215 Siku ya Utukufu wa Mungu

1 Siku moja, ambapo ulimwengu mzima utarudi kwa Mungu, kitovu cha kazi Yake katika ulimwengu wote kitafuata matamko ya Mungu; kwingineko watu watapiga simu, wengine watapanda ndege, wengine watapanda boti na kupita baharini, na wengine watatumia leza kupokea matamshi ya Mungu. Kila mmoja atakuwa anatamani na mwenye shauku, wote watakuja karibu na Mungu, na kukusanyika kwa Mungu, na wote watamwabudu Mungu—na yote haya yatakuwa matendo ya Mungu. Kumbuka hili! Mungu hawezi kuanza tena kwingineko. Mungu atatimiza ukweli huu: Atawafanya watu wote ulimwengu mzima kuja mbele Yake, na kumwabudu Mungu duniani, na kazi Yake katika maeneo mengine itakoma, na watu watalazimishwa kutafuta njia ya kweli.

2 Jumuiya yote ya kidini itapitia njaa kubwa, na ni Mungu tu wa leo ndiye chemchemi ya maji ya uzima, akiwa na kisima chenye maji yasiyokauka kilichotolewa kwa ajili ya furaha ya mwanadamu, na watu watakuja na kumtegemea. Siku ambapo ufalme wote utafurahia ni siku ya utukufu wa Mungu, na mtu yeyote atakayewajia, na kupokea habari njema za Mungu atabarikiwa na Mungu, na nchi hizi na watu hawa watabarikiwa na kulindwa na Mungu. Mwelekeo wa maisha yajayo utakuwa hivi: Wale ambao watapata matamshi kutoka katika kinywa cha Mungu watakuwa na njia ya kutembea duniani, na wawe wafanya biashara au wanasayansi, au waelimishaji au wataalamu wa viwandani, wale ambao hawana maneno ya Mungu watakuwa na wakati mgumu wa kuchukua hata hatua moja, na watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Hiki ndicho kinamaanishwa na, “Ukiwa na ukweli utatembea ulimwengu mzima; bila ukweli, hutafika popote.”

3 Maneno ya Mungu yataenea katika nyumba zisizohesabika, yatafahamika kwa wote, na wakati huo tu ndipo kazi yake itaenea ulimwenguni kote. Ambapo ni sawa na kusema, ikiwa kazi ya Mungu itaenea ulimwenguni kote, basi maneno Yake ni lazima yaenee. Katika siku ya utukufu wa Mungu, maneno ya Mungu yataonesha nguvu yake na mamlaka. Kila neno Lake kuanzia wakati huo hadi leo litatimizwa na kuwa la kweli. Kwa njia hii, utukufu utakuwa wa Mungu duniani—ambavyo ni sawa na kusema, kazi yake itatawala duniani. Wote ambao ni waovu wataadibiwa na maneno katika kinywa cha Mungu, wale wote ambao ni wa haki watabarikiwa na maneno katika kinywa Chake, na wote watathibitishwa na kukamilishwa na maneno katika kinywa Chake. Yote yatakamilishwa na maneno Yake.

Umetoholewa kutoka katika “Ufalme wa Milenia Umewasili” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 214 Mungu ni Mungu, Mwanadamu ni Mwanadamu

Inayofuata: 216 Wamebarikiwa Wale Wanaokubali Kazi Mpya ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp