201 Kuzinduka kwa Barakala

1

Nilikuwa barakala, nikifuatilia falsafa za maisha za Shetani,

nikithamini amani na uvumilivu kuliko vyote na kamwe kutobishana na mtu yeyote.

Nilipofanya mambo au kuingiliana na wengine, nililinda majivuno, kiburi na hadhi yangu.

Nilijifanya kutojua ukweli, na singesema kile nilichoona waziwazi sana.

Kama kitu hakikunihusu, basi niliacha kanuni zangu na kutokitilia maanani.

Nilijilinda, nikasaliti dhamiri yangu mwenyewe ili nisimkasirishe mtu yeyote.

Nilikubali shida bila kulalamika, niliishi maisha ya aibu na nikapoteza ubinadamu wangu.

Bila unyoofu au heshima, sikustahili kuwa mwanadamu.

2

Nilipopitia hukumu ya maneno ya Mungu, nilizinduka mara moja.

Nilipoelewa ukweli, niliona waziwazi ukweli wa uovu na upotovu wa wanadamu.

Nilianguka mbele za Mungu na nikahisi majuto makuu moyoni mwangu.

Nilichukia ubinafsi na ubahili wangu mwenyewe, na nikajichukia kwa kupoteza uaminifu na heshima yangu.

Huyu barakala alikuwa amefichuliwa mwishowe: Niliwaumiza wengine, nikajidhuru na Mungu alinichukia.

Mjanja, mdanganyifu, mnafiki, siwezi kuitoroka hukumu ya Mungu.

Maneno ya Mungu ni ukweli, kanuni za juu zaidi maishani.

Watu waaminifu humtii Mungu, wao hutenda kwa unyoofu na kwa moyo mkunjufu.

Wao hutenda ukweli na kupokea kibali cha Mungu, wakiishi katika nuru.

Ninaamua kuwa mtu mwaminifu, kuishi kwa kufuata maneno ya Mungu,

kuacha upotovu na udanganyifu wangu, na kumcha Mungu na kuepukana na maovu.

Nitatenda wajibu wangu kwa uaminifu na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu ili nimtukuze Mungu.

Iliyotangulia: 199 Ninapoamka Katika Ukungu

Inayofuata: 202 Toba ya Dhati

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

263 Njia Yote Pamoja na Wewe

1 Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani. Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga....

132 Mradi tu Usimwache Mungu

Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za...

273 Upendo Safi Bila Dosari

1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki