468 Maneno ya Mungu Yanakimu Mahitaji Yote Katika Maisha ya Mwanadamu
1 Haijalishi kama maneno yanayonenwa na Mungu ni makavu au makubwa katika mwonekano wa nje, yote ni ukweli ulio lazima kwa mwanadamu anapoingia katika uzima; ni chemichemi ya maji ya uzima yanayomwezesha kuishi katika roho na mwili. Yanatosheleza kile ambacho mwanadamu anahitaji ili awe hai; kanuni na imani ya kufanya maisha yake ya kila siku; njia, lengo, na mwelekeo ambao lazima apitie ili kupokea wokovu; kila ukweli ambao anapaswa awe nao kama kiumbe aliyeumbwa mbele za Mungu; na kila ukweli jinsi mwanadamu anavyotii na kumwabudu Mungu. Ni uhakika ambao unahakikisha kuishi kwa mwanadamu, ni mkate wa kila siku wa mwanadamu, na pia ni nguzo ya msaada inayowezesha mwanadamu kuwa na nguvu na kusimama.
2 Yamejaa utajiri wa ukweli wa ubinadamu wa kawaida anavyoishi binadamu aliyeumbwa, yamejaa ukweli ambao mwanadamu anatumia kutoka kwa upotovu na kuepuka mitego ya Shetani, yamejaa mafunzo bila kuchoka, kuonya, kuhamasisha na furaha ambayo Muumba anampa binadamu aliyeumbwa. Ni ishara ambayo inawaongoza na kuwaelimisha wanadamu kuelewa yale yote yaliyo mazuri, hakika inayohakikisha kuwa wanadamu wataishi kwa kudhihirisha na kumiliki yale yote yaliyo ya haki na mema, kigezo ambacho watu, matukio, na vitu vyote vinapimwa, na pia alama ya usafiri inayowaongoza wanadamu kuelekea wokovu na njia ya mwanga.
Umetoholewa kutoka katika “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu” katika Neno Laonekana katika Mwili