135 Kazi ya Mungu ni Mpya Daima na si Nzee Kamwe

1 Wakati huo, Yesu alisema kuwa kazi ya Yehova ilikuwa imebaki nyuma kwa Enzi ya Neema, kama Nisemavyo leo kwamba kazi ya Yesu imebaki nyuma. Kama kungekuwa tu na Enzi ya Sheria na siyo Enzi ya Neema, Yesu hangeweza kusulubiwa na hangeweza kuwakomboa wanadamu wote; kungekuwa tu na Enzi ya Sheria, kungekuwa na uwezekano wa mwanadamu kuendelea hadi siku ya leo? Historia inaendelea mbele; historia sio asili ya sheria ya kazi ya Mungu? Hii sio picha ya usimamizi Wake wa mwanadamu ndani ya ulimwengu mzima? Historia inaendelea mbele, na pia kazi ya Mungu, na matakwa ya Mungu yanaendelea kubadilika. Haingewezekana kwa Mungu kudumisha hatua moja ya kazi kwa miaka elfu sita, kwani kila mwanadamu anajua kwamba Yeye daima ni mpya na kamwe si mzee. Hangeweza kuendelea kuendeleza kazi sawa na kusulubiwa, na mara moja, mara mbili, mara tatu…. kupigwa misumari kwa msalaba. Huu ni mtazamo wa mwanadamu mjinga.

2 Mungu haendelezi kazi sawa, na kazi Yake daima inabadilika na daima ni mpya, jinsi kila siku Nazungumza nanyi maneno mapya na kufanya kazi mpya. Hii ndiyo kazi Ninayofanya, umuhimu wake ukiwa kwa maneno “mpya” na “ajabu.” “Mungu habadiliki, na Mungu daima Atakuwa Mungu”; usemi huu hakika ni ukweli. Kiini cha Mungu hakibadiliki, Mungu daima ni Mungu, na Hawezi kamwe kuwa Shetani, lakini haya hayathibitishi kwamba kazi Yake ni ya daima na kabambe kama kiini Chake. Unatangaza kwamba Mungu yuko hivyo, lakini ni jinsi gani basi unaweza kueleza kwamba Mungu daima ni mpya na kamwe si mzee? Kazi ya Mungu inaendelea kuenea, na mapenzi ya Mungu yanaendelea kujitokeza na kufanywa kujulikana na mwanadamu.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 134 Asili ya Mungu Haibadiliki

Inayofuata: 136 Kazi ya Mungu Haisimami

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp