942 Mungu ni Mwenye Huruma Kuu na Mwenye Ghadhabu Kubwa

Rehema na uvumilivu wa Mungu kwa kweli vipo, lakini utakatifu na uhaki wa Mungu Anapoachilia hasira Yake pia inaonyesha binadamu upande wa Mungu usiyovumilia kosa lolote.

1 Wakati binadamu anaweza kabisa kutii amri za Mungu na kutenda kulingana na mahitaji ya Mungu, Mungu anakuwa mwingi katika huruma Yake kwa binadamu; wakati binadamu amejawa na upotoshaji, chuki na uadui kwake Yeye, Mungu anakuwa mwenye ghadhabu nyingi. Na anakuwa na ghadhabu nyingi hadi kiwango kipi? Hasira yake itaendelea kuwepo mpaka pale ambapo Mungu hataona tena upinzani wa binadamu na matendo maovu, mpaka vyote hivi havipo tena mbele ya macho Yake. Hapo tu ndipo ghadhabu ya Mungu itakapotoweka.

2 Haijalishi mtu husika ni yupi, kama moyo wake umekuwa mbali na Mungu, na yeye amemgeukia Mungu, asirudi tena, basi haijalishi ni vipi, kwa mwonekano wote au kuhusiana na matamanio yake ya kibinafsi, atapenda kuabudu na kufuata na kutii Mungu katika mwili wake au katika kufikiria kwake pindi tu moyo wake utakapokuwa mbali na ule wa Mungu, hasira ya Mungu itaachiliwa bila kikomo. Itakuwa kwamba wakati Mungu anapoiachilia kabisa ghadhabu Yake, akiwa amempa binadamu fursa za kutosha, pindi inapoachiliwa hakutakuwepo na njia yoyote ya kuirudisha, na hatawahi tena kuwa mwenye huruma na mvumilivu kwa mtu kama huyo.

3 Huu ni upande mmoja wa tabia ya Mungu isiyovumilia kosa. Yeye ni mvumilivu na mwenye huruma kwa viumbe walio wenye wema na wazuri na wa kupendeza; kwa vitu viovu, na vyenye dhambi, na vilivyojaa maovu, Yeye anayo hasira kali, kiasi cha kwamba Hawachi kuendeleza hasira Yake. Hivi ndivyo vipengele viwili vikuu na vinavyojitokeza zaidi kuhusu tabia ya Mungu, na, zaidi, vimefichuliwa na Mungu kutoka mwanzo hadi mwisho: wingi wa huruma na ghadhabu nyingi.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 941 Tabia ya Haki ya Mungu ni ya Pekee

Inayofuata: 943 Tabia ya Mungu ni Yenye Huruma, Upendo, Haki na Uadhama

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp