413 Imani Ambayo Mungu Hasifu

1 Kwamba mtu hawezi kumtii Mungu ni kwa sababu amefungwa na kitu kilichotangulia kabla. Mambo ambayo yalikuja kabla yamewapatia watu kila namna ya dhana na njozi za uongo kuhusu Mungu ambazo zimekuwa ndiyo taswira ya Mungu akilini mwao. Hivyo, kile wanachoamini ni dhana zao wenyewe, na viwango vya mawazo yao wenyewe. Ikiwa utampima Mungu ambaye anafanya kazi halisi leo dhidi ya Mungu wa mawazo yako mwenyewe basi imani yako inatoka kwa Shetani, na ni kulingana na mapendeleo yako mwenyewe—na Mungu hataki imani kama hii.

2 Bila kujali sifa zao ni za juu sana kiasi gani, na bila kujali kujitoa kwao—hata kama wamejitoa jitihada za maisha yao yote katika kazi Yake, na wamejitoa mhanga—Mungu hakubali imani yoyote kama hii. Anawaonyesha tu neema kidogo, na kuwaacha waifurahie kwa muda. Watu kama hawa hawawezi kuuweka ukweli katika vitendo, Roho Mtakatifu hafanyi kazi ndani yao, na badala yake Mungu atamwondoa kila mmoja wao. Bila kujali ama ni wazee au vijana, wale ambao hawamtii Mungu katika imani yao na wana motisha mbaya, ni wale ambao wanapinga na kuingilia, na watu kama hao bila kuhoji wataondolewa na Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 412 Nini Hutokea kwa Kuchukulia Imani Yako Bila Makini

Inayofuata: 414 Sababu za Watu Kushindwa Katika Imani Yao kwa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp