248 Msingi wa Mungu wa Kuwashutumu Watu

1 Kwa wakati ambao Mungu bado hakuwa amegeuka mwili, kipimo cha iwapo mwanadamu alimpinga Mungu kilitegemea iwapo mwanadamu alimwabudu na kumheshimu Mungu aliye mbinguni asiyeonekana. Ufafanuzi wa upinzani kwa Mungu wakati huo haukuwa halisi, kwani mwanadamu wakati huo hangemwona Mungu wala kujua mfano wa Mungu ama jinsi Alivyofanya kazi na kuongea. Mwanadamu hakuwa na dhana za Mungu na alimwamini Mungu kwa njia isiyo dhahiri, kwani Hakuwa amejitokeza kwa mwanadamu. Kwa hivyo, vile mwanadamu alivyomwamini Mungu katika mawazo yake, Mungu hakumlaumu mwanadamu ama kuulizia mengi kutoka kwa mwanadamu, kwani mwanadamu hangemwona Mungu hata kidogo.

2 Mungu anapopata mwili na kuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu, wote wanamtazama Mungu na kusikia maneno Yake, na wote wanaona vitendo ambavyo Mungu anafanya kutoka ndani ya mwili Wake wa nyama. Katika wakati huo, fikira zote za mwanadamu zinakuwa povu tu. Kwa wale wanaomwona Mungu anayejitokeza katika mwili, wote walio na utiifu ndani ya mioyo yao hawalaaniwi, ilhali wanaosimama dhidi Yake kimakusudi watachukuliwa kuwa wapinzani wa Mungu. Wanadamu kama hao ni maadui wa Kristo na ni maadui wanaosimama dhidi ya Mungu kimakusudi. Wale walio na dhana kumhusu Mungu lakini bado wanatii kwa furaha hawatalaaniwa. Mungu anamlaani mwanadamu kulingana na nia yake na vitendo vyake, kamwe sio kwa mawazo na fikira zake. Iwapo mwanadamu angelaaniwa kwa misingi hiyo, basi hakuna mmoja ambaye angeweza kutoroka kutoka katika mikono ya Mungu ya ghadhabu.

3 Wale wanaosimama makusudi dhidi ya Mungu mwenye mwili wataadhibiwa kwa sababu ya kutotii kwao. Upinzani wao wa makusudi unatokana na dhana zao kumhusu, ambao unasababisha usumbufu wao kwa kazi ya Mungu. Wanadamu kama hao wanapinga na kuiharibu kazi ya Mungu wakijua. Hawana tu dhana za Mungu, lakini wanafanya kile kinachosumbua kazi Yake, na ni kwa sababu hii ndiyo wanadamu kama hao watahukumiwa. Wale wasioshiriki katika usumbufu wa kazi ya Mungu kimakusudi huwatahukumiwa kama wenye dhambi, kwani wanaweza kutii kwa bila kulazimishwa na kutosababisha vurugu na usumbufu. Wanadamu kama hao hawatahukumiwa.

Umetoholewa kutoka katika “Watu Wote Wasiomjua Mungu Ni Watu Wanaompinga Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 247 Itafute Njia ya Upatanifu na Kristo

Inayofuata: 249 Hadithi ya Tomaso ni Onyo kwa Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp