1 Mwana wa Adamu Ashuka Duniani

Umeme waja kutoka Mashariki, ukiangaza kuelekea Magharibi.

Mwana wa Adamu Ameshuka duniani.

Mungu mwenye mwili, Akionekana, Akifanya kazi Uchina,

Yeye ni Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho.

Ameonyesha ukweli, Akitikisa kila taifa.

Kazi ya hukumu inaanzia katika nyumba ya Mungu.

Maneno Yake yana mamlaka, yanashinda mioyo ya wote.

Wakiwa wameshawishika kabisa, wanainama katika ibada.

Mwenyezi Mungu ameketi kwenye kiti Chake cha utukufu.

Mwana wa Adamu ameonekana na kufanya kazi,

Akitikisa kila taifa duniani.

Maneno ya Mungu yanaenea ulimwenguni,

kwa sauti ya baragumu ya Enzi ya Ufalme

kusikika kote ulimwenguni.

Mwana wa Adamu azungumza na kutembea kati ya makanisa,

maneno na kazi Yake viko kati yetu.

Kila mmoja wetu anachungwa, kunyunyiziwa na Mungu,

kufurahia kazi ya Roho, ana kwa ana na Mungu.

Maneno ya Mungu ya hukumu kama upanga wenye makali kuwili,

yakifunua na kuchangua ukweli wa upotovu wa mwanadamu.

Hukumu na kuadibu hutakasa

upotovu na uasi wetu,

kutuokoa kikamilifu kutoka kwa nguvu za Shetani.

Tumepata ukweli na uzima, tunatoa sifa kwa Mungu.

Mwana wa Adamu ameonekana na kufanya kazi,

Akitikisa kila taifa duniani.

Maneno ya Mungu yanaenea ulimwenguni,

na sauti ya baragumu ya Enzi ya Ufalme

kusikika kote ulimwenguni.

Mwenyezi Mungu huonyesha ukweli

kuhukumu na kumtakasa mwanadamu.

Amefanya kundi la washindi Uchina.

Akimshinda Shetani, Mungu anapata utukufu.

Maneno Yake yanatimizwa moja baada ya lingine.

Mwana wa Adamu ameonekana na kufanya kazi,

Akitikisa kila taifa duniani.

Maneno ya Mungu yanaenea ulimwenguni,

na sauti ya baragumu ya Enzi ya Ufalme

kusikika kote ulimwenguni.

Baragumu za malaika, nyimbo za malaika,

hizi zote hutumikia kumtukuza Mungu.

Mwenyezi Mungu atatawala duniani hata milele.

Iliyotangulia: 1038 Masharti Manne ya Mungu Kumkamilisha Mwanadamu

Inayofuata: 2 Mwana wa Adamu Ameonekana

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

132 Mradi tu Usimwache Mungu

Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki