216 Kugutuka Kupitia Hukumu

1 Katika miaka hiyo yote ya kumwamini Bwana, nililenga tu kufafanua nadharia za Biblia. Kamwe sikutii maneno na amri za Bwana. Nilijitahidi, lakini ilikuwa tu kwa ajili ya hadhi na thawabu. Niliishi katika dhambi, lakini bado nilikuwa natarajia unyakuo wangu kuingia kwenye ufalme wa mbinguni baada ya kufika kwa Bwana. Baada ya kupitia hukumu ya maneno ya Mungu, niligutushwa kutoka ndotoni mwangu. Naona kuwa mimi ni mbaya, mwenye kustahili dharau, na ni mpotovu sana. Naongea mafundisho mazuri na kujivuna kila mahali. Najipamba katika mafundisho kuwadanganya wengine na kujidanganya. Siishi kwa kudhihirisha ukweli wa maneno ya Mungu, sina sura ya binadamu. Natembea kwenye njia ya Mafarisayo, lakini bado najiona kuwa mwaminifu. Ni bahati iliyoje kwamba hukumu ya maneno ya Mungu imenigutusha! Bila kukubali hukumu ya Kristo katika siku za mwisho, singestahili kabisa kumwona Mungu.

2 Hukumu ya Mungu inaniruhusu kuona wazi ukweli wa upotovui wa wanadamu. Nimejaa dhana na mawazo juu ya Mungu, nimo hatarini mwa kumsaliti wakati wowote. Bila majaribio ya kuifichua, hakuna mtu ambaye angeiona asili yake wazi. Binadamu wamepotoshwa kwa kina, na hawatatakaswa bila kupitia hukumu. Tabia ya haki ya Mungu inafichuliwa kabisa ndani ya hukumu Yake. Mungu anaamua mwisho wa mwanadamu kulingana na ikiwa ana ukweli au la. Haijalishi anateseka vipi, ikiwa hajapata ukweli, basi haina maana yoyote. Ni kwa kupitia hukumu na kupata ukweli tu ndiyo mwanadamu anaweza kuishi maisha ya binadamu. Ni muhimu sana kwa Mungu kutumia hukumu na kuadibu kumwokoa mwanadamu. Ni heshima iliyoje kujua haki na utakatifu wa Mungu! Ni hukumu ya Mungu ambayo inaniokoa na kuugutusha moyo wangu. Naazimia kufuatilia ukweli na kuishi kwa kudhihirisha uhalisi ili nimshuhudie na kumtukuza Mungu.

Iliyotangulia: 211 Kupata Ukweli Kupitia Imani kwa Mungu Kuna Thamani Sana

Inayofuata: 217 Hukumu Iliuzindua Moyo Wangu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

263 Njia Yote Pamoja na Wewe

1 Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani. Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga....

132 Mradi tu Usimwache Mungu

Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki