942 Ni Msingi wa Maneno ya Mungu tu Unaotoa Njia ya Kutenda

1 Kwa kutafuta ukweli tu ndipo utapata mabadiliko katika tabia yako: Hili ni jambo unalofaa kulielewa na kulielewa vizuri kabisa. Usipoelewa ukweli vya kutosha, utateleza kwa urahisi na kupotoka. Kutafuta kukua katika maisha lazima utafute ukweli katika kila kitu. Haijalishi suala gani laweza kutokea, lazima utafute kukumbana nalo katika njia inayopatana na ukweli, kwa sababu ukikumbana nayo kwa njia isiyo safi kabisa, basi unaenda kinyume na ukweli. Chochote ufanyacho, lazima kila wakati ufikirie thamani yake. Unaweza kufanya yale mambo yaliyo na maana na lazima usifanye mambo yasiyo na maana. Kuhusu mambo ambayo unaweza kuyafanya ama kutoyafanya, kama yanaweza kuachiliwa, basi yaachilie. Ama ukifanya mambo haya kwa muda fulani na lazima uyaachilie, basi yaachilie haraka, ukifanya uamuzi kwa upesi. Hii ndiyo kanuni unayofaa kufuata unapofanya kitu chochote.

2. Katika mchakato wa kutafuta kuingia, kila jambo lazima lichunguzwe na kulinganishwa na neno la Mungu na kulinganishwa na ukweli; lazima yafikiriwe kabisa ili kujua jinsi ya kuyafanya kwa njia ambayo inalingana kabisa na mapenzi ya Mungu. Mambo yanayotokea kutoka kwa mapenzi yako kisha yanaweza kuachwa. Utajua jinsi ya kufanya mambo ukizingatia mapenzi ya Mungu na basi utaenda uyafanye, kana kwamba kila kitu kinafuata mkondo wake, na itahisi ikiwa rahisi kabisa. Watu walio na ukweli hufanya mambo kwa njia hii. Kisha unaweza kuonyesha wengine kuwa umebadilisha tabia yako kwa kweli, wengine wataona kuwa kwa kweli una matendo mazuri, na kuwa unafanya mambo kwa njia ya kufuata kanuni, na kufanya kila kitu sawa. Wataona kuwa huyu ni mtu anayeelewa ukweli, ambaye kwa hakika ana mfano fulani wa ubinadamu na, hakika kabisa, neno la Mungu limevuna matokeo nao.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Iliyotangulia: 941 Tafuta Ukweli katika Vitu Vyote ili Kuendelea Mbele

Inayofuata: 943 Jinsi ya Kuchukulia Agizo la Mungu

Maudhui Yanayohusiana

47 Furaha Katika Nchi ya Kanaani

1 Kurudi nyumbani kwa Mungu, nahisi furaha na msisimko. Nina bahati kuona hatimaye Mwenyezi Mungu wa vitendo. Maneno Yake huwaongoza watu...

84 Umuhumi wa Maombi

1 Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki