78 Kutazama Sura ya Mwana wa Adamu Katika Hukumu na Kuadibu Kwake
1 Katika mibubujiko ya kuadibu na hukumu, Mwana wa Adamu Anaonyesha tabia Yake ya asili kupitia kuzungumza kwa maneno, Akiwaruhusu wale wote wanaokubali kuadibu Kwake na hukumu kuuona uso wa kweli wa Mwana wa Adamu, uso ulio mfano wa kuaminika wa Mwana wa Adamu Alivyooneka na Yohana. (Bila shaka, yote haya hayatawaonekania wote wasioikubali kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme.) Uso wa kweli wa Mungu hauwezi kuelezwa kikamilifu na maneno ya mwanadamu, na hivyo Mungu Hutumia maonyesho ya tabia Yake asili kuuonyesha uso Wake wa kweli kwa mwanadamu. Ambayo ni kusema wote ambao wamepitia tabia asili ya Mwana wa Adamu wameuona uso wa kweli wa Mwana wa Adamu, kwa kuwa Mungu ni mkuu zaidi na Hawezi kuelezwa kikamilifu na maneno ya mwanadamu.
2 Mara tu mwanadamu amepitia kila hatua ya kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme, basi atapata kujua maana kamili ya maneno ya Yohana alipozungumza kuhusu Mwana wa Adamu kati ya vinara vya taa: “Kichwa chake na nywele zilikuwa nyeupe mithili ya sufu, nyeupe mithili ya theluji; na macho yake yalikuwa mithili ya ulimi wa moto; Na miguu yake mithili ya shaba safi, kama kwamba ilikuwa imechomwa ndani ya tanuru; na sauti yake ilikuwa mithili ya sauti ya maji mengi. Na katika mkono wake wa kulia kulikuwa na nyota saba: na alitoa kinywani mwake upanga mkali wenye sehemu mbili za makali: nao uso wake ulikuwa mithili ya jua liangazavyo kupitia nguvu zake yeye.” Wakati huo, utajua bila shaka yoyote kwamba mwili huu wa kawaida uliozungumza maneno mengi ni kwa hakika Mungu mwenye mwili mara ya pili. Na utahisi ni jinsi gani kwa kweli umebarikiwa, na kujiona mwenyewe kama mwenye bahati kubwa. Je, ungekuwa huna radhi kuikubali baraka hii?
Umetoholewa kutoka katika Dibaji ya Neno Laonekana katika Mwili