Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

105. Neno la Mungu ni Nuru

I

Umeme kutoka Mashariki uliniamsha,

Niliona neno la Mungu likionekana katika mwili.

Maneno ya hukumu, kuadibu

yamenitakasa sasa na kunikomboa.

Kushindwa, majaribio na dhiki yalinirarua vipande vipande.

Upotovu wangu ulifichuliwa na

mimi, niliyekuwa na majivuno, nikashusha kichwa changu.

Katika uchafu wangu, niliona kutostahili kwangu.

Kwa hali yangu na madeni yangu ya zamani,

Je! mimi, katili na mpotovu,

ningestahili kumtumikia Mungu?

Vipingamizi, kushindwa huniweka

katika njia sahihi ya imani.

Mapigo, utakaso na taabu

yanaunda mnyororo wa ukombozi wangu.

Yananifunga karibu na upendo wa Mungu,

na kujua tabia ya haki ya Mungu ni baraka.

Maneno ya Mungu yamenitakasa na kunikamilisha,

yakiniruhusu niishi kwa kudhihirisha maisha halisi.

Kumjua Mungu na kuwa shahidi Wake,

Nitampenda na kumtumikia Mungu milele.

II

Mungu katika mwili, Mwokozi njoo, njoo tena.

Kupitia hukumu, dhiki na majaribio,

Nimekutana uso kwa uso na Mungu.

Nimeonja wokovu na kumjua Mungu wa vitendo.

Kupitia mateso makali ya giza,

Nilijifunza cha kuchukia au kupenda.

Kupitia nuru ya maneno ya Mungu, nilielewa siri za maisha.

Mwili wa wanadamu, ni potovu, ni Shetani aliyepata mwili.

Maneno ya Mungu yamenitakasa na kunikamilisha,

yakiniruhusu niishi kwa kudhihirisha maisha halisi.

Kumjua Mungu na kuwa shahidi Wake,

Nitampenda na kumtumikia Mungu milele.

III

Ni kukuzwa kwa pekee na Mungu

kwamba ninaweza kumpenda na kumshuhudia Yeye.

Kulipa Upendo Wake, tamanio langu la pekee.

Hukumu na adhabu Yake yana maana na yanafichua upendo wa Mungu.

Kumtii na kumpenda Mungu kwa uchaji ni wajibu wangu.

Napaswa kushuhudia na kuwa mwaminifu Kwake.

Najitolea kwa mapenzi Yake na kwa utukufu Wake.

Maneno ya Mungu yamenitakasa na kunikamilisha,

yakiniruhusu niishi kwa kudhihirisha maisha halisi.

Kumjua Mungu na kuwa shahidi Wake,

Nitampenda na kumtumikia Mungu milele.

Maneno ya Mungu yamenitakasa na kunikamilisha,

yakiniruhusu niishi kwa kudhihirisha maisha halisi.

Kumjua Mungu na kuwa shahidi Wake,

Nitampenda na kumtumikia Mungu milele.

Iliyotangulia:Kusubiri Habari Njema za Mungu

Inayofuata:Matamanio ya Dhati ya Kutubu

Maudhui Yanayohusiana