253 Ninaomba tu Kwamba Mungu Aridhike

Ubeti wa 1

Nimemwamini Mungu kwa muda mrefu sana

lakini sijafuatilia ukweli.

Inaujaza moyo wangu majuto.

Nimekosa nafasi ya kukamilishwa

mara nyingi zaidi, na bado, jambo baya zaidi,

nimeuumiza moyo wa Mungu katika njia hii.

Mungu alionyesha upole na huruma mara kwa mara.

Alinipa nafasi za kutubu.

Hukumu, kuadibu na nidhamu-

vilifanya moyo wangu wa ganzi ujisikie.

Kiitikio cha awali 1

Kwa kuelewa ukweli,

napitia upendo wa Mungu na kuishi mbele Yake.

Wema Wake ni mkuu,

lakini sijamrudishia Mungu chochote.

Nina aibu sana kuonana na Yeye

wakati ambapo sijampa upendo.

Kiitikio 1

Kufuatilia ukweli na kuzaliwa upya,

kulipa upendo wa Mungu,

hili ni tamanio langu moja la kweli, hili ni tamanio langu moja la kweli.

Ubeti wa 2

Naweka ushawishi wa Mungu moyoni mwangu kwa uthabiti,

ili kutimiza agizo ambalo Amenipa.

Natenda ukweli, natimiza wajibu wangu

kila siku ili kuuridhisha moyo wa Mungu.

Kwa mpango Wake mtakatifu na enzi kuu,

ninakabiliwa na majaribu yaliyokusudiwa kwangu.

Ninawezaje kufa moyo au kujaribu kuficha?

Kitu cha kwanza ni utukufu wa Mungu.

Hukumu, adhabu na nidhamu—

vilifanya moyo Wangu uliokufa ganzi uhisi.

Kiitikio cha Awali 2

Wakati wa shida,

maneno ya Mungu yananiongoza na imani yangu inakamilishwa.

Nimejitoa kabisa na kikamilifu,

kujitoa kwa Mungu bila hofu ya kifo.

Mapenzi Yake daima yako juu ya yote.

Kishikizi

Naahidi kabisa kulipa upendo wa Mungu.

Namsifu bila pingamizi moyoni mwangu.

Nimeona Jua la haki,

ukweli unadhibiti vitu vyote vilivyo duniani.

Tabia ya Mungu ni ya haki

(na inastahili sifa za wanadamu).

Moyo wangu utampenda Mwenyezi Mungu milele,

na nitaliinua jina Lake juu.

Kiitikio 2

Bila kujali mustakabali wangu, bila kufikiria faida au hasara,

Natamani tu Mungu aridhike.

Nashuhudia ushuhuda mkubwa sana

na kumwaibisha Shetani kwa ajili ya utukufu wa Mungu.

Iliyotangulia: 252 Nampa Mungu Moyo Wangu Mwaminifu

Inayofuata: 254 Toba

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp