379 Kumsaliti Mungu ni Asili ya Binadamu
1 Kwa hiyo, asili ya mwanadamu hutoka kwenye nafsi, si kutoka kwa mwili. Nafsi ya kila mtu tu ndiyo inayojua jinsi alivyopitia majaribu, mateso na upotovu wa Shetani. Mwili wa mwanadamu hauyajui mambo haya. Kwa hiyo, bila kujua, wanadamu huwa waovu zaidi, wachafu zaidi, na wabaya zaidi, wakati umbali kati ya mwanadamu na Mimi unazidi kuwa mkubwa, na maisha yanakuwa yenye giza zaidi kwa wanadamu. Shetani huzishika nafsi za wanadamu kwa nguvu, kwa hiyo, bila shaka, mwili wa mwanadamu pia umemilikiwa na Shetani. Mwili kama huo na wanadamu kama hao wangewezaje kutompinga Mungu? Wangewezaje kulingana naye kiasili? Sababu iliyofanya Nimtupe Shetani chini angani ni kwa sababu alinisaliti. Je, basi wanadamu wanawezaje kutohusishwa? Hii ndiyo sababu usaliti ni asili ya kibinadamu.
2 Haijalishi umekuwa mfuasi wa Mungu kwa muda upi—asili yako bado ni kumsaliti Mungu. Yaani, ni asili ya mwanadamu kumsaliti Mungu, kwa sababu watu hawawezi kupevuka kabisa maishani mwao, na kunaweza tu kuwa na mabadiliko madogo katika tabia zao. Kupitia sura hizi mbili, Mungu anawakumbusha watu wote kwamba bila kujali jinsi maisha yako yalivyopevuka, jinsi uzoefu wako ulivyo wa kina, jinsi ujasiri wako ulivyo mkuu, bila kujali ulikozaliwa na unakoenda, asili yako ya kumsaliti Mungu inaweza kujifichua wakati wowote na mahali popote. Mungu anataka kumwambia kila mtu jambo hili: Ni asili ya kuzaliwa ya kila mtu kumsaliti Mungu. Bila shaka, nia ya Mungu ya kueleza sura hizi mbili si kupata sababu za kuwaondoa ama kuwashutumu wanadamu, ila ni kuwafanya watu wafahamu zaidi asili ya mwanadamu, ili waweze kuishi kwa uangalifu mbele za Mungu nyakati zote kupokea mwongozo Wake, jambo litakalowazuia kupoteza uwepo wa Mungu na kuingia kwenye njia mbaya.
Umetoholewa kutoka katika “Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili