307 Kuachana kwa Hisia

1

Tunapokumbuka nyakati zetu na Mungu:

Kulikuwa na shangwe za vicheko na machozi ya uchungu.

Siku zetu pamoja na Mungu zilikuwa za furaha kweli.

Zilitupa kumbukumbu ambazo hatutasahau kamwe.

Ee Mungu! Katika miaka mingi ya mikusanyiko,

ukweli Wako umetakasa upotovu wetu.

Sasa kwa kuwa tunaelewa ukweli, tumebadilika na kuwa watu wapya.

Upendo Wako, safi sana, umekita mizizi ndani ya mioyo yetu.

Maneno Yako yamekuwa imani yetu, upendo wetu.

Hisia zetu Kwako ni za kina sana, hatuwezi kuvumilia kuwa mbali na Wewe.

Lakini leo Utatuacha hivi karibuni.

Tungekosaje kusita?

2

Uliishi na sisi usiku na mchana.

Kila siku Ulionyesha ukweli kutunyunyizia.

Tulifichua upotovu mwingi sana, na tukakuletea uchungu.

Mvumilivu na mastahimilivu, Uliendelea kutuongoza.

Ee Mungu! Ulipitia uchungu mwingi kutuokoa.

Uliona jinsi vimo vyetu vilivyokuwa vichanga, na Ulikua na wasiwasi na mwenye wahaka.

Ulishiriki kwa uvumilivu juu ya ukweli, Ukitusaidia na kutukimu.

Ulikuwa nasi wakati wa majaribu na shida.

Ulitutia moyo tuelewe ukweli na kuwa na ushuhuda Kwako.

Hukumu na utakaso wetu vilikuwa neema Yako kabisa.

Baada ya kufurahia upendo Wako mwingi, tutakosaje kukupenda?

Upendo Wako hutuhimiza mbele; hatutajuta kukupenda kamwe.

3

Kazi Yako imekamilika, hivi karibuni Utarudi Sayuni.

Hatuwezi kuvumilia kukuona Ukienda.

Tulikumbuka miaka hiyo, Wewe ukituongoza hatua kwa hatua.

Picha za zamani zilionekana mbele ya macho yetu.

Ulituhukumu, na kutakasa tabia zetu potovu.

Ulituokoa, na kutuondoa kutoka katika mateso ya joka kubwa jekundu.

Maneno Yako yalituongoza, na kuturuhusu kusimama imara katika ushuhuda wetu.

Baada ya kuvumilia dhiki na majaribu, maisha yetu yalikua.

Upendo Wako ni mkubwa sana, kupendeza Kwako kwingi sana.

Wewe Unastahili sifa na ibada ya mwanadamu.

Neema ya wokovu Wako imechorwa moyoni mwangu.

Naweka azimio langu kutekeleza wajibu wangu na kutoa ushuhuda mzuri na mkuu.

Upendo Wako utadumu milele moyoni mwangu, nitakupenda na kukuthamini daima.

Iliyotangulia: 306 Niliumbwa na Wewe, Mimi ni Wako

Inayofuata: 308 Lazima Tukutane Tena Siku Moja

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

132 Mradi tu Usimwache Mungu

Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za...

273 Upendo Safi Bila Dosari

1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki