129 Kazi ya Mungu Haijirudii

1 Maneno yaliyozungumzwa na Mungu katika mwili wa siku za mwisho ni kutokana na hulka ya asili ya mwanadamu, kulingana na tabia ya mwanadamu, na kulingana na kile ambacho mwanadamu anapaswa kuingia kwacho leo. Maneno ni halisi na ya kawaida: Hazungumzi juu ya kesho, wala Haangalii nyuma, jana; Anazungumza kile tu ambacho kinapaswa kuingiwa kwacho, kuwekwa katika vitendo, na kueleweka leo. Kama, wakati wa zama hizi, kutatokea mtu mwenye uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, na kutoa mapepo, kuponya wagonjwa, na kufanya miujiza mingi, na kama mtu huyu anadai kwamba yeye ni Yesu ambaye amekuja, basi hii itakuwa ni ghushi ya roho wachafu, na kumuiga Yesu.

2 Kumbuka hili! Mungu Harudii kazi ile ile. Hatua ya kazi ya Yesu tayari imekwisha kamilika, na Mungu Hataichukua tena hatua hiyo ya kazi. Ikiwa, wakati wa siku za mwisho, Mungu bado Angeonyesha ishara na maajabu, na bado Angetoa mapepo na kuponya wagonjwa—kama Angefanya vilevile ambavyo Yesu Alifanya—basi Mungu Angekuwa Anarudia kazi ile ile, na kazi ya Yesu isingekuwa na maana au thamani yoyote. Hivyo, Mungu Anatekeleza hatua moja ya kazi katika kila enzi. Mara tu kila hatua ya kazi Yake inapokamilika, baada ya muda mfupi inaigizwa na roho wachafu, na baada ya Shetani kuanza kufuata nyayo za Mungu, Mungu Anabadilisha na kutumia mbinu nyingine.

Ikiwa tu Mungu Atafanya sehemu nyingine ya kazi Yake wakati wa siku za mwisho, kazi inayowakilisha sehemu ya mpango wa usimamizi Wake, ndipo mwanadamu anaweza kupata maarifa ya kina ya Mungu, na baada ya hapo tu ndipo mpango wa usimamizi wa Mungu unaweza kukamilika.

Umetoholewa kutoka katika “Kuijua Kazi ya Mungu Leo” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 128 Kazi ya Mungu Inaendelea Kuboreshwa

Inayofuata: 130 Enzi Tofauti, Kazi Tofauti ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp