maneno yaliyonenwa na Mungu inaweza kuonekana kwamba tayari Ameulaani mwili wa mwanadamu. Je, haya maneno, basi, ni maneno ya laana? Maneno yaliyonenwa na Mungu hufichua tabia halisi ya mwanadamu, na kupitia ufichuzi kama huo anahukumiwa, na anapoona kwamba hawezi kuyaridhisha mapenzi ya Mungu, ndani anahisi huzuni na majuto, anahisi kwamba anapaswa kumshukuru Mungu sana, na asiyetosha kwa ajili mapenzi ya Mungu. Kuna nyakati ambapo Roho wa Mungu hukufundisha nidhamu kutoka ndani, na nidhamu hii hutoka kwa hukumu ya Mungu; kuna nyakati ambapo Mungu hukushutumu na kuuficha uso Wake kutoka kwako, wakati ambapo hakusikilizi, na Hafanyi kazi ndani yako, akikuadibu bila sauti ili kukusafisha. Kazi ya Mungu ndani ya mwanadamu ni hasa ili kuweka wazi tabia Yake yenye haki. Ni ushuhuda gani ambao mwanadamu hatimaye huwa nao kwa Mungu? Yeye hushuhudia kwamba Mungu ni Mungu mwenye haki, kwamba tabia yake ni haki, ghadhabu, kuadibu, na hukumu; mwanadamu hushuhudia kwa tabia yenye haki ya Mungu. Mungu hutumia hukumu Yake kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, Amekuwa Akimpenda mwanadamu, na kumwokoa mwanadamu—lakini ni kiasi gani kiko ndani ya upendo Wake? Kuna hukumu, uadhama, ghadhabu, na laana. Ingawa Mungu alimlaani mwanadamu katika wakati uliopita, Hakumtupa mwanadamu kabisa ndani ya shimo la kuzimu, lakini Alitumia njia hiyo kuisafisha imani ya mwanadamu; Hakumuua mwanadamu, lakini alitenda ili kumfanya mwanadamu awe mkamilifu. Kiini cha mwili ni kile ambacho ni cha Shetani—Mungu alikisema sahihi kabisa—lakini ukweli unaotekelezwa na Mungu haukamilishwi kufuatana na maneno Yake. Yeye hukulaani ili uweze kumpenda, na ili uweze kujua kiini cha mwili; Yeye hukuadibu ili uweze kuamshwa, kukuruhusu wewe ujue kasoro zilizo ndani yako, na kujua kutostahili kabisa kwa mwanadamu. Hivyo, laana za Mungu, hukumu Yake, na uadhama na ghadhabu Yake—yote ni kwa ajili ya kumfanya mwanadamu awe mkamilifu. Yote ambayo Mungu anafanya leo, na tabia yenye haki ambayo Yeye huifanya kuwa wazi ndani yenu—yote ni kwa ajili ya kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, na huo ndio upendo wa Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 88)
Katika dhana za mwanadamu za kitamaduni, upendo wa Mungu ni neema Yake, fadhili, na huruma kwa udhaifu wa mwanadamu. Ingawa mambo haya pia ni upendo wa Mungu, yanaegemea upande mmoja sana, na si njia za msingi ambazo kwazo Mungu humfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Wakati ambapo watu wengine wameanza tu kumwamini Mungu, ni kwa sababu ya ugonjwa. Ugonjwa huu ni neema ya Mungu kwako; bila huo, hungemwamini Mungu, na kama hungemwamini Mungu basi hungefika umbali huu—na hivyo hata neema hii ni upendo wa Mungu. Katika wakati wa kumwamini Yesu, watu walifanya mengi ambayo hayakupendwa na Mungu kwa sababu hawakuelewa ukweli, lakini Mungu ana upendo na rehema, na Amemleta mwanadamu umbali huu, na ingawa mwanadamu haelewi chochote, bado Mungu humruhusu mwanadamu amfuate Yeye, na, zaidi ya hayo, Amemwongoza mwanadamu mpaka leo. Je, huu si upendo wa Mungu? Kile ambacho kinadhihirishwa katika tabia ya Mungu ni upendo wa Mungu—hili ni sahihi bila shaka! Wakati ambapo ujenzi wa kanisa ulifikia kilele chake, Mungu alifanya hatua ya kazi ya watendaji huduma na akamtupa mwanadamu katika shimo la kuzimu. Maneno ya wakati wa watendaji huduma yote yalikuwa laana: laana za mwili wako, laana za tabia yako potovu ya kishetani, na laana za mambo kukuhusu wewe ambayo hayayaridhishi mapenzi ya Mungu. Kazi iliyofanywa na Mungu katika hatua hiyo ilidhihirishwa kama uadhama, karibukaribu sana baadaye Mungu alitekeleza hatua ya kazi ya kuadibu, na kisha kukaja majaribio ya kifo. Katika kazi kama hiyo, mwanadamu aliona ghadhabu, uadhama, hukumu, na kuadibu kwa Mungu, lakini aliona pia neema ya Mungu, na upendo na rehema Yake; yote aliyofanya Mungu, na yote yaliyodhihirishwa kama tabia Yake, ulikuwa upendo wa mwanadamu, na yote ambayo Mungu alifanya yaliweza kutimiza mahitaji ya mwanadamu. Aliyafanya ili kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, na Alimkimu mwanadamu kadri ya kimo chake. Kama Mungu hangefanya hili, mwanadamu hangekuwa na uwezo wa kuja mbele za Mungu, na hangekuwa na njia ya kuujua uso wa kweli wa Mungu. Tangu wakati ambapo mwanadamu alianza kwa mara ya kwanza kumwamini Mungu mpaka leo, Mungu amemkimu mwanadamu polepole kwa mujibu wa kimo chake, ili kwamba, ndani, mwanadamu amekuja kumjua Yeye polepole. Ni kwa kuweza kufika leo tu ndiyo mwanadamu ametambua hasa vile hukumu ya Mungu ni ya ajabu. Hatua ya kazi ya watendaji huduma ilikuwa tokeo la kwanza la kazi ya laana tangu wakati wa uumbaji mpaka leo. Mwanadamu alilaaniwa kwenda katika shimo la kuzimu. Kama Mungu hangefanya hivyo, leo mwanadamu hangekuwa na ufahamu wa kweli wa Mungu; ilikuwa kupitia tu laana ya Mungu ndiyo mwanadamu alikutana rasmi na tabia ya Yake. Mwanadamu alifichuliwa kupitia majaribu ya watendaji huduma. Aliona kwamba uaminifu wake haukukubalika, kwamba kimo chake kilikuwa kidogo sana, kwamba hakuwa na uwezo wa kuridhisha mapenzi ya Mungu, na kwamba madai yake ya kumridhisha Mungu wakati wote yalikuwa maneno matupu tu. Ingawa katika hatua ya kazi ya watendaji huduma Mungu alimlaani mwanadamu, tukitazama nyuma leo, hatua hiyo ya kazi ya Mungu ilikuwa ya ajabu: Ilileta mgeuzo mkubwa kwa mwanadamu, na kusababisha mabadiliko makuu katika tabia yake ya maisha. Kabla ya wakati wa watendaji huduma, mwanadamu hakuelewa chochote kuhusu ukimbizaji wa maisha, ni nini maana ya kumwamini Mungu, au hekima ya kazi ya Mungu, wala hakufahamu kwamba kazi ya Mungu inaweza kumjaribu mwanadamu. Tangu wakati wa watendaji huduma mpaka leo, mwanadamu huona vile kazi ya Mungu ni ya ajabu, haiwezi kueleweka kwa mwanadamu, na akitumia akili yake hawezi kufikiria jinsi Mungu hufanya kazi, na pia huona vile kimo chake ni kidogo na kwamba kiasi kikubwa chake ni cha kutotii. Mungu alipomlaani mwanadamu, ilikuwa ili Atimize athari, na Hakumuua mwanadamu. Ingawa Alimlaani mwanadamu, Alifanya hivyo kupitia maneno, na laana Zake hazikumwangukia mwanadamu kwa kweli, kwani kile ambacho Mungu alilaani kilikuwa kutotii kwa mwanadamu, na kwa hiyo maneno ya laana Zake pia yalikuwa kwa ajili ya kumfanya mwanadamu awe mkamilifu. Kama Mungu atamhukumu mwanadamu au kumlaani, yote mawili humfanya mwanadamu kuwa mkamilifu: Yote mawili yanafanywa ili kukifanya kamili kile ambacho ni kichafu ndani ya mwanadamu. Kupitia njia hii mwanadamu anasafishwa, na kile ambacho kinakosekana ndani ya mwanadamu kinafanywa kamilifu kupitia maneno na kazi Yake. Kila hatua ya kazi ya Mungu—kama ni maneno makali, au hukumu, au kuadibu—humfanya mwanadamu kuwa mkamilifu, na inafaa kwa uhalisi. Kotekote katika enzi zote Mungu hajawahi kufanya kazi kama hii; leo, Yeye hufanya kazi ndani yenu ili muweze kufahamu hekima Yake. Ingawa mmepitia maumivu fulani ndani yenu, mioyo yenu inajisikia thabiti na kwa amani; ni baraka yenu kuweza kufurahia hatua hii ya kazi ya Mungu. Haijalishi kile mnachoweza kupata katika siku za baadaye, yote mnayoona kuhusu kazi ya Mungu ndani yenu leo ni upendo. Kama mwanadamu hapitii hukumu na kuadibu kwa Mungu, matendo yake na ari daima yatakuwa nje, na tabia yake daima itaendelea kutobadilika. Je, hii inahesabika kama kupatwa na Mungu? Leo, ingawa bado kuna mengi ndani ya mwanadamu ambayo ni yenye kiburi na yenye majivuno, tabia ya mwanadamu ni imara zaidi kuliko awali. Mungu kukushughulikia wewe ni ili kukuokoa, na ingawa unaweza kuhisi maumivu kidogo wakati huo, siku itafika ambapo kutatokea mabadiliko katika tabia yako. Wakati huo, utakumbuka ya nyuma na kuona vile kazi ya Mungu ni ya hekima, na huo utakuwa wakati ambao utaweza kufahamu kwa kweli mapenzi ya Mungu. Leo, kuna watu wengine ambao husema kwamba wanafahamu mapenzi ya Mungu—lakini hiyo si ya kweli kamwe, wao wanazungumza upuuzi, kwa sababu wakati huu bado hawajafahamu kama mapenzi ya Mungu ni kumwokoa mwanadamu au kumlaani mwanadamu. Labda huwezi kuliona kwa dhahiri sasa, lakini siku itafika ambapo utaona kwamba siku ya kutukuzwa kwa Mungu imefika, na uone jinsi ni ya maana kumpenda Mungu, ili utakuja kuyajua maisha ya binadamu, na mwili wako utaishi katika ulimwengu wa kumpenda Mungu, kwamba roho yako itawekwa huru, maisha yako yatajaa furaha, na kwamba daima utakuwa karibu na Mungu, na utamtegemea Mungu daima. Wakati huo, utajua kweli jinsi kazi ya Mungu ni ya thamani leo.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 89)
Kazi inayofanywa sasa ni kuwafanya watu kumtoroka Shetani, kutoroka babu zao wa kale. Hukumu zote kwa neno zinalenga kufichua tabia potovu ya binadamu na kuwawezesha watu kuelewa kiini cha maisha. Hukumu hizi zote zilizorudiwa zinapenyeza mioyo ya watu. Kila hukumu inaathiri kwa njia ya moja kwa moja hatima yao na inalenga kujeruhi mioyo yao ili waweze kuachilia yale mambo hayo yote na hivyo basi kuja kujua maisha, kuujua ulimwengu huu mchafu, na pia kujua hekima ya Mungu na uweza Wake na kujua mwanadamu huyu aliyepotoshwa na Shetani. Kadri aina hii ya kuadibu na kuhukumu inavyozidi, ndivyo moyo wa binadamu unavyoweza kujeruhiwa zaidi na ndivyo roho yake inavyoweza kuzinduliwa zaidi. Kuzindua roho za watu hawa waliopotoka pakubwa na kudanganywa kabisa ndiyo shabaha ya aina hii ya hukumu. Mwanadamu hana roho, yaani, roho yake ilikufa kitambo na hajui kwamba kuna Mbingu, hajui kwamba kuna Mungu, na bila shaka hajui kwamba yeye mwenyewe anang’ang’ana kwenye lindi kuu la kifo; anaweza kujuaje kwamba anaishi katika kuzimu hii yenye maovu hapa ulimwenguni? Angewezaje kujua kwamba maiti hii yake ambayo imeoza, kwa kupotoshwa na shetani, imeanguka Kuzimuni kwenye kifo? Angewezaje kujua kwamba kila kitu hapa ulimwenguni kimeharibiwa kitambo kiasi cha kutokarabatika na mwanadamu? Na angewezaje kujua kwamba Muumba amekuja ulimwenguni leo na anatafuta kundi la watu waliopotoka ambao Anaweza kuokoa? Hata baada ya mwanadamu kupitia kila usafishaji na hukumu inayowezekana, ufahamu wake wa chini unashtuka kwa shida na kwa kweli hauitikii chochote. Binadamu wamezoroteka kweli! Ingawa aina hii ya hukumu ni kama mvua katili ya mawe inyeshayo kutoka mbinguni, ni yenye manufaa makubwa zaidi kwa binadamu. Kama isingekuwa ya kuhukumu watu hivi, kusingekuwa na matokeo yoyote na haingewezekana kabisa kuwaokoa watu dhidi ya janga la umaskini. Kama isingekuwa kwa kazi hii, ingekuwa vigumu sana kwa watu kutoka Kuzimuni kwa sababu mioyo yao imekufa kitambo na roho zao kukanyagiwa kitambo na Shetani. Kuwaokoa nyinyi ambao mmeanguka kwenye kina kirefu cha uozo kunahitaji kuwaita kwa bidii sana, kuwahukumu kwa bidii sana, na kwa kufanya hivi tu ndipo mioyo hiyo yenu migumu itakapozinduka.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Waliokamilishwa Pekee Ndio Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 90)
Mungu alipata mwili katika mahali palipokuwa nyuma kimaendeleo na pachafu zaidi, na ni kwa njia hii tu ndiyo Mungu anaweza kuonyesha wazi tabia Yake yote iliyo takatifu na yenye haki. Na tabia Yake yenye haki inaonyeshwa kupitia nini? Inaonyeshwa Anapozihukumu dhambi za mwanadamu, Anapomhukumu Shetani, Anapochukia dhambi sana, na Anapowadharau maadui wanaompinga na kuasi dhidi Yake. Maneno Ninayonena leo ni kwa ajili ya kuzihukumu dhambi za mwanadamu, kuhukumu udhalimu wa mwanadamu, kulaani uasi wa mwanadamu. Upotovu na udanganyifu wa mwanadamu, maneno na vitendo vya mwanadamu—yote ambayo hayapatani na mapenzi ya Mungu lazima yatapitia hukumu, na uasi wa mwanadamu kushutumiwa kama dhambi. Maneno Yake yanahusu kanuni za hukumu; Yeye hutumia hukumu ya udhalimu wa mwanadamu, laana ya uasi wa mwanadamu, na mfichuo wa asili mbaya za mwanadamu ili kudhihirisha tabia Yake mwenyewe yenye haki. Utakatifu ni kielelezo cha tabia Yake yenye haki, na kwa kweli utakatifu wa Mungu ni tabia Yake yenye haki. Tabia zenu potovu ni muktadha wa maneno ya leo—Ninazitumia kunena na kuhukumu, na kutekeleza kazi ya ushindi. Hii pekee ndiyo kazi halisi, na hii pekee inadhihirisha kabisa utakatifu wa Mungu. Ikiwa hakuna dalili ya tabia potovu ndani yako, basi Mungu hatakuhukumu, wala hatakuonyesha tabia Yake yenye haki. Kwa kuwa unayo tabia potovu, Mungu hatakusamehe, na ni kwa njia hii ndiyo utakatifu Wake unaonyeshwa. Mungu angaliona kuwa uchafu na uasi wa mwanadamu vilikuwa vikubwa sana lakini Asinene au kukuhukumu, wala kukuadibu kwa ajili ya udhalimu wako, basi hii ingethibitisha kwamba Yeye si Mungu, kwa maana Asingeichukia dhambi; Angelikuwa mchafu sawasawa na mwanadamu. Leo, ni kwa sababu ya uchafu wako ndiyo Ninakuhukumu, na ni kwa sababu ya upotovu na uasi wako ndiyo Ninakuadibu. Mimi sijivunii nguvu Zangu kwenu au kuwadhulumu kwa makusudi; Ninafanya mambo haya kwa sababu ninyi, ambao mmezaliwa katika nchi hii ya uchafu, mmenajisiwa vikali kwa uchafu. Mmepoteza uadilifu na ubinadamu wenu kabisa na mmekuwa kama nguruwe waliozaliwa katika pembe chafu zaidi za ulimwengu, na kwa hiyo ni kwa sababu ya jambo hili ndiyo mnahukumiwa na ndiyo Ninawaachia huru hasira Yangu. Ni kwa sababu hasa ya hukumu hii ndiyo mmeweza kuona kuwa Mungu ndiye Mungu mwenye haki, na kwamba Mungu ndiye Mungu mtakatifu; ni kwa sababu hasa ya utakatifu Wake na haki Yake ndiyo Anawahukumu na kuachia huru hasira Yake juu yenu. Kwa sababu Anaweza kufichua tabia Yake yenye haki Aonapo uasi wa mwanadamu, na kwa sababu Anaweza kufichua utakatifu Wake anapoona uchafu wa mwanadamu, hii inatosha kuonyesha kuwa Yeye ndiye Mungu Mwenyewe ambaye ni mtakatifu na wa asili, na bado Anaishi katika nchi ya uchafu. Mungu angelikuwa mtu na kufuata mfano wa mwanadamu na kugaagaa na wanadamu katika matope machafu, basi kusingelikuwa na chochote kitakatifu kumhusu, na Asingelikuwa na tabia yenye haki, na kwa hiyo Asingelikuwa na haki ya kuhukumu uovu wa mwanadamu, wala Asingelikuwa na haki ya kutekeleza hukumu ya mwanadamu. Mtu angelimhukumu mtu mwingine, haingekuwa kana kwamba anajipiga kofi usoni? Watu ambao wote ni wachafu kwa kiwango sawa wanastahili vipi kuwahukumu wale ambao ni sawa na wao? Ni Mungu mtakatifu Mwenyewe pekee ndiye Anayeweza kuwahukumu wanadamu wote wachafu. Mwanadamu angewezaje kuhukumu dhambi za mwanadamu? Mwanadamu angewezaje kuona dhambi za mwanadamu, na mwanadamu angewezaje kuwa na sifa za kulaani dhambi hizi? Mungu Asingelikuwa na sifa ya kuzihukumu dhambi za mwanadamu, basi Angewezaje kuwa Mungu mwenye haki Mwenyewe? Tabia potovu za watu zinapofichuliwa, Mungu hunena ili Awahukumu watu, na ni hapo tu ndipo watu wanapoona kuwa Yeye ni mtakatifu. Anapomhukumu na kumwadibu mwanadamu kwa ajili ya dhambi zake, wakati huo wote Akizifichua dhambi za mwanadamu, hakuna mtu au kitu kinachoweza kuepuka hukumu hii; mambo yote ambayo ni machafu yanahukumiwa na Yeye, na ni kwa sababu hiyo tu ndiyo tabia Yake inaweza kusemwa kuwa yenye haki. Kama ingekuwa vinginevyo, ingewezaje kusemwa kwamba ninyi ni foili kwa jina na kwa kweli?
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi Athari za Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Zinavyotimizwa
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 91)
Kuna tofauti kubwa kati ya kazi iliyofanywa Israeli na kazi ya leo. Yehova aliyaongoza maisha ya Waisraeli, na hakukuwa na kuadibu na hukumu nyingi, kwa sababu wakati huo, watu walielewa kidogo sana kuhusu ulimwengu na walikuwa na tabia chache zilizokuwa potovu. Hapo zamani, Waisraeli walimtii Yehova kabisa. Alipowaambia wajenge madhabahu, walijenga madhabahu haraka; Alipowaambia wavae mavazi rasmi ya makuhani, walitii. Katika siku hizo, Yehova alikuwa kama mchungaji akilichunga kundi la kondoo, na kondoo wakifuata mwongozo wa mchungaji na kula nyasi katika malisho; Yehova aliyaongoza maisha yao, Akiwaongoza katika jinsi walivyokula, kuvalia, kuishi, na kusafiri. Huo haukuwa wakati wa kuweka wazi tabia ya Mungu, kwa kuwa wanadamu wa wakati huo walikuwa waliozaliwa karibuni; kulikuwa na wachache waliokuwa waasi na wapinzani, hakukuwa na uchafu mwingi kati ya wanadamu, na kwa hivyo watu hawangeweza kutenda kama foili kwa tabia ya Mungu. Ni kupitia watu ambao wanatoka katika nchi ya uchafu ndipo utakatifu wa Mungu unaonyeshwa; leo, Yeye hutumia uchafu ulioonyeshwa katika watu hawa wa nchi ya uchafu, naye Anahukumu, na kwa kufanya hivyo, kile Alicho kinafichuliwa katika hukumu Yake. Kwa nini Anahukumu? Anaweza kunena maneno ya hukumu kwa sababu Anadharau dhambi; Je, Angewezaje kukasirika sana hivyo ikiwa hakuchukia uasi wa wanadamu? Kusingekuwa na karaha ndani Yake, kusingekuwa na machukio, Asingejali uasi wa watu, basi hiyo ingethibitisha Yeye kuwa mchafu kama mwanadamu. Kwamba Yeye anaweza kumhukumu na kumwadibu mwanadamu ni kwa sababu Yeye huchukia uchafu, na Anachokichukia hakimo ndani Yake. Kama pia kungekuwa na upinzani na uasi ndani Yake, Asingewadharau wale ambao ni wapinzani na waasi. Kazi ya siku za mwisho ingekuwa ikifanywa Israeli, hakungekuwa na maana yoyote kwayo. Mbona kazi ya siku za mwisho inafanywa nchini China, mahali paovu na palipo nyuma kabisa kimaendeleo kuliko sehemu zote? Ni ili kuonyesha utakatifu na haki Yake. Kwa kifupi, kadri mahali palivyo paovu, ndivyo utakatifu wa Mungu unavyoweza kuonyeshwa wazi zaidi. Kwa kweli, yote haya ni kwa ajili ya kazi ya Mungu. Ni leo tu ndipo mnatambua kuwa Mungu ameshuka kutoka mbinguni ili Asimame kati yenu, Ameonyeshwa kupitia uchafu na uasi wenu, na ni wakati huu tu ndipo mnamjua Mungu. Je, hii siyo sifa kubwa zaidi? Kwa kweli, ninyi ni kikundi cha watu nchini China waliochaguliwa. Na kwa sababu mlichaguliwa na mmefurahia neema ya Mungu, na kwa sababu hamfai kufurahia neema kubwa kama hiyo, hii inathibitisha kwamba haya yote ni kuwapa sifa kubwa kabisa. Mungu amewatokea, na kuwaonyesha tabia Yake nzima iliyo takatifu, na Amewapa yote hayo, na kuwasababisha mfurahie baraka zote ambazo mnaweza kufurahia. Hamjaionja tu tabia ya Mungu yenye haki, lakini, zaidi ya hayo, mmeuonja wokovu wa Mungu, ukombozi wa Mungu na upendo wa Mungu usio na kikomo. Ninyi, wachafu zaidi ya wote, mmefurahia neema kubwa kama hii—je, hamjabarikiwa? Je, huku si Mungu kuwainua? Ninyi ni wa chini zaidi ya wote, kwa asili hamstahili kufurahia baraka kubwa kama hiyo, lakini Mungu anang’ang’ania kukuinua. Je, huoni aibu? Ikiwa huwezi kutekeleza wajibu wako, basi mwishowe utaaibika, nawe utajiadhibu. Leo, hufundishwi nidhamu, wala huadhibiwi; mwili wako uko salama salimini—lakini mwishowe, maneno haya yatakuaibisha. Hadi leo, bado Sijamwadibu mtu yeyote waziwazi; maneno Yangu yanaweza kuwa makali, lakini Ninawatendeaje watu? Ninawafariji, na kuwashawishi, na kuwakumbusha. Ninafanya hivi ili kuwaokoa tu. Je, kwa kweli hamwelewi mapenzi Yangu? Mnapaswa kuelewa Ninachosema, na kutiwa moyo nacho. Ni sasa tu ndipo kunao watu wengi wanaoelewa. Je, hii si baraka ya kuwa foili? Je, kuwa foili si jambo la kubarikiwa zaidi? Mwishowe, mnapoenda kueneza injili, mtasema hivi: “Sisi ni foili wa kawaida.” Watawauliza, “Inamaanisha nini kwamba ninyi ni foili wa kawaida?” Nanyi mtasema: “Sisi ni foili kwa kazi ya Mungu, na kwa nguvu Zake kuu. Tabia nzima ya Mungu yenye haki imefunuliwa kupitia uasi wetu; sisi ni vyombo vya kutumikia kwa kazi ya Mungu ya siku za mwisho, sisi ni viambatisho vya kazi Yake, na pia vifaa vya kazi hiyo.” Wanaposikia hivyo, watavutiwa sana. Baadaye, utasema: “Sisi ni vielelezo na mifano ya Mungu kukamilisha kazi ya ulimwengu wote, na ya ushindi Wake wa wanadamu wote. Iwe sisi ni watakatifu au wachafu, kwa jumla, bado tumebarikiwa zaidi kuliko ninyi, kwa maana tumemwona Mungu, na kupitia fursa ya Yeye kutushinda, nguvu kuu za Mungu zimeonyeshwa; ni kwa sababu tu sisi ni wachafu na waovu ndiyo tabia Yake yenye haki imetokea. Je, hivyo mnaweza kuishuhudia kazi ya Mungu ya siku za mwisho? Hamstahili! Hii ni Mungu kutuinua tu! Ingawa tunaweza kukosa kuwa wenye kiburi, tunaweza kumsifu Mungu kwa kujivunia, kwa kuwa hakuna mtu anayeweza kurithi ahadi kubwa kama hiyo, na hakuna mtu anayeweza kufurahia baraka kubwa kama hiyo. Tunashukuru sana kwamba sisi, ambao ni wachafu sana, tunaweza kufanya kazi kama foili wakati wa usimamizi wa Mungu.” Na wanapouliza, “Vielelezo na mifano ni nini?” unasema, “Sisi ni wanadamu waasi zaidi na wachafu zaidi; tumepotoshwa kwa kina kabisa na Shetani, nasi ni viumbe tulio nyuma kimaendeleo na duni zaidi kimwili. Sisi ni mifano bora ya wale ambao wametumiwa na Shetani. Leo, tumechaguliwa na Mungu kama wa kwanza kati ya wanadamu walioshindwa, na tumeona tabia ya Mungu yenye haki na kurithi ahadi Yake; tunatumiwa kuwashinda watu zaidi, kwa hiyo sisi ndio vielelezo na mifano ya wale wanaoshindwa kati ya wanadamu.” Hakuna ushuhuda bora zaidi kuliko maneno haya, na huu ndio uzoefu wako bora kabisa.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi Athari za Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Zinavyotimizwa
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 92)
Kazi ya kushinda inayofanywa kwenu nyie ni ya umuhimu mkubwa sana: Kwa upande mmoja, kusudi la hii kazi ni kukikamilisha kikundi cha watu, yaani, kuwakamilisha na kuwa kundi la washindi, kama kundi la kwanza la watu waliofanywa wakamilifu, yaani matunda ya kwanza. Kwa upande wa pili, ni kuruhusu viumbe wa Mungu kufurahia mapenzi ya Mungu, kupokea wokovu mkubwa wa Mungu, na kupokea wokovu kamili wa Mungu, na kumfanya mwanadamu kufurahia si tu huruma na ukarimu wa upendo, ila muhimu zaidi ni kuadibu na hukumu. Tangu uumbaji wa dunia hadi sasa, yote ambayo Mungu amefanya katika kazi Yake ni upendo, bila chuki yoyote kwa mwanadamu. Hata kuadibu na hukumu uliyoiona ni mapenzi pia, upendo wa kweli na wa dhati zaidi; upendo huu huwaongoza wanadamu kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu. Kwa upande wa tatu, ni kushuhudia mbele ya Shetani. Kwa upande wa nne, ni kuweka msingi wa kueneza kazi ya baadaye ya injili. Kazi yote Aliyoifanya ni kumwongoza mwanadamu kwenye njia sahihi ya maisha ya wanadamu, ili kwamba wawe na maisha ya kawaida ya wanadamu, kwani mwanadamu hajui jinsi ya kuishi. Bila uongozi kama huo, utaishi maisha tupu yasiyo na maana wala thamani, na kamwe hutajua jinsi ya kuwa mwanadamu wa kawaida. Huu ndio umuhimu mkuu wa kumshinda mwanadamu. Nyote ni wa ukoo wa Moabu. Kufanya kazi ya kushinda kwenu ni wokovu wenu mkuu. Nyinyi nyote mnaishi mahala pa dhambi na ufisadi; nyinyi nyote ni watu wapotovu na wenye dhambi. Leo hii hamwezi tu kumwona Mungu, ila la muhimu zaidi, mmepokea kuadibu na hukumu, mmepokea wokovu wa kina, yaani, mmepokea upendo mkubwa zaidi wa Mungu. Yote Ayafanyayo ni mapenzi ya dhati kwako; Hana nia mbaya. Anawahukumu kwa sababu ya dhambi zenu, ili kwamba mweze kujichunguza wenyewe na kupokea wokovu mkubwa. Haya yote hufanywa kwa kusudi la kumkamilisha mwanadamu. Tangu mwanzo hadi mwisho, Mungu amekuwa Akifanya kila Awezalo kumwokoa mwanadamu, na hakika hayuko tayari kuwaangamiza kabisa wanadamu Aliowaumba kwa mikono Yake Mwenyewe. Sasa Amekuja miongoni mwenu kufanya kazi; je, huu si wokovu zaidi? Je, Angalikuchukia, Angaliendelea kufanya kazi ya kiwango hicho cha juu ili kukuongoza wewe Mwenyewe? Ni kwa nini Ateseke hivyo? Mungu hawachukii wala hana nia mbaya juu yenu. Mnapaswa kufahamu kuwa mapenzi ya Mungu ndiyo mapenzi ya kweli zaidi. Anawaokoa kupitia hukumu kwa sababu tu ya uasi wa mwanadamu; la sivyo, hawangepata wokovu. Kwa kuwa hamjui jinsi ya kuishi, na mnaishi katika mahala pa ufisadi na dhambi na ni mapepo wenye ufisadi na uchafu, Hana moyo wa kuwaacha mpotoshwe zaidi; wala Hana moyo wa kutaka kuwaona mkiishi mahala pachafu kama hapa, mkikandamizwa na Shetani apendavyo, Hana moyo wa kuwaacha mtumbukie Kuzimu. Anataka tu kulipata hili kundi lenu na kuwakomboa vilivyo. Hili ndilo kusudi kuu la kufanya kazi ya kushinda miongoni mwenu—ni kwa ajili ya wokovu tu. Iwapo huwezi kuona kuwa kila kitu unachofanyiwa ni mapenzi na wokovu, ukidhani kuwa ni mbinu tu, njia ya kumtesa mwanadamu na kitu kisichoaminika, basi ni bora urudi duniani mwako uendelee kupata mateso na ugumu wa maisha! Ikiwa uko tayari kuwa kwenye mkondo huu na kufurahia hukumu hii na wokovu huu wa ajabu, na kufurahia baraka hizi ambazo haziwezi kupatikana kokote katika ulimwengu wa wanadamu, na kufurahia upendo huu, basi kuwa mzuri: Salia kwenye mkondo huu ili kukubali kazi ya ushindi ili uweze kufanywa mkamilifu. Leo, unaweza kupitia mateso na usafishaji kidogo kwa sababu ya hukumu ya Mungu, mateso haya ni ya thamani na ya maana. Japo kuadibu na hukumu ni usafishaji na ufichuzi usio na huruma kwa mwanadamu, uliokusudiwa kuadhibu dhambi zake na kuadhibu mwili wake, kazi hii haijanuiwa kukashifu na kuuzima mwili wake. Ufichuzi mkali wa neno ni kwa kusudi la kukuongoza kwenye njia sahihi. Ninyi wenyewe mmeipitia sana kazi hii na ni wazi, haijawaongoza kwenye njia mbaya! Yote ni ili kukufanya uishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na yote yanatimizwa na ubinadamu wako wa kawaida. Kila hatua ya kazi hufanywa kwa misingi ya mahitaji yako, kulingana na udhaifu wako, kulingana na kimo chako halisi, na hamjatwikwa mzigo msioweza kuubeba. Japo huwezi kuliona hili wazi kwa sasa, na unajihisi Ninakuwa mgumu kwako, japo unadhani kuwa Ninakuadibu na kukuhukumu na kukuadibu kila siku kwa kuwa Ninakuchukia, na ingawa unachokipokea ni kuadibu na hukumu, hali halisi ni kuwa yote ni mapenzi kwako, pia ni ulinzi mkubwa kwako. Ikiwa huwezi kung’amua maana ya ndani ya kazi hii, basi huna njia ya kuendelea katika uzoefu wako. Unapaswa kuliwazwa kwa sababu ya huo wokovu. Usikatae kuzirudia busara zako. Baada ya kusafiri umbali huu, unapaswa kuuona wazi umuhimu wa kazi hii ya kushinda. Hupaswi tena kushikilia mtazamo fulani kama huo!
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (4)
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 93)
Wanaoweza kusimama imara wakati wa kazi ya Mungu ya hukumu na kuadibu siku za mwisho—yaani, wakati wa kazi ya mwisho ya utakaso—watakuwa wale watakaoingia katika raha ya mwisho na Mungu; kwa hivyo, wanaoingia rahani wote watakuwa wametoka katika ushawishi wa shetani na kupokewa na Mungu baada tu ya kupitia kazi Yake ya mwisho ya utakaso. Hawa watu ambao hatimaye wamepokewa na Mungu wataingia katika raha ya mwisho. Kiini cha kazi ya Mungu ya kuadibu na hukumu ni kutakasa binadamu, na ni ya siku ya raha ya mwisho. Vinginevyo, binadamu wote hawataweza kufuata aina yao ama kuingia katika raha. Hii kazi ni njia ya pekee ya binadamu kuingia rahani. Kazi ya Mungu ya utakaso pekee ndiyo itatakasa udhalimu wa binadamu, na kazi Yake ya kuadibu na hukumu pekee ndiyo itadhihirisha hayo mambo yasiyotii miongoni mwa binadamu, hivyo kutenga wanaoweza kuokolewa kutoka wale wasioweza, na wale watakaobaki kutoka wale ambao hawatabaki. Kazi Yake itakapoisha, wale watu watakaoruhusiwa kubaki wote watatakaswa na kuingia katika hali ya juu zaidi ya ubinadamu ambapo watafurahia maisha ya pili ya binadamu ya ajabu zaidi duniani; kwa maneno mengine, wataingia katika siku ya binadamu ya raha na kuishi pamoja na Mungu. Baada ya wasioweza kubaki kupitia kuadibu na hukumu, umbo zao halisi zitafichuliwa kabisa; baada ya haya wote wataangamizwa na, kama Shetani, hawatakubaliwa tena kuishi duniani. Binadamu wa baadaye hawatakuwa tena na aina yoyote ya watu hawa; watu hawa hawafai kuingia eneo la raha ya mwisho, wala hawafai kuingia siku ya raha ambayo Mungu na mwanadamu watashiriki, kwani ni walengwa wa adhabu na ni waovu, na si watu wenye haki. Walikuwa wamekombolewa wakati mmoja, na pia walikuwa wamehukumiwa na kuadibiwa; walikuwa pia wamemhudumia Mungu wakati mmoja, lakini siku ya mwisho itakapofika, bado wataondolewa na kuangamizwa kwa sababu ya uovu wao na kwa sababu ya kutotii na kutokombolewa kwao. Hawatakuwa tena katika ulimwengu wa baadaye, na hawatakuweko tena miongoni mwa jamii ya binadamu ya baadaye. Watenda maovu wote na yeyote na wote ambao hawajaokolewa wataangamizwa wakati watakatifu miongoni mwa binadamu wataingia rahani, bila kujali kama wao ni roho za wafu ama wale wanaoishi bado katika mwili. Bila kujali enzi ya hizi roho zitendazo maovu na watu watenda maovu, ama roho za watu wenye haki na watu wanaofanya haki wako, mtenda maovu yeyote ataangamizwa, na yeyote mwenye haki ataishi. Iwapo mtu ama roho inapokea wokovu haiamuliwi kabisa kulingana na kazi ya enzi ya mwisho, lakini inaamuliwa kulingana na iwapo wamempinga ama kutomtii Mungu. Kama watu wa enzi ya awali walifanya maovu na hawangeweza kuokolewa, bila shaka wangekuwa walengwa wa adhabu. Kama watu wa enzi hii wanafanya maovu na hawawezi kuokolewa, hakika wao pia ni walengwa wa adhabu. Watu wanatengwa kwa msingi wa mema na mabaya, sio kwa msingi wa enzi. Baada ya kutengwa kwa msingi wa mema na mabaya, watu hawaadhibiwi ama kutuzwa mara moja; badala yake, Mungu atafanya tu kazi Yake ya kuwaadhibu waovu na kuwatuza wema baada ya Yeye kumaliza kutekeleza kazi Yake ya ushindi katika siku za mwisho. Kwa kweli, Amekuwa akitumia mema na mabaya kutenga binadamu tangu Afanye kazi Yake miongoni mwa binadamu. Atawatuza tu wenye haki na kuwaadhibu waovu baada ya kukamilika kwa kazi Yake, badala ya kuwatenga waovu na wenye haki baada ya kukamilika kwa kazi Yake mwishowe na kisha kufanya kazi Yake ya kuwaadhibu waovu na kuwatuza wazuri mara moja. Kazi Yake ya mwisho ya kuadhibu waovu na kuwatuza wazuri inafanywa kabisa ili kutakasa kabisa binadamu wote, ili Aweze kuleta binadamu watakatifu mno katika pumziko la milele. Hatua hii ya kazi Yake ni kazi Yake muhimu zaidi. Ni hatua ya mwisho ya kazi Yake yote ya usimamizi. Kama Mungu hangewaangamiza waovu lakini badala yake kuwaacha wabakie, basi binadamu wote bado hawangeweza kuingia rahani, na Mungu hangeweza kuleta binadamu katika ulimwengu bora. Kazi ya aina hii haingekuwa imekamilika kabisa. Atakapomaliza kazi Yake, binadamu wote watakuwa watakatifu kabisa. Mungu anaweza kuishi kwa amani rahani kwa namna hii pekee.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 94)
Nyayo Zangu zinatembea katika ulimwengu wote na katika miisho ya dunia, macho Yangu yanachunguza kila mtu daima, na hata zaidi Natazama picha yote ya ulimwengu. Maneno Yangu ya utendaji yanafika katika kila pembe ya ulimwengu. Yeyote anayethubutu kutotoa huduma yake Kwangu, yeyote anayethubutu kutokuwa mwaminifu Kwangu, yeyote anayethubutu kulihukumu jina Langu, na yeyote anayethubutu kuwatukana na kuwapaka tope wana Wangu—wale wote ambao kwa kweli wanafanya vitu hivi lazima wapitie hukumu kali. Hukumu Yangu inaanguka kikamilifu. Hivi ni kusema, sasa ni enzi ya hukumu, na kwa uchunguzi wa makini utapata kuwa hukumu Yangu inaendelea kote katika ulimwengu dunia. Bila shaka, familia Yangu haijaachwa; wale ambao fikira zao, maneno, na vitendo havipatani na mapenzi Yangu watahukumiwa. Lazima uelewe, hukumu Yangu inaelekezwa kwa ulimwengu dunia wote, sio tu kikundi kimoja cha watu ama vitu—je, umegundua hili? Ikiwa unapambana kimawazo kunihusu kwa dhati, basi utahukumiwa ndani yako mara moja.
Hukumu Yangu huja kwa maumbo na aina zote. Jua hili! Mimi ni Mungu wa kipekee na wa busara wa ulimwengu dunia! Hakuna kitu kinachozidi nguvu Yangu. Hukumu Zangu zote zimefichuliwa kwako: Ikiwa unapambana kimawazo kunihusu, Nitakutia nuru kama onyo. Kama hutasikia, basi Nitakuacha mara moja (hili halihusu kushuku jina Langu, lakini kwa tabia za nje—zile zinazohusu raha za kimwili). Kama mawazo yako ni ya kunikataa, unanilalamikia, unakubali tena na tena mawazo ya Shetani na hufuati hisia za maisha, basi roho yako itakuwa gizani na mwili wako utapitia uchungu. Lazima uwe karibu na Mimi. Hutaweza kabisa kurejesha hali yako ya kawaida kwa siku moja au mbili tu, na maisha yako yataonekana kubaki nyuma zaidi. Wale ambao hotuba yao haifai Nitaadhibu midomo yako na ndimi na kufanya ndimi zako kupitia ushughulikaji. Wale ambao bila kupinga ni wapotovu kwa matendo Nitakuonya kwa roho zenu, na Nitaadhibu vikali wale ambao hawasikii. Wale ambao wananihukumu na kunikana kwa wazi, yaani wale ambao wanaonyesha kutotii kwa neno ama kwa tendo, Nitawaondoa kabisa na kuwaacha, Nitawafanya kuangamia na kupoteza baraka za juu; hao ni wale ambao wanaondolewa baada ya kuchaguliwa. Wale ambao ni wajinga, yaani wale ambao maono yao sio wazi, bado Nitawapa nuru na kuwaokoa. Lakini wale ambao wanaelewa ukweli lakini hawauweki katika vitendo watapewa adhabu kulingana na sheria ambazo zimetajwa awali, iwe hawajui au la. Kwa wale watu ambao nia zao hazijakuwa sahihi tangu mwanzo, Nitawafanya wasiweze milele kuelewa uhalisi na mwishowe wataondolewa hatua kwa hatua, mmoja kwa mmoja—hakuna hata mmoja atakayebaki—lakini wanabaki sasa kwa mpango Wangu (kwani Sifanyi vitu kwa haraka, ila kwa mtindo wa utaratibu).
Hukumu Yangu imefichuliwa kabisa, imelengwa kwa watu tofauti, na wote lazima wachukue nafasi zao zinazostahili. Ikitegemea ni sheria gani iliyovunjwa, Nitawaadhibu na kuwahukumu kulingana na sheria hiyo. Na kwa wale ambao hawako katika jina hili na hawamkubali Kristo wa siku za Mwisho, kuna sheria moja tu: Nitachukua roho mara moja, roho na mwili wa yeyote anayenikataa na kuwatupa Kuzimu; wowote ambao hawanikatai Mimi, Nitangoja mkomae kabla ya kufanya hukumu ya pili. Maneno Yangu yanaeleza yote kwa uwazi kamili na hakuna kilichofichwa. Ninatarajia tu kuwa mtaweza kuyaweka akilini kila wakati!
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 67
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 95)
Siku za mwisho ni wakati ambao vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina zake kupitia kushinda. Kushinda ni kazi ya siku za mwisho; kwa maneno mengine, kuhukumu dhambi za kila mtu ni kazi ya siku za mwisho. La sivyo, watu wangeainishwa vipi? Kazi ya kuainisha inayofanywa miongoni mwenu ni mwanzo wa kazi ya aina hiyo ulimwenguni kote. Baada ya hii, wale wa kila nchi na watu wote watapitia kazi ya ushindi. Hii inamaanisha kuwa watu wote wataainishwa kimakundi na kufika mbele ya kiti cha hukumu kuhukumiwa. Hakuna mtu na hakuna kitu kitakachoepuka kupitia huku kuadibu na hukumu, na hakuna mtu au kitu kinaweza kukwepa uainishaji huu; kila mtu atawekwa katika jamii. Hii ni kwa sababu mwisho u karibu kwa vitu vyote na mbingu zote na dunia zimefikia hatima yake. Mwanadamu anawezaje kukwepa hatima ya maisha yake? Hivyo, mnaweza kuendelea na matendo yenu ya uasi kwa muda gani zaidi? Je, hamuoni kwamba siku zenu za mwisho ziko karibu sana? Ni vipi ambavyo wale wanaomcha Mungu na kutamani sana Aonekane watakosa kuona siku ya kuonekana kwa haki ya Mungu? Wanawezaje kukosa kupokea thawabu ya mwisho ya wema? Je, wewe ni yule atendaye mema, au yule atendaye maovu? Je, wewe ni yule akubaliye hukumu yenye haki na kisha kutii, au kisha hulaaniwa? Umekuwa ukiishi katika nuru mbele ya kiti cha hukumu, au katika giza jahanamu? Je, wewe mwenyewe si unayejua kwa dhahiri sana kama mwisho wako utakuwa wa thawabu au wa adhabu? Je, wewe si unayejua kwa dhahiri sana na kufahamu kwa kina sana kwamba Mungu ni mwenye haki? Kwa hiyo, kweli, mwenendo wako uko vipi na una moyo wako wa aina gani? Ninapoendelea kukushinda leo, unanihitaji Mimi kwa kweli kukueleza kinagaubaga kama mwenendo wako ni wa uovu au wa mema? Je, umeacha kiasi gani kwa ajili Yangu? Unaniabudu Mimi kwa kina gani? Wewe mwenyewe unajua kwa dhahiri sana ulivyo Kwangu—je, hiyo si kweli? Unapaswa kujua vizuri zaidi kuliko mtu yeyote jinsi utakavyokuwa hatimaye! Kweli Nakwambia, Niliwaumba tu wanadamu, na Nilikuumba wewe, lakini Sikuwakabidhi kwa Shetani; wala kuwafanya kwa makusudi muasi dhidi Yangu au kunipinga Mimi na kwa hivyo kuadhibiwa na Mimi. Hamjapata majanga haya kwa sababu mioyo yenu imekuwa migumu mno na mienendo yenu yenye kustahili dharau mno? Kwa hiyo si kweli kwamba mnaweza kuamua hatima yenu wenyewe? Je, si kweli kwamba mnajua ndani ya mioyo yenu, bora zaidi kuliko yeyote, vile mtaishia? Sababu ya Mimi kuwashinda watu ni kuwafichua, na pia kuhakikisha bora zaidi wokovu wako. Sio kukusababisha ufanye uovu au kwa makusudi kukusababisha uingie katika jahanamu ya uharibifu. Wakati utakapofika, mateso yako yote makuu, kulia kwako na kusaga meno—je, hayo yote hayatakuwa kwa ajili ya dhambi zako? Kwa hiyo, uzuri wako mwenyewe au uovu wako mwenyewe sio hukumu bora zaidi kukuhusu? Je, sio thibitisho bora zaidi ya kile ambacho mwisho wako utakuwa?
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 96)
Sauti ya mngurumo inatoka, ikiutetemesha ulimwengu mzima, ikiwahanikiza watu, na kuwafanya wachelewe kukwepa, na wengine wanauawa, baadhi wanaangamizwa, na wengine wanahukumiwa. Kweli ni kioja ambacho hakuna yeyote amewahi kukiona awali. Sikiliza kwa makini, milio ya radi inafuatana na sauti za kuomboleza, na sauti hii inatoka kuzimu, sauti hii inatoka jahanamu. Ni sauti yenye uchungu ya wale wana wa uasi ambao wamehukumiwa nami. Wale wasiosikiza kile Ninachosema na hawatendi maneno Yangu wanahukumiwa vikali na kupokea laana ya ghadhabu Yangu. Sauti Yangu ni hukumu na ghadhabu, nami si mpole kwa yeyote na simwonei mtu yeyote huruma, kwa kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki Mwenyewe, na Mimi ni mwenye ghadhabu, Nina kuchoma, utakaso, na maangamizo. Ndani Yangu, hakuna kitu kilichofichika, au chenye mhemuko, lakini badala yake, kila kitu kiko wazi, chenye haki, na kisicho na upendeleo. Kwa sababu wazaliwa Wangu wa kwanza tayari wako nami katika kiti cha enzi, wakitawala mataifa yote na watu wote, yale mambo na watu walio dhalimu na waovu wanaanza kuhukumiwa. Nitawafanyia uchunguzi mmoja baada ya mwingine, bila kukosa kitu chochote, Nikiwafichua kabisa. Kwa kuwa hukumu Yangu imefichuliwa kikamilifu na imefunguliwa kikamilifu, na hakuna chochote ambacho kimebakizwa; Nitatupa chochote kisichokubaliana na mapenzi Yangu na kukisababisha kiangamie kuzimu milele; Nitakisababisha kiungue kuzimu milele. Hii ni haki Yangu; huu ni uaminifu Wangu. Hakuna mtu anayeweza kubadilisha hili, na lazima kinitii.
Watu wengi hupuuza maneno Yangu na kufikiri maneno ni maneno tu na ukweli ni ukweli. Wao ni wajinga! Hawajui kwamba Mimi ni Mungu mwaminifu Mwenyewe? Maneno Yangu na ukweli hutokea sawia—si hii kwa hakika ni kweli? Watu hawaelewi maneno Yangu kabisa, na wale tu ambao wamepata nuru wanaweza kuelewa kweli—huu ni ukweli. Mara tu watu wanapoona maneno Yangu wanaogopa sana, wakijificha kila mahali, sembuse wakati hukumu Yangu inaposhuka. Nilipoumba vitu vyote, Ninapouharibu ulimwengu, na Ninapowakamilisha wazaliwa wa kwanza—mambo haya yote yanatimizwa kwa neno moja kutoka katika kinywa Changu. Hii ni kwa maana neno Langu lenyewe ni mamlaka; hilo nihukumu. Inaweza kusemwa kuwa mtu Niliye ni hukumu na uadhama; huu ni ukweli usiobadilika. Huu ni upande mmoja wa amri Zangu za utawala; njia moja Kwangu kuwahukumu watu. Machoni Pangu, watu wote, masuala yote, na vitu vyote—vitu vyote kabisa—viko mikononi Mwangu na viko chini ya hukumu Yangu, hakuna mtu na hakuna kitu chochote kinachothubutu kutenda bila mpango na kwa makusudi, na yote lazima yatimizwe kwa mujibu wa maneno Ninayonena. Kutoka katika mawazo ya binadamu kila mtu anaamini maneno ya mtu Niliye. Wakati Roho Wangu anatoa sauti, watu wanakuwa na wasiwasi. Hawajui kudura Yangu kabisa, nao wananisingizia. Ninakuambia! Yeyote anayeyatilia shaka maneno Yangu, yeyote anayeyadharau maneno Yangu, hawa ndio watakaoangamizwa, ni wana wa kudumu wa kuangamia kabisa. Kutokana na hili inaweza kuonekana kuwa kuna wachache sana ambao ni wazaliwa wa kwanza, kwa sababu hii ndiyo mbinu Yangu ya kufanya kazi. Kama Nilivyosema, Sijitahidi kufanya lolote, lakini badala yake Mimi hutumia maneno Yangu tu kutimiza kila kitu. Hii, basi, ndipo ambapo kudura Yangu huwa. Katika maneno Yangu hakuna mtu anayeweza kupata chanzo na madhumuni ya hotuba Yangu. Watu hawawezi kutimiza hili, na wanaweza tu kutenda kulingana na mwongozo Wangu, na wanaweza tu kufanya kila kitu kulingana na mapenzi Yangu kufuatana na haki Yangu, ili familia Yangu iwe na haki na amani, ikiishi milele, thabiti na imara milele.
Hukumu Yangu inamjia kila mtu, amri Zangu za utawala zinamgusa kila mtu, na maneno Yangu na nafsi Yangu vinafichuliwa kwa kila mtu. Huu ndio wakati wa kazi kuu ya Roho Wangu (wakati huu wale watakaobarikiwa na wale watakaopitia taabu wanabainishwa). Mara tu maneno Yangu yatakapotamkwa, Nimewabainisha wale watakaobarikiwa na wale watakaopitia taabu. Yote ni dhahiri nami Ninaweza kuyaona mara moja. (Yanasemwa kuhusu ubinadamu Wangu, kwa hiyo hayahitilafiani na majaaliwa na uteuzi Wangu.) Ninatembeatembea hapa na pale milimani na mito na vitu vyote, anga ya ulimwengu, Nikichunguza kila mahali na kutakasa kila mahali, ili yale maeneo yasiyo safi na zile nchi zilizochangamana zote zitakoma kuwepo nazo zitateketea kabisa kwa sababu ya maneno Yangu. Kwangu, kila kitu ni rahisi. Ikiwa wakati huu ungekuwa wakati ambao Niliamua kabla kuiangamiza dunia, Ningeimeza kwa neno moja, lakini sasa si wakati. Lazima kila kitu kiwe tayari kabla Yangu kufanya kazi hii, ili visiuvuruge mpango Wangu na kuingilia usimamizi Wangu. Ninajua jinsi ya kufanya hivyo kwa busara: Nina hekima Yangu nami Nina mpango Wangu wenyewe. Watu hawapaswi kufanya lolote—jihadhari usiuawe kwa mkono Wangu; tayari hii inagusa amri Zangu za utawala. Kutokana na hili mtu anaweza kuona ukali wa amri Zangu za utawala, na mtu anaweza kuona kanuni za amri Zangu za utawala, ikiwa ni pamoja na vipengele viwili: kwa upande mmoja Ninawaua wote wasiokubaliana na mapenzi Yangu na ambao wanazikosea amri Zangu za utawala; kwa upande mwingine, Nikiwa na ghadhabu Ninawalaani wote wanaozikosea amri Zangu za utawala. Vipengele hivi viwili ni muhimu navyo ni kanuni zenye mamlaka ya uamuzi za amri Zangu za utawala. Kila mtu hutendewa kulingana na kanuni hizi mbili, bila hisia, bila kujali jinsi watu walivyo waaminifu. Hii inatosha kuonyesha haki Yangu na inatosha kuonyesha uadhama Wangu na ghadhabu Yangu, ambayo itaviteketeza vitu vyote ya kidunia, vitu vyote vya kidunia, na vitu vyote ambavyo havikubaliani na mapenzi Yangu. Katika maneno Yangu kuna siri zilizofichwa, na katika maneno Yangu pia kuna siri zilizofichuliwa, hivyo katika dhana ya binadamu, katika akili ya binadamu, maneno Yangu hayaeleweki milele na moyo Wangu haueleweki milele. Kwa maneno mengine, lazima Niwaondolee wanadamu dhana na kufikiria kwao. Hiki ni kipengee muhimu zaidi cha mpango Wangu wa usimamizi. Lazima Nifanye hivi ili Niwapate wazaliwa Wangu wa kwanza na ili Niyakamilishe mambo ambayo Nataka kufanya.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 103
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 97)
Sayuni! Salamu! Sayuni! Ita kwa sauti! Nimerudi kwa ushindi, Nimerudi nikiwa mshindi! Watu wote! Harakisheni mpange foleni kwa utaratibu! Vitu vyote! Mtakuja kusimama kabisa, kwa sababu nafsi Yangu inaukabili ulimwengu mzima na nafsi Yangu inaonekana katika Mashariki ya dunia! Nani anayethubutu kutopiga magoti katika ibada? Nani anayethubutu kutoniita Mungu wa kweli? Nani anayethubutu kutoangalia juu kwa kumcha? Nani anayethubutu kutotoa sifa? Nani anayethubutu kutangaza kwa shangwe? Watu wangu wataisikia sauti Yangu, Wanangu watasalia ndani ya ufalme Wangu! Milima, mito, na vitu vyote vitashangilia bila kukoma, na kurukaruka bila kupumzika. Wakati huu, hakuna atakayethubutu kurudi nyuma, hakuna atakayethubutu kusimama katika upinzani. Hili ni tendo Langu la ajabu, na hata zaidi ni nguvu Yangu kuu! Nitafanya kila kitu kiniche Mimi katika moyo wake na hata zaidi Nitafanya kila kinisifu Mimi. Hili ni lengo la msingi la mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita, nami Nimeamua hili. Hakuna hata mtu mmoja, hakuna hata kitu kimoja wala jambo moja, linathubutu kusimama kunipinga Mimi, au linathubutu kusimama kushindana na Mimi. Watu wangu wote wataelekea mlimani Kwangu (hili linaonyesha dunia ambayo Nitaiumba baadaye) nao watatii mbele Zangu kwa sababu Ninao uadhama na hukumu, nami Nina mamlaka. (Hili linahusu wakati Niko katika mwili. Pia Ninayo mamlaka katika mwili lakini kwa sababu upungufu wa muda na nafasi hayawezi kuzidi kiwango katika mwili, kwa hiyo haiwezi kusemwa kwamba Nimepata utukufu kamili. Ingawa Nawapata wazaliwa wa kwanza katika mwili, bado haiwezi kusemwa kwamba Nimepata utukufu. Ni wakati tu Nitakaporudi Sayuni na kubadilisha sura Yangu ndipo inaweza kusemwa kwamba Nina mamlaka, yaani, Nimepata utukufu.) Hakuna kitu kitakuwa kigumu Kwangu. Kila kitu kitaharibiwa kwa maneno kutoka kinywani Mwangu, na ni kwa sababu ya maneno kutoka kinywani Mwangu ndipo yatatukia na kufanyika kamili, hiyo ni nguvu Yangu kuu na hayo ni mamlaka Yangu. Kwa sababu Nina nguvu tele na nimejawa na mamlaka, hakuna mtu anayeweza kuthubutu kunizuia Mimi. Tayari Nimepata ushindi juu ya kila kitu na Nimewashinda wana wote wa uasi. Nawaleta wazaliwa Wangu wa kwanza pamoja kurudi Sayuni. Si Mimi pekee Yangu Ninayerejea Sayuni. Kwa sababu hii wote watawaona wazaliwa Wangu wa kwanza na hivyo watakuza moyo wa uchaji kwa ajili Yangu. Hili ni lengo Langu katika kuwapata wazaliwa Wangu wa kwanza na umekuwa mpango Wangu tangu wakati Wangu wa kuiumba dunia.
Wakati kila kitu kiko sawa, hiyo ndiyo siku ambayo Nitarudi Sayuni, na siku hii itakumbukwa na watu wote. Nitakaporudi Sayuni, vitu vyote duniani vitakuwa kimya na vitu vyote duniani vitakuwa na amani. Wakati ambapo Nimerudi Sayuni, kila kitu kitarejelea sura yake ya awali. Wakati huo, Nitaianza kazi Yangu katika Sayuni, Nitawaadhibu waovu na kuwatuza wazuri, Nitaleta mamlakani haki Yangu nami Nitatekeleza hukumu yangu. Nitatumia maneno Yangu kukamilisha kila kitu na kumfanya kila mtu na kila kitu kipitie mkono Wangu unaoadibu. Nitawafanya watu wote wauone utukufu Wangu mzima, waione hekima Yangu nzima, wauone ukarimu Wangu mzima. Hakuna mtu yeyote atathubutu kusimama kutoa hukumu kwani yote imekamilika nami. Katika hili, kila mtu ataiona heshima Yangu yote na wote watapata uzoefu wa ushindi Wangu wote kwa kuwa kila kitu kimewekwa wazi nami. Kutokana na haya, mtu anaweza kuuona uwezo Wangu mkubwa vizuri, na kuyaona mamlaka Yangu. Hakuna mtu atathubutu kunikosea Mimi, hakuna mtu atathubutu kunizuia Mimi. Yote yamewekwa waziwazi nami, nani angethubutu kuficha kitu chochote? Nina uhakika wa kutomwonyesha huruma! Mafidhuli mno kama wao lazima waipokee adhabu Yangu kali na watu wabaya kabisa kama wao lazima waondolewe kutoka machoni Pangu. Nitawatawala kwa fimbo ya chuma nami Nitayatumia mamlaka Yangu kuwahukumu, bila huruma yoyote na bila kutowaudhi kabisa, kwa maana Mimi ni Mungu Mwenyewe Nisiye na hisia na ambaye ni mwadhimu na Siwezi kukosewa. Hii inapaswa kueleweka na wote na kuonekana na wote ili kuepuka “bila kusudi au sababu” kuangushwa nami, kuangamizwa nami, wakati utakapofika, kwa kuwa fimbo Yangu itawaangusha wote ambao wananikosea. Sitajali kama wanajua amri Zangu za utawala au la; hilo halitakuwa muhimu Kwangu kwa kuwa nafsi Yangu haiwezi kuvumilia kosa la mtu yeyote. Hii ndiyo sababu imesemwa kwamba Mimi ni simba; yeyote Ninayemgusa, Nitawaangusha. Hii ndiyo sababu inasemwa kuwa sasa kusema kwamba Mimi ni Mungu wa huruma na wema ni kunikufuru. Kwa asili Mimi si Mwanakondoo bali ni simba. Hakuna mtu anayethubutu kunikosea na yeyote anayenikosea Nitamwadhibu mara moja kwa kifo, bila hisia hata kidogo! Kutokana na hili, mtu anaweza kuiona tabia Yangu vizuri. Kwa hiyo, katika enzi ya mwisho kundi kubwa la watu likijitoa, hilo ni jambo ambalo ni gumu kwa wanadamu kuvumilia, lakini Nina raha na furaha na sioni hii kama kazi ngumu hata kidogo, hiyo ni tabia Yangu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 120
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 98)
Katika ufalme, vitu vingi visivyohesabika vya uumbaji vinaanza kufufuka na kupata nguvu ya maisha yao. Kwa sababu ya mabadiliko katika hali ya dunia, mipaka kati ya nchi moja na nyingine pia inaanza kusonga. Hapo awali, Nimetabiri: Wakati ardhi itagawanywa kutoka kwa ardhi, na ardhi kujiunga na ardhi, huu ndio utakuwa wakati ambao Nitayapasua mataifa kuwa vipande vidogo. Katika wakati huu, Nitafanya upya uumbaji wote na kuugawa tena ulimwengu mzima, hivyo kuweka ulimwengu katika mpangilio, Nikibadilisha hali yake ya awali kuwa mpya. Huu ndio mpango Wangu. Hizi ni kazi Zangu. Wakati mataifa na watu wa dunia watakaporudi mbele ya kiti Changu cha enzi, basi Nitachukua fadhila ya mbinguni na kuiweka kwa sababu ya ulimwengu wa binadamu, ili, kwa mujibu Wangu, itajazwa na fadhila isiyo ya kufananisha. Lakini ulimwengu wa kitambo ukiendelea kuwepo, Nitavurumisha hasira Yangu kwa mataifa yake, Nikieneza amri Zangu za utawala katika ulimwengu mzima, na kuleta kuadibu kwa yeyote anayezikiuka:
Ninapougeuza uso Wangu kwa ulimwengu kuzungumza, binadamu wote wanasikia sauti Yangu, na hapo kuona kazi yote ambayo Nimefanya katika ulimwengu. Wale wanaoenda kinyume na mapenzi Yangu, hivyo ni kusema, wanaonipinga kwa matendo ya mwanadamu, watapitia kuadibu Kwangu. Nitachukua nyota nyingi mbinguni na kuzitengeneza upya, na kwa mujibu Wangu jua na mwezi vitafanywa upya—anga hazitakuwa tena jinsi zilivyokuwa hapo awali; vitu visivyohesabika duniani vitafanywa kuwa vipya. Yote yatakuwa kamili kupitia maneno Yangu. Mataifa mengi katika ulimwengu yatagawanishwa upya na kubadilishwa kuwa taifa Langu, ili kwamba mataifa yote yaliyomo duniani yatatoweka milele na kuwa taifa linaloniabudu Mimi; mataifa yote ya dunia yataangamizwa, na hayatakuwepo tena. Kati ya binadamu walio ulimwenguni, wale wote walio wa Shetani wataangamizwa; wale wote wanaomwabudu Shetani watalazwa chini na moto Wangu unaochoma—yaani, isipokuwa wale walio ndani ya mkondo, waliobaki watabadilishwa kuwa jivu. Nitakapoadibu watu wengi, wale walio katika dunia ya kidini, kwa kiasi tofauti, watarudi kwa ufalme Wangu, wakiwa wameshindwa na kazi Yangu, kwani watakuwa wameona kufika kwa Aliye Mtakatifu akiwa amebebwa juu ya wingu jeupe. Wanadamu wote watafuata aina yao, na watapokea kuadibu kunakotofautiana kulingana na kile walichofanya. Wale ambao wamesimama kinyume na Mimi wataangamia; na kwa wale ambao matendo yao duniani hayakunihusisha, kwa sababu ya vile wamejiweka huru wenyewe, wataendelea kuwa duniani chini ya uongozi wa wana Wangu na watu Wangu. Nitajionyesha kwa mataifa mengi yasiyohesabika, Nikipaza sauti Yangu kote duniani Nikitangaza kukamilika kwa kazi Yangu kuu ili wanadamu wote waone kwa macho yao.
Sauti Yangu inapoimarika kwa uzito, pia Ninaichunguza hali ya ulimwengu. Kupitia kwa maneno Yangu, vitu visivyohesabika vya uumbaji vyote vinafanywa upya. Mbingu inabadilika, kama ifanyavyo dunia. Binadamu wanafunuliwa wakiwa katika hali yao halisi na, polepole, kila mtu anatengwa kulingana na aina yake, na kutafuta njia bila kujua wanajipata wakirejea katika ngome za familia zao. Hii itanifurahisha sana. Niko huru kutokana na vurugu, na bila kutambulika, kazi Yangu kuu inatimizwa, na vitu visivyohesabika vya uumbaji vinabadilishwa, bila kujua. Nilipoumba ulimwengu, Niliunda kila kitu kulingana na aina yake, Nikiweka vitu vyote vilivyo na maumbo pamoja na mifano zao. Wakati mpango wa usimamizi Wangu unapokaribia tamati, Nitarejesha hali ya awali ya uumbaji, Nitarejesha kila kitu kiwe katika hali ya awali, Nikibadilisha kila kitu kwa namna kubwa, ili kila kitu kirudi ndani ya mpango Wangu. Muda umewadia! Hatua ya mwisho katika mpango Wangu iko karibu kutimika. Ah, dunia ya kitambo yenye uchafu! Kwa hakika mtaanguka chini kwa maneno Yangu! Kwa hakika mtafanywa kuwa bure kwa mujibu wa mpango Wangu! Ah, vitu visivyo hesabika vya uumbaji! Wote mtapata maisha mapya katika maneno Yangu—utapata uhuru wako Bwana Mkuu! Ah, dunia mpya, safi isiyo na uchafu! Kwa kweli mtafufuka katika utukufu Wangu! Ah Mlima Zayuni! Usiwe kimya tena. Nimerudi kwa ushindi! Kutoka miongoni mwa uumbaji, Ninaichunguza dunia nzima. Duniani, wanadamu wameanza maisha mapya, wameshinda tumaini mpya. Ah, watu Wangu! Mtakosaje kurudi kwa maisha ndani ya mwanga Wangu? Mtakosaje kuruka kwa furaha chini ya uongozi Wangu? Ardhi zinapiga kelele kwa furaha, maji yanapiga kelele kali na vicheko vya furaha! Ah, Israeli iliyofufuka! Mtakosaje kuhisi fahari kwa mujibu wa majaaliwa Yangu? Ni nani amelia? Ni nani ameomboleza? Israeli ya kitambo haiko tena, na Israeli ya leo imeamka, imara na kama mnara, katika dunia, imesimama katika mioyo ya binadamu wote. Israeli ya leo kwa hakika itapata chanzo cha uwepo kupitia kwa watu Wangu! Ah, Misri yenye chuki! Hakika, bado hamsimami dhidi Yangu? Mnawezaje kuichukulia huruma Yangu kimzaha na kujaribu kuepuka kuadibu Kwangu? Mtakosaje kuwa katika kuadibu Kwangu? Wale wote ambao Nawapenda wataishi milele kwa hakika, na wale wote wanaosimama dhidi Yangu wataadhibiwa na Mimi milele kwa hakika. Kwani Mimi ni Mungu mwenye wivu, Sitawasamehe kwa urahisi wanadamu kwa kile watakachokuwa wametenda. Nitaiangalia dunia yote, na, Nikitokea Mashariki ya dunia na haki, adhama, ghadhabu, na kuadibu, Nitajionyesha binafsi kwa wanadamu wengi wa tabaka mbalimbali!
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 26