90 Neno la Mungu ni Mamlaka na Hukumu

1 Watu wengi hupuuza maneno Yangu na kufikiri maneno ni maneno tu na ukweli ni ukweli. Wao ni wajinga! Hawajui kwamba Mimi ni Mungu mwaminifu Mwenyewe? Maneno Yangu na ukweli hutokea sawia—si hii kwa hakika ni kweli? Nilipoumba vitu vyote, Ninapouharibu ulimwengu, na Ninapowakamilisha wazaliwa wa kwanza—mambo haya yote yanatimizwa kwa neno moja kutoka katika kinywa Changu. Hii ni kwa maana neno Langu lenyewe ni mamlaka; hilo nihukumu.

2 Inaweza kusemwa kuwa mtu Niliye ni hukumu na uadhama; huu ni ukweli usiobadilika. Huu ni upande mmoja wa amri Zangu za utawala; njia moja Kwangu kuwahukumu watu. Machoni Pangu, watu wote, masuala yote, na vitu vyote—vitu vyote kabisa—viko mikononi Mwangu na viko chini ya hukumu Yangu, hakuna mtu na hakuna kitu chochote kinachothubutu kutenda bila mpango na kwa makusudi, na yote lazima yatimizwe kwa mujibu wa maneno Ninayonena. Yeyote anayeyatilia shaka maneno Yangu, yeyote anayeyadharau maneno Yangu, hawa ndio watakaoangamizwa, ni wana wa kudumu wa kuangamia kabisa. Kama Nilivyosema, Sijitahidi kufanya lolote, lakini badala yake Mimi hutumia maneno Yangu tu kutimiza kila kitu. Hii, basi, ndipo ambapo kudura Yangu huwa.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 103” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 89 Kazi ya Mungu Inatimizwa Kupitia Maneno

Inayofuata: 91 Kazi ya Siku za Mwisho ni Hasa ili Kumpa Mwanadamu Uzima

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp