97 Mungu Hutumia Maneno Kuushinda Ulimwengu Mzima Katika Siku za Mwisho

1 Mungu atatumia maneno kuushinda ulimwengu. Atafanya hivi si kwa kupata kwake mwili, lakini kwa kutumia matamshi kutoka kwa Mungu katika mwili kushinda watu wote duniani; Namna hii tu ndiye Mungu katika mwili, na huu tu ndio kuonekana kwa Mungu katika mwili. Labda kwa watu, inaonekana kana kwamba Mungu hajafanya kazi kubwa—lakini Mungu analazimika kutamka maneno Yake ili watu washawishike kabisa, na wao kutishika kabisa. Bila kweli, watu wanapiga makelele na kupiga mayowe; kwa maneno ya Mungu, wote wananyamaza kimya. Mungu hakika atakamilisha ukweli huu, maana huu ni mpango ulioanzishwa na Mungu: kukamilisha ukweli wa Neno kuwasili duniani.

2 Kuwasili kwa Ufalme wa Milenia duniani ni kuwasili kwa neno la Mungu duniani. Kushuka kwa Yerusalemu mpya kutoka mbinguni ni kuwasili kwa maneno ya Mungu kuishi miongoni mwa mwanadamu, kuenenda na kila tendo la mwanadamu, na mawazo yake yote ya ndani. Huu pia ni ukweli kwamba Mungu atatimiza, na mandhari mazuri kabisa ya Ufalme wa Milenia. Huu ndio mpango uliowekwa na Mungu: Maneno Yake yataonekana duniani kwa miaka elfu moja, na yatashuhudia matendo yake yote, na kukamilisha kazi Yake yote duniani, ambapo baada ya hatua hii mwanadamu atakuwa amefikia kikomo.

Umetoholewa kutoka katika “Ufalme wa Milenia Umewasili” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 96 Watu Wanamjua Mungu Bora Kupitia Kazi ya Maneno

Inayofuata: 98 Hakuna Awezaye Kuondoka Kutoka Neno la Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp