59 Kukubali Ukweli ni Kuwa Mwanamwali Mwenye Busara
1
Nikiamini kwa miaka hii yote, nilishikilia jina la Bwana, nikitarajia kunyakuliwa.
Nilidhani kwamba nikimwamini Bwana na kusamehewa dhambi zangu, ningepewa taji.
Nilwaza kuhusu kuokoka kwa neema, nikitamani kwamba kwa hatua moja ningepanda angani na kuingia katika ufalme wa mbinguni.
Hakuna anayeelewa hakika umuhimu wa kweli wa unabii wa Bwana Yesu.
Watu hubuni ndoto zao wenyewe kulingana na maneno ya Paulo.
Wanatumaini bure kwamba Bwana atafika ghafla juu ya wingu.
Macho yao yanaona janga kubwa, lakini bado hawaoni kuonekana kwa Bwana.
Hawajui kuwa maneno ya Bwana Yesu yalitimizwa zamani sana.
Wanawali wapumbavu wanashikilia kwa ukaidi dhana zao, hawasikii sauti ya Mungu.
Na hivyo wanaikosa nafasi ya kunyakuliwa, na watahisi majuto makubwa.
2
Kristo wa siku za mwisho anaonyesha ukweli kumhukumu na kumtakasa mwanadamu.
Wanawali wenye busara husikia sauti ya Mungu, na kukaribisha kuonekana kwa Bwana.
Wanakula na kunywa maneno ya Mungu, na kuhudhuria sherehe ya harusi ya Mwanakondoo.
Baada ya kupitia hukumu, wanaona kwamba tabia ya Mungu ni takatifu na yenye haki.
Watu wamepotoshwa sana, wamejaa uasi, hawastahili kuingia katika ufalme wa mbinguni.
Ni wakati tu wanapokubali hukumu na kuadibu kwa Mungu ndipo wanaweza kutakaswa.
Mafarisayo wamelaaniwa na Bwana kwa unafiki wao.
Ni wale tu ambao ni waaminifu na hutenda ukweli ndio watapata baraka na sifa za Mungu.
Ni wale tu wanaomfuata Kristo na kutekeleza wajibu wao ndio watu wanaomtii Mungu.
Ni wale tu wanaompenda na kushuhudia kuhusu Mungu ndio wanaweza kukamilishwa.