86 Mungu Anafanikisha Vyote Katika Siku za Mwisho Hasa Kwa Maneno

1 Katika siku za mwisho, Mungu anapokuwa mwili, kimsingi Anatumia neno kukamilisha yote na kufanya yote yawe wazi. Katika maneno Yake pekee ndipo unaweza kuona kile Alicho; ni katika maneno Yake pekee ndiyo unaweza kuona kwamba yeye ni Mungu Mwenyewe. Mungu katika mwili Anapokuja duniani, hafanyi kazi nyingine ila kuongea maneno—hivyo basi hakuna haja ya kutumia uhakika; maneno yanatosha.

2 Mungu amekuja duniani wakati wa siku za mwisho ili kutekeleza huduma ya neno ili mwanadamu amtambue, na ili mwanadamu aone kile Alicho, na aone hekima Yake na matendo Yake yote ya maajabu kutoka kwa neno Lake. Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno kimsingi kushinda watu wote. Baadaye neno Lake litakuja katika kila dini, kikundi, taifa na madhehebu; Mungu hutumia neno kushinda, kuwafanya wanadamu wote waone kuwa neno Lake lina mamlaka na nguvu—na kwa hivyo leo, mnakumbana tu neno la Mungu.

3 Katika siku ya utukufu wa Mungu, maneno ya Mungu yataonesha nguvu yake na mamlaka. Kila neno Lake kuanzia wakati huo hadi leo litatimizwa na kuwa la kweli. Kwa njia hii, utukufu utakuwa wa Mungu duniani—ambavyo ni sawa na kusema, kazi yake itatawala duniani. Wote ambao ni waovu wataadibiwa na maneno katika kinywa cha Mungu, wale wote ambao ni wa haki watabarikiwa na maneno katika kinywa Chake, na wote watathibitishwa na kukamilishwa na maneno katika kinywa Chake. Wala hataonyesha ishara zozote na maajabu; yote yatakamilishwa na maneno Yake, na maneno Yake yatazalisha ukweli.

Umetoholewa kutoka katika “Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 85 Hukumu kwa Neno Inawakilisha Mamlaka ya Mungu Bora Zaidi

Inayofuata: 87 Mungu Mwenye Mwili wa Siku za Mwisho Humkamilisha Mungu kwa Maneno

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp