484 Imani ya Kweli Katika Mungu ni Kutenda na Kupitia Maneno Yake

1 Katika uzoefu wa vitendo wa maneno ya Mungu tu ndipo mwanadamu anaweza kupewa ukweli na uzima; humu pekee ndimo anaweza kuja kupata kuelewa ubinadamu wa kawaida ni nini, maisha yenye umuhimu ni nini, kiumbe halisi ni nini, utiifu wa kweli kwa Mungu ni nini; humu pekee ndimo anaweza kuja kuelewa anavyofaa kumjali Mungu, jinsi ya kutimiza wajibu ya kiumbe aliyeumbwa, na jinsi ya kumiliki mfano wa mwanadamu wa kweli; humu tu ndimo anaweza kupata kuelewa maana ya imani halisi na ibada halisi; humu tu ndimo anaweza kuelewa nani ndiye Mtawala wa mbingu na nchi na vitu vyote; humu tu ndimo mwanadamu anaweza kuja kuelewa njia ambayo Yule ambaye ni Bwana wa uumbaji wote Anatawala, anaongoza, na kuutosheleza uumbaji; na hapa pekee ndipo anaweza kuja kuelewa na kushika njia ambayo Yule aliye Bwana wa uumbaji wote Anakuwa, Anadhihirishwa na kufanya kazi.

2 Akitenganishwa na uzoefu wa kweli wa maneno ya Mungu, mwanadamu hana maarifa ya kweli ama ufahamu katika maneno ya Mungu na ukweli. Mwanadamu wa aina hii ni maiti inayoishi tu, ganda lililoisha, na ufahamu wote unaohusiana na Muumba hauna chochote kingine kumhusu. Katika macho ya Mungu, mwanadamu kama huyo hajawahi kumwamini, ama kuwahi kumfuata, na hivyo Mungu hamtambui yeye kama mwumini Wake wala mfuasi Wake, ama hata kama kiumbe halisi aliyeumbwa.

Umetoholewa kutoka katika “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 483 Fuata Njia Ya Mungu katika Vitu Vyote Vikubwa na Vidogo

Inayofuata: 485 Kupitia Maneno ya Mungu Hakutenganishwi na Maneno Yake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp