220 Waumini Lazima Wafuate Nyayo za Mungu kwa Karibu

1 Kwa kuwa mwanadamu anamwamini Mungu, ni sharti afuate kwa ukaribu nyayo Zake, hatua kwa hatua; anapaswa “kumfuata Mwanakondoo popote Aendapo.” Hawa tu ndio watu wanaotafuta njia ya kweli, na wao tu ndio wanaoifahamu kazi ya Roho Mtakatifu. Watu wanaofuata tu kanuni na mafundisho ya dini kiutumwa ni wale ambao wameondolewa na kazi ya Roho Mtakatifu. Katika kila kipindi cha wakati, Mungu ataanza kazi mpya, na katika kila kipindi, patakuwepo na mwanzo mpya kwa mwanadamu. Laiti mwanadamu ashikilie tu ukweli kwamba “Yehova ni Mungu” na “Yesu ni Kristo,” ambao ni ukweli unaozingatiwa katika enzi moja tu, basi mwanadamu hatawahi kwenda sambamba na kazi ya Roho Mtakatifu, na daima hataweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Ni wale tu wanaofuata nyayo za Mwanakondoo hadi mwisho kabisa ndio wanaoweza kufaidi baraka za mwisho.

2 Wale wasiofuata hadi mwisho kabisa, ambao hawazingatii kazi ya Roho Mtakatifu, na ambao wanashikilia kazi ya zamani hawajakosa tu kupata uaminifu kwa Mungu, bali kwa kinyume, wamekuwa wale wanaompinga Mungu, wamekuwa wale ambao wamekanwa na enzi mpya, na watakaoadhibiwa. Kuna wa kuhurumiwa zaidi kuliko wao? Watu wale wanaoshikilia kiutumwa sheria huwa wanadhihirisha uaminifu wa hali ya juu kwa sheria, na kadri wanavyodhihirisha uaminifu jinsi hiyo kwa sheria, ndivyo wanavyokuwa waasi wanaompinga Mungu. Kwa kuwa sasa ni Enzi ya Ufalme na wala si Enzi ya Sheria, na kazi ya leo na kazi ya zamani haziwezi kulinganishwa, wala kazi ya zamani haiwezi kulinganishwa na kazi ya sasa. Kazi ya Mungu imebadilika, na vitendo vya mwanadamu pia vimebadilika; si kushikilia sheria au kuubeba msalaba. Basi, uaminifu wa watu kwa sheria na msalaba hautapata kibali cha Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 219 Amkeni Karibuni, Ninyi Mlio Werevu

Inayofuata: 221 Unaifuata Kazi ya Sasa ya Mungu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp